Ndugu na dada zangu wapendwa,

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa,

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

United Pentecostal Church June 2017

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Kiu Cha umtafuta Mungu

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Human Rights Are Universal And Yet...

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Oktoba-Desemba

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

Maisha Yaliyojaa Maombi

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

MAFUNDISHO YA UMISHENI

2 LILE NENO LILILONENWA

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

MSAMAHA NA UPATANISHO

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

Kwa Kongamano Kuu 2016

Makasisi. Waingia Uislamu

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi. Iliyoendelea sana

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

PDF created with pdffactory trial version

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

K. M a r k s, F. E n g e l s

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi

Transcription:

UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, NOVEMBA 2011 Na Rais Thomas S. Monson Simama Pahali Patakatifu Mawasiliano na Baba yetu aliye Mbinguni pamoja na maombi yetu Kwake na maongozi Yake kwetu ni muhimu ili tuweze kuepuka dhoruba na majaribu ya maisha. Ndugu na dada zangu wapendwa, tumesikia jumbe nzuri asubuhi ya leo, na nampongeza kila mmoja ambaye ameshiriki. Tumefurahia hasa kuwepo kwa Mzee Robert D. Hales pamoja nasi tena na akihisi kuwa na nafuu. Tunakupenda, Bob Kama nilivyotafakari kile nilingesema kusema nanyi asubuhi ya leo nimepata ari ya kushiriki mawazo na hisia kadha ambazo naonelea kuwa muhimu na za kufaa. Ninaomba kwamba niweze kuelekezwa katika maneno yangu. Nimeishi duniani kwa miaka 84 sasa. Ili kuwapa mtazamo kidogo, nilizaliwa mnamo mwaka ambao Charles Lindbergh aliposafiri bila kutua kutoka New York hadi Paris kwa kutumia ndege ya injini moja, kiti kimoja na seti moja ya bawa. Mengi yamebadilika katika miaka 84 tangu wakati huo. Imekuwa muda mrefu tangu binadamu kuwa mwezini na kurejea. Kwa hakika, sayansi bunifu ya wakati uliopita sasa imekuwa halisi. Na uhalisi huo, kwa msaada wa teknolojia ya wakati wetu, unabadilika kwa kasi hata ni vigumu kushikamana nao ikiwa tunaweza kamwe. Kwa wale kati yetu wanaokumbuka simu zenye mviringo wa kupiga namba, na mashine ya chapa ya mikono, teknolojia ya leo ni ya kushangaza zaidi sana. Pia inayogeuka kwa kasi ni dira ya maadili ya jamii. Tabia ambazo wakati mmoja zilionekana kutofaa na zisizo za kimaadili sasa hazivumiliwi tu bali zinaonekana na watu wengi kama zinazokubaliwa. Hivi majuzi nilisoma katika Wall Street Journal makala yaliyoandikwa na Jonathan Sacks, rabbi mkuu wa Uingereza. Miongoni mwa vitu vingine, aliandika: Katika takriban kila jamii ya Magharibi mnamo 1960 kulikuwa na mapinduzi ya maadili, kuachwa kwa mfumo wa kitamaduni wa kujizuia. Yote unayohitaji, waliimba Beatles, ni upendo. Mfumo wa maadili wa Uyahudi-Ukristo ulitupwa. Mahali pake, ukaja [usemi]: [Fanya] chochote kinachokufaidi. Amri Kumi ziliandikwa upya kama Mapendekezo Kumi Bunifu. Rabbi Sacks anaendelea kuomboleza: Tumekuwa tukitumia mtaji wetu wa kimaadili kwa uzembe huo huo ambavyo tunavyotumia mtaji wetu wa kifedha.... Kuna sehemu nyingi [za dunia] ambapo dini ni jambo la kale na hakuna sauti ya kusawazisha utamaduni wa nunua, fuja, vaa, punga kwa madaha kwa sababu unastahili. Ujumbe huu ni kwamba uadilifu umepitwa na wakati na dhamiri ni ya wadhaifu na amri kuu ya pekee ni Wewe usipatikane. 1 Akina ndugu na dada, hii kwa bahati mbaya inaeleza kuhusu wingi wa dunia inayotuzunguka Je! tuwe na wasiwasi kwa kukata tamaa na kushangaa jinsi tutakavyonusurika katika dunia kama hii? La. hasha. Kwa hakika, tunayo katika maisha yetu injili ya Yesu Kristo na tunajua uadilifu haujapitwa na wakati, kwamba dhamiri yetu ipo kutuongoza, na kwamba tunawajibikia matendo yetu. Ingawa dunia imebadilika, sheria za Mungu zinabaki thabiti. Hazijabadilika; hazitabadilika. Amri Kumi ni hizo tu amri. Nazo si mapendekezo. Zinahitajika kwa kila njia hivi leo kama zilivyokuwa wakati Mungu alipowapa wana wa Israeli. Ikiwa tu tutasikiliza, tunasikia mwangwi wa sauti ya Mungu ikituzungumzia hapa na sasa: Usiwe na miungu mingine ila mimi. 1

