MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Maisha Yaliyojaa Maombi

United Pentecostal Church June 2017

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

Roho Mtakatifu Ni Nini?

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Human Rights Are Universal And Yet...

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

Ndugu na dada zangu wapendwa,

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

Kiu Cha umtafuta Mungu

Sura ya 7 Kielelezo: Tumepatanishwa na Mungu na Wanadamu

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

UNABII WA HABARI ZA BIBLIA

MSAMAHA NA UPATANISHO

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

Oktoba-Desemba

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

PDF created with pdffactory trial version

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Kwa Kongamano Kuu 2016

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

MAFUNDISHO YA UMISHENI

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

KANISA NA UAMSHO Na Mchg. Dkt. Faith Lugazia

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Kiumbe Kipya Katika Kristo

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Patanishwa, Hesabiwa Haki, Takaswa

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Transcription:

6-15 Mei 2005. MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10. Kujenga kifuniko cha maombi juu ya mabara yote ya ulimwengu. Kufurikisha Jamii zetu kwa Maombi. Anzisha vituo vitakavyofukuta moto mkali wa maombi ya siku 10 mchana na usiku vijae ulimwenguni kote ili kuomba kwa ajili ya uponyaji wa mataifa na udhihirisho wa utukufu wa Bwana. Maelekezo kuhusu Siku 10 za Maombi ya Mchana na Usiku. 6 15 Mei 2005. Lengo: Anzisha mpango wa maombi ya masaa 24 kwa siku 7 yafanyike kwa siku 10 mfululizo katika kila taifa ili kuinua kifuniko cha maombi katika ulimwengu wote kupitia Kanisa la Yesu Kristo na kudhihirisha utukufu wa Bwana duniani (Habakuki 2:14) mahali ambapo maombi yamefanyika,- - Kuleta uamsho katika Kanisa. - Kwa ajili ya majirani zetu na watu wa ulimwengu ambao hawajafikiwa na Injili. - Kuleta mabadiliko katika Sharika, Jamii, Miji, Nchi, Bara, Ustawi wa Jamii, Uchumi na Siasa. Mtazamo: Kuendelea kuomba ili Mungu alete mabadiliko ya kiroho na kijamii katika Kanisa, Jamii yote na Mataifa yote. Mkakati: Hamasisha makusanyiko mbalimbali, vikundi vya maombi ambavyo siyo vya kidhehebu, na mashirika ya kikristo katika kila nchi ili yatumie hizo siku 10 kuanzia tarehe 6 15 Mei 2005 kuomba kwa saa 24 kila siku. Siku 10 za Maombi ya Mchana na Usiku: 6-15 Mei 2005. Tarehe 15 Mei 2005 ni siku ya maombi ulimwengu wote. Tunapenda kuwatia moyo makusanyiko na jamii mbalimbali, kutumia siku 10 zitakazofikia kilele Jumapili ya Pentekoste tarehe 15 Mei 2005 kuomba kama lilivyofanya Kanisa la kwanza kama tunavyosoma katika Matendo ya Mitume mlango wa kwanza. Wakristo ulimwenguni kote watahamasishwa kuomba mchana na usiku katika siku hizo 10 wakimwomba Mungu atumiminie Roho Mtakatifu kwa upya, na kuleta wokovu na uponyaji kwa walio na dhambi na ambao hawajafikiwa na injili katika mataifa yote ulimwenguni. 1

Siku ya Maombi Ulimweguni kote. 15 Mei 2005. Siku ya Maombi tuliyokuwa nayo tarehe 2 Mei 2004, Africa, itageuka kuwa siku ya maombi ya kiulimwengu tarehe 15 Mei 2005 siku ya Jumapili ya Pentekoste wakati ambapo mabara yote sita ya ulimwengu yataungana katika maombi ya umoja. Baada ya tarehe 15 Mei 2005, Kuelekea Jumapili ya Pentekoste ya 2006. Hamasisha sharika zilizoko katika eneo lako zitenge siku moja katika kila wiki ziombe kwa masaa 24. Kwa kufanya hivyo, mtandao wa maombi umeanzishwa katika eneo lako. Ukiunganisha maeneo yenu, mtaweza kuhamasisha kanisa lote katika mji, jimbo na hatimaye taifa zima. Kwa mfano, makusanyiko ya madhehebu 7 yanaweza kuomba kwa masaa 24 kwa siku 7 kila wiki kwa mwaka mzima. Ukizidisha idadi ya makanisa yatakayoomba masaa 24 kwa siku moja kwa wiki moja, hii itaongeza eneo lililofunikwa kwa maombi. Kuelezea Mfumo huu wa Siku 10. Katika kipindi hiki cha siku 10 za maombi, tunawaasa wakristo, wamtafute huyu Bwana wa Mabwana na kuongea naye uso kwa uso. Wakristo wawe na uhusiano na ushirikiano mzuri na Mungu, wakiliitia Jina lake ili aingilie mambo yetu hapa duniani, huku tukiomba Neema na Huruma zake. Kwa siku 10 mchana na usiku tutasimama mbele ya kiti cha Mungu, tukimwabudu na kufanya maombezi kwa ajili ya mahitaji na dharura za kanisa na ulimwengu uliotuzunguka. Tutasimama katika andiko la Habakuki 2:14 ili kumwomba Bwana Mungu aujaze ulimwengu kwa Utukufu wake: Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya Utukufu wa Bwana kama maji yaifunikavyo bahari. Tujulishe kushiriki kwako katika mpango huu kwa kujiandikisha kupitia tovuti www.globaldayofprayer.com. Tutafurahi endapo utafanya hivyo ili tuweze kuratibu tukio hili na kuwapa watu wote taarifa sahahi za maombi. Kwa namna hii tutaweza pia kugundua maeneo ambayo hayana waombaji wengi au hakuna maombi kabisa, ili tuweke mipango ya kuhamasisha kanisa katika maeneo hayo. Baada ya Siku 10. Tafadhali tuletee taarifa isiyozidi ukurasa mmoja kupitia barua pepe (info@globaldayofprayer.com), katika taarifa hiyo weka baadhi ya shuhuda. Angalizo: Tunatazamia watu watahamasika kiasi kwamba watapenda kuendelea kuomba mpaka Yesu arudi Hili ni zuri, lakini uwe mwangalifu: chukua muda upumzike, kisha panga tena kwa uangalifu, katika kipindi cha miezi mitatu au sita, ndipo urudie tena mpango huu wa siku 10. Baadae utaweza kupanga mara nyingi zaidi na kuomba sharika nyingine zishirikiane nawe mpaka mmefikia kiwango cha kuomba masaa 24 kwa wiki kwa siku 365. 2

