MTI KWA MATUMIZI YA KILA AINA HDRA

Similar documents
KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST HABARI MOTO MOTO

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

PYRINEX. 1 Liter INSECTICIDE

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London. Maelezo

Uzalishaji wa mboga na matunda ni muhimu kwa afya na kipato

Mfumo na maelezo ya kina ya mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) Juni 2017

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

pages/mkulima-mbunifu/

KUZALISHA MBEGU YA MAHARAGE KIJITABU CHA KWANZA

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

4 WADUDU,MAGONJWA NA MAGUGU

MBINU ZA IPM KWENYE KILIMO CHA KAHAWA

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Njia bora za ukusanyaji na upimaji maziwa

Njia Bora za Ukusanyaji na Upimaji Maziwa

Wadudu na magonjwa ya mazao

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Lesson 11 Weather and Seasons Hewa Majira

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

Human Rights Are Universal And Yet...

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Matumizi ya Matunda na Mboga baada ya kuvuna

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Utunzaji, Uhifadhi na Usafirishaji Bora wa Maziwa

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Usindikaji bora wa maziwa

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Mwongozo huu wa ufugaji kuku wa Asilia umezinduliwa rasmi leo tarehe 1 Agosti 2009 wakati wa sikukuu ya Wakulima Tanzania mjini Mbeya

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

Upande 1.0 Bajeti yako

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

MTIHANI WA MWIGO WA WILAYA YA NANDI KASKAZINI 2013

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Issue No.1 Morogoro school of journalism May Salma :Wanachuo lipeni ada kwa wakati

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

Alama za maelezo. mastakimu. dimbwi. kidimbwi. mto. kijito. ndani mchangani / chini ya ardhi. mchana / usiku. mchana. usiku

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi.

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Muongozo wa utatuzi. Kwa wasimamizi wa malaria RDTs 06/11/16. MALARIA Rapid Diagnostic Test

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

GENIUS CUP FINAL STANDART SEVEN

K. M a r k s, F. E n g e l s

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Njia za upimaji wa mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) VYAKULA VINYWAJI VYA KAWAIDA

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Transcription:

MZUNZE MTI KWA MATUMIZI YA KILA AINA HDRA Kwa huduma za Kilimo - hai Moringa oleifera a multipurpose tree

Mzunze ni nini? Mzunze au Mrongo au Mronge ni mti uliotokea Kaskazini mwa India. Kwa sasa Mti huu unakuzwa pembe nyingi za dunia, na hasa sehemu za hari(tropics). Mzunze umetambulikana kote ulimwenguni kama Sahibu au mwandani wa Mama. Mti huu hukua kwa wepesi na haraka hadi kufikia meta 12 za urefu. Gome lake ni la rangi ya kijivu. Mti huu hupoteza majani mwezi wa Desemba hadi Januari. Majani mapya hutokeza mwezi wa pili hadi wa tatu. Maua ya mti huu ni aina ya rangi ya mtindi (manjano nyeupe) na hujitokeza baada ya miezi minane (8) na hasa katika mwezi wa Januari hadi Machi. Tunda la mzunze lina urefu wa sentimeta 30 hadi 50 Mbegu zake zina mafuta. Ukurasa 1

Ni vipi tunavyokuza Mzunze? Mvua na mwinuko wa ardhi Mzunze huhitaji kiasi cha mvua kisichopungua 250 na 3000 mm kila mwaka. Mmea huu huhimili ukame. Wakati wa kiangazi majani huweza kupotea. Hii haimaanisha kwamba mmea umekufa, kwani matawi hujitokeza punde majira ya mvua kuwadia. Mmea huu hukua vyema kwenye sehemu za urefu wa meta 600. Vilevile waweza kukuzwa katika sehemu zilizo na mwinuko wa meta 1000 kutoka usawa wa bahari. Kadiri ya joto Mzunze huweza kuhimili kiasi cha joto kuanzia nyuzi joto 25c hadi 40c. Halikadhalika unaweza kuhimili kiwango cha baridi kali. Udongo Mzunze huhitaji udongo wa kadiri, wenye tindikali kiasina usiotuamisha maji. Ukurasa 2

