Ndugu na dada zangu wapendwa,

Similar documents
Ndugu na dada zangu wapendwa,

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

United Pentecostal Church June 2017

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Ndugu na dada zangu wapendwa,

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Kiu Cha umtafuta Mungu

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

MSAMAHA NA UPATANISHO

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

Roho Mtakatifu Ni Nini?

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Maisha Yaliyojaa Maombi

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Human Rights Are Universal And Yet...

Oktoba-Desemba

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

MAFUNDISHO YA UMISHENI

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Kwa Kongamano Kuu 2016

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Makasisi. Waingia Uislamu

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi. Iliyoendelea sana

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Patanishwa, Hesabiwa Haki, Takaswa

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

2 LILE NENO LILILONENWA

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Transcription:

UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, MEI 2014 Na Rais Thomas S. Monson Upendo Asili ya Injili Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya maisha duniani. ninafurahia mawazo yanayoonyeshwa katika hili shairi fupi: Nimelia usiku mzima Kwa ukosefu wa maono Hayo kwa mahitaji ya mtu yalinifanya mimi kipofu. Lakini kamwe sijaweza Kusikia athari ya majuto Kwa kuwa mkarimu kiasi. 5 Ndugu na dada zangu wapendwa, wakati Mwokozi wetu alipohudumu miongoni mwa wanadamu, Yeye aliulizwa na wakili aliyetaka kujua, Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Mathayo imeandikwa kwamba Yesu alijibu: Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 1 Marko anamalizia tukio kwa kauli ya Mwokozi: Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. 2 Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari ya hapa duniani. Vile vile, sisi hatuwezi kikamilifu kuwapenda wenzetu kama sisi hatumpendi Mungu, Baba wa sisi sote. Mtume Yohana alitwambia sisi, Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake pia. 3 Sisi sote ni watoto wa kiroho wa Baba yetu wa Mbinguni, hivyo basi, sisi ni kaka na dada. Tunapokuwa na ukweli huu katika mawazo yetu, kuwapenda watoto wote wa Mungu kutakuwa rahisi. Hakika, upendo ni asili kabisa ya injili, na Yesu Kristo ni Mfano wetu. Maisha yake ni urithi wa upendo. Wagonjwa aliwaponya; waliogandamizwa aliwainua; mwenye dhambi alimwokoa. Mwishoni kundi la watu wenye hasira likaangamiza maisha Yake. Na bado kuna mwangwi kutoka kilima cha Golgotha ya maneno: Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. 4 maonyesho ya kipeo katika huruma na upendo wa maisha ya duniani. Kuna sifa nyingi ambazo ni maonyesho ya upendo, kama vile ukarimu, subira, kujitolea, kuelewa, na msamaha. Katika mahusiano yetu yote, sifa hizi na zinginezo kama hizo zitasaidia kufanya kuwa wazi upendo katika mioyo yetu. Kwa kawaida upendo wetu utaonyeshwa katika mainginiliano yetu na wengine ya siku hadi siku. Kitakachokuwa muhimu sana kitakuwa uwezo wetu wa kutambua mahitaji ya mtu na kisha kujibu. Mimi daima Hivi majuzi nilifahamishwa juu ya mfano wa kugusa sana wa upendo mkarimu mmoja ambao ulikuwa na matokeo yasiyotarajiwa. Ulikuwa mwaka 1933, ambapo kwa sababu ya Mdororo Mkuu, nafasi za ajira zilikuwa nadra. Eneo lilikuwa sehemu ya mashariki mwa Marekani. Arlene Biesecker alikuwa tu ndiye alikuwa amehitimu kutoka shule ya upili. Baada ya kutafuta ajira kwa muda mrefu, yeye hatimaye aliweza kupata kazi katika kiwanda cha nguo kama mshonaji. Wafanya kazi wa kiwanda walikuwa wanalipwa tu kwa vile vipande walivyoshona pamoja kwa ukamilifu kila siku. Jinsi vipande vingi walivyoshona, ndivyo walivyolipwa. Siku moja baada ya kuanza kazi katika kiwanda, Arlene alipambana na utaratibu ambao ulimkanganya na kumvunja moyo. Yeye alikaa kwenye mashini akijaribu kufumua majiribio yaliyoshindikana ili kukamilisha kipande ambacho alikuwa anafanyia kazi. Ilionekana kama hamna mtu wa kumsaidia, kwani washonaji wengine walikuwa wanaharakisha kukamilisha vipande vingi inavyowezekana. Arlene alihisi kukosa usaidizi na matumaini. Kimya, alianza kulia. 1