Kwa namna nyingine, inawezekana watu wa mji/mkoa wako wanataka kuanza na mtindo wa kuomba masaa 24 kwa wiki kwa siku 365 ambapo kila kanisa litaomba kwa saa 24 kwa wiki au kwa mwezi mpaka mmeweka kifuniko cha maombi juu ya mji/mkoa wenu. Mtazamo wa Maombi. Katika kuweka mtazamo mzuri wa maombi, (angalia pia chini ya kichwa maelekezo ya maombi baada ya siku 10 yaliyo mwishoni mwa taarifa hii). Uguse moyo wa Mungu kwa kusifu na kuabudu mchana na usiku na kuzidi kumkaribia Yeye ili kuonana Naye uso kwa uso (Ufunuo 4:8-11). Wale viumbe wanne wenye uhai, kila mmoja alikuwa na mabawa sita, na pande zote na ndani wemejaa macho, wala hawapumziki mchana na usiku wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyenzi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja Na hao wenye uhai wanampa Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani Yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kumsujudia Yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, Umestahili, wewe Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu, na heshima na uweza kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa. Tuungame dhambi zetu, tujinyenyekeshe na kuomba kwa ajili ya uponyaji wa nchi yetu: 2Nyakati 7:14: Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina laingu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi, nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Omba kwa ajili ya ahadi za Mungu: Isaya 62:6-7: Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku, ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya mpaka atakapofanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani. Tumwombe Mungu alete matengenezo na marekebisho katika maeneo yote ambayo tumetenda vibaya kama katika uhalifu, ujambazi, uporaji, rushwa, umaskini, madawa ya kulevya, uzinzi na maadili mabaya, uenevu, uharibifu katika ndoa, utoaji mimba na mwenendo mzima wa Ukimwi. Luka 18:7 Na Mungu, je, Hatawapatia haki (lipiza kwa kufanya sawa kilichofanyika vibaya) wateule wake wanaomlilia mchana na usiku naye ni mvumilivu kwao. Tuombee kizazi hiki cha vijana kimrudie Mungu na Mungu ainue wanaume na wanawake watakaoendeleza Amri Kuu na Utume Mkuu. Maombolezo 2:18-19 Mioyo yao ilimlilia Bwana, Ee ukuta wa binti Sayuni. Machozi na yachuruzike kama mto mchana na usiku usijipatie kupumzika. Mboni ya jicho lako isikome. Inuka, ulalamike usiku, mwanzo wa makesha yake. Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana. Umwinulie mikono yako. Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa. Mwanzo wa kila njia kuu. Tumwombe Mungu kwa ajili ya wokovu wa majirani na marafiki zetu, pamoja na mamilioni ya watu ulimwenguni ambao hawajafikiwa na injili. Tuombe kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi pia. Matendo ya Mitume 2:16-21. Lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha Nabii Yoel. Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitamwagia watu wote Roho yangu, na wana 3

wenu na binti zenu watatabiri, na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu nao watatabiri. Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Luka 19:10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Tuombe kwa ajili ya mahitaji yetu binafsi. Mathayo 6:11 Utupe leo riziki yetu Wafilipi 4:6-7: Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane kwa Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Elekeza maombi ya mahitaji yako binafsi katika ngazi tatu ambazo ni: ulimwengu na bara lako, nchi yako, na kisha mji na mkoa wako. Kumbuka kwamba unashiriki mpango wa kuanzisha mfuniko wa maombi juu ya taifa lako, bara lako na ulimwengu kwa ujumla. Kwa hiyo hakikisha unaomba katika ngazi zote hizi katika maombi haya ya siku 10. Hufungwi kuombea mambo haya peke yake. Unaweza kuombea mahitaji mengine kama uamsho, mambo yanayohusu jamii na Kanisa nk. Maelekezo Halisi: Mwongozo wa maombi ya siku 10 umeandaliwa ili kuweka wazi zaidi namna ya kufanya maombi haya. Mwongozo wa kurasa mbili (2) wenye maelekezo ya maombi na jinsi ya kukutana na Mfalme wa Wafalme umetayarishwa kwa lugha mbalimbali ili kuwasaidia watu kuomba kwa saa moja. Unaweza kupatikana katika tovuti: www.globaldayofprayer.com. Unaruhusiwa kutafsiri katika lugha nyingine. Tafuta chumba maalum cha maombi ili watu waje hapo katika hizi siku 10. Uwe shupavu na jasiri katika hili, ndipo watu wataona fotauti. Tayarisha vituo vidogo katika chumba au kituo kikubwa cha maombi, kwa mfano ukuta wa kuabudia, ukuta wa Ahadi (andika vifungu vya biblia vyenye ahadi na kubandika juu ya ukuta huu) ukuta wa Mahitaji ya Maombi (andaa karatasi ili watu waandike mahitaji yao na kubandika ukutani) Ukuta wa Majibu ya maombi (andaa sehemu katika ukuta ili watu wabandike majibu ya maombi). Ukuta wa ubunifu (andaa sehemu ili watu wabandike kazi za ubunifu kama uchoraji, mashairi nk. walivyobuni wakati wa maombi) Ukuta wa Maombolezo (ukuta ambao waombaji wanaweza kubandika majina ya watu wanaowaombea kama wagonjwa, marafiki hawajaokoka, au ndugu nk. Sehemu iliyotengwa (mahali pa kimya penye uhuru na upweke. 4