Usijifanyie sanamu ya kuchonga.... Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.... Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.... Waheshimu baba yako na mama yako.... Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo.... Usitamani. 2 Mfumo wetu wa kanuni ya maadili ni wa mkataa, hauna mjadala. Haupatikani tu kwa Amri kumi, bali pia katika Mahubiri Mlimani tuliyopewa na Mwokozi alipotembea duniani. Unapatikana kote katika mafundisho Yake. Unapatikana katika maneno ya ufunuo wa kisasa. Baba yetu wa Mbinguni ni yule yule, jana leo na milele. Nabii Mormoni anatuambia Mungu habadiliki kutoka milele hadi milele yote. 3 Katika ulimwengu huu ambapo karibu kila kitu kinaonekana kubadilika, uthabiti wake ni kitu ambacho tunaweza kutegemea, nanga ambayo tunaweza kushikilia na kuwa salama, ili tusisombwe kwenye maji ya hatari. Inaweza kuonekana kwako wakati mwingine kuwa wale walioko duniani wana raha kukushinda wewe. Wengine wenu mnaweza kuhisi kuwa mnafinywa na mfumo wa kanuni za maadili ambayo sisi katika Kanisa tunazingatia. Akina ndugu na dada, nawatangazia hata hivyo kwamba hapana chochote kinachoweza kuleta shangwe maishani mwetu au amani kuliko Roho inayoweza kutujia tunapomfuata Mwokozi na kuweka amri. Kwamba Roho hawezi kuwa kati aina ya matendo ambayo wingi wa ulimwengu hujihusisha. Mtume Paulo alitangaza ukweli huu: Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu: maana kwake hayo ni upuuzi wala hawezi kuyafahamu kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 4 Maneno mwanadamu wa tabia ya asili yanaweza kutuhusu ikiwa tutakubali kuwa hivyo. Ni lazima tuwe macho katika ulimwengu ambao umesonga mbali sana kutoka kwa kile kilicho cha kiroho. Ni muhimu tukatae chochote kisichopatana na viwango vyetu, kwa njia hiyo tukikataa kupoteza kile tunachotamani zaidi uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu. Mawimbi bado yatapiga milangoni mwetu mara kwa mara, kwani ni sehemu isiyoepukika ya uzoefu wetu katika maisha ya muda. Sisi, hata hivyo tutakuwa tayari kukabiliana nayo, kujifunza kwayo na kuyashinda ikiwa tuna injili kwenye kiini chetu na upendo wa Mwokozi mioyoni mwetu. Nabii Isaya alitangaza, Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa utulivu na matumaini daima. 5 Kama njia ya kuwa katika ulimwengu lakini si wa ulimwengu ni muhimu kuwa tunawasiliana na Baba wa Mbinguni kupitia kwa maombi. Anatutaka tufanye hivyo; Atajibu maombi yetu. Mwokozi alitushauri kama ilivyorekodiwa katika 3 Nefi 18, mjihadhari na kusali siku zote, msije mkaingia majaribuni; kwani Shetani amewataka nyinyi.... Kwa hivyo lazima msali siku zote kwa Baba katika jina langu; Na chochote mtakachomwomba Baba katika jina langu, ambacho ni haki, mkiamini kwamba mtapata, tazama, kitapeanwa kwenu. 6 Nilipata ushuhuda wangu wa nguvu za maombi nilipokuwa karibu umri wa miaka 12. Nilikuwa nimefanya kazi kwa bidii ili kupata pesa na nilikuwa nimeweza kuweka akiba dola tano. Huu ulikuwa wakati wa Mfadhaiko Mkuu wakati dola tano ilikuwa pesa nyingi hasa kwa mvulana wa miaka 12. Nilipeana sarafu zangu zote za jumla za dola tano kwa baba yangu, naye akanipa noti badala yake ya dola tano. Najua kulikuwa na kitu maalum nilichokuwa nimepanga kununua kwa dola tano ingawa miaka hii yote baadaye siwezi kukumbuka kilikuwa nini. Nakumbuka tu jisni hizo pesa zilivyokuwa muhimu kwangu. Kwa wakati huo, hatukuwa na mashine ya kufulia nguo, kwa hivyo mama yangu alikuwa akituma nguo zetu zilizohitaji kufuliwa kwa dobi kila wiki. Baada siku kadha mzigo wa nguo zilizolowa maji ungerudishwa kwetu na Mama angezianika nguo katika kamba ya kuanikia nguo nyuma ya nyumba ili zikauke. Nilikuwa nimeweka noti yangu ya dola tano katika mfuko wa jinzi. Kama unvyoweza kukisia, jinzi yangu ilipelekwa kwa dobi pamoja na pesa zikiwa bado mfukoni. Nilipogundua kilichofanyika, niliugua kwa wasiwasi. Nilijua kuwa mifuko ilikuwa ikiangaliwa kwa kawaida kwenye dobi kabla ya kuoshwa. Ikiwa pesa zangu hazikugunduliwa na kuchukuliwa kwa njia hiyo, nilijua ilikuwa hakika pesa zingeangushwa wakati wa kuoshwa na zingechukuliwa na mfanyikazi kwenye dobi ambaye hangejua arudishie nani pesa hizo hata kama angekuwa na nia hiyo. Nasibu ya kupata dola zangu tano ilionekana mbali sana jambo ambalo mama yangu mpendwa alihakikisha nilipomwambia kwamba nilikuwa nimeacha pesa mfukoni. Nilitaka hizo pesa; nilihitaji hizo pesa; nilikuwa nimefanya kazi sana ili kupata pesa hizo. Nilifahamu kulikuwa na kitu kimoja tu ningefanya. Kwa hali ya kufa moyo, nilimgeukia Baba yangu wa Mbinguni na kumsihi aweke pesa zangu salama mfukoni humo hadi kwa njia yoyote hadi nguo zetu zilizoloa zirudi. Siku mbili ndefu sana baadaye, nilipojua ilikuwa karibu saa ya gari la mizigo kuleta nguo zetu, niliketi karibu na dirisha, nikingoja. Gari lilipoingia kwenye ukingo wa barabara moyo wangu ulikuwa unapiga kwa kasi. Mara wakati nguo zilipofika nyumbani nilichukua jinzi yangu na kukimbia kwa chumba changu. Niliweka mikono yangu iliyokuwa ikitetemeka kwenye mfuko. Wakati sikupata chochote mara moja, nilidhani yote yamepotea. Kisha vidole vyangu vikagusa hiyo noti iliyoloa ya dola tano. Nilipoivuta 2