Upande mwengine kutoka kwa Arlene alikaa Bernice Rock. Alikuwa mzee na mwenye ujuzi zaidi kama mshonaji. Akiangalia masumbuko ya Arlene, Bernice aliacha kazi yake mwenyewe na kwenda upande wa Arlene, kwa ukarimu kutoa maelezo na msaada. Alikaa mpaka Arlene akapata kujiamini na kuweza kukamilisha kipande kimoja. Bernice akarudi kwa mashini yake, baada ya kukosa nafasi ya kukamilisha vipande vingi sana ambavyo angeweza kutengeneza, kama hangesaidia. Kwa tendo hili moja la upendo wa dhati, Bernice na Arlene wakawa marafiki wa maisha. Wote wakaolewa na kuwa na watoto. Wakati fulani katika miaka ya 1950, Bernice, ambaye alikuwa mshiriki wa Kanisa, alimpatia Arlene na familia yeke nakala ya Kitabu cha Mormoni. Mnamo 1960, Arlene na mumewe na watoto wake walibatizwa kama washiriki wa Kanisa. Baadaye walifunganishwa katika hekalu la Mungu. Kama matokeo ya ukarimu ulioonyeshwa na Bernice alipokwenda kusaidia mtu ambaye yeye hakumjua lakini ambaye alikuwa kwenye masumbuko na alihitaji msaada, watu wasio na hesabu, wote walio hai na wafu, sasa wanafurahia ibada za ukoaji ya injili. Kila siku ya maisha yetu sisi tunapatiwa nafasi za kuonyesha upendo na ukarimu kwa wale walio karibu nasi. Alisema Rais Spencer W. Kimball: Sisi sharti tukumbuke kwamba wale watu tuliokutana nao katika bustani, ofisi, lifti, na mahali pengine katika sehemu ya wanadamu Mungu ametupa sisi nafasi ya kupenda na ya kuhudumu. Itatusaidia kidogo kuongea juu ya undugu mkuu wa wanadamu kama hatuwezi kutuwathamini wale ambao waliokaribu nasi kama kaka na dada zetu. 6 Kila mara nafasi zetu za kuonyesha upendo wetu huja bila kutarajiwa. Mfano wa nafasi kama hizo ilitokea kwenye makala ya gazeti katika Oktoba ya 1981. Nilikuwa nimevutiwa na upendo na ukarimu kama huo uliosemwa hapo ambao nimeweka makala iliyokatwa katika faili zangu kwa zaidi ya miaka 30. Makala yanaonyesha kwamba ndege ya Alaska Airlines ya moja kwa moja kutoka Anchorage, Alaska, hadi Seatle, Washington---ikibeba abiria 150 - - - iligeuezwa kwenda mji mdogo wa Alaska ili kumsafirisha mtoto aliyejeruhiwa sana. Mvulana wa miaka miwili alikuwa amekatwa mshipa wa damu katika mkono wake wakati aliangukia kipande cha kioo akicheza karibu na nyumbani kwao. Mji ulikuwa maili 450 (725 kilometa) kusini mwa Anchorage na kwa hakika haikuwa njia ya safari za ndege. Hata hivyo, wahudumu wa hospitali huko walituma maombi ya msaada, na kwa hivyo ndege iligeuzwa kwenda kumchukua mtoto huyu na kumpeleka Seatle ili kwamba aweze kupata matibabu katika hospitali. Wakati ndege ilipotua katika mji mdogo, wahudumu wa hospital walimtaarifu rubani kwamba mvulana alikuwa anavuja