JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Similar documents
HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

ARCHDIOCESE OF MWANZA

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

Human Rights Are Universal And Yet...

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Early Grade Reading Assessment for Kenya

MUONGOZO WA UTUNZAJI WA URITHI WA UTAMADUNI 1 SECURITY AT MUSEUMS

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Upande 1.0 Bajeti yako

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

United Pentecostal Church June 2017

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

PDF created with pdffactory trial version

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Deputy Minister for Finance

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Ufundishaji wa lugha nyingine

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MOJA. Kikao cha Hamsini na Tatu Tarehe 19 Juni, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Transcription:

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS-TAMISEMI Namba za Simu Mkuu wa Shule: 0742 770 656 Makamu Mkuu wa Shule: 0767 312 266 Matron: 0766 464 076 Shule ya Sekondari Nsimbo, S.L.P.304, MPANDA. Kumb. Na. NDC/NSS/JI/A.L/02 15/05/2018. Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi S.L.P... YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO SHULE YA SEKONDARI NSIMBO, HALMASHAURI YA NSIMBO, MKOA WA KATAVI MWAKA 2018. Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika shule hii mwaka 2018 Katika tahasusi ya Shule yetu ni ya bweni na ni ya wasichana, ipo katika Halmashauri ya (W) Nsimbo mkoa wa Katavi. Tafadhali wahi kufika maana ukichelewa zaidi ya wiki tatu (3) nafasi itachukuliwa na mwanafunzi mwingine. Shule itafunguliwa muhula wa kwanza tarehe 02/07/2018. Hongera kwa kuchaguliwa katika Shule hii, nakutakia maandalizi mema na safari njema. Karibu Nsimbo Sekondari. Karibu Katavi. BEATRICE A. MWALUGAJA MKUU WA SHULE 1

YAFUATAYO NI MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE HII AMBAYO NI MUHIMU KUZINGATIA: A. USAFIRI Kila mwanafunzi atajitegemea kwa usafiri. Kwa wanafunzi kutoka Tabora kuja Mpanda (Katavi) kuna usafiri wa treni (gari moshi) na Mabasi, usafiri wa gari moshi toka Tabora kuja Mpanda (Katavi) upo kila Jumatatu, Jumatano na Jumamosi na kufika Mpanda Jumanne, Alhamisi na Jumapili. Pia kuna usafiri wa mabasi kila siku. Usafiri wa kutoka Mbeya hadi Mpanda (Katavi) ni wa mabasi, unapatikana kwa mabasi ya Mbeya Express, Katavi tours, Ndenjela Epress na Mugumo Express kila siku. Na usafiri toka Kigoma ni wa mabasi, unapatikana kwa basi la Adventure Connection na Saratoga Line kila siku. Ukifika Mpanda: I. Kutoka stesheni ya gari moshi shule iko mashariki umbali wa km 12 ukipiti barabara ya Mpanda Tabora. II. Kutoka kituo cha mabasi (stand kuu) shule iko mashariki umbali wa km 12 ukipitia barabara ya Mpanda Tabora. NB: Ili kukusisitiza usafiri wa kutoka Mpanda kuja shuleni usafiri ni wa daladala na bodaboda na uwaambie wakuteremshe Mtakuja maarufu TANKI REFU. III. Ukitokea Tabora kwa njia ya barabara huna haja ya kufika Mpanda mjini ukishaingia Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo waambie wakuteremshe Tanki refu. B. VITU MUHIMU VYA KUJA NAVYO; 1. SARE ZA SHULE a) Kila mwanafunzi aje na Tsh. 32,000/= kwa ajili ya kitambaa na mashono ya sketi mbili za darasani na sh. 16,000/= sketi ya kushindia. NB: Si jukumu la shule kushona sare za wanafunzi, mwanafunzi husika ataelekezwa kwa mtu aliyeteuliwa na shule kwa kazi hiyo. Utaratibu huu umewekwa ili wanafunzi wawe na sare zinazofanana. Wanafunzi wote watashona sketi ndefu. Kama mzazi utaamua kumshonea mwenyewe na rangi au mshono ukawa tofauti na shule, basi mzazi utalazimika kumshonea sare nyingine. b) Shati nyeupe mbili 2 za mikono mirefu zisiwe na urembo wa aina yoyote, uvaaji wa shati utaambatana na hijab nyeupe kwa wanafunzi wa kiislam. c). Sweta ya shule rangi dark - blue ya kawaida Sh. 13,500/=. d). Viatu vya ngozi nyeusi vyenye kisigino kifupi vya kufunga kamba jozi 2. e). Soksi fupi nyeupe jozi mbili na nyeusi jozi mbili. f). Raba kwa ajili ya michezo nyeusi/dark blue jozi 2. g). Aje na shilingi 13,000/= kwa ajili ya T-shirt ya shule 2

