OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

Similar documents
HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

ARCHDIOCESE OF MWANZA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

ORDER NO BACKGROUND

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Human Rights Are Universal And Yet...

Early Grade Reading Assessment for Kenya

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Ufundishaji wa lugha nyingine

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Upande 1.0 Bajeti yako

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Kutetea Haki za Binadamu

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Transcription:

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA SANDUKU LA POSTA 569 IRINGA TANZANIA Kumb... MZAZI/MLEZI WA...... YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018/2019 Ninayo furaha kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha TANO... katika Shule ya Sekondari Tosamaganga. Ushirikiano wako na Wafanyakazi wote pamoja na wanafunzi wenzako ni siri kubwa ya mafanikio. Hii inawezekana ukiwa na NIDHAMU, JUHUDI na MAARIFA. Ukiwa hapa shuleni utakuwa na wajibu mkubwa wa kusoma kwa bidii, kufuata sheria za shule, kushiriki katika mipango ya Elimu ya kujitegemea na kufuata taratibu zote za shule zitakazo tolewa na viongozi wako shuleni. HILI LIWE NDILO LENGO LAKO UTAKAPOKUWA SHULENI. Shule itafunguliwa Tarehe... kwa kidato cha tano. Unatakiwa kufika shuleni siku hiyo bila kukosa. Mwisho wa kuripoti shuleni ni Tarehe... Iwapo hutaripoti hadi tarehe hiyo utahesabiwa kuwa umekataa nafasi uliyopewa, hivyo nafasi itahesabiwa kuwa wazi na itajazwa kwa kufuata taratibu za uchaguzi wa wanafunzi wanao chaguliwa kujiunga na shule za serikali. Mwanafunzi anatakiwa aje na Cheti halisi cha kuzaliwa kiambatane na kivuli chake (Birth certificate photocopy), cheti halisi cha kumaliza kidato cha Nne (Form four Leaving certificate) kiambatane na kivuli chake pamoja na Statement of Results original ya matokeo yake ya Kidato cha Nne pamoja na kivuli chake kwa ajili ya matumizi ya ofisi. Shule ya Sekondari Tosamaganga ipo umbali wa kilomita kumi na saba (17) kutoka Iringa mjini. Unaanzia stendi ya daladala eneo la Posta-Iringa mjini. Utakutana na gari zilizoandikwa Posta- Ipamba/Tosa ambazo zitakufikisha hadi Tosamaganga karibu kabisa na shule. Ufikapo shuleni onana na mwalimu wa zamu ambaye atakupokea na kukuelekeza nini cha kufanya. Aidha ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kumiliki simu ya mkononi shuleni. Atakayepatikana na simu Atapewa adhabu kali na kulipa fidia za uharibifu wa miundombinu ya umeme. NB. Mawasiliano: +255 763 499 331 (Ofisi ya Malezi) KARIBU SANA TOSAMAGANGA SEKONDARI MOTTO: ELIMU NI HAZINA MGIMWA, D K L MKUU WA SHULE 1

