USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

Size: px
Start display at page:

Download "USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI"

Transcription

1 USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI MWONGOZO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA WASTANI WANAOUZA BIDHAA NJE YA NCHI TOLEO LA PILI Geneva 2011

2 ii IKISIRI YA HUDUMA YA HABARI ZA BIASHARA ID= F EXP Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) Physikalisch-Technische Bundesanstalt (PTB) Usimamizi wa Ubora wa Mauzo ya Nje: Mwongozo kwa Wafanyabiashara Wadogo na wa Wastani Wanaouza katika Nchi za Nje. Toleo la pili. Geneva: ITC, xii, kurasa 270 Mwongozo huu unalenga kuwapa wafanyabiashara wadogo na wa wastani wanaouza nje ya nchi uelewa madhubuti kuhusu masuala ya ubora yanayoambatana na mfumo wa ubora. Unajumuisha maswali na majibu juu ya udhibiti wa ubora, mahitaji ya kifundi ( viwango, kanuni na masuala ya afya na usalama wa wanyama na mimea), mifumo ya usimamizi mkuu, ukadiriaji wa kukidhi mahitaji (upimaji, ukaguzi, uhakiki), mfumo wa vipimo, uthibitishaji, na mikataba ya shirika la biashara duniani kuhusiana na vikwazo vya biashara vya kiufundi na matumizi ya masuala ya afya na usalama wa wanyama na mimea; majibu kwa maswali yanaambatana na marejeleo ya bibliografia na kutoka kwenye hazina ya mtandao. Maneno ya msingi: Kudhibiti ubora, Usimamizi Mkuu wa Ubora, Viwango, Ukadiriaji wa kukidhi, Tathmini, Mahitaji (ulinganifu), Ukaguzi, Upimaji na mauzo katika nchi za nje, Mfumo wa vipimo (ugezi), Uhakiki, Ithibati (kibali), Uthibitishaji, Afya na usalama wa wanyama na mimea (SPS), Vikwazo vya Biashara vya Kiufundi(TBT). Kingereza, Kifaransa, Kihispania (matoleo tofauti) ITC, Palais des Nations, 1211 Geneva 10, Switzerland ( Uwasilishaji wa taarifa na maelezo yaliyotolewa katika chapisho hili, kwa namna yoyote yasichukuliwe kama ndio msimamo wa Kituo cha Biashara Duniani na Physikalisch- Technische Bundesanstalt kuhusiana na hali ya kisheria ya nchi, taifa, jiji au eneo la mamlaka yake au kuhusiana na upungufu uliopo katika mipaka yake. Kutajwa kwa mashirika/kampuni, bidhaa, nembo za bidhaa haina maana kuwa vimethibitishwa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa au PIB. Usanifu wa jalada na vielelezo: Kituo cha Biashara cha Kimataifa, Kristina Golubic 2011 Kitua cha Biashara cha Kimataifa (International Trade Centre) 2011 Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuchapisha, kurudufu au kunakili kwa njia yoyote ile, iwe ya kielektroniki, tepu za sumaku, kuhifadhiwa kwa njia ya kurejelewa au kutumwa bila kupata ruhusa iliyoandikwa kutoka katika Kituo cha Biashara Duniani. P247.E/DBIS/EC/11-XI ISBN United Nations Sales No. E.12.III.T.2

3 Dibaji Ubora ni sharti muhimu la kuyafikia masoko na katika kuongeza ushindani wa wanaouza bidhaa nje ya nchi. Hata hivyo, ni kazi ngumu au changamoto kwa wanaouza nje kukidhi vigezo vya kiufundi, ukizingatia wingi wa viwango vilivyopo. Nchi nyingi zimeweka viwango vingi kwa nia ya kulinda usalama na afya za wananchi wao, na kukidhi mahitaji ya wanunuzi kufuatana na mahitaji yao. Hali hii imethibitishwa na tafiti zilizofanywa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) ambazo zimeonyesha kwamba matatizo mengi ya wanaouza bidhaa nje yanatokana na mashauri yasiyohusu kodi kwa sababu ya mahitaji ya kukidhi taratibu zilizopo, kanuni/sheria nyingi, na mashauri yanayohusu afya za mimea na wanyama(sps). Wafanyabiashara ambao wana nia ya kuuza nje sharti wajikumbushe na kuambatana na mabadiliko ya mahitaji ya kiufundi yaliyopo; yale ya lazima na ambayo ni ya hiari katika masoko lengwa. Baada ya kupata taarifa hizo, hawana budi kuzitayarisha bidhaa ili ziweze kukidhi mahitaji yaliyopo. Inawezekana wakawa hawafahamu au hawana uwezo wa kuwapata wataalam wanaoweza kuwasaidia kutokana na kuwapo kwa maendeleo duni ya huduma za namna hiyo katika nchi zao. Kutokana na hali hiyo, hulazimika kutumia huduma za wataalam wa kimataifa ambao ni ghali, matokeo yanakuwa ni kuongeza kwa gharama zao. ITC kwa kutambua hali hii na Physikalisch-Technische Bundesanstalt, PTB (Taasisi ya Kitaifa ya Vipimo ya Ujerumani) iliona umuhimu wa kurejea mwongozo wa mameneja wa biashara ndogo na za wastani (SMEs) katika nchi zinazoendelea na zile zinazoinukia zinazojishughulisha na usimamizi uuzaji bidhaa bora katika nchi za nje. Mwongozo wa kwanza ulioandaliwa mwaka 2001, ulitokana na utafiti uliofanya kufahamu maswali muhimu 100 ambayo wanaouza nje hupenda kujua kuhusu usimamizi wa ubora. Mwongozo huu ulioboreshwa umezingatia mabadiliko yaliyotokea katika biashara duniani katika miaka kumi iliyopita, bila kuathiri uzoefu na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na mwongozo wa zamani. Mwongozo huu mpya ambao uko katika aina 15 na lugha 8 umeandaliwa kukidhi mahitaji ya nchi 18; kutokana na utafiti uliofanywa kufahamu kuhusu uhalali wa maswali yaliyokuwemo katika mwongozo wa awali pamoja na mapya. Kitabu hiki kinatoa majibu kwa maswali yanayohusu ubora, mahitaji ya kiufundi(viwango, kanuni,vigezo vya afya ya wanyama na mimea), mifumo ya usimamizi, ukadiriaji wa kukubaliana na mahitaji (kupima, ukaguzi, uhakiki), vipimo, kuthibitishwa, na mikataba ya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kuhusu Vikwazo vya Biashara vya Kiufundi na matumizi ya vigezo vya afya ya wanyama na mimea (SPS). Tunaamini, kitabu hiki ambacho ni kati ya msururu wa maswali na majibu elekezi ya Siri za Biashara yaliyoandaliwa na ITC, kitakuwa chenye faida kwa tasnia ndogo na za kati katika nia ya kuuza katika nchi za nje. Patricia Francis Executive Director International Trade Centre Ernst Otto Göbel President Physikalisch-Technische Bundesanstalt

4

5 Shukrani Chapisho hili lililoboreshwa limewezekana kutokana na utaalamu, uzoefu na ujuzi wa watu wengi na taasisi; ambao hatuna budi kuwashukuru. Majina yao yameorozeshwa hapa chini. Shukrani Toleo hili Jipya limetokana na ujuzi, tajriba na uelewa wa watu an Mashirika mengi. Wameorodheshwa hapa chini na shukrani. Washiriki: Physikalisch-Technische Bundesanstalt (PTB), Taasisi ya kitaifa ya vipimo ya Ujerumani walishirikiana na Kituo cha Biashara cha Kimataifa(ITC) kutoa chapisho hili la pili lililoboreshwa kutokana na lile la kwanza lililotolewa na ITC mwaka Ushiriki wa PTB ulidhaminiwa na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani kupitia Wizara yake ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ). Uboreshaji wa Kiufundi Kitabu hiki kilitengenezwa na timu ya wataalamu wa kiufundi wakiongozwa na Shyam Kumar Gujadhur, Mshauri Mwandamizi wa Viwango na Usimamizi wa Ubora, akishirikiana kwa karibu na Ludovica Ghizzoni, Mshauri wa Usimamizi wa Ubora kwa Mauzo ya Nje, Hema Menon, Mkufunzi wa Masuala ya Biashara, wote wa ITC; Uwe Miesner, Mratibu wa Mradi, Ushirikiano wa Kiufundi wa PTB, pamoja na wataalam wafuatao: Subhash Chander Arora, Digby Gascoine, John Gilmour, Martin Kellermann na Eberhard Seiler. Pia, tunashukuru ushirikiano wa Stefan Wallerath, Martin Stavenhagen na Martin Kaiser wa PTB. Kurejelewa Masuala ya kiufundi ya chapisho yalirelejewa na watu mbalimbali kutoka DCMAS, STDF, na Ukatibu wa Kamati za WTO zinazoshughulikia TBT na SPS, pamoja na Navin Dedhia kwa uwezo wake. Michango ITC wanatoa shukrani za dhati kwa watu mbalimbali ambao walishirikiana katika kutoa maoni yao kwenye utafiti uliofanywa ili kuchangia rasimu ya chapisho. Watu binafsi walikubali na kujitolea kushiriki kutoka taasisi mbalimbali zinazoshughulikia biashara, pamoja na mashirika ya kitaifa ya viwango, pamoja na wataalam binafsi. Kadhalika Shirin Abrar, Mkutubi Mshiriki wa ITC, alichangia kuhusu vyanzo vya habari wakati wa utafiti. Flavia Alves na Eu Joon Hur, ambao walikuwa wako kwenye mazoezi ya nyanjani ITC, walichangia katika kuwahoji SMEs na kuainisha vyanzo vya taarifa za utafiti. Natalie Domeisen, meneja wa machapisho wa ITC aliratibu uchapishaji na uvumishaji wa chapisho. Evelyn Jereda alitoa usaidizi wa kiutawa hapo ITC. Uhariri na Mpangilio Chapisho lilihaririwa na kusahihishwa na Leni Sutcliffe. Isabel Droste na Carmelita Endaya alihariri vyanzo katika kitabu chote. Mpangilio wake ulifanywa na Carmelita Endaya. Kristina Golubic ndiye aliyesanifu jalada.

6

7 Yaliyomo Dibaji Shukrani Angalizo iv v xii TANBIHI 1 UTANGULIZI 3 KUELEWA UBORA 7 1. Ubora ni nini? 9 2. Je, bidhaa au huduma bora hugharimu zaidi na kuna faida gani kutengeneza bidhaa bora au kutoa huduma bora? Usimamizi wa ubora ni nini na sehemu zake nne ni zipi? Je, shughuli za mfumo wa kudhibiti ubora zinahusianaje na usimamizi wa ubora? Nianze na mfumo wa kudhibiti ubora kabla ya kuweka mfumo wa usimamizi wa ubora? Ni njia ipi ya usimamizi mkuu wa ubora itakayosimamia mafanikio endelevu ya shirika/kampuni? Tuzo za kitaifa za ubora zikoje? Zina umuhimu wowote kwa SMEs? Nini dhana ya majukumu matatu katika usimamizi wa ubora? Ni zipi nyenzo saba za kudhibiti ubora na zinasaidiaje kutatua matatizo yanayohusu ubora? Six Sigma ni kitu gani? S za Kijapani ni kitu gani na faida zake ni nini? Nitawahamasishaje wasaidizi wangu kufanikisha ubora? Nifanye nini ili niweze kuwa sambamba na maendeleo yanayohusu ubora? 39 MAHITAJI YA KIUFUNDI Kiwango ni nini? Viwango binafsi ni vipi na vina mchango gani katika biashara? Viwango vipi vinahitajika katika kuuza chakula na mazao ya kilimo nje ya nchi? Viwango vipi vinatakiwa kuuza bidhaa za nguo nje? Viwango gani vinahitajika na baadhi ya wanunuzi ili kushughulikia matatizo ya kijamii, mazingira na kimaadili? Kanuni za kiufundi ni nini? Sheria za afya ya wanyama na mimea zikoje? Kuna uhusiano gani kati ya viwango, kanuni za kiufundi, na sheria ya SPS? Je, viwango kanuni za kiufundi na sheria ya SPS ni vikwazo vya biashara na jinsi gani vinaweza kuepukika? Kuna tofauti gani kati ya mahitaji ya lazima na mahitaji ya kibiashara ya wanunuzi? Nitapata wapi taarifa kuhusu mahitaji ya kiufundi kwa mahuruji? Nawezaje kufuatia mabadiliko katika kanuni za kifundi zinye umuhimu kwangu? 71

8 viii 25. Je, naweza kushawishi uandaaji wa viwango, kanuni za kiufundi na sheria ya SPS? Kanuni za RoHS ni zipi na zinaathiri vipi biashara ya nje? Kanuni za REACH ni zipi na zinaathiri vipi biashara ya kupeleka bidhaa nje ya nchi? Mahitaji ya ufungashaji wa bidhaa zangu ni yapi? 81 MIFUMO YA USIMAMIZI Nini maana ya familia ya viwango vya ISO 9000 na kwa kiasi gani viwango hivyo hutumika? Je vinasaidia biashara ya nje? Ni yapi matoleo rasmi ya kisekta ya ISO 9000? Kuna gharama na faida gani za kupata uthibitisho wa ISO 9001? Nitawezaje kuanzisha mfumo wa usimamizi bora wa ISO 9001? Nini maana ya malengo bora na yanalisaidiaje shirika kufikia ahadi ilizozitoa katika sera yake ya ubora? Rasilimali gani zinahitajika kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa ISO 9001? Kuna fikra potovu na changamoto gani katika utekelezaji wa ISO 9001 na SMEs? Nitahakikishaje kuwa malighafi yangu, vifaa nilivyonunua na pembejeo kutoka kwa wagavi wa nje ni salama kwa matumizi? Tutatangazaje mafanikio yetu katika usimamizi wa ubora? ISO ni kitu gani? Je, inatoka kote kwenye uzalishaji na sekta za huduma? Je, kutekeleza ISO kutalifanya shirika lidhihirishe ulinganifu wake na mahitaji ya sheria za mazingira? ISO inawasaidiaje SMEs kuongeza kukubalika kwa bidhaa au huduma zao za kupeleka nchi za nje? Kuna gharama na faida gani za kutekeleza ISO 14001? Nini maana ya mfumo wa kuchanganua majanga na hatua muhimu za udhibiti (Hazard Analysis and Critical Control Points (HACCP) na kwa nini ni muhimu kwa SMEs katika sekta ya chakula? HACCP inatekelezwaje? Kuna tofauti gani kati ya HACCP na ISO 22000? Hatua za kutekeleza ISO zikoje? Je,uhakiki wa HACCP/ISO utafanya shirika langu lidhihirishe kuwa linaulinganifu na sheria za nchi za usalama wa chakula? Kuna gharama na faida ngani za kupata uhakiki wa ISO 22000? 132 MIFUMO YA USIMAMIZI Kuna mahitaji gani kufikia ulinganifu na SA 8000 na faida zake kwa biasharanje ni zipi? OHSAS ina maana gani na inahusianaje na biashara ya nje? WRAP ni nini na inahusika na sekta zipi za viwanda? Viwango vingine vya mifumo ya usimamizi ni vipi? Vigezo vipi vya kuzingatia wakati wa kuchagua kiwango cha mfumo wa usimamizi kwa ajili ya kampuni yangu? Nini madhumuni ya ukaguzi wa ndani wa mifumo ya usimamizi na namna gani inafanyika? Je, naweza kujumuisha mifumo mbalimali ya usimamizi katika mfumo mmoja wenye uwiano na nitafanyaje? 153

9 ix TATHMINI YA ULINGANIFU Tathmini ya ulinganifu ni nini? Aina gani ya tathmini ulinganifu inahitajika ili kuthibisha kukubalika katika matakwa ya kiufundi/kitaalamu? Nini maana ya tamko la mgavi kuhusu ulinganifu (SDoC)? Alama ya CE ni nini na inasaidiaje kuuza nje ya nchi? Upimaji ni nini na una umuhimu gani katika masoko ya kimataifa? Nitahakikishaje kuwa taarifa ya upimaji wa bidhaa yangu inakubalika ng ambo? Kwa nini ustadi wa upimaji ni muhimu na wapi naweza kupata wapimaji mahiri? Je niweke maabara yangu ya vipimo au nitumie maabara za nje? Kwa nini niwe na vifaa vyangu vya kupimia na virekebishwe kila baada ya muda gani? Nini maana ya ufuatiliaji wa vifaa vya kupimia na jinsi ya kuonyesha vinavyofanya kazi? Kuna aina ngapi za ukaguzi? Kwa jinsi gani ukaguzi unahusika na aina nyingine za tathmini ya ulinganifu na ni nini nafasi yake katika biashara za kimataifa? Jinsi gani ninaweza kupata kibali cha kuuza bidhaa nje chini sheria ya SPS? Nini maana ya uhakiki (au uthibitisho) wa bidhaa na namna gani unapatikana? Ni nini maana ya uhakiki wa mfumo wa usimamizi? Ni vigezo gani vinavyotumika kuchagua mashirika ya uhakiki wa bidhaa? Vigezo gani vinatumika kuchagua mashirika ya kuhakiki mifumo ya usimamizi? Je, uhakiki niliopata utakubalika katika nchi nyingine? Je,, kuna mifumo ya kimataifa ya uhakiki (uthibitisho) wa bidhaa? Nitapata wapi taarifa kuhusu mashirika ya uhakiki yanavyofanya kazi kwenye nchi zingine? Shughuli gani hufanywa na mashirika ya uhakiki kabla na baada ya kutoa uhakiki wa mfumo wa usimamizi? Je, kupata uhakiki wa viwango binafsi kunahakikisha upatikanaji wa masoko? Jinsi gani nitapata uthibitisho kupitia viwango binafsi kama WRAP, Biashara ya haki (Fairtrade), SA 8000, GLOBALG. A.P, na kwa gharama gani? Nini maana ya Eco-labelling? 208 UGEZI Ugezi ni nini na unaumuhimu gani katika biashara ya kimataifa? Je, ugezi ni muhimu kwangu na nini natakiwa kuzingatia? Kipi kati ya vifaa vyangu kinatakiwa kurekebishwa na kwa nini? Wapi vifaa vyangu vinaweza kurekebishwa na kwa mihula ipi? Nani anaweza kushauri kuhusu matatizo ya vipimo? Nini maana ya ufuatiliaji vipimo na upimaji wenye mashaka/ usiokua na uhakika? Nitafanya nini kuhusu vipimo ikiwa ninahitaji kuthibitishwa kwa mujibu wa ISO/IEC 9001:2008? Kuna mahitaji gani ya vipimo kwa bidaa zilizofungashwa kabla ya kuuzwa? 228

10 x KIBALI (ITHIBATI) ITHIBATI Nini thamani ya ithibati (kibali)? Nini kinaweza kupewa Ithibati? Nini tofauti kati ya uhakiki na ithibati ( kibali)? Je, ithibati inapelekea moja kwa moja kutambuliwa kwa ripoti zangu za vipimo na uhakiki? Nini maana ya makubaliano ya pamoja kuhusu utambuzi? (Mutual Recognition Agreements -MRAs)? Yanawezeshaje biashara? 244 MIKATABA YA WTO JUU YA TBT NA SPS Ipi Mikataba ya WTO juu ya TBT na SPS na kuna tofauti gani kati ya mikataba hii? Namna gani jumuiya ya wafanyabiashara inaweza kunufaika kutokana na Mkataba wa WTO juu ya vikwazo vya kiufundi kwenye biashara (Technical Barriers to Trade)? Jinsi gani jumuiya ya wafanyabiashara itanufaika na Mkataba wa WTO kuhusu matumizi ya Sheria za usafi na afya ya wanyama na mimea? Jinsi gani mbinu za kupenya katika soko zinaweza kuboreshwa kwa kutumia Mkataba wa WTO juu ya SPS? 258 VIAMBATISHO- APPENDICES 261 Utafiti wa ITC kuboresha usimamizi bora wa bidhaa zinazouzwa nje: (ITC survey to update Export Quality Management:) Kitabu cha majibu kwa ajili ya wauzaji wa bidhaa nje wadogo na wa tasnia za kati 262 Tovuti muhimu 272

11 TANBIHI Kurejelea kote kwa dola ($) kunahusu dola za Marekani mpaka itakapoelezwa vinginevyo,. Neno Bidhaa limetumiwa kumaanisha kitu au huduma kutegemea muktadha lilivyotumiwa hasa katika sura zinazohusu uhakiki wa bidhaa, usimamizi wa ubora na ISO Pia, neno hili wakati mwingine limetumiwa kumaanisha usimamizi mkuu, na kuna maneno mengi ya Kiswahili ambayo hutumiwa kwa namna tofauti kutegemea maana au ujumbe unaoelezwa. Neno kanuni kwa mfano, linaweza kumaanisha sheria, desturi au utaratibu. Yametumika pia maneno mengi ya kutohoa ambayo si rasmi lakini yametumiwa kwa uzoefu wa mfasiri, pamoja na tafsiri za majina ya taasisi/mashirika ya kimatafa nayo inaweza kuwa si rasmi.

12

13 Utangulizi 3 UTANGULIZI Muundo Msingi wa Ubora sharti la biashara Kuanzia zama za kale, viwango na ubora vilikuwa sehemu ya jamii. Vitaendelea kuwepo na kwa sasa uzoefu unaonyesha kuchangia katika kukua kwa biashara katika nchi zinazoendelea na zile zenye uchumi wa kati. Kwa namna moja au nyingine vimekuwa nguzo ya masuala ya kibiashara na biashara. Viwango vinasaidia uunganishwaji na huweza kupunguza gharama kwa kuchangia vipuri, vipimo na njia. Huchangia katika kuanzisha viwanda vipya na uibuaji wa teknolojia. Kadhalika, huchangia katika utafutaji na kuyatunza masoko. Viwango na dhana zinazofanana katika miongo iliyopita, navyo vimepata umuhimu na kuwa chanzo cha uchunguzi zaidi wa kisayansi na kiteknolojia na fasili. Wakati huohuo ulimwengu wa biashara na jamii umekuwa ukibadilika kwa haraka. Bidhaa nyingi hutengenezwa kwa vifaa vilivyotafutwa kutoka sehemu mbalimbali na havina budi kuungana na kufanya kazi kama inavyotarajiwa kwa sababu ya biashara za kilimwengu,. Mzunguko wa bidhaa unakuwa mfupi, lakini maendeleo ya kiteknolojia yanakua kwa haraka. Yote haya inabidi kunadiwa ili kuwa yenye manufaa na ufanisi kupitia mtandao wa watoa huduma, unojulikana kama muundo msingi wa ubora. (QI). Nini maana ya muundo msingi imara? Muundo msingi wa ubora wa kitaifa, unaweza kueleweka kama ndio mhimili wa utaratibu kwa taasisi(za umma au binafsi) kuweka na kutekeleza viwango, sayansi ya vipimo (kisayansi,viwandani na kisheria) na uthibitisho na ukadiriaji ulinganifu wa huduma (ukaguzi, upimaji, na utaratibu wa mfumo wa uhakiki wa bidhaa) unaotakiwa kutoa ushahidi unaokubalika kuwa bidhaa na huduma vilikidhi viwango; iwe vile vilivyoweka na mamlaka (kanuni za kiufundi na vigezo vya afya ya wanyama na mimea, SPS) au za masoko( k.m. kwa mkataba au kutarajiwa). Mtindo rahisi unaainisha sehemu kuu tano za muundo msingi wa ubora wa kitaifa(nqi): kusanifiwa, kupima na sayansi ya vipimo, uhakiki na uthibitisho, ambavyo vinahusiana kwa karibu na kutegemeana (ona kielelezo). Tanbihi: CE and GS inarejelea alama za Uingereza za CE na za Kijerumani Geprüfte Sicherheit or tested safety certification mark respectively. Viwanda vinatakiwa kutengeneza bidhaa kwa kuzingatia viwango, kanuni za kiufundi na vigezo vya afya ya wanyama na mimea vilivyopo kwenye masoko ya nje; inabidi viweze kutumia maabara kwa kupima kufahamu kama bidhaa wanazotengeneza vinakidhi mahitaji; maabara hizi sharti ziwe na uwezo wa kupata huduma ya sayansi ya vipimo na ukadiriaji; kuhakikisha kuwa vifaa/vyombo vya kupimia vinatoa majibu sahihi; bidhaa/mifumo inaweza kuhakikiwa na watu wengine kuwapa imani wanunuzi mamlaka za kusimamia sheria kuwa mahitaji husika yanatimizwa wakati wote. Mashirika ya uhakiki na maabara yanahitaji kuthibitishwa kuonyesha umahiri wake. Mtengenezaji anaweza kutumia tamko la mgavi kuhusu ulinganifu (SDoC) kama mbadala wa uhakiki wa watu wengine. Kwa nini pawe na muundo msingi wa ubora? Nchi zilizostawi, zenye viwanda, pamoja na zile zenye uchumi wa kati na zile zinazoendelea zitapata faida kubwa kutokana na muundo msingi wa ubora: mahusiano ya kimataifa, kubadilishana ujuzi, kuongezeka kwa biashara na maendeleo, na hali ya maisha kwa jumla itaimarika. Faida za kitendaji za muundo msingi wa ubora ni kama zifuatazo:

14 4 Utangulizi Unasaidia kushinda changamoto za soko huria na utandawazi. QI ni muhimu katika kuondoa vikwazo vya kiufundi vya biashara kwa kuleta ulinganifu katika uagizaji bidhaa toka nje (maduhuli) na mahitaji ya kuyafikia masoko. Kwa hivyo, huu ni msingi mkubwa katika uwiano wa nchi katika mfumo wa biashara ya kimataifa. Muundo msingi wa ubora Unawezesha kufikia masoko ya kimataifa na unalinda masoko ya ndani. Makubaliano kati ya mataifa au kanda juu ya maafikiano ya pamoja ya mahitaji, njia za uchunguzi, ukaguzi au matokeo ya vipimo vyote inasaidia kupunguza au kuondoa vikwazo vya kiufundi kwa biashara, matokeo yake ni kuimarisha masoko ya ndani na kufungua masoko ya nje. Unahamasisha uvumbuzi na ushindani. Kwa kuwa uzalishaji na utoaji huduma unaimarishwa kwa misingi ya ubora, usalama na upatanifu, ambavyo mwisho wake ni kuongezeka kwa wanaotaka; wagavi wanaweza kuitumia fursa ya huduma za muundo msingi wa ubora kuongeza uvumbuzi na ushindani. Unalinda wateja. Wateja hupata faida na ukadiriaji wa ulinganifu kwa kuwa huwasaidia katika uchaguzi wa bidhaa au huduma: wanakuwa na imani zaidi na bidhaa au huduma ambazo zina alama au cheti cha ukadiriaji ulinganifu wakati wa kupima ubora, usalama au sifa yoyote inayofaa. Kanuni za kiufundi ambazo ziko kisheria ni muhimu hasa kwenye masuala ya afya, usalama na ulinzi wa mazingira. Kadhalika, vigezo vya afya ya wanyama na mimea, ambazo sharti zifuatwe, ni muhimu kwa usalama wa chakula na afya ya wanyama na mimea. Unawasaidia wasimamizi wa sheria na watoa huduma. Vyombo vya usimamizi wa sheria ya masuala ya afya kiserikali, usalama na sheria ya mazingira, na watoa huduma kama vile taasisi za kitaifa za sayansi ya vipimo, upimaji na huduma za ukadiriaji zinaweza kutegemea muundo msingi uliopo. Kwa njia hii, zinaweza kuepuka kurudufu vifaa na huduma, hasa katika nchi zenye rasilimali kidogo. Husaidia maendeleo ya kiuchumi. QI inasaidia kuleta maendeleo ya kuimarika kwa kuonyesha fursa ambazo zinaongeza ushindani wa bidhaa na huduma za ndani katika masoko ya ndani na kimataifa.

15 Utangulizi 5 QI kwa hivyo inatoa njia ya kuongeza mahusiano kati ya nchi shiriki katika kufikia hali ya haki katika biashara za kimaataifa. Pia, huanzisha taasisi na kuchochea mazingira bora ndani ya nchi. Unahamasisha ushirikiano wa kikanda. Majadiliano ya awali yaliyolenga masuala ya kiufundi yanaweza kujenga kujiamini na kuweza kuleta ushirikiano wa uwezo wa muundo msingi wa ubora, utaalam wa kiufundi, upimaji na maabara za ukadiriaji,n.k., matokeo ni kupunguza gharama. Kutambulika kimataifa kwa muundo msingi wa ubora wa kitaifa (NQI) ni muhimu kutokana na faida hizi zote kupatikana. Kila nchi inapenda kushiriki katika mikutano mwafaka ya kimataifa, ili kutambulika na kuepuka viwango vingi, kanuni,vipimo na uthibitisho, na kuelekeza nguvu katika kuwa na ukaguzi, upimaji na uhakiki wa mara moja, unaokubalika kote kutokana na kuwa na viwango vinavyokubalika duniani kote. Vigezo vya afya ya wanyama na mimea (SPS) Moja kati ya mambo muhimu katika utekelezaji wa NQI yanayolenga sekta hii ni katika kuhakikisha usalama wa chakula na mazao ya kilimo pamoja na afya ya wanyama na mimea kupitia vigezo vya SPS na kusaidia mauzo ya nje na ya nchini ya bidhaa hizi kuyafikia masoko kunategemea hali ya kutokuwa na wadudu na magonjwa katika nchi maduhuli au mahuruji. Kwa hivyo, nchi inabidi kuwa na vyombo madhubuti vya chakula na mazao ya kilimo, yaani mamlaka ya usalama wa chakula, shirika la huduma ya kulinda afya za wanyama. Wanaweza kuhakiki mauzonje na kudhibiti maduhuli ili kulinda mimea na wanyama wa ndani kutokana na wadudu na magonjwa ambayo yanaweza kuathiri mahuruji. Muundo msingi wa ubora katika taswira ya kibiashara Uhusiano wa viwango ukizingatiwa, kanuni za kiufundi, vigezo vya afya ya wanyama na mimea na ukadiriaji ulinganifu kwenye biashara ya kimataifa, ni dhahiri kuwa biashara, na hasa tasnia ndogo na za wastani, zina hamu kubwa katika mfumo tendi wa QI. Muktadha huu ukirejelewa, jamii ina majukumu tofauti ya kutekeleza ili kujenga muundo msingi huu Hali ikiwa hivi, jamii ya wafanyabiashara ina majukumu tofauti ya kutekeleza ili kufanya madhubuti ukuaji wa muundo msingi huu: Tukirejelea viwanda kama mteja, vinahitaji kushawishi matumizi nchini kwao, huduma za QI zinazotambulika kimataifa. Hali hii ni kweli kabisa kwa SMEs ikilinganishwa na makampuni makubwa, kwa maana huwa hazina uwezo wa ukadiriaji wa vipimo na kupima kama ilivyo kwa makampuni makubwa; badala yake, hutegemea msaada kutoka kwa mashirika ya kitaifa ya QI. Jambo la kutia faraja katika ushawishi ni kwamba, viwanda/biashara huwezesha kuongeza mauzo ya bidhaa kwa kuwa vinaweza kuthibitisha ubora wake. Biashara kama wabia, zinashauriwa kushirikiana kikamilifu na serikali, mashirika ya kijamii kama vile vyama vya watumizi ili kuendeleza muundo msingi wa ubora wa kitaifa. Mfano mmoja mkubwa ni usawazishaji ambao hujikita katika ushirikiano baina ya vitengo mbaimbali husika. Kadhalika, jumuiya ya wafanyabiashara inaweza kuisadia serikali katika majadiliano ya biashara ya kimataifa, k.m. kutoa taarifa kuhusu vipaumbele vya kitaifa katika kuitambulisha kimataifa NQI na kutambua makubaliano ya pamoja. Viwanda kama mgavi, vinaweza kutumia fursa ya kibiashara ya huduma ya ukadiriaji ulinganifu, k.m. kwa kuanzisha upimaji, ukaguzi na uhakiki wa vifaa vya watu wa nje. Hata hivyo, hili huyahusu zaidi makampuni makubwa. Siyo kwamba utoaji huduma za binafsi za QI unawezekana katika nchi zilizoendelea peke yake, lakini hata kwenye nchi zinazoendelea ambazo sekta ya umma haina uwezo wa kutoa huduma zinazokubalika kwenye masoko ya kimataifa zinatumika. Sekta za kibinafsi hivyo basi, inakuwa mdau muhimu wa muundo msingi wa ubora wa kitaifa. Chapisho hili lina nia ya kuwapa wauzanje wa tasnia ndogo na za wastani, uelewa wa kina kuhusu mambo muhimu ya ubora yanayohusiana na muundo msingi wa ubora, ili kuwawezesha kuendelea kufanya vizuri zaidi, na kufanikiwa katika mabaraza ya biashara ya kikanda na kimataifa. Ni imani yetu kuwa, chapisho hili, pia litachangia kuendeleza mazungumuzo na ubadilishanaji wa uzoefu kati ya ITC, BTB, na taasisi shiriki katika masuala ya usimamizi mkuu wa ubora wa Mahuruji, eneo lenye mabadiliko ya haraka na kwa hiyo inaendelea kuwa changamoto kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

16 6 Utangulizi KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Physikalisch-Technische Bundesanstalt (PTB). Quality Infrastructure in almost 5 minutes Sinema hii inawasilisha mashirika muhimu zaidi katika muundo msingi wa ubora na kuonyesha faida yake kwa jamii, uchumi na wateja kwa mifano mitatu iliyofafanuliwa. Sanetra, Clemens and Rocío M. Marbán. The Answer to the Global Quality Challenge: A National Quality Infrastructure. Physikalisch-Technische-Bundesanstalt(PTB) Chapisho hili linafafanua jinsi muundo msingi wa ubora wa kitaifa unavyotegemea vipengele vitano muhimu, jinsi vinavyohusiana, na kwa upande mwingine muundo msingi wa kitaifa unavyohusiana na mfumo wa ubora wa kimataifa. International Trade Centre. Innovation in Export Strategy Chapisho hili linatoa utaratibu halisi wa kutayarisha mkakati wa kuweka mazingira mwafaka ya muundo msingi wa ubora katika nchi zinazoendelea.

17 KUELEWA UBORA

18

19 9 Kuelewa Ubora 1. Ubora ni nini? Utafiti wa haraka kwenye mtandao utakupa maelezo mengi kuhusu maana ya ubora. Kamusi ya Oxford, kwa mfano, inaeleza ubora kuwa kiwango cha kitu kama kikipimwa kwa kulinganishwa na vitu vinavyofanana; daraja la uzuri wa kitu. Kamusi ya Biashara inaainisha ubora unaohusiana na utengenezaji, lengo kuu hapa ni kigezo cha uzuri au hali ya kutokuwa na kasoro, upungufu na mabadiliko muhimu, ambayo yameleta udhibiti madhubuti na kuwa katika vipimo na viwango vilivyothibitishwa kufikia usawa wa matokeo yanayoridhisha mteja au mahitaji ya watumizi. Kadhalika, ISO 9000 inaainisha ubora kuwa kiwango ambacho sifa za kitu zinakidhi matarajio/mahitaji. Mahitaji haya ni matakwa au mategemeo tarajiwa au ya lazima kwa wadau kama vile wateja, wagavi, na jamii. Kwetu sisi, ubora wa bidhaa au huduma unategemea makubaliano ya watu wawili; mmoja mgavi wa bidhaa au huduma na mwingine anayepokea bidhaa hizo au huduma. Mgavi na mteja wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu ubora, na hili linaweza kusababisha kutoelewana na kushindana. Ubora katika muktadha huu, unaweza kueleweka kama Kukubaliana na mahitaji ya wateja au kufaa kwa matumizi. Jambo la kwanza la kutambua ni kuwa mteja ndiye anayeainisha kama bidhaa inafaa kwa matumizi au la. Sifa za bidhaa au huduma, zisipofanana na zile za mteja, basi haiwezi kuwa bidhaa bora kwa mteja huyo. Gari kwa mfano linalotumia mafuta kwa wingi haliwezi kuwa bidhaa bora kwa mtu anayetafuta gari ambalo hutumia mafuta kidogo. Mgavi anaweza kuandaa vigezo vya bidhaa zake kutokana na kile wateja wanaona kuwa ndiyo mahitaji yao, na kutengeneza bidhaa zinazolingana na vipimo kamili/vigezo hivyo. Ikidhihirika kuwa bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya wateja, basi zitafikiriwa kuwa na kasoro; katika hali hii, vigezo vitakuwa havikukadiria mahitaji ya wateja, na hapo ndipo tunafikia msemo mteja ni mfalme. Ubora wa bidhaa haulingani kwa mtazamo wa wateja wote, lakini unahusiana. Bidhaa inaweza kuwa bora kwa mtu fulani lakini hafifu kwa mwengine. Mtu mmoja kwa mfano, anaweza kuridhika na viatu vyenye kisigino kirefu ilhali mwengine akapendelea visivyo na kisigino (bapa). Maelezo ya Snyder kuwa, ubora unategemea mtazamo wa mteja kikamilifu ulivyo wala si jinsi utakavyomwitikia, unapimwa na jinsi utakavyokidhi mahitaji ya wateja wako. Jambo la pili la kuzingatia ni kwamba, mahitaji ya mteja hubadilika na muda, kadiri uwezo wa kifedha unavyoongezeka au panapokuwa na bidhaa mpya sokoni ndivyo mahitaji yanavyobadilika. Mteja ambaye mwanzoni aliridhika na televisheni ya rangi nyeusi na nyeupe, sasa hivi atapenda kuwa na televisheni ya rangi na yenye skrini bapa. Ubora kwa kawaida huainishwa na ubora wa usanifu na ulinganifu (angalia swali 2). Hata hivyo, kwa bidhaa za muda mrefu kama vile kompyuta na friji, ambazo huhitaji huduma baada ya mauzo, kuna vigezo viwili zaidi husika, ; upatikanaji kwa ajili ya matumizi (bidhaa iweze kutumika kwa muda wa kutosha bila kuharibika)na huduma katika eneo la kazi, ambayo inatakiwa kuwa ya uhakika ikifanywa na wafanyakazi stadi. Tunapozungumzia ubora, neno daraja huja akilini; ambalo limeainishwa na ISO 9000 kama kategoria au cheo kinachopewa maeneo tofauti ya mahitaji ya ubora wa bidhaa, michakato au mifumo yenye aina moja ya matumizi. Baadhi ya mifano ni madaraja ya tiketi za ndege na makundi ya hoteli katika kitabu cha kuongoza. Ubora una aina nyingi za vipimo kama ilivyoainishwa na Garvin (1987) ifuatavyo: Utendakazi ambao unaelezea sifa muhimu za matumizi ya bidhaa; Sifa ziada ambazo zinachangia sifa muhimu za bidhaa; Tegemeo, hili linaashiria uwezekano wa bidhaa kutofanya vizuri au kushindwa kufanya kazi katika kipindi fulani; Ulinganifu, ambao ni kiasi cha usanifu wa bidhaa na sifa muhimu zinazokidhi viwango vilivyopo; Umadhubuti, ambao ni muda wa matumizi kabla ya bidhaa kuharibika au kupungua sifa zake kwa matumizi yaliyokusudiwa;

20 10 Kuelewa Ubora Uhudumiwaji, ambao hutegemea kasi ya timu ya wakaguzi, uungwana, umahiri na urahisi wa kufanyia (marekebisho) bidhaa; Umadoido, ambao wahusika na (taswira) huleta mvutio; Ubora unaotambulika ambao unahusishwa na sifa za rajamu. Kufuatana na ISO 9000 ainisho la ubora, yaani kiasi(digrii) ambayo sifa za bidhaa zinatimiza mahitaji, pia inatumika kwenye huduma. Tukilinganisha, ni rahisi kupima sifa za kifaa cha ujenzi, lakini huduma ambayo huwezi kuishika ni ngumu kuieleza kwa kipimo. Parasuraman, Zeithami and Berry (1988) wametaja sifa jumla za huduma na kuzipa kifupisho cha RATER: Mwitiko: kukubali na/au utayari wa wafanyakazi kuwasaidia wateja na kutoa huduma ya haraka na kwa wakati ufaao. Uhakika: maarifa na uungwana wa wafanyakazi wako na uwezo wao wa kujenga imani na kujiamini, kwa maana ya umahiri, uaminifu na kuaminiwa. Dhahiri: taswira halisi ya huduma kama vile vifaa, vyombo, sifa za watoa huduma(rasilimali watu) na nyenzo/vifaa vya mawasiliano. Uwezo wa kuhisi/kutambua kinachotakiwa: kutoa nafasi ya kuhudumia mteja kibinafsi, kumpa mteja taarifa kwa lugha anayoielewa, kuelewa mahitaji maalum ya mteja. Kutumainiwa: uwezo wa kutekeleza ahadi kwa usahihi na kutegemewa, kwa mfano, kutoa huduma kwa mara ya kwanza kwa usahihi, kutoa taarifa sahihi kwenye ankara. Washindi katika masoko, watakuwa wale watakaotoa bidhaa au huduma ambazo ni nzuri (kwa maana ya ubora), rahisi (kigharama) na kusambazwa kwa ufanisi (kufikia wateja kwa wakati na utoaji huduma - baada ya mauzo kwa wakati). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Zirek, Mehmet. Qualitopia, the Quest for Perfection Through Quality Management Principles. 6 January Inanapatikana kwenye tovuti SSRN: Makala haya yanachunguza mambo ya kufikirika ya kilimwengu; yanalenga kujua jinsi misingi ya ubora kwa ujumla na misingi ya usimamizi wa ubora kwa uchache inavyotuelekeza katika ubora wa kusadikika. MAREJELEO Business Directory. Garvin, David A. Competing on the Eight Dimensions of Quality. Harvard Business Review, November-December Shirika la Kimataifa la Viwango. ISO 9000: 2005, Quality management systems Fundamentals and vocabulary. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (orodha ipo Juran, J. and F. Gryna. Quality Planning and Analysis. McGraw-Hill, New York Kamusi za Oxford Mtandaoni. Parasuraman, Zeithaml and Berry. Studies PBZ90 and PBZ Cited in George R. Milne, Mark A. McDonald (eds.). Sport marketing: managing the exchange process, 1999, pp (cited at Snyder, I. G. The Quality Revolution. Quality Progress, vol. 18, No. 10, October 1985, pp

21 11 Kuelewa Ubora 2. Je, bidhaa au huduma bora hugharimu zaidi na kuna faida gani kutengeneza bidhaa bora au kutoa huduma bora? Gharama ya bidhaa au huduma bora Ukweli ni kwamba, jibu la sehemu ya kwanza ya swali linakinzana, yaani laweza kuwa ndio au la. Mbona iwe hivyo? Inategemea aina gani ya ubora unazungumuzia; ukitaka kuwa na gari la anasa (limuzini) lenye zana/vifaa vingi, itakugharimu zaidi ya gari dogo lenye vifaa vya kimsingi. Kadhalika, kama unataka kukaa kwenye hoteli ya hadhi ya nyota 5 (ghali) itakugharimu zaidi ya hoteli ya nyota 2 (ya bei nafuu). Hapa tunazungumzia usanifu wa ubora ambao unahusiana na sifa za bidhaa au utoaji wa huduma. Gharama ni kubwa kwa bidhaa au huduma zenye sifa za ziada na ndogo kwa bidhaa au huduma zenye sifa chache (finyu) katika usanifu wake. Watengenezaji au watoa huduma wanaposema kuwa ubora una gharama wakifikiria kuhusu suala la usanifu. Ubora wa usanifu unapaswa kutofautishwa na ubora wa ulinganifu ambao ni kiasi ambacho bidhaa au huduma hulingana na ubora wa usanifu. Ubora wa ulinganifu wa juu, unaweza kupatikana kwa kuwa na usimamizi wa ubora (angalia swali namba 4). Katika mfano wetu wa gari, baada ya kusanifu gari, limuzini au gari dogo, utekelezaji wa udhibiti wa ubora wakati wa utengenezaji, utapunguza kazi za kurudia na kuwa na mabaki (scrap/waste) machache. Ukichagua njia ya kuzuia, utaweza kupata bidhaa zaidi zinazokidhi viwango au mahitaji; na matukio ya bidhaa kurudishwa yatapungua na hii itafanya gharama ziwe chini. Maana yake ni kuwa gharama ndogo kwa ubora zaidi kwa sababu ya kupunguza mabaki na bidhaa za kurudishwa. Gharama ya ubora ambazo zinahusiana na ubora wa ulinganifu zimegawanyika katika gharama za tathmini na kutofaulu. Hizi zimefafanuliwa hapa chini: Gharama za kuzuia. Hizi zinahusu shughuli ambazo zinafanyika ili kuzuia bidhaa na huduma hafifu. Kwa mfano, kampuni ya magari inaweza kuamua kutekeleza mradi wa kuongeza ubora, au kuwekeza katika elimu na mafunzo kwa nia ya kupunguza bidhaa hafifu kwenye uzalishaji. Gharama za tathmini. Hizi zinahusu vipimo, kufanya tathmini au ukaguzi wa bidhaa na huduma ili kupima ulinganifu wake na mahitaji. Kwa mfano, kampuni yetu ya magari inataka kukagua vipuri vinavyotoka kwa wagavi ili kujiridhisha kuwa vinakidhi mahitaji ya ubora wake. Gharama za kushindwa. Hizi zinahusika na bidhaa au huduma ambazo hazilingani na mahitaji au matakwa ya wateja. Gharama za kushindwa zimegawanyika kama ifuatavyo: a) Gharama za kushindwa za ndani - ambazo hutokea kabla ya bidhaa au huduma kupelekwa kwa mteja; na b) Gharama za kushidwa za nje - hutokea baada ya bidhaa kusafirishwa au wakati huduma inatolewa. Katika mfano wa kampuni ya magari, gharama za kushindwa za ndani ni kama kurudia mlango ambao haukufaa kwenye gari lililoundwa, kwa upande mwingine gharama za kushindwa za nje zitatokana na malalamiko ya mteja kwamba gia boksi haifanyi kazi vizuri. Inawezekana ukapima gharama zako za ubora; lakini hizi hakika siyo gharama za kuzalisha bidhaa bora, bali ni gharama za ubora hafifu unaotokana na upungufu katika bidhaa au huduma zitolewazo kwa wateja, ikijumuisha shughuli ambazo zilichangia hali hiyo. Briscoe na Gryna (2002) walitoa mukhutasari wa takwimu za gharama za ubora katika tasnia za wastani na kubwa kama ifuatavyo: Gharama zinazohusu ubora ni kubwa kuliko zile huonyeshwa kwenye ripoti za hesabu za kampuni nyingi katika sekta ya uzalishaji na utoaji huduma. Gharama hizi huwa kati ya asilimia 10 hadi 30 ya mauzo au asilimia 25 hadi 40 ya ghrama za uendeshaji. Baadhi ya gharama hizi ziko wazi, zingine zimefichika. Kujulikana kwa faida hizi kunasaidia kuhimiza maendeleo. Ukilenga shughuli zinazohusu kuzuia, kwa kiasi utapunguza gharama za tathmini na kushindwa; katika hali hali hii matokeo yake ni kupungua katika gharama za ubora na kuongezeka kwa faida. Faida za kutengeneza bidhaa bora au kutoa huduma bora

22 12 Kuelewa Ubora Baada ya kusanifu bidhaa kwa ajili ya soko fulani, unaweza kupata ulinganifu mkubwa wa ubora kwa kutekeleza mbinu za uthibiti wa ubora zingatia swali 8 na usimamizi wa ubora swali 4. Ukilenga kuzalisha vyema kwa mara ya kwanza na daima, utapunguza upotevu/taka na kupunguza gharama. Utakuwa na wateja walioridhika na hawatakuwa na shida na bidhaa au huduma zako. Wateja watarudi kupata bidhaa zaidi na biashara itakuwa kadiri rajamu au alama ya biashara yako inavyoimarika sokoni. Bidhaa au huduma yako itakuwa ikidhaminiwa, basi gharama zitapungua kwa kuwa hutapata kuitwa mara kwa mara kwa matengenezo ( marekebisho) katika kipindi cha huduma baada ya mauzo. Yote haya yatasababisha kuongezeka kwa tija katika uzalishaji na kupungua kwa gharama. Utaweza kutumia ziada itakayopatikana kutokana na ulinganifu wa ubora wa juu kuongeza sifa ya bidhaa au huduma zako bila gharama za ziada au ongezeko la gharama kwa mteja. Kupitia kwa njia hii, utakuwa umeongeza usanifu wa ubora bila ya ongezeko la bei. Hali hii italeta mabadiliko makubwa katika mauzo, kuboresha soko lako na kujenga imani ya wateja kuridhika na bidhaa au huduma zako. Unaweza kuwa na utaratibu wa daima wa kuboresha kwa njia ya ulinganifu ubora wa juu, ukifuatiwa na usanifu ubora wa juu, ukifuatiwa tena na ulinganifu ubora wa juu, n.k. wa hali hii. KWA TARIFA ZAIDI REJELEA: Dhawan, Sanjeev. Cost of Quality (COQ). Makala ya kurasa nne yanayoainisha njia za kibiashara kwa gharama za ubora. Inajadili kwa ufupi nini, kwa nini, lini na faida za COQ. Kajiwara, Takehisa. Factors Influencing the Use of Quality Costs in TQM Environments: Evidence from Japan. December AAA 2010 Management Accounting Section (MAS) Meeting Paper. Available at SSRN: Makala haya yanachunguza baadhi ya sababu zinazoshawishi matumizi ya gharama za ubora katika mazingira ya TQM (usimamizi mkuu wa ubora kamili); imetokana na misingi ya ithibati za utafiti uliofanywa katika kampuni za uzalishaji za Kijapani. Keogh, William (et al). Data Collection and the Economics of Quality: Identifying Problems, (2006). Makala haya yanafafanua matatizo yanayotokea katika ukusanyaji wa ithibati sahihi za shughuli za gharama ya ubora na tathmini ya gharama ya ubora kiuchumi. Ryan, John. Making the Economic Case for Quality. An ASQ white paper. (2004). Downloadable at; Hili ni rejeleo kuhusu hali ya sasa ya ufahamu juu ya matokeo kwa uchumi ya utaratibu unaolenga katika kuendeleza ubora. Inaelezea matokeo ya usimamizi mkuu wa ubora karibu katika kila eneo la ufanisi wa muundo, na hatua za msingi, vigezo vya masoko na vigezo vya utendaji wa ndani. MAREJELEO American Society for Quality. Basic Concepts Cost of Quality (COQ). Inapakuliwa kutoka: Briscoe, Nat and Frank M. Gryna. Assessing the Cost of Poor Quality in a Small Business. Inapakuliwa kutoka : Brust, Peter J. and Frank M. Gryna. Quality and Economics: Five Key Issues. October Inapakuliwa kutoka: inapatikana bure kutoka kwa wanachama wa Chama cha Ubora cha Marekani au kwa malipo kutoka kwa wengine.

23 13 Kuelewa Ubora 3. Usimamizi wa ubora ni nini na sehemu zake nne ni zipi? Kufuatana na ISO 9000 neno usimamizi wa ubora (QM) ni shughuli zinazoratibiwa ili kuliongoza na kudhibiti shirika kuhusiana na ubora. Ili kuongoza na kudhibiti shirika inabidi kwanza(usimamizi mkuu wake sharti uandae sera yake ya ubora na malengo husika. Baada ya hapo, ianishe shughuli kuhusiana na mpango wa ubora, kudhibiti ubora, kuhakikisha ubora, na kuendeleza ubora. Nia ya QM ni kuhakikisha kwamba shughuli zote za kampuni ambazo ni muhimu katika kuwaridhisha wateja na wadau zinafanyika vyema na kwa ufanisi. QM hailengi ubora wa bidhaa au huduma pekee yake, lakini pia mbinu za kuufikia. Yafatayo ni maelezo ya sehemu nne za QM: 1. Kupanga ubora (QP) Kupanga ubora ni sehemu ya usimamizi wa ubora inayolenga uwekaji wa malengo ya ubora na kuainisha mikakati ya utekelezaji na rasilimali zinazohitajika kuyafikia malengo (ISO 9000: ) QP ni mtiririko wa mchakato ambao unatafsiri sera ya ubora katika malengo yanayopimika na mahitaji ya rasilimali na huainisha hatua zenye mantiki kufikia malengo kwa muda uliopangwa. Matokeo ya QP huwasilishwa kwa matumizi ya wahusika wote. Katika mfano wa mpango wa ubora. Kabrasha hili huainisha njia na rasilimali husika na wale watakaotekeleza na lini. Aina hii ya mipango ya ubora huandaliwa tofauti kwa michakato tofauti, bidhaa au mikataba. 2. Kudhibiti Ubora (QC) Kudhibiti Ubora ni sehemu ya usimamizi wa ubora inayolenga kutimiza mahitaji ya ubora (ISO 9000: ) QC inasaidia katika kutathmini uhalali wa ufanisi wa utendaji wa mchakato na bidhaa na, baada ya kulinganisha utendaji halisi na malengo yaliyowekwa, inachochea uchukuaji hatua kwa yale yaliyokiukwa kama yapo. QC ni duka uwanjani na shughuli kazini ambayo inahitaji rasilimali za kutosha; ikijumuisha watu wenye ujuzi, kwanza kudhibiti mchakato na kufanya marekebisho ya haraka pindi mchakato na/au paremeta za bidhaa zinatoka kwenye vikomo vilivyowekwa. 3. Kuhakikisha Ubora (QA) Kuhakikisha Ubora ni sehemu ya usimamizi wa ubora inayolenga katika kujenga imani kuwa mahitaji ya ubora yatatimizwa. (ISO 9000: ) Wateja na wasimamizi wakuu wote wanahitaji kuhakikishiwa ubora kwa maana hawana uwezo wa kusimamia utendaji wenyewe. Shughuli za QC huthibitisha kama mchakato wa ubora utafikiwa au unafikiwa au umeshafikiwa. Njia ya kutoa uhakika inabidi kujengwa ndani ya mchakato, kama vile kuweka nyaraka za mipango ya udhibiti, nyaraka za mahitaji, kuainisha majukumu, kutoa rasilimali, kufanya ukaguzi wa ubora, kuweka kumbukumbu, ripoti za marejeo, QA ina mambo mengi zaidi ya QC, ambayo ni sehemu yake. 4. Kuendeleza Ubora (QI) Kuendeleza ubora ni sehemu ya usimamizi wa ubora inayolenga katika kuongeza uwezo wa kutimiza mahitaji ya ubora. (ISO 9000: ) Kubakia katika ngazi fulani uliyofikia siyo chaguo la kampuni/shirika lako kama linahitaji kuendelea kuwepo. Kuweza kutunza utendaji wako katika soko, sharti ufanye shughuli ambazo zitaendeleza ubora daima. Shughuli za uboreshaji huo zinajumuisha kuboresha njia zilizopo, kufanya marekebisho katika mchakato ili kupunguza mabadiliko na pili kuongeza uzalishaji na zaidi kupunguza matumizi na rasilimali. Kama utataka

24 14 Kuelewa Ubora mafanikio, basi mara nyingi huhitaji mbinu/njia mpya, teknolojia na michakato. Kielelezo kilicho hapa chini kinaonyesha mabadiliko kutoka kudhibiti ubora mpaka usimamizi wa ubora. Uibuaji dhana ya usimamizi wa ubora kama unavyoainishwa ndani ya ISO 9000:2005 Kielelezo kinaonyesha kuwa kudhibiti ubora (QC) ni shughuli ya msingi ya QM. Unapofanya QC ndani ya mfumo fulani, unakuwa umeboresha QC kwa kuhakikisha ubora (QA). Ukiendelea kuendeleza ubora kutokana na uchanganuzi wa taarifa/takwimu kutokana na upimaji wa michakato/bidhaa na zile za rejea ya wateja, unakuwa umefika kwenye QM. Kwa hali hiyo, Kupanga ubora ambo ni sehemu ya hatua zote katika usimamizi wa wa ubora. Kwa kifupi sehemu nne za QM ni kama ifuatavyo: Kuandaa mpango wa ubora Je, tutaweza? Kudhiti ubora tunafanya ifaavyo? Kuhakikisha ubora tutaendelea kufanya au kukifanya sawasawa? Kuendeleza ubora tunaweza kuifanya vizuri/nzuri zaidi? k udhibiti ubora ni jambo la msingi katika usimamizi wa ubora,hivyo basi, inabidi uanzishwe kwanza katika kampuni/shirika. Pamoja na mambo mengine, kutahitajika vifaa na mashine vyenye uwezo sahihi, wafanyakazi wenye ujuzi, vifaa barabara vya kupimia na huduma muhimu za usaidizi. Yaliyotajwa yakikosekana, haitakuwa rahisi kufanya udhibiti wa ubora stahiki na kuweza kusonga mbele na kuhakikisha ubora na usimamizi wa ubora. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Dale, Barrie and Jim Plunkett. Managing Quality. Blackwell s Publishing. Blackwell s Online Bookshop, Blackwell s Extra, 50 Broad Street, Oxford OX1 3BQ, United Kingdom, bob.online@blackwell.co.uk Internet: Habari hii inatoa ukubalifu wa dhana na nyezo za usimamaizi wa dhati (TQM). International Organization for Standardization. Quality management principles. This brochure can be freely downloaded as a PDF file from ISO ( Nyaraka hii inatoa utangulizi juu ya misingi 8 ya menejimenti ya ubora ambayo ndiyo msingi wa viwango vya familia ya ISO Misingi hii inaweza kutumiwa na uongozi wa juu wa mashirika mwongozo wa kuendeleza ufanisi.

25 15 Kuelewa Ubora Lakhal, Lassâad (et al). Quality management practices and their impact on performance. International Journal of Quality & Reliability Management, vol. 23, Issue 6, 2006, pp Mada hii inalenga kufafanua uhusiano kati ya utendaji usimamizi mkuu wa ubora na matokeo yake kwenye utendaji. Office of the Secretary of Defense. Small Business Guidebook to Quality Management. Quality Management Office. Washington,D.C This guide book is freely downloadable from Madhumuni ya kitabu hiki cha mwongozo ni kusaidia biashara ndogo kufanya maamuzi kuelekea kwenye kupenda ubora. Kiliandaliwa na serkali ya shirikisho na Idara ya Ulinzi ili kuzisaidia biashara ndogo kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka kuelekea kwenye ubora. MAREJELEO International Organization for Standardization. ISO 9000:2005, Quality management systems Fundamentals and vocabulary. Obtainable from ISO or ISO members (list at Price, Frank. Right First Time Using quality control for profit. Gower Publishing (Customer Service) A priced publication of Book Point Limited, 130 Milton Park, Abingdon, Oxon OX14 4SB, United Kingdom. orders@bookpoint.co.uk, Internet:

26 16 Kuelewa Ubora 4. Je, shughuli za mfumo wa kudhibiti ubora zinahusianaje na usimamizi wa ubora? Nianze na mfumo wa kudhibiti ubora kabla ya kuweka mfumo wa usimamizi wa ubora? Shughuli za mfumo wa kudhibiti ubora zinalenga kazi zote ambazo zinahitajika kufanywa ili kuzalisha bidhaa inayokidhi mahitaji. Kazi hizi zinajumuisha kuwa na muundo msingi wa kutosha na mazingira ya kazi sahihi, viwango vya malighafi na bidhaa zilizotengenezwa, maelekezo ya wafanyakazi, ununuzi wa malighafi na vitu, ubora stahiki, kuudhibiti mchakato wa uzalishaji, kushughulikia na kuhifadhi vizuri malighafi na bidhaa zilizotengenezwa, ukaguzi wa bidhaa wakati wa uzalishaji na baada ya kukamilika, matengenezo ya wakati ya vyombo na vifaa vya kupimia. Mahusiano ya shughuli za QCS yako kwenye kielelezo cha mfano wa QCS kinachofuata. Mfano wa QCS Source: S.C. Arora, India. Kudhibiti ubora ni sehemu muhimu zaidi katika usimamizi wa ubora (angalia swali 3). Kama udhibiti wa ubora hautafanyika kwa makini, usimamizi wa ubora hautakuwa na mafanikio. Kwa hivyo kabla ya kuanzisha mfumo wa usimamizi wa ubora(qms), sharti uwe na mfumo wa kudhibiti ubora(qcs) mzuri. Baada ya QCS kuimarika, ndipo inafaa kuongeza mahitaji mengine ya QMS (angalia swali namba 32). Hata hivyo, kabla ya kuweka QCS ni vema kuwa na utaratibu mzuri wa utunzaji nyumba, kwa kutumia utaratibu wa Kijapani wa 5S (angalia swali 10). Inabidi urejelee mfumo wako wa QC wa sasa na kutekeleza shughuli zifuatazo kama msingi, kama hazifanyiki: a. Andaa muundo msingi wa kutosha. Hii inajumuisha kujenga majengo, kuwa na vyombo na vifaa, huduma za umma na aina nyingine ya usaidizi. Kwa mfano, mashine za kuandaa na kusindika bidhaa, barabara na njia zinazopitika wakati wote katika eneo la kazi, mfumo mzuri wa maji/maji taka, kuta (mpaka meta 1.3) zilizopigwa lipu vizuri au kuwekewa vigae, sakafu zenye vigae, milango ya kujifunga, mahali pa kunawia mikono, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo, huduma za kudhibiti na kuangamiza wadudu/wanyama waharibifu n.k. b. Anzisha mazingira sahihi ya kazi na usafi. Maana yake ni kuwa mwanga wa kutosha, hewa, joto na unyevu sahihi, udhibiti wa kelele. Pia, kufuata

27 17 Kuelewa Ubora mbinu bora za usafi wa wafanyakazi( k.m. matumizi ya vitambaa vya kichwani, kinga za macho, mdomo, kutokula au kutafuna, matumizi ya vidani na mapambo mengine yanayoweza kuhatarisha usalama wa bidhaa au mitambo hasa katika viwanda vya chakula). c. Kuwaelimisha wafanyakazi kuhusu utaratibu bora. Kwa mfano, ni vyema wafanyakazi watambue umuhimu wa kuifahamu kazi kabla ya kuianza. Washughulikie bidhaa vizuri bila kuziharibu au kuzichafua na pia washughulikie zile mbovu. d. Andaa viwango (mahitaji) vinavyoeleweka kirahisi, vya malighafi na bidhaa. Kama viwango au mahitaji hayaeleweki vyema kwa wote wanaohusika, hata ukifanya ukaguzi wa aina yoyote hautasaidia. Kwa mfano, aina yoyote ya dosari au upungufu usioruhusiwa/kukubalika, lazima uwe wazi kwa wafanyakazi na wanaokagua. e. Tengeneza na hakikisha yanakuwepo maelezo yanayoeleweka kirahisi- jinsi ya kufanya kazi. Kama ujuzi wa wafanyakazi wako hautoshi, itahitajika maelezo ya mdomo na maandishi (vyema yakawa katika lugha wanayoielewa vizuri) yakituma vielelezo vya kutosha. Wakati mwingine ni vyema pakawa na sampuli halisi ya kitu kinachotarajiwa kutengenezwa (k.m. kwa bidhaa za ngozi au nguo) itatoa maelekezo vizuri zaidi. f. Ununuzi wa malighafi zenye ubora unaokubalika kutoka kwa wagavi. Ununuzi unaozingatia bei ya chini pekee yake, bila kuangalia vifaa na vyanzo vingine, siyo utaratibu mzuri. Kushughulika na wagavi wachache unaowafahamu ni vizuri zaidi kuliko kuwa na wagavi wengi wapya. Ni vyema kufanya uchunguzi mwenyewe kuhakiki uwezo wa wagavi wako au kupata taarifa kutoka kwa wanaofahamu kazi. Ili upokee bidhaa zinazokidhi mahitaji, ni muhimu kuwaelewesha wagavi wako viwango/mahitaji ya bidhaa na utaratibu utakaoutumia kupokelea mali kutoka kwao. g. Hifadhi malighafi na vifaa vizuri kuepuka kuharibika au kuchanganyika. Ili kuendesha biashara yako unahitaji kuwa na hifadhi ya kiasi ya malighafi na vifaa vya matumizi; hivi inabidi vishughulikiwe na kuhifadhiwa kwa uangalifu kuzuia visichanganyike au kuharibika. Kwa mfano, katika usindikaji vyakula, vifaa visivyo vyakula kama mafuta ya kulainishia mitambo, sabuni, kemikali, vipuri n.k., havistahili kuchanganywa na vyakula. Viwekwe kila kimoja sehemu yake. Vifaa vya hatari kama dawa za wadudu, vihifadhiwe kwa uangalifu. Kadhalika, mazingira yote ya chakula sharti yawe mwafaka, kwa mfano yawe yenye nyuzi joto zinzzokubalika ili kuzuia uharibifu. h. Angalia na kukagua malighafi na vifaa vingine kabla ya matumizi. Kagua malighafi uliyoagiza kutoka kwa wagavi kabla ya kuipokea kama inakidhi mahitaji. Kwa mfano mazao ghafi yakiletwa toka shambani kwa ajili ya kuwekwa kwenye madaraja au usindikaji yasipokelewe kama yana uchafu au yamevunda/kuoza, n.k. i. Fanyia matengenezo(marekebisho) ya mashine/mitambo, majengo na vifaa vingine vya uzalishaji mara kwa mara. Sharti uwe na mpango wa utunzaji wa kulinda mashine zako ili zibakie katika hali bora wakati uzalishaji utakapoanza. Matengenezo ya kinga hupunguza matukio ya mashine kuharibika; kwa mfano katika usindikaji wa vyakula, sharti kuwe na utaratibu unaofuatwa wa usafi na kutakasa sehemu zote za jengo, vifaa na mashine. Mashimo na mifereji ya maji na sehemu zingine ziwe safi na kuzibwa wakati wote ili kuzuia wadudu/wanyama waharibifu kuingia. j. Fanyia matengenezo ya vifaa vya kupimia na kagua kama viko barabara (tumia vipimo). Kama unatumia vifaa kama kipima joto, geji ya kinaeneo, mikromita, visicosity meters sharti vikaguliwe mara kwa mara na kufanyiwa ukarabati. Ratiba ya ukaguzi/matengenezo sharti ifuatwe. Usawa wa vifaa hivi hubadilika kutokana na muda wa matumizi. Kwa hivyo, vitahitaji kukadiriwa kwa kulinganishwa na vifaa vinavyoeleweka vipimo vyake kuwa barabara. k. Fuata taratibu nzuri za hatua za uzalishaji. Kwanza changanua mchakato wako wa uzalishaji na kila hatua ya uzalishaji sharti irekodiwe kwenye fomu ya mtiririko wa uzalishaji. Kufanya hivyo kutawasaidia wafanyakazi wako kufuata hatua, kuzuia makosa na kwa hiyo kupunguza haja ya kurudia usindikaji. l. Thibiti mchakato ili kufikia mahitaji ya bidhaa. Baadhi ya hatua katika uzalishaji zinahitaji udhibiti, kwa mfano kudhibiti uzito, joto, muda, ph, Brix, rangi na, muonekano. Inabidi uweke vikomo vya kudhibiti kwa kila kimojawapo na kuvifuatia.

28 18 Kuelewa Ubora m. Zuia utengenezaji wa bidhaa zenye kasoro. Inabidi kufanya ukaguzi makini ya mchakato na kukagua bidhaa kwa vipindi vya kurudia kutokana na hali iliyotajwa awali. Kama kutaonekana ukiukwaji, basi huna budi kuchukua hatua ya haraka. Kwa namna hii, utaongeza uhakika wa kuzalisha bidhaa zisizo na kasoro. Maana yake utakuwa karibu na kufanya vyema kwa mara ya kwanza. n. Tumia mbinu za kitakwimu, kama vile utaratibu wa kuchukua sampuli na chati za udhibiti kwa kuudhibiti mchakato, na njia zingine za kudhibiti ubora. Kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kudhibiti ubora kwa utaratibu wa kusanya na kurekodi udhibiti wa mchakato na takwimu za ukaguzi wa bidhaa, na kuzichanganua kwa shabaha ya kuchukua hatua kwenye chanzo cha matatizo yakitokea (angalia swali namba 8). Fomu ya ukaguzi ni sahili, lakini ni njia yenye manufaa kwa kufuatia kasoro za bidhaa zako. o. Fanya ukaguzi kwa hatua wakati wa utengenezaji. Pamoja na ukaguzi unaofanywa na wafanyakazi wako kwenye bidhaa kwa kuangalia au kwa kutumia vifaa sahili, ukaguzi wa hatua ( kwa kila bidhaa au kwa kuchukua sampuli) unaweza kufanywa na msimamizi au na mkaguzi wa kudhibiti ubora (QC) baada ya kukamilika kila mchakato au seti ya hatua za mchakato. Kwa namna hii itahakikisha kugundulika kwa bidhaa zenye kasoro, na kuchukua hatua ya kuzirekebisha mapema. p. Fanya ukaguzi wa mwisho wa bidhaa iliyozalishwa na kufungasha kufuata mahitaji yaliyowekwa. Hii ndiyo nafasi yako ya mwisho kuikagua bidhaa. Baada ya hatua hii, bidhaa inaondolewa kiwandani na kama mteja au mtumiaji atabaini ina mapungufu, haitakuwa sifa njema. Kwa maana utahitaji pesa nyingi kusahihisha hali hiyo. Kwa sababu ukaguzi huo wa mwisho wa bidhaa, lazima ufanyike kwa makini; unaweza ukahitajika kufanya vipimo fulani katika maabara. Kadhalika, sharti uamue ni nani atakayefikisha bidhaa kwa mteja. Kama wakati wa ukaguzi wa mwisho kutagundulika kukiukwa kwa mahitaji, itabidi uisindike upya bidhaa na kama hili haliwezekani, basi ikatae. Vinginevyo, unaweza kuamua kuiachia kwenda; lakini katika hali hiyo itabidi kuwafahamisha wateja na kupata kibali chao kabla ya kuisafirisha bidhaa. q. Shughulikia bidhaa kwa uangalifu wakati wa kutengeneza na wakati wa kusambaza kwa wateja. Bidhaa nzuri zaweza kuharibika kama hazitashughulikiwa kwa uangalifu wakati wa uzalishaji, kwa kutohifadhiwa vizuri (k.m. katika hali ya nyuzi joto zinazohitajika), kwa kutofungashwa (kutopakiwa) vizuri au wakati wa kusafirisha kwenda kwa mteja. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na uangalizi wa karibu (ukaguzi wa kina) kwa bidhaa katika mchakato mzima. r. Omba taarifa za matokeo ya ukaguzi wa mwisho na chukua hatua ifaayo. Matokeo ya ukaguzi wa mwisho. Pamoja na taarifa za ukiukwaji uliobainika ( kama p juu), sharti ufahamishwe kwa wafanyakazi ili kuhakikisha ukiukwaji huo hautokei tena. s. Changanua malalamiko au marejesho/maoni ya wateja na chukua hatua ya kuondoa malalamiko. Ukipata malalamiko kutoka kwa wateja, hatua ya kwanza ni kudhibitisha kuyapokea na kuyakubali. Chukua hatua ya kuwatuliza kwa kuirekebisha bidhaa au kuwapa nyingine bila malipo. Hatua utakazochukua zitategemea aina ya malalamiko na makubaliano yenu/mkataba wenu. Tatizo hili lisiishie hapa, bali inabidi kurudi kiwandani na kuchuguza kiini cha malalamiko. Kwa kufanya hiyo, mtachukua hatua ya kuhakikisha malalamiko ya aina hiyo hayatokei tena. Kadhalika, kuna wateja wengine wanaweza kuwapa maoni ambayo yatasaidia katika kurekebisha kasoro zilizojitokeza. Itabidi kuwashukuru na (kuzingatia) maoni yao. t. Chukua hatua kwa kasoro zilizojitokeza, kama zipo. Unaweza ukapata fursa ya kufanya marekebisho kwa ukiukwaji uliobainika kwenye malighafi kutoka kwa wagavi, katika ukiukwaji uliojitokeza wakati wa udhibiti wa mchakato au kutokana na ukaguzi wa hatua na mwisho; inawezekana ukawa umepata mawazo ya wateja kutokana na malalamiko yao. Katika hali hii, itabidi uchanganue tatizo na kutafuta kiini chake. Baada ya kubaini chanzo chake, sharti hatua zichukuliwe kuzuia kujirudia kwa tatizo. Ili uweze kufanikiwa katika kudhibiti ubora, wafanyakazi wa ngazi zote sharti washirikishwe. Maana yake ni kuwa,

29 19 Kuelewa Ubora kuwaelimisha/kuwaendeleza wafanyakazi wako lazima kuwe endelevu. Mapinduzi ya Wajapani katika ubora kwa kiasi kikubwa yametokana na mafunzo/elimu nzuri wanayopewa wafanyakazi wa ngazi zote kutoka wasimamizi wakuu hadi wafanyakazi wa ngazi ya chini. Katika hatua za mwanzo wakati wa kuweka mfumo wa kudhibiti ubora, inawezekana ukaona gharama zaidi zitahitajika. Lakini gharama zitokanazo na uzalishaji wa kurudia, kurekebisha na kukataliwa kwa bidhaa zitapungua kwa kiasi kikubwa wakati mfumo utakapokuwa unafanya kazi vizuri. Kadhalika, gharama za kuondoa bidhaa yako kwenye soko, kushughulikia malalamiko ya wateja na kuwabadilishia bidhaa nazo zitapungua; matokeo yake ni kuokoa rasilimali. Mfano wa mfumo wa kudhibiti ubora ulioelezwa hapo juu ulitekelezwa na tasnia ndogo na za wastani(smes) zilizochaguliwa katika sekta ya bidhaa za uhandisi sahala huko Bangladesh ( ) chini ya mradi wa Bangladesh wa kusaidia ubora (Bangladesh Quality Support) uliotekelezwa kwa ushirikiano wa UNIDO na ITC. SMEs zilizochaguliwa, kwanza zilitekeleza mfumo wa 5S wa Kijapani na baada ya kupata matokeo yenye mwelekeo mzuri (k.m. SME moja iliongeza uzalishaji kwa 30%), waliandaa na kutekeleza mfumo wa kudhibiti ubora (QCS). Viwanda ambavyo vilikuwa vinazalisha bidhaa za ngozi walitekeleza mfumo wa 5S (angalia swali namba 10) na kupata matokeo ya kuvutia baada ya baadhi yao kupatiwa mafunzo juu ya kuuelewa, kuutekeleza na kuukagua mfumo wa usimamizi wa ubora, ISO KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Caplen, R.H. A Practical Approach to Quality Control. 5th ed A priced publication of Random House Business Books Ltd, 20 Vauxhall Bridge Road, London SW1V 2SA, United Kingdom, enquiries@randomhouse.co.uk, Internet: Kitabu hiki kinatoa utangulizi wa masuala ya kimsingi katika kudhibiti ubora, kuelezea mbinu zipi mwafaka zinazoweza kutambuliwa na kuhusishwa katika mfumo unaozingatia thamani. Office of the Secretary of Defense. Small Business Guidebook to Quality Management. Quality Management Office. Washington, D.C This guide book is freely downloadable from Kiini cha mwongozo huu ni kusaidia biashara ndogo ndogo kujiendeleza ili kufikia hadhi ya juu. Kimetayarishwa na serikali ya Marekani na Wizara ya Usalama. Inasaidia biashara ndogo ndogo kuwa kwa pamoja na usambaaji wa kasi wa ubora. Webber, Larry and Wallace. Quality Control for Dummies. Publisher for Dummies ISBN Can be purchased from Kitabu hiki kinatoa mbinu muhimu za kiufundi muhimu katika mbinu za utekelezaji wa ubora katika kampuni husika, jinsi ya kukusanya data, kutekeleza miundo msingi ya ubora na mengineyo. Mwongozo huu tekelezi unatoa mwongozo muhimu unaohitajika kuboresha kampuni yako. MAREJELEO International Organization for Standardization. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at

30 20 Kuelewa Ubora 5. Ni njia ipi ya usimamizi mkuu wa ubora itakayosimamia mafanikio endelevu ya shirika/kampuni? Kama inavyofafanuliwa kwenye ISO 9004, mafanikio endelevu ni uwezo wa shirika kufikia na kulinda malengo yake ya muda mrefu. Malengo ya haraka au muda mfupi ya shirika lolote ni kuridhisha wateja wake kwa kuwapa bidhaa au huduma ambazo zinakidhi matakwa yao. Utekelezaji mzuri wa ISO 9001 utakusaidia kufikia lengo hili. Hata hivyo, ukitaka kufikia lengo lako la muda mrefu la kukomaa kiuchumi, sharti utumie ISO 9004 ambayo inasaidia kampuni zinazotaka mafanikio endelevu. ISO 9004 inaweza kutumiwa na shirika/kampuni yoyote bila kujali ukubwa, aina au shughuli zake. ISO 9004 inatoa wigo mpana juu ya usimamizi wa ubora kuliko ISO Wakati ISO 9001 inashughulikia mahitaji na matarajio ya wateja, ISO 9004 inazingatia matakwa na matarajio ya wadau wote wanaohusika. Wateja wanataka na kutarajia bidhaa bora, bei inayokubalika na ufanisi katika kuwafikishia bidhaa; wafanyakazi wanatafuta mazingira bora ya kazi na uhakika wa kuendelea na kazi; jamii inatarajia uthibitisho wa maadili mema na ulinzi wa mazingira; wenye mali na wanahisi wanataka faida endelevu. Kufikia matakwa na matarajio haya yote kutakuhakikishia kufikia mafanikio endelevu. Misingi muhimu ya ISO 9004 inajumuisha: Usimamizi kwa ajili ya mafanikio endelevu ya shirika inajumuisha michakato inayotakiwa kwa ajili ya mafanikio endelevu, mazingira ya muundo, matakwa na matarajio ya wadau. Sera na mkakati ikijumuisha uanzishwaji, usambazaji, na mawasiliano. Usimamizi wa rasilimali ikijumuisha fedha, rasilimali watu, wagavi na washirika, miundo msingi, mazingira ya kazi, maarifa, teknohama na maliasili. Usimamizi wa mchakato ikijumuisha kupanga mchakato, udhibiti na mamlaka na wajibu juu ya mchakato. Uangalizi, vipimo, uchanganuzi na marekebisho ikijumuisha vigezo muhimu vya ufanisi, ukaguzi wa ndani, kujitathmini na kuweka alama za msingi. Kuendeleza ubunifu na kujifunza pamoja na uendelezaji mdogo-kwa hatua katika sehemu za kazi(small-step continual improvement in the workplace)na uendelezaji wa muhimu katika shirika, ubunifu kwa ajili ya kukidhi matakwa na matarajio ya wadau, na kuhimiza uboreshaji na ubunifu kwa kujifunza. ISO 9004:2009 hushamirisha ISO 9001:2008 (ni kinyume chake). Kama hujawahi kutekeleza ISO 9001 na unataka kuanza na ISO 9004 moja kwa moja, unaweza kufanya hivyo. Kwa kuwa ISO 9004 ni kiwango elekezi, siyo kwa ajili ya uhakiki, usimamizi wa sheria au mkataba au kama mwongozo wa kutekeleza ISO Kiambatisho C kwenye ISO 9004 kinatoa kifungu kwa kifungu mawasiliano kati ya ISO 9001:2008 na ISO 9004:2009. Chombo cha kujifanyia tathmini kilichomo kwenye kiambatisho A kwenye ISO 9004:2009, kinaweza kusaidia tathmini ya ufanisi wa shirika lako na kiasi cha kuimarika kwa mfumo wa usimamizi mkuu. Matokeo ya tathmini binafsi yanaweza pia kuasidia kutambua maeneo ya kuendeleza au ubunifu na kubainisha vipaumbele kwa hatua zitakazochuliwa baadaye. The self-assessment tool, given in Annex A to ISO 9004:2009, can help you to assess the performance of your organization and the degree of maturity of its management system. The results of the self-assessment can also help you to identify areas for improvement or innovation and determine priorities for subsequent actions. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Al-Dabal, Jamal K. Is Total Quality Management Enough for Competitive Advantage? Realities in Organizations Implementing Change Initiatives: with examples from the United States and the Developing World. 15 March ISBN /126/1. Inatoa hojaji/mjadala halisia katika utekelezaji wa mabadiliko muhimu katika shirika. Makadirio ya TQM katika sekta ya huduma pia yamejidiliwa huku kuridhika kwa mmnunuzi kukitiliwa mkazo au kupewa kipau mbele.

31 21 Kuelewa Ubora From Certification to Excellence, Quality Management to Sustained Success. Maelezo ya kina kwa njia ya PowerPoint yaliyotayarishwa na Mark Fraser, Menaja wa bidhaa wa kundi katika British Standards Institution (BSI). Maelezo kwa ufupi ya kutazama ya ISO 9004:2009. IRCA INform. Issue 23, Wavuti hii ina andiko linalotoa maelezo ya ISO 9004: Towards sustained success na David Hoyle ambapo mwandishi anaeleza marekebisho yaliyofanywa kwa ISO 9004 na maana rejeshi kwa ISO Powell, Thomas C. Total Quality Management as Competitive Advantage: A Review and Empirical Study. Strategic Management Journal, vol. 16, pp , Makala haya yanaangazia TQM kama mbinu sahihi ya kuleta ushindani wa manufaa, yanaelezea mapitio ya utafiti na kuripoti majibu ya utafiti juu ya athari za kutekeleza TQM. MAREJELEO International Organization for Standardization ISO 9004:2009, Managing for sustained success of an organization A quality management approach. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 9001:2008, Quality Management Systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (Orodha ipo kwenye tovuti New edition of ISO 9004 maps out the path forward to sustained success. ISO press release (Ref of 2009). Freely downloadable from

32 22 Kuelewa Ubora 6. Tuzo za kitaifa za ubora zikoje? Zina umuhimu wowote kwa SMEs? Tuzo za kitaifa za ubora (NQA) zina kazi kubwa ya kuhamasisha na kuzawadia ufanisi wa kimuundo uliotukuka. Kwa kifupi, historia ya maendeleo ya NQAs, tuzo tatu zimefanya kazi kubwa nazo ni; Tuzo ya Deming Prize (Japan, 1951), na Malcolm Baldrige National Quality Award (United States, 1987) na EFQM (European Foundation for Quality Management) Excellence Award (Europe, 1992). Nchi nyingi zimeandaa tuzo zake kwa kuiga hizi tatu. Tuzo za ubora kwa sasa zimeenea dunia kote. Kwa mfano kuna tuzo za kitaifa Australia, karibu nchi zote za Marekani ya Kusini na Caribbean, Masharika ya Kati (Misri na Israeli), Asia (Hong Kong SAR, India, Malaysia, Singapore, Sri Lanka), na Africa (Mauritius, South Africa). Baadhi ya serikali zimekuwa na utashi mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa NQAs. Kwa mfano, tuzo ya Malcolm Baldrige National Quality Award na Tuzo zinazoambatana nayo zilianzishwa na sheria ya Malcolm Baldrige National Quality Improvement Act ya 1987 na tuzo hutolewa na rais wa Marekani. Mfano mwingine ni wa tuzo ya kitaifa ya Argentina ambayo ilianzishwa kwa sheria na husaidiwa na fedha za serikali. NQAs zimeandaliwa kuhamasisha uelewa juu ya ubora, kufahamu mahitaji ya ubora wa kutukuka, kubadilishana taarifa juu ya mikakati iliyofanikiwa na faida zake. Kwa ujumla, vigezo vya kupata tuzo ya kitaifa ya ubora ni 7 hadi 10 kwa ufanisi wa juu (pamoja na vigezo vidogo vidogo 20 mpaka 30). Vigezo 10 vya kawaida ni kama ifatavyo: Uongozi Mpango/mikakati Kulenga wateja na soko Taarifa na uchanganuzi Kulenga rasilimali watu Usimamizi wa mchakato Matokeo ya kibiashara Faida kwa jamii Rasilimali Ufanisi na usimamizi wa wagavi/washirika Kwa mfano European Foundation for Quality Management wana vigezo 9 ambavyo vimegawanyika katika vipengele viwili: wawezeshaji na matokeo (angalia kielelezo kilicho hapa chini). Kigezo cha uwezeshaji kinahusika na jinsi shirika linavyojiendesha, jinsi linavyosimamia wafanyakazi wake na rasilimali, jinsi linavyopanga mikakati yake na jinsi linavyorekebisha na kufuatia michakato muhimu. Matokeo ya shirika, ni kile wanachopata. Hii ikijumuisha kiwango cha kuridhika kwa wafanyakazi na wateja, matokeo/athari yake kwa jamii na vigezo muhimu vya ufanisi. Taasisi ya British Quality Foundation (BQF) nayo imebuni chombo cha kieletroniki kinachoitwa BQF snapshot ambacho kinaweza kutumika katika kompyuta nyingi za Windows. Chombo hiki ni nyenzo ya haraka na rahisi ya kukuwezesha kutathmini shirika lako linajilinganishaje kwenye sifa za ubora wa kutukuka. Taratibu za kawaida za kuwapata washindi wa NQA zinajumuisha uchunguzi wa awali na tathmini ya takwimu za mwombaji kwa uteuzi wa mwanzo, ikifuatiwa na kutembelea sehemu za kazi na mwisho uteuzi utakaofanywa na jopo la majaji. Ripoti za mrejesho kwa yale yaliyopatikana/au kujulikana ikijumuisha tathmini ya uwezo na maeneo ya kurekebisha ya mwombaji hutolewa. Majina ya washindi huwekwa kwenye tovuti ya taasisi inayosimamia NQA na, tuzo hutolewa katika sherehe ya hadhara yenye utangazaji mkubwa.

33 23 Kuelewa Ubora Muundo wa Mfano wa Ufanisi wa EFQM (The EFQM Excellence Model Framework) Chanzo: British Quality Foundation. Nchi nyingi hutoa tuzo zingine mbalimbali kwa tasnia za ukubwa tofauti na kisekta. Kwa mfano, katika tuzo ya Malcolm Baldrige Award, makundi yanayozawadiwa yanajumuisha wazalishaji kiwandani, tasnia ndogo, taasisi za tiba, shughuli zisizo za faida na elimu. SMEs wanazidi kuwa muhimu katika ushindani wa kitaifa na ajira (kule Marekani SMEs huchangia nusu thamani ya vitu vinavyozalishwa nchini, lakini viwango vinavyochangiwa na SMEs nchini Singapore na Hong Kong SAR ni 91% na 98%, mtawalia. Nchi nyingi na maeneo mengi yamefanya mabadiliko katika utoaji wa tuzo kwa SMEs; kwa mfano taasisi za kitaifa za tuzo ya ubora za Australia, Chile, India na Hong Kong SAR zimerahisisha vigezo vya NQA kwa SMEs. SMEs nazo zinaweza kuomba NQA. Tuzo ya namna hii itaongeza kujulikana kwa tasnia hizi ndani na nje kwenye masoko ya kimataifa. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Australian Business Excellence Awards. Mashirika yote nchini Australia yanaweza kushirika tuzo hizi. Hii ni pamoja na kampuni za kibinafsi na za kiserikali, miungano ya kimataifa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali. European Foundation for Quality Management (EFQM). EFQM Excellence Award: Tovuti ya EFQM ambayo ni wasimamizi wa EFQM Excellence Model, mchakato unaosaidia zaidi ya mashirika dunia nzima kuazimia kujiboresha kila mara. (page 24) Malcolm Baldrige National Quality Award. Inatoa maelezo kamilifu ya tuzo ya kitaifa ya Malcolm Baldrige na umuhimu wa kushirika katika tuzo hiyo. Pia inaeleza kwa kina kila sekta ya tuzo hii. (page 24) National Quality/Business Excellence Awards in different countries. Tovuti hii inatoa orodha ya tuzo 103 za kitaifa za ubora za kibiashara katika nchi tofauti tofauti. Orodha hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanya kwa niaba ya National Institute of Standards and Technology (NIST) na Musli Mohammad na Robin Mann Centre for Organizational Excellence Research, Rajiv Gandhi National Quality Award (India).

34 24 Kuelewa Ubora Tuzo ya kitaifa ya Rajiv Gandhi iliyoidhinishwa na Shirika la Ubora la India mnamo mwaka wa 1991, ukiwa na mtazamo wa kuchochea mashirika ya huduma na bidhaa kupania mafanikio na kutoa mtajo/utambuzi maalum kwa viongozi wa ubora nchini India. Tuzo hii inatazamia kuleta mnato na ushirika wa mashirika ya India katika programu za ubora, kupeleka bidhaa kutoka india katika ngazi za juu za ubora na kuyatayarisha mashirika ya India kukumbana na changamoto za soko la nyumbani na la kimataifa. Singapore-Quality-Award. Tuzo hii ya Singapore ilizinduliwa mwaka wa 1994 na waziri mkuu kama msimamizi wake. Singapore Quality Award ni tuzo inayopewa mashirika yanayoridhisha ubora wa juu zaidi kibiashara. Sri Lanka National Quality Award. Tuzo ya Kitaifa ya Sri Lanka hutolewa kila mwaka ili kutambua mashirika yanayofuzu katika usimamizi bora wa mashirika ya Sri Lanka. Tuzo hii huandaliwa na kutekelezwa na kitengo cha mauzo cha Shirika la kudhibiti ubora la Sri Lanka. (page 25) MAREJELEO British Quality Foundation. Tan, Kay C. A comparative study of 16 national quality awards. The TQM Magazine, vol. 14, Issue 3, pp Available free from

35 25 Kuelewa Ubora 7. Nini dhana ya majukumu matatu katika usimamizi wa ubora? Kila mmoja katika shirika anaweza kuwa na majukumu matatu, kama mteja, msindikaji/mzalishaji na mgavi. Ubora ni kukidhi matarajio ya mteja (angalia swali la 1) na hupatikana kwa uratibu na usimamizi wa shughuli nyingi zinazohusiana, utafiti wa masoko, usanifu, manunuzi, uzalishaji, upimaji,ukaguzi, ufungashaji na usafirishaji. Kama ilivyonenwa na Ruskin ( ): Ubora siyo ajali; daima ni matokeo ya juhudi stadi. Kukidhi matarajio ya wateja wetu, lazima tupate mahitaji yao na, kuzalisha na kusambaza kufuatana na mahitaji hayo. Kusimamia hali hii ya mgavi na mteja ni muhimu katika kusimamia ubora. Tuna tabia ya kuwaona wagavi na wateja kuwa nje ya mashirika yetu. Wagavi hutupa malighafi, vipuri na taarifa, na wateja hununua bidhaa na huduma zetu. Tunajisahau kwamba hata kwenye mashirika yetu tunao wagavi na wateja. Kwa mfano idara ya masoko huainisha sifa zinazotakiwa na watumiaji. Basi idara ya masoko ikifanya kazi kama mgavi inawasilisha taarifa hizo kwenye idara ya usanifu, ambao ni wateja wa ndani. Idara hii ya usanifu, ikiwa imechukua jukumu la msindikaji, wanatayarisha mahitaji/sifa kwa kuzingatia taarifa zilizopokewa, na kuyapeleka mahitaji waliyoyatayarisha kwenye idara ya uzalishaji, ambao ndiyo wateja wa ndani. Hapa idara ya usanifu wanakuwa wagavi wa idara ya uzalishaji. Katika mfano huu, idara ya usanifu imetimiza majukumu matatu; wamekuwa wateja, wasindikaji na wagavi. Dhana hii ya majukumu matatu iko wazi katika njia ya mchakato katika usimamizi wa ubora. Shughuli ambayo inatumia rasilimali na kusimamiwa ili kubadilisha pembejeo kuwa bidhaa inaweza kuitwa mchakato au usindikaji. Pembejeo huletwa na mgavi kwa mteja (msindikaji) ambaye huzibadilisha kuwa bidhaa ambazo zitapewa mteja mwingine. Ubadilishaji wa pembejeo hii kuwa bidhaa huwa umefanywa na mteja wa awali akiwa kama msindikaji. Kielelezo kinachofuata kinafafanua mnyororo wa mgavi-mteja: Mnyororo wa mteja-mgavi Chanzo: Oakland (2003), imeigwa. Mashirika yote ya kile kinachojulikana kama mnyororo wa ubora wa wateja na wagavi ni muhimu kuhakikisha kuwa minyororo hii ya ubora haikatiki mahali popote ili kuwa na uhakika matarajio ya wateja yanaafikiwa. Vinginevyo shirika litakumbana na wateja waliogadhabika na usambazaji wa bidhaa au huduma zenye kasoro kwa sababu ya kushindwa kwa moja ya minyororo ya ubora. Kwa mfano, kama uliagiza chakula cha mbogamboga kwa ajili ya safari ya ndege kupitia kwa wakala wako, naye hakuwasilisha taarifa hii kwa wenye ndege, hutaweza kupata chakula hicho maalumu na wahudumu wa ndege itabidi wavumilie gadhabu yako kuhusu hili. Wakati wote panapokuwa na suala la mgavi-mteja kwenye shirika, ni muhimu kukubaliana juu ya mahitaji; kwa maana kuna sababu ya kupokea bidhaa zisizofaa kwa matumizi. Hali hii itahakikisha pembejeo zinazopokelewa kwa usindikaji, ambao nao utahakikisha ukiukwaji wakati wa mchakato unakuwa mdogo. Ili bidhaa zitakazopatikana ziweze kukidhi matakwa ya mteja anayefuata. Katika kila hatua ya mgavi-mteja, wahusika wasikubali bidhaa isiyo na ulinganifu uliowekwa; na kurudishwa kwa wagavi. Hii itapeleka ujumbe

36 26 Kuelewa Ubora kwamba bidhaa linganifu tu ndizo zinakubalika, punguza taka, na kupunguza malalamiko ya wateja na kuondolewa kwa bidhaa sokoni. Dhana ya majukumu matatu itachochea utamaduni wa kutengeneza bidhaa bora kwa mara ya kwanza na daima. Kama utaratibu, kila mtu katika shirika anatakiwa kuikubali dhana ya majukumu matatu, kuwatambua wagavi na wateja wake, kuchukua jukumu la usindikaji na kupunguza ukiukwaji kwa kiasi. Kama mteja uliza maswali kama haya: Akina nani ni wagavi wangu wa karibu? Je, nimekwisha wasilisha mahitaji yangu ya uhakika kwao? Je, tumekubaliana namna ya kukagua pembejeo zao kama zinakidhi mahitaji? Kama mgavi uliza maswali kama haya: Wateja wangu wa karibu ni kina nani? Je, wameshawasilisha mahitaji yao ya uhakika kwangu? Je, wameshakubaliana nami namna ya kukagua ulinganifu wa bidhaa zangu kwao? Kama msindikaji uliza maswali kama haya: Je, mchakato wangu unaweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu wa karibu? Kama hapana, je, mchakato wangu ufanyiwe marekebisho gani ili ukidhi mahitaji haya? Ni vema shirika likajiweka sawa kwanza kwa kuimarisha minyororo yake ya ndani ya ubora ya wagavi na wateja, kabla ya kuwashirikisha wagavi na wateja wa nje katika dhana ya majukumu matatu. Kujenga utamaduni ambao unavumisha dhana hii utajenga mazingira ya kuaminiana kati ya wagavi na wateja wa ndani. Mafanikio ya minyororo ya ndani ya wagavi na wateja itapelekea mafanikio ya mahusiano ya wagavi na wateja wa nje. Katika mazingira hayo kutakuwa na mahusiano mazuri yatayowezesha kupata maoni ya mara kwa mara kutoka kwa wadau na matokeo yake ni kupungua kwa taka/uharibifu, ongezeko katika kuwaridhisha wateja na maendeleo katika mchakato wa uzalishaji. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Department of Trade and Industry, United Kingdom. Total Quality Management in the series on From Quality to Excellence. Makala haya yanaeleza kwamba maswala ya nje na ndani ya mnunuzi na muuzaji ndio kiini muhimu cha TQM. Inaangazia mifumo katika kila swala na umuhimu wa kujitolea katika kutekeleza ubora, kuwasilisha jumbe za ubora na kutambua hitaji ya mabadiliko ya tabia za kimsingi za shirika. Gašparík, Josef and Sylvia Szalayová. Quality Management System in Construction Firm. Inaelezea mbinu tatu muhimu zinazozingatiwa katika sekta ya ujenzi. MAREJELEO Hutchins, David C. Just in Time. Gower Publishing Ltd., Oakland, John S. Total quality management: Text with cases. Butterworth-Heinemann,

37 27 Kuelewa Ubora 8. Ni zipi nyenzo saba za kudhibiti ubora na zinasaidiaje kutatua matatizo yanayohusu ubora? Nyenzo saba za kudhibiti ubora ni seti ya grafu/picha ambazo zitakusaidia katika kutatua masuala yanayohusiana na ubora. Kaoru Ishikawa, Mjapani anayejulikana kama baba wa ubora alirasimisha vyombo saba vya msingi vya kudhibiti ubora. Ishikawa aliamini kuwa asilimia 95 ya matatizo ya kampuni yangeweza kutatuliwa kwa kutumia nyenzo hizi saba na zote ukitoa chati zinaweza kufundishwa kwa mjumbe wa shirika. Utaratibu wake wa urahisi wa kutumia pamoja na matumizi ya grafu/ishara zinazoonekana inafanya uchanganuzi wa kutumia takwimu rahisi kuuelewa na kuutumia. Vyombo hivyo saba vinafafanuliwa kama ifuatavyo: Nyenzo Mfano-kielelezo 1. Chati ya mtiririko wa usindikaji/mchakato. Ripoti ya msururu wa matukio na shughuli, hatua na maamuzi katika hali ambayo inaweza kueleweka kwa urahisi na kuwasilishwa kwa wote (angalia kielelezo). Katika chati hii: Mstatili unaonyesha hatua za mchakato. Almasi zinaonyesha maamuzi, au matawi ya mchakato. Duara zinaonyesha viunganishi, ambavyo vinaunganisha sehemu moja ya mchakato na nyingine. Duara dufu inaonyesha mipaka ya mchakato, vikionyesha chanzo cha mchakato na mwisho wake. Mishale inaonyesha mwelekeo wa mtiririko. 2. Fomu ya Ukaguzi. Fomu ya ukaguzi au fomu ya majumuisho ni njia rahisi ambamo data inayokusanywa hurekodiwa kwa kuweka alama mahali pa aina ya kipimo kilichofanywa. Nia ya kukusanya data inabidi ifahamike vyema. Kwa mfano, fomu ya ukaguzi inaweza kutumika kufuatilia matukio kwa vigezo kama muda (kwa wakati, kuchelewa siku moja,kuchelewa siku mbili),sababu za kushindwa (kasoro kama uharibifu wa matunda na wadudu,kuwepo kwa unyevu nje, saizi siyo sare), idadi ya malalamiko ya wateja kwa siku (angalia kielelezo). 3. Grafu. Hii ni njia nzuri ya kuandaa, kufupisha na kuonyesha data kabla ya uchanganuzi. Kati ya grafu za kawaida ni histogramu na chati za pai(angalia kielelezo cha histogramu).

