Banana Investments Ltd

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Human Rights Are Universal And Yet...

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

United Pentecostal Church June 2017

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

ORDER NO BACKGROUND

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Upande 1.0 Bajeti yako

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Newsletter. RC Arusha: I assure you my full support for Zone office. Motto: Fair Regulation for Positive IMPACT NOT FOR SALE SEPTEMBER 2017

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

TIST HABARI MOTO MOTO

Ndugu na dada zangu wapendwa,

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

MSAMAHA NA UPATANISHO

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Mipango ya miradi katika udugu

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

K. M a r k s, F. E n g e l s

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

PDF created with pdffactory trial version

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NNE. Kikao cha Nane Tarehe 23 Juni, 2006

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

2

EWURA scoops the highest rank in Africa s regulatory dispensation

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Transcription:

Toleo la 21 Jarida litolewalo na; Banana Investments Ltd TOLEO NAMBA 21 HALIUZWI APRIL JUNE HALIUZWI

BODI YA WAHARIRI YALIYOMO Augustine Minja Mwenyekiti 078 5451 004 Gerald Lyimo Mjumbe Beatha Anthony Mhariri Mkuu 0717 350 971 Emanuel Nevava Mjumbe 0756 601 830 1.MAONI YA MHARIRI.02 2. HABARI KUTOKA SINGIDA...02 3. BANANA SPORTS CLUB YAJIPANGA UPYA..03 4. KAMPUNI YABORESHA MASOKO.03 5. SAFARI YANGU YA LOLIONDO.03 6. KAMPUNI YASHIRIKI MEI MOSI 2011...04 7. BOHARI MPYA YAFUNGULIWA MOROGORO...05 8 HABARI HUTOKA BOHARI YA DSM..05 9. MPANGO WA KAMPUNI KUSAFISHA MAJI TAKA 06 10. DONDOO MUHIMU ZA UNYAJI WA VILEO.. 06 11. AJIRA MPYA NGUVU MPYA..07 12. Y S MEN ARUSHA WAPOKEA UGENI KUTOKA GENEVA...07 SALAMU ZA MHARIRI Ni mara nyingine tena toleo la Mbiu ya Banana linatoka na kwa habari mbalimbali. Toleo hili tumeweka habari kutoka mikoa mbalimbali ambayo kampuni yetu inasambaza bidhaa zake. Hii ni kuonyesha kwamba kampuni inawajali wateja wake wote popote pale walipo. Tungependa sana kupokea makala kutoka kwa wateja wetu. Pia tunashauri kwamba makala hizo ziwe fupi na pia kwa namna moja au nyingine zihusiane na kampuni. Kwa wale wateja wetu ambao wataandika makala yao wazitume kwa kupitia magereva wetu wa Mauzo au wasambazaji. Pia unaweza kuleta hapa kiwandani na ukakabidhi mapokezi. Makala itakayochapishwa kwenye jarida mwandishi atalipwa kiasi cha shilingi 10,000/=. Tunatumia tena nafasi hii kuwakarisha katika kampuni ya Banana Investments Ltd watengenezaji na wasambazaji wa mvinyo halisi wa Ndizi. Kwa mawasiliano zaidi tumia namba za simu zilizopo ukurasa wa mwisho wa Jarida hili. WATU NA MATUKIO BI TECLA EDUARD, AFISA UGAVI APATA MWENZA Ilikua ni siku ya Alhamis tarehe 5/5/2011 yalisikika matatumbeta katika kijiji cha Oloirien, pale Bi Tecla akitokea nyumbani kwao kuelekea katika ukumbi wa kifahari wa Golden Rose ambapo wazazi wake alikua wamemuandalia tafrija kwa ajili ya kumuaga kwenda kuanza maisha ya kifamilia na Bw. Godbless Msuya wa Moshi. Baada ya sherehe hizo siku ya Jumamosi tarehe 7/5/2011 ilifanyika ibada ya ndoa takatifu katika kanisa la KKKT CKMC Moshi na kufuatiwa na sherehe zilizofanyika ukumbu wa chuo cha Ushirika hukohuko Moshi. Bwana harusi ni Afisa masoko wa TBL na Bibi harusi ni Afisa Ugavi wa Banana Investments Ltd. Beatha Anthony. 2 HALIUZWI