A: MAHITAJI YA SHULE. (i) Ada ni Tshs 70,000/=kwa mwaka au Tshs 35,000/= kwa muhula (ii) Fedha ya tahadhari ni Tshs 5,000/= (Haitarudishwa) (iii) kitambulisho Tshs 5,000/=, Nembo 4000/=(mashati 2) (iv) Kuboresha taaluma Tshs 30,000/= kwa mwaka au Tsh 15,000/= kwa Muhula (v) Mchango wa Mpishi Tshs 15,000/= kwa mwaka. (vi) Mchango wa ulinzi Tshs 15,000/= kwa Mwaka. (vii) Mchango wa matengenezo ya samani za shule ( kitanda, kiti na dawati )Tshs 20,000/= (viii) Ukarabati mdogomdogo(miundo mbinu ya umeme,maji safi na majitaka) Tshs 12,000/= (ix) Michezo Tshs 7000/= (x) Karatasi bunda moja (Duplicating paper) lenye karatasi 500 (A 4 ). Kwa matumizi ya ofisi kama vile mitihani, ripoti, n.k (hatupokei fedha). (xi) Huduma ya kwanza Tshs 5,000/= B: MAHITAJI YA MWANAFUNZI Ni lazima kila mwanafunzi aje na kadi ya bima ya afya kwa ajili ya matibabu SARE ZA SHULE (i) Suruali mbili za khaki (esteem 2) zenye malinda mawili, pindo (turn up) na zisizobana zenye upana wa si sentimita 17. (asiyefuata maagizo haya hatapokelewa) (ii) Shati mbili nyeupe mikono mirefu, tetroni aje nazo. (iii) Viatu vya ngozi nyeusi jozi mbili vya kufunga kwa kamba.(lizingatiwe. (iv) Soksi jozi mbili rangi Nyeusi (v) Sweta moja la muundo wa V rangi ya Siafu( Brick red) (Pia linapatikana kwenye maduka yaliyopo karibu na shule). (vi) T-shirt moja yenye kola (maarufu kama form six) rangi ya kijivu (Pia linapatikana kwenye maduka yaliyopo karibu na shule). (vii) Mkanda mweusi (Jozi mbili), na usiwe mpana, Kandambili jozi moja. (viii) Tai mbili ndefu rangi ya dark blue (Pia zinapatikana kwenye maduka yaliyopo karibu na shule). NB.Kwa rangi za Sare za shule angalia kiambatanisho A, ukurasa wa mwisho. SARE ZA KUSHINDIA (AFTER CLASSES DRESS) 1. Suruali mbili za kitambaa rangi nyeusi zenye mkunjo (turn up) zisizo za kubana,upana si chini ya 17cm. 2. Track suit moja rangi ya blue bahari 3. Sweta moja zito Rangi nyeusi( lisilo la kufunika kichwa) kwa ajili ya kujikimu na baridi 4. Mashati mawili ya mikono mirefu rangi ya blue bahari. 5. Viatu vya kushindia Raba nyeusi za kufunga na kamba NB. Mwanafunzi hataruhusiwa kuwa na mavazi mengine zaidi ya haya yaliyoelekezwa Michango yote ilipiwe kwenye Akaunti namba 60501100042, Jina la Akaunti ni TOSAMAGANGA SECONDARY SCHOOL benki ya NMB Tawi lolote. Kwa mchanaganuo ufuatao; 1 Ada 35,000/= au 70,000/= 2 Taaluma 15,000/= au 30,000/= 3 Tahadhari 5,000/= 4 Ulinzi 15,000/= 5 Mpishi 15,000/= 6 Kitambulisho na Nembo 9,000/= 7 Ukarabati Mdogomdogo 12,000/= 8 Michezo 7,000/= 9 Matengenezo ya samani za shule (Kitanda,Kiti na dawati) 20,000/= 10 Huduma ya kwanza 5,000/= JUMLA Tshs 138,000/= kwa MUHULA au 188,000/= kwa mwaka 2

MALAZI NA CHAKULA (i) Aje na Blanketi moja, Shuka mbili za rangi ya Pinki, Godoro upana wa futi 2.5 (Godoro anaweza kulipata pia katika maduka yaliyopo karibu na maeneo ya shule), Mto na foronya na Chandarua. (ii) Sabuni za kufulia na kuogea za kutosha, Mswaki na dawa ya meno. (iii) Sanduku moja imara la kutunzia vitu.(tranka) (iv) Ndoo mbili(2) za kuchotea maji za ujazo wa lita kumi (atakabidhi moja anaporipoti, nyingine kwa matumizi binafsi), Aje na kidumu cha lita tano kwa ajili ya kuwekea maji ya kunywa Aje na vyombo vya chakula.vitu hivi vinapatikana katika duka lililopo shuleni. (v) Aje na tochi/taa ya betri isiwe ya kuchaji kwa kutumia umeme. (vi) Kila mwanafunzi aje na vifaa vya michezo; EGM na CBG aje na ( raba/viatu, Bukta,Tshirt(fulana) na soks ndefu Rangi ya bluu), PCB na PCM aje na (raba/viatu,bukta,tshirt(fulana) na soksi ndefu Rangi nyekundu), HGE na PGM aje na (raba/viatu, Bukta,Tshirt(fulana) na soksi ndefu Rangi nyeusi). Kwa ajili ya michezo (vitakaguliwa) VIFAA VYA TAALUMA NA MAZINGIRA (i) Mzazi anashauriwa kumnunulia mwanae vitabu vya kiada na ziada, Madaftari makubwa aina ya counter books yasiyopungua matano,peni(kalamu ya wino), Penseli na mfuto, zana za Hisabati kama Mathematical set na Scientific Calculator kwa matumizi binafsi NB. Orodha ya vitabu vya masomo husika angalia ukurasa wa saba (7) (ii) Kila mwanafunzi aje na squeezer (isipokuwa wanafunzi wa CBG), kwa ajili ya usafi shuleni (iii) Kama ni PCM aje pia na hard bloom moja, PCB aje pia na soft bloom moja, EGM na HGE waje na mifagio ya chelewa mitano kwa kila mmoja, PGM aje na Mkasi wa kupunguzia au kukatia maua/miti, CBG- aje na jembe 1 lenye mpini imara, 3