damu sana na hangeweza kusafiri hadi Seatle. Maamuzi yalifanywa ya kusafiri maili 200 (320 kilometa) mbali na njia hadi Juneau, Alaska, mji ulio karibu wenye hospitali. Baada ya kumsafirisha mvulana hadi Juneau, ndege ilielekea Seatle, sasa ikiwa masaa mengi kama imechelewa. Hakuna abiria hata mmoja ambaye alilalamika, hata ingawa wengi wao walikosa miadi yao na ndege miunganisho. Kwa kweli, dakika na masaa yaliposonga mbele, walifanya michango, kupata kiwango kikubwa kwa mvulana na familia yake. Ndege ilipokuwa karibu kutua katika Seatle, abiria walijawa na furaha wakati rubani alipotangaza kwamba amepokea habari kwa njia ya redio kwamba mvulana atakuwa salama. 7 Akilini mwangu yanakuja maneno ya maandiko: Lakini hisani ni upendo msafi wa Kristo,... na yeyote atakayepatikana nayo katika siku ya mwisho, itakuwa vyema kwake. 8 Ndugu na kina dada, baadhi ya nafasi kubwa za kuonyesha upendo wetu zitakuwa katika kuta za nyumbani mwetu wenyewe. Upendo unafaa kuwa kitovu cha maisha ya familia, na hali mara nyingi sivyo. Kunaweza kuwa na ukosefu wa subira, mabishano mengi, vita vingi sana, majonzi mengi sana. Rais Gordon B. Hinckley alisikitika: Kwa nini [wale] tunaowapenda [sana] wanakuwa kila mara wanalengwa wa maneno yetu makali? Kwa nini [sisi] wakati mwengine tunasema kama kwa visu ambavyo vinakata upesi? 9 Majibu ya maswali haya yanaweza kuwa tofauti kwa kila mmoja wetu, na hali jambo la msingi ni kwamba sababu hazijalishi. Kama sisi tutaweka amri ya kupendana mmoja na mwengine, sisi sharti tutendeane kwa ukarimu na heshima. Kwa kweli kutakuwa na nyakati ambapo nidhamu inahitajika kutolewa acha sisi tukumbuke, hata hivyo, ushauri unaopatikana katika Mafundisho na Maagano hasa, ambapo inakuwa ni muhimu kwetu sisi kurudiana mmoja na mwengine, sisi baadaye kuonyesha ongezeko la upendo. 10 Mimi ningetumaini kwamba sisi tungejitahidi daima kuwa wazingativu na kuwa wasikivu kwa mawazo na hisia na hali za wale walio karibu nasi. Acha sisi tusidharau au tusipuuze. Badala yake, acha tuwe na huruma na wenye kutia moyo. Sisi ni sharti tuwe makini kwamba tusiharibu kujiamini kwa mtu mwengine kupitia maneno au matendo ya kiholela. Msamaha unafaa kwenda pamoja bega kwa bega na upendo. Katika familia zetu, vile vile na marafiki zetu, kunaweza kuwa na hisia za kuumizwa na kutoelewana. Tena, haijalishi sana jambo ni ndogo kiasi gani. Haiwezi na haifai kuachwa kuharibu, kereketa, na hatimaye kuangamiza. Lawama huacha vidonda kuwa wazi. Msamaha pekee ndio huponya. Mwanamke mwema ambaye kwa sasa ameshaaga dunia alizungumza nami siku moja na bila kutarajia alisimulia majuto fulani. Aliongea 2

