Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Similar documents
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

ORDER NO BACKGROUND

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

TIST HABARI MOTO MOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Deputy Minister for Finance

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

Je! imezingatia maslahi ya mkulima mdogo?

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kutetea Haki za Binadamu

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Govt increases vetting threshold of contracts

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

Human Rights Are Universal And Yet...

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

The Government is committed to improve marine transport and has a number

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

MWONGOZO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI WORLD BANK

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA MHANDISI DKT. CHARLES JOHN TIZEBA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO KWA

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Transcription:

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Athari Zake Kwa Mifumo Ya Mbegu Inayosimamiwa Na Wakulima Na Kwa Wakulima Wadogo April 2016

CONTENTS UTANGULIZI 3 MAELEZO YA JUMLA YA SEKTA ZA MBEGU NCHINI TANZANIA 4 Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Sekta ya Mbegu 4 Udhibiti wa Sekta Rasmi ya Mbegu 4 Kutotambuliwa kwa mchango wa Mfumo wa Mbegu Unaosimamiwa na Mkulima kwenye Sheria 5 MAPITIO YA SHERIA YA MBEGU YA 2003 NA KANUNI ZAKE KUHUSIANA NA WAKULIMA WADOGO NCHINI TANZANIA 5 Uwiano wa Sheria Kikanda na Athari zake kwa Sheria ya Mbegu 6 Udhibiti wa Ubora na Upatikanaji wa Mbegu Bora 6 ULINZI WA AINA ZA MIMEA (PVP) NCHINI TANZANIA 7 Shirika la Biashara la Dunia na Vifungu Vinavyohusiana na Biashara ya Haki za Mali za Kitaalamu 7 Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea (PBR) na Athari zake kwa wakulima wadogo 7 Athari kwa Zanzibar 8 Haki za Wakulima na Mkataba wa Mbegu 8 HITIMISHO 8

Tarehe saba mwezi wa nne, mwaka wa elfu mbili na kumi na tano, shirika la African Centre for Biosafety (ACB) ilibadilisha jina lake kuwa African Centre for Biodiversity (ACB). Kubadili kwa jina ilitokana na makubaliano ndani ya shirika la ACB kuzingatia upana wa kazi ndani ya miaka iliyopita. Makala yote ya ACB kabla ya tarehe hii zitabaki chini ya jina letu la zamani la African Centre for Biosafety na zinapaswa zinukuliwe vile. Tunabaki kuwa na nia ya kuondoa ukosekanaji wa usawa kwenye mifumo ya chakula na kilimo Afrika na tunaamini kwenye haki ya watu kuwa na chakula chenye afya na kilichotayarishwa sahihi kitamaduni na kilichotengenezwa kupitia njia endelevu na kiikolojia na haki yao ya kufafanua mifumo yao ya chakula na kilimo. The African Centre for Biodiversity www.acbio.org.za S.L.P 29170, Melville 2109, Johannesburg, Afrika Kusini. Simu: +27 (0)11 486 1156 Ubunifu na Mpangilio: Adam Rumball, Sharkbouys Designs, Johannesburg Picha: Wild cultivated cowpea. Ton Tulkens, Flicker Acknowledgements Shirika la ACB linatambua ukarimu na msaada wa Bread for the World na pia kazi ya Sabrina Nafisa Masinjila, aliyepo Tanzania, pamoja na mchango kutoka kwa Gareth Jones na Haidee Swanby kutengeneza hii ripoti. 2 AFRICAN CENTRE FOR BIODIVERSITY