Maombi Halisi ya Kuzunguka:- Pale inapowezekana waombaji watoke katika kituo cha maombi kuzunguka mji/mkoa wakiombea waalimu na mashule, polisi na vituo vya polisi, maduka na wenye maduka, watu katika vituo vya tax watu na masoko na maombi ya muda (hata siku mbili) katika kituo kikubwa cha maduka. Tafuta watu wachache wanye ujuzi na uzoefu katika mambo ya uongozi na utawala waweze kusaidia katika mambo haya. Hakikisha kuna karatasi na kalamu kwa ajili ya watu kuandika mashairi, mahitaji ya maombi, majibu ya maombi na michoro. Tafuta msaada kutoka kwa watu wenye magari ili wasaidie kuleta watu katika kituo cha maombi hasa usiku. Tayarisha maji moto na ya kunywa, watu wanaweza kunywa kahawa na chai. Hakikisha kituo cha maombi ni kisafi wakati wote na vyumba vya kuogea/vyoo vinabakia wazi masaa 24. Tungependa kuona na kuwatia moyo, vikundi vya vijana, vikundi vikubwa vya maombi, Kanisa wenyeji na makanisa mengi wenyeji, au makanisa ya vitongoji au ya mkoa washirki maombi haya ya siku 10. Ikibidi wekeni usalama wa nje wa masaa 24 kutegemea mahali pa kituo cha maombi. Pawepo muda kwa ajili ya wazee na wamama wanaonyonyesha watoto waweze kuja kuomba wakati wa mchana kwa makundi na vijana wapangiane zamu siku za mwisho wa wiki (mfano wa Ijumaa usiku au Jumamosi usiku: mradi wasaidiwe kupanga hiyo mikesha.) Pawepo maombezi wakati kundi moja linapokea kutoka kwa kundi lingine katika mikesha hii. Linaweza kuwa jambo la kubariki sana endapo watu wanaokuja kwa maombi haya ya siku 10 wataleta nguo, chakula, viti, mablanketi nk. ili baadae wapewe masikini na mwenye shida mbalimbali katika jamii. Mnapowapa zawadi hizi, baadae mnaweza kwenda katika nyumba zao ili kuomba nao na kuwabariki katika Jina la Yesu. Viwepo vikundi vya kuabudu katika maombi haya angalau kwa muda wa saa 2 mara moja au mbili kwa siku wakiabudu tu. Kwa baadhi, mnaweza kuangalia uwezekano wa :- Kuhamasisha shule yenu kuomba kwa siku 10 wazazi waombe muda wa masomo kisha wewe na wanafunzi wenzako mkaombe katika muda uliobaki mchana na usiku. Kama kikundi cha vijana mnaweza kuomba masaa 40 kutoka (Ijumaa saa 12:00 jioni hadi Jumapili saa 6:00 mchana). Kujiunga sharika chache kwa siku 10. 5

Kubuni njia nyingine yo yote yenye mawazo mapana zaidi na ambayo itampendeza Mungu. Usisite kuwa mmbunifu. Roho wa Mungu ni mmbunifu. Usisahau ndiye aliyekuumba. 24 7 Maombi Kupitia Majira ya Kale. Katika Agano la Kale tunafundishwa katika kitabu cha Kutoka na Mambo ya Walawi kwamba makuhani walitakiwa kuweka taa zinazowaka, na kwamba wahakikishe moto uliwaka saa zote katika madhabahu. Kutoka katika hekalu tunajifunza kwamba makuhani waligawanyika katika vituo ili kukidhi masaa 24 ya maombi, kuabudu na kuimba. Wakati wa Yesu Kristo, moja ya matawi makubwa ya dini ya Kiyahudi (Judaism) iliyoitwa Essenes, walitumia mtindo wa masaa 24-7 wa maombi. Usiku sehemu ya tatu ya jumuiya (kwa mzunguko) walibaki macho wakiomba na kuimba. Walitumia mtindo wa 24-7 wa maombi. Kanisa la kwanza lilizaliwa katika mtindo wa 24-7 wa maombi. Kwa ujumla, hata mitume waliendelea kuomba kwa siku 10 kabla a kumwagiwa Roho Mtakatifu siku ile ya Pentekoste. Baba wa Jangwani (Nyikani) walioishi katika karne ya tatu hadi tano walitumia mtindo wa 24-7 kwa maombi. Maelfu kumi ya watawa, walioishi Mashariki mwa Jangwa la Misri waliomba kwa kiwango cha masaa 12-20 kwa siku, zaidi sana wakitumia maandiko katika Zaburi, vitabu vya kinabii, na sehemu kubwa vitabu vya Agano Jipya. Baadhi yao waliishi katika nyumba za watawa, wengine katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya watawa, utumishi wao mkubwa ukiwa ni maombi yaliyogusa jumuia yao yote na ulimwengu kwa ujumla. Baada ya kujitokeza kwa watawa miaka 300 baada ya kuwepo Yesu Kristo, mtindo wa maombi wa 24-7 uliendelea kwa muda mrefu. Hakuna mashaka yo yote kwamba ni maombi haya yaliyofanya Kanisa liwe na nguvu katika majira yote ya mateso. Mwaka 558AD Cumgall, mtawa Mwalrish alianzisha chuo cha utawa katika eneo la Bangore karibu na jiji la Belfast. Alikusanya watawa 3000 na kuwagawa katika makundi matatu ya watawa 1000 kila kundi na akawapangia kuomba kufuatana na kitabu cha Zaburi katika mpangilio wa masaa 8 kila kikundi hivyo kufanya mtindo wa 24-7. Mpango huu uliendelea kwa miaka 300. Mwaka 700AD Mtawa aliyeitwa Columbanus aliondoka Bangore na kwenda Ufaransa. Naye akaanzisha mtindo wa maombi wa 24-7 kama uliokuwa unaendelea kule Bangore. Mwaka 1727, Wamoravian wakaanzisha mtindo huu wa maombi wa 24-7 eneo la Herrnhut, ambao ulidumu kwa miaka 125. Walianza na watu 48 wanaume kwa wanawake wakiomba wawili wawili kwa saa moja kwa wakati mmoja. Katika kipindi cha miaka 25 kanisa dogo la Moravian lililoanza maombi haya likiwa na waumini 600, liliweza kutuma wamisionari wengi ulimwenguni, kuliko ambavyo yalikuwa yamefanya makanisa yote ya Kiprotestanti katika kipindi cha miaka 200. 6

