PICHA JALADANI. Naye ataona ni upuuzi usiopimika akiambiwa radio haikutengenezwa na yeyote bali ilijitengeneza:

Similar documents
Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Kiu Cha umtafuta Mungu

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

PDF created with pdffactory trial version

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

United Pentecostal Church June 2017

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

Oktoba-Desemba

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Human Rights Are Universal And Yet...

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Roho Mtakatifu Ni Nini?

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

MSAMAHA NA UPATANISHO

K. M a r k s, F. E n g e l s

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Shabaha ya Mazungumzo haya

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Wanawake katika Uislamu

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

H. M. Baagil, M. D. WAMY Studies on Islam

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Maisha Yaliyojaa Maombi

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Makasisi. Waingia Uislamu

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

Ufundishaji wa lugha nyingine

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Transcription:

PICHA JALADANI Mwamini mageuzi (evolution) huamini viumbe na hayawani, hata mimea vyote vilifikia hali yake kwa ugeukaji wa karne nyingi: Havikuumbwa, vilijiumba. Naye ataona ni upuuzi usiopimika akiambiwa radio haikutengenezwa na yeyote bali ilijitengeneza:

Yaliyomo MOJA... 4 MBILI... 8 MWANDISHI WA BIBLIA NI NANI?... 8 TATU... 12 DINI NA MADHEHEBU MBALI MBALI... 12 NNE... 16 BAADA YA DHAMBI MDHAMBI AKATE TAMAA?... 16 TANO... 19 BAADHI HAWATAOA NA BAADHI HAWATAOLEWA ILI KUMTUMIKIA BWANA... 19 SITA... 23 KUABUDU MSALABA NI KOSA?... 23 SABA... 27 TAFSIRI ZA BIBLIA... 27 NANE... 31 MUNGU HUTAKA NINI? UTII... 31 Habari za Mwandishi... 32

MOJA Aulizwaye jina la Muumbaji wa vyote ni nani? Aangalie asije kukimbilia kujibu Jina la Muumbaji wa vyote ni Mungu. Mwenye kutoa jibu hilo huenda akawa sawa na ambaye angeulizwa Rais wa nchi ya Ughaibu ni nani? na kutoa jibu la Rais wa nchi ya Ughaibu ni Rais. Jina maana yake hasa ni nini? Jina ni neno wakilishi la nafsi la kumtajia mtu au kitu: Ni neno litumikalo katika kutaja nafsi pekee ya mtu, myama, sehemu ya nchi au kitu. Utaratibu wa kuwa na majina upo ili kile kitajwacho katika mawasiliano au maongezi kiwe ni kile kile pekee pasipo na hisia tofauti kuhusu kinachoongelewa. Kila mmoja wa jamii ya watu ni mtu. Na kila mmoja huwa na jina binafsi kumtofautisha na mtu mwingine katika kuitwa au kutajwa tu. Jina binafsi la Muumbaji wa vyote ni YEHOVA. Majina mengine yatumikayo kumtajia Muumbaji wa vyote ni sifa za utenzi au utendaji wake, na yanazo tafsiri mbali mbali. Na kwa vile ni sifa tu: hutofautiana kimataifa. Katika kiingereza isemekanapo kwamba muumbaji wa vyote is God kwa Kiswahili huyo God ni Mungu na kibantu pia ni Mungu au Mulungu. Lugha nyinginezo katika mataifa mbalimbali huwa na neno Fulani lenye maana ya God au Mungu. Kwa kufafanua dhana hii; chukulia wasukuma na wanyamwezi kama mmojawapo katika jamii za kibantu: Wao humuita muumbaji wa vyote kwa majina mbalimbali ambapo kila moja ni moja huwa ni sifa tu ya uwezo na ukuu wake. Majina hayo ni Mungu, Limulungu, Mulungu, Limudimi, Likube, Lyangasa, Lyuba, -Nsubi, Seba, Lyangalula-, Liwelelo, Nyanhalemelwa, Libunanze, Likunze n.k. Majina hayo ya muumbaji yana sifa mbalimbali hutumika na Wanyamwezi au Wasukuma kufuatana na mazingira

yenyewe, katika mazingira Fulani muumbaji ataitwa Limudimi na katika mazingira mengine Muumbaji huyohuyo ataitwa Lyuba. Wakati mwingine watu wa jamii hiyohiyo moja huwa na chaguo lao la jina mojawapo kwa sehemu wanayoishi. Jina binafsi la mmojawapo wa mitume wa yesu lina maana ya kwamba au jiwe. Mtume huyo haitaeleweka iwapo jina lake katika Kiswahili litachukuliwa kwa tafsiri yake kwa sababu ni jina hasa ambalo mwenye kuliitwa alilikubali kuwa lake binafsi. Kwa hiyo jina hilo kutofautiana kiasi tu kufuatana na tamaduni tofauti na matamshi. Jina hilo hubaki lenye asili maalumu. YEHOVA ni jina binafsi la muumbaji wa vyote ambalo halibadilishwi kama itokeavyokwa kiwakilishi cha sifa. Jina la YEHOVA hubakia na asili yake katika lugha mbalimbali za mataifa mbalimbali kama inavyojidhihirisha hapa chini. LUGHA Kidachi Kiingereza Kifaransa Kijerumani Kiibo Kiitaliano Kijapan Kireno Kiromania Kihispania Kiswahili Kiyoruba Kizulu Kisukuma KIBANTU JINA Jehovah Jehovah Jehovah Jehova Jahova Geova Ehoba Jeeva Iehova Jehova Yehova Jehofah Ujehova Yehoya Yehova, Yehova, Jehova.

Pamoja na ukweli kwamba kuna jina na sifa ya mtu au kitu isisahaulike kuwa baadhi ya majina binafsi huwakilisha sifa. Jina YEHOVA kwa kiebrania liliandikwa kwa herufi nne tu, YHWH au JHVH. Jina lenyewe kwa kiebrania lina maana ya kuwapo au Aviwezeshaye kuwapo. Jina hilo huonekana mara 7,000 katika maandiko Matakatifu ya Kiebrania halisi. Yasemekana jina hilo lililowekewa kichwa kikubwa kiwango cha kuandikwa tu bali msomaji wa maandiko hayo hakulitamka kila lilipotokeza. Uchaji mkubwa huo huenda ndio baadaye umesababisha jina YEHOVA kutoonekana katika Maandiko Matakatifu hadi siku ya zama tulizo nazo. Katika zama hizi sifa zinatumika tu kama vile kwa Kiswahili ni BWANA MUNGU: Baadhi ya tafsiri za Kiswahili za Maandiko,atakatifu huweka Bwana kwa herufi kubwa (BWANA) kila pahala ambapo kwa kiebrania palikuwa na YHWH au JHVH. Katika mawasiliano ya kila siku kuhusu uongozi au utawala mashuhuri au mkuu kipi ni heshima; jina binafsi? Au cheo au sifa tu? Kwa mfano, ingetokea kwamba Rais wa Ughaibu ni Ghibu, msemaji yupi ana heshima kwa Rais wake yule ambaye ataendelea kwa kusema Mheshimiwa Ghibu alisema Bwana Ghibu alisisitiza Mtukufu Ghibu alimaliza kwa kueleza Au yule ambaye ataendelea kusema Mheshimiwa Rais alisema Bwana Rais alisisitiza Mtukufu Rais alimaliza kwa kueleza Katika mila na desturi za wengi ni heshima nzuri kumtaja mkuu kwa cheo au sifa zake badala ya jina lake binafsi. Hali ikiwa hivyo kwa ukuu wa kawaida wa walimwengu duniani; kwa nini isiwe vema kuwa na heshima hata kubwa Zaidi kwa Bwana wa mabwana? Dhana iliyopo hapa inafumbata uwezekano wa heshima na kutopea katika kutaja kiwango cha jina binafsi kutokukumbukika kirahisi. Kuna ubaya gani? Ngazi au upeo/upenu wa maandishi haya hautafikia kiwango cha kulijadili swali hilo.

Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako (Mat. 6:9) jina lipi? Kwa nini Yesu aliishia kutaja Baba, Jina katika heshima, tuliyo nayo mazoea ya kibantu, n.k. Mwana hutaja jina binafsi la mzazi au la?.

MBILI MWANDISHI WA BIBLIA NI NANI? Biblia kama inavyotumika hivi sasa ni Maandiko Matakatifu. Ni Maktaba ya aina ya pekee inayohifadhiwa katika kitabu kimoja. Neno biblia linatokana na neno la kigiriki ambalo ni wingi wa Biblos. Kila kijitabu (Biblos) kilichoandikwa kilitumika pekee pamoja na kuhusishwa na vijitabu (Biblia) vingine vilivyosimulia mambo Matakatifu. Baadhi ya vijitabu hivyo baadaye viliteuliwa na kuhifadhiwa kwa pamoja kama kitabu kimoja na hiyo ndiyo biblia itumikayo katika zama hizi. Maandiko matakatifu husimulia habari za aina aina. Sehemu ya kwanza Biblia au Agano la Kale husimulia mambo ya historia, mafunzo ya msingi, Sanaa ya kishairi na mambo ya unabii. Katika sehemu ya pili yaani Agano jipya husimulia habari njema au injili na Matendo ya Mitume ambayo pia ni mambo ya kihistoria. Pia mna nyaraka mbali mbali za upashanaji habari njema na mambo ya Unabii yako kwenye kijitabu cha Ufunuo. Masimulizi katika Biblia yenye mtazamo wa maudhui ya historia husimulia hadi matukio ya kabla ya nyakati (Mwanzo); Kitabu kinachotaja ya mwanzo kabla ya kuwepo mwanadamu; uandishi wake ni wa aliyekuwapo kabla ya wakati. Aliyekuwapo kabla ya wakati ni mungu (Mwa. 1:1 3; Yah. I:1,2). Maandiko Matakatifu yaliandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Wanadamu walioshika kalamu na kuyaweka penye karatasi walifanya hivyo kwa kuongozwa na Mungu (2 Tim. 2:16,17).

