JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

Similar documents
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

ARCHDIOCESE OF MWANZA

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Human Rights Are Universal And Yet...

Upande 1.0 Bajeti yako

Early Grade Reading Assessment for Kenya

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010

Deputy Minister for Finance

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Transcription:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI. Namba za simu: SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA, S. L. P 8824, MOSHI. TAREHE... MKUU WA SHULE : 0688 460 242/ 0754 824 621 MAKAMU MKUU WA SHULE: 0787 762 476/ 0715 762 476 PATRON: 0688 406 655/ 0753 096 504 MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI.... S. L. P... YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA HALMASHAURI YA MOSHI MANISPAA. MKOA WA KILIMANJARO MWAKA.. 1. Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule hii mwaka.tahasusi ya PCB Shule ya sekondari Anna Mkapa ipo umbali wa km 3 kutoka stendi kuu ya mabasi ya Moshi Mjini barabara ya kuelekea Pasua.Usafiri wa kutoka stendi ya mabasi Moshi Mjini unapatikana kwa kutumia mabasi ya kwenda Pasua utashuka kituo cha msikitini kwa nauli ya Tsh 400/=.Au stendi ya mabasi ya Moshi Mjini mabasi yatokayo KCMC kwenda Getifonga unashuka kilipo kibao cha shule kituo cha Temere kwa nauli ya shs. 400/=. Muhula wa masomo unaanza tarehe.. Hivyo mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni tarehe. Mwisho wa kuripoti ni tarehe.. 2. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA. 2.1. SARE YA SHULE a) Sare ya shule ni suruali mbili (2) KAKI ziwe na makunjo mawili mbele kila upande na mfuko mmoja nyuma na kunjo la (turn up) chini na suruali zisiwe 1

nyembamba ziwe na inchi kumi na nane (18) na mashati mawili meupe (2) mikono mifupi.(aje nazo ) b) Viatu vyeusi vya ngozi jozi mbili (2) vya kufunga na kamba vyenye visigino vifupi.. c) Soksi nyeusi jozi nne. d) Bukta na fulana ya dark blue na raba kwa ajili ya michezo. e) Sweta ya rangi ya suruali yenye shingo V. f) Nguo za kushindia suruali mbili nyeusi mshono sawa na sare ya shule na fulana (Tshirt) mbili zenye kola na zinapatikana shuleni kwa bei ya shs. 10,000/= moja taslimu. g) Mkanda wa kuvalia suruali wa ngozi mweusi. h) Nguo za kulalia pajama zisizopungua jozi mbili na sweta/ jaketi kwa ajili ya baridi jioni. 2.2:ADA NA MICHANGO YA SHULE a). Ada ya shule kwa mwaka itakuwa shilingi elfu sabini (70,000) kwa mwanafunzi wa bweni.ada hii inaweza kulipwa kwa awamu mbili ambayo ni kiasi cha elfu thelathini na tano (35,000) kwa muhula. b). Michango inayotakiwa kulipwa na kila Mzazi ni: i) Sh. 15,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani. ii) Sh. 5,000/= kwa ajili ya tahadhari (haitarejeshwa) iii) Sh. 6,000/= kwa ajili ya kitambulisho na picha iv) Sh. 30,000/= kwa ajili ya kuwalipa walinzi, wapishi na vibarua wengine. v) Sh. 20,000/= kwa ajili ya taaluma. vi) Sh. 2,000/= kwa ajili ya nembo ya shule. vii) Sh.10,000/= kwa ajili ya matibabu 5,000/= kwa ajili ya huduma ya kwanza na 5,000/= kwa ajili ya bima ya afya kama mwanafunzi ana bima atatoa sh. 5,000/= ya huduma ya kwanza. viii) Sh. 20,000/= kwa ajili ya mitihani ya kujipima mock (kidato cha sita) ix) Mwanafunzi anayelipiwa na Halmashauri au Taasisi yoyote aje na utambulisho wa barua. NB: Fedha zote zilipwe kwenye Akaunti ya shule Na. 40301200141 MMC ANNA MKAPA SECONDARY katika benki ya NMB (Tafadhali andika jiina la mwanafunzi kwenye pay in slip halisi na aje nayo) Fedhas tasslimu hazitapokelewa. C: Mahitaji muhimu ambayo mwanafunzi anatakiwa kuleta shuleni ni; i) Ream moja ya karatasi A4 (photocopy paper) kwa mwaka ii) Dissecting kit kwa wanafunzi wa Biolojia. iii) Scientific calculator. iv) Godoro la sponji (Inch. 3) v) Mashuka jozi 2 rangi ya blue, blanket moja, mto mmoja, foronya mbili rangi ya shuka na chandarua kimoja pembe nne ndogo. vi) Vyombo vya kulia chakula (sahani, kikombe, bakuli na kijiko) 2

