LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Human Rights Are Universal And Yet...

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

K. M a r k s, F. E n g e l s

If a tree falls - Deforestation in Africa"

Oktoba-Desemba

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

2

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Kiu Cha umtafuta Mungu

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

Upande 1.0 Bajeti yako

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

United Pentecostal Church June 2017

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

2 LILE NENO LILILONENWA

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

2

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Makasisi. Waingia Uislamu

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Ndugu na dada zangu wapendwa,

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

TIST HABARI MOTO MOTO

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

MAANA HALISI IMAAN ( I )

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Cambridge International Examinations Cambridge Ordinary Level

Transcription:

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents Author: Marta Barroso Editor: Thomas Mösch Characters: Narrator 1: female Narrator 2: male Inserts (English): male, (42) Voice ( Passport, please!, No passport?, No passport! ) Intro: Hujambo na karibu kwenye makala ya Noa Bongo Jenga Maisha Yako kuhusu uhamiaji. Katika kipindi hiki tutakueleza kisa cha mwanamume mmoja kutoka Liberia aneishi maisha ya kujificha. Ameishi humu nchini Ujerumani kwa miaka minne sasa. Ijapokuwa amefaulu kufika alikotaka kwenda, lakini mpaka sasa hana uhakika kama uamuzi aliofanya ulikuwa sawa. Tutaona jinsi anavyoishi na wewe msikilizaji utapata kujua zaidi juu ya safari yake kutoka Afrika kuja Ulaya. Kwa sababu hana kibali kinachomruhusu kuishi hapa 1

Ujerumani hatuwezi kulitaja jina lake sahihi katika kipindi hiki. Kwa hivyo tutamwita John. 1. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, motor boat, sea waves, car) 2. Sound Clip John: Ukianza safari kama hii, hufikirii kurudi nyuma. Unafikiria kwenda mbele tu. Hakuna kusimama. 3. Narrator 1: John hakufikiria kuwa safari yake hii itamfanya aishi maisha ya kuwa mhamiaji haramu. maisha ya kuishi chini kwa chini yaani maisha ya kujifichaficha. Kabla hajaanza safari yake, hakufikiria kama siku moja atajikuta kwenye hali kama aliyonayo sasa. 4. Sound Clip John: Ukiona kwenye Televisheni, utadhani kwamba Ulaya ni mahala ambapo mtu anaweza kuwa na maisha mazuri.. ni mahala bora, kwenye raha na mafanikio matupu loo! nimejionea mwenyewe! 5. Narrator 2: Nyumbani, Liberia: John ni mkulima, maisha ni mazuri. Lakini anafikiria kuwa kuna uwezekano wa maisha kuwa mazuri zaidi. Na kufanikisha hilo, anaanza safari ya kilomita 5,300 ambayo inamlazimu kuvuka mipaka saba. Safari yake inamchukua miaka minne. Katika kila nchi anafanya kazi ili kupata fedha za kumwezesha kuendelea na safari yake. 2

6. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, barrier opening, sea waves, car) 7. Narrator 1: Sasa John ametambua kuwa hajafanikisha kile alichoahidiwa na Televisheni. Anaishi na rafiki yake. Anasafisha nyumba na rafiki yake analipa kodi. John anapika lakini hawezi kununua chakula hana fedha hata za kujinunulia viatu na nguo. Kanisa la Kiprotestanti ndio linamsaidia kumpatia chakula na nguo. 8. SFX: War sounds, shootings 9. Narrator 2: Liberia katika mwaka wa 1990 nchi iliyokumbwa na vita: John anaacha kila kitu na anakwenda kuishi kwenye kambi ya wakimbizi iliyo mpakani baina ya nchi yake na Guinea-Conakry. Wakati huu wazo la kutaka kuwa na maisha bora halimtoki akilini. Anapata visa ya kuingia Senegal na hapo anajiunga na watu wengine ambao wana malengo kama yake: Kuondoka Guinea. Hapa ndipo safari yake ilipoanzia. Sound Clip John: Tulipata habari kuwa kuna maajenti, unajua hawa watu wanaohusika na usafirishaji, au uende kwenye uwanja wa magari yanayofanya safari, utawakuta watu wengine huko. Useme tu kuwa unataka kusafiri. Nina nauli na nitasafiri kwa usafiri wa kawadia hadi mahala hapa. 10. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, sea waves, car) 3