Hapo juu pametaja kwamba vijitabu mbalimbali viliandikwa na baadaye baadhi yake viliteuliwa na kuhifadhiwa kama Biblia ilivyo leo. Katika biblia hakuna panapoelezea wazi ni vingapi viliandikwa. Ni historia ya elimu-dunia tu ndiyo huelezea ya kuwa mamia kadhaa ya vijitabu aina hiyo viliandikwa. Vijitabu visivyozidi mia ndivyo vilitumika katika uhifadhi wa maktaba hiyo maalumu na kutunzwa katika kitabu kimoja kiitwachi biblia. Biblia itumikayo na Waprotestanti inavyo vijitabu 66, na madhehebu ya katoliki wana vijitabu vipatavyo 72 katika Biblia waitumiayo. Matumizi ya vijitabu vya maandiko matakatifu katika kuelezea habari za Mungu yalianza karne nyingi kabla ya kuzaliwa Kristo (K.K). Pamoja na kutokujulikana wazi ni lini hasa vijitabu vya agano la kale vilikusanywa na kuhifadhiwa kama kitabu kimoja; inafahamika kuwa tafsiri ya watafsiri 70 ilikamilishwa miaka mia mbili kabla ya kuzaliwa Kristo (200 K.K). Wakatafsiri Kiebrania katika Kigiriki. Yasemekana watafsiri hao 70 wakifanya kazi kila mmoja lwake (kivyake), walikamilisha kazi iliyofanana sana ilipolinganishwa. Hapo hata kazi hiyo ya kutafsiri ilionyesha kuwa ilihusu kazi iliyoongozwa na Mungu. Uandishi wa vijitabu vilivyo katika Agano Jipya ulianza mnamo miaka ipatayo kumi hivi baada ya kufa na kufufuka Yesu Kristo. Uandishi wa vijitabu hivi ulikamilika mnamo karne ya kwanza baada ya kuzaliwa Kristo (96 B.K.). Kwa ujumla wake, uandishi wa vijitabu vyote vilivyomo katika biblia ulikuwa nyakati mbalimbali na ulikamilishwa katika kipindi cha zaidi ya karne 16. Ni kazi iliyowahusisha wasika kalamu wapatao 40 kuikamilisha, Mwanzo Ufunuo. Inakisiwa kijitabu cha

Mwanzo Musa alikikamilisha mnamo mwaka 1513 K.K naye Yohane akakikamilisha kijitabu cha ufunuo mnamo mwaka 96 B.K. Viongozi wa Kanisa mara nyingi wanashauri ilivyo muhimu kujisomea neno la mungu kwa ustawi wa roho. Si hivyo tu, bali pia wameonya ilivyo muhimu kusoma Maandiko Matakatifu na kupata ufafanuzi wake sahihi. Kitabu hicho ni tofauti na vitabu vya elimu dunia. Baadhi ya watu mashuhuri wa dunia iliwahi kuwabidi kutaka msaada kuyaelewa maandiko. Mfano ni yule mkurugenzi maarufu wa hazina ya malkia wa Ethiopia (Mate. 8:26-38). Hali kadhalika siyo rahisi kwa msomaji kuelewa kutokupunguza au kuongeza katika kitabu hiki (Yoh. 22:18 Kumb. 4:2, 12:32; Dan.). Je washika kalamu haowalisema juu ya walichokiandika juu ya vijitabu vyao tu? Au hayo ni juu ya vijitabu mamia vilivyopata kuandikwa, au juu ya biblia ilivyo sasa ipi yenye vijitabu 66 au 72? Upeo wa maelezo haya hautafikia kujibu swali hilo. Dhana kinzanifu nyingine akutanayo msomaji wa Maandiko Matakatifu na vitabu vya elimu dunia ni juu ya kuumbwa kwa vitu vyote na mageuko (evolution). Hizo ni kama imani mbili zisizoyakinishika. Mwenye imani katika vyote kuumbwa naye hawezi kufafanua kwa yakini, pia mwamini juu ya mageuko hawezi kuyahakikisha kwa majaribio ya kisayansi katika maabara kimbilio la Mwanasayansi. Bali ichunguzwapo zaidi huenda mwandishi na mwanasayansi huenda wakawa wanazungumzia jambo linalofanana. Dhana ya mageuko huhusika vipindi virefu vya miaka mingi kupita kufikia hatua hadi hatua. Dhana ya uumbaji hutaja siku sita za vyote kufanyika. Neno siku katika lugha iliyotumika enzi za uandishi wa kijitabu cha Mwanzo lina maana pia ya kipindi kirefu cha miaka mingi. Hufikirika ya kwamba, siku hizo sita huenda hazikuwa kama siku zilivyo leo zifuatazo kuonekana na kuchwa kwa jua. Kama hivyo ndivyo,

haieleweki siku tatu za mwanzo zilikuwaje, maana jua halikuwa limeumbwa hadi siku ya nne (Mwa 1:14-19). Pia labda siku ilivyo kwa mwanadamu huenda ikawa sivyo ilivo kwa Muumbaji wa vyote, katika Maandiko Matakatifu miaka elfu moja hufananishwa na siku moja kwa Mungu (Zab. 90:4). Kwa kifupi na uchache wa maelezo, Waamini wa Neno la Mungu duniani leo hutumia Biblia katika sura kuu tatu; wapo walimwengu wa leo wasioamini ya kwamba Masiha ameshazaliwa, hao Biblia kwao ni Agano la Kale tu. Waaminio kuwa Masiha au Kristu alizaliwa, kafa na kufufuka wamegawanyika makundi makuu mawili; wapo ambao Biblia yao ni yenye vijitabu 66 na wengine 72. Historia ya sasa bado ina kumbukumbu changa juu ya mjadala ni vijitabu vipi ni vitakatifu. Martin Luther, mwanzilishi wa upinzani kidini aliwahi kususia vijitabu saba kutoka katika Agano Jipya. Alisusia kijitabu cha Waebrania, Yakobo na Waraka wa pili wa Petro. Vinginevyo alivyosusia ni pamoja na Nyaraka mbili za Yohana (2 Yoh. Na 3 Yoh.). Yuda na Ufunuo. Baada ya upinzani huo ulikwisha na Agano Jipya likawa na idadi ya vijitabu ileile kwa makundi hayo makuu mawili ya Wakristo. Pamoja na yote yaliyoelezwa katika sura hii, lililo la muhimu ni kukiri Maandiko Matakatifu ni kumbukumbu za matukio na maelekezo maalumu ya Muumba kwa Viumbe wake. Mwandishi wake Mkuu ni Mungu alieongoza wanadamu kushika kalamu na kuyaandika yote katika lugha ya kuweza kueleweka na wanadamu.

TATU DINI NA MADHEHEBU MBALI MBALI Dini mtindo wa kuabudu katika imani iyahusuyo mambo ya kiroho baina ya wanadamu na Mungu, ni njia ya kuwasiliana na Mwenyezi Mungu katika masuala ya Kiroho. Dini ni namna ya kuabudu yenye muundo maalumu wa wafuasi wa Kiongozi Mkuu wa kuelekeza mambo ya uhai na Muumbaji wa nguvu za asili na vitu vyote. Dini ni Dhana au falsafa kuu yenye kuunganisha kundi kubwa la wafuasi kama ilivyo kwa wafuasi ambao kwa ujumla wao huitwa Wakristo. Dini yao wafuasi wa Kristo ni ni Ukristo. Dini ya Wakristo iliyo safi humtaka kila mfuasi wake kujilinda kwa usafi wa kiroho na kutenda maadili wengine kumpendeza mungu na kuwasaidia walimwengu (Yak.1:27). Wakristo wamegawanyika katika vikundi viitwavyo madhehebu. Dhehebu ni kikundi cha wafuasi wa mambo ya dini. Wafuasi walio katika dhehebu moja huwa na msimamo unaofanana kifikra katika baadhi ya masuala na dhana kuhusiana na mambo ya kiroho. Dhehebu moja hutofautiana na jingine kinadharia hata kama anayeabudiwa ni mmoja. Mara nyingi madhehebu yenye kutofautiana hupishana kidogo tu kwa vile hata msahafu au kitabu cha Maandiko Matakatifu huwa kile kile. Hufikirika huenda kukawa dini ya kweli na dini potovu. Ukweli huo yawezekana ni huohuo kwa madhehebu. Kwa bahati mbaya sana, sio rahisi au pengine haiwezekani kubainisha kipi ni kweli na kipi sio kweli. Yasemekana kuna dini kuu 10 na madhehebu 10,000 duniani. Kati ya madhehebu hayo, madhebu yapatayo 6,000 yana wafuasi barani Afrika.