Fomu Na A KANUNI ZA SHULE 1. Mwanafunzi anapaswa kuwepo eneo la shule wakati wote isipokuwa anapopata ruhusa maalum kutoka kwa mwalimu wa zamu,makamu Mkuu wa Shule au Mkuu wa Shule. 2. Mwanafunzi anatakiwa kuvaa sare rasmi ya shule muda wote wa shule, isipokuwa muda wa kazi za mikono na michezo ambapo atavaa nguo rasmi za kazi/michezo. 3. Lugha chafu, matusi, ugomvi, fitina na kupigana kwa mwanafunzi ni marufuku. 4. Mwanafunzi lazima awahi popote anapotakiwa na wakati uliowekwa. 5. Mwanafunzi ni lazima aiheshimu kazi ya darasani na nje na kuifanya vizuri. Ni lazima kufanya mazoezi ya mitihani yote inayotolewa darasani awapo shuleni. 6. Unywaji wa vileo, kuuza pombe na uvutaji wa aina yoyote ya sigara au madawa ya kulevya ni marufuku kwa mwanafunzi. Hairuhusiwi kufanya biashara yoyote shuleni. 7. Wizi wa aina yoyote ni marufuku na ni kosa kubwa kwa mwanafunzi. 8. Uharibifu na upotevu wa mali binafsi au ya Umma ni kosa kubwa. 9. Mwanafunzi anapaswa kuwa na heshima, mtiifu na mwenye adabu wakati wote na kwa kila mtu. Ukaidi na ubishi kwa viongozi/walezi wake ni kosa. 10. Wageni wa wanafunzi wanaruhusiwa kuonana na wanafunzi,baada ya kujitambulisha na kupokelewa na mwalimu wa zamu. wanafunzi watembelewe siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuanzia saa sita mchana mpaka ya saa kumi na moja jioni, ili kuondoa usumbufu siku za masomo. 11. Mwanafunzi haruhusiwi kuoa wakati akiwa bado shule. Akibainika atafukuzwa shule mara moja. Aidha ni marufuku kuwa na mahusiano ya mapenzi awapo shuleni. Akibainika atafukuzwa shule mara moja. 12. Ni marufuku kwa wanafunzi kwenda nyumba za Walimu na Wafanyakazi wasio walimu bila ruhusa au kibali maalum toka kwa Mwalimu mlezi/uongozi wa shule. 13. Mapambo na nakshi za aina yoyote na mavazi ya kihuni kwa mwanafunzi ni marufuku, nywele ziwe fupi, ndevu ni marufuku.mitindo ya kunyoa nywele kama pank, kunyoa kipara pasipo sababu hatutavumilia na adhabu kali itatolewa kwa atakayefanya kinyume na haya (Aidha kofia aina yoyote, mikanda mipana na majaketi Marufuku Kabisa shuleni). 14. Simu haziruhusiwi ukikamatwa utapewa adhabu kali na kulipa fidia za uharibifu wa miundombinu ya umeme. 15. Ni marufuku kwa mwanafunzi kukataa/kugomea adhabu kwani kukataa adhabu ni kukataa malezi bora ya walezi wako shuleni yenye maana ya kukataa kuwa mwanafunzi wa shule hii. 16. Mgomo wa aina yoyote ni marufuku na ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania. Matatizo yote yatashughulikiwa kwa kufuata ngazi zilizowekwa kuanzia Darasa/ Bweni hadi Baraza la Shule. Atakaye goma au kusababisha mgomo adhabu yake ni kufukuzwa shule. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE 1. Wizi, Kuoa, Kusababisha mimba, Uasherati, Ushoga, Ubakaji, kushikwa ugoni na kupiga/kupigana. 2. Ulevi, Uvutaji wa bangi na sigara ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya. 3. Kuharibu kwa makusudi mali ya Umma /binafsi. 4. Kudharau wimbo wa Taifa,wimbo wa Shule na Bendera ya Taifa. 5. Kugoma,kuchochea au kuongoza mgomo, ikiwa ni pamoja na kukataa adhabu kwa makusudi ikiwemo kuvuruga amani na usalama wa shule. 6. Kushiriki au kuendekeza imani za kishirikina shuleni. 7. Kunyanyapaa au Uonevu wa aina yoyote kwa mwanafunzi mwenzake. 9. Kujihusisha na siasa za chama chochote anapokuwa shuleni. 10.Kufanya mikutano isiyo halali au isiyokuwa na kibali kutoka uongozi wa shule. 11.Kuharibu miundombinu na samani za shule kama viti, umeme, maji, vitanda kwa makusudi.. JINA LA MWANAFUNZI SAHIHI TAREHE MKUU WA SHULE 4