11. Sound Clip John: Mwisho wa safari yangu ulikuwa hapa. Hapa kwenye nchi hii, hapa nilipo sasa: Ujerumani. Sasa niko hapa. Swali jingine ni: Itakuwaje? Ninajiuliza kila saa, kama kweli ninataka. 12. SFX: People on the street 13. Narrator 1: Hapa Ujerumani, anajaribu kujumuika na jamii. Lakini haiwezekani. Anahofia kuingia mikononi kwa maofisa wa usalama, hofu hii anayo wakati wote. Akipanda basi au treni anahakikisha kuwa hafanyi kosa lolote litakalomfanya afikishwe mbele ya utawala. Hataki kujulikana. 14. SFX: Mixed sounds of journey (car, sea waves, lorry) 15. Sound Clip John: Unapitia kwenye jangwa la Sahara. Hiyo ni safari ya hatari, unajua, kwa sababu ya joto, vumbi na kila kitu. Lazima uwe umejitayarisha kwa hali yoyote ile itakayokukuta. 16. SFX: Lorry on gravel ground, then fade under 17. Narrator 2: Usafiri huo mara nyingi huwa ni wa Lori, Lori aina ya Mercedes 911, ambalo limebadilishwa na kuwa gari la kubeba abiria. 18. Sound Clip John: Siwezi kusema ni usafiri wa kawaida kwa sababu huwa limebeba wahamiaji haramu (laughs) ( ) Hakuna mtu aliyekuwa na makaratasi halali. 4

19. SFX: Lorry on gravel ground 20. Sound Clip John: Huwa tunawaita pushers. Kwa sababu wanatakikana walete taarifa, mara nyingine inabidi wapate makaratasi ya uongo ili tuweze kupita. 21. Voice: Passport please! 22. SFX: coins falling, barrier opening, car going away (fade under) 23. Narrator 2: Dola 40 hiki ndicho kiwango anachohitaji kuweza kufika Morocco. Pesa hizi ni baadhi ya fedha alizokusanya na kuweka wakati alipokuwa anafanya kazi ya kulima nchini Liberia. Lakini kiasi kikubwa cha fedha hizo hakitumiki kwa ajili ya usafiri 24. Sound Clip John: Inabidi kuwahonga walinzi wa mipakani. Mpaka tutoe rushwa, pesa, pesa ni mpaka tuwahonge hawa askari wa mpakani, unajua ndio tupate kuvuka. Wenye malori na madereva wanajuana na hawa askari wa mpakani vizuri. Kwa hivyo wanawahonga halafu tunapita. 25. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, sea waves) 5

26. Sound Clip John: Makaratasi yangu yote niliyo kuwa nayo, nilipokuwa Morocco, sasa sina hata moja. Kwa sababu yote yametupwa. Nilipokuwa Uhispania sikutakikana kuwa na karatasi yoyote kwa sababu yangepatikana ningerudishwa Morocco. Na huko ningekamatwa. Narrator 1: Kuna watu ambao wanawaita watu walio kwenye hali kama ya John kuwa ni watu wanaoishi kinyume cha sheria. Lakini sio hivyo ni kwa sababu hawana vitambulisho vyenye kuwatambulisha majina, miaka, mahala alipozaliwa mtu huyo au uraia wake. 27. Voice: Passport, please! 28. SFX: heart beating 29. Sound Clip John: Nina hofu kwa sababu ninaishi kinyume cha sheria hapa. Ninaogopa kuulizwa vitambulisho. Ninajitenga sana na shughuli zinazowahusisha watu wengi. Moyo wangu unadunda, yeah. Uso wangu hauonyeshi. Hawawezi kuniona jinsi moyo wangu ulivyo ndani... ninapita bila wasiwasi...kwa sababu ukionyesha wasiwasi usoni...wakikushuku tu basi watataka ujitambulishe. 30. Narrator 1: Mambo mengi yanayotokea kwenye maisha yake kwa sasa yamemkuta bila ya yeye kutarajia. Japokuwa alikuwa na hamu 6