Historia ya Ukristo ina masimulizi ya chanzo cha utengano kimadhehebu. Baada ya kutoweka kwa Kiongozi Mkuu wa Ukristo Bwana Yesu Kristo, uongozi wa kanisa aliwaachia mitume wake. Yaelekea Kristo aliwaacha mitume na kanisa chini ya usimamizi wa mmoja wao hao mitume. Usimamizi huo baadaye kihistoria ulikuwa ukirithishwa kwa kiongozi mmoja wa Ukristo duniani. Dhehebu moja la Ukristo latambua uongozi huo wa Ukristo duniani aliachiwa msimamizi ambaye kwa cheo cha sasa ni papa. Kwa hoja hiyo husemekana papa wa kwanza alikuwa Mtume Petro aliyepokelewa uongozi huo na Linus, naye Linus kapokelewa na Anakleti baada ya Anakleti akaja Klementi, halafu Evaristi, Alexanda I, Sisti I, na kuendelea hadi kufikia papa wa 264, Yohani Paulo II, 265, Benedicto XVI na 266, Fransis (Taz NYONGEZA A.) Hapo awali yaelekea Ukristo ulistawi ukiwa wa kufanana kifikra na kwa hiyo dhana ya dhehebu haikuwapo. Mawazo tofauti yalijipenyeza wakati ulipowadia wa kutofautiana kinadharia. Upinzani kidini ukaanza, mtindo na muundo wa kikundi cha kuabudu ukalazimika kubadilishwa. Kiongozi Martin Luther alitengana na papa kwa misingi ya utengano alioutolea hoja 95. Baada ya utengano huo wa awali Ukristo ulikuwa na madhehebu makuu mawili. Mambo yalivyo hivi leo, Ukristo unayo madhehebu mengi sana. Suala la kujiuliza ni hili Iwapo Ukristo ni dini ya kweli, madhehebu yote hayo hufuata misingi ukweli ama baadhi yamepotoka? Baada ya walimwengu wenye namna fulani ya kuabudu kuona mfarakano wa madhehebu uliopo, pameanzishwa mikutano ya umoja wa makanisa (Ecuminism). Mikutano aina hiyo hukutanisha wafuasi wa dini

na madhehebu mbalimbali. Ukweli kamili wa mikutano na mihadhara aina hiyo, uchunguzwapo mchunguzi hukumbana na wingi wa viunganishi na uhaba wa vitenganishi. Pamoja na ukweli huu, mara nyingi mikutano aina hiyo haigusii viini vya utengano bali kusoma tu katika Maandiko Matakatifu na kutolea ufafanuzi kwa jinsi mtoa neno. Kwa bahati huweza kutokea somo lililochaguliwa likawa la kuwajenga wote au wengi waliohudhuria. Hali pia, wakati mwingine yaweza kutokea somo likasomwa kwenye mihadhara / mikutano hiyo likaacha dukuduku mbalimbali kwa wasikilizaji. Wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali hutofautiana maoni yao juu ya sanamu, watakatifu, sala, dua n.k. Pamoja na misahafu yao kuelezea kuelezea juu ya hayo yote bado wafuasi hutofautiana kwa sababu mbali mbali. Cha muhimu ni neno (Biblia: Mwa. Ufu) wala si madhehebu. Ukurumbeza na matakwa binafsi ya waanzishaji madhehebu mbalimbali husababisha mfarakano kati ya wafuasi wao. Ni kweli utofauti katika fikra umewahi kusababisha utengano, lakini pia ni sababu za kiuchumi zimewahi kuchukua nafasi yake katika kuleta mifarakano na utengano. Harakati za maisha kiroho ni kama safari ya kwenda mbinguni. Vyombo watumiavyo wasafiri mbalimbali wa safari hiyo ni madhehebu mbalimbali, na lililo muhimu ni kuimaliza safari hiyo salama. Hata katika safari za hapa duniani kuwa na vyombo aina mbalimbali, msafiri hujichagulia chombo atakacho kusafiria au kutumia. Bwana Yesu Kristo alitumia mwanapunda kwenda Yerusalemu (Math. 21:4-12; Mk. 11:7-11; Lk. 19:35-45, Yoh. 12:14-15). Baada ya kufika Yerusalemu Yesu aliingia

hekaluni, katika nyumba ya Baba, chombo alichotumia kusafiria kilibaki nje. Chombo cha kusafiria na njia ya kupita vyote ni muhimu katika kukamilisha safari. Kristo kwa safari aliyotumia mwanapunda angaliweza kuikamilisha kwa chombo kinginecho mradi njia ya kupita ilijulikana. Wakristo katika safari ya kwenda mbinguni waijua njia. Bwana Yesu ndiye njia ya kuendea mbinguni (Yoh. 14:16). Ni nani ajuaye kwa uhakika madhehebu mbalimbali ni vyombo mbali mbali katika safari ya kwenda mbinguni? Kwa hiyo basi, kila msafiri aijuaye njia ya kufikia mbinguni aifuate kwa makini hiyo njia katika chombo cha dini ambacho usukani wake ni Maandiko Matakatifu, Rubani wake akiwa Mungu mwenyewe. Kwa namna ya pekee Maandiko Matakatifu hayana sifa ya kuwa usukani tu bali pia ni chombo. Naye Mungu hana sifa ya urubani tu bali ndiye Muundaji wa vyote, chombo ni usukani wake, kuunda vyote katika uumbaji wa vyote. Mungu baba ni vyote. Yeye ndiyo mwenye kila sifa. Hapo juu amepewa sifa ya urubani. Mwache Mungu awe rubani wako kwelikweli. Mungu na awe rubani wa mawazo yako, rubani wa matendo yako, kwa fikra zako, furaha, huzuni, matakwa, upendo, wasiwasi na mengineyo; pamoja na kuwa rubani hukuongoza katika dhehebu la dini yako uweze kuikamilisha salama sfari ya kwenda mbinguni.

NNE BAADA YA DHAMBI MDHAMBI AKATE TAMAA? Dhambi ni kosa linalovunja amri ya mungu. Mdhambi huweza kuvunja mojawapo ya amri za Mungu kwa mawazo,matendo,mazungumzo au kwa kutokutimiza wajibu. Baada ya dhambi kutendeka kinachohitajika ni mdhambi kutubu. Kwa vile ni Mungu ambaye hutendewa dhambi, msamaha wa dhambi hutolewa na Mungu peke yake. Msamaha wa dhambi hutolewa na Mungu kwa mdhambi aliyetubu kwa dhati kabisa. Kwa vile yeye Mungu huona yaliyo sirini mwa mwanadamu ni toba ya kwelikweli huhitajika ili maondoleo ya dhambi yafanyike. Ishara ya nje iliyo wazi ya mdhambi ni ile hatua aichukuayo kuonesha toba. Ishara hiyo ya wazi ionekanayo na watu au mtu ikiwa toba ya dhati, kufuatwa na ishara ya ndani sirini ya maondoleo ya dhambi. Mdhambi akinesha kwa nje kutubu bila toba, moyoni mwake, hapati msamaha wa dhambi kutoka kwa aonaye yaliyo sirini. Katika kutekeleza yaliyo wazi ya maondoleo ya dhambi Yesu Kristo, Mungu Mwana, aliwaachia wafuasi wake mamlaka ya kutamka maondoleo ya dhambi (Yoh. 20:21-23). Neno la kuasa hapa, ni kwamba Yesu alipowaagiza akiwaambia mkiwaondolea watu dhambi zao, wameondolewa haina maana ya kwamba wajibu wa mdhambi kutubu kwa dhati uliondolewa. Mdhambi kama hana toba ya dhati moyoni maneno ya muondoa dhambi wa ishara ya nje hayana maana.

Maandiko Matakatifu yanayo historia ya dhambi za mdhambi kuondolewa bila toba ya dhati ya mdhambi. Msamaha wa aina hiyo Mungu huutoa kwa makusudio yake maalumu. Msamaha wa bila hiyari ya mdhambi unajidhihirisha kwa yaliyompata Saulo ambaye baadae aliitwa Paulo (1Tim.1:13). Mungu akishatoa msamaha wa dhambi kwa mdhambi aliyekiri kosa lake Mungu husamehe kabisa. Wanadamu mashuhuri waliowahi kuwa na dosari za kidhambi katika Biblia ni kama vile kina Musa, Daudi na Paulo. Nabii Musa aliwahi kuvunja amri ya Mungu inayokataza kuua (Mwa. ). Musa alikiri kosa lake akasameheka. Baada ya Musa kusamehewa aliaminika katika maadili hadi kunurulishwa Ya Ufalme wa mbingu na kuyaandika. Musa angalikua mdhambi asiyekiri makosa yake kwa dhati hangalimtumia kama mshika kalamu aliyeandika vijitabu vitano vya kwanza katika Biblia. Mfalme Daudi alikua ni mwanadamu mwadilifu tangu enzi za ujana wake. Daudi katika kipindi cha ufalme wake alitenda dhambi kwa kitendo cha uzinzi (2 Sam.11:2-) na baadaye kwa hila kusababisha kifo cha mtu asiyekua na hatia (2 Sam.11:14-17). Mfalme Daudi alikiri kosa lake (2 Sam.12:13, 12:16,17. Zab.139:1-18) kwa dhati na kwa kusameheka kabisa hadi kuwa mfano bora wa utakaso katika Biblia. Mtume Paulo alianzia katika kulinyanyasa kanisa (Mdo.8:3, 9:1,2) hadi kuongoka (Mdo.9:3-19, 22:6-16, 26:12-18) na kuwa Mtume wa

Kristo Paulo aliyeitwa Saulo hapo awali alisamehewa na kuongolewa bila hiyari yake. Paulo alisamehewa bila kuomba msamaha. Pana msemo kwamba bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Pamoja na ukweli kuwa baadhi ya misamaha ya dhambi toka kwa Mungu huja kwa neema tu, mdhambi anaowajibu wa kuomba msamaha wa dhambi kwa toba timilifu. Kutenda dhambi na kukata tamaa juu ya msamaha wake hakuna maana. Dhambi hata ikiwa ya uzito au ukubwa wowote Mungu mpendelevu huisamehe. Dhambi yoyote hata ikitisha sana iombee msamaha. Husameheka. Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