Kabla tu ya kuanza kwa mwaka 1900, mtindo wa 24-7 ulianza tena na unaweza kuunganishwa na uamsho wa Kipentekoste ulioanza 1906. Katika miongo (decades) iliyopita, kutoka mwishoni mwa miaka ya 1980, vikundi vya mtindo wa 24-7 vya maombi vipatavyo 5000 kutoka nchi 150 ulimwenguni vimeanzishwa. Lilifanyika jambo la kiulimwengu lililoleta uamsho mkubwa ulioenea haraka katika nchi mbalimbali. Vikundi hivi vinajiongoza vyenyewe katika mifumo tofauti na malengo mbalimbali. Mifano hii, ni matukio ya haraka kutoka katika historia inayoweza kutusaidia kuelewa kwamba mtindo wa 24-7 wa maombi ni sehemu ya historia ya Kanisa wala siyo jambo jipya la kigeni. Vitabu vya Kusoma: Red Moon Rising - Pete Greig (Kingsway Communications) Fast Forward More practical guidelines on how to practically do a watch. Praying the Bible, the Pathway to Spirituality Wesley and Stacey Campbell (Regal). Praying the Bible; the Book of Prayers Wesley and Stacey Campbell (Regal) The Watchmen Tom Hess (Progressive Vision International). Tovuti Nyingine zenye Taarifa za Maombi: www.24-7prayer.com, www.30-days.net, www.30kd.org, www.bethany.com, www.calebproject.org, www.concertofprayer.org, www.copgny.org, www.ehc.org, www.fotb.com, www.g8prayer.org, www.gfa.org, www.globalharvest.com, www.globalharvest.org, www.gmi.org, www.global-prayer-digest.org, www.gospelcom.net, www.internetprayers.com, www.ipcprayer.org, www.joelnews.org, www.jwipn.com, www.joshuaproject.net, www.missionamerica.org, www.missionmobilisation.com, www.navpress.com/magazines/pray!, www.ndptf.org, www.nppn.org, www.operationworld.org, www.persecutedchurch.com, www.persecution.com, www.prayerweek.com, www.prayforchina.com, www.prayworld.org, www.thecause.org, www.thesecondcall.org, www.transformationafrica.com, www.usprayercenter.org, www.waymakers.org, www.win1040.com, www.worldprayer.org.uk, www.xs4all.nl/~mvdwoude. Mambo ya Kuzingatia katika Maombi ya Siku 10: Baada ya Yesu Kufufuka kutoka kwa wafu, Alikutana na wanafunzi wake mara nyingi katika kipindi cha siku arobaini. Alithibitisha kwamba Alikuwa anaishi. Alizungumza tena na tena kuhusu Ufalme wa Mungu, kukaribia kwa Ufalme wa Mungu hapa duniani. Katika siku ya mwisho aliyokuwa nao, aliwaagiza wabaki Yerusalemu na kusubiri Ahadi ya Baba toka juu. Mara tu Yesu alipopokelewa mbinguni, wanafunzi wake wakakusanyika pamoja Yerusalemu kufanya kile alichowaagiza kwamba wakasubiri ahadi ya Baba. Lakini haikuwa subira ya 7

kustarehe. Walisubiri huku wakiomba kwa uaminifu kwa siku kumi. Walimtafuta Mungu kwa mioyo yao yote wakiwa katika nia moja wakisubiri ahadi ya Mungu kuhusu Roho Mtakatifu. Waliomba bila kukoma kuhusu ahadi nyingine za Ufalme wa Mungu ambao Yesu alikuwa ametumia muda mwingi kufundisha. Tunaposoma maombi yao, na kusikiliza kile kilichotoka katika mioyo yao, wakati ule wa Pentekoste, tunapata picha nzuri inayotuonyesha jinsi walivyoomba. Maombi na maelezo yao yalitokana na Neno la Mungu lililoandikwa. Waliomba kwa bidii katika tumaini lililojaa tegemeo kwa Mungu kutimiza ahadi zake kuhusu ufalme wake hapa duniani. Kristo analiita tena Kanisa lake liunganike katika maombi. Tunalazimika kuomba kwa sababu matatizo yanayoutikisa ulimwengu wetu hayawezi kutatuliwa kibinadamu. Lililo la maana zaidi ni kwamba tumeitwa kuomba kwa sababu ya ahadi za ajabu ambazo Mungu amekusudia kutimiza kupitia Yesu Kristo na Nguvu katika watu wake hapa duniani. Huu ni wakati wa watu wa Mungu kukusanyika tena katika maombi ya pamoja. Kuna njia ipi bora zaidi ya kuunganika katika maombi ya pamoja isipokuwa kujiweka wakfu kwa Mungu wakati huu wa maombi ya siku kumi, kama walivyofanya wanafunzi wa Yesu, wakahitimisha siku ile ya Pentekoste? Kwa kufuata mfano ule wa wanafunzi wa kwanza ambao walikaa pamoja katika maombi (Matendo ya Mitume 1:14) katika zile siku kumi kati ya kupaa kwa Yesu na kushuka kwa Roho Mtakatifu siku ile ya Pentekoste, waamini waandae jinsi watakavyoomba pamoja mchana na usiku kuanzia Ijumaa tarehe 6 Mei mpaka mwisho wa siku ya Pentekoste, Jumapili tarehe 15 Mei 2005. Mwongozo wa maombi unaofuata unaweza kutumika kama njia ya kuwasaidia kuomba pamoja katika tumaini na imani pamoja na wakristo wengine ulimwenguni mwote. Kila moja katika hizo siku kumi ina ujumbe wake ambao unatokana na ujuzi au maandiko ya Kanisa la Kwanza kama tunavyosoma katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Tumia maandiko haya kama mahali pa kuanzia kuandaa maombi na mahitaji katika jumuiya yako. Matazamio ya tumaini yaliyo katika mwongozo huu yatatusaidia kuomba katika njia mbili. Kwanza, kila siku tutaomba Yesu alete kwa wingi zaidi utimilifu wa maisha yake na utukufu kwa Kanisa lake. Pili tutasogeza mbele za Mungu mahitaji makubwa ya miji yetu na mataifa. Ameahidi kulijaza Kanisa lake kwa uzuri na maisha ya Roho wake. Pia ameahidi kuubariki ulimwengu, kila mji, watu na nchi kwa nguvu za utawala wa Kristo. SIKU YA KWANZA. IJUMAA 6 MEI 2005. Kubadilishwa na Kristo: Kwa nguvu ya Kristo inayobadilisha ufalme. Na kuyanena mambo yaliyohusu ufalme wa Mungu. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu. (Matendo ya Mitume 1:3-4). 8