UTANGULIZI Kilimo kinatambuliwa kama moja ya sekta muhimu ambazo ni sehemu ya mageuzi ya kiuchumi katika kuifikisha Tanzania katika hadhi ya kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025 (Tume ya Mipango Tanzania, Dira ya Maendeleo Tanzania 2025). Dhima ya mageuzi haya ni kilimo cha biashara zaidi kuelekea Mapinduzi ya Kijani. Kwa sasa sekta hii inahusisha asilimia 75 ya Watanzania wote na wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo ambao hulima takribani asilimia 91 ya ardhi yote inayofaa kwa kilimo. Aidha, sekta huchangia takribani asilimia 26.5% ya pato la taifa (GDP) (ACB, 2015a). Mbegu kwa ajili ya kilimo hupatikana kutokana na mifumo wa ugavi rasmi na isiyo rasmi (pia hujulikana kama mfumo wa mbegu unaosimamiwa na mkulima); asilimia 90 hutokana na mfumo wa mbegu unaosimamiwa na mkulima wakati asilimia 10 hutokana na sekta rasmi ya mbegu (Majamba & Longopa, 2012). Nafasi ya sekta binafsi katika utoaji na biashara ya mbegu bora inathibitishwa na idadi ya jitihada mbali mbali za ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPT) pamoja na maboresho ya sera za kilimo na sekta ya mbegu. Mfano wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Binafsi ni Muungano Mpya wa Usalama wa Chakula na Lishe wa Nchi za G8 (NAFSN) uliozinduliwa mwaka 2012 ambao umeunganishwa na Mpango wa Tanzania wa Utekelezaji wa Usalama wa Chakula (TAFSIP) na mipango mingine iliyojumuishwa katika Programu Jumuishi ya Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP). Mpango wa G8 (NAFSN) umekuwa na ushawishi mkubwa katika malengo ya sera zinazovutia zaidi uwekezaji wa sekta binafsi ya ndani na ya kimataifa. Kutokana na kushamiri kwa Miradi ya Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), sheria za mbegu zinafanyiwa mapitio. Mwaka 2012 Sheria mpya ya Wazalishaji wa Mbegu inayoendana na Muungano wa Ulinzi wa Mimea (UPOV) wa mwaka 1991 ilianza kutumika, na kwa sasa Sheria ya Mbegu ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 inafanyiwa mapitio. Hivi karibuni uoanishaji wa mkataba wa (PVP) kwa nchi za Afrika uliidhinishwa Arusha nchini Tanzania ukiwa Africa Rising, Babati Tanzania. S. Malyon, CIAT na lengo la kuchochea maendeleo ya aina mpya za mimea kutoka kwenye sekta binafsi na kuwezesha usambazaji na upatikanaji wa mbegu bora kama bidhaa kwenye bara zima. Kwa bahati mbaya, PPP pamoja na maboresho ya sheria zinashindwa kutambua mchango wa wakulima wadogo ambao hutoa asilimia 90 ya mbegu kutoka kwenye mfumo wa mbegu unaosimamiwa na mkulima au haki za wakulima kama zilivyoainishwa katika Mkataba wa Kimataifa kuhusu Rasilimali za Vinasaba za Mimea katika Chakula na Kilimo (ITPGRFA). Athari kwa wakulima wadogo na mifumo yao ya mbegu inayosimamiwa na wakulima bila shaka zitajitokeza kufuatia mapitio haya ya sheria za mbegu na kuridhiwa kwa Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea (PBR) ya mwaka 2012. Mapitio katika sheria yanajikita katika udhibiti wa ubora, kuondoa mbegu bandia, upanuzi wa mifumo ya Mbegu Zilizothibitishwa Ubora (QDS) na kudhibiti uuzaji wa mbegu zisizothibitishwa. Ingawa panaweza kuwepo na mambo mazuri yanayotarajiwa kutokana na mapitio ya sheria hiyo kama vile upanuzi wa mfumo wa QDS kutoka ngazi ya kata hadi wilaya, kuna wasiwasi unaotokana na kuzuiwa kwa uuzaji wa mbegu zisizothibitishwa, ambao hautoi mwanya kwa mbegu zinazosimamiwa na wakulima. Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania 3