BANANA SPORTS CLUB YAJIPANGA UPYA KAMPUNI YADHAMIRIA KUBORESHA MASOKO Baada ya kimya kirefu sasa ile Club maarufu ya Banana imeanza kujipanga upya ili kuendeleza shughuli za michezo na utalii wa ndani na nje ya nchi. Ili kuhakikisha kuwa mipango yake yote inafanikiwa Club hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi katika ngazi za Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina na wajumbe wane. Viongozi hao wanatarajiwa kuwa wabunifu hasa kwa kuanzisha miradi itakayoongeza kipato cha Vlubu na kukusanya ada za wanachama kwa wakati. Pia Club hii inatarajia kuingia ubia na Club ya Genuine Sports Club iliyopo maeneo ya Kijenge Backdad kwaajili ya kufanya mazoezi ya viungo ya kunyanyua vyuma na Aerobics. Wanachama wanaombwa kuwa tayari kulipa ada zao za mwezi ili kuwezesha mipango yote hii. Adrian Anthony Katika kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, kampuni imesogeza huduma zake kwa karibu zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Dodoma. Hii ni pamoja na kuajiri wawakilishi wa masoko katika mikoa hiyo. Wawakilishi hao ambao wameanza kazi ya rasmi mwezi wa tano, 2011 pamoja na mambo mengine watasikiliza na kutatua matatizo mbalimbali ya wateja, watatoa fursa kwa wateja wapya watakaokua tayari kufanya biashara na kampuni yetu pia kuhakikisha kwamba bidhaa zetu zinafika kwa wateja kwa wakati unaotakiwa. Wawakilishi hao ni 1. MANYARA Patrice B. Menda - Namba ya simu 0754 299529 0785 945067 2. DODOMA Denis Kessy- Namba ya simu 0713 778958 0762 966988 3. KILIMANJARO Tumaini A Mungete Namba ya simu 0754 299529 0688 299529 0715 229529 Kwa wateja wetu waliopo maeneo hayo wawasiliane na hawa wawakilishi ili waweze kupata huduma kwa haraka zaidi. Emanuel Nevava NI M BAYA KWA KULINGANISHWA NA NINI HASA? Kuna mengi tusiyoyajua! Miongoni mwa wanafalsafa maarufu duniani ni Mgiriki Socrates. Kwa wale wanaosoma na kufuatilia maisha ya wanafalsafa wa kale hapa duniani, huenda watakuwa wanajua kuhusu ndoa ya mwanafalsafa huyu maarufu. Wanaofuatilia maisha ya wanafalsafa hao watakubaliana nami kuhusu mke wa Socrates. Watu au wenzake Socrates walipokuwa wanamuuliza kuhusu mke wake, wakitegemea kusikia akilalamika, kwa sababu mama huyu alikuwa na ghubu sana, hawakusikia malalamiko yoyote. Badala yake aliwauliza, mnataka kujua yukoje kwa kulinganisha na nini? Ni hivi, iwe ni kwa watu, maeneo, hali, matukio, na hata hisia zetu vyote hivyo havina maana yenye kulingana kwa watu wote. Vyote hivyo ni vizuri au vibaya kwa viwango kwa kutegemea tunavilinganisha na nini. Hebu tuchukue vikombe vya aina moja, kama kimoja kimebenduka, tunaweza kusema hakiko kamili. Ni rahisi kusema hivyo kwa sababu, tuna mahali pa kulinganisha, ambapo ni kwenye vile vikombe vingine vizima. Kwa binadamu hali ni tofauti kabisa, kwa sababu wote ni tofauti. Hebu fikiria kuhusu tukio fulani kwenye maisha yako. Lakini bado kuna swali, kwa kulinganisha na tukio lipi? Kila tukio linatokea mahali pake, muda wake na kwa sababu fulani ili maisha yaendelee kuwepo. Kwa nini kama ni hivyo udhani tukio fulani ni baya au zuri? Huu ubaya au uzuri ni kwa kulinganisha na tukio lipi wakati kila tukio lina mahali, muda,na sababu ya kutokea kwake? Tunaambiwa kwamba kila jambo ambalo linaingia kwenye mfumo wetu wa kufikiri ni vizuri au vema likawa limepimwa kwa mujibu wa tafsiri zetu ambazo hazipaswi kutuumiza. Unaona jambo ambalo linataka kukuumiza kihisia, ni kwa nini usijiulize kama jambo hilo ni baya, ni kwa kulinganisha na lipi? Kumbuka ni lazima kuwe na mahali ambapo tunasimama ili kupima uzuri au ubaya wa jambo kwa kulinganisha na mengine, ambayo kwa kawaida hayatarajiwi kubadilika. Kama yanabadilika, basi ni vigumu kusema kuwa ni mabaya au mazuri, kwani hatuna mahali pa kuyalinganisha. Kama vikombe vinavyofanana kabatini vingekuwa wakati mwingine kimoja kinakuwa kirefu kingine kifupi au kinabadilika rangi, tusingeweza kuvilinganisha pia. Binadamu kila mmoja ana haiba yake, kila mmoja ni yeye kwa tabia, mienendo na hata miili. Na, Peter Mapunda. 3 HALIUZWI