Matumizi ya Mzunze? Sehemu zote za mti zina matumizi ya kila aina. Mzunze una madini mengi na Vitamini kwa matumizi ya Binadamu na mifugo. Mzunze pia husafisha maji machafu na pia hutumiwa kama dawa. Katika kilimo cha mseto, majani huweza kutoa mboji. Kuna matumizi mengi ambayo yamejadiliwa katika kitabu hiki: Chakula cha Binadamu Chakula cha mifugo Kusafisha maji Madawa ya kiasili Mbolea Ua Katika kilimo cha mseto Dawa ya kuua wadudu Matumizi katika usafi wa nyumbani Kuni na mengine mengi.. Ukurasa 3

Chakula cha Binadamu Chakula chochote kitokanacho na Mzunze kina madini mengi ya hali ya juu. Majani yaweza kutafunwa au kupikwa. Tunda lenye mbegu changa, maua, mizizi na hata gome la mti, hutumiwa kama chakula. Majani hayana mafuta, lakini yana wingi wa madini na vitamini B. Chakula hiki hufaa sana hasa wakati wa ukame pale vyakula vingi vinapokosekana. Majani Majani ndio hutumiwa sana kuliko sehemu zinginezo za Mzunze. Ni vyema kuchuma sehemu zilizo changa kwani zingine ni ngumu. Wakati wa kupika tayarisha majani na wala sio sehemu za vijiti. Matawi haya yaweza kutumiwa kama figili (spinach). Njia rahisi ya kutayarisha ni kuchemsha vikombe viwili vya majani kwa dakika chache kwenye kikombe kimoja cha maji, pamoja na vitunguu, siagi, chumvi na viungo vinginevyo. Ukurasa 4

Majani makavu Majani makavu yaweza kutengenezwa unga ambao waweza kuongezwa kwenye mchuzi. Maua Maua yaweza kupikwa au kuchanganywa na vyakula vingine. Pia yaweza kuwekwa kwenye maji moto kwa dakika tano ili kufanyiza dawa. Maua pia huvutia nyuki. Matunda Matunda yaweza kutumiwa punde yanapotokeza hadi yafikiapo sentimeta30. Hupikwa kama maharagwe na harufu yake ni kama ya asparagus. Ni vyema kutahadhari kula kupita kiasi kwani baadhi yaweza kuwa na ladha kali yenye sumu. Matunda yaliyo komaa yaweza pia kuchemshwa hadi yakaiva. Tunda lililo komaa hupasuliwa na mbegu zake kuchemshwa ili kutumiwa katika mchuzi na vitoweo. Ukurasa 5

Mbegu Mbegu hujulikana kama choroko-mbaazi. Mbegu zaweza kutumiwa zingali changa hadi pale zinapo komaa. Mazoea yatapelekea kufahamu wakati bora wa kuchuna na kupika mbegu. Wakati wa kupika utadondoa kutoka kwenye ganda. Utahitajika kuosha mbegu ili kutoa ile ngozi iliyo chungu na majimaji. Au waweza kuchemsha kidogo halafu kumwaga maji hayo na kuchemsha ukitumia maji mengine. Mbegu zinapo komaa ganda lake huwa gumu na lenye ukali fulani. Mbegu kama hizi huweza kukunwa ili kutoa mafuta. Iwapo hakuna kifaa cha kukuna, mbegu zaweza kukaangwa kisha kupondwa na kuyeyushwa kwenye maji moto, kisha kuteka mafuta yanayoelea. Mbegu hujumuisha asilimia 35 ya mafuta yanayoweza kupikiwa. Mafuta haya pia yaweza kutumiwa kama yale ya taa na hayana moshi. Mizizi Mmea unapofikia urefu wa sentimeta 60, mizizi yaweza kung'olewa na kutumiwa kama horseradish. Ganda la mzizi sharti kutolewa kwani linayo sumu. Kisha mizizi hupondwa na kuongezwa chumvi na vinegar. Chakula hiki kisiliwe kwa wingi na ni vyema kukiweka kwenye friji (jokofu). Gundi Gundi hupatikana kwenye maganda na gome la mti. Gundi hutumiwa kukoleza chakula. Ukurasa 6