MAELEZO YA JUMLA YA SEKTA ZA MBEGU NCHINI TANZANIA Sekta rasmi ya mbegu nchini Tanzania husambaza kiasi kidogo sana cha mbegu bora kwa wakulima nchini Tanzania (takribani asilimia 4-10) lakini bado ndiyo inayopata uungwaji mkono mkubwa wa serikali, fedha na taratibu za udhibiti huku mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima ambao hutoa asilimia 90, inabaki kutotambuliwa na haipati msaada. Utafiti uliofanywa na ACB mwaka 2014 huko Morogoro na Mvomero uligundua kwamba zaidi ya asilimia 80 ya mbegu za asili za mahindi, mazao aina ya kunde na mpunga zinazotumika na wakulima hazijathibitishwa, na wakulima wengi huendelea kutumia kwa kurudia mbegu zinazotokana na mavuno ya msimu uliopita. Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Sekta ya Mbegu Sekta ya biashara ya mbegu Tanzania ilianzia miaka ya 1970 wakati msaada kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ilisaidia kuanzishwa kwa mashamba ya mbegu, kampuni ya Mbegu ya Taifa (Tanseed) na Wakala wa Uthibitisho wa Mbegu Tanzania (TOSCA). Soko huria na kulegezwa kwa masharti ya kiuchumi kwenye miaka ya 1990 ilipelekea makampuni makubwa ya kimataifa ya mbegu kuingia Tanzania, ambapo yalilenga mbegu zenye faida (kwa sehemu kubwa ikiwa ni mahindi chotara na mpunga kiasi); ambapo kati ya mwaka 1993 na 2000 makampuni binafsi ya mbegu yalitoa aina 17 za mbegu za mahindi chotara. Katika kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 1990, Chama cha Wafanyabiashara ya Mbegu Tanzania (TASTA) kilianzishwa lakini kilikuja kusajiliwa mwaka 2002. Takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2011 Kampuni ya Mbegu ya Zimbabwe Seed Co inahodhi asilimia 46 ya soko la mbegu, ikifuatiwa na Pannar, Monsanto (zote zikiwa na asilimia 9) na Dupont (asilimia 6). Monsanto na Sygenta zimedhamiria kupanua shughuli zao nchini Tanzania chini ya mwavuli wa Muungano wa NAFSN wa Nchi za G8; Monsanto kwenye biashara ya mbegu za mahindi na mboga, na Sygenta katika mbegu za mpunga na mboga. Mawili kati ya makampuni makubwa ya kimataifa ya mbegu kutoka Asia na Ulaya, Kampuni ya East-West Seed ya Ufilipino, na Kampuni ya Uholanzi ya Rijk Zwaan, zimeingia ubia na unaoitwa Afrisem kwa ajili ya kuzalisha mbegu za mboga za kitropiki kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi katika jiji la Arusha (ACB, 2015c). Kampuni nyingine kubwa ya kimataifa kutoka India, Advanta Seed imeingia mkataba na Muungano wa NAFSN wa Nchi za G8 nchini Tanzania katika kuongeza matumizi ya aina za mbegu bora. Kampuni nyingine nyingi za mbegu za ukanda wa Afrika pia zinafanya biashara nchini Tanzania, ambazo ni pamoja na East Africa Seed Company (Kenya), FICA (Uganda) na MRI (Zambia, ambayo kwa sasa inamilikiwa na Sygenta). Kampuni ya Mbegu ya Kenya (KSC) pia ipo nchini Tanzania kupitia kampuni zake tanzu za Simlaw (mboga) na Kibo Seed (ACB, 2015c). Muungano wa Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA) umekuwa ni mtendaji mkubwa katika sekta ya mbegu zinazotumika ndani ya Tanzania na imetoa ruzuku kwa makampuni 11 ya Kitanzania ya mbegu, zaidi ya nchi nyingine zote zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Tanseed ambayo ilibinafsishwa kwa asilimia 100 mwaka 2002 (ACB, 2015c). Biashara ya usambazaji wa mbegu inaonekana ni eneo lenye kutengeneza faida kubwa, huku makampuni makubwa yakilenga soko la mbegu barani Afrika. Athari zake kwa wakulima wadogo ni utegemezi mkubwa kwa mbegu kutoka sekta ya biashara na kuingia gharama kubwa zinazoambatana na kununua mbegu zilizothibitishwa na mbolea ambazo zinakuja pamoja. Aidha, kupuuza mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima kutasababisha kupungua kwa aina za mbegu za wakulima na koo za mimea; msingi muhimu wa uhifadhi wa anuwai kilimo. Udhibiti wa Sekta Rasmi ya Mbegu Sheria ya mbegu ya 2003 ndio inayosimamia sekta rasmi ya mbegu na inatoa msingi wa kuanzishwa kwa taasisi mbalimbali: Kamati ya Mbegu ya Taifa ambayo hufanya kazi kama chombo cha ushauri kwa serikali, na pia hutoa 4 AFRICAN CENTRE FOR BIODIVERSITY