TANO BAADHI HAWATAOA NA BAADHI HAWATAOLEWA ILI KUMTUMIKIA BWANA Kuoana ni kufikia uamuzi wa mwanamume na mwanamke kuishi pamoja ili kuwa mke na mume kwa kanuni zinazokubalika na jamii inayohusika. Wenye kufikia uamuzi wa kuoana mara nyingi hufunga ndoa. Ndoa ni maungano ya mwanaume na mwanamke kuishi kama mke na mume kulingana na sheria au mila na desturi za jamii. Maisha ya ndoa yana mujibu wa kuzaa na kulea watoto kihalali. Katika kusawazisha, wenye ndoa huwa wameoana pamoja na matumizi ya Kiswahili ya kawaida yatenganishayo ya kwamba mwanaume kaoa na mwanamke kaolewa. Kuoana ni kutekeleza mojawapo ya kanuni asilia au maagizo aliyotoa muumbaji wa vyote kwa wanadamu. Mungu alimuumba mtu. Kwa kumuondolea mtu upweke, Mungu kaamua kuwaumba wawili, mwanamume na mwanamke (Mwa. 2:20-22, 1:27). Baadaye Mungu alielekeza mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao hao watakuwa mwili mmoja. (Mwa. 2:24). Yesu Kristo baadaye alikuja kusisitiza ya kwamba, maungano katika ndoa ni ya kudumu wakati wote ambao wenye kuishi hivyo wangali hai. Ni maungano yenye kufuata maelekezo ya Muumba na mwanadamu haruhusiwi kuyatenganisha (Mt. 19:4-6). Katika dhehebu la Katoliki kanuni kutokuwa na ndoa ili kumtumikia Bwana ilianza ifuatavyo. Awali ya yote palizuka mitindo mbalimbali ya watu kumtumikia Bwana. Katika makanisa ya mashariki ya enzi hizo

wanaume waliooa waliweza kupatiwa daraja la ukasisi. Kwenye makanisa yaliyokuwa magharibi desturi ilikuwa kuwapa daraja za ukasisi wanaume waliohiari wenyewe kutokuoa kwa ajili ya ya kumtumikia bwana. Yasemekana kwa pande zote mbili mtu baada ya kupata daraja za ukasisi hakuruhusiwa kufunga ndoa. Yaani aliyepata daraja hizo akiwa kapera aliendelea hivyo na aliyekuwa kaoa hakuruhusiwa kumwacha mke huyo mmoja. Mambo yaliendelea kuwa hivyo kwa watumishi wa bwana hadi hapo baadaye kanuni ya watumishi hao kutokuwa watu wa ndoa ikatawala. Pameshakuwa na mijadala mbali mbali kutaka kanuni hii ifutiliwe mbali katika dhehebu la Katoliki. Bali kwa vile kanisa halimlazimishi mtu kutokuwa mtu wa ndoa, dhehebu halivunji sheria ya Haki za binadamu. Pamoja na hayo, dhehebu Katoliki linayo mamlaka ya kulegeza baadhi ya masharti kwa wafuasi wake. Kanuni ya kutokuwa mtu wa ndoa kumtumikia Bwana ni sharti mojawapo liwezalo kurekebishwa endapo itabidi kufanya hivyo. Kwa mkristo kuamua kutokuwa mtu wa ndoa kumtumikia Bwana si jambo la ajabu lisilo na msingi wake katika Maandiko Matakatifu. Yesu mwenyewe alikuwa na maoni hayo hayo ya kwamba baadhi ya watu ni sawa wakiamua kutokuoa kwa kuutumikia Ufalme wa mbinguni (Mt. 19:12). Yesu Kristo katika ushauri wake juu ya suala hili ameonesha wazi kwamba kufuata kawaida hii kwa hiari (Mt. 19:12B). Naye Mtume Paulo akishauri juu ya masuala ya ndoa (1 Kor. 7:5) aligusia juu ya hiari ya

kuamua kutokuwa mtu wa ndoa ili kumtumikia Bwana (1 Kor. 7:6,7, &:8,9). Imewahi kusemwa vile vile ya kwamba waishio maisha yasiyo ya ndoa hapa duniani hufanana na wanaoishi kama itakavyokuwa huko mbinguni. Hapatakuwa na kuoa wala kuolewa. Pamoja na uwezekano wa kuwa na fafanuzi mbali mbali wateule safi miamoja arobaini na nne elfu (144,000) aliowaona Yohana katika maono walikuwa wanamume ambao hawakuoana kimwili na wanawake katika uhai wao duniani. (Uf. 14: 1:3,4).

Msalaba si sanamu bali sanamu huweza kuwekwa juu yake: Usiabudu msalaba wala sanamu juu yake.

SITA KUABUDU MSALABA NI KOSA? Neno kuabudu lifafanuliwapo kidini ni kuheshimu, kuogopa, kumnyenyekea au kutumikia. Kwa maana hizo zote; anayestahili kuabudiwa ni Mungu YEHOVA. Kwa wivu na mapenzi yake haruhusu kinginecho kuabudiwa. Pamoja na hayo, matumizi mengineyo ya neno kuabudu yana maana ya kuhusudu au kupenda kupindukia. Kwa maana hiyo nyingine, mtu au kitu kinginecho chaweza kuabudiwa. Katika kuabudu msalaba ichukuliwe maana ipi? Maelezo ya makatazo ya kuabudu sanamu yanapatikana wa Kikristo kitabu cha Kutoka 20:4-5. Maelekezo katika aya hii ni kutokutengeneza sanamu na kuziabudu. Haiishii kukataza tu bali adhabu ya mkosaji inatajwa katika kijitabu cha kumbukumbu la Torati 27:15. Laana kutoka kwa Mungu inamwandama ajitengenezeaye sanamu kutokana na mawe, miti au chuma na kuiabudu. Baadhi ya askari wa Yuda walimchukiza mungu kwa kuvaa visanamu vya miungu wakaangamizwa vitani (2 Mak. 12:39-42). Ukweli ulio wazi ni kwamba msalaba sio sanamu, sanamu maana yake ni kitu au kiumbe kilichotengenezwa kwa kuchonga au kufinyanga kuiga umbo la viumbe vilivyoumbwa na Mungu kama vile binadamu au hayawani. Kitu kinginecho kitengenezwacho kufuatia uvumbuzi wa kifundi stadi wa mafundi waliotangulia hakiwi sanamu ya kilichotangulia kuundwa. Huo ni ufundi ambao watu hupokezana kwa sababu hii, msalaba uliotengenezwa na ukatumiwa kumpigilia Kristo juu

yake ni matokeo ya kiufundi tu siyo uumbaji. Na misalaba itengenezwayo kwa kifaa cho chote leo ni misalaba itengenezwayo kufuatia ufundi stadi wa awali. Pamoja na ukweli huo ya kwamba msalaba si sanamu bali kazi halisi ya kiufundi isiyoiga umbo wala kiumbe uheshimike kwa kiwango cha kuabudiwa au kuhusudiwa tu. Yesu Kristo sawa na binadamu wengine wazaliwao, alichukua umbo la binadamu aliyeumbwa na Mungu. Sanamu ya Yesu msalabani ni sanamu ya kuiga kilichoumbwa na Mungu. Kwa hali hiyo ni uangalifu mkubwa sana unahitajika katika kuheshimu msalaba ukiwa na sanamu ya Yesu. Sanamu yo yote iwe ya Yesu au ya Mungu wa kufikirika (Hakuna aliyemwona Mungu). Hairuhusiwi kuabudiwa. Msalaba ambao ni kifaa kilichotumika kuhitimisha ukombozi wa wanadamu hustahili nafasi ya pekee katika kumbukumbu akilini mwa wakombolewa. Upekee wa nafasi ya msalaba katika kumbukumbu akilini sharti utenganishwe na hicho kinachomstahili Muumba. Sanamu ya yesu msalabani ikumbushie tu tukio hilo maalumu bali usitumike katika kuabudu ukiabudiwa wenyewe. Yaelekea makatazo ya utengenezaji wa sanamu hayana maana na sanamu za kiufundi kwa kupamba pahala pa kuishi zinakatazwa. Na pengine hata mungu hakuzikataza ikiwa zitatengenezwa kwa matumizi mengine yasiyo ya kuabudu. Vinginevyo mtu angechunguza Maandiko Matakatifu kijuujuu angeona Mungu mwenye kigeugeu. Maana hapo juu pametajwa kukataza utengenezwaji wa sanamu, mara mwenye kukataza hivyo aamua atengenezwe nyoka wa shaba. Nyoka huyo wa shaba (Hes. 21:9) amefananishwa na kuinuliwa kwa Yesu msalabani katika injili ya Yohana (Yoh. 3:14).

Maagizo mengi ya Mungu huhitaji jambo moja tu, utii. Ni kwa kukosa utii tu dhambi nyingi zimetendeka. Alipoagiza nyoka wa shaba atundikwe juu alitaka watu kutii ya kwamba aliahidi uponyaji kwa kila aliyeumwa na nyoka kwa kuinua macho juu na kumtazama nyoka wa shaba. Mwenye kumtazama nyoka wa shaba aliokoa maisha yake, hakupona kwa ajili ya huyo nyoka aliyeonekana bali kwa ajili ya yeye aliyeahidi uponyaji (Hek. 16:7). Nyoka huyo wa shaba aligeuka kuwa chukizo kwa bwana walipoanza kumuabudu. Maandiko Matakatifu yasema mfalme Hezekia alimfurahisha Mungu alipomvunjavunja yule nyoka wa shaba baada ya kuwa watu walianza kumwabudu (2 Fal. 18:4). Ikilazimika kukufananisha kuinuliwa kwa Kristo msalabani na kuinuliwa kwa nyoka wa shaba jangwani ilazimike pia kuamini kwa utii kwamba ni juu ya huo msalaba ambapo ukombozi wa watu ulitundikwa. Ikumbukwe ya kuwa Mwabudiwa alitundikwa hapo msalabani bali sanamu yake juu ya huo msalaba ni kitu kilichokatazwa kutengenezwa na kuabudiwa. Bali kama ilivyoelezwa hapo juu huenda ikawa utengenezwaji wa hiyo sanamu kwa matumizi mengine yasiyo ya kuiabudu hayana ubaya kama ilivyojitokeza kwa nyoka wa shaba. Swali linalobakia ni hili lifuatalo, Katika ufundishaji wa elimu dunia wenye kufundishwa huweza kuonyeshwa vitu halisi wafundishwayo habari zake. Vitu hivyo itokeapo kuwa havipatikani sehemu ya mafunzo, sanamu na picha zake hutumika katika kufundishia. Je, sanamu na picha za yahusuyo Ufalme wa mbinguni hufaa katika kufundishia? Kilichokatazwa katika kutoka 20:4,5 ni kuabudu kwa sanamu na kitu kinginecho isipokuwa YEHOVA (Kut. 20:3). Kwa mfano, hairuhusiwi

kumwabudu mwanadamu, mnyama wala mmea kwa kile hali iwayo; halisi au sanamu. Kwa hiyo kila inapobidi kufundisha mambo ya Ufalme wa mbinguni kwa kuandika kwa sanamu au picha, ili kurahisisha ufundishaji, ihakikishwe ya kuwa walengwa wametanabahishwa kutokuviabudu. Swali hili ni muhimu kuzingatiwa katika kuwafundisha ya Ufalme wa mbingu watoto (utoto udogo hapa usichukuliwe kwa namna ya umri tu bali ni pamojana wengine wote ambao ni wachanga katika Maandiko Matakatifu). Wa kuabudiwa ni Mungu Muumbaji wa vyote. Bwana haruhusu, ni dhambi kuabudu sanamu au cho chote kilicho duniani angani na mbinguni (Kut. 20:3-5).

