YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

Similar documents
HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

ARCHDIOCESE OF MWANZA

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Human Rights Are Universal And Yet...

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Upande 1.0 Bajeti yako

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Ufundishaji wa lugha nyingine

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

ORDER NO BACKGROUND

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

TIST HABARI MOTO MOTO

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MUONGOZO WA UTUNZAJI WA URITHI WA UTAMADUNI 1 SECURITY AT MUSEUMS

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Banana Investments Ltd

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Deputy Minister for Finance

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Transcription:

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI SHULE YA SEKONDARI WERUWERU Nambari ya simu 073-2744003/0759 659681 Email:weruweru23@gmail.com S.L.P 575, MOSHI, Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi... S.L.P. YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018 1. Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule hii mwaka 2018 tahasusi ya.shule ya Sekondari weruweru ipo umbali wa kilometa kumi (10) kutoka mji wa Moshi.Usafiri wa basi kutoka mjini unapatikana katika kituo cha mabasi maili sita nauli ni shillingi 400. Mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni tarehe. mwisho wa kuripoti ni tarehe. Mwanafunzi akichelewa kuripoti ndani ya kipindi hicho nafasi yake itajazwa na mwanafunzi mwingine A. MAAGIZO YA FEDHA Kwa kuwa binti yako anahitaji vitu kadhaa akiwa hapa shuleni tuma fedha kwa njia ya benki jumla ya shilingi 170,000/-(laki moja na elfu sabini tuu),kwa jina la Mkuu wa shule kupitia akaunti namba 40301100091 Weruweru sekondari iliyopo Benki ya NMB tawi lolote, kumbuka kuandika jina la mwanafunzi, kidato chake na tahsusi(combination) sehemu ya ujumbe.fedha TASLIMU HAZIPOKELEWI SHULENI. Mwanafunzi aje na Nakala ya hati ya malipo. NAKALA HALISI (original Bank pay in slip) 1

Fedha hizo zitatumika kukidhi mahitaji yafuatayo:- (a). Ada ya shule kwa mwaka.70,000/- (b) Fedha ya kuweka kwa ajili ya tahadhari 5000/- (c) Matibabu ya dharura 12,000/- (d) Kitambulisho,nembo ya shati na picha.8000/- (e) Mfuko wa kuboresha elimu..20,000/- (f) Mchango kwa ajili ya walinzi,wapishi na wauguzi kwa mwaka...30,000/- (g) Kukodisha godoro kwa mwaka.10,000/- (h) Ukarabati wa samani...15,000/- JUMLA YA FEDHA ZOTE NI 170,000/- B. MAAGIZO NA MAHITAJI MENGINE Binti yako aje shuleni na mahitaji yafuatayo:- B.1 SARE ZA SHULE (a) Sketi zinazotakiwa ni mbili(02)zenye rangi ya light blue (SUIT MATERIAL)yenye v shape mbele isiyo ya kubana ndefu yenye kuvuka magoti muundo wa solo. Ili kurahisisha mfanano katika rangi,mshono na ubora wa kitambaa bodi ya shule imeona ni vyema sare hii ishonewe shuleni kwa usimamizi makini kwa gharama ya shilingi Tsh 32000/-(elfu thelathini na mbili)pesa hii itumwe kwenye A/C No 40301100091 NMB. (b)aje na mashati mawili (02) meupe yenye mikono mifupi aina ya TOMATO (c) Aje na sweta v -shape shingoni ya rangi ya dark blue(navy) (d) Aje na sketi yake ya shule aliyokuwa anaitumia akiwa kidato cha nne wakati akisubiria sare ya shule. (e) Aje na soksi nyeupe(white stockings)jozi mbili (02),kandambili jozi moja,khanga,gauni la kulala,taulo na Viatu vyeusi jozi mbili visivyo na kisingino(flat shoes vya kufunga kwa kamba). Ni muhimu kuzingatia hili kinyume na hapo mwanafunzi atarudishwa. (f) Aje na magauni mawili marefu yanayovuka magoti ya rangi ya light blue( mshono wa solo pamoja na suruali yake)yenye mikono mifupi na kola (baby colar) kama nguo za kushindia. Nguo zingine haziruhusiwi. (g) Aje na truck suit nyeusi yenye mistari mieupe na raba nyeusi kwa ajili ya michezo. 2