Village Based Agricultural Adviser and QDS farmer, Mr. Bakari, showing rice nursery on a Farmer Field Plot in Mvomero, Tanzania. kanuni za uthibitisho kwa mujibu wa sheria wa mbegu, kupima mbegu kwenye maabara, tathmini na usajili wa aina za mbegu chini ya Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI), taasisi huru yenye jukumu la uthibitishaji wa mbegu na udhibiti wa ubora wa mbegu. Wizara ya Kilimo nchini Tanzania ndio mdhibiti mkuu wa sekta rasmi ya mbegu nchini. Serikali inasema kwamba haki za wakulima kupata mbegu bora imezingatiwa kwenye sheria za mbegu. Sheria pia imejumuisha ushiriki wa wakulima wadogo katika uzalishaji wa mbegu kupitia mfumo wa Mbegu Zilizothibitishwa Ubora (QDS). Kutotambuliwa kwa mchango wa Mfumo wa Mbegu Unaosimamiwa na Mkulima kwenye Sheria Sheria ya mbegu haitambui kwa uwazi mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima na aina za mbegu za kienyeji na haisemi chochote kuhusu haki za wakulima. Watunga sera wanasisitiza kwamba hakuna zuio lolote kuhusiana na jinsi wakulima wanavyotumia, wanavyohifadhi na kubadilishana mbegu zao ili mradi mbegu hizo haziiingii katika soko la biashara, na inathibitisha kwamba haihusiki na mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima/sekta ya mbegu isiyo rasmi. Njia pekee ambayo serikali inaweza kutambua mfumo wa mbegu usio rasmi ni iwapo utaundwa ukiambatana na taasisi za utawala. Jambo hili huwatenga wakulima wadogo, kwani fedha zinazotolewa kupitia ubia baina ya sekta ya umma na binafsi huelekezwa kwenye sekta binafsi. MAPITIO YA SHERIA YA MBEGU YA 2003 NA KANUNI ZAKE KUHUSIANA NA WAKULIMA WADOGO NCHINI TANZANIA Hitaji la kufanya mapitio ya Sheria ya Mbegu ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 inalenga katika kuwezesha: (a) uwiano wa sheria unaoendelea katika kanda ili kuondoa vikwazo katika ngazi ya kitaifa na kikanda na kuhimiza uwekezaji katika soko la mbegu unaofanywa na wajasiriamali wapya na waliopo; (b) kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uzalishaji wa mbegu ili kufanya mbegu zipatikane pamoja na kutumia njia ya ubia wa sekta ya umma na binafsi kuhusiana na uzalishaji wa mbegu za umma; (c) kudhibiti mbegu bandia (Kitengo cha Sheria, Wizara ya Kilimo). Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania 5