Fomu Na -B- TAARIFA MUHIMU ZA MWANAFUNZI Shule inapenda kupata taarifa muhimu za kila mwanafunzi kwa ajili ya mawasiliano wakati wote awapo shuleni. Fomu hii ijazwe kwa usahihi na ukamilifu. Jina la mwanafunzi Kidato mchepuo... Mwaka Anwani ya nyumbani (anayotumia) Tarehe ya kuzaliwa Namba ya simu(ya nyumbani/ya mzazi) Mtaa/Kijiji anachotoka...kata. Tarafa...Wilaya Mkoa..shule ya msingi aliyosoma. Shule ya Sekondari atokayo Namba ya Mtihani ya Kidato cha Nne. Anwani ya shule.matokeo yake ya kidato cha nne. Dini yake ni [Mkristo, Mwislamu n.k.]dhehebu lake ni Mkatoliki, Mlutheri,Suni n.k} Sahihi Tarehe... NB. Mwanafunzi haruhusiwi kubadili Dini akiwa shuleni. AHADI YA MWANAFUNZI Mimi.. NAKUBALI / SIKUBALI nafasi niliyopewa katika shule ya sekondari Tosamaganga. Naahidi kuwa nitazitii taratibu, kanuni na sheria zote za shule. Nitafuata masharti yote yanayotolewa na Mkuu wa shule, Wafanyakazi wote na Viongozi wote wa shule. Ninaahidi pia nitashirikiana na wanafunzi wenzangu katika shughuli za masomo, kazi za nje na katika michezo kwa muda wote nitakaokaa Tosamaganga Sekondari. Nakiri kuwa kwa akili zangu timamu, taarifa zote nilizotoa hapo juu ni sahihi na zinanihusu. Jina.. sahihi. Tarehe.. TAARIFA YA MZAZI/ MLEZI Jina la Mzazi/ Mlezi. Anwani yake Namba ya simu.. Kazi anayofanya Wilaya/Mji anakofanyia kazi Anwani ya kazini.. Namba ya simu ya kazini... AHADI YA MZAZI/MLEZI Mimi..MZAZI/MLEZI NAKUBALI / SIKUBALI nafasi aliyopewa mwanangu katika shule ya sekondari Tosamaganga. Naahidi kuwa nitawajibika/sitawajibika na kumhimiza mwanangu kuzitii taratibu, kanuni na sheria zote za shule. Nitashiriki/sitashiriki kumhimiza kufuata masharti yote yanayotolewa na Mkuu wa shule, Wafanyakazi wote na Viongozi wote wa shule. Ninaahidi pia nitashirikiana/sitashirikiana na uongozi wa shule kumhimiza mwanangu kushirikiana na wanafunzi wenzake katika shughuli za masomo, kazi za nje na katika michezo na kuwa na nidhamu kwa muda wote atakaokaa Tosamaganga Sekondari. Nitapenda/sitapenda kupata taarifa zote zinazomhusu mwanangu muda wote awapo shuleni (futa isiyohusika) Jina la mzazi/mlezi..sahihi Tarehe. WATU WA KARIBU(KIUHUSIANO/UNDUGU) NA FAMILIA AMBAO UNGEPENDA WAPATE TAARIFA ZAKO ZAIDI YA WAZAZI/ WALEZI (i) Jina Anwani Namba ya simu Kazi anayofanya.. Uhusiano wake na mwanafunzi... (ii) Jina Anwani. Namba ya simu Kazi anayofanya.... Uhusiano wake na mwanafunzi... (iii) Jina. Anwani Namba ya simu Kazi anayofanya.. Uhusiano wake na mwanafunzi... NB; Iwapo anwani ya mmojawapo wa Mzazi/Mlezi au ndugu wa karibu amehama au Amefariki lazima mwanafunzi atoe taarifa na kubadilisha jina na kuandika mtu mwingine ambaye atawajibika kwa mwanafunzi 5