h). Track suit jozi moja kwa ajili ya kuvaa usiku wakati wa maandalio ya usiku/michezo, rangi ya dark blue 30,000/= i). Aje na T-shirt ya njano ambayo haina maandishi yeyote kwa ajili ya michezo. j). Tai ya rangi ya Dark blue **Malipo haya yote yawekwe kwenye Akaunti ya shule, 61910022051 NSIMBO SEC SCHOOL FUND Benki ya NMB** NB: MWANAFUNZI HARUHUSIWI KUJA NA MAVAZI YA AINA YEYOTE ZAIDI YA SARE ZILIZOTAJWA HAPO JUU II. ADA NA MICHANGO MUHIMU YA SHULE a) Ada ya shule ni elfu sabini (Sh. 70,000/=) inaruhusiwa kulipa nusu yaani elfu thelathini na tano (Sh. 35,000/=) kwa kila muhula. Mwanafunzi atakaye fika shuleni bila ada atarudishwa nyumbani. b) Sh. 5,000/= kwa ajili ya tahadhari c) Sh. 6,000/= kwa ajili ya kitambulisho na picha d) Sh. 20,000/= kwa ajili ya taaluma e) Sh. 30,000/= kwa ajili ya vibarua (walinzi, wapishi n.k) f) Sh. 2,000/= kwa ajili ya nembo ya shule g) Sh. 15,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani h) Sh. 40,000/= kwa ajili ya Mitihani ya Utamilifu (Mock) Mkoa. i) Aje n ash 10,000/= kwa ajili ya mahafali j) Aje na pesa sh. 10,000/= kwa ajili ya huduma ya kwanza pesa hiyo haitarudishwa. NB: Ni vema mwanafunzi aje na bima ya Afya ya Taifa kwa ajili ya matibabu. Michango yote tajwa hapo juu kipengele II a j inatakiwa kulipwa benki, mwanafunzi aje na bank pay in slip (stakabadhi ya malipo ya benki) hakuna pesa ya mwanafunzi itakayo pokelewa shuleni. Michango hiyo pamoja na ada ilipwe kwenye akaunti namba 61910022051 ya NSIMBO SEC SCHOOL FUND katika benki ya NMB Tawi la Mpanda. Benki ya NMB ipo kila makao makuu ya Wilaya unaweza kulipa katika tawi lolote lile la NMB. 3

NB: NYUMA YA BENKI PAY IN SLIP UANDIKWE MCHANGANUO WA MALIPO HUSIKA HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYE POKELEWA BILA BENKI PAY IN SLIP (NAKALA YA STAKABADHI YA MALIPO YA BENKI) III. MALAZI a) Godoro la sponge 2.5 x6 Na lisiwe nene sana (hakuna magodoro ya kukodisha) b) Shuka jozi mbili rangi ya Pinki. c) Mto na foronya ya rangi ya Pinki. d) Blanketi moja/shuka moja nzito e) Aje na chandarua nyeupe pembe nne. f) Taulo g) Doti ya khanga au kitenge. h) Nguo za ndani za kutosha j) Pedi IV. VITENDEA KAZI a) Ream ya karatasi (1 kwa mwaka) b) Jembe moja lenye mpini na fyekeo c) Fagio 1 (hard bloom na soft bloom) d) Mathematical set, pencel, rula n.k. e) Ndoo 2 za plastiki (Kuogea na kutunzia maji ya kunywa) lita 20 na lita 10. f) Fagio ngumu aina ya chelewa (1) g) Mwanafunzi wa sayansi (PCB) na (CBG) Aje na dissecting kit, scientific calculator, stop watch, tray, laboratory coat, kwa mwanafunzi wa PCM aje na laboratory coat, scientific calculator na stop watch na kwa mwanafunzi wa HGE na EGM waje na scientific calculator. h) Madaftari makubwa (Quire three) yasiyo pungua kumi (10) V. TAALUMA Kwa sababu shule ina uhaba wa vitabu, ikiwezekana ni vizuri aje na vitabu vitakavyo msaidia kwa masomo husika 4