Toleo la 21 KAMPUNI YASHIRIKI MAONESHO SIKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI Kampuni ya Banana Investments Ltd imekua ikishiriki maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi kwa miaka mingi. Na kila mwaka huibuka na ushindi mnono. Mwaka huu vilevile kampuni imejinyakulia makombe mawili ikiwa ni pamoja na mashindano ya maandamano ya miguu na naonesho ya bidhaa kwenye maandamano ya magari. Magari ya Maonesho ya kampuni yakipita mbele ya mkuu wa Mkoa yakiwa yamepambwa vizuri. Maandamono ya Magari yakiongozwa na Pikipiki za kampuni Katika kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapongeza uongozi wa kampuni uliandaa tafrija fupi iliyofanyika katika ukumbi wa kampuni mara baada ya sherehe ya uwanjani. Karika tafrija hiyo ambayo ilijumuisha wafanyakazi tu, mkurugenzi mkuu alitoa hotuba fupi akiwashukuru wafanyakazi wote kwa moyo wao wa utendaji pamoja na kushiriki katika maonesho hayo. Pia aliahidi kuwa kampuni itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi kwa uaminifu na kuomba pia wafanyakazi wonyeshe uzalendo na uaminifu katika kufanya kazi za kampuni. Pia aliwatakia sherehe njema ingawa na yeye pia alikuwepo mpaka mwisho wa tafrija. Mkurugenzi msaidizi akikabidhiwa ngao ya ushindi na mkuu wa Mkoa. Baada ya hotuba ya Mkurugenzi mtendaji wafanyakazi waliendelea kupata chakula na vinywaji na baadae lilipigwa disco la nguvu na Dj Rogaa. Sherehe iliisha salama na kila mfanyakazi kurejea nyumbani. Beatha Anthony Wafanyakazi wakiburudika na kinywaji na Muziki. 4 HALIUZWI