(h) T shirt ya rangi ya kijivu(180 type ashgrey) kwa ajili ya michezo, alipie Tsh elf kumi(10,000)kwenye A/C tajwa hapo juu atapata t shirt yenye nembo ya shule hapa shuleni. (i) Aje na hijabu ya rangi nyeupe kwa ajili ya darasani na rangi ya light blue kwa ajili ya kuvalia nguo za kushindia. Hii ni kwa waislamu tu N.B: MWANAFUNZI HARUHUSIWI KUJA NA NGUO ZA NYUMBANI ISIPOKUWA SARE ZILIZO ELEKEZWA. B.2 Mahitaji mengine (a). Madaftari makubwa (counter books yasiopungua kumi) (b). Nakala ya cheti cha kuzaliwa na Result slip ya kidato cha nne. (c) Shuka za kulalia (02), Blanket la kawaida (student size), mto na foronya mbili,chandarua nyeupe ya duara na shuka la kutandika juu ya kitanda Bed cover (01) ya rangi ya light blue (plain) (d) Mathematical set, rula ndefu,kalamu za wino za kuandikia,penseli,kifutio,stepler mashine na graph pad na scientific calculator kwa wanao chukua masomo ya jiografia na hisabati. (e) Taulo spesheli (pedi) paketi tano. (f) Sanduku dogo (size ya kati )la bati la kuwekea nguo zake na kufuli lake imara. Asije na suit case hatutalipokea. (g) Alete Rim moja ya karatasi aina ya Rotatrim (h)fyekeo lililonolewa/reki ya mpini wa chuma/panga lililonolewa/jembe lililonolewa na mpini wake(hge-fagio LA BUIBUI,HKL-REKI,HGK-BRUSH LA CHOONI,EGM-FLOOR SQUIZER,PCB-JEMBE,ECA-FYEKEO) (I) Ndoo moja(01) ya kuchotea maji yenye ujazo wa lita 10 kwa matumizi yake binafsi. (j)kila mwanafunzi aje na fagio mbili(02) fupi za chelewa na brush ngumu(scrubing brush 02) zisizo na mpini.(tafadhali zingatia ubora). (k) Kuna mahitaji mengine madogo kama vile mafuta ya kujipaka sabuni n.k ambavyo binti yako atahitaji. Tafadhali usikose kumpa fedha kidogo za matumizi (pocket money). TANGAZO KWA WAZAZI i. Hakikisha binti yako amepimwa na daktari na kujaziwa ripoti kwenye FORM FOR MEDICAL EXAMINATION Iliyoambatanishwa. Ijazwe na mganga mkuu wa hospitali ya serikali. 3