Fomu Na -C- FOMU HII IJAZWE NA MGANGA MKUU WA MKOA /WILAYA NA MWANAFUNZI AJE NAYO SHULENI NA KUIKABIDHI KWA MKUU WA SHULE. Mimi (Jina la Mganga Mkuu wa Mkoa/Wilaya).. Ninathibitisha kuwa mwanafunzi huyu (Jina la mwanafunzi).. Amepimwa na mimi kikamilifu na kuonekana kuwa anayo /hana afya nzuri kwa mujibu wa taarifa zifuatazo; (A) Hali ya Mwili. (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) Mapigo ya moyo Damu (Haemoglobin).... Kundi la Damu (Blood group).... Mkojo. Haja kubwa. Macho. Masikio... NB. Weka maoni yako kuhusu kile kilichotajwa.... (B) Magonjwa. Amewahi /hajawahi au hana magonjwa yafuatayo; (a) Kifua kikuu (TB). (b) Kifafa (Epilepsy) (c) Shinikizo la damu (BP).. (d) Magonjwa ya tumbo.. (e) Seli mundu (Sickle cells). (f) Ukoma (g) Magonjwa ya zinaa (taja aina) (h) Ugonjwa wa akili.. (i) Ugonjwa mwingine nje ya orodha hapo juu....... Maoni ya Daktari. Saini na Muhuri wa Daktari/Mganga wa Hospitali ya Serikali... MGIMWA, D K L MKUU WA SHULE 6

ORODHA YA VITABU VYA MASOMO (mzazi unaweza ukamnunulia mwanao) PHYSICS 1. Nelkon and Parker, Advanced level Physics 7 th edition. 2.S. Chand s principles of physics class XI 3.S. Chand s principles of physics,class XII 4.Jim breithaupt, understanding physics 2 nd / 4 th edition 5.Roger Monastery, Advanced Level physics 4 th edition 6.Tom Duncan, Advanced Level physics 7.Calculations, For Advanced level Physics 8. University Physics, New edition CHEMISTRY 1.Physical chemistry, by Delungu (Mzumbe bookshop project 1998) 2. Advanced inorganic chemistry part I and II(Tanzania institute of education). 3.Organic Chemistry part 1, The fundamental principles I.L finar (longman LTD) 4. Conceptual Chemistry for class XI-Chand 5. Conceptual Chemistry for class XII-Chand GEOGRAPHY 1.Principles of physical geography by F J monk house 2. Geography integrated approach by D.waugh 3.Fundamental of Practical Geography by Josephat Mwita 4.General geography in diagram by R B burnet 5. Simplified physical Geography(A-LEVEL) by D M 6. Statistical methods and the geographers by s. Gregory BIOLOGY 1.Biological science;cambridge university press 1997 3 rd edition 2.functional approach by Mbv Robert 3.New Understanding Biology By Suzan Toole 4. Advance biology Principles and application By C J Clegg and Mackean 5.Advanced Biology By Michael kent (2000).Oxford university press uk. ADVANCED AND BASICAPPLIED MATHEMATICS 1. Basic applied Mathematics by Kiza and Septine I sillem 2. Advanced mathematics by shayo 3.Advanced Mathematics book 1 and 2 by Backhouse 4.Advanced Mathematics Chand s 1 and 2 HISTORY 1.Advanced learners, History form V and six(history 1 and 2)( oxford 2011) 2.Advanced level History for Africa, From Neolithic Revolution to present(zist Kamili 2010) 3. Major events in the world History 4. Advanced level History (Nyambari nyangwine 2007 5.Focus on Modern world history by Japhace, Ponsian, Chakupewa, Mpandije Yusuph P Maunda (2012 GENERAL STUDIES 1.General studies for A- Level certificate form v 2.Contemporary approach for A level general studies notes for form v and six 3.General studies supplementary book for A level and colleges. ECONOMICS 1.Economics Theory by Gupta 2.Micro-economics by Dwiverd 3.Economicsimplified By N A Saleemi 4.Modern Economics By Robert Mudida. 7

Kiambatanisho A RANGI ZA SARE ZA SHULE RANGI YA SHATI NA TAI RANGI YA SWETA RANGI YA T-SHIRT RANGI YA SURUALI 8