mbegu zake kabla ya kufanya biashara yoyote ya mbegu. Inapotokea mbegu zimeshindwa kuota, muuza mbegu anatakiwa kumlipa fidia mkulima au mnunuzi wa mbegu zile, kupitia ushahidi uliotolewa na maafisa uthibitisho wa mbegu, wakaguzi, wapimaji na wachambuzi wa mbegu. Marekebisho ya sheria pia yanazuia zaidi uuzaji wa mbegu zisizothibitishwa, mbegu zisizopimwa au mbegu yoyote ambayo haikufuata taratibu chini ya Sheria, kwa adhabu ya faini au kifungo. Rwanda Seed Systems, Bean seeds. SGeorgina Smith, CIAT Uwiano wa Sheria Kikanda na Athari zake kwa Sheria ya Mbegu Tanzania ni mwanachama wa jumuiya 2 za kiuchumi katika kanda ya Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Sheria ya Mbegu ya 2003 ilitayarishwa chini ya michakato ya uwiano wa sheria za Jumuiya za Afrika Mashariki /ASARECA wakati Tanzania kama mwanachama wa SADC pia ilisaini Mkataba wa Maelewano wa SADC kuhusu Mbegu (MoU) ambao unaruhusu usajili wa aina za mimea uliotolewa baina ya nchi wanachama mbili zozote bila ya kufanyiwa majaribio ya ziada (ACB, 2015a). Udhibiti wa Ubora na Upatikanaji wa Mbegu Bora Imeripotiwa na wadau wote wa sekta ya umma na binafsi kwamba si chini ya 25-30% ya mbegu zilizothibitishwa ni mbegu bandia 1 (USAID, 2013). Hii inaonyesha kushindwa kwa mfumo rasmi wa mbegu katika umakini wa mchakato wa udhibiti wa ubora wa mbegu, wakati hii ndiyo sekta inayopata msaada na fedha kutoka serikalini. Vifungu vingi vya Marekebisho ya Sheria ya Mbegu ya mwaka 2014 vinashughulika na udhibiti wa ubora kupitia kuteuliwa kwa maafisa uthibitisho wa mbegu, wakaguzi wa mbegu, wapimaji na wachambuzi katika ngazi za serikali za mitaa. Sheria inahitaji kwamba muuza mbegu ahakikishe ubora wa Wakati mabadiliko katika sheria kuhusiana na udhibiti wa ubora yanaonekana kuwa na manufaa kwa wakulima, kupitia kuzuia wafanyabiashara wasio na maadili, vifungu kuhusu kutambuliwa kwa mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima vimeachwa. Kwa ujumla, wakulima wanafahamika kwa kujishughulisha kikamilifu katika sekta ya mbegu, hususani kuhusiana na kubadilishana mbegu na wakati mwingine mauzo ya mbegu za kienyeji au mbegu zilizohifadhiwa kutoka shamba kwa ndugu zao, majirani au marafiki (mitandao ya kijamii), vikundi vya mbegu kwenye jamii na kwenye masoko ya maeneo yao (McGuire & Sperling, 2016). Mianya maalumu kwa wakulima wadogo lazima izingatiwe kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Mbegu ya Ethiopia ambayo inatambua na kuondoa zuio kwa mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani. Serikali ya Tanzania inapaswa kuridhia kuondoa zuio kwa mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani, lakini pia izuie watu wanaouza mbegu ambazo hazijathibitishwa kama vile zimethibitishwa ilivyopendekezwa katika mkutano wa mapitio ya sheria ya mbegu. Upanuzi wa mfumo wa Mbegu Zilizothibitishwa Ubora (QDS) hadi ngazi ya wilaya ni kipengele muhimu ambacho serikali inaweza kukifikiria katika Sheria ya Mbegu na hii itaungwa mkono katika kuziba pengo katika mfumo wa mbegu kama vile uhaba wa rasilimali fedha na kujenga uwezo. Hata hivyo, mchakato wa mapitio bado unaendelea na bado kuna mashaka iwapo mapendekezo ya mfumo wa Mbegu Zilizothibitishwa Ubora (QDS) utajumuishwa katika rasimu 1. Mbegu bandia ni pamoja na aina ambazo ni: 1) zenye ubora duni na hazichipui vizuri; 2)zenye ubora duni na imechangnyika na aina nyingine; 3) zimebadilishwa punje; 4) zimefungashwa kwenye vifungashio bandia; 5) zimeuzwa na lebo zilizoisha muda wake; na/au 6) hazijasajiliwa katika daftari la taifa la aina za mbegu. 6 AFRICAN CENTRE FOR BIODIVERSITY