38 28 Kuelewa Ubora Nyenzo Mfano-kielelezo 4. Uchanganuzi wa Pareto. Juran aligundua ajabu ya kuwa na vichache vyenye maana na vingi visivyokuwa na faida/upuuzi kama msimamo unaotawala, na kufaa katika maeneo mengi. Alitumia hali hiyo katika kuyakabili matatizo ya ubora na kuiita Msingi wa Pareto, kumuenzi Vilfredo Pareto, mchumi wa Kiitaliano. Chombo hiki pia huitwa Kanuni ya 80-20, ikionyesha kuwa 80% ya matatizo hutokana na 20% ya sababu. Ni grafu ya pao na chati ya mistari ambayo huonyesha wakala walio muhimu kuliko wengine. Grafu ya pao huorodhesha kwa kuteremka umuhimu wa sababu zinazoathiri mchakato. Grafu ya mstari hurundika pamoja asilimia zilizopewa kila sababu; kutafuta sababu iliyo muhimu zaidi, chora mstari kutoka 80% ya shina la y ya chati kuunganisha na grafu ya mstari na mstari kuteremshwa mpaka kwenye shina la x. Hii hutenganisha sababu muhimu ( vichache vyenye maana) kutoka kwenye vingi vya kipuuzi (angalia kielelezo). 5. Mchoro wa sababu na athari. Mchoro unawakilisha uhusiano uliopo kati ya tatizo na sababu zinazowezekana. Inajulikana pia kama mfupa wa samaki au Mchoro wa Ishikawa. Inashughulika na mawakala na siyo idadi. Kuweza kutayarisha mchoro wa Ishikawa sababu zote zinazohusiana na tatizo huainishwa katika kipindi cha kuchangiana mawazo kati ya wahusika. Tatizo huandikwa sambamba na mshale uliolala. Sababu zote zitakazoibuliwa wakati wa kuchangiana mawazo hupangwa kwenye makundi kutegemea wazo (kibinadamu, vitu, mashine, njia, n.k.). Kila wazo litawakilishwa na mshazari uliounganishwa na mstari au mfupa wa katikati. Kila sababu zinaorodheshwa kufuta mshazari. Baada ya kuchangiana mawazo, sababu ambazo zitaonekana kujirudiarudia, huchaguliwa ili hatua zichukuliwe. (angalia kielelezo). 6. Mchoro kutawanya. Mchoro wa kutawanya hutumiwa kutafiti uhusiano kati ya badiliko moja na lingine. Inaweza kutumiwa kujaribu mahusiano kati ya uwezekano wa sababu na nathari. Haithibitishi kwamba badilko moja husababisha lingine, ila huonyesha dhahiri kama kuna mahusiano na aina na nguvu ya mahusiano. Kielelezo kinachoonekana hapa, kinaonyesha mchoro wa kutawanya wenye mahusiano sahihi. Katika mchoro shina la x linaweza kuwakilisha, kwa mfano unyevu nje ya tunda, na shina la y laweza

39 29 Kuelewa Ubora Nyenzo Mfano-kielelezo kuhusiana idadi ya matunda yaliyoharibika baada ya muda Fulani. 7. Chati za Udhibiti. Chati za udhibiti ni grafu zinazoonyesha tofauti zilizopatikana katika vipimo au uchanganuzi wa mchakato na kuwekwa kwenye grafu ya tokeo dhidi ya muda. Chati hizi zina mistari miwili inayoitwa UCL(kikomo cha juu cha udhibiti-upper control limit) na LCL( kikomo cha chini cha udhibiti-lower control limit). Hivi siyo sawa viwango vya kuvumilika, ila kama matokeo ya vipimo yataonyesha kupitwa kwa vikomo hivi, basi sharti sababu zichunguzwe na hatua kuchukuliwa mara moja. Kupunguza ukiukwaji uliojitokeza katika mchakato, inabidi kufanyike mabadiliko ya msingi kwenye njia, mashine, vifaa au vitu vingine. Chati za udhibiti zinaweza kuchorwa kwa badiliko au data zinazoendelea (kwa mfano uzito wa mfuko, nyuzijoto katika stoo ya baridi, muda wa kuoka, mwendo wa mkanda wa kuchukulia), Chati za udhibiti wa mabadiliko zipo za wastani na masafa. Chati za udhibiti zinaweza kuchorwa kwa kutumia sababu(variable) au data za kuendelea (kwa mfano idadi ya mapungufu/dosari zilizokutwa kwenye fungu,nambari ya mipasuko katika kitu, kiasi cha mishono isiyokuwepo kwenye pochi ya ngozi, kiasi cha asilimia cha kuchelewa kusafirisha au kujibu malalamiko ya wateja). Aina mbili za chati za data za sababu zinazotumika zaidi chati ya np (kwa namba ya kasoro zilizomo kwenye fungu) na Chati p ( kwa kiasi cha vitu vyenye kasoro). Chati za udhibiti zinasaidia kufuatilia na kudhibiti ubora kwa kufanya kazi kama taa za trafiki na zinafaida katika shughuli za aina mbalimbali. KWA TAARIFA ZAIDI Ishikawa K. Guide to Quality Control (Industrial Engineering & Technology). Asian Productivity Organization. ISBN Kitabu hiki kinazingatia kunga kuu za kudhibiti ubora pamoja na kukusanya data, chati za kueleza udhibiti, histogramu, michoro, michoro ya kuonyesha kisa na tukio, stadi bahatishi, michoro ya pareto, grafu na kadhalika. Imeandikwa kwa lugha rahisi na inayoeleweka. Kitabu hiki kinawapa changamoto wafanyakazi kutumia vigezo katika kazi zao, pia inaelezea shida halisia zinazoweza kutokea. Office of the Secretary of Defense. Small Business Guidebook to Quality Management. Quality Management Office. Washington, D.C This guide book is freely downloadable from Kiini cha mwongozo huu ni kusaidia biashara ndogo ndogo kujiendeleza ili kufikia hadhi ya juu. Kimetayarishwa na serikali ya Marekani na Wizara ya Usalama. Inasaidia biashara ndogo ndogo kuwa kwa pamoja na usambaaji wa kasi wa ubora. (page 34) MAREJELEO BreezeTree Software. source for figure of flow chart. Cause and effect diagram, source: Ho, Samuel K. TQM: An Integrated approach. ISBN A priced publication obtainable from Dr. Samuel Ho, Leicester Business School, De Montfort University, Leicester LE1 9BH, United Kingdom. SKHCOR@dmu.ac.uk Seven QC Tools: Q-BPM. source for figures except flow chart and cause and effect diagram.

40 30 Kuelewa Ubora 9. Six Sigma ni kitu gani? Six Sigma ni muundo unaotegemea data kama mbinu ya kutatua matatizo sugu yanayokabili biashara kwa nia ya kupunguza ukiukwaji katika mchakato wa kibiashara. Mbinu ya Six Sigma alianzishwa na kuenezwa mwaka 1987 na Kampuni ya Motorola nchini Marekani, inatoa vifaa na mbinu za kuboresha uwezo wa mchakato na kwa hiyo kupunguza makosa. Six Sigma ina misingi miwili: sauti ya mteja na sauti ya mchakato. Inadhamiria kupunguza tofauti zilizopo kati ya sauti hizi mbili, ili zipatane. Juhudi ya Six Sigma zinalenga maeneo matatu muhimu: Kuendeleza furaha ya mteja Kupunguza muda wa mzunguko Kupunguza kasoro Six Sigma inalenga kuwa na ufanisi wa biashara usiokuwa na makosa. Kufikiwa malengo ya Six Sigma inahitaji maendeleo ya kutosha katika kila nyanja ya biashara kuliko kutegemea maendeleo kidogo kidogo. Sigma ambayo ni herufi ya Kigriki, alama σ ; inatumika katika kueleza wastani wa kukiuka kwa mchakato. Kwa maneno mengine sigma ni kipimo kinachotumiwa kubainisha hali ya uzuri au ubaya wa mchakato, yaani makosa mangapi yamefanywa katika mchakato. Kimapokeo, Sigma Six inamaanisha wastani 6 za ukiukwaji kutoka wastani wa mchakato. Jedwali lifuatalo linaonyesha matokeo katika hatua mbalimbali za sigma. Matokeo ya mchakato katika hatua mbalimbali za Sigma Hatua ya Sigma Bidhaa zinazokidhi mahitaji: % Kasoro katika kila fursa milioni (Defects per million opportunities) (DPMO)* , , , , Chanzo: David Hoyle, ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6th ed *DPMO na yenye shift ya Sigma 1.5 (with a 1.5 Sigma shift). DPMO ni matokeo ya DPU (makosa kwa kitu) ukizidisha mara na kugawanya kwa fursa za makosa katika kitu. Kwa mfano kama oda ya ununuzi ini fursa 50 za makosa na ukichukua kuwa mfanyakazi anayeandaa oda ya manunuzi anafanya kosa 1 kwa wastani, DPMO katika mfano huu itakuwa 1 kuzidisha na , kugawa na 50 au 20,000. Tuseme unafanya biashara ya kupeleka pizza kwenye ofisi zilizo karibu; una sifa ya kutengeza pizza nzuri na una wateja wengi na kufuatana na mkataba wako na wateja, utawasilisha pizza kwa wakati na zenye moto kati ya saa asubuhi na mchana. Hii inafanya wapokee oda yao kwa wakati kwa ajili ya chakula cha mchana (mahitaji yao). Pia mmekubaliana kuwa, kama pizza zitafikishwa kabla ya asubuhi au baada ya 12.15mchana, utawapa punguzo la 50% katika oda itakayofuata; na kwa kuwa wafanyakazi wako hupata marupurupu)kwa kuwasilisha kwa wakati, wote mnahamasika kufikisha pizza katika kipindi cha nusu saa. Tukizingatia hali kama hii, Six Sigma, kama kipimo, ingeweza kufanya kazi katika mchakato huu rahisi. Kama utawasilisha 68% ya pizza kwa wakati, mchakato wako utakuwa katika hatua 1 ya sigma. Kama utawasilisha kwa wakati pizza kwa 99.73%, ambayo inaokana ni vizuri, utakuwa unafanya kazi katika hatua ya 3 ya sigma kwa ufanisi. Ili uwe duka la pizza la hatua ya 6, unahitaji kuwasilisha pizza kwa wakati kwa kiwango cha %. Ufanisi unaofaa; kwa hakika katika kila pizza milioni utakazotengeneza, utachelewa kuwasilisha mara 3 au 4 tu.

41 31 Kuelewa Ubora Hatua ya kwanza katika kukokotoa sigma au kuelewa umuhimu wake, ni kufahamu anachotegemea mteja. Katika lugha ya Six Sigma, mahitaji na matarajio ya mteja yanaitwa CTQ (kihakiki cha ubora). Katika mfano wa pizza, moja ya mahitaji ya muhimu ya mteja ni kuwasilisha kwa wakati kwa pizza; mahitaji mengine yanaweza kuhusiana na nyuzi joto ya pizza, usawa wa oda, ladha na kadhalika. Kwa hakika moja ya funguo za Six Sigma ni kuelewa vizuri na kutathmini ni kwa kiasi gani mchakato unakwenda vizuri katika CTQ zote, na siyo moja au mbili tu. Kampuni zinazofanya kazi katika ngazi ya 3 au 4 sigma, hutumia kati ya asilimia 25 na 40 ya mapato yao kushughulikia matatizo. Hali hii hujulikana kama gharama ya ubora, au kwa uhakika ni gharama ya ubora hafifu. Makampuni yanayofanya kazi katika hatua ya Six Sigma hutumia chini ya asilimia tano ya mapato yao kutatua matatizo. Kutegemea ukubwa wa kampuni na ukubwa wa uzalishaji wake, gharama (dola) ya mapungufu haya yanaweza kuwa makubwa sana. Kwa mfano, upungufu kati ya sigma 3 au 4 na six sigma yalikuwa yanawagharimu Genera Electric kati ya US$ bilioni 8 na 12 kwa mwaka. Six Sigma hutumia vyombo na njia kadhaa zilizothibitika, lakini vyombo hivyo vinatumika katika mfumo rahisi unaojulikana kama DMAIC (Ainisha-Pima-Changanua-Endeleza-Dhibiti (Define-Measure-Analyse- Improve-Control). Jambo muhimu la Six Sigma ni kuwa na muundo msingi ambao utahakikisha kuwa shughuli za kuongeza ufanisi zinapata rasilimali zinazohitajika. Asilimia ndogo ya mameneja kwa muda wote hupangiwa kazi ya kuainisha na kutekeleza miradi ya kuendeleza ya Six Sigma. Hujulikana zaidi kama Mikanda Mieusi ya Sigma, Mikanda ya Kijani au Mabingwa. Six Sigma kwa hakika ndiyo njia ya kwanza katika masuala ya ubora iliyowafanya mameneja wasimamizi kuchukua hatua pamoja na mameneja wa ubora, wahandisi wa ubora na wakaguzi, na kuwafanya wawe Mikanda Mieusi, Green Belts au Mabingwa. Mahitaji ni makubwa ; kwa mfano, Mkanda Mweusi, lazima awe na elimu ya chuo kwenye Hesabu, afahamu vifaa vya msingi vya kufanyia uchanganuzi wa kina na awe amepitia saa 160 za mafunzo darasani pamoja na mafunzo ya ana kwa ana na gwiji wa Mkanda Mweusi. Ili kuhakikisha taarifa zinazotakiwa katika kuendeleza miradi zinapatikana, Six Sigma inabidi iwe sehemu ya mfumo wa habari wa shirika. Kwa hakika, upatikanaji wa ujuzi na mafunzo ya Six Sigma Mikanda Mieusi sharti kuwe na uwekezaji kwenye teknohama. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: De Mast, Jeroen. Six Sigma and Competitive Advantage. Total Quality Management, vol. 17, No. 4, May 2006, pp Karatasi hii inachunguza uhakiki wa Six Sigma kwamba inatoa ubora wa ushindani kwa kuiweka kati ya fasihi za kunga za kiusomi ikitumia sanaa ya ushindani mwafaka. International Organization for Standardization. ISO 13053:2011, Quantitative methods in process improvement Six Sigma. Obtainable from ISO or ISO members (list at Vitengo vipya vya ubora vinarejelea utumizi wa Six Sigma kuendeleza matukio yake. Imechapishwa katika sehemu mbili: ISO :2011, Mbinu Chanya katika kuboresha Matukio Six Sigma sehemu ya 1: Mbinu katika DMAIC, na ISO :2011, Mbinu Chanya katika kuboresha Matukio Six Sigma sehemu ya 2: Vigezo na mbinu tumizi. Pande, P. et al. The six sigma way: How GE, Motorola and other top companies are honing their performance. McGraw-Hill Companies, 2 Penn Plaza, New York, NY ISBN Kitabu hiki kimeandaliwa kwa matumizi ya wasomaji mbalimbali, kuanzia wale wasioijua six sigma mpaka wale waliobobea katika mambo hayo. Sehemu ya kwanza ya kitabu hiki inatoa mukhtasari wa six sigma; na Sehemu ya Pili inakwenda kwa undani zaidi ili kusaidia kuikbali six sigma; Sehemu ya tatu inashughulikia utekelezaji, kwa kuonyesha njia na nyenzo zinazotakiwa. Pande, P. and L. Hollp. What is Six Sigma? McGraw-Hill Companies, 2 Penn Plaza, New York, NY ISBN Kitabu hiki kinatoa utangulizi rahisi wa Six Sigma.

42 32 Kuelewa Ubora MAREJELEO Chowdhury, Subir. The Power of Six Sigma. Pearson Education (Singapore) Pte Ltd, Indian branch 482, FIE, Patparganj, Delhi ISBN Obtainable from Hoyle, David. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6th ed ISBN It is a priced publication of Butterworth- Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X2 8DP, United Kingdom. Also available from Pyzdek, Thomas. The six sigma revolution. This article is freely available in Quality America magazine on their website:

43 33 Kuelewa Ubora 10. 5S za Kijapani ni kitu gani na faida zake ni nini? 5S za Kijapani ni njia nzuri ya utunzaji wa ndani na inafafanuliwa na maneno matano ya Kijapani: Seiri, Seiton, Seiso, Seiketsu na Shitsuke. Matumizi ya njia hii yalianza mwaka wa 1972 na Henry Ford nchini Marekani, kama program ya CANDO: Kusafisha, Kupanga, Umaridadi, Nidhamu na Kuendeleza daima (Cleaning up, Arranging, Neatness, Discipline and Ongoing improvement). Mbinu hii ilienezwa kama Japanese 5S mwaka 1980 na Hiroyuki Hirano. Unaweza kudhani kuwa utunzaji wa ndani ni kazi rahisi na kwamba tayari unaifanya. Kweli ni rahisi, lakini inabidi kufanywa kwa mpangilio. Hutoa matokeo mazuri baadaye na inaweza kukufanya ukaokoa fedha. 5S za Kijapani zinajumuisha hatua zifuatazo: Hatua tano za 5S za Kijapani Seiri Chambua Seiton Weka katika mstari Seiso Ng ara Seiketsu Sanifisha Shitsuke Endeleza Chanzo: S.C. Arora, India. Tofautisha kati ya vitu vya lazima na visivyo vya lazima. Ondoa cha mwisho Tekeleza maamuzi/tamko sehemu ya kila kitu na kila kitu katika sehemu yake. Safisha mahali pa kazi na tafuta njia za kuhakikisha panabaki safi. Dumisha na simamia kubakia katika Ss tatu za kwanza. Fuata kanuni kuweka 5S za mahali pa kazi sawasawa. Tunza unachopata. Kila hatua imeelezwa kwa ufupi hapa chini. Njia zilizopendekezwa, mifano ya hatua na faida za kila hatua zimeorodheshwa. 1. SEIRI CHAMBUA Hii ina maana kutofautisha au kuchambua vitu vinavyotakiwa na vile visivyotakiwa katika sehemu ya kazi na kuviondoa. Mifano na njia zinazopendekezwa: Kwanza inabidi uamue ni yapi ya muhimu na yasiyo muhimu( vitu visivyo vya muhimu vinaweza kuwa kwenye sakafu, rafu, kwenye makabati, katika stoo, ghala, kwenye ngazi, paa, vibao vya matangazo, nk.) Itakubidi uviwekee alama vitu visivyotakiwa na kuviweka kwenye eneo tofauti. Unaweza kuviacha au kuvitupa vitu ambavyo havikutumika mwaka uliopita; vitu ambavyo hutumika mara moja katika miezi 6 au 12, vinaweza kuhifadhiwa kwenye stoo ya mbali na sehemu ya kazi, na vile vinavyotumika zaidi ya mara moja kwa mwezi, vipatikane kwenye eneo la kati katika sehemu ya kazi. Ni vyema kuweka vitu vinavyotumika kila mara /kila siku/mara moja kwa wiki karibu na sehemu ya kazi; vitu vingine vinaweza kuvaliwa au kuwekwa mfukoni mwa wafanyakazi katika sehemu ya kazi. Faida za SEIRI: Nafasi ya sakafu yenye manufaa hutunzwa; muda wa kutafuta vyombo, vifaa na karatasi hupungua; mtiririko wa kazi huwa bora zaidi; gharama za vifaa visivyohitajika hupungua.

44 34 Kuelewa Ubora 2. SEITON WEKA KATIKA TARATIBU Wakati, Seiri inasaidia kuainisha vifaa gani vinahitajika, Seiton inamwezesha mtu kuamua jinsi gani vitatunzwa. Panga vitu kwa namna itakayorahisisha matumizi, kuviwekea lebo, ili iwe rahisi kukitafuta na kukirudisha. Matokeo yake Seiton yanahitaji kuwe na sehemu ya kila kitu na kwamba kila kitu kiwe kwenye sehemu yake. Seiton inafanya kuwe na mwisho wa kuwa na vitu zisivyokuwa na mahali pake. Mifano ya njia inayopendekezwa: Kwanza inabidi utambue sehemu zinazostahili kuweka kila kitu na kuweka vitu vyote na vyombo katika sehemu zake, ukiziandikia majina yake( labels) na kuziwekea alama zinazostahili. Kwa mfano unaweza kuweka vielelezo kwenye ubao wa vyombo, ili kurahisisha kujua mahali pa kila chombo. Unaweza kutumia rangi kuweka alama kwenye sakafu kwa ajili ya kutambulisha maeneo ya kazi, njia,sehemu za kuingilia, sehemu za kutokea, vyombo vya usalama, toroli au mkokoteni ulipo, na kutumia rangi za kutambulisha mabomba ya mvuke, maji, gesi, mifereji, n.k. Pia, unalazimika kuweka wazi na dhahiri onyo la maandishi, ujumbe, maelekezo katika sehemu stahili panapoonekana kwa urahisi. Pia, unaweza kutumia tahadhari au ishara kuepuka hali ya kutokuwa na mali (stock). Faida za SEITON: Inakuwa rahisi kutunza na kutoa vitu; unafanya makosa machache; muda wa kutafuta unapungua; mazingira ya kazi yanakuwa salama zaidi. 3. SEISO NG ARA Maana yake ni kuondoa uchafu, madoa, kinyaa, masizi na vumbi kutoka sehemu ya kazi. Inajumuisha kusafisha na kutunza vyombo na vifaa na kuvikagua kama vina walakini. Mifano ya njia zilizopendekezwa: Amua sehemu za kusafisha, mpangilio wa kusafisha, aina ya usafishaji, nyezo zinazohitaji; weka wazi ratiba ya usafi; wakati wa kusafisha angalia hali zenye kasoro (nati zilizolegea, mitikisiko, kelele zilizokithiri, joto la juu/nyuzi joto za juu, vifaa vilivyodondoka) na visahihishe. Faida za SEISO: Sehemu za kazi zinakuwa safi (hazina taka au madoa) ambao ni mwanzo wa ubora; muda wa matumizi wa vyombo unaongezeka; matukio ya kuharibika hupungua na ajali zinazuilika. 4. SEIKETSU SANIFISHA Seiri, Seiton na Seiso ni rahisi kufanya mara ya kwanza, lakini ngumu sana kudumisha, kwa sababu zinahitaji kuwa na mfumo wa utendaji. Kwa maana hiyo inabidi, kuhakikisha kuwa hatua yoyote ya usafi au mpangilio iliyofikiwa inadumishwa. Hali hii inahitaji kuwe na muundo wa kazi ambao utasaidia kufanya mbinu mpya za utekelezaji kubadilika na kuwa tabia. Njia zilizopendekezwa na mifano: Kila mmoja katika kampuni yako sharti atumie majina yaleyale ya vifaa, kiasi kilekile, muundo na rangi kwa ajili ya ishara, alama kwenye sakafu, n.k. Kufanikisha hili, unaweza kuandaa mwongozo kwa ajili ya 3Ss za kwanza na kufaya tathmini za mara kwa mara kwa kutumia orodha ya mambo ya kuangalia. Faida za SEIKETSU: Shughuli hurahisishwa; ustadi wa utendaji kazi huimarika; makosa huepukika. 5. SHITSUKE ENDELEZA Kuendeleza, pia kuna maana ya nidhamu. Unaonyesha jinsi gani umedhamiria kudumisha mpangilio mzuri na kutekeleza 3S za kwanza kama utaratibu wa maisha. Kunawahitaji wafanyakazi wako kuonyesha

45 35 Kuelewa Ubora kuvutiwa na utaratibu huo na kutokuwa na vizuizi vya kukubali mabadiliko. Kwa sababu hii huna budi kuwaelewesha na kuzitangaza 3S za kwanza. Njia zinaazopendekezwa/mifano: Toa habari za 5S, mabango, misemo, n.k. mameneja wakuu wako sharti waunge mkono Shitsuke kwa kutoa rasilimali na uongozi, na kutoa zawadi na kuwatambua wale wanaofanya vizuri. Faida za SHITSUKE: Huhamasisha tabia ya kukubaliana na sheria na taratibu za mahali pa kazi, hujenga hali bora mahali pa kazi. Kabla ya kuanza shughuli za udhibiti wa ubora (angalia swali la 4), ni muhimu kujenga hali ya ndani ya kampuni kuwa na utaratibu mzuri. Mfumo mzuri wa kushughulikia mambo ya ndani ndiyo msingi wa kuthibiti ubora. KWA TAARIFA ZAIDI Harper-Franks, Kathy. The 5S for the Office User s Guide. Published by MCS Media Inc., 888 Ridge Road, Chelsea MI 48118, United States (info@theleanstore.com). ISBN Can be purchased from Kitabu hiki kinatoa mwongozo kutumia fomu, sehemu za kufanyia kazi ambazo ni muhimu kuhakikisha kwamba mswada wa 5S umepangwa vema kutoka mwanzo na kuendelea kwa muda. Mwongozo huu unalenga jinsi kunga za 5S zinatumika ofisini na kwenye tarakilishi. The 5S Implementation Process in Detail. An article on 5S freely downloadable from the Lean Expertise website. MAREJELEO Hirano, Hiroyuki. 5S for Operators: 5 Pillars of the Visual Workplace. Created by The Productivity Press Development Team, Productivity Press, Portland, Oregon (service@productivityinc.com). ISBN Ho, Samuel K. TQM: An Integrated approach. ISBN A priced publication obtainable from Dr. Samuel Ho, Leicester Business School, De Montfort University, Leicester LE1 9BH, United Kingdom. SKHCOR@dmu.ac.uk

46 36 Kuelewa Ubora 11. Nitawahamasishaje wasaidizi wangu kufanikisha ubora? Hata kama utakuwa na mfumo mzuri wa ubora, hutaweza kufikia ubora uliotarajiwa kama wafanyikazi wako hawana hamasa/motisha. Moja ya misingi minane ya usimamizi wa ubora ndani ya ISO 9000 inasisitiza ushirikishwaji wa watu. Wafanyakazi katika ngazi zote ni chimbuko la shirika/kampuni na ushirikishwaji wao kamili hufanya uwezo wao kutumika katika kulinufaisha shirika. Unaweza kutumia baadhi ya mahitaji ya ISO 9001(angalia swali namba 29) kuwapa motisha wafanyakazi wako kwa: Kuhakikisha sera yako ya ubora inafahamika na kueleweka ndani ya shirika; Matumizi ya malengo mahususi ya ubora yanayopimika kwa kufikia mahitaji ya bidhaa yako; Kuainisha majukumu na mamlaka na kuyafahamisha ndani ya shirika lako; Kujenga uwezo wa wafanyakazi wako; Kutoa miundo msingi ya kutosha na mazingira ya kazi ya kufaa; Kuanzisha maboresho, k.m. kutekeleza mapendekezo/maoni ya wafanyakazi wako. Matokeo ya tafiti ya hivi karibuni juu ya motisha kama yalivyotolewa kwa muhutasari kwenye makala ya Nohria et al (2008), yanatoa njia ya mwelekeo wa mfumo mpya wa motisha kwa wafanyakazi. Watu hutilia maanani mambo manne ya mahitaji ya mhemuko wa msingi, au vichocheo vya kupata (k.m. hadhi katika jamii), mapatano (k.m. weka mahusiano na wafanyakazi- wenzako), kufahamu ( k.m. kuridhisha haja zetu), na kujilinda (k.m. sisi wenyewe, mawazo yetu na kujiamini dhidi ya matishio ya nje). Mfumo wa zawadi uliojengwa kwa misingi ya ufanisi ambao unatofautisha kati ya watendaji wazuri, wastani au wabaya na inalingana na malipo ya washindani wako inaweza kukidhi mhemuko wa kutaka kupata. Hali hii itaweka mazingira ambapo wafanyakazi wanahudumiwa kwa haki na usawa. Uzalishaji wa wafanyakazi huongezeka wakigundua kuwa mameneja wanawajali kuliko hata kama kulivyo na mabadiliko mazuri katika mazingira ya kazi. Utamaduni wa shirika unaojenga kuaminiana na urafiki kati ya wafanyakazi unathamini ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja, na kuhimiza kubadilishana mbinu nzuri zinazoweza kukidhi mahitaji ya mhemko wa mapatano. Njia bora ama nyenzo bora, vikundi vidogo vya wafanyakazi hukutana mara kwa mara kutatua matatizo, ambavyo vyote hivi, vinapelekea ongezeko katika ubora na ufanisi, na kupungua kwa gharama, ni njia nzuri ya kuendeleza utamaduni huu. Hali hii inawafanya wafanyakazi kukidhi haja zao za kijamii, mahitaji binafsi na kujisikia kufikia matarajio yao, ambazo ni hisia za kila binadamu, kama zinavyoainishwa katika madaraja ya mahitaji ya binadama kama ilivyofafanuliwa na Abraham Maslow. Uboreshaji wa kazi kwa kusanifu kazi za maana na kuongeza thamani kwenye shirika vinaweza kukidhi mhemuko wa haja ya kufahamu. Kazi zinaweza kusanifishwa kwa namna ambayo waamuzi wanafanya katika ngazi husika (k.m. maamuzi ya kimikakati yanafanywa na mameneja, wakati wasaidizi wanaruhusiwa kuamua masuala yaliyo katika ngazi ya utendaji bila kuingiliwa na mameneja). Mfano wa uwezeshaji ulifanyika katika kiwanda cha Corning ambapo wasimamizi wakuu walianzisha ushirikiano na wafanyakazi ambao waliwaita washiriki na waliwapa madaraka ya kufunga kiwanda endapo kitazalisha bidhaa zenye kasoro kama ilikuwa lazima ili kurekebisha au kutatua tatizo kabisa. Moja kati ya njia za kushughulikia mahitaji ya mhemuko wa kujilinda ni kuwa na haki, uaminifu na uwazi katika michakato ya shirika, kwa mfano katika kusimamia ufanisi na ugawaji wa rasilimali. Wafanyakazi hupenda kutumikia shirika linalosimamia haki, lenye malengo chanya na linaloruhusu wafanyakazi kutoa mawazo na maoni yao. Watahamasika katika mazingira ambayo hawaogopi kusema ukweli na pale ambapo wanalazimishwa kuyaficha matatizo yao. Utaratibu huu utakidhi moja ya misingi ya usimamizi mkuu katika falsafa ya W.E. Deming; yaani, kuondoa hofu mahali pa kazi. Mazingira haya yanaweza kuimarishwa kama mikakati ya haki katika maamuzi inafuatwa; utaratibu inabidi uwe katika misingi ya uchanganuzi wa taarifa kwa kutumia takwimu. Katika mazingira haya wafanyakazi hawatalaumiwa kwa matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa na usimamizi mkuu pekee yake. Mifumo mingine ya kutoa motisha kwa wafanyakazi hulenga fikira zawasimamizi wakuu. Kwa mfano, unaweza kuwahamasisha wafanyakazi kwa kuamini uwezo wa kuzalisha bidhaa bora. Douglas McGregor

47 37 Kuelewa Ubora alitoa nadharia mbili za usimamizi mkuu. Kufuatana the Nadharia ya X, inasema kuwa binadamu wa kawaida hapendi kazi na kuwajibika; anahitaji utaratibu wa kusukumwa. Nadharia ya Y inasema kuwa binadamu wa kawaida anapenda kazi kama mchezo na hukubali kuwajibika kwa kazi yake. Nadharia Y ikizingatiwa, unaweza kuwapa motisha wafanyakazi wako. Hata hivyo, inabidi ufahamu athari ya Pygmalion ikikolezwa na unabii wake wa kujitosheleza: kama unaamini kwamba wafanyakazi wako watazalisha kiasi kikubwa cha bidhaa zenye kasoro, watafanya hivyo kuzingatia kile unachowapa. Kwa kawaida kuna njia nyingi za kutekeleza mambo katika uzalishaji, na wafanyakazi wanazifahamu njia hizo, kwani ndio walio karibu na kazi yenyewe. Wanaweza kufanya hivyo kama unawapa hamasa, vifaa, mafunzo na motisha. Kadhalika, unaweza kuwapa motisha wafanyakazi wako kwa kuwafanya wafuate dhana ya majukumu matatu, ambapo kila mmoja wao anakuwa mteja, msindikaji na mgavi (angalia swali namba 7). Hali hii itazindua ari ya mgavi na mteja ndani ya shirika/kampuni, badala ya kuwafikiria wagavi na wateja wa nje. Pia, italeta hali ya kuridhika kati ya wafanyakazi wako, na kufanya watoe mchango wa kuridhisha kutoka kwa wagavi wao wa karibu. Kadhalika, kutoa huduma za kuridhisha kwa wateja wao wa karibu. Kwa kutekeleza dhana ya majukumu matatu utajenga uhusiano wa kuaminiana ndani ya shirika. Daniel Freeman na Jason Freeman. Tumia Kichwa Chako: Mwongozo wa Safari ya Fikra za Binadamu (Use Your Head: A Guided Tour of the Human Mind), wameorodhesha marupurupu manane muhimu kutokana na utafiti wao wa muda mrefu katika masuala ya motisha kwa wafanyakazi. Nayo ni kama ifuatavyo: Kazi inayokidhi mhemuko, utendaji, haja za kijamii na taaluma za wafanyakazi wako Kazi ambayo inaambatana na hadhi ya mfanyakazi wako na inalingana na mahitaji yake. A Mazingira ya kazi ambayo yanaendeleza wafanya kazi wako na kukuza ujuzi wao. Malengo magumu lakini yanayofikika. Zawadi za kweli ambazo wafanyakazi wanahitaji kwa kufikia malengo. Hisia ya kwamba mfanyakazi anatunukiwa kwa haki akilinganishwa na wakubwa wake. Mazingira ya kazi ambayo yanamfanya mfanyakazi ajitume zaidi. Wafanyakazi kuamini kuwa wasimamizi wao wakuu wana heshima, ni nyoofu na wa kuaminika. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Lester, John. ISO 9001 and Personal Quality Development. Chartered Quality Institute (CQI). Inaangazia utumizi wa ISO 9001 kwa maendeleo ya kibinafsi. Inaeleza jinsi tabia tofauti za watu, mahitaji yao, imani yao, maarifa na uongozi unaafikiana. Thareja, P. Each One is Capable (A Total Quality Organisation Thru People). (14 October 2009). FOUNDRY, Journal For Progressive Metal Casters, vol. 20, No. 4, July/August Available at SSRN: Karatasi hii inawaangazia wafanyakazi kama uti wa mgongo wa shirika. Inajadili jinsi mashirika yanaweza kuchangamanisha umairi wa wafanyakazi ili kufunika mianya ya uwezo binafsi wa watu. Thomas, Kenneth and Walter Tyman Jr. Bridging the Motivation Gap in Total Quality. Quality Management Journal, vol. 4, No. 2, January 1997, pp Makala haya yanaeleza kuwa TQM inahitaji kutilia mkazo kuwapa motisha wafanyakazi na sio tu kuwapa tuzo na kuwaadhibu. Motisha hii ni ile ya mfanyakazi kuridhishwa na kazi anayoifanya. Makala haya yanatoa mbinu chanya ya kuelezea motisha na pia kujadili athari ya kutumia na kutekeleza mbinu hizi.

48 38 Kuelewa Ubora MAREJELEO Feigenbaum, A.V. Spring into Action. Quality Progress, November Freeman, Daniel and Jason Freeman. Use Your Head: A Guided Tour of the Human Mind John Murray, ISBN Heller, Robert. Motivating People. Essential Managers Collection. Dorling Kindersley, International Organization for Standardization ISO 9000 Quality Management Systems. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at Nohria, Nitin and others. Employee Motivation: A Powerful New Model. Harvard Business Review, July-August 2008,

49 39 Kuelewa Ubora 12. Nifanye nini ili niweze kuwa sambamba na maendeleo yanayohusu ubora? Baadhi ya njia zinazoweza kufuatwa ili kuwa sambamba na maendeleo yanayohusu ubora zimeorodheshwa hapa chini. Mashirika mengi ambayo tunayapendekeza uwe mwanachama, hukusanya ada ndogo ya mwaka; yatakuwezesha kupata fursa ya kukutana na watu wenye malengo yanayofanana na kukuwezesha kuwa sambamba na maendeleo yanayotekea, na kwa hiyo kusaidia kuendeleza biashara yako. Shirika lako linaweza kuwa mwanachama wa Chama cha Ubora au taasisi ya nchi yako. Kama unatoka nchi kubwa, kuna vyama vingi vya ubora na unaweza kuamua kuwa mwanachama wa mojawapo (unaweza kupata taarifa ya vyama hivi kutoka katika shirika la viwango la nchi yako), Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda, vyama vya wauzaji bidhaa nje au mashirika ya kuendeeza biashara, tovuti ya Chama cha Ubora cha Marekani (American Society for Quality), Shirika la Ubora la Ulaya (European Organization for Quality) na Shirika la Ubora la Asia na Pasifiki (Asia Pacific Quality Organization) yanatoa taarifa za mashirika mengi ya ubora. Unaweza kuwa mwanachama wa shirika kama Chama cha Ubora cha Marekani au Taasisi Idhinishwa ya Ubora ya Uingereza (Chartered Quality Institute of the United Kingdom) ambazo ni komavu. Unaweza kutembelea tovuti zao kwani ziko wazi kwa watu wote. Unaweza kushiriki katika mikutano ya mwaka ya mashirika kama Chama cha Ubora cha Marekani na Shirika la Ubora la Ulaya. Unaweza kuchangia majarida kama Quality World (Chartered Quality Institute of the United Kingdom), Quality Progress (American Society for Quality), ISO Focus (International Organization for Standardization; nakala za PDF za Focus hupatikana bure kwenye tovuti ya Shirika la Viwango Duniani, ISO na katika vijarida vinavyochapishwa na mashirika ya viwango vya kitaifa. Kadhalika, unaweza kutembelea kurasa za jarida kama Quality Progress mtandaoni na kuweza kusoma baadhi ya makala bure. Kurasa za tovuti ya mashirika kama Juran Institute nazo zinaweza kufikiwa bila malipo kwa kupata habari, baadhi ya makala na chunguzi kifani. Tovuti ya ISO inayo sehemu ya Habari na vyombo vya habari ( News and Media ) ambayo hutoa taarifa kuhusu maendeleo katika masuala ya ubora, hasa kuhusiana na viwango vya kimataifa vinavyoandaliwa na machapisho ya viwango vipya. Makala na uchunguzi kifani kutoka magazeti ya ISO kama ISO focus (kutoka 2004 na kuendelea) na mifumo ya usimamizi mkuu ya ISO (ISO Management Systems) kutoka 2001 mpaka 2009 pia zinaweza kupatikana bure kutoka sehemu ya Habari na vyombo vya habari. Pamoja na hizi, kuna vipeperushi mbalimbali vya ISO, video na miongozo mbalimbali inayopatikana bila malipo. Ushiriki wa mara kwa mara katika warsha na mafunzo juu ya ubora yanayoandaliwa na vyama vya ubora, shirika la viwango, chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda, chama cha wauza bidhaa nje au mashirika ya kuendeleza biashara katika nchi yako zitakufanya kuwa sambamba na maendeleo yanayotokea katika sehemu ya ubora. Unaweza kununua nakala ya Kiongozi Cha Ubora cha Juran: Muongozo Kamili Kufikia Ufanisi wa Kutukuka (Juran s Quality Handbook: The Complete Guide to Performance Excellence) ambacho kwa sasa kiko katika toleo la sita, na kimekuwa kitabu cha marejeleo kwa zaidi ya miaka 50. Kinawakilisha njia mpya, tafiti na vifaa vinanavyohusiana na ubora. Toleo la tano (1999) la kitabu hiki kwa sasa linapatika mtandaoni (angalia: kwa taarifa zaidi, chini). Kwa taarifa zinazohusu ubora wa bidhaa fulani au mifumo, tafadhali rejelea maswali nambari 23, 24, 74 na 77. Unaweza kupata taarifa kuhusu masuala mengine yanayohusu ubora kama vile uwekaji viwango na ithibati na sayansi ya vipimo kwa kutembelea tovuti ya Shirika la Kimataifa la Sayansi ya Vipimo {International Bureau of Weights and Measures (BIPM)}, ambayo ina uhusiano na taasisi za sayansi ya vipimo, mashirika ya ithibati, mashirika ya viwango, mabaraza ya upimaji, n.k. Unaweza kutembelea tovuti ya DCMAS, mtandao wa Sayansi ya Vipimo, Ithibati na Uwekaji Viwango kwa nchi zinazoendelea.dcmas ilianzishwa na mashirika makuu ya kimataifa yenye wajibu wa kuimarisha miundo msingi ya kiufundi na kutoa huduma katika kuimarisha sayansi ya vipimo, uwekaji

50 40 Kuelewa Ubora viwango, na kutathmini ulinganifu ( pamoja na ithibati). Tovuti yake inatoa na inawasiliana na tovuti za mashirika haya. Unaweza kutembelea tovuti ya Huduma ya Viwango na Maendeleo ya Biashara (STDF, the Standards and Trade Development Facility), ari ya ushirikiano katika kujenga uwezo na ushirikiano wa kiufundi wenye lengo la kuongeza uelewa wa umuhimu wa masuala ya afya ya wanyama na mimea, kuongeza uratibu wa utoaji msaada katika masuala yanayohusu SPS na kutafuta rasilimali za kusaidia nchi zinazoendelea kuimarisha uwezo wao kufikia viwango vya SPS. Tovuti yake ina mahusiano na mashirika washiriki. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA Juran, Joseph and Blanton Godfrey. Juran s Quality Handbook, 5th ed. McGraw-Hill, Kazi ya marejeleo ya uhandisi dhabiti na usimamizi bora. Kitabu hiki kinazingatia upangaji na mbinu za udhibiti na matukio katika nyanja ya ubora. Quality Magazines. Tovuti hii inaelekeza kwa mbinu zingine za usimamizi bora. MAREJELEO American Society for Quality. Asia Pacific Quality Organization. Chartered Quality Institute. European Organization for Quality. International Bureau of Weights and Measures. Useful links at International Organization for Standardization. Juran Institute. Juran, Joseph and Joseph De Feo. Juran s Quality Handbook: The Complete Guide to Performance, 6th ed. McGraw-Hill Professional Network on Metrology, Accreditation and Standardization for Developing Countries (DCMAS), Quality Progress magazine. Standards and Trade Development Facility (STDF).

51 MAHITAJI YA KIUFUNDI

52

53 Mahitaji ya kiufundi Kiwango ni nini? Kiwango ni nyaraka inayoainisha sifa za bidhaa au huduma. Sifa hizi zinaweza kujumuisha usanifu, uzito, kiasi, utendaji, mahitaji ya kimazingira, mwingiliano katika utendaji, vifaa, michakato ya uzalishaji au utoaji huduma au itifaki/makubaliano ambayo yanaruhusu kompyuta au simu za mkononi kuunganika. Kiwango kinaweza kujumuisha au kushughulikia pekee maana ya maneno/istilahi, alama, ufungashaji, mahitaji ya kuweka lebo kulingana na bidhaa husika na mchakato au njia ya uzalishaji. Kuna viwango vya aina nyingine kama vile vinavyohusu upimaji, ambavyo vinashughulikwa chini ya swali la 1. Kwa kawaida, viwango vimegawanyika katika makundi mawili; viwango vya umma na binafsi. Viwango vya umma huandaliwa na kuchapishwa na taasisi zinazojulikana, kwa kawaida ni mashirika ya viwango. Kazi hii hufanyika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Kielelezo kinachofuata kinatoa mifano ya viwango vya umma na binafsi katika ngazi mbalimbali. Chanzo: Martin Kellermann, Afrika Kusini Angalizo: Majina kamili ya viwango na mashirika ya viwango yaliyoorodheshwa yameonyeshwa tena hapa chini na katika swali 14, ambalo linaelezea viwango binafsi. Viwango vya umma vikiandaliwa, mahitaji na matakwa ya wadau wengi hutiliwa maanani, yaani vinaandaliwa kwa makubaliano. Hii ina maana kuwa viwango vitapeleka ujumbe unaofanana kwa wagavi na walaji wote, na mambo mengine kama afya, usalama na masuala ya mazingira huwa yametiliwa maanani. Mifano hasa ya viwango vya kimataifa ni vile vilivyoandaliwa na Shirika la Viwango Duniani (ISO), Tume ya Ufundi wa Umeme ya Kimataifa (IEC), Muungano wa Mawasiliano Duniani (ITU), Tume ya Kodeksi Alimentarius (CAC), Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (IOE), Mapatano ya Ulinzi wa Mimea Kimataifa (IPPC-International Plant Protection Convention) na mengine. Viwango vya kikanda vinavyojulikana zaidi ni vile vilivyopatanishwa (EN) vya Jumuiya ya Ulaya, hata hivyo, kuna viwango vingine kama Viwango vya Kiserikali (GOST) vya Serikali ambazo zilikuwa chini ya Shirikisho la Kisovieti na viwango vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAS). Viwango vya kitaifa vimechapishwa na zaidi ya nchi 150 katika dunia nzima, na ni vingi sana kuviorodhesha hapa. Kati ya viwango hivyo ni vile vya taasisi ya kitaifa ya viwango ya Marekani (American National Standards Institute (ANSI), the Australian Standards (AS), British Standards (BS), viwango vya taasisi ya viwango ya Ujerumani (German Institute for Standardization (DIN), Indian Standards (IS), Korean Industrial Standards (KS) na Shirika la Viwango la Afrika ya Kusini (South African National Standards (SANS). Siyo kazi rahisi kusema idadi ya viwango vya umma duniani, lakini Pernorm, ambayo ni database ya kibibliografia, kwa mfano imeorodhesha viwango zaidi ya 700, 000, vikijumuisha viwango muhimu tu vya umma. Kwa hali hiyo viwango vya umma viko kila mahali katika dunia hii, vikielekeza mengi yale binadamu, bidhaa na michakato huingiliana pamoja na mazingira yao.

54 44 Mahitaji ya kiufundi Viwango huandaliwa na kamati za kiufundi zilizoanzishwa na mashirika ya viwango vya kitaifa, kikanda na mashirika ya viwango vya kimataifa, yakiwakilisha wadau wote. Jinsi viwango vinavyoandaliwa inaongozwa na agizo la ISO/IEO na mahitaji ya kiambatisho 3 cha mkataba wa WTO juu ya TBT(angalia swali 93). Kamati za kuifundi za kitaifa ni vyombo muhimu sana kwa kuhakikisha matakwa ya wagavi yanazingatiwa, lakini ina maana kwamba wagavi hao wanakuwa wajumbe wa kamati hizo na kushiriki kikamilifu katika vikao vyake. Kadhalika kwa kamati za kikanda na kimataifa. Viwango hupatikana kutoka kwenye mashirika ya viwango ya kitaifa, au kutoka katika mashirika ya kimataifa yaliyotajwa hapo juu. Vinaweza kuwa katika nakala halisi au katika diski (CD-ROM) au kwenye tovuti za mashirika ya viwango. Viwango vilivyoandaliwa na ISO na IEC vinahitaji hati za kunakili, kwa hivyo lazima zinunuliwe. Hata kwa viwango vya kitaifa, pamoja na vile vinavyochukuliwa (adopted) kutoka katika mashirika ya kimataifa au kikanda. Viwango vingine vya kimataifa kama vile kutoka CAC, OIML and mashirika kama hayo yanayohusu serikali mbalimbali, hupatikana bila malipo kwa kupakuliwa kutoka tovuti za mashrika/taasisi hizo. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Gausch, Luis and others. Quality Systems and Standards for a Competitive Edge The World Bank. =22561 Jarida hili lina mifano mingi juu ya aina ya viwango na mifumo ya ubora, umuhimu wake katika biashara na hali ilivyo Marekani. International Organization for Standardization and United Nations Industrial Development Organization. Fast Forward: National Standards Bodies in Developing Economies Inatoa maelezo muhimu kuhusu Viwango, jinsi viwango hivi vinaafikiwa na orodha ya viwango hivi. International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC Directives Parts 1 and 2, ISO, Maelekezo haya yanazingatia kunga na mbinu za kuandaa viwango vya kimataifa. Mashirika mengi ya viwango vya kitaifa hutumia mbinu hizi kama msingi wa kuandaa viwango vyao. International Organization for Standardization. 10 good things ISO standards do for SMEs. Obtainable from ISO or ISO members (list at Kijitabu kinachofafanua jinsi Mameneja wa biashara ndogo katika nchi kumi duniani wanaeleza jinsi ambavyo viwango vya ISO huchangia katika ufanisi wao. Maur, Jean-Christophe and Ben Shepherd. Product standards. In Jean-Pierre Chauffour and Jean-Christophe Maur (eds.), Preferential Trade Agreement Policies for Development. A Handbook. The World Bank Mapitio ya uhusiano kati ya viwango vya bidhaa na biashara, sheria za kuzingatia viwango vya ubora katika makubaliano ya biashara, na kwa upana uwiano wa mashirika na utangamano wao katika mikanda tofauti. United Nations Industrial Development Organization. Role of standards: A guide for small and medium-sized enterprises. Working Paper. Vienna, MAREJELEO International Organization for Standardization International standards and private standards. A freely downloadable brochure published by ISO. ISO 9000:2005, Quality management systems Fundamentals and vocabulary. Obtainable from ISO or ISO members (list at International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC Guide 2:2004, Standardization and related activities General vocabulary. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at Perinorm. World Trade Organization. Agreement on Technical Barriers to Trade, Annex 1: Terms and their definitions for the purpose of this Agreement, and Annex 3: Code of good practice for the preparation, adoption and application of standards,

55 Mahitaji ya kiufundi Viwango binafsi ni vipi na vina mchango gani katika biashara? Viwango vingi huandaliwa nje ya mfumo rasmi wa kitaifa, kikanda au kimataifa (angalia swali namba 130). Sababu za kuandaa viwango hivi ni nyingi na tofauti. Mashirika makubwa kama yale ya mnyororo wa ugavi huweka mahitaji kinaganaga kwa bidhaa watakazofanyia biashara, tasnia ya mafuta inafanya kazi dunia nzima kwa kutumia mahitaji ya kiufundi yanayofanana na watengeza magari wa Marekani wameandaa viwango vya jumla kwa ugavi wa vipuri (yaani viwango vya SAE-yaani Chama cha Wahandisi wa Magari). Wagavi wanashirikiana kupata faida kwa kusambaza bidhaa zinazofanana kiteknolojia. Kwa mfano, CD ya muziki ilikuwa kiwango cha pamoja cha Phillips na Sony na Viwango vya mfumo wa mawasiliano wa simu za mkononi duniani (GSM-Global System for Mobile Communications) zimeridhiwa na watengenezaji wachache. Kawaida viwango hivi hujulikana kama viwango binafsi. Baadhi ya viwango binafsi wakati mwingine hubadilika na kuwa viwango vya umma kama soko lake likikua au pale inapodhihirika kwamba kusudio la kuwanufaisha waliokianzisha halipo tena. Viwango binafsi huandaliwa na vikundi mahususi visivyo vya kiserikali, yaani mashirika ya kisekta ikijumuisha mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vilivyoungana, mashirika ya uhakiki au wauzaji rejareja wakubwa. Kwa kawaida, viwango binafsi hutayarishwa kwa nia ya kukidhi mahitaji ya wale walivyoandaa siyo kwa matumizi ya lazima kwa serikali. Kwa kawaida viwango binafsi vinahitaji uhakiki (angalia swali 75) la wagavi, kwa sababu kujitangazia ulinganifu /kukidhi viwango (angalia swali 57) kwa kawaida haikubaliki na soko. Kwa upande mwingine serikali haina sheria ya kulazimisha matumizi ya viwango binafsi; kwa sababu hiyo maamuzi ya mgavi kupata uhakiki huwa ni maamuzi ya kibiashara, kutegemea na faida itakayopatikana kwa kufanya hivyo. Viwango binafsi vinaweza kuwekwa kwenye makundi manne kama ifuatavyo: Viwango vya makundi katika miliki ya vyakula na kilimo cha bustani. Mifano ni taratibu za kilimo bora za Kundi la Wauza Rejareja wa Ulaya (European Retailer Group s good agricultural practice (GLOBAL G.A.P.) na viwango vya Umoja wa Wauza Rejareja wa Uingereza (the British Retail Consortium (BRC)-angalia pia swali 15. Viwango hivi ni muhimu kwa kuwa Jumuiya ya Ulaya ni wanunuzi wakubwa wa maduhuli ya chakula duniani. Viwango hivi vimetayarishwa na makundi yanayoshirikiana ya wauza rejareja wa Ulaya na Uingereza kwa nia ya kuhakikisha kuwa wagavi wao wanakidhi sheria zote za usalama wa chakula, pamoja na mahitaji ya ziada yaliyoandaliwa na mashirika ya rejareja, ikijumuisha wajibu kwa jamii. Kuna mifumo changamano ya uhakiki kwa ajili ya viwango hivi; na kama unahitaji kuuza nje chakula na mazao ya bustani katika nchi za Ulaya, uhakiki utakusaidia kuyafikia masoko hayo na kuongeza faida. Hata hivyo, uhakiki siyo lazima na si rahisi. Maamuzi ya kupata uhakiki ni ya kibiashara na yatategemea ushindani anaoutarajia muuzaji nje. Viwango binafsi vya wauza rejareja. Wakati mwingine huitwa viwango vya manufaa pekee; viwango binafsi vya wauza rejareja vina dhoruba kubwa kwa wagavi wa mnyororo wa rejareja wa makampuni ya kimataifa kama vile Carrefour, Metro, Tesco, Unilever and Wal-Mart. Kampuni hizi zimetengeneza viwango binafsi vya mazao ya kilimo na vyakula vilivyosindikwa kwa ajili ya ushindani au kulinda chapa; zinaweza kupanua viwango hivi katika maeneo mengine hapo baadaye. Wanatumia viwango kinaganaga kwa ajili ya manunuzi yao kwa sababu mbalimbali, kati ya hizo ni kama zifuatazo: Kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotoka kwa wagavi wao ziko katika hali itakayopunguza gharama na kuongeza faida; kuhakikisha wanauza bidhaa ambazo zinakidhi mahitaji ya kisheria (viwango vya umma, kanuni za kiufundi za SPS); kupunguza uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kisheria na wateja ambao hawakuridhika; kuhakikisha kuwa bidhaa zinakidhi uadilifu unaotegemewa na wateja wao kuhusu mambo kama mahitaji ya wanyama na ulinzi wa mazingira; na kuwashawishi wateja kuwa bidhaa zinazotolewa kwa mauzo ni nzuri kwa sababu ni salama au zina ubora wa juu kwa kukidhi viwango binafsi. Kama mgavi anataka kupeleka bidhaa kwa makampuni haya makubwa ya rejareja, sharti bidhaa zake zilingane na viwango vya manufaa pekee; matokeo ya viwango hivi vya manufaa pekee yanaweza kuwa makubwa mno. Kwa upande mwingine makampuni haya ya rejareja hutoa msaada maridhawa kwa SMEs kufikia viwango vyao. Hata hivyo, kufikia mahitaji ya mnunuzi mmoja, hakukuhakikishii kwamba mahitaji ya mnunuzi mwingine utayafikia.

56 46 Mahitaji ya kiufundi Viwango vinavyohusiana na ustawi wa mazingira na haki kwa jamii. Viwango binafsi ni muhimu katika masoko yaliyoendelea, ambako walaji wana shauku kuhusu masuala kama kufanyisha kazi watoto, ulinzi wa mazingira, biashara ya haki, vyakula vivyozalishwa kwa kubadilisha vinasaba na mambo kama hayo (pia angalia swali 17). Wanunuzi wanaweza kusisitiza kuwa bidhaa ambazo zitapelekwa kwenye masoko kama yao ziwe zimezalishwa kwa namna ambayo haitaathiri mahusiano yao na jamii na mazingira. Mapendekezo mwafaka hutolewa na mashirika kama Shirika la Kimataifa la Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability International) na kiwango chake cha SA 8000, kuhusu mwenendo mzuri katika jamii kiwandani, Baraza la Utumishi wa Misitu (Forest Stewardship Council (FSC) kwa viwango kwenye viwanda vya mbao na karatasi, na Shirika la Kimataifa la Uwekaji Lebo za Fairtrade {Fairtrade Labelling Organizations International (FLO)}. Kuonyesha ulinganifu, yaani kupitia uhakiki, wa viwango binafsi kwa hiyo ni muhimu kama utakuwa mshindani wa kweli. Viwango vya makundi katika sekta ya teknolojia ya juu. Kundi la nne la viwango ni muhimu katika sekta mahususi, kwa kawaida kwenye teknolojia ya juu; viwango vya GSM kwa tasnia ya simu za mkononi ni mifano ya viwango vya aina hii. Mahitaji ya ulinganifu na uhakiki wa viwango hivi binafsi vya kisekta ni hali ambazo zinapishana kama jinsi sekta zinavyotofautiana; kwa hiyo utafiti wa mahitaji ya sekta ni muhimu kabla ya kufanya maamuzi yoyote. Wanunuzi kama minyororo ya rejareja huainisha sifa wanazozitaka ziwe kwenya bidhaa watakazonunua; husema kuwa wanapofanya hivyo ndivyo wanavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wao. Hata hivyo, matatizo ya biashara ya kimataifa huzuka, hasa pale wanunuzi wakubwa kama wauzaji rejereja katika mataifa yaliyoendelea wanapokuwa na nguvu kubwa ya soko ukilinganisha na wagavi wadogo katika nchi zinazoendelea. Matatizo haya yanakuwa makubwa zaidi pale wanunuzi tofauti wanapotumia viwango tofauti vya kibinafsi kwa wagavi walewale, au panapokuwa na gharama kubwa kwa wagavi kudhibitisha kuwa wanakidhi viwango vya mnunuzi. Kwa kiasi fulani, kutokana na shauku za nchi zinazoendelea kwamba kuwa na viwango vingi vya binafsi kunaongeza gharama za ulinganifu, mashirika binafsi ya sekta ya rejareja yamechukua hatua ya kuunganisha viwango ya kampuni binafsi kuwa viwango tasnia nzima ya viwanda ili kuepuka matokeo mabaya katika biashara ya kimataifa. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Trade Centre Standards Map: Kielekezi cha Viwango kinapatikana katika tovuti ya ITC, programu iitwayo Trade for Sustainable Development (T4SD); ni jitihada ya ushirikiano ya kuhakikisha uwazi katika viwango na kuongeza vyanzo vya ukuaji na uzlishaji katika biashara. Export Quality Management Bulletin No. 86, Directory of marks and labels related to food safety, environmental integrity and social equity. British Retail Consortium (BRC). MAREJELEO Fairtrade Labelling Organizations International (FLO). Forest Stewardship Council (FSC). Global Good Agricultural Practices (GLOBALG.A.P.). International Organization for Standardization (ISO). International standards and private standards. A freely downloadable brochure. Social Accountability International (SAI). UNIDO. Making private standards work for you: A guide to private standards in the garments, footwear and furniture sectors. Vienna, World Trade Organization. World Trade Report 2005: Exploring the links between trade, standards and the WTO

57 Mahitaji ya kiufundi Viwango vipi vinahitajika katika kuuza chakula na mazao ya kilimo nje ya nchi? Mahuruji sharti daima zikidhi mahitaji ya kisheria yaliyowekwa na serikali ya nchi inayoagiza bidhaa kutoka nje (mahitaji ya lazima), na mahitaji ya kibiashra ya mnunuzi kutoka nje. Ufafanuzi wa kina wa kiwango fulani ni kazi ngumu kwa kuwa kuna bidhaa lukuki katika sekta ya chakula na kilimo. Bidhaa hizi lazima zitimize masharti ya SPS na kanuni za kiufundi na viwango vinavyobadilika kati ya nchi na nchi na kati ya sekta na sekta. Kufuatana na mkataba wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) juu ya SPS, nchi zinahimizwa kuandaa mahitaji yao kwa misingi ya viwango vya kimataifa, kwa mfano zile za Tume ya Kodeksi Alimentarius (CAC), OIE, IPPC. Tume ya Kodeksi ilianzishwa na Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuandaa viwango vya vyakula, miongozo na maandiko husika kama vile sheria/kanuni za kusimamia uendeshaji chini ya Programu ya Viwango vya Chakula ya Pamoja FAO/WHO. Malengo yake yakiwa ni kulinda afya za walaji, kuhakikisha kunakuwa na ufanyaji biashara wa chakula wa haki, na kuweka uratibu wa kazi yote ya kuandaa viwango vya chakula inayofanywa na mashirika ya kimataifa ya kiserikali au yasiyo ya kiserikali. Baadhi ya kamati muhimu za Kodeksi ni Codex Committee on Contaminants katika chakula, Codex Committee on Fish and Fishery Products, Codex Committee on Food Additives, Codex Committee on Food Hygiene, Codex Committee on Food Import and Export Inspection and Certification Systems, Codex Committee on Food Labelling na Codex Committee on Fresh Fruits and Vegetables. Nchi nyingi zimeuchukua mfumo wa Uchambuzi wa Majanga na Hatua Muhimu za Udhibiiti (HACCP) kama hitaji la lazima katika uandaaji wa viwango mbalimbali vya vyakula. Swali nambari 42 linaeleza maana ya Hazard Analysis and Critical Control Points (HACCP) na umuhimu wake kwa SMEs katika sekta ya chakula. Shirika la Afya ya Wanyama la Dunia (OIE) ni shirika la kiserikali linaloshughulikia uendelezaji wa afya ya wanyama duniani. Dhamira ya shirika hili pamoja na mambo mengine ni kusimamia biashara ya kimataifa kwa kuchapisha viwango vya afya kwa ajili ya biashara ya kimataifa ya wanyama na bidhaa za wanyama, kuhakikisha uwazi katika hali ya magonjwa ya wanyama kidunia na kukusanya, kuchanganua na kusambaza taarifa za kisayansi za maradhi ya wanyama. Mapatano ya Kimataifa ya Kulinda Mimea (IPPC) ni makubaliano ya kimataifa juu ya afya ya mimea, yenye lengo la kulinda mimea iliyolimwa/kupandwa na ile ya porini kwa kuzuia kuleta na kusambaza wadudu/wanyama waharibifu. IPPC inaziruhusu nchi kuchanganua hatari zilizopo kwenye hazina ya mimea waliyonayo na kutumia misingi ya kisayansi kulinda vilivyopandwa na mimea ya porini. Kamati ya Kifundi ya Bidhaa za Chakula (ISO/TC34) ya Shirika la Viwango la Kimataifa inashughulika na uandaaji wa viwango vya vyakula vinavyotokana na wanyama na mimea. Inajumuisha mnyororo wa chakula kuanzia uzalishaji wa msingi mpaka kuliwa/kutumiwa, pamoja na mbegu za wanyama na mimea. Inafanyakazi zinazohusu nahau, uchukuaji sampuli, njia za upimaji na uchanganuzi, sifa za bidhaa, usalama wa chakula na chakula cha mifugo na usimamizi wa ubora, na mahitaji ya ufungashaji, kuhifadhi na usafirishaji. ISO ambayo iliandaliwa na ISO/TC 34, inalinganisha mahitaji ya mifumo ya usimamizi wa usalama wa chakula. Swali la 44 linaelezea tofauti kati ya HACCP na ISO Swali nambari 45 linaelezea hatua zinazotakiwa kuweza kutekeleza ISO Ongezeko kubwa la matumizi ya viwango binafsi vya chakula na mazao ya kilimo likizingatiwa, Taasisi ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula (Global Food Safety Initiative (GFSI), taasisi isiyolenga kupata faida ilianzishwa chini ya sheria za Ubeligiji hulinganisha viwango vilivyopo na vigezo vya usalama wa chakula. Pia inadhamiria kuandaa njia ya kubadilishana habari katika mnyororo wa ugavi na kuongeza uelewa wa wateja na kuzirejea taratibu nzuri za rejareja. Ndani ya GFSI, uwekaji msingi wa kulinganisha ni njia ambayo utaratibu unaohusiana na usalama wa chakula unalinganishwa na mwongozo wa GFSI. Swali 22 linaelezea uhusiano kati ya mahitaji ya lazima yaliyowekwa chini ya sheria ya nchi zinazoagizwa kutoka nje na viwango binafsi ambavyo wanunuzi wanaweza kuweka. Kwa hali hii ni wanunuzi tu ndio wataweza kutoa taarifa juu ya viwango binafsi

58 48 Mahitaji ya kiufundi vitakavyotumika. Kwa kawaida mnunuzi pia atapenda kujua kama bidhaa inayouzwa itakidhi sheria za lazima za nchi; vinginevyo itakuwa vigumu kwa bidhaa kutoka nje kuingia katika nchi iliyoagiza. Swali 23 linatoa mwongozo wa mahali ambapo taarifa kuhusu mahitaji ya kiserikali katika nchi iliyoagiza bidhaa yanapatikana. Inaweza kuwa viwango vya vyakula kama vile kanuni za usafi na afya na viwango vya vikomo kwa mabaki ya madawa/mbolea za kilimo. Kadhalika kunaweza kuwa na zuio kuhusiana na kulinda afya ya wanyama na mimea (kutokuwa na wadudu au magonjwa fulani katika nchi inayouza nje ya nchi, kama kuna udhibiti katika mipaka ya kuingia katika nchi iliyoagiza, na kadhalika). Inawezekana kukawa na mahitaji machache au mengi ya kutilia maanani, hii itategemea aina ya chakula inayohusika na hali halisi ya nchi iliyoagiza. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 86, Directory of marks and labels related to food safety, environmental integrity and social equity. Will, Margret and Doris Guenther. Food Quality and Safety Standards, as required by EU Law and the Private Industry: A Practitioners Reference Book. 2nd ed GTZ. Marejeleo ya usimamizi bora wa vyakula, ikijumuisha mahitaji ya kampuni za serikali na za kibinafsi katika soko la muungano wa bara Ulaya kwa vitengo tofauti ya vyakula kama vile matunda na mboga. Codex Alimentarius Commission. MAREJELEO Færgemand, Jacob and Dorte Jespersen. ISO to ensure integrity of food supply chain. ISO Global Food Safety Initiative (GFSI). International Organization for Standardization (ISO). International Plant Protection Convention (IPPC). World Organisation for Animal Health.

59 Mahitaji ya kiufundi Viwango vipi vinatakiwa kuuza bidhaa za nguo nje? Kipindi cha muda kilichowekwa kwa shughuli za kuzalisha na kutengeneza nguo kikizingatiwa, ni muhimu kutofautisha shughuli zinazoweza kufanywa kwa urahisi na miradi midogo na ile ya kati (SMEs), na miradi ambayo inahitaji kiasi kikubwa cha fedha na teknolojia. Kwa nyuzi asilia shughuli zifuatazo zinahusika: (i) kupanda na kuvuna; (ii) uchambuaji wa pamba kwa kina au maandalizi mengine ya nyuzi ili zifae kwa usokotaji; (iii) usokotaji wa nyuzi kwenda katika nyuzi zilizosokotwa; (iv) ufumaji/useketaji wa nyuzi zilizosokotwa kwenda katika kitambaa; (v)utengenezaji wa bidhaa halisi (m.f. blauzi, kitambaa cha mezani); na (vi) uwekaji alama/nembo na ufungaji. Shughuli zinazohusu nyuzi sanisi (zilizotengenezwa na binadamu) zipo sawa, isipokuwa ukweli ni kwamba nyuzi hazitokani na wanyama wanaotakiwa kufugwa na manyoya yao kutumika. Bidhaa nyingi za nguo ni mchanganyiko wa nyuzi asilia na zilizotengenezwa na binadamu. Hatua za mwanzo za uzalishaji wa nyuzi, usokotaji, ufumaji na utiaji wa rangi (yaani nguo) zinahitaji mtaji mkubwa, hivyo mara nyingi hutengwa kwa shughuli kubwa za biashara na mashirika makubwa. Pia zipo chini ya mahitaji muhimu zaidi ya kiufundi kuliko hatua zinazofuata. Zao la mwisho (bidhaa), m.f. mavazi, vitambaa vya meza, leso, matakia (mto), kwa upande mwingine zina kazi kubwa, na ingawa wazalishaji wakubwa ni wa kawaida kabisa, kuna idadi kubwa ya shughuli za aina ya SME katika nchi nyingi zinazotengeneza mavazi na bidhaa nyingine zinazotengenezwa kutokana na nguo. Katika kila hatua ya mchakato wa shughuli, matokeo yanaweza kuhitajika kuendana na mahitaji ya kifundi na kutakiwa kupimwa na kuthibitishwa. Viwango vingi vya nguo na mavazi vya umma na binafsi (tazama swali namba 13 na 14) vimekuwepo kwa miaka mingi, lakini vichache tu, vingi vikihusiana na nguo vimetangazwa kuwa ni vya lazima. Hivyo, vichocheo vya soko vinaainisha kwa kiasi kikubwa viwango vipi ni vya lazima kutumiwa na watengenezaji wa mavazi na bidhaa nyingine zinazotengenezwa kutokana na nguo. Mahitaji ya kifundi ya kimataifa na mengineyo Shirika la Kimataifa la Viwango [The International Organization for Standardization (ISO)] limeasisi na kuchapisha mamia ya viwango vya kimataifa vya nguo. Hii inaweza kuonekana katika katalogi ya ISO iliyoko mtandaoni. Orodha hiyo ina msaada mkubwa, na kwa kurejea kwenye kamati kuu nne za ISO zilizohusika inaweza kupunguza taabu ya utafutaji zaidi. Hizi ni TC 38 Textiles, TC 94/SC 13 Protective clothing, TC 219 Floor coverings na TC 221 Geosynthetics. Licha ya uwepo wa viwango hivi vya kimataifa, vichache kama vipo vimepitishwa na nchi zote. Viwango vingi vya taifa na kanda vimebaki. Mashirika ya viwango ya taifa na binafsi pia yamechapisha makusanyo ya kina ya viwango vya nguo na bidhaa za nguo. Hii ni mifano miwili: Huko Uchina, msururu mzima wa viwango vipya vya nguo ulichapishwa mwaka 2008 kwa ajili ya utekelezaji, kuchukua nafasi ya viwango vingi vya nyuma vilivyopitwa na wakati. The American Society for Testing and Materials (ASTM) imechapisha vitabu viwili pamoja na mkusanyiko wa zaidi ya nguo 350 zilizohusika na njia ya upimaji ya ASTM, utendaji na vipimo vinavyoshughulikia matumizi ya nguo, utaratibu wa majina, tabia na mali. Baadhi ya mahitaji ya lazima ya kiufundi kwa ajili ya nguo na mavazi huko Ulaya yanatakiwa kuonekana katika muongozo wa EACH (EACH Directive) (tazama swali namba 27 kwa mjadala mzima). Mwongozo huu, kwa mfano, hauruhusu matumizi ya baadhi ya bidhaa katika utengenezaji wa nguo na mavazi kama vile azo dyes, organotin compounds, dimethyl fumarate substances na vingine kama hivyo. Huko Marekani, Kamati ya Usalama wa Bidhaa za mteja ya Marekani imepewa mamlaka ya kutekeleza mahitaji ya usalama kwa ajili ya bidhaa za nguo zilizoko sokoni, m.f. kuzuia moto na kupiga marufuku aina ya baadhi ya mavazi ya juu ya watoto ambapo inashirikisha masharti, kwa kuwa hizi zinachukuliwa kuwa na athari kubwa kwenye bidhaa. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwa wasambazaji kupata taarifa sahihi kuhusu viwango au kanuni za kiufundi kwa ajili ya soko lililodhamiriwa. Local NSB or TPO zinaweza kusaidia katika kutambua hayo (pia tazama swali namba 23). Mahitataji ya mnunuzi Mavazi na bidhaa nyingine zinazotengenezwa kutokana na nguo ni biashara kubwa, na mashirika makubwa ya uchuuzi na kampuni zilizobobea kibiashara yatakuwa na mitazamo yao wenyewe juu ya viwango vya bidhaa hizi.

60 50 Mahitaji ya kiufundi Hii inaweza kuhusiana na ubunifu wa mavazi, mahitaji ya kiufundi kwa ajili ya kitambaa na michakato ya uzalishaji, uwekaji alama/lebo na ufungaji na masuala mengine. Hii inatofautiana na ukosefu wa jumla wa mahitaji ya kiufundi ya lazima kwa ajili ya mavazi katika nchi karibu zote, tofauti kabisa na nguo ambazo ni lazima ziambatane na idadi ya kanuni za kiufundi. Muuzaji bidhaa nje kwa hivyo anahitajika kufahamu kabisa ni yapi mahitaji maalum ya mnunuzi, na vipimo vipi na serikali ipi ya uthibitisho inatahitajika. Pia, mahitaji ya lazima ya kiufundi kwa ajili ya nguo hayatakiwi kupuuzwa na watengenezaji wa mavazi. Watatakiwa kuhakikisha kwamba nguo, nyuzi na pembejeo nyingine za viwanda zinashabihiana na mahitaji ya lazima, vinginevyo, mavazi yaliyotengenezwa kutokana nazo hayataruhusiwa kuingia sokoni. Kwa kuzingatia tathmini ya ulinganifu, baadhi ya mashirika makuu ya uchuuzi yanafanya kazi na maabara zao wenyewe za upimaji wa nguo, wakati wengine wanategemea maabara huru zenye kibali na mashirika ya uthibitisho kwa ajili ya huduma hizi. Mashirika mengi ya viwango vya taifa katika nchi zinazotengeneza nguo yameanzisha maabara za nguo. Kuweka alama/lebo Baadhi ya nchi zina kanuni za kiufundi zinazohitaji uwekaji sahihi wa alama/lebo katika nguo. Marekani, kwa mfano, bidhaa yoyote ambayo kipekee inajumuisha nyuzi za nguo, au bidhaa ambayo angalau ina asilimia 80 ya kiasi cha nyuzi za nguo, zinatakiwa kuwekewa lebo inayoonyesha uwepo wa nyuzi, m.f. pamba 80%, polyester 15%, nylon 5%. Aina ya majina ambayo lazima yatumike pia yanaelezwa. Baadhi ya bidhaa ambazo zina nyuzi za nguo zimesamehewa na mahitaji haya, nazo ni pamoja na kijaruba(kifuko) cha tumbaku, viatu, tanga, glavu za oveni. Nchi za Ulaya zina mahitaji sawa ya nyuzi yanayotumika. Taarifa zingine ambazo ni lazima zitokee kwenye lebo zinahusiana na jinsi gani bidhaa za nguo zinatakiwa kutunzwa. Mifano ni zinaweza kufuliwa kwenye maji yenye joto kiasi gani; kama ni lazima zifuliwe kwa mashine tu; zinatakiwa kukaushwa kwa mashine au kunyooshwa, na kama ni hivyo kwa kiasi gani cha joto. Lebo/alama hizi zinatofautiana kidogo kutoka nchi moja hadi nyingine. Hivyo, picha halisi ni lazima ipatikane katika kila soko. Mifano ya kawaida imeonyeshwa katika mchoro hapo chini. Baadhi ya nchi (kwa mfano Uchina, Misri, Indonesia, Malaysia, Pakistan na Switzerland) hazina mahitaji ya taifa ya uwekaji lebo/alama na mahitaji ya mnunuzi ni lazima kuzingatiwa. Ukubwa/saizi za mavazi-clothing sizes Hakuna mfumo wa kimataifa unaotambulika kwa ajili ya ukubwa wa mavazi uliotekelezwa mpaka sasa, hivyo mavazi yanatakiwa kuwekwa alama mahsusi kwa masoko yanayodhamiriwa kupelekwa. Shati la mwanaume lililotiwa alama ya saizi15 Marekani litakuwa sawa na la shati ya saizi 38 katika bara la Ulaya. Kwa wanawake, 12 ya Marekani itatafsiriwa takribani mpaka 14 huko Uingereza na 42 Ufaransa. Katika nchi za Ulaya, viwango viwili vya lazima vimekuwa vikitumika tangu 2006 kuchukua nafasi ya mifumo mingi ya kitaifa, vinaitwa: EN : Masharti, maelezo na taratibu za vipimo vya mwili na EN : Vipimo vya msingi na sekondari. Kinyume na hayo, hakuna viwango vya lazima vilivyopo Marekani, na mlolongo mzima wa desturi na mazoea umekuwepo kwa miaka mingi, kuanzia na viwango vya Marekani vya ukubwa wa nguo ambavyo nafasi yake inachukuliwa taratibu na katalogi ya Marekani ya ukubwa wa nguo. Nchi chache zinatumia ipasavyo viwango vya ISO kwa saizi ya nguo. Hivi ni ISO 3635:1981 Saizi zilizoteuliwa za nguo Maelezo na taratibu za vipimo vya mwili, ISO 8559:1989 Uundwaji wa nguo na uundwaji wa mavazi na tafiti za sayansi ya vipimo na uwiano wa mwili wa binadamu vipimo vya mwili, na ISO/TR 10652:1991 mifumo ya viwango vya ukubwa/saizi ya nguo. Kufua kwa mikono tu na kupiga pasi/kunyoosha, joto la wastani la mashine ya kukaushia haviruhusiwi na kusafishwa kwa maji pia hakuruhusiwi. Ufungaji Ufungaji wa bidhaa za watu binafsi pamoja na ufungaji wa shehena za nguo na mavazi lazima ushabihiane na viwango vingi na kanuni za kiufundi. Tazama swali namba 2 kwa maelezo zaidi.

61 Mahitaji ya kiufundi 51 Viwango vya uthibitisho binafsi Inawezekana hakuna bidhaa iliyoathiriwa zaidi au kulengwa na mahitaji ya jamii, kimaadili na kimazingira kuliko nguo na mavazi. Hivyo, uthibitisho wa SA 8000 (uwajibikaji kijamii social accountability), Biashara ya haki/halali - Fairtrade (Masuala ya kimaadili ethical considerations) na WRAP (Masuala yahusuyo mazingira - environmental concerns) unaweza kuhitajika ili kuweza kukubalika au kupokelewa na soko. Haya yamejadiliwa kikamilifu katika maswali nambari 17 na 77. Aina chache kabisa za miradi ya ecolabelling zipo ambazo zinaweza kutumika kwenye nguo na mavazi (tazama pia swali nambari 78) na katika masoko machache hivi ni vigezo muhimu kwa mafanikio ya masoko. Miradi michache ya nyongeza na mipango maalum ya nguo na mavazi imeonyeshwa chini. Ipo mingi ya namna hii; hivyo msambazaji atatakiwa kufahamu vizuri sana ni ipi kati ya mifumo mingi inahusika na mtazamo wa soko katika soko la nje lililochaguliwa. Woolmark Woolmark ni moja kati ya alama/lebo nyingi za nguo zinazotambulika duniani. Inamilikiwa na Australian Wool Innovation Limited (AWI). Kampuni inayoshughulikia mpango wa kimataifa wa leseni kuhakikisha kwamba bidhaa yoyote inayobeba nembo ya Woolmark inatimiza vigezo madhubuti vya ubora wa sufu na utendaji makini. Kuwa mmoja wa wenye leseni, unatakiwa kuwasiliana na ofisi ya AWI iliyoko karibu yako (orodha ya ofisi zinaweza kupatikana kwenye tovuti za AWI). Ada ya maombi inatakiwa kulipwa, na bidhaa zinatakiwa kupimwa katika maabara za AWI kuhakikisha zinafikia viwango. Ikifanikiwa, leseni ya kutumia Woolmark itatolewa. Lebo na msaada wa vifaa hutolewa kwa waliopatiwa leseni. Viwango Hai vya Nguo Duniani. (Global Organic Textile Standard (GOTS) Viwango Hai vya Nguo Duniani {Global Organic Textile Standard (GOTS)} ni nguvu ya pamoja kati ya United States Organic Trade Association, Soil Association, International Association of Natural Textile Industry (IVN), na Japan Organic Cotton Association (JOCA). GOTS inatengeneza vigezo kwa ajili ya mlolongo mzima wa usambazaji kuanzia kuvuna malighafi, kupitia uwajibikaji wa kimazin gira na kijamii wa viwanda, mpaka uwekaji lebo/alama. Inatumika kwa bidhaa za nyuzi zilizosokotwa, vitambaa na nguo, pia inashughulikia uzalishaji, usindikaji, utengenezaji, ufungaji, uwekaji lebo, uuzaji bidhaa nje, uagizaji wa bidhaa nje na usambazaji wa bidhaa zote za nyuzinyuzi asilia. Kwa hivyo, ni udhibiti endelevu wa ubora na mfumo wa uthibitisho kutoka shambani hadi kabatini/kwenye rafu(field to shelf) GOTS inabeba vigezo vya kijamii vya kina: haitakiwi kulazimishwa au kutumikishwa kazi; wafanyakazi hawatatakiwa kukwamisha amana au nyaraka za utambulisho na waajiriwa wao; ajira za watoto haziruhusiwi; wafanyakazi wanatakiwa kuwa huru kuondoka baada ya taarifa sahihi; mazingira ya kazi yanatakiwa kuwa salama na ya kuzingatia afya. Mahitaji kwa ajili ya matibabu ya maji taka ni pamoja na vipimo na ufuatiliaji wa kiasi cha mashapo (takataka za chini), joto la majitaka na ph ya majitaka. Uthibitisho wa GOTS unatolewa tu kwa nyuzinyuzi asilia; haifanyiki hivyo kwa nyuzi sanifu. Taarifa zaidi juu ya GOTS, pamoja na orodha na viunganishi vya mashirika ya uthibitisho ambayo yamepewa kibali cha kutoa uthibitisho wa GOTS inaweza kupatikana kwenye tovuti yao ya GOTS. Kubadilishana kwa nguo - Textile Exchange Textile Exchange (zamani Organic Exchange) ni shirika lisilo la kutengeneza faida likiwa na mbinu ya kimataifa ya kuwa na wadau wengi ili kuboresha masoko katika mlolongo wa thamani ya nguo. Lina zaidi ya mashirika 230 ya kimataifa ambayo ni wanachama, likijumisha bidhaa na wachuuzi wengi maarufu sana duniani, ambao mauzo yao kwa ujumla ni kiasi kinachozidi dola za kimarekani bilioni 755 katika mwaka Kubadilishana kunajumuisha mlolongo mzima wa thamani, kutoka shambani au kwa mzalishaji kupitia viwandani hadi rejareja. Hivyo inajishughulisha na kutengeneza vyote; mahitaji na ugavi wakati huo huo. Inahitaji juhudi inayolenga kwenye bidhaa na

62 52 Mahitaji ya kiufundi mauzo ya rejareja. Utangazaji wa bidhaa unawapa wasambazaji motisha ya kuongeza uzalishaji na kusaidia kusawazisha ratiba za uzalishaji za kipindi kifupi na kirefu. Kubadilishana kunatoa mifano na vifaa kwa ajili ya mipango shirikishi, utatuzi wa matatizo, uboreshaji wa bidhaa na vyanzo, na elimu kwa wateja. Taarifa kuhusu shughuli za kubadilishana nguo inaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti yao. Mpango wa Pamba Bora - Better Cotton Initiative (BCI) Better Cotton Initiative (BCI) ni mpango mpya wa kufanya uzalishaji wa pamba kuwa bora kwa watu wanaozizalisha, bora kwa mazingira ambayo zinapandwa,na hatimaye bora kiujumla katika sekta nzima. Mwanzoni mwa awamu ya kwanza ya utekelezaji, lengo la BCI kijiografia liko kwenye kanda nne: Brazil, India, Pakistan na Magharibi na Afrika ya Kati (Benin, Burkina Faso, Cameroon, Mali, Senegal na Togo). Kanda hizi zinakabiliwa na utofauti wa hali ya hewa, ukubwa wa mashamba, kazi za kilimo na masuala ya kimazigira na kijamii. Pia BCI itatoa upenyo wa vifaa, zana na miongozo kuwezesha nchi yoyote kuzalisha pamba bora. Mfumo wa pamba bora utatengeneza mlolongo wa takwimu za shamba na ugavi/usambazaji na kuweka usimamizi imara, tathmini na taratibu za kujifunza. Mfumo utafanyiwa ukaguzi wa nje mwishoni mwa mwaka 2012 kutathmini kama umeleta matokeo na athari zilizokusudiwa. BCI inahitaji kujifunza kutoka kwenye miaka mitatu ya utekelezaji ili kufanya marekebisho yoyote muhimu kuboresha mfumo wa pamba bora na namna mpango unavyofanya kazi. Oeko-Tex Oeko-Tex (pia inaandikwa Őko-Tex) ni mradi mwingine wa uthibitisho wa nguo na mavazi unaolenga katalogi/orodha ya vitu vyenye madhara ambavyo vinaweza kudhuru afya ya binadamu. Katalogi hii huboreshwa mara kwa mara kwa kuzingatia matokeo ya kisayansi ya karibuni. Wajibu wa viwango vya Oeko-Tex 100 unachangiwa kwa pamoja na taasisi 17 za vipimo ambazo zinatengeneza Chama cha Kimataifa cha Oeko-Tex. Chama kina matawi ya ofisi katika zaidi ya nchi 40. Kiujumla zaidi ya vyeti vilivyotolewa kwa ajili ya mamilioni ya bidhaa tofauti tofauti za watu binafsi, na zaidi ya kampuni 6500 zilihusika duniani kote, viwango vya Oeko-Tex 100 vimekuwa moja ya lebo/alama bora maarufu za nguo zilizopimwa ili kuangalia vitu vyenye madhara. Mifano bora inapimwa na taasisi huru za Oeko-Tex, kwa mfano, kwa ajili ya kuangalia thamani ya ph, kiasi cha formaldehyde kilichopo na uwepo wa wadudu, madini mazito yanayochimbwa, chlorinated organic carriers na vihifadhi kama pentachlorophenol na tetrachlorophenol. Vipimo pia vinajumuisha kuangalia MAC Amines zozote katika azo dye stuffs na allergy-inducing dye stuffs. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Centre for the Promotion of Imports from developing countries (CBI). Website at Inatoa taarifa juu ya nguo na mavazi kwa kulinganisha na masoko ya Ulaya; inatoa taarifa ya masoko na taarifa kuhusu sekta mbalimbali, wasambazaji, wasaidizi, wanunuzi. United States Consumer Product Safety Commission. Inatoa taarifa na machapisho yanayohusiana na biashara na bidhaa zinazoleta madhara ya moto, umeme, kemikali, au mitambo au zinazoweza kudhuru watoto. US Consumer Product Safety Improvement Act. Guidance for Small Manufacturers, Importers, and Crafters of Children s Products. Inaelezea jinsi mahitaji ya uthibitisho yanavyoathiri wazalishaji wadogo, waagizaji bidhaa nje na watengenezaji wa bidhaa za watoto.

63 Mahitaji ya kiufundi 53 ASTM International. Australian Wool Innovation Limited (AWI). Better Cotton Initiative (BCI). MAREJELEO Global Organic Textile Standard (GOTS) certification. Hong Kong Trade Development Council (HKTDC). Textile Safety Update, International Organization for Standardization (ISO). Oeko-Tex. Textile Exchange. Wikipedia, Oeko-Tex Standard information. of signature, ISBN (Vol. 1) and ISBN (Vol. 2), United Nations Economic Commission for Europe (UN-ECE), Sea transport/usafiri wa majini au baharini International Maritime Dangerous Goods (IMDG) Code. ISBN , International Maritime Organization, IMO Publishing Service United Nations/Umoja wa Mataifa Mapendekezo kuhusu usafirishaji wa bidhaa hatari: Mapendekezo kielelezo. ISBN , United Nations. United Nations Publication Service, Palais des Nations, Geneva 10, CH =1211, Switzerland. Tel: , Fax: , Internet: KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: EN 13427:2004, Packaging Requirements for the use of European Standards in the field of packaging and packaging waste. Inapatikana kutoka kwa mashirika ya taifa ya viwango ya Wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka katika shirika la viwango la taifa lako. EN 13428:2004, Packaging Requirements specific to manufacturing and composition Prevention by source reduction. Inapatikana kutoka kwenye mashirika ya taifa ya viwango ya wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka kwa shirika la viwango la taifa lako. EN 13429:2004: Packaging Reuse. Inapatikana kutoka kwa mashirika ya taifa ya viwango ya wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka kwa shirika la viwango la taifa lako. EN 13430:2004, Packaging Requirements for packaging recoverable by material recycling. Inapatikana kutoka kwa mashirika ya taifa ya viwango ya wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka kwa shirika la viwango la taifa lako. EN 13431:2004, Packaging Requirements for packaging recoverable in the form of energy recovery, including specificationof minimum inferior calorific value. Inapatikana kutoka kwenye mashirika ya taifa ya viwango ya wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka katika shirika la viwango la taifa lako. EN 13432:2000, Packaging Requirements for packaging recoverable through composting and biodegradation Test scheme and evaluation criteria for the final acceptance of packaging. Inapatikana kutoka katika mashirika ya taifa ya viwango ya wanachama wa Umoja wa nchi za Ulaya, au kutoka katika shirika la viwango la taifa lako. International Trade Centre. Export Packaging website.

64 54 Mahitaji ya kiufundi Tovuti inayotoa bure nyaraka za ufungaji; inatoa tovuti zinazoelezea kanuni za kuweka alama na lebo katika nchi mbalimbali; inatoa marejeleo yanayohusu mazingira kwa bidhaa nyingi nyingi. MAREJELEO European Parliament and Council Directive 94/62/EC of 20 December 1994 on packaging and packaging waste. EUR-Lex, European Union. Green Dot. Wikipedia. International Air Transport Association (IATA). Dangerous Goods Regulations (DGR). International Civil Aviation Organization (ICAO). International Maritime Dangerous Goods (IMDG) Code. International Maritime Organization, International Organization of Legal Metrology (OIML). United Nations Recommendations on the transport of dangerous goods: Model Regulations Recommendations on the transport of dangerous goods: Model Regulations, ISBN United Nations Publication Service.

65 Mahitaji ya kiufundi Viwango gani vinahitajika na baadhi ya wanunuzi ili kushughulikia matatizo ya kijamii, mazingira na kimaadili? Matatizo ya kimaadili, mazingira na kijamii yanayotokana na miundo, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na yamejitokeza kwa nguvu sana miongo michache iliyopita. Wasambazaji hawawezi tena kupuuza matokeo haya, na katika masoko mengi ya bidhaa lazima waambatane na mahitaji ya kiufundi kuhusiana na masuala hayo. Mahitaji ya kiufundi yanaweza kuwa katika viwango vya kitaifa na/au binafsi, na wakati mwingine yamekuwa sehemu ya kanuni ndogo za kiufundi au sheria za SPS. Mifano kadhaa imejadiliwa hapa chini; Uwajibikaji kwa jamii Uwajibikaji kwa jamii umeelezwa katika viwango binafsi vya SA 8000:2008, vilivyochapishwa na taasisi ya Kimataifa ya Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability International) ya New York. Viwango hivi ni toleo la tatu la SA 8000, viwango ambavyo vinaweza kukaguliwa kwa ajili ya mfumo wa uhakiki, kuweka mahitaji ya hiari ambayo hufuatwa na wafanyakazi pahali pa kazi, ikijumusha haki za wafanyakazi, hali ya mahali pa kazi na mifumo ya usimamizi mkuu. Vipengele muhimu vya viwango hivi vina misingi sheria ya kitaifa ya haki za binadamu kama ilivyoainishwa na Umoja wa Mataifa na makubaliano ya Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO). Viwango vya SA 800 vinaweza kutumiwa pamoja na Nyaraka za Mwongozo ya SA 8000 (SA 8000 Guidance Document) kutathmini ukamilifu wa sehemu ya kazi. Nyaraka za Mwongozo zinasaidia kuielezea SA 8000 na jinsi ya kutekeleza mahitaji yake; inatoa mifano ya njia za kuthibitisha ulinganifu/ukamilifu; na kama rejea muhimu kwa wakaguzi na makampuni yanayotafuta uhakiki wa ulinganifu kwa SA Viwango hivi vinaweza kupakuliwa bila malipo kutoka kwenye tovuti ya SA 8000, lakini Nyaraka ya Mwongozo hulipiwa. Katika ngazi ya kimataifa ISO walitengeneza ISO 26000:2010, Mwongozo wa uwjibikaji kwa jamii (Guidance on social responsibility). ISO inatoa mwongozo kwa mashirika ya aina mbalimbali bila kujali ukubwa au lilipo, juu ya: Dhana, istilahi na fasili zinazohusiana na wajibu kwa jamii; Usuli, mwenendo na sifa za uwajibikaji kwa jamii; Misingi na taratibu zinazofanana na uwajibikaji kwa jamii; Masuala na hoja za uwajibikaji kwa jamii; Kuoanisha, kutekeleza na kuhimiza tabia zinazojali jamiii katika shirika na, kupitia sera zake na taratibu, ndani ya eneo lake la ushawishi; Kuwatambua na kuwashirikisha wadau; na Ahadi za mawasiliano, ufanisi na arifa zinazohusu uwajibikaji kwa jamii. ISO ni viwango vya mwongozo vya hiari na havitumiki kwa uhakiki, siyo kama ISO 9001:2008 (Usimamizi wa Ubora) na ISO 14001:2004 (Usimamizi wa mazingira), ambavyo vinaweza kutumiwa kwa uhakiki. Matatizo ya Maadili Biashara-haki (Fairtrade) ni kundi la viwango vinavyohusika zaidi na maadili katika biashara. Nia ni kuwapa wakulima (mwanzo katika mnyororo wa uzalishaji) katika nchi zinazoendelea mikataba yenye tija kama wanafanya biashara na masoko yaliyoendelea. Kuna makundi mawili tofauti ya Viwango vya Biashara; haki ambavyo vinahusika na aina mbili za wazalishaji wenye mapungufu. Kundi moja la viwango linahusu wazalishaji wadogo ambao wanafanya kazi pamoja katika ushirika au mashirika mengine yaliyo na muundo wa kidemokrasia. Kundi jingine linahusu kampuni zenye wafanyakazi walioajiriwa ambao walipewa ujira mzuri na wana haki ya kuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi. Viwango vya Biasharahaki, pia hushughulika na masharti ya biashara. Bidhaa nyingi katika mawanda ya viwango zina bei za Bidhaahaki, ambayo ni kima cha chini ambacho lazima kilipwe kwa wazalishaji.

66 56 Mahitaji ya kiufundi Wazalishaji hawa hupata fedha zaidi, nyongeza ya Biasharahaki ya kuwekeza katika jumuiya yao. Maelezo ya kina yanapatikana kwenye tovuti ya Fairtrade. Viwango binafsi vingi ambavyo viko katika misingi ya kisekta, hujumuisha matatizo ya kimaadili au masuala ya uwajibikaji kwa jamii kwa kiasi kidogo au kikubwa. Mfano halisi ni viwango vya Nguo Hai vya Kimataifa (Global Organic Textile Standard (GOTS), ambavyo vina mahitaji ya malipo bora kwa wafanyakazi na hujumuisha wafanyakazi wasiokuwa na mikataba katika viwango vya nguo (angalia swali 16 kwa ufafanuzi). Viwango vya mazingira Kundi la viwango vya usimamizi mkuu wa mazingira ISO inaweza kuwa familia yenye viwango vinavyofahamika zaidi vinavyoshughlikia masuala ya mazingira. Vinahitaji shirika linaloweza kuhakikisha kuwa, katika muundo wa kawaida usimamizi wa mfumo unaweza: Kuchunguza athari yake kwenye mazigira; kuweka ahadi ya ufanisi na michakato ya kutegemewa na katika kuzuia uchafuzi; Kuweka malengo na matarajio ya kuendelea kuboresha hadhi yake: na Kudhihirisha kuwa kuna ulinganifu na sheria zote za kitafa za mazingira. Kuna viwango vingi ambavyo vimechapishwa katika kundi la ISO 14000, na idadi inazidi kuongezeka, pamoja na kuwa uchapishaji umepungua kasi ukilinganishwa na muongo uliopita. Viwango vingi vinapitiwa upya kama ilivyo kawaida katika uandaaji wa viwango. Kwa sababu hiyo, wagavi wanatakiwa wakati wote kuhakikisha wanapata nakala (toleo jipya) iliyoko kwenye matumizi ya ISO Kielelezo kinachofuata kinaonyesha baadhi ya viwango, jinsi vinavyohusiana na namna vinavyo- hitajika katika mfumo mzima wa usimamizi mkuu wa mazingira. Mapitio ya viwango vyote yanapatikana katika chapisho la ISO The ISO Family of Standards, ambalo unaweza kulipakua kutoka kwenye tovuti ya ISO. Maswali 38 mpaka 41 yanatoa maelezo zaidi kuhusu mifumo ya usimamizi wa mazingira. Kuhusu masuala ya uhakiki na matatizo yanayohusiana na mazingira, angalia swali nambari 78.

67 Mahitaji ya kiufundi 57 * Mfumo wa usimamizi mkuu wa mazingira (Environmental Management System). Makampuni ambayo yanataka kudhihirisha ulinganifu yanahitaji kuhakikiwa chini ya ISO Kuna mashirika mengi yanayoweza kufanya uhakiki. Lakini ni bora kupata lile lenye ithibati kutoa uhakiki (angalia swali 71 kwa ufafanuzi zaidi kuhusu uchaguzi wa shirika la uhakiki). Manufaa ya kiuchumi ya ISO yanaongezeka polepole na makampuni yanayopata uhakiki wa ISO yanaongezeka; kama inavyoonyeshwa kwenye taarifa ya kila mwaka ya ISO ulimwenguni juu ya rejea ya vyeti vya mifumo ya usimamizi. Vilevile, kuna viwango vingi binafsi vinavyohusu masuala ya mazingira, na zaidi vinahusika na mipango ya uhakiki ambayo imeibuka katika nchi zilizoendelea. Mara nyingi zinahusisha masuala ya uwekaji lebo za kiekolojia (eco-labelling), angalia swali 78. Mifano halisi imeorodheshwa hapa chini: Greenguard. Greenguard wametayarisha mwongozo binafsi kuhusu uchafuzi wa ubora wa hewa ya ndani kwa misingi ya miongozo ya serikali na viwanda. Ulizinduliwa mwaka 2000 na Kampuni ya Sayansi ya Ubora wa Hewa (Air Quality Sciences (AQS) ya Atlanta, Marekani. Cradle to Cradle. Viwango hivi vinapelekea uhakiki wa bidhaa zinanazotokana na malighafi/pembejeo salama. Ina vipengele vya nishati, maji na wajibu kwa jamii. Katika kemia ya vifaa, cradle to cradle huelezea nguvu/uimara; viambato vyote katika bidhaa vinavyotambuliwa kwa kiasi cha mia katika milioni (100/ au 100ppm) na kuchunguzwa kufuata vigezo 19 vya afya ya binadamu na mazingira. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Trade Centre. Standards Map. Inatoa uwezo wa kuona takwimu za kielekitroniki kwenye tovuti ya ITC ambazo ni taarifa za kina kuhusu viwango binafsi na taarifa za kisomi, kisayansi na makala za utafiti juu ya masuala ya viwango binafsi katika minyororo ya thamani kimataifa. Ramani ya viwango iko katika mazingira yanayoingiliana ya kielektroniki na inawezesha kulinganisha mahitaji ya viwango binafsi katika ngazi tofauti za uchanganuzi, kutoka kwenye mambo ya kawaida ya jamii na mahitaji ya kimazingira mpaka vigezo kinaganaga na viashiria vya usalama wa chakula na utoaji wa kaboni, pamoja na haki za wafanyakazi na masuala ya jinsia. Cradle to Cradle. MAREJELEO Fairtrade Labelling Organizations International (FLO). FLO-CERT. GREENGUARD. International Organization for Standardization Environmental Management The ISO family of International Standards. International Organization for Standardization. ISO 26000:2010, Guidance on social responsibility. Obtainable from ISO or ISO members (list at International Trade Centre. Standards Map:

68 58 Mahitaji ya kiufundi 18. Kanuni za kiufundi ni nini? Bidhaa zikishindwa kukidhi mahitaji, zinaweza kuhatarisha afya na usalama wa watu, au kuwa na madhara kwa mazingira, au kuwahadaa wateja. Kushughulikia masuala haya, serikali zinatekeleza mambo rasmi ya udhibiti; mambo hayo ndiyo kanuni za kiufundi kama zilivyoainishwa katika Mkataba wa WTO-TBT (angalia swali 92). Kanuni za kiufundi sivyo viwango, lakini wakati mwingine hudhaniwa kuwa viwango kwa sababu zinaonekana kufanana (angalia swali 13). Kanuni za kiufundi zinaweza kuwa makabrasha ya kipekee, lakini yanaweza kuwa na msingi wa viwango au kuhusiana kimarejeo. Wakati viwango kwa kawaida huchukuliwa kama ni vya hiari, yaani wagavi wanaweza kuamua kuvifuata au la, kanuni za kiufundi kwa kawaida ni vya lazima, yaani kila mtu anabidi kuvitekeleza kufuatana na sheria. Kanuni za kiufundi ni nyaraka au sheria ambayo inaelezea sifa za bidhaa au michakato husika na njia za uzalishaji. Kanuni za kiufundi zinaweza kujumuisha au kulenga mahitaji ya istilahi, ishara, ufungashaji, kumaki na kuweka lebo kuhusiana na bidhaa, au njia ya uzalishaji. Katika hali zote, kanuni za kiufundi zitajumuisha vigezo vya kiutawala vinavyohitajika katika utekelezaji wake; kwa mfano kuainisha mamlaka itakayohusika, kuorodhesha mahitaji ya tathmini ya ulinganifu, na majukumu ya utafiti wa soko na utekelezaji wa maagizo katika hali kushindwa kukidhi mahitaji. Hatua za kuweka kanuni ya kiufundi mfano, zimeonyeshwa katika kielelezo hapa chini. Kanuni za kiufundi huandaliwa na kutekelezwa na wizara mbalimbali za serikali au mawakala wa kusimamia au wote, kutegemea taratibu na mfumo wa sheria za nchi husika. Kawanda hutayarishwa bila misingi ya makubalino/maridhiano, hata hivyo katika nchi zingine wadau hupewa nafasi ya kutoa maoni yao na kushawishi mwelekeo wa kanuni katika hatua ya rasimu. Kanuni za kiufundi hupewa majina tofauti. Katika nchi za Jumuiya ya Ulaya, zinaitwa Maagizo, Kanuni, Maamuzi. Katika nchi zingine huitwa Viwango vya lazima; wakati mwingine hata Mahitaji ya Lazima au kama Kanuni. Tatizo linalojitokeza linatokana na ukweli kwamba kanuni za kiufundi zimekuwepo kwa miongo mingi, baadhi hata zaidi ya miaka 70 au zaidi tukirudi nyuma, na kupata kanuni za zamani inaweza kuwa changamoto. Zinaweza kuwa matumizi yake yalishapitwa na wakati, lakini bado zina nguvu ya kisheria, kwa kwa hivyo ni lazima zifuatwe. Kanuni za kiufundi zinatumika kwa bidhaa zote za kutoka kiwandani na bidhaa za kilimo. Kwa hivyo bidhaa za kilimo zinaweza kutathminiwa kwa kutumia kanuni za kiufundi na sheria ya SPS (angalia swali 19). Mara nyingi hutokea bidhaa moja inalinganishwa na kutumia zaidi ya kanuni/shera moja. Kwa mfano, mashine ya faksi inaweza kutahminiwa kwa mahitaji ya usalama wa vyombo vya umeme, kuingiliwa na umemesumaku (EMI) na mahitaji ya uwezo wake wa kuunganika na mtandao wa mawasiliano wa nchi. Zaidi ya hapo kanuni zote tatu, zinaweza kusimamiwa na taasisi tatu tofauti.