kubwa ya kuja Ujerumani, lakini hakujua mengi kuhusu nchi hii, hata ingawa alipewa ushauri kabla ya kuanza safari yake: Sound Clip John: Kwanza utahitajika kutafuta mwanamke, umuowe ili upate kuishi kwenye nchi hiyo. Utapata makaratasi na hivyo ndivyo utakavyo fanikiwa kupata makaratasi mengine, utapata kila kitu bure, kazi na hata nyumba ya kuishi. 31. SFX: Mixed sounds of journey (car, sea waves, lorry) Fade under 32. Narrator 2: Ni safari ya siku mbili kutoka Senegal mpaka Morocco. Anabeba maji mengi na vitafunio vya Kiafrika, mikate, mfuko wenye nguo na mswaki. Huo ndio ulikuwa mzigo wake. 33. SFX: Lorry on gravel ground - Fade under 34. Sound Clip John: Tulikuwa tunazungumza sisi wenyewe kwa wenyewe, tuliulizana kuhusu kile kitakachotupata. Kuhusu ndoto ulizonazo. Kile utakachofanya Ulaya. Mazungumzo kama hayo. ( ) kwa mfano vile utakavyo weza kuendelea na safari kutoka Morocco, baada ya kufika hapa utafanya nini. Utaishi vipi. 35. SFX: Lorry on gravel ground, then fade out 7

36. Sound Clip John: Nilifikiria kuwa mambo yatakuwa mazuri, shwari na kila kitu kitakwenda vizuri kabisa. Nilidhani kuwa nikifika hapa nitapata kazi kwa urahisi, nitapata kibali cha kuishi. Halafu maramoja nianze maisha mapya. Sio kama ilivyo hivi sasa. 37. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, sea waves, car) 38. Narrator 1: Bila kibali cha kuishi hapa, hakuna njia nyingine ila kuishi chini kwa chini tu. Kwa mujibu wa sheria yeye hayupo hapa Ujerumani, hatambuliki kwa mujibu sheria za nchi. 39. Sound Clip John: Sina marafiki wengi hapa kwa sababu ya hali yangu hii...ninaweza kujiingiza kwenye matatizo. Sina marafiki wengi. 40. Narrator 1: Mara nyingine yeye hutembelea mkahawa wa internet. Huko anakutana na marafiki zake wachache. Anasoma, anapika na mara nyingine anabahatika kupata kibarua cha kutengeneza bustani au kusafisha kwa siku moja au mbili. Bila shaka hiyo ni kazi isiyo halali. Yaani anafanya kazi bila serikali kufahamu kwa hivyo anakwepa kulipa kodi. 8