Maombi Kwa Kanisa lake: Mioyo yetu iwake moto wa upendo na utii kwa Yesu kama Mfalme na Bwana wa wote. Sote tusimame katika imani ili tufuatilie kwa nguvu ahadi zote tulizopewa. Watu wa Mungu wakusanywe tena na Yesu ili tuweze kumtii Yeye bila kujali tulikuwa tumegawanyika na kutawanyika kwa kiwango gani. Maombi Kwa Ulimwengu wetu: Yesu awasimamishe waamini katika miji ambayo upenyo wa baraka haujatokea. Tuombe kwamba watu wafuatilie kwa utulivu ahadi za Mungu kuhusu baraka za Ufalme wake katika maeneo magumu kufika. Uzuri na Utukufu wa Yesu hasa katika upendo wake wa Kifalme ujulikane kwa watu wote katika miji huku ukileta mabadiliko katika jamii na jumuiya zote. SIKU YA PILI. JUMAMOSI 7 MEI 2005. Maombi ya Pamoja: Kuomba Yawepo Maombi ya pamoja. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, (Matendo ya Mitume 1:14(a)). Kwa Kanisa lake: Tuombe kwamba Roho wa Mungu atupe roho ya maombezi, huruma, na tumaini ili tuombe bila kukoma kwamba ahadi za Ufalme Wake zitimie. Kwamba Mungu atuunganishe katika maombi katika moyo mmoja akitukirimia nguvu za kuomba pamoja na utukufu wa Kristo na huruma ulimwenguni. Maombi kwa Ulimwengu wetu: Watu katika jumuiya zetu wavutwe kutafuta msaada kutoka kwa Mungu kuliko wakati mwingine wo wote. Viongozi wa jumuiya zetu watafute msaada kutoka kwa Mungu. Mungu atukuzwe kutokana na sifa za walio maskini, vijana, na waliodharauliwa kutokana na majibu ya maombi yao. SIKU YA TATU. JUMAPILI 8 MEI 2005. Roho wa Kristo: Mungu amwage Roho wake kwa wote. Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu (Matendo ya Mitume 2:17.) Kwa Kanisa lake: Tuombe ili Roho wa Mungu awashukie wakristo kwa nguvu ili kuwapa maisha mapya. Roho Mtakatifu alipe Kanisa nguvu ya kumshuhudia Yesu Kristo katika ulimwengu. 9

Maombi kwa Ulimwengu: Tumwombe Roho wa Mungu awaamshe wote katika jumuiya yetu, kwa Roho wake ili waweze kusikia sauti yake na kuona kazi zake. Kwamba, kwa mara nyingine, Mungu amwage kutoka mbinguni kile kinachoonekana na kusikika na watu wote (Matendo ya Mitume 2:33.) SIKU YA NNE. JUMATATU 9 MEI 2005. Amani ya Kristo: Tuombe mahusiano yetu yabadilishwe. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote ushirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha Kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. (Maetendo ya Mitume 2:44-47.) Kwa Kanisa lake: Tuombe Mungu alete uponyaji katika migawanyiko na magomvi yaliyopo katika Kanisa. Watu wa Mungu wageuke na kuacha uchoyo na tamaa za dunia na wawe wakarimu sana kuliko walivyokuwa huko nyuma. Upendo, furaha na uchangamfu ujaze mioyo ya watu wa Mungu. Makanisa yafurahie upendeleo waliopewa katika jumuiya zote. Maombi kwa Ulimwengu: Tumwombe Mungu aponye mahusiano yaliyovunjika katika nyumba zetu na za majirani. Mungu atawanye ugaidi na kuleta ufumbuzi wa vita vilivyopo. Mungu ashughulikie maovu makubwa yanayosababisha wengi kuendelea kuwa maskini ili asiwepo atakayebakia na njaa. Mungu alete mfumko wa amani ya Kristo ulimwenguni kote kupitia maisha ya watu aliowabadilisha. SIKU YA TANO. JUMANNE 10 MEI 2005. Kizazi kinachokuja: Tuombe kwa ajili ya Kusudi la Mungu katika familia na watoto. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu (Matendo ya Mitume 2:39) Kwa Kanisa lake: Tuombe Yesu aimarishe na kutengeneza ndoa na familia za jumuiya yetu. Watoto na vijana waweze kumfuata na kumpenda Yesu wangali wadogo. 10

Maombi kwa Ulimwengu: Tuombee watoto 130 milioni ambao hawana uwezo wa kupata elimu ulimwenguni kote. Watoto wengi ambao ni Yatima au ambao wanateseka kwa sababu ya vita na maambukizo ya Ukimwi. Inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2010 watoto milioni 25 duniani watakuwa wamepoteza mzazi mmoja au wote kutokana na Ukimwi. Mungu ainue kizazi kinachokuja ili kitimize ahadi zake kwa nguvu na Roho wa Mungu. SIKU YA SITA. JUMATANO 11, MEI 2005. Wito wa Mungu: Mataifa yasikie Sauti ya Mungu. Na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wenu wamjie. (Matendo ya Mitume 2:39) Kwa Kanisa lake: Tumwombe Mungu awajaze Wakristo kwa Roho wake ili walihubiri neno lake kwa ujasiri na hekima. Neno la Mungu lihubiriwe kwa watu wa kila lugha, kabila na taifa. Maombi kwa Ulimwengu: Tuombe ili ulimwengu usikie matendo makubwa ya Mungu katika lugha zao na kwa njia za mila zao wenyewe. Biblia itafsiriwe katika lugha 3,000 za makundi ya watu ambao hivi sasa hawana hata kifungu kimoja kwa lugha yao. Kristo awe ndiye Bwana wa watu wengi ambao hawajafikiwa na injili na ambao hawana makanisa yanayokuwa na kuongezeka. Mungu awaite wengi kwake nao waokolewe. SIKU YA SABA. ALHAMISI 12 MEI 2005. Kwa Utukufu wa Yesu: Katika uaminifu wa watu wake. Wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo (Matendo ya Mitume 5:41) Kwa Kanisa lake: Tuombe kwa ajili ya wale wanaolipinga Jina la Yesu, ili waonyeshwe tabia ya ujasiri na uungwana, wa Yesu. (Matendo ya Mitume4:13). Tuombe kwa ajili ya wakristo wanaoteswa kwa ajili ya Yesu Kristo ili watiwe nguvu wawe na furaha na imani. Mungu azidi kutukuzwa kwa matendo yake makuu katika maeneo ambayo amekuwa akipingwa (Matendo ya Mitume 4:21) 11