Chakula cha Mifugo Ng'ombe, kondoo, nguruwe, mbuzi na kuku hutumia maganda, matawi na mimea michanga kama chakula. Lishe mwafaka ni asilimia 70ya mzunze kwa nguruwe, asilimia kumi ya leucaena na asilimia 20 ya matawi mengineyo. Waweza kuzidisha asilimia hadi asilimia 100 bali usizidishe ile ya leucaena juu ya asilimia 30 Nyama ya nguruwe wanaotumia Mzunze ni nyororo. Iwapo mmea umenuiwa kuwalisha mifugo basi ukatwe chini ya meta nne. Iwapo ni matumizi mengine basi waweza kufikia meta sita kurahisisha kuvuna. Chakula cha mifugo huimarishwa kwa kuongezewa mzunze Ukurasa 7

Kusafisha maji Moringa oleifera mti kwa matumizi ya kila aina Makapi ya mbegu baada ya kuchuja mafuta au zile zilizo pondwa zaweza kutumiwa kufanya maji machafu kuwa masafi. Makapi haya hunasa chembechembe za uchafu na kuzama chini. Bakteria pia huuawa kwa asilimia 90-99. Mzunze hutumiwa badala ya kemikali zinazo tokana na aluminium sulphate ambazo. Hudhuru afya, mazingira na pia ni ghali. Lita Ishirini za maji zaweza kutayarishwa kama ifuatavyo: 1. Chagua mbegu zilizo bora na kuzitoa ganda la juu. 2. Ponda ponda hadi kufanya unga laini. Kuponda mbegu za mzunze ili kusafisha maji Ukurasa 8

3. Ongeza gramu 2 (vijiko viwili vidogo) kwenye kiasi cha maji kikombe kimoja yaliyo kwenye chupa, kisha tikisa kwa dakika tano. 4. Chuja maji hayo kwenye kitambaa kisafi na kumwaga kwenye ndoo iliyo na maji machafu unayonuia kusafisha. 5. Koroga kwa kasi kwa dakika mbili na kisha polepole kwa dakika 10 hadi 15 (usitumie chuma kukoroga). 6. Wacha ndoo kwa saa moja hadi pale maji yametulia na uchafu kuzama. 7. Chuja maji hayo kwa kitambaa safi. 8. Ni vyema kuchemsha kabla ya kunywa. Maji yatategemea viwango tofauti vya unga huu kulingana na mahali yalipochotwa, kwani sehemu zote hazilingani na pia uchafu waweza kuwa kwenye viwango tofauti. Mbegu na unga zaweza kuhifadhiwa, lakini mchanganyiko katika sehemu ya tatu hautahifadhiwa. Mchanganyiko huo hufanywa tu pale unapotaka kutayarisha maji. Asali na machujo ya miwa yaweza kusafishwa ili kuondoa chembe chembe kwa kutumia njia hii. Aina ya mzunze ujulikanao kama Moringa stenopetala unasafisha vyema kuliko Moringa oleifera. Ukurasa 9