SABA TAFSIRI ZA BIBLIA Tafsiri ya Biblia ni Maandiko Matakatifu yaliyotolewa kutoka katika lugha moja hadi nyingine. Mawazo yatolewayo kutoka lugha moja kwenda nyingine hutakiwa yawe yasiyobadilisha maana asilia. Bali kama asemavyo mtafsiri wa kitabu cha Hekima ya Yoshua bin Sira, Kusema kweli, habari asilia kama zilivyoandikwa kwanza katika kiebrania hazilingani na jinsi zilivyofasiriwa katika lugha nyingine. Aidha mtu akiichunguza Torati yenyewe, Manabii, na vitatu vinginevyo ataona kuwa ufasiri wake ni tofauti sana na maneno yake asilia (utang. Ybs. 1:21 26). Mwandishi mmoja maarufu nchini Tanzania, Shaban Robert, aliwahi kuwa na maoni ya kushauri juu ya maandiko ya dini na Maandishi ya Kisayansi na elimu duniani zinginezo. Kwa masuala ya dini ya zamani ni bora na kwa upande wa sayansi maandishi ya hivi karibuni ni bora. Tafsiri za Biblia hapo kale zililenga katika uhifadhi wa maana iliyokusudiwa. Baadhi ya tafsiri za hivi karibuni kuwa na malengo ya kuwavutia wasomaji wapya wa Biblia hata wasioamini. Kuwavutia wasomaji siyo kubaya iwapo ujumbe unaokusudiwa hautapotoshwa. Kwa bahati mbaya wakati mwingine hutokea watafsiri na wafafanuzi huwa na malengo yao. Katika kujilinda dhana fulani zijitokezazo katika majadiliano mbali mbali, mtafsiri au mfafanuzi wa leo hujichagulia maneno ya kutumia kukidhi matakwa yake.

Ni bahati mbaya isiyoyakinika ya kwamba kuna namna mbalimbali za kuelewa jambo lililoandikwa. Habari iliyosimuliwa kwa mdomo wakati ikisikilizwa huweza kuwa na maana isiyowasilishwa na maneno ya wasemaji. Habari iliyotolewa taarifa kwa maandishihuweza kueleweka kwa namna mbalimbali, kuna namna tatu za uelewaji wa Maandiko. Kuna kuelewa maandiko kinyume cha kilichokusudiwa, au kuelewa kama ilivyokusudiwa na uelewaji wa kilichokusudiwa kwa nyongeza ya kilichokusudiwa kwa manufaa ya kilichokusudiwa. Hapa chini patatajwa mifano michache ya jinsi tafsiri mbalimbali zinavyoweza kutoa taarifa kwa namna mbalimbali. Tafsiri mbalimbali za biblia katika lugha mbalimbali zaelekea kutokutaja bayana ya kwamba enzi za mateso ya yesu kulikuwa na kina Yesu wawili gerezani, katika baadhi ya baadhi ya lugha hutafsiriwa mle gerezani mlikuwa na Yesu Baraba na Yesu aliyeitwa Kristu (Yesu Kristu) (Soma Mt. 27:16,17 katika lugha mbali mbali). Panao ubishano mwingi kuhusu kinywaji cha kulevya kiitwacho divai. Kinyaji alichonyweshwa Lutu na binti zake na kulewa kupindukia kilikuwa divai (Yh. 2:3. Mt.11:18,19. Lk. 7:33,34, Mwa. 19:30-36). Divai hiyo hiyo pamoja na kujulikana kuwa na sifa za kulevya inayo matumizi mengine. Huenda ikawa siyo kila chenye kulevya hakifai au hali ya kulewa haifai, yawezekana ni matumizi ndiyo yasiyofaa. Maisha hufaa kuyaishi kwa kiasi siyo kweli kwamba sumu zote ni mbaya ila baadhi ya matumizi yake ni mabaya. Dawa zote ni sumu. Ubaya wake sumu ni kudhuru kisichokusudiwa. Dawa ya malaria kiasi kinachotakiwa ni dawa kwa kiumbe anayetakiwa kuishi. Bali isisahaulike kwamba katika kiasi

hichohicho ni sumu kwa asiyetakiwa kuishi, yaani mdudu wa malaria (Plasmodium spp). Pia baadhi ya matumizi ya kieo kama divai huwa katika kufaa kutuliza maradhi, mfano unajitokeza kwenye ushauri wa Mtume Paulo kwa Timotheo na matumizi ya divai katika huduma ya kwanza aliyompatia Msamaria yule majeruhi. (1 Tim. 5:23, Lk. 10:34). Pamoja na yote yaliyosemwa hapo juu kuhusiana na divai, sehemu hizo zitajazo divai hutumia maneno tofauti katika tafsiri za lugha fulani fulani. Baadhi ya tafsiri hutumia neno lilelile humo mwote palimotajwa (Yh.2:3, Mt.11:18,19, Lk.7:33,34; Mwa.19:19:30-39). Watumiaji wa lugha yenye tafsiri itumiayo neno lile lile humo patajamo divai, hubadilisha hisia zao kufuatana na matakwa yao. Wapo baadhi ya divai hulevya na baadhi hailevyi. Utata mwingine ujitokezao ni ule utokanao na baadhi ya lugha kuwa na maneno ya promosino yawakilishayo jinsia na lugha zingine hazina. Bila kuangalia vizuri ujumbe uliotolewa kwa watu wote unaweza kuonekana kuwaandama wana jinsia moja tu. Ukichukulia Kiswahili na Kiingereza, ujumbe ufuatao kwa kiswahili ni kwa watu wote, Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke (1 Kor. 10:12). Kwa Kiingereza ujumbe huo unao mchepuo wa jinsia Whoever thinks he is standing firm had better be careful that he does not fall (1 Co, 10:12). Panayo mifano mingi ya sehemu ambazo huhitilafiana katika tafsiri mbali mbali na kwa kila hali haikusudiwi mifano yote kwa kumalizia tu, ufuatao ni mfano mwingine mdogo wa jinsia. Huko Efeso watu aliowabatiza Mtume Paulo na kuwawekea mikono na wakajazwa na Roho mtakatifu walikuwa 12. Kwa kiswahili inaelezwa kwamba wote

jumla waliobatizwa walikuwa watu wapatao kumi na wawili. Kwa kiingereza maelezo kuhusu hao waliobatizwa hutajwa kwa kubainisha jinsia They were about twelve men in all (Mate. 19:7 Acts 19:7).

NANE MUNGU HUTAKA NINI? UTII Utii ni ile hali ya kutayari kutii. Na kutii ni kufanya ilivyoamriwa. Kwa maneno mengine ni kufuata amri. Nidhamu na adabu njema ya tabia ya kutokuasi na kutofanya madhara ni mambo yanayosisitizwa na utii. Baada ya ufafanuzi wa utii hapo juu ufuatao ni mjadala baina ya Mheshimiwa Mchunguzi na Mheshimiwa Hekima. Mjadala wao unahusiana na mambo ya Mwenyezi Mungu. MCHUNGUZI: Hivi inawezekana Muumbaji wa vyote alikusudia kiumbe wake aitwaye mwanadamu awe mbumbumbu? Kama sivyo kiumbe huyo alipopatiwa mwenzi na kwa pamoja wakaamua kuyala matunda ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwa. 2:9, 3:4-6) walitaka kuelimika, walikosa nini? HEKIMA: Kwa mawazo yao, yawezekana walifikiri kutenda hivyo haikuwa kukosea bali walikosa utii (Rom. 5:19) Muumba wao alitoa amri ya kukataza kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwa. 2:17a). Suala la kubakia mbumbumbu halina msingi maana ujuzi wa

kutenda mema na mabaya walikuwa nao. Ujuzi uliofumbatwa katika mti huo ni ule uwezao wa kuwa na uweza wa kujipa mamlaka ya kujiamulia cho chote atakavyo mwenyewe. Hayo ni mamlaka ya Muumbaji wa Vyote. Yeye aliwaumba viumbe vyake, na huo ujuzi na kinginecho cho chote alikiumba yeye, wanadamu hao kwa matakwa yao walitaka kujitegemea kana kwamba Muumba wao hakuwapo! Yaani walikusudia kuishi kwa kutenda walivyotaka na matakwa yao na uwezo viwe katika miliki yao pasipo kuwa na mwanzo wake toka kwa Mweza. Kwa hali hiyo walikosa UTII na kutenda dhambi ya kiburi na ukaidi. MCHUNGUZI: Baada ya kiburi na ukaidi uliowasukuma wanadamu hao kumwasi Muumba wao kwa kutenda alichokataza; aliwafukuza kwenye bustani ya Eden kuwaepusha na ukaidi mwingine wa kuweza kula matunda ya mti wa uzima (Mwa. 3:22b). Ina maana Muumba wa Vyote amewahi kuwa na woga wa jambo lolote? HEKIMA: La hasha; Muumba wa vyote hajawahi na hatawahi kushikwa na woga, ni uwingi wa huruma kwa viumbe vyake ndio uliomsukuma kuwafukuza bustani ya Edeni na kuwapa nafasi ya kujirekebisha. Ili wajirekebishe, Muumba wa wanadamu aliwapa bure/neema ya utashi wa mema na mabaya. Kwa vile Muumba hana kigeugeu kwa neema azitoazo utashi huo alishawapa; kibinadamu yafikirika huenda aliwahurumia wangeutumia utashi huo kuamua kula matunda ya mti huo. MCHUNGUZI:

Yasemekana kuwa kifo ni adhabu mojawapo waliyopewa wanadamu baada ya kutenda dhambi hiyo ya asili (Mwa. 2:17b) ;3:3b; 3:9). Ina maana ya kuwa wanadamu wasingelitenda dhambi wangekuwa hawafi? Yapo masimulizi mengine katika Maandiko Matakatifu yasemayo kifo ni utengano wa roho na mwili. Baada ya kifo roho kwa vile ilitoka kwa Mungu humrudia Mungu; na mwili uliotoka udongoni hurudi kwenye udongo. Bila ya kutenda dhambi ya asili na kuadhibiwa kifo roho ya mwanadamu na mwanadamu mwenyewe angefikaje mbinguni? Nasema hivyo kwa sababu yasemekana pia kwamba pamoja na utengano wa roho na mwili kwenye kifo, kwenye ufufuko roho na mwili vitaungana na kwenda mbinguni baadae. HEKIMA: Kwa mawazo ya kibinadamu unazo hoja nzuri. Hali cha kuwezea kusema ni kwamba baadhi ya masuala ya Muumba ni kumuachia Mwenyewe. Maelezo mengine yaliyo katika Maandiko Matakatifu ni jinsi yalivyoandikwa kumrahisishia mwanadamu kwa lugha ya kibinadamu. Ujuzi finyu wa mwanadamu hujikuta akitafakari yasiyofikirika. Ujuzi finyu huo ni ukomo wa mwanadamu utolewao na Muumba wa vyote katika mamlaka yake yasiyopimika. Kwa suala lako hilo, miye, pamoja na kumwachia Muumba baadhi ya mambo, nagusia kwa ufahamu wa kibinadamu. Unajua, yasemekana ukali na uchungu katika dhambi iliyokisababisha (1 Kor. 15:56). Kifo ni hatua yenye uchungu katika safari ya kwenda mbinguni. Kwa hiyo kifo si kitu chochote bali ni hatua katika safari ya kuondokea huku mwanadamu alikowekwa ili ajirekebishe. Kwa ufupi maoni yangu ni kwamba huenda wanadamu bila ya dhambi ya asili wangalibaki katika bustani ya Edeni na baadaye kuenda mbinguni bila hatua ya kifo walivyoenda kina Eliya (2 Fal. 2:11) na Henoko (Mwa. 5:24).

Isitoshe, pamoja na maelezo yangu hayo hapo juu, swali la kujiuliza ni hili; Hiyo bustani ya Edeni iko wapi kwa leo? Kwa lugha ya unabii kifo kina maono utengano wa milele na Mungu. Kifo kwa maana ya kujitenga milele na Mungu ndiyo hali hasa iliyoletwa na dhambi ya asili. Na kwa maana hii mwanadamu asiyejirekebisha huku alikotupwa ili ajirekebishe atatengana na Muumba wake milele. Hata baada ya ufufuko wa wanadamu wote, walio wakosaji bila kujirekebisha watahukumiwa na kwenda kuishi milele pahala ambako hawatamwona Mungu kamwe. Walio wema wataenda mbinguni kuishi na Muumba wao milele na milele. Inawezekana wanadamu bila ya kutenda dhambi wangeishi milele huko katika bustani ya Edeni na Mungu akiwatembelea mara kwa mara alivyokuwa akifanya kabla ya kuwafukuza huko (Mwa. 3:8) MCHUNGUZI: Mheshimiwa Hekima, naona mjadala wetu utatufikisha mbali. Sasa nakushukuru kwa maelezo yako juu ya UTII. Vile vile nakushukuru na kushika ushauri wako wa baadhi ya mambo ya Muumba kumwachia mwenyewe. Ujuzi wa mwanadamu ni finyu kiasi cha kutokuweza kuyafahamu ya Mweza. HEKIMA: Mheshimiwa Mchunguzi, nakushukuru kwa kukubaliana nami hivyo, Lakini kabla ya kuufunga mjadala huu na kusambaana naomba unisikilize kwa mengine machache ambayo ni mojawapo ya mambo ambamo Mungu hutaka UTII. Huenda kwa akili zako za kibinadamu hukwazika ni kwa nini Muumba kaumba tamaa, hamu na matamanio na kuweka vikwazo mbali

mbali. Maoni yangu ni kuwa tamaa, hamu na matamanio havina ubaya. Kinachotakiwa mwanadamu ukitamani mwombe Muumba akufundishe namna ya kutamani. Si hivyo tu kwa lolote hata ukifurahi mwombe Muumba akufundishe namna ya kufurahi. Ukihuzunika mwombe Muumba akufundishe namna ya kuhuzunika. Ukicheka mwombe Muumba akufundishe namna ya kucheka. Na kwa mengineyo mengi fanya hivyo. Pia usisahau, nikimalizia nilivyoanza; katika kupenda na kutamani upendo na matamanio viliumbwa kwa manufaa maalumu. Wakati ukiwadia kwa cho chote haina ubaya alimradi upo UTII juu yake. Kwa mfano, tamaa, hamu na matamanio baina ya mwanaume na mwanamke hairuhusiki kumwendekeza mwanadamu kuzama katika uasherati; uzinzi na mambo mengine kama hayo. Kwa nini hayo kuwapo? Ni hayo hayo ambayo hata wayatekelezao kwa kanuni na mila zenye UTII huwasaidia kuendelea kuwa pamoja. Bila matamanio yaliyowekwa yawezekana kwa utungu aupatao mke wakati wa kuzaa ungesababisha kutorudia kilichosababisha yote hayo. Matatizo katika uja uzito na utungu ulizidishwa kwa mzazi ikiwa ni sehemu ya adhabu ya dhambi. Pamoja na hayo yote, hamu na matamanio yapo kumwezesha aliyetaabika kumrudia mwenzi (Mwa. 3:16). Ujuzi wa mambo mbali mbali pamoja na kugusia hapo awali, umeumbwa utumike kwa UTII. Yote ni mambo mazuri kwa mwanadamu kujaliwa kujua dawa na sumu bali dosari zaweza kujitokeza kwa uasi katika matumizi. Ujuzi wa utoaji hoja hauna ubaya bali wenye kuwa na ujuzi huo huwahi kutoa hoja za kupingana ya Muumba na Uumbaji wake. Yote hayo humpata aliyeumba vyote. Mojawapo ya lugha za kibantu ina msemo LUSHU lukanchima noji maana yake kisu pia huweza kumkata aliyekinoa. Mwanadamu mwenye kujaliwa akili, fikara kisha kutumia karama hizo kupinga hakuna aliyeziumba. Chukulia fikara za mwamini mageuko (evolution) humcheka aaminie vyote vilivyoumbwa na Muumba. Naye

katika elimu ifunzayo juu ya mageuko huamini vyote vilianza kwa kutokea kwa ugeukaji wa karne nyingi. Cha kushangaza ni kuwa mwana mageuko haamini aliumbwa, lakini pia hoja ifananayo na yake ikitolewa kwake huona ni upuuzi usiopimika; Ati aambiwe ya kwamba radio hiyo haikuundwa na kiumbe bali bati, mimea na madini mbalimbali vilijizoazoa na kukusanyika kwa pamoja na kwa miaka mingi kukatokea kuwapo kwa radio. Kwa hiyo kutengenezwa kwa radio hakupingiki, nako kwaweza kuyakinishwa kwa sayansi na teknolojia. Isisahaulike ya kwamba sayansi na teknolojia havina uthibitisho juu ya imani katika uumbaji wala mageuko. Biblia husema akaviumba vyote kwa aina yake (viume na vike) Mwa. 1:12, 21, 24, 25. Mwanamageuko ana nini cha kuelezea juu ya mpangilio wa vyote; Mageuko yalichukua karne nyingi bila Mratibu (Muumbaji), yalifanyika vipi kwa mpangilio ulivyo. Vingapi kwa wakati mmoja viliufikia ukamilifu vikiwa viwili viwili (kike na kiume). Wakati wa mageuko vilikuwa umbali gani kutoka kimoja hadi kingine mpaka vikafikia makutano ya kuendeleza vizazi vyake? Iwapo mageuko yalitokea kwa kimoja kimoja, baada ya karne nyingi, cha jinsia moja kiliishi karne ngapi hadi cha jinsia kukamilika na kuendeleza kizazi? Ukamilikaji wakati wa mageuko ulitokea katika sehemu moja na vyenye kukamilika viliishi umbali upi toka cha jinsia moja hadi kingine? Haya ni maswali ya msingi na msomaji asiye na jibu asijisumbue nayo (asiyakumbuke) na kuendelea kusoma. Kujitengeneza kwa radio kupingike bali kujiumba kwa viumbe kusipingike? Yuko aliyetengeneza vitengenezwavyo pia Yuko aliyeviumba viumbe. Mkosa UTII humkosea muumba UTII. Nguvu afya na ulemavu vipo kuwa na wanadamu kwa wakati wake. Ajabu iliyopo ni kwa mwenye nguvu kukosa UTII na kumwonea myonge na kwa mwenye afya kumnyanyasa asiyekuwa nayo, naye mlemavu kuonewa na kuonea kwa kukosa UTII.