41. SFX: street traders, then fade under 42. Narrator 2: Rabat: John anajikimu kimaisha kwa biashara ya kuuza nyembe, krimu za kunyolea na vifaa vya kunyolea. Baada ya miezi minane, amefanikiwa kukusanya dola1,600. Nusu ya fedha hizo atazitumia kwa safari ya kuvuka bahari ya Mediterranean. Tena sio kwa kutumia feri ya kawaida 43. SFX: Motor boat, sea waves, then fade under 44. Sound Clip John: Hiyo ni sawa na kujinyonga(laughs). Unaweza kurudishwa mara moja. Maanake huna makaratasi. ( ) Unakutana nao, unajua biashara wanayoifanya. Wanakuita halafu mnakubaliana, lini utakuwa tayari, saa ngapi, unajua. Unalipa halafu basi hapo unakuwa tayari kwa safari. Tulikuwa kama watu 14 hivi na hao pushers wawili jumla tulikuwa kama watu16 hivi. 45. SFX: Sea waves, then fade under 46. Sound Clip John: Tulisafiri baharini usiku, sikumbuki tulisafiri kwa saa ngapi. ( ) sikuwa na hamu ya kujua, kwa sababu wakati wote nilikuwa nimefumba macho yangu. Naomba tu. Unajua!. Kwa sababu sio wote waliofaulu kukamilisha safari. Huwezi kuamini maji. 9

47. SFX: Sea waves, then fade out 48. Narrator 2: Wakati wa safari hiyo ya kuvuka bahari ya Mediterranean, kama anavyokumbuka, askari walinzi wa pwani ya Uhispania walifika na kumuokoa yeye pamoja na wenzake wengine waliokuwa ndani ya mashua ile. Walipelekwa nchi kavu na kuwekwa wote ndani ya nyumba moja ambako walifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kuhojiwa. 49. SFX: typing machine (fade in) 50. Voice: No passport? 53b. SFX: Footsteps running away, then fade under 51. Narrator 2: Hakuna askari, Kwa hivyo John anakaa hapo kwa siku tano halafu anatoroka. Kwa mara ya kwanza maishani mwake anaanza maisha ya barabarani yaani maisha bila makaazi maalum, lakini ni hapa katika mji wa Marbella, nchini Uhispania ambako anaishi kwa mwaka mmoja kukusanya fedha zitakazo mwezesha kumaliza mkondo wa mwisho wa safari yake. 52. Sound Clip John: Nilifanya kazi shambani. Kwenye shamba la nyanya, na pia kwenye shamba la zucchini. Ilinibidi nitumie makaratasi ya mtu 10

mwingine kuweza kupata kazi nzuri. ( ) Ili kujaribu kukusanya fedha za kunifikisha Ujerumani. 53. SFX: Car on street, then fade under 54. Narrator 2: Sehemu ya mwisho ya safari yake ilimgharimu Euro 280. Rafiki wa rafiki yake ndie aliyemfikisha kwa gari hadi katika mji wa Freiburg, nchini Ujerumani. 55. SFX: Car on street, then fade under 56. Narrator 2: Hatimae John amefika Bonn, magharibi mwa Ujerumani. Rafiki yake anaeishi hapa na aliyekuwa anategemea kumuona hapa Ujerumani tangu alipoanza safari yake, hayupo amesafiri, ameondoka nchini wiki mbili kabla yeye kufika. Bila anuani nyingine yoyote na kutokujua lugha ya Kijerumani, bila kazi au mahala pa kuishi na bila mke, mwisho wa safari yake umekuwa maisha ya kujificha. 57. Sound Clip John: Miaka hii yote niliyoishi hapa, sijawa na maisha halisi. Sijapata mafanikio yoyote tangu nilipofika hapa. 58. SFX: Mixed sounds of journey (lorry, sea waves, car) 11

59. Voice: No passport! 60. Outro: Na mpaka hapo ndio tumekamilisha makala ya leo katika Noa Bongo Jenga Maisha Yako, kuhusu uhamiaji. Hadithi hii imeandikwa na Marta Barroso. Iwapo ungetaka kujua zaidi kuhusu maswala ya uhamiaji ya Ujerumani, tembelea mtandao wa idara kuu ya Uhamiaji na maswala ya wakimbizi: anuani yao ni: w w w. b a m f. d e Na ukitaka kukisikiliza tena kipindi hiki au kipingine chochote cha Noa Bongo Jenga Maisha Yako jiunge nasi kwenye mtandao wetu, anuani yetu ni: www.dw-world.de/lbe Baki salama, Kwaheri! 12