ii. iii. Soma kwa makini na binti yako sheria za shule kisha weka saini HATI YA UTII WA SHERIA ambayo imeambatanishwa. Binti yako aje nazo shule itakapofunguliwa. Aje na kijiko cha kulia chakula, sahani na kikombe atapata shuleni. SHERIA ZA SHULE A. MAKOSA YATAKAYOSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE i. Wizi ii. Kutohudhuria masomo kwa zaidi ya siku 90 bila taarifa/utoro iii. Kugoma na kuhamasisha mgomo iv. Kutoa lugha chafu kwa wanafunzi wenzake,walimu/walezi na jamii kwa ujumla. v. Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi, kumpiga mwalimu au mtu yeyote Yule. vi. Kusuka nywele kwa mtindo usiokubalika. Wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi wakati wote wawapo shuleni vii. Kutinda nyusi viii. Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya ix. Uvutaji sigara x. Uasherati,uhusiano wa jinsia moja,kuoa au kuolewa. xi. Kupata ujauzito au kutoa mimba xii. Kushiriki matendo ya uhalifu,siasa na matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi. xiii. Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni. xiv. Kuondoka katika eneo la shule bila kibali cha mkuu wa shule/utoro. xv. Kumiliki,kukutwa au kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya shule. xvi. Kudharau bendera ya Taifa xvii. Kufanya jaribio lolote la kujiua, au kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k. xviii. Uharibifu wa mali ya Umma kwa makusudi. B. MAKOSA YAFUATAYO YATASABABISHA MWANAFUNZI KUPEWA ADHABU KALI NA MARUDIO YA MAKOSA HAYA YANAWEZA KUSABABISHA KUACHISHWA MASOMO 1. Ni marufuku kukanyaga majani katika eneo la madarasa,nyumba za kulala na bwalo la chakula. Nilazima kutumia njia zilizoezekwa tu.(covered ways) Kosa lakukanyaga majani adhabu itatolewa na viongozi wa wanafunzi. 2. Mwanafunzi lazima awe katika mavazi rasmi ya shule 4

(a) Siku za masomo tangu asubuhi hadi saa ya kulala (b) Jumapili saa za sala.baada ya sala ataruhusiwa kuvaa nguo za shule za kushindia. (c) Wakati wowote wa kutoka kwa shughuli mballimbali kama mkutano,matibabu na safarini, sare ya shule lazima ivaliwe (d) Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa nguo ya mwanafunzi mwingine. 3. Ni marufuku mwanafunzi kujipamba mfano:kutinda nyusi,kupaka rangi kucha,manukato(perfumes,spray,deodorant),kuvaa hereni na kupaka rangi za midomo. 4. Mwanafunzi haruhusiwi kufuga nywele ndefu wala kusuka. Nywele ziwe fupi urefu wa sentimita moja zilizokatwa kwa kulingana ndizo zinazoruhusiwa. 5. Mwanaunzi haruhusiwi kuja shuleni na vyombo vifuatavyo:redio,pasi, heater,thermos,kamera,simu YA MKONONI,LINE YA SIMU. Hot pot,walk man au kifaa chochote cha muziki,sufuria, kilevi cha aina yoyote,madawa ya kulevya,sukari,majani ya chai au chakula cha aina yoyote na albamu za picha(photo-album) 6. Nimarufuku kwa mwanafunzi kuingia jikoni bila ruhusa ya Makamu Mkuu wa shule. 7. Ni marufuku kwa mwanafunzi kuweka chakula cha aina yoyote katika nyumba ya kulala au katika kabati la vitabu (locker). Kwa hiyo mwanafunzi asije na chakula cha aina yoyote wakati wa kufungua shule. 8. Wanafunzi wote wanatakiwa waishi na kushirikiana kindugu. Ni marufuku kutumia lugha ya matusi 9. Ni marufuku kuandika katika vitabu(text books) kuta,milango, viti,madawati,au mbao za matangazo. Adhabu kali itatolewa kwa atakaekiuka sheria hii. 10. Mwanafunzi anatazamiwa kufanya kila kazi,iwapo ana matatizo ya kiafya mzazi/mlezi atume taarifa ya Daktari kwa mkuu wa shule. 11. Kila mwanafunzi lazima ahudhurie masomo ya Dini yake bila kukosa kama anavyohudhuria masomo mengine. Mwanafunzi haruhusiwi kubadili dini akiwa hapa shuleni. 12. Mwanafunzi haruhusiwi kulala bwenini wakati wa vipindi(1:30 asubuhi hadi 9:30mchana) wala wakati wa kujifunza (preparation)jioni kuanzia saa 1:30usiku hadi saa5:00 usiku. 13. Mwanafunzi haruhusiwi kuwa darasani saa 5:00 usiku hadi saa12:00 asubuhi C. MAAGIZO KWA WAZAZI: Sheria za shule zimeorodheshwa hapo juu. Wazazi na wanafunzi ni muhimu kusoma kwa uangalifu na kutia saini zenu za makubaliano katika FOMU YA UTII WA SHERIA 5