ya mwisho ya Sheria. Kama itajumuishwa, basi itawakilisha ushindi muhimu kwa wale wakulima wanaojihusisha kwenye QDS. Nguvu zaidi itakuwa katika kuzuia mauzo ya mbegu zisizothibitishwa kwa zile mbegu tu ambazo huuzwa kwa udanganyifu kama vile ni mbegu zilizothibitishwa, na kuepuka kuzuia mauzo ya mbegu zisizothibitishwa. ULINZI WA AINA ZA MIMEA (PVP) NCHINI TANZANIA Shirika la Biashara la Dunia na Vifungu Vinavyohusiana na Biashara ya Haki za Mali za Kitaalamu Tanzania kama mwanachama wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) inatakiwa chini ya Vifungu Vinavyohusiana na Biashara ya Haki za Mali za Kitaalamu (TRIPS) kutekeleza muundo wa Ulinzi wa Aina za Mimea (PVP) chini ya Ibara 27.3.b. Vifungu vya TRIPS vinaruhusu nchi uwezo wa kufanya marekebisho, na kutamka kwamba nchi wanachama zinaweza kutekeleza mfumo ambao ni wa kipekee, au ni wa aina ya peke yake, na ambao umeundwa kulingana na mahitaji ya wazalishaji wa mimea (sui generis). Hata hivyo, mfumo wa ulinzi uliotayarishwa chini ya Muungano wa Ulinzi wa Aina Mpya za Mimea (UPOV) unahimizwa na sekta ya mbegu ya kimataifa kama mfumo pekee ambao utawapa imani wawekezaji. Muungano wa UPOV na hususani mkataba wa sasa wa wazi, UPOV 91, huziongezea nguvu haki za wazalishaji wa mimea, wakati huo huo zikikandamiza kwa nguvu haki za wakulima za kubadilishana na kuuziana mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani za aina zinazolindwa. Jambo hili ni ukweli ulio wazi kwamba halifai kwa nchi ambazo mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima ndiyo iliyotawala. Tanzania ilijiunga na Mkataba wa UPOV 91 mnamo Novemba 2015 na ni moja ya nchi za kwanza zilizo na maendeleo duni kujiunga na UPOV kupitia mapitio na kuridhia kwa Sheria mpya ya Haki za Wazalishaji wa Mimea (PBR) ya mwaka 2012, na Sheria ya PBR ya Zanzibar ya mwaka 2014. Pia kuna shinikizo kubwa kuleta uwiano wa kikanda wa sheria za aina ya UPOV na PVP kupitia Jumuiya za Kiuchumi za Kanda (RECS) na Taasisi za Haki za Mali za Kitaalamu kama vile Shirika la Kanda ya Afrika la Mali za Kitaalamu (ARIPO). Uwiano kama huo utaruhusu wazalishaji wa mimea pamoja na hasa sekta ya mbegu kudai ulinzi wa haki za mali za kitaalamu kwenye nchi nyingi kwa mpigo, katika ukanda wa ARIPO. Hii sio tu itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama zao za miamala lakini pia itawahakikishia ulinzi wa mbegu zao unatambulika na kutekelezwa kwa usawa kwenye ukanda mzima. Mnamo Julai 6 2015 Itifaki ya Arusha ya ARIPO kwa ajili ya Ulinzi wa Aina za Mimea iliridhiwa na itaanza kutumika mara baada ya nchi nne kuidhinisha Itifaki hiyo. Tanzania iliandaa Kongamano la Kidiplomasia wakati huo na ilitia saini Itifaki baadaye mwezi Septemba 2015. Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea (PBR) na Athari zake kwa wakulima wadogo Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea ya mwaka 2012 inatoa nguvu kwa haki za wazalishaji wa koo za mimea, na kuupuza haki za wakulima, kuhusiana na kuhifadhi, matumizi ya kurudia na kubadilishana mbegu na vipandikizi vya aina zinazolindwa, ziwe zinatokana na sekta binafsi au ya umma. Serikali inadai kwamba chini ya Sheria hii, haki za wakulima hazijakandamizwa kwani inaruhusu shughuli zinazofanyika kwa matumizi binafsi na kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara chini ya Kifungu 31 (1) (a) na kwamba haki za wazalishaji hazijumuishi wakulima wanaotumia mbegu zilizovunwa kutoka kwenye aina zinazolindwa kwa madhumuni ya kuzizalisha kwenye mashamba yao. Hata hivyo, mara kwa mara wakulima hutumia aina bora za mbegu zinazolindwa, na kuzuia uhifadhi na kubadilishana kwa aina hizi za mbegu bila ya ruhusa kutakuwa na athari mbaya kwenye mifumo yao ya uzalishaji wa chakula. Zaidi ya hayo, wakulima bado hufanya biashara ya mbegu zote kwenye mifumo yao hata kwa kiwango kidogo, na Sheria hii itakuwa na athari ya kudhoofisha desturi hizi. Na isitoshe, zuio la kisheria kwa wakulima wasibadilishane mbegu kutasababisha kupotea kwa jinni za mimea ambazo zinachangia katika kuendeleza mbegu stahiki kwa eneo husika na uanuwai wa mazao. Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania 7