Toleo la 21 BOHARI MPYA YAFUNGULIWA MOROGORO Maendeleo ni hatua. Banana Investsments Ltd imepiga hatua moja kati ya hatua nyingi, ya kufungua bohari mjini Morogoro ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja wake. Bohari hii ipo maeneo ya Kihonda Magorofani Polyester Club mkabala na Carmel/Kanisa Katoliki. Fika ofisini au: Picha: Jengo ambalo linatumika kama bohari kabla ya marekebisho. Polyester Club Kihonda. 0713791119/0788791119/0759980851 Simu: Wateja wa mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani sasa Email: michael@banana.co.tz watahudumiwa vizuri kutokana na uwepo wa bohari RAHA: RAHISI: HALISI. BIDHAA BORA YA BANANA hii. Kampuni inakaribisha maoni, ushauri na mawainvestments LTD - ARUSHA kala maeneo ya Turiani, Kilosa, Ifakara, Morogoro vijijini, na Mahenge. Wasiliana na afisa masoko Michael Emanuel kwa maelezo zaidi. TANZIA HABARI KUTOKA SINGIDA Kampuni ya Banana Investments Ltd unasikitika kutangaza vifo vya wafanyakazi wawili wafuatao:- Baada ya kampuni kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma mojakwa moja kwa wateja wake, sasa wananchi wa Mkoa wa Singida wanafurahia huduma hiyo kwani wanapata bidhaa yetu hususani Raha kwa bei nzuri inayo wawezesha kupata faida nono. Kampuni kwa kushirikiana na wasambazaji wake wanefanya upatikanaji wa kinywaji cha RAHA kuwepo na pia kuhakikisha kwamba bei yake inamuwezesha hata mwananchi ya kawaida kuweza kununua. Kampuni kupitia muwakilishi wake aliyeko mkoani Singida Ndg Frank Joseph Urio inakaribisha ushauri,maoni, kutoka kwa wateja mbalimbali katika kuboresha biashara yake kwa faida ya wateja na kampuni kwa ujumla. Mwakilishi wetu sasa anapatikana kwenye ofisi iliyoko eneo la Shule ya Msingi Mughanga chumba namba 23, Au wasiliana nae kwa simu namba 0754 607715, 0786 607718. Frank Joseph Urio Bi. Editha Joachim alifariki tarehe 03.02.2011 na kuzikwa tarehe 08.02.2011 nyumbani kwake Moshono - Arusha. Bi Editha aliyekuwa anafanya kazi katika Idara ya Uzalishaji ameacha mtoto mmoja na wajukuu wawili. Mungu ailaze roho ya Marehemu Editha mahala pema peponi Amina. 5 Bw. Uhuru Kawiche alifariki tarehe 15.05.2011 na kuzikwa tarehe 19.05.2011 nyumbani kwake Marangu Mamba mkoa wa Kilimanjaro. Bw. Uhuru alikuwa anafanya kazi katika Idara ya Uzalishaji. Bw. Uhuru ameacha mke pamoja na watoto. Mungu ailaze roho ya Marehemu Uhuru mahala pema peponi Amina. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE Joan Mrema HALIUZWI