Kwa Ulimwengu: Kwa ajili ya Viongozi wetu na Serikali zetu Kubarikiwa. Tuombe kwamba wale viongozi wa serikali wanaompinga Kristo (Matendo ya Mitume 4:25) waweze kubarikiwa na kupewa hekima ya kuacha kupingana na Mungu. (Matendo ya Mitume 5:39). SIKU YA NANE. IJUMAA 13 MEI 2005. Uponyaji wa Kristo: Kristo alete uponyaji mkubwa. Ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa Jina la Mtumishi wako Mtakatifu Yesu (Matendo ya Mitume 4:30) Kwa Kanisa lake: Tuombe Mungu awatembelee wagonjwa ili alete uponyaji wa kimiujiza (Matendo 5:14-16). Wakristo waonyeshe huruma (kwa wagonjwa) bila kuchoka na kufanya kazi ya kuondoa magonjwa kwa bidii. Wakristo wajihusishe kwa wingi katika kutoa huduma ya afya kwa walio na mahitaji makubwa. Maombi kwa Ulimwengu: Ugonjwa na madhara ya Ukimwi uishe katika kizazi chetu. Kiwango cha maambukizo ya Ukimwi kwa sasa ni vijana 250,000 kila mwezi. Tuombe kwa ajili ya wale wanaohitaji afya ya msingi waweze kupatiwa. Zaidi ya watoto 30,000 hufa kila siku ulimwenguni kote kutokana na magonjwa ambayo yangeweza kuzuiwa. SIKU YA TISA. JUMAMOSI 14 MEI 2005. Baraka za Kristo: Tuombe Mungu aweze kudhihirisha baraka alizoahidi watu wake. Alimwambia Abrahamu kupitia uzao wake kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa (Matendo ya Mitume 3:25). Kwa Kanisa lake: Tuombe Kristo awabariki watu wake kwa kuwaepusha katika dhambi (Matendo 3:26) Zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana nyakati hizo ziwageuze waamini huku zikiwalazimisha kumtafuta Bwana (Matendo ya Mitume 3:19-20). Maombi kwa Ulimwengu: Tuombe Yesu abariki nchi zetu kwa maendeleo mengi na maisha tele. 12

Uwepo wa Amani ya Mungu iokoayo iwaguse watu wa makabila yote. SIKU YA KUMI. JUMAPILI YA PENTEKOSTE, 15 MEI 2005. Tumaini la Kristo: Utimilifu wa baraka zote za Mungu. Apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokelewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya, vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu (Matendo ya Mitume 3:20-21) Kwa Kanisa lake: Tuombe ili wakristo waendelee kusubiri kwa mategemeo kuwa ahadi zote za mabadiliko zitatimizwa katika muda wa maisha yao. Tuombe makanisa yafanye kazi pamoja katika umoja huku Mungu akiendelea kutimiza ahadi zake za mabadiliko katika maisha, miji na mataifa. Maombi kwa Ulimwengu: Tuombe kwamba Haki ya Mungu ibadilishe njia za uchumi na hali ya siasa. Amani ya Ufalme wa Kristo, ibadilishe jinsi miji na mataifa yanavyotawaliwa. Furaha ya maisha ya Kristo imiliki, na kutawala jumuiya zetu zote. Kukutana na Mfalme. Kutafuta uso wake ili kufunuliwa Utukufu wake. Msifu na Kumwabudu Yeye. Mwalike. Fanya ushirika naye. Simama mbele Yake. Sema naye na umruhusu aseme nawe. Mwulize maswali. Hojiana naye. Mwamini. Omba, Tafuta, Bisha. Mwongozo wa maombi ya saa moja kwa wakristo siku ya maombi ya ulimwengu tarehe 15 Mei 2005 na baadaye. Dakika 0-5. Kutangaza Utukufu wake. Mungu, kiini cha ukamilifu wote na kutiwa moyo, Mungu mwenye Rehema na Huruma, El Shaddai (anayejitosheleza na mtoshelezaji), Yehova Yire (Mungu atatupatia), Yehova Rafa (Mungu akuponyaye), Yehova Shalom (Mungu akupaye kupumzika, Bwana wa Amani), Bwana wa ulimwengu wote, Yesu Kristo ambaye ni Njia, Kweli na Uzima, Kristo ambaye ni Nguvu, na Hekima ya Mungu, Mwana Kondoo aliye katikati ya Kiti cha Enzi, Mwana Kondoo aliyechinjwa, Kristo Tumaini la Utukufu, Roho aletaye Uhuru, Kuona, Mshauri na Nguvu, Mwenye Nguvu, Maarifa na kumwogopa Bwana, Neema na Mwombezi, Utakatifu, Upendo, Ukweli Nguvu Kiasi, Hekima na Ufalme wa Ufahamu wake na Roho wa Utukufu. Dakika 6-10. Kutafuta Utukufu wa Mfalme kwa Utakatifu; (1) Kuna dhambi ninayoijua ambayo sijaitubu? (2) Nina hali ya kutosamehe na uchungu katika maisha yangu? 13