Utajiri na ufukara ni hali mbali mbali tofauti ambazo mtu mmoja hawi nazo kwa pamoja. Kwa mwenye kutii huridhika na hali ya maisha aliyo nayo bila kumwonea wivu aliye na hali kinyume na yake. Bali mtu huyo mtiifu hufanya kila liwezekanalo kuondokana na hali aliyo nayo iwapo haimridhishi. Wala kuingia au kutokuingia mbinguni hakuathiriwi na hali mojawapo ya hizo hali mbili. Maelezo yaliyozagaa ni kwamba ni vigumu kwa tajiri kuingia mbinguni kutegemea hali hiyo ikimlevya mwenye kuwa nayo na kugeuka dhulumati. Na pia ni hivyo iwapo njia za dhuluma zilitumika kuiwezesha hali hiyo kuwapo. Ufukara nao siyo hati ya kuingilia mbinguni. Fukara huweza kuwa mbali zaidi na Muumba wake kwa wivu wa wenye kuwa tofauti naye, na pia aghalabu hiushilia kumlaumu Muumba huyo, kwa dhana duni fukara huweza kumwomba Mungu aibadili hali yake bila kujishughulisha kwa lolote, Mwisho wa hayo humlaumu Mungu kwa kutomfanyia aliloomba. Kwa hali hata kuomba kwake huukaribia ukaidi wa kumlazimisha Mungu atekeleze alilomwomba. Katika masimulizi ya ilivyo vigumu kwa baadhi ya matajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni, ukristo haukusudii kutukuza ufukara. Kwa mali ipatikanayo kihalali hata Yesu mwenyewe alikuwa nayo mpaka ikamlazimu kuwa na mweka hazina wake. Yuda Eskarioti, aliyelewa usarifu hadi kumsaliti baadaye kwa tamaa ya sarafu. Elimu juu ya mambo mbalimbali ni ya muhimu kuwa nayo. Elimu pamoja na kuilipia karo na ada mbali mbali, kwa upande wake Mola, hupatikana bure. Ni Mungu amjaliaye mtu kuelimika, kwa maana ingekuwa kazi bure kulipa cho chote kama Mungu hakutoa karama hiyo. Elimu ya mtiifu haina wivu ni elimu ya kufundishana. Ufundishaji huikuza elimu pamoja na ukweli kwamba, katika ngazi fulani ya kuelimishwa pana ushindani wa nafasi darasani kiasi cha wahusika kuacha kufundishana! Huo ni ukweli mchungu juu ya jinsi mitihani iwezavyo kuwazuia kufundishana wenye kufundisha madarasani iwapo

uelewa wao unahitilafiana. Baada ya kuelimika kiasi cha kuridhisha kufundisha wengine ni sawa na kuzalisha talanta mtu aliyokabidhiwa kwa manufaa ya umma. Elimu iliyopatikana ikitumiwa isivyofaa ni matokeo ya mwenye elimu hiyo kutokuwa na utii. Mfano mwingine juu ya UTII kwa muumba, napenda kukupasha ni huu: Kwanza kabisa pana mnong ono umezagaa ya kwamba dhambi ya asili ilikuwa ni Adamu kumjamii Hawa. Mawazo haya, kama ulikuwa nayo, yafute. Kumbuka mwanzo wa mjadala wetu. Jambo hilo lisemwalo kwa minon gono lingalikuwa ndivyo ilivyokuwa Maandiko Matakatifu yangesema bila kuficha. Jambo hilo lilipofanyika Maandiko hayafichi hivyo kusema. Maandiko yanaeleza bayana wakati Adamu amejuana kimwili na Hawa (Mwa. 4:1) Mfalme Daudi akimfariji katika mafiwa/kilio mke aliyempora toka kwa askari wake Uria yasemekana pia alihusiana naye kimwili (2 Sam. 12:24). Na mifano mingine mingi imo katika Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo hata jambo hili la kujamiiana panahitajika UTII, lisifanyike kinyume na makusudio yake Muumba. Kwa kifupi kujamiiana kusifikiriwe kuwa kulianzishwa na kina Adamu na Hawa na hakukuwapo kabla ya dhambi ya asili? La hasha; vinginevyo pia ya kwamba hao wanadamu ndio waliowafunza hayawani na wadudu juu ya kujamiiana. Nasisitiza; wanadamu kwa kitendo chao cha ndoa huwa hawamkosei Mungu, aliwaumba na kuwapa uwezo huo ili kuzaana na kuongezeka (Mwa.1:28) alimradi watafanya hivyo kwa adabu na UTII. Utii umekosekana katika masuala yahusianayo na kitendo halali cha wenye ndoa kiasi cha kugeuka machukizo kwa Bwana kitendekapo nje ya ndoa. Kimegeuzwa uasharati na uzinzi aina aina. Kimegeuka mauaji! Jifikirie mwenyewe kama ungemkuta mwanamke wa heshima zake akimwambia binti wa miaka 18, yafuatayo Binti yangu mpenzi, mbona umekaa mda wote huu bila ya kukosea lolote ; Hujanikosea mimi mama yako wala mtu mwingine ye yote na umekuwa kama haupo kwa

kukosa dosari. Kwa hali hiyo naamua kukuulia mbali, sitaki kuwa na binti asiyekuwa na kosa lolote. Ntakuua. Kitendo cha mama kama huyo kingelaaniwa na kila mwanadamu mwenye akili timamu. Na kama angeelekea kuichukua hatua ya kumvamia binti yake haikosi binti huyo angefanya kila njia ya kumkimbia mama yake ili kujisalimisha. Bahati yake binti huyu katika umri wake wa kuweza kujisalimisha asidhuriwe na mama yake mwendawazimu. Mauaji ya namna hiyo ya asiyekuwa na hatia, yametapakaa pahala pengi duniani. Na kwa kukosa UTII baadhi ya serikali za dunia hufikiri kuyahalalisha! Ole wao wanadamu wamekigeuza kitendo cha ndoa kifanyike kinyume na kilivyokusudiwa na Muumba. Burudani imekuwa muhimu zaidi kuliko kuzaana na kuongezeka (Mwa. 1:28). Bila utaratibu mzuri kitendo kiwapasacho wenye ndoa hufanyika kiholela na kuwa chanzo cha mauaji ya wasiokuwa na hatia. Nafuu ya binti aliye kwenye mfano hapo juu, ya katika hali ya kuweza kujitetea angalau kumkimbia mama yake muuaji. Uwezo huo wa kujitetea hanao binti ambaye bado apiga mbizi katika maji ya mfuko wa uzazi wa mama anayejikuta kamwagwa mwa katika kitendo cha utoaji mimba bila UTII. Mamlaka za dunia zinazoruhusu utoaji mimba kiholela zinaruhusu pia mama kama aliye kwenye mfano huu, anayeamua kumuua binti yake mtiifu mwenye umri wa miaka kumi na minane? Ni wazimu ulioje! Kukubaliana na mama huyo kumuua binti yake mkubwa vile ni sawa na uamuzi wa kutoa mimba aliouchelewesha. Amri ya Mungu isemayo Usiue na izingatiwe kwa UTII. Mwimbaji mmoja aliimba Sweetest taboo

Baada ya kusema hayo, Imani bin Hekima akamwona msikilizaji wake katulia tuli na dalili za lepe la usingizi likimwinda. Hapo hapo, pamoja na hamu yake ya kutaka kuendelea aliamua kumshukuru msikilizaji wake kwa kukubaliana katika mjadala wao. HEKIMA Mjuaji bin Mchunguzi, nashukuru sana kwa kukubaliana nami juu ya suala la UTII kwa Mungu. Nakuomba pia kuzingatia mifano yangu niliyoiongezea. Mjadala wetu umefungwa. Msikilizaji mtulivu, Mjuaji bin Mchunguzi, alikuwa amekaa na kuinua kichwa kidogo na mikono kaikunja na kuiweka mezani mfano wa kuandika namba saba (7) mbili zinazotazamana na kuingiliana. Akatabasamu. Akaukubali ufungaji wa mjadala. MCHUNGUZI: Umefungwa. Mungu hutaka UTII. Omunia munda mundi. Kwa heri ya kuonana

NYONGEZA A: Ufuatano wa mapapa kuanzia Petro hadi Yohana Paulo II PAPA MWAKA 1. Mt Petro 33 67 2. Mt. Linus 67 76 3. Mt. Cletus (76-88) 4. Mt. Clement 1 (88-97) 5. Mt. Evaristus (97-105) 6. Mt. Alexander I (105-1l5) 7. Mt. Sixtus I (1l5-125) 8. Mt. Telesphorus (125-136) 9. Mt. Hyginus (136-140) 10. Mt. Pius I (140-155) 11. Mt. Anicetus (155-166) 12. Mt. Soter (166-175) 13. Mt. Eleutherius (175-189) 14. Mt. Victor I (189-199) 15. Mt. Zephyrinus (199-217) 16. Mt. Callistus (217-222) 17. Mt. Urban I (222-230) 18. Mt. Pontian (230-235) 19. Mt. Anterus (235-236) 20. Mt. Fabian (236-250) 21. Mt. Cornelius (251-253) 22. Mt. Lucius I (253-254) 23. Mt. Stephen I (254-257) 24. Mt. Sixtus I1 (257-258) 25. Mt. Dionysius (256-268) 26. Mt. Felix I (269-274) 27. Mt. Eutychian (275-283) 28. Mt. Caius (283-296)

29. Mt. Marcellinus (296-304) 30. Mt. Marcellus I (308-309) 31. Mt. Eusebius (309) 32. Mt. Miltiades (31l-314) 33. Mt. Sil Vester I (314-335) 34. Mt. Mark (336) 35. Mt. Julius I (337-352) 36. III (352-366) 37. Mt. Damasus I (366-384) 38. Mt. Siricius (384-399) 39. Mt. Anastasius I (399-401) 40. Mt. Innocent I (401-417) 41. Mt. Zosimus (417-418) 42. Mt. Boniface I (418-422) 43. Mt. Celestine I (422-432) 44. Mt. Sixtus III (432-440) 45. Mt. Leo I (440-461) 46. Mt. Hilarus (461-468) 47. Mt. Soter (468-483) 48. Mt. Felix III (483-492) 49. Mt. Gelasius I (492-496) 50. Anastasius II (496-498) 51. Mt. Symmachus (498-514) 52. Mt. Hormisdas (514-523) 53. Mt. John I (523-526) 54. Mt. Felix IV (526-530) 55. Boniface II (530-532) 56. John II (533-535) 57. Agapitus I (535-536) 58. Mt. Silverius (536-537)