69 Mahitaji ya kiufundi 59 Kutawanywa kwa taarifa za kanuni za kiufundi, upana/kutofautiana kwa mamlaka za udhibiti zinazohusika na kusimamia, na aina mbali mbali za ukaguzi, upimaji na uhakiki wa mahitaji-vyote hivi huchangia kwenye shida wanazozipata wagavi kupata habari na kuhakikisha ulinganifu na mahitaji yote ya bidhaa za kuuza ndani na je ya nchi. Ingawaje mkataba wa WTO juu ya TBT unajaribu kuhakikisha kuwa kanuni za kiufundi hazileti vikwazo visivyolazima kwa biashara na vinalinganishwa na viwango vya kimataifa kwa kiasi kinachokubalika; ulimwengu bado mbali kufikia lengo hilo. Kwa hiyo wagavi wanalazimika kuhakikisha wanapata taarifa sahihi juu ya bidhaa zao kwa ajili ya masoko wanayoyalenga, kabla ya kuuza na kusafirisha. Hii itaepusha matarajio yao kutofikiwa, kuingia gharama ambazo hazikutegemewa au hasara (angalia swali 21) KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: European Commission. Guide to the Implementation of Directives Based on the New Approach and the Global Approach guide/guidepublic_en.pdf Kwa ujumla mwongozo huu unazingatia maelezo chanya juu ya udhibiti kwa jumla mbali na kuzingatia na kueleza mbinu mpya zinazotumika na muungano wa bara Ulaya. (World Trade Organization. Agreement on Technical Barriers to Trade Inawasilisha ujumbe kuhusu makubaliano ya WTO na TBT na makubaliano mengine ya WTO na pia kupeana ufafanuzi wa makubaliano haya na kupeana ufafanuzi wa migogoro iliyosuluhishwa na inayoendana na makubaliano ya biashara. MAREJELEO Physikalisch-Technische Bundesanstalt and International Trade Centre. Technical Regulations, Recommendations for their Elaboration and Implementation, Guide 1/2009, Alex Inklaar, World Trade Organization Technical Barriers to Trade Gateway. World Trade Report 2005: Exploring the links between trade, standards and the WTO,

70 60 Mahitaji ya kiufundi 19. Sheria za afya ya wanyama na mimea zikoje? Sheria za Afya ya Wanyama na Mimea (SPS) zinatoa mahitaji yaliyowekwa na serikali kuhusu bidhaa ili kupunguza au kudhibiti hatari zinazoweza kuathiri afya ya binadamu, wanyama na mimea. Sheria nyingi za SPS zinahusu kuhakikisha usalama wa chakula, na kulinda afya za wanyama na mimea zaidi ya wadudu/wanyama waharibifu na magonjwa. Sheria za afya ya wanyama zinashughulikia ulinzi wa maisha na afya za binadamu na wanyama; sheria za afya ya mimea zinajihusisha na ulinzi wa maisha au afya mimea. Kazi inayofanywa na serikali kuzuia kuingia kwa wadudu/wanyama waharibifu wa kigeni kwa kawaida huitwa usalama wa uhai (biosecurity). Kufuatana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), usalama wa uhai ni mkakati na njia ya uwiano inayojumuisha sera na taratibu za kanuni za uchunguzi na kusimamia hatari zinazoweza kujitokeza katika sekta za usalama wa chakula,maisha na afya ya wanyama, na maisha na afya ya mimea, pamoja na matukio yanayoweza kuathiri mazingira. Makubaliano ya WTO juu ya utekelezaji wa Sheria ya SPS yanaainisha kuwa sheria ya afya ya wanyama na mimea inatumika kwa: Kulinda maisha na afya za binadamu kutokana na vitu vinavyoingia, vichafuzi, sumu au vimelea waletao magonjwa katika chakula na vinywaji, au kutokana na magonjwa ya wanyama na mimea au bidhaa zake au kutoka kwa wadudu/wanyama waharibifu; Kulinda maisha na afya ya wanyama kutokana na hatari zinazoweza kutokea kutokana na vitu vinavyoingia, vichafuzi, sumu au vimelea waletao magonjwa kwenye chakula cha wanyama, au magonjwa ya wanyama na mimea, au wadudu/wanyama waharibifu au vimelea waletao magonjwa. Kulinda maisha au afya ya mimea kutokana na wadudu/wanyama waharibifu, magonjwa au vimelea waletao magonjwa; na Kulinda au kupunguza uharibifu mwingine wowote katika nchi kutokana na kuingia, kuimarika au kusambaa kwa wadudu/wanyama waharibifu. Sheria vilevile inajumuisha hatua zinazochulkuliwa kulinda afya ya samaki na wanyama wa porini, misitu na mimea mingine. Vipengele vya mazingira vya kulinda haki za walaji au maisha ya wanyama nje ya waliotajwa hapo juu haviko katika jumuisho la sheria ya SPS. Sheria inajumuisha sheria zote husika, amri/maagizo, kanuni, mahitaji na taratibu. Hivi vinaweza kuelekeza vigezo vya mwisho wa bidhaa; michakato na njia za kuzalisha; upimaji, ukaguzi, taratibu za uhakiki; mahitaji namna ya kushughulikia guarantine kwa usafirishaji wa wanyama na mimiea, na kwa vifaa vya kulinda uhai wakati wa safari. Kadhalika, zinaweza kuwekewa majukumu ya lazima kuhusiana na njia za kitakwimu, uchukuaji sampuli na njia za kutathmini hatari. Mwisho, wanaweza kuelezea mahitaji ya ufungaji na kuweka lebo kuhusiana na usalama wa chakula. Usimamizi wa serikali katika kutekeleza viwango vya vyakula kuhakikisha usalama wa chakula, na udhibiti wa usalama wa uhai unaotekelezwa katika mipaka ya kimataifa kuzuia wadudu/wanyama waharibifu wa kigeni ni mifano dhairi ya Sheria ya SPS. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Trade Centre. Quality & Standards. International Trade Forum Magazine, Issue 3, 2010, Swala la Ubora na Viwango inaangazia viwango vya ubora katika udhibiti wa kiufundi, mikakati ya SPS na majukumu yao katika kupigia debe mauzo ya nje kutoka nchi zinazoendelea. Inapatikana katika lugha ya Kingereza, Kifaransa na Kispanyola. Standards and Trade Development Facility (STDF). Muungano wa kuongeza nafasi ya kujijenga na ushirikiano wa kiufundi zinalenga kuongea hamasisho juu ya umuhimu wa kuzingatia usafi, kuongeza uhusiano kwa usaidizi wa SPS na kuchochea rasili mali ili kuwezesha uwezo wa nchi zinazoendelea kuafiki viwango vya SPS. (pg 72)

71 Mahitaji ya kiufundi 61 World Trade Organization. Sanitary and Phytosanitary Measures. Tovuti hii inatoa maelezo mengi yakumwezesha msomaji kuelewa zaidi maana ya makubaliano ya SPS na kusababisha utekelezaji wake kupitia wanachama wa WTO. MAREJELEO Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO). World Trade Organization. Sanitary and Phytosanitary Measures.

72 62 Mahitaji ya kiufundi 20. Kuna uhusiano gani kati ya viwango, kanuni za kiufundi, na sheria ya SPS? Istilahi ya viwango, kanuni za kiufundi na sheria ya SPS mara nyingi ni chanzo cha utatanishi. Matumizi ya kawaida ya misemo hii katika nchi nyingi inaweza ikutofanana na maana ya kisheria iliyoko katika Sheria za Vikwazo vya Biashara vya Kiufundi (TBT) na SPS. Kwa mfano, nchi nyingi zina viwango vyake vya chakula ambavyo sharti zifuatwe, lakini Sheria ya TBT inasema ulinganifu na Viwango (kama ilivyoainishwa kwenye Sheria) siyo lazima. Zaidi ya hayo, neno hilo lina maana nyingine katika Sheria ya SPS na TBT. Kuelewa vizuri mahusiano kati ya maneno/misemo kwa muktadha wa Sheria za WTO, ni muhimu kuzingatia sheria kwa utenganisho. Inafaa kufahamu kwamba Sheria TBT na SPS hukamilishana. Sheria ya SPS inahusu mahitaji rasmi yaliyoainishwa chini ya sheria hiyo, yanahusu udhibiti wa hatari fulani kwa maisha na afya ya binadamu, wanyama na mimea (angalia swali 190). Yaliyomo kwenye Sheria ya SPS ni vikwazo kwa biashara, lakini hayamo kwenye Sheria ya TBT. Sheria ya TBT inahusisha vikwazo vya kiufundi vya biashara ambavyo havimo kwenye Sheria ya SPS. Tofauti kati ya Sheria ya SPS na TBT Sheria ya SPS kawaida inashughulikia: Vichafuzi vinavyoingia katika chakula au vinywaji Vichafuzi/uchafu kwenye chakula au vinywaji Sumu kwenye chakula au vinywaji Mabaki ya madawa ya mifugo au madawa ya wadudu/mashambani katika chakula au vinywaji Uhakiki: usalama wa chakula, afya ya wanyama au mimea Njia za usindikaji na kwa mtazamo wa usalama wa chakula Mahitaji ya uwekaji lebo kuhusiana na usalama wa chakula Quarantine za mimea na wanyama Matamko kuhusu maeneo yasiyokuwa na magonjwa au wadudu/wanyama waharibifu Kuzuia magonjwa au wadudu/wanyama waharibifu kuenea kwenye au ndani ya nchi Mahitaji mengine kuhusu maduhuli (k.m. maduhuli ya toroli zinazotumiwa kusafirishia wanyama); Chanzo: Shirika la Biashara Duniani(WTO). Sheria ya TBT kkawaida inashughulikiia: Uwekaji lebo kuhusiana na vilivyomo au ubora wa chakula, vinywaji na madawa Ubora wa vyakula vibichi Ujazo, muundo na muonekano wa kifungashio Ufungashaji na uwekaji wa lebo za kemikali hatari na vitu vyenye sumu, viuadudu na mbolea Kanuni juu ya vifaa vya umeme Kanuni juu ya simu zisizo na mkonga, vifaa vya radio,n.k. Kuweka lebo kwenye nguo Kupima magari na vifaa vyake Kanuni juu ya meli na vifaa vyake Kanuni za usalama vidude vya kuchezea watoto Chini ya Sheria ya TBT kanuni za kiufundi ni chapisho/kabrasha linaloeleza sifa za bidhaa au michakato inayohusika na njia za uzalishaji. Utekelezaji wa kanuni hizi ni wa lazima, maana yake ni kwamba ni sheria ya lazima kufikia masoko. Wajibu wa kuandaa na kutangaza na kusimamia utekelezaji wa kanuni za kiufundi na Shera ya SPS ni wa Serikali na vymbo vyake. Mwisho wake, majukumu haya huwekwa kwenye mfumo wa sheria na maamuzi ya jinsi yatakavyotelezwa ni kwa ridhaa ya Serkali. Sheria ya TBT inafanana na makabrasha yaliyotajwa hapo juu lakini siyo kwa matumizi ya lazima kama viwango. Viwango ni mapendekezo; watumiaji wa viwango wanaweza kuamua kuchagua vile wanavyovitaka na kama matumizi yake yataleta manufuu ya gharama. Majukumu ya kuandaa viwango ni ya mashirika ya viwango. Udhibitisho wa viwango ni kazi ya mabaraza au bodi za mashirika ya viwango, ambayo kufuatana na utendaji bora kimataifa, zinajumuisha wawakilishi wa wadau husika, ikijumuisha serikali. Mchakato wa kuandaa viwango hufuata misingi iliyokubalika kimataifa, kama vile uwazi, kuafikiana na kuwa bayana. Kama ilivyokwishaelezwa, Sheria ya SPS ni mahitaji yaliyowekwa na Serkali kudhibiti aina fulani ya hatari kwa maisha na afya ya binadamu, wanyama na mimea. Sheria ya SPS imeelezwa katika Sheria ya WTO juu ya matumizi ya Sheria ya SPS ambayo ilianza kutumika 1995.

73 Mahitaji ya kiufundi 63 Sheria inasisitiza haki ya wanachama wa WTO kuitumia sheria kwa ulinganifu wa makubaliano. Sheria ya SPS inawaomba wanachama wa WTO kuandaa sheria zao za SPS kwa misingi ya viwango, kanuni na mapendekezo yaliyoandaliwa kimataifa; hasa na CAC, IOE na IPPC. Hizi ni taasisi za kimatafa za umma zinazoshirikisha nchi wanachama kuandaa kanuni zinazojumuisha viwango vingi ambavyo vinatarajiwa kutekelezwa (lazima) na nchi. Kwa hivyo, kuna uhusiano mkubwa kati ya viwango, kanuni za kiufundi na Sheria za SPS, lakini kuna tofauti za msingi hasa katika utekelezaji na uandaaji wake. Yaliyomo katika kanuni za kiufundi na sheria ya SPS yanaweza kufanana sana na yale ndani ya viwango. Hata wakati mwingine yaweza kuwa sawa, kwa sababu makubaliano ya WTO, SPS na TBT huhitaji kanuni na sheria ya SPS kuwa na msingi wa viwango vya kimataifa kama vipo. Hata hivyo, nchi zina haki, ya kutofautiana na viwango vya kimataifa kama sababu za kufanya hivyo zipo na zimewekwa wazi. Katika nchi zingine, kiwango cha kitaifa kinaweza kutangazwa kuwa cha lazima, na kwa hivyo kuongeza hadhi ya kanuni za kiufundi. Hizi zinafahamika kama viwango vya lazima au wakati mwingine kama sheria. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: European Commission. Guide to the implementation of Directives Based on the New Approach and the Global Approach, Makala haya yanajadili kwa kina mbinu kinyume cha a marejeleo ya kujumuisha viwango vya Ulaya katika mielekeo mipya. International Organization for Standardization. Using and referencing ISO and IEC Standards for technical regulations, September Makala haya yanaelezea kwa kina manufaa na mbinu za kuandika marejeleo ya viwango vya ISO na IEC kwa njia ya moja kwa moja au kinyume. World Trade Organization Understanding the WTO Agreement on Sanitary and Phytosanitary Measures Utangulizi kwa mkataba wa WTO ulio na maswali na majibu. Agreement on Technical Barriers to Trade, Inatoa ujumbe kamilifu juu ya mapatano ya WTO TBT pamoja na tafsiri za jumbe hizi na matumizi ya Viwango katika kuendeleza mikakati. MAREJELEO Physikalisch-Technische Bundesanstalt and International Trade Centre. Technical Regulations: Recommendations for their Elaboration and Implementation. Guide 1/2009, Alex Inklaar, World Trade Organization. World Trade Report 2005: Exploring the links between trade, standards and the WTO

74 64 Mahitaji ya kiufundi 21. Je, viwango kanuni za kiufundi na sheria ya SPS ni vikwazo vya biashara na jinsi gani vinaweza kuepukika? Vikwazo vya biashara ni sheria zilizoko katika nchi ambayo unataka kupeleka bidhaa, ambazo zinafanya upelekaji kuwa mgumu au usiowezekana kabisa kuuza katika nchi hiyo. Zinaweza kuwa za aina mbalimbali, lakini kwa kawaida ziko katika makundi mawili: vikwazo vya forodha na vikwazo visivyo vya forodha. Kanuni za kiufundi na sheria ya SPS ziko katika kundi la visivyovya forodha. Kazi ya msingi ya sheria za WTO, TBT na SPS ni kupunguza athari mbaya katika biashara kutokana na kanuni za kiufundi na sheria ya SPS kama vikwazo kwa biashara kwa kuruhusu vizuizi halali, lakini kukataza ambavyo havina msingi wa maana. Pale ambapo kanuni za kiufundi na sheria za SPS za nchi inayoagiza zinakubaliana na Sheria za TBT na SPS, wauza nje wanaotafuta masoko hawana uchaguzi, bali kukidhi mahitaji. Biashara inaweza kushindikana pale viwanda vya nchi inayoendelea havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya kiufundi yaliyowekwa na nchi iliyoagiza kwa bei yenye manufaa. Kadhalika, hitaji la SPS lililowekwa na nchi iliyoagiza kwa shabaha ya kulinda usalama wa uhai, kwa mfano katazo la kuingiza bidhaa za wanyama kutoka nchi zinazofahamika kuwa na hali mbaya ya ugonjwa fulani wa wanyama. Hali hii itakwamisha biashara na nchi hizo. Viwango vya hiari vinaweza kuwa vikwazo vya biashara kama wanunuzi katika nchi inayoagiza hawako tayari kununua bidhaa ambazo hazikidhi kanuni za ndani zilizoandaliwa na shirika la viwango. Wauza bidhaa nje wanaweza kuamua kufuata au kutofuata viwango vya hiari, kwa vyovyote vile lazima wakidhi mahitaji ya mnunuzi. Toka enzi za makubaliano ya Jumla ya Forodha na Biashara (GATT), wapatanishi wameweka mikataba na nchi wanachama wa GATT na baadaye na WTO kuondoa vikwazo vya biashara vinavyotokana na viwango, kanuni za kiufundi na sheria ya SPS. Dhana ya kulinganisha viwango kimataifa, ndiyo msingi wa mikataba hii, ambayo inaziomba nchi kuvikubali viwango vya kimataifa kuwa vya kitaifa. Kanuni za kiufundi na sheria za SPS sharti ziwe katika misingi ya viwango vya kimataifa au vilivyofanywa vya kitafa. Kadhalika, inahusu viwango vya mfumo wa kutahmini ulinganifu (angalia swali 55) inayotumika katika kuthibitisha ulinganifu wa bidhaa au huduma na mahitaji ya kimataifa. Makubaliano kati ya nchi kutambua matokeo ya ukaguzi, upimaji na uhakiki, hata kama kuna tofauti katika matumizi kati ya nchi, inasisitizwa na mikataba ya WTO, mradi mifumo hiyo tofauti inaleta matokeo yanayofanana katika ubora wa bidhaa. Kutatua vikwazo vya biashara kutatokea ikiwa Wanachama wa WTO watang amua fursa walizonazo kushawishi vipengele ambayo vinabana biashara katika nchi zinazoagiza. Uwazi na ukweli uliopo chini ya sheria za TBT na SPS unaruhusu wanachama wa WTO kuonyesha mapema maoni ya au nia yao ya kupendekeza mabadiliko katika kanuni/vipengele na kuandaa na kupeleka mapendekezo ambayo yatachkuliwa na nchi inayotoa taarifa. Kwa hivyo kila nchi ina wajibu wa kufuatilia mapendekezo yanayotolewa ambayo mara kwa mara husambazwa na ofisi ya ukatibu ya WTO, na hatua za haraka huchukuliwa kutokana na taarifa hiyo ambayo inaweza kuathiri biashara yake( angalia pia swali 25). Shirika linalopewa kazi ya kufuatilia matangazo hayo, sharti liwe karibu na mashirika ya sekta binafsi yanayowakilisha wauza bidhaa nje kwa nia ya kuwapa taarifa mpya na kupokea maoni yao kuhusu uwezekano wa kuwa na vikwazo vipya vya biashara. Kama nchi inayouza nje itaona kanuni za kifundi au sheria za SPS zilizowekwa na nchi inayoagiza siyo halali kufuatana na mikataba ya WTO (TBT au SPS), kuna njia nyingi za kutumia ili kikwazo kiondolewe au kubadilishwa. Njia hizi zinaanza kwa mazungumzo na mamlaka katika nchi iliyoagiza kwa nia ya kupata ukweli wa kizuizi hicho. Kituo cha mauzo katika nchi inayoagiza kinaweza kuwa mwanzo wa mashauri haya, lakini njia ya mapatano ya pande mbili inaweza kutumika (angalia swali 23). Mazungumuzo ya namna hii yanaweza kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu marekebisho ya kikwazo husika. Ikibidi swala hilo linaweza kufikishwa kwenye mkutano wa wengi, kwenye mkutano wa kamati ya WTO ya sheria ya afya ya wanyama na mimea au kamati ya vikwazo vya kiufundi vya Biashara, na kuomba nchi inayoagiza kuelezea kikwazo husika kwa wajumbe, hatimaye utaratibu wa WTO wa kutatua mgogoro unaojumuisha majadiliano ya kawaida kati ya serikali na jopo la wasuluhishi kusikiliza kesi hiyo lipo kwa nchi inayolalamika. Hatua zifuatazo sharti zifuatwe na mamlaka na viwanda katika kutatua vikwazo vya biashara:

75 Mahitaji ya kiufundi 65 Mashirika ya viwango ya kitaifa yanasisitizwa kuandaa viwango kwa misingi ya kimataifa, na endapo kuna sababu ya kuwa tofauti lazima iwe wazi. Wadau/Viwanda na mashirika ya viwango vya kitaifa yanahimizwa kushiriki daima katika kamati husika za kimataifa katika kuandaa viwango ili kulinda masilahi ya nchi/viwanda. Kwa hiyo, ni vema kuchagua kamati za kushiriki ambazo zitaleta manufaa kwa uchumi wa nchi, yaani zinazoshughulikia mazao/ bidhaa za kuuza nje, ili kushiriki mara kwa mara. Mamlaka zihamasishwe kutumia viwango kama msingi wa kuandaa kanuni za kiufundi na sheria za SPS. Njia ya kufanya rejea sharti ifuatwe kwa nguvu zote, na mamlaka zisisite kuingiza vipengele vya mahitaji ya kiufundi katika maandiko ya sheria. Kupitia njia hii, watahakikisha mienendo mizuri ya kimataifa itakuwa imezingatiwa; wadau watakuwa washiriki katika mchakato wa kuandaa mahitaji kupitia utayarishaji wa viwango, na kukubalika kwa kanuni za kiufundi na sheria ya SPS kutakuwa kumepewa nguvu. Viwanda/wadau na mamlaka katika nchi zinazoendelea sharti wafanye kazi kwa kushirikiana na kuwa na juhudi ya kuandaa mifumo ya udhibiti (hasa kwa chakula na chakula cha mifugo) ambayo itakidhi matakwa ya masoko changamano kama ya Jumuiya ya Ulaya (EU). EU inatekeleza utaratibu wa shambani mpaka mezani kwa bidhaa hizi na wanasisitiza ufuatiliaji, upimaji na uhakiki wa mazao na vyakula vilivyosindikwa kutoka kupandwa shambani mpaka bidhaa inafika kwenye meza ya mtumizi. Hali hii inafanyika pia katika uanzishaji wa Uwezo wa kupima na kuhakiki na ithibati( angalia swali 87, 88 na 90). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: European Commission. Guide to the implementation of directives based on the New Approach and the Global Approach. Makala haya yanajadili kwa kina mbinu kinyume ya marejeleo ya kujumuisha viwango vya Ulaya katika mielekeo mipya. Iacovone, Leonardo. Analysis and Impact of Sanitary and Phytosanitary Measures. Final Dissertation. Inatoa utangulizi wa maswala chanya yanazotoa kwa ujumla sifa za mikakati chanya na mikakati ya SPS, inapeana mapitio ya shirika iliyotengwa na makubaliano ya WTO SPS, inajadili ugumu unaoletwa na uchunguzi wa uchumi na mikakati ya kinyumbani juu ya biashara. Ignacio, Laura. Implications of Standards and Technical Regulations on Export Competitiveness. African Economic Research Consortium. June Karatasi hii inajadili jinsi viwango na mahitaji ya kiufundi inaathiri ushindani wa mauzo ya nje na kupeana mwelekeo juu ya utafiti kama mbinu ya kusaidia katika kufanya uamuzi. Magalhães, João. Regional SPS Frameworks and Strategies in Africa. Report for the Standards and Trade Development Facility. July Inachunguza mikakati na sheria ya SPS katika maeneo ya Afrika, kati ya changamoto nyingi za kuangazia mambo yanayoikumba SPS pasipo na mikakati ya kitaifa ya kupigana na baa la njaa, maslahi ya wanyama na mimea. Inajadili jinsi mikakati dhaifu ya SPS mara nyingi huwa bila msingi wa kisheria na kwa kiwango kikubwa hupunguza ukuaji wa biashara katika nchi za nje na ndani. Jambo linalohitajika ni kubadili sura hii. United Nations Industrial Development Organization and International Organization for Standardization. The Conformity Assessment Toolbox. Inajadili maswala, mbinu na uwiano wa bodi za uchunguzi. Inaelezea jinsi UNIDO inaezasaidia kuekeza katika miundo msingi ya kisasa kwa kutolea mifano. MAREJELEO Physikalisch-Technische Bundesanstalt/International Trade Centre. Technical Regulations: Recommendations for their Elaboration and Implementation. Guide 1/2009, Alex Inklaar World Trade Organization Sanitary and phytosanitary measures. Technical barriers to trade. World Trade Report 2005: Exploring the links between trade, standards and the WTO,

76 66 Mahitaji ya kiufundi 22. Kuna tofauti gani kati ya mahitaji ya lazima na mahitaji ya kibiashara ya wanunuzi? Kutofautisha kati ya mahitaji ya lazima (kiserikali/rasmi) na mahitaji ya kibiashara ya wanunuzi huwa jambo la utatanishi. Wakati mahitaji ya lazima yamewekwa na serikali na kutekelezwa chini ya sheria, mahitaji ya kibiashara kwa kawaida huwekwa na mashirika ya sekta ya kibinafsi. Kwa kawaida mahitaji ya lazima huwa kama kanuni za kiufundi au sheria ya SPS kama ambavyo imeainishwa na Mikataba ya WTO juu ya TBT na SPS kwa mfuatano huo, na hutumiwa kwa bidhaa ambazo zitapelekwa sokoni. Mara nyingi, mahitaji yapo kwa ajili ya kulinda afya na usalama, kuepusha undanganyifu na wizi, au kuepuka kutokubaliana kiufundi. Mahitaji ya kibiashara kwa kawaida huwekwa na makapuni ambayo hununua mali kwa ajili ya usindikaji au kwa kuwauzia wateja moja kwa moja. Wakati mwingine mahitaji haya yanaweza kumlenga mnunuzi fulani; au yanaweza kuwa yameandaliwa kwa pamoja kwa ajili ya wanunuzi wa sekta fulani, kama vile maduka makubwa ya rejareja (supermarkets). Mahitaji binafsi mara nyingi yanahusu zaidi ubora kuliko ishara za usalama wa bidhaa. Kupambanua tofauti kati ya mahitaji ya lazima na mahitaji ya kibiashara, hebu angalia bidhaa kama tufaha (fresh apple); mahitaji ya lazima kwa matufaha kutoka nje yanaweza kujumuisha kutokuwa na mabaki ya viuawadudu, wadudu/wanyama waharibifu na magonjwa ambayo yanaweza kusambazwa katika nchi iliyoagiza bidhaa hiyo. Mahitaji ya kibiashara yanaweza kutoa vigezo kama vile; aina ya tufaha, rangi, saizi, utamu, ubichi/upya, kutokana na kilimo hai au cha kawaida, kutokuwa na mikwaruzo au madoa, matayarisho kama kuoshwa au kuwekewa nta (waxing), na kadhalika. Mahitaji ya kibiashara yanaweza kujumuisha pia vipengele vinavyohusu kulinda mazingira au masuala ya kazi katika nchi bidhaa ilitoka; mahitaji ya kibiashara yanaendelea kupanuka kwa kuongeza mambo ambayo pia yamo kwenye mahitaji ya lazima. Hali hii inatokea hasa pale sheria za nchi inayoagiza bidhaa kutoka nje zinapoweka hitaji la kisheria kwa waagizaji bidhaa na wauzaji kuhakikisha bidhaa zao ni salama kwa matumizi. Makampuni binafsi nayo yako makini kuepuka hali yoyote ambayo inaweza kuhusisha bidhaa zao na uvunjifu wa mahitaji ya afya na usalama na kuharibu sifa zao. Kwa hiyo, mahitaji ya kibiashara kwa ajili ya manunuzi ya mazao gafi ya bustani, kwa mfano, yaweza kuhitaji uthibitisho kuwa kaanuni bora za kilimo zimefutwa katika kulima na uvunaji, kwamba matumizi ya viuawadudu yalisimamiwa vizuri, kwamba kanuni za afya zilifuatwa wafanyakazi wote wa shambani wakati wa kufungasha. Vipengele vya namna hii vinapunguza shauku kwamba bidhaa maduhuli ikifika na kukaguliwa itaonyesha ukiukwaji wa mahitaji ya lazima. Yafuatayo inabidi yazingatiwe: Mahitaji ya lazima, namna yalivyoonyeshwa kwenye kanuni za kiufundi (angalia Tume ya Kimataifa ya Ufundiumeme) na Sheria ya SPS (angalia swali 190, inabidi zitekelezwe na wagavi wote wanaoweka bidhaa sokoni au kusambaza, iwe za ndani au za kutoka nje. Hata kama zinauzwa au kwa matumizi ya nyumbani lazima zikidhi mahitaji hayo. Kwa hili hakuna uchaguzi kwani ni hitaji la kisheria. Mahitaji ya kibiashara yanategemea makubaliano, kwa kawaida katika mfumo wa mkataba halisia kati ya mgavi na shirika kubwa la rejareja, au oda halisiai kwa mauzo ya moja kwa moja kwa mnunuzi binafsi. Mkataba unaweza kujumuisha msururu wa mahitaji ya kiufundi yanayofanana kwa karibu na viwango, na inawezekana yakawa ya kurejelea kwa kiwango zaidi ya kimoja. Mkataba pia unaweza kueleza kinaganaga ushahidi wa ulinganifu (k.m. ukaguzi, upimaji na uhakiki) kwamba mgavi alimpatia mnunuzi kabla, wakati au baada ya kupeleka bidhaa au kutoa huduma. Ikiwa mgavi mtarajiwa ataamua kutokubali au hawezi kutimiza mkataba, hapatakuwa na mauzo; katika hali hii, mahtaji ni ya lazima kwa mgavi. Wagavi wana hiari ya kukubali au kukataa mahitaji ya kimkataba au mahitaji ya kibiashara ya wanunuzi fulani na wako huru kuuza bidhaa zao kwa wanunuzi wengine bila kuvunja sheria. Utashi huu hawana ikiwa mahitaji ni ya lazima. Kwa kuogopa kuvunja sheria, katika hali yoyote ile mahitaji ya lazima sharti yatimizwe bila kujali aina ya wanunuzi na mahitaji yao ya kibishara. Kwa sababu ya gharama kubwa ya kufanya ukaguzi wa maduhuli, uchunguzi wa kiwanda na ukaguzi wa bidhaa, wingi wa bidhaa na ukubwa wa gharama za upimaji na uhakiki, mamlaka nyingi za usimamizi haziwezi kukagua bidhaa zote zinazohusishwa na kanuni za kiufundi na sheria ya SPS. Ukweli ni kwamba,

77 Mahitaji ya kiufundi 67 wataridhika hata kama wangeweza kukagua asilimia tano ya bidhaa hizo. Kwa hiyo, mamlaka ya usimamizi hutegemea sana wagavi kutimiza majukumu yao kwanza. Wanaweza kwa uchache kufanya uchunguzi kwenye soko, yaani kufanya ukaguzi wa bidhaa zilizoko sokoni (kuliko kuzikagua bidhaa kabla hazijaingia sokoni) na kuwa na ufuatiliaji wa wagavi wasio na rekodi safi. Hata hivyo, utaratibu huu sio mzuri wa kujitosheleza, haswa kwa mashirika makubwa ya rejareja au wanunuzi wakubwa kwa kuwa uwezekano wa kupokea bidhaa zisizokidhi viwango ni mkubwa mno. Wanunuzi hawa wakubwa wana rajamu (brand) za kuzilinda, kwa maana bidhaa yoyote ile inatangaza jina lao; kwa hiyo ikiwa hafifu itaharibu jina lao. Tukirejelea hali hiyo, wanunuzi hawa wakubwa wengi wao hujumuisha mahitaji ya kiufundi na sheria za SPS kwenye mikataba na huwataka wagavi wao kuwasilisha ushahidi wa kukudhi mahitaji haya. Viwango vya GLOBAL G.A.P. na BRC (angalia swali 14) ni matokeo ya maamuzi yaliyofanywa na wauza rejareja wakubwa wa Ulaya na Uingereza. Viwango hivi vinajumuisha mahitaji ya sheria ya chakula ya Ulaya pamoja na mahitaji mengine mengi ambayo wauza rejareja wamekubaliana. Uhakiki kufuata viwango hivi unahitaji kuonyesha bayana kwamba mahitaji ya sheria ya chakula ya jumiya ya Ulaya yametimizwa. Uhakiki wa ISO 14001, kiwango cha kimataifa cha usimamizi wa mazingira, pia unayahitaji makampuni kutoa ushahidi kuwa wanatimiza au kwa zaidi majukumu yao kulinda mazingira nchini mwao kwa mujibu wa sheria za mazingira walizo nazo. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: BRC Global Standards. Viwango vya kimataifa vya BRC ndivyo vinavyoongoza kimataifa kwa kudhibitisha programu za ubora na usalama wa bidhaa zinazotumika na wauzaji waliothibitishwa katika zaidi ya nchi mia moja. Food and Agriculture Organization of the United Nations. Private standards in the United States and European Union markets for fruit and vegetables Implications for developing countries, Part 2: Overview of existing analytical work on the impacts of private standards on trade. ftp://ftp.fao.org/docrep/fao/010/a1245e/a1245e03.pdf Inatoa mukhtasari wa kazi za utafiti juu ya viwango vya kibinafsi katika biashara, ikitilia mkazo kwa mauzo ya matunda na mboga katika nchi za nje kutoka nchi zinazoendelea. GLOBALG.A.P. Certification. GLOBALG.A.P (hapo mbeleni ilijulikana kama EUREPG.A.P) imejijenga kama kielelezo chema cha kilimo (GAP) katika soko la kidunia. Ni bodi ya kibinafsi inayotunga viwango kwa hiari vya udhibitisho katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo (ikiwemo ufugaji wa samaki) dunia nzima. International Organization for Standardization. International standards and private standards. A freely downloadable brochure. Karatasi hii inaelezea majukumu muhimu ambayo viwango vya kimataifa vya ISO huchangia katika kuendeleza biashara na kuchangia katika kutekeleza sheria za umma na pia kukubalisha mbinu bora za udhibiti kwa misingi ya matokeo kinyume na uwajibishaji wa sheria za kiufundi/sanaa. Standards and Trade Development Facility. STDF is ni mfumo wa kutoa ujumbe kuhusu matukio ya kiufundi ya SPS. Pia inaazimia kuchochea raslimali ili kutatua maswala ya SPS ambayo huzuia uwezekano wa biashara katika nchi zinazokua na hivyo kulinda binadamu, wanyama na mimea kutokana na athari za SPS World Organisation for Animal Health (OIE). OIE ni shirika la muungano wa serikali tofauti ambazlo lina jukumu la kuboresha maslahi ya wanyama dunia nzima. Inatambulika na WTO kama shirika kielelezo. Mwaka wa 2011 ilikua na nchi wanachama 178. Makala haya yanapeana athari za viwango vya kibinafsi kwa biashara ya wanyama na bidhaa kutoka kwa wanyama katika soka la kimataifa. World Trade Organization. Research and Researchers on Private Standards Inatoa orodha ya mashirika ambayo yamethibitishwa na WTO ambayo yanachangia na kuhusika na utafiti wa athari za wiwango vya kibanfsi. MAREJELEO EU Food Safety Legislation. International Organization for Standardization :2004, Environmental management systems Requirements with guidance for use. Obtainable from ISO or ISO members (list at

78 68 Mahitaji ya kiufundi 23. Nitapata wapi taarifa kuhusu mahitaji ya kiufundi kwa mahuruji? Unahitaji aina mbili za taarifa za kiufundi ili uweze kuuza bidhaa nje ya nchi kwa mafanikio. Kwanza, inabidi ufahamu kama kuna kanuni za kiufundi na sheria ya SPS katika nchi inayoagiza bidhaa au huduma. Ulinganifu na mahitaji ya suala la kisheria, kwa hivyo ni muhimu chanzo cha taarifa hizi kiwe cha uhakika, yaani chanzo rasmi. Pili, inabidi ufahamu mahitaji ya kibiashara ya bidhaa au huduma yako; kama ni za uhakika au zinafikiriwa tu kwa soko hilo, na kama ni sehemu ya mkataba wa wanunuzi wakubwa (angalia swali 22) au kama kuna faida za ziada zitakazopatikana kwa kukidhi viwango vya kitaifa. Sehemu hii inatoa maelezo kuhusu mahali utakapopata taarifa kuhusu kanuni za kiufundi za sheria za SPS, viwango vya umma na binafsi. Majukumu ya mashirika ya kuendeleza biashara (TPO) na jinsi unavyoweza kunufaika nayo pia yameelezwa. Kanuni za kiufundi Kila mwanachama wa WTO hana budi kuanzisha na kuendeleza kituo cha kitaifa cha maulizo kuhusu TBT, kwa ajili ya kujibu maswali yoyote kuhusu viwango, kanuni za kiufundi za sasa na tarajiwa, na utaratibu wa kutathmini ulinganifu uliopo na unavotarajiwa. Kituo hiki ndicho kiwe cha kwanza kwa maulizo ya mgavi anayetaka taarifa juu ya kanuni za kiufundi katika masoko ya nje. Kuna uamuzi wa aina nyingi: Kama nchi yako ni mwanachama wa WTO, basi ina wajibu wa kuwa na kituo cha maulizo cha TBT. Unaweza kukiomba kituo hiki kupeleka maombi ya taarifa unazohitaji kwenye kituo dada katika nchi inayoagiza au unakotaka kupeleka bidhaa zako. Pia, unaweza kupeleka maombi yako moja kwa moja kwenye vituo vya maulizo vya TBT ng ambo. Ukitumia njia yoyote ile, ni sahihi ya kupata taarifa. Tafadhali angalia sehemu ya mwisho ya ibara hii kwa maelekezo jinsii ya kupata taarifa kutoka kwenye tovuti ya WTO. Hata kama nchi yako siyo mwanachama wa WTO, unaweza kuwasiliana moja kwa moja na kituo cha maulizo katika nchi unayotaka kuuza bidhaa zako; pamoja na kuwa vituo hivi havilazimiki kutoa taarifa kwa asiye Mwanachama wa WTO, ni mara chache watakataa kukuhudumia. Kama unataka kupeleka katika soko la nchi ambayo sio mwanachama wa WTO na haina kituo cha maulizo cha kitaifa cha TBT, mambo yanaweza kuwa changamano. Mahali pazuri pa kuanzia utafutaji wa taarifa ni kwa mwambata wa kibiashara katika ubalozi wa nchi unayotarajia kupeleka bidhaa zako, nchini mwako. Kama hawataweza kukupa majibu bila shaka wataweza kukupa maelekezo ya kukusaidia kupata mahali utakapopata habari maalum unazohitaji. Endapo yote hapo juu yatashindwa kukupatia unachohitaji, itabidi usake taarifa kutoka vyanzo vingine rasmi kama vile wizara za biashara, kilimo, afya, usafirishaji, nyumba na mawasiliano, yaani wizara zinazohusika na kanuni za kiufundi katika nchi unayolenga kupeleka bidhaa zako. Kazi hii inaweza kukupotezea muda na kukukatiza tamaa. Wakati mwingine shirika lenu la kuendeleza biashara linaweza kuwa na msaada wa kutambua vyanzo rasmi vya taarifa unazozitaka. Mshiriki wako anayeishi katika nchi unakotaka kupeleka bidhaa, au mnunuzi mkubwa unayetaka kufanya naye biashara anaweza pia kukusaidia. Asilimia 60 ya nchi wanachama wa WTO, vituo vyao vya maulizo vya TBT viko katika mashirika ya kitaifa ya viwango (BSB). Katika nchi zingine (kiasi cha 15% ya wanachama wa WTO), vituo vya TBT vya maulizo vinamilikiwa kwa pamoja na NBS na wizara ya biashara. WTO inatunza kumbukumbu mpya ya orodha ya vituo vya kitaifa vya maulizo ya wanachama na anwani zake. Orodha hii inapatikana bila malipo katika tovuti yao kuweza kuipata orodha mpya nenda katika eneo la kutafuta kwenye ishara ya nyaraka, andika G/TBT/ENQ. Sheria za SPS Kila mwanachama wa WTO ameanzisha na kuendeleza kituo cha kitaifa cha kutoa taarifa juu ya sheria ya SPS. Vituo hivi vya SPS mara nyingi viko katika wizara zinazoshughulikia kilimo na afya. Tukirejelea vituo vya maulizo vya TBT, WTO huweka orodha mpya daima ya vituo vya SPS vya wanachama wake. Kadhalika orodha hii inapatikana katika tovuti yao: kwenye ishara ya nyaraka ukiandika G/SPS/ENQ utaipata orodha bila malipo yoyote.

79 Mahitaji ya kiufundi 69 Kuna wanachama wa WTO ambao wana tovuti ambazo huweka kwenye orodha masharti ya SPS yanayohusu maduhuli ya chakula na wanyama wengine na bidhaa za wanyama. Tovuti hizo kuna uwezekano zinahusiana na wizara za kilimo na afya. Ili mauzo yaweze kwenda nje katika nchi zisizowanachama wa WTO, itabidi kuwasiliana na wizara husika katika nchi inayoagiza, ili kupata ushauri kuhusu masharti ya kuingiza bidhaa nchini mwao. Balozi za ndani ya nchi yako zinaweza kutoa msaada jinsi ya kupata taarifa unazotaka. Washiriki wa kibiashara katika nchi husika, pia wanaweza kusaidia kukupa taarifa unazohitaji. Hata hivyo, kuna uwezekano wa kuwa na hatari kama ukitegemea taarifa kutoka vyanzo visivyokuwa rasmi, kupata kutoka mamlaka za nchi inayoagiza. Viwango vya umma Hatua ya kwanza ni kupatana na shirika la viwango la taifa katika nchi yako, ambalo kwa kawaida huwa na kituo cha habari za viwango. NSBs huweka mkusanyiko wa viwango vya kitaifa, kadhalika wana uwezo wa kupata viwango vya kimataifa kama vile vya ISO, IEC, na daima wana mahusiano ya kibiashara na mashirika ya viwango katika nchi ambazo ni masoko muhimu ya mahuruji. Mahusiano haya huyawezesha mashirika haya ya kitaifa ya viwango kuweza kuwa wagavi wa taarifa za viwango kutoka nchi washiriki muhimu za kibiashara. Kama NSB haina taarifa inayotakikana, katika maktaba yake, basi huweza kuitafuta kutoka kwa NBS mwenzi wa nchi nyingine. Vituo vya habari vya NSB huwa vina faida ya kuendeshwa na watu wenye uelewa na masuala ya viwango kwa hiyo watakuhudumia upesi, bila kukupotezea muda. Pia, kuna ongezeko la NBSs ambao wanauza viwango kupitia mtandao wa kelektroniki; matumizi ya mtandao katika kutafuta taarifa za viwango yameongezeka sana duniani kote. Njia rahisi ya kuweza kuzifikia tovuti za kitaifa, kikanda na kimataifa ni kupitia tovuti ya mtandao wa huduma za viwango (Standards Services Network (WSSN). Mahusiano ya moja kwa moja kwenda kwenye mashirika karibu yote ya viwango duniani; kwa kawaida viwango havipatikani bure. Viwango vya ISO na IEC vina hatimiliki, kwa hivyo sharti vinunuliwe. Viwango kutoka mashirika ya kiserikali kama OILM, CAC na mengineyo vyaweza kuchukuliwa kutoka kwenye tovuti ya mashirika hayo. Viwango vya kikanda ni mara chache kutoka katika mashirika ya kikanda; inabidi vinunuliwe toka NBSs ambazo zinahusika na uandaaji wake. Viwango vya Ulaya vilivyopatanishwa (EN) na viwango vya Afrika Mashariki ni mifano ya viwango vya kikanda. Viwango vya kitaifa kwa kawaida hununuliwa, hasa kama vimeridhiwa toka ISO na IEC. Bei ya viwango inatofautiana sana kutegemea kama NSB inaziona kama vyanzo vya mapato au la. Ni vyema kuangalia bei kutoka sehemu mbalimbali, hasa kama ni viwango vya kuridhia vya kimataifa. Viwango binafsi Taarifa kuhusu viwango binafsi (angalia swali 14) zinategemewa kuwa kwenye mshiriki wako wa kibiashara katika nchi unayopeleka bidhaa. Kwa nyongeza, baadhi ya viwango binafsi hasa vile vinavyotumika katika uhakiki, vinapatikana kwenye tovuti za mashirika husika. Mifano hai inajumuisha viwango vya GLOBALG.A.P., Viwago vya SA 8000 na viwango vya FSC. Viwango vingine kama BRC, inabidi ulipie kuweza kuiona na kupata nakala. Utumiaji wa mtandao wa kompyuta kwa ajili ya kupata taarifa, ni muhimu sana siku hizi. Kadhalika kutafuta kupitia mtandaoni kunarahisisha kuunganika na mashirika mengi ambayo hupenda kujitangaza. Wajibu wa mashirika ya kuendeleza biashara Wajibu mkubwa wa TPOs ni kutoa taarifa halisi na tarajiwa kuhusu masoko ya nje, ili kuwawezesha wagavi kuuza nje kwa mafanikio, na kujenga mahusiano yanayotakiwa kati ya wauzanje na waagizaji. Kwa sababu hiyo, TPOs wamekusanya takwimu nyingi kuhusu mahuruji ya nchi zao na kuhusu masoko katika nchi inayoagiza. Hizi zinaweza kuhusu matakwa ya soko, usanifu unaotakiwa, ubora na kadhalika. Kuna faida kwa wagavi kuwasiliana na TPOs zao ili kufahamu kama wanaweza kuwasaidia kupata taarifa kuhusu mahitaji ya kanuni za kiufundi.

80 70 Mahitaji ya kiufundi KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: EU Help Desk for Developing Countries. Meza ya mauzo ya nje ni huduma ya mtandao inayotolewa na European Commission to facilitate market access to the European Union haswa kwa nchi zinazokua. Huduma hii ya bure na rahisi kutumiwa na wateja inatoa maelezo yanayohitajika na wauzaji katika nchi za nje walio na hamu katika kupeleka bidhaa zao kwenye soko la muungano wa Ulaya (EU) FAO, IPCC, WTO, OIE, CBD, Codex Alimentarius, WHO. International Portal on Food Safety, Animal and Plant Health (IPFSAPH). Kusanyiko la data jumuishi juu ya ujumbe rasmi juu ya usalama wa vyakula, afya ya wanyama na mimea; inatoa maelezo juu ya viwango, sheria, kuchunguza usalama, marejeleo, na jumbe zingine katika viwango vya kimataifa, eneo, kitaifa ndiposa iwezeshe ubsdilishaji kati ya nchi na maeneo, na pia kushinikiza biashara ya chakula na kilimo kimataifa. International Bureau of Weights and Measures. BPIM inashughulikia maswala ya hali ya anga ya dunia nzima, haswa inakadiria mashine ya viwango vya kupimia vya kisasa, na pia inakadiria usawa kati ya vipimo vya kitaifa. Tovuti yake ina hifadhi mwafaka juu ya mashirika ya utabiri, mashirika ya utabiri ya maeneo na maabara n.k. International Trade Centre Export Quality Management Bulletin No. 72, Information retrieval on standards, technical regulations and conformity assessment procedures. Tovuti ya Export Quality Management chini ya ITC inakuwezesha kupata maelezo kwa kifupi au vitabu vilivyochapishwa na shirika hili; nyingi yazo zinapatikana katika lugha ya Kingerza, Kifaransa na Kispanyola. Taarifa za ITC 72 zinapeana mielekeo ya jinsi ya kurejelea maelezo juu ya viwango, sheria za kiufundi na maelezo ya uwiano. Export Quality Management Bulletin No. 81, Information retrieval on sanitary and phytosanitary measures (SPS). Tovuti ya Export Quality Management chini ya ITC inakuwezesha kupata maelezo kwa kifupi au vitabu vilivyochapishwa na shirika hili; nyingi yazo zinapatikana katika lugha ya Kingerza, Kifaransa na Kispanyola. Taarifa za ITC 72 zinapeana mielekeo ya jinsi ya kurejelea maelezo juu ya viwango, sheria za kiufundi na maelezo ya uwiano. Perinorm. Ilizinduliwa na AFNOR (Ufaransa), BSI (Uingereza) na DIN (Ujerumani), Perinorm ni marejeleo ya viwango vya ubora na sheria za kiufundi. Inapatikana kwenye CD na kwenye mtandao baada ya usajili kutoka kwa washikadau watatu. World Trade Organization. SPS Information Management System. Database of WTO information on SPS (notifications, concerns raised, other documents, enquiry points, etc). TBT Information Management System. Kusanyiko la data ya WTO ya jumbe juu ya SPS (pg 86) MAREJELEO International Trade Centre and International Organization for Standardization. Building Linkages for Export Success Print versions can be obtained online from ITC s e-shop ( and ISO ( PDF files can be obtained at: and at International Trade Centre. Innovations in Export Strategy: A strategic approach to the quality challenge World Standards Services Network (WSSN). World Trade Organization. WTO Agreements on TBT and SPS. Once you enter in this link, type G/TBT/ENQ and G/SPS/ENQ to obtain the updated lists.

81 Mahitaji ya kiufundi Nawezaje kufuatia mabadiliko katika kanuni za kifundi zinye umuhimu kwangu? Kuweza kujua pindi mabadiliko yanapotokea katika mahitaji ya kiufundi yana umuhimu sawa kwa muuza bidhaa na kama ilivyo katika kupata mahitaji hayo kwa mara ya kwanza. Kuna mifano mingi ya viwanda kufilisika katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea kwa sababu ya kutotilia maanani ufuatiliaji wa mabadiliko katika soko. Hali hii inajitokeza zaidi katika biashara ya bidhaa zinazonunuliwa sana, kama vile vifaa vya elektroniki; hata hivyo kumekuwa na mabadiliko makubwa katika mwongo uliopita, maana hata viwanda vya chakula na vifaa vya ujenzi vimejikuta vinaingia katika hali hiyo ya kufilisika. Viwango vya umma Tembelea shirika la viwango la nchi yako (NSB), ambalo linaweza kukupa taarifa kuhusu viwango ambavyo vinaandaliwa au vinarejelewa na kuweza kuathiri biashara yako. Mashirika ya kitaifa ya viwango, pia yanaweza kukupa habari za viwango vya kikanda na kimataifa ambayo yanarejewa au kuandaliwa kwa mara ya kwanza, hasa kwa vile NSB linashiriki. Kama kuna taarifa zinazotakiwa kutoka kanda zingine, basi NSB watakuwa na uwezo wa kuzipata kwa wenzi wao dunia nzima. Mashirika ya kitaifa ya viwango ya wanachama wa WTO yana wajibu wa kutoa taarifa juu ya viwango vinavyoandaliwa katika nchi zao kupitia kituo cha habari cha ISO? IEC ( Siku za nyuma haya yalikuwa orodha ya majarida, lakini siku hizi yapo kwenye tovuti za BSBs. Kwa hivyo, kama una mtandao, basi utapata faida ukiweza kukokoora kwenye tovuti za NSBs na mashirika ya kikanda ya viwango yanayohusu biashara yako. Mashirika mengi ya viwango daima huwa na orodha mpya (up-to-date) ya viwango vinavyoandaliwa, taarifa ambazo zinaweza kufikiwa/kuonwa na mtu yeyote. Sehemu hii ni chanzo kizuri cha kupata taarifa wakati rasimu ya kiwango inaposambazwa kwa umma/wadau kwa maoni; kabla ya kupitishwa rasmi na kuchapwa kama nyaraka rasmi, yaani kiwango cha kitaifa. Njia nyingine ni kuwa mjumbe wa kamati ya kiufundi ya kitaifa inayoshughulikia eneo la bidhaa yako, nayo itakupa nafasi ya kufuatilia maendeleo/mabadiliko ya viwango vya kimataifa, kikanda na kitaifa. Kwa hakika, kushiriki kwenye kamati husika, inaweza kuwa ndiyo kati ya njia bora zaidi ya kuwa sambamba na mabadiliko; kwani utapata taarifa mapema na kuweza kurishiri katika kurejelea viwango vilivyopo, au kufuatia jinsi mambo yanavyokwenda wakati wa kuandaa kiwango kipya na kuweza kushawishi mchakato ili uweze kutilia maanani mambo ambayo yatafanya kiwango kiwe cha manufaa kwa sekta na/au biashara yako. Kanuni za kiufundi na sheria za SPS Majukumu ya wanachama wa WTO kufuatana na mikataba ya TBT na SPS, wanawajibika kutoa taarifa kwa ukatibu wa WTO kwa uchache wa siku 60 kabla ya kukubali kanuni za kiufundi au sheria mpya ya SPS. Hii ni kwa sababu ya kutoa nafasi ya kutosha kwa washiriki wa kibiashara kutoa maoni yao juu ya pendekezo la kanuni au sheria ya SPS kabla ya toleo la mwisho. Taarifa hizi zinaweza kupatana kwa njiambili: unaweza kupata matangazo yoyote yaliyowekwa kwenye tovuti ya WTO. Hata hivyo, hii ni shughuli inayochukua muda, kwani matangazo huchapishwa kufuata tarehe, na hukuna njia nyingine inayokuwezesha kukokoora kwa urahisi. Ina maana kuwa kila wiki mmoja wa wafanyakazi wako itamlazimu kutumia muda kupekua matangazo yote. Ikigundulika kwamba kuna tangazo/taarifa ambayo inaweza athiri biashara yako, yaani inahusika na zao au bidhaa, na inatoka kwa mnunuzi au mnunuzi mtarajiwa wa bidhaa zako, itabidi upate ufafanuzi kutoka kwenye kituo cha maulizo cha kitaifa katika nchi husika(liliko soko). Matangazo huwa mafupi na hutoa mawanda ya kanuni ya kiufundi au sheria ya SPS mpya; tangazo huwa halitoi anwani ya shirika/kampuni ambako ufafanuzi unaweza kupatikana. Baadhi ya vituo vya maulizo vya kitaifa vina mfumo wa kutahadharisha juu ya matangazo ya TBT na SPS yaliyopelekwa kwenye ukatibu wa WTO. Kwa kifupi, hufanya kazi kama ifuatavyo: kituo cha maulizo hutathmini tangazo lililotumwa na ukatibu wa WTO kila wiki, na kubaini ni matangazo yapi yanaweza kuwahusu mamlaka na viwanda nchini. Kama shirika lako la viwango lina mfumo huu wa kutahadharisha, itakuwa mwafaka kwako kuwa mmoja wa wale wanaopata taarifa hizi daima katika sekta, mazao au bidhaa unazohuzika nazo. Wasiliana na kituo chako cha maulizo kujua kama wana huduma kama hiyo, na kama hawana, jaribu kuwashawishi waianzishe; jinsi ya kufahamu kituo cha maulizo unachokitaka unaweza kuangalia kwenye tovuti ya WTO. Njia ya tatu itakuwa ya biashara au chama cha wazalishaji kuwa na mfumo wa kutahadharisha wa kisekta, kama ambavyo kituo cha maulizo kingefanya. Huduma za shirika la kuendeleza biashara, kadhalika

82 72 Mahitaji ya kiufundi zingeweza kutumika katika hili. Matumizi ya teknohama yamerahisisha mambo, na waweza kuibua taratibu zingine zitakazokuwa na faida kwako. Viwango binafsi Kwenda sambamba na maendeleo ya viwango binafsi ni changamani zaidi kwani mashirika yanayohusika hayafanyi kazi kupitia WTO au mfumo wa ISONET, NSBs wakati mwingine huwa na maktaba ya viwango binafsi, lakini ni kwa hiari siyo kanuni. Kama wewe ni kampuni iliyopata uhakiki kupitia viwango binafsi, shirika lililokupa uhakiki ndilo lina nafasi nzuri ya kukupa taarifa kuhusu marejea yanayotarajiwa. Marejea ya namna hii yanaweza kukuhitaji kurekebisha mfumo ulionao ili kubakia na uhakiki ulionao, shirika lililokuhakiki halitapenda kukupoteza kama mteja wake. Mashirika yanayoandaa viwango binafsi kwa kawaida huwa na tovuti hai na iambatanayo na wakati kama sehemu ya kioo chao kwa jamii. Matukio yote yanayohusu marejea, mabadiliko au matukio mapya hupewa nafasi ya kutosha katika tovuti hizo, na kwa sababu hiyo huwa rahisi kufuatilia kama unafahamu zilipo. Hii ni huduma nyingine ambayo makampuni au vyama vya wazalishaji vinaweza kuwa wanachama, na hasa kama ni SMEs ambao wanapata ugumu wa kupata imtandao kwa sababu yoyote ile. KWA TAARIFA ZAIDI International Trade Centre. Standards Map: Inatoa maelezo mengi kwenye mtandao wa ITC juu ya viwango vya kibinafsi, na kutolea maelezo ya kiusomi, kisayansi na utafiti juu ya viwango hivi vya kibinafsi juu ya masuala ya manufaa ya dunia nzima.ramani za viwango hufnya kazi katika mazingira ya kimtandao. Huwezesha ulinganisho wa mahitaji ya viwango vya kibinafsi katika viwango tofauti vya utathmini kutoka hali ya kawaida hadi hali ya kuangalia kila hitaji ya mabo kama usafi wa chakula na gesi chafuzi za kaboni na vilevile mahitaji maalum yanayohusu haki za kazi na masuala ya jinsia. ISONET Directory. Katika kitengo cha Related addresses tovuti hii inapeana mielekeo ya moja kwa moja kwa orodho za punde za wanachama wa ISO na IEC katika tovuti za ISO na IEC. Pia inajumuisha orodha za punde za WTO, orodha za majina na anwani za vituo vya usaidizi vilivyo anzishwa chini ya makubaliano ya TBT na SPS. (pg 89 ISO/IEC Information Centre. Inatoa ujumbe juu ya ulinganishi na uwiano, viwango na mambo rejelea;inatumika kama tovuti rasmi ya jumbe zinazopatikana katika kurasa za tovuti za ISO na IEC, kwa mfano; katalogi za ISO na IEC za kuelezea viwango; inakubalisha kuuliza maswali na tovuti za mashirika ya viwango vya kitaifa. (page 89) National Institute of Metrology, Quality and Technology (INMETRO), Brazil. Exporter Alert! Inatolea onyo la mapema kwa wauzaji ambao wamejisajili katika huduma hii. Standards Council of Canada. Export Alert! Inatolea onyo la mapema kwa wauzaji ambao wamejisajili katika huduma hii. World Trade Organization SPS Information Management System (SPSIMS). Inapeana uafiki kwa makala na rekodi za kutekelezwa kwa mikakati ya usafi iliyowekwa chini ya mapatano ya WTO. SPSIMS inawakubalisha watumiaji kufuatilia jumbe juu ya mikakati ya SPS ambayo serikali wanachama wametambulisha WTO, masuala tata yaliyotambulika katika komitii ya SPS, makala ya SPS yaliyowasilishwa kwa WTO, maswala yaliyowasilishwa na serikali wanachama wa SPS, na uwanachama wa WTO, Codex Alimentarius, IPPC na OIE. TBT Information Management System (TBTIMS). Inawakubali watumiaji kufuatilia na kupata ujumbe juu ya mikakati ya TBT ambayo serikali wanachama wamejulisha WTO juu ya maswala tata ya wanachama, juu ya bodi za kudhibiti ubora ambazo zimekubali sheria na masharti ya mapatanao ya TBT, juu ya toleo zilizotumika kutoa ujumbe juu ya mikakati ya kiufundi, viwango, uwiano; na juu ya maelezo ya utekelezaji na usimamizi wa mapatano ya TBT. Nyaraka za WTO kwenye mtandao wa komputa (kielekitroniki). Kusanyiko la data ambalo linatoa nafasi ya kupata nyaraka rasmi za WTO, na hufanywa mpya kila siku. Huwezesha kupata matangazo yanayohusiana Mkataba wa WTO juu ya TBT na SPS.

83 Mahitaji ya kiufundi Je, naweza kushawishi uandaaji wa viwango, kanuni za kiufundi na sheria ya SPS? Sehemu hii inatoa maelezo jinsi gani unaweza kushawishi uandaaji wa viwango, kanuni za kiufundi na sheria ya SPS: Viwango Hakika unaweza kushawishi uandaaji wa viwango. Jambo la msingi katika utayarishaji wa viwango ni uwazi, ukweli, uadilifu, kufuata mahitaji ya wadau na mchakato wa maridhiano. Ili kazi hiyo kufanywa kwa nguvu ya wadau, kwa wale wote wenye masilahi na jambo hili sharti wapewe nafasi ya kutoa michango yao muhimu wakati wa mchakato wa uandaaji. Karibu nchi zote zilizoendelea, zenye uchumi wa kati na zinazoendelea zina mashirika ya viwango ya kitaifa (au mashirika) yenye wajibu wa kuchapisha viwango vya kitaifa. Mengi ya mashirika haya ni wanachama wa ISO na mengi pia ni wanachama wa IEC. Sheria za mashirika haya ya kimataifa zinawataka wanachama kufuata utaratibu wa msingi wa maridhiano kati ya wadau katika uandaaji wa viwango vya kitaifa; misingi hii imo kwenye maagizo ya ISO/IEC. Mashirika ya viwango ya kitaifa ya wanachama wa WTO wanatakiwa kufuata kanuni za utendaji bora katika utayarishaji, kuridhia na matumizi ya viwango vilivyo kwenye kiambato cha tatu cha mkataba wa WTO TBT. Kanuni hii ya utendaji inataka mchakato wa kutayarisha viwango vya kitaifa kuwa kwa nguvu (matakwa) ya wadau. Unaweza kushiriki katika mchakato wa kuandaa viwango kupitia shirika la viwango la nchini mwako, liwe la kiserikali au siyo-kiserikali. Ushiriki wa dhati katika kamati za kiufundi za kitaifa, kamati ndogo au vikosi kazi ambavyo vinajadiliana juu ya kuandaa viwango vipya au kuvirejelea vya zamani unahitajika. Omba kwenye shirika lako la viwango kuwa mshiriki katika kamati za kitaifa au kushiriki katika kazi zao kupitia chama cha kibiashara kinachohusiana na biashara yako. Kazi za kamati za kitaifa zinatoa mchango katika kazi za kikanda na kimataifa. Kama wewe ni muuzaji bidhaa nje ya nchi na unafahamu kuwa kuna matayarisho ya viwango katika kanda au kimataifa, sharti uliombe shirika lako la kitaifa la viwango, kupitia kamati husika ya kitaifa, kushiriki kwa dhati katika majadiliano, ikiwezekana kuwashirikisha wagavi. Kwa njia hii nchi zinazoendelea zimeweza kulinda viwanda vyake kuathiriwa na mahitaji yasiyo ya lazima na kutaabisha yaliyo katika viwango vya kikanda au kimataifa ambavyo vingeweza kuleta madhara kwa viwanda hivyo kama vingekubalika. Mfano mzuri ni ule wa kiwanda cha mipira asili cha Malaysia, ambacho kiliweza kubaini mapema kusudio la kupigwa marufuku matumizi ya glovu za upasuaji (surgical gloves) za mipira asili, wakati wa marejea ya kiwango cha kimataifa kilichokuwepo kwa kuibua njia mpya ya utakasaji ambayo iliondosha kiambato ambacho kilikuwa chanzo cha tatizo la tishio kwa maisha kwa kuleta mzio kwa madakitari na wagonjwa. Tendo hili lilihakikisha matumizi ya mpira asili kuendelea kutumika katika utengenezaji wa glovu za upasuaji) (kitabibu). Kanuni za kiufundi Kanuni za kiufundi kwa kawaida haziandaliwi kwa misingi ya maridhiano (angalia swali 18). Katika hali hiyo, siyo rahisi kushawishi utayarishaji wake; hata hivyo hali inabadilika hata kwa hizi kwa maana serikali nyingi zinajaribu kufuata njia zilizowazi zaidi na adilifu katika mfumo wa udhibiti. Kwanza, katika nchi nyingi, kanuni za kiufundi zimeandaliwa kwa misingi ya viwango na hata viwango rejea kwa ujumla wake (angalia swali 18). Kwa sababu utayarishaji wa viwango ni wa wazi na adilifu, unaweza kushawishi kama ilivyokwishaelezwa hapo juu. Hii ni sababu nyingine inayoeleza kwa nini ushiriki wako katika uandaaji wa viwango ni wa muhimu kwa biashara yako. Pili, nchi nyingi huchapisha rasimu za kanuni za kiufundi mapema kwa ajili ya maoni ya wadau kabla ya kuanza kutumika; kwa kawaida huchapishwa kwenye gazeti la serikali au magazeti ya kawaida. Kwako wewe ni kazi ya kufuatilia matukio hayo. Vyama vya wafanyabiashara na wenye viwanda navyo vinaweza kuwa wafuasi wazuri wa kuwapa habari wagavi matokeo yoyote ya kisheria yanayojitokeza. Baada ya rasimu kuchapishwa kwa maoni ya wadau. Tumia fursa hii kutoa maoni, kama hutafanya hivyo, itabidi kukubali maamuzi ya wengine. Katika ngazi ya kimataifa, kanuni za kiufundi sharti zifahamishwe kwa WTO kwa uchahe wa siku 60 kabla ya kuanza kutumika. Mfumo wa kutahadharisha mapema ambao kwa kawaida unafanywa na vituo vya maulizo vya kitaifa ni njia nzuri ya kufuatilia matukio ya kimataifa kama haya (angalia swali 24). Ukipata taarifa mapema, inabidi utoe maoni yako kwenye kituo cha maulizo au kwa wizara zinazoshughulikia mkataba wa TBT (kwa kawaida ni wizara ya biashara), ambao watakusanya maoni na kuyapeleka kwa mamlaka husika katika nchi inayoagiza kwa kufikiriwa. Kama ni changamani, basi yatapelekwa kenye Kamati ya WTO TBT, Geneva.

84 74 Mahitaji ya kiufundi Sheria za SPS Kufuatana na mkataba wa SPS, wanachama wa WTO sharti waandae sheria zao za SPS kuhusu viwango vya kimataifa, miongozo, na mapendekezo yaliyoandaliwa na mashirika ya kimataifa husika, Tume ya Kodeksi Alimentarius, Shirika la Kimataifa la Afya ya Wanyama, na mashirika ya kikanda na kimataifa ambayo yanafanya kazi ya muundo wa mapatano ya mataifa ya kulinda mimea, bila kuwataka wanachama kubadili ngazi zao sahihi za ulinzi wa binadamu, wanyama au maisha au afya ya mimea. Kwa hivyo, fursa ya kwanza ya nchi inayouza bidhaa nje ya nchi kushawishi mabadiliko ya sheria ya SPS ya nchi inayoagiza, ni kupitia ushiriki wa dhati katika kazi ya mashirika haya na hasa katika uandaaji na kuzikubali sheria za kimataifa za viwango vya SPS. Kwa kuwa kazi ya mashirika ya viwango hufanywa na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya binafsi na watu binafsi inabidi kushirikiana na serikali katika mchakato wa kuandaa kiwango. Njia ya pili kuweza kutoa ushawishi juu ya sheria ya SPS ya nchi zinazoagiza bidhaa inatolewa na taratibu za uadilifu katika mkataba wa SPS. Kama ilivyokwishaelezwa awali (angalia swali 21 na 24), taratibu hizi zinawaagiza wanachama wote wa WTO kutoa taarifa mapema juu ya mapendekezo mapya au marejeo ya sheria na kuyawasilisha mapendekezo hayo kutolewa maoni ambayo yatatiliwa maanani na nchi inayotoa tangazo. Matokeo yake, kila nchi inabidi kufuatilia mtiririko wa matangazo, ambayo husambazwa mara kwa mara na ukatibu wa WTO, na haraka nchi hiyo iweze kuainisha na kuchukua hatua juu ya matangazo ambayo yanaweza kuathiri vibaya biashara. Shirika lililopewa majukumu ya kufuatilia matangazo, inabidi liwe karibu na mashirika binafsi ya sekta ya kibinafsi yanayowakilisha wauza bidhaa nje, kuwapa taarifa zinazowahushu mara kwa mara, na kupokea maoni yao juu ya vikwazo tarajiwa vya biashara. Maamuzi yoyote yaliyoafikiwa kwa pamoja kitaifa, sharti yapelekwe kwenye kituo/mamlaka ya kitaifa ya matangazo. Kama ikiwezekana, mwanachama ambaye anatoa maoni juu ya tangazo la mapendekezo mapya au marejea ya sheria ya SPS anaweza kumwuliza mwanachama anayetoa matangazo kuingiza majadiliano ya masuala husika na njia zinazowezekana kupunguza athari mbaya kwa biashara. Mara nyingi hutokea kwamba katika biashara kuna hatari kwa afya ya wanyama au mimea ambayo nchi inayoagiza itataka kuanza kutayarisha sheria ya SPS chini ya misingi yake tathmini hatari waliyofanya kwa kuwa hakuna viwango vya kimataifa au wanaona viwango hivyo havitoshelezi kenye mazingira yaliyopo. Ili kutambua na kutathmini hatari inayoweza kutokea, nchi inayoagiza inaweza kuhitaji data kutoka katika nchi mgavi. Katika hali hiyo, mazungumzo lazima yaanzishwe kati ya muuzaji wa nje na mnunuzi wa nchi nyigine. Hii ni nafasi nyingine tena kwa mamlaka ya nchi inayouza nje kushawishi maamuzi katika nchi mnunuzi juu ya vigezo vya usimamizi wa hatari zinazoweza kutokea kuhusiana na SPS. Mashirika ya sekta ya kibinafsi katika nchi inayouza nje sharti yasaidie mamlaka katika kuandaa maoni ya kupeleka kwa wenzi katika nchi inayoagiza. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Commonwealth Secretariat and International Trade Centre. Influencing and Meeting International Standards Challenges for developing countries, Vol. Two, Mukhtasari wa bodi za kimataifa za kudhibiti ubora, na jinsi zinajizatiti katika kusaidia nchi zinazoendelea; inajumuisha mifano chavhe za nchi nyingine na jinsi zilijiwezesha kushawishi na kutekeleza viwango vya kimataifa. (Vol. 1: Background Information, Findings from Case Studies and Technical Assistance Needs.) International Organization for Standardization. Joining in. Participating in International Standardization, ISO, Inaelezea uhusishi mwafaka katika viwango vya kimataifa; ni mwongozo bayana wa kozi ya uhusiano bayana na unapambanua jumbe za kimsingi zilizopeanwa kwenye kijitabu My ISO Job'. Supporting stakeholders Disseminating ISO Documents to National Mirror Committees, Huduma ya moja kwa moja inayowawezesha wanachama wa ISO kutoa kila aina ya makala ya kamati ya ISO kwa washikadau wa kitaifa kwa muda mfupi kabisa. Kijikaratasi hichi kinaelezea jinsi huduma hii inatekelezwa na kile wanachama wa ISO wanahitaji kufanya ili kuitumia na kufaidisha washikadau wake. MAREJELEO World Trade Organization. Code of Good Practice for the Preparation, Adoption and Application of Standards. Annex 3 to the Agreement on Technical Barriers to Trade.

85 Mahitaji ya kiufundi Kanuni za RoHS ni zipi na zinaathiri vipi biashara ya nje? Sehemu hii inajadili agizo la jumuiya ya ulaya juu ya zuio la dutu zenye hatari (European Union s Directive on the Restriction of Hazardous Substances (RoHS), mahitaji yake, mawanda ya bidhaa na utekelezaji wake. Kadhalika inatoa habari juu ya kanuni za RoHS duniani. Agizo la Jumuiya ya Ulaya juu ya Zuio la Vitu Hatari Agizo 2002/95/EC la Jumuiya ya Ulaya kuhusu kuzuia matumizi ya baadhi ya dutu zenye hatari katika vyombo vya umeme na elekitroniki lina umuhimu mkubwa kwa watengenezaji na wagavi wa vyombo. Lina shabaha ya kupunguza dutu zenye hatari ambazo tunakabiliana nazo katika maisha yetu ya kila siku na inawezekana kuingia katika mfumo wa ikolojia. RoHS kwa kawaida ni wajibu wa watengenezaji wa vyombo, waagizaji kutoka nje ya Jumuiya ya Ulaya na hata wale wanaobadilisha ishara ndani ya Jumuiya. Pamoja na kuwa lengo kuu la kanuni ya RoHS limekuwa kupunguza risasi (lead) katika bidhaa, linazuia dutu sita: Cadmium; Hexavalent chromium (also known as chromium VI or Cr6+); Lead; Zaibaki Polybrominated biphenyls (PBB); and Polybrominated diphenyl ethers (PBDE). Cadmium hupatikana katika asili ikiwa na zinc; kama zinc isipotakaswa vizuri ulinganifu unaweza kutokuwapo. Hexavalent chromium ina rangi ya mafuta-ya-dhahabu/kijani na bado inatumika kama tabaka la kuzuia kulika kwa chuma na watengenezaji. PBB na PBDE kwa kawaida hutumika kama vizuizi vya ndimi za moto katika plastiki. Mahitaji na bidhaa ndani ya mawanda ya RoHS Agizo la RoHS linahusu vyombo vilivyoainishwa na EU katika Agizo 2002/96/EC juu ya taka za vyombo vya umeme na elektroniki (WEEE). Agizo la WEEE linalenga kupunguza taka zitokanazo na vyombo vya umeme na elektroniki, na kuboresha ufanisi wa kimazingira kwa wale wote wanojihusisha na mzunguko wa maisha wa bidhaa za umeme na elektroniki. Inajumuisha vyombo vya umeme na elektroniki vinavyotumiwa na watumiaji binafsi na wa kitaaluma. Inajumuisha: Vyombo vikubwa na vidogo vya nyumbani; Vyombo teknohama; Vyombo vya mawasiliano (vyombo vya miundombinu havihusiki katika zingine); Vyombo vya wateja; Vyombo kwa ajili ya mwanga; Vifaa vya elekitroniki na umeme; Mwanasesere, vyombo vya starehe na michezo; na Vimiminio vya kujiendesha. Kikomo cha 0.1% kwa uzito wa ukolezi wa kitu chenye mchanganyiko sawia, vikomo hivi havihusiki tu kwa bidhaa kamili, ila hata kwa sehemu, kipuri au dutu ambayo inaweza kutenganishwa na bidhaa. Kwa mfano, kikomo kinaweza kujumuisha sehemu inayotumika katika bodi za saketi iliyopigwa chapa. Kadhalika inaweza ikahusisha plastiki inayohami waya; kwa ujumla kila kitu kinachotumiwa katika ujenzi lazima kikidhi mahitaji ya RoHS. Kati ya vitu ambavyo havihusiki na agizo la RoHS ni betri, pamoja na kuwa na dutu zenye kiasi kikubwa cha sumu. Betri za risasi-asidi, nickel-cadmium na betri za zaibaki ni mifano muhimu. Kadhalika mitambo

86 76 Mahitaji ya kiufundi iliyofungwa na vifaa kiwandani navyo havihusiki; ulinganifu na mahitaji ya vifaa hivi ni jukumu la kampuni inayovitumia. Utekelezaji wa kanuni za RoHS Bidhaa zote katika makundi husika inabidi vikidhi mahitaji (ulinganifu) ya agizo la RoHS kabla ya kuuzwa. Kila nchi ya EU inaweza kuwa na sheria tofauti kidogo, lakini kwa ujumla, watengenezaji au wagavi/waagizaji bidhaa nje inabidi: Wahakikishe bidhaa inayoingia sokoni ikiwa na dutu zilizokatazwa lazima ziwe chini ya kikomo cha juu; Watayarishe nyaraka zinazoonyesha kuwa bidhaa zinakidhi mahitaji; Ripoti sahihi za upimaji uliofanya na maabara mahiri ni sehemu ya nyaraka hizo; Kama mamlaka ya usimamizi yatahitaji kujua, basi toa nyaraka hizo katika kipindi ulichopewa, kwa kawaida huwa mwezi mmoja; na Hakikisha nyaraka za kiufundi zinatunzwa vizuri kwa uchache miaka mnne (4) baada ya mtengenezaji kuacha kuuza bidhaa. Hata hivyo, RoHS ni zaidi ya kutokuwa na risasi katika uzalishaji. Moja ya mwelekeo wa watengenezaji wa vifaa vya elektroniki imekuwa kukubali mchakato wa kutumia rehemu ambazo hazina risasi ili kupata ulinganifu kwa RoHS. Wakati fulani risasi ilikuwa sehemu kubwa ya rehemu, kanuni hii imesaidia katika kuibua rehemu zisizokuwa na risasi. Na sifa zake ni tofauti kidogo na zile zenye risasi, kwa hiyo inahitaji umakini mkubwa katika kuvitumia ili kupata ubora wa hali ya juu kama ambao ulikuwa unapatikana kwa kutumia rehemu zenye risasi. RoHS duniani Kanuni za RoHS ambazo ziko ndani ya agizo la EU, na kwa maoni ukiangalia ukubwa wa soko la EU, mahuruji kwenda EU sharti zikidhi mahitaji. Kwa sababu hii, inafanya matumizi ya kanuni hizi kuwa makubwa duniani; na nchi nyingi zikiwa na ufahamu kuhusu RoHS na kwa hiyo hutengeneza bidhaa ambazo ni linganifu. Kwa hiyo, nchi nyingi zinalikubali agizo la RoHS au wanatengeneza kanuni zenye kukidhi misingi ya agizo hilo. China wameandaa sheria inayofanana na hiyo na wengi wanavifahamu viwango hivyo kama China RoHS. Moja ya tofauti kubwa iliyopo kati ya sheria hii na ile ya EU ni kwamba viwango vya Wachina vinahusisha mawanda ya bidhaa. Katika EU bidhaa hazimo kama hazikuwekwa mahususi kwenye mawanda; katika Uchina kinyume chake kinafanyika. Kutokana na hilo RoHS ya China inaweza jumuisha bidhaa ambazo katika sheria ya EU hazimo. Katika nchi ya Marekani, Jimbo la California limekubali sheria ya RoHS kuanzia January 1, Kanuni za California za RoHS ziko katika misingi ya agizo la EU la RoHS. Nchini Japani, hali ni tofauti kidogo. Utaratibu tofauti unafuatwa; wakati Japani ina sheria ya RoHS, lakini sheria ya Japani ya urejeshaji imefanya wazalishaji kutumia njia zisizo na risasi. Zaidi ya hayo, kuna ziada kijani (green bonus)kwa wazalishaji ambao wanatumia mbinu rafiki kwa mazingira. Jambo linalosaidia uvumishaji wa bidhaa zao. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: National Measurement Office, United Kingdom RoHS-related website: Information on due diligence, enforcement, decision tree, RoHS exemptions, conformity. RoHS Guidance Producer Support Booklet, Kitabu hiki kinatoa mwongozo kwa mzalishaji na/au mnunuzi jinsi ya kuafikia sheria za RoHS.

87 Mahitaji ya kiufundi 77 MAREJELEO European Union. Directive 2002/96/EC, EUR-Lex. European Chemicals Agency (ECHA). Information on RoHS for California. Information on RoHS for China. Information on RoHS for Japan.

88 78 Mahitaji ya kiufundi 27. Kanuni za REACH ni zipi na zinaathiri vipi biashara ya kupeleka bidhaa nje ya nchi? Sehemu hii inaelezea Kanuni juu ya Usajili, Tathmini, Kuruhusu na Kuzuia Kemikali za Jumuiya ya Ulaya (European Community Regulation on Registration, Evaluation, Authorisation and Restriction of Chemicals (REACH), mahitaji yake, mawanda ya bidhaa, utekelezaji, nyaraka za miongozo, na sheria ya upambanuzi husika, uwekaji lebo na ufungashaji (CLP).1 Usajili, Tathmini, Kuruhusu na Kuzui Kemikali (REACH) REACH ni kanuni ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu usajili, tathmini, kuruhusu na kuzuia kemikali. Ilianza kutumika tarehe mosi Juni 2007 kurekebisha na kuendeleza mfumo mkanganyiko wa sheria za Jumuiya ya Ulaya juu ya kemikali na kuchukua nafasi ya sheria mbalimbali 40. Kutokana na mtazamo huu, sheria hii ilikuwa mwafaka, lakini athari za REACH kwenye biashara ni nyingi. REACH inawafanya wafanyabiashara kuchukua majukumu makubwa katika kusimamia mashaka yaliyopo kuwa kemikali zinaweza kuhatarisha afya za watu na mazingira, na inahitaji sekta kutoa maelezo sahihi ya usalama kwa watumiaji. Sambamba na hili inasadikiwa kuwa Jumuiya ya Ulaya, itachukua hatua zaidi kwa dutu ambazo hatari zaidi, pale inapodhihirika kuna haja ya kudhibiti zaidi katika ngazi ya EU. REACH pia imeunda Wakala wa Kemikali wa Ulaya-European Chemicals Agency (ECHA) ambao una wajibu wa uratibu na utekelezaji wa mchakato mzima. Mahitaji na bidhaa chini ya REACH Kwa ujumla REACH inahusisha kemikali zote za viwandani na zile zinazotumika kila siku katika maisha yetu; kwa mfano kemikali za usafi, rangi, nguo, samani na vifaa vya umeme. Hivyo, matumizi ya REACH ni mapana na utangulizi mfupi kama huu hauwezi kuorodhesha bidhaa zote zinazohusika. Wagavi wana wajibu wa kutafuta taarifa zaidi zinazohusika na bidhaa zao. Inawezekana ukatafuta taarifa hizi katika tovuti ya ECHA ambao wana kifaa kinachoweza kurahisha utafutaji, kinaitwa Nahodha (Navigator). Nahodha ni nyenzo inayoingiliana ambayo inawezesha makampuni kupata majibu kwa maswali juu ya dutu na kuweza kubainisha haraka wanataka kufanya nini chini ya REACH. Kama huna mtandao, wasiliana na kituo chako cha kitaifa cha maulizo, shirika lako la viwango (NSB), au shirika la kuendeleza biashara, TPO kwa msaada (angalia swali 23). Sheria zingine zinazosimamia kemikali (k.m. vipodozi, sabuni za maji) na sheria zinginezo (k.m. zinazohusu afya na usalama wa wafanyakazi wanaotumia kemikali kazini, usalama wa bidhaa, bidhaa za ujenzi) ambazo haziko chini ya REACH zinaendelea kutumika. REACH haikuandaliwa ili ilete mkanganyiko/kubishana na sheria zingine za kemikali; sheria hii imekuwa ikitumika na itatumika kwa miaka mingi ijayo. Kwa mfano, Novemba ilikuwa mwisho wa usajili wa dutu ambazo zilikuwa zinazalishwa au zilifika sokoni kabla ya sheria kuanza kutekelezwa. Iilihusu kemikali ambazo zinazalishwa na/au kusambazwa kwa kiwango cha zaidi ya tani 1000 kwa kampuni kwa mwaka;uzito wa kemikali/dutu carcinogenic, mutagenic au sumu kwa uzalishaji uliwekwa kuwa tani 1 au zaidi na kwa dutu zenye sumu kwa mazingira ya maji ilikuwa tani 100 kwa mwaka. Mwisho mwingine ilikuwa 31 Mei, 2013 kwa kiasi cha tani 100 au zaidi kwa mwaka na Mei 31, 2018 kwa kiasi cha tani 1 au zaidi kwa mwaka. Dutu zingine hazifaidiki na huu utaratibu wa sasa, na zinatakiwa kusajiliwa kabla ya kuzalisha, kuagizwa toka nje au kuwekwa sokoni katika Jumuiya ya Ulaya. Imenukuliwa kutoka) and Utekelezaji wa REACH Wazalishaji na waagizaji wa kemikali, wote sharti watambue na kusimamia hatari ambazo zinaweza kutokea kutokana na dutu wanazotengeneza au kuuza. Kwa dutu zinazozalishwa au kuagizwa kutoka nchi za nje kwa kiasi zaidi ya tani moja kwa mwaka kwa kila kampuni, wazalishaji na waagizaji inabidi wadhibitishe kuwa wamefuata taratibu za usajili na kuandaa nyaraka stahiki, ambazo hupelekwa ECHA. Baada ya kupokelewa nyaraka hizo,echa huzikagua kwamba bidhaa ni linganifu kwa utaratibu na kutathmini mapendekezo ya upimaji kuhakikisha kuwa uchunguzi wa dutu kemikali hautaleta upimaji usio

89 Mahitaji ya kiufundi 79 wa lazima, hasa kwa wanyama. Kadri itakavyowezekana, mamlaka nayo yanaweza kuchagua dutu yenye mashaka kwa tathmini pana zaidi. Wazalishaji na waagizaji bidhaa, inabidi wawafahamishe watumiaji wao wa mwisho kwa taarifa kuwa kuna hatari kama hawatatumia dutu kwa usalama. Hili lazima lifanywe kupitia shiti za uchambuaji na mfumo wa kuweka lebo na data za usalama SDS. REACH pia inatarajia kuwa na mfumo wa kuruhusu ukilenga kuhakikisha dutu zenye Shaka Kubwa (Substances of Very High Concern (SVHC) zinadhibitiwa kikamilifu, na kwa kuendelea zinaondolewa kupisha dutu au teknolojia au kutumiwa tu, kama jamii itapata faida kwa matumizi haya. Dutu zimepewa umuhimu katika orodha ya wateja kwenye tovuti ya ECHA, ambayo hurejelewa kila baada ya kipindi cha miezi sita. Baada ya kukamilika, kiwanda kinatakiwa kuwasilisha maombi kwa wakala kwa kupata kibali cha kuendelea kuvitumia. Zaidi ya hayo, mamlaka za EU zinaweza kuweka vizuizi vya kuzalisha, kutumia au kuuza dutu zinazohatarisha afya ya binadamu au mazingira. Dutu zinaweza kusamehewa kwa yote au baadhi ya mahitaji ya REACH. Taarifa kuhusu msamaha zinapatikana kupitia Nahodha kwenye tovuti ya ECHA. Makampuni yanahimizwa kumtumia Nahodha kujua kama dutu zao zimesamehewa chini ya REACH. Mwongozo wa kutekeleza REACH Nyaraka zenye maelekezo zimeandaliwa katika miaka michache iliyopita kwa ajili ya sekta na mamlaka, ili zisaidie katika utekelezaji mzuri wa REACH. Nyaraka hizo ziliandikwa na kujadiliwa ndani ya miradi inayosimamiwa na huduma za Tume ya Ulaya, ikijumuisha wadau kutoka viwandani, nchi wanachama na mashirika yasiyo ya kiserikali. Nyaraka za miongozo zilizokamilika zilichapishwa na kuwekwa kwenye tovuti ya ECHA. Maeneo ya kuchangisha msaada ya kitaifa yameanzishwa katika kila nchi mwanachama wa EU, kwa ajili ya kutoa ushauri kwa viwanda na wadau juu ya wajibu wao na jinsi ya kuutimiza kwa mujibu wa REACH, hasa kuhusiana na usajili. Sheria ya Kupambanua, Kuweka Lebo na Ufungasha (CLP) Upande mmoja muhimu wa Sheria ya EU wenye athari nyingi inayohusiana na REACH; ni kanuni za upambanuzi, kuweka lebo na ufungashaji wa dutu na michanganyiko iliyomo katika Sheria (EC) Na. 1272/2008. Kanuni hii inawataka watengenezaji wa bidhaa hizi kuwasilisha upambanuzi na yaliyomo kwenye lebo (uwasilishaji huu hujulikana kama taarifa) kwa ECHA. Taratibu za kutoa taarifa za CLP za dutu umeanza kutekelezwa tangu Desemba 1, 2010; ikilinganishwa na za michanganyiko itakuwa Juni 1, Kutokana na taaratibu hizi, ECHA itakuwa na Orodha ya Upambanuzi na Uwekaji Lebo, ambayo hatima yake ni kuchukua nafasi ya orodha tatu tofauti ambazo zilikuwa zinatunzwa na mamlaka za EU. Kama bidhaa yako ilikuwa imepangwa katika moja ya orodha za zamani, itabidi uipambanue upya na kuwasilisha taarifa kama inavyotakiwa. Kuna msururu wa nyaraka nyingi za miongozo kuhusu CLP zilizoandaliwa na kuwekwa kwenye tovuti ya ECHA. Watengenezaji na waagizaji wa bidhaa kutoka nje wanawajibika kutoa taarifa kwa ECHA ifikapo Januari 2011 kuhusu upambanuzi wa dutu zilizoingizwa kwenye soko kwamba: Kufuatana na masharti ya usajili wa REACH (dutu ambazo zilitakiwa kusajiliwa ifikapo Novemba 30, 2010, uwasilishaji ulikuwa sehemu ya jarida la usajili); Imepambanuliwa kama ni hatari (bila kujali ujazo/kiasi chake); Katika mchanganyiko kuzidi vikomo vya kukolea na kuhitaji kupambanuliwa. Inabidi kuzitambua dutu au michanganyiko ambayo uuzaji wake unadhibitiwa na agizo 98/8/EC (juu ya viuauhai) au na agizo 91/414/EEC (juu ya bidhaa za kulinda mimea) kwamba nazo zinahusika na CLP. Hii ina maana kwamba, dutu kufatana na maagizo hayo au bidhaa inayoweza kuuauhai au kuawadudu (mchanganyiko) iliyo aina hiyo ya dutu sharti iwekewe lebo na kupambanuliwa chini ya CLP pia.

90 80 Mahitaji ya kiufundi KWA TAARIFA ZAIDI ECHA. Navigator. Viashiria vya kutambua iwapo bidhaa inapatikana katika REACH na CLP; inawasaidia wazalishaji, wanunuzi, wateja wa chini, wasambazaji wa bidhaa za kemikali, na waandishi au wannunuzi wa makala kutambua mahitaji yao chini ya REACH. European Commission. Enterprise and Industry website on REACH. Inatoa ujumbe juu ya REACH, jinsi inavyofanya kazi, usajili, ukaguzi, ruhusa, vigezo, na mikazo; inapeana ujumbe juu ya CLP, jinsi inavyofanya kazi, bidhaa hatari, karatasi salama za data, na jinsi ya kujielekeza kwenye maabara. MAREJELEO European Chemicals Agency (ECHA). Regulation (EC) No. 1272/2008 on classification, labelling and packaging of substances and mixtures.

91 Mahitaji ya kiufundi Mahitaji ya ufungashaji wa bidhaa zangu ni yapi? Somo la mahitaji ya vifungashio ni changamani, lakini kwa ujumla mahitaji haya inabidi yaangaliwe kwa muktadha wa soko na sheria zilizopo kuhusiana na vipimo (ugezi), ukamilifu wa ufungashaji na athari kwa mazingira ya vifungashio. Kwa hiyo, ni muhimu kuliangalia suala la vifungashio kwa makini. Mahitaji ya lazima inapaswa yatimizwe kwa kuwa mahuruji ambayo hayakidhi mahitaji yanaweza kukataliwa katika nchi yalikopelekwa au hata yakiwa njiani. Wakati mwingine hutokea bidhaa zikarudishwa katika nchi zilikotoka na kusababisha hasara kubwa kwa aliyezipeleka. Sehemu hii inajadili mahitaji ya masoko, ugezi wa kibiashara, ukamilifu wa ufungashaji na, shauku za kimazingira ambazo unastahili kuzitilia maanani. Kadhalika inaelezea baadhi ya viwango vya ufungashaji ambavyo unaweza kuvihitaji, kutegemeana na aina ya bishara na kule bidhaa zinatarajiwa kwenda/kuuzwa. Mahitaji ya masoko Usanifu au muonekano wa kifungashio unasaidia sana katika kufanikiwa kwako katika masoko. Kifungashio ndiyo kitu cha kwanza ambacho mteja anaona, na usanifu/muonekano mzuri ndiyo nguzo ya kuvuta hisia za mteja na kumwelekeza kwenye bidhaa yako kati ya zingine nyingi zilizopo. Kwa sababu hiyo, inahitaji utumie wataalam wa usanifu katika kuandaa vifungashio vyako. Taasisi za ufungashaji na mashirika mengi ya kuendeleza biashara yanaweza kukusaidia katika hili. Wengine hutoa huduma zao za usanifu hata kwa wenye tasnia ndogo na za wastani (SMEs); kwa hivyo ni vyema ukawasiliana na shirika lako la kuendeleza biashara au taasisi ya ufungashaji kwa msaada. Kadhalika, wenye maduka makubwa ya rejareja mara nyingi huwa na mahitaji mahususi ya ufungashaji na uwekaji wa lebo, ambayo wewe kama mgavi sharti uyatimize Mahitaji ya ugezi wa kibiashara Kuna mahitaji kiasi ya ugezi wa lazima katika ufungashaji yanayotekelezwa katika nchi mbalimbali. Nchi nyingi zimeweka mahitaji ya ugezi wa kibiashara au kisheria (wakati mwingine huitwa vipimo ) kwa bidhaa zilizofungashwa. Mahitaji haya hayahusishi tu uzito, ujazo na vipimo vya kiasi, lakini pia vinajumuisha ufungashaji wenyewe na kuelekeza ujazaji, mfano nafasi ya kuacha wazi ndani ya kifungashio baada ya kujaza bidhaa. Mahitaji haya kwa kawaida yametayarishwa yakifuata mapendekezo ya Shirika la Kimataifa la Ugezi wa Kisheria (OIML), ambayo yanapatikana bila malipo kwenye tovuti ya shirika hilo. Hata hivyo, ni vizuri zaidi kupata taarifa kutoka katika nchi unayotarajia kupeleka bidhaa (angalia swali 23); maana nchi nyingi huyabadilisha mapendekezo ya OIML ili kulingana na taratibu na ushuru wa ndani. Idara yako ya kitaifa ya vipimo, pia inaweza kukupa taarifa kuhusu mahitaji ya masoko muhimu ya ng ambo. Ukamilifu wa vifungashio na shauku za kimazingira Kama kuna kanuni za kiufundi au sheria ya SPS kuhusu mazao au bidhaa; mara nyingi huwa zina mahitaji ya ufungashaji wa bidhaa au zao husika. Unalazimika kuzisoma na kuzielewa vizuri na kuzitekeleza kikamilifu. Katika nchi nyingi kwa kuongezea, zinaweka masharti ya jumla ya ufungashaji kuhakikisha kunakuwa mwendelezo wa ukamilifu katika ufungashaji wakati wa usafirishaji na kuzingatia athari kwa mazingira vikitupwa. Kuana taarifa kidogo hapa chini kuhusu viwango vy ufungashaji katika Jumuiya ya Ulaya. Mifano zaidi imetolewa ya viwango vilivyotayarishwa na mashirika mbalimbali kwa ajili ya ufungashaji na usafirishaji wa mizigo/bidhaa hatari. Jumuiya ya Ulaya Katika ngazi ya lazima, Jumuiya ya Ulaya imetangaza rasmi Agizo 94/62/EC la Desemba 20, 1994 kuhusu Vifungashio na Taka za Vifungashio (na miswada ya marekebisho) na imechapisha viwango vya Ulaya vilivyopatanishwa (EN EN 13432) ambazo inaaminiwa kukidhi viwango vinavyotakiwa kulitekeleza agizo. Mahitaji yanajumuisha chupa, mifuko ya plastiki au makasha ambamo bidhaa imewekwa, pamoja na katoni kwa ufungashaji wa jumla; matoroli ya mbao ambapo bidhaa zimerundikwa na shiti ya plastiki iliyofunika mzigo wote. Baadhi ya gundi zilizokuwa zinatumika kutengenezea makasha zimepigwa marufuku; wino wa kupigia chapa hautakiwi kuwa na risasi, na mbao zinazotumika kutengenezea matoroli ziandaliwe kwa namna ambayo hazitakuwa na minyoo ya mbao au wadudu ambao wanaweza kuingizwa katika mfumo wa mazingira (sheria ya SPS-angalia swali 19) wa nchi inayoagiza bidhaa.

92 82 Mahitaji ya kiufundi Mpango wa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa ufanisi (The Green Dot scheme) (vilevile tazama swali 78) umejumuishwa katika Agizo la Vifungashio na Taka za Vifungashio na, linazihusu kanuni zote kama wanafungasha bidhaa; mpango huu unawataka wazalishaji kuchangia gharama za kurejeresha na kufanya tena upya kupitia leseni ya mpango wa Green Dot uwepo wa kodi zingine. Kufuatana na Agizo, kama kampuni haijiungi na mpango wa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa ufanisi, itabidi ifanye kazi ya kukusanya mabaki ya vifungashio kwa ajili ya kutumika tena yenyewe, ingawa hii ni shughuli ngumu kutimiza kwa bidhaa zinazozalishwa kwa wingi, inawezekana tu kwa wazalishaji wa bidhaa chache. Mamlaka za usimamizi katika kila nchi zimepewa uwezo wa kutoza faini kwa makampuni ambayo hayakidhi viwango, hata hivyo utekelezaji wa sheria unatofautiana kati ya nchi na nchi. Tangu mpango huu uanzishwe, umeweza kuambaa katika nchi 23 za Ulaya. Ufungashaji na usafirishaji wa mizigo hatari Maelekezo ya kiufundi juu ya usafirishaji wa mzigo hatari kwa ndege; Kitengo cha Mauzo cha Mamlaka ya Anga (ICAO). Montreal, Canada. Kanunu za mizigo hatari. Chama cha Kimataifa cha usafiri wa Anga (International Air Transport Association (IATA). Ulaya Makubaliano ya Wazungu kuhusu uchukuzi wa kimataifa wa mizigo hatari kwa njia ya barabara (ADR) itifaki ya saini, ISBN (Vol. 1) na ISBN (Vol. 2), Tume ya Uchumi ya Ulaya ya Umoja wa Mataifa (UN-ECE), Usafiri wa baharini Kanuni ya Kimataifa kuhusu usafiri wa mzigo ya haatari baharini (International Maritime Dangerous Goods (IMDG) Code. ISBN , Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Bahari (International Maritime Organization), IMO Publishing Service Umoja wa Mataifa Mapendekezo juu ya usafirishaji wa mizigo hatari: Kanuni za Mfano. ISBN , Umoja wa Mataifa, United Nations. United Nations Publication Service, Palais des Nations, Geneva 10, CH =1211, Switzerland. Tel: , Fax: , Internet: KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: EN 13427:2004, Packaging Requirements for the use of European Standards in the field of packaging and packaging waste. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako. EN 13428:2004, Packaging Requirements specific to manufacturing and composition Prevention by source reduction. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako. EN 13429:2004: Packaging Reuse. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako. EN 13430:2004, Packaging Requirements for packaging recoverable by material recycling. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako.