(3) Kuna mambo yo yote yenye mashaka ndani yangu? (4) Huwa ninamtii Roho Mtakatifu mara moja katika mambo yote? (5) Huwa ninamkiri Yesu Kristo bila aibu? Dakika 11-15. - Kutafuta Utukufu wa Mfalme kwa kuwapatia wakovu walio katika dhambi. - Ombea familia tano za watu ambao ni marafiki au ndugu zako ambao hawajaokoka. Andika majina yao; 1. 2. 3. 4. 5. Omba kwa ajili ya wokovu wao. Kisha Mungu awabariki (kiroho, kijamii na kihisia). Omba kwa ajili ya mahitaji yao. Dakika 16-20. Kuleta Utukufu wa Bwana katika Kanisa. 1. Majengo yote ya makanisa yarejeshwe kuwa nyumba ya sala kwa mataifa yote (Isaya 56:7, Mathayo 21:13) 2. Makanisa yatimize Utume Mkuu (Mathayo 28:18-20). 3. Makanisa yatimize Amri Kuu (Mathayo 22:37-40) 4. Patokee uamsho mkubwa wa kiroho. 5. Kanisa litende kwa uaminifu utumishi wake katika neno la Mungu, na kushughulikia mahitaji ya watu. Dakika 21-25. Kutafuta utukufu wa Bwana kwa kuomba mkate wako wa kila siku na kujiombea mahitaji binafsi matano;- 1. 2. 3. 4. 5. Dakika 26-30. Kutafuta Utukufu wa Bwana kwa Kumwangalia na Kumsikiliza Yeye. Mwombe Bwana akufunulie mambo mapya. Mambo ambayo anataka uyaone na kuyafanyia kazi. Mwombe akufunulie mapenzi na mikakati/mipango yako. Mwombe akuonyeshe mambo yaliyo ndani ya moyo wake uyaombee. Andika yale unayohisi anakuambia. 14

Dakika 31-35. Kutafuta Utukufu wa Bwana katika Mataifa. 1. Omba kwamba Mataifa yaone kuwa Kristo ndiye njia, kweli na uzima. (Yohana 14:6). 2. Omba kwamba watu ambao hawajafikiwa waweze kufikiwa na injili. 3. Omba amani ya Mungu ije, na utukufu wake ufike katika nchi na serikali na kwamba watanyenyekea na kukubali kwamba Yesu ni Bwana na Mfalme wa Wafalme. 4. Mwombe Mungu abariki mataifa. Dakika 41-45. Kutafuta Utukufu wa Bwana ili kupitia kwake upatikane upenyo katika mambo yafuatayo ya Kiulimwengu. 1. Kupungua maambukizi ya Ukimwi. 2. Kupungua kwa watu maskini na walio na mahitaji makubwa. 3. Rushwa katika ngazi zote. 4. Mateso yaliyo katika makanisa katika nchi nyingi. 5. Vita, umwagaji damu, na vurugu za kikabila. Ombea pia mamilioni ya wakimbizi. Dakika 46-50. Kutafuta Utukufu wa Bwana ili awaguse vijana. 1. Ombea vijana wa kizazi hiki waweze kufikisha injili mwisho wa kizazi chao. 2. Omba vijana waweze kuwa na uhusiano wa karibu sana na Mungu kisha wamtii. 3. Omba Mungu ainue wanafunzi/ wafuasi wenye mzigo katika utumishi na wanaishi maisha ya utakatifu. 4. Wamtumikie Mungu na kumfuata po pote atakapowaelekeza. 5. Mungu ainue watu wenye Huruma, watakaokuwa tayari kwenda hata kwenye maeneo machafu wanamoishi maskini. Dakika 51-55. Kutafuta Utukufu wa Bwana kupitia msamaha na upatanisho. 1. Tuombe kwamba nchi mbalimbali zitatubu dhambi za kuwaumiza, kuwaonea na kuwanyanyasa wananchi wao na wa nchi nyingine. 2. Pawepo upatanisho katika ngazi zote (familia, kuwakandamiza wanawake na watoto, kati ya madhehebu, makabila au watu wa mataifa mbalimballi, nchi kwa nchi.) 3. Tuombe na kuvunja ngome zote, misimamo ya kisiasa na maagizo yenye nia ya kuharibu maisha ya watu. 4. Tuombee watu kibinafsi, familia, ukoo na makabila waweze kuwasamehe wale walio wakosea kwa njia yo yote. 5. Turudiane na kutengeneza sisi kwa sisi. Dakika 56-60. Kutafuta Utukufu wa Bwana kwa Kumsifu na Kumwabudu. 15

Malizeni maombi haya kwa kumsifu Mungu na kumwabudu Mungu. Mshukuru Mungu kwa wema wake na chukua muda kidogo kuwabariki watu watakaokuja katika moyo wako kwa Jina la Yesu Kristo. MWONGOZO HALISI: 1. Mwombe Bwana akupe majina mengine 5 ya wakristo ambao watajiunga nawe katika maombi angalau kwa muda wa saa moja kwa siku. 2. Toa nakala za mwongozo huu na uwape wakristo wengine bure. 3. Kwa ajili ya tafsiri zaidi za mwongozo huu angalia tovuti www.jwipn.com,www.globaldayofprayer.com. TAARIFA ZA MAWASILIANO: Siku za Maombi Ulimwenguni, 15 Mei na Siku 10 za Maombi 6-15 Mei 2005. info@globaldayofprayer.com, www.globaldayofprayer.com. Jericho Walls International: info@jwipn.com, www.jwipn.com. Transformation Africa: info@transformationafrica.com, www.transformationafrica.com. Kuwakusanya vijana kuomba: www.24-7prayer.com. MAOMBI KWA AJILI YA ULIMWENGU 15 MEI 2005: Mungu Mwenyenzi Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tumekusanyika kama mwili mmoja wa waamini ulimwenguni ili kulienzi na kulitukuza Jina lako. Tunasujudu mbele ya kiti chako cha Rehema na kukubali kwamba wewe ndiwe uliyeumba mbingu na nchi. Umekuwepo tangu milele na milele na kwa wewe vitu vyote vimeshikamanishwa pamoja. Hakuna aliye kama wewe Mtakatifu na Mwenye Haki katika njia zako zote, Mwenye Huruma na Rehema, uliyeumia lakini uliyejaa Wema na Ukweli. Tunajinyenyekesha katika mamlaka na ukuu wako kama Mfalme wa Ulimwengu, na kuomba kwa sauti moja umiliki mioyo yetu. Hivyo tunakuheshimu na kukuenzi mbele ya ulimwengu wote. Kusanyiko: Bwana Mungu, Wewe peke yako umestahili sifa zetu. Tunakuabudu Bwana. Baba yetu wa Mbinguni. Asante kwa kuupenda ulimwengu kiasi hicho, hata ukamtoa Mwanao pekee Yesu Kristo afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu ili tupatanishwe na nafsi yako. Asante kwa kutupa haki ya kukuita Baba kwa kuwa tumemwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wetu. Hakuna kitu, wala falme, mamlaka au nguvu yo yote inayoweza kututenga na upendo wako, ambao uliudhihirisha kupitia Mwanao Yesu Kristo. Kusanyiko: Asante Baba, kwa kutukubali katika familia yako. Sasa tunalia Abba Baba. Bwana Yesu Kristo. 16