Madawa ya kiasili Moringa oleifera mti kwa matumizi ya kila aina Duniani kote Mzunze umetumiwa kutibu aina mbalimbali ya magonjwa. Baadhi ya tiba zimejadiliwa hapa lakini sio hakikisho kwamba zote zitafanya kazi. Matawi Maua Matawi yanapo suguliwa kwenye paja au paji la uso huondoa maumivu ya kichwa. Maji yatokanayo kwa kufinya majani hupunguza kuvuja kwa damu kwenye kidonda. Maji ya majani hupunguza maumivu yanaponyunyizwa kwenye kidonda au mahali ulipoumwa na mdudu. Maji hayo pia huponya harara au upele wa ngozi. Maji yatokanayo kwa majani huponya vidonda vya tumbo na kuzuia kuhara. Bidhaa za mzunze husaidia watoto walio na shida ya utapiamlo. Maji yatokanayo kwa kuponda maua husaidia katika kuwezesha maziwa ya mama anaye nyonyesha kutiririka vilivyo. Halikadhalika maji hayo husaidia katika shida za mikojo kwani husaidia kuwezesha kukojoa. Matunda Maganda yatazuia na kutoa minyoo iwapo yataliwa yangali mabichi. Pia huponya magonjwa ya ini, wengu na viungo. Kwa sababu ya wingi wa proteni na nyuzinyuzi, maganda hutumiwa kutibu utapiamlo na kuhara. Ukurasa 10

Mbegu Hutumiwa kutibu ugonjwa wa viungo, ugonjwa wa zina, majipu na ugonjwa wa kiharusi. Mbegu zilizo kaangwa na mafuta yake husaidia kutoa mkojo. Mbegu hutumiwa kutibu au kuzuia mgonjwa wa kifafa kuanguka. Mizizi, gome la mti na gundi Mizizi na gome la mti yaweza kufanya hayo yote yaliyo tajwa hapo juu, ila tuu koleo la madini na kemikali ni la juu zaidi. Hivyo basi yapaswa kutumiwa kwa uangalifu zaidi. Mbolea Maganda na mabaki ya mbegu zilizo tumiwa kutoa mafuta hayawezi kuliwa, lakini yanayo madini na kemikali nyingi. Hatahivyo yanafanyiza mbolea nzuri. Uzio Iwapo utapanda kama uzio, basi miti ya mzunze huzuia upepo. Iwapo mimea itapandwa kwa karibu itahitaji miezi mitatu kufanya ua linaloweza kuwazuia mifugo kupita. Kilimo cha mseto Mzunze una mzizi mmoja mkuu na hivyo basi hautazuia mimea mingine kutumia madini na maji. Mmea huu huzalisha matawi mengi ili kuongeza nitrojeni katika udongo. Maumbile ya matawi hayawezi kusababisha kivuli kwa mimea mingine. Mmea huu huimarisha sehemu zisizotumika kwa kikamilifu. Ukurasa 11

Dawa ya kuua wadudu Moringa oleifera mti kwa matumizi ya kila aina Iwapo utalima na kufunika matawi ya mzunze chini ya udongo, basi utakuwa umezuia vijidudu wanao sababisha miche kuoza (Pythium debaryanum). Matumizi katika usafi wa nyumbani Matawi hutumiwa kusafisha vyombo na hata ukuta. Kuni na matumizi mengine Kuni za mzunze ni nyepesi na hutumiwa katika kupika. Walakini, sio nzuri katika ujenzi. Gome la mti huu laweza kutumiwa kama kamba au kutengeneza aina ya mikeka. Mmea huu pia hutumika kutengeneza karatasi. Mti huu hutoa pia aina ya nyuzi zinazo tumiwa katika viwanda vya nguo. Ukurasa 12