kutoka mfukoni nilijawa na faraja Nilitoa maombi ya dhati na shukrani kwa Baba yangu wa Mbinguni kwani nilijua alikuwa amejibu ombi langu. Tangu wakati huo, nimepata kujibiwa maombi yasiyohesabika. Hapana siku iliyopita ambayo sijawasiliana na Baba yangu wa Mbinguni kupitia maombi. Ni uhusiano ambao ninahifadhi kwa upendo mkubwa mmoja ambao bila ningekuwa nimepotea kabisa. Ikiwa hauna uhusiano kama huo na Baba yako wa Mbinguni, ninakuhimiza kufanya bidii kuelekea shabaha hio. Unapofanya hivyo, utapewa haki ya uongozi na mwelekezo Wake maishani mwako muhimu kwa kila mmoja wetu ikiwa tutanusurika kiroho katika safari yetu hapa duniani. Mwongozo na mwelekezo kama huo ni karama ambazo anatupatia bila malipo tukiutafuta. Je! ni hazina iliyoje! Ninanyenyekezwa na kushukuru wakati Baba yangu wa Mbinguni anapowasiliana nami kupitia kwa mwongozo wake. Nimejifunza kuutambua, kuuamini na kuufuata. Mara na mara tena nimekuwa mpokeaji wa mwongozo kama huo. Uzoefu mmoja wa ajabu uliotokea katika mwezi wa Agosti 1987 wakati wa kuwekwa wakfu kwa Hekalu ya Frankfurt Ujerumani. Rais Ezra Taft Benson ambaye alikuwa nasi kwa siku mbili za kwanza ilibidi arejee nyumbani, kwa hivyo ikawa nafasi yangu kusimiamia vikao vilivyobakia. Siku ya Jumamosi tulikuwa na kikao kwa washiriki wetu wa Kiholanzi waliokuwa katika wilaya ya Hekalu la Frankfurt. Nilikuwa namfahamu mmoja wa viongozi wetu mkakamavu kutoka Uholanzi Ndugu Peter Mourik. Kabla tu baada ya kikao, nilipata msukumo dhahiri kuwa Ndugu Mourik angefaa kuitwa kuzungumzia washiriki wenzake wa Kiholanzi wakati wa kikao hicho, na kwamba kwa kweli, angeitwa kuwa mnenaji wa kwanza. Kwa kuwa sikumwona Hekaluni asubuhi hiyo, nilimpitishia Mzee Carlos E. Asay, Rais wetu wa Eneo, barua ndogo nikiuliza ikiwa Peter Mourik alikuwa amehudhuria katika kikao hicho. Kabla tu ya kusimama kuanzisha kikao, nilipata barua ndogo kutoka kwa Mzee Asay ikinifahamisha kuwa Ndugu Mourik kwa hakika hakuwa amehudhuria, kwamba alikuwa anashughuli kwingine na kuwa alikuwa na mpango wa kuhudhuria kikao cha kuweka wakfu hekaluni siku iliyofuata pamoja na vigingi vya wanajeshi. Niliposimama katika mimbari kukaribisha watu na kutoa muhtasari wa mpango, nilipokea msukumo dhahiri tena kuwa nitangaze Peter Mourik kama mnenaji wa kwanza. Hii ikiwa kinyume na hisia zangu kwani nilikuwa nimefahamu kutoka kwa Mzee Asay kuwa Ndugu Mourik kwa hakika hakuwepo kwenye hekalu. Nikiamini msukumo huo, hata hivyo, nilitangaza toleo la kwaya na maombi na kueleza kuwa mnenaji wa kwanza angekuwa Ndugu Peter Mourik. Niliporejea kwenye kiti changu, nilitupa macho kwa upande wa Mzee Asay na niliona katika uso wake sura ya wasiwasi. Baadaye aliniambia nilipotangaza Ndugu Mourik kama mnenaji wa kwanza, hakuamini masikio yake. Alijua kuwa nilipokea barua yake, na hata nikaisoma, na hakuelewa kwa nini nilitangaza Ndugu Mourik kama mnenaji nikijua hakuwa popote hekaluni. Wakati hayo yote yalipokuwa takitendeka, Peter Mourik alikuwa katika mkutano katika ofisi za eneo huko Porthstrasse. Wakati mkutano wake ukiendelea ghafula alimgeukia Mzee Thomas A. Hawkes Jr ambaye alikuwa mwakilishi wa eneo na kumwuliza Itamchukua muda gani kunifikisha hekaluni? Mzee Hawkes, ambaye alijulikana kuendesha kwa kasi gari lake ndogo la spoti, akajibu, Ninaweza kukufikisha kwa dakika 10! Lakini kwa nini unahitaji kuwa hekaluni? Ndugu Mourik alikubali kuwa hakujua kwa nini alihitaji kwenda hekaluni lakini alijua alilazimika kufika huko. Wawili hao walielekea hekaluni mara moja. Wakati wa wimbo mzuri wa kwaya nilitupa macho huku na kule, nikifikiri kwa wakati wowote ningemwona Peter Mourik. Sikumwona. La ajabu hata hivyo, sikuhisi wasiwasi wowote. Nilikuwa na hakikisho dhahiri kuwa yote yangekuwa sawa. Ndugu Mourik aliingia kwenye mlango wa mbele wa hekalu wakati maombi ya kufungua yalipokuwa yakiitimishwa, akiwa bado hajafahamu kwa nini alikuwa pale. Alipotembea kwa kasi ukumbini aliona picha yangu kwenye runinga na akanisikia nikisema, Na sasa tutasikia kutoka kwa Ndugu Peter Mourik. Kwa mshangao wa Mzee Asay, Peter Mourik mara moja akaingia chumbani na kuchukua nafasi yake katika jukwaa. Baada kikao hicho, ndugu Mourik nami tulijadili kile kilichokuwa kimetendeka kabla ya fursa yake kuongea. Nimetafakari msukumo huo uliokuja siku hiyo, sio tu kwangu bali pia kwa Ndugu Peter Mourik. Huo uzoefu wa ajabu imenipa ushuhuda dhahiri kuhusu umuhimu wa kustahili kupokea msukumo kama huo, kisha kuuamini na kuufuata unapokuja. Ninajua bila tashwishi kwamba Bwana alitaka kwa wale waliokuwa katika kikao hicho cha kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Frankfurt kusikiliza ushuhuda wa nguvu na wa kugusa wa mtumishi Wake Ndugu Peter Mourik. Akina ndugu na dada zangu, mawasiliano na Baba yetu wa Mbinguni pamoja na maombi yetu kwake na ufunuo wake kwetu ni muhimu kwetu kuweza kustahimili mawimbi na mateso ya maisha. Bwana anatualika, Sogeeni karibu nami na mimi nitasogea karibu na nyinyi; nitafuteni kwa bidii nanyi mtanipata. 7 Tunapofanya hivyo, tutahisi Roho Wake maishani mwetu, akitupa hamu na ujasiri kusimama kwa nguvu na imara katika haki kusimama... katika mahali pa takatifu, na wala msiondoshwe. 8 3