93 Mahitaji ya kiufundi 83 EN 13431:2004, Packaging Requirements for packaging recoverable in the form of energy recovery, including specification of minimum inferior calorific value. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako. EN 13432:2000, Packaging Requirements for packaging recoverable through composting and biodegradation Test scheme and evaluation criteria for the final acceptance of packaging. Inapatikana katika bodi kitaifa za kudhibiti ubora/viwango za nchi wanachama wa muungano wa Ulaya, au pia yawezapatikana katika bodi za kudhibiti ubora/viwango katika nchi yako. International Trade Centre. Export Packaging website. Nyaraka za upakiaji zaweza kupatikana katika tovuti hii. Pia, inaonyesha tovuti zinazoelekeza kwenye jumbe za sheria za kutia alama au lebo katika bidhaa katika nchi nyingi; vile vile inatoa marejeleo yanayozingatia mazingira ya bidhaa tofauti tofauti. MAREJELEO European Parliament and Council Directive 94/62/EC of 20 December 1994 on packaging and packaging waste. EUR-Lex, European Union. Green Dot. Wikipedia. International Air Transport Association (IATA). Dangerous Goods Regulations (DGR). International Civil Aviation Organization (ICAO). International Maritime Dangerous Goods (IMDG) Code. International Maritime Organization, International Organization of Legal Metrology (OIML). United Nations Recommendations on the transport of dangerous goods: Model Regulations Recommendations on the transport of dangerous goods: Model Regulations, ISBN United Nations. Publication Service.

94

95 MIFUMO YA USIMAMIZI

96

97 Mifumo Ya Usimamizi 87 A. MIFUMO YA USIMAMIZI WA UBORA 29. Nini maana ya familia ya viwango vya ISO 9000 na kwa kiasi gani viwango hivyo hutumika? Je vinasaidia biashara ya nje? Ilikuwa mwaka 1987 ambapo Shirika vya Viwango la Kimataifa (International Organization for Standardization (ISO) lilianzisha na kuchapisha ISO 9001, 9002 na 9003 na miongozo mingine inayohusika na viwango vya kimataifa. Hii ilisababisha kuzaliwa kwa familia ya viwango ya 9000 iliyo maarufu hadi sasa. Marekebisho ya kwanza ya viwango vya ISO 9001, 9002 na 9003 yalifanywa mwaka 1994 bila ya mabadiliko mengi katika muundo wake. Marekebisho makubwa ya pili yalifanyika mwaka 2000, ambapo ISO 9001, 9002 na 9003 nafasi yake ilichukuliwa na kiwango kimoja ISO 9001:2000 Mifumo ya usimamizi ya ubora-mahitaji. Hiki kilirekebishwa tena mwaka 2008 kama ISO 9001:2008. Matoleo yote ya mwaka 2000 na 2008 ya viwango vya ISO 9001 yanahamasisha kupitishwa/kukubalika kwa mbinu ya mchakato. Familia ya ISO 9000 Familia ya viwango ya ISO 9000 inawakilisha makubaliano ya kimataifa kuhusu utendaji bora wa usimamizi bora. Inajumuisha viwango na miongozo inayohusiana na mifumo ya usimamizi bora yaani quality management systems (QMS) na viwango visaidizi. Familia ya ISO 9000 inashirikisha viwango vikuu vinne vifuatavyo: Viwango vya ISO na yaliyomo Viwango ISO 9000:2005 ISO 9001:2008 ISO 9004:2009 ISO 19011:2011 Chanzo: S.C. Arora, India. Yaliyomo Inaeleza misingi, dhana umuhimu na istilahi zinazotumiwa katika kundi la viwango vya ISO. Inafananua mahitaji ya QMS, lengo lake likiwa kuliwezesha shirika kuendelea kutoa huduma zinazolizisha wateja wake. Ndiyo kiwango pekee katika kundi la ISO 9001 ambayo mashirika yanaweza kupata uhakiki. Inatoa mwongozo wa jinsi shirika linaweza kuwa na mafanikio endelevu kwa kutumia misingi ya usimamizi bora. Inaelekeza juu ya misingi ya ukaguzi, usimamizi wa programu za ukaguzi, kufanya ukaguzi wa mfumo wa usimamizi wa ubora, kadhalika maelekezo juu ya ufanisi wa wakaguzi wa ubora na mfumu wa usimamizi wa mazingira. Kupitishwa kwa viwango vyote vilivyochapishwa na ISO, ikijumuisha viwango katika familia ya ISO 9000, ni hiari kiasilia. Nchi nyingi zimepitisha viwango vya familia ya ISO 9000 kama mfumo wa hesabu zake kwa ajili ya viwango vyao vya taifa. Kwa mfano huko Uingereza, ISO 9001 inafahamika kama BS EN ISO 9001:2008, BS ikimaanisha British Standard na EN European Norm. Huko Sri Lanka viwango huandikwa SLS ISO 9001:2008, SLS ikimaanisha Sri Lankan Standard. Viwango vya ISO vinaweza kununuliwa kama programu au kitabu (hard or soft version) kupitia tovuti ya ISO mtandaoni. Ofisi yako ya viwango vya taifa inaweza pia kuuza machapisho ya ISO pamoja na toleo lake lililochapishwa la viwango hivi (unaweza pia ukalipia kiasi kidogo kwa toleo la taifa). ISO 9001 ISO 9001 inaweza kutumika kwa sekta zote za uzalishaji, ikiwa ni pamoja na viwanda na huduma, na kwa mashirika ya aina zote. Sio viwango vya bidhaa bali viwango vya mfumo wa menejimenti vinavyotakiwa kuonyesha uwezo wa shirika mara kwa mara ili kutoa bidhaa au huduma ambazo zinafikia mahitaji ya mteja na udhibiti. ISO 9001 inaweka bayana nini kinahitajika kufanywa na shirika lakini haionyeshi wazi namna gani kifanyike, hivyo kukupa uhuru mwingi wa kuendesha biashara yako. Mbali na hayo, ISO 9001 haipangi

98 88 Mifumo Ya Usimamizi kiwango chohote cha ubora. Wewe na wateja wako ndio wanaotakiwa kufanya hivyo. Viwango vitakusaidia wewe kufikia ngazi unayoitaka. Kwa mfano, kama ukiweka lengo kuwa asilimia 99 ya muda fulani utatimiza ahadi unazozitoa, mfumo utakusaidia wewe kufanya hivyo. Katika ngazi zote za kitaifa na kimataifa, uthibitisho wa ISO 9001 wa mashirika ya uthibitisho yenye kibali yamepata kibali sehemu nyingi. Mnamo tarehe 31/ , vyeti vya ISO 9001 vilitolewa katika nchi 178. Shea/ushiriki mkubwa (47%) ulifanikiwa Ulaya, ikifuatiwa na 37.4% katika mashariki ya mbali, 7.3% Afrika na Magharibi mwa Asia, 3.4% katika Amerika ya kati na kusini na 1.0% Australia na New Zealand 3%. ISO 9001 na biashara ya nje Familia ya viwango ya ISO 9000 inazidi kuwa ishara ya ubora katika sekta ya viwanda na huduma. Itaweza kuleta uaminifu mkubwa wa wateja kwa kuwa utekelezaji unahakikisha kwamba mahitaji ya mteja na matarajio yanaendelea kutimizwa na kupunguza au kuondoa malalamishi ya wateja. kampuni ndogo na za wiastani za zinazidi kufanya uamuzi wa kutumia familia ya viwango vya ISO 9000 mara nyingi kwa sababu wateja wao wanatarajia wao kuwa navyo. Kuzingatia viwango vya ISO kunaweza pia kutangazwa ili kupata upenyo wa soko nje ya nchi kwasababu wanunuzi wengi wa kigeni wanalipia bonasi kwa uwepo wa viwango hivi. Nyaraka za mwongozo Kwa kuongezea kwenye viwango vya kimataifa vya hapo juu, kuna idadi ya muongozo wa viwango na stakabadhi za muongozo zinazotoa msaada katika kutekeleza na kuboresha QMS (mfumo wa usimamizi bora). Nyaraka hizi zimeorodheshwa hapa chini. Kama ilivyo kwa viwango vya ISO, hivi pia vinaweza kununuliwa mtandaoni kutoka kwenye tovuti ya ISO au kutoka kwenye mashirika ya viwango ya taifa lako. Viwango vya mwongozo ISO 10001, Quality Management (TQM) Kuridhika kwa mteja Miongozo ya sheria za mienendo ya mashirika ISO 10002:2004, usimamizi bora Kuridhika kwa mteja Miongozo kwa ajili ya malalamishi yanayoshughulikiwa ISO 10003:2007, usimamizi bora Kuridhika kwa mteja Miongozo kwa ajili ya usuluhishi wa migogoro nje ya mashirika ISO/DIS 10004, usimamizi bora Kuridhika kwa mteja Miongozo kwa ajili ya ufuatiliaji na vipimo ISO 10005:2005, Mifumo ya usimamizi bora Miongozo kwa ajili ya mipango bora ISO 10006, Miongozo kwa ajili ya usimamizi bora katika miradi Nyaraka za mwongozo * ISO 9001 Ina maana gani katika mlolongo wa ugavi/usambazaji p_standards/quality_management/more_resources_9000/9001su pchain.htm * Uchaguzi na matumizi ya familia ya viwango ya ISO * Kanuni za usimamizi bora * Kutangaza ISO 9001:2008 zako au uthibitisho wa ISO 14001: ** ISO 9001 kwa ajili ya biashara ndogo Nini cha kufanya: Ushauri kutoka ISO/TC ** Matumizi jumuishi (integrated use) ya viwango vya mfumo wa usimamizi wa (The integrated use of management system standards )

99 Mifumo Ya Usimamizi 89 Viwango vya mwongozo ISO 10007:2003, Mifumo ya usimamizi bora Miongozo ya usimamizi wa muundo ISO/TR10013:2001, Miongozo ya nyaraka za QMS ISO 10014:2006, Usimamizi bora Miongozo ya kutambua faida za kimaslahi na kiuchumi Nyaraka za mwongozo *1 Kuanzishwa na msaada wa jumla: muongozo kuhusu michakato ya kufanya kazi na wasambazaji wa nje *2 Kuanzishwa na msaada wa jumla: Muongozo kuhusu mahitaji ya nyaraka za ISO 9001:2008 ISO/TR10013:2001, Miongozo ya nyaraka za QMS *3 Kuanzishwa na msaada wa jumla: Muongozo juu ya nadharia na matumizi ya mbinu ya mchakato kwa ajili ya mifumo ya usimamizi *4 ISO 9000 Kuanzishwa na msaada wa jumla: Muongozo kuhusu istilahi iliyotumika katika ISO 900I na SO 9004 ISO 10015:1999, Usimamizi bora Miongozo ya mafunzo ISO/TR 10017:2003, Muongozo wa mbinu za kitakwimu za ISO 9001:2000 ISO/DIS 10018, Usimamizi Miongozo juu ya uhusika wa watu na ushindani ISO 10019:2005, Miongozo ya uchaguzi wa washauri wa mfumo wa Usimamizi bora ISO/IEC 90003:2004, Uhandisi wa programu - Miongozo kwa ajili ya maombi ya ISO 9001:2000 kwa programu za kompyuta 9001:2000 to computer software *Nyaraka hizi zinaweza kuchukuliwa bure kutoka kwenye tovuti ya ISO ** Nyaraka hizi zinaweza kununuliwa ISO. *1 Inaweza kuchukuliwa bure kutoka: sses.htm *2 Inaweza kuchukuliwa bure kutoka: n_requirements_of_iso_9001_2008.htm *3 Inaweza kuchukuliwa bure kutoka: ss_approach_for_management_systems.htm *4 Inaweza kuchukuliwa bure kutoka: KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Grajek, Michal. ISO 9000: New Form of Protectionism or Common Language in International Trade? ESMT European School of Management and Technology. Inapitia maandiko yanayozingatia jukumu la mitandao katika kupunguza gharama za taarifa zinazohusiana na biashara za kimataifa. Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Shirika la Viwango la Kimataifa (International Trade Centre and International Organization for Standardization). ISO 9001 kwa ajili ya biashara ndogo Nini cha kufanya: Ushauri kutoka ISO/TC 176, ISBN Kinapatikana kutoka ISO au kwa wanachama wa (list at Kitabu hiki kinatoa mwongozo kwa mashirika madogo kuhusu kuboresha na kutekeleza mfumo wa usimamizi bora kwa kulenga ISO 9001:2008. Kinatoa ushauri kadhaa wa kiutendaji kuhusu chaguzi tofauti unazohitaji kuanzisha kwa mfumo wa usimamizi bora katika shirika lako au kuliboresha lililoko.

100 90 Mifumo Ya Usimamizi International Organization for Standardization ISO catalogue. MAREJEO ISO 9001:2008, Mfumo wa usimamizi bora Mahitaji. Inapatikana kutoka ISO au kwa wanachama wa ISO (orodha katika Utafiti wa vyeti vya ISO 9000 vilivyotolewa mwezi wa kumi na mbili

101 Mifumo Ya Usimamizi Ni yapi matoleo rasmi ya kisekta ya ISO 9000? ISO/TC 176, kamati ya kiufundi inayowajibika na uboreshaji wa familia ya viwango ya ISO 9000 ilikuwa na mtazamo kwamba ISO 9001, kwa kuwa viwango vya jumla, vinaweza kutumika na sekta yoyote ya uzalishaji, ikiwa ni pamoja vifaa, sekta ya vitu vilivyosindikwa, huduma na programu. Hatahivyo, sekta maalum za uzalishaji, kama vile gari, miundombinu, anga, vifaa vya madawa, mafuta na gesi, na sekta za teknolojia ya mawasiliano, ziliona zinahitaji mahitaji maalum ya QMS katika kuongezea yale yaliyojumuishwa katika ISO Hii ilipelekea uboreshaji wa viwango vya QMS vya sekta maalum, kwa kutumia vyote ISO na kwa makundi ya viwanda kama ilivyoelezewa hapa chini. Viwango vya sekta maalum vilivyochapishwa na ISO; 1. Viwanda vya magari ISO/TS 16949:2009. Mifumo ya usimamizi bora Quality Mahitaji fulani kwa ajili ya maombi ya ISO 9001:2008 kwa ajili ya uzalishaji wa magari na huduma husika kwa mashirika. for automotive production and relevant service part organizations Vipimo hivi vya kifundi, yaani technical specification (TS) vilianzishwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1999 na International Automotive Task Force (IATF), ikiwa na wawakilishi wa watengenezaji tisa wakubwa wa magari nchini Marekani na Ulaya na wawakilishi wa ISO/TC 176. Toleo lake la karibuni, ISO/TS 16949:2009, linashirikisha mahitaji ya ISO 9001:2008 (yameandikwa ndani ya boksi) na maelezo ya mahitaji ya sekta maalum ya nyongeza (yamewekwa nje ya viboksi) kwa ajili ya ufanisi wa wafanyakazi, ufahamu na mafunzo, ubunifu na maendeleo, uzalishaji na utolewaji huduma, udhibiti wa ufuatiliaji na vifaa vya vipimo, na vipimo, uchambuzi wa data na uboreshaji. Mradi wa kawaida wa uthibitisho wa kimataifa kwa ajili ya TS hii (tofauti na ule unaotumika na ISO 9001) umeanzishwa/kuboreshwa na IATF kwa uthibitisho wa wauzaji wa magari. 2. Vifaa vya matibabu ISO 13485:2003. Vifaa vya matibabu. Mifumo ya usimamizi bora. Mahitaji kwa ajili ya madhumuni ya udhibiti Kiwango hiki kimelenga katika kanuni za kimataifa za vifaa vya matibabu pamoja na mahitaji ya QMS katika ISO Imedhamiriwa kwa matumizi ya mashirika yaliyohusika katika ubunifu, uzalishaji, ufungaji mitambo na huduma kwa vifaa vya matibabu pamoja na huduma nyingine husika. Ripoti ya kifundi (techinical report -TR) ya mwongozo wa maombi ya ISO pia imechapishwa na ISO kama ISO/TR Vifaa vya msingi vya ufungaji wa bidhaa za dawa ISO 15378:2011 Vifaa vya msingi vya ufungaji wa bidhaa za dawa mahitaji husika kwa maombi ya ISO 9001:2008, kwa kurejea uzalishaji bora yaani( Good Manufacturing Practice (GMP). Kiwango hiki cha kimataifa kinabainisha mahitaji ya mfumo wa bora ambapo shirika linahitaji kuonyesha uwezo wake wa kutoa vifaa vya msingi vya ufungaji wa bidhaa za dawa ambazo zinatimiza mahitaji ya mteja mara zote pamoja na mahitaji ya udhibiti na viwango vya kimataifa kwa ajili ya vifaa vya msingi vya ufungaji. Ni viwango vinavyotumika kwa ajili ya ubunifu, utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya msingi vya ufungaji wa bidhaa za dawa. Pia vinaweza kutumika kwa ajili ya madhumuni ya uthibitisho. 4. Viwanda vya Mafuta ya petroli, usindikaji wa petroli na gesi asilia ISO/TS 29001:2010. Viwanda vya mafuta ya petroli, usindikaji wa petroli na gesi asilia. Mifumo ya usimamizi mkuu bora kwa sekta maalum Mahitaji ya mashirika kwa usambazaji wa bidhaa na huduma. TS hii inafafanua mfumo wa usimamizi bora kwa mashirika ya usambazaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya viwanda vya petroli, usindikaji wa petroli na gesi asilia. Imekusudiwa kuhakikisha usalama na uhakika wa vifaa na huduma katika kipindi chote cha msururu wa usambazaji na usindikaji wa petroli,

102 92 Mifumo Ya Usimamizi mafuta na gesi. Imedhamiriwa kwa matumizi ya wazalishaji, wanunuzi na watoa huduma wa vifaa na nyenzo zinazohitajika katika viwanda vya usindikaji wa petroli, mafuta na gesi. Viwango vyote hapo juu vinaambatana kabisa na ISO 9001:2008 (vile ambavyo ni sambamba na ISO 9001:2000 vinarudiwa upya ili kulingana na ISO 9001:2008). Hawajachanganya au kurekebisha mahitaji ya viwango vya jumla vya ISO 9001, lakini wameongea baadhi ya mahitaji ya sekta-maalum, miongozo na ufafanuzi. Uthibitisho wa mashirika ya uthibitisho yenye kibali unapatikana kwa viwango vyote. Hadi mwishoni mwa 2009, jumla ya vyeti vilitolewa kwa ISO/TS na vyeti kwa ISO Maelezo ya mipango ya uthibitisho kwa ajili ya viwango hivi yanaweza kupatikana kutoka kwenye mashirika ya uthibitisho au kutoka kwenye tovuti zao. Miongozo ya viwango vya sekta-maalum na IWAs iliyochapishwa na ISO Kwa kuongezea katika viwango vya sekta-maalum ambavyo vinaweza kutumika kwa ajili ya ufafanuzi pia, ISO imeweka miongozo ya viwango vifuatavyo na mapatano ya warsha ya kimataifa [international workshop agreements (IWAs)]. Mwisho ni nyaraka za ISO zilizotengenezwa kupitia mikutano ya warsha na si kwa kupitia mchakato wa kamati za kiufundi. 1. ISO/IEC 90003:2004 Uhandisi wa programu Miongozo kwa ajili ya matumizi ya ISO 9001:2000 kwa programu za kompyuta Hiki kinatoa mwongozo kwa mashirika katika kutumia ISO 9001:2000 kwa upatikanaji, usambazaji, maendeleo, shughuli na maandalizi ya programu za kompyuta na huduma husika zenye msaada. (Mwongozo wa kiwango hiki upo chini ya marekebisho ili kuulinganisha na ISO 9001:2008.) 2. ISO 16106:2006 Ufungaji Fedha za usafiri kwa bidhaa zenye madhara Ufungaji wa bidhaa zenye madhara, Vyombo vya kubeba bidhaa zenye wingi wa wastani-[ intermediate bulk containers (IBCs)] na ufungaji mkubwa Miongozo kwa maombi ya ISO 9001 Hi inatoa muongozo juu ya masharti ya usimamizi bora yanayotumika kwenye utengenezaji, upimaji na ufuatiliaji wa kubuni aina ya ufungaji wa bidhaa zenye madhara zilizopitishwa, (intermediate bulk containers) na ufungaji mkubwa. 3. ISO 22006:2009 Mifumo ya usimamizi bora miongozo kwa ajili ya matumizi ya ISO 9001:2008 kwa uzalishaji wa mazao Hiki kinatoa miongozo kuhusu matumizi na utumiaji wa ISO 9001:2008 kwa uanzishwaji na usimamizi wa mfumo wa usimamizi bora na shirika lililohusika katika uzalishaji wa mazao. Kiwango hiki kimewezesha uelewa wa lugha ya ISO 9001:2008 kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji wa mazao. 4. IWA 1:2005 mifumo ya usimamizi bora Miongozo kwa ajili ya maboresho ya mchakato katika mashirika ya huduma za afya. Hiki kinatoa muongozo kwa shirika lolote la huduma za afya linalohusika katika usimamizi, utoaji au utawala wa huduma/bidhaa za huduma ya afya, ikijumuisha mafu nzo na/au utafiti, katika mchakato wa utoaji maisha kwa binadamu, bila ya kujali aina, kiwango, na bidhaa au huduma inayotolewa. 5. IWA 2:2007 Mifumo ya usimamizi bora Miongozo kwa ajili ya matumizi ya ISO 9001:2000 katika elimu Hiki kinatoa miongozo kusaidia mashirika ambayo yanatoa bidhaa za kielimu za aina yoyote ili kutekeleza mfumo thabiti wa usimamizi bora unaotimiza mahitaji ya ISO 9001: IWA 4:2009 Mifumo ya usimamizi bora Miongozo kwa ajili ya matumizi ya ISO 9001:2008 katika serikali za mitaa Hiki kinazipa serikali za mitaa miongozo ya matumizi ya hiari ya ISO 9001:2008 katika misingi imara. Inasaidia serikali za mitaa kuwahakikishia masharti nafuu ya kutegemea michakato ambayo ni muhimu kwa kutoa huduma zinazohitajika kwa wananchi wake katika mazingira endelevu na ya kuaminika.

103 Mifumo Ya Usimamizi 93 Miongozo ya viwango vya hapo juu na IWAs haiongezi, haifanyi mabadiliko au hata kwa njia nyingine kuboresha mahitaji ya ISO 9001:2000 au ISO 9001:2008 na haikusudiwi kwa ajili ya kutumika katika mikataba ya tathmini ya ulinganifu au uthibitisho. Hatahivyo, inasaidia mashirika husika katika kuendeleza ISO 9001 QMS kwa bidhaa na huduma zilizotajwa hapo juu na baadaye kupata uthibitisho dhidi ya ISO Viwango vya sekta-maalum vilivyoanzishwa na mashirika mengine 1. Telecommunications industry: TL 9000 (sekta ya mawasiliano) TL 9000 ni seti ya mahitaji maalum ya mfumo wa usimamizi bora ya mawasiliano, uliochapishwa na jukwaa la uongozi wa shirika la Quality Excellence for Suppliers of Telecommunications (QUEST) Leadership Forum. Jukwaa linawapa wanachama wake seti ya nyaraka zinazolenga utendaji, mahususi kwa kutambua kilicho bora katika daraja, yaani the best in class kwa kila bidhaa au huduma inayotolewa na wauzaji/wasambazaji. 2. Aerospace Industry: AS 9100 (sekta ya anga) AS 9100 iliandaliwa na International Aerospace Quality Group (IAQG) kwa ajili ya kutumiwa na sekta ya ufundi wa vyombo vya anga, anga na ulinzi. Kinaweza kutumika katika msururu mzima wa usambazaji wa sekta hizi, ikiwa ni pamoja na mashirika yanayotoa msaada wa kutoa huduma ya kutuma na ukarabati. Kiwango hiki kimsingi kipo ISO 9001:2008 na kinabeba mahitaji ya ziada kwa ajili ya sekta zilizotajwa hapo juu. 3. Information technology: TickIT. (teknolojia ya mawasiliano) TickIT ni mwongozo wa mifumo bora ya programu. Kinaungwa mkono na Kiwanda cha programu cha Uingereza na Sweden kwa kutumika katika maeneo kama vile ya maendeleo ya programu na huduma. Kinaweza kutumika tu katika mchanganyiko na ISO TickIT inajumuisha tathmini na uthibitisho wa mfumo wa shirika la usimamizi bora wa programu na ISO Uthibitisho wa mashirika ya uthibitisho yenye kibali pia unapatikana kwa viwango vyote hapo juu. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization. Quality Management Systems: Advice from ISO/TC 176 for Sector-specific applications. Ufafanuzi wa mada nzima ya ISO/TC 176 s na viwango vya QMS; sera za sekta-maalum na maelekezo ya ISO s; nyaraka za mwongozo wa nyaraka za sekta-maalum za QMS; tathmini ya mahitaji ya sekta-maalum na msaada wa kiufundi kutoka ISO/TC 176. MAREJELEO Hoyle, D. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6th ed Hili ni chapisho la gharama la Butterworth-Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X28DP, United Kingdom. ISBN Pia hupatikana kutoka International Aerospace Quality Group (IAQG). Details about AS ISO/TC 176 N881R3 List of ISO 9001 Sector Applications developed by ISO/TC 176, usimamizi wa Ubora na Uhakikisho wa Ubora (Quality Management and Quality Assurance.) Orodha hii inaboreshwa na ISO/TC 176 katika kipindi Fulani kutegemea upatikanaji wa taarifa /habari. International Organization for Standardization The ISO Survey of Certifications ISO/TS 16949:2009, Mifumo ya usimamizi wa Ubora Hasa mahitaji ya matumizi ya ISO 9001:2008 kwa uzalishaji wa magari na huduma za vipuli. Hupatikana kutoka ISO au kutoka kwa wanachama. (orodha ipo katika

104 94 Mifumo Ya Usimamizi ISO 13485:2003, Vifaa Maabara/hospitalini Mifumo ya usimamizi wa ubora. Mahitaji kwa ajili ya kanuni/sheria hupatikana ISO au kutoka kwa wanachamawa ISO (orodha ipo ISO 15378:2011, Vifaa vya ufungashaji kwa ajili ya bidhaa za matibabu/maabara hasa mahitaji kwa ajili ya matumizi ya ISO 9001:2008, kwa mrejezo mzuri wa uzalishaji {Good Manufacturing Practice (GMP)}. Hupatikana kutoka ISO au wanachasma wa ISO (Orodha ipo ISO/TS 29001:2010, Petroleum, petrochemical and natural gas industries Sector-specific quality management systems Matakwa ya Mashirika ya Ugavi wa bidhaa na huduma hupatikana kutoka ISO au wanachama wa ISO (orodha ipo TickIT: Undani wa TickIT.

105 Mifumo Ya Usimamizi Kuna gharama na faida gani za kupata uthibitisho wa ISO 9001? Hakuna jibu la uhakika kwa swali hili maarufu, kwa kuwa gharama za uthibitisho wa ISO 9001 zinategemeana na sababu mbalimbali, m.f. muda gani unachukua kuweka mfumo wa usimamizi bora, wafanyakazi wangapi wanahusika na kama mshauri kutoka nje ataajiriwa au laa. Kwa kutazama hili, sehemu hii inaangalia tu makundi ya gharama kubwa na orodha ya gharama kubwa ya vitu. Makundi makubwa ni pamoja na gharama za kuanzisha na kutekeleza mfumo wa usimamizi bora, gharama za kuudumisha, na gharama ya uthibitisho wa mwanzo na matengenezo yake. Gharama za kuanzisha na kutekeleza QMS Mafunzo ya mmoja au wawili wa mameneja (wasimamizi) wa kampuni yako na mkufunzi kutoka nje (ikiwezekana kutoka kwenye chama au tawala za sekta) ili kuwawezesha kuelewa mahitaji ya ISO 9001 na nyaraka husika za QMS zinazohitajiwa na shirika lako. Kutathmini utendaji wa sasa wa ubora na kutengeneza vifaa/nyenzo za ziada za vipimo pale inapohitajika. Kufufua sehemu ya kazi, vifaa, mashine, manufaa, vifaa vya kusaidia huduma, n.k, kama ikihitajika. Kwa mfano, vifaa vya vipimo vya ziada vinaweza kuhitajika kwa ufanyaji wa vipimo wa mara kwa mara wakati wa uzalishaji na kabla ya kupelekwa kwa wateja. Kupitia upya utoaji wa mwanga, uingizaji hewa, udhibiti wa joto, unyevu, sauti na mtikisiko, masuala ya usafi, kama inavyohitajika. Kupitia upya na kufufua mipango kwa ajili ya utunzaji sahihi na salama na uhifadhi wa malighafi, bidhaa zilizokamilika na zilizokamika nusu, ambapo ni muhimu kufanya hivyo. (katika hatua hii ikiwa unafikiri ni unaweza kutekeleza utunzaji bora wa nyumba/jengo au Japanese 5S (tazama swali namba 10). Kupitia taratibu za sasa/utendaji na kuorodhesha taratibu mpya za kuweka orodha na rekodi zinazotakiwa kuandaliwa. kuboresha nyaraka husika za QMS (m.f. sera bora, malengo bora, taratibu za mwongozo za QMS, mipango bora, vipimo na michoro, miundo ya kuweka kumbukumbu Kuendesha mafunzo ya kutoa ufahamu kwa watu wote wenye kazi na wajibu wa kutekeleza QMS. Matumizi tofautitofauti kama kuandaa maneno, steshenari na matumizi mengine yanayohitajika kwa ajili ya uandaaji wa mwongozo, taratibu na mengine kama hayo. Gharama za kudumisha QMS Kuangalia mara kwa mara mazingira ya vifaa vya vipimo kwa ajili ya ukarabati, matengenezo na marekebisho yake. Kuwapa mafunzo baadhi ya mameneja wako ili kufanya kaguzi za ndani mara kwa mara. Kufanya kaguzi za ndani za QMS mara kwa mara, hatua za marekebisho na mapitio ya usimamizi. Kubadilisha mwelekeo, kuongeza ufahamu, na kuwapa mafunzo wafanyakazi wako ili wapate kufahamu maboresho ya mabadiliko katika QMS kwa wakati, maboresho ya daima ya QMS na masuala mengine. Shughuli nyingi zilizoorodheshwa hapo juu zinaweza kufanywa na wafanyakazi wako baada ya kusoma ISO 9001 na miongozo ya viwango na vipeperushi vilivyochapishwa na ISO (tazama swali namba 29). Wakati ambapo hawataingia gharama za moja kwa moja, wataingia gharama ambazo sio za moja kwa moja zinazotokana na juhudi za wafanyakazi wako kujielimisha wenyewe na kufanya shughuli hizi. Kwa kuongezea maarifa, unaweza kumwambia mmoja au wawili wa wafanyakazi wako kupata mafunzo mafupi yanayohusu utekelezaji wa ISO Kingine ni kwamba unaweza kupata kutoka vyanzo vya nje baadhi ya shughuli zilizotajwa hapo juu kwa washauri au wataalam maarufu katika kazi hizo.

106 96 Mifumo Ya Usimamizi Gharama za uthibitisho wa mwanzo na gharama zinazohusiana na maandalizi ya uthibitisho Usajili au ada inayolipwa kwa shirika la uthibitisho kwa kipindi cha miaka mitatu. Ada kwa ajili ya hatua ya pili ya ukaguzi unaofanywa na shirika la uthibitisho lililoteuliwa. Ada kwa ajili ya kaguzi za ufuatiliaji wa mara kwa mara na shirika la uthibitisho lililoteuliwa. Usafiri, bodi na makaazi ya mkaguzi/wakaguzi kutoka shirika la uthibitisho. Inatakiwa kufahamika kuwa uthibitisho wa ISO 9001 sio hatua ya lazima kuelekea utekelezaji wa QMS. usimamizi wako lazima uangalie kama itakuwa sahihi kimkakati na sababu nyingine kwa kampuni yako kutekeleza ISO 9001 na kufanya uthibitisho kabla ya kuingia gharama za hapo juu. Faida za ISO 9001 Ikiwa utatekeleza na kuendelea kufanya vizuri mfumo utakupatia faida nyingi kama vile: Ubora utaonekana kama wajibu wa kila mmoja badala ya kuwa wajibu wakipekee kwa mkaguzi au meneja wa udhibiti. QMS itakupatia namna ya kutunza nyaraka za uzoefu wa kampuni katika muundo sahihi (mwongozo wa ubora, taratibu, maelekezo, n.k). Utazalisha akiba, kwa kuwa gharama za kurudia mchakato, kurudia kazi, kurudia ukaguzi, kubadilisha bidhaa, adhabu kutokana na ucheleweshaji wa kufikisha bidhaa, rejea za wateja, rejea za wateja na madai ya hati vitapungua hatua kwa hatua. Utaweza kupata uaminifu wa wateja wako kwa kuwa mahitaji na matarajio yao yatakuwa yanatimizwa hatua kwa hatua, na kupelekea fursa nyingi zaidi kwako. Unaweza kutumia ISO 9001 kujitangaza na kupata mauzo mengi zaidi. Unapata upendeleo kutoka kwa wateja muhimu ambao wao wenyewe wametumia ISO Masoko ya nje yatakuwa ni rahisi kwako, kwakuwa wanunuzi wa kigeni wengi wanalipia bonasi kwenye mifumo ya ISO Utapata uwanja wa kukutana na makampuni makubwa unapopata mikataba mipya. Kupata uthibitisho kutapunguza kaguzi za mfumo wako mara kwa mara kwa wateja tofauti tofauti. Faida kubwa inayopatikana kutokana na kutunza QMS (ambao ni uwekezaji katika kuzuia kushindwa) ni akiba kubwa unayoweza kupata kwa kupunguza mno gharama za kushindwa. (tazama swali namba 2). KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Shirika la Viwango la Kimataifa (International Organization for Standardization) ISO 9000 Family Global management standards (Video). Video hii ni bure na inapatikana kutoka katika tovuti ya ISO Katika video hii watumiaji wa ISO 9000 wanazungumza kutokana na uzoefu wa masharti ya usimamizi, masuala ya mita, lengo la mteja, maboresho endelevu, ubadilinashaji wa maharifa, ukoaji wa gharama na kanuni nane za menejimenti bora. ISO Management Systems magazine database. Matoleo kuanzia 2001 hadi 2009 ya magazeti ya ISO Mifumo ya usimamizi wa ISO inapatikana kwa ushauri na kuchukuliwa bure kabisa kutoka kwenye sehemu ya habari na vyombo vya habari ya tovuti za ISO. Yanabeba habari, masuala na maendeleo yanayohusiana na viwango vya menejimenti vya ISO na utekelezaji wake duniani. MAREJELEO 1. Shirika la Viwango la Kimataifa (International Organization for Standardization). Uchaguaji na utumiaji wa ISO 9000 family of standards: Jarida hli ni bure na hupatikana kutoka katika tovuti ya ISO International Trade Centre. ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

107 Mifumo Ya Usimamizi Nitawezaje kuanzisha mfumo wa usimamizi bora wa ISO 9001? Inaaminika sana kwamba ni makampuni makubwa tu yanayoweza kutekeleza ISO 9001, kwakuwa inahitaji nyaraka zilizofafanuliwa kwa kina ambapo inaweza kuwa ngumu kwa makampuni madogo. Hii ni imani potovu. Kama neno la tahadhari, kabla ya kuamua kutekeleza mfumo, usimamizi wako lazima kwanza uwe wazi kuhusu kusudi la mfumo kuhitajika na shirika lako. Kama kinachosukuma tu ni kupata orodha za zabuni za wateja au kwa sababu mshindani wako tayari amepata, kuna uwezekano mkubwa kwamba QMS yako itabaki kuwa seti ya nyaraka kwa madhumuni ya uthibitisho tu. Matokeo yanayopatikana kutokana na mbinu hiyo hayatakupatia madhumuni yenye manufaa kwako na yapunguza/ondoa kwa kiasi kikubwa rasilimali zako. Badala yake, usimamizii wako unatakiwa kwanza uwe na malengo maalum yatakayotimizwa kupitia QMS, kama vile kuwapa imani wateja kwamba shirika lako lina uwezo wa kutimiza mahitaji yao wakati wowote. Kwa kuzingatia hali ya sasa ya utendaji wa usimamizi bora wa SMEs katika nchi zinazoendelea, utekelezaji wa ISO 9001 inatakiwa kuchukuliwa kama mradi, msururu wa hatua ambazo unaelezewa hapa chini. Hatua ya 1: Uteuzi wa timu Inahitajika timu ndogo yenye mwandamizi/kiongozi katika kila kazi anayetakiwa kuteuliwa na menejimenti yako kwa maendeleo ya mfumo. Mwanachama mmoja wa timu anatakiwa kuteuliwa kama mratibu; wawakilishi wa usimamizi wanaweza kupatiwa jukumu hili. Kwanza kabisa lazima timu ipewe mafunzo ya ufahamu na nyaraka za familia ya viwango vya ISO 9000 na shirika la watalaamu wa mafunzo. Kuhusisha mshauri mzuri wa kutoa msaada kwa timu yako inaweza kuwa uwezekaji wenye thamani. Mshauri mzuri atawezesha ubadilishanaji wa haraka wa maarifa na ujuzi kwa watu wako. Hatahivyo, kuajiri mshauri haitakiwi kuchukuliwa kama zoezi la kuhamisha majukumu ya kuanzisha mfumo kwa mtu mwingine. Badala yake, watu wako watatakiwa kufanya hili wenyewe kwa msaada wa mshauri husika ili kuhifadhi umiliki wa mfumo. Hatua ya 2: Uchambuzi wa hitilafu Kwa uchambuzi wa hitilafu, chati (mchoro wenye kuonyesha hatua kwa hatua uhusiano/utaratibu wa vitu) inatakiwa kuchorwa, kuonyesha jinsi gani taarifa inasambaa kwa wakati, kuanzia mteja anapoweka oda/ kuagiza hadi bidhaa au huduma zinavyofikishwa kwa mteja.tukirejelea mchoro huu, chati ya shughuli zote katika kila idara inatakiwa kuandaliwa. Baadaye, kwa kwa kutumia michoro uliyoitengeneza, unaweza kuandaa orodha ya taratibu zilizopo na maelekezo ya kazi kwa shughuli husika. Pia unaweza kuongeza shughuli nyingine na michakato ambayo unafikiri ni muhimu katika hatua hii kwa kuzingatia mahitaji yaliyowekwa na ISO Tukirejelea mchakato ambao umefafanuliwa awali,, unaweza kugundua baadhi ya hitilafu/pengo la miundombinu kama vile: Uhitaji wa nafasi ya ziada kwa ajili ya kujenga, vifaa na mashine, matumizi, huduma saidizi au kutengeneza upya mpango wa sasa. Uhitaji wa mwanga wa kutosha, upitishaji wa hewa safi, udhibiti wa joto, udhibiti wa unyevu, kelele sahihi na kiasi cha mtikisiko, utendaji bora wa usafi (katika usindikaji wa chakula). Uhitaji wa utunzaji sahihi na uhifadhi wa malighafi ili kuepuka kuchanganya na uharibifu. Uhitaji wa vifaa vya ziada vya upimaji kwa ajili ya upimaji wa mara kwa mara wa bidhaa wakati wa uzalishaji na kabla ya kupeleka kwa wateja. Uhitaji wa ukaguzi wa mara kwa mara kwa vifaa vya upimaji na ukarabati wa baadae, matengenezo au urekebishaji. Uhitaji wa utunzaji sahihi wa bidhaa katika hatua zote ili kuepuka hasara. Mpango wa utekelezaji kwa muda sahihi, wa kuziba mapengo yaliyoonekana wakati wa zoezi unatakiwa kuandaliwa na hatua kuchukuliwa kama ilivyopangwa.

108 98 Mifumo Ya Usimamizi Hatua ya 3: Utunzaji kumbukumbu/nyaraka Nyaraka husika za QMS kama vile za sera bora, malengo bora, vigezo vya kufanya mchakato, mahitaji ya ujuzi, mwongozo bora, mipango bora, na maelekezo ya taratibu na kazi zinatakiwa kuandaliwa. Ni vizuri kuhusisha watu wote wanaohusika katika uboreshaji wa taratibu na maelekezo ya kazi yanayotumika kwenye maeneo yao. Nyaraka za taratibu na maelekezo ya kazi zinatakiwa zioane na utendaji wa sasa na sio mawazo yako ya ni nini kifanyike. Tengeneza fomu mpya na orodha kama itakusaidia; vinginevyo tumia zilizopo kadiri inavyowezekana. Hatua ya 4: Mafunzo na utekelezaji Wapatie mafunzo wafanyakazi wote juu ya namna ya kutumia QMS yako. Kadiri mfumo unavyozidi kuendelea (rejea hatua ya 3 juu) awamu/mchakato wa utekelezaji unatakiwa uendelee kwa wakati huo huo, yaani ushahidi utakaosaidia kama vile rekodi, dondoo za vikao na data za rejea za wateja vinatakiwa kutunzwa. Hatua ya 5: Ukaguzi wa ndani na uboreshaji Baadhi ya mameneja wako na wafanyakazi wapatiwe mafunzo na mkufunzi/mtaalamu ili waweze kufanya ukaguzi wa ndani wa QMS. Mwakilishi wa usimamizi yako anaweza pia kufanya shughuli za ukaguzi wa usimamizii. Baada ya mfumo kuwa umewekwa kwa karibuni miezi mitatu, wakaguzi wako waliopatiwa mafunzo wanatakiwa kufanya ukaguzi wa ndani. Pengo/hitilafu yoyote itakayoonekana wakati wa ukaguzi lazima irekebishwe; maboresho yoyote yanayohitajika katika nyaraka za mfumo lazima yafanyike; uhitaji wowote wa ufahamu wa ziada na mafunzo ya ujuzi au kuboresha miundombinu lazima vishughulikiwe. Pale mfumo unapokuwa imara, kaguzi za ndani lazima zifanyike kwa muda uliopangwa, kila baada ya miezi sita kwa mfano, au kama inavyohitajika. Unatakiwa pia kutumia kaguzi za ndani, data za rejea za wateja, data za ufuatiliaji wa mchakato na bidhaa, ushahidi wa kufikia au kutofikia malengo bora, hatua za marekebisho, n.k. kama rasilimali kwa ajili ya kuboresha mfumo. usimamizi wako unatakiwa utoe rasilimali za fedha na nyingine kwa ajili ya kuboresha miradi na kufuatilia maendeleo ya maboresho. Hatua ya 6: Mapitio ya usimamizi Usimamizi wako unatakiwa kupitia matokeo ya ukaguzi wa ndani, data za rejea za wateja, hali ya malengo bora, uchambuzi wa mchakato, mwenendo wa uwiano wa bidhaa, hali ya hatua za marekebisho na uzuiaji. Kwa kupitia matokeo ya mapitio haya, usimamizi unaweza kupanga malengo mapya kwa ajili ya madhumuni yenye ubora na kufanya maboresho yanayohitajika katika QMS. Mapitio ya usimamizi yanatakiwa kufanyika mara kwa mara, kwa mfano angalau mara moja kila miezi sita. Hatua ya 7: Uthibitisho Uthibitisho wa ISO 9001 ni wa hiari; kwa hiyo uhitaji wake unaamuliwa na usimamizi wako. Pale mfumo unapokuwa umeanzishwa kwa miezi kadhaa na angalau ukaguzi mmoja wa ndani na mapitio ya usimamizi (mara 1) yamefanyika, unaweza kufikiria kufanya maombi ya uthibitisho. Mpango wa utekelezaji wa kuboresha QMS unaojumuisha shughuli zilizotajwa hapo juu unatakiwa kuandaliwa. Mpango unatakiwa kufafanua majukumu ya washiriki wa timu na usimamizi na kupanga tarehe za kutimiza lengo. Kipindi kizima cha miezi sita hadi tisa kitahitajika kwa ajili ya maboresho kamili na utekelezaji wa mfumo. Mfano wa mpango kazi umetolewa katika jedwali hapa chini.

109 Mifumo Ya Usimamizi 99 KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization. Selection and use of the ISO 9000 family of standards. This brochure is freely available from ISO Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya viwango katika familia ya ISO 9000 na kuonyesha namna kwa pamoja, zinavyotengeneza msingi wa maboresho endelevu na ubora wa biashara. Kwa kuongezea kutoa mifano ya uzoefu wa watumiaji wa viwango, kina sehemu zenye mada zifuatazo: maelezo ya mfululizo wa viwango vya msingi vya ISO 9000; mchakato wa hatua kwa hatua kwa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi bora; kudumisha faida na maboresho endelevu; familia ya ISO 9000 kipindi kichajo. MAREJELEO Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Shirika la Viwango la Kimataifa (International Trade Centre and International Organization for Standardization). ISO 9001 kwa biashara ndogo Nini la kufanya: Ushauri kutoka ISO/TC 176, ISBN Inapatikana kutoka ISO au wanachama wa ISO (orodha kutoka Kituo cha Biashara cha Kimataifa (International Trade Centre). ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

110 100 Mifumo Ya Usimamizi 33. Nini maana ya malengo bora na yanalisaidiaje shirika kufikia ahadi ilizozitoa katika sera yake ya ubora? Sera ya ubora ni tamko la shirika kuhusu dhamira (matarajio na mwelekeo) yake kuhusiana na ubora. Moja ya madhumuni ya sera ya ubora ni kuwakumbusha wafanyakazi wako kuhusu wajibu walionao wa kuhakikisha wateja wao wanaridhika. Kuweza kuitekeleza sera ya ubora sharti usimamizi uanishe malengo bora yanayolenga wafanyakazi. Kwa hiyo usimamizi lazima itambue kuwa wakati sera ya ubora inaandaliwa, vilevile iweze kuibuka na malengo ya kusaidia kuelekeza yanayodhamiriwa. Kwa mfano tamuko la sera ya ubora linaweza kuwa: Tumedhamiria kukidhi matakwa ya wateja wetu na tutawawasilishia bidhaa na huduma zisizo na kasoro, kwa wakati daima. Kutokana na sera hii malengo yafatayo, kati ya mengine, yanaweza kunyambulishwa: Sera Tumedhamiria kutoa bidhaa na huduma zisizo na kasoro (bora). Kutoa bidhaa na huduma kwa wakati. Malengo 99% ya kinachozalishwa kutokuwa na kasoro (kupimwa kutokana na mrejesho wa wateja). 98% kuwasilishwa kwa wakati (kupimwa kwa kulinganisha ahadi na ahadi zilizotimizwa). Ubora wa malengo utakuwa SMART, yaani: S Specific, Bayana M Measurable, Inapimika A Achievable, Inawezekana R Realistic, Enye Ukweli Yanahusika na mchakato au madhumuni ya kazi/shughuli inayofanywa. Iwekwe katika aina ambayo inaweza kupimwa kwa kutumia teknolojia iliyopo. Katika hali ya rasilimali zitakazotolewa. Katika muktadha wa sasa na matarajio ya kazi zijazo. T Timely (Time bound), wakati Kwa Sharti kuwe na kipindi maalumu cha kukamilisha, yaani tarehe ya kuanza na kuhitimisha. Kumbuka kuwa malengo sharti yaweze kupimika. Kwa mfano lengo la tutafanya vizuri zaidi, halipimiki. Kuwa na lengo linalopimika, utakuwa na Uwezo wa kugagua au kufatia kama unafanikiwa, na kama sivyo, basi utaamua cha kufanya. Vilevile utahitaji kuweka kusudio la lengo ukizingatia utendaji wa sasa na upatikanaji wa rasilimali. Kwa mfano kama kwa sasa unaweza kufikia 75% ya lengo la kufikisha kwa wakati na sasa unakusudia ufikisha 85% katika kipindi cha miezi sita, basi kwanza itabidi utathmini kama rasilimali na michakato ya lengo hili la juu liko tayari. Mifano ambayo inaweza kukusaidia kuongeza kuridhika kwa wateja wako na ufanisi katika biashara yako ni kama ifatayo: Punguza makosa na kasoro katika mchakato wa manunuzi kutoka 1% mpaka 0.5% katika kipindi cha miezi sita; Punguza muda unaohitajika kujenga kila kifaa katika karakana ya kuunganishia kutoka dakiki 60 za saa na kuwa dakika 45; Punguza idadi ya vitu vilivyotengenezwa kwenye stoo kutoka milioni x mpaka milioni y katika kipindi cha miezi sita;

111 Mifumo Ya Usimamizi 101 Hakikisha ufikishaji wa bidhaa kwa wakati unafikia 98%; Hakikisha malalamiko yanapatiwa suluhisho ndani ya saa 48 baada ya kupokelewa; Jibu maswali ya wateja ndani ya saa 48 baada ya kupokelewa; Hakikisha kwamba mashini ziko katika hali ya kufanya kazi kwa 90% ya muda. Kila mfanyakazi sharti ajue malengo mahususi ya ubora kwa kazi atakayo/anayoifanya na jinsi malengo hayo yatakavyofikiwa. Kadhalika ni wajibu kuwafahamisha mara kwa mara utendaji unavyoelekea katika kuyafikia malengo na maboresho yanayohitajika. Kwa kila lengo, kuwe na mpango wa kazi unaobainisha jinsi na ni nani atafanikisha lengo na mahitaji ya rasilimali. Malengo yanahitaji kupitiwa mara kwa mara kama sehemu kuendeleza mchakato. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Hoyle, David. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6 th ed ISBN It is a priced publication of Butterworth-Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X2 8DP, United Kingdom. Also available from Kitabu hiki kinaelezea maana ya kila hitaji la ISO 9001:2008 kwa mifano. Orodha, majedwali na vielelezo/michoro. Kila hitaji linafafanuliwa kwa maswali matatu maana yake ni nini, kwa nini ni muhimu na namna gani inabainishwa. Sura ya 15 na 16 ya kitabu hiki inaelezea Sera ya Ubora na Malengo ya Ubora kwa mfuatano huo. Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Shirka la Viwango la Kimataifa. ISO 9001 for Small Businesses What to do: Ushauri kutoka ISO/TC 176, ISBN Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (angalia tovuti Aya ya 5.3 na za kitabu hiki zinashughulikia Sera ya Ubora na Malengo ya Ubora kwa kufuatana hivyo. MAREJELEO Shirka la Viwango la Kimataifa. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Inapatika kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (angalia tovuti Kituo cha Biashara cha Kimataifa. ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

112 102 Mifumo Ya Usimamizi 34. Rasilimali gani zinahitajika kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa ISO 9001? ISO 9001 inapendekeza kuwa uainishe na kutoa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza na kudumisha mfumo wa usimamizi wa ubora (QMS), kuendelea kuuboresha kiufanisi na kuongeza kuridhika kwa waateja. Kiwango pia kinatamka kuwa ni jukumu la uongozi wa juu kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali zinazotakiwa. Sehemu hii inaangalia rasilimali zinazotakiwa kutekeleza ISO 9001 katika msururu mzima wa biashara yako: Rasilimali watu, miundombinu na mazingira ya kazi. Rasilimali watu Mfanyakazi wako lazima wawe na ujuzi wa kufanya kazi zao. Lazima wawe na ujuzi sahihi kwa kazi husika ( yaani, elimu, mafunzo, ujuzi na uzoefu). Kwa mfano, mfanyakazi anawea kuhitaji mafunzo juu ya: Jinsi ya kusahihisha vigezo vya mchaakato; Jinsi ya kurekebisha kifaa cha kupimia kabla ya kutumika; Njia za kuunganisha sehemu, n.k. Kama ni kampuni ya huduma, wafanyakazi wako wanaweza kuhitaji kuelewa jinsi ya kutumia komputa kwa ajili ya kushughulikia maulizo au malipo ya wateja, kwa mfano katika mapokezi ya kwenye benki au hoteli lazima kuelewa hatua zinazohusika. Kunatakiwa kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi maalumu kama vile wakaguzi wa ndani, mwakilishi mahiri wa usimamizii, wataalamu wa kuweza kubaini vyanzo vya matatizo ya ubora wa bidhaa au upungufu wa mfumo na njia za kutatua. Zaidi ya hayo, uwe na Uwezo wa kuhamasisha wafanyakazi wako kutambua umuhimu wa kuendelea kuwaridhisha wateja kutokana na shughuli zao. Miundombinu Mashine, vifaa vya mkono, komputa, mahali pa kufanyia kazi, sehemu ya kuhifadhia( stoo/ghala, rafu) vifaa vya kubebea bidhaa, vifaa ya kupimia, n.k. lazima viwe vya kutosha kuhakikisha ulinganifu wa bidhaa. Huduma za kusaidia zisiwe na upungufu, kwa mfano umeme usiokatikakatika, maji, mafuta ya mitambo, mvuke, hewa iliyogandamizwa, kadiri inavyohitajika, umeme wa dharura na vifaa ya utupaji taka sharti viwepo. Vifaa kwa ajili ya maandalizi ya vipindi lazima viwepo. Vyanzo ya habari ( kama vitabu vya rejea na machapisho mengine, vitita vya data kuhusu mahuruji, maduhuli na mahitaji ya kisheria) viwepo. Tekinolojia inayohitajika (kwa mfano programu za komputa) kubadilisha takwimu kuwa katika hali ya kutumia wa kampuni sharti ziwepo. Mazingira ya kazi Kuwe na udhibiti mzuri wa joto, unyevu kwenye hewa, hewa, kelele, mtikisiko, nk. Katika sehemu ya kazi. Katika kampuni za huduma, pawe na sehemu nzuri ya kusubiria wateja/wageni yenye huduma muhimu. Kuwe na huduma nzuri za afya/usafi (kwa mfano chakula, vinywaji na matibabu). Sehemu ya kazi sharti iwe na mazingira ambayo yanahamasisha uzalishaji wenye tija, ubunifu na staha kwa watu. Kiasi cha mahitaji ya rasilimali zilizotajwa hapo juu itategemea aina ya bidhaa inayotolewa na upana wa huduma za kampuni. Kutekeleza ISO 9001 QMS kwa kawaida hakuhitaji uwekezaji zaidi katika miundombinu na katika mazingra ya kazi. Zaidi ya kuwa na rasilimali ya kutosha, utahitaji kupitia tena mchakato, majukumu ya wafanyakazi, uchanganuzi wa matokeo ya vipimo na hatua zilizochukuliwa kuzuia kutokea tena kwa matatizo yanayohusu uboa. Wakati mwingine ikiwa rasilimali zako hazitoshi (ujuzi na miundobinu), kiwango kinaelekeza njia mbadala ya kupata huduma hizo kwingine kama zitaathiri ulinganifu wa bidhaa, ilimradi usimamizi wa hizo huduma za nje unawezekana.

113 Mifumo Ya Usimamizi 103 KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Kituo cha biashara cha Kimataifa na Shirka la Viwango la Kimataifa. ISO 9001 for Small Businesses What to do: Ushauri kutoka ISO/TC 176, ISBN Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO members (angalia tovuti Aya ya 6.1 mpaka 6.4 ya kitabu hiki inashughulika na usimamizi wa rasilimali. MAREJELEO Hoyle, David. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6 th ed ISBN It is a priced publication of Butterworth- Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X2 8DP, United Kingdom. Also available from Shirika la Viwango la Kimataifa. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wnachama wa ISO (angalia Tovuti Kituo cha Biashara cha Kimataifa. ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

114 104 Mifumo Ya Usimamizi 35. Kuna fikra potovu na changamoto gani katika utekelezaji wa ISO 9001 na SMEs? Baadhi ya fikra potovu kuhusu ISO Vigumu kutekeleza ISO 9001 katika kampuni ndogo Kiwango ni cha jumla na kinaweza kutumiwa na mashirika ya ukubwa na aina mbalimbali. Kwa kweli ni rahisi zaidi kwa kampuni ndogo kutekeleza ISO 9001 kwa kuwaa msururu wa madaraka ni mfupi na majukumu yanaweza kuainishwa na kuwasilishwa kwa urahisi. Kiwango hiki kimweza kutekelezwa na kampuni ndogo nyingi na hata zile zinazoendeshwa na mfanyakazi mmoja. Kubainisha muundo rasmi wa Usimamizi siyo lazima. Kama kampuni yako haijihusishi na ubunifu na usanifu, na hutegeneza kufuta usanifu/michoro iliyoletwa na mteja, QMS yako itasamehewa majukumu ya kubuni na kusanifu. ITC na ISO wameshirikiana kuchapisha kitabu mahususi cha ISO 9001 kwa matumizi ya kampuni ndogo. 2. Kuna gharama kubwa katika kutekeleza ISO Pamoja na kuwa na gharama za kutekeleza ISO 9001, lakini matokeo yake ni faida kwa kampuni, maana haitakuwa na matukio mengi ya upungufu ambayo huwa na gharama kubwa. Gharama ya kuanzisha mfumo wa QMS zinajumuisha mafunzo kwa wafanyakazi watakaohusika, kuweka mfumo wa kuweka kumbukumbu na ripoti; kushughulikia mapungufu kwenye mfumo; ongezeko la mashine, vifaa, huduma zingine, etc. kama zitahitajika. Kama utahitaji kupata uhakiki, ada ya uhakiki itakuwa gharama nyingine. Hata hiyo, kufuatia ongezeko la mashirika ya uhakiki, ada hii inapungua. 3. Ni lazima kuajiri mshauri wa kukusaidia kuanzisha mfumo wa ISO Kukodisha huduma mahususi kwa ajili ya kuweka mfumo wa QMS siyo lazima, ila kama wafanyakazi wako hawana ujuzi na uzoefu wa kazi hiyo. Mfumo unaoanzishwa na wafanyakazi wako una faida kubwa ya kuwa sehemu yao ya kujivunia na gharama yake huwa nafuu. Kuna Makala mengi yaliyoochapishwa katika tovuti ya ISO, mashirika ya viwango ya kitaifa, wachapishajibinafsi, mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile ITC na UNIDO na katika vitabu vya mwanzo vilivyochapishwa na vyama vya sekta ya viwanda, ambavyo vinaweza kukusaidia kuanzisha mfumo mwenyewe. Hata hivyo, kuajiri mshauri mahrli ( baada ya kufanya uchunguzi) kufikiriwa kwa misingi ya uchanganuzi wa faida na hasara. 4. Ni lazima kwa kampuni kuwa na wakaguzi wake wenye mafunzo stahiki na wakaguzi binafsi kufanya ukaguzi wa ndani. Kwa kampuni ndogo isiyokuwa na Uwezo wa kuwa na mkaguzi huru wa ndani, basi wanaweza kuajiri mkauguzi wa nje ambaye atafanya ugaguzi wa QMS kwa vipindi vinavyotakiwa. 5. Kuna kuandika sana kwenye utekelezaji wa ISO Miongozo mizuri, taratibu na fomu hutengenezwa na kampuni, wakati mwingine kwa msaada wa washauri. Hata hivyo wafanyakazi wanakatishwa moyo wakati wakitakiwa kuandika kumbukumbu/ripoti nyingi, bila kuwa na mafuaa ya msingi kwenye mchakato. Kumekuwa na hisia kuwa ili uweze kupata uhakiki sharti uandike kumbukumbu nyingi. Hata hiyo siyo lazima kuweka kumbukumbu kwa kila mchakato. Kwa kawaida mtiririko wa mchakato unatosha. ISO 9001 ina hatua sita tu ambazo lazima ziwe na kumbumbukumbu/ripoti. Nazo ni: nyaraka za udhibiti, udhibiti wa kumbukumbu, ukaguzi wa ndani, udhibiti wa bidhaa zenye kasoro, hatua za kurekebisha na kuzuia. Vile vile kiwango kinazipa kampuni uamuzi wa kuweka nyaraka (mwongozo, taratibu, kumukumbu,n.k.) katika nakala halisi au katika hali ya kielektroniki au kwa njia zote mbili.

115 Mifumo Ya Usimamizi 105 Changamoto na mapendekezo ya uvumbuzi katika uanzishaji na utekelezaji wa ISO 9001 Changamoto Mapendekezo ya ufumbuzi Ukosefu wa habari na mafunzo Ugumu wa kupata habari na nyaraka za viwango vya ISO 9000 Uelewa mdogo kati ya wafanyakazi wa kampuni juu ya mahitaji ya kiwango na matumizi yake katika michakato ya kampuni. Gharama kubwa za mafunzo kwa wafanyakazi kuelewa, kuandaa na kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora. Nyaraka zisizofaa Taratibu nyingi na ripoti zinaanzishwa ili kudumisha mfumo. Kutokuwa na maamuzi dhabiti ya usimamizi Watu katika kampuni hawaoni kama mfumo utawanufaisha wao au kampuni. Ugumu wa kushughulikia mabadiliko hasa kati ya mameneja ambao wamezoea taratibu za mkato katika kushughulikia matatizo na kukwepa taratibu zilizowekwa. Kutokuwa na ukaguzi wa ndani wa kutosha Wakaguzi mahiri wa ndani hawapo na kwa hivyo upungufu katika mfumo yanaweza kutogundulika kwa masahihisho. Hatua za haraka hazichuliwi kwa wakati kwa upungufu uliyobainishwa na tathmini ya mchakato au bidhaa na ukaguzi wa ndani. Taarifa mpya kabisa ya kundi la viwango vya ISO 9000 ipo kwenye tovuti (bofya ISO 9000 kwenye ukurasa wa nyumbani tovuti). Au unaweza kusoma nyaraka hizi au nukuu zake kwenye maktaba ya mashirika ya viwango vya kitaifa (angalia swali 29 kwa ufafanuzi). Ufinyu huu wa elimu unaweza kuondolewa kwa kusoma nyaraka husika kama ilivyoelezwa hapo juu, kuhudhuria mafunzo mafupi juu ya somo husika au kwa kuajiri mshauri mahiri atakayeweza kutoa mafunzo kazini kwa baadhi ya wafanyazi wako. Katika nchi zingine mafunzo haya huendeshwa na vyama vya wenye viwanda/wafanyabiashara au mashirika ya viwango.n.k. kwa gharama nafuu. Baada ya wafanyakazi wako kupata mafunzo, itakuwa vizuri kuandaa mfumo wa QMS wenyewe kw msaada wa msahauri mahili. Taratibu ziwe chache za kutosheleza mahitaji. Kiwango kinahitaji mwongozo mmoja, taratibu sita na ripoti kiasi ya 20. Taratibu na ripoti za ziada zinaweza kuandaliwa kama zitaleta faida/ufanisi. Itakuwa vyema kuzitumia taratibu zilizopo, maelezo na ripoti kwa marekebisho stahiki. Nyaraka zote za taratibu na ripoti zihifadhiwe kama nakala halisi au kielekitroniki au vyote. Polepole watu wataanza kuamini kuwa mfumo utakuwa wa faida kwao baada ya kuona matokeo yake, kwa mfano kufikiwa kwa malengo na matarajio yao, kuona kampuni inakuwa na mazingira mazuri ya kazi, elimu na uelewa juu ya matumizi ya nyenzo za kudhibiti ubora, kupungua kwa bidhaa zenye kasoro kurudishwa na wateja, malalamiko ya wateja, n.k. Tatizo hili haliwezi kuisha siku moja. Uongozi wa juu inabidi ulishughukie suala hili kwa karibu, yaani wasikubali kukiukwa kwa taratibu zilizowekwa au kuruhusu vitu au bidhaa zenye upungufu. Kuwa na msimamo wa namna hii kutawafanya mameneja kuheshimu utaratibu na kufuata mahitaji ya mfumo. Mafunzo ya muda mfupi yanaweza kutumiwa kuwaelimisha/kujenga Uwezo wa wakaguzi wa ndani. Mafunzo kama haya hutolewa na vyama vya tasnia ya viwanda/wafanyabiashara. Usimamizi uwahamasishe wafanyakazi kuyatolea maoni upungufu unaojitokeza kila siku juu ya mchakato na bidhaa. Vyanzo vyote vya upunguzfu katika mchakato au bidhaa, malalamishi ya wateja na kasoro zozote zile lazima zishughulikiwe kikamilifu kuzui zisitokee tena. Usimamizi lazima utoe rasilimali zozote zinazotakiwa kurekebisha upungufu uliyotokea kwa wakati.

116 106 Mifumo Ya Usimamizi Changamoto Kuhimiza kupita kiasi uhakiki kampuni zina haraka ya kupata uhakiki hata kabla ya mfumo haujatekeleza kwa ufanisi. Mashirika yanahitaji uhakiki kwa kuwa wanahitaji cheti kwa ajili ya kutafutia masoko, ukandarasi n.k. Chanzo: S.C. Arora, India. Mapendekezo ya ufumbuzi Kabla ya kuomba uhakiki, hakikisha kuwa mfumo wako wa QMS unatekelezwa kwa ufanisi. Mfumo lazima uwe umetekelezwa kwa miezi 3 na ufanisi wake kukaguliwa na wakaguzi wa ndani na kufatiwa na hatua za marekebisho kwa yale yaliyobainishwa na ukaguzi huo. Uhakiki siyo wa lazima. Kwa hivyo ni vyema kufanya uchanganuzi wa faida na hasara kabla ya kuomba uhakiki, (angalia swali 31 kwa ufafanuzi). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Hoyle, David. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6th ed ISBN Chapisho linauzwa na Butterworth- Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X2 8DP, United Kingdom. Pia inapatika kwenye tovuti Kitabu hiki kinatoa maelezo kwa kila hitaji la ISO 9001:2008 kupitia ufafanuzi, mifano, orodha, majedwali na vielelezo. Kila hitaji limefafanuliwa kwa misingi ya maswali matatu: ina maana gani, kwa nini ni muhimu na inadhihirishaje. Sura ya 6 ya kitabu inashughulika na utaratibu wenye ufa na kutoa taarifa juu ya jinsi ya kuepuka makosa katika uanzishaji wa QMS iliyoungezwa thamani. MAREJELEO Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Shirika la Viwango la Kimataifa. ISO 9001 for Small Businesses What to do: Advice from ISO/TC 176, ISBN Kinapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (angalia Tovuti Shirika la Viwango la Kimataifa. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (orodha ipo Kituo cha Biashara cha Kimataifa ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

117 Mifumo Ya Usimamizi Nitahakikishaje kuwa malighafi yangu, vifaa nilivyonunua na pembejeo kutoka kwa wagavi wa nje ni salama kwa matumizi? Malighafi, vifaa/vijenzi na huduma Inawezekana ukawa unafanya kazi nzuri sana ya kudhibiti shughuli zako, lakini kama wagavi wako hawatekelezi majukumu yao kikamilifu, wewe na wateja wako mnaweza kuathiriwa vibaya sana. Kwa hivyo ni muhimu kuwa na wagavi waaminifu na wanachukuwa jukumu la kudhibiti ubora kwa kiasi fulani. Itabidi ufanye yafuatayo: Utambue ni zipi malighafi, vijenzi na huduma ambazo ni za muhimu kwa kufikia ubora unaotakiwa kwa bidhaa au huduma yako. Uainishe mahitaji ya malighafi, vijenzi na huduma itakayonunuliwa. kuweka vigezo vya tathmini na uchaguzi wa mahitaji na wagavi. Kuainisha taratibu za kukubali malighafi na huduma kutoka kwa wagavi wako. Kujua mahitaji ya kitakachonunuliwa, hatua yako ya kwanza ni kutafuta viwango vya kitaifa au kimataifa kuliko kuanza kuandaa viwango vyako; hii itakupuguzia gharama na muda; hata hivyo, uhakikishe viwango unavyochagua vinakidhi matakwa ya wateja wako na ya kwako. Kama hakuna kiwango muafaka, basi utalazimika kuandaa viwango vyako vya ununuzi. Viwango hivi vitajumuisha mahitaji ya kifundi, vijenzi vya malighafi, sifa au ufanisi wake, kati ya mambo mengine. Unazo njia kadhaa za namna ya kuwapata wagavi ambao watakupa vitu/vifaa vinavyokidhi viwango vya ununuzi: Wagavi wa zamani. Unaweza kuwachagua wagavi wako wa zamani kutokana na kuwaelewa uwezo wao wa kutimiza matakwa yako. Kampuni zilizo sajiliwa chini ya ISO Unaweza kuchagua wagavi kwa kuangalia orodha ya wale ambao wana usajili wa ISO Kuwachagua hawa utakuwa umepata uhakika kwamba watakuletea vitu bora; kwa kuwa utendaji wao ni kwa misingi ya viwango. Wagavi wenye bidhaa zilizohakikiwa. Unaweza kununu kutoka kwa wagavi ambao tayari wana bidhaa ambazo zimethibitishwa kuwa linganifu, na mamlaka husika. Kumtathmini mgavi. Uweza kufanya zoezi la kuwatathmini wagavi ili kujua Uwezo wao wa kukidhi mahitaji ya ununuzi wako. itabidi uainishe vegezo ambavyo utavitumia kuwatathmini na hatimaye kuwachagua wanaotimiza vigezo hivyo. Utawajibika kuwafahamisha wagavi utakaowachagua juu ya mahitaji ya bidhaa au huduma unayohitaji na muda dhahiri wa kuwasilisha. Vilevile unaweza kujumuisha katika oda yako ya ununuzi taratibu za kuupokea mzigo. Hizi zinzweza kuwa pamoja na kuwasilisha hati ya mfumo wa usimamizi wa ubora anaofuata, uthibitisho wa kuonyesha kuwa bidhaa yake ya kwanza ilikuwa nzuri, uhakiki wa vifaa vinavyotumika kuzalishia, ujuzi/elimu ya wafanyakazi wake, n.k. Kadhalika itabidi uhakikishe kuwa bidhaa au huduma unayoipata kwa mgavi inakidhi mahitaji yako: Unaweza kutegemea mfumo wa kuhakiki ubora wa mgavi na kupokea bidhaa bila ukaguzi mwingine wowote. Hata hivyo kwa kila fungu la bidhaa unaweza kumpa data za upimaji kupata uhakika. Kuchukua sampuli au kwa asili mia 100 kwa ajili ya ukaguzi na kupima wakati wa kupokea bidhaa. Ukaguzi wa mahali/eneo la mgavi kabla ya maligafi/vijenzi kuchukuliwa. Kuajiri taasisi nyingine mahiri kufanya ukaguzi kabla ya ununuzi. Michakato kutoka nje Inabidi kuwa na uhakika wa ubora wa pembejeo unazopokea toka kwa wagavi wa nje. Huduma zinazotolewa na watu wengine kwa niaba yako, zinaweza kufanyika katika eneo lako au la nje. Mifano ya

118 108 Mifumo Ya Usimamizi michakato ya kufanyia nje ni kama: kupiga rangi au uwekaji tabaka la keletroniki kwenye vijezi kufanywa kandarasi ya nje; kupata huduma za tekinohama; usafi wa kiwanda na mafunzo kutolewa na mashirika mengine; utengenezaji na huduma kwa mitambo/vifaa vya uzalishaji kufanywa na kampuni ya nje; n.k. Sababu za kuchukuwa huduma za nje inaweza kuwa moja au mbili. Unaweza kuwa na Uwezo wa kufanya mwenyewe, lakini hutaki kutumia raslimali zako katika hicho, au huna Uwezo wa kufanya mwenyewe na kwa hiyo unahitaji huduma ya walio na Uwezo wa kufanya vizuri. Kwa kazi zote zinazofanyika nje au na watu wengine, itabidi kuainisha na kutekeleza vigezo vyako mwenyewe katika kudhibiti ubora; hivi vitajumuisha tathmini ya watoa huduma, na ukaguzi au tathmini ya bidhaa au huduma unazopokea kutoka kwao. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA International Organization for Standardization. Introduction and support package: Guidance on Outsourced process. Document No. ISO/TC 176/SC 2/N 630R3, issued in October Freely obtainable from ISO website: ntation_requirements_of_iso_9001_2008.htm Inatoa mwongozo juu ya kina cha ISO 9001:2008 sehemu 4.1, kuhusu udhibiti wa shughuli zilizonunuliwa. International Trade Centre and International Organization for Standardization. ISO 9001 for Small Businesses What to do: Advice from ISO/TC 176, ISBN Obtainable from ISO or ISO members (list at Aya 7.4 ya kijitabu hiki kinashughulika na taratibu za ununuzi, maelezo kuhusu ununuzi na udhibitishaji wa ununuzi wa bidhaa. MAREJELEO Hoyle, David. ISO 9000 Quality Systems Handbook, 6 th ed ISBN It is a priced publication of Butterworth- Heinemann, Linacre House, Jordan Hill, Oxford 0X2 8DP, United Kingdom. Also available from International Organization for Standardization. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at International Trade Centre. ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

119 Mifumo Ya Usimamizi Tutatangazaje mafanikio yetu katika usimamizi wa ubora? Njia zinazoweza kutumika kutangaza mafanikio katika usimamizi wa ubora zimefafanuliwa kama ifutavyo: Kutumiza ahadi uzliowapa wateja Hatuwezi kukosea tukisema kwamba, katika soko wateja ni mabalozi wazuri. Wateja wakiridhika, watawambia wengine kuhusia ubora waliupata/kuuona kwa bidhaa/huduma waliyotumia. Kwa upande mwingine, maandiko yanavyoonyesha, wateja wasiporidhika wataeneza sifa za kutoridhika kwao haraka sana na kwa mapana. Vilevile kwa kuwa wateja ambao hawakuridhika huwa hawalalamiki, wanaweza kukukimbia na kufanya biashara kwingine/watu wengine. Haitakuwa vema kuamini kwamba waliridhika ndiyo maana hawalalamiki. Baadhi ya njia za kuridhisha wateja ni: Kuwapa wateja bidhaa na huduma zinazotimiza haja zao na kukidhi matarajio yao. Kuwasilisha bidhaa au huduma katika muda mliokubalina. Kutoa huduma baada ya mauzo haraka kama mlivyokubaliana. Kushughulikia matatizo au malalamiko ya wateja yanayojitokeza, haraka na kikamilifu. Kuwapa wateja huduma ya bure au kubadilishiwa bidhaa bila malipo kama wana idhini ya kufanyiwa hivyo. Ni muhimu kuwa na utaratibu wa kupokea mrejesho kutoka kwa wateja mara kwa mara ili kubaini kiasi gani wanaridhika au hawaridhiki na bidhaa au huduma uliowapa, na kuchukuwa hatua kuhusiana na mrejesho huo. Wakati mwingine mawazo/maoni ya wateja yanaweza kukusaidia kuendeleza mfumo wako wa usimamizi wa ubora. Utangazaji uliopangwa Hii itajumuisha kuweka wazi mafanikio yako kwa: Kupeleka vipeperushi vya matangazo au barua kwa wateja au wateja tarajiwa kila baada ya muda fulani. Kutoa maelezo kwa ufupi juu ya mafanikio yako kwenye brosha na maandiko juu ya bidhaa. Na unaweza kunukuu matamko uliyopata kutoka kwa wataja wlioridhika na bidhaa au huduma;siku hizi imekuwa kawaida kuziweka taarifa hizi kwenye tovuti ya kampuni. Kutangaza katika magazeti, majarida ya viwanda, magazeti ya muda maalumu, majarida ya muda maalumu ya viwanda na vyama vya biashara, kurasa za njano na katika machapisho mengine na habari za kielekitroniki; kuwa na tovuti hai yenye habari mpya; na barua mbalimbali kwa wateja tarajiwa. Kushiriki katika maonyesho ya biashara, kujitahidi kupata Tuzo za kitaifa za ubora, n.k. Baadhi ya viwanda na vyama vya wafanyabiashara huchapisha Makala maalumu kuhusu kampuni ambazo mafanikio yake yametokana na utekelezaji wa mfumo wa kusimamia ubora au nyezno zingine za kuendeleza ubora; njia hii pia inaweza kutumiwa kujitangaza. Vivyohivyo, mashirika mbalimbali na vyama vya wenye viwanda huandaa semina ambazo zinakupa nafasi ya kuwasilisha makala yako yanayohusu QMS. Njia zote hizi za kujitangaza unaweza kuzitumia. Kuhakiki mfumo wako wa kusimamia ubora na mashirika ya ithibati Kuhakiki mfumo wako wa usimamizi wa ubora (QMS) na shirika la ithibati inakupa kujiamini mbele ya wateja wako wa sasa na watarajiwa na wengine wanaohusika kuwa una Uwezo wa kuzalisha au kusambaza bidhaa/huduma bora wakati wote.

120 110 Mifumo Ya Usimamizi Mashirika mengi ya uhakiki yana orodha ya kampuni zenye uhakiki na huitoa orodha hii pindi inapotakiwa na wanunuzi watarajiwa au wahusika wengine. Katika nchi zingine orodha ya kampuni zenye uhakiki wa ISO 9001 hutunzwa na serikali au mashirika yasiyo ya kiserikali. Rejesta hizi ni chanzo muhimu cha uhakika cha habari kwa wateja watarajiwa juu ya Uwezo wa kampuni kuridhisha wateja, na huweza kukuongezea fursa za kibiashara. Kama ni kampuni yenye uhakiki, hakikisha jina lake linaorodheshwa kwenye rejesta hizi. Pamoja na kwamba uhakiki wa ISO 9001 QMS unawapa wateja wako imani kuwa utawapa bidhaa au huduma inayokidhi matakwa yao, huwezi kutumia nembo ya shirika la ithibati kwenye bidhaa yako, lebo za bidhaa au vifundashio au kwa namna yoyote ile yenye maana ya kuonyesha kuwa bidhaa yako imehakikiwa. Kwa hakika si bidhaa au huduma iliyohakikiwa, bali Mfumo wa Usimamizi wa Ubora (QMS), na hapatakiwi taarifa yoyote ambayo inasababisha kumfanya mteja awe na imani kuwa bidhaa imehakikiwa. Hata hivyo unaweza kuitumia nembo ya shirika la ithibati sambamba na nembo yako kwenye barua zako na matangazo ya mafanikio yako kutokana na uhakiki wa ISO Kwa hali hiyo, masharti na miongozo ya shirika lako la uhakiki sharti yazingatiwe. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Shirika la kimataifa la Viwango. Kutangaza uhakiki wako wa ISO 9000 au ISO Kipeperushi hiki kinalenga kuwasaidia wenye uhakiki wa ISO 9000 na ISO kuepuka adha ya udanganyifu,upotoshaji au kutoa madai changamani, vifaa vya matangazo na njia zingiine za kulfahamisha soko kuwa wanatekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora ambao umetathminiwa na kuhakikiwa kwa kujitegemea. ISO Management Systems Magazine Database. Matoleo ya kielekitroniki tangu 2001 mpaka 2009 katika lugha ya kiingereza na Kifaransa ya gazeti la ISO Mifumo ya Usimamizi ya ISO ( ISO Management Systems ) hupatikana kwa kupata habari au kupakua(download) bila malipo kutoka kwenye sehemu ya Habari na Njia za Mawasiliano ya tovuti ya ISO. Database hii inatoa maelezo ya jumula kidunia kuhusu ISO 9001, ISO na viwango vingine ya kimataifa vilivyotayarishwa na ISO na kutoa mifano ya makampuni yalioutumia mfumo huu wa ISO kwa mafanikio. MAREJELEO Shirika la Kimataifa la Viwango Kijikaratasi kinachohusu kutangaza uhakiki wako wa ISO 9001:2008 au ISO 14001:2004 (Brochure on publicizing your ISO 9001:2008 or ISO 14001:2004 certification). Hupatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (orodha iko kwenye Nembo ya ISO siyo kwa matumizi (ISO s logo is not for use.

121 Mifumo Ya Usimamizi 111 B. MIFUMO YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA 38. ISO ni kitu gani? Je, inatoka kote kwenye uzalishaji na sekta za huduma? Familia ya viwango vya ISO Mashirika pamoja na wadau duniani kote wanaendelea kutambua umuhimu wa kulinda mazingira. Ili kuyawezesha mashirika kusimamia masuala ya mazingira kwa ufanisi, ISO imeandaa viwango wa familia ya ISO kama viwango vya kusimamia mazingira. Katika hivi viwango viwili muhimu ni: ISO 14001:2004 Mifumo ya usimamizi wa mazingira-mahitaji pamoja na mwongozo wa matumizi (Environmental management systems Requirements with guidance for use ) na ISO 14004:2004 Mifumo ya usimamizi wa mazingira-mwongozo wa jumla juu ya misingi, mifumo na mbinu za kusaidia (Environmental management systems General guidelines on principles, systems and support techniques ). Kamati ya ufundi ya ISO TC-207, ambayo inahusika na uandaaji wa viwango vya familia ya ISO toka 1996 vilevile imekuwa ikiandaa viwango katika maeneo mengine, kama vile uwekaji lebo za mazingira, tathmini ya mzunguko wa maisha, usimamizi wa gesi kutoka nyumba ya mimea na shughuli husika, na wayo (footprint) wa kaboni ya bidhaa. ISO 14001:2004 ISO ndicho kiwango kinachojulikana ulimwenguni kote kama msingi wa mifumo wa usimamizi wa mazingira (EMS). Madhumuni ya EMS kwa misingi ya ISO ni kusaidia ulinzi wa mazingira na kuzuia uchafu kulingana na mahitaji ya kijamii na uchumi. ISO inawezaa kutekelezwa na aina yoyote ya shirika (la umma, binafsi, wazalishaji, watoa huduma) na ukubwa (dogo, wastani au kubwa) kusaidia kutambua vipengele vya shughuli zako ambavyo vina athari kwenye mazingira, kuweka malengo na makusudio ya kupuguza athari hizo, na kutayarisha programu za kufikia malengo na kutekeleza shughuli zingine za udhibiti kuhakikisha unatimiza mahitaji ya sera yako ya mazingira. ISO haina kiwango cha chini katika ufanisi kwa mazingira; bali, inakuhimiza kuyafikia malengo ya ufanisi wa mazingira ambao usimamizi wako umeweka kwenye sera yenu ya mazingira. Kadhalika inakuhitaji uonyeshe kinaganaga nia ya kukidhi mahtaji ya sheria ya mazingira na kuendelea kuboresha ufanisi wako katika mazingira. Itawezekana kuziweka katika uwiano ISO na ISO 9001 QMS kwa kuwa zinapatana. Matokeo ya ufanisi wa mazingira wa shirika unakuwa zaidi ya wateja na wagavi, maana unawahusu na wadau mbalimbali-raia wa kawaida, wasimamizi, wafanyakazi, makampuni ya bima na wanahisa. Kila mmoja wao anapenda kuwa na mazingira bora yanayomzunguka. Kwa hiyo ulinganifu na mfumo wa usimamizi wa mazingira chini ya misingi ya ISO 14001:2004 ni uamuzi mzuri wa kibiashara. Uhakiki kupitia ISO umekuwa ukikua daima; kufikia mwisho wa Desemba 2009, jumla ya hati zilikuwa zimetolewa kwa mashirika ya aina/ukubwa mbalimbali katika nchi zaidi ya 159. Kwa taarifa zaidi kuhusu ISO na mchoro wa viwango vinavyohusiana na mazingira, angalia swali 17. Matumizi katika sekta ya huduma Kama ilivyokwisha elezwa mapema, ISO ni msururu wa viwango vinavyohusu mifumo ya usimamizi wa mazingira na vinatumika na aina yoyote ya shirika/kiwanda, na kufaa katika hali mbalimbali za kijiografia, kitamaduni na kijamii. Mfumo unawanufaisha wazalishaji na watoa huduma, kwa kuwa shughuli zote za kibiashara na athari kwenye mazingira. Pamoja na kuwa utekelezaji wa ISO uko zaidi kwenye uzalishaji, lakini una umuhimu huohuo kwenye sekta ya huduma; mashirika ya huduma za umma kama ya umeme, maji, usafirishaji, ukusanyaji na utupaji taka, usambazaji wa mafuta na gesi, vituo ya mafuta ya petroli, dizeli na gesi. Utekelezaji wa ISO EMS utayasaidia mashirika/kampuni hizo kupunguza uharibifu wa mazingira na kuyaweka katika hali ya kupendeza wakitekeleza mahitaji ya viwango hivyo. Kwa mfano, huduma za usafiri zinaweza kutumia petrol

122 112 Mifumo Ya Usimamizi kidogo, kuwa na injini zenye ufanisi mzuri, na kupta njia zenye tija. Pamoja na mashirika haya ya huduma ya umma, watoa huduma wengine wameweza kuitumia ISO EMS kwa mafanikio; mfano mahoteli, kampuni ya ujenzi na maofisi ya huduma mbalimbali. Hoteli inaweza kupunguza gharama ya nishati, fueli na matumizi ya maji kwa kutekeleza ISO Shughuli za kawaida za maofisi huzalisha kiasi kikubwa cha taka kama vile kiwambo cha komputa, mashine za kuchapia/kudurufu, simu, maganda, kamera na vyombo vingine vya kielekitroniki (e-waste) ambavyo vinatakiwa kutupwa kwa uangalifu na salama. Utekelezaji wa ISO katika maofisi unaweza kuyasaidia mashirika husika jinsi ya kushughulikia e- waste kurejeshwa na kutupwa. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Euromines. The ultimate SME implementation guide for QMS and EMS Mwongozo huu wa utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa ubora (QMS) na mifumo ya usimamizi wa mazigira (EMS) umeandaliwa kwa tasnia ndogo na za kati na Euromines. Kituo cha Biashara cha Kimataifa (International Trade Centre). Gazeti la Usimamizi wa Ubora wa Mahuruji (Export Quality Management Bulletin) Na. 78, Utangulizi wa ISO Environmental management systems. Gazeti hili linatoa taarifa juu ya viwango vya familia ya ISO kwa mifumo ya usimamizi wa mazingira na unalenga kuwasaidia wafanyabiashara wanaouza nje ya nchi kutekeleza mifumo hiyo. MAREJELEO International Organization for Standardization Environmental management The ISO family of International Standards (brochure). Survey of ISO certificates issued as on December ISO Technical Committee ISO/TC 207 on Environmental Management. ISO 14001:2004 Environmental Management Systems Requirements with guidance for use. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 14004:2004 Environmental Management Systems General guidelines on principles, systems and support techniques. Obtainable from ISO or ISO members (list at

123 Mifumo Ya Usimamizi Je, kutekeleza ISO kutalifanya shirika lidhihirishe ulinganifu wake na mahitaji ya sheria za mazingira? Matumizi ya ISO EMS ni njia nzuri ya kuonyesha ulingaifu na mahitaji ya sheria ya mazingira. Hata hivyo, uhakiki chini ya viwango hivi, haukuondelei haja ya kukaguliwa, kupima sampuli za maji taka na mamlaka ya udhibiti wa mazingira ya nchi yako. Pamoja na kuwa uhakiki kwa ISO ni wa hiari, wanunuzi wengi kutoka ng ambo wanapenda kufanyabiashara na wagavi ambao daima watadhihirisha ulinganifu na mahitaji ya mazingira. Wanunuzi wengine wanawaagiza wagavi wao kupata uhakiki wa ISO Vilevile kwa kuzingatia dhana ya maendeleo endelevu inayozidi kupata nguvu, mashirika mengi ya biashara ya rejareja na watengeneza magari wanaelekea katika haja ya kuwa rafiki wa mazigira katika milolongo yao ya ugavi (greening their supply chain); katika michakato yao wanajitahidi kuwahamasisha wagavi wao kukubali kufuata teknolojia ambazo zinapunguza taka na athari kwenye mazingira na, kuweka mfumo wa ISO EMS. Lengo kuu la ISO ni kusaidia ulinzi wa mazingira na kuzuia uchafuzi. Kuweza kulifikia lengo hili kuu itabidi kuwa na sera ambayo itaelekeza utekelezaji wa viwango. Sera hii sharti itamke yafuatayo, kati ya mengine: Ahadi ya daima kuendeleza na kuzuia uchafuzi. Ahadi ya kutii sheria na mahitaji mengine kuhusu mazingira kuhusiana na shughuli zako, bidhaa na huduma. Kudhihirisha ulinganifu na mahitaji ya kisheria juu ya mazingira sehemu zifuatazo za mfumo wa ISO sharti vitekelezwe: Kama hatua ya kwanza, tambua na tafuta njia ya kupata mahitaji ya kiashria juu ya mazingira yanayohusiana na biashara yako; na hakikisha kuwa unapoweka Mfumo wako wa Usimamizi wa Mazingira (EMS) mahitaji haya ya kisheria yamezingatiwa. Zingatia mahitaji ya kisheria kwa mazingira wakati unaweka malengo na matarajio. Kuweza kulifiki lengo na matarajio andaa programu za usimamizi wa mazingira zinazojumuisha majukumu, usimamizi, rasilimali, njia na muda wa kutekeleza kuyafikia. Wafanyakazi wako sharti wafahamu umuhimu wa ulinganifu na sera yako ya mazingira ( pamoja na ahadi za kulingana na mahitaji ya kisheria). Kadhalika wafanyakazi wako wafahamishwe madhara ya kutofuta mahitaji yaliyoainishwa ( ukijumuisha mahitaji ya kisheria). Shughuli zote zinazohusiana ulinganifu na mahitaji ya kisheria, lazima zipangwe na taratibu za udhibiti wake ziwekwe na kufuatwa na wahusika wote. Kila baada ya muda fulani tathmini ulinganifu na mahitaji ya kisheria yanayohusika. Tambua hali yoyote ile ya kukiuka ulinganifu na mahitaji ya kisheria ( au dalili za kukiuka) na kuchukua hatua mara moja njia ya kutekeleza na kuihakikisha itumike kurekebisha kasoro iliyojitokeza au inatarajiwa kutokea. weka kumbukumbu za ulinganifu na mahitaji ya kisheria. Wakati unafanya ukaguzi wa ndani kila baada ya muda fulani, fanya tathmini kuhusiana na ulinganifu na mahitaji ya kisheria. Tumia data hizi katika kufanya rejea/marekebisho Mfumo wako wa Usimamizi wa Mazingira (EMS).

124 114 Mifumo Ya Usimamizi KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Institute for Environment and Development (IIED). Profiles of Tools and Tactics for Environmental Mainstreaming. No. 5. Environmental Management Systems (EMS). Inaelezea mifumo ya usimamizi wa mazingira (EMS), masuala yaliyolengwa, hatua zake umuhimu, na faida au hasara za mifumo hiyo. International Organization for Standardization. ISO 14004:2004, Environmental management systems General guidelines on principles, system and support techniques. Obtainable from ISO or ISO members (list at Viwango hivi vinatoa mwongozo jinsi ya kuweka, kutekeleza, kuufanyia marekebisho na maboresho ya EMS na uratibu wake na mifumo mingine ya usimamizi. MAREJELEO International Organization for Standardization. ISO 14001:2004, Environmental management systems Requirements with guidance for use. Inapatikana kutoka ISO au Wanachama wa ISO (Orodha ipo kwenye

125 Mifumo Ya Usimamizi ISO inawasaidiaje SMEs kuongeza kukubalika kwa bidhaa au huduma zao za kupeleka nchi za nje? Kila biashara hai, iwe kubwa, yenye ukubwa wa wastani au ndogo, zina uwezekano wa athari kwenye mazingira kuanzia kwenye matumizi ya malighafi, mali asili na, nishati, mpaka kwenye utoaji wa taka wakati wa uzalishaji, usambazaji wa bidhaa, matumizi ya bidhaa na wateja na mwisho utupaji wa taka/mabaki. Kwa hiyo utekelezaji wa ISO EMS una umuhimu uleule hata kwa SMEs na kwa maendeleo yao. Utekelezaji wa ISO EMS unaweza kuwasaidia SMEs kwa njia ambazo zinafafanuliwa hapa chini kuongeza kukubalika kwake katika masoko ya nje ya nchi. Mwezeshaji wa biashara ya mahuruji Kama ulivyo mfumo wa usimamizi ubora wa ISO 9001 kuwa mwezeshaji wa biasharanje, uandaaji wa mfumo wa kisimamia mazingira nzuri, utawasaidia SMEs kuepuka vikwazo vya biashara. Pamoja na mwelekeo wa kufanya mnyororo wa ugavi kuwa green, yaani unopuguza uzalishaji taka matumizi ya vitu/vifaa vyenye athari ndogo kwenye mazingira, kampuni nyingi makubwa yanagiza mahitaji yake kupitia kwa wagavi ambao wameonyesha ulinganifu na mahitaji ya kimazingira. Kwa hiyo utekelezaji wa ISO EMS, utawasaidia SMEs kuchaguliwa na minyororo ya wauza rejareja wakubwa. Kwa mfano kuwa mgavi wa mashirika kama Wal-Mart, Tesco na Macy sharti uchunguzwe kama unakidhi mahitaji ya mazingira. Kama wagavi kama hao baada ya kufaulu uchunguzi wa awali wa kukidhi mahitaji ya wanunuzi, wataonyesha kuwa pia wanatekeleza ISO EMS na kwamba wana uhakiki kupitia viwango hivi, basi wawe na uhakika wa kupewa nafasi ya juu katika kuteuliwa kuwa wagavi. Kipandisha hadhi SMEs wanatekeleza ISO EMS wanaweza kuonesha kuwa wanajali mazingira mbele ya wateja wao, raia wa kawaida, wenye hisa, wasimamizi, wawekezaji na kampuni ya bima. udhihirisho huu ulioboreshwa utawapa imani wanunuzi wa ndani na nje kupendelea kuwatumia SMEs hao kama wagavi wao. Bei za ushindani Nia ya ISO EMS ni kulinda mazingira na kuzuia uchafuzi. Hii itahitaji shirika kuandaa mipango na kuonyesha uangalifu (kupunguza taka na mabaki) katika mtumizi ya malighafi na rasilimali kama umeme, maji na fueli. Utekelezaji wa mipango hii, utawafanya SMEs kupunguza gharama za uzalishaji na kwa hiyo kuwafanya wawe na bei ya ushindani kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, Hogarth katika utafiti wake wa Milan Screw, SME wa Michigan aliripoti kupunguza gharama kwa US $ 20, 000 pale kampuni ilipobuni mbinu bora ya mfumo wa kuondoa oili baada ya kuweka na kutekeleza ISO EMS. Kampuni moja iligundua kuwa pamoja na kuweza kurejeresha asili mia 94 ya taka zake,matumizi ya ISO EMS, iliiwezesha kuanzisha kituo cha faida (Fielding, 1999). Mfano mwingine unahusika na uzalishaji usiochafua mazingira na kampuni ya Ming Chi Computor ya China iliyopata zaidi ya US $ 1.8 milioni kama ziada kutokana kupunguza matumizi ya nishati na kurejea kwa rasilimali na maji (ITC, 2007). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization. ISO The world s environmental management system standard. A concise video freely downloadable from ISO. Filamu hii inaelezea kuhusu ISO na athari yake katika dunia nzima tangu uzinduzi wake mnamo mwaka wa Inapatikana katika lugha ya Kingereza pekee. Muda wa filamu: dakika tano na sekunde saba. International Trade Centre and International Organization for Standardization. ISO Environmental Management Systems: An easy-to-use checklist for small business. Are you ready? ISBN Obtainable from ITC ( and ISO ( ISO Environmental Management Systems Benefits. Ujumbe kuhusu manufaa ya kimazingira katika ISO imetolewa na Transformation Strategies katika tovuti yao.

126 116 Mifumo Ya Usimamizi MAREJELEO Fielding, S. Going for the Green: ISO Delivers profits. Industrial Management pp International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 78, An introduction to ISO Environmental management systems. Masero, Sonny. Eco-Competitiveness: Safeguarding Profitability and the World s Natural Resources. Wal-Mart Sustainability Index.

127 Mifumo Ya Usimamizi Kuna gharama na faida gani za kutekeleza ISO 14001? Gharama za kutekeleza ISO na kupata uhakiki wake hutofautiana sana. Zinategemea ukubwa wa kampuni/shirika na shughuli zake. Zinaweza kugawanywa katika aina tatu: Gharama za kuanzisha na kutekeleza EMS; Gharama za kuendeleza EMS; Gharama za mwanzo za uhakiki na gharama zinazohusika na kuhakikisha uhakiki unaendelea. Gharama muhimu kwa kila eneo zimeorodhesha chini ya kila aina katika sehemu inayofuata. Maelezo ya faida za kutekeleza ISO 14001, pia yametolewa. Gharama ya kuweka na kutekeleza EMS Kununua viwango na kulipia ada za majarida ili kukuwezesha kuwa sambamba na maendeleo katika elimu/ujuzi wa viwango vya EMS na kanuni husika za mazingira. kufundishwa kwa meneja mmoja au wawili wa kampuni yako ili waweze kuelewa vizuri mahitaji ya ISO Mafunzo haya yanafanywa na wakufunzi wa nje. Tathmini ya hali halisi ya sasa kuhusu uzalishaji wa taka na vichafuzi, na matumizi ya rasilimali (maji, fueli, umeme, malighafi, n.k.) katika kampuni yako. Katika hatua hii pia orodhesha sera yoyote na taratibu inayohusiana na EMS ambayo inawezekana tayari mnatekeleza kwenye kampuni. Shughuli hii injulikana kama hatua ya awali ya tathmini ya mazingira. Kutokana na matokeo ya pointi namba 3 hapo juu, unaweza kuona kwamba kuna haja ya kufufua baadhi ya vifaa vya kupunguza uchafuzi au kusimika vipya. Vilevile inawezekana kukawa na haja ya kuandaa utaratibu mzuri wa kuhifadhi kemikali, fueli na taka za hatari kwa usalama. Utayarishaji wa nyaraka zinazohusiana EMS (sera ya mazingira na malengo, mwongozo wa EMS, taratibu za kudhibiti uendeshaji, taraibu zinazohusiana- na-mfumo). Wafahamishe watu wote ambao wa wajibu na majukumu kuhusiana na shughuli za EMS na kutoa mafunzo penye haja na iwapo yanahitajika. Gharama ya kudumisha EMS Upimaji wa maji taka kila baada ya muda fulani. Uhaakiki wa usawa wa vipimo vya vifaa vya upimaji kila baada ya muda fulani. Mafunzo ya mara kwa mara kwa mameneja ili waweze kufanya ukaguzi wa ndani kila baada ya muda fulani. Maelekezo ya mara kwa mara, kuongeza ufahamu na mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi ili kuwaendeleza na kuwafahamisha mabadiliko yaliyotokea kwenye sheria na uendelevu wa EMS. Shughuli nyingi za mafunzo zinaweza kufanywa na wafanyakazi wenyewe baada ya kuelimika juu ya viwango vya ISO 14001:2004, ambavyo ndiyo mwongozo. Mfanyakazi mmoja au wawili wanaweza kuombwa kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi juu ya utekelezaji wa ISO kuongeza maarifa yao. Vinginevyo unaweza kuajiri washauri au wataalamu wenye ujuzi katika fani ili waendeshe mafunzo hayo kwa wafanyakazi. Pollution abatement refers to the technology applied or measure taken to reduce pollution and/or its impacts on the environment. The most commonly used technologies are scrubbers, noise mufflers, filters, incinerators, waste-water treatment facilities and composting of wastes. United Nations Statistics Division, Glossary of Environmental Statistics, Sales number: 96.XVII.12.