Jinsi ya kupanda Mzunze Kupanda Mbegu Mbegu zaweza kupandwa punde zinapo komaa. Usiweke mbegu kwa muda unao zidi miezi mitatu. Kabla ya kupanda utaloweka mbegu ndani ya maji kwa siku moja kisha panda kwa nafasi ya sentimeta 2 kutoka shina moja na jingine na kina cha sentimeta moja. Nyunyizia maji. Baada ya siku 15 miche itaota. Miche itapunguzwa ifikiapo sentimeta 30 ili kuwacha nafasi ya sentimeta 10. Hatimaye zing'olewe na kupanda kwengineko wakati zifikiapo urefu wa sentimeta 60-90. Tahadhari kwani huwa ni dhaifu. Kupanda Kipandikizi kilicho katwa Vipandikizi ( sm 45- m 1.5 na upana wa sm 10) vikatwe kutoka kwa mimea yenye afya wakati wa mvua. Toa sehemu zenye majani kisha kuacha vipandikizi mahali palipo na kivuli kwa siku tatu. Waweza kupanda moja kwa moja kwenye udongo au vifuko vya plastiki vilivyo na sehemu 3 za udongo na sehemu 2 za mchanga. Theluthi ya kipandikizi iwe kwenye udongo. (Iwapo pandikizi ni 1.5 sm, panda 50 sm chini.). Udongo uwe na unyevu lakini sio maji mengi (uliolowa chepechepe). Vipandikizi vilivyo kwenye plastiki huchukua muda mrefu kuota mizizi na hupandwa baada ya miezi 2 au 3. Idadi ya Mazao Katika kipindi cha miaka mitatu mti mmoja waweza kutoa matunda ya mbegu 300 hadi 400 kila mwaka. Mti ulio komaa waweza kutoa matunda ya mbegu 1000. Ili kuzuia mti kurefuka waweza kuchuna mara kwa mara, hii husaidia kutoa matawi mengi na kurahisisha wakati wa mavuno. Ukurasa 13

Marejeo Moringa oleifera mti kwa matumizi ya kila aina `Moringa oleifera' (Undated) Baraza la Kihindi kuhusu Utafiti wa Misitu na Elimu, (Indian council of Forestry Research and Education, Dehra Dun, India. 10pp) `The Miracle Tree. Moringa oleifera: Natural Nutrition for Tropics' (1999) LJ Fuglie. Church world service, Dakar Senegal. 63pp `Dried Moringa leaves' (2001) L Fuglie, Footsteps 46:14. `The Moringa tree: your multipurpose tree for the family' (1998) Uganda Environews 5 (2):7. `The Moringa Workshop' (1999) workshop 2-4 September 1999, Christian Village, Kumasi, Ghana. Inter care and GOAN. 45pp. `Trees and Shrubs of the Sahel' (1986) HJ Von Maydell. GTZ Eschborn, Germany. 525pp `The Moringa Tree' (2000) ML Price. ECHO Technical Note. ECHO, Florida, USA. 12pp. http://www.echonet.org/tropicalag/moringa3.htm. Ukurasa 14

Maelezo ya ziada kuhusu; Viunga vya miche, Mboji ya Kijani, Kuzuia kwekwe, Miti yenye manufaa kama vile Mwarobaini na Mzunze, Kilimo Hai, na jinsi ya kukabili Magonjwa na wadudu yanaweza kupatikana kutoka HDRA: The Organic Advisory Service HDRA International Development Programme Ryton Organic Gardens Coventry CV8 3LG UK Simu: +44 (0)24 7630 3517 Kipepesi: +44 (0)24 76623 9229 Barua-pepe: ove-enquiry@hdra.org.uk Mtandao: www.gardenorganic.org.uk/international_programme/ Madhumuni ya shirika la HDRA ni kufanya utafiti, kutoa na kueneza habari kuhusu Kilimo Hai, Ukulima na chakula katika Uingereza (UK) na Dunia nzima. Mwongo mmoja uliopita, shirika hili limekuwa likisaidia katika kubuni njia za kuboresha na kutafiti aina ya ukulima hasa Kilimo Hai katika nchi za hari (Tropics). Vilevile kutoa maelezo na majarida kuhusu Kilimo Hai na pia kutoa mbegu na maelezo ya upanzi. Maelezo haya yanaweza kunakiliwa bure kwa njia yoyote pasipo malipo. Tafsiri na: Patrick Bunyali Kamoyani, P.O Box 1, 50321-Magada via Maragoli, Kenya. pbkamoyani@excite.com Kimehaririwa na Leonard Mtama 2006 HDRA Publishing