ambayo imeambatanishwa halafu mzirudishe fomu hizo kwa mkuu wa shule. Ni dhahiri kuwa wanafunzi watakuwa wanapoteza wakati wao bure kama wasipotaka kufanya kazi zote kwa bidii na kutii sheria za shule. i. WAZAZI WAGENI KUTEMBELEA SHULE: Wazazi hawaruhusiwi kuonana na watoto wao wawapo shuleni. Hii itawasaidia kutumia muda wao vizuri zaidi katika kujisomea. Baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kufika shuleni na kutaka kuwaona wanafunzi na hii huwasumbua na kuathiri utendaji wao kimasomo. Iwapo kuna umuhimu wa mzazi kufika shuleni ataonana na uongozi wa shule. Mwanafunzi asifike shuleni siku za week-end wakati wa kuripoti kwani hatapokelewa. NB: Shule ina utaratibu wa kuwa na vikao vya wazazi hivyo unapaswa kuja kwenye kikao cha wazazi tarehe 25/8/2018. ii. iii. iv. WANAFUNZI KUTEMBELEA NYUMBANI Mwanafunzi haruhusiwi kwenda nyumbani isipokuwa:- a. Ametumwa/amepelekwa na shule b. Wazazi wake waje kumchukua kukitokea shida kubwa nyumbani mfano kifo cha baba mzazi,mama mzazi au mlezi wake anayetambulika kisheria. Ni lazima waje na barua yenye saini na muhuri wa mtendaji wa kijiji/mtaa kudhibitisha tukio hilo. c. Mapumziko mafupi ya katikati ya muhula (mid-term break)wanafunzi wanaruhusiwa kwenda nyumbani kwa wazazi au walezi wao wanaotambulika kisheria tu. BARUA A. Barua zenye habari ya msiba zitumwe moja kwa moja kwa mkuu wa shule. Barua hizo ni lazima ziwe na saini na muhuri wa serikali ya kijiji/mtaa. B. Wanafunzi wanaruhusiwa kuandika barua wakati wa saa za mapumziko. C. Iwapo mzazi hataki binti yake apate barua toka kwa watu ulani,ni vema amwarifu Mkuu wa Shule. TIBA (MEDICAL ATTENTION): a. Meno,macho,masikio na kadhalika vikaguliwe wakati mwanafunzi akiwepo nyumbani. Mwanafunzi auguapo akiwa shuleni atapewa matibabu katika zahanati ya shule na kama ni lazima atapelekwa Hospitali ya Mawenzi au KCMC. Akilazwa mzazi atajulishwa mara moja na 6