juu ya tukio ambalo lilitokea miaka mingi iliyopita mapema na lilihusisha mkulima jirani, wakati mmoja rafiki mwema lakini ambaye yeye na mumewe walikuwa wamekosana mara nyingi. Siku moja mkulima aliomba atumie njia ya mkato kupitia katika shamba lake ili afike shambani mwake. Wakati huu alitua katika usimulizi wake kwangu na, kwa sauti ya kutetemeka, alisema, Ndugu Monson, mimi sikumuacha yeye apitie kwenye shamba letu wakati huo au siku zote bali nilimhitaji yeye achukue njia ndefu kwa miguu kufikia shamba lake. Mimi nilikuwa na makosa, na mimi najuatia hayo. Ameshaenda sasa, lakini eh, mimi natamani ningesema kwake, Nimekosa sana. Jinsi gani natamani ningepata nafasi ya pili ya kuwa mkarimu. Nilipokuwa ninamsikiliza, kulikuja katika akili yangu utambuzi wa kuhuzunisha wa John Greenleaf Whittier: Kati ya maneno yote ya huzuni ya ulimi au kalamu, cha kuhuzunisha sana ni: Ingeweza kuwa! 11 Ndugu na kina dada, tunapowatendea wengine kwa upendo na ukarimu wa kuzingatia, sisi tutaepuka majuto kama hayo. Upendo unaonyeshwa kwa njia nyingi za kutambulika: tabasamu, kupunga mkono, neno la ukarimu, pongezi. Maonyesho mengine yanaweza kuwa si wazi sana, kama vile kuonyesha upendeleo wa shughuli za wengine, kufundisha kanuni kwa ukarimu na subira, kutembelea mtu ambaye ni mgonjwa au hajiwezi kutoka nyumbani. Maneno na vitendo hivi, na vingine vingi, vinaweza kuwasilisha upendo. Dale Carnegie, mtunzi Mmarekani maafuru na mhadhiri, aliamini kwamba kila mtu anayo ndani yake uwezo wa kuongeza jumla ya furaha ya ulimwengu... kwa kutoa maneno machache ya shukrani ya kweli kwa mtu ambaye ni mpweke au amevunjika moyo. Alisema, Labda utaweza kusahau kesho maneno ya ukarimu unayosema leo, lakini mpokeaji ataweza kuyafurahia katika maisha yake yote. 12 Na tuanze sasa, siku ya leo, kuonyesha upendo kwa watoto wote wa Mungu, iwe wao ni wanafamilia wetu, marafiki zetu, watu tunaofahamiana, au hata wageni tu. Tunapoamka kila asubuhi, acha sisi tuamue kujibu kwa upendo na ukarimu kwa kile chochote kinachoweza kuja njia yetu. Zaidi ya ajili ya ufahamu, ndugu na kina dada, ni upendo wa Mungu kwetu sisi. Kwa sababu ya upendo huu. Yeye alimtuma Mwanawe, ambaye alitupenda sisi ya kutosha kutoa maisha Yake kwa ajili yetu, kwamba tuweze kupata uzima wa milele. Tulipokuja kuelewa kipawa hiki kisischokuwa na kifani, mioyo yetu itajawa na upendo kwa Baba yetu wa Milele, kwa Mwokozi wetu, na kwa wanadamu wote. Kwamba hiyo iwe hivyo ndiyo maombi yangu ya dhati katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina MUHTASARI 1. Mathayo 22:36 39 2. Marko12:31 3. 1 Yohana 4:21. 4. Luka 23:34 5. Mtunzi hajulikani, katika Richard L. Evance, The Quality of Kindness, Improvement Era 6. The Teachings of Spencer W. Kimball, ed. Edward L. Kimball (1982), 483. 7. Ona Injured Boy Flown to Safety, Daily Sitka Sentinel (Alaska), Oct. 22, 1981. 8. Moroni 7:47. 9. Gordon B. Hinckley, Let Love Be the Lodestar of Your Life, Ensign, Mei 1989, 67. 10. Ona Mafundisho na Maagano 121:43. 11. Maud Muller, in The Complete Poetical Works of John Greenleaf Whittier (1878), 206; emphasis added. 12. Dale Carnegie, in, for example, Larry Chang, Wisdom for the Soul (2006), 54 Mafundisho ya Wakati Wetu Kuanzia Mei 2014 hadi Oktoba 2014, masomo ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina mama katika Jumapili ya nne lazima yaandaliwe toka kwenye moja ya maongezi yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa Aprili 2014. Mwezi Oktoba 2014, maongezi yanaweza kuchukuliwa toka kwenye mkutano mkuu wa Aprili 2014 au Oktoba 2014. Marais wa wilaya na vigingi lazima wachague ni maongezi gani yatatumika kwenye maeneo yao, au wanaweza kutoa majukumu kwa maaskofu au maraisi wa tawi. Hotuba zinapatikana kwa lugha nyingi katika conference.lds.org. 2014 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Printed in USA. English approval: 6/13. Translation approval: 6/13. Tafsiri ya First Presidency Message, May 2014. Swahili. 10865 743 3