Athari kwa Zanzibar Ili Sheria ya Tanzania ya Haki za Wazalishaji wa Mimea iidhinishwe, Muungano wa Ulinzi wa Aina za Mimea (UPOV) ulihitaji kwamba zote Tanzania Bara na Zanzibar ziwasilishe sheria zao. Hata hivyo, kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kilimo sio suala la muungano baina ya Tanzania bara na Zanzibar, hivyo inahitajika kwa kila upande wa Muungano kutunga sheria tofauti lakini zinazowiana. Inaonekana mchakato wa Zanzibar wa kutunga Sheria inayokidhi matakwa ya UPOV ulifanyika kwa pupa, pakiwepo na uelewa mdogo wa kwa wakulima wao, asasi za kiraia na wadau wengine kuhusu athari za kuridhia Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea. Haki za Wakulima na Mkataba wa Mbegu Mkataba wa Kimataifa kuhusu Rasilimali za Mimea na Jenetiki kwa Chakula na Kilimo (ITPGRFA) unathibitisha kwamba haki zinatambulika za kuhifadhi, kutumia, kubadilishana na kuuza mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani na aina nyingine za vipandikizi, na kushiriki katika kufanya maamuzi, na katika kushirikishana kwa njia ya haki na usawa manufaa yatokanayo na matumizi ya rasilimali za mimea za kijenetiki kwa ajili ya chakula na kilimo, kwamba ni msingi katika kufikia haki za wakulima, pia kukuza haki za wakulima katika ngazi za kitaifa na kimataifa. Mkataba unawataka wahusika wa mkataba kubeba jukumu la kuhakikisha haki za wakulima zinapatikana na kuchukua hatua za kulinda na kukuza haki za wakulima. Tanzania iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa ITPGRFA mnamo Aprili 2004 na kuanza mchakato wa kuubadilisha kwenye sheria za ndani mwaka 2007 wakati Tanzania ilipoanzisha matayarisho ya muundo wa kisheria wa Rasilimali za Kijenetiki za Mimea kwa Chakula na Kilimo. Kwa bahati mbaya mchakato wa kubadilisha Mkataba na kuuweka kwenye sheria za ndani nchini Tanzania umekwama, waraka wa rasimu ukiwa katika ngazi ya Baraza la Mawaziri kwa kipindi kirefu sasa. Inaonekana kama vile hakuna haraka kwa upande wa Serikali ya Tanzania kuridhia Mkataba huu, kwa vile utekelezaji wa haki za mkulima unategemea kwa njia ya kipekee kwenye mamlaka za wahusika wa mkataba, tofauti na kuwa ni sharti la sheria ya kimataifa. Kwa vyovyote itakavyokua, hata kama sheria itatungwa kuwezesha vifungu vya Mkataba kutumika kwenye haki za wakulima, kuna uwezekano mkubwa kwa sheria hiyo kuwa chini ya Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea. Kwa