DONDOO MUHIMU ZA UNYWAJI SALAMA WA KILEO ALCOHOL Kileo ni kitu chochote kinacholevya kilicho katika mfumo wa bia, mvinyo, ama spirits. Jamii yote duniani iwe Africa, Ulaya, Asia na hata Amerika, imekuwa na aina yake ya kileo kulingana na utamaduni wake. Wengi wameathirika kutokana na kutozingatia njia nzuri za unywaji salama. Umri wako unaruhusu? Kama una miaka chini ya miaka 18, USIJARIBU NA ACHA KILEO. Hapa chini ni dondoo muhimu kuhusu unywaji ulio salama: Daima zingatia chakula kwanza kabla ya kileo/ pombe. Watalamu wanashauri ule vyakula vyenye protini mfano nyama, samaki, jibini cheese kwa kuwa vyenyewe vinauwezo wa kupunguza kasi ya kileo kuingia katika mzunguko wa damu kukuepusha na madhara. Kubali kinywaji pale ukitakapo. Wengi wetu tumekuwa wataalamu wa ofa ya hapa na pale hata kama mtu umetoka hospitalini leo ukiambiwa ebwana karibu tule vitu, unavamia kileo. Je nafsi yako ipo tayari? Kumbuka nafsi yako ni muhimu sana kwenye maamuzi. Epa kileo kama unatumia Dawa. Kama unaumwa na unatumia dawa, acha kileo. Kama kuna umuhimu sana wa kunywa, omba ushauri kwa mtaalamu wa afya kwanza. Epa unywaji ukiwa na njaa na kwenye joto kali (juani). Wataalamu wanasema utapata kizunguzungu, udhaifu/legea, na kupoteza mood hali iitwayo hypoglycemia, Zingatia usalama wa maisha yako na wengine barabarani. Kama unajua utaendesha chombo cha moto (gari, pikipiki hata baiskeli) Uhalali wa kinywaji chenyewe; Kila kinywaji kina utaalamu wake unaokubalika kwa mnywaji kutoka kwa mamlaka husika. Tanzania tuna mamlaka inayoitwa TBS-hawa ni wataalamu wa viwango nchini na TFDA ni wataalamu wa vyakula na madawa. Kinywaji chako hakikisha kimeruhusiwa na kupewa nembo ya TBS kwa usalama wa afya yako Fahamu kiwango chako. Kama wewe ni mnywaji wa Raha kwa mfano, kwanini leo unywe Raha + bia + viroba? Ni hatari kuzidisha kiwango cha kileo. Kwa sababu huwezi kubaini kiasi ulichokunya kwa urahisi. Zingatia unywaji wa maji. Kama ulipata kileo kiwe kingi ama kidogo, shurti unywe maji mengi. Unywaji wa kileo husababisha upotevu wa maji mwilini kwa njia ya mkojo hivyo ukaribishaji wa mning inio hang over na kuumwa sana kichwa. Dawa yake ni maji Mwisho zingatia uchumi wako. Tunajua kuwa unapenda kunywa ila sasa uchumi wako unaruhusu? Kinywaji unachotaka kunywa unamudu kukinunua? Au unataka kunywa kwa mkopo, upigwe, au kupewa ofa daima huku familia yako ikidhalilika? Imeandikwa ma Michael Massawe - Deport Incharge Simu: 0713791119/0788791119/0759980851 Email: michael@banana.co.tz Morogoro 6 HALIUZWI