A. VITABU VYA KEMIA 1. BYS. Chand conceptual chemistry for class XI and XII 2. BY Tanzania institute of education ADVANCED LEVEL INORGANIC CHEMISTRY part I and II 3. Advanced chemistry review (2000) (2012) Paper I & II 4. Advanced Chemistry (Michael Ramsden) B. VITABU VYA BIOLOJIA 1. Taylor at el (1999) biological science, third edition. Tong printing press hong kong 2. Genn and Tods (1999) Understanding biology 4th Ed. Stanley Thomes Ltd UK. 3. MODERN BIOLOGY SECOND EDITION 4. FUNCTIONAL APPROACH 5. ADVANCED BIOLOGY BY MICHAEL KENT SECOND EDITION C. VITABU VYA PHYSICS: 1. S. CHAND conceptual physics XI na XI 2. NELKON AND PARKER 3. RAMSDEN PHYSICS 4. UNIVERSITY PHYSICS (UP) 5. PHYSICS FOR SECONDARY SCHOOL FORM FIVE & SIX (TIE 2016) 6. TOM DUNCAN, PRINCIPLE OF PHYSICS. D. VITABU VYA GEOGRAPHY 1. Pritchard J.M. (1979), Afrika a study Geography for advanced students. London longman. 2. Msabila D.T (2003) Success in Geography Climatology and Soil science Dar es salaamafroplus industries L.T.D 3. Prichard J.M. (1990) Practical Geography for Africa. Longman. 4. Kamili, 2, Physical Geography for Africa. Dar es salaam Afroplus industries. 5. Msabila D.T. Physical Geography. Dar es salaam, Nyambari Nyangwine Publishers. 5

6. Msabila D.T. (2006) Human and Economic Geography (Advaced level paper 2.) Nyambari Nyangwine publishers. E. VITABU VYA BASIC APPLIED MATHEMATICS (BAM) 1. Basic Applied Mathematics for secondary school 2. Basic Applied Mathematics Review 3. Basic Applied Mathematics (TIE) F. VITABU VYA ECONOMICS 1. Ambilikile C.M (2010) Economics for Advanced Level (Part I&II) 2. Gupta S.L and Chaturved D.D (2003) Managerial Economics, Texts and Cases 3. Othieno Okoth (2005), Contemporary Economics 4. Mudida R (2003) Modern Economics 1st Ed. Nairobi Kenya G. VITABU VYA GENERAL STUDIES (GS) 1. Richard R.F Mbalase, General Studies For Advanced Level Certificate 2. Mgaywa, B.M General Studies for Advanced Level, 3rd Ed 3. Joannes, B & S.M Deogratias Understanding Advanced Level General Studies; Advanced Secondary School Education H. VITABU VYA ADVANCED MATHEMATICS 1. S. CHAND, ADVANCED MATHEMATICS I & II 2. PURE MATHEMATICS I & II 3. TRANTA ADVANCED MATHEMATICS VI. VYOMBO VYA CHAKULA a) Sahani na kijiko b) Kikombe na Bakuli VII. MWANAFUNZI LAZIMA AJE NA RESULTS SLIP YA MATOKEO YAKE YA KIDATO CHA NNE NA CHETI CHA KUZALIWA ORIGINAL SIO KIVULI ASIPOKUJA NAYO HATAPOKELEWA C. FOMU ZIFUATAZO ZIMEAMBATANISHWA NA NIMUHIMU KUZIKAMILISHA 6

1. Historia ya wazazi na mtoto 2. Kukubali kujiunga na shule 3. Fomu ya kupima Afya (medical examination) TAFADHALI NI MUHIMU SANA KUPIMA AFYA YAKO NA KUJA NA VYETI ILI KUONDOA USUMBUFU MWISHO Shule hii inathamini Umoja, amani na juhudi katika masomo na kazi za nje pamoja na michezo. Nidhamu safi ni msingi wa mafanikio ya kila binadamu, hivyo kila atakaye kubali kujiunga na shule hii atatakiwa kuzingatia maelekezo hayo. Sheria za shule zimeambatanishwa, zisome kwa makini na uwe tayari kuzifuata. BEATRICE A. MWALUGAJA MKUU WA SHULE 7