mkuu wa shule kwa njia ya simu au barua. Zingatia taarifa za ugonjwa/kuugua mtoto wako unazoletewa na uongozi wa shule tu. b. Mwanafunzi haruhusiwi kuja na dawa zake binafsi kwani atahudumiwa katika zahanati ya shule lakini ikiwa amepewa dawa na daktari atatakiwa kumkabithi muuguzi wa shule ambaye atafuatalia matumizi yake. c. Wagonjwa wote ni lazima walale katika zahanati ya shule na siyo bwenini tena kwa kibali cha muuguzi wa shule. v. MATUMIZI YA SIMU (TELEPHONE) a. Mwanafunzi haruhusiwi kupiga simu,kupigiwa simu na kupokea simu. Iwapo kuna jambo muhimu ambalo mzazi /mlezi anataka kumjulisha ataacha ujumbe kwa karani/uongozi wa shule kwa simu Na 073-2744003 b. NI MARUFUKU MWANAFUNZI KUJA NA SIMU YA MKONONI AU (LINE) (TELEPHONE) SHULENI:-Mwanafunzi akikutwa na simu ya mkononi au line atafukuzwa shule. vi. USAFIRI: Mzazi anatakiwa kumsafirisha binti yake wakati wa kuja shuleni na anaporudi nyumbani wakati wa likizo. Ni muhimu fedha za usafiri zitumwe mapema ili usafiri wa pamoja upagwe na shule. vii. MAHITAJI:- Shule inajitahidi kuwapa wanafunzi chakula bora na cha kutosha. Mwanafunzi haruhusiwi kuja shuleni na chakula cha aina yoyote. Wanafunzi wanaruhusiwa kujinunulia vitu muhimu katika duka la shule,lakini binti asipewe fedha nyingi mno kwa ajili ya vitu hivi vya ziada. Siku za mahafali shule inatengeneza chakula (special) kwa ajili ya wahusika wote. Wazazi hawataruhusiwa kuingiza chakula wala kinywaji chochote shuleni. Mzazi haruhusiwi kuingiza zawadi yoyote shuleni. Zawadi zozote hazitapokelewa. Wawekeeni watoto wenu zawadi hizo muwakabidhi warudipo nyumbani. viii. PESA ZA MATUMIZI:- Ni wazi kuwa mwanafunzi lazima apewe pesa za matumizi. Ni wajibu wa mzazi/mlezi kumpa binti yake kiasi cha pesa anunue sabuni,stampu.bahasha na vitu vingine vidogo. Kuna wazazi wengine wanawaletea binti zao pesa nyingi mno mpaka inashangaza. Hivi ni kumzoesha mtoto vibaya, husababisha wizi, mashindano,ubaguzi,tabaka, ugomvi na urafiki usio na msingi. Siyo busara kumpa mtoto fedha nyingi mno. 7

ix. TAARIFA ZA MAENDELEO YA MWANAFUNZI:- Kila mwisho wa muhula kila mzazi atapelekewa kimaandishi taarifa ya maendeleo ya binti yake katika masomo,shughuli za kazi na tabia. Ni muhimu mzazi /mlezi usome taarifa hiyo na kuwasiliana na shule kama kuna agizo lolote. Tafadhali wazazi someni taarifa hizo na KUZINGATIA YALIYOANDIKWA KISHA UWEKE SAINI KATIKA HATI YA UTHIBITISHO na rudisha kwa mkuu wa shule kwa njia ya posta. Chunguza taarifa anazokuletea binti yako ambazo hazikutumwa ma mkuu wa shule kwa makini,nyingine hazina ukweli. Kama kuna taarifa ya ugonjwa au safari ya kishule Uongozi wa shule utawasiliana nawe. Mara nyingi wanafunzi wanatoa visingizio vya ugonjwa, safari au Tuition ili wapate fedha za ziada kutoka kwa wazazi wao. x. MAHAFALI: Siku ya mahafali ya kidato cha sita ni wazazi/walezi wawili tu wanaotambulika kisheria wa wahitimu watahudhuria. Wazazi/walezi hao ni lazima waje na kadi zao za mwaliko. Kuhusu chakula na zawadi rejea kipengele(vii) hapo juu na kukizingati. Upigaji picha siku ya mahafali utafanywa na mpiga picha wa shule peke yake. xi. WAJIBU WA MWANAFUNZI AWAPO SHULENI:- a. Kutii sharia zote za shule b. Kuhudhuria vipindi vyote vilivyopagwa kwenye ratiba,kufanya mazoezi yote atakayopewa na walimu na kujisomea kwa bidii. c. Kushiriki shughuli zote za usafi,utunzaji wa mazingira ya shule,bustani,shamba na mirandi mingine ya shule. HITIMISHO: Wazazi tunaomba sana tuwe na malezi ya pamoja ili watoto waendelee na wapate kile walichokifuata hapa shuleni Weruweru,yaani ELIMU. Msisitizo wa bodi ya shule ni kwamba kila mwanafunzi anatakiwa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kiwango cha alama 60% au zaidi katika kila somo. Sheria zote hizo zitalenga kumfanya mtoto apate mazingira bora ya kujisomea na hatimaye aweze kufaulu vizuri masomo yake. TUNATEGEMEA USHIRIKIANO WENU. MKUU WA SHULE 8