vii) Ndoo mbili ndogo zenye mifuniko. viii) Taulo, miswaki, dawa ya meno, ndala, sabuni ya kufulia na kuogea za kutosha. ix) Tochi ya kuchaji kwa mwanga wa jua/betri, mishumaa hairuhusiwi. x) Mabuti, mwavuli au koti la mvua. xi) Lab coat nyeupe. xii) Aje na nakala ya cheti cha kuzaliwa na matokeo ya kidato cha nne (Result slip) xiii) Unatakiwa uje na vifaa vifuatavyo kwa ajili ya usafi: - Dekio aina ya pusher (dryier) ya kusukuma maji -Ufagio mrefu wa chelewa -Jembe 1 lenye mpini 3.SHERIA NA KANUNI MUHIMU ZA SHULE. MAKOSA YAFUATAYO YANAWEZA KUSABABISHA UFUKUZWE SHULE. 1. Wizi. 2. Kutohudhuria masomo kwa zaidi ya siku 90 bila taarifa / utoro. 3. Kugoma na kuhamasisha mgomo. 4. Kutoa lugha chafu kwa mwanafunzi wenzake, walimu, /walezi na jamii kwa ujumla. 5. Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi, kumpiga mwalimu au na mtu yeyote. 6. Kufuga ndevu 7. Kudharau Bendera ya Taifa 8. Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya mfano kuberi, cocaine. 9. Uvutaji wa sigara. 10. Kushiriki matendo ya uhalifu, siasa na matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi. 11. Kusababisha mimba au kumpa mimba msichana. 12. Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni. 13. Kumiliki au kukutwa na simu ya mkononi katika mazingira ya shule au kutumia simu za wafanyakazi, walimu au mtu yeyote. 14 Kufanya jaribio lolote la kujiua au kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k. 15. Uasherati, uhusiano wa jinsi moja, kuoa au kuolewa. 16. Uharibifu wa mali ya umma kwa makusudi. 4. VIFAA VYA MAFUNZO. A. VITABU. Shule haina vitabu Wazazi wawanunulie watoto wao vitabu vya masomo husika. Vichwa vya vitabu vimeambatanishwa. B. VIFAA VINGINE VYA MASOMO. 1. Daftari kubwa yasipungue 7 2. Mathematical set, kalamu za wino, risasi, rula n.k. 3. Vitabu vya ibada kwa mujibu wa madhehebu / dini yako. 5. FEDHA ZA MATUMIZI MADOGO MADOGO (POCKET MONEY). 3