KIAMBATA A JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO Kumbukumbu Namba: SHULE YA SEKONDARI NSIMBO HISTORIA YA WAZAZI NA MTOTO ALIYE CHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE HII A. WAZAZI/WALEZI 1. Jina la Baba.....Hai/Si hai 2. Jina la Mama Hai/ Si hai 3. Kama Baba si hai jina la Mlezi.. 4. Kazi/shughuli ya Mzazi/Mlezi.... 5. Anwani ya Mzazi/Mlezi... 6. Uraia wa Wazazi -Baba mtanzania/si mtanzania -Mama mtanzania/si mtanzania 7. Wakati wa likizo Mtoto/Mwanafunzi unatakiwa uende wapi?. 8. Jina la mtu aendako... Uhusiano na Mtoto/Mwanafunzi SAHIHI YA BABA/MAMA/MLEZI TAREHE SAHIHI YA MWANAFUNZI. TAREHE. PICHA YA MZAZI/MLEZI PICHA YA MWANAFUNZI 8

KIAMBATA B FOR MEDICAL EXAMINATION To be completed by medical officer in respect to all forms of entrants Student s full name Age.Years.Sex... Blood count (red and white).. Stool examination.... Urine analysis. Syphilis and other venereal disease test. T.B test...... Eye Test.... Ears...... Abdomen Urine for plant test. Test for pregnancy. ADDITIONAL INFORMATION Defects, impotents (e.g. arms, legs etc) infections, chronic or family diseases etc.. I certify that the named above is fit to pursue further studies in agricultural/domestic education Station signature.. Date designation. 9

KIAMBATA C JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO SHULE YA SEKONDARI NSIMBO FOMU YA KUKUBALI KUJIUNGA NA SHULE Mimi.nimesoma kwa makini maagizo yote ninatambua kuwa kuchaguliwa kwangu kuingia shule ya sekondari ni bahati na zawadi kubwa kwa kuwa wengi wamekosa nafasi si kwa kuwa wameshindwa ila kwa sababu ni chache. Hivyo nakubali kujiunga na shule yasekondari Nsimbo ya Wasichana. Nitatii na kufuata sheria na taratibu zote za shule. Nitajitahidi kufanya kazi/kusoma kwa juhudi na maarifa na nitajitahidi kushirikiana na wenzangu kweli daima. Nitalinda hadhi/heshima ya shule ya Sekondari Nsimbo na nitashirikiana na wenzangu kujenga misingi na historia nzuri ya shule. Tarehe Sahihi ya mwanafunzi.. Mimi.. Mzazi/Mlezi..... Nimeshuhudia mtoto wangu. akikubali kwa hiari kujiunga na shule hiyo ninaamini mtajitahidi kumfunza na kumlea vizuri. Mimi pia naahidi kushirikiana nanyi kikamilifu katika kumlea binti yangu naamini tutakuwa tunawasiliana. Tarehe.. Sahihi ya Mzazi/ Mlezi.... 10

KIAMBATA D JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO SHULE YA SEKONDARI NSIMBO SHERIA ZA SHULE MIPAKA YA SHULE Mwanafunzi haruhusiwi kutembelea vijiji jirani wala kwenda mjini bila kupata kibali cha mkuu wa shule. Mwanafunzi haruhusiwi kwenda kwenye nyumba za wafanya kazi wa shule bila idhini ya mkuu wa shule. Mwanafunzi haruhusiwi kuonekana maeneo ya idara za masomo baada ya saa 12 jioni. MAVAZI RASMI YA SHULE DARASANI Sketi ya Dark blue ndefu shati jeupe la mikono mirefu na hijabu nyeupe kwa wanafunzi wa kiislamu. Viatu vyeusi vya kamba visivyo na visigino virefu na visiwe vya kugonga Soksi nyeupe fupi. KAZINI Mwanafunzi anatakiwa kuvaa sketi ya rangi ya damu ya mzee ndefu na t-shirt, au hijabu nyeupe kwa waislam. MICHEZONI Mwanafunzi awapo michezoni avae traki suti ya rangi ya dark-blue na T- shirt ya njano. NJE YA SHULE Mwanafunzi akiwa nje ya shule avae sketi ya rangi ya damu ya mzee na T- shirt ya rangi ya kijivu yenye nembo ya shule na viatu vyeusi, kwa waisilamu wavae sketi ndefu na hijabu nyeupe. SAFARI Mwanafunzi anapokuwa safarini avae sketi ndefu pamoja na T-Shirt ya shule yenye nembo. 11