128 118 Mifumo Ya Usimamizi Gharama ya uhakiki wa kwanza na gharama za kuudumisha, zinazolipwa kwa shirika la uhakiki ulilochagua Usajili au ada zinazolipwa kwa shirika la uhakiki lililochaguliwa kwa muda wa miaka mitatu. Ada kwa ajili ya ukaguzi wa uhakiki katika hatua mbili unaofanywa na wakaguzi wa shirika la uhakiki. Ada ya ukaguzi wa uchunguzi unaofanywa na wakaguzi wa shirika la uhakiki kila baada ya kipindi fulani. Gharama za usafiri na malazi za wakaguzi wa shirika la uhakiki kwa kazi za ukaguzi zilizotajwa hapo juu. Labda ni vyema kufahamisha kuwa uhakiki wa ISO siyo wa lazima baada ya kutekeleza EMS. Kawaida ni jambo la kufanya kutegemea mahitaji, kwa hiyo usimamizi inabidi kufanya maamuzi kama unahitajika kabla ya kungia gharama tulizoziorodhesha hapo juu. Faida za kutekeleza ISO EMS Pamoja na gharama nyingi zinazohusika na utekelezaji na kuudumisha mfumo wa usimamizi wa mazingira (EMS), faida nyingi za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa kwa moja zinazopatikana zinafidia gharama hizi. Faida muhimu kutokana na kutekeleza EMS zinajumuisha zifuatazo: kupanda hadhi mbele ya jamii uaoendana na kuongezeka kwa fursa za biashara kwa soko la ndani na nje ya nchi. wateja wengi, ikijumuisha na mamlaka za ununuzi wa serikali hutumia ISO EMS kama moja ya vigezo vya tathmini kwa wagavi watarajiwa. Utekelezaji wa ISO utakupa sifa zaidi juu ya wagavi wengine. Kuendeleza ulinganifu na mahitaji ya kisheria na usimamizi yatapunguza adha ya kulipa faini na gharama za mashauri/marekebisho. EMS itasaidia kupunguza matukio ya utoaji vichafuzi, fueli au kumwagika/kuvuja kwa kemikali bila udhibiti na kwa hiyo kutakuwa na kupungua gharama za kuyapata tena. Unaweza kuokoa gharama kutokana na kurejeresha na kutumia tena vitu. Moja ya malengo ya EMS ni kupunguza taka na kama inawezekana kuitumia tena au kurejereshwa, matokeo yake kupunguza gharama za kutupa. Wafanya kazi watakuwa na mazingira salama ya kazi, ambayo yataongeza tija, kupuguza siku za ugonjwa na mashaka ya hatari za kuwekea bima. Hapa kuna baadhi ya mifano ya faida ambazo zinapatikana kutokana na kuwa na EMS inayofaa. Kule Singapore, SGS-Thomson waliweza kuokoa US$ 200,000 baada ya kuboresha matumizi ya nishati katika mtambo wake wa poza. Kampuni nyingine Sony Display Devices, iliokoa kiasi cha US$ 7.5 milioni kwa mwaka baada ya kuondoa upotevu wa malighafi. Baxter ambao wamepata uhakiki wa ISO wametangaza kuokoa na kupunguza matumizi kwa kiasi cha US$ 3.4 milioni kwa kutekeleza mfumo wa usimamizii wa mazingira. Tasnia ya kati ya mtengezaji wa vifaa mahususi kwa ajili ya viwanda vya mitambo na vitia baaridi, waligundua kasoro katika taratibu zake za kupata tena oili wakati wa utekelezaji wa EMS. Kwa kulitatua tatizo hilo kampuni inategemea kuokoa zaidi ya US$ 20,000 kwa mwaka. mzalishaji mwingine aliripoti kuwa alipata kupunguza gharama za utupaji taka kwa asili mia 70 baada ya kutekeleza mfumo wa usimamizi wa mazingira (ISO EMS). Kampuni kubwa zinaweza kutekeleza EMS kwa urahisi kwani wana nguvu ya fedha na faida ya uzalishaji mkubwa. Kwa upande mwingine SMEs wanaweza kupata shida kutekeleza EMS kwa sababu ya changamoto za kuweza kutekeleza udhibiti wa mazingira kwa ajili ya uhaba wa rasilimali. Baadhi ya serkali, kwa kulitambua hili wanawasaidia SMEs mitaji ya kutekeleza EMS. Kwa mfano, katika nchi ya Singapore, wakala wa serikali SPRING (Standards, Productivity and Innovation Board) Bodi ya Viwango, Tija na Uvumbuzi ilipanua mpango wake wa kusaidia tasnia za dani kifundi ili uweze kutoa msaada wa fedha kwa SMEs wanaotaka kutekeleza EMS na kuapata uhakiki wa ISO nchini India, msaada wa fedha hutolewa kwa SMEs ili wapate mifumo ya usimamizi wa ubora, mazingira na usalama wa chakula (HACCP).

129 Mifumo Ya Usimamizi 119 KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Commission for Environmental Cooperation (USA). Successful Practices of Environmental Management Systems in Small and Medium-Size Enterprises: A North American perspective. Inajumuisha maana ya EMS na SME; inajadili umuhimu wa kulinda mazingira katika kuboresha utendakazi wa kimazingira, manufaa na sifa za EMS, na miongozo na vizingiti vya kutekeleza EMS katika biashara ndogo na za wastani na mengineyo. Environmental Management Systems (EMS). EMS case studies. Inatolea mifano ya kampuni na kibinafsi na za kiserikali ambazo zinatumia ISO International Organization for Standardization Environmental management The ISO family of International Standards. This brochure is freely available from ISO. Kipeperushi hiki kinatoa utangulizi wa kimsingi juu ya familia za ISO 14000, inapeana (ingawa kwa kifupi) maoni ya jinsi zimekua ili kutoa suluhu toshelezi kwa maswala tata mengi ya kimazingira ambayo yanakumba biashara, serikali, jamii ya kisasa na pia inaashiria kwamba matokeo ya viwango vya ISO sio tu kimazingira, lakini pia umuhimu wake kiuchumi. ISO The world s environmental management system standard. (page 144) Video hii inapatikana kupitia tovuti ifuatayo ya ISO. Filamu hii inaelezea kuhusu ISO na athari yake katika dunia nzima tangu uzinduzi wake mnamo mwaka wa Inapatikana katika lugha ya Kingereza pekee. Muda wa filamu: dakika tano na sekunde saba. ISO Environmental Management Systems Benefits. Information displayed by Transformation Strategies on their website ISO 14004:2004, Environmental management systems General guidelines on principles, systems and support techniques. Obtainable from ISO or ISO members (list at Viwango hivi vinatoa mwongozo wa jinsi ya kuanzisha, kutekeleza, kudumisha na kuendeleza EMS na uratibu wake na mifumo mingine ya usimamizi. Sehemu ya utangulizi ya viwango in taarifa juu ya namna gani ISO EMS inaweza kulisaidia shirika daima kuendeleza ufanisi wake katika mazingira na kupata faida za kiuchumi kutokana nalo. International Trade Centre and International Organization for Standardization. ISO Environmental Management Systems: An easy-to-use checklist for small business. Are you ready? ISBN Obtainable from ITC ( and ISO ( Shaheen, Rafi Khan and others. The Costs and Benefits of Compliance with International Environmental Standards. International Institute for Sustainable Development Utafiti wa gharama na faida za ulinganifu na mfululizo wa viwango vya ISO MAREJELEO Development Commissioner (MSME), Ministry of Micro, Small & Medium Enterprises, Government of India. Quality Upgradation/Environment management for small scale sector through incentive for ISO 9000/ISO 14001/HACCP Certifications Environment International Ltd. Q & A: Environmental Management Systems and ISO Environmental Management Standards in Singapore. International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 78, An introduction to ISO Environmental management systems. United Nations Statistics Division. Environment Glossary.

130 120 Mifumo Ya Usimamizi C. MIFUMO YA USIMAMIZI WA USALAMA WA CHAKULA 42. Nini maana ya mfumo wa kuchanganua majanga na hatua muhimu za udhibiti (Hazard Analysis and Critical Control Points (HACCP) na kwa nini ni muhimu kwa SMEs katika sekta ya chakula? Kila mtu ana haki ya kutegemea kuwa chakula ambacho anakula ni salama na hakitamuumiza au kumletea magonjwa. Majanga yanayohusika na usalama wa chakula yanafahamika kama; majanga ya kibiolojia, kemikali na kimaumbile ambayo kama yakiwa kwenye chakula huweza kusababisha maumivu au ugonjwa kwa binadamu. Mfumo wa kuchanganua majanga na hatua muhimu za udhibiti (HACCP) unaainishwa kama mfumo ambao unatambua, changanua na kudhibiti majanga ambayo ni muhimu kwa usalama wa chakula (FAO).HACCP ni dhana ya kinga. Inasaidia kuhakikisha chakula kinakuwa salama kuanzia uvunaji hadi kuliwa ( kutoka shambani hadi kwenye uma ). Kila hatua inayohusika katika uzalishaji wa chakula, yaani kununua, kupokea, uhifadhi, usindikaji, ufungashaji, kuweka ghalani, usambazaji mpaka hatua ya kula vyote hufanyiwa uchaganuzi wa majanga na udhibiti kuwekwa. Mantiki ni rahisi: kama kila hatua ya mchakato ikifanyika vyema, bidhaa ya mwisho itakuwa salama. Kwa mara ya kwanza HACCP ilibuniwa mwaka 1960, mwanzo wa programu ya kwenda angani. Taasisi ya kitaifa ya masuala ya anga ya Marekani (NASA (National Aeronautics and Space Administration) ilitaka kupata kuwa vyakula vinavyoliwa kwenye vyombo vya angani havitasababisha magonjwa yatokanayo-nachakula. Kwa sababu ya hitaji hili, kampuni ya Pillsbury na Maabara za Utafiti za Jeshi, Natick Marekani yalivumbua mchakato ambao ungehakikisha uzalishaji wa chakula salama; mchakato huo uliitwa HACCP. Mwaka 1993, Tume ya Kodeksi Alimentarius (CAC) ilichapisha mwongozo wa utekelezaji wa mfumo wa HACCP. Baadaye mwaka 1997, CAC iliijumuisha HACCP kama kiambatisho cha mapendekezo ya kanuni za kimataifa za utendaji wa jumla wa misingi ya afya. Recommended International Code of Practice General Principles of Food Hygiene (latest version: Rev ). Mfumo wa HACCP una misingi saba ambayo inatoa maelezo kwa ufupi jinsi ya kuanzisha, kutekeleza na kudumisha mpago wa HACCP. Misingi saba ya mfumo wa HACCP 1. Fanya uchanganuzi wa majanga andaa mchoro wa mtiririko wa mchakato/uzalishaji ukipitia kila hatua kuanzia upokeaji wa malighafi mpaka kutuma bidhaa iliyokamilika. Tambua majanga yanayoweza kutokea katika kila hatua na ainisha njia za kudhibiti majanga katika kila hataua ya mchakato. 2. Ainisha hatua muhimu za udhibiti (CCPs) changanua kila hatua kwa kutumia mti wa maamuzi; na tambua zile hatua ambapo ni muhimu udhibiti kufanywa kuhakikisha usalama wa bidhaa 3. Weka vikomo muhimu ainisha mwisho wa kuweza kulidhibiti janga katika kila CCP (k.m. nyuzi joto, muda, kasi, ph, unyevunyevu). 4. Anzisha mfumo wa kufuatilia udhibiti wa CCP 5. Anzisha hatua za kusahihisha zitakazochukuliwa, endapo matokeo ya ufuatiliaji yatabaini kuwa CCP fulani haidhibitiki 6. Anzisha taratibu za kuhakikisha kuwa mfumo wa HACCP unafanya kazi kwa ufanisi 7. Anzisha uwekaji kumbukumbu/ripoti za taratibu zote kwa mjibu wa misingi ya HACCP na utekelezaji wake Chanzo: S.C. Arora, India. amua utaratibu utakaotumika kufuatilia, ambao utaelezea jinsi ya kufuatia (kuangalia, kupima), mara ngapi na majukumu ya kuweka kumbukumbu za matokeo. Buni njia za kushughulika na ukiukwaji wa vikomo muhimu unapotokea na namna ya kurudisha udhibiti wa CCP, ikijumuisha jinsi ya kushughulika na bidhaa iliyoathiriwa na ukiukwaji huu. Tayarisha taratibu za kuhakikisha kuwa mpango wa HACCP unakwenda vizuri (k.m. ugakuzi baada ya muda Fulani, kuchukua sampuli bila mpangilio na kuzipima, kuurejea mfumo wa HACCP na kumbukumbu zake). Tayarisha na fuata taratibu na maelekezo ya kazi kwa kila kigezo cha udhibiti, ikijumuisha vile vinavyohitajika kudumisha hali ya usafi/afya; weka kumbukumbu.

131 Mifumo Ya Usimamizi 121 HACCP ni mfumo usiofanya kazi peke yake; kanuni bora za afya na masharti mengine ya usindikaji vyakula, pamoja na kujitolea dhati kwa usimamizi ni mahitaji muhimu. HACCP haichukui nafasi ya mambo hayo. Kama kampuni yako inazalisha bidhaa nyingi utalazimika kuwa na mpango wa HACCP tofauti kwa kila bidhaa, ukizingatia misingi saba iliyotajwa hapo juu. Katika miaka ya 1990, HACCP ilikubaliwa na nchi nyingi (Australia, Denmark, Germany, India, Ireland, Netherlands, United States na zingine) katika viwango vya kitaifa vinavyoainisha mahitaji ya mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula. Kadhalika ilijumuishwa katika kanuni za Jumuiya ya Ulaya zinazohusika na usafi wa vyakula. Mwaka 2005 Shirika la Viwango la kimataifa (ISO) lilitayarisha viwango vya kimataifa ISO 22000:2005 juu ya Mifumo wa usimamizi wa Usalama wa Chakula-mahitaji ya shirika lolote katika mnyororo wa chakula (Food Safety Management Systems Requirements for any organization in the food chain ), ambavyo vinajumuisha misingi ya HACCP (angalia maswali 44 na 45). Kuna umuhimu wa SMEs kwa wanaosindika vyakula kwa kutumia HACCP kwa sababu mbili zifuatazo: kwanza, kuleta faida za ndani kama kupunguza mashaka ya kutengeneza na kuuza bidhaa zisizo salama, ambazo zitaaminiwa zaidi na wateja. Pili, mamlaka za usimamisi wa sheria katika nchi nyingi wanautumia au wanamatarajio ya kutumia HACCP katika kanuni zao za chakula. Kwa hiyo, ukitekeleza HACCP utakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kama muuzaji bidhaa kwenda nchi hizo (angalia swali 46). Kwa mfano katika kabrasha la mwongozo lijulikanalo kama Maswali Muhimu Kuhusu Mahitaji ya Maduhuli na Sheria Mpya ya Usafi wa Chakula na Udhibiti Rasmi wa Chakula (Key questions related to import requirements and the new rules on food hygiene and official food control), iliyotolewa na Idara Kuu ya Afya na Ulinzi wa Wateja ya Tume ya Ulaya, Jumuiya ya Ulaya imefafanua kwamba sheria mpya za EU juu ya usafi wa chakula (kuanzia 1 Januari 2006) zitatumika na biashara zote zinazoshughulikia chakula baada ya kuvuna. Kwamba zitaweka na kutekeleza na kudumisha taratibu zenye misingi ya HACCP. Hata hivyo sheria hizi zinauwezekano wa kubadilika kuliko zile za mfumo wa zamani, kwa kuwa msingi ya HACCP inaweza kutumiwa katika mazingira mbalimbali (Tume ya Ulaya, 2006). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Asian Productivity Organization. Hazard Quality Enhancement in Food Processing Through HACCP (Analysis and Critical Control Point) Repoti ya Utafiti wa APO Juu Mkutano wa Uendelezaji Ubora Katika Tasnia Ndogo na za Kati Kupitia HACCP, ulifanyika India APO ni Shirika la Tija la Asia (Asian Productivity Organization) Food and Agriculture Organization of the United Nations and World Health Organization. Assuring Food Safety and Quality: Guidelines for Strengthening National Food Control Systems. Nyaraka hii inajumuisha uaslama wa chakula,ubora na ulinzi wa wateja na maelezo mafupi kuhusu masuala mahususi ya nchi zinazoendelea. International Trade Centre Export Quality Management Bulletin No. 71, Introduction to HACCP. Gazeti hili linatoa taarifa kuhusu HACCP, misingi yake; utekelezaji wake, HACCP katika biashara ya kimataifa; linatoa mifano ya matumizi ya mti wa maamuzi katika kuainisha CCP; linaorodhesha tovuti ambamo utapata habari za HACCP na Vitabu na nyaraka zingine kuhusu HACCP. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management. Inatoa habari kuhusu usalama wa chakula, sheria za SPS, Misingi ya HACCP na usalama wa chakula, mfumo wa usiamizi wa usalama wa chakula (FSMS) ya ISO 22000, faida za FSMS, utekelezaji na uhakiki wa FSMS,n.k. MAREJELEO Codex Alimentarius Commission. Recommended International Code of Practice General Principles of Food Hygiene (CAC/RCP , Rev ). Freely obtainable from European Commission. Guidance document: Key questions related to import requirements and the new rules on food hygiene and on official food controls (Brussels, ).

132 122 Mifumo Ya Usimamizi 43. HACCP inatekelezwaje? Kabla ya mfumo wa HACCP kuwekwa, mambo muhimu yafuatayo sharti yawekwe/sanifiwe kufuata misingi ya usafi na afya, yaani mahali, majengo, vifaa, mashine na vyombo vya usindikaji. Kadhalika utaratibu wa maandalizi, usafi, kudhibiti wadudu/wanyama waharibifu na usimamizi wa taka uwekwe; afya njema kwa wafanyakazi na taratibu za usafi nazo pia ziwepo. Vyote hivi vinajulikana kama Njia Nzuri za Uzalishaji(GMP-Good Manufacturing Pratices) na Njia Nzuri za kutunza Usafi/Afya (GHP-Good Hygiene Practices) kadiri inavyohusika. Njia/taraibu nzuri za uzalishaji zimefafanuliwa katika ISO/TS :2009 Prerequisite programmes on food safety (Mahitaji ya awali ya programu ya usalama wa chakula), Ambapo Njia Nzuri za Kutunza Usafi/Afya zinaweza kunukuliwa kutoka Recommended International Code of Practice: General Principles of Food Hygiene, kwenye tovuti ya Kodeksi Alimentarius. Baada ya kukamilisha usanifu wa vifaa/kiwanda katika misingi ya usafina afya, na misingi ya uzalishaji mzuri, usimamizi wa kiwanda nao unabidi kuahidi kusaidia katika kuweka na kutekeleza mfumo wa HACCP. usimamizi unaweza kuonyesha msaada wake kwa kumteua mratibu, kutoa rasilimali za kuwezesha utekelezaji na utaratibu wa kufanya tathmini baada ya kipindi fulani utekelezaji wa mpango wa HACCP. Vilevile kuwe na mafunzo ya daima kwa wasimamizi na wafanyakazi, ili kuwapa ujuzi juu ya HACCP na utekelezaji wake. Hatua zinazoelezwa hapa chini zimependekezwa na Misingi ya Jumla ya Usafi wa Chakula (General Principles of Food Hygiene) ya Kodeksi kwa ajili ya kuandaa na kutekeleza mpango wa HACCP. 1. Teua timu ya HACCP (Hatua-awali1) Teua timu ya waelewa mbalimbali na mratibu wa HACCP, wakiwemo wataalamu wale wenye elimu na uzoefu kwenye eneo la uhakiki wa ubora wa chakula, uzalishaji, uhandisi, ununuzi, matengenezo; hawa wanaweza kuwa watendaji wa ndani au waliokodishwa. Timu sharti ifahamu hadidu za rejea/upana wa mfumo wa HACCP pamoja na bidhaa aina ya majanga yatakayoshughulikiwa, yawe ya kibiolojia, kikemikali, kimaumbile au mchanganyiko. 2. Elezea bidhaa (Hatua-awali 2) Maelezo ya bidhaa sharti yajumuishe jina la bidhaa, viambato, viambaupishi vinavyoingia, sifa za bidhaa, mujumuiko, aina, ufungashaji, muda wa kuishi, hali ya uhifadhi (joto, ubaridi, kugandisha kwa barafu), usambazaji, maelekezo kwenye lebo, udhibiti maalum wa usambazaji n.k. 3. Ainisha matumizi yanayokusudiwa (Hatua awali 3) Matumizi yaliyokusudiwa yalenge matarajio ya matumizi kwa mtumiaji wa mwisho wa bidhaa au mlaji. Mfano makundi yaliyo katika hatari kwenye jumuia, makundi yaliyo na mzio (k.m. watoto, wazee, wagonjwa hospitalini, wajawazito). 4. Kutengeneza mchoro wenye mtiririko (Hatua awali 4) Andaa mchoro wenye mtiririko (sharti utengenezwe na timu ya HACCP) ukizingatia hatua zote kwenye operesheni. Ni rahisi kuainisha mikondo muhimu ya uchafuzi, kupendekeza njia za kudhibiti na kujadili mambo haya baina ya timu ya HACCP kama kuna mtiririko na mchoro ueleze mpangilio wa sakafu na vifaa, njia za wafanyakazi, mikondo muhimu ya uchafuzi unaoingiliana sehemu ya kutenganisha mtiririko wa kiambato na vifungashio, sehemu vilipo vyumba vya kubadilishia nguo, vyumba vya kuoshea, vyumba vya kulia chakula, vituo vya kuoshea mikono, vyoo n.k. 5. Uthibitisho wa mtiririko wa mchoro kwenye eneo (Hatua-awali 5) Fuatilia uzalishaji/shughuli siku ya kawaida ya kazi shifti zote na hata mwisho wa wiki halafu rekebisha mtiriko kadiri inavyostahili.

133 Mifumo Ya Usimamizi Orodhesha majanga yote yanayotarajiwa katika kila hatua, changanua janga, zingatia njia za kudhibiti majanga (Msingi 1 wa Kodeksi) Orodhesha majanga yote yanayotarajiwa (kama yalivyoainishwa) katika kila hatua ya mchakato. Changanua mashaka/hatari zilizopo katika kila janga ( uwezekano wa kutokea na athari yake), kutambua vyema kila janga ni muhimu na njia za kuliondoa au kupunguza athari zake kwa usalama wa chakula. Elezea kwa kina njia za kinga kwa kila janga lililotambuliwa (k.m njia ya mgavi kudhibiti, kupunguza joto, kuchemsha, kuchekecha, kuondoa metali, usafi kama kuosha mikono, kuvaa kofia, usafishaji na matengenezo) 7. Ainisha hatua muhimu za udhibiti (CCP) (Msingi 2) Tumia mti wa maamuzi (kama ulivyoelezewa katika misingi ya Jumla ya Usafi/Afya ya Kodeksi) katika kila hatua (kwa kila janga) na ainisha hatua ambazo udhibiti ni muhimu kwa kuhakikisha usalama wa chakula; hatua hizo huitwa CCP. 8. Weka vikomo kwa kila CCP (Msingi 3) Sahihisha kikomo (kigezo cha udhibiti ambacho lazima kifikiwe ili kuhakikisha usalama wa chakula, kwa mfano vipimo vya nyuzi joto, muda, kiasi cha unyevu, ph, water activity (Aw), kiasi cha klorini iliyopo na vipimo vya hisia kama mwonekano, ulaini kwa kila CCP. Vikomo vinaamuliwa kwa misingi ya sheria, viwango vya kitaifa au kimataifa au data za kisayansi. 9. Weka mfumo wa kufuatilia kila CCP (Misingi wa 4) Chagua njia sahihi ya ufuatiliaji (k.m. kuangalia, kukagua, kupima, kipimo ). Amua kasi ya kufuatia, gawa majukumu ya kufuatia na weka kumbukumbu za matokeo ya ufuatiliaji. 10. Weka hatua za kuchukua kurekebisha (Msingi wa 5) Ainisha hatua za kuchukua kurekebisha mchakato ili uendelee kudhibitiwa kama matokeo ya ufuatiliaji yataonyesha mwelekeo wa kupoteza udhibiti. Ainisha hatua zitakazochuliwa kukabiliana na bidhaa zilizozalishwa wakati CCP ilikuwa nje ya udhibiti. Ainisha majukumu ya hatua za kurekebisha na kushughulikia bidhaa zilizozalishwa bila udhibiti wa CCP. Weka kumbukumbu za hatua zilizochukuliwa. 11. Anzisha taratibu za kudhibitisha (Msingi wa 6) Ukiwa na lengo la kujua kama mfumo w HACCP unafanya kazi sawasawa, andaa utaratibu wa shughuli za kudhibitisha na panga uwajibikaji kwa ajili yake. Shughuli za kuthibitisha zinajumuisha kuurejea mfumo wa HACCP na kumbukumbu zake, ukaguzi wa ndani na nje, uchukuaji sampuli usio na mpangilio, upimaji wa bidhaa, uchunguzi wa kilichopanguswa (swabs). 12. Anzisha uandaji ripoti na kuweka kumbukumbu (Msingi wa 7) Andaa nyaraka na kutunza kumbukumbu kwa ufanisi, kama inavyohitaji na mfumo wa HACCP. Kwa mfano, uchanganuzi wa majanga, CCP zilizotambuliwa na vikomo vyake (ikijumuisha marekebisho, kama yapo) lazima yaandikwe. Mifano ya kumbukumbu ni kama, kumbukumbu za kufatilia CCP, kumbukumbu za ukiukaji uliobanika na hatua zilizochukuliwa kurekebisha, kumbukumbu za kuthibitisha.

134 124 Mifumo Ya Usimamizi Uhakiki huru wa HACCP Kwa kuwa HACCP ya Kodeksi ni nyaraka ya mwongozo, huwezi kuhakikiwa chini yake. Kuziba pengo hilo nchi kama Australia, Denmark, Ujerumani, India, Ireland, Uholanzi na Marekani walitayarisha viwango ya kitaifa vya mfumo wa usalama wa chakula kwa misingi ya HACCP ya Kodeksi; uhakiki kupitia viwango hivi unawezekana kama ilivyo kwenye mfumo mingine ya usimamizi, uhakiki wa HACCP ni wa hiari. Kama usimamizi wako utaona unahitajika, basi maombi yanaweza kupelekwa kwa shirika la uhakiki watakalolichagua. Mahitaji ya awali kwa uhakiki wa namna hii unajumuisha utekelezaji wa mfumo kwa miezi mitatu, uthibitisho wa ndani kwamba mfumo unafanya kazi vyema, ukifuatiwa na kupitiwa tena na usimamizi. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA International Organization for Standardization. ISO/TS :2009. Prerequisite programmes on food safety Part 1: Food manufacturing. Obtainable from ISO or ISO members (list at Inaainisha mahitaji ya kuanzisha, kutekeleza na kudumisha mahitaji awali (PRP) kusaidia kudhibiti majanga ya usalama wa chakula. International Trade Centre Export Quality Management Bulletin No. 71, Introduction to HACCP. Gazeti hili linatoa taarifa kuhusu HACCP, misingi yake; utekelezaji wake, HACCP katika biashara ya kimataifa; linatoa mifano ya matumizi ya mti wa maamuzi katika kuainisha CCP; linaorodhesha tovuti ambamo utapata habari za HACCP na Vitabu na nyaraka zingine kuhusu HACCP. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management. Inatoa habari kuhusu usalama wa chakula, sheria za SPS, Misingi ya HACCP na usalama wa chakula, mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula (FSMS) ya ISO 22000, faida za FSMS, utekelezaji na uhakiki wa FSMS,n.k. Technical Manual 38, HACCP: A Practical Guide, 2nd ed. A priced publication of Campden and Chorleywood Food Research Association, Chipping Campden Gloucestershire, GL55 6LD United Kingdom, website pbs@campden.co.uk Mwongozo huu unaelezea misingi ya HACCP na kuelekeza matumizi yake. World Health Organization. Strategies for Implementing HACCP in Small and/or Less Developed Businesses Food Safety Programme, Avenue Appia 20, 1211 Geneva 27, Switzerland. Ripoti hii inaeleza faida za, na vikwazo kwa,kutekeleza HACCP, linatoa ushauri juu ya utayarishaji wa miongozo inayolenga viwanda Fulani na inatoa mwongozo wa matumizi ya mfumo wa HACCP katika tasnia ndogo na /au biashara changa. MAREJELEO Codex Alimentarius Commission. Recommended International Code of Practice General Principles of Food Hygiene (CAC/RCP , Rev ). Freely obtainable from

135 Mifumo Ya Usimamizi Kuna tofauti gani kati ya HACCP na ISO 22000? Malengo ya msingi ya HACCP ya Kodeksi na Mfumo wa usimamizi wa Usalama wa Chakula ISO (FSMS) ni kuhakikisha kwamba chakula kinachozalishwa na shirika/kampuni kiko salama kwa matumizi ya binadamu. Vipengele vya mfumo wa HACCP Kodeksi vina misingi saba (angalia swali 42) na hatua 5 za awali za kuandaa na kutekeleza Mpango wa HACCP (angalia swali 43). Vipengele vyote hivi vimeshajumuishwa kwenye ISO (iliyochapishwa mwaka 2005 kama ISO 22000:2005-Mifumo ya usimamizi ya Usalama wa Chakula-Mahitaji ya shirika lolote katika mnyororo wa chakula ) na mahitaji mengi zaidi ya mifumo ya usimamizi yameongezwa. Muundo wa ISO unafanana na ule wa ISO 9001 ( Mfumo wa usimamizii wa ubora,), kwa hiyo unakuwa rahisi kupatana na mifumo mingine ya usimamizi. Utayarishaji wa ISO ulikuwa kwa kuamini kuwa mifumo mahiri ya chakula ilikuwa imeshaundwa, inatekelezwa na mara kwa mara inaboreshwa kufuatana na mfumo wa usimamizi uliopo. Kwa hiyo ISO ina baadhi ya mahitaji ya mfumo wa usimamizi ambao haukuainishwa bayana ndani ya HACCP ya Kodeksi. Hizi zinajumuisha sera ya usalama wa chakula na malengo husika, Kupanga na kuweka kumbukumbu za mfumo wa usalama wa chakula, taratibu nzuri za mawasiliano ya ndani na nje, upangaji wa majukumu kwa kiongozi timu ya usalama wa chakula, ukaguzi wa ndani, rejea ya usimamizi, kuendelea kuboresha na kuupa upya FSMS. Kwa kifupi mahitaji ya ISO ni ujumuishi wa vipengele muhimu vinne vifuatavyo: Mwingiliano wa mawasiliano Usimamizi wa mfumo Programu za masharti ya awali Misingi ya HACCP. HACCP ya Kodeksi inatumia kipengele cha mwisho (nne) (misingi ya HACCP ilifafanuliwa katika swali 42) na inapendekeza pia programu za awali zinazohusu usafi wa chakula (angalia swali 43) ziwe tayari zinatekelezwa kabla ya kuandaa mpango wa HACCP. ISO ikiwa imeungwa mkono na jumuyia ya kimataifa, inasawazisha mahitaji ya kuweza kuusimamia mfumo wa usalama wa mnyororo wa chakula, na unatoa fursa ya kipekee ya kuwa na utaratibu mzuri kiulimwengu. ISO walishirikiana kwa karibu sana na CAC katika kuandaa viwango hivi. ISO imerejelea kwa kiasi kikubwa mapendekezo afya(usafi) ya Kodeksi katika kutayarisha programu za masharti ya awali kwa ajili ya sekta mbalimbali za tasnia ya chakula. Katika kiambatisho B cha ISO 22000, kuna ulinganisho wa mahitaji mbalimbali ya FSMS na ile ya HACCP ya Kodeksi.!SO imebuniwa ili kuwezesha mashirika mbalimbali katika mnyororo wa chakula kutekeleza mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula. Inajumuisha wazalishaji mazao, wazalishaji wa chakula cha wanyama, wazalishaji wa msingi, wasindikaji vyakula, wasafirishaji na wenye maghala, wauza rejareja, watoa huduma za chakula, wachukuzi wa vyakula na mashirika kama ya watengenezaji wa vyombo na mashine za chakula, vifungashio, watu wa usafi, vingio na viambato vinavyohitajika wakati wa usindikaji wa chakula. Kwa kuwa HACCP ya Kodeksi ni nyaraka ya mwongozo, huwezi kuhakikiwa nayo. Lakini kuna nchi nyingi ambazo zina viwango vya kitaifa vilivyoandaliwa kwa misingi ya HACCP ya Kodeksi; ambayo unaweza kuhakikiwa nayo. Nchi hizo ni kama Australia, Denmark, Ujerumani, India, Ireland, na Marekani. Kadhalika nchi ya Uholanzi wana viwango vinavojulikana zaidi kama Dutch HACCP, hiki nacho unaweza kupata uhakiki kwa kukitumia. Kutokana na kupatanisha (havibadiliki kutokana na nchi, bidhaa au huduma husika) viwango mbalimbali vya HACCP duniani kwa misingi HACCP ya Kodeksi mashirika mengi duniani huona rahisi kutekeleza ISO ISO inaweza kutumiwa kwa uhakiki, na inaweza kukubalika kama mbadala wa uhakiki kupitia viwango vya kitaifa. Jedwali lifatalo linalinganisha ISO na HACCP ya Kodeksi.

136 126 Mifumo Ya Usimamizi Ulinganishi wa iso na haccp ISO Viwango vya kimataifa vilivyoandaliwa na ISO pamoja na ushiriki wa wadau mbalimbali; toleo la kwanza lilikuwa 1 Septemba Imekubalika na nchi nyingi kama viwango vya kitaifa na nakala halisi na za kielekitroniki zinaweza kununuliwa kutoka ISO ( au mashirika ya viwango ya kitaifa. Imeandikwa katika mfumo wa viwango vya mfumo wa usimamizi vyenye mahitaji ya kukaguliwa; mwongozo wa matumizi yake umechapishwa pekee kama ISO/TS Viwango vinaweza kutumiwa na mashirika katika mnyororo wa chakula-wazalishaji wa chakula. Wasindikaji wa chakula, wasafirishaji na wenye maghala, wauza rejareja na watoa huduma za chakula, mashirika husika kama wazalishaji wa vyombo/mashine, vifungashio, vifaa vya kuasaishia, vigio na viambato, na watoa huduma. Viwango vinajumuisha vipengele vifuatavyo ili kuhakikisha usalama wa chakula katika mnyororo wa Chakula: Mwigiliano wa mawasiliano Usimamizi wa mfumo Programu za mahitaji ya awali (PRPs) Misingi ya HACCP Muundo wa viwango umefungamanishwa na ISO 9001 ( Mahitaji ya QMS) ili kuongeza upatanifu wa viwango hivi viwili. Mashirika yanaweza kutafuta uhakiki wa mifumo yao ya usimamizi wa usalama wa chakula au kutamika wenyewe kuwa wana ulinganifu na ISO Chanzo: S.C Arora, India. HACCP Nyaraka ya mwongozo iliyotayarishwa na Tume ya Kodeksi(Codex Alimentarius Commission); Toleo la kwanza lilikuwa mwaka Kwa kawaida huchukuliwa na mashirika ya kitaifa ya usimamizi kama sehemu ya sheria zake za usalama wa chakula. Hupatika bure kwa kupakuwa kutoka tovuti ya Kodeksi ( Imeandikwa kama maelekezo katika sehemu mbili: misingi 7 ya HACCP na Hatua 12 za kutekeleza hiyo misingi 7. Inaweza kutumika katika mnyororo mzima wa chakula, kuanzia kwa mzalishaji wa msingi mpaka mlaji wa mwisho. HACCP ya Kodeksi inatumia misingi saba ya HACCP na hatua 12 ili kutekeleza hiyo misingi. Kadhalika inatoa mapendekezo kwamba mahitaji ya awali ya usafi wa chakula sharti ya tekelezwe kabla ya uandaaji wa mpango wa HACCP. Hii inapatana na ISO 9001 kwa kiasi Fulani-mfumo wa usimamizi na mwingiliano wa mawasiliano hayakujumuishwa vya kutosha na HACCP ya Kodeksi. Kwa kuwa ni nyaraka ya mwongozo huwezi kuhakikiwa kwake moja kwa moja, lakini uhakiki wa HACCP unawezekana kupitia viwango vya HCCP vya kitaifa, kwa mfano Dutch au Danish HACCP. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management. Jarida hili linatoa maelezo juu ya usalama wa vyakula, sheria za SPS, maelezo ya kimsingi ya usalama wa vyakula ya HACCP, usimamaizi mwema wa usalama wa vyakula katika ISO (FSMS), mahitaji na umuhimu wa FSMS, utekelezaji na udhibitishaji wa FSMS. (page 155) MAREJELEO: Codex Alimentarius Commission. Recommended International Code of Practice General Principles of Food Hygiene (CAC/RCP , Rev ). Freely obtainable from International Organization for Standardization ISO 22000:2005. Food safety management systems Requirements for any organization in the food chain. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO Press Release: ISO for safe food supply chains.

137 Mifumo Ya Usimamizi 127 Comparison of ISO and HACCP 45. Hatua za kutekeleza ISO zikoje? Kabla ya kuanza utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula ISO 22000, ni muhimu viongozi wa juu wa kampuni au shirika lako kujitolea kwa dhati katika kutayarisha na kutekeleza huo mfumo. Hii inajumuisha kutoa rasilimali (fedha, miundombinu na wafanyakazi mahili) kwa ajili ya kuandaa mfumo huo. Hatua katika utekelezaji wa ISO umefafanuliwa hapa chini. Hatua 1: Kuteua timu ya watalaam wa usalama wa chakula (FST) Uongozi wa juu sharti uteue timu yenye wataalam mahili wa usalama wa chakula na kiongozi wao. Inapendekezwa timu iwe na wataalamu wafatao: mtaalamu wa tekinolojia ya chakula, mtaalamu wa vidubini, wasimamizi wa udhibiti wa ubora, mhandisi, mzalishaji na fundi wa matengenezo. Mmoja kati yao ni vyema akawa na elimu/ufahamu mzuri wa HACCP/FSMS. Kama timu itahitaji mafunzo ya ziada, basi yaandaliwe na kiongozi wao. Timu itafanya kazi kubwa katika kujenga mfumo wa menejimwnti ya usalama wa chakula katika shirika lako. Kama ukipenda unaweza kuajiri mshauri wa usalama wa chakula ili kuiongezea nguvu timu (FST), lakini ikumbukwe kuwa huyu atakuwa wa msaada tu siyo kuchukua majukumu ya FST. Hatua 2: Kuweka mahitaji ya awali (Setting up prerequisite programmes (PRPs) Kutegemeana na sehemu ya mnyororo wa chakula ulipo, utahitaji kuweka programu ya mahitaji ya awali, PRPs kwa ajili ya kudumisha mazingira safi ya kitengo. Programu hizi zinajumuisha taratibu nzuri za afya/usafi (GHP), mfumo mzuri wa uzalishaji (GMP), Taratibu nzuri za Kilimo (GAP), Mfumo mzuri wa usambazaji (GDP) (angalia kiambato C cha ISO : 2005). Kama utaona PRPs zako hazitoshelezi, unaweza kuongeza fedha ili kuziendeleza. Kwa mfano, unaweza kutaka kubadili mpangilio wa kiwanda chako na muonekano wake, yaani kuta, sakafu,mfumo wa hewa na taa, na mifereji ya maji pamoja na ukusanyaji na utupaji wa taka. Hatua 3: Kuandaa mpango wa HACCP Kwanza kabisa kabla ya kuandaa mpango wa HACCP inabidi ufanye uchanganuzi wa majanga katika kila hatua ya mchakato (angalia swali 42). Uchanganuzi huu utapelekea kubainisha hatua(vituo) muhimu vya udhibiti (CCPs), hatua ambapo kwa kufanya udhibiti wa mchakato kutakuwa na matokeo ya kupunguza kufikia hali inayokubalika au kuonda kabisa hatari ambazo zingeweza kuleta madhara kwa watumiaji bidhaa. Mfumo wa kufuatilia CCPs na kuchukuwa hatua za marekebisho ikibainika udhibiti wake hauko madhubuti inabidi uwepo kwa bidhaa au mchakato. Mbinu za udhibiti ambazo zitakuwa zimeainishwa katika mpango wa HACCP na programu za PRPs, zihakikiwe (validated) kabla ya kuzitumia. Hatua 4: Kuandaa nyaraka (Kuweka kumbukumbu na ripoti) Nyaraka za FSMS zinajumuisha sera ya usalama wa chakula, miongozo ( kwa mfano taratibu za udhibiti wa nyaraka, utunzaji wa kumbukumbu, ukaguzi, utunzaji wa vitu hatari, udhibiti wa bidhaa zilizozalishwa wakati udhibiti umekiukwa, hatua za kurekebisha na uondoaji wa bidhaa iliyokamilika), mipango ya HACCP, na nyaraka za ziada zinazodhihirisha kuwa mpango wa HACCP ni thabiti na mahitaji mengine ya FSMS. Matumizi ya nyaraka nyinginezo zikijumuisha mtiririko wa uzalishaji, mahtaji halisi, njia za kupima, kumbukumbu, wakati zikihitajika na ziongezwe kwenye furushi la nyaraka zilizoandaliwa na timu. Kuwe na utaratibu mzuri wa kudhibiti utuzaji na matumizi ya nyaraka. Hatua 5: Mafuzo, kuhamasisha uelewa na utekelezaji Wafanyakazi wote wenye sughuli ambazo zina athari kwenye usalama wa chakula, sharti wawe mahiri katika kazi zao. Mafunzo juu ya ufuatiliaji na uchukuaji hatua za kurekebisha wapewe wafanyakazi ambao wanahusika na majukumu hayo. Vilevile, wafanyakazi wako sharti wafahamu maana na umuhimu wa shughuli za usalama wa chakula. Kaadhalika wafahamu umuhimu wa mawasiliano ya ndani kuhusu masuala ya usalama wa chakula. Baada ya mafunzo na ufahamu kuwafikia walengwa kama ilivyotarajiwa, utekelezaji wa mfumo unaweza kuanza na nyaraka zitunzwe kuonyesha kuwa mfumo wa usalama wa chakula (FSMS) unafanya kazi.

138 128 Mifumo Ya Usimamizi Hatua 6: Ukaguzi wa ndani wa FSMS Ukaguzi wa ndani wa mfumo wa usalama wa chakula unabainisha jinsi ya ufanisi wake. Baadhi ya wafanyakazi wako wafundishwe namna ya kufanya ukaguzi wa ndani, pamoja na shughuli zinazo ingiliana. Siku za mwanzo katika utekelezaji wa FSMS, ukaguzi unaweza kufanywa mara kwa mara; baada ya mfumo kukomaa, fanya ukaguzi ama ulivyoelekezwa kwenya mwongozo wa ukaguzi wa ndani. Hatua 7: Thathmini ya usimamizi Matokeo ya ukaguzi wa ndani, pamoja na data za mrejesho wa wateja na malalamiko, uchanganuzi wa matokeo ya shughuli ya kuthibitisha shughuli, mafunzo yaliyopatikana kutokana na dharura au ajili zilizotokea, kma zipo, kuondoa bidhaa, kama zipo nayo inabidi vipitiwe na uongozi wa juu na maamuzi yafanywe kwa kuendeleza FSMS. Mfumo wa kufanya mapitio kama haya ni vema ukawepo. Hatua 8: Uhakiki Kupata uhakiki wa ISO ni wa hiari. Kama uongozi wa juu utaona ni wa muhimu, basi munaweza kuomba kutoka kwa shirika la uhakiki mtakalolichagua. Hitaji la msingi kuhusu hili, ni kuutekeleza mfumo kwa uchache miezi mitatu, na ukaguzi wa ndani mara moja ikifuatiwa na mapitio ya usimamizi. Mpango kazi Kipindi cha miezi sita hadi tisa unakadiriwa kuwa muda wa kutosha kuimarisha utekelezaji wa FSMS. Mfano wa mpango kazi unaonyeshwa kwenye kielelezo kifuatacho. Mpango kazi wa utekelezaji wa ISO Chanzo: S.C. Arora, India.

139 Mifumo Ya Usimamizi 129 KWA TAARIFA ZAIDI Blanc, Didier. ISO 22000: kutoka wazo hadi utekelezaji (From intent to implementation). Katika ripoti maalum juu ya mifumo ya usimamizii wa ISO, Mei-Juni Shirika la Kimataifa la Viwango How close is the intent of ISO 22000:2005 to its implementation by users? Mtaamu aliyeshiriki katika usanifu na uandaaji amefanya mapitio ya marejesho kutoka kwa watumiaji wa mwanzo na anatoa mwelekeo wa jinsi ya kutatua masuala waliyoyatoa. Færgemand, Jacob. The ISO series: Global standards for safe food supply chains. In ISO Management Systems. May- June 2006, Special report. International Organization for Standardization. Kuanza rasmi kwa viwango vya ISO mwaka 2005 vilivyotayarishwa na kamati ya kifundi ISO/TC34 (food products) ya bidhaa za chakula, ilikuwa mwanzo wa kuwa na viwango vya kimataifa vyenye lengo la kuhakikisha minyororo salama ya chakula. Makala inatoa mapitio ya kifundi ya viwango mbalimbali katika familia ya viwango vya ISO na jinsi vinavyoweza kutumika. International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management. Gazeti hili linatoa taarifa juu ya usalama wa chakula, sheria za SPS, misingi ya usalma wa chakula ya HACCP, mfumo wa menejimeti ya usalama wa chakula wa ISO 22000, faida na hasara za FSMS, utekelezaji na uhakiki wa FSMS. Smith, David, Rob Politowski and Christina Palmer. Managing Food Safety the Way. BSI Standards, ISBN Kitabu hiki kianatoa msaada wa kirafiki kwa msomaji ili aweze kuelewa na kutekeleza mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula kukidhi mahitaji ya kiwango cha kimataifa cha ISO 22000:2005. Kinatoa njia rahisi, pamoja na nukuu kutoka kwenye kiwango na maelezo kinaganaga ya istilahi zilizotumika. Kitabu hiki kitakuwa cha msaada kwa mashirika ambayo yanataka kuunganisha mfumo wa ISO na mahitaji mengine ya mfumo wa usimamizi. MAREJELEO Shirika la Viwango la Kimataifa ISO 22000:2005, Food safety management systems Requirements for any organization in the food chain. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (angalia orodha kwenye tovuti ISO/TS 22004:2005, Food safety management systems Guidance on the application of ISO 22000:2005. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO (angalia orodha kenye tovuti Shirika la Kimataifa la Viwango na Kituo cha Biashara cha Kimataifa: An easy-to-use checklist for small business. Are you ready? ISBN Inapatikana kwenye tovuti ya ITC ( and ISO (

140 130 Mifumo Ya Usimamizi 46. Je,uhakiki wa HACCP/ISO utafanya shirika langu lidhihirishe kuwa linaulinganifu na sheria za nchi za usalama wa chakula? Kupata uhakiki wa HACCP/ISO ni njia innayofahamika ya kuonyesha kuwa unaulinganifu na, dalili za ufanisi katika utekelezaji wa, mifumo ya kuhakikisha usalama wa chakula. Hata hivyo mamlaka za usimamizi zinaweza kutotambua uhakikiki huu, kama haukuainishwa kwa sheria iliyopo. Kwa kawaida kanuni zinaelezea njia ya tathmini ya ulinganifu, na mamlaka ya usimamizi itakutegemea kwamba utadhihirisha ulinganifu kupitia njia hiyo. Kama kanuni inatamka kuwa uhakiki utakubalika kama njia ya kutathmini ulinganifu, kwa hali hiyo uhakiki utakusaidia kukidhi mahitaji ya kisheria pia. Kukubalika kwa HACCP katika kanuni za kitaifa na kikanda juu ya usalama wa chakula Kama inavyofahamika malengo ya msingi ya sheria ya chakula ni kulinda wateja kutokana na undanganyifu katika uwekaji lebo kwenye bidhaa za vyakula na kuhakikisha vyakula vinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu. Kukubalika matumizi ya misingi ya HACCP na Tume ya Kodeksi Alimentarius (CAC), ambayo ina serikali wanachama 180, ilikuwa maamuzi ya msingi katika kuhamasisha matumizi ya Mfumo wa Uchanganuzi wa Majanga na Utambuzi wa Hatua Kuu za Udhibiti (HACCP -Hazard Analysis and Critical Control Points) katika sheria za udhibiti wa usalama wa chakula. Kwa mfano Canada waliifanya HACCP kuwa ni ya lazima katika tasnia ya usindikaji samaki tangu 1992, ikafatiwa na Marekani kwenye usindikaji wa mazao ya bahari mwaka Vilevile Marekani ilizitaka viwanda vinavyosindika nyama, sharubati ya mboga na matunda kuwa na HACCP ifikapo Januari Sheria za Jumuiya ya Ulaya kuhusu usafi wa vyakula ( iliyoanza rasmi Januari 1, 2006 ; angalia marejeo hapa chini-tume ya Ulaya, 2006) nayo inatamka kuwa biashara zote za chakula ( yaani zinazoshughulika na vyakula kutokana na wanyama, na vile visivyotokana na wanyama na vyakula vyenye mchanganyiko wa viabato kutokana na wanyama au mimea) baada ya uzalishaji wa msingi(shambani), lazima wawe, na kutekeleza na kudumisha utaratibu wenye misingi ya HACCP. Mikataba ya WTO kuhusiana na sheria ya SPS unawataka Wanachama wake kuhimiza misingi na mapendekezo iliyowekwa na Tume ya Kodeksi Alimentarius wakati wa kutunga sheria zao za SPS. Sheria hizi zinahusiana na ulinzi wa binadamu au maisha ya wanyama kutokana na hatari ambazo zinaweza kuletwa na vingio, vichafuzi, sumu au vidubini waletao maradhi katika vyakula. Utekelezaji wa mfumo wa HACCP kama ulivyopendekezwa CAC, kadhalika utakusaidia kuepuka vikwazo vya kifundi vya biashara kuhusiana na usalama wa chakula. Ulinganifu na mahitaji ya kisheria wakati wa kutekeleza ISO Kutekeleza hatua zifuatazo, kama zinavyohitajika na ISO 22000, itawezekana kudhihirisha kwa kiasi ulinganifu na sheria pamoja na kanuni zingine za usalama wa chakula: Wakati shirika lako linachagua na kuweka programu za mahitaji ya awali (PRPs), sharti kuchukulia maanani sheria na kanuni husika. Sheria na kanuni sharti zianishwe kwenye mahitaji halisi ya malighafi, viambato na vitu vinavyogusana na bidhaa. Sheria na kanuni zinazohusu sifa za bidhaa za mwisho (end product) sharti nazo ziainishwe. Wakati unaweka viwango ya kukubalika vya hatari za usalama wa chakula katika bidhaa zako za mwisho, ni vema ukazingatia sheria na kanuni. Mahitaji haya ya kisheria, yazingatiwe pia unapoweka vikomo katika hatua muhimu za udhibiti. Kukubalika kwa ISO minyororo ya rejareja. Wauza bidhaa za vyakula na hasa wa rejareja, wameanza kunpendelea zaidi ukaguzi huru (Third party)wa wagavi na wana nia ya kuachana na ukaguzi wanaoufanya wenyewe kwa wagavi kwa gharama ndogo kupitia uhakiki. Kwa mjibu wa uchunguzi uliofanywa na ISO 2009, mpaka kufikia Desemba 2009, jumla ya vyeti 13, 881 vya ISO vilikuwa vimetolewa kwa nchi 127. Wateja wako wa mahuruji

141 Mifumo Ya Usimamizi 131 wanaweza kuwa wa kwanza kukuuliza kama tayari una uhakiki wa FSMS, kwa maana uhakiki utawadhihirishia kuwa umekidhi sheria za kitaifa na kanuni husika. Mpango wa FSSC 22000, wa kuhakiki mifumo ya usalama wa chakula, una misingi ya ISO 22000:2005 na mahitaji halisi yaliyopo ya wazi (Publicly Available Specification, PAS) ya programu za awali juu ya usalama wa chakula kwa wazalishaji (British Standard PAS 220:2008). FSSC 22000, a certification scheme for food safety systems, is based on ISO 22000:2005 and the Publicly Available Specification (PAS) for prerequisite programmes on food safety for food manufacturing (British Standard PAS 220:2008). FSSC ambacho ni kifupisho cha Food Safety System Certification mpango ambao ulianzishwa na taasisi ya uhakiki wa usalama wa chakula (Foundation for Food Safety Certification). Mpango huu unawahusu wasindikaji au watengeneza wa bidhaa za wanyama, bidhaa za mboga zinazoharibika haraka, bidhaa zinazokaa muda mrefu na viambato vingine vya chakula kama vile vingio, vitamin na bio-cultures. Mpango huu umetabuliwa rasmi na taasisi ya uaslama wa chakula ya dunia (Global Food Safety Initiative (GFSI). Kwa mujibu wa taasisi ya uhakiki na usalama wa chakula, FSSC inasaidiwa na umoja wa wazalishaji wa chakula na vinywaji wa Jumuiya ya Ulaya (Confederation of the Food and Drink Industries of the European Union (CIAA). KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Global Food Safety Initiative. GFSI Guidance Document. Tangu Novemba 2010 GFSI wameainisha mpango 8 ya sekta ya uzalishaji chakula ( ikijumuisha viwango vya kimataifa vya BRC, HACCP ya Kiholanzi na FSSC 22000), mitatu kwa ajili ya uzalishaji wa msingi(primary production) ikijumuisha GLOBALG.A.P na mmoja kwa ajili ya sekta ya msingi na uzalishaji. International Portal on Food Safety, Animal and Plant Health. Inatoa Uwezo wa kupita njia moja kufikia taarifa rasmi za kimataifa na kitaifa kwenye masuala ya usalama wa chakula, na afya ya wanyama na mimea. International Trade Centre. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management. Gazeti hili linatoa taarifa za usalama wa chakula, sheria za SPS, HACCP kwa masuala ya msingi ya usalama wa chakula, mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula ya ISO (FSMS), gharama na faida za utekelezaji na uhakiki wa FSMS. MAREJELEO Waraka wa Mwongozo wa Tume ya Ulaya: Key questions related to import requirements and the new rules on food hygiene and on official food controls. Health & Consumer Protection Directorate-General, Brussels, 5 January Foundation for Food Safety Certification. Founded in 2004 which developed FSSC International Organization for Standardization ISO 22000:2005, Food safety management systems Requirements for any organization in the food chain. Inapatikana kutoka ISO au kwa Wanachama wa ISO; (angalia orodha kenye tovuti Survey of ISO certificates issued as on December International Organization for Standardization and International Trade Centre. ISO Food Safety Management Systems: An easy-to-use checklist for small business. Are you ready? ISBN Inapatikana kutoka tovuti ITC ( and ISO (

142 132 Mifumo Ya Usimamizi 47. Kuna gharama na faida ngani za kupata uhakiki wa ISO 22000? Kuweka mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula, ISO FSMS na kuwa na uhakiki kuna gharama. Gharama hizo ziko katika maeneo yafutayo: Gharama ya kuuweka na kuutekeleza Mfumo( FSMS); Gharama ya kudumisha FSMS; Gharama ya kupata uhakiki mara ya kwanza na kuudumisha. Gharama hizi zinaweza kutofautiana sana kutegemea na ukubwa wa biashara yako, aina ya bidhaa zinazohusika, aina ya shughuli au mchakato, miundombinu na vifaa. Gharama na faida za kutekeleza FSMS zimefafanuliwa hapa chini. Gharama za kuweka na kutekeleza FSMS Gharama za kupata nakala za viwango vya kitaifa na kimataifa na sheria za chakula. Vilevile utahitaji mwongozo wa Kodeksi juu ya kanuni za jumla na misingi halisi ya usafi wa chakula, hata hivyo nyaraka hizi za Kodeksi zinaweza kupakuliwa bila malipo kutoka kwenye tovuti ya Kodeksi. Gharama ya mafunzo ya FST na kiongozi wake itategemea ufahamu wao juu ya majanga ya usalama wa chakula, na vigezo vya kuyadhibiti, uchanganuzi wa majanga, uandaaji wa mpango wa HACCP, njia za kuanzisha nyaraka za FSMS na vigezo vya udhibiti wake. Gharama itajumuisha gharama za moja kwa moja za mafunzo na zisizo za moja kwa moja, yaani muda uliotumiwa kwenye mafunzo na FST, badala ya kazi. Kutakuwa na gharama za kufanya mabadiliko katika mpangilio wa eneo lako, sakafu, kuta, dari, mfumo wa hewa, huduma za wafanyakazi, mfumo wa utupaji taka, mfumo wa kuangamiza wadudu, mfumo wa maji; kutegemea aina ya bidhaa na majanga tarajiwa. Gharama zitakuwepo za kuweka udhibiti zaidi ili kuzuia, kuondosha au kupunguza majanga kufikia hali inayokubalika. Gharama za moja kwa moja zinaweza kuwa za uchakuzi na ununuzi wa vifaa au teknolojia mpya ya uzalishaji; kurekebisha mfumo wa kudhibiti joto wa ghala au stoo ( hasa kwenye majokovu na vyumba vya baridi) za malighafi na bidhaa za mwisho (k.m. zilizokwisha sindikwa); kuweka vifaa vya kutambua uwepo wa metali, vifungashio, upashaji joto/kuchemsha, kugandisha kwenye barafu, uchachuaji, usafirishaji, afya ya wafanyakazi, kama inavyotakiwa; na njia ya kudhibitisha hatuwa zote hizi za udhibiti. Gharama ya uwekaji nyaraka za FSMS, kwa mfano, nyaraka za sera ya usalama wa chakula na malengo, taratibu za usalama wa chakula, programu za awali, programu za msingi wa utekelezaji, mpango wa HACCP. Gharama za kuongeza uelewa wa watu wote wanaohusika/wana majukumu katika shughuli za FSMS na kgharama ya mafunzo kama yatahitajika. Gharama za kila siku za ufuatiliaji, urekebishaji wa vifaa, upimaji wa malighafi na bidhaa, shughuli za uthibitishaji, uondoaji wa bidhaa na hatua/kazi za kurekebisha. Gharama ya kudumisha FSMS Gharama za mafunzo ya mara kwa mara na kuongeza ufahamu wa wafanyakazi sambambamba na mabadiliko katika sekta ( sheria mpya na mabadiko ya FSMS). Gharama za kuwafundisha baadhi ya mameneja wako ili waweze kufaya ukaguzi wa ndani kila baada ya kipindi Fulani. Gharama za ukaguzi wa ndani wa kila baada ya muda Fulani, kufanya marekebisho, maendeleo ya daima na mapitio ya usimamizi wa FSMS.

143 Mifumo Ya Usimamizi 133 Gharama zinazohusisha uhakiki wa mwanzo na gharama za kuudumisha zinazolipwa kwa shirika la uhakiki ulilochagua Ada za usajili au uhakiki zinazolipwa kwa shirika la uhakiki lililoteuliwa kwa miaka mitatu. Ada ya ukaguzi wa mara mbili na wakaguzi wa shirika la uhakiki. Ada ya ukaguzi wa kichunguzi ( unaofanyika kila baada ya miezi 6-12) unaofanywa na wakaguzi wa shirika la uhakiki. Gharama za usafiri na malazi ya wakaguzi wa shirika la uhakiki. Ikumbukwe pia kuwa uhakiki wa ISO sio wa lazima baada ya kutekeleza FSMs. Uamuzi wa kupata uhakiki unategemea mahitaji, na ni jukumu la usimamizi kuamua kabla ya kuingia gharama zilizoelezwa hapo juu. Faida Utekelezaji wa FSMS utaleta faida za ndani na nje. Kwa mfano: Kuongezeka kwa umahiri wa wafanyakazi kutokana na mafunzo na uelekezi wanaoupata unaleta uelewa mzuri wa kazi, kujiamini zaidi na kutambua majukumu yao vyema katika kutekeleza mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula (FSMS). Kutakuwa na mfumo mzuri unaoeleweka wa kupata taarifa kuhusu majanga ya usalama wa chakula yanayojitokeza na udhibiti wake, na juu ya mahitaji ya kanuni na sheria. Kupunguwa kwa gharama kutokana na kupungua matukio ya kuzalisha chakula kisicho salama, kupungua malalamiko ya wateja, kupungua kwa matukio ya kuondosha chakula kibovu kutoka kwenye mnyororo wa ugavi. ulinganifu kwa ISO na uhakiki wake kunaweza kuongeza fursa za biashara mpya, ikijumuisha nafasi ya kuwa mgavi wa upendeleo wa mashirika/maduka makubwa ya rejareja. Wateja watakuwa na imani zaidi kwenye bidhaa zilizozaalishwa na kampuni yenye ulinganifu kwa/ au uhakiki wa ISO KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Færgemand, Jacob. The ISO series: Global standards for safe food supply chains. In ISO Management Systems. May- June 2006, ripoti maalumu. Shirika la kimataifa la Viwango. Uzinduzi wa viwango vya familia ya ISO vilivyoandaliwa na kamati ya kifundi ya ISO/TC 34 ya Bidhaa za Chakula, uliofanyika tarehe 1 Septemba 2005 uliaashiria mwanzo wa kuaminika kwa hatua ya kimataifa ya kuhakikisha usalama wa chakula katika minyororo ya ugavi. makala haya yatoa mapitio ya kifundi juu ya viwango mbalimbali vya familia hii na jisi ya kuvitumia Shirika la Viwango la Kimataifa na Kituo ch Biashara cha Kimataifa. ISO Food Safety Management Systems: An easy-to-use checklist for small business. Are you ready? ISBN Inapatikana kwenye tovuti ya ITC and ISO ( Orodha ya kujipima katika kitabu hiki cha maelezo iko katika sehemu 13, kila moja ikishughulikia eneo moja la ISO 22000, na maelezo mafupi kuhusu mahitaji na maelekezo jinsi ya kuyaingiza mahitaji katika mfumo wa usimamizi ukilenga mahitaji ya kiwanda/shirika fulani. swali 1.5 linatoa taarifa juu ya namna ya kuukubali mfumo wa FSMS. International Portal on Food Safety, Animal and Plant Health: Inatoa Uwezo wa kupita njia moja kufikia taarifa rasmi za kimataifa na kitaifa kwenye masuala ya usalama wa chakula, na afya ya wanyama na mimea.

144 134 Mifumo Ya Usimamizi MAREJELEO Shirika la Viwango la Kimataifa. ISO 22000:2005, Food safety management systems Requirements for any organization in the food chain. Inapatikana ISO au kwa Wanachama wa ISO ( angalia orodha kwenye tovuti Kituo cha Biashara cha Kimataifa. Export Quality Management Bulletin No. 85, An introduction to ISO Food safety management.

145 Mifumo ya usimamizi

146

147 Mifumo ya usimamizi 137 D. MIFUMO MINGINE YA USIMAMIZI 48. Kuna mahitaji gani kufikia ulinganifu na SA 8000 na faida zake kwa biasharanje ni zipi? Kufuatana na mashaka yanayoongezeka katika nchi zilizoendelea kwamba kuna mazingira ya kikatili ya kazi katika nchi zinazoendelea, ulipelekea kutayarishwa kwa kiwango SA 8000 juu ya wajibu kwa jamii (social accountability) mwaka Nia ya kutayarisha kiwango hiki ilikuwa kuwezesha kuandaliwa sheria ya kuhusu taratibu za kazi ili wateja katika nchi zilizoendelea wawe na uhakika kuwa bidhaa wanazonunuahasa nguo, mwanasesere/vikaragosi, vipodozi na bidhaa za elekitroniki zimetengenezwa kwa misingi ya mazingira rafiki (yasiyo katili) ya kazi. Inakisiwa kuwa, takribani watoto milioni 100 duniani kote wako katika ajira kamili (Idara ya kazi ya Marekani, 2010). Wengi wa hawa wako katika mabara ya Afrika, Asia na Amerka ya Kusini. Kufuatana na SA 8000, kampuni hazitakiwi kuajiri watoto au kusaidia ajira yao. Kiwango pia kinaziagiza kampuni kuhakikisha kuwa hakuna mfanyakazi wao yoyote au wale wanaofanya kazi kwa wagavi wao wanakuwa kazini zaidi ya masaa 48 kwa wiki au zaidi ya siku sita kwa juma. Vilevile, ujira unaendana na sheria au siyo chini ya kima cha chini kisekta ; na uwe unatosheleza mahitaji ya msingi ya kujikimu kwa mfanyakazi. SA 8000 iliibuniwa na Social Accountability International (SAI), mshiriki wa Baraza la Vipaumbele vya Kiuchumi (Council on Economic Priorities shirika lisilo la kiserikali ambalo liliasisi masuala ya wajibu wa mashirika kwa jamii). Katika toleo la sasa (2008) SA 8000 ina misingi ya kanuni za makubaliano ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Azimio kuhusu Haki za Binadamu na Mapatano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto (the Universal Declaration of Human Rights and the United Nations Convention on the Rights of the Child). Mfumo wa SA 8000 una mahitaji tisa yafuatayo: 1. Ajira ya Watoto; hapatakiwi kuwa na mfanyakazi wa chini ya miaka 15 (isipokuwa pale sheria husika inatamuka umri mkubwa zaidi) aliyeajiriwa. Kama za nchi husika zimeweka umri wa chini kuwa 14 kufuatana na mambo ya kipekee kwa nchi inayoendelea kama ilivyoainishwa chini ya Mapatano 138 ya ILO, umri huo utaruhusiwa. 2. Ajira ya Lazima; kampuni haitaruhusiwa kumfanyisha mtu yoyote kazi kwa lazima ( kazi kama adhabu), wala wafanyakazi whawatalazima kuweka rehani au vitambulisho wanapoanza kazi. 3. Afya na usalama. Kampuni itatoa mazingira salama na rafiki ya kazi; watachukua hatua kuhakikisha wafanyakazi hawaumii; wawe na utaratibu mzuri wa kuhisi majanga na tishio kwa afya na usalama; watoe huduma za maji ya kunywa na choo, nk. 4. Uhuru wa kushirikiana na utetezi wa pamoja. Kampuni iheshimu haki ya wafanyakazi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi na utetezi wa pamoja; pale sheria imepiga marufuku uhuru huu, kampuni iwasaidie wafanyakazi kuwa na umoja wa kajadili na kuomba haki zao. 5. Ubaguzi. Pasiwe na ubaguzi kwa misingi ya kabila, asili, hadhi, dini, unakotoka, rangi, ulemavu, jinsia, chama cha kisiasa au uhusiano na, umri, akili au matamshi. 6. Saa za kazi. Kampuni itafuata sheria, lakini kwa vyovyote vile wafanyakazi wasifanye kazi zaidi ya saa 48 kwa wiki na siku moja ya kupumuzika katika siku saba za wiki. Saa za kujitolea ya kazi yalipwe kwa ujira stahiki na zisizidi saa 12 kwa wiki. Kama wafanyakazi walikubaliana kwa pamoja kufanya kmasaa ya ziada, basi kwa hali hiyo itakuwa ni lazima. 7. Fidia. Ujira wa kazi ya kawaida kwa wiki lazima ulipwe kufuata sheria na kanuni za sekta na ukidhi mahitaji ya lazima ya wafanyakazi na familia zao. Basiwe na adhabu ya kukata mshahara. 8. Mifumo ya usimamizi. Tasnia zinazo hitaji kupata na kudumisha uhakiki, sharti zifanye zaidi ya kutaka ulingafu na kuoanisha kiwango na mifumo na taratibu zao za usimamizi.

148 138 Mifumo ya usimamizi Uhakiki huru wa SA 8000, ambao kwa kawaida ni wa hiari, hutolewa za mashirika ya uhakiki yenye ithibati na kusimamiwa na Social Accountability Accreditation Services (SAAS). Aina zote za viwanda vinaweza kupata uhakiki wa SA Kufuatana na SAAS kufikia Septemba 2010, tasnia 2330 katika nchi 62 na kujumuisha viwanda 66 walikuwa na uhakiki wa SA Viwanda vingi vyenye uhakiki ni vya sekta ya nguo, vifaa vya ujenzi, kilimo. Ujenzi, kemikali, vipodozi, huduma za usafi na usafirishaji katika nchi kama Brazil, China, India na Italia. Utekelezaji wa SA 8000 unamanufaa kwa wadau wote ukijumuisha wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi. Biashara, walaji, wawekezaji. Wafanyakazi wanaelewa zaidi haki zao za kikazi; vyama vya wafanyakazi wapata Uwezo wa utetezi wa pamoja; biashara zinaweza kuvutia na kubaki na wafanyakazi wazuri. Faida halisi ya biashara zinazouza nje ni kwamba: zitaboresha sifa zake na kujitakasa vyema katika soko, kuwapa uhakika wanunuzi wake katika nchi zilizoendelea kwamba wagavi wao wana mazingira yanayokubalika ya kazi, na kupata fursa za kuungana na minyororo ya wagavi wanaowajibika kwa jamii. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Center for International Private Enterprise/Social Accountability International. From Words to Action: A Business Case for Implementing Workplace Standards Experiences from Key Emerging Markets. Chapisho hili lina mifano mingi ya uchunguzi kifani. Uchunguzi wa China unalenga masuala ya kujenga uwezo, kuimarisha fikira/mtazamo na umiliki wa programu za ulinganishi na wafanyakazi na mameneja ndani ya kiwanda cha nguo. Uchunguzi kifani wa India unamwangalia mtengenezaji wa chuma anayefahamika duniani, unafatilia manufaa ya SA 8000 katika kusimamia wafanyakazi wa mikataba na kampuni ambazo ni wagavi wa hao wafanyakazi wa mkataba, hata katika kampuni yenye historia ya kuwa na taratibu nzuri za kazi. Kifani cha Uturuki unachanganua vichocheo muhimu vya, na matokeo uhakiki wa SA 8000 kwa wafanyakazi, mameneja na wateja wa kiwanda cha nguo. International Institute for Sustainable Development (IISD). Tovuti ya IISD inatoa taarifa zenye manufaa kuhusu maendeleo endelevu na uchunguzi kifani kutoka nchi zingine. Social Accountability International Social Accountability International From Principles to Practice: The Role of SA8000 in Implementing the UN Global Compact. 24 June Chapisho hili linaonyesha washiriki sita wa kampuni zenye ukubwa tofauti, sekta tofauti na kutoka sehemu tofauti dunianiwanaotumia SA 8000 kama nyenzo ya utekelezaji na kutoa ripoti juu ya ahadi zao kutimiza misingi ya kazi (Principles 3-6) ya Compact. SAI and CIPE Case Study. From Words to Action: A Business Case for Implementing Workplace Standards. Chuguzi kifani hizi zinaangalia masuala tofauti ya kuendeleza hali ya sehemu za kazi na kuchanganua faida za kufanya hivyo kwa wafanyakazi na biashara. Stigzelius, Ingrid and Cecilia Mark-Herbert. Tailoring corporate responsibility to suppliers: Managing SA8000 in Indian garment manufacturing. Imechapishwa katika Scandinavian Journal of Management 25, pp. 46/56, Makala haya yanaangalia shabaha ya usimamizi wa pahala husika kutekeleza SA 8000 katika kiwanda cha nguo cha Wahindi. Matokeo katika taaratibu za kibiashara, kuhusiana na vikwanzo na fursa, vimeangaliwa kwa kulinganisha chunguzi kifani, zinazoonyesha kuwa wagavi hutaka bei kubwa au mikataba ya muda mrefu kama hamasa ya kiuchumi kwa utekelezaji. Hata hivyo, mahitaji ya juu ya kukidhi sheria na mahitaji ya kijamii, yanaweza kupelekea upataji wa fursa zaidi za kibiashara, kama vile kupungua kwa wafanyakazi wanaoacha kazi, kuongezeka kwa oda. United Nations Economic and Social Commission for Asia and the Pacific. Linking Sustainable Business and Export Promotion: Strategies for Exporters in Asia and the Pacific Region. Makala haya yanatoa uzoefu wa nchi mbali mbali katika ukanda wa Asia na Pacific, kupendekeza njia rahisi ya mkakati wa kujenga ujuzi wa pamoja katika kukabiliana kikamilifu na mahitaji ya minyororo ya ugavi. Wang, Huimin. The Influence of SA 8000 Standard on the Export Trade of China. Department of Economics and Trade, Beijing Institute of Economic Management, Beijing , China. Published in Asian Social Science, vol. 4, No. 1, January Makala hay yanaangalia ushawishi unaoletwa na kiwango cha SA 8000 katika biashanje ya China na jinsi Serikali ya nchi hyo itakavyofikira kusaidia tasnia kusimamia na kuimarisha mifumo ya usimamizi na kuzifanya tasnia hizo kuwa na mvuto kwa wanunuzi wa ng ambo. Tasnia zenyewe sharti zikione kiwango hiki katika mtazamo huo.

149 Mifumo ya usimamizi 139 MAREJELEO Social Accountability Accreditation Services. Provides quarterly updated information on SA 8000 certified facility details and summary statistics. Website: Social Accountability International. SA 8000:2008 Standard on Social Accountability. 220 East 23rd Street, Suite 605, New York NY Ripoti ya Idara ya kazi ya Marekani: Over 100 Million Worldwide Are Child Workers. 15 December Inapatikana kwenye tovuti :

150 140 Mifumo ya usimamizi 49. OHSAS ina maana gani na inahusianaje na biashara ya nje? OHSAS kiwango cha uanzishaji na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa afya ya wafanyakazi na usalama kazini. Kinatoa utaratibu wa shirika kuweza kuainisha na kudhibiti mashaka juu ya afya na usalama, kupunguza matukio ya ajali, kuhakikisha ulinganifu na mahitaji ya kisheria, na kuendeleza ufanisi wa afya na usalama kwa ujumla. OHSAS siyo kiwango cha ISO kwa sababu hakikuandaliwa na Shirika hilo. Kiliandaliwa na mashirika matatu ya viwango ya kitaifa (mashirika ya Ireland, Afrika ya Kusini na Uingereza), kwa kushirikiana na mashirika 10 ya uhakiki na wadau wengine. Madhumuni yakiwa kushughulikia pengo ambalo halikuwa na mashirika huru ya uhakiki. Wakati wa kuaanda kiwango hiki, na kwa nia ya kukioanisha na viwango vingine vya mifumo ya usimamizi, waandaaji walizingatia vipengele vilivyomo kwenye ISO 9001, ISO na kanuni za mfumo wa kusimamia afya na usalama kazini zilizochapishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Kiwango hiki kinaweza kutumiwa na tasnia za aina zote (binafsi, umma, wazalishaji, watoa huduma) na zaizi (ndogo, za wastani na kubwa). Kadhalika kinaweza kuhudumia katika mazingira mbalimbali ya kijiografia, kitamaduni na kijamii. OHSAS inashughulikia masuala ya afya na usalama kazini-kwa mfano, katika sehemu yoyote ile ambapo shirika linafanya kazi zake. Afya na usalama kazini inajumuisha wafanyakazi, wenye mikataba binafsi, wateja na raia. Kiwango hiki hakishughuliki na masuala mengine ya afya na usalama kama hali ya afya ya mfanyakazi mwenyewe na maisha yake, usalama wa bidhaa, uhabifu wa vifaa au athari kwa mazingira. OHSAS inajumuisha maeneo muhimu yafuatayo: Mipango ya kuainisha majanga ya OHS, tathmini ya hatari zinazoweza kutokea na jinsi ya kidhibiti; Programu za usimamizi ya OHS; Muundo na uwajibikaji kwa OHS; Mafunzo, uelewa na umahiri; Majadiliano na mawasiliano na wateja; kudhibiti utendaji kuhusiana na OHS; kuwa tayari kukabiliana na dharura za OHS; na Upimaji wa mafanikio, ufuatiliaji na maendeleo ya OHS. Kama ilivyo kwa viwango vingine vya mfumo wa usimamizi, itabidi kufuata hatua zifuatazo katika utekelezaji wake (wa OHSAS 18001): Andaa sera ya OHS na Malengo; Fanya tathmini ya hatari za majanga ya OHS zinazoweza kutokea na kuleta athari kwa OHS; Ainisha aina ya OHS katika shughuli za biashara yako zenye mahitaji ya kisheria/; Ainisha malengo ya OHS na programu zinazohitajika katika kutekeleza malengo hayo; Andaa mwongozo wa OHS pamoja na taratibu za kudhibiti utendaji na nyaraka zingine kwa kufanya mipango madhubuti na udhibiti wa michakato wa OHS; ikijumuisha kumbukumbu zitakazowekwa; Tekeleza mfumo na kufatilia ulinganifu na ufanisi kwa njia ya ukaguzi wa ndani. Baada ya utekelezaji wa mfumo kukomaa, kama unapenda unaweza kuomba uhakiki, kupitia mashirika yenye kibali kati ya yale yanayotoa huduma ya uhakiki wa OHSAS Kufuatana na taarifa ya kikundi cha BSI, kufikia Desemba 2009, jumla ya vyeti 54, 357 ya OHSAS au vinafanana na hivyo vilikuwa vimetolewa na mashirika mbalimbali ya uhakiki. Hatua za kupata uhakiki zinafanana na zile zinazofuatwa kwa mifumo ya usimamizi kama vile ISO 9001, ISO and ISO Pia ni muhimu kuelewa kuwa, uhakiki wa OHSAS haukuondolei haja ya kukidhi majukumu ya kisheria. Hata hivyo, utakuwezesha kuonyesha kuwa unakidhi mashariti ya kisheria kwa utaratibu Fulani.

151 Mifumo ya usimamizi 141 Kwa kutekeleza OHSAS 18001, utaweza kuwahakikishia wanunuzi wako wa nje kuwa unatimizha masharti ya taratibu za usalama kazini; kwani hupenda kufanya biashara na wagavi wanao-toa mazingira salama ya kazi kwa wafanyakazi wao. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: A Practical Guide to Construction Site Safety Management. June Jointly developed by The Real Estate Developers Association of Hong Kong and the Hong Kong Construction Association. Kitabu cha mwongozo kwa wenye mahitaji, kikijumuisha wanakandarasi wanaowasaidia, katika kusimamia usalama na hatari zinazoweza kuleta madhara kwa afya katika sehemu za ujezi na kukidhi sheria za usalama za Hong Kong (China). Chao, Chin-Jung and others. A Study for Safety and Health Management Problem of Semiconductor Industry in Taiwan. Industrial Health vol. 46. No. 6, 2008, pp Utafiti unaelezea kwa upana masuala menejimenti ya usalama na afya katika tasnia ya semiconductor. European Commission. Safety and Health for New Workers (SHNW). Comparative analysis of the training experiences in labour prevention risks. Utangulizi juu ya afya na usalama kazini (OHS), maagizo na mikakati nchi za Ulaya, na ufafanuzi wa ukweli kuhusu OHS za kitaifa. Shirika la Kazi la Duniani. Guidelines on Occupational Safety and Health Management Systems (ILO-OSH 2001) Mwongozo kamili wa kurasa nne juu ya ILO-OSH International Register of Certified Auditors. Safety in numbers. Ulinganisho kati ya matumizi ya ISO 9001 na OHHSAS 18001, na SMEs. OHSAS 18002:2007, Occupational health and safety management systems Guidelines for the implementation of OHSAS The OHSAS Project Group Secretariat, c/o British Standards Institution. Kiwango hiki kinaweza kununuliwa kutoka BSI. Barua pepe: cservices@bsigroup.com, website: Kiwango hiki kinaweza kuchukuliwa na kutumiwa na shirika lolote linalopenda kutekeleza taratibu za kawaida kupunguza matukio ya hatari yanayohusiana na afya na usalama katika mazingira ya kazi ya wafanyakazi, wateja na jamii kwa ujumla. MAREJELEO OHSAS 18001:2007, Occupational health and safety management systems Requirements. The OHSAS Project Group Secretariat, c/o British Standards Institution This standard can be purchased from BSI. cservices@bsigroup.com

152 142 Mifumo ya usimamizi 50. WRAP ni nini na inahusika na sekta zipi za viwanda? Katika miaka ya mwisho wa 1990s, Chama cha nguo na viatu cha Marekani (American Apparel and Footwear Association (AAFA) kililipia utafiti wa miaka mitatu kuangalia hali ya ufanyaji kazi katika viwanda vinavyotengeneza bidhaa zilizoshonwa duniani kote. Utafiti huu ulipelekea kuazishwa kwa programu ambaayo baadaye ikaitwa WRAP (Worldwide Responsible Accredited Production)-uzalishaji wa uhakika na ithibati ulimwenguni kote. Lengo lilikuwa kuhamasisha na uhakiki wa kisheria, wa kibinadamu na uizalishaji wa kimaadili katika sekta za nguo, viatu na bidhaa zingine zilizoshonwa. Kadhalika inajumuisha viwanda vingine ambavyo vina nguvu kazi kubwa kama vile katika sekta za hoteli na ujenzi, na zile zinazotengeneza mapambo na vito vya dhamani, samani, chakula, vifaa ya majumbani, vyombo vya kulia, glasi, mazulia na vitambaa, taa na bidhaa zinginezo duniani kote. WRAP ni nembo/alama ya biashara ya shirika la kimataifa lisilo la faida na binafsi na husimamia programu ya uhakiki. Misingi ya WRAP Misingi 12 ya WRAP iliyoorodheshwa hapa chini inatokana misingi inayokubalika duniani kote ya viwango sehemu ya kazi, sheria za ndani na kanuni za sehemu ya kazi. Zinajumuisha usimamizi wa rasilimali watu, usalama na afya, shughuli za mazingira, na ulinganifu wa kisheria ukijumuisha ulinganifu na maduhuli, mahuruji na sheria za forodha na viwango vya ulinzi. 1. Ulinganifu kwa sheria na kanuni za sehemu ya kazi. Tasnia zitakidhi mahitaji ya sheria na kanuni za sehemu ya kazi, popote pale wanapofanyia shughuli zao. 2. Marufuku ya kazi za kulazimishwa. Tasnia hazitatumia wafanyakazi wa kulazimisha. 3. Marufuku kazi kwa watoto. Tasnia hazitaajiri watoto chini ya umri wa miaka 14 au chini ya umri ulioruhusiwa kisheria. Aidha hawataruhusiwa kuajiri wanafunzi kwa mujibu wa sheria. 4. Marufuku kuwaonea/kugandamiza wafanyakazi. Tasnia watatoa mazingira rafiki ya kazi bila unyanyasaji wa aina yoyote ile, kati ya wasimamizi na wafanyakazi au kati ya wafanyakazi wenyewe. 5. Kulipa fidia na stahili za kikazi. Tasnia zitalipa kikamilifu ujira kadiri sheria au kanuni za kazi zinavyosema. 6. Saa za kazi. Saa za kazi, na siku za kazi kila wiki hazitazidi viwango vilivyoainishwa kisheria. Tasnia zitatoa angalau siku moja ya mapumziko kwa wiki ya siku saba, ila tu pale panapokuwa na dharura ya kikazi. 7. Marufuku ya ubaguzi. Tasnia zitawaajiri, zitawalipa, pandisha cheo na kuachisha wafanyakazi kwa misingi ya Uwezo wa kufanya kazi, kuliko sababu zingine binafsi au za kishirikina. 8. Afya na usalama. Tasnia zinawajibika kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya kazi yanayoleta usalama na afya mahali pa kazi. Pale palipo na nyumba za wafanyazi mahali pa kazi lazima afya na usalama wao uzingatiwe. 9. Uhuru wa kujumuika/kujiunga na kuwa na majadiliano au utetezi wa pamoja. Tasnia sharti ziheshimu haki za wafakazi kujiunga, kujadiliana/utetezi wa pamoja uliopo kisheria. 10. Environment. Tasnia zitaheshimu kufuata sheria za mazingira na viwango/kanuni zilizopo; popote wanapofanyia shughuli zao. 11. Ulinganifu na Forodha. Tasnia zitakidhi sheria za forodha, na hasa, watajiwekea taraibu ambazo zitahakikisha wanakidhi sheria za forodha zilizopo na zinazohusu usafirishaji wa bidhaa zilizo tayari bila kibali.

153 Mifumo ya usimamizi Usalama. Tasnia zinatakiwa kudumisha taratibu za ulinzi kujikinga na udanganyifu wa kuweka bidhaa ambazo hazikuorodheshwa/kukaguliwa katika mizigo ya kusafirisha nje (yaani madawa, baruti, bidhaa gushi na majanga ya kibiolojia). Uhakiki wa WRAP WRAP walikubali kutumia mfumo wa usimamizi kuhusu ulinganifu. Kwa hali hiyo inawahitaji viongozi wandamizi wa WRAP kudhibitisha kukubali kwao misingi ya WRAP kwa maandishi, kuteua wafanyakazi wanaotakiwa kuhakikisha taratibu za utekelezaji katika shughuli au tasnia nzima zinafanywa; na kuweka ukaguzi wa ndani kuhakikisha kunakuwa na ulinganifu endelevu. Tasinia sharti zijichunguze kwa kina na kukaguliwa na shirika huru la tathmini. WRAP inahakiki shughuli na siyo nembo au biashara. Tangu 2006, wamekuwa wakitoa uhakiki wa shughuli katika madaraja matatu. Cheti cha Platinum ni cha miaka miwili, hutolewa kwa shughuli ambayo imekidhi misingi yote ya WRAP kwa miaka mitatu mfurulizo na kufaulu ukaguzi bila kuwa na mahitaji ya kufanya masahihisho. Shughuli inaweza kukaguliwa bila taarifa katika hicho kipindi cha miaka miwili. Cheti cha Dhahabu ni cha mwaka mmoja na hutolewa kwa shughuli ambayo imedhihirisha ulinganifu kamili na misingi ya WRAP; na Cheti cha Fedha ni cha miezi sita, na hutolewa kwa shughuli iliyoonyesha ulinganifu wa kuridhisha na misingi ya WRAP, lakini kuna kasoro ndogo ndogo katika taratibu au mafunzo yanahitajia kuzitatua. Kwa miaka uhakiki wa WRAP umekuwa ukihitajika kati ya wanunuzi katika nchi zilizoendelea ambao wataka kupata uhakika kuwa shughuli/tasnia katika nchi zinzaoendelea zinafuata maadili katika shughuli zake. Katika nchi ya Bangladesh zaidi ya shughuli 140 zinazoshughulikia nguo na bidhaa zilizoshonwa kwa ajili ya masoko ya ng ambo zimepata uhakiki wa WRAP. KWA TARIFA ZAIDI Das, Subatra. Case Studies on Social Compliance issues in the apparel sector of Bangladesh. Hili linashughulikia suala la uwajibikaji kwa jamii nakanuni za kufuata katika tasnia za nguo. Worldwide Responsible Accredited Production (WRAP). Pamoja na taarifa kuhusu madhumuni ya WRAP, misingi na taratibu, tovuti hii ina miongozo na fomu kwa ajili ya viwanda vinavyopenda kujiunga na uhakiki wa WRAP, pia kuna fomu za mashirika ya ufuatiliaji kwa wanaotaka ithihati ya WRAP. MAREJELEO WRAP Certification programme. Available free of cost from Worldwide Responsible Accredited Production Wilson Boulevard Suite 601, Arlington, VA 22201, United States.

154 144 Mifumo ya usimamizi 51. Viwango vingine vya mifumo ya usimamizi ni vipi? Kwa kuongezea kwenye viwango vingine vya mifumo ya usimamizi wa ISO kama vile ISO 9001 (tazama swali namba 29), matoleo maalum ya sekta ya viwango vya ISO 9001 (tazama swali namba 30), ISO (tazama swali namba 38), ISO (tazama swali namba 44), na viwango vingine vya mifumo ya usimamizi kama vile taaluma ya afya na usalama (tazama swali namba 49), uwajibikaji wa kijamii (swali namba 48) na WRAP (swali namba 50), kuna viwango vingine vya nyongeza vya mifumo ya usimamizi unayoweza kuzingatia kutegemeana na aina yako ya biashara. 1. Viwango vya ISO Mfululizo wa viwango vya ISO/IEC Mifumo ya habari ya usimamizi wa usalama [ISO s information security management systems (ISMS] ni mfumo wa utaratibu wa kusimamia taarifa nyeti za kampuni ili zibaki kuwa salama. Inajumuisha watu, michakato na mifumo ya teknolojia ya habari (IT). Inazidi kuwa muhimu zaidi kuanzisha mfumo wa usimamizi wa kuzuia ukiukaji/uvujaji wa rekodi za kiusalama au data kwenye vyombo vya habari na mitandao (kama vile data za miundo, shughuli za kibenki, biashara za hisa). Mfululizo wa ISO/IEC/27000 ni pamoja ISO/IEC 27001:2005 teknolojia ya habari mbinu za usalama Mifumo ya habari ya usimamizi wa usalama, Mahitaji ambayo ni viwango vilivyothibitishwa. Mfululizo unatoa muongozo bora wa utendaji, utekelezaji, ukaguzi na uthibitishaji wa mfumo wa habari za usimamizi wa usalama ili kulinda siri, uadilifu na upatikanaji wa habari. ISO/IEC viwango vya kimataifa vya usimamizi wa huduma za IT Viwango hivi vimechapishwa katika sehemu mbili. ISO/IEC :2005 teknolojia ya habari usimamizi wa huduma Sehemu ya kwanza: Vipimo ni vipimo rasmi na vinafafanua mahitaji kwa ajili ya shirika kuweza kutoa huduma zenye viwango vyenye kukubalika kwa wateja wake. ISO/IEC :2005 teknolojia ya habari usimamizi wa huduma Sehemu ya 2: Kanuni za utendaji inafafanua utendaji bora wa michakato ya usimamizi wa huduma katika wigo/eneo la ISO/IEC Kanuni za utendaji ni maalum kwa mashirika yanayojiandaa kukaguliwa dhidi ya ISO/IEC au yanayopanga kuboresha huduma. Viwango vinaweza kutumiwa na shirika lolote ambalo linatumia huduma za IT. Watumiaji wanaohusika ni pamoja na idara za IT za ndani, zinazotoa huduma kwa idara nyingine za kampuni zao na mashirika ambayo yanafanya kazi zake za IT nje. ISO mfululizo wa viwango vya mifumo ya usimamizi wa usalama wa msururu wa usambazaji Mfululizo wa viwango vya kimataifa vya ISO vinaweka bayana mahitaji ya mfumo wa usimamizi wa usalama ili kuhakikisha usalama katika mlolongo wa usambazaji. Viwango vinashughulikia masuala mazito ya usalama kwenye hatua zote za mchakato wa usambazaji; kwahiyo vinalenga vitisho kama vile ugaidi, udanganyifu na uharamia. Mifumo ya usimamizi wa usalama ISO 28001:2007 Utendaji bora kwa ajili ya utekelezaji wa usalama wa msururu wa usambazaji, tathmini na mipango Mahitaji ni mahitaji na viwango vya muongozo ambavyo vinaweza kutumika kwa ajili ya uthibitisho na mashirika ya ukubwa wowote yanayojihusisha katika uzalishaji, huduma, uhifadhi au usafirishaji wa anga, reli, barabara na bahari katika hatua yoyote ya mchakato wa uzalishaji au usambazaji. Viwango vinaweza kutumika kwenye meli zote, bila kujali ukubwa, aina, lengo na kama inaendeshwa kimataifa, kitaifa au katika eneo la bahari linalohusika na nchi husika. Hivyo ndivyo hufanyika katika makundi mengine yote usafirishaji katika msururu wa usambazaji. ISO mifumo ya usimamizi wa nishati ISO 5001:2011 Mifumo ya usimamizi wa nishati Mahitaji na muongozo wa matumizi ulitolewa mwaka Lengo lake ni kuwezesha mashirika ya aina yote na ukubwa wowote kuanzisha mifumo na michakato muhimu ya kuboresha utendaji wa nishati, ikijumuisha uthabiti wa nishati na utumiaji wake. Utekelezaji utapelekea mapungufu ya uzalishaji wa gesi chafu na athari nyinginezo za mazingira. Vilevile itasababisha pia kupungua kwa gharama za nishati kupitia utaratibu wa usimamizi wa nishati. Neno nishati katika

155 Mifumo ya usimamizi 145 viwango linashughulika na umeme, mafuta, mvuke, joto, hewa iliyogandamizwa, na vinginevyo kama vyombo vya habari. Viwango vina hatua ya juu sana ya utengamano pamoja na ISO 9001 na ISO Viwango vingine muhimu Mkakati wa Eco-simamizi na ukaguzi [Eco-Management and Audit Scheme (EMAS)] EMAS ni Eco-simamizi ya Ulaya na mpango wa ukaguzi. Kanuni No 1221/2009 ya tarehe 25/11/2009 kuhusu ushiriki wa hiari wa mashirika katika jumuiya ya eco-simamizi na mpango wa ukaguzi. (EMAS). Mpango unalenga kampuni na mashirika mengine yanayonuia kufanya tathmini, kusimamia na kufanya maboresho endelevu katika utendaji wao wa mazingira. Mfumo umeanza kutumika tangu mwaka Unashirikisha mfumo wa usimamizi wa mazingira ndani yake pamoja na EN/ISO Mashirika ambayo yana ISO EMS iliyothibitishwa, yanaweza kuendelea na usajili wa EMAS kwa kushirikisha mambo mengine ya nyongeza. EMAS III ilianza kufanya kazi tarehe 11/1/2010. Toleo hili limeanzisha utumiaji wa mradi na kuimarisha sura na mafanikio ya EMAS. Kwa mfano, EMAS inaimarishwa kwa uanzishaji wa viashiria vya msingi vya mazingiira, dhidi ya ambavyo utendaji wa mazingira umeweza kuwekwa kumbukumbu. Ushiriki katika EMAS ni wa hiari na upo wazi kwa mashirika ya umma au binafsi yanayofanya kazi katika umoja wa nchi za Ulaya na Eneo la kiuchumi la Ulaya [European Union and the European Economic Area (EEA)]-Iceland, Liechtenstein na Norway. Idadi kubwa ya nchi pia inatekeleza mkakati kama maandalizi ya kutawazwa kuingia EU. EMAS III inawezesha usajili wa mradi kufanyika hata kwa mashirika na maeneo yaliyoko nje ya EU na EEA. Sheria ya kimataifa ya usimamizi wa usalama-international Safety Management (ISM) Code Sheria ya ISM, iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la bahari [International Maritime Organization (IMO)] na kufanywa kuwa ya lazima chini ya Mkataba wa kimataifa wa usalama wa maisha katika bahari (International Convention for the Safety of Life at Sea), inatoa viwango vya kimataifa kwa ajili ya usimamizi wa salama na ushughulikaji wa meli; pia inashughulika na uzuiaji wa uchafuzi wa mazingira. Kusudi la sheria ya ISM ni: Kuhakikisha usalama katika bahari; Kuzuia madhara kwa binadamu au upotezaji wa maisha; na Kuepuka uharibifu wa mazingira na kwenye meli. Ili kuoana na sheria ya ISM, kila daraja la meli lazima liwe na mfumo wa usimamizi wa usalama kazini (SMS). Sheria pia inaweka mfumo wa mpango wa lazima wa matengenezo, ambao kwa kupitia hivyo vyombo ni lazima vitengenezwe katika muda maalum. Kila ISM-meli yenye kulaumiwa, inakaguliwa mara kwa mara na jumuiya iliyoainishwa ili kuangalia ufanisi wa SMS (usimamizi) wake. Pale tu jumuiya iliyoainishwa inapothibitisha kwamba SMS inafanya kazi na inatekelezwa ipasavyo, meli inapatiwa cheti cha usimamizi salama. Ofisi ya Marekani ya Usafirishaji (The American Bureau of Shipping) ni mfano wa jumuiya iliyoainishwa. Mpango wa kimataifa wa usalama wa chakula-global Food Safety Initiative (GFSI) Mchakato wa uwekaji vigezo wa GFSI umeboreshwa kwa msingi wa mahitaji ya kimataifa yaliyokubalika kwa ajili ya usalama wa chakula, utendaji bora wa viwanda na sayansi imara na kupitia mchakato wa ujenzi wa makubaliano ya wadau wakuu katika msururu wa usambazaji wa chakula. Mahitaji yanaweza kupatikana katika nyaraka za muongozo wa GFSI, ambazo zinapatikana bure kwenye tovuti zao. GFSI inashughulikiwa na jukwaa la bidhaa za wateja (Consumer Goods Forum), mtandao huru pekee wa kimataifa kwa ajili ya wachuuzi wa bidhaa za wateja na watengenezaji duniani. GFSI imeweka alama mwezi wa , miradi nane ya sekta za uzalishaji, ikijumuisha BRC Global Standards, Dutch HACCP na FSSC Pia imeweka alama miradi mitatu ya uzalishaji wa mwanzo (pamoja na GLOBALG.A.P.) na mmoja wa sekta ya msingi. Maelezo mafupi ya miradi mitatu kati ya ile iliyowekwa alama na GFSI imetolewa chini.

156 146 Mifumo ya usimamizi Msingi wa uthibitisho wa usalama wa chakula-foundation for Food Safety Certification: FSSC Mradi wa FSSC ulianzishwa na msingi wa uthibitisho wa usalama wa chakula(ffsc) na kusaidiwa na FoodDrinkEurope. FSSC ni mpango wa uthibitisho wa mifumo ya usalama wa chakula juu ya viwango vya usimamizi wa usalama wa chakula ISO 22000:2005 Mahitaji kwa kila shirika katika msururu wa chakula na vipimo vinavyopatikana kwa watu wote [publicly available specification (PAS)] viwango vya British PAS 220:2008 kwa mipango ya masharti juu ya usalama wa chakula kwa ajili ya uzalishaji wa chakula. Viwango vingine vinavyofuata vinalingana na ISO/TS :2009. Mradi unaweza kutumika na wazalishaji ambao wanasindika au kutengeneza bidhaa za wanyama, bidhaa za mboga mboga zinazoharibika haraka, bidhaa zinazokaa/kuhifadhiwa muda mrefu na viungo vya chakula kama viungio, vitamini na viungo asilia yaani bio-cultures. Uthibitisho unapatiwa kibali chini ya viwango vya ISO/IEC Wazalishaji ambao tayari wamethibitishwa na ISO watahitaji tu mapitio ya ziada dhidi ya BS PAS 220 ili kufikia mahitaji ya mpango huu wa uthibitisho. Mpango wa uthibitisho wa FSSC umetambuliwa kikamilifu na mpango wa kimataifa wa usalama wa chakula -Global Food Safety Initiative. GLOBALG.A.P. Viwango vya GLOBALG.A.P. vimetokana na EUREPGAP, viwango ambavyo vimeanzishwa na wachuuzi wakubwa wa chakula Ulaya. GLOBALG.A.P. ni chombo cha sekta binafsi kinachopanga viwango vya hiari kwa ajili ya uthibitisho wa bidhaa za kilimo, ikiwa ni pamoja na bidhaa freshi, mifugo, maua freshi, n.k. duniani kote. Viwango vya msingi vimebuniwa kimsingi kuhakikishia wateja kuwa chakula kinazalishwa kwenye mashamba ambayo yamepunguza athari mbaya za mazingira katika kazi zao kwa kupunguza matumizi ya pembejeo zenye kemikali, na kuhakikisha utaratibu wa uwajibikaji wa kulinda afya na usalama, pamoja na ustawi wa wanyama. GLOBALG.A.P. imejifanya kuwa kielelezo kikuu cha utendaji bora wa kilimo [Good Agricultural Practices (GAP)] katika eneo la soko la kimataifa. GAP imetafsiri mahitaji ya wateja katika uzalishaji wa kilimo katika orodha ya nchi inayoongezeka kwa kasi. Viwango vya kimataifa vya British Retail Consortium (BRC) Viwango vya kimataifa vya BRC vina viwango vinne vya kiufundi ambavyo vinaainisha mahitaji yanayohitajika kutimizwa na shirika kuwezesha uzalishaji, ufungaji, uhifadhi na usambazaji wa chakula salama na bidhaa za wateja. Kiasilia, vilianzishwa kutokana na mahitaji ya wanachama wa Uingereza wa British Retail Consortium, viwango vya kimataifa vya BRC vimepata umaarufu duniani kote na vimeainishwa na idadi kubwa ya wachuuzi na watengenezaji wenye majina katika nchi za Ulaya, Kaskazini mwa Marekani na kanda nyinginezo. Uthibitisho wa mashirika yenye kibali unapatikana kwa ISO iliyotajwa hapo juu na viwango binafsi. Maelezo ya ziada ya mradi/mpango yanaweza kupatikana moja kwa moja kutoka kwenye tovuti za mashirika husika ya uthibitisho. KWA MAELEZO ZAIDI International Organization for Standardization. International standards and private standards. A freely downloadable brochure. Kipeperushi kinachofafanua tofauti kati ya viwango vya kimataifa vya aina iliyoboreshwa na mfumo wa ISO, kwa kutumia kanuni na nidhamu zilizoelezewa vizuri na kukubalika, na viwango binafsi vilivyoboreshwa na industry consortia na makundi mengineyo. The Consumer Goods Forum. Jukwaa la bidhaa za wateja -The Consumer Goods Forum (CGF) ni mtandao wa kimataifa, ulio katika misingi ya usawa, unaoendeshwa na wanachama wake. Unaleta pamoja CEOs na menejimenti ya ngazi ya juu ya zaidi ya wachuuzi 650, watengenezaji, watoaji huduma na wadau wengine katika nchi 70 na kuonyesha viwanda mbalimbali katika jiografia, ukubwa, kundi la bidhaa na muundo. British Retail Consortium. Global Standards. MAREJELEO Eco-Management and Audit Scheme.