Mzazi anaweza kumpa mwanafunzi kiasi cha fedha cha kuridhisha lakini zitunzwe benki ili kuondoa vishawishi vya wizi. 6. MAMBO MENGINE MUHIMU. i) FOMU ZILIZOAMBATANISHWA. A. Hati ya makubaliano B. Fomu ya uraia C.Fomu ya Uchunguzi wa afya (Medical examination form) ambayo itajazwa na Mganga Mkuu wa hospitali ya serikali. Fomu hii itakabidhiwa kwa Mkuu wa shule mara atakaporipoti shuleni. D. Fomu ya maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi / mkataba wa kutoshiriki katika migomo, fujo na makosa ya jinai. E. Fomu ya usajili wa mwanafunzi. F. Fomu ya ahadi na picha za wazazi /walezi na ndugu wawili. MUHIMU: Tafadhali soma kwa makini maelezo, maelekezo na maagizo haya na kuyatekeleza kikamilifu. KARIBU SANA ANNA MKAPA SEKONDARI.. MKUU WA SHULE ANNA MKAPA SEKONDARI. 4

FOMU A HATI YA MAKUBALIANO. MKUU WA SHULE, SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA, S. L. P 8824, MOSHI. YAH: KUKUBALI KUFUATA SHERIA NA MASHARTI YA SHULE. Mimi.. Nakubali nafasi ya kidato cha..niliyopewa katika shule yako. Ninayakubali masharti na kuwa nitatii sheria za shule hizo zilizoko na zile zitakazotolewa kwa muda wote wa masomo yangu. Naahidi kuwa nitawaheshimu na kuwatii walimu wote wa shule na wafanyakazi kama walezi wangu. Naahidi kuwa nitatii wale wote watakaoteuliwa au kuchaguliwa kuwa viongozi kwa mujibu wa sheria. Naahidi kuwa nitakuwa mwanafunzi mwaminifu na naahidi pia kuwa nitajielimisha kwa nguvu zangu na akili zangu zote kwa manufaa yangu binafsi na Taifa langu kwa ujumla. Natambua kuwa nikikiuka ahadi hizi nitapoteza nafasi yangu hapa shuleni. JINA.. MWANAFUNZI SAHIHI MWANAFUNZI JINA LA MZAZI /MLEZI.. SAHIHI MZAZI / MLEZI /MWANAFUNZI ANWANI YA MZAZI / MLEZI. SIMU... Email. Namba ya kuandikishwa (Admission No.)..Tarehe Darasa ulilopangiwa..bweni. Jina la mwalimu wa malezi..sahihi 5

FOMU B FOMU YA URAIA WA WAZAZI WA MWANAFUNZI. SEHEMU YA MKUU WA WILAYA. Mimi Mkuu wa Wilaya ya. Mkoa.nadhibitisha kuwa wazazi wote wa mwanafunzi. wanao uraia ufuatao: 1. WAZAZI WOTE NI RAIA WA TANZANIA KWA KUZALIWA. i)jina la Baba.. ii)tarehe ya kuzaliwa.. iii)mahali alipozaliwa iv)jina la Mama. v)tarehe. vi)mahali 2. WAZAZI WOTE NI RAIA WA KUJIANDIKISHA. i) Jina la Baba ii) Pasipoti au namba ya kujiandikisha uraia iii) Ilitolewa wapi. iv) Jina la Mama v) Tarehe iliyotolewa vi) Pasipoti au Namba ya kujiandikisha uraia vii) Ilitolewa wapi. viii Tarehe iliyotolewa.. i) MMOJA WA WAZAZI NI RAIA WA KUZALIWA / KUJIANDIKISHA KAMA RAIA WA KUZALIWA. Jina la Baba/Mama.. Mahali alipozaliwa.. AMA RAIA WA KUJIANDIKISHWA. Jina la Baba / Mama... Pasipoti au Namba ya kuandikishwa uraia. Tarehe ya kujiandikisha.. Mzazi asiye raia anatokea wapi.. Ninahakikisha kuwa habari nilizozijaza hapo juu sawa na za kweli SAHIHI... MUHURI WA OFISI NA TAREHE.. 6