Upepo wa mabadiliko unapovuma ukituzunguka, na mfumo wa jamii kuendelea kuvunjika mbele ya macho yetu, acha tukumbuke ahadi za thamani za Bwana kwa wale wanaomwamini: Usiogope; kwa maana mimi ni pamoja nawe: usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako: nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 9 Ni ahadi gani hii! Na baraka namna hiyo iwe yetu, naomba katika jina takatifu la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, amina. MUHTASARI 1. Jonathan Sacks, Reversing the Decay of London Undone, Wall Street Journal, Aug. 20, 2011, online.wsj.com; mkazo umeongezwa. Muhtasari: Lord Sacks is the chief rabbi of the United Hebrew Congregations of the Commonwealth. 2. Kutoka 20:3 4, 7 8, 12 17. 3. Moroni 8:18. 4. 1 Wakorintho 2:14. 5. Isaya 32:17. 6. 3 Nefi 18:18 20. 7. Mafundisho na Maagano 88:63. 8. Mafundisho na maagano 87:8. 9. Isaya 41:10. Mafundisho kwa Nyakati Zetu Masomo katika Jumapili ya nne ya Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama utazingatia Teachings for Our Time. Kila somo linaweza kutayarishwa kutoka kwa moja au zaidi ya hotuba zilizotolewa katika mkutano mkuu wa majuzi sana (ona cheti hapo chini) Marais wa Kigingi na wilaya wanaweza kuchangua ni hotuba gani zitatumika, au wanaweza kutoka jukumu hilo kwa maaskofu na marais wa matawi. Viongozi wanafaa kusisitiza thamani kwa ndugu wa Ukuhani wa Melkizedeki na kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama hotuba sawa sawa katika Jumapili sawasawa. Wale wanaohudhuria masomo ya Jumapili ya nne wanahimizwa kujifunza na kulete darasani toleo la majuzi kabisa la gazeti ya mkutano mkuu. Ushauri kwa Matayarisho ya Somo kutoka kwa Hotuba Omba kwamba Roho Mtakatifu awe na wewe jinsi unayojifunza na kufunza hotuba hizi. Unaweza kushawishika kutayarisha somo kutoka kwa vifaa vingine, lakini hotuba za mkutano mkuu ndio mtalaa ulioidhinishwa. Wajibu wako ni kuwasaidia wengine kujifunza na kuishi injili kama inavyofunzwa kutoka katika mkutano mkuu wa Kanisa wa majuzi kabisa. Rejelea hutoba hizi, ukitafuta kanuni na mafundisho ambayo yanafaa kwa mahitaji ya washiriki wa darasa. Pia tafuta hadithi, rejeleo za maandiko, na semi kutoka kwa hotuba hizi ambazo zitakusaidia kufunza kweli hizi. Tengeneza mpangilio wa jinsi ya kufunza hizi kanuni na mafundisho. Mpangilio unafaa kujumuisha maswali ambayo yatasaidia washiriki wa darasa: Tafuta kanuni na mafundisho kutoka kwa hotuba hizi. Fikiria kuhusu maana yake. Shiriki uelewa, mawazo, uzoefu, na shuhuda. Kutumia hizi kanuni na mafundisho katika maisha yao. MASOMO YA MWEZI YANAFUNZWA Novemba 2011 Aprili 2012 Mei 2012 Oktoba 2012 VIFAA VYA SOMO LA JUMAPILI YA NNE Hotuba zilizochapwa katika November 2011 Liahona * Hotuba zilizochaowa katika Mei 2012 Liahona * * Hizi hotuba zinapatikana katika lugha nyingi katika conference.lds.org. 2011 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/10. Tafsiri iliidhinishwa: 6/10. Tafsiri ya First Presidency Message, November 2011. Swahili. 09771 743 4