UTARATIBU KATIKA BWALO LA CHAKULA Ni muhimu kufuata utaratibu na muda uliopangwa wa kula kufuatana na ratiba ya shule. Kila mwanafunzi awe na sahani, bakuli, kijiko na kikombe. Vyombo hivi vitunzwe bwenini. Wanafunzi wakae mezani wakati wa chakula Wanafunzi hawaruhusiwi kupiga kelele wakati wa chakula Mwanafunzi haruhusiwi kuingia na ndala au kiatu cha wazi ndani ya bwalo la chakula. JIKONI Viranja wa chakula na afya ndio wanao ruhusiwa kuingia jikoni wakati wa chakula. MABWENINI Wanafunzi hawaruhusiwi kulala wawili kitanda kimoja Kila mwanafunzi ni lazima alale katika bweni na chumba alicho pangiwa Wanafunzi hawaruhusiwi kuoga, kutembea mabwenini au nje ya bweni baada ya saa 5:00 usiku Ni marufuku kupiga na kusikiliza muziki bwenini Upotevu/uharibifu wowote wa mali ya umma bwenini utalipwa na wakazi husika wa bweni. Mwanafunzi haruhusiwi kuwepo bwenini wakati wa masomo au wakati ratiba ya shule ikiendelea. Mwanafunzi haruhusiwi kuingia na chakula au kula chakula bwenini Kila mwanafunzi azingatie usafi wa bweni siku zote na siku maalumu za usafi DARASANI Wanafunzi wawe madarasani mnamo saa moja na dakika ishirini na tano asubuhi. Mwalimu anapo ingia darasani wanafunzi wasimame na kumuamkia mwalimu. Wanafunzi wasipige kelele wawapo darasani Wanafunzi wasitoke nje ya darasa wakati wa masomo bila ruhusa maalumu Ni wajibu wa kila mwanafunzi kujibu na kuuliza maswali na kukamilisha kazi alizo achiwa na mwalimu wa somo. Usafi wa darasani ni wajibu wa kila mwanafunzi 12

NJE YA DARASA Wanafunzi wasimame na kumsalimia mwalimu au mtu aliye wazidi umri anapo pita. Wanafunzi wawaheshimu wafanyakazi wengine waliopo shuleni kama inavyostahili Wanafunzi watumie lugha ya heshima kwa walimu, watu wengine na hata wao kwa wao. Wanafunzi wawe watii, wasiwe wagonvi, wasengenyaji, wavivu, walevi na wazururaji Wanafunzi wawe na moyo wa kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha Wanafunzi waheshimu bendera ya Taifa na alama zingine za taifa pamoja na ukumbi wa mikutano Mwanafunzi anatakiwa kuongea kiingereza wakati wote awapo shuleni. MATIBABU Wagonjwa wote watatibiwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya pamoja na dispensary ya shule tu. NB: Bima ya Afya ya Taifa ni muhimu kwa ajili ya matibabu au mzazi atalazimika kulipa gharama za matibabu ya motto wake. MAKTABA Wanafunzi hawaruhusiwi kuingia maktaba wakiwa wamebeba mikoba ya vitabu/madaftari Wanafunzi waingie maktaba wakiwa wamevaa vazi rasmi la shule Mwanafunzi haruhusiwi kutoka nje ya maktaba na kitabu au gazeti bila ruksa ya mkutubi au mwalimu mhusika wa maktaba Mwanafunzi ataingia maktaba katika muda maalumu uliopangwa WAGENI Wageni wa aina yeyote ile hawaruhusiwi kuingia au kupita shuleni bila shida maalumu na idhini ya mlinzi wa zamu Wageni wa aina yeyote ile hawaruhusiwi kuonana na mwanafunzi isipokuwa kwa wale wenye shida za kiofisi tu. Maagizo yote ya wageni kwa mwanafunzi au wanafunzi yatapokelewa na mwalimu wa zamu (vyakula na vivywaji pombe na dawa za kienyeji havitapokelewa). 13