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRESIDENT S OFFICE MINISTRY OF REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT MOSHI DISTRICT COUNCIL WERUWERU SECONDARY SCHOOL-P.O.BOX 575, MOSHI STUDENT INFORMATION SHEET:- (This form is to be completed by from five and student transferred to the school. Parts A, B and C to be completed by the student) A: PERSONAL PARTICULARS: NAME. DATE OF BIRTH TRIBE:.. RELIGION..DENOMINATION FATHER S NAME..OCCUPATION.. MOTHER S NAME.OCCUPATION. GURDIAN S NAME OCCUPATION. NUMBER OF SISTERS NUMBER OF BROTHERS.. FARTHER S TELEPHONE NUMBER....MOTHER S TELEPHONE NO. HOME ADDRESS.. ANY PHYSICAL/ MEDICAL DISABILITY. B: SECONDARY EDUCATION:-..SECONDARY SCHOOL: FROM..TO. SECONDARY SCHOOL: FROM TO.. SECONDARY SCHOOL: FROM.TO. C: PREVIOUS SECONDARY SCHOOL ( IF TRANNSFER TO THIS SCHOOL) NAME OF THE SCHOOL ADDRESS. I IDENTIFT THAT THE ABOVE INFORMATION IS CORRECT TO THE BEST OF MY KNOWLEDGE.. DATE NAME OF STUDENT STUDENT SIGNATURE D: (TO BE COMPLETED BY FORM CO-ORDINATOR): DATE OF ADMISSION TO THIS SCHOOL. ADMISSION NUMBER YEAR. FORM ADMITTED YEAR.. DATE OF LEAVING SCHOOL. HIGHEST FORM REACHED.. CSEE (FORM IV) EXAMINATION NO SIGNATURE OF FORM CO-ORDINATOR..DATE.. SIGNATURE OF THE HEADMISTRESS.DATE.. 9

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRESIDENT S OFFICE REGIONAL ADMINSTRATION AND LOCAL GOVERNMENT MOSHI DISTRICT COUNCIL WERUWERU SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 575 MOSHI FORM FOR MEDICAL EXAMINATION To be complete by Medical Officer in respect of all form entrants. Full Name: Age: Blood Count (Red and white). Stool Examination:.. Urine analysis: Stuphilia test:.. T.B Test:... Eye Test:. Ears:.. Chest: Spleen: Abdomen:. ADDITIONAL INFORMATION: e.g physical or chronic family diseases etc..... I certify that the above is fit to purpose studies Signature. Designation Section.. Date.. STUDENT: You must bring this completed form when you come to school. No student will be allowed to enroll without certificate of physical fitness. HEADMISTRESS 10

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI. Shule ya Sekondari Weruweru S.L.P 575, MOSHI Tarehe HATI YA UTII WA SHERIA Mimi Bwana/Bibi..Mzazi/Mlezi wa.nimesoma kwa makini sheria za shule kama zilivyoandikwa katika maagizo kwa wazazi na nazikubali Sheria hizo na nitashirikiana na shule kuona kuwa mwanangu anazingati kwa manufaa ya Umma. Mimi.Binti wa Bwana/ Bibi.. Nimesoma kwa makini Sheria za shule kama zilivyoandikwa na ninazikubali Sheria hizo. Naahidi kuwa nitazifuata na kuzitii nikijua kuwa naelimishwa na Umma kwa manufaa ya Umma... SAINI YA MWANAFUNZI.. SAINI YA MZAZI TAREHE TAREHE 11