UJUMBE WA MAFUNDISHO, NOVEMBA 2011 Musa mmoja wa manabii wakuu ambao dunia imewahi kufahamu, alilewa na bintiye Farao na akatumia miaka 40 ya kwanza ya maisha yake katika kumbi za enzi za Misri. Alielewa kwa njia ya kibinafsi utukufu na ufahari wa ufalme huo wa kale. Miaka baadaye, juu ya mlima wa mbali, mbali na fahari na uzuri wa Misri yenye nguvu, Musa alisimama katika uwepo wa Mungu na kunena naye uso kwa uso kama vile mtu hunena na rafiki yake. 1 Katika mkondo wa matembeleo haya, Mungu alimwonyesha Musa kazi ya mikono yake, akimpa tazamo la mara moja la kazi na utukufu wake. Wakati maono yalipoisha, Musa alianguka chini mchangani kwa muda wa masaa mengi. Wakati nguvu zake ziliporejea, aligundua jambo fulani, ambalo kwa miaka yake yote katika kitala cha Farao, lilikuwa kamwe halijamtokea hapo mbeleni. Ninajua, alisema, kwamba mwanadamu si kitu 2 Na Rais Dieter F. Uchtdorf Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza Wewe ni wa maana Kwake Bwana hutumia mizani tofauti sana na ya ulimwengu kupima thamani ya nafsi. Sisi tu Wapungufu kuliko Tunavyodhani Tunanvyojifunza zaidi kuhusu Ulimwengu, ndivyo zaidi tunavyoelewa, ingawa kwa sehemu ndogo kile ambacho Musa alikijua. Ulimwengu ni mkubwa sana, usivyofahamika, na mtukufu kwamba haieleweki katika akili ya binadamu. Na dunia zisizo na idadi nimeziumba, Mungu akamwambia Musa. 3 Maajabu ya anga ya usiku ni ushuhuda mzuri wa ukweli huu. Kuna vitu vichache vinavyonijaza na staha isiyo kifani kama kusafiri kwa ndege kwenye weusi wa usiku kuvuka bahari na bara na kuona nje ya dirisha la chumba changu cha rubani kutazama utukufu usiokoma wa mamilioni ya nyota. Wanasayansi wa sayari wamejaribu kuhesabu idadi ya nyota katika Ulimwengu. Kikundi kimoja cha wanasayansi wamekadiria kuwa idadi ya nyota katika upeo wa darubini zetu kuwa mara 10 zaidi ya chembe zote za mchanga zinazopatikana katika pwani na majangwa yote ulimwenguni. 4 Hitimisho hili lina mfanano wa kuvutia na matamko ya nabii wa kale Henoko: Na kama ingeliwezekana mwanadamu aweze kuhesabu vipande vya dunia, ndiyo, mamilioni ya dunia kama hii, isingelikuwa mwanzo wa idadi ya viumbe vyako. 5 Kulingana na upana wa viumbe vya Mungu, si ajabu mfalme mkuu Binyamini aliwashauri watu wake na kila wakati mshikilie ukumbusho, wa ukuu wa Mungu, na unyonge wenu. 6 Sisi tu Wakuu kuliko Tunavyodhani Lakini hata ingawa binadamu ni mnyonge, ninajawa na staha na kustajabu kufikiri kuwa thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu. 7 Na huku tunapoweza kutazama upana mkubwa wa Ulimwengu na kusema, Mtu ni nini kulingana na utukufu wa viumbe? Mungu mwenyewe alisema sisi ndio sababu yake kuumba Ulimwengu! Kazi Yake na utukufu dhamira ya ulimwengu huu tukufu ni kuokoa na kutukuza mwanadamu. 8 Kwa maneno mengine, upana mkubwa wa milele, utukufu na siri za anga isiyo na mipaka na nyakati zote zimejengwa kwa faida ya watu wa kawaida kama mimi na wewe. Baba yetu wa Mbinguni aliumba Ulimwengu ili tuweze kufikia uwezo wetu usiodhihirika kama wana na binti zake. Huu ni ukweli kinza kwa mtu: akilinganishwa na Mungu, mtu si kitu, na hali sisi ni kila kitu kwa Mungu. Katika muktadha wa uumbaji usio na mipaka tunaweza kuonekana kuwa si kitu, tuna spaki ya moto wa milele ukiwaka ndani ya vifua vyetu. Tuna ahadi isiyoeleweka ya kuinuliwa dunia bila mwisho katika mfiko 1