157 Mifumo ya usimamizi 147 FSSC GLOBALG.A.P. GFSI Guidance Document. International Organization for Standardization ISO 50001: Energy management progresses to Draft International Standard. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 28001:2007, Security management systems for the supply chain Best practices for implementing supply chain security, assessments and plans Requirements and guidance. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO/TS :2009, Prerequisite programmes on food safety Part 1: Food manufacturing. Obtainable from ISO or ISO members (list at International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission ISO/IEC 27001:2005, Information technology Security techniques Information security management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from the IEC or IEC National Committees (list at ISO/IEC : Information technology Service management Part 1: Specification. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from the IEC or IEC National Committees (list at ISO/IEC : Information technology Service management Part 2: Code of practice. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from the IEC or IEC National Committees (list at International Safety Management (ISM) Code.

158 148 Mifumo ya usimamizi E. KUTEKELEZA MIFUMO YA USIMAMIZI 52. Vigezo vipi vya kuzingatia wakati wa kuchagua kiwango cha mfumo wa usimamizi kwa ajili ya kampuni yangu? Vigezo vyako kwa ajili ya kuchagua kiwango cha mfumo wa usimamizi vitategemea yafuatayo. Je, unahitaji mfumo kamili unaolenga kwenye eneo la usimamizi au mfumo wa sekta maalum? Ikiwa unalenga katika mfumo kamili, eneo gani unahitaji kuzingatia: ubora, mazingira, usalama wa taarifa, au mchanganyiko wa haya yote? Ikiwa unahitaji mfumo wa sekta maalum, katika kitengo gani unafanyia kazi: sehemu za gari, vifaa vya matibabu, ubunifu wa programu? Jedwali A hapo chini linatoa maelezo ya mfumo mzima wa viwango vilivyoanzishwa na wote, ISO na sekta binafsi. Jedwali B inatoa taarifa hiyo hiyo kuhusu mifumo ya sekta maalum. Jedwali A Viwango kuhusu mfumo wa menejimenti Madhumuni ya utekelezaji Kiwango Rejea Kupata maridhiano ya mteja kwa kutoa mara kwa mara bidhaa au huduma zinazokidhi viwango Kuhakikisha usalama wa taarifa muhimu za kampuni yako na kujijengea imani kwa wateja katika usalama wa taarifa wanazozitoa Kuonyesha kwa wadau wako kwamba kampuni yako inawajibika kimazingira Kuweka salama eneo la kazi kwa wafanyakazi wako kwa kusimamia taaluma ya afya na usalama katika eneo la kazi Kuhakikisha ustawi wa wafanya kazi wako na kuonyesha tendo la kuendana na sera za uwajibikaji kijamii, taratibu na utendaji wa vyama husika Kuboresha utendaji wa nishati, ikiwa ni pamoja na uthabiti wa nishati na matumizi ya nishati ISO 9001 Angalia swali 29 ISO Angalia swali 51 ISO14001 Angalia swali 38 OHSAS Angalia swali 49 SA 8000 Angalia swali 48 ISO Angalia swali 51 Mifumo ya usimamizi 173 Jedwali B Viwango vya mfumo wa sekta maalum Eneo: Usimamizi wa ubora Madhumuni ya utekelezaji Kiwango Rejea Ili kuwa msambazaji wa kuaminika wa vifaa vya uzalishaji wa gari, sehemu na huduma zinazoendana/timiza mahitaji ya OEM Ili kuwa msambazaji wa kuaminika wa vifaa vinavyohitajika kwa usindikaji wa bidhaa zitokanazo na mafuta, mafuta na msururu wa usambazaji wa gesi ISO/TS16949 Angalia swali 30 ISO/TS Angalia swali 30

159 Mifumo ya usimamizi 149 Ili kuwa msambazaji wa kuaminika kwa kampuni yanayohusika katika ubunifu, uzalishaji, ufungaji mitambo na huduma ya vifaa vya matibabu Ili kuwa msambazaji wa kuaminika kwenye msururu wa usambazaji wa vifaa vya ufundi wa vyombo vya anga, nafasi na sekta ya ulinzi. Kuainisha uwezo wako wa kusambaza bidhaa au huduma kwa watoaji huduma ya mawasiliano na wasambazaji wao ISO Angalia swali 30 AS 9100 Angalia swali 30 TL 9000 Angalia swali 30 Ili kuwa msambazaji wa kuaminika wa huduma na programu za kompyuta TickIT Angalia swali 30 Ili kuwa mtoaji wa kuaminika wa huduma za IT ama kwenye kampuni yako mweyewe au kwa mashirika ya nje yanayopokea huduma za nje kutoka kwako ISO/IEC Angalia swali 51 Eneo: Usimamizi wa usalama wa mlolongo wa usambazaji Kupunguza hasara kwa watu na mizigo katika msururu wa usambazaji ISO Angalia swali 51 Eneo: Usimamizi wa mazingira Kutathmini, kuongoza na maboresho endelevu ya utendaji wako wa mazingira ama ndani ya Umoja wa nchi za Ulaya au nje yake Eneo: Usalama wa eneo la kazi EMAS na Kanuni (EC) No. 1221/2009 (EMAS III) Angalia swali 51 Kukuza uhalali, ubinadamu na maadili ya uzalishaji katika viwanda vya mavazi, viatu na ushonaji pamoja na katika sekta nyingine za nguvu kazi kama vile viwanda vya ujenzi na hoteli na sekta za uzalishaji wa vito, samani, chakula, vyombo vya nyumbani, vyombo vitumikavyo kulia mezani, vyombo vya vioo, mazulia na mablanketi madogo na taa. WRAP Angalia swali 50 Kuhakikisha usalama katika bahari, kuzuia madhara kwa binadamu au upotevu wa maisha na kuepuka uharibifu wa mazingira na meli yako. Kanuni ya ISM Angalia swali 51 Eneo: Usalama wa chakula Kuhakikisha kwamba chakula kinachoandaliwa na kampuni yako ni salama kwa matumizi ya binadamu Kuhakikisha usalama wa aina ya vyakula mbalimbali, yaani vile vilivyotengenezwa kutokana na bidhaa za wanyama, bidhaa za mboga mboga zinazowahi kuharibika, bidhaa zinazokaa/kuhifadhiwa kwa muda mrefu na viungo vya chakula kama viungio, vitamini na viungo asilia yaani bio-cultures. Kuhakikisha uzalishaji, ufungaji, uhifadhi na usambazaji wa chakula salama na bidhaa za wateja Mfumo wa usalama wa chakula chini ya misingi ya HACCP FSSC (muunganiko wa ISO na BS PAS 220) Viwango ya Kimataifa vyabrc Angalia swali 42 Angalia swali 51 Angalia swali 51 Kuwahakikishia wateja kwamba chakula kinatengenezwa kwenye shamba lililopunguza athari mbaya za mazingira kwenye shughuli za kilimo, kwa kupunguza matumizi ya pembejeo zenye kemikali na kwamba wanatumia mbinu bora kulinda afya ya wafanyakazi na usalama pamoja na ustawi wa wanyama. GLOBALG.A.P. Angalia swali 51 Chanzo: S.C. Arora, India.

160 150 Mifumo ya usimamizi Kama unapenda kuwa na mfumo kamili wa usimamizi ambao unaunganisha maeneo kadhaa ya usimamizi, kama vile uhakika wa ubora, usalama wa mazingira na usalama wa taarifa, unaweza kuchagua mifumo sahihi iliyoorodheshwa katika table A. Ikiwa unahitaji mfumo jumuishi lakini ambao ni wa sekta maalum, unaweza kutumia mifumo kadhaa iliyoorodheshwa katika jedwali B. Unaweza kwa mfano, kutumia yote yaani, mfumo wa usalama wa chakula wa ISO na viwango vya kimataifa vya BRC. Mchanganyiko wa mifumo kamili na ya sekta maalum pia inawezekana. Kwa mfano, mtengenezaji wa viungo vya gari anaweza kuunganisha ISO/TS na mfumo wa usimamizi wa mazingira wa ISO (tazama swali namba54). KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Chartered Quality Institute (CQI). Management system standards. Inaeleza kwa kina viwango vya mifumo ya menejimenti ni vipi na jinsi gani vimekua vikitolewa. Standards Australia International (SAI). British Standards Institution (BSI). DNV Certification services. MAREJELEO

161 Mifumo ya usimamizi Nini madhumuni ya ukaguzi wa ndani wa mifumo ya usimamizi na namna gani inafanyika? Pale utakapoanzisha mfumo wa usimamizi, itakuwa ni muhimu kwa wewe kuanzisha hatua ambazo zitaboresha usimamizi wako kama mfumo unatekelezwa ipasavyo. Kuweka mfumo wowote bila kupima kama unafanya kazi kunaweza tu kuwa upotevu wa muda na nguvu. Ukaguzi wa ndani ni moja ya hatua hizo. Ni jambo moja wapo muhimu la viwango vingi vya mfumo wa usimamizi (ISO 9001, ISO 14001, ISO 22000, ISO 27001, OHSAS and others). Ukaguzi unatoa ushahidi katika maeneo yanayohitaji umakini kupunguza, kuondoa, na zaidi sana kuzuia upotevu wa uhakika/makosa katika mfumo. Ukaguzi wa ndani unafanyika kwa moja au zaidi ya madhumuni yafuatayo: Kubainisha kiwango cha mlingano (kuendana) wa mfumo wa usimamizi na vigezo vya ukaguzi vilivyowekwa; Kubainisha ufanisi wa mfumo uliowekwa katika kufikia malengo yaliyoainishwa; na kuwapatia wanaokaguliwa fursa ya kuboresha mfumo wa usimamizi wao. Hutakiwi kutumia ukaguzi katika njia ambayo inapelekea kuhamisha wajibu wa kuchunguza na mchakato wa kurekebisha upotofu kutoka kwa uendeshaji wa wafanyakazi kwenda kwa wakaguzi. Mchakato wa ukaguzi wa ndani kawaida una hatua saba zilizoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao. Hatua za ukaguzi wa ndani Chanzo: S.C. Arora, India. Ufafanuzi zaidi wa hatua za ukaguzi kwenye mchoro hapo juu unatolewa katika jedwali lifuatalo;

162 152 Mifumo ya usimamizi Hatua Hatua 1 Tayarisha ratiba ya mwaka ya ukaguzi. (idadi ya kaguzi zinaweza kuwa nyingi zaidi kwa michakato ya kibiashara na pungufu kwa huduma za msaada.) hakikisha una wakaguzi mahiri na wape mazingira huru ya kufanya kazi yao ya ukaguzi. Hatua 2 Chuguza michakato itakayokagulia, nyaraka zinazohusika na matokeo ya ukaguzi uliopita. Andaa orodha ya vitu vitakavyokaguliwa ukaguzi ukianza. Hatua 3 Fanya ukaguzi siku uliyopanga na kukusanya data kwa kuwauliza maswali wahusika, angalia shughuli zinavyokwenda, kagua nyaraka na kumbukumbu zilizopo. Kadhalika omba uone matokeo ya michakato mbalimbali, k.m. kama malengo yalifikiwa au la na sababu husika. Fanya hivyo kwa kila lengo. Hatua 4 Andaa ripoti ya ukaguzi na ya ulinganifu uliopotoka kama upo, kwenye fomu za kufanyia ukaguzi. Ukiukwaji wowote wa ulinganifu, ujadiliwe na anayekaguliwa na kukubaliana. Hatua 5 Muhusika katika eneo lililokaguliwa sharti achukue hatua za kurekebisha ukiukwaji huo na kuondosha visababishi vyake bila kuchelewa. Hatua 6 Angalia hatua zilizochukuliwa katika hatua ya 5 kama zinatosheleza, kufunga ukiukwaji; vinginevyo vitaendelea kuwepo kwa hatua zaidi. Hatua 7 Tayarisha muhutasari ya matokeo ya ukaguzi na uwezekano wa maboresho ambayo yanaweza kufanywa katika mfumo wa usimamizi na itumike katika kurejea usimamizi. Muhusika Mwakilishi wa usimamizi Mkaguzi Mkaguzi Mkaguzi Msimamizi wa eneo lililokaguliwa na mwakilishi wa usimamizi Mwakilishi wa usimamizi au mkaguzi aliyemteua. Mwakilishi wa wasimamizi Wakati mwingine uthibitisho wa hatua ya 6 hapo juu unaweza kufanywa na mwakilishi wa usimamizi, kwa kutathmini ushaidi wa maandishi kama vile kubadilishwa kwa njia au maelekezo. Kama matokeo ya uthibitishao yaataonyesha kuwa ukiukwaji bado upo, aliyekaguliwa itabidi atafute njia zingine hadi ufumbuzi upatikane. KWA TAARIFA ZAIDI Chartered Quality Institute (CQI). Surviving internal auditing. maelezo mazuri juu ya mchakato wa ukaguzi wa ndani: madhumuni, hatua, upana wake,n.k. International Trade Centre and International Organization for Standardization. ISO 9001 for Small Businesses What to do: Advice from ISO/TC 176, ISBN Obtainable from ISO or ISO members (list at Kitabu hiki kinatoa mwongozo kwa tasnia ndogo juu ya utayarishaji na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi kwa misingi ya ISO 9001:2008. Inatoa mifano halisi na ushauri kama utapenda kuwa na mfumo wa usimamizi wa ubora katika shirika/kampuni yako, au kuendeleza mfumo ulionao. Para 8,2,2 ya kitabu hiki inashughulikia ukaguzi wa ndani. MAREJELEO Kituo cha Biashara cha Kimataifa. ISO 9001:2008 Diagnostic Tool.

163 Mifumo ya usimamizi Je, naweza kujumuisha mifumo mbalimali ya usimamizi katika mfumo mmoja wenye uwiano na nitafanyaje? ISO wamekuwa akitayarisha viwango vya kimataifa vya mifumo ya usimamizi tangu mwaka Viwango vya kwanza kutayarishwa vilikuwa familia ya ISO 9000 juu ya mifumo ya menejimenti ya ubora ( sasa hivi iko katika toleo la nne, la mwaka 2008). Hivi vilifatiwa na viwango vya usimamizi wa mazingira ISO (toleo lake la pili lilikuwa 2004), vingine vilikuwa ISO juu ya mifumo ya usimamizi wa usalama wa chakula iliyotoka 2005, ISO/IEC juu ya taarifa za ulinzi ya mwaka 2005, na OHSAS juu ya afya a usalama wa wafanyakazi (katika toleo lake la pili la 2007). Mashirika yalianza kutekeleza mifumo hii mara tu viwango vilipotoka, na kuleta mchanganyiko wa mifumo waliyoitekeleza. Kama kampuni yako inatarajia kutekeleza mifumo hii ina uchaguzi wa aina mbili. Aidha kuitekeleza yote kama mifumo inayojitegemea na kama ndivyo, basi unaweza kuitekeleza kwa mpagilio ufuatao: ISO 9001, ISO 14001, OHSAS 18001, ISO/IEC Na kama huko katika tasnia ya usindikaji chakula, basi unaweza kuanza na HACCP/ISO na kuendelea na mfuatano uliotajwa hapo juu. Kila moja ya mifumo hii ina madhumuni yake (angalia swali 52). Lakini, kama unataka kuwa na mfumo wa uwiano unaojumuisha zaidi ya mfumo mmoja, pia unaweza kufanya hivyo. Kwa mfano ungeweza kuunganisha mfumo ulio nao na mwingine mpya; au unaweza kuanzisha mfumo wa uwiano tangia mwazo, ukipenda kuanza na mfumo zaidi ya mmoja. ISO 9001, ISO na ISO zina muudo unaofanana, kama vile ISO na OHSAS Viwango hivi vyote vina sura zinazoshabihiana kama ifuatavyo: Kwa wote wanaohusika, ukijumuisha mwakilishi wa usimamizi, ufafanuzi wa majukumu na kukasimu madaraka; Usimamizi wa rasilimali; Udhibiti wa nyaraka; Udhibiti wa kumbukumbu; Ukaguzi wa ndani; Hatua za kurekebisha; Hatua za kuzuia; kuendelea kuboresha mfumo; na Kurejea mfumo unaofanywa na usimamizi wa juu kila baada ya muda fulani. Kwa kuwa mfumo unawiana, utairekebisha njia zilizoelezwa hapo juu ili kupuguza idadi ya nyaraka zinazofanana, kupunguza muda na rasilimali zinazohitajika kutekeleza shughuli zinazofanana. Mbinu ya kutayarisha mfumo wa usiamizi wenye uwiano inajumuisha: Kuchagua timu ya wataalamu wenye tofauti na kiongozi wao kufanya kazi ya kutayarisha shughuli kwa ajili ya mfumo wa usimamizi wenye uwiano. kuwa na uelewa mzuri wa yaliyomo kwenye viwango na nia ya kuviunganisha. Kuainisha michakato itakayojumuishwa katika mfumo wa uwiano. Kufanya uchunguzi wa shughuli ambazo matokeo yake yanaweza kuwa na madhara kwa wateja na watumiaji wa mwisho, wafanyakazi, kwenye mazingira na taarifa za ulinzi. Kuanzisha udhibiti na taratibu za ufuatiliaji kwa shughuli zote zenye masuala muhimu. Bainisha muundo wa kuandika nyaraka na kuandaa mpango wa kuwa na nyaraka; ambazo zitajumuisha matamuko ya kisera na malengo, miongozo, mipango ya udhibiti, nyaraka zinazoelezea udhibiti katika utendaji, taratibu za jumla na maelekezo. Muundo wa nyaraka hizi kadhalika uamuliwa. Mafunzo kwa wafanyakazi wote wanaohusika kuhusu wajibu na majukumu yao katika mfumo wa usimamizi wenye uwiano. Baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za juu sharti nao wapate mafunzo ili waweze kufanya ule ukaguzi wa mfumo kila baada ya muda fulani.

164 154 Mifumo ya usimamizi Kufuatia ukiukwaji na kutoka katika mahitaji mahususi. Wakati wowote ikiletwa taarifa ya ukiukwaji wa mahitaji na wateja, wafanyakazi, wakaguzi wa ndani na wadau wengine, anzisha hatua za kurekebisha. Kama wasimamizi wataamua kuwa na uhakiki, basi ni vema kuchagua shirika la uhakiki linalofaa, ambaalo liaweza kuwapatia huduma ya ukaguzi kwa mfumo wa usimamizi wenye uwiano. Kuweza kuelewa upatanishaji wa michakato tofauti, rejea kwenye viwango husika vya ISO; kwa kuwa kila kiwango kinashabihiana na kiwango kingine sana au kidogo. Kwa mfano, majwedali mawili katika kiambatisho A cha ISO 9001 kinaonysha kushabihiana kwake na ISO na vilevile kwa ISO na ISO OHSAS inaonyesha uhusiano wa vipengele vyake na vile vya ISO 9001 na ISO 14001, kadhalika ISO na ISO Vilevile ISO inafafanua kufanana kwake na ISO 9001 na ISO katika kiambatisho chake C. Baadhi ya gharama zinazopugua kwa sababu ya kuunganisha viwango vinatokana na: Kupungua kwa majukumu na muda ambao ungetumiwa na usimamizi wa juu kutoa maelekezo na kufanya rejea ya mfumo. Matumizi bora ya rasilimali (k.m. kuteua wawakilishi wa usimamizi pamoja, matumizi ya mchakato unaofanana wa nyaraka za udhibiti, ukaguzi wa ndani, rejea zinazofanywa na usimamizii). Punguzo la muda na nguvu inayotumika katika uchanganuzi wa chanzo mapungufu na uchukuaji wa hatua za kurekebisha. Gharama za kufanya ukaguzi na mshirika ya uhakiki nazo zitapungua kwa kuwa mashirika haya yanaweza kufanya ukaguzi wa mifumo pamoja. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: British Standards Institution (BSI). PAS 99 Integrated Management: or PAS 99 ni mbinu husishi ya usimamizi inayoegemea mahitaji sita ya mwongozo wa 72 wa ISO. Inakuwezesha kupanga utaratibu wako kuwa yakini na hivyo kuwezesha kutekeleza majukumu yako kwa urahisi. International Organization for Standardization. The integrated use of management system standards. ISBN Obtainable from ISO or ISO members ((list at Kitabu hiki kinatoa maelezo ya mwongozo kwa mashirika kwa jinsi ya kuambatanisha mahitaji ya viwango vya usimamizi vya ISO na viwango vya usimamizi visivyo vya ISO na mfumo wao wa kisasa wa usimamizi. Haiegemei kwa mfumo wowote wa usimamizi ns si maelezo ya lazima. (page 188) Spilka, M., A. Kania and R. Nowosielski. Integration of management systems on the chosen example. Journal of Achievements in Materials and Manufacturing Engineering, vol. 35, issue 2, August Karatasi inaeleza kuhusu athari za kuambatanisha mifumo ya usimamizi. Uambatanishaji unaboresha shirika na kuengeza bidii katika kazi. Zaffora-Reeder, Scot and Doug Stoddart. Integrated Systems for Quality, Occupational Health & Safety, and Environmental Management (One Company s Approach). Published by ASQ. PowerPoint with a good visual presentation on the integrated implementation of ISO and OHSAS MAREJELEO International Organization for Standardization ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 14001:2004, Environmental management systems Requirements with guidance for use. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 22000:2005, Food safety management systems Requirements for any organization in the food chain. Obtainable from ISO or ISO members (list at

165 Mifumo ya usimamizi 155 International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC 27001:2005, Information technology Security techniques Information security management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at OHSAS 18001:2007, Occupational health and safety management systems Requirements. The OHSAS Project Group Secretariat, c/o British Standards Institution This standard can be purchased from BSI.

166

167 TATHMINI YA ULINGANIFU

168

169 Tathmini Ya Ulinganifu 159 A. DHANA YA TAHMINI YA ULINGANIFU 55. Tathmini ya ulinganifu ni nini? Tathmini ya ulinganifu ni msamiati wa ujumla unaohusisha vitu vingi vinavyohitajika kuonyesha kwamba bidhaa au huduma inakidhi matakwa yanayohitajika kiufundi na mengineyo. Kwa ujumla, majaribio, ukaguzi na hati ya uthibitisho/uhakikisho vinachukuliwa kama kiini cha huduma ya tathmini ya ulinganifu (angalia swali namba 59, 65, 68 na 69) na pia vinatumika kipekee au kwa pamoja kulingana na mazingira yanavyohitaji. Majaribio, ukaguzi na hati ya uthibitisho/uhakikisho vinasaidiwa na mfumo wa mita pamoja na alama za vipimo/nyuzi ili kuhakikisha uthabiti wa vipimo(angalia swali namba 79), na kwa kutambuliwa rasmi kuhakikisha ufanisi wa kiufundi wa tathminii ya makubaliano ya watoa huduma(angalia swali namba 88). Tathmini ya ulinganifu inaweza kufanyika kwenye bidhaa, huduma, michakato, mifumo na hata kwa binadamu. Mfumo kamili unaonyeshwa kwa kuchora katika mchoro wa grafu ufuatao. Mfumo wa tathmini ya ulinganifu Chanzo: Martin Kellermann, Afrika ya Kusin.i. Tathmini ya ulinganifu inaweza kutolewa na mtengenezaji- ambapo hii inachukuliwa au itahesabika kama namba moja ya tathmini ya makubaliano au tamko la msambazaji la makubaliano)(angalia swali namba 57). Inaweza pia kufanywa na mnunuzi yaani kundi namba mbili ambapo pia hii ina gharama zaidi kwa kwa

170 160 Tathmini Ya Ulinganifu mnunuzi, kwa hiyo tathmini ya kikundi namba mbili kwa ujumla hufanywa tu na wanunuzi wakubwa katika kuendesha shughuli zao za ukaguzi na majaribio ya miundombinu. Ni njia inayokubalika zaidi na mahususi kwa Wajasiriamali wa Kati na wale Wadogo (SMEs) katika kuendeleza bidhaa au huduma zinazofikia viwango, wanunuzi, walaji, mamlaka za kisheria, Wazalishaji na Mashirika ya Kuhakiki Wagavi, Mamlaka za kuhakiki Maabara za Upimaji, Watoa huduma za Tathmini ya ulinganifu wa Masoko, Mahitaji ya Makubaliano ya Tathmini, Maabara za Taasisi za Kurekebisha vipimo na Mamlaka za kutoa ithibati (vibali). Uchumi- ni utolewaji wa huduma ya tathmini ya ulinganifu na shirika ambalo ni huru/au halihusiani na mnunuzi wala kwa msambazaji. Shirika kama hilo litakua ni kundi nambari tatu la chombo cha tathmini ulinganifu. Kundi nambari tatu la tathmini ya ulinganifu linaweza kuwa la umma au mashirika binafsi. Jambo muhimu ni kuwa mashirika hayo yanatakiwa yawe na uwezo wa kuonyesha ushindani wao kiufundi na kutambuliwa na kukubalika kimataifa na ripoti zao za majaribio (angalia swali namba 60) na vyeti vinatambuliwa na masoko ya nje (angalia swali namba 70 katika kuchagua chombo/bodi ya uthibiti). Ukweli kwamba mtoaji wa huduma ya tathmini makubaliano ni chombo cha serikali yaani shirika la viwango la Taifa au maabara ya serikali, haipelekei kukubalika moja kwa moja kwa ripoti zao za majaribio au vyeti. Zaidi ya hapo, wakati mwingine soko au mamlaka za nje za udhibiti zinaweza zisikubali ripoti zao za majaribio na vyeti hata kama ikiwa zimethibitshwa. Hali kama hii huwa njema kadiri ya siku/ muda unavyokwenda. Kwa nchi zinazoendelea,huduma za ukaguzi, jaribio na uthibitisho mara nyingi hutolewa tu na shirika la taifa la viwango na maabara ya serikali. Hata hiyvo, kuna vyombo vingi binafsi vya ukaguzi, maabara za majaribio na vyombo ya uthibitisho ambavyo vinajiendesha katika eneo la soko. Baadhi yao yaimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani baadhi ya mashirika makubwa ya kimataifa yana ofisi katika nchi zaidi ya 100. Ukaribu wa mtoa huduma, kiwango cha huduma yake, kukubalika kwake katika soko lililolengwa na bei ya huduma zake ni maswala ya kuzingatiwa kwa makini zaidi kwani lengo kuu ni kukaguliwa kwa bidhaa au huduma zako, kupimwa na kupatiwa cheti cha uhakiki na kisha kukubalika popote pale. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Shirika la Viwango la Kimataifa (International Organization for Standardization-ISO) Tathmini ya ulinganifu. Iliyowasilishwa na Sean Mac Curtain. Oktoba, Hiki ni kitini kilichowasilishwa na kinachodadavua tathmini makubaliano na majukumu ya ISO Tathmini ya ulinganifu. Uchambuzi wa kina wa tathmini makubaliano, jinsi inavyofanya kazi, misamiati na maana zake,; maelezo yaliyotolewa na makampuni yote yanayoanza kutafiti uwezekano wa kupata uthibitisho wao au wa bidhaa na wateja ambao wanatafuta ufafanuzi/changamoto za madai mbalimbaliwanayokabiliananazo. Taarifa zinazohusiana na Machapisho. Shirika la Viwango la Kimataifa la Viwango na Kamisheni ya Kimataifa ya Kielektroniki ISO/IEC 17000:2004, Tathmini ya ulinganifu: Misamiati na Kanuni kwa ujumla zinazopatikana kutoka kwa wanachama wa ISO or ISO (imeorodheshwa katika na kutoka Kamitii za Kitaifa za IEC au IEC (imeorodheshwa katika Masuala ya jumla yaliyobainishwa na ufafanuzi kuhusiana na tathmini ya ulinganifu ukijumuisha bodi za vibali juu ya utumiaji wa tathmini ulinganifu. Ufafanuzi wa matumizi ya tathmini ya ulinganifu umejumuishwa kama chombo cha ziada cha kuelewesha watumiaji wa tathmini ya ulinganifu na bodi ya vibali katika mazingira ya kujitolea na mazingira ya kisheria. Shirika la Kimataifa la Vipimo na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Kimataifa. Kujenga Uaminifu Zana ya Tathmini ya ulinganifu Hii inazingatia masuala ya msingi ya tathmini ulinganifu, mbinu, mipango na mifumo, bodi za tathmini makubaliano, namna UNIDO inavyoweza kusaidia kuandaa miundomtika biasharambinu bora,; includes case studies; Kamati ya ISO ya Tathmini ya ulinganifu, ISO/CASCO; kuratibu bodi za vibali na tathmini ya ulinganifu na Makubaliano na Shirika la Biashara la kimataifa ( WTO) katika Vikwazo vya kitaalamu. Shirika la Biashara la Kimataifa. Jarida la Export Quality Management Bulletin No. 77, Maelezo ya tathmini makubaliano katika biashara za kimataifa. Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (United States Agency for International Development), Viwango, Hali ya Hewa, Tathmini Makubaliano na Makubaliano ya TBT. Jarida la kurejea: Yaliyowasilishwa kwa undani katika mada zilizowasilishwa juu. Chanzo kizuri sana katika kuelewesha kwa kina katika hali ya hewa na tathmini makubaliano.

171 Tathmini Ya Ulinganifu Aina gani ya tathmini ulinganifu inahitajika ili kuthibisha kukubalika katika matakwa ya kiufundi/kitaalamu? Mbinu zinazohitajika katika kudadavua tathmini makubaliano hupatikana katika ISO/IEC ambapo hii ndio njia muhimu ya kutatua swali hili. Katika hili kuna njia tatu za kuonyesha kuwa matakwa ya kiufundi yanatoshelezwa: Uchaguzi; Dhamira; na Mapitio na kushudia. Taratibu za kiutendaji katika kutathmini ulinganifu Chanzo: Musingi wake ni ISO/IEC Aina nyingi na mchanganyiko wa tathmini ya makubaliano unaweza kuhitajika ili kuthibitisha kukubaliana na matakwa ya kiufundi/kitaalamu. Changamoto ni kubaini ni aina gani inahitajika. Kutokana na mbinu za kufuata (kama ilivyoonyeshwa katika mchoro awali, juu) tunachagua matakwa ya kiufundi yanayohitajika ili kuonyesha na kubaini kutokana na kukagua, kupima, kukagua na njia nyingine iwapo matakwa ya kiufundi yalifikiwa, matokeo yalipitiwa ili kubaini iwapo matakwa yaliyotajwa yametoshelezwa na yameshuhudiwa (mf. Kuthibitishwa) kwamba matakwa yamefikiwa/yametoshelezwa. Mchakato huu unaweza kutumika iwapo matakwa ya kiufundi yamehitajika na kanuni za kifundi na hatua za SPS (angalia swali la 18 na 19) au wajibu/jukumu la mkataba lililowekwa na wanunuzi maalum (angalia swali la 22), au iwapo makubaliano ynahitajika ilimradi tu kukoleza ushindani wa mgavi. Kwa kuzingatia

172 162 Tathmini Ya Ulinganifu muktadha wa kanuni za kifundi na hatua za SPS; tathmini ya ulinganifu inaweza kushughulikiwa na bodi maalumu za ukaguzi, maabara au mashirika ya kuthibitisha yaliyoteuliwa na mamlaka kama vile bodi za taarifa katika Jumuia ya Ulaya. Katika baadhi ya nchi zina uhakika wa kukubaliana na kanuni za kiufundi na hatua za SPS zinaweza kutolewa na shirika lililoteuliwa, vinginevyo na mashirika ya serikali tu. Iwapo mgavi atatamka kutoshelezwa kwa makubaliano (SDoC), wigo utapanuka zaidi. Mifano imetolewa katika aya ifuatayo chini na katika baadhi ya sehemu za kiongozi hiki. Maelezo zaidi yanatolewa chini juu ya aina za makubaliano yanayohitajika ili kuonyesha kukubaliana dhidi ya kanuni za kiufundi, matakwa ya wanunuzi na matakwa ya soko. Kanuni za Kiufundi (Technical regulations) Chini ya Maelekezo Mapya ya EU, aina ya tathmini makubaliano inayohitajika kwa bidhaa muhimu huwekwa bayana kabisa. Kimsingi michanganyiko minane ya tathmini makubaliano hupatikana kisheria kwa Watungaji/Watengenezaji wa Kanuni. Maelekezo mapya na moduli zake nane za tathmini makubaliano yamejadiliwa kwa undani zaidi katika swali la 58. Hali hiyo hiyo inakubaliana na baadhi ya kanuni za kifundi huko Marekani. Kwa mfano, Kanuni ya Ubora wa Vishikizo (Fastener Quality Act), ambayo inaamua ubora wa vishikizo vyote vinavyouzwa Marekani huhitaji kuvipima/kuvijaribu vishikizo vyote katika maabara zilizopitishwa/zilizopasishwa na kukubalika na Chuo cha Taifa cha Viwango na Teknolojia (NIST) dhidi ya viwango vilivyobainishwa katika orodha ya Kanuni ya Vishikizo. Katika nchi nyingi zinazoendelea kukubaliana na kanuni za kiufundi au viwango vya lazima huonyeshwa na alama ya uthibitisho wa viwango ya Bodi ya Viwango (NSB), kama ilivyo huko Kenya na katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Iwapo mgavi atahitaji alama ya uthibitisho kutoka NSB ili kuonyesha kukubaliana na matakwa ya kanuni za kifundi/kitaalamu. Katika baadhi ya uchumi mbalimbali, alama ya NSB inathibitisha kukubaliana na viwango vya lazima katika bidhaa ijapokuwa alama ya NSB sio ya lazima. Kwa mfano huko Afrika ya Kusini ni jukumu la kampuni za ujenzi kuwapatia wafanyakazi wake mavazi ya usalama yanayokubaliana na kanuni za viwango vya taifa. Kuwa na alama ya Shirika la Viwango ya Afrika ya Kusini (SABS) kunaonyesha kukubaliana na kanuni za usalama. Kuna njia zingine kwa mgavi kuonyesha kukubaliana lakini utumiaji wa alama ya NSB mara kwa mara ni rahisi. Katika baadhi ya nchi mahitaji ya tathmini makubalianao sio hazieleweki kama ilivyoelezewa. Kukubaliana kunaweza kuamuliwa na mamlaka zinazohusika au hata na mkaguzi wa zamu wakati wa kukagua mzigo unaoingia nchini. Matakwa ya Mnunuzi Matakwa ya mnunuzi ni rahisi sana kuyatambua kwani kwa kawaida wanunuzi wanajua sawasawa kile wanachokitaka na kuelezea barabara matakwa yao. Hata hivyo iwapo mgavi anaweza kutoa bidhaa ambayo itaonyesha kukubalika kwake hili litakuwa jambo jingine. Mchakato wakubaini kukubalika ni wazi na unajumuisha kupitishwa kwa usanifu wake, hati ya kupimwa kabla ya kusambazwa kwa vielelezo/sampuli na ufuatiliaji endelevu wa upimaji na uhakiki wakati wote wa usambazaji. Viwango vya kimataifa, kitaifa, binafsi, na hata vilivyochanganywa vinaweza kuainishwa/kujumuishwa na mnunuzi katika mkataba. Wakati mwingine alama ya uthibitisho wa bidhaa unaweza kutolewa kwa upendeleo na mnunuzi. Mifano ya alama hizo ni ULya Umoja wa Maabara kwa bidhaa Fulani tu zilizolengwa kwenda Marekani, alama ya CSA ya Kanada au alama ya IEC kwa uchumi mbalimbali (angalia swali la73) Kwa hiyo mgavi anahitaji kutambua na kuelewa kwa undani zaidi maelezo au masharti ya mkataba yaliyowekwa na mnunuzi. Mahitaji ya Soko (Market requirements) Inaweza kuwa muhimu kuwa na alama ya uthibitisho wa bidhaa katika baadhi ya masoko ili kushawishi watumiaji kuwa bidhaa ni ya ubora wa hali ya juu (angalia swali la 68). Hiki ni kitu maalumu iwapo alama ya biashara bado haijulikani sokoni. Alama ya NSB ya nchi iliyoagiza bidhaa inaweza kuwa inajulikana na kukubalika ambapo alama ya NSB katika nchi inayouza nje inaweza kuwa haijulikani, katika hali hii mgavi

173 Tathmini Ya Ulinganifu 163 itabidi kupata alama ya NSB kwa kila nchi atakayochagua kufanya shughuli nayo. Papo hapo maamuzi haya asifanywe kwa wepesi wepesi tu. Katika masoko yaliyoendelea zaidi, mazingira na uthibitisho wa jamii unaweza kuwa muhimu katika kupenyeza soko (angalia swali la 17). Kwa hali hii baadhi ya masoko yanaweza kukubaliana na uthibitisho utakaokuwa na gharama ndogo zaidi kwa mgavi. Kwa vile kuna aina nyingi za uthiboitisho, uchaguzi wa mwisho utaamuliwa na mgavi. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Shirika la Viwango la Kimataifa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Kimataifa. Kujenga Uaminifu Zana ya Tathmini Makubaliano ya 2010: Hii inajumuisha dhana/mawazo ya msingi ya tathmini Makubaliano kama vile mbinu, taratibu na mifumo, bodi za tathmini makubaliano, jinsi UNIDO inavyoweza kusaidia kuweka. Miundombinu bora, uchunguzi kifani(case study), Kamitii ya ISO ya Tathmini Makubaliano, ISO/CASCO; uratibu wa bodi za kuthibitisha na tathmini makubaliano kati ya Shirika la Biashara la kimataifa juu ya vikwazo yva Kiufundi. MAREJELEO CSA Marks. Kamisheni ya Ulaya.Viwango vya Ulaya: Orodha ya marejeo ya viwango vilivyoridhiwa. Miongozo ya Mbinu Mpya. Fastener Quality Act. International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC 17000:2004, Conformity assessment Vocabulary and general principles. Obtainable from ISO or ISO members (list at SABS Mark Scheme.

174 164 Tathmini Ya Ulinganifu 57. Nini maana ya tamko la mgavi kuhusu ulinganifu (SDoC)? Sehemu hii inadadavua tamko la mgavi kuhusu ulinganifu (SDoC), inaonyesha sehemu kuu zilizopo, inajadili ni wakati gani tamko la makubaliano lianze kutumika, na kuonyesha mahali ambapo SDoC inakubalika. Tamko la Mgavi la ulinganifu Wakati ambapo mgavi anaweka wazi maazimio ya bidhaa, huduma, mifumo ya utawala au bodi kuwa yanafikia matakwa yaliyowekwa ya kiufundi/kitaalamu bila ya ushirikishwaji wa mtu au chombo kingine, hapo tunasema ya kuwa mgavi amezungumzia tamko la makubaliano la SDoC). Maelezo ya uthibitisho binafsi pia husikika lakini msamiati huu ni lazima kuukwepa kwani unapelekea mkanganyiko. Uthibitisho utumike pale tu ambapo mtu/chombo kingine kinajumuishwa. Hii ni dhahiri kwa mgavi iwapo anatumia huduma toka nje ya maabara lakini anatoa tamko la makubaliano kwa niaba yake mwenyewe. Nchi zinazoendelea zinaweza kuwa hatarini kwani soko lipo tayari kukubaliana na mzalishaji mkubwa na anayejulikana sana tu. SDoC ndiyo yenye gharama nafuu zaidi kuonyesha kukubaliana kwani haihitaji mtu mwingine kukagua, kupima na kuthibitisha. Hata hivyo kitu kikubwa kinachoweza kuokoa gharama kinahusishwa na hasara za mauzo kutokana na mtu mwingine kuhitaji muda mwingi wa kuhakiki. Hii imeonyeshwa katika utafiti uliofanywa na Shirika la Uchumi na Maendeleo {Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD) angalia hapo kwa taarifa zaidi} Utumiaji wa SDoC badala ya makubaliano na mtu mwingine (wa tatu) unasababisha kuongezeka kwa biashara. Kutokana na hili ni dhahiri kuwa sio jambo la kushangaza kuona kuwa mgawanyiko wa makundi makuu ya kiwandani kama vile teknolojia na habari (IT) au viwanda vya magari husisitiza matumizi ya SDoC. Viwango vya Kimataifa vya ISO/IEC Sehemu ya 1 na 2kwa undani zaidi huhitaji SDoC. Viwango hivivimekubaliwa na Jumuia ya Ulaya na bodi nyingi za kitaifa. Yaliyomo kwenye SDoC Kulingana na ISO/IEC (angalia/rejea kwa kichwa cha habari kamili), SDoC ni lazima ijumushe taarifa zifuatazo: Jina na anwani ya mgavi; Utambulisho wa bidhaa, mchakato au huduma Taarifa /waraka wa makubaliano: The conformity statement; Nyaraka za kawaida zinazorejezwa (viwango,kanuni za kufundi n.k.); Tarehe na mahali tamko lilipotolewa; na Mweka saini aliyeidhinishwa au watia saini walioidhinishwakwa niaba ya mgavi. Pale ambapo SDoC inakubalika na kuonyesha kukubalika katika kanuni za kiufundi, yaliyomo ndani yake yanaweza kuonyeshwa katika kanuni hizi. Iwapo yaliyomo yanaweza kutofautiana na orodha ya ISO/IEC 17050, orodha ya kanuni zilizopo zitatumika kwa uangalifu sana. Ni wakati gani SDoC hutumika? SDoC kwa ujumla hukubalika iwapo chochote kile au kundi la yeyote yule yatakuwepo: Matakwa ya soko au iruhusiwe tu; Hatari zinazohusishwa na kutokubalika kwa ujumla ni ndogo; Adhabu kwa yasiyokubalika hufanya kazi ya kuzuia/kukataza. nafasi/fursa ya msaada yakinifu iwapo kuna hali ya kutokukubalika; na

175 Tathmini Ya Ulinganifu 165 Idara ya kiwanda ambayo inatumika inawajibika na historia ya kukubalika. Iwapo kuna sheria za kiufundi, SDoC zinakubalika tu iwapo sheria au hatua maalumu zinakubaliana. Vinginevyo matakwa ya kundi la tatu (third party) katika tathmini ya makubaliano ni lazima yakubalike barabara. Mifano ya SDoC zinazotumika kama kanuni zimeonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo. SDoC zinazokubalika kwa matumizi kama kanuni Nchi/eneo Mwaka Aina ya bidhaa Australia/New Zealand Mwisho 1990s Brazil Canada EU 1950s Vifaa vya mawasiliano, komputa na vifaa za pembezoni mwa komputa. Viberiti vya sigara vya kutupa, vifaa vya kufungia mfumo wa gesi asili kwenye magari, chuma cha pua kwa ajili ya kusafilishia nishati. Vifaa vya utangazaji 1971 Magari na sehemu/vipuri vyake 1990s Vifafaa vyenye vya radio vyenye athari ndogo 2002 Vifaa vya vituo vya mawasiliano 1990 mwanasesere /vikaragosi 1992 Vifafaa vya ulinzi binafisi 1993 Bidhaa za tiba (daraja la 1) 1993 Mashine/mitambo 1996 Bidhaa za umeme na elekitroniki 1996 Vifaa vya michezo 1996 Vifaa vya matumizi katika mazingira yenye uwezekano wa milipuko 2000 Vifaa vya pembezoni vya radio na mawasiliano Japan 2004 Baadhi ya vifaa vya radi o na vituo vya mawasiliano Jamhuri ya Korea Chinese Taipei 2002 Marekani 2003 Sekta ya magari/mitambo 2007 Baadhi ya vifaa vya wateja vyenye athari ndogo (47 items) Vitu 19, hasa vipuri na vifuasi vya vifaa ya tekinohama kama vile sehemu au vijimtambo, vikokoteo, na electronic calculators, hard disk drives, storage units and power supplies 1966 Magari na sehemu/vifaa vyake 1999 Komputa na vifaa vyake vya pembezoni 2003 Vifaa katika vituo vya mawasiliano Chanzo cha taarifa hizi: Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (Organisation for Economic Co-operation and Development). MAREJELEO Fliess, B., F. Gonzales and R. Schonfeld. Technical Barriers to Trade: Evaluating the Trade Effects of Supplier s Declaration of Conformity. OECD Trade Policy Working Papers, No. 78. OECD Publishing, International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission ISO/IEC :2004, Conformity assessment Supplier s declaration of conformity Part 1: General requirements, ISO/IEC, Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees ( ISO/IEC :2004, Conformity assessment Supplier s declaration of conformity Part 2: Supporting documentation, ISO/IEC, Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at

176 166 Tathmini Ya Ulinganifu 58. Alama ya CE ni nini na inasaidiaje kuuza nje ya nchi? Sehemu hii itajadili kanuni zinazohusiana na matumizi ya alama CE, maswala ya kukubalika ambayo lazima kuyazingatia, moduli zinazojumuishwa kanuni za kuweka alama CE na mchanganyiko wa moduli zinazohi-tajika katika viwanda muhimu. Kanuni Alama za CE kisheria zinayoongoza na kuhakikisha kuwa Jumuia ya Ulaya inazitumia ili kutambua kuwa bidhaa imekidhi viwango fulani. Hata kama ni kitu kipya (mf. Kanuni za Jumuia ya Ulaya za ufundi angalia swali la 18 ). Sio tu kwa Jumuia ya Ulaya au hata kwa mwingine yeyote yule anayetoa huduma ya tathmini makubaliano hafanyi hivyo bali mtengenezaji au mgavi ambao huchumua dhamana ya ubora wa bidhaa. Yote haya msingi wake ni Maelekezo ya Kanuni Mpya iliyochapishwa 1985: Kisheria kuoainisha kunadhibitiwa katika matakwa muhimu pale ambapo bidhaa inawekwa/inaingizwa katika masoko ya Ulaya EU ni lazima ifikie viwango lengwa. Sifa za kiufundi za bidhaa kufikia matakwa maalumu yaliyowekwa katika muongozo uliozizitizwa wa EN (harmonized standards -EN); Matumizi ya Viwango vilivyowianishwa (harmonized standards) yatabakia ya kujitolea/kibinafsi na mtengenezaji anaweza kutumia sifa za kifundi zingine ili kufikia matakwa ya muhimu, na Bidhaa zilozozalishwa kwa kuzingatia viwango vilivyowianishwa hufaidika kutokana na kusadikika/kuamini kuwa kukubalika kwake kumekidhi matakwa muhimu. Katika kuunga mkono kanuni za Maelekezo Mapya, mnamo mwaka 1989 EU ilitengeneza kiwango cha Kimataifa cha Majaribio na Kuthibitisha kukubalika na Maelekezo yaliyopo. Kiwango cha Kimataifa (The Global Approach) kinaorodhesha moduli nane za makubaliano ambapo moja au zaidi ni lazima zichaguliwe na kutokana yale maelekezo mapya. Zaidi ya hizo moduli, sheria inayotumika kusisitiza CE lazima ifafanuliwe barabara/vizuri. Masuala ya ulinganifu (Compliance issues) Huu ni mfumo wa kawaida kwa Jumuiya yote. Mara bidhaa yako inapokubaliana na matakwa muhimu na ufanisi wake kuonyesha kukubalika kwake na mojawapo ya moduli husika, basi hapo inaweza kuomba kutumia alama ya CE na bidhaa inaweza kuuzwa katika Jumuia ya Ulaya yote. Hii ni fursa nzuri lakini kuna maswala machache ambayo ni ya kuzingatiwa kwa makini: Kutambua Kanuni maalumu ambayo bidhaa yako inaangukia. Maelekezo mapya yote yameorodheshwa katika tovuti ya Jumuia ya Ulaya EU. Pia viunganishi vimetolewa hapo chini kwa ajili ya taarifa zaidi. Kutambua Kiwango kinachofaa cha EN kutoka katika orodha inayotambulika katika: Ijapokuwa unaweza kutumia viwango nje ya viwango vya EN mara kwa mara ni rahisi zaidi kuvitumia kama vinakubaliana na viwango vilivyoorodheshwa na EN ambavyo vimeaminika kukubaliana na matakwa muhimu ya Maelekezo Mapya. Tambua moduli ya tathmini makubaliano inayohitajika iwapo inajumuisha maabara zaidi ya mbili au mashirika ya kuthibitisha na halafu ni lazima upate huduma ya bodi inayotambulika. Hawa watoa huduma za tathmini makubaliano huonekena washindani na serikali yao na hutambulishwa ipasavyo na serikali yao katika Jumuia ya Ulaya (EU). Orodha ya Bodi zilizotambulishwa huweza kupatikana katika tovuti ya NANDO (New Approach Notified and Designated Organisations) ya Jumuia ya Madola. Pia kuna orodha ya nchi na watoa huduma ya tathmini ya ulinganifu inayotambulika na kukubalika kimataifa (MRAs) kati ya Jumuiya ya Ulaya na nchi zilizo nje ya Jumuiya ya Ulaya ( EU). Ukiwa mzalishaji nje ya Jumuia ya Ulaya, lazima uteue au kuidhinisha mwakilishi mkazi wa EU ambaye atawasiliana kwa niaba yako iwapo patatokea hoja au matatizo katika bidhaa. Mzalishaji ni lazima

177 Tathmini Ya Ulinganifu 167 akusanye na kudumisha faili la ufundi la bidhaa ili kutoa taarifa za usanifu/ubunifu utengenezaji, jinsi bidhaa hiyo inavyofanya kazi na vilevile kuhakikisha kukubalika kwake na muongozo unaohusika. Faili hili lazima litunzwe kwa muda wa miaka 10 baada ya mzalishaji kusitisha kuuza bidhaa katika soko fulani. Mzalishaji au mwakilishi aliyeidhinishwa lazima akubaliane na tamko la EC la mabubaliano kama sehemu ya mchakato wa tathmini makubalianoya Maelekezo mapya. Tamko la EC la kukubaliana lazima litambue maelekezo ya chini, mzalishaji, mwakilishi aliyeidhinishwa, bodi iliyopewa taarifa, bidhaa na kiwango kilichoainishwa. Moduli za tathmini ulinganifu Moduli za tathmini ya ulinganifu zinahusiana na awamu za usanifu, awamu za uzalishaji au vyote. Moduli nane za msingi zinaweza kuchanganywa katika mtindo au njia mbalimbali ili kufanya hatua za tathmini ya ulinganifu iliyokamilika. Moduli halisi itakayotumika inaweza kutambuliwa kutoka katika maelekezo yanayohusika. Iwapo mzalishaji atapewa nafasi ya kuchagua basi patakuwa na vigezo vitakavyoorodheshwa pia. Mchoro rahisi wa moduli nane umeonyeshwa hapa chini ili kuelezea muongozo halisi na kutoa uchambuzi muhimu kwa ajili ya utekelezaji. Maagizo mpya ya EU: moduli za thathmini ya ulinganifu Chanzo: Tume ya Ulaya. Moduli A inatumika iwapo bidhaa ni za hatari/riskiau iwapo sekta ya uzalishaji ina sifa nzuri za kukubalika. Mzalishaji anapima na kutathmini bila kumhusisha mtu wa tatu isipokuwa Moduli za Aa1 na Aa2. Katika utaratibu huu wa msingi Moduli A inaweza kufikiriwa katika tamko la makubaliano la mzalishaji (angalia sawli 57). Katika Moduli b B, bodi iliyoidhinishwa inatakiwa/inahijajika kama ilivyo katika Moduli C hadi H. Moduli B wakati wote inachanganywa na moduli mojawapo zilizopo kati a Moduli C na F. Moduli za kawaida zimeonyeshwa katika mabano karibu na majina ya bidhaa katika aya ifuatayo. Bidhaa Bidhaa ambazo Mwongozo mpya umechapishwa na ambapo alama za CE ni lazima ni pamoja na vifaa vya umeme/volti kidogo (A); vyombo vyenye mkandamizo mwepesi(a+, B, Cbis2, F); mwanasesere/vikaragosi (A); vifaa vya ujenzi, electromagnetic compatibility (A, B, C); mashine (B,A); vifaa vya usalama binasi (A, B, Cbis2, D); vifaa vya kupima uzito visivyo automatiki(b, D, F, G); active implantable medical devices (B, D, F, Hbis); vifaa vya gesi (B, C, D, F, G); boila za kuchemsha maji (B, Cbis2, D, E); baruti za matumizi ya kawaida (B, Cbis2, D, E,F, G); vifaa vya tiba (A to F); mazingira ya ulipuaji (A, A+, B, Cbis1, D, E, F); sanaa za mikono mpya (A to H); lifti (A to G); vifaa vya majokofu (A); vifaa vya presha/mkandamizo (A to G); vifaa vya mawasiliano (B, Cbis2, D, H); in vitro diagnostic medical devices

178 168 Tathmini Ya Ulinganifu (A to H); vifaa vya vituo cha radio na mawasiliano (A, Aa+, H). Miongozo mipya pia inaweza kuchapwa kwa ajili ya uchafu wa ufungaji na ufungashaji, mifumo ya treni za mwendo kasi na vifaa vya mitambo ya baharini lakini alama ya CE kwa ujumla haihitajiwi kwa hizo. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: BSI technical handbooks. Machapisho ya vifaa vya kiufundi wa vifaa vya umeme, mashine, vifaa vya magari,vyombo vyenye mkandakizo,(presha),vifaa vya kujikinga na majanga na bidhaa za ujenzi na sherian za kimataifa zinazotumika na matakwa ya kuidhinishwa, alama za CE, miongozo na matakwa mengine ya kisheria. Kamisheni ya Ulaya. Mwongozo wa utekelezaji wa miongozo katika misingi ya Mbinu Mpya na Mbinu za Kimataifa Inapatikana katika lugha 11 za Serikali za Jumuia ya Ulaya. Inatoa sura safi na uliokamilika wa Miongozo Mipya na Mfumo wa Kimataifa na inu mpya. Kamisheni ya Ulaya, Biashara na Viwanda. Utiaji wa alama ya CE Taarifa juu ya kuandaa uwekaji alama ya CE katika bidhaa. Tovuti inamwongoza mzalishaji katika mchakato wa kuweka alama ya CEkatika bidhaa zake maalumu kwa kuonyesha mtiririko wa hatua za kufuata tangu mwanzo hadi uuzwaji wa bidhaa. Kamisheni ya Ulaya (European Commission)/EFTA/CEN/CENELEC/ETSI. Mbinu Mpya za Viwango katika Soko la Ndani.( New Approach Standardisation in the Internal Market). Hii intatoa upatikanaji wa taarifa za miongozo, viwango na taratibu za kufikia mchakato mzima wa kuweka viwango bila kujali ni aina gani ya viwangokatika Mashirika ya Viwango Ulaya kwa kuzingatia kile kinachohusika na bidhaa ile. MAREJELEO Kamisheni ya Ulaya Viwango vya Ulaya: Orodha ya marejeo ya viwango vinavyokubalika. Miongozo ya Viwango Vipya. NANDO (New Approach Notified and Designated Organisations).

179 Tathmini Ya Ulinganifu 169 B. UPIMAJI (TESTING) 59. Upimaji ni nini na una umuhimu gani katika masoko ya kimataifa? Kwa minajili ya kitabu hiki, ufafanuzi wa kipimo na kupima umetolewa katika: ISO/IEC 17000:2004 Msamiati na Kanuni za Ujumla za Tathmini ya Ulinganifu, umechapishwa kwa pamoja kati ya ISO na IEC. Inaaminika kujielezea kiufasaha. Kupima hufafanuliwa kama upembuzi yakinifu wa kiufundi/kitaalamu unaojumuisha tabia/sifa moja au zaidi inayokubalika kulingana na hatua za utengenezaji.upimaji wa kawaida unahusisha vipimo vya ukubwa/umbile, uwepo wa kemikali, utakaso wa kibaioljia na uwezo/nguvu au sifa zinginezo zozote zile za kimaumbile au uwezo wa kutopondeka kudhurika kutokana na vitu vingine. Majibu/matokeo ya upimaji mara kwa mara hutoa taarifa zinazotosheleza ili kuruhusu mtu mwenye sifa/ushindani kuhitimisha iwapo ndivyo au sivyo kwa bidhaa ile kufikia viwango/matakwa ya bodi ya udhibiti, wanunuzi au watumiaji wengine. Wakati mwingine katika ukaguzi wa lifti katika majengo na magari (angalia swali la 65) inweza kujitosheleza. Ni vyema kukubali kuwa mipaka kati ya upimaji na ukaguzi ni dhaifu sana kwani kuna shughuli zingine zinaweza kuwekwa lebo ya kutofautisha bidhaa/kazi. Shughuli/kazi hii kubwa inaitwa tathmini makubaliano ambayo yanajumuisha upimaji, ukaguzi na uhakiki/uthibitisho. Wakati upimaji na kukaguaji ni njia ya kawaida ya kubaini kukubalika, wakati mwingine upimaji au ukaguaji unachukuliwa kama hautoshi kwa wadhibiti au wateja. Wakati mwingine uthibitisho wa mtu wa tatu pia unahitajika. Hivi ndivyo ilivyo katika sekta ya bidhaa ambapo zile bidhaa zinaweza kuwa ndogo kwa umbile au za hatari/athari/riski kubwa. Mifano ni kwa vifaa vya tiba/hospitalini na vya umeme kwa ajili ya mazingira ya ulipuaji. Uthibitisho huu wa bidhaa wakati wote unaungwa mkono kwa kupimwa au kukaguliwa. Uthibitisho dhidi ya viwango (mf. ISO 9001, ISO 14001) hupatikana kwa ajili ya huduma au shughuli ya uzalishaji na haijumuishi upimaji katika kiwango kwa kina ambacho shughuli za kiufundi/kitaalamu huhitajika kuonyeshwa. Mara kwa mara upimaji hufanyika katika maabara kabla ya kumpelekea au kupokea bidhaa toka kwa mteja. Hata hivyo mara nyingi inaweza kufanyika katika eneo la tukio/uzalishaji au eneo la usimikaji. Huu ni ukweli usiofichika hasa katika mitambo/mashine kubwa na katika mabomba yaliyochomelewa pamoja na njia za reli. Viwango na tathmini ya ulinganifu vimetengenezwa kama vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mingi na kwa mara ya kwanza vilitamkwa kimataifa katika Mkutano/kongamano la Tokyo la GATT miaka ya Matokeo yake ni kutengenezwa kwa Viwango vya GATT vyenye Code ya 1979 inayotanguliwa na Makubaliano ya WTO TBT. Bodi zenye zinazohusika na biashara kama vile WTO, Kamisheni ya Ulaya na Asia-Pacific Economic Cooperation forum (APEC), zimeendelea kukbali kwamba upungufu wa kukubalika au kutambulika kwa matokeo ya vipimo vya nje yanabakia kuwa kikwazo cha soko huria. Mashirika ya Udhibiti na Wanunua bidhaa za nje mara kwa mara wamehitaji upimaji katika eneo la kupokelea mzigo toka nje kwa kutumia maabara zao wanazoziamini/wanazozitambua hata kama upimaji wa kina ulifanyika katika nchi ambapo bidhaa ilizalishwa. Utaratibu huu umesababisha kuelewana na kutengeneza mazingira yanayoheshimu pande zote zinazohusika, inajadiliwa zaidi katika swali la 91 ili kupunguza athari zake. Utaratibu huu unaonekana kama vikwazo vya kiufundi katika biashara kwa sababu zinaongeza gharama kwa kurudia kazi hiyo hiyo na ucheleweshwaji. Iwapo upimaji umefanyika nje ya kituo/eneo la uzalishaji, basi upimaji huo utafanywa tena kwa makini sana na kwa kuzingatia matakwa ya mteja au kwa kuzungatia soko la nje na kasha hapatakuwa na sababu ya kupimwa tena; labda itokee hali isiyoridhisha wakati wa kusafirisha ambapo bidhaa itaonekana kudhoofu. Mzalishaji mwenye busara wakati wote atahakikisha kuwa bidhaa zisizokubalika zitasanifiwa na kupimwa tenaili kukubaliana na matakwa ya soko la nje kabla hazijafirishwa/hazijatumwa. Ucheleweshwaji wowote ule wa kuingiza bidhaa katika soko la nje unaipunguzia bidhaa ushindani wake kwa kuongeza gharama(kwa mfano- kupimwa tena) na ucheleweshwaji wa malipo, na hivyo kutoa fursa kwa washindani na wagavi wa bidhaa za ndani. Iwapo upimaji katika nchi inayopeleka mzigo/inayouza nje umefanywa barabara, kwa kiasi kikubwa inapunguza matakwa ya kupimwa tena kabla ya kuruhusiwa bidhaa kuingia sokoni katika nchi iliyoagiza.

180 170 Tathmini Ya Ulinganifu Sio upimaji wote ni tathmini ya ulinganifu, kwani upimaji mwingi unahusishwa na ukusanyaji wa takwimu na sio kukubalika kwa bidhaa. Baadhi ya hizi zinaweza kuhusishwa na maswala kama vile vipimo vya mazingira ambavyo havihusiki na bidhaa fulani bali yana maana/umuhimu katika maswala ya biashara. Kadri bidhaa zinazozalishwa zinavyizidi kuwa za kisasa zaidi mahitaji ya soko kuzidi kuwa na masharti mengi, umuhimu wa upimaji utazidi kuongezeka na kuwa itifaki katika biashara. Harakati za kuelekea soko la usawa zinahitaji kutambuliwa kwa upimaji unaofanyika katika nchi ya asili ya bidhaa (bidhaa inapotoka) lakini litawezekana tu iwapo mtumiaji wa mwisho atakuwa na imani na utimilifu wa maabara zinazopima bidhaa hizo. Lengo kuu ni kuwa na bidhaa zilizopimwa na kuthibitishwa mara moja tu na kisha kukubalika popote pale (angalia swali la 91) MAREJELEO Shirika la Viwango la Kimataifa na Shirika la Kimataifa la Kielektriniki (International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission). ISO/IEC 17000:2004, Tathmini makubaliano Msamiati na kanuni za ujumla hupatikana kutoka ISO au wanacama wa ISO (orodha ipo: na kutoka IEC au IEC Kamitii ya Taifa (orodha katika

181 Tathmini Ya Ulinganifu Nitahakikishaje kuwa taarifa ya upimaji wa bidhaa yangu inakubalika ng ambo? Hakuna mfumo mmoja wa kutumika kwa bidhaa zote na sekta zote ili kuhakikisha kuwa taarifa za upimaji kutoka nchi inayouza nje itakubalika nchi iliyoagiza bidhaa. Pia ni kweli kusema kuwa katika baadhi ya masoko kuwa sheria mbalimbali hutumika katika sekta maalumu/fulani tu kutegemea aina ya bidhaa na muongozo wa watu binafsi ambao wana uhuru wa maamuzi yao ya utekelezaji katika sekta zao (mfumo wima - a vertical system). Hii inaweza kulinganishwa na mfumo wa lala (horizontal system) ambao wadhibiti wote wanafanya kazi katika sheria za ujumla kama ilivyo katika Mbinu za Kimataifa za EU. Kwa mathlani hii hutokea katika masoko kama vile Marekani na Japan ambapo kuna mufumo wima ya kanuni. Taasisi kama vile lile la Chakula na Dawa la Marekani, (The US Food and Drug Administration - USFDA), Idara ya Kilimo (US Department of Agriculture - USDA) na Kamisheni ya Mawasiliano (Federal Communications Commission - FCC) yote yana mitazamo tofauti ya kukubaliana na vipimo vya maabara za nje. USFDA inachohitaji ni kutoa usimamizi wa moja kwa moja kwa wazalishaji wote popote pale walipo nao FCC watakubali majibu/matokeo ya upimaji kutoka katika maabara za nje zilizidhinishwa na bodi za za uthibitisho. Licha ya kutegemea uthibitisho, Mamlaka za Japani mara kwa mara huhitaji kiambato/kiambatanisho maalumu kutoka katika serikali ya nchi ambayo inauza kabla ya kukubali bidhaa kufanyiwa uchunguzi wa takwimu katika maabara. Kutokana na hayo ni jukumu la muuzaji nje ya nchi, mzalishaji au wakala wa unuaji nje ya nchi kuhakikisha kwamba sheria za soko kwa ajili ya bidhaa fulani zimetoshelezwa. Utambuaji wa taarifa/ripoti ya upimaji yeyote ile, iwe ni ya ndani ya nchi au ya kigeni utahitajika kukubaliwa katika mamlaka zote za sheria zilizo na nia ya bidhaa na mnunuzi katika soko lililodhamiriwa. Wafanya biashara wakubwa na wanunuzi wakubwa wa rejareja ya wanaweza kuwa na matakwa maalumu ya ubora zaidi ya yaliyowekwa na mamlaka husika na katika hali hiyo maslahi yote ni lazima yazingatiwe. Kwa uwazi kabisa bila ya kanuni kukubalika hakuna bidhaa itakayouzwa kwa yeyote japokuwa mahitaji ya soko ni lazima yazingatiwe. Kanuni za ujumla zilizowekwa na Shirika la Kimataifa la Biashara (WTO) katika Makubaliano katika Vikwazo vya Ufundi (WTO Agreement on Technical Barriers to Trade (the TBT Agreement), yanabainisha kuwa vikwazo vya kiufundi vitaepukwa na wanachama wanahamasishwa sana kukubaliana na thathmini makubaliano katika nchi ambapo bidhaa ilitengenezwa. Kanuni hizi zinakubalika japokuwa katika hali fulani na katika nchi fulani wanaruhusiwa kuwa na viwango vyao vya kujikinga ambavyo vitahakikishiwa kukubalika na bodi za nje zinazotoa ripoti/taarifa za tathmini makubaliano. Wakati ambapo makubaliano ya TBT yanataja matumizi ya makubaliano yenye faida kwa wote (MRAs), msingi wa vibali unafaa kuwa dhana yenye kutoa ushindani na papo hapo kuruhusu uendelezaji wa hatua zingine kama vile kubadilishana wataalamu na kulinganisha vipimo katika kipindi fulani. (swali la 91 linajadili MRA kwa undani zaidi. Kutambuliwa au vinginevyo kupata vibali ni haki ya nchi iliyoagiza bidhaa na sio haki ya nchi iliyotuma/uza bidhaa. Kulingana na MRA, Makubaliano ya TBT yanarejea katika kanuni na taratibu za serikali. Hii ina maana kuwa MRAinawezekana kujadiliana kati ya serikali mbili au zaidi ambapo mojawapo kisheria inatarajia kuwa upande wa serikali zinazoshiriki. Mifano miwili ya MRA inayojulikana sana ni ile ya Maabara ya Kimataifa ya Kutoa Vibali (Laboratory Accreditation Cooperation - ILAC) na Jukwaa la Kimataifa la Kutoa Vibali (International Accreditation Forum -IAF). Hata hivyo hivi ni taasisis binafsi naserikali zipo huru kutambua makubaliano hayo au la, kutokana na itakavyoona. Vivyo hivyo sekta binafsi za biashara hazilazimishwi na makubaliano hayo bali hawa watumiaji binafsi wanaweza kuamua wenyewe iwapo wakubali au wakatae makubaliano hayo kwa kutoa maelezo ya kuaminika juu ya shughuli za tathmini makubaliano zinazohusika. ILAC na IAF wanazo habari za sababu hizi na wapo makini sana katika kutambua MRA na kushughulikia mapungufu yeyote yale. Kwa muhtasari, wakati WTO inawataka wanachama kukubali vipimo vya nchi inayouza nje, kuna uwigo mkubwa wa taratibu zinazotumika katika mamlaka mbalimbali. Hizi zinazitaka maabara zinazopima kutoa takwimu/taarifa zifuatazo: Inafanya kazi katika mamlaka za kisheria katika nchi inayoagiza bidhaa (Operated by the regulatory authority of the importing country;) Ina sifa nzuri iliyoanzishwa na mamlaka inayokubali (one with a good reputation established with the accepting authority;)

182 172 Tathmini Ya Ulinganifu Inatambulika na bodi ya kanuni (Recognized by the regulatory body;) Imekubaliwa na Bodi ya Taifa ya katika nchi inayoagiza bidhaa. Inatambuliwa na mojowapo wa washirika kati ya serikali moja na nyingine katika MRA; au Inayokubalika na bodi katika Mipangilio ya ILAC. Katika mazingira ya biashara za leo; utoaji vibali ni nyenzo inayotumika katika kubaini na kudumisha uaminifu katika bodi za tathmini makubaliano na ni wajibu wa muuzaji nje ya nchi kuelewa sheria za soko lililoagiza bidhaa. Kwa mtazamo wa utumiaji kwa vitendo wa ISO/IEC kwa ajili ya vyakula vya baharini na bidhaa zinginezo za baharini katika Jumuia ya Ulaya, angalia/jiunganishe na kiunganisho kwa taarifa zaidi chini. KWA TAARIFA ZAIDI Kamisheni ya Ulaya (European Commission), Kurugenzi ya Afya na Walaji (Directorate General for Health & Consumers). Taratibu za EU za kuagiza toka nje ya nchi za vyakula vya baharini na bidhaa zingine za uvuvihttp://ec.europa.eu/food/international/trade/im_cond_fish_en.pdf Katika Jumuia ya Ulaya kupata kibali toka ISO/IEC huhitajika kwenye bidhaa za uvuvi. Kwa matokeo yaliyodadavuliwa kwa makini ni lazima yawe na muda rasmi wa kutumika, na lazima itoke katika maabara iliyoidhinishwa kwa kuwa na viwango vinavyohitajika katika uchambuzi. Maabara ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Vibali (International Laboratory Accreditation Cooperation). Hadithi simulizi za mafanikio kutoka ILAC, Marketing & Communications Committee (MCC). ILAC MCC wamewataka wanachama kutoa taarifa nzuri za simulizi ambazo zinasisitiza mafanikio ya vibali na Mipangilio ya ILAC yaliyofikishwa na washikadau mbalimbali. Mkusanyiko wa taarifa nzuri hupatikana katika tovuti ya ILAC. Shirika la Kimataifa la Viwango na Kamisheni ya Kimataifa ya Electroniki (International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission). ISO/IEC 17025:2005, Mahitaji ya ujumla kwa ajili ya upimaji na urekebishaji wa vipimio katika maabara hupatikana kutoka ISO au wanachama wa ISO (angalia katika orodha ya na kutoka IEC au IEC National Committees (Orodha katika: ISO/IEC 17025:2005 inaelezea matakwa ya jumla kiushindani ili kupima au kurekebisha vipimio pamoja na sampuli. Inajumuisha Upimaji na urekebishaji vipimio kwa kutumia mbinu zilizo katika viwango, mbinu zisizokuwa katika viwango na mbinu zilizobuniwa katika maabara. Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Kimataifa (UNIDO) huzingatia ISO 17025:2005 au viwango vinavyofanana. Angalia: Kitabu kinachoongoza jinsi ya kufikia matakwa ya kukubalika kimaabara yapo: ISO 17025:2005 au viwango vya kitaifa vilivyopo. MAREJELEO Shirika la Biashara la Kimataifa. Makubaliano juu ya Vikwazo vya Kiufundi katika Biashara,

183 Tathmini Ya Ulinganifu Kwa nini ustadi wa upimaji ni muhimu na wapi naweza kupata wapimaji mahiri? Upimaji mahiri (Proficiency testing -PT) ni seti ya programu zilizopangiliwa kwa ajili ya kulinganisha upimaji kwa vitendo wa maabara mbalimbali kwa lengo la kuamua utendaji kazi halisi wa maabara binafsi/mojawapo ili kuthibitisha ushindani wake. Baadhi ya maabara kutambulika au mipango yakeya kuthibitishwa hutegemea moja kwa moja katika mpango huu wa kutathminiwa lakini zaidi ustadi wa kupima unapatikana kwa kukubaliwa na thathmini kwa vipindi fulani. Kwa hali yeyote ile mafanikio mfululizo ya kushiriki katika program za PT, kitaalamu inawezekana lakini ikumbukwe kwamba ni vyema kuzingatia hali ya kukubalika kwa hali yeyote ile. Ni muhimu kukubali kwamba kushiriki katika program moja ya PT ni mara chache tu kwani hutoa mounekano wa juu juu tu wa kimaabara kwani majibu sahihi ya mwisho yanaweza kuwa ya bahati tu. Vivyo hivyo majibu yasiyotosheleza yanaweza kutokana na makosa madogo yasiyozuilika katika maabara mara kwa mara lakini haimaanishi kuwa maabara iliyohusika sio nzuri/shidani. Jambo muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa ufanyaji kazi unaendelea kwa kipindi chote na ustadi wa utumiaji wa takwimu katika maabara unakuwa nyenzo ya kuboresha mifumo ya menejimenti na utendaji kazi wa mafundi. Programu zilizopitishwa kwa ustadi wake wa kupimwa huhitaji ushiriki wa mara kwa mara na uchambuzi yakinifu wa matokeo/majibu kwa ufumbuzi wa haraka. Ni ghali sana kuendesha shughuli ya upimaji na kwa baadhi ya sehemu zingine ni vigumu sana kudumisha upimaji. Baadhi ya urekebishaji vipimio na umahiri wa program za kupimia huhitaji muda mrefu wa kumaliza na thamani yake ni ndogo kama programu iliyoidhinishwa. Kwa sababu hizi, mifumo ya vibali ambayo ipo katika mtazamo wa kimakundi kwa mujibu wa ISO/IEC 17011:2004 na ISO/IEC17025:2005 (angalia rejeo mbalimbali kwa ajili ya vichwa vya habari vya viwango hivi), Utumiaji wa vipimo kwa ustadi kama chombo muhimu kwa ajili ya maandalizi ya ufuatiliaji wao ni muhimu lakini hata hivyo hautoshi kwa vibali wala kutambuliwa. Mifumo mingi ya upimaji mahiri imebuniwa, tangu uchukuaji vipimo na upimaji katika maabara kama msingi wa kukubalika bidhaa. Kwa kawaida programu ziliendeshwa na mmojawapo wa wadau mpaka uuzaji, au mnunuzi au muuzaji lakini katika miaka hii ya karibuni pamekuwa na maendeleo katika ustadi wa kupima kama shughuli huru (third party) hasa anapolenga utoaji wa huduma ya kibiashara. Viwango kama vile ISO/IEC 17043:2010 vimetengenezwa ili kusisitiza uaminifu wa programu wakati mifumo ya utoaji vibali ilianzishwa ili kuongeza uaminifu katika ushindani kwa watoaji. Zana za upimaji stadi (zana za kulinganisha maabara za kimataifa) nazo hutumika katika kuhalalisha na mafunzo yanayohusika na maendeleo ya mbinu za kupima viwango kama vile kutathmini uimara/umadhubuti wa njia fulani. Zana hizo hizo hutumika kama rejea za watengenezaji wa vifaa mbalimbali wanapotumia maabara za kimataifa katika kulinganisha upimaji wa maabara mbalimbali mahiri ili kuzipa thamani na kuondoa wasiwasi katika kumbukumbu za vifaa ambavyo tayari vilishapimwa. Kamati ya Kimataifa ya Mizani na Vipimo (The International Committee for Weights and Measures -CIPM) pia inatumia aina fulani ya kulinganisha maabara mbalimbali (vitu muhimu vya kulinganishwa tu - Key Comparisons) ili kufuatilia urekebishaji na uwezo wa kupima wa maabara za kitaifa (angalia swali la 79). Programu za PT zenyewe wakati mwingine hutumika katika mashindano ya kulinganisha na sio mara kwa mara katika changamoto zinazohusishwa na matumizi ya baadhi ya viwango na njia za asili za upimaji. Njia hii peke yake inaongeza thamani kwa kiasi kikubwa na kwa ustadi wa upimaji serikalini. Utafutaji wowote ule katika mtandao kwa wapimaji stadi/mahiri utapata/utavuna matokeo mengi. Baadhi ya watoa vipimo/wapimaji hubobea katika utaalamu wa vitu vichache tu kama vile upimaji wa kitabibu(hospitalini),maji na vyakula, wakati wengine hutoa programu katika nyanja kadhaa. Chanzo cha taarifa kwa kina cha amu ya PT ni takwimu za European Proficiency Testing Information System (EPTIS, linki inaonyeshwa chini) hii inarejea katika maelfu ya PT duniani kote. Programu stadi za Kimataifa za upimaji hutoa vifaa na zana za aina nyingi na kuendesha program hizo. Hata hivyo Sheria za kimataifa za usafirishaji wa angani/hewani kanuni nyingi za kitaifa za ushuru wa forodha na karantini zinazuia moja kwa moja kutegemea programu za PT kutoka vyanzo vya nje,hasa pale ambapo vifaa vinaweza kuhusishwa na hatari kama vile sumu au ya kuwaka moto. Pale inapowezekana inapendekezwa kuwana uwezo wa kitaifa wa kutoa vipimo kwa ustadi hasa vile vya maeneo ya kiufundi ambayo yanahusika sana na vifaa vya matumizi ya nyumbani au uzalishaji. ISO/DTR inatoa taarifa za usambazaji wa kimataifa wa rejea za vifaa. Katika miaka hii ya karibuni ambapo kuna ongezeko kubwa la vipimo stadi, pamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wa watoa huduma wa PT na dhamira ya kuwa na

184 174 Tathmini Ya Ulinganifu mfumo wa kutoa vibali unaoeleweka. Baadhi ya wanachama wa ILAC sasa wanatoa huduma hizo ambazo ni za uwazi na haki kubwa. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: European Proficiency Testing Information System (EPTIS). EPTIS ni shirika lenye mashirika wanachama 39 kutoka mabara yote.mengi ya mashirika haya wanachama ni Vyuo vya Taifa vya Hali ya Hewa, Vyuo vya Upimaji au Bodi za kutoa vibali. Takwimu za EPTIS hujumuisha orodha ya vipimo stadi/mahiri (PT schemes) vinavyofanya kazi Ulaya, Amerika na Australia. Hivi vyote ni vile vilivyopata vibali na vile ambavyo havijapata vibali. Taarifa zilizopo katika database msingi wake ni matamko binafsi kutoka watoa huduma za vipimo mahiri. International Laboratory Accreditation Cooperation Benefits for Laboratories Participating in Proficiency Testing Programs Didactic brochure ambayo inajadili uthibitisho wa ushindani bora (competent performance),jinsi ya kutambua matatizo ya vipimo au upimaji, jinsi ya kulinganisha mbinu na hatua za kufuata n.k. The American Association for Laboratory Accreditation. R302 Mahitaji ya Jumla: Kibali cha ISO/IEC Ustadi wa wapimaji (Proficiency Testing Providers) Waraka huu ni wa nje ya mahitaji ya jumla kwa A2LA (Chama cha Kimarekani cha Kutoa Vibali kwa Maabara - American Association for Laboratory Accreditation) A2LA ni shirika lisilokuwa la kutengeneza faida, lisilokuwa la kiserikali ambalo limejitolea kufanya kazi kwa upana zaidi a nchini kotekatika mfumo wa kutoa vibali. MAREJELEO Shirika la Viwango la Kimataifa (International Organization for Standardization) ISO Guide 35:2006, Reference materials General and statistical principles for certification. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO/DTR 11773, Global Distribution of Reference Materials. Obtainable from ISO or ISO members (list at International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission ISO/IEC 17025:2005, General requirements for the competence of testing and calibration laboratories. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at ISO/IEC 17011:2004, Conformity assessment General requirements for accreditation bodies accrediting conformity assessment bodies. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at ISO/IEC 17043:2010, Conformity assessment General requirements for proficiency testing. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at

185 Tathmini Ya Ulinganifu Je niweke maabara yangu ya vipimo au nitumie maabara za nje? Kimsingi hili ni swala la maamuzi ya kifedha. Kukiwa bidhaa nyingi uwepo wa maabara nzuri ni muhimu kwa ajili ya kupima ili kudhibiti mchakato wa uzalishaji na kwa ajili ya upimaji wa mwisho wa kukubalika kabla ya kuingiza bidhaa katika soko. Maabara ni ghali sana kuzianzisha na kuzidumisha hata kama ni katika hatua ya awali/mwanzo. Kwa ujumla kadri upimaji unavyokuwa wa kisasa zaidi/mgumu ndivyo gharama za mtaji, za nguvu kazi(wafanyakazi) na gharama za matengenezo zinakuwa juu. Kwa hivyo yeyote yule anayefikiria jambo/sawli hili vema kufikiria mambo mengi kama ilivyoorodheshwa chini na kuwianisha gharama na faida. Kitu cha kwanza kufikiria ni wingi wa vipimo vitakavyohitajika. Inahisiwa kuwa ; je kutakuwa na kipengere cha kuendeleza bidhaa? Hii inaweza kuwa motisha ya ziada ya kuanzisha kituo hiki. Je ni nini tofauti ya asili ya bidhaa na mchakato na je hii inamaanisha kwamba kuna umuhimu wa haraka wa kuwa na vifaa vya maabara? Je ni kiasi gani cha vipimo vya lazima ili kukubalika? Unapofikiria uwezekano wa kutafuta shughuli za kimaabara nje, jambo la msingi ni kudumisha uwezo wa ndani wa kupima kwanza huku ukifikiria kupata vifaa vya kitaalamu zaidi pale ilipoonekana kuwa haina faida/maana kujenga uwezo wa ndani. Mfano ni dhamira ya kuwa na mabaki kidogo sana katika bidhaa za samaki. Hili linazusha swali la urahisi wa kupata vifaa vinavyofaa kutoka nje. Pale ambapo kuna vikundi vidogovidogo vya wazalishaji waliopo karibu karibu ni kawaida kuwepo kwa maabara za kibiashara zitakazokuwa zinahudumia wote ambazo zinaweza kuanzishwa na kampuni ya kigeni au kama juhudi za wenyeji. Licha ya gharama za upimaji wa moja kwa moja, masuala mengine hujumuisha gharama za msingi ambazo zinaweza kuibuka kwa sababu ya upimaji mbaya. Je ni hatari gani na gharama gani bidhaa inaposhindwa? Je ni masuala gani ya kiusalama yanayohusishwa na mchakato wa uzalishaji na utumiajiwa bidhaa kwa watumiaji? Je ni gharama gani za bidhaa itakapokataliwa katika soko lengwa na gharama gani za kuirudia au kuiharibu iwapo haitengezeki n.k? Kitu kingine cha kutilia maanani hasa katika nchi zinazoendelea ni kufikiria ugumu utengenezaji, vifaa/vipuri na mahitaji mengine ya kiufundi kwa ajili ya vifaa vya kupimia. Pale ambapo ugumu hautatuliki na iwapo upimaji maalumu unahitajika, basi hapo utaalamu wa maabara za nje utahitajika kwani hiyo ndiyo njia ya pekee ya kupima. Kuna faida za haraka za kuwa na uwezo wa ndani wa vifaa vya kupimia hasa pale ambapo muda wa ufuatiliaji ni muhimu katika mchakato wa uzalishaji lakini pia katika kuelewa zaidi bidhaa na tabia yake wakati wa kuizalisha. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Mtandao wa Maabara, (Labnetwork). Kazi zake muhimu na njia/mbinu za upimaji (Key Functions and Test Methods). Kuweka majadiliano ya vipimo vya ukumba na uzito, kudhibiti ubora wa sampuli, tabia za maumbile na ufaaji wa bidhaa kati ya zilizopo.

186 176 Tathmini Ya Ulinganifu 63. Kwa nini niwe na vifaa vyangu vya kupimia na virekebishwe kila baada ya muda gani? Swali hili linainua idadi kadhaa ya dhana ambazo inawezekana kuwa hazijulikani sana kwa wasomaji wa kawaida. Sababu muhimu za kurekebisha ni msimamo, kuaminika, kujiamini katika kupima na vipimo vyenyewe (angalia swali la 87). Wote wenye nia wanastahili kuamini uadilifu wa upimaji na takwimu za vipimo ambavyo wanavitumia katika shughuli zao zozote. Kurekebisha vipimio katika ngazi yake/kizio chake ni sharti. Urekebishaji unahusisha kuwafanya watu waamini kuwa vipimo hubeba uhusiano unaojulikana katika maswala ya viwango kilo, volti, mita, n.k.(angalia swali la 84). Jinsi vipimo sahihi vinavyozidi kutakiwa,ndivyo uhusiano kati ya vifaa vya kupimia na viwango vinakuwa muhimu. Ufuatiliaji katika urekebishaji wa vipimo unatambuliwa kama daraja kati ya upimaji na viwango vinavyohitajika kama ilivyoelekezwa kwa maandishi. Kutokatika kwa ulinganisho kati ya vifaa vya upimaji hasa vile vinavyojulikana kwa usahihi zaidi katika upimaji huongoza na kusababisha vipimo kuwa na kiwango cha juu katika Mifumo ya ufuatiliaji wa Kimataifa ya Vizio SI (SI units mfano ph). Katika hali hii kimataifa rejea zinakubalika. Pia inakubalika kutambua kuwa vifaa tata (complicated) vya kupimia vinarekebishwa moja kwa moja kulingana na rejea za vifaa hivyo ambavyo uthibitisho wake utatosheleza kanuni zilezile za msingi. Hata hivyo hali ya sasa ya vifaa viliyopo inaweza kuwa ya makubaliano tu dhidi ya hali halisi. Ukweli huu unaweza kuhusishwa na kauli ya ushindi katika thamani halisi. Vifaa vyote ni lazima kurekebishwa kabla ya kuanza kutumika hata kama vipimo hivyo ni vya usahihi mdogo. Ni muhimu kuelewa kwamba usahihi wa urekebishaji wa vifaa lazima uwe katika viwango vinavyohitajika katika kazi fulani na vifaa vya kupimia vyote lazima kukaguliwa ili kuhakikisha kuwa kifaa au mfumo uliotarajiwa unafaa katika matumizi yaliyotarajiwa. Urekebishaji wa vifaa unafanywa kwa kina sana katika vifaa vya hali ya hewa, lakini kutokana na idara hii inatosha kusema kwamba mchakato wa kulinganisha kifaa kimoja cha kupimia na kingine kinachojulikana/maarufu kwa usahihi zaidi na ambacho mchakato wake unaendelea hadi kufikia kiwango kinachohitajika. Vipimo hivi wakati mwingine ni muhimu kujua uwigo wa tofauti ya zilizopo za kutokuwa na uhakika katika vipimo. Ukishajua uhusiano kati ya thamani halisi na ile ya wasiwasi kutokana na vipimo ni rahisi kukadiria usahihi wa vipimo vilivyopatikana. Katika upimaji mwingine hata hivyo, ni muhimu tu kujua kuwa vipimo/matokeo yapo katika wastani unaokubalika kwa kazi. Vifaa vinaweza kupangwa katika madaraja kama vile daraja A, B n,k. Ni dhahiri kusema kwamba mchakato huu unaitwa Ukaguzi lakini mara nyingi unajulikana kama urekebishaji wa vifaa vya kupimia. Wakati wa kutumia vifaa vilivyokaguliwa kwa njia hii hakuna masahihisho yanayoweza kutumika na takwimu zitakazotolewa zinakubalika moja kwa moja. Huu ndio utaratibu wa kawaida unaotumika katika vipimo vya biashara. Kazi ya kupima na kujaribu vifaa inaweza kubadilika kutokana na wakati, mazingira yaliyopo, uchakaaji wa vifaa, ukubwa/wingi wa kazi au matumizi yasiyostahili. Hii ni kwa vifaa vyote vya upimaji na sio kwa vifaa vya teknolojia ya juu (tata) ambavyo hutegemewa kubadilika kutokana na wakati. Usahihi wa vipimo unaotolewa na vifaa inabidi kuangaliwa mara kwa mara na kipindi cha usahihi wa matokeo baada ya kurekebishwa kwa vipimo huitwa recalibration. Vipindi vya kufanya marekebisho ya vifaa (rekebisho moja hadi jingine) mara nyingi hupendekezwa na mtengenezaji wa upimaji au aliyetengeneza chombo cha upimaji na ni lazima kufanya hivyo isipokuwa kwa sababu maalumu. Ufanyaji kazi wa vifaa hutegemea utunzaji wake na utumiaji wake. Watumiaji wa vifaa wakati wote ni lazima wawe na tahadhari ya usomaji wa vifaa utakaoonekana mapungufu. Kwa hali ya mapungufu ya usomaji vipimo, kifaa kilichokuwa na mapungufu ni lazima kuondolewa katika huduma na kurekebishwa mara moja. Urekebishaji pia ni muhimu iwapo kifaa kinafanya kazi zaidi/kwa muda mrefu zaidi au iwapo kifaa kimeshtushwa, kimetingishwa, kimepatwa na umeme usiokidhi mahitaji ya kifaa, n.k. Kwa ujumla utumiaji bora na urekebishwaji wa vifaa/vipimio ni jukumu la mtumiaji wa kifaa/vifaa. Pale ambapo kifaa hutumika katika mazingira yanayokubalika na bodi ya kutoa vibali, bodi hiyo inaamuru muda wa kurekebishwa vifaa hivyo ambao ni pungufu ya muda uliopangwa na mtengenezaji wa vifaa hivyo. Matakwa hayo yatatangulia zaidi ya yale ya mtengenezaji. Hata hivyo haya ni kwa hali yoyote ile hivi ni vipindi vya kuwekwa/maelekezo tu kwani hali halisi ya kurekebisha vifaa ipo mikononi mwa mtumiaji wa vifaa hivyo ili kuhakikisha kuwa vifaa hutumika ipasavyo na kudumishwa ubora wake ikiwepo urekebishwaji

187 Tathmini Ya Ulinganifu 177 wa mara kwa mara kutegemea yaliyozungumziwa juu. Vilevile kwa vifaa vinavyotumika mfululizo/kila siku huhitaji kukaguliwa kila siku (angalia swali la 82) KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Maabara za kurekebisha zilizopewa vibali zimeorodheshwa na bodi ya kutoa vibali ya taifa. ILAC na mashirika ya kutoa vibali kwa kanda yana tovuti ambazo zinaunganisha wanachama wake ambao ni ni bodi za kitaifa za kutoa vibali kama ifuatavyo: Asia Pacific Laboratory Accreditation Cooperation (APLAC). European co-operation for Accreditation (EA). InterAmerican Accreditation Cooperation (IAAC). International Laboratory Accreditation Cooperation (ILAC). Southern African Development Community Accreditation (SADCA). International Laboratory Accreditation Cooperation and International Organization of Legal Metrology. Miongozo ya kutambuavipindi/muda wa kurekebisha wa vifaa vya kupimia - ILAC-G24/OIML D 10) or Nyaraka hizi zinafafanua na kuchambua mbinu zinazopatikana na kujulikana kwa ajili ya vipindi vya kurekebishwa na imedhamiriwa kwa matumizi ya maabara. Watumiaji wa kawaida watategemea mapendekezo ya mtengenezaji ijapokuwa nyaraka zimejumuisha taarifa za jumla hata hivyoni ushauri ili kuelewa vizuri matakwa yanavyopatikana. Shirika la Kimataifa la Viwango (International Organization for Standardization - ISO 10012:2003, Mifumo ya Kudhibiti Vipimo (Measurement management systems) Mahitaji ya hatua za upimaji na vifaa/vyombo vya kupimia hupatikana kutoka ISO or wanachama wa ISO (orodha ipo: Viwango hivi hutoa mwongozo wa kuthibiti hatua za upimaji na vitendo vinavyokubaliana katika vifaa hivi.

188 178 Tathmini Ya Ulinganifu 64. Nini maana ya ufuatiliaji wa vifaa vya kupimia na jinsi ya kuonyesha vinavyofanya kazi?. Ufuatiliaji ni mnyororo usiokatika wa utaratibu na nyaraka za kurekebisha unaounganisha vifaa vinavyofanya kazi na ile hali ya awali ya vifaa vile. Mnyororo huu wa thamani ni mrefu sana na madhara yake ni kutokuwa na uhakika wa urefu huo hata kama kifaa cha upimaji bado kinafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa. Viwango vya muhimu au vya msingi moja kwa moja vinakubaliana na kujulikana na Mfumo wa Kimataifa wa Vizio (International System of Units (SI)). Kwa mfano, tunapozungumzia kilogramu ni dhahiri kuwa hapa tunajihusisha na Ofisi ya Kimataifa ya vipimo vya Uzito (International Bureau of Weights and Measures -BIPM) huko Paris (angalia swali la 84). Viwango vingine vyote hupatikana kutokana na majaribio ya kisayansi katika vyuo vya kitaifa na vya hali ya juu kwa kutumia mbinu zilezile na kwa kulinganisha matokeo ya maabara zilizoshiriki. Katika ngazi hii lazima pawe na makubaliano imara kati ya maabara zilizo katika ubora/thamani halisi kabla ya kupokelewa kuwa zinafaa kwa shughuli fulani. Maabara za namna hii mara kwa mara hutafuta kutambuliwa vizuri zaidi katika vipimo vya SI na ni pale tu ambapo jumuia ya kimataifa kupitia kwa Kamitii ya Kimataifa ya Vipimo na Upimaji (International Committee for Weights and Measures (CIPM), itakaporidhika kwamba mbinu mpya hutoa viwango safi na vinavyokubalika. (angalia swali la 91) Viwango vya kati (Secondary standards) ni vifaa vinavyolinganishwa moja kwa moja na vile vya msingi. Vyote ni sahihi sana na havina wasiwasi katika upimaji. Katika nchi nyingi viwango vya kati hutoa viwango vya kitaifa. Viwango vinavyofanya kazi ni hatua nyingine ya ziada kutoka katika viwango vya msingi na moja kwa moja vinalinganishwa na vipimo vya ksti/sekondari. Viwango vinavyofanya kazi moja kwa moja hutosheleza katika viwango vya taifa katika nchi ambazo hazina uwezo wa kutengeneza bidhaa za teknolojia ngumu/tata. Hivi hukubalika sana kwa ajili ya viwanda na shughuli za kibiashara. Maabara ya kurekebisha vifaa vya hali ya juu huweza pia kudumisha viwango vya kati kama rejea za viwango vinavofanya kazi. Maabara inayohitaji kurekebisha vifaa vyake kwa kawaida huwaendea wataalamu wa maabara za kurekebisha vifaa au Chuo cha vipimo cha taifa au huduma za kigeni za kurekebisha vifaa. Pia, itahitajika kuhakikisha kwamba maabara inayotoa huduma hizo inaweza kurekebisha vifaa katika viwango sahihi vya upimaji visivyo na shaka. Maabara maalumu za kurekebisha zitatoa huduma zao katika ngazi tofauti kwa usahihi kutegemea matarajio ya matumizi ya vifaa/chombo. Warekebishaji hawa wanavumisha/tangaza huduma zao katika misingi ya idadi ya vitu vyote vinavyoshikika/vinavyoonekana, upeo wa vipimo vilivyotolewa na pahala pote ambapo hakuna uhakika. Uwezo wa kurekebisha vfaa vya kupimia mkandamizo (presha) na vakumu (vacuum) vinaweza kuelezewa katika njia hii: Urekabishaji kutegemea matakwa fulani ya AS 1349, ASME B40.1, BS 1780, EN Na viwango vinavyofanana; Geji za kupima mkandamizo (Pressure gauges) pamoja na vile vya kujaribia. Kutoka 0 mpaka 70 MPa katika hewa au maji (air or liquid) katika kutokuwa na uhakika kwa vipimo vya 0.02 au 1.4 k Pa bila kuangalia ni ipi kubwa. Geji za Vakumu (Vacuum gauges) Geji za Bourdon Kutoka -95 mpaka 0 kpa katika kutokuwa na uhakika wa 0.02 kpa. Angalizo: kpa = kilopascal; MPa = megapascal (a million Pascals)

189 Tathmini Ya Ulinganifu 179 Kuongezeka kwa ufahamu kimataifa katika ufuatiliaji kumeilazimisha bodi ya kutoa vibali kuwa makini zaidi katika dhana yote ya tathmini makubaliano. Wameweka kanuni/sheria na miongozo kwa ajili ya kutoa vibali kwa maabara kwa kutumia huduma ambazo zipo wazi zaidi katika mchakato mzima ili kujijengea imani ya uwezo walionao. Utumiaji wa huduma ya vibali vya kurekebisha vifaa vya kupimia kwa njia hii unakuwa safi na wazi katika ufuatiliaji. Hata hivyo huduma za urekebishaji usio na vibali (usiotambulika) unatumika, na kwa utaratibu huu ni jukumu la mtumiaji mwenyewe kuridhika kuwa kuna ufatiliaji thabiti. Hata hivyo kwa utaratibu huu, mazungumzo kati ya watoa huduma ya urekebishaji vifaa watahitajika kulinganisha matokeo ya vipimo vyao na vile vya watoa huduma wengine ili kujiridhisha katika ufuatiliaji. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: EURACHEM/Cooperation on International Traceability in Analytical Chemistry. Quantifying Uncertainty in Analytical Measurement. 2 nd ed. EURACHEM/CITAC Guide CG 4. Mwongozo huu kwa uwazi kabisa umetolewa kwa ajili ya kuhalalisha na kulinganisha taarifa katika utengenezaji wa makisio ya kutokuwa na uhakika (kiasi cha kosa) kinachokubaliana na Kanuni na mwongozo wa ISO. Toleo la pili la mwongozo lipo wazi na linapatikana lakini lile la tatu bado linaendelea kutengenezwa. EURAMET. Metrology In Short. 3rd ed. July Wasiliana na: secretariat@euramet.org Kijitabu hiki kina maelezo ya kina kuhusu metrolojia kwani kinaelezea masuala muhimu, kinachambua mashirika ya kimataifa na kikanda na pia hutoa linki muhimu na hutoa mifano ya vipimo. International Bureau of Weights and Measures (BIPM). The International System of Units (SI). 8 th ed Vipeperushi (brochure) vya vizio/units vya SI, uandikaji wa alama za vizio/units na majina yake,na vizio/units nje ya SI vimeambatanishwa na hupatikana katika lugha mbalimbali. Ushirika wa Ulaya wa Kutoa Vibali (European co-operation for Accreditation). Ufuatiliaji Vifaa vya Kupimia na Kujaribia katika Viwango vya Kitaifa EAL_G12. (Traceability of Measuring and Test Equipment to National Standards. EAL-G12). November Wasiliana na: secretariat@european-accreditation.org Chapisho hili huelekeza mashirika jinsi ya kukubaliana na matakwa ya ufuatiliaji katika viwango stahiki katika EN ISO 9000 na EN Ushirika wa Kimataifa wa Maabara za Kutoa Vibali - International Laboratory Accreditation Cooperation. ILAC Policy on Traceability of Measurement Results. ILAC-P10: Haya yanadadavua dhana ya Ufuatiliaji na majibu ya upimaji/vipimo vya ILAC. International Organization for Standardization. ISO/REMCO for reference materials. Vijitabu hivi huweza kuperuziwa ( downloaded) bure kutoka katika tovuti ya ISO International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC Guide 98-3:2008, Uncertainty of measurement Part 3: Guide to the expression of uncertainty in measurement (GUM:1995). Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at Laboratory Accreditation Bureau. Rejea nzuri za viwango vya kutokuwa na uhakika: Angalia maswali na majibu: Nini kinachoweza kuhesabika kama bajeti ya kiwango kisichokuwa na uhakika? Ni kwa jinsi gani kiwango kisichokuwa cha uhakika hutumika katika upimaji wakati wa kulinganisha na kutoa maelazo kulingana na ILAC G8? Iwapo unajua kile mtoaji wa matokeo ya vipimo au thamani ya viwango ambavyo ni lazima nyaraka idai ufuatiliaji ni lazima kutafuta taarifa katika tovuti hiyo hapo juu.