UJUMBE WA MWALIMU MTEMBELEZI, MEI 2014 Ndugu na dada zangu, baadhi yenu mlialikwa katika mkutano huu na wamisionari wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hao wamisionari huenda tayari walishawaalika kufanya chaguzi za kuweka maagano na Mungu kwa njia ya ubatizo. Wengine mnasikiliza kwa sababu mliitikia wito wa mzazi, mke, au huenda mtoto, uliotolewa kwenu kwa matumaini kwamba mtachagua kuweka maagano ambayo tayari mmeweka na Mungu katika ya maisha yako. Baadhi yenu ambao mnasikiliza tayari mmeshafanya uchaguzi wa kurudi kumfuata Mwokozi na leo mnahisi furaha ya kumkaribisha. Yoyote yule na popote ulipo, katika mkono wako unashikilia furaha ya watu wengi zaidi ya vile unavyofikiria. Kila siku na kila saa unaweza kuchagua kuweka au kushika agano na Mungu. Popote ulipo katika njia ya kurithi zawadi ya uzima wa milele, una nafasi ya kuwaonyesha watu wengi njia ya furaha kubwa. Unapochagua kama utafanya ama utaweka agano na Mungu, unachagua kama utaacha Na Rais Henry B. Eyring Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza Urithi wa Tumaini Lisilo na Gharama urithi wa tumaini kwa wale ambao huenda wakafuata mfano wako. Wewe na mimi tumebarikiwa na ahadi ya urithi kama huo. Ninawajibika kwa ajili ya wingi wa furaha yangu maishani kwa mtu ambaye sikuwahi kutana naye katika maisha ya duniani. Alikuwa yatima ambaye alikuwa mmoja wa mababu zangu. Aliniachia urithi wa tumaini wa thamani mno. Acheni niwaelezee jukumu alilotekeleza katika kujenga urithi huo kwa ajili yangu. Jina lake lilikuwa Heinrich Eyring. Alizaliwa katika utajiri mwingi. Baba yake, Edward, alikuwa na ardhi kubwa huko Coburg, ambayo sasa ni Ujerumani. Mama yake aliitwa Viscountess Charlotte Von Blomberg. Babake alikuwa mlinzi wa ardhi kwa ajili ya Mfalme wa Prussia. Heinrich alikuwa mtoto wa kwanza wa Charlotte na Edward. Charlotte aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 31, baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa tatu. Edward aliaga dunia punde baadaye, akiwa amepoteza nyumba zake na mali yake yote katika biashara iliyoanguka. Alikuwa na umri wa miaka 40 peke yake. Aliwaacha watoto watatu mayatima. Heinrich, babu yangu, alikuwa amewapoteza wazazi wake wote na urithi mkubwa wa kidunia. Hakuwa na hela. Aliandika katika historia yake kwamba alihisi kwamba tumaini lake la maisha mazuri lilikuwa kwenda Marekani. Ingawa hakuwa na familia wala marafiki kule, alikuwa na hisia ya tumaini kuhusu kwenda Marekani. Kwanza alikwenda katika Jiji la New York. Baadaye alihamia St. Louis, Missouri. Huko St. Louis mmoja wa wafanyakazi wenzake alikuwa ni Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Kutoka kwake alipata kijitabu kilichoandikwa na Mzee Parley P. Pratt. Alikisoma na kisha akajifunza kila kitu angepata kuhusu Watakatifu wa Siku za Mwisho. Aliomba kujua kama ni kweli kulikuwa na malaika ambao waliwajia binadamu, kama kulikuwa na nabii aliye hai, na kama alikuwa amepata dini ya kweli. Baada ya miezi miwili ya kujifunza na kuomba kwa makini, Heinrich alikuwa na ndoto ambayo aliambiwa abatizwe. Mtu ambaye jina lake na mamlaka ya ukuhani ninaheshimu, Mzee William Brown, angetekeleza agizo hili. Heinrich alibatizwa katika bwawa la maji ya mvua mnamo Machi, 11, 1855, saa 7:30 asubuhi. Ninaamini kwamba Heinrich alijua wakati huo kwamba kile ninawafunza hivi leo ni kweli. Alijua kwamba furaha ya uzima wa milele huja kupitia uhusiano wa familia ambao huendelea milele. Hata wakati alikuwa amepata mpango wa furaha wa Bwana hivi karibuni, alijua kwamba tumaini lake la furaha ya milele lilitegemea 1