wetu. Na ni ari kubwa ya Mungu kutusaidia kuifikia. Upumbavu wa Kiburi Mdanganyifu mkuu anajua kuwa mojawapo wa vifaa vyake vyenye nguvu katika kuwapotosha watoto wa Mungu ni kuvutia upeo wa kweli kinza ya mtu. Kwa wengine anavutia mwelekeo wao wa kiburi, akiwafurisha na kuwatia moyo kuamini katika utungaji wao wa taswira ya umuhimu wao wa kibinafsi na kutoshindika kwao. Anawaambia wamepita yale ya kawaida na hiyo kwa sababu ya uwezo, haki ya kuzaliwa, au hadhi, wametengwa kutokana na kipimo cha kawaida cha wote walio karibu nao. Anawaongoza kuamua kuwa kwa sababu hiyo hawako chini ya sheria yoyote na wasisumbuliwe na shida za mtu mwingine yeyote. Abraham Lincoln anasemekana kuwa alipenda shairi ambalo lililosema: Kwa nini roho ya mtu huwa na kiburi? Kama kimondo kinachoruka, kama wingu linalopaa kwa upesi, Mwasho wa radi, kuvunjika kwa mawimbi, Mtu huaga kutoka kwa uhai hadi mapumziko yake katika kaburi. 9 Wanafunzi wa Yesu Kristo wanaelewa kuwa kulinganishwa na milele, kuwepo kwetu katika tufe hili la muda ni muda mdogo sana katika uwanda na wakati. 10 Wanafahamu kuwa thamani ya kweli ya mtu haihusiani na yale ambayo dunia inathamini. Wanajua kuwa ungeweza kurundika fedha zilizokusanywa za dunia nzima na hazingeweza kununua mkate katika uchumi wa mbinguni. Wale watakao kurithi ufalme wa Mungu 11 ni kwa wale wanaokuwa kama mtoto, mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, mwenye upendo tele. 12 Kila ajikwezaye atadhililishwa; naye ajidhililishaye atakwezwa. 13 Wanafunzi kama hawa pia uelewa kuwa mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu. 14 Sisi Hatujasahaulika Njia nyingine ambayo Shetani anatumia kudanganya ni kupitia kwa kuvunjika moyo. Anajaribu kuelekeza kuona kwetu katika uhafifu wetu hadi tunapoanza kushuku kuwa tuna thamani yoyote. Anatuambia kuwa sisi ni wadogo kwa yeyote kututambua, kwamba tumesahaulika hasa na Mungu. Hebu nishiriki nanyi uzoefu wa kibinafsi unaoweza kuwa wa usaidizi kwa wale wanaohisi kuwa hafifu, wamesahaulika au wapweke. Miaka mingi iliyopita, nilihudhuria mafunzo ya urubani katika Jeshi la Angani la Marekani. Nilikuwa mbali na nyumbani, kijana askari wa Ujerumani Magharibi, aliyezaliwa Czechoslovakia, ambaye alikuwa amekulia Ujerumani Mashariki na kuzungumza Kiingereza kwa ugumu mno. Nakumbuka kwa njia dhahiri safari yangu kwenda katika kituo cha mafunzo cha jeshi huko Texas. Nilikuwa katika ndege, nikiwa nimeketi karibu na abiria aliyekuwa na athari nzito ya lafudhi ya Kusini. Ningeelea kwa shida sana neno alilosema. Nilishangaa kama nilikuwa nimefundishwa lugha kimakosa wakati huu wote. Nilihofu kwa fikira kuwa ningeshindania nafasi za juu katika mafunzo ya urubani dhidi ya wanafunzi ambao walikuwa wazungumzaji wa asili wa Kiingereza. Nilipowasili katika kituo cha wanahewa katika mji mdogo wa Big Spring, Texas, nilitafuta na kupata tawi la Watakatifu wa Siku za Mwisho, lililokuwa na washiriki wachache wa ajabu waliokuwa wakikutana katika vyumba vilivyokodiwa katika kituo cha wanahewa. Washiriki walikuwa katika mpango wa kujenga jumba dogo la mikutano ambalo lingetumika kama mahali pa kudumu pa Kanisa. Siku hizo, washiriki walifanya ujenzi wa majengo mapya. Siku baada ya siku nilihudhuria mafunzo yangu ya urubani nilisoma kwa bidii kadiri nilivyoweza na kutumia wakati wangu wa akiba nikifanya kazi katika jumba jipya la mikutano. Pale nilijifunza kwamba mbili-mara-nne si mtindo wa densi bali ni kipande cha mbao. Nilijifunza pia maarifa ya kuishi ya kukwepa gumba wakati wa kipigalia msumari. Nilitumia wakati mwingi kufanya kazi katika jumba la mikutano hadi Rais wa tawi ambaye pia alikuwa mmoja wa wakufunzi wetu wa urubani akadhihirisha wasiwasi kuwa huenda ingekuwa bora kuwa ningetumia wakati zaidi nikisoma. Marafiki zangu na wanafunzi wenzangu pia walijihusisha na shughuli za wakati wa akiba ingawa nafikiri ni bora kusema kuwa baadhi ya shughuli hizo hazingefungamana na kijitabu cha hivi leo cha For the Strength of Youth. Kwa upande wangu, nilifurahia kuwa sehemu ya tawi la magharibi Texas, kutumia maarifa yangu mapya ya useremala na kuboresha Kiingereza nilipokuwa nikitimiza miito yangu kufundisha katika jamii ya wazee na katika shule ya Jumapili. Wakati huo, Big Spring, licha ya jina lake, palikuwa pahali padogo, pasipoonekana wala kujulikana. Na Mara nyingi nilihisi hivyo kuhusu mimi mwenyewe nisiyeonekana asiyejulikana na mpweke kabisa Hata hivyo, sikushangaa kama Bwana alikuwa amenisahau au kama angeweza kunipata huko. Nilijuwa haikuwa jambo kwa Baba wa Mbinguni popote nilipokuwa, mahali niliorodheka na wengine katika mafunzo yangu urubani au ni nini mwito wangu Kanisani. Kilichokuwa muhimu kwake ni kuwa nilikuwa nikifanya bidii jinsi nilivyoweza, na kwamba nilikuwa niko radhi kuwasaidia wale waliokuwa karibu nami. Nilijua kuwa ningetenda vyema 2