190 180 Tathmini Ya Ulinganifu 65. Kuna aina ngapi za ukaguzi? C. UKAGUZI Tukizingatia ufafanuzi, ukaguzi hujumuisha aina zote za tathmini makubaliano na zinaweza kujulikana kwa kuwa cha zamani zaidi. Hata hivyo katika hali ya kisasa tunaweza kufafanua ukaguzi zaidi kidogo tu kwani upeo wake hutofautiana sana na mifumo ya kiutawala na taratibu za kimila. Kuna idadi kadhaa za ufafanuzi wa ukaguzi lakini zote hujumuisha dhana ya kutafuta taarifa (upimaji, majaribio), uchunguzi (wa hali zilizopo) na kutoa maamuzi juu ya kufaa kwake katika kutumika au kukubaliana na matakwa. Kwa vile uamuzi ni jambo la muhimu katika mchakato, ukaguzi wake unakabiliwa na matokeo mbalimbali. Kwa sababu hii, ni muhimu kwamba wakaguzi wanafundishwa katika sekta ambazo wanatarajiwa kufanya kazi. Ukaguzi hautumiki tu katika mchakato wa utengenezaji na bidhaa bali pia unaweza kutumika katika shughuli mbalimbali kama vile uthibitisho wa usanifu/ubunifu, ufungaji mitambo na kukabidhi mitambo kwa ajili ya kutumika, ufuatiliaji wafanyakazi, masuala ya kisheria, ukaguzi wa mahesabu ya fedha na uchunguzi ulioshindwa. Jedwali linalofuata linaonyesha baadhi ya shughuli za mashirika ambazo hutumia huduma za ukaguzi wa kawaida. Ukaguzi katika biashara Ukaguzi Mtumiaji Mzalishaji Mteja Msimamizi Mfanyabiashara Udhibiti wa mchakato Ulinganifu/kukidhi kuhusiana usalama na masuala ya kisheria X X X X X Uthibitisho wa usanifu/ubunifu X X Usimikaji wa mtambo mkuu X X Kuanza kazi rasmi kwa mtambo mkuu X X Matengenezo/service X X kiasi /wingi X X Ubora X X X Chanzo: John Gilmour, Australia. Katika jamii nyingi ukaguzi mara kwa mara hufanyika na hutumika katika kudibiti kisheria na kwingineko kwa ajili ya kulinda usimamizi wa kibiashara kwa bodi ngazi ya wa tatu (third party) na katika kudhibiti uzalishaji kiwandani kwa mtengenezaji mwenyewe. Kisheria ukaguzi unaweza kulazimu bidhaa kukubaliana na kanuni za kitaalamu/kifundi kabla ya kuingia sokoni. Katika baadhi ya jamii, bidhaa zinazojulikana kwa mtindo huo ni zile zinazotoka Jumuiya ya Urusi ambapo inawezekana kuwa na maelfu kadhaa ya bidhaa zinatakiwa kuthibitishwa kisheria kabla ya kuingia sokoni. Shughuli hii inalenga katika bidhaa za nyumbani japokuwa inaweza kutumika katika baadhi ya sekta mbalimbali. Wakati hii hujulikana kama ukaguzi; shughuli hii kwa ujumla ni upimaji unaoongoza kwenye uthibitisho wa kukubaliana. Ukaguzi pia hujumuisha shughuli za utafiti wa masoko kabla na baada ya uwepo wa bidhaa na ukaguzi wa mara kwa mara wa usimikaji wa mitambo/vifaa kwa ajili ya usalama. Kwa kawaida ukaguzi wa aina hii hutumika katika magari, kreni na vinyanyua vitu vizito, boila na vyombo vyenye mkandamizo (boilers and

191 Tathmini Ya Ulinganifu 181 pressure vessels). Kwa ujumla ukaguzi wa kisheria hufanyika katika usalama na usafi wa vyakula na vilevile baadhi ya shughuli za ukaguzi huhusishwa na shughuli za ushuru na forodha. Katika sekta ya utengenezaji/uzalishaji, ukaguzi, upimaji na uangaliaji vifaa vya upimaji ni chombo muhimu katika udhibiti wa uzalishaji. Hii inaweza kusababisha ukaguzi kwa vitendo wa bidhaa zilizo katika mchakato wa utengenezaji ili kufuatilia kuwa zinafaa/ni bora ( mf. Usafi) ili kuendelea na hatua nyingine. Idara ya ukaguzi inaweza pia kuwajibika na urekebishaji na udhibiti wa vifaa hadi kitakapokabidhiwa kwa mteja. Ukaguzi hutumika katika huduma za kisekta ili kubaini kukubalika kwake kiutendaji na viwango vya utoaji wa huduma. Hii inaweza kujumuisha utayari au kukubaliana na ukaguzi wa mtiririko wa mchakato na sifa /maelezoikiwa ni pamoja na muda unaofaa na unaotosheleza sifa za huduma nyingine. Katika utengenezaji bidhaa tata/ngumu au usimikaji wa bidhaa zisizokubalika inaweza kusababisha majanga kwa mteja.hili sio jambo la kawaida kwa wateja katika kushiriki kwenye mchakato wa ukaguzi wa uzalishaji mwingi au kuhusisha kutimiza azma yake. Katika hali hiyo hasa katika utengenezaji wa ndege na meli, wateja watakuwa makini zaidi na mifumo ya ukaguzi inayotumiwa na watengenezaji Ukaguzi kabla ya kusafirisha mara kwa mara unafanywa na mtengenezaji lakini pale ambapo bidhaa inasafirishwa nje ya nchi, ukaguzi wa ziada unaweza kuhitajika katika kituo cha mwisho kabla ya bidhaa kuondoka. Msamiati unaotumika mara kwa mara unajulikana kwa jina la Mkaguzi wa Mizigo (Cargo superintending). Shughuli hii haijumuishi ukaguzi wa bidhaa tu bali ufungashaji, ubebaji, ubora wa bidhaa na nyaraka zilizotumiwa. Kampuni inayosimamia mizigo inafanya kazi zake kama wakala wa mteja. Iwapo nchi zina bidhaa zilizotengwa kama za thamani kubwa lakini ni zinazoweza kuharibika wakati wa kusafirishwa au zinapokingwa na uharibifu sokoni, hapa serikali yenyewe hulazimisha ukaguzi kabla ya kusafirisha bidhaa. Huu ulikuwa mpango mkakati wa Japani kwa bidhaa kadhaa kama vile vifaa vya macho vyenye ubora wa juu. Australia nayo huhitaji cheti cha uthibitisho wa kuuza nje kwa ajili ya bidhaa zinazoharibika kwa haraka/baada ya muda mfupi. Mwisho kabisa mteja anaweza kutaka ukaguzi wa ziada katika kituo cha kupokelea bidhaa (katika nchi iliyoagiza bidhaa). Nchi kadhaa zinaamuru ukaguzi ili kuhakikisha watumiaji hawatadhurika na magonjwa kutokana na bidhaa zisizokuwa bora. Sheria hizi ni ngumu sana kwa nchi ambazo kwa ujumla hazina magonjwa ya wanyama na mimea kama vile Australia na New Zealand lakini pia nazo zinaweza kuweka sheria za dharura pale panapozuka magonjwa ya binadamu. Nchi zilizoagiza bidhaa zinaweza kuteua mashirika yao kama mawakala wa ukaguzi kabla mzigo haujaondoka au kufanya ukaguzi kabla mzigo haujaondoka ili kujiridhisha kwamba mzigo umekidhi vigezo/sheria za serikali. Wakati ambapo ukaguzi unaweza kuwa aina ya tathmini makubaliano ya zamani sana, imekuwa ya mwisho kuwekewa viwango vya kimataifa. Kuenea kwa matumizi ya ukaguzi katika viwanda vyote kumeiongoza Jumuia ya Ulaya kuweka kiwango cha ujumla cha EN Vigezo vya jumla kwa ajili ya kuendesha Bodi zinazofanya Ukaguzi. (EN General Criteria for the Operation of Various Types of Bodies Performing Inspection) Jitihada hizi zilifuatiwa na jumuia ya kimataifa pale ilipokubaliana na EN kama ISO/IEC 17020:1998, inayobeba wadhifa ule ule na kufanana na EN. Kwa hivi sasa Kiwango hiki kinatumiwa na bodi za kutoa vibali ili kutoa vibali kwa bodi za vibali katika nchi mbalimbali. Kiwango hiki hufafanua aina za bodi katika misingi ya kujitofautisha na vyanzo vingine vyenye ushawishi: Aina ya A. Bodi ni wale ambao hawahusiki moja kwa moja na usanifu/ubunifu, utengenezaji, utumiaji na utengenezaji wa vifaa vinavyokaguliwa; Aina ya B. Bodi zinaweza kuwa na mtumiaji na shirika linalogawa bidhaa lakini pia kujitenganisha na mzalishaji. Aina ya C. Bodi hizi zinafanana na zile za B lakini hazilazimishwi kujitenganisha na mzalishaji. Kukubalika kwa kiwango na bodi za ukaguzi umewekwa katika sekta ya biashara na huduma za ukaguzi zimekusudiwa kubakia katika mifumo ya kitamaduni. Katika nchi nyingi zilizoendelea shughuli za ukaguzi wa kibiashara zina matokeo makubwa katika katika sekta zote na kwa ujumla ni salama, humtosheleza mteja na zimetengenezwa katika kiwango cha juu cha ubora wa bidhaa. Vilevile kuna mwelekeo wa serikali, vyombo vyake vya sheria na mawakala wakubwa ya ununuzi kutafutahuduma za ukaguzi kutoka bodi za ukaguzi za biashara.

192 182 Tathmini Ya Ulinganifu KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Vigezo vya ukaguzi Anjoran, Renaud (Anjoran, Renaud. Quality Inspection Tips). Vyanzo vya Ushauri kwa Vitendo Asia mwezi Februari, (Practical Advice for Importers Sourcing in Asia. February 2010.) Hii inakupa mchoro mzuri wa aina nne za huduma bora za ukaguzi, ukaguzi kabla ya uzalishaji, ukaguzi wakati wa uzalishaji, ukaguzi wa sampuli chache na ukaguzi wakati wa kupakia katika konteina. Kubofya katika jina la kila huduma kutamfikisha msomaji kwenye taarifa zaidi za huduma hiyo. FAO/WHO. Codex Alimentarius Ukaguzi na uthibitishaji wa mufumo ya ukaguzi katika taarifa mchanganyiko 2005.ISBN (Food Import and Export Inspection and Certification Systems. Combined Texts ISBN ftp://ftp.fao.org/docrep/fao/008/y6396e/y6396e00.pdf Following the FAO/WHO Conference on Food Standards, Chemicals in Food and Food Trade in March 1991, the Codex Alimentarius Commission undertook the development of guidance documents for governments and other interested parties on food import and export inspection and certification systems. This guide includes texts up to International Accreditation Forum and International Laboratory Accreditation Cooperation. Guidance on the Application of ISO/IEC IAF/ILAC-A4: Mwongozo huu wa nyaraka unatengeneza msingi sawa wa kutambua mipangilio kati ya bodi ya kutoa vibali na kile kinachoitwa maombi ya mara kwa mara ya ISO/IEC Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO). Hutumia Orodha ya Ukaguzi ya Kudhibiti Ubora. Mwongozo huu mzuri unalenga matumizi ya orodha ya ukaguzi wa kuthibiti ubora. Uchunguzi wa kutumia na matumizi ya Huduma ya Ukaguzi kabla ya Kusafirisha. Mark Dutz. Waraka wa Benki ya Dunia namba.278. Benki ya Dunia, Washington, D.C Waraka huu unapitia ushahidi uliopo wa ufanisi wa huduma ya ukaguzi kabla ya kusafirisha katika maeneo matatu: Ukaguzi uliotolewa, ukusanyaji wa mapato na uwezeshaji wa biashara. Sakthivel, K. Mbinu Mbalimbali za Mifumo ya Ukaguzi wa Mavazi. Fibre 2 fashion. Mfano wa ukaguzi bora uliotumika katika viwanda vya nguo. MAREJELEO Shirika la Viwango la Kimataifa na Kamisheni ya Kimataifa ya Ki-Elektroniki (International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission). ISO/IEC 17020:1998, Vigezo vya jumla vya matumizi katika bodi mbalim bali za ukaguzi hupatikana kutoka ISO au wanachama wa ISO (angalia orodha katika na kutoka IEC au Kamitii za Kitaifa za IEC (orodha katika

193 Tathmini Ya Ulinganifu Kwa jinsi gani ukaguzi unahusika na aina nyingine za tathmini ya ulinganifu na ni nini nafasi yake katika biashara za kimataifa? Katika misamiati ya kifundi shughuli ambazo kwa kawaida hujulikana kwa mapana katika ukaguzi kutoka kile kinachoweza kutiwa lebo ya upimaji hadi uthibitishaji. Kwa upande mwingine mwisho wa wigo wa ukaguzi, bodi zitapima kile ambacho kingefanywa na maabara na ukaguzi huo utakuwa sehemu ya mpango wa uthibitishaji. Kwa urahisi zaidi, ukaguzi unajumuisha kuonekana kwa macho ambapo hata hivyo huhitaji utaalamu wa hali ya juu, ujuzi na uzoefu wa mkaaguzi. Kwa hali hii ukaguzi unaweza kuwa zana pekee ya uthibitisho na utoaji vyeti. Kama ilivyojadiliwa katika swali la 65, ukaguzi unajumuisha sehemu nyingi za tathmini ya ulinganifu lakini hutofautishwa na kiwango cha binafsi na maamuzi binafsi hufanywa katika hali mbalimbali. Je makala hii inafaa kwa shughuli hii? Ni salama? haya ni maswali ambayo yanahitaji takwimu (matokeo ya vipimo) na maamuzi ya mkaguzi mwenye ufahamu na uzoefu. Maswali kama haya vilevile yanawezesha mchakato wa maamuzi ya kutotoa au kutoa cheti cha kukubalika kwa uzao (batch) mmoja wa bidhaa au bidhaa binafsi au usimikaji/ufungaji mitambo. Kwa vile ukaguzi una mila zenye nguvu sana katika baadhi za nchi na katika baadhi ya sekta viwandani, kuna maoni tofauti katika nyaraka ambazo zinaitwa vyeti na zile nyaraka ambazo haziwezi kuitwa vyeti na ambazo zinaweza kuitwa ripoti tu. Kwa bahati mbaya zilizofichika sio wakati wote zitatambuliwa na sheria na mamlaka husika. Majibu ya swali la 66 yanathubutu kuchukua mtazamo wa kisayansi na kutambua tofauti zilizopo. ILAC na IAF kwa pamoja zimechapisha waraka (A4 2004) wa kuongoza ambao unazungumzia tofauti kati ya sehemu tatu za tathmini makubaliano. Katika mazingira ya biashara ukaguzi unatumika kudhibiti na kufuatilia sio mazingira ya ubora na ufundi tu kwa bidhaa za kuuzwa nje au bidhaa zilizoagizwa toka nje tu bali pia wingi, ufungashaji, ubebaji na taratibu (logistics). Kwa bidhaa zisizoharibika upesi, ukaguzi wa bidhaa zinazouzwa nje kwa kawaida zinajumuisha nyaraka za ukaguzi ili kuhakikisha kuwa bidhaa zilizotumwa ni sawa na zile zilizopokelewa zikiwa bora na salama. Katika hali hii ukaguzi kwa kawaida utakuwa wa kuona tu bila ya kupima Bidhaa zinazoharibika upesi huhusika na ukaguzi makini mno katika kituo cha mwisho cha kupeleka bidhaa nje ambapo mamlaka zinazohusika na uuzaji bidhaa nje na wateja wanahitaji kuhakikishiwa kuwa bidhaa zimesafirishwa vizuri/ipasavyo kutoka pale ilipozalishiwa au tengenezewa na kwamba bidhaa zilizopokelewa zinafaa kuuzwa. Hizi zinaweza kuhusisha baadhi ya uchunguzi utakaochaguliwa utakaohusisha kulingana na hali ya kibaiolojia ya bidhaa. Tena mchanganyiko wa ukaguzi unaweza kuwa wa kuchunguza na vipimo. Baadhi ya nchi zingine zina sheria kali sana katika matakwa ya karantini, kama ilivyoruhusiwa na Shirika la Biashara Duniani na Makubalianoya SPS (WTO SPS Agreement) na baadhi ya madaraja ya bidhaa wakati wote zinatakiwa kufanyiwa ukaguzi wa kina sana katika kituo cha kusafirishia bidhaa nje ambapo msisitizo wa kutokuwa na wadudu na magonjwa ambavyo vinaweza kusababisha matatizo makubwa mno katika kilimo kwenye nchi iliyoagiza bidhaa ma gonjwa ya mimea kama vile moulds and fungi. KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Shirka la Viwango la Kimataifa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Viwanda na Shirika la Viwango la Taifa. (International Organization for Standardization and United Nations Industrial Development Organization National Standards) Bodi katika Nchi Zinazoendelea (Bodies in Developing Countries) Hii inajumuisha kanuni kuu za uwekaji viwango katika taifa, kanda na katika ngazi ya kimataifa inaonyesha miundo ya vitu muhimu vya kuchagua ili kuwezesha mchakato katika ngazi ya taifa. Mchoro namba 1 (ukurasa wa 11) una mtazamo mzuri wa utaalamu wa vipimo/metrolojia, utoaji vibali, tathmini makubaliano, viwango na mifumo mizuri ya biashara vinahusiana. MAREJELEO: Kongamano la Kimataifa la Utoaji Vibali na Ushirikiano wa Maabara ya Kimataifa ya Utoaji Vibali. Muongozo katika maombi ya ISO/IEC IAF/ILAC-A4:

194 184 Tathmini Ya Ulinganifu 67. Jinsi gani ninaweza kupata kibali cha kuuza bidhaa nje chini sheria ya SPS? Sheria ya msingi ni kwamba bidhaa zinaweza kuuzwa nje kama zinakidhi mahitaji rasmi, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya SPS ya nchi inayoagiza bidhaa. Ni wajibu wa muuzaji wa bidhaa nje kuhakikisha kwamba bidhaa zinaendana na mahitaji husika, na kawaida hakuna haja ya kuingiliwa na mamlaka za nchi zinazouza bidhaa nje. Bidhaa nyingi haziihtaji kibali kuuzwa nje. Nchi inayoagiza bidhaa nje inaweza kuangalia bidhaa wakati zinapowasili kukagua iwapo zinaendana na viwango vya chakula vya ndani ya nchi, au hazina wadudu au magonjwa kabla ya kuruhusu kuingia. Ukaguzi huu mara nyingi hautambuliwi kama ni taratibu za kibali. Hatahivyo, katika matukio mengine, nchi zinazoagiza bidhaa nje zinaweka mahitaji ya ukaguzi wa bidhaa katika nchi zilipozalishwa kama sharti la kuingia katika masoko yao. Kwa mfano, nchi zinazoagiza bidhaa nje zinaweza kuweka bayana bidhaa kama nyama freshi zinazopelekwa katika masoko ya Ulaya na Marekani-inaweza kuwa imeelezewa kwa kina na utekelezaji wake unaweza kuwa chini ya ukaguzi unaofanywa na mashirika husika katika nchi inayoagiza bidhaa. Mara nyingi sheria za ukaguzi wa mwanzo, kabla ya kutoa bidhaa nje utahitaji mahitaji ya usajili wa kuanzisha bidhaa (kwa m.f. Machinjio na mitambo ya usindikaji samaki) ambapo kwa kufanya hivyo bidhaa zitakua na haki ya kuuzwa nje. Wakati mwingine, nchi zinazoagiza bidhaa zinaweza kuhitaji usafirishaji wa matunda na mbogamboga kuambatana na cheti cha afya ya mmea kilichotolewa na mamlaka za nchi inayouza bidhaa. Cheti ni lazima kionyeshe wazi kwamba bidhaa zimefanyiwa ukaguzi au ufukizaji ili kuhakikisha kuwa hakuna wadudu. Taarifa kuhusu mahitaji hayo inaweza kupatikana kutoka kwa mamlaka thabiti kwenye nchi inayotoa bidhaa nje. Inaweza pia kupatikana kutoka kwa balozi za nchi iliyoagiza bidhaa, au kutoka kwa mamlaka sahihi za nchi iliyoagiza bidhaa. Wakala wa kutangaza bidhaa nje pia anaweza kutoa msaada. Nchi zinazoagiza bidhaa nje zinaweza kuwaambia mashirika binafsi kufanya ukaguzi wa mwanzo kabisa kwa niaba yao au kibali cha bidhaa zilizoagizwa pamoja na mahitaji rasmi. Kwa mfano, cheti kinaweza kuhitajika kutoka kwa shirika huru kikieleza kuwa bidhaa za chakula zilizofika zimetimiza viwango vya chakula vya nchi iliyoagiza bidhaa. Katika hali kama hii, wauzaji bidhaa nje wanatakiwa kukutana na wakala wa shirika kupata taarifa kuhusu mahitaji maalum yanayohitajika. Kawaida, ada itatozwa kwa ajili ya ukaguzi na huduma za uthibitisho zilizotolewa na wathibitishaji huru. Chini ya Sheria ya Maboresho ya Usalama wa Chakula 2011 (Food Safety Modernization Act 2011), Utawala na Chakula na Madawa Marekani wana mamlaka ya kuhitaji cheti cha mkaguzi huru mwenye kibali cha chakula na vifaa kule vilipotoka, kutegemeana na aina, historia au kanda. Mashirika huru yanaweza kuwa serikali za kigeni au wakaguzi binafsi ambao wanatimiza mahitaji ya kibali. Baadhi ya nchi kama vile Australia zinatumia serikali zinazodhibiti bidhaa zinazouzwa nje, ambapo kwa bidhaa za aina nyingi kama vile matunda freshi na mbogamboga, kuuzwa nje hairuhusiwi kabisa isipokuwa tu mamlaka za nchi zinazoagiza chakula zikiwa zimepanga masharti maalum ya kuruhusu kwa kuzingatia uchambuzi wa hatari inayoweza kutokea. Katika mazingira kama hayo, itakua muhimu kwa serikali inayouza bidhaa nje kuomba mamlaka za nchi iliyoagiza bidhaa kuweka masharti maalum ambapo upenyo katika masoko unaweza kuwepo. Ushughulikaji wa utaratibu rasmi wa kibali uko chini ya masharti ya Kipengele cha nyongeza C cha mkataba wa SPS. Kwa kifupi, masharti yanahitaji udhibiti, ukaguzi na taratibu za kibali zinatakiwa kuwa wazi, za ufanisi na zisizosumbua kuelewa. Kwakua kufanyika kwa uchambuzi wa hatari kwa nchi inayoagiza bidhaa kunaweza kumaanisha kwamba mamlaka za nchi inayouza bidhaa zinatakiwa kukusanya na kusambaza data nyingi za kisayansi na nyinginezo kwa wenzao katika nchi inayoagiza bidhaa, maombi rasmi ya kupenya sokoni yanaweza kutumia rasilimali muhimu. Maombi hayo yanaweza kushuhudiwa na biashara nyingi sana za kuuza bidhaa nje, ikiwa matokeo mazuri yataafikiwa. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Bathan, Bates and Flordeliza Lantican. Economic Impact of Sanitary and Phytosanitary Measures on Philippine Pineapple Exports. Journal of ISSAAS vol. 15, No. 1, 2009, pp Kitabu hiki kinachambua athari za uchumi za hatua ya usafi na afya ya mmea juu ya mananasi yanayouzwa Filipino (Philippine pineapple exports) chini ya mkataba wa SPS wa WTO na katika uso wa mahitaji ya nchi zinazoagiza nje. Ministry of Agriculture, Government of India. Standard Operating Procedures for Export Inspection and Phytosanitary Certification of Plants/ Plant Products & other Regulated Articles. December Inatoa mwongozo wa shughuli za mfumo wa taifa wa uthibitisho wa bidhaa zinazouzwa nje- India na kuelezea taratibu rasmi za ushughulikaji wa taratibu za uthibitisho halali na kuaminika za afya ya mmea kwa ajili ya mali za bidhaa za mmea na bidhaa za mmea na makala zilizowekwa. Lengo ni kutimiza mahitaji ya afya ya mmea za nchi zinazoagiza bidhaa na wakati huohuo

195 Tathmini Ya Ulinganifu 185 kukamilisha wajibu wa kimataifa unaozingatiwa katika mkataba wa kimataifa wa kulinda (mmea International Plant Protection Convention) na mkataba wa WTO juu ya SPS. Neeliah, Shalini and others. Sanitary and phytosanitary issues for fishery exports to the European Union: A Mauritian insight. February Kinaelezea matokeo ya hatua za SPS kwenye biashara ya chakula ya Mauritius. Kitabu kinadai kwamba nchi inatakiwa ipitishe sio tu msimamo wa kiutendaji lakini pia ulio makini sana kulinda soko lake, kufahamu mara moja soko linalojitokeza na kulinda taswira yake kama muuzaji salama wa samaki nje. Strickland, Ella. EU Sanitary and Phytosanitary Standards. Uganda Maonyesho yaliyojadili soko la Ulaya na maana ya hatua za SPS kwa nchi zinazoendelea. Will, Margret and Doris Guenther. Food Quality and Safety Standards. As required by EU law and the Private Industry. A Practitioner s Reference Book. 2 nd ed. GTZ Kitabu cha marejeo kwa ajili ya mifumo ya usimamizi wa ubora wa chakula; kinajadili mahitaji ya soko ya kisheria na uzalishaji ndani ya Ulaya kwa ajili ya makundi ya bidhaa zilizochaguliwa kama vile matunda freshi na yaliyosindikwa na mbogamboga. MAREJELEO SPS: The Sanitary and Phytosanitary Export Database. US Food and Drug Administration. The New FDA Food Safety Modernization Act (FSMA). World Trade Organization. Sanitary and Phytosanitary Agreement Annex C.

196 186 Tathmini Ya Ulinganifu D. UHAKIKI 68. Nini maana ya uhakiki (au uthibitisho) wa bidhaa na namna gani unapatikana? Mambo ya msingi ya uthibisho wa bidhaa Uthibitisho wa bidhaa ni utaratibu ambao shirika la uhakiki linatoa ushahidi kwamba bidhaa, ama kwa makundi au uzalishaji endelevu, zimeshakaguliwa na kufanyiwa upimaji na wao na kwamba bidhaa kwa pamoja zinaendana na mahitaji maalum, mara nyingi yaliyopo kwenye kiwango. (tazama swali namba 13). Ushahidi wa shirika la uhakiki uko katika mfumo wa cheti pamoja na alama ya uthibitisho wa bidhaa ambayo mtengenezaji au mzalishaji anaambatanisha juu ya bidhaa baada ya kupatiwa leseni ya kufanya hivyo. Shirika la uhakiki kwa hivyo linatoa uhakika kuhusu ubora wa bidhaa. Huduma za uthibitisho wa bidhaa zinatolewa na mashirika mengi kote katika nyanja za umma na binafsi, kwenye ngazi za taifa na kimataifa. Katika nchi zinazoendelea, mashirika ya taifa ya viwango mara kwa mara yanatoa uthibitisho pekee wa bidhaa wa soko husika lolote. Katika nchi zilizoendelea, mashirika binafsi ya uthibitisho mara nyingi ndiyo muhimu zaidi kutokana na mtazamo wa soko. Uthibitisho wa bidhaa unakubalika tu zaidi katika soko la nyumbani la shirika la uthibitisho, lakini kuna machache yanafanikiwa kufanya shughuli zake kwenye ngazi ya kanda au hata ya kimataifa. Mifano ya kawaida ya alama za uthibitisho wa bidhaa ni BSI Kitemark (general products Uingereza), the SABS mark (general products Afrika kusini), the GS mark (product safety Ujerumani), the VDE mark (electrical and electronic equipment Ujerumani), the UL mark (product safety Marekani), the ASME mark (pressure vessels Marekani), the CSA mark (general products Canada), KEMA (electrical equipment the Netherlands) na AGMARK (agricultural products India), na nyingine nyingi zaidi. Inatakiwa kufahamika kwamba alama ya CE siyo alama ya uthibitisho wa bidhaa ila kifaa cha udhibiti cha Ulaya (tazama swali namba 58). Michakato inaweza kuthibitishwa kama inaendana na mahitaji yaliyotajwa ni kwa mujibu wa ufafanuzi wa bidhaa. Mchakato huo wa uthibitisho pia unachukuliwa kama uthibitisho wa bidhaa. Mfano ni uthibitisho wa utendaji bora wa kilimo au GAP. Mchakato wa uhakiki wa bidhaa Mchakato siku zote utajumuisha tathmini ya bidhaa, uwe umefanyiwa sampuli kiwandani, kwenye makundi au kutoka kwenye eneo la soko. Inaweza kujumuisha ukaguzi wa mchakato wa uzalishaji awali au kwenye msingi endelevu, au inaweza ikawa tu kupima ufuatiliaji katika soko. Kuendana na mifumo ya uongozi kama vile ISO 9001 (tazama swali namba 69) au HACCP kunaweza kuhitajika (tazama swali namba 46). Pale tendo la kuendana linapokuwa limeonyeshwa, mzalishaji anaweza kupewa leseni ya kuambatanisha alama ya uthibitisho wa bidhaa ya shirika la uthibitisho kwenye bidhaa au kwenye ufungaji au vyote, na hivyo kuashiria tendo la kuendana na viwango. Mchoro hapo chini unaonyesha kwa upana zaidi aina tofauti za uthibitisho wa bidhaa kama ilivyofafanuliwa katika ISO/IEC Muongozo namba 67. Ufafanuzi wa mfumo (ISO/IEC muongozo 67) Mfumo 1a na 1b Mfumo 2 Mfumo 3 Mfumo 4 Mfumo 5 Ukaguzi wa kikundi Upimaji wa ufuatiliaji kwenye soko Upimaji wa bidhaa katika kiwanda Upimaji wa aina/makundi pamoja na udhibiti wa bidhaa Upimaji wa aina pamoja na uhakikisho wa ubora ikijumuisha upelelezi wa soko Huduma Mfumo 6 Baadhi ya vyeti ni halali kwa kipindi maalum (kawaida mwaka mmoja), baada ya muda huo shirika la uthibitisho litafanya mapitio na kutoa cheti upya. Wengine hawana mipaka ya muda ili mradi tu mtengenezaji atimize mahitaji na kulipa ada ya mwaka ndipo cheti kinakuwa halali. Ni wazi, mtengenezaji anatakiwa kulipia mchakato wa uthibitisho. Malipo yatashughulikia upimaji wa bidhaa (wa awali na vipimo vya udhibiti baada ya leseni), ukaguzi wa awali na ufuatiliaji wa mchakato wa uzalishaji, ushughulikaji wa makosa yoyote yaliyoonekana wakati wa ukaguzi, ada ya mwaka ya leseni, n.k. Ada ya

197 Tathmini Ya Ulinganifu 187 leseni inaweza kuwa flati, lakini mara nyingi ina uhusiano na namba ya kiasi kilichozalishwa na alama. Ni vigumu sana kutoa taarifa juu ya bei ya kawaida ya uthibitisho wa bidhaa, na wazalishaji wanaombwa kupata taarifa mpya kwa wakati kutoka kwa mashirika husika ya uthibitisho. Utawala ya kidole gumba (a rule of thumb) uliothibitika kuwa na manufaa ni kwamba gharama ya jumla ya uthibitisho wa bidhaa kawaida itaongeza 1% mpaka 2.5% kwenye gharama ya kiwanda ya bidhaa. Mchakato wa uhakiki wa bidhaa Chanzo: Martin Kellermann, Afrika ya Kusini. Thamani ya uthibitishaji bidhaa Kwanini unahitaji uthibitisho wa bidhaa? baadhi ya sababu ni pamoja na: Mtengenezaji anahitaji kujenga sifa yake ili kupanua ushiriki/hisa zake za soko, kuzidisha upenyo kwenye masoko mapya, kuboresha ushindani, au kutangaza bidhaa mpya. Kuwasilisha maombi ya uthibitisho wa mapitio sahihi ya msambazaji kwa shirika la uthibitisho, Tathmini ya tendo la kuendana kwenye eneo, Upimaji wa sampuli ya bidhaa, Kitendo cha marekebisho na ukaguzi wake. Cheti

198 188 Tathmini Ya Ulinganifu Ukaguzi wa ufuatiliaji, Upimaji wa bidhaa kutoka kwenye uzalishaji, Kitendo cha marekebisho na ukaguzi wake, Utolewaji upya wa cheti baada ya miaka kadhaa Mnunuzi (m.f mtu binafsi, mwanahisa, mzalishaji, shirika la umma la ugavi, muagizaji bidhaa nje, msambazaji, mwajiri) anatamani kuwa na dhamana huru ya ubora wa bidhaa iliyonunuliwa. Katika baadhi ya nchi, alama za uthibitisho wa bidhaa zinachukuliwa kama ushahidi kwamba bidhaa zimetimiza kanuni za kiufundi au viwango vya lazima. Alama ya CSA (bidhaa za umeme Canada), alama ya ASME (pressure vessels Marekani), alama ya BIS (mitungi ya LPG India), alama ya TBS (viwango vya lazima Tanzania) ni mifano hai. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Agricultural Marketing Information Network (AGMARK) India. Inatoa taarifa kuhusu upangaji ubora wa AGMARK s na uthibitisho wa biashara ya nje na ndani, na vilevile katika kupanga ngazi ya bidhaa za kilimo. American Society of Mechanical Engineers (ASME), United States. BSI Kitemark, United Kingdom. Kitemark ni ile ya BSI, shirika binafsi lisilo la kutengeneza faida ambalo linajihusisha katika maendeleo ya viwango binafsi, vya kitaifa na kimataifa, tathmini na uthibitisho wa mifumo ya uongozi na vifaa vya madawa, upimaji na uthibitisho wa bidhaa na huduma, utolewaji wa suluhu za utawala, hatari na ulinganifu, na huduma za mafunzo. Bureau of Indian Standards (BIS). Canadian Standards Association (CSA). Geprüfte Sicherheit (GS) Mark, Germany. Geprüfte Sicherheit ( Tested Safety ) au alama ya GS ni alama ya uthibitisho wa hiari wa vifaa vya kiufundi. Inaonyesha kwamba vifaa vimefikia mahitaji ya kiusalama ya Ujerumani, kama yapo na Ulaya ya vifaa hivyo. Tofauti kuu kati ya GS na CE ni kwamba tendo la kuendana na mahitaji ya usalama ya Ulaya limefanyiwa vipimo na kukaguliwa na shirika lililopewa kibali (ambalo ni huru). Mashirika ya uthibitisho kadhaa, kama vile TUV, yanatoa alama ya GS. International Organization for Standardization and United Nations Industrial Development Organization. Building Trust The Conformity Assessment Toolbox. Geneva, Mtazamo mpana na wa kina wa aina zote mbalimbali za mifumo ya kufanya tathmini makubaliano iliyopo, faida zake, hatari na ukubalikaji katika eneo la soko. KEMA, Netherlands. South African Bureau of Standards (SABS). Tanzania Bureau of Standards (TBS). Underwriters Laboratories Inc. (UL), United States. Verband der Elektrotechnik Elektronik Informationstechnik (VDE), Germany. MAREJELEO International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC Guide 67:2004, Conformity assessment Fundamentals of product certification. Geneva Obtainable from ISO or ISO members (list at: and IEC or IEC National Committees (

199 Tathmini Ya Ulinganifu Ni nini maana ya uhakiki wa mfumo wa usimamizi? Mambo ya msingi ya uhakiki wa mfumo wa usimamizi Katika uthibitisho wa bidhaa, bidhaa inatolewa ushuhuda (tazama swali namba 68). Uthibitisho wa mfumo wa uongozi unashughulika na michakato na taratibu za mtengenezaji, mzalishaji, msambazaji au mtoaji huduma. Mfumo wa uongozi unaweza kufanyiwa tathmini dhidi ya mahitaji ya viwango husika na, kama ikigundulika unaendana vizuri huthibitishwa na shirika la uthibitisho. Hivyo mifumo hii miwili ya uthibitishaji ina tofauti kubwa moja. Katika uthibitishaji wa bidhaa, ubora wa bidhaa unashuhudiwa kuwa unaambatana na viwango maalum; mara kwa mara ni suala la msambazaji-mteja. Uthibitishaji wa mfumo wa usimamizi mara nyingi ni mahitaji ya biashara kwa biashara na kiwango cha bidhaa kinaweza kutofautiana kutoka kwa mteja mmoja hadi mteja mwingine. Ni suala tu la uwezo wa mtengenezaji kuambatanaa na mahitaji ya mteja yanayofanyiwa tathmini na sio ubora wa bidhaa pekee. Mfumo wa uthibitisho wa uongozi unaojulikana sana unaegemea kwenye ISO 9001, ambapo zaidi ya vyeti milioni moja vimetolewa duniani kote tangu kuanzishwa kwake mwishoni mwa mwaka 1980s. Orodha ya viwango vingine vya kimataifa vya ISO vinatumika kwa ajili ya uthibitisho wa mfumo wa uongozi, na vilevile orodha inayoongezeka ya viwango binafsi (tazama swali namba 14 na 52). Baadhi ni muhimu katika sekta maalum za uchumi; vingine ni vya ujumla sana katika utumiaji wake. Baadhi ya mifumo muhimu sana ya uthibitisho wa uongozi imeonyeshwa kwenye mchoro hapo chini. Orodha sio kubwa, na wasambazaji watahitaji kujua ipi ni muhimu kwa sekta zao na kwa zilizotajwa au soko halisi lililolengwa. NGAZI SEKTA KIWANGO Viwango vya kimataifa Vifaa vya tiba ISO 13485:2003 Magari ISO/TS 16949:2009 Usalama wa chakula HACCP ISO 22000:2005 Usalama wa habari ISO/IEC 27001:2008 Usalama wa usimamizi wa mnyororo ya ugavi wa huduma za Tekinohama(IT) ISO/IEC ISO 28000:2007 Mafuta ya petrol na gesi ISO 29001:2003 Viwango binafsi Masuala ya anga AS 9100 Usalama wa chakula na ukulima wa bustani British Retail Consortium GLOBALG.A.P. FSSC Wajibu kwa jamii SA 8000 Mawasiliano kwa simu TL 9000 Afya na usalma kazini OHSAS Viwango vingi ni dhahiri na mfumo mmoja wa uhakiki wa usimamizi unatumika duniani kote. Ubaguzi unatokea katika sekta ya chakula na maua ambapo kuna orodha nyingi ya viwango vinavyotumika. HACCP ndiyo ya asilia na ambayo imetengenezwa kama hitaji la lazima na nchi nyingi sana na maeneo, ikiwa ni pamoja na Ulaya, Canada, Afrika ya Kusini na Marekani. Baada ya hapo, mashirika ya uchuuzi ya Ulaya na Uingereza yaliboresha matoleo yao ya usalama wa chakula katika GLOBAL.A.P. na BRC kwa pamoja. ISO imechapishwa ili kuoanisha mahitaji ya mifumo ya usimamizi wa usalama wa chakula (tazama swali namba 44) na ISO Hata hivyo, kwa kuangalia ukweli kuwa mambo kadhaa ya usalama wa chakula yanahitaji kuwekewa msisitizo, viwango vipya binafsi, FSSC 22000, vimeboreshwa. (tazama swali namba 51). Mchakato wa uthibisho Mchakato wa uthibitisho unaoanishwa katika viwango vya ISO/IEC (angalia swali namba 75). Linatoa mchakato wa hatua mbili. Hatua ya kwanza ya ukaguzi wa shirika la ukaguzi ni pamoja na upitiaji wa nyaraka na inatoa mwelekeo wa kupanga hatua ya pili ya ukaguzi. Kutokana na mifumo mingi ya uongozi, inapendekezwa kuwa angalau sehemu ya hatua ya kwanza ya ukaguzi ifanyike katika jengo la mteja. Pale hatua ya pili ya ukaguzi inapokuwa imefanikiwa kuisha na makosa yote yamerekebishwa na

200 190 Tathmini Ya Ulinganifu kuthibitishwa kuwa ni hivyo, cheti ambacho ni halali kwa miaka mitatu hutolewa. Kipindi cha miaka mitatu ya uhalali, ukaguzi wa ufuatiliaji hufanyika, kawaida mara moja kwa mwaka. Baada ya miaka mitatu, shirika la uthibitisho linatakiwa kutathmini upya utendaji wa shirika. Kama mfumo mzima unaenda sawasawa kikamilifu, cheti kingine cha miaka mitatu ijayo hutolewa. Kwa nini kuthibitishwa? Uthibitisho wa mfumo wa uongozi, hasa wa ISO 9001, unaonekana kama ni wa kwanza unaotakiwa kuendana nao ili kupata kukubalika katika soko, yaani inafungua mlangokwa majadiliano zaidi ya biashara. Uthibitisho wa ISO 9001 hautoi dhamana kwa biashara yoyote, lakini pasipo hiyo unaweza kupata wakati mgumu kuwashawishi wateja muhimu ambao unaweza kuwapelekea bidhaa zenye ubora unaofaa. Hali hii inasaidiwa na ukweli kwamba mashirika ya kimataifa kama vile Jukwaa la kimataifa la kibali (International Accreditation Forum (IAF) lina mtazamo bora juu ya mfumo wa kibali kwa mashirika ya uthibitisho, kupelekea kukubalika kwa vyeti duniani katika eneo la soko na kwa wingi na mamlaka za udhibiti (tazama swali namba 87). Hii ni habari njema kwa mashirika yaliyothibitishwa, kwasababu ni dhahiri kwamba mfumo wa uongozi unakaguliwa mara moja, kuthibitishwa mara moja na kukubalika mahali popote. Baadhi ya mifumo mingine ya uthibitisho wa uongozi ni muhimu sana ikiwa utapenda kuwa mshindani katika masoko ya kisasa. Mifano hai ni sekta za chakula na maua za Ulaya ambapo cheti cha GLOBAL.A.P. na BRC ni muhimu ikiwa utahitaji kusambaza kwa makundi makubwa ya uchuuzi/rejereja. Uthibitisho wa HACCP utakusaidia kuthibitisha tendo la kuendana na kanuni za usalama wa chakula za nchi nyingi. Mfano mwingine mzuri ni uthibitisho wa ISO/TS katika sekta ya magari ikiwa utahitaji kusambaza vifaa asilia kwa watengenezaji katika dunia iliyoendelea. Utekelezaji wa mifumo ya uongozi/usimamizi kama vile ISO 9001 unahimiza udhibiti thabiti wa michakato ya uzalishaji na mengine. Hii hupelekea utambuzi bora wa alama, kupungua kwa urejeshaji na wateja, kupunguzwa kwa gharama za hati, kuongezeka kwa uzalishaji na gharama za uzalishaji kwa ujumla. Kwa kuongezea kwenye mamlaka ya soko au serikali za udhibiti zinazohitaji uthibitisho wa uongozi, baadhi ya wasambazaji wanaona uthibitisho kama tuzo kwa ajili ya kutekeleza nidhamu ambayo inapelekea faida zote zilizoorodheshwa hapo juu. Wasambazaji hao mara nyingi wana mbinu bora kwenye mifumo ya uongozi na kufaidika zaidi kwasababu wanafanya hivyo kwa msukumo binafsi na sio kwa kulazimishwa. Gharama ya uthibitisho Uthibitisho wa mfumo wa uongozi ni biashara kubwa duniani kote. Kwa sababu hiyo inavutia mashirika ya aina zote yanayotoa huduma ya uthibitisho kutoka kwenye mashirika ya gharama ndogo sana na sio mazuri sana, mpaka kwa mashirika yenye gharama ya juu na yenye utaalam wa hali ya juu. Uthibitisho pekee unaotakiwa kuzingatia ni ule wa kutoka kwenye shirika la uthibitisho lililopewa kibali na mwanachama wa shirika la kimataifa la mpango wa kuheshimu utambuzi (multilateral arrangement of mutual recognition). Mashirika ya uthibitisho ambayo hayajapewa kibali yanaweza kutoa huduma kwa gharama ya chini lakini, lakini mara nyingi pia wanafuata utendaji wa biashara unaohitajika kama vile kutoa huduma ya ushauri kuboresha uongozi wako au utunzaji kumbukumbu bora, kutekeleza mfumo na kuthibitisha katika muda mfupi sana. Uthibitisho huo unaweza usikubalike kwa wanunuzi. Njia bora ni kupata tamko kutoka kwa mashirika kadhaa ya uthibitisho yenye sifa bora yanayofanya shughuli zake katika soko lako (tazama swali namba 7 juu ya kuchagua shirika la uthibitisho). Mashirika mengi ya uthibitisho yatatoza ada ya maombi, ada kwa ajili ya ukaguzi unaojitosheleza, na gharama kubwa kiasi cha ada kwa ajili ya tathmini ya uangalia kama unaendana sawasawa kwenye eneo, kwakuwa hii itahusisha wakaguzi wa kutosha na wabobeaji ambao watahitaji kutumia muda kwa matakwa yako. Hivyo ndivyo inavyofanyika pia kwenye ukaguzi wa makosa. Pale utakapothibitishwa, utatakiwa kulipa ada ya uthibitisho ya mwaka ambayo ni pamoja na shughuli za ukaguzi wa ufuatiliaji. Zoezi la kurudiwa uthibitisho baada ya miaka mitatu litatozwa pekeyake. Baadhi ya mashirika ya uthibitisho kama vile mashirika ya viwango vya taifa yana mipango maalum kwa ajili ya SMEs katika nchi inayodadisi kutoka kwenye nchi zenye ukaribu nawe. Katika baadhi ya nchi, serikali zinatoa vifuta jasho kwa SMEs kuthibitishwa na kurudisha asilimia ya ada ya uthibitisho pale utakapopata uthibitisho, na malipo ya ziada kubaki na uthibitisho kwa kipindi cha miaka mitatu. SMEs pia wanatakiwa kufanya udadisi na wizara yao ya biashara. Wakati mwingine mipango/miradi hii hufanywa na shirika la kutangaza/kukuza biashara kwa niaba ya serikali.

201 Tathmini Ya Ulinganifu 191 KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization. The integrated use of management system standards. 1 st ed Inayapa mashirika miongozo ya namna ya kuingiliana na mahitaji ya ISO mbalimbali au viwango vya mifumo ya uongozi isiyo ya ISO na mfumo wa uongozi wa mashirika yao. International Organization for Standardization and United Nations Industrial Development Organization. Building trust The Conformity Assessment Toolbox. Geneva, The handbook can also be downloaded as a PDF file free of charge from the ISO ( and UNIDO ( Websites. Mtazamo mpana na wa kina wa mifumo yote ya aina mbalimbali za tathmini makubaliano iliyopo, faida zake, hatari, na kukubalika kwake katika soko. MAREJELEO BRC Global Standards. GLOBALG.A.P. ISO/TS 16949: Quality management systems Particular requirements for the application of ISO 9001:2008 for automotive production and relevant service part organizations. Obtainable from ISO or ISO members (list at

202 192 Tathmini Ya Ulinganifu 70. Ni vigezo gani vinavyotumika kuchagua mashirika ya uhakiki wa bidhaa? Kuchagua shirika la uthibitisho sahihi kunahakikisha ushirikiano mzuri kwa kipindi kirefu. Hivyo Mbinu iliyoundwa kwenye mchakato wa uchaguzi ni muhimu sana. Baadhi ya maswali muhimu yanayoweza kukusaidia katika mchakato wa uchaguzi yameelezewa hapa chini. Tazama pia swali namba 71 juu ya uchaguzi wa mfumo wa mashirika ya uthibitisho kwakuwa vigezo vingi vitakuwa vinafanana sana. Je, shirika la uthibitisho lina kibali? Maswali unayotakiwa kujiuliza mwanzoni kabisa ni: Je, shirika la uthibitisho limepewa kibali kwa ajili ya viwango ambavyo vimepelekea kuhitaji uthibitisho, na kama ni hivyo, na shirika gani la kibali? Je, shirika hilo la kibali liko chini ya mpango wa kimataifa wa kuheshimu utambuzi (multilateral recognition arrangement (MLA) unaosimamiwa na shirika kama vile Jukwaa la kimataifa la kibali (International Accreditation Forum (IAF)? Je,shirika la uthibitisho lina kibali chenye wigo mpana ambao unashughulikia bidhaa za kampuni yako? Kwa ujumla, kwa uthibitisho wa bidhaa (tazama swali namba 68), shirika la uthibitisho linatakiwa kupewa kibali na shirika la kibali ambalo liko chini ya IAF MLA husika. Linatakiwa pia kupewa kibali cha wigo sahihi wa bidhaa zako kwa ISO/IEC muongozo namba 65 (kubadilishwa na ISO/IEC mwaka 202). Hatahivyo, kuna miradi ya uthibitisho wa bidhaa, hasa ile yenye sifa nyingi za kimataifa, kwa ambayo mashirika ya uthibitisho wa bidhaa yamekubalika au kutambuliwa na mashirika ya kimataifa yanayodhibiti miradi hiyo, kwa mfano: Miradi mbalimbali ya tathmini makubaliano ya IEC, kama vile miradi ya IECEE CB, IECX na IECQ schemes (tazama swali namba 73). Cheti cha msingi cha mradi wa OIML Orodha na mawasiliano ya mashirika ya uthibitisho yanayotambulika kwa ajili ya miradi hii yanapatikana kwenye tovuti za mashirika ya kimataifa yenye mamlaka. Aina zinatofautiana kutoka mradi mmoja hadi mwingine, na itakua sahihi kujua wao ni kitu gani kabla ya kuanza mpango wa kuendana sawasawa na mahitaji yao. Je, soko linatambua alama za uthibitisho wa bidhaa? Baadhi ya alama za uthibitisho wa bidhaa zimepata nafasi kubwa na bidhaa zinazobeba alama hizo zinatambulika kama zenye thamani nzuri ya pesa au kama bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na wanunuzi katika masoko mengi. Hii ni kweli hasa katika masoko ya nyumbani ya mashirika makuu ya uthibitisho wa bidhaa kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, hivyohivyo katika masoko nje ya nchi. Kwa hivyo ni muhimu kupata taarifa husika kwa kuzingatia hili (tazama swali namba 72 na 74). Baadhi ya alama za uthibitisho wa bidhaa zimekubalika na soko katika masoko makubwa zaidi. Taarifa hii inaweza kuwa na thamani katika kupata hisa/ushirika wa soko pale ambapo soko bado halitambui majina ya alama ya bidhaa za kigeni, hususani ikiwa mtengenezaji sio maarufu au ni mgeni kwenye soko. Je, mamlaka za udhibiti zinatambua alama za uthibitisho wa bidhaa? Ikiwa una bidhaa unayotaka kuingiza sokoni katika wigo wa kanuni za kiufundi, na unahitaji uthibitisho kwa ajili ya bidhaa yako au mchakato, basi ni lazima uhakikishe kwamba uthibitisho wa bidhaa uliotolewa na shirika la uthibitisho ulilochagua unakubalika kwenye mamlaka za udhibiti katika soko unalolenga. Kuna njia nyingi ambazo hili limepangiliwa katika masoko tofauti na mamlaka tofauti: Shirika la uthibitisho linahitaji kupata kibali. Shirika la uthibitisho linahitaji kupewa kibali na kutambuliwa, kuteuliwa au kufahamika na mamlaka, m.f mashirika yanayofahamika kwa Miongozo mipya ya Ulaya (EU New Directives) (tazama swali namba 56).

203 Tathmini Ya Ulinganifu 193 Shirika la uthibitisho linatakiwa kuwa mwanachama mshiriki wa mradi/mpango wa kimataifa wa uthibitisho, kama vile baadhi ya mipango ya IEC na OIML (tazama swali namba 73). Shirika la uthibitisho linatakiwa kuteuliwa maalum na mamlaka husika za udhibiti. Mamlaka hizi zinakubali tu uthibitisho wa bidhaa kutoka kwa mashirika ya taifa ya uthibitisho wa bidhaa yaliyoainishwa katika kanuni au tawala nyingine. Shirika lolote la uthibitisho lenye sifa nzuri litakubalika. Itagharimu kiasi gani? Miradi ya uthibitisho wa bidhaa inatofautiana sana katika jinsi inavyofadhiliwa. Katika kesi nyingine, kuna ada ya mwaka kutegemeana na uzalishaji halisi ambao utajumuisha alama ya uthibisho wa bidhaa; ada hii inajumuisha pia shughuli zote za ufuatiliaji na upimaji wa baada ya cheti. Kwa wengine, hizi zinatakiwa kulipiwa tofauti. Wengine wana malipo ya msingi ambayo ni huru na uzalishaji pamoja na ada iliyohesabiwa kutoka kwenye gharama za uzalishaji. Unatakiwa kufahamu gharama zote, na mara kwa mara kuuliza kuhusu viwango vya wakaguzi, ada ya maombi, gharama ya sera (m.f. kusafiri na per diem), ada ya ukaguzi wa ufuatiliaji, malipo ya upimaji, malipo ya uthibitisho, malipo ya ufuatiliaji wa masahihisho ya makosa, na malipo ya kurudia uhakiki. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Electrotechnical Commission. Tovuti inaelezea kanuni kuu za mifumo ya tathmini makubaliano za IEC, zinazoitwa unyofu, uwazi na wajibu wa kuheshimu utambuzi ( openness, transparency and obligatory mutual recognition). Ina maelezo kuhusu sera, taratibu, tathmini rika, utawala wa miradi/mipango na majukumu nchi shiriki. International Organization for Standardization. ISO and conformity assessment, Utangulizi wa faida za tathmini makubaliano kwa wasambazaji, wateja na wadhibiti, na kwa biashara kwa ujumla. MAREJELEO International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission ISO/IEC Guide 65: 1996, General requirements for bodies operating product certification systems. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at ISO/IEC DIS Conformity assessment Requirements for bodies certifying products, processes and services. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at International Organization of Legal Metrology. OIML Certificate System for Measuring Instruments.

204 194 Tathmini Ya Ulinganifu 71. Vigezo gani vinatumika kuchagua mashirika ya kuhakiki mifumo ya usimamizi? Kuchagua mfumo bora zaidi wa uongozi wa shirika la uthibitisho kunahakikisha ushirikiano wenye thamani kwa kipindi kirefu. Kwahiyo mbinu iliyoundwa vizuri kwenye mchakato wa uchaguzi ni muhimu sana. Baadhi ya maswali yanayoweza kukusaidia katika mchakato wa uchaguzi yametolewa chini. Tazama pia swali namba 70 juu ya uchaguzi wa mashirika ya uthibitisho wa bidhaa, kwakuwa vigezo vingi vitakuwa na msingi sawa. Je, shirika la uhakiki lina kibali (ithibati)? Maswali matatu unayotakiwa kuuliza mwanzoni ni: Je, shirika la uthibitisho limepewa kibali kwa ajili ya viwango ambavyo vimepelekea kuhitaji uthibitisho, na kama ni hivyo, ni shirika gani la kibali? Je,, shirika hilo la kibali liko chini ya mpango wa kimataifa wa kuheshimu utambuzi (multilateral recognition arrangement (MLA) linalosimamiwa na shirika kama vile Jukwaa la kimataifa la kibali (International Accreditation Forum (IAF)? Je, shirika la uthibitisho lina kibali chenye wigo mpana ambao unashughulikia mifumo au michakato ya kampuni yako? Mashirika ya uthibitisho yanayotoa uthibitisho wa mfumo wa uongozi (tazama swali namba 69) yanatakiwa kupewa kibali kwa ISO/IEC na shirika la kibali lililoko chini ya IAF MLA husika. Wigo wao wa kibali unatakiwa kujumuisha viwango ambavyo kupitia hivyo unahitaji kupata uthibitisho, m.f. ISO 9001, ISO 14001, ISO 22000, HACCP, GMP. Unatakiwa pia kuangalia ISO 9001, kwa mfano, kama wigo wao wa kibali unajumuisha sekta ya biashara, m.f. kilimo na uvuvi, bidhaa za chakula na vinywaji, bidhaa za nguo, bidhaa za karatasi, uzalishaji, usafiri na kuhifadhi. Kwa miradi ya uthibitisho wa sekta maalum mbalimbali au viwango binafsi, shirika la uthibitisho linatakiwa kuthibitishwa au kutambuliwa, kwa mfano: Kwa GLOBALG.A.P. na viwango vya BRC, shirika la uthibitisho lililopewa kibali na GLOBALG.A.P. na BRC kwa ajili ya wigo wa sughuli zako, m.f. bidhaa za chakula, usafiri na hifahi au maua. Kwa kiwanda cha magari (ISO/TS 16949), shirika la uthibitisho chini ya mkataba na International Automotive Task Force (IATF). Orodha ya mashirika ya uthibitisho yaliyopewa kibali au yenye mkataba na mashirika haya ya udhibiti yanaweza kupatikana katika website zao husika. Je,, soko linatambua shirika la uthibitisho? Ikiwa shirika la uthibitisho lina majina mazuri maarufu katika orodha yake ya mashirika yaliyothibitishwa, hii inaweza kuwa dalili nzuri. Shirika la uthibitisho linalojiamini katika shughuli zake halitapinga kukuweka kwenye uchaguzi wa wateja wake kwa ajili ya maoni juu ya utendaji wake. Kama shirika la uthibitisho linafanya kazi katika nchi nyingi itakuwa ni vizuri zaidi, hasa ikiwa unazingatia msimamo wake katika masoko ya nje yanayokuvutia. Pia upendeleo wa wanunuzi wakuu hautakiwi kupuuziwa. Je, shirika la uthibitisho linaweza kutoa huduma jumuishi? Mahitaji ya uthibitisho wako yanaweza kuwa mbalimbali, ama sasa au kipindi kijacho. Baadhi ya mashirika ya uthibitisho yanaweza kutoa huduma ya uthibitisho jumuishi, yaani mfumo unaojumuisha uthibitisho wa uongozi bora na uthibitisho wa usimamizi wa mazingira na au afya na usalama na au usimamizi wa hatari, na hata uthibitisho wa bidhaa. Kama unahitaji hili katika kazi zako, itapelekea ukaguzi bora wa gharama na wenye ufanisi. Je, shirika la uthibitisho ni makini kwenye mahitaji ya wajasiriamali wa wastani na wadogo? (SMEs?) Ni muhimu kwa shirika la uthibitisho kutambua vikwazo na utendaji wa kazi ambao ni wa kipekee kwa SMEs na kuzingatia hayo.

205 Tathmini Ya Ulinganifu 195 Kufanya uchaguzi Wakati wa kuchagua shirika la uthibitisho, unatakiwa kuzingatia yafuatayo: ufanisi, kukubalika sokoni, sifa bora na gharama. Unatakiwa pia kuchagua shirika ambalo liko tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na wewe. Baada ya kuchagua shirika la uthibitisho, fanya juhudi kuwapa maoni yako na wengine. Wengi watashukuru na kujifunza kutokana na maoni yako. Itagharimu kiasi gani? Gharama inaweza kutofautiana kwa sababu ya ushindani katika mashirika mengi ya uthibitisho. Kuhakikisha kuwa unapata huduma bora ina maana unahitaji kutathmini vigezo na sio kuzingatia unafuu wa gharama. Unatakiwa kufahamu gharama zilizojificha, na mara kwa mara kuuliza kuhusu viwango vya wakaguzi, ada ya maombi, gharama za sera (e.g. usafiri na per diem), ada ya ukaguzi wa ufuatiliaji, malipo ya upimaji, malipo ya uthibitishaji, malipo ya ukaguzi wa kufuatilia masahihisho ya makosa, na malipo ya kurudia uthibitisho. Mashirika ya uthibitisho yenye sifa nzuri kawaida yapo wazi kuhusu malipo yao, na unatakiwa uweze kupata makadirio ya kina ya gharama zao ambazo zinategemeana na utata na kiwango cha kazi yako. Hii inamaana kwamba unaweza kuhitajika kukamilisha idadi ya maswali ili kupata tamko rasmi. Hii ni muhimu ili shirika la uthibitisho liweze kupata makadirio mazuri ya kazi zako pasipo kutembelea majengo/mahali unapofanyia kazi. Mashirika mengi ya uthibitisho yatatuma mwakilishi kwenye eneo lako. Shirika lenye sifa nzuri halitakuwa na hofu ya kupuuza kazi kama ipo nje ya eneo lake la ufanisi au wigo wa kibali. Linaweza hata kupendekeza shirika lingine sahihi zaidi kwa mahitaji yako. Pengine, linaweza kukupa makadirio ya muda utakaotumika kupanua wigo wake wa kibali ipasavyo. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Automotive Task Force (IATF). Habari zinazohusu IATF, ofisi zake angalizi,mashirika ya mapatano, sanctioned auditor training, sanctioned interpretationsof ISO/TS and OEM customer-specific requirements. International Organization for Standardization. ISO and conformity assessment, Inatoa utangulizi wa faida za tathmini makubaliano kwa wasambazaji, wateja na wadhibiti, na kwa biashara kwa ujumla.

206 196 Tathmini Ya Ulinganifu 72. Je, uhakiki niliopata utakubalika katika nchi nyingine? Kwa ujumla, kukubalika kwa uthibitisho wa bidhaa bado una mipaka kwenye nchi ya makazi ya shirika la uthibitisho ingawa baadhi ya miradi imeanza kupanuka kibara na hata kimataifa, mazingira mazuri zaidi yanapatikana kwa usimamizi wa mipango ya uthibitisho. Vyeti vya ISO 9001 na ISO kutoka kwa mashirika ya uthibitisho yenye kibali hukubalika zaidi. Hali ni tofauti pia kwa bidhaa zinazoangukia ndani ya wigo wa kanuni za kiufundi au hatua za SPS. Mashirika machache yametajwa chini, ila ni lazima kufanya uamuzi kutokana na soko unalonuia iwe cheti chako kinatambulika au laa. Mikataba/mapatano ya kuheshimu utambuzi -Mutual recognition agreements (MRA) Wakati wa majadiliano kati ya nchi na/au vitalu vya biashara, mipango ya utambuzi au mikataba ya kuheshimu utambuzi ya mifumo ya uthibitisho, hasa kwa ajili ya madhumuni ya udhibiti inaweza kuwekwa saini na pande zote za majadiliano. Mifano miwili ni mkataba wa kuheshimu utambuzi wa alama za uthibitisho wa bidhaa za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika Mashariki na Jukwaa la dunia la kuoanisha kanuni za magari za Umoja wa mataifa za tume ya uchumi ya Ulaya. [WP 29 World Forum for Harmonization of Vehicle Regulations of the United Nations Economic Commission for Europe (UNECE)]. Mipango (ya hiari) ya vyama vya ushirika Mashirika ya uthibitisho ya ndani na ya kigeni yanaweza kujiunga na mipango ya hiari ya utambuzi. Inaweza kujumuisha mipango katika mashirika ya vibali, maabara binafsi na mashirika ya ukaguzi. Mipango hiyo imekuwepo kwa miaka mingi na imekuwa ikiboreshwa kwa ajili ya manufaa ya biashara za washiriki. Serikali na mamlaka ya udhibiti imetambua baadhi ya mipango hiyo kwenye wigo wa udhibiti kama msingi wa kukubali matokeo ya jaribio/vipimo na shughuli za uthibitisho katika sekta mama. Mfano ni Tume ya Kimataifa ya Kielektoniki ya mfumo wa kupima mfuatano na kuthibitisha vifaa vya umeme na vya kielektroniki. (The International Electrotechnical Commission s system for conformity testing and certification of electrical and electronic equipment.) IEC inasimamia mifumo mitatu, ambayo ni IEC CBmpango/utaratibu wa kuheshimu utambuzi wa ripoti za vipimo na vyeti kuhusiana na usalama wa umeme na vipengele vya elektroniki. The IEC EE- mpango/utaratibu unaohusu vifaa vya umeme; na; The IECXmpango/utaratibu wa vifaa vitakavyotumika katika mazingira ya kulipuka. Haya ni makubaliano ya kimataifa kati ya mashirika ya uthibitisho na nchi zinazoshiriki.mtengenezaji anayetumia utaratibu wa IEC CB wa ripoti za vipimo anaweza kupata cheti cha uthibitisho wa bidhaa kwenye nchi nyingine nyingi ambazo ni washiriki wa utaratibu huo. Tazama swali namba 73 kwa maelezo zaidi. Mfano mwingine ni mpango/utaratibu wa OIML kwa ajili ya majaribio ya kupima vifaa va umeme. Ripoti ya vipimo kutoka kwa maabara inayotambulika na OIMTL inaweza kukubaliwa na mamlaka za kisheria za utaalam wa vipimo kwenye nchi nyinginezo ambazo zinashiriki katika utaratibu au mpango huu. (tazama swali namba 73). Kibali(Ithibati) Mashirika ya vibali yamekuwa yakifanya juhudi kuelekea kukubalika kimataifa kwa ripoti za vipimo na vyeti kutoka kwa mashirika ya vibali kwa miaka mingi. Hii imetokea kwa mitandao ya kimataifa inayosimamiwa na IAF (mifumo ya uongozi) na ILAC (maabara). Mashirika haya ya kimataifa yameasisi na kusimamia mipango ya kimataifa ya utambuzi kwa ajili ya sekta/vitengo wanavyoviwakilisha (tazama swali namba 91), ambapo kila mshirika hana budi kutambua vyeti vinavyotolewa na nchi nyinginezo ndani ya mfumo na kwamba viko sawasawa na vile vinavyotolewa na nchi husika au hata udhibiti wa ndani. Kwa ujumla hii hutokea zaidi ndani ya nchi za Ulaya, Australia, New zealand na Afrika ya kusini tofauti na China, India na Amerika ambapo bado hawajawezeshwa kikamilifu, vilevile maabara yaliyoteuliwa na mashirika ya uthibitisho bado ni wa kawaida sana. Kwa upande mwingine, kuna ongezeko kubwa la kukubalika kwa majibu ya vipimo na vyeti kutoka kwa watoa huduma za vibali wa kimataifa. Uteuzi wa serikali Serikali au mamlaka ya udhibiti inaweza kuteua/kutaja maabara na mashirika ya uthibitisho wanayoyaamini, ikiwa ni pamoja na mashirika ya nje ya mipaka yao kufanya vipimo na uthibitisho kuhusiana na kanuni za kiufundi pamoja na vipimo vya SPS. Kwa mfano, Ulaya imeteua maabara ya vipimo

207 Tathmini Ya Ulinganifu 197 vya shirika la viwango la kusini mwa Afrika kufanya vipimo vyote muhimu vya bidhaa za samaki zinazotoka katika eneo hilo ili kupelekwa kwa ajili ya soko la Ulaya. Uteuzi ulikua ni desturi kwa miaka mingi iliyopita, na zaidi ilikua ni maabara za serikali zilizokuwa zikichukuliwa kuwa na zina uwezo wa kweli kwa msimamo au nafasi yao. Hali hii inabadilika taratibu, na kibali kinaitajika zaidi na zaidi kwakuwa inatambulika kuwa uwezo au umahiri unachumwa/unapatikana kwa kufanya bidii na si kutolewa na sheria. Utambuzi wa nchi moja moja Serikali au mamlaka za udhibiti zinaweza kwa upande mmoja mmoja kutambua matokeo ya tathmini makubaliano ya mashirika ya kigeni. Shirika la tathmini makubaliano linaweza kupata kibali kimataifa, au kuonyesha umahiri wake kupitia njia nyinginezo hata kwa kutumia utamaduni wa muda mrefu au kutoa matokeo ya kuaminika. Njia hii hutumika mara kwa mara na nchi zinazoendelea kiuchumi, ambapo mamlaka ya udhibiti itatambua kwa urahisi matokeo ya vipimo na vyeti kutoka kwa maabara maarufu au za serikali na mashirika ya uthibitisho ya nje ya nchi. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: IECEE, IEC X and CB. Taarifa juu ya IEC, shughuli zake, tathmini makubaliano, maendeleo ya viwango. Maelezo ya mipango ya IEC, ambayo yanaelezea zaidi kanuni za kuheshimu utambuzi na kukubalika kubadilishana kwa majibu ya vipimo kwa wanachama wake kwa ajili ya uthibitisho au kibali katika ngazi ya nchi yametolewa. IECx ina suluhisho kwa ajili ya vifaa katika mitambo ya mafuta, na CB inatumika kwa umeme na vifaa vya kiufundi. OIML Certificate System for Measuring Instruments. Inatoa maelezo juu ya OIML, machapisho, miundo ya kiufundi, mifumo ya OIML, Kanuni za nchi, mikutano, semina na matukio. Maelezo ya utaratibu wa vyeti vya OIML yamewekwa kwenye tovuti hii na nyingine zinazofuatia. Pia inaorodhesha makundi ya vifaa, utoaji mamlaka na wapokeaji. MAREJELEO Permanent Tripartite Commission for East African Co-operation. World Forum for Harmonization of Vehicle Regulations. World Trade Organization. Second Triennial Review of the TBT Agreement. Annex 5.

208 198 Tathmini Ya Ulinganifu 73. Je,, kuna mifumo ya kimataifa ya uhakiki (uthibitisho) wa bidhaa? Kuna mifumo wa kimataifa wa uthibitisho wa bidhaa. Baadhi imeelezewa chini. Mashirika ya uhakiki ya kimataifa Uhakiki umekuw ni biashara kubwa sana, zaidi ya vyeti milioni vya ISO vilitolewa Hivyo ni suala lisiloepukika kwamba ukaguzi wa kimataifa wa mashirika ya uhakiki umehusishwa, yanafanya ukaguzi, vipimo na huduma ya uthibitisho duniani kote, mengi yao yakifanya shughuli zake kwenye nchi zaidi ya 100. Mifano halisia ni katika sekta ya uzalishaji ambapo mashirika yamefanyiwa ukaguzi wa meli kwa miaka mingi, kama vile SGS, BVQI, DNV na Lloyds. Kuna mashirika pia yaliyopanua biashara zao kutoka misingi ya awali ya kitaifa kuingia nyanja ya kimataifa kama vile baadhi ya mashirika ya TUV na UL. Katika chakula na nyanja ya maua, the GLOBALG.A.P. uthibitisho unatambuliwa kimataifa kutokana na kiasi kikubwa cha chakula EU wanachoingiza kutoka nchi nyingi duniani (angalia swali namba 14 na 15). Aina nyingine za uthibitisho ambazo ni muhimu kutokana na dhana za kimataifa za biashara ni biashara ya haki, SA 8000 na FSC (angalia swali namba 17). Mashirika ya uthibitisho yanafanya kazi kwa kutumia kanuni za biashara, yanamilikiwa na kusimamiwa binafsi na mara kwa mara yanapewa kibali kwa huduma wanazotoa. Yanatoa ukaguzi muhimu, vipimo na huduma ya uthibitisho kwa soko na nyanja ya udhibiti. Mengi yao pia ni vyombo vya taarifa kwa nchi za Ulaya, hivyo vinaweza kutoa huduma ya kina inayolenga ni nini wateja wanataka au wanahitaji. Ni uchaguzi ambao hautakiwi kupuuzwa, ila unaweza kugharimu. Tume ya Kimataifa ya Ufundi wa Umeme IEC inashughulikia namba kubwa ya mipango/miradi ya uthibitisho ya kimataifa kwa aina tofauti tofauti ya bidhaa. Haya ni maelezo mapana ya miradi hii. The IECEE CB mradi unaolenga vifaa vya umeme kimsingi iliyokusudiwa kwa matumizi ya nyumbani, ofisini, warsha/karakana, huduma za afya na maeneo yanayofanana na hayo The IECEx mradi unaoshughulikia vifaa vitakavyotumika katika mazingira yenye uwezekano wa kulipuka kama vile, kusafisha mafuta, migodi ya makaa ya mawe, mimea, kemikali, mitambo ya gesi, utunzaji na uhifadhi nafaka Mpango wa IECQ unaotathmini vipengele vya elektroniki dhidi ya mahitaji ya ubora na kuthibitisha ulinganifu wao na viwango vyao. Inashughulikia vipengele vya umeme, vifaa vinavyohusiana na taratibu, watengenezaji na wasambazaji, makandarasi wataalamu, maabara za vimipo na usimamizi wa taratibu za vitu vyenye madhara. Miradi imelenga juu ya kanuni za kutambulika kwa pande zote (kukubalika kubadilishana) kwa IEC wanachama wa majibu ya vipimo na ukaguzi wa viwanda unaofanyika kwa ajili ya kupata hati uthibitisho au kibali katika ngazi ya kitaifa. Bidhaa au huduma zinakaguliwa, kufanyiwa vipimo na kukaguliwa chini ya mwavuli wa mwanachama wa muhimu wa mpango wa IEC inaojulikana kama shirika la kuthibitisha la kitaifa au NCB. Listi ya kutambuliwa ya NBC. Listi iliyotambuliwa na NCBs imepostiwa kwenye mtandao wa miradi. Chini ya miradi, NCBs inateua maabara zitakazotumika. Sasa unaweza kuchukuwa mtihani wa vipimo na kukagua majibu kwenda nchi nyingine, na NCB kwenye nchi hiyo itashughulikia uthibitisho kama inavyotakiwa na mazingira ya Soko au mamlaka ya udhitibi. Mradi wa IECx inakuwezesha kuongeza leseni ya kubandika alama ya kuendana na IECEx kwenye bidhaa zako, ambayo inatambuliwa na nchi nyingine ambazo ni wanachama wa mradi kama ushahidi kwamba bidhaa zinakidhi viwango vya IEC vinavyohusika. Vifaa vinavyotumika kwenye mazingira ya kulipuka viko chini ya kanuni za kiufundi kwenye nchi nyingi, na kanuni hizi mara kwa mara zinalenga juu ya viwango vya IEC. Hivyo, miradi hii inatoa njia ya gharama nafuu ili kukidhi mahitaji ya kikanuni na kutosheleza vipaumbele vya soko katika kuongezeka kwa idadi ya uchumi (nchi zinazoendelea kukua kiuchumi).

209 Tathmini Ya Ulinganifu 199 Shirika la Kimataifa la Ugezi wa Kisheria OIML inashughulikia miradi miwili ya kimataifa: The OIML Basic Certificate System- Mfumo wa cheti cha msingi cha OIML Mutual Acceptance Arrangement au MAA-Mpango wa kuheshimu utambuzi mfumo wa cheti cha msingi cha OIML kwa ajili ya kupima vifaa unawezesha watengenezaji kupata cheti cha msingi cha OIML na ripoti ya msingi ya tathmini kuonyesha kwamba aina ya kifaa husika kinafuata mahitaji ya mapendekezo ya kimataifa ya OMIL yanayohusika. Vyeti vinatolewa na nchi wanachama wa OIML ambao wameanzisha mamlaka moja au kadhaa inayohusika na maombi ya usindikaji kutokana na watengenezaji kuomba aina za vifaa vyao kuthibitishwa. Vyeti vinakubaliwa na huduma ya sayansi ya vipimo kitaifa kwa msingi wa kujitolea, na chini ya utambuzi wa pande zote za majibu ya vipimo yaliyoandaliwa na wanachama wa OIML. Mfumo wa cheti cha msingi unarahisisha aina ya utaratibu wa kukubaliwa na watengenezaji na mamlaka ya mfumo wa vipimo kwa kuondoa gharama ya marudio ya maombi na utaratibu wa vipimo. Kwa kuongezea kwa cheti cha msingi cha OIML, OIML imeboresha mpango wa kuheshimu utambuzi (MAA). Mfumo unatumia MAA kama nyenzo ya ziada ya kuongeza kujiamini pande zote katika mfumo mzima. Wakati wa kuandika haya, ilikua bado ni mfumo wa hiari ikiwa na makala yafuatayo: Kuongeza kujiamini katika kupima maabara zilizohusika kwenye aina ya vipimo, maabara hizi zimefanyiwa tathmini katika misingi ya viwango vya kimataifa ISO/IEC Tathmini inaweza kufanywa kwa kibali au na tathmini ya rika Inatoa msaada kwa nchi wanachama ambao bado hawana vifaa vya kufanya vipimo na kufanikisha kwa shirika la kisheria kitaifa la utaalam wa vipimo kutegemea vifaa na ufanisi wa mashirika ya nchi nyingine. Inawezesha vyama/vikundi vyenye nia na kuchukulia umuhimu (katika azimio la imani la pande mbili, au DoMC) mahitaji ya ziada yaliyowekwa na nchi mbalimbali zaidi ya yale yaliyoainishwa na mapendekezo ya OIML. Mdhumuni ya MAA ni kwa washiriki kukubali na kutumia ripoti za tathmini ya MAA zilizohalalishwa na cheti cha makubaliano cha OIML MAA. Kwa mwisho huu, washiriki wa MAA wanatoa washiriki au kutumia washiriki. Kwa wazalishaji, MAA husaidia kuepuka kurudia vipimo kwa ajili ya aina ya idhini katika nchi tofauti tofauti na inawafanya kufahamu, mwanzoni mwa mchakato wa tathmini ya mahitaji ya ziada yaliyowekwa katika nchi mbalimbali ambayo watatumia kwa ajili ya idhini. Uoanishwaji wa Kimataifa wa Viwango vya Magari Jukwaa la kimataifa la kuoanisha kanuni za magari la Shirika la Uchumi la Umoja wa Mataifa ya Ulaya (UNECE WP 29) hivi punde lina nafasi ya kuongoza kimataifa katika uoanishwaji wa kimataifa wa kanuni ya magari. Lina wajibu wa utekelezaji wa mikataba mikubwa miwili uliyofikiwa na nchi zilizoshiriki, zinazojulikana kifupi kama mikataba ya mwaka 1958 na Mikataba ya kimataifa ya Mikataba ya UNECE ya mwaka 1958 hutoa kwa ajili ya kuheshimu utambuzi wa vyeti vya serikali vinavyolenga kwenye kanuni za ECE (kwa makadirio ni 120 wakati wa machapisho haya), wakati huohuo dhumuni la Mkataba wa kimataifa wa 1998 unaoanisha kanuni. Kuheshimu utambuzi kunajumuishwa kutoka Mkataba wa kimataifa wa Kanuni za ECE chini ya Mkataba wa 1958 na kanuni za kimataifa za kiufundi (GTR) chini ya Mkataba wa kimataifa wa mwaka 1998 yote inajadiliwa katika WP 29. Kuheshimu utambuzi wa vibali viliyotolewa chini ya mkataba wa mwaka 1958 kunakusudia kurahisisha biashara ya kimataifa katika magari na sehemu zake. Ikiwa aina ya sehemu imepitishwa kwa mujibu wa kanuni za UNECE na wanakikundi wowote wanafungana wa mkataba wa 1958, wanakikundi wengine waliosaini kanuni watatambua mkataba huo. Hii inaepusha marudio ya vipimo na vibali vya vipengele/sehemu katika nchi mbalimbali ambapo vipengele vinapelekwa nje. Pia inasaidia kupunguza muda na malighafi zinazotolewa kubuni, kutengeneza, kupwa kibali, na hata kuingia kwenye huduma za magari na vipengele/sehemu zake. Nchi kama 50 ni wanakikundi wanaofungana na mkataba wa 1958, na bidhaa zenye kibali zimewekewa alama ya kawaida na E kubwa ndani ya duara ambayo pia ina idadi ya namba zilizo chini ya mkataba kwa nchi iliyoidhinishwa.

210 200 Tathmini Ya Ulinganifu IECEE CB. IECE X. IECQ. MAREJELEO United Nations Economic Commission for Europe (UNECE). WP.29 Inavyofanya kazi Jinsi ya kujiunga.

211 Tathmini Ya Ulinganifu Nitapata wapi taarifa kuhusu mashirika ya uhakiki yanavyofanya kazi kwenye nchi zingine? Kuna vyanzo vingi vya taaarifa kuhusu vyombo au mashirika yauthibitisho unayoweza kuyapata. Inajumuisha vyombo vya uthibitisho vyenyewe, mashirika ya taifa ya vibali, upendeleo wa wateja wako, na mamlaka hususani kama kanuni zinahusika.vilevile hutakiwi kuacha kutumia huduma za shirika la kitaifa la kukuza biashara ili kukusanya taarifa kuhusu vyombo vya uhakiki. Vyombo vya uhakiki na maabara Uthibitisho ni biashara kubwa, na kuna mashirika mengi ya kuthibitisha yanayofanya kazi ndani ya soko. Hivyo, mashirika mengi yanatakiwa kutangaza uwepo wao na huduma zao kwa bidii sana. Karibu mengi yao, ila hususani yale ya viwanda binafsi, yataendeleleza tovuti kwa haki na kina. Ikiwa utafikia tovuti ya kimataifa ya vyombo vya uthibitisho kama SGS, DNV, TUV, BVQI, na mengine, utaweza kupata taharifa kwa haraka kufahamu kama yanafanya shughuli zake katika soko ambalo umenuia. Kwenye nchi zinazoendelea kiuchumi, mashirika ya viwango vya taifa mara kwa mara ndiyo yanayothibitisha huduma, na faida ya kuyatumia ni kwamba mara nyingi yako na bei nafuu kulinganisha na mashirika ya uthibitisho ya binafsi. Pia ndio yaliyo rahisi zaidi kupatikana kwa sekta ya SME. Itakuwa vizuri zaidi kuwasiliana nao vilevile, hata kama tovuti zao hazitakuwa za kisasa mara kwa mara au kamili kama yale mashirika ya kuthibitisha ya binafsi (angalia swali namba 70 juu ya kufanya uchaguzi wa mashirika ya kuthibitisha) Majina ya mashirika ya uthibitisho au maabara ambayo yanashiriki kwenye miradi ya kimataifa kama ile inayosimamiwa na IEC, OIML and WP 29 (angalia swali namba 73) yanaweza kupatikana kwenye tovuti za mashirika haya. Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa mashirika ya uthibitisho yaliyopitishwa kwa viwango kama vile vya GLOBALG. A.P., BRC, FSC na SA Mashirika ya Ithibati Kila shirika la taifa la kibali linatakiwa kudumisha orodha ya mashirika ambayo inawapa vibali. Hii inaweza kuwa kupima na maabara za alama za vipimo, au ukaguzi na mashirika ya uthibitisho. Orodha hizi karibu wakati wote zinapatikana kwenye mtandao. Ili kuweza kutambua shirika la taifa la vibali ambalo ni aidha tayari limesainiwa na IAF Multilateral Recognition Arrangement (Utaratibu wa Kimataifa wa Utambuzi) (angalia swali namba 91) au ni wanachama wa IAF pekeyake, rejea kwenye tovuti ya IAF. Hii itatoa kiunganishi (link) cha shirika la kibali ndani ya nchi unayonuia. Unaweza kupata kiunganishi cha mashirika ya vibali yaliyojumuishwa kwenye maabara ya vibali katika tovuti ya ILAC. Mteja wako Kama unatafuta soko la bidhaa au huduma moja kwa moja kwa mteja kwenye soko la nje, unaweza ukakuta kuwa huyu mteja ana upendeleo wake wa shirika la uthibitisho. Hapo Utatakiwa kuheshimu uchaguzi wake huo kama unapenda kudumisha uhusiano chanya na yeye (mteja) na kufanikiwa katika jitihada ya masoko. Kama ikiwa mteja hana upendeleo wa pekee kwa shirika maalum la uthibitisho, anaweza kukueleza ni shirika lipi lenye sifa njema kwenye soko lake la bidhaa fulani au huduma unayonuia kupeleka nje. Mamlaka ya Udhibiti Ikiwa bidhaa au huduma unayonuia kupeleka nje inaangukia kwenye wigo wa kanuni za kiufundi au vipimo vya SPS, hapo utatakiwa kupata taharifa kuhusu shirika la uthibitisho linalopendekezwa au lililoteuliwa kutoka mamlaka inayohusika na soko la nje. Vituo vya uchunguzi vya nchi yako kuhusu TBT na SPS, (angalia swali namba 23) wanatakiwa waweze kukupa msaada kupata taharifa hii.

212 202 Tathmini Ya Ulinganifu Mashirika ya kukuza biashara Kwa ujumla, TPOs hukusanya habari zote kuhusu masoko ya nje ya sasa au yenye uwezo wa kusaidia sekta ya kuuza nje. Pia yana msaada katika kuweka mawasiliano kati ya wagawaji/wasambazaji na waagizaji kwa lengo la kufanya mikataba ya biashara. Kwa maana hiyo mashirika ya kukuza biashara mara kwa mara yanafahamu ni mashirika gani ya uthibitisho yanayofanya shughuli zake kwenye soko la nje na yapi yana sifa nzuri katika soko, kama sivyo wanao mtandao mkubwa ambao unaweza kutumika kupata taaarifa sahihi. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Trade Centre (Kituo cha Biashara cha Kimataifa) Products Map. Mtandao unaofungua mlango kwa viwanda 72, uliokusanya taarifa za kiuchunguzi kuhusu soko la kimataifa na maendeleo ya biashara. Kwa ujumla, bidhaa 5,300 (katika HS ngazi sita) zilizofanyiwa biashara na nchi zaidi ya 180 zinatazamwa. Standards Map. Mtandao wa msingi unaoruhusu watumiaji kupitia taarifa za viwango vya hiari zaidi ya 30 unaoambatanisha makundi ya bidhaa zaidi ya 40. World Directory of Trade Promotion Organizations Mwongozo uliounganishwa moja kwa moja hewani wa mashirika ya kukuza biashara na taasisi zinazotoa msaada juu ya biashara. World Trade Organization Technical barriers to Trade, national enquiry points. Inaorodhesha majina na mawasiliano juu ya pointi za kiuchunguzi na kutoa taaarifa za zaidi. Sanitary and Phytosanitary Measures, National enquiry points. Orodha yenye taaarifa za WTO na kuarifiwa kuhusu SPS, hoja zilizotolewa, nyaraka zilizopo, pointi za kiuchunguzi, n.k MAREJELEO International Accreditation Forum (IAF). International Laboratory Accreditation Cooperation (ILAC).

213 Tathmini Ya Ulinganifu Shughuli gani hufanywa na mashirika ya uhakiki kabla na baada ya kutoa uhakiki wa mfumo wa usimamizi? Kuna wakati ambao tofauti iliweza kutokea katika mbinu na michakato ya mashirika ya uthibitisho hapo nyuma, kipindi hiki mashirika mengi ya kuthibitisha yanafuata michakato iliyoorodheshwa katika ISO/IEC na viwango vya kimataifa kwa ajili ya vibali vyao. Hii ni habari njema kwa msambazaji yeyote mwenye nia ya kuthibitishiwa, kwa kuwa inabainisha na kuoanisha utendaji upande wa mashirika ya uthibitisho. Mchakato unaonyeshwa bayana kwenye mchoro hapa chini. Hatua ya Maombi ya kujiunga Pale utakapofanya maamuzi ya kupata uthibitisho na umefanya uchaguzi wa shirika lipi la uthibitisho (angalia swali namba 71), utatakiwa kuomba rasmi uthibitisho. Fomu za maombi zinatakiwa kukamilishwa na kueleza kiasi kikubwa kuhusu kampuni yako na shughuli zake ili kuwezesha shirika la uthibitisho kubainisha/kuamua wigo wa hali ya utendaji na kuteua kiongozi wa timu kwa ajili ya mchakato wa ukaguzi. Zoezi la ukaguzi wa mwanzo kwa ajili ya kuthibitisha lina hatua mbili za ukaguzi kama ilivyoelezewa hapo chini. Hatua ya kwanza - ukaguzi Katika hatua hii, unatakiwa kutoa uwerevu/usimamizi wako unaostahili na nyaraka zote muhimu. Shirika la uhakiki litaamua kutokana na msingi wa nyaraka hizi kama wewe upo tayari/unastahili kupiti hatua ya pili au ridhaa ya ukaguzi. Kama shirika la uthibitisho litagundua kuwa haupo tayari kwa ridhaa ya ukaguzi, litakuarifu kama inavyotakiwa na kusimamisha mchakato. Ikiwa majibu ni upo tayari, ila vichache ambavyo haviko sawa vinatakiwa kurekebishwa kabla ya ridhaa ya ukaguzi kufanyika, shirika la uhakiki litakupatia ripoti. Baada ya kurekebisha makosa na kutoa taarifa kwa shirika na wakaafikiana na hatua lizochukua, ridhaa ya ukaguzi inaweza kupangwa. Hatua ya pili- ukaguzi Kiongozi wa timu ataunganika pamoja na timu ya wakaguzi na wataalamu kufuatana na wigo wa kazi/shughuli zako, ugumu na ukubwa wa shughuli zako, na watafanya hatua ya pili ya ukaguzi kutathmini utekelezaji na uchakarikaji wa mfumo mzima kutokana na kauli na muda uliopangwa na pande zote. Baada ya kikao cha kufungua, kila mkaguzi au mtaalamu atakagua eneo fulani la shuhguli zako. Atafanya tathmini kuwa yaliyomo kwenye nyaraka ni thabiti na sawasawa na shughuli za kampuni yako pamoja na viwango.

214 204 Tathmini Ya Ulinganifu Unatakiwa kuhakikisha kuwa unaye mwakilishi atakayeambatana na kila mkaguzi au mtaalamu, kuchukuwa maelezo na kuondoa yale yote yatakaonekana hayako sawa. Mwishoni mwa hatua ya pili ya ukaguzi, kiongozi wa timu ataitisha mkutano wa kufunga ambapo atawasilisha matokeo yote kwa ujumla na orodha ya upungufu wote (kama yapo). Timu hiyo inaweza kugundua kuwa umetimiza vigezo/upo sawasawa na mahitaji ya viwango (m.f ISO 9001, ISO 14001) na itapendekeza kwa tume ya uthibitisho kwamba unapaswa kuthibitishwa. Pia kuna uwezekano mkubwa kwa timu kugundua kwamba bado kuna baadhi ya makosa/upungufu ambao unatakiwa kufanyiwa kazi kabla ya wao kupendekeza kupata uthibitisho. Kwa kesi kama hii, watapanga pamoja nawe ratiba ya muda na taratibu za kurekebisha upungufu uliyoonekana. Wanaweza kutaka kushuhudia taratibu mpya au kama upungufu kiasili ni madogo, watapenda zaidi ukiwapelekea ushahidi kuwa upungufu huo umepatiwa suluhu. Pale upungufu wote utakapofanikiwa kupatiwa uvumbuzi ndani ya muda uliopangwa, kimsingi miezi mitatu, kiongozi wa timu atapeleka mbele mapendekezo ya wewe kupata uthibitisho kwa ajili ya marejeo na maamuzi kwa watu au tume yenye mamlaka. Uhakiki Mchakato wa kufanya maamuzi ni huru kabisa na mchakato wa ukaguzi. Watu au tume yenye mamlaka ambayo haikuhusika kwenye ukaguzi itapitia ripoti ya ukaguzi na ripoti ya kusawazisha mapungufu na kufanya maamuzi kuhusu uthibitisho. Uamuzi utafuatiwa na swala la uthibitisho wa nyaraka ambazo kawaida zina muonekano wa cheti na au bila viambatisho vielezeavyo wigo wa uthibitisho na maeneo yanayoguswa na cheti. Ukaguzi wa ufuatiliaji Baada ya uthibitisho, shirika la uthibitisho litaendesha ukaguzi wa ufuatiliaji kwa kawaida mara moja kwa mwaka. Hii ni kuhakikisha kwamba mfumo wako umewekwa imara na bado unafanya kazi kwa mujibu wa viwango na nyaraka zako. Kawaida ukaguzi huu hautokuwa wa kina kama ule wa mwanzo wa uthibitishaji. Kuna maeneo machache hataivyo, ambayo mara kwa mara yatakua yanahusishwa kwenye ukaguzi wa ufuatiliaji kama vile ukaguzi wa ndani, usimamizi wa kitaalam na hata mfumo wako wa kusawazisha makosa. Ni wazi, upungufu wowote utakapojitokeza wakati wa ukaguzi wa ufuatiliaji unatakiwa kushughulikiwa kwa ufanisi katika muda uliopangwa/kubaliana. Kinyume na hapo, unaweza kupoteza cheti chako. Ukaguzi wa kutengenezwa upya kwa cheti Katika mwaka wa tatu tangia kuthibitishwa, ukaguzi kwa ajili ya utengenezwaji mpya wa cheti/uthibitisho utafanyika, sawa na ufuatiliaji wa awali. Kama majadiliano yatafanikiwa, kampuni yako itapewa uthibitisho kwa kipindi kingine cha miaka mitatu, na mzunguko mzima kujirudia tena. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ( ISO/IEC 17021:2011, Conformity assessment Requirements for bodies providing audit and certification of management systems. Obtainable from ISO or ISO members (list at and IEC or IEC National Committees management systems. Kanuni na mahitaji kwa ajili ya ustadi, uthabiti na usawa wa ukaguzi, uthibitisho wa mifumo ya uongozi wa aina zote (m.f. mifumo ya usimamizi bora na mifumo ya usimamizi mazingira) na kwa ajili ya mashirika yanayofanya shughuli hizi. ISO/IEC 17011:2004, Conformity assessment General requirements for accreditation bodies accrediting conformity assessment bodies. Obtainable from ISO or ISO members (list at and IEC or IEC National Committees ( Mahitaji ya jumla kwa mashirika ya vibali kutathmini na kutoa kibali kwa mashirika ya tathmini makubaliano (CABs); pia sahihi kama hati ya mahitaji kwa ajili ya mchakato wa tathmini rika kwa mipango ya kuheshimu utambuzi katika ya mashirika ya vibali.

215 Tathmini Ya Ulinganifu Je, kupata uhakiki wa viwango binafsi kunahakikisha upatikanaji wa masoko? Kwanza kabisa, ni muhimu kufafanua kuwa hakuna uthibitisho, iwe wa binafsi au unaotolewa na shirika la serikali, utakaojihakikishia wenyewe juu ya aina yoyote ya mauzo. Kupata mauzo yenye mafanikio itategemea maswala mengi, ikiwa ni pamoja na masuala kama vile bei, utoaji wa huduma, uwasilishaji, msaada wa huduma, kubuni bidhaa na ubora wa bidhaa. Pia, unatakiwa kufahamu kuwa bidhaa na huduma zinatakiwa kukubaliana na kanuni za kifundi na vipimo vya SPS kisheria (angalia swali namba 18 na 19). Bila kuenda sawasawa na mahitaji haya, upatikanaji wa masoko hautakuwepo. Ikiwa uthibitisho kwa viwango binafsi haujumuishi taratibu za kiufundi, haiwezi kuhakikisha chochote. Kwa hali yoyote, ni wajibu wako kuenda sawasawa na mahitaji ya lazima; hakuna shirika la uthibitisho litakalochukuwa wajibu huu. Lakini ambacho uthibitisho/hati inaweza kufanya ni kufungua milango na kukuwezesha kufikia masoko ili wewe uanze kufanya majadiliano ya mauzo. Hivi ndivyo ilivyo kwa viwango binafsi kama vile GLOBALG.A.P., BRC, WRAP, SA 8000 na FSC. Wanunuzi wanahitaji uhakika kuwa wewe ni mzalishaji au mtengenezaji wa uadilifu, hasa kama wewe umeegemea katika uchumi wa nchi zinazoendelea mbali na eneo la soko linalolengwa. Unaweza kulitazama hili kama aina ya mawasiliano ya kabla ya mchakato wa idhini/kibali ambao bila huo hutoweza hata kufungua milango kwa majadiliano zaidi. Pia angalia swali namba 70 juu ya uchaguzi wa mashirika ya uthibitisho, na swali namba 72 juu ya kukubalika kwa uthibitisho katika soko la nje kwa maelezo ya ziada. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Kituo cha Biashara cha Kimataifa Market Access, Transparency and Fairness in Global Trade: Export Impact for Good ISBN Inatoa uchambuzi wa kina wa matokeo na athari za biashara ya haki ya viwango vya hiari kwa wazalishaji na wauzaji bidhaa nje katika nchi zinazoendelea; Inadili na mtazamo wa wazalishaji juu ya kuwezesha upatikanaji wa soko au kukabili kizuizi kipya cha soko. Standards Map. Standards Map ni lango la mtandao wa ITC s (Vituo vya kimataifa vya biashara) Mpango wa Biashara kwa Maendeleo Endelevu na juhudi za ushirikiano kuzidisha uwazi kwenye viwango vya hiari na kuongeza fursa kwa ajili ya uzalishaji na biashara endelevu.

216 206 Tathmini Ya Ulinganifu 77. Jinsi gani nitapata uthibitisho kupitia viwango binafsi kama WRAP, Biashara ya haki(fairtrade), SA 8000, GLOBALG. A.P, na kwa gharama gani? Mchakato wa uthibitisho wa viwango vya binafsi kiasili hautofautiani na mchakato wa uthibitisho ulioelezewa katika swali namba 68, 69, 71, na 72, ila uchaguzi wa shirika la kuthibitisha ni maalum sana. Mifano michache ya uthibitisho wa viwango binafsi imetolewa chini. Kwa maelezo juu ya viwango vya kijamii, kimazingira, na kimaadili, angalia pia swali namba 17. Shirika linalowajibika na uzalishaji vibali duniani kote- Worldwide Responsible Accredited Production (WRAP) The Worldwide Responsible Accredited Production (WRAP) ni shirika huru kabisa, lisilo la faida lenye wakfu wa kuzalisha uhakiki/uthibitisho wa halali au kisheria, kibinadamu na kimaadili duniani kote. Idadi kubwa ya vyama vya mavazi, vitambaa na viatu kutoka nchi mbali mbali ni wanachama washiriki wa WRAP. Kanuni za WRAP zimeegemea katika kukubalika kwa ujumla viwango vya kimataifa mahali pa kazi, sheria za mahali maalum na kanuni mahali pa kazi ambayo imezunguka usimamizi wa rasilimali watu, afya na usalama, vitendo vya mazingira na kufuata kisheria ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni za kuagiza/kuuza nje na viwango vya usalama. WRAP imepitisha mbinu ya mfumo wa usimamizi kufikia maridhiano. Hii inamaanisha kuwa uongozi wa juu unatakiwa kutumia kanuni za WRAP katika kuandika, kuteua watumishi makini kuhakikisha kwamba vitendo/mambo yanayohitajika yanatekelezwa popote kwa nyenzo, na kuhakikisha kuwa mfumo wa ukaguzi wa ndani upo sawasawa kwa maafikiano endelevu.. Nyenzo zinazohitaji kuthibitishwa ni lazima zifanyiwe tathmini ya ndani halafu ndio zikaguliwe na kampuni/shirika huru la usimamizi la nje. Maelezo ya ziada juu ya uthibitisho wa WRAP (taratibu, maombi ya kuthibitishwa, ada, fomu ya maombi kwa wasimamizi wanaohitaji kibali cha WRAP) yanapatikana kwenye tovuti ya Biashara ya haki Alama ya uthibitisho ya FAIRTRADE ni nembo ya bidhaa inayodhibitiwa na kampuni mama ya Fairtrade international inayowakilisha mashirika 25 duniani kote. Alama imekusudiwa kwa matumizi ya ufungashaji wa bidhaa. FLO inafanya kazi kupitia FLO-CERT GmbH, kampuni binafsi ya kuthibitisha iliyosajiliwa Ujerumani na kupewa kibali na Deutsche Akkreditierungsstelle (DAkkS, Shirika la Kijerumani la Kibali). Maombi ya kutumia alama ya FAIRTRADE ni ya michakato ya ngazi mbili. Ya kwanza, muombaji anatakiwa akaguliwe na FLO-CERT kubainisha kuwa inashabihiana na mahitaji viwango husika vya Fairtrade. Hii inaweza kuchukuwa muda wowote kuanzia siku nne kwa shirika lenye uzalishaji mdogo hadi wiki sita kwa mashirika/makampuni makubwa. Pale makubaliano yanapokuwa bayana, mwombaji anaweza kuomba leseni ya kutumia alama ya FAIRTRADE ama kutoka kwa waendeshaji wa Fairtrade ndani ya nchi ya muombaji (waendeshaji wa Fairtrade wapo Ulaya, Amerika ya kusini, Australia, Japan na New Zealand, jumla ya nchi 23) au, kama hakuna waendeshaji wa Fairtrade ndani ya nchi ya muombaji, moja kwa moja kutoka FLO. Pale itapothibitishwa, muendeshaji atakuwa anakaguliwa kila mwaka kama sehemu ya mzunguko wa miaka mitatu ya kuthibitishwa/kuhakikishwa upya. Maelezo ya kina juu ya FLO yanaweza kupatikana kwenye tovuti yake; mawasiliano na taratibu za maombi ya kuthibitishwa yanaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti ya FLO-CERT. SA 8000 Uthibitisho wa SA 8000 unadhibitiwa duniani kote na Social Accountability Accreditation Services [(SAAS) yaani Huduma za Kibali Ziwajibikazo kijamii]. Ili kuthibitishwa, SAAS inapendekeza nyenzo ziwasilishwe angalau kwa mashirika ya SAAS matatu ya kibali ya uthibitisho na kuomba kwa ajili ya huduma ya uthibitisho. Wakaguzi kutoka mashirika teule ya uthibitisho wanatembelea vifaa, kutathmini utendaji wa ushirika juu ya masuala mbalimbali na kutathmini hali ya mfumo wa usimamizi wa kampuni, kujua kama utendaji wake wa kila siku unakubaliana na mtazamo wa viwango vya SA8000. Vifaa vilivyothibishwa vinaweza kuonyesha cheti cha SA8000, lakini bidhaa za mtu binafsi haziwezi kutambulishwa hivyo

217 Tathmini Ya Ulinganifu 207 kwakuwa cheti kinashughulikia taratibu za mahali pa kazi na sio uthibitisho wa bidhaa yenyewe. Kwa sasa, karibuni mashirika 20 ya uthibitisho hwuko Ulaya, Hong Kong (China), India, Uruguay na nchi za Amerika zimefanyiwa uthibitisho na SAAS; mengi yao yakiwa yanafanya shughuli zake kwa misingi ya kimataifa. Orodha na mawasiliano yao yanaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti ya SAAS. GLOBALG.A.P. GLOBALG.A.P. Uthibitisho/Cheti kinachohusiana na utendaji mzuri wa kilimo na kinachoweza kupatikana kwa mazao, mifugo, kilimo cha samaki, viwanja vya malisho, na nyenzo za kuzalisha mimea. Uthibitisho wa GLOBALG.A.P. unatolewa na zaidi ya mashirika huru 100 ya kuthibitisha ndani ya zaidi ya nchi 80 ambayo yamehalalishwa na shirika la GLOBALG.A.P. Kwa kuongezea, kuna karibuni nchi 20 ambazo zinazoshughulika na kile kinachojulikana kama miradi linganifu. Inatambulika na shirika la GLOBALG.A.P kwa misingi ya uwezo wao wa kiufundi waliouonyesha. Wauzaji wanaweza kufanya maombi katika moja ya mashirika haya, mengi yakiwa yanaendesha shughuli zake katika zaidi ya nchi moja kwa ajili ya cheti/uthibitishaji wa GLOBALG.A.P. Orodha kamili ya mashirika ya uthibitisho na njia ya mawasiliano yanaweza kupatikana kwenye tovuti ya GLOBALG.A.P. Gharama za uthibitishaji Sio rahisi kutoa makisio sahihi ya gharama za uthibitishaji. Itategemea na muda wa siku ambazo wakaguzi watatumia kupitia ubora wa miongozo na taratibu, ukaguzi kwenye tovuti na kutathmini urekebishwaji wa makosa pamoja na ada inayochajiwa na mashirika mengi kwa mwaka. Kwa kawaida ada ya maombi huwa inatozwa vilevile na inaweza kufikia kiasi cha dola za kimarekani 1, Hivyo ni muhimu kupata dondoo sahihi na kamilifu kutoka kwa shirika la uthibitishaji (angalia pia swali namba 70 juu ya kuchagua shirika la uthibitishaji) kabla ya kusaini fomu za maombi na mikataba ya uthibitishaji. MAREJELEO Certification for Development (FLO-CERT). Fairtrade Labelling Organizations International (FLO). GLOBALG.A.P. Certification. Social Accountability Accreditation Services (SAAS). Worldwide Responsible Accredited Production (WRAP).