59. Vigilius (537.555) 60. Pelagius I (556-561) 61. John III (561-574) 62. Benedict I (575-579) 63. Metropolis 2 (579-590) 64. Mt. Gregory I (590-604) 65. Sabinian (604-606) 66. Boniface III (607) 67. Mt. Boniface IV (608-615) 68. Mt. Adrian (615-618) 69. Boniface V (619-625) 70. Honorius I (625-638) 71. Severinus (640) 72. John IV (640-642) 73. Theodore I (642-649) 74. Mt. Martin I (649-655) 75. Mt. Eugene I (654-657) 76. Mt. Vitalian (657-672) 77. Adrian 2 (672-676) 78. Donus (676-678) 79. Mt. Agatho (678-681) 80. Mt. Leo II (682-683) 81. Mt. Benedict II (684-685) 82. John V (685-686) 83. Conon (686-687) 84. Mt. Sergius I (687-701) 85. John VI (701-705) 86. John VII (705-707) 87. Sissinius (708) 88. Constantine (708-715)

89. Mt. Gregory II (715-731) 90. Mt. Gregory III (731-741) 91. Mt. Zacharias (741-752) 92. Stephen II (752-757) 93. Mt. Paul I (757-767) 94. Stephen III (768-772) 95. Hadrian I (772-795) 96. Mt. Leo III (795-816) 97. Stephen IV (816-817) 98. Mt. Paschal I (817-824) 99. Eugene II (824-827) 100. Valentine (827) 101. Gregory IV (827-844) 102. Sergius II (844-847) 103. Mt. Leo IV (847-855) 104. Benedict III (855-858) 105. Mt. Nicholas (858-867) 106. Hadrian II (867-872) 107. John VIII (872-882) 108. Marinus I (882-884) 109. Mt. Hadrian III (884-885) 110. Stephen V (885-891) 111. Formosus (891-896) 112. Boniface VI (896) 113. Stephen VI (896-897) 114. Roman (897) 115. Theodore II (897) 116. John IX (898-900) 117. Benedict IV (900-903) 118. Leo V (903)

119. Sergius III (904-91l) 120. Anastasius III (91l-913) 121. Country (913-914) 122. John X (914-928) 123. Leo VI (928) 124. Stephen VII (928-931) 125. John XI (931-935) 126. Leo VII (936-939) 127. Stephen VIII (939-942) 128. Marinus II (942-946) 129. Agapitus II (946-955) 130. John XII (955-964) 131. Leo VIII (963-965) 132. Benedict V (964-966) 133. John XIII (965-972) 134. Benedict VI (973-974) 135. Benedict VII (974-983) 136. John XIV (983-984) 137. John XV (985-996) 138. Gregory V (996-999) 139. Silvester II (999-1003) 140. John XVII (1003) 141. John XVIII (1004-1009) 142. Sergius IV (1009-1012) 143. Benedict VIII (1012-1024) 144. John XIX (1024-1032) 145. Benedict IX (1032-1044) 146. Silvester III (1045) 147. Benedict IX (1045) 148. Gregory VI (1045-1046)

149. Clement II (1046-1047) 150. Benedict IX (1047-1048) 151. Damasus II (1048) 152. Mt. Leo IX (1049-1054) 153. Victor II (1055-1057) 154. Stephen IX (1057-1058) 155. Nicholas II (1059-1061) 156. Alexander II (1061-1073) 157. Mt. Gregory VII (1073-1085) 158. Mwenyeheri. Victor III (1086-1087) 159. Mwenyeheri. Urban II (1088-1099) 160. Paschal II (1099-1118) 161. Gelasius II (1118-1119) 162. Callistus II (1119-1124) 163. Honorius II (1124-1130) 164. Innocent II (1130-1143) 165. Celestine II (1143-1144) 166. Lucius II (1144-1145) 167. Mwenyeheri. Eugene III (1145-1153) 168. Anastasius IV (1153-1154) 169. Hadrian IV (1154-1159) 170. Alexander III (1159-1181) 171. Lucius III (1181-1185) 172. Urban III (1185-1187) 173. Gregory VIII (1187) 174. Clement III (1187-1191) 175. Celestine III (1191-1198) 176. Innocent III (1198-1216) 177. Honorius III (1216-1227) 178. Gregory IX (1227-1241)

179. Celestine IV (1241) 180. Innocent IV (1243-1254) 181. Alexander IV (1254-1261) 182. Urban IV (1261-1264) 183. Clement IV (1265-1268) 184. Mwenyeheri. Gregory X (1272-1276) 185. Mwenyeheri. The Innocent (1276) 186. Hadrian V (1276) 187. John XXI (1276-1277) 188. Nicholas III (1277-1280) 189. Martin IV (1281-1285) 190. Honorius IV (1285-1287) 191. Nicholas IV (1288-1292) 192. Mt. Celestine V (1294) 193. Boniface VIII (1294-1303) 194. Mwenyeheri. Benedict XI (1303-1304) 195. Clement V (1305-1314) 196. John XXII (1316-1334) 197. Benedict XII (1335-1342) 198. Clement VI (1342-1352) 199. Innocent VI (1352-1362) 200. Mwenyeheri. Urban V (1362-1370) 201. Gregory XI (1371-1378) 202. Urban VI (1378-1389) 203. Boniface IX (1389-1404) 204. Innocent VII (1404-1406) 205. Gregory XII (1406-1415) 206. Martin V (1417-1431) 207. Eugene IV (1431-1447) 208. Nicholas V (1447-1455)

209. Calixtus III (1455-1458) 210. Pius II (1458-1464) 211. Paul II (1464-1471) 212. Sixtus IV (1471-1484) 213. Innocent VIII (1484-1492) 214. Alexander VI (1492-1503) 215. Pius III (1503) 216. Julius II (1503-1513) 217. Leo X (1513-1521) 218. Hadrian VI (1522-1523) 219. Clement VII (1523-1534) 220. Paul III (1534-1549) 221. Jules III (1550-1555) 222. Marcellus II (1555) 223. Paul IV(1555-1559) 224. Pius IV (1560-1565) 225. Mt. Pius V (1566-1572) 226. Gregory XIII (1572-1585) 227. Sixtus V (1585-1590) 228. Urban VII (1590) 229. Gregory XIV (1590-1591) 230. Innocent IX (1591) 231. Clement VIII (1592-1605) 232. Leo XI (1605) 233. Paul V (1605.1621) 234. Gregory XV (1621-1623) 235. Urban VIII (1623-1644) 236. Innocent X (1644-1655) 237. Alexander VII (1655-1667) 238. Clement IX (1667-1669)

239. Clement X (1669-1676) 240. With. Innocent XI (1676-1689) 241. Alexander VIII (1689-1691) 242. Innocent XII (1691-1700) 243. Clement XI (1700-1721) 244. Innocent XIII (1721-1724) 245. Benedict XIII (1724-1730) 246. Clement XII (1730-1740) 247. Benedict XIV (1740-1758) 248. Clement XIII (1758-1769) 249. Clement XIV (1769-1774) 250. Leo 6 (1775-1799) 251. Pius VII (1800-1823) 252. 12 Riley (1823-1829) 253. Pius VIII (1829-1830) 254. Gregory XVI (1831-1846) 255. Pius IX (1846-1878) 256. 13 Riley (1878-1903) 257. Mt. Pius X (1903-1914) 258. Benedict XV (1914-1922) 259. 11 Paul (1922-1939) 260. 12 Paul (1939-1958) 261. Mwenyeheri. John XXIII (1959-1963) 262. Paul VI (1963-1978) 263. John Paul I (1978) 264. Mt. Yohani Paul II (1978-2005) 265. Benedict XVI (2005-2013) 266. Francis (2013-

Habari za Mwandishi Mwandishi Alphonse Shija Mahuyemba, alianza kufuata mafundisho ya kikristu mnamo mwaka 1967. Tarehe 11/4/1960 alibatizwa katika madhehebu ya Katoliki huko Kasamwa parokia ya Geita. Alihitimu elimu ya msingi katika shule ya Bulela, elimu ya sekondari sekondari alimalizia shule ya Sekondari ya Nsumba. Ana stashahada ya Range Management toka A.H.I.T.I Kabete Kenya, Stashahada ya Ranch Management ya M.A.T.I Morogoro. Baadaye alipata elimu ya juu kwa kupata shahada ya kwanza katika kilimo (B.sci. Agric.) toka chuo kikuu cha Dar es Salaam (Morogoro) na shahada ya uzamili (M. Agr. Sc.) aliipata toka chuo Kikuu cha Lincoln nchini New Zealand. Ndugu Mahuyemba amewahi kufanya kazi ya ushauri wa ufugaji wilayani Kondoa, mkoa wa Dodoma, baadaye alikuwa mkufunzi katika idara ya Range management LTI Morogoro. Baada ya hapo alikuwa Naibu Afisa Mifugo (M) mkoani Mtwara. Ameufanya uandishi huu akiwa Meneja wa shamba Kituo cha kuzalisha Mitamba cha Kahama mkoani Shinyanga, Tanzania. Wakati huo huo akiwa Naibu Mwenyekiti wa Kigango Katoliki cha Seeke/Zongomela, Kahama. Baadae alifanya kazi kama Afisa Mifugo wilayani Kahama na Mkoani Shinyanga. Mwandishi kwa sasa ni mstaafu na anajishughulisha na kilimo na uandishi mbalimbali.