FOMU C ANNA MKAPA SECONDARY SCHOOL, P. O. BOX 8824, MOSHI. MEDICAL OFFICER, To be completed by medical officer from a recognized Government Hospital, Name of student.. Blood count (Red and White). Stool examinations.. Sexually Transmitted Diseases... T.B.Skin. Eye test Ears Chest Spleen Abdomen. ADDITIONAL INFORMATION. Physical defects /impairment pediatric disorders. I certify that the above is fit /unfit to pursue studies as stated above. Signature MEDICAL OFFICER DATE.Rubber Stamp NOTE: Student should send or bring the completed form to school together. 7

FOMU D OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA. SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA, S. L. P 8824, MOSHI. MAELEZO BINAFSI YA MWANAFUNZI. 1. Andika majina kamili i)majina ya shule ii)majina ya nyumbani LAKO LA BABA LA MAMA JINA BABA UKOO UMRI TAREHE YA KUZALIWA 2.NYUMBANI. Kijiji/ Mtaa.Kata Tarafa Wilaya.. 3. Anwani ya nyumbani.simu 4. Kukiwa na matatizo taarifa ipelekwe kwa nani (jina) Simu. Uhusiano na wewe. Anafanya kazi gani na wapi 5. Wazazi na ndugu: Baba yuko hai?. Mama yuko hai?. Baba ana watoto wangapi wavulana.wasichana. Wewe ni mtoto wa ngapi?..baba ana wake wangapi?.. Wewe ni mtoto wa mke wa ngapi?.mko wangapi kwa mama huyo? Wewe ni wa ngapi kwa mama huyo? 6. Dini yako.madhehebu UNAOWATEGEMEA. 7.Unaishi na nani na wapi? Simu yake... Nani anayekupa mahitaji ya shule.simu yake. Toa sababu kama siyo Mzazi.. 8

FOMU E OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA S. L. P 8824, MOSHI. TAREHE.. FOMU YA USAJILI WA MWANAFUNZI 1.Jina Kidato cha 2. Kumb.Na.ya barua ya Uhamisho / kupangiwa... 3. Shule alikotoka... 4.Tarehe ya kuingia. 5.MALIPO i) C /Money / Nembo ya shule /Kitambulisho Tshs R/S... ii) Ada ya shule Tshs ERVNo. iii) Matibabu Tshs..R/S.. iv) Taaluma R/S v) Ulinzi /Wapishi na Vibarua vi)ukarabati wa samani.. 6. UKAMILISHAJI WA MAHITAJI: i) Sare ya shule : Amekamilisha / Bado. Anadaiwa. ii) Vifaa vya masomo : Amekamilisha /Bado Anadaiwa. Amekamilisha Ream.. iii) Vifaa vya Bweni : Amekamilisha /Bado Anadaiwa. iv) Vifaa vya usafi. a )Dekio aina ya Pusher ( ) b)ufagio mrefu wa chelewa ( ) c)jembe1 lenye mpini( ) JINA LA MHASIBU SAHIHI TAREHE... JINA LA MWALIMU WA ZAMU. SAHIHI TAREHE.. 9

FOMU F FOMU HII IJAZWE NA MWANAFUNZI, WAZAZI/ WALEZI WAWILI NA NDUGU WAWILI PICHA ZAO ZIAMBATANISHWE KWENYE VISANDUKU. AHADI YA MWANAFUNZI. Mwanafunzi Ninaahidi kufuata taratibu na sheria zote za shule ikiwa ni pamoja na kutoshiriki katika migomo, fujo na makosa ya jinai. SAHIHI TAREHE AHADI YA MZAZI/MLEZI. Mimi Mzazi wa Mwanafunzi.. Kidato cha.mwaka. Ninakiri kukubaliana na sheria, kanuni, kulipa ada, michango ya shule na maelekezo mengine yatakayotolewa na shule kwa kipindi chote mwanangu atakapokuwa katika Shule ya Sekondari Anna Mkapa. JINA LA MZAZI/ MLEZI. 1.. 2 SAHIHI.. SAHIHI TAREHE TAREHE.. NDUGU WAWILI 3. JINA 4.JINA SAHIHI.. SAHIHI. 10

11