ninavyoweza, yote yangekuwa mema. Na yote yalikuwa mema. 15 Wa Kwanza Watakuwa wa Mwisho Kwa Bwana haijalishi hata kidogo ikiwa tutatumia siku zetu tukifanya kazi kwenye kumbi za mawe au katika vibanda vya wanyama. Anafahamu tulipo, haijalishi jinsi ya hali zetu za unyonge. Atatumia kwa njia yake na kwa makusudi yake matakatifu wale ambao mioyo yao inaelekea kwake. Mungu anafahamu kuwa baadhi ya nafsi kuu waliowahi kuishi ni wale ambao hawatawahi kuonekana katika kumbukumbu za historia. Ni wale waliobarikiwa,wanyenyekevu wanaofuata mfano wa Mwokozi na kutumia siku za maisha yao wakitenda mema. 16 Wachumba wa mfano kama huu, wazazi wa rafiki yangu, walinionyesha kwa mfano kanuni hii Mume alifanya kazi katika kiwanda cha chuma huko Utah. Wakati wa chakula cha mchana angetoa maandiko yake au jarida la Kanisa na kusoma. Wafanyi kazi wengine walipoona haya walimkejeli na kupinga imani yake. Walipofanya hivyo, aliwazungumzia kwa hisani na kwa ujasiri. Hakukubali ukosefu wao wa heshima kumkasirisha wala kumvuruga. Miaka baadaye, mmoja wa wale waliomkejeli aliyesikika zaidi akawa mgonjwa sana. Kabla ya kufa aliuliza kuwa huyu mtu mnyenyekevu azungumze katika mazishi yake ambavyo alifanya. Huyu mshiriki mwaminifu wa Kanisa kamwe hakuwa na mengi kwa staha ya kijamii au mali, lakini ushawishi wake ulienea ndani kwa wale wote waliomjua. Alikufa katika ajali ya kiwandani wakati alipokuwa amesimama kumsaidia mfanyakazi mwingine aliyekuwa amekwama kwenye theluji. Katika muda wa mwaka mmoja, mjane wake alifanyiwa upasuaji wa ubongo ambao umemfanya kukosa kuweza kutembea Lakini watu wanapenda kuja kukaa naye kwa sababu anasikiliza. Anakumbuka. Anajali. Kwa kuwa hawezi kuandika, anakariri nambari za simu za watoto wake na za wajukuu wake Kwa upendo anakumbuka siku za kuzaliwa kwao na siku za maadhimisho. Wale wanaomtembelea wanatoka huko wakihisi vyema zaidi juu ya maisha na kujihusu wenyewe. Wanahisi upendo wake. Wanajua kuwa anajali. Kamwe halalamiki lakini anatumia siku zake akibariki maisha ya wengine. Mmoja wa marafiki zake alisema mwanamke huyu alikuwa mmoja wa watu wachache aliowafahamu ambao kwa kweli walionyesha kwa mfano wa upendo na maisha ya Yesu Kristo. Wachumba hawa wangekuwa wa kwanza kusema hawakuwa na umuhimu sana hapa duniani. Lakini Bwana hutumia mizani tofauti sana na ile ya dunia ili kupima thamani ya nafsi. Anafahamu wachumba hawa waaminifu; Yeye anawapenda. Matendo yao ni ushuhuda hai wa imani yao yenye nguvu katika Yeye. Wewe ni wa Maana Kwake Akina ndugu na dada zangu wapendwa, inaweza kuwa kweli kwamba mtu si kitu kulingana na ukubwa wa Ulimwengu. Wakati mwingine, tunaweza kuhisi kutokuwa na umuhimu, kutoonekana, wapweke au kusahaulika. Lakini daima kumbuka wewe ni wa maana Kwake! Ikiwa utawahi kushuku kuwa wewe ni wa maana kwake, fikiria kanuni hizi nne za kiungu: Kwanza, Mungu anawapenda wanyenyekevu na wapole kwani wao ndio walio wakuu katika ufalme wa Mbinguni. 17 Pili, Bwana amekabidhi utimilifu wa injili [Yake] uweze kutangazwa na watu walio dhaifu na wa kawaida hata mwisho wa dunia. 18 Amechagua mambo dhaifu ya dunia [yata] kuja kuyavunja yale yaliyo makubwa na yenye nguvu. 19 kuyatia aibu mambo yaliyo makuu. 20 Tatu, haijalishi unakoishi, haijalishi unyonge wako, uduni wa kazi yako, uhaba wa vipawa vyako, sura yako kuwa ya kawaida, au jinsi mwito wako Kanisani ulivyooneka kuwa mdogo, wewe si wa kutoonekana kwa Baba wa Mbinguni. Anakupenda. Anafahamu moyo wako mnyenyekevu na matendo yako ya upendo na hisani. Pamoja yanaunda ushuhuda wa kudumu wa uaminifu wako na imani. Nne, na la mwisho, tafadhali elewa kuwa kile unachoona na kupata uzoefu sasa si yote ambayo utakuwa milele. Hautahisi upweke, huzuni, uchungu na kuvunjika moyo milele. Tuna ahadi ya uaminifu ya Mungu kuwa yeye hatasahau wala kuwaacha wale wanaoelekeza mioyo yao Kwake. 21 Kuwa na matumaini na imani katika ahadi hiyo. Jifunze kumpenda Baba yako wa Mbinguni na kuwa mwanafunzi wake kwa maneno na matendo. Muwe na hakika kuwa ukivumilia, kumwamini na kubaki mwaminifu katika kuweka amri zake, siku moja utapata uzoefu wako binafsi wa ahadi zilizofunuliwa kwa Mtume Paulo: Jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 22 Akina ndugu na dada, Kiumbe aliye na nguvu zaidi katika Ulimwengu ni Baba wa roho yako. Anakufahamu. Anakupenda kwa upendo mkamilifu. Mungu anakuona, si kama mtu wa maisha ya muda katika sayari ndogo anayeishi kwa muda mfupi Yeye anakuona kama mtoto Wake. Anakuona kama mtu unayeweza kuwa kile ulichopangiwa kuwa. Anataka ujue kuwa wewe ni wa maana Kwake. Acha daima tuamini, tukubali na tulinganishe maisha yetu ili tuelewe thamani yetu ya milele na uwezo wetu. Na tuwe wa kustahili baraka za thamani ambazo Baba yetu wa Mbinguni ametuwekea ni ombi langu katika jina la Mwanawe, hata Yesu Kristo. Amina. 3

