KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Human Rights Are Universal And Yet...

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Kiu Cha umtafuta Mungu

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

United Pentecostal Church June 2017

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Makasisi. Waingia Uislamu

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Oktoba-Desemba

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Khatib Khamis Saleh

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

K. M a r k s, F. E n g e l s

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Ufundishaji wa lugha nyingine

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

KUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHI ZA KUSADIKIKA NA ADILI NA NDUGUZE

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

MUHTASARI WA SEMINA YA TAASISI YA BIBLIA NA UTUMISHI MOROGORO TAREHE 18/11/2014

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

2 LILE NENO LILILONENWA

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

KUCHUNGUZA MCHOMOZO KATIKA FASIHI YA KISWAHILI: UTAFITI LINGANISHI WA USHAIRI KATIKA DIWANI YA USTADHI ANDANENGA

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

Banana Investments Ltd

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Usimulizi katika Utenzi wa Swifa ya Nguvumali

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

2.1.1 Kabla ya Ukoloni

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Forum:MyElimu Home for Students to Share Knowledge Thread: Dunia Uwanja Wa Fujo

Transcription:

SWAHILI FORUM 23 (2016): 144-153 KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO Wasifu wa Marehemu hadi kufika chuoni Mwalimu Edwin Charles Semzaba alizaliwa Muheza tarehe 12/01/1951 wazazi wake wakiwa Bwana Charles Joseph Semzaba na Bi. Mary Esther Semzaba. Alipata elimu ya msingi kuanzia mwaka 1959 hadi mwaka 1966 katika shule ya msingi Temeke. Kisha alijiunga na Shule ya Sekondari Kigoma akasoma hapo mwaka 1967-1970. Baadaye alisoma katika Shule ya Sekondari Mkwawa (1971-1972), na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada ya awali (1973-1976) na shahada ya umahiri hadi mwaka 1983. Athari za Brecht na drama ya kiepiki katika utunzi wa Edwin Semzaba Katika utunzi wa baadhi ya tamthiliya mbalimbali, marehemu Edwin Semzaba, alitumia mkabala wa Aristotle na Brecht. Mkabala wa Kiaristotle unasimamia misingi kadhaa ikiwemo: uhusiano kati ya mwigizaji na mhusika; kujibainisha kabisa na mwigizaji (kuingia kwenye hisia bila kutoka); mihemko inasisitizwa ili kuibua hisia za woga kwa hadhira ili wamwonee huruma mhusika mkuu; jukwaa lina mandhari halisi ili kuibua illusion; mhusika mkuu anajitokeza tangu mwanzo hadi mwisho; muundo wa Kiaristotle una sehemu tatu ambazo ni mwanzo, kati na mwisho. Vilevile tamthiliya ya Kiaristotle ina vipengele sita ambavyo ni pamoja na: ploti/mtiririko wa matukio (mwanzo, katikati, mwisho); wahusika (kisaikolojia, kijamii, kiuchumi na kimaadili); maudhui; maneno; muziki na kionwa. Vipengele hivi sita vya Kiaristotle vimejitokeza sana katika kazi za Edwin Semzaba zikiwemo Tendehogo (1974/1980) na Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe (1988[1967]). Mkabala wa Kiepiki unasisitiza matumizi ya akili na sio hisia kwamba kazi ya sanaa izindue urazini wa wanajamii ili washughulikie matatizo yao. Vilevile, Brecht alisisitiza matumizi ya mbinu mbalimbali kama vile mchezo ndani ya mchezo; matumizi ya nyimbo zenye kugonga sikio siyo hisia; matumizi ya slaidi, filamu, na mabango; mandhari ina vitu vichache tu; maswali na majibu kutumika katika mchezo; matumizi ya maleba machache na rahisi; kutojibainisha na mhusika bali mwigizaji aingie na kutoka katika uhusika. Tutachambua kazi moja ya Edwin Semzaba ambamo ametumia mkabala wa kiepiki yaani kazi yake ya Mkokoteni (1987). Mkokoteni ni tamthiliya inayoangazia nafasi ya kodi katika maisha ya mwanadamu. Kulipa kodi ni amri ya serikali na hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kuikwepa asiilipe. Katika mchezo huu kuna wahusika wakuu wawili ambao ni Tandale na Makorora ambao wanajitokeza kuanzia 144

ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO mwanzo hadi karibia na mwishoni lakini Tandale anauliwa na Makorora kwa kutumbukizwa baharinina Makorora anajitajirisha kwa mali za Tandale. Hivyo, Tandale hafiki mwisho wa mchezo. Katika tamthiliya hii, kuna dhamira mbalimbali ambazo mtunzi anazigusia zikiwemo umaskini, hali ngumu ya maisha, mauaji, tamaa ya kutajirika bila kufanya kazi kwa bidii, uvivu, mapenzi na ndoa, ulipaji kodi, majanga ya kiasili kama vile tufani na kilimo cha minazi. Katika tamthiliya hii ya Mkokoteni mwandishi amedhihirisha kuathiriwa kwake namkabala wa kiepiki alioubuni wa utunzi na uongozaji wa michezo ya kuigiza. Vifuatavyo nivipengele vitatu vya kiepiki tutakavyovieleza. Kwanza, hakuna kujinasibisha kwa mhusika na mwigizaji kwa kuwa mhusika anaigiza jambo halafu anajitoa na kuwa yeye mwenyewe kwa maana anakosoa baadhi ya mambo ambayo ameyasema mwenyewe au ameyaigiza. Nakumbuka, siku moja kulikuwa na onesho pale FPA, ni siku tulipoigiza mchezo huu wa Mkokoteni (ambapo mimi [E. Mahenge] nilicheza kama mhusika Kaundime). Baada ya onesho kwisha, yaani mwisho wa onesho, marehemu Edwin Semzaba alikaribisha mjadala, ili watazamaji watoe maoni yao. Maswali yaliulizwa na mwigizaji mkuu (aliyekuwa Mwalimu Semzaba mwenyewe) na watazamaji waliyajibu kulingana na mitazamo yao mbalimbali na wakatoa maoni yao ili kurekebisha matatizo na changamoto zilizoibuliwa na mchezo. Pili, bakigraundi ya onesho haina vitu vingi. Kwa mfano, katika kitendo cha tatu onesho la tatu, mwandishi anatueleza Makorora akiendeshwa na Kicheema mchana mmoja kando kando ya bahari pana mwinuko mkubwa sehemu waliyopo. Maelezo hayo ni pekee katika onesho hilo na hivyo ndivyo Brecht alivyokuwa anataka.brecht hakuhitaji jukwaa lijazwe vitu vingi bali liwe la kawaida. Tatu, matumizi ya wimbo wenye kugonga sikio na siyo kugusa hisia. Katika kitendo cha pili na onesho la kwanza, tunamwona Makorora anaumwa.hawezi kwenda kumwendesha Tandale aende ufukweni kuoga, kwa hivyo anaamua kuwatuma binti zake wawili ambao ni Kaundime na Shangwe ili wakamsaidie kumsukuma Mzee Tandale kwenye mkokoteni wake. Tandale anampenda Kaundime na hivyo kwa ujanja anawaambia wasichana wakaoge ili waburudike. Wanapomaliza kuoga wanarudi alipokuwa na wanamwendesha na wanaondoka na wanapokaribia nyumbani, Tandale anasema amesahau ufunguo. Hivyo anamtuma Shangwe arudi ufukweni akautafute. Anatumia mwanya huo kufanya mapenzi na Kaundime na anampa ujira (fedha) na baada ya kumaliza kufanya kazi hiyo, anaimba wimbo ili kushadidia utunzwaji wa siri wakati Shangwe anapofika mkokotenini. Wimbo unasema hivi: Siri yako oooooo usiseme eee Siri yako oooooo usiiseme eee Ni siri Kaundime siri ee 145

KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA Ni siri Kaundime usiseme Usiseme eee siri yaaaakoooo (Semzaba 1987: 20) Wasifu wa kazi na vyeo vya marehemu Edwin Semzaba 1 Mtunzi na mwandishi wa hadithi na riwaya - hadithi fupi [kichwa hakijapatikana] iliyochapishwa katika Umma 4/2 (1974): 91-93 - Tausi wa Alfajiri (Dar es Salaam: HEKO, 1996) - Funke Bugebuge (Dar es Salaam: DUP, 1999) - Tamaa ya Boimanda (kuandikwa 2002; kuchapishwa Dar es Salaam: DUP, 2004) - Marimba ya Majaliwa (Dar es Salaam: E&D, 2008/ 2 2015) - Adventures of Tunda and Zamaradi (Dar es Salaam: Exodia, 2016) Mtunzi, mwandishi, mwigizaji na mwongozaji wa michezo ya kuigiza (jukwaani na redioni, TV na filamu) - Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe (kuandikwa akiwa anasoma kidato cha pili, mwaka 1967/kuchapishwa Dar es Salaam: DUP, 1988; Dar es Salaam: General Booksellers 2006; taarifa za chapa ya mwaka 2008 na ya nyingine baada ya hapo hazijapatikana kwa ukamilifu) - Magunia Yaliyojaa (Umma 3/1 (1973): 24-27) - Nimekwama (Umma 3/2 (1973): 3-7) - Hesabu Iliyoharibika (in John P. Mbonde (mh.). 1976. Uandishi wa Tanzania. Michezo ya Kuigiza. Dar es Salaam: East African Literature Bureau. k. 49-95) - Tendehogo (1974/1980; Umma 4/1 (1974): 29-43 na Dar es Salaam: Tanzania Publishing House 1980) - Sofia wa Gongo la Mboto (Peramiho: Benedictine Publications Ndanda, 1984) - Mkokoteni (Dar es Salaam: Swahili Press, 1987 [vyanzo vingi hutaja 1988]; Dar es Salaam: Exodia, 2014) - Kinyamkera (Dar es Salaam: Exodia, 2014) - Joseph na Josephine (Dar es Salaam: Exodia, 2014) 1 Orodha zifuatazo za kazi, vyeo na tuzo zinajumlisha taarifa zote tulizoweza kuzikusanya. Huenda kuna kazi zake nyingine ambazo hatujaziorodhesha kutokana na kutozifahamu. Kumehitajika utafiti zaidi kwa ndugu zake marehemu huenda wakafahamu mambo mengi mengine ambayo sisi hatukuweza kuyajua zikiwemo kazi nyinginezo ambazo hatujaziandika hapa. Mbali na ujuzi wetu tulirejelea hasahasa Kubegeya 2014 na vyanzo vingine vya mtandaoni ikiwemo tovuti husika ya wikipedia, pamoja na taarifa za kina katika Bertoncini-Zúbková & wengine 2009 na Noronha 2009, ingawaje vyanzo hivi hapa na pale havijakubaliana kuhusu taarifa zote. Waandishi wa kumbukumbu na Lutz Diegner kwa niaba ya wahariri wote wa SWAHILI FORUM. 146

ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO - Ujio wa Mburamatali [haijachapishwa] Mwalimu mbobezi wa sanaa na ubunifu, mhariri, meneja wa duka la vitabu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUP), na afisa tawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu 1976 hadi 2016 Miongoni mwa kazi zake za kitaaluma alizoziandika ni muswada wa utangulizi wa tamthiliya ya Kiswahili iliyotumiwa hasa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: OSW 208: Tamthilia ya Kiswahili, Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, 1997. Vilevile aliandika makala fupi Kiswahili na Vyombo vya Habari iliyochapishwa katika jarida la Mulika 23 (1996): 73-74. Vyeo katika vyama, mashirika na vikundi mbalimbali vya wasanii na waandishi: Tuzo - Mwenyekiti wa UWAVITA (Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania) - Mjumbe wa BAMVITA (Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania) - Mwongozaji, University Drama Group (Kikundi cha Michezo ya kuigiza cha Chuo Kikuu) - Kiongozi na/ama mshiriki wa miradi mbalimbali ya kitaaluma na kisanii: (1) TUSEME huu ni mradi uliokuwa unaendeshwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwawezesha wanafunzi wa sekondari wa kike, wajitambue na watimize ndoto zao. Lengo lilikuwa ni kuwawezesha wajiamini na kusoma masomo ya sayansi ili kuvunja dhana potofu kuwa wasichana hawana akili ya kusomea masomo ya sayansi ila ya sanaa. Mradi wao ulizaa matunda kwa kuwa wasichana wengi walifanya vizuri katika masomo ya sayansi na baadhi yao wakafanikiwa kujiunga na Idara ya Uhandisi ili kusoma shahada mbalimbali. (2) Children s Theatre Project (CTP) mradi ulioanzishwa mwaka 1989/90 pamoja na Prof Penina Mlama Muhando na kuendeshwa na Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (3) Mradi wa Creative Insights into Good Governance ulihusu dhana ya utawala bora nchini Tanzania. Marehemu Semzaba alishiriki kutunga na kuigiza pamoja na kuongoza michezo yenye mada hii iliyoonyeshwa televisheni na pia redioni kwa ajili ya kuelimisha umma wa Watanzania juu ya utawala bora katika ngazi mbalimbali. - Tuzo ya ushindi, Mashindano ya Saba Saba ya Uandishi na Ushairi, Kanda za Magharibi, Kigoma mwaka 1967 - Tuzo ya mwigizaji bora, shule ya sekondari ya Mkwawa, Iringa, mwaka 1971-1972 - Tuzo ya ushindi, uandishi wa michezo ya kuigiza, Idara ya Fasihi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1974 [vyanzo vingine vinasema mwaka 1975] 147

KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA - Tuzo ya ushindi, uandishi wa riwaya, mashindano ya East African Literature Bureau na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), University of Dar es Salaam (UDSM), mwaka 1976 - Tuzo ya ushindi, Mashindano ya Uandishi wa Vitabu vya Jusura vya Watoto, Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA) (Jubilei ya Miaka 100 ya kuchapishwa kwa Jusura za Ajabu za Nils Holgersson ya mwandishi Mswidi Selma Lagerlöf aliyepata Tuzo ya Nobel akiwa mwanamke wa kwanza), mwaka 2007 - Tuzo ya ushindi, mashindano ya Burt Award for African Literature (BAAL) Tanzania, mwaka 2016 Elizabeth Mahenge: Nilivyomfahamu Marehemu Mwalimu Edwin Semzaba Mimi binafsi nilimfahamu kama mwalimu na rafiki mkubwa katika maisha yangu ya kitaaluma na kiutunzi. Marehemu Edwin Semzaba alinifundisha sanaa ya uigizaji, utunzi, na uongozaji wa michezo ya jukwaani kuanzia mwaka 2002 hadi 2006 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ninakumbuka marehemu Edwin Semzaba alikuwa akiniambia you are very complex character. Aliponiambia hivyo nilimwuuliza, Mwalimu, una maana gani? Na yeye hakujibu swali bali aliimba Siri ni yangu ee siri, basi mjadala uliishia hapo. Hakuniambia sentensi hiyo mara moja, bali ni mara kwa mara alipojaribu kunifuatilia kitabia na kushindwa kupata hitimisho kuwa Eliza ni mtu wa aina gani. Kwa kuwa yeye alikuwa ni mwongozaji wa michezo ya redioni, jukwaani, na filamuni, na kwa upande mwingine alikuwa mtunzi ambaye alitaka kumwumba mhusika fulani, lakini hakuweza kunifahamu tabia yangu ikoje. Mara nyingi nilibadili mitindo ya uvaaji na hapo ndipo alipokuwa akisema you are very complex character. Kuna wakati nilivaa suruali, vimini, nguo za heshima kama za kwendea kanisani, na wakati mwingine nilivaa ushungi (kama sehemu ya utamaduni). Kwa mabadiliko haya yalimzuia Mwalimu Semzaba kunifahamu mimi ni nani. Ulipofika mwaka 2014 nilimwomba Marehemu Mwalimu Edwin Semzaba aniandikie barua ya kunipendekeza ili kusoma shahada ya uzamivu, katika barua hiyo ndipo nilipojigundua kuwa nilikuwa mwanafunzi wa aina gani. Mwalimu aliandika alikuwa anasoma kozi zangu bila kufanya mitihani kutokana na idadi ya kozi kupitiliza. Ni mwanafunzi wa ajabu sijawahi kuona katika kipindi ambacho nimefundisha wanafunzi wangu. Nilijishangaa sana lakini nikakumbuka kuwa alichokiandika ni kitu cha ukweli, kwa kuwa, wakati huo tulitakiwa kusoma vigezi 56 kwa mwaka na si zaidi ya hapo. Lakini kuna kozi zilikuwa zinanivutia na sikukubali kuzikosa. Hivyo, nilimwomba marehemu Mwalimu Edwin Semzaba, aniruhusu nisome kozi zake bila kufanya mtihani, naye alikubali akanichukulia sawa na wanafunzi wake waliojisajili kusoma kozi zake hakunibagua. 148

ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO Mbali na kuwa mwalimu wangu, alikuwa ni mtu aliyenifundisha kazi, hasa ufundishaji wa kozi za tamthiliya na uandishi wa kubuni. Kuanzia mwaka 2008 nilipangiwa kumsaidia Marehemu Mwalimu Edwin Semzaba kufundisha kozi ya tamthiliya ya Kiswahili na uandishi wa kubuni, ili niweze kujifunza kutoka kwa nguli huyu. Nilijitahidi kuibeba mikoba na hatimaye kuanzia mwaka 2010 nikatakiwa nifundishe mimi kama mwalimu wa kozi. Sikumwacha Mwalimu Semzaba bali niliendelea kuwa naye karibu kwa ushauri na mara kwa mara nilimwalika darasani kwangu kama mgeni, ili azungumze na wanafunzi wangu. Mbali na taaluma darasani, marehemu mwalimu Semzaba alinitambulisha katika maeneo mbalimbali yaliyohusiana na utunzi na taaluma ikiwemo Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA), Chama cha Hakimiliki ya Waandishi wa Vitabu (KOPITAN; Reproduction Rights Society of Tanzania) ambacho kiko ndani ya Chama cha Hakimiliki nchini Tanzania (COSOTA; Copyright Society of Tanzania) kiwajumuishacho wasanii wote.walakini, mpaka mauti yalipomkuta Mwalimu Semzaba, KOPITAN ilikuwa bado haijaanza kazi, kwa maana yeye nami tulikuwa tukishiriki katika kikao cha wadau wa tasnia ya uandishi na uchapishaji tukijadiliana kuhusu uanzishwaji wake. Lengo la pamoja la COSOTA ni kusimamia hakimiliki za wasanii na kuwapatia mrabaha kila mwaka. Pia Marehemu Edwin Semzaba alinishirikisha katikasemina mbalimbali na mafunzo mbalimbali yaliyohusiana na uandishi mahali popote yaliyokuwa yakifanyika. Mathalani, nilishiriki katika semina za waandishi wa vitabu zilizoandaliwa na Mradi wa Vitabu vya Watoto (CBP; Children s Book Project), miongoni mwa shughuli nyingine. Mara ya mwisho kabla hajaanza kuumwa tena na mauti kumfika, alinialika tukaenda pamoja Ubalozi wa Uchina kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa fasihi ya watoto kutoka China ambapomarehemu Mwalimu Semzaba alitoa hotuba yake kuhusiana na hali ya uandishi, uchapishaji na usomaji nchini Tanzania. Kijamii, Marehemu Edwin Semzaba alikuwa ni rafiki yangu mkubwa kutokana na mambo mbalimbali aliyokuwa akinishirikisha tukayajadili pamoja na kumpa ushauri kwa mtazamo wangu. Mara nyingi nilipojisikia kutafuta mawaidha, nilifunga safari ya kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) na kwenda ofisini kwake katika idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho (FPA; Fine and Performing Arts). Na yeye wakati mwingine alipopenda kuisikia sauti yangu, alifunga safari kutoka FPA na kuja TATAKI. Kwa hakika, watu wa TATAKI walituzoea sana kutuona tukiwa pamoja mikahawani Hill Park au UDASA. Ikafika wakati mtu akija TATAKI kumtafuta Semzaba, watu watamwambia Unamjua Eliza? Ahaaa, kama unamjua Eliza basi Semzaba umeshampata. Watu wengi walikuja ofisini kwangu kuniomba niwaelekeze namna ya kumpata Mwalimu Semzaba. 149

KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA Niliwaelekeza na kabla ya kuwashauri wamfuate FPA nilimpigia simu na kumjuza kuwa kuna mgeni wako..., naye bila kusahau kicheko chake, alicheka kwa nguvu sana akimalizia kuongea kwa simu na kisha kutabasamu na hapo akaikata simu. Nakumbuka nilipomtembelea FPA kitu cha kwanza alichokifanya kilikuwa aende kunichukulia soda almaarufu Selemani kama alivyoiita yeye mwenyewe. Alinichukulia kwa Mama Rose na alimjulisha kuwa nina mgeni, Eliza amekuja kunitembelea, kisha utasikia kicheko kwa sauti kubwa hadi huwezi kujizuia na wewe utacheka tu. Alipofika ofisini aliniambia nimemwambia Mama Rose nina mgeni, Eliza Mahenge amekuja kunisalimu, na hapo ataangusha kicheko kingine. Kwa kweli alikuwa anapenda kicheko chake, na watu wote tulikipenda kicheko hicho kwani kilitufanya tuseme Semzaba huyo!, na kisha tukacheka nasi. Ni mambo mengi ya kuandika kumhusu Marehemu Mwalimu Edwin Semzaba, lakini yatosha kuishia hapa. Emmanuel Mbogo: Nilivyomfahamu Marehemu Edwin Semzaba Kuna watu, katika jamii, ambao hata wakiondoka na kuingia dunia ya pili, bado inakuwa vigumu kufutika katika kumbukumbu zetu. Edwin Semzaba ni mfano wa watu wachache wa aina hii. Mimi nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Juni, 1976. Na ni mwaka huohuo Amandina Lihamba alikuwa amerudi toka Marekani na kujiunga na Idara ya Sanaa za Maonesho. Idara hii ilikuwa na magogo wa sanaa kama Godwin Kaduma, Ebrahim Hussein, Penina Muhando na baadaye Eberhard Chambulikazi na wengine. Mwaka ule wa kwanza hatukufanya kazi yoyote na Marehemu Semzaba. Tamthilia ya kwanza tuliyoicheza ilikuwa Mabatini (iliyochapishwa mwaka 1980) ya Godwin Kaduma. Marehemu Semzaba hakushiriki. Baadaye tulicheza Mashetani (1971) ya Ebrahim Hussein na The Strong Breed (1964) ya Wole Soyinka, na baadaye sana A Season in the Congo (1968 [1966]) ya Aimé Césaire; yote hii ikiwa imetayarishwa na Amandina Lihamba. Katika michezo hii yote Edwin Semzaba hakushiriki. Hata kama tulikuwa watu wa dau moja, lakini kwa wakati ule sikujisumbua kujua ni kwa nini hakushiriki.katika kuadhimisha miaka 25 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1986 ndipo nilipofanya kazi ya sanaa kwa karibu na Marehemu Semzaba, yeye akiwa kiongozi (director) na mtunzi wa Tendehogo (iliyochapishwa mwaka 1974 katika jarida la Umma na mwaka 1980 kama kitabu) na mimi kama meneja wa jukwaa. Usiku ule pale kwenye Ukumbi wa Nkrumah watu walifurika. Marehemu Semzaba alikuwa amefanya kazi nzuri. Hadhira ilijikuta ikivunjika mbavu kwa cheko na wakati mwingine ilikuwa kimya. Katikati ya burudani mwandishi alifaulu kuwafanya watazamaji watafakari kuhusu historia ya mateso ya Mwafrika. 150

ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO Baadaye mimi na wenzangu wachache tulianzisha University Drama Group. Lakini Marehemu Semzaba hakuwa katika kundi hili. Nilihisi alikuwa na matatizo ya afya mwilini. Tamthilia nyingi za Semzaba alizitayarisha akiwa mhadhiri wa Idara ya Sanaa za Maonesho. Baada ya miaka 17 ya kuishi nchini Kenya na mwaka mmoja Rwanda, Kigali, nilirudi Tanzania na kujiunga na Chuo Kikuu Huria. Wakati huo Marehemu Semzaba alikuwa ameandika tamthilia nyingine zaidi. Tamthilia ya Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe (1988) ndiyo inayojulikana kuliko zote hapa Tanzania. Wakati huu sababu tatu zilitukutanisha. Moja,alipata fikra ya kufanya shahada ya uzamivu pale Chuo Kikuu Huria akapendekeza niwe msimamizi wake. Pili, kila alipotayarisha mchezo wa kuigiza na wanafunzi wake hakukosa kunialika, nami sikukosa kufika. Maigizo matatu ya mwisho niliyoyaona yalikuwa (1) Jose na Josephine, (2) Ujio wa Mburamatali alizoziandika yeye mwenyewe, na (3) Fumo Liongo niliyoiandika mimi mwaka 1989 (na iliyochapishwa mwaka 2009). Nililalamika nikamwambia, We Semzaba! Vipi idara haina ukumbi sahihi wa sanaa za maonesho! Mbona ukumbi huu ni mdogo; hautoshi. Tazama baadhi ya watazamaji wamesimama!? Kama kawaida yake, badala yakunijibu, alipasua kicheko, Aa sijui, hayo ni mambo ya wakubwa. Kaa pale mbele; mchezo karibu utaanza. Hatukujadili jambo hili tena. Lakini kama nilivyodokeza hapo juu, Semzaba afya yake haikuwa nzuri. Alikuwa mgonjwa. Labda miguu. Hakunambia. Labda uzito mkubwa. Sijui. Hakunambia. Katika hali ya mzahamzaha alidokeza kuwa, Labda inaweza kuwa ni masuala ya sihiri. Nilicheka. Siku nyingine nilipita pale ofisini kwake nikampa kitabu changu Dawa Dhidi ya Magonjwa Yote (2012). Hata baada ya kukisoma Semzaba hakuniuliza chochote kuhusu kitabu hiki. Alisema kwa furaha, Aa! Kitabu chako kizuri, Mbogo! Katika kitabu hiki cha Dawa, naonesha njia mbalimbali za kupigana dhidi ya ushirikina, lakini Semzaba hakuniuliza; na mimi nikanyamazia kuhusu hili. Leo hii, nikitafakari tena kuhusu Semzaba na changamoto kuhusu afya yake; kiroho, namwona kuwa aling ang ania na kubaki Mprotestanti. Hata kama Semzaba alikuwa ameokoka; lakini, nadhani aliyatilia shaka baadhi ya madhehebu ya makanisa ya kiroho (Pentecostal Churches). Na Dawa Dhidi ya Magonjwa Yote si kitabu kinachoweza kukubalika kwa urahisi na Muanglikana damudamu kama Semzaba. Lakini nichukue jusura na kusema kuwa; maisha marefu aliyoyaishi Semzaba yalitokana na sababu tatu: Kwanza, aliwaamini wahusika wake; aliwapenda wahusika aliowaumba katika tamthilia na riwaya zake. Walikuwa marafiki wa kweli. Hawakuwa na kigeugeu! Pili, imani yake isiyotetereka ya kumtegemea Mungu pia ilimfanya aishi haya maisha marefu ; na tatu, ucheshi na futuhi iliyojitokeza katika maisha yake na miongoni mwa wahusika wake ilikuwa hijabu; ilichangia kurefusha maisha yake. Kuhusu ucheshi, Biblia, katika Mithali (17: 22) inasema: Moyo Mchangamfu ni Dawa, bali Moyo wenye Huzuni Hudhoofisha Mwili. 151

KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA Kwa kuhitimisha, ningependa kumwomba Mkuu wa Idara ya Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa idara ifanye juhudi za ziada, iwaone kaka zake Edwin Semzaba; wakusanye miswada ya tamthilia zake zote, na kwa mkataba kati yao na Idara, juzuu moja ya tamthilia zake ichapishwe, labda na TATAKI. Tanzania naulimwengu wote wenye mapenzi na Fasihi ya Kiswahili watafaidika kutokana na kazi alizotuachia Edwin Semzaba. Pumzika Kwa Amani Marehemu Edwin Semzaba alifia Dar es Salaam katika Hospitali ya Tumaini akazikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam tarehe 20 Januari mwaka 2016, siku ya Jumatano saa 10 jioni. Siku ya mazishi yake, aliagwa katika Kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakahudhuria watu mbalimbali kutoka Tanzania nzima. Waombolezaji walifanya sanaa mbalimbali za kimaonesho kwa ajili ya kuenzi na kumuaga Marehemu Edwin Semzaba, wasanii, waigizaji, wanamuziki, na waandishi, kwa kuwataja kwa uchache walioomboleza kwa njia ya uigizaji, uimbaji na utambaji. Pia wasanii wa Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (FPA) ambako marehemu Edwin Semzaba alikuwa akifanya kazi waliigiza na kutamba wasifu wake. Familia yake ilitoa neno la shukrani kutokana na maisha ya marehemu wakasema kwamba wenyewe katika familia yao walikuwa wanamwita Zimwi kutokana na vituko vyake. Kwa upande wa kanisani, Mchungaji aliyeadhimisha ibada ya maziko yake, alianzisha wimbo ambao marehemu alikuwa anaupenda sana, wimbo uliomo kwenye Tenzi za Rohoni unaoitwa Bwana u sehemu yangu. Kanisa zima liliimba huku watu wakibubujikwa na machozi. Mchungaji alieleza kuwa huo ulikuwa ni wimbo ambao marehemu aliupenda sana akauimba kila wakati. Kila mtu kwa namna yake alimshukuru Mwenyezi Mungu (kulingana na imani zao) kuhusu zawadi ambayo Tanzania na dunia ilipewa, nayo ni Edwin Charles Semzaba. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe. Pumzika kwa amani, Mwalimu. Raha ya milele umpe, Ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Amina. Marejeleo Bertoncini-Zúbková, Mikhail D. Gromov, Said A.M. Khamis & Kyallo W. Wamitila. 2009. Outline of Swahili Literature. Prose Fiction and Drama. 2 nd edition. Brill: Leiden. Edwin Semzaba. Wikipedia. <https://en.wikipedia.org/wiki/edwin_semzaba> (Last accessed 28/02/2017). Kubegeya, Maimuna. 2014. Semzaba: Niliandika Ngoswe nikiwa kidato cha pili. Mwananchi 05/08/2014. <http://www.mwananchi.co.tz/makala/semzaba--niliandika-ngoswe-nikiwakidato-cha-pili/1597592-2408828-cpm1ex/index.html> (Last accessed 28/02/2017). 152

ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO Noronha, Lourenco. 2009. Einführung in die Swahili-Literatur. Zweiter Teil: Post-Uhuru- Literatur 1961-1985 ( Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Sehemu ya Pili: Fasihi ya Baada-ya-Uhuru 1961-1985). Wien: Institut für Afrikanistik, Universität zu Wien/Vienna: Taasisi ya Taaluma za Afrika, Chuo Kikuu cha Vienna. <http://www.swahililiteratur.at/links/einfuerungswahililit.htm> (Last accessed 28/02/2017). 153