chaguo la kibinafsi la wengine kufuata mfano wake. Tumaini lake la furaha ya milele lilitegemea watu ambao bado hawakuwa wamezaliwa. Kama sehemu ya urithi wa familia yetu ya tumaini, aliaacha jarida la historia kwa kizazi chake. Katika jarida hilo la historia ninaweza kuhisi upendo wake kwa wale miongoni mwetu ambao wangemfuata. Kutoka kwa maneno yake ninahisi tumaini lake kwamba kizazi chake kingechagua kumfuata kwenye njia kurudi nyumbani kwetu mbinguni. Alijua kwamba haingekuwa chaguo moja kuu kufanya hivyo lakini chaguo nyingi ndogo ndogo. Ninanukuu toka kwenye historia yake: Kutoka mara ya kwanza nilimsikia Mzee Andrus akizungumza daima nimehudhuria mkutano wa Watakatifu wa Siku za Mwisho na nyakati ambazo nimeshindwa kuhudhuria mkutano, wakati huohuo ukiwa ni wajibu wangu kufanya hivyo. Ninaandika haya katika jarida langu ili kwamba watoto wangu waweze kuiga mfano wangu na kamwe wasipuuze wajibu huu muhimu kukusanyika pamoja na Watakatifu. 1 Heinrich alijua kwamba katika mikutano ya sakramenti tungeweza kufanya upya ahadi yetu kumkumbuka Mwokozi daima na kupata Roho Wake kuwa nasi. Ni roho hiyo ambayo ilimhimili kwenye misheni yake ambako aliitwa miezi michache tu baada ya kukubali agano la ubatizo. Aliacha kama urithi wake mfano wake wa kubaki mwaminifu kwa misheni yake kwa miaka sita katika sehemu ambayo wakati huo iliitwa Indian Territories. Ili kupokea kuachiliwa kwake kutoka misheni yake, alitembea kutoka Oklahoma hadi Jiji la Salt Lake, umbali wa takribani maili 1,100 (1,700km). Muda mfupi baadaye aliitwa na nabii wa Mungu kuhama na kwenda Utah kusini. Kutoka hapo alikubali wito mwingine kuhudumu misheni katika nchi yake ya kuzaliwa, Ujerumani. Kisha alikubali aliko la Mtume wa Bwana Yesu Kristo kusaidia kujenga makoloni ya Watakatifu wa Siku za Mwisho kule Mexico kaskazini. Kutoka hapo aliitwa kwenda Jiji la Mexico kama mmisionari wa muda. Alitekeleza wito huu. Amezikwa katika mavani madogo kule Colonia Juárez, Chihuahua, Mexico. Nasoma mambo haya si kudai ukuu kwa ajili yake ama kwa ajili ya yale aliyofanya ama kwa ajili ya kizazi chake. Ninayasoma ili kumheshimu kwa ajili ya mfano wake wa imani na tuamini ambalo lilikuwa moyoni mwake. Alikubali miito hii kwa sababu ya imani yake kwamba Kristo aliyefufuka na Baba yetu wa Mbinguni walikuwa wamemjia Joseph Smith katika kichaka cha miti katika jimbo la New York. Alizikubali kwa sababu alikuwa na imani kwamba funguo za ukuhani katika Kanisa la Bwana zilikuwa zimerejeshwa na uwezo wa kuunganisha familia milele, kama tu wangekuwa na imani ya kutosha kuweka maagano yao. Kama Heinrich Eyring, babu yangu, huenda ukawa wa kwanza katika familia yako kuongoza njia kuelekea kwa uzima wa milele kwenye njia ya maagano matakatifu yaliyofanywa na kuwekwa kwa bidii na imani. Kila agano linaleta majukumu na ahadi. Kwa kila mmoja wetu, kama tu vile yalivyokuwa kwa Heinrich, majukumu hayo wakati mwingine huwa ni rahisi lakini mara nyingi huwa ni ngumu. Lakini kumbuka, majukumu lazima wakati mwingine yawe magumu kwa sababu malengo yao ni kutusongesha kwenye njia ya kuishi milele na Baba wa Mbinguni na Mwana Wake Mpendwa, Yesu Kristo. Unakumbuka maneno kutoka katika kitabu cha Ibrahimu: Na hapo akasimama mmoja miongoni mwao ambaye alifanana na Mungu, naye akasema kwa wale waliokuwa pamoja naye: Sisi tutakwenda chini, kwani kuna nafasi huko, nasi tutachukua vifaa hivi, nasi tutaifanya dunia mahali ambapo hawa watapata kukaa; Nasi tutawajaribu kwa njia hii, ili kuona kama wao watafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu wao atawaamuru; Na wao ambao watatunza hali yao ya kwanza wataongezewa; na wao ambao hawatatunza hali yao ya kwanza hawatapata utukufu katika ufalme ule ule pamoja na wale walioitunza hali yao ya kwanza; nao wale watakaoitunza hali yao ya pili watapata kuongezewa utukufu juu ya vichwa vyao kwa milele na milele. 2 Kutunza hali yetu ya pili kunategemea kufanya kwetu maagano na Mungu na kwa imani kutekeleza majukumu ambayo yanatutarajia. Inahitaji imani katika Yesu Kristo kama Mwokozi wetu kuweka maagano takatifu kwa maisha yetu yote. Kwa sababu Adamu na Hawa walianguka, kila mmoja wetu hupitia majaribio, mateso, na kifo kama urithi wetu. Hata hivyo, Baba yetu mpendwa wa Mbinguni alitupa karama ya Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo, kama Mwokozi wetu. Karama hiyo kuu na baraka ya Upatanisho wa Yesu Kristo unaleta urithi kwa kila mtu: ahadi ya Ufufuo na uwezekano wa uzima wa milele kwa wote wazaliwao. Baraka kuu ya zote za Mungu, uzima wa milele, itatujia tu tunapofanya maagano yanayowezeshwa katika Kanisa la kweli la Yesu Kristo na watumishi wake walio na mamlaka. Kwa sababu ya Kuanguka, sote tunahitaji matokeo ya kusafisha ya ubatizo na kuwekelewa mikono ili kupokea karama ya Roho Mtakatifu. Ibada hizi lazima zifanywe na wale ambao wana mamlaka sahihi ya ukuhani. Kisha, kwa usaidizi wa Roho ya Kristo na Roho Mtakatifu, tunaweza kuweka maagano yote tunayofanya na Mungu, hasa yale ambayo yanatolewa katika mahekalu Yake. Ni kwa njia hii peke yake, na kwa usaidizi huo, yeyote anaweza kudai urithi 2