MUHTASARI 1. Ona Musa 1:2. 2. Musa 1:10. 3. Musa 1:33. 4. Ona Andrew Craig, Astronomers Count the Stars, BBC News, July 22, 2003, http://news. bbc.co.uk/2/hi/science/nature/3085885.stm. 5. Musa 7:30. 6. Mosia 4:11. 7. Mafundisho na Maagano 18:10. 8. Ona Musa 1:38 39. 9. William Knox, Mortality, katika James Dalton Morrison, ed., Masterpieces of Religious Verse (1948), 397. 10. Mafundisho na Maagano 121:7. 11. 3 Nefi 11:38. 12. Mosia 3:19. 13. Luka 18:14; ona pia mistari ya 9 13. 14. Mosia 2:17. 15. Dieter F. Uchtdorf alihitimu nambari moja katika darasa lake. 16. Oan Matendo ya Mitune 10:38. 17. Mathayo 18:4; ona pia mistari ya 1 3. 18. Mafundisho na Maagano 1:23. 19. Mafundisho na Maagano 1:19. 20. 1 Wakorintho 1:27. 21. Ona Waebrania 13:5. 22. 1 Wakorintho 2:9. 2011 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/10. Tafsiri iliidhinishwa: 6/10. Tafsri ya Visiting Teaching Message, November 2011. Swahili. 09771 743 4