Bw. Eliabu Joram Machine Operator Bw. Eliabu ana cheti cha Technician in Mechanical Engineering kutoka chuo cha Ufundi Arusha (ATC). Pia amehitimu kidato cha IV katika shule ya Iyunga Technical Secondary School. Ana uzoefu wa miaka 3 katika taasisi mbalimbali Bw. Marko Andongolile Machine Technician Bw. Marko ana Diploma ya Mechanical Engineering katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC). Pia amehitimu kidato cha IV katika shule ya Ifunda Technical iliyopo Iringa. Ana uzoefu katika kazi hii kwa zaidi ya miaka 3 katika taasisi mbalimbali. AJIRA MPYA, NGUVU MPYA KAMPUNI YA BANANA Bw. Tumaini A. Mungete Marketing Development Supervisor (Kilimanjaro Region) Bw. Tumaini ana Stashahada ya Biashara na utawala katika chuo cha Biashara (CBE). Pia amehitimu kidato cha VI Kolila High School Moshi na kidato cha IV Highlands Secondary iliyoko Iringa. Ana uzoefu wa miaka 10 katika taasisi mbalimbali. Bw. Denis F. Kessy Marketing Development Supervisor (Dodoma Region) Bw. Denis ana Shahada ya juu ya biashara na mahesabu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Pia amehitimu kidato cha VI Minaki High School na kidato cha IV Uru Seminary. Bw. Mohamed H. Luhindi Auditing Technician Bw. Mohamed ana cheti cha Accountancy Technician (ATEC II) kutoka National Board of Accountancy and Auditing (NBAA). Pia na Stashahada ya Elimu kutoka chuo cha Ualimu Dar es Salaam. Na amehitimu kidato cha VI katika shule ya Sekondari Union Islamic na kidato cha IV katika shule ya Same Sekondari. Bw. Patrice M. Melley Marketing Development Supervisor (Manyara region) Bw. Patrice ana cheti cha Biashara katika chuo cha Uchira Business College na cheti cha Auto mechanics grade two VETA Dar es Salaam. Pia amehitimu kidato cha IV Sarwatt Secondary School na anao uzoefu wa taasisi mbalimbali. miaka 10 katika Y S MEN ARUSHA WAPATA UGENI KUTOKA GENEVA Klabu ya kimataifa ya Y s Men imeendelea kujipatia umaarufu mjini Arusha kutokana na shuhuli zao ya kijamii wanazofanya kupitia wanachama wake waliopo mkoani hapo. Mnamo tarehe 12/04/2011 Klabu ya Y s Men Arusha walipata ugeni mkubwa kutoka makao makuu ya Taasisi hiyo iliyopo Geneva. Ugeni huo ulikua ni Mr Takao Nishimura ambae ni mtendaji mkuu wa taasisi hiyo. Pamoja na mambo mengine Mr Takao alitembelea kiwanda cha kuzalisha Net aina ya Olyset cha A to Z ambao wanatengeneza net zinazisambazwa na Y s Men hii ni kufanikisha project ya Y s Men ya kuzuia Malaria (Roll Back Malaria). Pia katika kuonyesha utendaji wake Mr Takao alishirikiana na wanachama wa Y s Men wa Arusha kupanda miti katika eneo la Mlima suye. Baadaye wanachama waliandaa chakula cha jioni katika mgahawa wa Albero uliopo barabara ya Haille Sillas na kubadilishana mawazo na mgeni huyo. Vilevile vijana hawakubaki nyuma kwani waliweza kutuma muwakilishi katika Mkutano wa Jimbo la Y s Men la kanda ya Africa, kusini Mashariki. iliyofanyika Kitwe, Zambia na pia walipokea ugeni kutoka Geneva ambae ni mtendaji mkuu Y s Youth Mami Hashikazi raia wa Japan. Katka Mkutano huu Tanzania iliwakilishwa na Willy Kwayu wa Club ya Arusha. Kutokana na changamoto zilizoonekana wakati wa mazungunzo na wakeni hao Club ya Y s Men Arusha pamoja na Y s Youth wamejipanga imara ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa jamii kulingana na mungu alivyowajalia. Mr Takao akipanda mti katika maeneo ya Mlima Suye. Pia wanajipanga kuendesha mafunzo kuhusu TB na vilevile kufungua rasmi club ya Y s Youth ya Moshi. Kwa wale watakaopenda kujiunga wawaliliane na Rais wa Club hiyo ambae ni Miss Lucy Tesha Mob +255716395497 kwa upande wa vijana na Mr Shanell Kavishe Mob +255717157128. Na Beatha Anthon 7 HALIUZWI

Tunawakaribisha wafanyabiashara kujiunga na Kampuni yetu ya Banana Investments Ltd kusambaza kinywaji chetu kwenye mikoa ambayo RAHA haijafika. Hali ya sasa katika usambazaji wa mvinyo wa Raha upo kama unavyoonyesha hapo juu kwenye Ramani Makao Makuu Kiwanja Na. 311, Kitalu jj Oloirien Village, P. O. Box 10123, Arusha TANZANIA S i m u : +255754224440,+255272506475 E-mail: banana@banana.co.tz.banana.co.tz Dar es Salaam Depot Ubungo Kibangu, S. L. P. 79407, Dar es Salaam TANZANIA Simu: +255 222 774 276, +255 756 707 983 Email: darsales@banana.co.tz Morogoro Deport Kihonda Area Simu +255713791119 +255788791119 +255759980851 Email: morosales@banana.co.tz Tanga Depot Barabara ya 4, S. L. P. 5150, Tanga TANZANIA Simu: +255 272 646 134 Email: tangasales@banana.co. tz 8 HALIUZWI