Wewe pekee umestahili kufungua hicho kitabu kwa kuwa ulichinjwa na kwa damu yako ukatukomboa na kutuleta kwa Baba. Asante kwa kutuombea kama Kuhani wetu Mkuu. Tunasimama mbele yako sisi tuliotoka katika makabila na mataifa mbalimbali tukikiri kwamba Wewe Ndiwe Kichwa cha Kanisa na Bwana wa kila kilichoumbwa mbinguni na duniani. Njoo Bwana uchukue wafuasi kutoka kila lugha na kabila wakutumikie. Tunaomba hawa wawe ndio urithi wako katika kila taifa ulimwenguni. Ufalme wako uimarishwe na kustawi katika kila taifa ulimwenguni ili serikali zote zitawale kwa haki na kutoa hukumu za haki. Tunaomba injili yako ijulikane kwa kila mtu duniani. Baraka zako zilete mabadiliko kwa kila mtu duniani. Na utukufu wako ufunike dunia yote kama maji yafunikavyo bahari. Kusanyiko: Bwana Yesu Kristo, tunakiri kwamba Wewe ndiwe Mwokozi wetu. Baba wa Huruma na Neema. Tunakubali kwamba tumetenda dhambi na kwamba ulimwengu wetu umekamatwa na nguvu ya dhambi. Mioyo yetu inahuzunishwa na hali za kutotendewa haki, na chuki, umwagaji damu, vurugu, hasira, kukataliwa, ubaguzi, uonevu, choyo na ubinafsi. Tunalia kwa sababu ya mauaji ya watu wasio na hatia kupitia vita, ugaidi, utoaji mimba, mateso na mauaji ya kikatili. Mioyo yetu inaumizwa na kila tukio la kumkataa Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Tunakuja mbele ya Kiti chako cha Rehema kuomba Huruma zako na msaada. Kusanyiko: Mungu wa Huruma, tafadhali tumwagie Neema yako utusamehe dhambi hizi. Bwana wa wote. Tunakiri kwamba hatuwezi kufanya neno lo lote bila Wewe. Tunaomba utumwagie Roho Mtakatifu juu ya wote wenye mwili siku hii ya Pentekoste. Lisaidie Kanisa litiwe nguvu na kubadilishwa lifanane na Yesu Kristo. Achia nguvu zako zilete uponyaji kwa wagonjwa, na kuleta mwisho katika maambukizi ya ukimwi, kuwafungua walioteswa na mapepo, kuwafariji wanaoomboleza, na kuwafungua wanaoonewa. Njoo Bwana uyeyushe mioyo wa watu wako waweze kuwa na upendo tena. Amsha Kanisa liweze kuwakumbatia wanyonge, yatima, wajane, wazee na kuwafariji. Amsha Kanisa liweze kusikia kilio cha wasio na makazi, wenye njaa, wasiojiweza na walio katika hatua za kufa. Dhihirisha huruma zako na utupatie mahitaji yetu. 17

Tupe hekima na uwezo wa kuona kila jambo katika maisha yatu ili tuweze kupata majibu ya mahitaji ya ulimwengu. Tusaidie tuweze kutumia mali za dunia hii kuwasaidia watu wote. Mwanga wa upendo wako ndani ya mioyo yetu na utujaze kwa huruma zako na Roho Mtakatifu atusaidie katika maisha yetu. Kusanyiko: Roho Mtakatifu, tunaomba faraja yako na utuongoze. Njoo ubadilishe mioyo yetu. Bwana Yesu Kristo. Kwa sababu ulikuwa umekufa na sasa umefufuka, kwa sababu Baba amekukirimia Jina Kuu kuliko majina yote, Utazishinda nguvu zote za yule mwovu. Umetangaza kwamba milango ya kuzimau haitalishinda Kanisa lako. Tunaomba utukomboe kutoka katika vifungo vya shetani. Tunaomba uvunje vipande vipande, ngome zote, mapokeo yote, uharibu mipango yote ya ugaidi na mateso kwa Kanisa. Tunapinga mipango yote ya shetani ya kuyafanya mataifa yabaki katika giza la kutomjua Yesu Kristo na kuomba kwamba utaondoa ule utando unaozuia watu wasimwone Yesu. Tunaomba ufungue milango ya injili kwa mataifa yote. Mzuie shetani anayeleta vurugu na mauaji. Vunja hali ya utumwa na vitisho. Tupe ujasiri wa kulihubiri neno lako bila hofu na kwa uaminifu. Tujaze Roho wa maombi na maombezi ili kulia kwa niaba ya waliopotea. Kusanyiko: Mungu Mwenyenzi, tuokoe na yule mwovu. Mfalme wa Utukufu. Tunakualika Bwana, njoo katika mataifa ya ulimwengu. Mungu alituahidi zamani kuwa Wewe utakuja kuturejeshea vitu vyote. Tunakukaribisha umalize kazi yako katika miji, kwa watu wako, na mataifa yako. Kwa pamoja tunalia: Inueni vichwa vyenu enyi malango! Inukeni,, enyi malango ya milele, Mfalme wa Utukufu apate kuingia. Mfalme wa Wafalme, utainuliwa katika mataifa ya dunia. Sasa tunaungana katika mioyo yetu na waamini wote duniani. Kutoka Afrika, Mashariki ya Kati, Amerika ya Kaskazini na Kusini, Asia, Ulaya, Australia na Visiwa vya Pasifiki: Tunainua sauti zetu kwa Pamoja Tukisema: Roho na Bwana Harusi NJOO BWANA YESU. A M E N. 18