218 208 Tathmini Ya Ulinganifu 78. Nini maana ya Eco-labelling? Kanuni Eco-labelling ni mfumo wa uwekaji nembo kutambua bidhaa zitumiwazo zinazotengenezwa katika njia ambayo inaepuka au inapunguza madhara makubwa katika mazingira kulingana na mzunguko wa maisha. Hivyo ni aina ya uthibitishaji wa bidhaa (angalia pia swali namba 68). Ingawaje eco-labelling ilianzishwa na mashirika yasiyo ya kiserikali miaka mingi iliyopita, kwa sasa imekuwa ni biashara kubwa ikiwa na ongezeko kubwa la miradi inayotolewa katika eneo la soko. Mataifa ya Ulaya yametangaza rasmi sheria ya kuleta baadhi ya amri katika soko hili linalozidi kukua. Aina yoyote ya bidhaa inaweza kuwa chini ya eco-labelling, lakini ni zaidi ya kawaida kukuta bidhaa zitumiwazo zimewekwa nembo hii. Eco-labelling inaweza kuwa sehemu ya kwanza au tamko la muuzaji/msambazaji la uzingatiaji (angalia swali namba 57) pia inajulikana kama taarifa ya kijani. Ikiwa mtengenezaji au muuzaji atatangaza kuwa bidhaa ni rafiki kwa mazingira, hiyo inafanyika kukuza taswira yake ya kuwa makini na masuala ya mazingira. Baadhi wanaweza hata kutumia ishara/alama ya kimataifa ya kusindika katika ufungaji wao, ingawa hii bado ni tamko la muuzaji/msambazaji. Jambo la muhimu zaidi katika taswira ya masoko ni kikundi cha tatu cha miradi ya eco-labelling. Kuna ongezeko la orodha ya mashirika ya kuthibitisha ambayo yamebobea katika miradi ya eco-labelling; hayo yako huru au hayaingiliani kabisa na watengenezaji au wauzaji na wanunuzi, na yanaweza kuwa kielelezo/ya umuhimu katika masoko maalum (angalia swali namba 16 juu ya uwekwaji nembo katika nguo maalum). ISO imechapisha idadi ya viwango vya kimataifa vya ecolabelling katika mfululizo wake wa ISO kwa ajili ya kutumiwa na mashirika ya eco-labelling ya kuthibitisha. Ni pamoja na ISO 14020, Nembo na tamko la mazingira- Kanuni za jumla ; ISO 14021, Nembo za mazingira na tamko-kutangaza binafsi madai ya mazingira (aina namba mbili ya kuwekwa nembo ya mazingira); ISO 14024, nembo za mazingira na matangazo-aina ya kwanza ya kuweka nembo ya mazingira- Kanuni na taratibu; na ISO/TR 14025, Nembo za mazingira na tamko/matangazo- Aina ya tatu ya kuweka nembo ya mazingira (angalia swali namba 17). Mtandao wa Ecolabelling Duniani- Global Ecolabelling Network Mtandao wa Ecolabelling duniani ni jumuiya isiyo yakifaida ya kikundi cha tatu, shirika la kuweka nembo ya utendaji wa mazingira lililoanzishwa mwaka 1994, kuimarisha, kukuza na kuendeleza ecolabelling kwa bidhaa na huduma. Hivi sasa, lina wanachama 26 kutoka Asia, Ulaya, Kaskazini na Kusini mwa Amerika ikijumuisha mashirika makubwa kama vile Good Environmental Choice (Australia), Green Seal (Nchi za Amerika), Federal Environmental Agency (Ujerumani), Japan Environment Association (JEA), Nordic Ecolabelling Board (inayojumuisha nchi tano za Nordic) na Department for Environment, Food and Rural Affairs (Uingereza). Shughuli zao ni pamoja na ukusanyaji na ukuzaji/utangazaji wa habari juu ya mipango na ushiriki katika shughuli za ecolabelling za Mradi wa mazingira wa Umoja wa mataifa [United Nations Environment Programme (UNEP)], Shirika la Kimataifa la Viwango [the International Organization for Standardization (ISO)] na Shirika la Biashara la Kimataifa [the World Trade Organization (WTO)]. Pia wanafanya utafiti juu ya mipango ya kutambulika pande zote na kutoa utaratibu wa kubadilishana habari/taharifa. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti ya Mtandao wa Kimataifa wa Ecolabelling (Global Ecolabelling Network).

219 Tathmini Ya Ulinganifu 209 Nembo ya mazingira ya nchi za Ulaya Nembo ya mazingira ya Ulaya ( the EU Ecolabel) inatambulika kwa nchi wanachama wote 27 wa Ulaya pamoja na Iceland, Liechtenstein na Norway. Mradi unatambua bidhaa na huduma bora kimazingira kwa kuwazawadia alama/ishara ya pekee na rahisi kutambulika ya ubora wa mazingira-ua. Ua linasaidia watengenezaji, wachuuzi na watoa huduma kutambulika kwa viwango vizuri vya mazingira na wakati huo huo kusaidia wanunuzi kutambua bidhaa ambazo hazina madhara makubwa kwenye mazingira. Mradi huu wa hiari unajumuisha aina 26 za bidhaa na huduma (2010), pamoja na makundi mengine yanayoendelea kuongezwa. Bidhaa zilizojumuishwa ni pamoja na bidhaa za usafi, vifaa vya umeme, bidhaa karatasi, nguo, bidhaa za majumbani na bustani, mafuta ya kulainisha na huduma kama hifadhi ya watalii. Nembo inazawadiwa tu kwa bidhaa ambazo ni rafiki kwa mazingira katika kila kikundi cha bidhaa. Mradi huo hivi karibuni umefanyiwa mabadiliko ili kurahisisha taratibu za mashirika kufanya maombi kwa ajili ya nembo na kuongeza idadi ya makundi ya bidhaa. Baadhi ya mabadiliko muhimu ni pamoja na kupunguza ada, kupunguza mizigo ya utawala ya makampuni, kuongezeka harambee/ushirikiano na Nembo/Vitambulisho vingine vya kitaifa, kuendeleza vigezo madhubuti na marekebisho ya taratibu. Taharifa zaidi juu ya Ecolabel ya Umoja wa nchi za Ulaya inawweza kupatikana kutoka kwenye tovuti yake. Baraza la Usimamizi wa Misitu- Forest Stewardship Council (FSC) Baraza la usimamizi wa misitu ni shirika lingine ambalo ecolabelling ni moja ya mradi wake. Shirika hilo limeanzishwa mwaka 1993 kuboresha utunzaji wa misitu na kupunguza ukataji miti. Kuongezeka kwa idadi ya bidhaa za mbao, karatasi na bidhaa za karatasi zinazopatikana kwa idhini ya FSC. Inafanya kazi katika kanuni ya mlolongo wa ulinzi, mchakato ambao chanzo cha mbao zinazotumika katika utengenezaji/uzalishaji wa bidhaa hizi unathibitishwa kinyume na viwango vya mazingira sahihi, manufaa kijamii na usimamizi wa faida kiuchumi. Mbao hufuatiliwa kwa njia ya msururu wa ugavi hadi mwisho wa bidhaa, ili wateja waweze kuchagua kufanya manunuzi endelevu ya mbao zilizovunwa tayari, kinyume na njia mbadala ambayo inaweza kuchangia ukataji wa miti duniani kote. Maelezo zaidi juu ya mradi wa FSC na mashirika ya uthibitisho yanayohusika yanaweza kupatikana kwenye tovuti ya FSC. Baraza la Usimamizi wa bahari- Marine Stewardship Council (MSC) Ecolabel ya blue ya kipekee ya baraza la usimamizi wa bahari inawezesha wanunuaji/wateja kutambua chakula cha baharini ambacho kimefika kutoka chanzo stahili na endelevu. Mradi wa MSC ni wa hiari na wavuvi ambao wamekaguliwa/fanyiwa tathmini na kukidhi viwango vya mazingira vya MSC wanaweza kutumia ecolabel ya MSC. Kama 2010, karibu bidhaa 4000 katika zaidi ya nchi 60 duniani wanatumia ecolabel ya blue. Viwango vya MSC ni thabiti na miongozo ya ecolabelling kwa samaki na mazao ya uvuvi kutoka ukamataji uvuvi pori baharini yaani (Marine Wild Capture Fisheries) iliyopitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (United Nations Food and Agriculture Organization -FAO) mwaka Uvuvi wowote unaotakiwa kuthibitishwa na MSC na kutumia ecolabel utakaguliwa kama ni kinyume na viwango vya MSC na shirika huru la kuthibitisha lililopewa kibali cha kufanya tathmini ya MSC na shirika la kimataifa la huduma ya vibali (Accreditation Services International -ASI). Msururu wa kuthibitisha ulinzi pamoja na ugavi kutoka kwenye mashua mpaka hatua ya kuuza unahakikisha kwamba chakula cha kutoka baharini kilichouzwa na kina ecolabel ni kutoka uvuvi uliothibitishwa na MSC. Ufungaji na Kusindika- Packaging and recycling Kuna miradi mingi ya kusindika inayoweza kuchukuliwa kama ecolabelling, haswa katika sekta/kitengo cha ufungaji. Baadhi ni ya umuhimu wa kiuchumi tu katika nchi yao ya asili, kwingine umepata umuhimu mkubwa. Mifano miwili imetolewa maelezo chini.

220 210 Tathmini Ya Ulinganifu Nukta ya kijani- Green Dot. Alama ya nukta ya kijani (German: Grüner Punkt) asili yake ni Ujerumani, lakini kwa sasa imeanzishwa nchini kote Ulaya kama ishara ya leseni ya mtandao wa Ulaya wa mfumo wa sekta ya ufadhili kwa ajili ya kusindika vifaa vya ufungaji wa bidhaa za wateja. Alama hiyo ni alama ya biashara inayolindwa duniani kote. Tangu Kuanzishwa kwake Ulaya, mradi umekwishaendeshwa kwenye nchi 27 za Ulaya. Nukta ya kijani inatumiwa na makampuni zaidi ya na karibia vitu bilioni 460 vinafungwa huwekwa nembo pamoja na nukta hiyo kwa mwaka. Wazo la msingi la nukta ya kijani ni kuwa wateja watakaoona alama wafahamu kwamba mtengenezaji wa bidhaa anachangia gharama za kufufua na kusindika. Hii inaweza kuwa kusindika taka za nyumbani zilizokusanywa na mamlaka mfano kusindika (kwenye mabegi maalum-kwa Ujermani mifuko hiyo ni ya njano), au kwenye vyombo maeneo maeneo ya umma na nje ya maduka makubwa. Mfumo huu unafadhiliwa na ada ya leseni ya Nukta ya kijani (Green Dot) inayolipwa na wazalishaji wa bidhaa. Ada inatofautiana kutegemea na nchi husika na inategemea na vitu/vifaa vya vilivyotumika katika ufungaji (mfano karatasi, plastiki, chuma, mbao, kadi) pamoja na gharama ya kukusanya, kuchagua na njia za usindikaji zilizotumika. Kila nchi pia ina ada tofauti ya kujiunga na mradi/mpango na ada ya kudumu au inayobadilika badilika. Kwa maneno rahisi, mfumo unahamasisha wazalishaji kukata kwenye ufungaji kwasababu hii inawapunguzia gharama za ada ya leseni. Matumizi ya Nukta ya kijani yanasimamiwa na shirika linalounga mkono Ulaya (Europe). Maelezo ya kina yanapatikana kwenye tovuti yao. Kanuni za Utambuzi wa resini- Resin identification codes. Seti hizi za Kanuni zimetengenezwa na Jamii ya viwanda vya plastiki (the Society of the Plastics Industry (SPI)) mnamo mwaka 1988, sasa zinatumika duniani kote kwa sababu ya msingi ya kuruhusu kujitenga kiufanisi kwa aina nyingi tofauti za usindikaji. Ishara/alama (mbili tu zimeonyeshwa kwenye mchoro) zilizotumika katika kanuni/sheria zina mishale ambayo inazunguka upande wa kulia kutengeneza pembetatu iliyo ndani ya duara iliyoambatana na namba, mara nyingi kwa ufupisho kuwakilisha plastiki chini ya pembetatu. Maelezo ya ziada juu ya ishara, matumizi yake na ubunifu yanaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti ya SPI. Kanuni za urejereshaji za Japan. Japan ina mfumo wa alama za utambulisho wa urejereshaji ambazo zinaonyesha na kuainisha makundi ya vifaa vya kurejereshwa. Ni sawa na kanuni za utambuzi wa resini kwamba zina mishale iliyozunguka ikiwa na maandishi ndani kuonyesha aina ya kifaa. Badala ya kutumia alama ya pembetatu ya urejeshaji kwa vifaa vyote vyenye maandishi tofauti, umbo lililoundwa na mishale pia linatofautiana, ambapo inaruhusu kuweza kutofautishwa kwa kutazamwa tu. Aluminium Paper Plastic Steel KWA TAARIFA ZAIDI REJELEA: Tume ya Ulaya (European Commission). Mawasiliano juu ya matumizi, uzalishaji na mpango wa hatua endelevu wa sera ya viwanda. Mawasiliano kutoka tume ya Ulaya kwa Vyombo vya Umoja wa Ulaya. Tume za Biashara ya Kimataifa. Export Quality Management Bulletin No. 86, Muongozo wa alama na maandiko yanayohusiana na usalama wa chakula, uadilifu wa mazingira na usawa katika jamii. Regulation (EC) No. 66/2010 of the European Parliament and of the Council of 25 November 2009 on the EU Ecolabel. Kanuuni halisi za Ulaya kuhusu Ecolabel.

221 Tathmini Ya Ulinganifu 211 MAREJELEO EU Ecolabel. Forest Stewardship Council. Global Ecolabelling Network (GEN). Green Dot. Pro-Europe Organization. Resin identification codes. The Plastics Web.

222

223 UGEZI

224

225 Ugez Ugezi ni nini na unaumuhimu gani katika biashara ya kimataifa? Ugezi ni neno la kiufundi likimaanisha shughuli zote na taratibu zinazohusiana na vipimo. Lengo la mwisho la ugezi, pia likitafsiriwa kama sayansi ya vipimo na matumizi yake Msamiati wa kimataifa wa utaalamu wa vipimo, 2010) kuhakikisha usahihi, na kulinganishwa na majibu ya kuaminika ya vipimo. Ugezi unaweza kugawanywa katika vipengele vidogovidogo kwenye maeneo yafuatayo: Utaalamu wa jumla au kisayansi. Kipengele hiki cha utaalamu wa vipimo kinashughulika na matatizo ya pamoja katika maswali yote ya utaalamu wa vipimo bila ya kujali wingi wenyewe. Kwa mfano, inagusa kwenye matatizo ya jumla ya nadharia na vitendo kuhusiana na vitengo vya vipimo, tatizo la makosa katika vipimo, na matatizo ya tabia za sayansi ya vipimo za kupima vyombo. Utaalamu wa vipimo wa viwanda. Kipengele hiki kinalenga katika vipimo kwenye uzalishaji na udhibiti wa ubora. Masuala ya kawaida ni taratibu na vipindi vya urekebishwaji, udhibiti wa michakato wa vipimo na usimamizi wa vifaa vya kupimia. Utaalamu wa vipimo wa kisheria. Neno hili linahusiana na mahitaji ya lazima ya kiufundi. Huduma ya utaalamu wa vipimo wa kisheria inaangalia mahitaji haya ili kuhakikisha vipimo sahihi katika maeneo ya maslahi ya umma, kama vile biashara, afya, mazingira na usalama (Misamihati ya kimataifa ya maneno katika utaalamu wa vipimo wa kisheria- International Vocabulary of Terms in Legal Metrology, 2000). Vipimo vinaingia kivitendo katika shughuli zote za kibiashara, kutoka biashara ya bidhaa za wingi (mafuta ya petroli, gesi asilia, mawe na madini ya chuma) mpaka kwenye mauzo ya rejareja ya bidhaa kwa umma katika maeneo ya masoko. Hasa, Biashara ya kimataifa katika bidhaa za viwandani na michakato ya uzalishaji kutumia vipande na vipengele vilivyozalishwa katika kanda/mabara mbalimbali duniani kunahitaji vipimo sahihi, kimsingi katika utaalamu/mfumo wa viimo wa kimataifa. Hii inaweza kufafanuliwa kutumia mifano hapo chini. Biashara ya kimataifa na umuhimu wa mfumo uliokubaliwa kimataifa wa vitengo Tuseme unataka kujua mduara wa bomba, Unataka vipimo katika sentimita au inchi? Kipimo kipi kimeombwa na mteja wako? Sentimita na inchi ni vitengo vinavyohusu mifumo tofauti ya vitengo. Ambapo sentimita ni kigawe kidogo cha mita, kitengo cha urefu cha mfumo wa kimataifa wa vitengo (International System of Units -SI), inchi, ni mali ya kitu kinachoitwa Mfumo wa Vipimo wa kifalme, yaani (Imperial Measurement System). SI (Mfumo wa kimataifa wa vitengo) ni mfumo unaopendekezwa na kutumiwa duniani kote, ambapo vitengo vya kifalme (imperial units) unatumika katika nchi chache au kwa matumizi maalumu. Vipimo vya usahihi wa hali ya juu kama msingi wa teknolojia ya mawasiliano ya simu na habari. Wakati/muda mara nyingi ndio kiasi kinachopimwa. Kwa teknolojia ya leo, muda sahihi unasambazwa/tangazwa kupitia redio, televisheni(runinga), simu, mtandao na kwa njia ya setilaiti/nyota. Mfano wa usahihi wa kupita kiasi wa vipimo vya muda ni mfumo wa kimataifa wa nafasi yaani global positioning system (GPS), ambapo ishara za wakati/muda wa saa ya atomu kutoka katika angalau setilaiti tatu zinatumika kuhesabu nafasi ya kupokea kwenye ardhi na usahihi wa sehemu ya mita. Matokeo haya sahihi ya ajabu yanaweza kupatikana tu kwa sharti kwamba kila saa inazalisha ishara za muda kwa usahihi uleule/mmoja. Teknolojia hii inasaidia kufanya usafirishaji wa bidhaa kuwa rahisi na wa haraka, Unawezesha na kuchochea kasi ya kubadilisha na kurudishwa kwa taarifa/habari na hufanya msingi wa biashara na mauzo ya umeme (Secrets of Electronic Commerce, 2009). Mchango wa utaalamu wa vipimo kwenye tathmini makubaliano na uthibitishaji. Katika masoko ya kimataifa, vyeti mara nyingi huhitajika kama ushahidi wa kukubalika kwa bidhaa au huduma na viwango au kanuni maalum. Katika matukio mengi, tathmini makubaliano na kuangalia tendo la kukubaliana na viwango na kanuni kunahitaji vipimo na majaribio. Kwahiyo vipimo na majaribio ni lazima viwe sahihi ndani ya mipaka fulani, ya kuweza kulinganishwa na kuaminika ili kuhakikisha kujiamini kwa vyeti.

226 216 Ugez Kwa ujumla, usahihi wa vifaa vya kufanyia vipimo unapatikana kupitia urekebishwaji wa mara kwa mara. Urekebishaji unahusisha kulinganisha kifaa cha kupimia na kiwango sahihi zaidi cha kipimo. Viwango vya taifa vya vipimo, ambavyo kawaida vinatoa vipimo sahihi zaidi katika nchi, vinalinganishwa na vya kimataifa au viwango ya nchi nyingine kuhakikisha usambazaji sahihi wa vitengo/kizio duniani kote. Ikiwa mlolongo usiovunjika wa kumbukumbu za alama za vipimo upo kuanzia vipimo vya juu kabisa hadi chini kwenye vifaa vya kupimia kawaida, hapo vipimo vilivyopatikana vinaitwa traceable yaani a kuonekana/kufuatilika. Katika nchi nyingi, taasisi za taifa za sayansi ya vipimo zinawajibika kuhifadhi na kusambaza vitengo vya vipimo ambavyo vinahitajika na maabara za urekebishaji, huduma za mfumo wa meta kisheria na nyinginezo. Urekebishaji wa kupimia kifaa cha majaribio ni wajibu wa mtumiaji au mmiliki. Wajibu rasmi wa kuangalia usahihi, ukaguzi, hufanywa na huduma ya utaalamu wa vipimo wa kisheria kwa ajili ya kupima vifaa katika maeneo yaliyowekwa tayari kama vile ya shughuli za kibiashara. Kila hatua ya kwenda chini katika ngazi ya urekebishaji (angalia mchoro swali namba 84) inashikamana na hupotea kwa usahihi au kuongezeka kwa wasiwasi. Ufuatiliaji ni sharti mojawapo kwa ajili ya kuhakikisha vipimo sahihi ndani ya wasiwasi wa vipimo fulani au, katika kesi ya utaalamu wa vipimo wa kisheria, ndani ya mipaka ya nafuu kimakosa. Mashirika ya kimataifa ya utaalamu wa vipimo kama vile Ofisi ya kimataifa ya uzito na vipimo[international Bureau of Weight and Measures (BIPM)] na Shirika la kimataifa la sayansi ya vipimo kisheria[international Organization of Legal Metrology (OIML)], yakishirikiana na mashirika ya kimataifa ya viwango na vibali, yameanzisha taratibu za kufuata ili kuhakikisha kunakuwa na vipimo sahihi na kuweka kujiamini katika ufanisi/uwezo wa hao wanaotengeneza vyeti. Hivyo Maabara ya vipimo na majaribio yanatakiwa yahakikiwe (angalia swali namba 87). Vipimo hivi vyote vinawezesha biashara ya kimataifa na kusaidia kuepuka kujirudia kwa vipimo. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: EURAMET. Metrology In Short, 3rd ed. July Contact: secretariat@euramet.org Kijitabu hiki kina maelezo ya kina kuhusu utaalamu wa vipimo. Kinaeleza masuala muhimu, kinaelezea mashirika ya kimataifa na kikanda na maelezo ya kuunganika nao pamoja na kutoa mifano ya athari za vipimo. Marbán, R.M. and J.A. Pellecer. Metrology for non-metrologists. ISBN Organization of American States, (Also available in Spanish). Kitabu hichi kina maelezo ya kina kuhusu utaalamu wa vipimo katika lugha itakayoweza kueleweka na mtu asiye mtaalamu wa mfumo wa vipimo. Kinatoa ufafanuzi na kushughulikia vitengo vyote vya vipimo na matumizi yake makuu. Kuhusu utaalamu wa vipimo kisheria na OIML, angalia: Mapendekezo yote, misamiati na nyaraka vinapatikana bure kabisa. Maelezo ya kina yametolewa kwenye tovuti ya OIML Basic Certificate System and Mutual Acceptance Arrangement for types of measuring instruments. Kuhusu utaalamu wa vipimo wa Kimataifa na Mfumo wa Kimataifa wa vitengo, Ufuatiliaji, kubadilishana kwa meta, Mipango ya kuheshimiana vibali, angalia Hii inajadili shughuli za ofisi ya kimataifa ya uzito na vipimo ( International Bureau of Weights and Measures- BIPMT) na kutoa majina ya taasisi ambazo ni muhimu kwa mipango ya kukubali kuheshimiana kwa pandezote. Maelezo ya kina ya mada zilizopo hapo juu. Vitabu bora kwa kuongeza uelewa wa utaalamu wa vipimo na tathmini makubaliano. MAREJELEO International Organization of Legal Metrology International Vocabulary of Metrology Basic and General Concepts and Associated Terms (VIM). 3rd ed International Vocabulary of Terms in Legal Metrology (VIML). English/French International Trade Centre. Secrets of Electronic Commerce: A Guide for Small- and Medium-Sized Exporters. Obtainable from

227 Ugez Je, ugezi ni muhimu kwangu na nini natakiwa kuzingatia? Majibu ya maswali yako katika mchoro yatakusaidia kufanya maamuzi ya ugezi. Timu bidhaa ni pamoja na huduma. Namba katika viboksi vidogo zinarejea maoni zaidi chini. Hatua kuelekea uamuzi wa mfumo/utaalamu wa vipimo(ugezi) Chanzo: Eberhard Seiler, Germany.

228 218 Ugez Maoni: 1. Vipimo ni muhimu kama unataka kufikia vipimo vinavyohitajika na kanuni, viwango, wateja wako, au kama unauza bidhaa zako, kwa mfano, kwa wingi (kg) au urefu (m). Kipaumbele hapa ni vipimo kuliko hivyo vingine vyenye lengo la hesabu, mfano kubaini kama malighafi za kutosha bado zinapatikana au ni kilogramu ngapi zimezalishwa. 2. Kipaumbele hapa ni mahitaji sahihi kama, kwa mfano: 100 mm +/- 0.5 mm or g + 1 g. 3. Mifano: Ikiwa hitaji sahihi ni gramu na uzito wa kifaa chako una nafasi ya mzani(udogo) wa gramu mgao wa uzito wa kifaa chako hautoshelezi. Hata hiyvo, kama nafasi ya mzani ni gramu na umbali katikati ya uzani wa karibu ni mkubwa wa kutosheleza kiasi kwamba gramu inaweza kuamuliwa kama katikati kati ya alama mbili za mzani, mahitaji yaliyotajwa hapo juu yametimia, ilimradi tu vifaa vya kupimia virekebishwa kwa usahihi. Lakini ni hatari kutegemea dhana hii kwakuwa sababu chochezi zinaweza kupunguza usahihi na kitabu kinaweza kua sio sahihi. 4. Usahihi unatakiwa kukaguliwa mara kwa mara ama kwa kulinganisha na vifaa vingine vya upimaji vyenye usahihi wa hali ya juu sana, au kwa kupima kitu kinachowakilisha thamani ya wingi au kiasi (mfano, kipimo sanifu kikubwa kinachowakilisha thamani fulani ya urefu kiasi) Vipimo na vifaa vya majaribio vinahitaji kurekebishwa mara kwa mara kuhakikisha vipimo sahihi kwa ajili ya mlolongo mzima. Unatakiwa kupata wasiwasi ikiwa kifaa chako:-hakikurekebishwa Muda umepita tangu urekebishaji wa karibuni kufanyika, umechukua muda mrefu kuliko inavyopendekezwa na mtengenezaji wa kifaa; au Kifaa chako kimetumika kupita kiasi, mshtuko au mtikisiko wa mitambo, kusambazwa kimakosa kwa volteji (nguvu ya umeme) au hali nyingine isiyo ya kawaida. Yoyote kati ya hali hizi inaweza kusababisha vipimo vyenye makosa na yatahitaji kurekebishwa. 5. Urekebishaji unatakiwa kutunzwa kumbukumbu haijalishi utafanyika ndani ya nyumba, na mtengenezaji au kundi la tatu, yaani shirika/maabara/mtu huru (urekebishaji ndani ya maabara) 6. Uthibitisho unaweza kuhitajiwa na wateja wako na inaweza kuzidisha ushindani. Hata kama uthibitisho hautahitajiwa na wateja wako, fikiria kuhusu matokeo chanya yanayoweza kuleta katika ushindani wako. Hata hivyo, itakulazimu kutumia muda na pesa katika mchakato mzima wa uthibitishaji. Maelezo ya mahitaji ya mfumo bora wa usimamizi yanatolewa katika swali namba 69, na kwa ajili ya uthibitisho wa bidhaa katika swali namba 68. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Measurement Practice Improvement Guide. Compiled and designed by the National Metrology Institute of South Africa (NMISA) and the Physikalisch-Technische Bundesanstalt (PTB), Germany. Mwongozo huu unatoa mfululizo kadhaa wa kauli ambazo unahitaji kupima moja baada ya nyingine kufikia kujitathmini binafsi. Itaweza pia kukusaidia kufikiria utendaji wako pamoja na kuhusu sheria za vipimo na kutambua hatua unayoweza kuchukua ili kuboresha shughuli zako za vipimo. Pia kinapatikana katika lugha ya Kifaransa na Spanish. Mawasiliano: NMISA: enquiries:info@nmisa.org PTB: enquiries: presse@ptb.de

229 Ugez Kipi kati ya vifaa vyangu kinatakiwa kurekebishwa na kwa nini? Vipimo vyote na vifaa vya majaribio vinatakiwa kurekebishwa. Urekebishaji unafanyika ili: Kuhakikisha makubaliano na vipimo vya bidhaa na mahitaji ya bidhaa bora Kuepuka hatari ya uchakavu na kukataliwa Kubaini/kuamua bei na; Kufikia mahitaji ya uthibitisho, mfano. Kulingana na ISO 9001:2008 Urekebishaji unatakiwa kufanywa kwa sababu utendaji wa vipimo na vifaa vya majaribio vinaweza kubadilika kulingana na muda kama matokeo ya shinikizo la mazingira ambapo vifaa hivyo vinawekwa, uchakavu (kwa matumizi), kutumika kupita kiasi au matumizi yasiyofaa. Usahihi wa vipimo na vifaa vya majaribio unatakiwa kuangaliwa kabla ya matumizi na mara kwa mara kuwa sanifu, au baada ya kuwekwa katika sababu chochezi (angalia swali namba 80). Kurudia urekebishaji (Recalibration) sio muhimu kwa baadhi ya vifaa vya kawaida vilivyotengenezwa na kioo kama vile silinda (mitungi ya kupimia), vipande vya bomba, bureti, au baadhi ya vipima joto (thermometers), kama vitatumika kwa masharti ya kazi yaliyowekwa. Wakati wa urekebishaji, thamani ya wingi unaopimwa na chombo au kifaa unalinganishwa na thamani ya wingi huo huo uliotolewa na kiwango cha vipimo. Ikiwa una vifaa vya madaraja tofauti yasiyo na hitilafu kwa wingi mmoja na tofauti sawa ya vipimo, angalau kifaa chenye usahihi wa hali ya juu pia kinajulikana kama precision instrument (yaani kifaa sahihi) kitatakiwa kurekebishwa na maabara ya urekebishaji, ikiwezekana na maabara yenye kibali cha kurekebisha. Vifaa vilivyorekebishwa kwa usahihi vinaweza kutumika kwa ajili ya urekebishaji wa nyumbani wa vifaa dhaifu. Maelezo ya urekebishaji kama vile ufafanuzi mdogo wa njia za kusanifu na/au mchoro, kiwango kilichotumika, majibu yaliyopatikana, tarehe na jina la mfanya kazi/muendeshaji vinatakiwaa kuwekwa kumbukumbu na kuhifadhiwa pamoja na mwongozo wa kazi na nyaraka nyingine zinazohusiana na vifaa. Mara nyingi, majibu ya urekebishwaji au vipimo yanatakiwa kujumuisha mahesabu ya makosa (hali ya wasiwasi). Haya ni mahitaji ya wataalamu wa maabara ya urekebishaji (angalia swali namba 84). Kwa kuwa hesabu zinahitaji maarifa kubwa ya mchakato wa kurekebisha na wa takwimu, inaweza kuwa ngumu sana na sio lazima kabisa kwa urekebishaji kuhitaji usahihi usio wa juu sana (hali ya mashaka isiyo ya chini sana). Badala ya kutumia njia kwa mujibu wa mwongozo unaoelezea hali ya wasiwasi katika vipimo- (Guide of expression of uncertainty in measurement) 2008, taarifa zingine zinaweza kutosheleza. Kwa mfano, kama uhakika wa viwango vilivyotumika ni mara 10 zaidi kuliko ule wa kifaa kinachotakiwa kurekebishwa, mahesabu ya kina hayatakua ya lazima kwa malengo ya ndani ya nyumba. Lakini vyeti vya urekebishaji ni lazima mara zote vionyeshe makosa (angalia swali namba 84). Ni lazima viambatanishwe kwenye kifaa baada ya urekebisho wenye mafanikio kuonyesha tarehe ya urekebishwaji na kuonyesha wazi mtu aliye fanya kazi hiyo. Haishauriwi kutaja tarehe inayofuata ya kufanya tena zoezi hilo kwasababu hii inaweza kuleta dhana kwamba urekebishaji mwingine siyo muhimu mpaka tarehe hiyo. Hii ni kweli pale tu kama kifaa hakijawekwa katika mazingira yasiyo ya kawaida au kama kinaonyesha matokeo yasiyotarajiwa. Ikitokea hali ya urekebishaji sio halali/thabiti tena au urekebishaji ni wa mashaka, kifaa kitatakiwa kuwekewa alama kuwa ni hivyo na kutotumika mpaka urekebisho mwingine utakapofanyika. Urekebishaji uunaongeza ushindani wako kwa kuwa inasaidia kuepuka uzalishaji wa mzozo wa malalamiko kutoka kwa wateja wako.

230 220 Ugez KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Laboratory Accreditation Cooperation and International Organization of Legal Metrology. Guidelines for the determination of calibration intervals of measuring instruments. ILAC-G24/OIML D 10) or Nyaraka hii inabainisha na kuelezea njia zilizopo na zinazojulikana kwa tathmni ya muda wa kurekebisha. Imedhamiriwa kwa matumizi ya maabara ya urekebishaji. Watumiaji wa kawaida wa vifaa wategemee mapendekezo ya watengenezaji/wazalishaji. Hata hivyo, nyaraka ina taarifa ya maslahi ya ujumla na inaweza kutumika kwa uelewa bora wa mahitaji. International Organization for Standardization. ISO 10012:2003, Measurement management systems Requirements for measurement processes and measuring equipment. Obtainable from ISO or ISO members (list at Viwango hivi vinatoa mwongozo juu ya usimamizi wa mchakato wa vipimo na hatua muhimu kuonyesha tendo la kukubaliana na vifaa vya upimaji vilivyotumika na mahitaji ya utaalamu wa vipimo. MAREJELEO International Bureau of Weights and Measures. Evaluation of measurement data Guide to the expression of uncertainty in measurement. JCGM 100: International Organization for Standardization. ISO 9001:2008, Quality management systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at

231 Ugez Wapi vifaa vyangu vinaweza kurekebishwa na kwa mihula ipi? Mara nyingi, mtengenezaji wa kifaa chako au mwakilishi wake katika nchi yako anaweza kurekebisha kifaa chako au maabara ya urekebishaji. Pia, unaweza kuwasiliana na moja ya taasisi hizi: National accreditation body, (Shirika la taifa la vibali) National calibration service, (Shirika la taifa la huduma ya urekebishaji) National metrology institute (Taasisi ya taifa ya utaalamu wa vipimo) National standards body, (Shirika la taifa la viwango) Chamber of commerce and industry, and (Taasisi ya biashara na viwanda) Engineering department of a university. (Kitengo cha ukandarasi kwenye chuo) Ikiwa hakuna maabara ya urekebishaji inayofaa kupendekezwa katika nchi yako, utakubidi uulizie inayofaa kwa nchi jirani. Majina na mawasiliano ya maabara zilizopewa kibali zinapatikana kwenye tovuti ya mashirika ya kikanda ya vibali (regional accreditation bodies) (angalia kwa maelezo zaidi). Chati ifuatayo inaonyesha hatua za kuchagua maabara sahihi ya urekebishaji. Hatua za kuchagua maabara ya urekebishaji * Maabara zenye kibali lazima zitimize masharti ya international standard ISO/IEC 17025:2005, ambapo inamaana kwamba zinatakiwa kutengeneza mfumo bora wa usimamizi, kuajiri wafanyakazi wenye sifa stahiki, kudumisha mazingira ya maabara yanayotakiwa na kutumia viwango vinavyoonekana vya urekebishaji. Maabara yanapewa vibali kwa wingi fulani, vipimo mbalimbali na utovu wa hakika/mashaka. Mambo yote haya matatu yanatakiwa kutimiza mahitaji yako. Cheti cha kibali kinatakiwa kuangaliwa kwa mtazamo huu na pia kuangaliwa/kukaguliwa kama ni halali. Zaidi ya yote, unatakiwa kuangalia ni kwa viwango vipi vya taifa vya vipimo ambavyo maabara inafuata. Majibu na wigo wa usanifu (vipimo mbalimbali, utovu wa hakika) unatakiwa kutajwa katika cheti cha usanifu au katika nyongeza, ambapo inatakiwa kuwa sehemu muhimu ya cheti. ** Kama mteja wako anaulizia cheti cha kimataifa chenye kibali cha urekebishaji, unatakiwa kuchagua maabara ambayo imepewa kibali na shirika la vibali ambalo limetia sahihi Mutual Recognition Arrangement (Mpango wa kuheshimu utambuzi) au MRA la ILAC. Inaitwa mpango wa ILAC, imeanza kufanya kazi rasmi tarehe 31/1/2001. Hata ikiwa hakuna mahitaji kama hayo kutoka kwa wateja wako, maabara zilizopewa kibali na Shirika la vibali na kusaini ILAC arrangement (mpango) zitapewa kipaumbele. *** Angalia swali namba 84 kwa maelezo juu ya ufuatiliaji. Yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa: Ikiwa haujapata maabara ya urekebishaji yanayokidhi mahitaji yako yote, unatakiwa kuchagua yale yanayokidhi mengi ya mahitaji yako na kutafuta maabara ambayo ina ubora kwa ajili ya urekebishaji unaofuata/ujao. Kwa kuongezea kwenye mahitaji ya kiufundi, gharama na muda, usafirishaji na taratibu za kibali vinatakiwa pia kuzingatiwa.

232 222 Ugez Muda wa urekebishaji mara nyingi unnapendekezwa na mtengenezaji wa vifaa vya upimaji au majaribio na inatakiwa uzingatiwe. Hatahivyo, utendaji wa kifaa unategemea na utunzaji na matumizi. Wakati mwingine, urudiaji wa marekebisho huhitajika haraka kwa mfano kwa sababu majibu ya vipimo yaliyopatikana yana mashaka au hayakutarajiwa. Kurekebisha upya pia ni muhimu baada ya kutumia kupita kiasi, usambazaji usio sahihi wa umeme au matukio ya utunzaji mbovu. Mtumiaji wa kifaa anawajibika kuomba kurudiwa kwa urekebishaji kwenye hali kama hizi; vinginevyo, patakuwa na hatari ya vipimo visivyo sahihi. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Maabara za urekebishaji zilozopewa kibali zimeorodheshwa na mashirika ya taifa ya vibali. ILAC na mashirika ya kikanda ya vibali yanatunza tovuti na viunganishi kwa mashirika ya vibali ya taifa katika wanachama wake: Asia Pacific Laboratory Accreditation Cooperation (APLAC). European co-operation for Accreditation (EA). InterAmerican Accreditation Cooperation (IAAC). International Laboratory Accreditation Cooperation (ILAC). Southern African Development Community Accreditation (SADCA). International Laboratory Accreditation Cooperation and International Organization of Legal Metrology. Guidelines for the determination of calibration intervals of measuring instruments. ILAC-G24/OIML D 10) or Nyaraka hizi zinaonyesha na kuelezea njia zilizopo na zinazojulikana kwa ajili ya kutathmini muda wa urekebishaji. Imedhamiriwa kwa matumizi ya maabara za urekebishaji. Watumiaji wa kawaida wa vifaa wategemee mapendekezo ya watengenezaji. Hatahivyo, nyaraka ina taarifa ya maslahi ya ujumla na inaweza kutumika kwa uelewa bora wa mahitaji. MAREJELEO International Laboratory Accreditation Cooperation. ILAC MRA and Signatories. International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC 17025:2005, General requirements for the competence of testing and calibration laboratories. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at

233 Ugez Nani anaweza kushauri kuhusu matatizo ya vipimo? Matatizo ya vipimo yanaweza kuwa makubwa na kuhitaji kufuata muktadha wa mazingira ya vipimo. Hivyo, kabla ya kuwasiliana na shirika lolote lililotajwa hapo chini, unatakiwa kuweka bayana/wazi, mfano: Kusudi la vipimo (m.f kubaini kipenyo cha ndani ya kisima); Kiasi kinachotakiwa kupimwa (m.f urefu)); Vipimo mbalimbali/tofauti (m.f mm 5 mpaka mm 50); Usahihi au mipaka ya makosa inayovumilika (m.f mm, mm); Mahali (benchi la kazi, katika pointi ya ufungaji mitambo, wakati wa uzalishaji, n.k) Mazingira (ya ndani, nje, kutokana na sababu chochezi n.k); Njia (endelevu, kurudia upimaji); The desired indication (direct reading, analogue, digital registration, electronic data transfer, etc.). Pale maswali haya yatakapokuwa yamejibiwa vizuri, utatakiwa uwasiliane kwanza na mwakilishi wa mtengenezaji wa vifaa vyako vya upimaji kwasababu mara nyingi yeye ana uelewa yakinifu wa matatizo yahusianayo na matatizo ya upimaji. Kwa msaada wa injini ya utafutaji, unaweza kupata taarifa ya jinsi ya kujiunga na watengenezaji kupitia mtandao. Ikiwa tatizo la vipimo limeshindwa kupatiwa uvumbuzi na mwakilishi au mtengenezaji wa vifaa, hapo unaweza kuamua kuwasiliana na mashirika au taasisi zifuatazo: Jumuiya ya taifa ya utaalamu wa vipimo- The national metrology association. Katika nchi nyingi, wataalamu wa sayansi ya vipimo wameanzisha chama au jamii kwa ajili ya kubadilishana maarifa kuhusu utaalamu wa vipimo na vifaa, na kuhimiza ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa. Taasisi ya taifa ya utaalamu wa vipimo- The national metrology institute. Hii ni mamlaka ya taifa kwa ajili ya kuhifadhi na kutunza viwango vya vipimo vya taifa; Inaweza pia kuitwa ofisi ya taifa ya viwango au ofisi ya taifa ya uzito na vipimo. Inayo uwezo wa kutoa uzoefu au kufahamu nani mwingine nchini wa kuwasiliana naye. Vitengo vya ukandarasi au fizikia vya chuo- Engineering or physics faculties of universities. Wafanyakazi ambao ni wakufunzi wa vitengo hivi wanaweza kufahamu tatizo lako, au pengine kujua wenzao ambao ni wataalamu katika eneo unalopenda kufahamu. Mashirika ya kikanda au Kimataifa- Regional or international organizations. Ikiwa hakuna mashirika ya kitaifa, au ushauri makini hauwezi kupatikana ndani ya nchi, kanda, mashirika ya kimataifa yanaweza kuombwa msaada. Mashirika makuu ya kikanda yameorodheshwa katika swali namba 82. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Laboratory Accreditation Cooperation. ILAC MRA and Signatories. Mpango wa ILAC unaunga mkono biashara ya kimataifa kwa kutangaza kujiamini na kukubalika kimataifa kwa data za maabara zenye kibali. Vikwazo vya kiufundi vya biashara, kama vile kupima kwa mara ya pili bidhaa kila mara wanapoanza uchumi mpya, kunaweza kupunguzwa.

234 224 Ugez 84. Nini maana ya ufuatiliaji vipimo na upimaji wenye mashaka/ usiokua na uhakika? Kuelezea maana ya ufuatiliaji, tumia mizani inayolingana kama mfano/ kiigizo. Unaweka mzigo kwenye kipimo kimoja na vipande vilivyorekebishwa vya uzito katika kipimo kingine mpaka uwiano ulingane/upatikane. Kuhakikisha matokeo sawia ya seti nyingine za uzito katika maeneo mengine, vipande vilivyorekebishwa vya uzito vinahitajika. Ufuatiliaji unamaanisha kwamba urekebishaji unaweza kufuatiliwa kutoka katika kiwango cha kimataifa, kutoka kwenye kigezo cha wingi na uzito mpaka kilogramu prototype ya kimataifa. Sampuli ya kilogramu hupatikana kwa mcheduara wa platinum-iridium inayowekwa Ofisi ya kimataifa ya uzito na vipimo [International Bureau of Weights and Measures in Sevres, near Paris,France.Vivuli vya sampuli hizi hutumika kama viwango vya uzito vya taifa na hutunzwa katika taasisi ya sayansi/utaalamu wa vipimo ya taifa. Ingawa zinatengenezwa kwa uhakiki/umakini wa hali ya juu kabisa, vivuli huonyesha tofauti binafsi ndogondogo zinapolinganishwa na sampuli za kilogramu. Vipimo vya ulinganishi vinaporudiwa hutofautiana kidogo kwa sababu ya vichochezi vilivyo pangiliwa na visivyokua kwenye mpangilio maalum[mf. Mazingira] na huongeza/hutia shaka katika matokeo. Matokeo kamili ya urekebishaji ni dalili ya kubadilika thamani ya kiwango[aidha kuongeza au kupunguza] na makadirio ya hitilafu/mashaka ya thamani hii[katika mielekeo yote kuongeza na kupunguza]. Sasa tuelekee katika nadharia ya makosa ya upimaji. Namna ya kugundua makosa ya upimaji inaelezewa kwa undani katika` Muongozo wa ISO/IEC kwa maelezo ya makosa katika upimaji, ambao pia inajulikana kama GUM. Kulingana na utaratibu wa GUM, viungo vyote muhimu ambavyo vinachochea makosa vinatakiwa vitambuliwe. Kila kiungo katika upimaji wa makosa kitaelezewa kama kiwango cha makosa cha aina A au B. Kwa aina A na B, migawanyo ya uwezekano tofauti inatumika. Kwa aina A, mgawanyo uliochunguzwa utatumika[uliotoka katika vipimo viliorudiwa], Kwa aina B mgawanyo uliosadikiwa utatumika. Mjumuisho huu wa makosa utakokotolewa kwa kuchanganya viungo binafsi vya makosa kulingana na sheria ya uenezaji/uzalishaji wa makosa. Ili kulinganisha makosa, sababu za taarifa za matukio K lazima itumike kwa ule mjumuisho wa mashaka na uelekezi.k=2 utatarajia kama asilimia 95% ya matokeo baina ya kiasi kilichopatikana kwa makosa. Makosa ya kipimo na sababu za taarifa za matukio lazima zitunzwe kama nyaraka ndani ya cheti cha marekebisho pamoja na taarifa zote kama vile hali za mazingira pamoja na mfumo wa urekebishaji. Ufuatao ni mfano wa matokeo yanayooneshwa katika cheti cha marekebisho: R = ( ± ) Coverage factor: 2 Kwa ukaguzi yakinifu wa ndani wa vifaa vya upimaji, ukokotoaji wa upimaaji wa makosa mara nyingi hauhitajiki, lakini taarifa za ukaguzi zinatakiwa zitunzwe katika nyaraka[angalia swali la 81] Ufuatiliaji kwa ujumla unahitaji mfululizo wa marekebisho na viwango sahihi tofauti tofauti. Ngazi hii ya urekebishaji wa presha ya kiasi (quantity pressure) inaonyeshwa kwenye mchoro chini.

235 Ugez 225 Ngazi ya urekebishaji kwa kutumia presha ya kiasi Chanzo: EAL-G12: Traceability of Measuring and Test Equipment to National Standards, November Presha ni SI unit iliyozalishwa na jina pascal, alama ya Pa. Ni kipimo cha fosi(force) kwa eneo na kinafafanuliwa kama newton 1 (N) ya fosi(force) inayotumiwa kwenye eneo la meta mraba moja. Inaelezewa katika SI units kama N/m². Inaweza kuelezwa katika SI base units kama kg/(m s²) (s ikiwa kama ya pili) Viwango vya msingi vya taifa vinatakiwa kutambuliwa kulingana na ufafanuzi. Hiki ni kifaa ambapo fosi ya uwezo unaojulikana inatendeka kwenye eneo husika. Utambuzi ni kazi ya kawaida ya maabara ya taifa ya mfumo wa meta. Mchoro hapo juu unaonyesha kwa juu vifaa viwili ambavyo vinatambua presha kulingana na ufafanuzi na comparator. Fosi inatengenezwa kwa ama kumiminika au solid masses chini ya mvutano wa ndani unaofanyika juu ya uso. Wingi, mvutano wa ndani na eneo linalohitajika kubainika na usahihi wa hali ya juu (mashaka kidogo) ili kutambua na kuzalisha presha ya kiasi kinachofahamika. Viwango vya taifa vya presha vinatumika kurekebisha kinachojulikana kama kumbukumbu ya viwango vya usahihi mdogo itumiwayo na maabara za marekebisho, mara nyingi zenye kibali, na pia taasisi za taifa za utaalamu wa vipimo ili kurekebisha viwango vya kazi. Viwango ambavyo vinatumika kwa ajili ya urekebishaji wa kila siku na maabara za marekebisho vinaitwa viwango vya kazi, au viwango vya viwanda kama zikitumiwa na viwanda kwa ajili ya usanifu wa ndani. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Da Silva, Ricardo Bettencourt. Uncertainty and Metrological Traceability. PowerPoint presentation. Inawasilisha nadharia ya ufuatiliaji, aina za kumbukumbu za vipimo, namna ya kudhihirisha ufuatiliaji na kuonyesha masomo husika. EURAMET. Metrology In Short, 3rd ed. July Contact: secretariat@euramet.org Kijitabu hiki kina mtazamo wa kina juu ya utaalamu wa vipimo. Kinaelezea maneno muhimu, kinafananua mashirika ya kimataifa na kikanda na jinsi ya kuwapata/kujiunganisha nao, na kutoa mifano ya matokeo ya vipimo. European co-operation for Accreditation. List of European co-operation for Accreditation Publications. Kinaorodhesha machapisho ya EA katika mifululizo tisa: Kwa ujumla, maombi na kimataifa, kati ya mengine. International Accreditation Service, Inc. IAS Policy Guide on Calibration, Traceability, and Measurement Uncertainty for Calibration Laboratories

236 226 Ugez Nyaraka hizi zinaelezea sera za LAS za maabara za usanifu (za nddani au nje) na ufuatiliaji wa usanifu, na kujadili makadirio ya utovu wa hakika wa vipimo. Laboratory Accreditation Bureau. Marejeo/kumbukumbu nzuri ya utovu wa hakika/mashaka. Inaangalia majibu ya maswali: Nini cha kuzingatia katika utovu wa hakika/mashaka juu ya bajeti ya vipimo? na namna gani utovu wa hakika unatumiwa kwenye vipimo wakati wa kuandaa maelezo ya maafikiano kulingana na ILAC G8? Maelezo ya kina zaidi ya ufuatiliaji wa makosa yakijumuisha michoro na mifano. Kama unataka kujua ni kitu gani mtoaji wa majibu ya vipimo au thamani ya viwango anatakiwa kuweka kumbukumbu ili kustahili ufuatiliaji, utapata maelezo kwenye: The American Association for Laboratory Accreditation. Policy Measurement Traceability Sera hii inaelezea nadharia ya ufuatiliaji wa vipimo, namna ya kuweza kuyapata, na namna yanaweza kuonyeshwa dhahiri. MAREJELEO European co-operation for Accreditation. Traceability of Measuring and Test Equipment to National Standards. EAL-G12. November Contact: International Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC Guide 98-3:2008. Uncertainty of measurement Part 3: Guide to the expression of uncertainty in measurement (GUM:1995). Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at

237 Ugez Nitafanya nini kuhusu vipimo ikiwa ninahitaji kuthibitishwa kwa mujibu wa ISO/IEC 9001:2008? Vipimo ni sehemu ya mfumo wa uongozi bora. Kwa mujibu wa kipengele cha 7.6 cha ISO 9001:2008, unatakiwa kujua wazi vipimo gani ni muhimu na vifaa gani vya vipimo vinatakiwa kutoa ushahidi wa usawa wa bidhaa kwa mahitaji yaliyoamuliwa. Kwanzia kwenye bidhaa unazozalisha, unatakiwa kutambua kigezo cha kupimwa na kusimamia wakati wa uzalishaji. Unatakiwa kuanza na ukaguzi wa nyenzo zinazofuata na sehemu au vipengele ambavyo vinatakiwa kuangaliwa kuwa vina ukubaliano na vipimo. Ikiwa kwa mfano, umeagiza karatasi ya chuma(sheet metal) ya unene/uzito kiasi, unatakiwa uiangalie au uichunguze kabla ya kuanza uzalishaji. Ni lazima uamue ama vernier caliper au micrometer screw inayohitajika kubainisha uzito wa usahihi wa kutosha (angalia swali namba 80). Vivyo hivyo, tendo la kukubaliana na vipimo linatakiwa kupimwa wakati wa uzalishaji. Hivyo, michakato inatakiwa kuanzwa ili kuhakikisha kwamba vipimo muhimu vinafanyika katika njia thabiti na mahitaji. Kwa mujibu wa ISO 9001:2008: Pale ambapo ni muhimu kuhakikisha matokeo halali, vifaa vya vipimo vinatakiwa kurekebishwa au kuthibitishwa ndani ya muda fulani, au kabla ya matumizi, dhidi ya viwango vya vipimo vinavyoonekana kwenye viwango vya vipimo vya kimataifa au kitaifa; pale viwango hivyo vinapokosekana, msingi wa marekebisho au ukaguzi ni lazima uwekwe katika kumbukumbu. (angalia swali namba 82). Kifungu kidogo cha kifungu cha 7.6 pia kinainisha marekebisho, utambulisho na ulinzi wa vifaa vya vipimo. Kumbukumbu ya majibu ya urekebishaji au ukaguzi lazima yatunzwe/yaimarishwe. Kwa kuongezea, vipimo, uchambuzi na maboresho ya michakato lazima yapangwe, yatekelezwe na yasimamiwe (kifungu cha 8). Lengo kuu ni kuainisha kwamba michakato yote ya vipimo inazingatia mahitaji kuonyesha ukubaliano na vipimo, inawekwa kumbukumbu na kutekelezwa vizuri. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Organization for Standardization. ISO 10012:2003, Measurement Management Systems Requirements for measurement processes and measuring equipment. Obtainable from ISO or ISO members (list at ISO 10012:2003 inaweka bayana mahitaji yote na kutoa muongozo wa mchakato wa usimamizi wa vipimo na uthibitisho wa utaalamu wa vipimo wa kupima vifaa vilivyotimika kusaidia na kuonyesha ukubaliano na mahitaji ya kiutaalamu ya vipimo. Inabainisha mahitaji ya usimamizi bora wa mfumo wa usimamizi wa vipimo ambao unaweza kutumika na shirika kufanya vipimo kama sehemu ya ujumla ya mfumo wa usimamizi na kuhakikisha mahitaji ya kimfumo wa meta yanazingatiwa. MAREJELEO International Organization for Standardization. ISO 9001:2008, Quality Management Systems Requirements. Obtainable from ISO or ISO members (list at

238 228 Ugez 86. Kuna mahitaji gani ya vipimo kwa bidaa zilizofungashwa kabla ya kuuzwa? Mahitaji ya bidhaa zinazofungwa kabla ya kuuzwa na zinazotolewa kwa ajili ya kuuza yamewekwa katika nchi nyingi na mara nyingi zinatofautiana. The International Organization of Legal Metrology (OIML) imeandaa mapendekezo mawili juu ya mahitaji haya: R 79, Labelling requirements for pre-packed products (1997) and R 87, Net content in packages (2004/2008). Ambapo R 79 inafafanua sheria za vifurushi na inaweka mahitaji kwa ajili ya kuvipatia lebo, yaani nembo, R 87 Inaweka bayana mahitaji ya utaalamu wa vipimo kwa ajili ya bidhaa zilizofungashwa katika ujazo mdogo wa mara kwa mara na kuainishwa kwa njia ya wingi au kiasi. Kiasi kingine kuacha wingi na ujazo (urefu, eneo, namba) siyo sehemu ya R 87. Mapendekezo yamechapishwa kwenye tovuti ya OIML. Mahitaji makuu yanahusu wastani wa ujazo: wastani halisi wa ujazo ulioelezewa na kiasi chochote cha bidhaa zilizofungwa tayari kwa ukaguzi lazima ziwe sawasawa au zizidi ujazo halisi kama ilivyolezwa katika kifurushi. Hii ni lazima itimie pale bidhaa zinapokuwa tayari kwa kuuza kwenye pointi ya kupaki/kufunga au, wakati husika, kwenye pointi ya kuagiza/kuingiza bidhaa. Mapungufu kutoka kwenye kiasi kilichotajwa ni ruhusa tu kwa vifurushi/mizigo binafsi, ilimradi siyo makubwa kuliko mipaka maalum iliyowekwa kama ilivyoelezewa na mapendekezo ya OIML. Nchi wanachama wa OIML wanatakiwa kutumia mapendekezo haya kama msingi wa kanuni zao za kitaifa. Taarifa kuhusu kama mapendekezo haya yalitumika katika kanuni za nchi inapatikana kwenye linki iliyotolewa katika sehemu Kwa maelezo zaidi chini ya kichwa cha habari uchunguzi juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya kimataifa ya OIML. Hata hivyo, tendo la kukubaliana na mapendekezo haipelekei sana kwa bidhaa kupata kibali katika kila nchi, kwa sababu inaweza isiwe mwanachama wa OIML au inaweza ikawa inatumia kanuni tofauti pamoja ya kwamba ni mwanachama wa OIML. Taarifa ya kanuni za utekelezaji zinaweza kupatikana kutoka national legal metrology services. Anwani za wanachama wa OIML sambamba na wanachama (kwa ujumla ni kama 100) wametajwa katika linki iliyowekwa sehemu ya Kwa maelezo zaidi. Hivi sasa, OIML inashughulikia marudio ya mapendekezo na mfumo wa uhakiki wa hiari kwa ajili ya bidhaa zilizofungwa kabla ya kuuzwa (angalia kipengele cha OIML katika marejeo). Kanuni za Umoja wa nchi za Amerika na Ulaya zimeorodheshwa chini. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: Council Directive of 20 January 1976, on the approximation of the laws of the Member States relating to the making-up by weight or by volume of certain prepackaged products (76/211/EEC) (OJ L 46, , p. 1). Amendments: M1 Commission Directive 78/891/EEC of 28 September 1978, OJL 311, , p. 21. M2 Directive 2007/45/EC of the European Parliament and of the Council of 5 September 2007, OJL 247, p. 17. European Cooperation in Legal Metrology, WELMEC: Guide for packers and importers of e-marked prepacked products, June Mwongozo huu unatumika kama kitabu cha muongozo kwa wafungaji wanaotumia E-mark ambao wanataka taratibu zao zitambulike kwa kuungana na kanuni za E-marking, au ambao wanataka kuboresha taratibu ambazo tayari zinatambulika. Maudhui/yaliyomo yanahusu zaidi mahitaji ya kisheria, tafsiri zake zilizotolewa na WELMEC na ufumbuzi wa vitendo na mapendekezo. European legislation on prepackages. C~&checktexte=checkbox&visu=#texte Mwongozo 2007/45/EC wa bunge la Ulaya na Tume (European Parliament and of the Council of 5 September 2007) ikiorodhesha sheria za majina ya kiasi(uzito) kwa ajili ya bidhaa zisizofungwa, repealing Council Directives 75/106/EEC and 80/232/EEC, and amending Council Directive 76/211/EEC. International Organization of Legal Metrology Member States and Corresponding Members, Addresses. OIML ni hifadhi ya data inayoonyesha nchi wanachama na anwani Inquiry on the implementation of OIML International Recommendations, Results. Hapo awalibiml ilifanya uchunguzi juu ya utekelezaji wa mapendekezo ya kitaifa ya OIML ambazo zilitayarishwa baada ya kila miaka minne ikijumuisha na warsha/hafla ya OIML. Kuanzia warsha/hafla ya Sydney mwaka wa 2008, swala hili

239 Ugez 229 limekua jambo la utafiti. Wanachama wa CIML, waakilishi wa OIML na waakilishi wa nchi tofauti walitoa ombi la kushiriki katika awala hilo na kutoa majibu yao kupitia mtandao hivyo kurahisisha kuongeza ujumbe kwa wavuti wakati wowote. National Institute of Standards and Technology. NIST Handbook 133, Checking the Net Contents of Packaged Goods as Adopted by the 89th National Conference on Weights and Measures (2004), United States regulations. Kitabu hiki kimeandaliwa kama mwongozo wa taratibu kwa majaribio ya makubaliano/ulinganifu wa taarifa za ujazo halisi kwenye bidhaa zilizofungwa. Majaribio ya ulinganifu wa bidhaa zilizofungwa ni maamuzi ya makubaliano/kufanana kwa matokeo ya ufungaji, usambazaji na mchakato wa rejareja (vifunrushi/mizigo) na mahitaji kadhaa ya kisheria kwa ajili ya matangazo au matamko ya ujazo halisi. MAREJELEO International Organization of Legal Metrology Labelling requirements for prepackaged products (1997). R Prepackaged products. OIML Bulletin, vol. LI; Number 3, July Quantity of product in packages (2004/2008). R 87. International Organization of Legal Metrology.

240

241 KIBALI (ITHIBATI) ITHIBATI

242

243 Kibali (Ithibati) Nini thamani ya ithibati (kibali)? Dhana Ithibati ni utambuzi rasmi wa ufanisi. Kwa kawaida idhini hutolewa na shirika la ithibati kutumia vigezo vilivyofafanuliwa katika miongozo na viwango vya kimataifa vilivyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Viwango (the International Organization for Standardization (ISO) na Tume ya Kiufundi (Electrotechnical Commission (IEC), yaani ISO/IEC jumuiya ya viwango. Huu unaweza kuwa mtazamo finyu katika baadhi ya mazingira na masoko, ambako viwango vingine vinaweza vikawa vinatumika. Kwa mfano, nchi nyingine bado zinatoa kibali kutumia viwango vya kitaifa ambavyo haviwiani na viwango vya kimataifa vya sasa. Kupata utambulisho wa kimataifa hatahivyo, kutumika kwa viwango vya kimataifa inapendekezwa zaidi. Maombi ya Tathmini ulinganifu Kutoka hatua ya mtazamo wa tathmini ya ulinganifu, ithibati inatumika kwenye maabara, vyombo vya ukaguzi na uthibitisho(cheti). Mchakato wa ithibati umekuwa ukitumiwa maabara tangu 1940s. Watumiaji wa huduma ya maabara mara nyingi wanao uelewa wa kibali na maarifa ya kisasa ya thamani yake. Kibali cha vyombo vya uthibitisho ni jambo linalofanyika zaidi siku hizi. Wakati panatokea uhitaji wa kustaajabisha wa kuthibitishwa, kibali chake pengine hakizingatiwi sana. Vivyohivyo, kibali cha vyombo vya ukaguzi ni zoezi linaloendelea hivi sasa, na kukua katika umuhimu kwakuwa ukaguzi wa serikali katika nchi nyingi unapungua na kazi yao kuchukuliwa na sekta ya binafsi. Katika mazingira haya ithibati hutoa uhakika wa kuendelea kwa ufanisi na kinatumika na serikali kama jambo la kiutaratibu la kupata leseni. ithibati inaongeza thamani kwa vyombo vya tathmini makubaliano na vilevile kwenye usimamizi wao katika njia nyingi, kama ilivyoelezwa kwenye Faida za kibali hapa chini. Hata hivyo, ni kipaumbele kwa maabara fulani, shirika la uthibitisho au la ukaguzi kutegemeana na mtazamo wa wadau wake na mazingira ya soko ambapo yanafanyia shughuli zake. Mmiliki au uongozi wa makampuni ya biashara yanaweza kutafuta uhakikisho kuwa, kuamua kutekeleza mfumo wa usimamizi bora (a quality management system (QMS) kama vile ISO 9001, shirika la uthibitisho lililochaguliwa lina uwezo wa kutoa huduma ya uthibitisho(cheti). Ithibati ya shirika la uhakiki inatoa uhakikisho kwa wote, mteja na wateja wao, kwamba shirika la uhakiki linashugulika kwa ufanisi na kwa hivyo uthibitisho au uhakiki wanaoutoa ni halali. Ithibati ya mashirika ya uhakiki ndani ya mfumo wa usimamizi wa ubora (QMS) kinatolewa katika suala la sekta ya viwanda kwa ujumla ambapo shirika la uhakiki linao uzoefu na baadhi ya utaalamu. Ithibati ya maabara, tofauti na ile ya shirika la uhakiki wa bidhaa au chombo cha ukaguzi, kinahusisha ukaguzi mkali katika ufanisi wa wafanyakazi wa kiufundi wa majaribio na vipimo fulani au bidhaa, kwa kuongezea kwenye tathmini ya mfumo wa usimamizi (uongozi). Faida za ithibati Watumiaji wa huduma ya maabara wanaguswa sana na kuaminika na usahihi wa majaribio ya data. Wamiliki wa maabara, hasa makampuni makubwa au wawekezaji, wanaweza kuhitaji maabara yao kupatiwa kibali cha kuweka nidhamu kwenye uongozi/usimamizi wao na hivyo kuwahakikishia kuwa maabara yanashughulika katika namna ya ufanisi kiufundi na kwamba data wanazozitoa ni za kuaminika. Kwa uongozi wa maabara, tathmini ya nje ya kiufundi inayofanywa na wataalamu wa chombo/shirika la kibali inaleta imani kuwa maabara inafanya bidii sana kiutendaji katika viwango na kwamba, ndani ya wigo wa kibali chake, linaaminika kwa kuwa na ufanisi kamili na kuongozwa vizuri angalau kufikia viwango vya washindani wake. Ithibati inaweza kujenga imani katika ufanisi wa maabara na uadilifu. Hii haimaanishi kwamba maabara ambazo hazina kibali hazina sifa hizo, bali inatoa ishara hiyo. Ithibati inaweza kuchukua nafasi ya aina yoyote ya tathmini ambayo ingekua imefanywa na mteja binafsi. Kwa maabara, Ithihati hakika haikingilii sana kuliko tathmini nyingi za wateja mbalimbali. Kwenye baadhi ya masoko au kwa wateja fulani, mahitaji maalum huwekwa juu/zaidi ya mahitaji ya kawaida ya kibali. Hizi mara nyingi huwa za kiutawala kiasili, lakini zinaweza kuwa na chembechembe za kiufundi kama vile ushiriki katika mipango fulani ya ustadi wa kupima. Katika mazingira haya, mteja wakati mwingine anafanya tathmini kwa mujibu wa mahitaji haya maalumu na, katika kufanya hivyo, anaweka/anatumia aina nyingine ya kibali. Katika kesi nyingine, mteja

244 234 Kibali (Ithibati) anaweza kuliambia shirika la kibali kushughulikia mahitaji ya nyongeza katika tathmini yake ya maabara ambapo mahitaji yamewekwa tayari. Tathmini ya nyongeza sasa inaweza kujumuishwa katika wigo wa kibali. Hii inatokea pale serikali zinapotumia mashirika ya vibali kwa ajili ya shughuli za udhibiti na kuwaambia mashirika ya vibali yafanye tathmini kinyume na kanuni pamoja na viwango vya kawaida vya kibali. Katika baadhi ya nchi ambapo, kwa mfano, serikali fulani yenye mamlaka inapohitaji kibali au pale kiwanda kinapopitisha kibali kama suala la kiwango, inaweza kuwa ngumu, hata isiwezekane, kufanya biashara bila kibali. Katika nchi hizi, kibali kinakuwa leseni ya moja kwa moja ili kufanya kazi/biashara. Mifano ya mazingira kama haya yanaweza kuonekana hasa katika nchi zilizoendelea. Sera hizo zinaweza kushughulikia maabara, vyombo vya ukaguzi na mashirika ya uhakiki. Huwa inasemwa kuwa ithibati ni gharama isiyo ya lazima au inagharimu sana. Kwenye baadhi ya mazingira hii inaweza kuwa kweli. Hata hivyo, kwa maabara mengi, gharama za ithibati ni ndogo ukilinganisha na gharama za kutekeleza viwango ambavyo ni lazima vitimizwe kwa hali yoyote. Kibali kinaondoa gharama nyingi zilizojificha zinazolandana na kujenga imani katika soko na kutunza imani hiyo kwa msingi endelevu. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA International Accreditation Forum (IAF). Tovuti ya LAF inatoa habari zaidi juu ya tathmini makubaliano ya mifumo ya uongozi, bidhaa, huduma, wafanyakazi na mipango kama hiyo ya tathmini makubaliano. International Laboratory Accreditation Cooperation. Tovuti ya ILAC inawapa wasomaji habari zaidi kuhusu ILAC, ILAC MRA, waliotia saini makubaliano pamoja na uanachama wake, matukio, na machapisho na rasilimali nyingine. International Laboratory Accreditation Cooperation. Why Use an Accredited Laboratory? Kipeperushi kidogo kuhusu sababu kuu za kuchagua maabara ya kibali kukamilisha upimaji wako, usanifu au mahitaji ya vipimo. International Accreditation Forum and International Organization for Standardization. Expected Outcomes for Accredited Certification to ISO Kipeperushi kuhusu unachotarajia kutoka uthibitisho/cheti cha kibali hadi ISO Expected Outcomes for Accredited Certification to ISO Kipeperushi hiki kinapeana maelezo kuhusu matarajio kutoka kwa ISO Unger, Peter. Accreditation: A Viable Tool for Import Safety. American Association for Laboratory Accreditation. Kitabu cha kurasa sita kinachojadili faida za kibali na wajibu wa American Association for Laboratory Accreditation (A2LA).

245 Kibali (Ithibati) Nini kinaweza kupewa Ithibati? ISO/IEC 17000:2004 inafafanua ithibati kama kundi la tatu la ushuhuda kuhusiana na shirika la tathmini makubaliano kuwasilisha udhihirisho rasmi wa ufanisi wake kushughulikia kazi maalumu za tathmini makubaliano. Hii ina maana kwamba, mashirika ya tathmini makubaliano-vyombo vya ukaguzi, maabara za majaribio, aina mbalimbali za mashirika ya uthibitisho-bidhaa na aina mbalimbali za mfumo wa mashirika ya uthibitisho, maabara za vipimo na vyombo vya ukaguzi wa ubunifu, vyote vinaweza kupewa kibali. Katika aina yake ya sasa, kibali kilianzishwa Australia mwaka 1947 na awali kililenga maabara kufanya upimaji wa kawaida wa bidhaa na vifaa katika masomo ya desturi kisayansi-biolojia, kemia, uhandisi na fizikia. Wigo wa kibali ulikuwa ukionyeshwa katika masuala ya mchanganyiko wa masomo, bidhaa, vipimo na viwango. Kwa mfano, maabara inaweza kupewa kibali kwa ajili ya uchambuzi wa kikemia wa chuma cha kaboni na chembechembe za aloi kwa kutumia njia zilizoainishwa katika viwango vya taifa husika au kwa kutumia mbinu maalum. Ithibati ya mashirika ya isthibati kilianza huko Uingereza mwanzoni mwa mwaka 1980s kutokana na maendeleo ya sheria za viwango katika General Agreement on Tariffs and Trade (GATT) yaani Mkataba wa Ujumla wa Ushuru na Biashara, mtangulizi wa WTO. Awali, ilijihusisha tu na bidhaa na viwango ikiyo na uhusiano na usalama na utendaji. Kibali cha mashirika yanayoshughulikia uthibitisho kinyume na mifumo ya viwango (kama ISO 9001) klikua kinatolewa sana miaka ya 1990s. Ufafanuzi wa wigo wa uthibitisho huo ni mpana sana kuliko ufafanuzi wenyewe unaotumika katika maabara au uthibitishaji wa bidhaa, kwa ababu kiujumla wanahusisha na viwanda na makundi ya shughuli. Kwa maelezo zaidi, rejea kwa IAF ID1:2010 (angalia kwenye kipengele kwa maelezo zaidi chini). Kwenye miaka ya karibuni, mipango ya uthibitisho imeboreshwa kwa mifumo mingine ya viwango kama vile ISO 14001, HACCP na ISO Hii pia imetokea kwenye viwango vilivyoandaliwa na biashara kubwa kama watengenezaji wa motokaa na misururu ya ununuzi wa rejareja. Kibali cha ukaguzi ni jambo la hivi karibuni katika tathmini makubaliano ambalo linatakiwa litambulishwe kwa upana zaidi. Kama ilivyoonekana katika swali la 65, ISO/IEC iliasisiwa mwaka Wigo wa kibali cha ukaguzi una uhusiana na bidhaa au huduma na zinaelezewa katika masuala ya viwango, sheria, na kanuni. Kibali cha maabara pia kijadi kimeshughulikia huduma za usanifu na, punde tu, huduma nyinginezo zinazounga mkono maabara kama vile Proficiency testing providers (mabingwa wa upimaji); Reference material providers (watoa marejeo ya vitabu/kumbukumbu); Research laboratories (maabara za utafiti). Mashirika kama hayo yanaweza kutafuta kibali kinyume na viwango sawa vilivyotolewa kutoka viwango vya ISO 9001 na ISO/IEC Katika miaka ya karibuni, kanuni hizo hizo zimekuwa zikitumika kwa upana zaidi pamoja na: Dawa za maabara, ambapo lengo kuu ni utambuzi wa tatizo na usimamizi kuliko tathmini makubaliano; Diagnostic imaging (medical radiology and others);- a kuchunguza na kubainisha ugonjwa Forensic science; sayansi ya kuchunguza chanzo cha kifo Personnel certification; uthibitishaji wa wafanyakazi Software testing, security-related activities. Majaribio ya software na shughuli za kiusalama Wakati haya hayahusiani sana moja kwa moja na tathmini makubaliano, mipango inatumia dhana kuu moja na vigezo (ufanisi wa kiufundi na uongozi bora) na kutumia mchakato wa tathmini rika kwa ajili ya tathmini ya ufanisi. Neno kibali lina matumizi makubwa ya jadi katika masuala mengine yasiyohusiana na tathmni makubaliano, lakini katika eneo hili, kibali mara zote kinatumika ipasavyo kwenye mazingira ambayo familia ya viwango vya ISO/IEC inatumika.

246 236 Kibali (Ithibati) Uthibitisho wa wafanyakazi- Personnel certification Haya ni maboresho ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakizidi kuongezeka umaarufu wake.uthibitisho wa wafanyakazi unahusiana na utambuzi wa wafanyakazi kuwa na maharifa fulani, utaalamu au ustadi na kuweza kuthibitisha uwezo wa kutumia ujuzi/ustadi huo. Hii ni tofauti na kuwa na sifa za elimu ya darasani ingawa inaweza kuwa sharti kwenye mchakato wa uthibitisho. Mashirika ya uthibitisho wa wafanyakazi yanapaswa kutii mahitaji ya ISO/IEC Mchakato wa uthibitisho lazima uwe huru na mipango ya mafunzo yaliyokusudiwa kuongoza uthibitishaji. Kama ilivyo kwa aina zote za uthibitisho, mchakato pia unahusisha utoaji usimamizi wa utendaji na marudio ya uthibitisho kwa mihula. Ithibati ya mashirika ya kawaida na makundi yanayofanya tathmini ya ulinganifu Makundi ya kawaida yenye ithibati ya tathmini na Ulinganifu (CABs) Maabara za udhibitishaji/urekebishaji wa vipimo Viwango vya kimataifa ambavyo Ithihati inatolewa kwa Mashirika na CABs ISO/IEC Viwango Mahitaji na viwango vya wateja wa CABs na mashirika Vipimo mbalimbali na vigezo mbalimbali vya vifaa Maabara za vipimo vya kawaida ISO/IEC Vipimo mbalimbali na mahitaji mahususi ya bidhaa Maabara za tiba ISO/IEC Vipimo mbalimali vya uchunguzi Mashirika ya ukaguzi ISO/IEC Mahitaji mbalimbali ya bidhaa na kisheria Mashirika ya Uhakiki i. Mfumo wa usimamizi wa ubora ISO/IEC ISO 9001 ii. Mfumo wa usimamizi wa mazingira ISO/IEC ISO iii. Mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula ISO/IEC ISO iv. Product certification ISO/IEC Guide 65 Mahitaji mbalimbali mahususi kwa bidhaa v. Uhakiki wa watu/wafanyakazi ISO/IEC Mahitaji maalum ya ujuzi Chanzo: John Gilmour, Australia. KWA MAELEZO ZAIDI REJELEA: International Accreditation Forum (IAF). IAF Informative Documents. IAF ID 1:2010 Issue 1 QMS Scopes of Accreditation. Waraka wenye maelezo ya kuwezesha matumizi thabiti ya ISO 17021:2006. Una orodha ya sekta/shughuli za uchumi na makala za sheria za LAF NACE (mgawanyo, kuundi, daraja). International Organization for Standardization. Mechanisms for performing conformity assessment. Waraka wenye kurasa tatu ambazo kwa kifupi zinajadili upimaji, vyombo vya ukaguzi, uthibitisho na uthibitisho wa mfumo wa usimamizi, kati yam engine. International Personnel Certification Association.

247 Kibali (Ithibati) 237 IPC inatoa utambuzi wa watu binafsi ambao, kwa wao kudhihirisha ufanisi kwa IPC-miradi iliyohakikiwa, inaweza kuboresha utendaji wa mashirika United Kingdom Accreditation Service (UKAS). UKAS inatathmini na kuhakiki maabara, vyeti na vyombo vya ukaguzi, kati ya mengine. MAREJELEO Organization for Standardization and International Electrotechnical Commission. ISO/IEC 17000:2004, Conformity assessment Vocabulary and general principles. Obtainable from ISO or ISO members (list at and from IEC or IEC National Committees (list at

248 238 Kibali (Ithibati) 89. Nini tofauti kati ya uhakiki na ithibati ( kibali)? Kwa maelezo rahisi, uhakiki ni taarifa ya taasisi huru ambapo bidhaa au huduma imekidhi viwango au mahitaji. Kwa upande mwingine ithibati ni taarifa ya shirika lenye mamlaka kwamba shirika lingine lina uwezo kiufundi wa kufanya shughuli fulani zilizoainiswa. Shughuli zote zinategemea viwango kama vigezo vya msingi, lakini ithibati imeongezewa mchakato wa mapitio ya wataalam husika kuhakikisha uwepo wa maarifa na utendaji bora wa eneo fulani la sayansi au teknolojia, ambapo kawaida haiwezekani katika viwango kiujumla. Mashirika ya ithibati, pale utambulisho wa kimataifa unapohitajika, yanafanya kazi kwa mahitaji ya ISO/IEC Mashirika ya uhakiki yanafanya kazi kwa viwango vingine sahihi (angalia swali namba 88). Kibali ni huduma ambayo inatoa usimamizi na uaminifu kwa mashirika ya tathmini ulinganifu. Yanaweza kutumika kuunga mkono biashara na ubadilishaji/ugawaji wa bidhaa au kwa malengo ya udhibiti. Baadhi ya mashirika ya ithibati yanazuia wigo wa shughuli zao kwa vitengo vya wataalamu, mfano majaribio na usanifu, maabara, au yanaweza kutoa kibali katika taswira pana ya tathmini ya ulinganifu. Kama ilivyoonekana katika swali la 88, mashirika yanayofanya aina yoyote ya uhakiki yako chini ya Ithibati pamoja na vyombo vya ukaguzi na maabara zinazofanya majaribio, usanifu na vipimo. Uhakiki wa bidhaa una historia ndefu na hakuna mashaka kuhusu nafasi yake katika tathmini ya ulinganifu. Utangulizi wa hivi karibuni wa aina mbalimbali za mifumo ya usimamizi, uthibitisho na upungufu wa maneno/misamihati thabiti (kwa mfano matumizi ya neno registration -usajili kwa ajili ya certification -uhakiki) imepelekea ukosefu wa maelewano, na zaidi upotofu wa habari, kulingana na uhusiano kati ya ithibati na uhakiki katika shughuli hizi. Tatizo liliibuka na kusambazwa sana kwa kupitishwa kwa mfululizo wa ISO 9000 na nadharia mbovu kwamba kwa njia moja au nyingine viwango viliainisha ufanisi wa kiufundi zaidi ya usimamizi wa mfumo bora, katika mazingira yoyote. Mwishoni mwa 1980s na mwanzoni mwa 1990s, kulikua na mtazamo kuwa ISO 9001 ingechukua nafasi ya mifumo ya awali kuhakikisha ufanisi na uadilifu ndani ya eneo la majaribio na vipimo, ambavyo viliegemea kwenye upitishwaji wa ISO/IEC Suala lilichochewa pale ISO/IEC ilipoingiza mahitaji ya mifumo ya ISO 9001, na kuweka mwingiliano mkubwa kati ya shughuli hizo mbili. Katika soko lolote lile, patakuwa na karibu mashirika ya uthibitisho machache ya kupewa kibali na wakati namba kubwa ya maabara zinazotakiwa kupewa kibali zitakuwa nyingi zaidi. Hata hivyo, maelezo ya mashirika ya uthibitisho yatakua ya juu/makubwa zaidi sokoni, kwasababu ya ukuaji wa biashara. Tofauti ya maelezo haya wakati mwingine yanasababisha kuchanganyikiwa katika maneno kibali na uthibitisho pale yatakapotumika kwa kubadilishana, hasa kuhusu uthibitisho wa ISO Kibali kinafuata tathmini ya ufanisi maalumu wa kiufundi, wakati uthibitisho ni matokeo ya kudhihirishwa kwa tendo la kukubaliana na viwango katika kesi ya ISO 9001, viwango vya mfumo wa uongozi bora ambao ni wa jumla badala ya kipekee wa bidhaa au kiwanda. Pamekuwa na motisha ya biashara kutangaza maoni ya kwamba uthibitisho na kibali ni karibu sawa kiasi cha kuweza kubadilishana. Ni vizuri kufahamu kwwamba katika baadhi ya masoko, hasa nchi za Amerika, neno usajili linatumika badala ya uthibitisho kwa ajili ya maombi ya miradi/mipango ya mfumo wa usimamizi, na vyombo vya ukaguzi vinajulikana kama wasajili badala ya mashirika ya uthibitisho. Neno uthibitisho lina mipaka kwa mashirika yanayothibitisha bidhaa. In any particular market, there will be relatively few certification bodies to be accredited while the potential number of laboratories to be accredited will be much higher. However, the profile of the certification bodies will, because of commercial exposure, be much higher in the market. This profile difference sometimes causes confusion in that the terms accreditation and certification are used interchangeably, particularly with respect to ISO 9001 certification. It must be remembered that accreditation follows an assessment of specific technical competence, while certification is the result of a demonstration of compliance with a standard in the case of ISO 9001, a quality management system standard that is generic rather than product or industry specific.

249 Kibali (Ithibati) 239 Kuondoa baadhi ya utata, na kudhihirisha vizuri zaidi tofauti ya kazi, baadhi ya serikali ama zimeweka mamlaka kwamba patakuwa na shirika moja la kitaifa la kibali (m.f katika nchi za Umoja wa nchi za Ulaya) au kutoa haki ya kutawala kwa shirika moja ndani ya sekta zilizotajwa, kama Australia na Afrika kusini. Kwenye mamlaka mengine kama nchi za Amerika, kiasi cha ushindani ni ruhusa. Mashirika ya vibali yamezuiliwa kufanya huduma zenye ushindani ambapo wanatoa kibali kwa wengine kutoa huduma hizo.

250 240 Kibali (Ithibati) Ngazi za tathmini ya ukadiriajiss shirika la ithibati ISO/IEC Maabara za kupimia na Kurekebisha vipimo ISO/IEC Mashirika ya ukaguzi ISO/IEC Mashirika ya uhakiki ISO/IEC Mwongozo 65 ISO/IEC etc. Wateja Mahitaji mbalimbali ya bidhaa na kiufundi Wateja Mahitaji mbalimbali ya bidhaa na kisheria Wateja ISO 9001 ISO n.k. Source: John Gilmour, Australia. Kiutekelezaji, moja ya tofauti kubwa kati ya uhakiki na ithibati inategemea maombi ya viwango kama vifaa vya ukaguzi kwa matumizi ya ama, ithibati (ISO/IEC 17025) au mashirika ya uhakiki (ISO 9001). Hapa, malengo shirika huru siyo sawawa. Shirika la ithibati linatumia viwango ili kulitathmini shirika na lingine kama linao uwezo na umahiri wa kiufundi kufanya kazi ya tathmini ya ulinganifu wa bidhaa au mfumo na kutoa uhakiki yaani, bidhaa au mfumo zinakidhi viwango. Wakati shirika la uhakiki linafanya ukaguzi ili kubaini kama bidhaa au mfumo vinakidhi viwango, katika mazingira haya, shirika la maabara ya ithibati linavutiwa na matumizi ya njia za upimaji na ujuzi wa watu binafsi katika kufanya vipimo kadhaa/ maalum, kwa hivyo hushirikisha wataalamu wa kiufundi kutathmini mambo haya ya shughuli za maabara. Vipengele vya usimamizi wa ubora wa viwango hivi viwili vimelinganishwa na kwa hivyo mashirika yote mawili la maabara ya ithibati na uhakiki hutumia wakaguzi na wakadiriaji wenye umahiri unaofanana katika kutathmini utekelezaji wa mambo hayo (QMS). Pamekuwa na majadiliano makubwa kuhusu hitaji la kuipa maabara kibali pale inapokuwa sehemu ya shirika lililothibitishwa na ISO Kwa kiasi kikubwa, hii inategemea mteja anayetumia, lakini baadhi ya watumiaji wa data za vipimo watasisitiza zaidi maabara kuwa na kupewa kibali peke yake. Ukaguzi wa kampuni kinyume na ISO 9001 ikilinganishwa na tathmini ya maabara kinyume na ISO/IEC inaweza kulinganishwa na tofauti kati ya ramani ya barabara na muongozo wa mtaa (kibao). Tathmini ya maabara ni uchunguzi muhimu sana kwenye shughuli za maabara na inahusiana na masuala ya ufanisi wa kiufundi.mfumo bora wa ukaguzi wa shirika kubwa utaona maabara kama jambo dogo kati ya makubwa. Hata kama shirika ni maabara iliyosimama peke yake, ukaguzi kinyume na ISO 9001 halizingatii maarifa ya wanasayansi, mafundi na waendeshaji. Mfano uliotolewa katika swali namba 64 kwa namna na kiasi cha undani ambapo kibali kinafafanuliwa (vipimo, nafasi/kadiri na utovu wa hakika) inaonyesha asili ya kiufundi ya kibali ambapo cheti cha ISO 9001 kinaweza kuonyesha hii kwa urahisi kutumia kumbukumbu ya sekta ya viwanda ya kutengeneza zana za kiufundi. Mashirika yote ya ILAC na IAF yamefanya kazi kubwa ya kufafanua masuala haya, na matokeo ni kwamba sasa kuna mjadala mdogo sana juu ya suala hilo katika ngazi ya kiufundi na katika jamii ya watumiaji wa tathmini makubaliano. Hata hivyo, dhana potofu bado zinaendelea kuwepo katika sehemu kubwa ya jamii.

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi 3.1 Utangulizi Miradi na jamii Lengo la sura hii ni mapitio ya mazingira pana ambayo chini ya ardhi kwa ajili ya maendeleo vijijini upatikanaji wa maji inafaa. majadiliano wakapanga meneja, au kiongozi

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji Sera ya Faragha Katika Sera hii ya Faragha ( Sera ), sisi, Qualcomm Incorporated na makampuni yetu tanzu (kwa pamoja sisi au yetu ), tunatoa maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na

More information

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko UPOTEVU WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA MAVUNO: CHANGAMOTO NA UBORESHAJI Usuli Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo,

More information

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Athari Zake Kwa Mifumo Ya Mbegu Inayosimamiwa Na Wakulima Na Kwa Wakulima Wadogo April 2016 CONTENTS UTANGULIZI 3 MAELEZO YA

More information

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI Paris, 20 Oktoba 2005 Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa linalohusisha

More information

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig KITINI CHA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA SIMU YA KIGANJANI KATI YA BARAZA LA FAMASI NA WAMILIKI WA MADUKA NA WATAALAMU WA DAWA YALIYOMO UTANGULIZI... 3 SEHEMU YA KWANZA: MALIPO YA KUHUISHA VIBALI... 4 1.1

More information

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized horized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized JAMHURI YA KENYA Mkakati wa Ushirikiano FY2014-2018 MUKHTASARI Mkakati wa Ushirikiano wa Jamhuri ya Kenya

More information

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Résumé non technique Version Swahili MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA

More information

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari

More information

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo TOLEO Na. 1, Desemba, 2012 Yaliyomo Orodha ya Vifupisho -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------3

More information

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR MUHTASARI WA RIPOTI YA YA MWISHO. JULY 2012 for Page i Muhtasari Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi

More information

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu

More information

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA NGUZO KUMI ZA KWANZA (MFUMO WA UTEKELEZAJI) NGUZO YA 1 DIRA YA TAIFA YA KWANZA 1.1 Kupitisha Dira ya KWANZA SHUGHULI MAJUKUMU MUDA MHUSIKA MKUU 1. AZIMIO LA KWANZA 2. mpango wa utekelezaji wa KWANZA 3.

More information

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania Modeli wa Ukodishaji Mradi Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini

More information

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI

More information

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa Songa kwenye kilele cha upeo Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa United Republic of Tanzania Photos provided

More information

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MFUMO WA RUZUKU YA MAENDELEO YA MTAJI WA SERIKALI ZA MITAA (LDCDG) UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI Kijitabu cha Mshiriki

More information

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo wa Lugha Rahisi wa Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo huu Umeandaliwa na Hakikazi Catalyst kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Uchumi. Desemba 2007 Dibaji Ripoti ya Mwaka ya

More information

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia HakiElimu & Policy Forum KUUELEWA MCHAKATO.indd a 1/20/10 11:00:56 AM KUUELEWA MCHAKATO.indd b 1/20/10 11:00:57 AM Kuuelewa Mchakato wa

More information

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY HABARI ISSN 1821-5335 Makala Maalum Miaka 15 ya Foundation for Civil Society MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY Uwezeshaji wa moja ya sekta madhubuti za asasi za kiraia barani Afrika

More information

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV) S.L.P 12183 Dar Es Salaam

More information

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. KUHUSU AFRODAD Dira ya AFRODAD AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. Dhamira ya AFRODAD Kupata sera zitakazorekebisha migogoro ya madeni ya Afrika kulingana

More information

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI Mwongozo huu utatumika kama njia ya kuwafunza watafiti watakaohusika na utafiti unaohusu binadamu. Muongozo huu utatumika

More information

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda WARAKA WA TAARIFA YA MRADI (PID) HATUA YA TATHMINI TAARIFA NA..: AB4376 Jina la Mradi Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda AFRIKA Sekta Madini na Uchimbaji mwingine (100%) Namba ya

More information

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump

More information

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery

More information

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa

More information

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)] This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b)

More information

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment Background 1. On 17 th May 2011 KUWASA submitted an application for

More information

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania Msingi wa Programu zote za Uimarishaji Ubora Toleo la 1 kwa Lugha ya Kiswahili

More information

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP 2011-2016) nchini Tanzania ulikuwa na mafanikio makubwa lakini

More information

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Empowered lives. Resilient nations. UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Kenya Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni

More information

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NOVEMBA, 2016 ISBN 978-9987 - 829-02 - 9 ii YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI... 1 2.0 MABORESHO YA MFUMO WA KIBAJETI... 2

More information

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI b Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI 1 Mwongozo wa Uzalishaji

More information

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania Benki Kuu ya Tanzania Septemba 2016 YALIYOMO 1.0 HALI YA UCHUMI WA TANZANIA... 3 1.1 UKUAJI WA UCHUMI... 3 1.2 MATAZAMIO YA UKUAJI WA UCHUMI MWAKA 2016... 4 1.3

More information

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment Background 1. On 4 th September, 2012, the Energy and Water Utilities

More information

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Wasiojua kusoma na kuandika katika karne ya 21 hawatakuwa wale wasiojua kusoma na kuandika lakini wale ambao hawawezi kujifunza, kutojifunza na kujifunza

More information

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Makala ya Mshiriki wa Mafunzo Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka

More information

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2010 Toleo la kwanza 2010 Machapisho ya Ofisi

More information

Kutetea Haki za Binadamu

Kutetea Haki za Binadamu Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and

More information

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako

More information

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo

More information

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya

More information

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 12(3): 296 309 (2003) KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania ABSTRACT Lugha za jamii hapa nchini

More information

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT. WILLIAM AUGUSTAO MGIMWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2013/2014 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 Leo napenda nizungumze nanyi, kwa lugha nyepesi iwezekanavyo, juu ya mahusiano tunayowania

More information

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA TWN Third World Network 1. WEMA ni nini? Mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi yajulikanayo kwa kingereza kama Water Efficient Maize for Africa (WEMA) ni mpango

More information

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza 1 Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA Kwa Wanaoanza For IT Services & Web Solutions Web: Email: info@dudumizi.com Phone: 0768816728 2 Matumizi bora ya Facebook kwa

More information

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? Februari, 2013 Februari, 2013 SHUKURANI

More information

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013 W N S E Muhtasari Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013 Kuinuka kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Ulimwengu Anuwai Empowered lives. Hati ya kunakili 2013 na Mradi wa Maendeleo ya Umoja wa

More information

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI International Records Management Trust RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI ukumbi wa British Council Tanzania Auditorium Machi 27-28, 2000 Dar es Salaam, Tanzania warsha imeandaliwa

More information

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU UKAGUZI WA MASHIRIKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu

More information

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE FACILITY

More information

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

More information

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017 TAARIFA Agosti 2017 NGUO MPYA ZA UKOLONI Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika Jumuiya ya Jamii ya 2007: Wajumbe wanaadhamana Nairobi dhidi ya EPAs. SwissInfo Tangu mwaka

More information

Ufundishaji wa lugha nyingine

Ufundishaji wa lugha nyingine CHUO CHA ELIMU CHA KIMATAIFA OFISI YA ELIMU YA KIMATAIFA Ufundishaji wa lugha nyingine Na Elizabeth B. Bernhardt ELIMU MAZOEA KITABU NA. 20 1 Chuo cha Elimu cha Kimataifa (The International Academy of

More information

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI David M. Mwayafu, Richard Kimbowa, Kristy Graham Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI Na: David M. Mwayafu, Richard Kimbowa (Uganda Coalition

More information

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano. HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB) WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI NA NAMNA BORA YA KUPIMA HALI YA UMASKINI AFRIKA,

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA MUSTAFA HAIDI MKULO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA

More information

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu: Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200

More information

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira Kiongozi hiki kimeandaliwa kikiwa ni sehemu ya mradi wa

More information

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi International Labour Office Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi 1 Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2007 Kimechapwa mara ya kwanza 2007 Machapisho ya Ofisi ya Shirika la

More information

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Kubadilishana Tamaduni za Kijerumani na za Kitanzania Limeandaliwa na Anna Hoppenau, Johannes Hahn, Oliva Lyimo na Lisa Bendiek German-Tanzanian Partnership (DTP)

More information

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA Toleo la kwanza 2012 Mwandishi: USAID DELIVER PROJECT Wachangiaji: Gary Steele, John Snow, Inc. and Judith

More information

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA Marekebisho ya 23 January 2013 YALIYOMO KURASA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF)... 0 KUHUSU HAKI ZA WATOTO... 0

More information

Mipango ya miradi katika udugu

Mipango ya miradi katika udugu Partnerschaftlich Projekte planen Mipango ya miradi katika udugu 2 Dibaji... 3 Utangulizi... 4 I. Nafasi ya (Wajibu wa) Fedha katika Udugu: Mtazamo wa Ki-indonesi... 5 II. Namna UEM Inavyowezesha Miradi

More information

Deputy Minister for Finance

Deputy Minister for Finance ISSN: 1821-6021 Vol XI - No - 34 DID YOU KNOW? A procuring entity is?s required to use suppliers pliers?pliers?pliers?pliers among those awarded ed?ed?ed?ed framework agreements by GPSA for procurement?ents

More information

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO Mradi wa Kuondoa Madini ya Risasi Katika Rangi Barani Afrika 2015 ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO 2015 SHUKRANI Tunachukua

More information

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa

More information

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA KUHUSU JINSI YA KUINGIZA MASUALA YA USAWA WA JINSIA KATIKA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA NINI MISINGI YA USAWA

More information

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 Kitabu hiki kimetayarishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) Equality

More information

Mwongozo wa Mwezeshaji

Mwongozo wa Mwezeshaji JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Mwongozo wa Mwezeshaji Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka lugha

More information

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/19 1 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted

More information

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria; HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri

More information

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu Nyenzo ya Mafunzo Vi Agroforestry Vi Agroforestry ni shirika la ushirikiano la maendeleo la Sweden, linalopambana dhidi ya umasikini na

More information

ORDER NO BACKGROUND

ORDER NO BACKGROUND In the matter of an Application by the DAR ES SALAAM URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (DAWASA) For a Tariff Adjustment, Submitted on January 8 th, 2008 (TR-W-08-001) ORDER NO. 08-001 1.0 BACKGROUND

More information

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna

More information

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST

More information

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Shukrani Ripoti

More information

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( ) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI (2008 2012) Dar es Salaam Oktoba 2007 YALIYOMO ORODHA YA VIFUPISHO DIBAJI SHUKRANI MUHTASARI RASMI SURA

More information

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Shukrani Ripoti

More information

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu BLOOD PRESSURE UK Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha ulemavu na vifo vya mapema kule Uingereza, kupitia kiharusi, mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.

More information

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina Bustani 10,000 Katika Afrika Alberto Prina K i j i t a b u Timu ya wahariri: Abderrahmane Amajou, Typhaine Briand, Roba Bulga Jilo, Davide Dotta, Emanuele Dughera, Michela Lenta, Velia Lucidi, Irene Marocco,

More information

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( ) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI (2008 2012) TOLEO LA PILI Dar es Salaam, Oktoba, 2007 i ii JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI

More information

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized!. viromen-alsc:a.. Environmental & Social MRADI WA UMEME WA GESI YA * Assessment & Management

More information

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika, HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI, (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2007/08 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA

More information