wake wa haki kama mtoto wa Mungu katika familia milele. Kwa baadhi wanaonisikiliza, hiyo inaweza kuonekana kuwa ndoto isiyowezekana kabisa. Mmewaona wazazi waaminifu wakihuzunika kwa ajili ya watoto wao ambao wamekataa ama ambao wamechagua kuvunja maagano yao na Mungu. Lakini wazazi hao wanaweza kupata faraja na tumaini kutoka kwa yale wazazi wengine wamepitia. Watoto wa Alma na Mfalme Mosia walitubu kutoka kwa uasi wao mkuu dhidi ya maagano na amri za Mungu. Alma Mdogo alimuona mwanawe Koriantoni akigeuka kutoka kwa kutenda dhambi mbaya sana hadi kwa utumishi wa imani. Kitabu cha Mormoni kinarekodi muujiza wa Walamani kutofuata tena utamaduni wa kuchukia haki na kuahidi hadi kifo kudumisha amani. Malaika alitumwa kwa Alma mdogo na wana wa Mosia. Malaika alikuja kwa sababu ya imani na maombi ya akina baba zao na ya watu wa Mungu. Kutoka kwa mifano hiyo ya uwezo wa Upatanisho kushawishi fikira na hisia za watu, mnaweza kupokea ujasiri na faraja. Bwana ametupa sote chanzo cha tumaini tunapopambana kuwasaidia wale tunaowapenda kukubali urithi wao wa milele. Ametupa ahadi tunapozidi kujaribu kuwakusanya watu Kwake, hata wakati wanapinga aliko Lake kufanya hivyo. Kupinga kwao kunamhuzunisha, lakini kamwe hakomi, nasi hatupaswi kukoma. Anatoa mfano mkamilifu kwetu sisi na upendo Wake unaoendelea: Na tena, mara ngapi ningemkusanya kama vile kuku hukusanya vifaranga wake chini ya mabawa yake, ndio, Ee ninyi watu wa nyumba ya Israeli, ambao mmeanguka; ndio, Ee ninyi mnaoishi Yerusalemu, kama vile wale ambao wameangamizwa; mara ngapi ningekuwa nimewakusanya kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake, na hamnikubali. 3 Tunaweza kuegemea hamu hiyo isiyokwisha ya Mwokozi kurudisha kila mmoja wa watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni nyumbani kwao kuwa Naye. Kila mzazi, akina babu, na wahenga waaminifu wanashiriki katika hamu hii. Baba wa Mbinguni na Mwokozi ni mifano yetu mikamilifu ya kile ambacho tunaweza kufanya na lazima tufanye. Kamwe hawatulazimishi kuchagua wema kwa sababu wema lazima ichaguliwe. Wao hufanya ili tuweze kutambua kile ambacho ni chema, na hutusaidia kuona kwamba matunda yake ni mazuri. Kila mtu azaliwaye duniani hupokea Mwanga wa Kristo, ambao hutusaidia kuona na kuhisi kile ambacho ni cha haki na kile ambacho ni kibaya. Mungu ametuma watumishi binaadamu ambao wanaweza, kupitia Roho Mtakatifu, kutusaidia kutambua kile angetaka tufanye na kile ambacho amekataza. Mungu hufanya iwe ya kuvutia kuchagua haki kwa kuturuhusu kuhisi madhara ya uchaguzi wetu. Kama tukichagua haki, tutapata furaha- hatimaye wakati huo Tukichagua mabaya, kunakuja huzuni na majuto baada ya muda. Madhara hayo hakika huja. Hata hivyo mara nyingi huchelewa kwa makusudi. Kama baraka zingekuja mara moja, kuchagua haki hakungejenga imani. Na kwa sababu huzuni pia wakati mwingine hucheleweshwa vikubwa, huchukua imani kuhisi haja ya kuomba msamaha kwa dhambi mapema badala ya baada ya kuhisi madhara yake na huzuni na uchungu. Baba Lehi alihuzunika juu ya chaguo zilizofanywa na baadhi ya wanawe na familia zao. Alikuwa mtu mzuri sana na mwenye haki - nabii wa Mungu. Mara nyingi alishuhudia Mwokozi wetu, Yesu Kristo, kwao. Alikuwa mfano wa utii na utumishi wakati Bwana alimwita kuacha mali yake yote ya kidunia ili kuokoa familia yake kutokana na maangamizi. Mwishoni mwa maisha yake, alikuwa bado anawashuhudia watoto wake. Kama Mwokozi na licha ya uwezo wake wa kubainisha mioyo yao na kuona siku za usoni za kusikitisha na za ajabu Lehi aliendelea kusaidia familia yake ili kuwaleta kwa wokovu. Hivi leo mamilioni ya watoto wa Baba Lehi wanatoa sababu ya tumaini lake kwa ajili yao. Unaweza kufanya nini ili kujifunza kutoka kwa mfano wa Lehi? Tunaweza kufanya hivyo kwa kujifunza maandiko kwa maombi na kwa uchunguzi. Napendekeza kwamba ufikirie kuhusu muda mfupi na muda mrefu unapojaribu kutoa urithi wa tumanini kwa familia yako. Katika muda mfupi, kutakuwa na matatizo na Shetani atatumia nguvu zake kutujaribu. Na kuna vitu vya kusubiri kwa uvumilivu, kwa imani, mkijua ya kwamba Bwana hutenda kwa wakati Wake mwenyewe na katika njia Yake mwenyewe. Kuna vitu unavyoweza kufanya mapema, wakati wale uwapendao ni wadogo. Kumbuka kwamba maombi ya familia ya kila siku, kujifunza maandiko kwa familia, na kushirikisha ushuhuda wetu katika mkutano wa sakramenti ni rahisi na ina mdhara zaidi wakati watoto ni wadogo. Watoto wadogo mara nyingi huwa na mvutio zaidi kwa Roho kuliko vile tunavyotambua. Wakati wamekuwa kiasi, watakumbuka nyimbo walizoimba na wewe. Hata zaidi ya muziki, watakumbuka maneno ya maandiko na ushuhuda. Roho Mtakatifu anaweza kuleta mambo yote kwa kumkumbuka yao, lakini maneno ya maandiko na nyimbo itakumbukwa kwa muda mrefu zaidi. Kumbukumbu hizo zitawashawishi kurudi wanapotanga kwa muda, pengine kwa miaka, kutoka kwa njia inayoelekeza nyumbani kwa uzima wa milele. Tutahitaji kufikiria juu ya muda mrefu wakati wale tunaowapenda wanahisi ushawishi wa dunia na 3