Tanzania, kujaribu kupata urari kati ya Mkataba na Sheria yake ya Haki za Wazalishaji wa Mimea, kutamaanisha kwamba marekebisho yatabidi yafanyike kwenye Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea, pamoja na kuzingatia haki za wakulima katika Sheria ya Haki za Wazalishaji wa Mimea. HITIMISHO Maboresho ya sasa ya sheria yamebuniwa kusaidia ubia baina ya sekta ya umma na binafsi na utendaji wa sera pia na kuvutia uwekezaji wa ziada kwenye kilimo. Ubia baina ya Sekta ya Umma na Binafsi ndio chombo kinachopendelewa kwa maendeleo ya kilimo kwa sasa na kuna uwezekano wa hili kuendelea hata kwa siku za usoni. Japokuwa ubia wa aina hii unaweza kujenga uwezo wa kitaasisi na kitaalamu katika mbegu, utafiti na maendeleo na huduma za ugani, pia unaweza kujielekeza katika kulinda maslahi na faida binafsi. Maboresho ya sheria ya mbegu yameiacha mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima na mchango wake katika sekta ya mbegu nchini Tanzania. Mahususi, Sheria ya Mbegu haiwapi ahueni wakulima wadogo kuhusiana na mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani. Kukosa ufahamu kuhusu dhamira na athari za sheria hii kumetapakaa kwenye makundi mengi tofauti; ni serikali na sekta binafsi ndio wanaoainisha na kuunda ajenda ya sera. Serikali ya Tanzania inapaswa kutayarisha sera ambazo zinazuia mwingilio wa mbegu za kibiashara ambao unaharibu mifumo ya mbegu ya wakulima na kusababisha upotevu wa bioanuwai ya kilimo. Inapaswa kutambua kwa uwazi haki za wakulima na kusaidia michakato ya udhibiti wa ubora wa mbegu inayoweza kubadilishwa na kutoholewa kulingana na mazingira ya wenyeji. Mahususi 8 AFRICAN CENTRE FOR BIODIVERSITY

inapaswa kutambua na kuruhusu mwanya katika sheria ya mbegu kwa matumizi yote ya mbegu zilizohifadhiwa kutoka shambani, ili kuepuka kufanya jinai shughuli za wakulima kuhusiana na mbegu, na kuondoa umiliki kwenye mbegu zote mara zitakapoingia kwenye mfumo wa mbegu wa wakulima. Aidha, rasilimali za umma na bajeti zielekezwe kwenye kufanya majaribio na kuendeleza mifumo ya mbegu ya wakulima kupitia maboresho na kuendeleza aina za mbegu za wakulima. Wakulima wasionekane kama ni watumiaji wa mwisho tu bali kama sehemu ya mchakato kama wazalishaji wa mimea na wazalishaji wa mbegu katika kukidhi uhitaji wa mbegu katika sekta ya mbegu. Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania 9

PO Box 29170, Melville 2109, South Africa www.acbio.org.za