HUDUMA ZA OFISI Ofisi ya shule itapokea taarifa za dharura za wanafunzi kama vile msiba au tatizo kubwa la kifamilia pamoja na maagizo yote ya wazazi/walezi kwa mwanafunzi Mwanafunzi haruhusiwi kupiga au kupokea simu bila idhini ya mkuu wa shule Mwanafunzi haruhusiwi kuingia ofisi yoyote shuleni isipokuwa ni lazima wagonge/wapige hodi kabla ya kuingia Barua za wanafunzi zitapokelewa na mwalimu wa zamu ambaye atazikabidhi kwa kiranja wa zamu ili azigawe kwa wahusika MAMBO YASIYO RUHUSIWA KUFANYWA i Uwasherati na uzururaji ii Wizi iii Kuchezea au kuharibu bendera ya Taifa iv Kugoma v Kumpiga au kumtukana mwalimu/mfanya kazi vi Kuharibu kwa makusudi mali ya umma vii Kutoroka shule au kuachana na wenzake wakati anapotoka nje ya shule kwa shughuli za kishule viii Kunywa au kulewa pombe/kuvuta sigara ix Kupigana x Kupiga kelele ovyo au kuita kwa sauti kubwa xi Ubaguzi wa aina yoyote xii Kuzungumza lugha nyingine yoyote isipokuwa kiingereza, Kiswahili kinaruhusiwa katika mazingira maalumu tu xiii Kuvaa mavazi yasiyo sare ya shule xiv Kutofika au kuchelewa sehemu ya parade xv Ni marufuku kwa mwanafunzi kuja na simu, kamera, pamoja na redio shuleni. 14

ADHABU ADHABU ZITATOLEWA KULINGANA NA UZITO NA MAKOSA YALIYOFANYIKA, ISIPOKUWA MWANAFUNZI AKIFANYA MAKOSA YAFUATAYO ATAFUKUZWA SHULE MARA MOJA; I. UASHERATI NA USHOGA II. UZURURAJI III. WIZI IV. ULEVI V. UTORO (KUTOONEKENA ENEO LA ROLL CALL) VI. KULALA NJE YA SHULE VII. UVUTAJI WA BANGI/SIGARA VIII. MAKOSA YA JINAI IX. KUPIGANA AU KUPIGA X. KUHARIBU KWA MAKUSUDI MALI YA UMMA XI. KUDHARAU BENDERA YA TAIFA XII. KUOLEWA XIII. KUPATA MIMBA XIV. KUTOA MIMBA XV. UBAKAJI. XVI. KUGOMA, KUCHOCHEA NA KUONGOZA AU KUVURUGA AMANI NA USALAMA WA SHULE XVII. KUKATAA ADHABU KWA MAKUSUDI XVIII. KUMILIKI AU KUKUTWA NA SIMU YA MKONONI Elewa kuwa si rahisi kutunga sheria za kila kosa linalo weza kufanywa na mwanafunzi. Sheria ni mwongozo wa kumuelewesha mwanafunzi mambo ambayo haruhusiwi kufanya. Kitu muhimu ni kwamba kila mwanafunzi atumie akili yake na busara kuweza kujua namna gani ya kuishi na walimu, wafanyakazi wasio walimu pamoja na wanafunzi wenzake ili kutumia nafasi yake kupitia elimu na kuishi kwa raha na amani katika jitihada za kujiendeleza mwenyewe, shule pamoja na taifa zima kwa ujumla. Kumbuka kuwa umepata bahati kubwa kuwa kati ya wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na shule hii kwa hiyo toa mchango wako katika kujenga msingi imara, sifa na mwenendo mzuri na maendeleo safi kwa shule yako ya Sekondari Nsimbo. ELIMU NI MWANGA WA MAISHA BEATRICE A. MWALUGAJA MKUU WA SHULE 15

16