wingu la shaka likionekana kushinda imani yao. Tuna imani tumaini na hisani kutuongoza na kuwapa nguvu. Nimeona kwamba kama mshauri kwa manabii hai wawili wa Mungu. Ni watu wenye sifa za kipekee zaidi. Hata hivyo wanaonekana kushiriki matumaini thabiti. Wakati mtu akileta jambo la wasiwasi kuhusu kitu katika Kanisa, majibu yao ya mara kwa mara ni Ee, mambo yatakuwa sawa. Wao hujua zaidi kuhusu tatizo hilo kwa kiwango kikubwa kuliko watu wanaoleta jambo hilo. Pia wanajua jinsi Bwana hufanya vitu, na hivyo wao daima huwa na matumaini kuhusu ufalme Wake. Wanajua anaongoza kanisa. Ana nguvu zote na anajali. Kama Ukimkubali awe kiongozi wa familia yako, mambo yatakuwa sawa. Baadhi ya wajukuu wa Heinrich Eyring hawajafuata njia ya wema. Lakini wengi wa wajukuu wake huenda mahekalu ya Mungu saa 12:00 asubuhi kuwafanyia maagizo mababu ambao hawajawahi kukutana nao. Wao huenda kwa sababu ya urithi wa tumaini alioacha. Aliacha urithi ambao unadaiwa na wengi wa kizazi chake. Baada ya yote tunayoweza kufanya katika imani, Bwana atahalalisha matumaini yetu kwa baraka kubwa zaidi kwa ajili ya familia zetu kuliko tunavyoweza kufikiria. Anataka mazuri kwa ajili yao na kwa ajili yetu, kama watoto Wake. Sisi sote ni watoto wa Mungu aliye hai. Yesu wa Nazareti ni Mwana Wake Mpendwa na Mwokozi wetu aliyefufuka. Hili ni Kanisa Lake. Ndani yake kuna funguo za ukuhani, na hivyo basi familia zinaweza kuwa milele. Huu ni urithi wetu wa tumanini. Nashuhudia kwamba ni kweli katika jina la Yesu Kristo, amina. MUHTASARI 1. Ona Henry Eyring reminiscences, 1896, typescript, Church History Library, 16 21. 2. Ibrahimu 3:24 26. 3. 3 Nefi 10:5. 2014 na Intellectual Reserve, Inc.Haki zote zimehifadhiwa. Printed in USA. English approval: 6/13. Translation approval: 6/13. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, May 2014. Swahili. 10865 743 4