ARCHDIOCESE OF MWANZA

Size: px
Start display at page:

Download "ARCHDIOCESE OF MWANZA"

Transcription

1 ARCHDIOCESE OF MWANZA Bukumbi Girls Secondary School P.O.Box 561 MWANZA. Tel: No / / / Website: YAH: MWONGOZO WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017 Amani na Baraka ya Mungu viwe nawe. Mpendwa.Ninafurahi kukutaarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na Kidato cha.. katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi. HONGERA SANA! Unatakiwa kufika shuleni tarehe.. ili uanze masomo. Mwanafunzi atakayechelewa kufika shuleni zaidi ya wiki moja hatapokelewa. TAARIFA YA SHULE Sekondari ya Wasichana ni Shule ya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza. Inaendeshwa na Masista Wabenediktine wa Mtakatifu Agnes. Shule hii iko katika Wilaya ya Misungwi umbali wa kilometa 34 kusini mwa Jiji la Mwanza karibu na Kanisa Katoliki la Bukumbi. Ni shule ya bweni kwa wasichana tu. Katika shule hii tunachukua wanafunzi ambao wamefaulu mtihani wetu NA WENYEE SIFA ZA KUJIUNGA NA Kidato cha Tano. MALEZI YETU ni katika MISINGI YA KIKRISTO (KIKATOLIKI) kama vile kusali pamoja kabla ya vipindi, Misa kwa wote siku zilizopangwa (yaani JUMATATU, JUMATANO, IJUMAA NA JUMAPILI) Mafungo na kadhalika. Mzazi/Mlezi ahakikishe kwamba kiambatanisho No. (i) na (ii) vinajazwa kikamilifu. DIRA YA SHULE Kwa Neema ya Mungu Baba, Munguu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, wanafunzi wetu wakue kama watumishi wa kuwahudumia watu. 1. MWONGOZO WA KUJIUNGA NA SHULE Soma kwa makini sana mwongozo wa kujiungana shule hii na kama unakubali, tafadhali jaza fomu iliyoambatanishwaa na uje nayo. 2. USAFIRI KUFIKA SHULENI Kwa kutokea Kigongo Ferry unaweza kutembea kwa miguu mpaka shuleni. Kwa kutokea mjini Mwanza kuna magari ya daladala.haya magari husimama katika kituo cha mabasi cha BUHONGWA. 3. TAARIFA YA AFYA YAKO Unatakiwa kupeleka Medical History Sheet kwa Mganga wa Hospitali (isiwe zahanati) yoyote inayotambuliwa na serikali. Fika shuleni na Medical History Sheet hiyo ikiwa 1 Tarehe

2 imejazwa na kusainiwa na mganga aliyekupima. Uthibitisho wa mganga wa kienyeji au mganga yeyote asiyetambuliwa na serikali hautakubaliwa na itabidi upimwe katika Hospitali ya Bukumbi kwa gharama yako. Ni vema magonjwa ya kudumu, ulemavu ubainishwe na uongozi ukaelewa. Shule haitapokea malalamiko yoyote ya kiafya ambayo hayana uthibitisho wa Mganga anayetambuliwa na serikali (Tumia medical History Sheet iliyoambatanishwa nyuma). 4. SARE YA SHULE Shule hii ina sare za aina mbili ambazo hutumika kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo i. Sare za darasani wakati wa masomo: Sketi mbili zitakazoshonwa hapa shuleni ili kuondoa utata wa rangi na mtindo wa mishono. Hivyo njoo na shilingi elfu kumi na nne (Tshs. 14,000/=) kwa ajili ya sketi mbili. Njoo na mashati (Blauzi) mawili meupe ya mikono mirefu ambayo hayabani na wala si mapana sana. Ni marufuku kujishonea sare za shule nje ya utaratibu huu. ii. Sare za nje ya darasa wakati usio wa masomo Njoo na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa ajili ya gauni mbili kwa sare ya nje ya darasa. Nazo sawa kama sketi mbili katika No. 4 (i) zitashonwa hapa hapa shuleni. Pia njoo na shilingi elfu saba kwa ajili ya T-shirt ya shule (7,000). iii. Mavazi ya michezo a. Bukta zenye mipira miguuni na gauni fupi (rangi nyekundu) b. Raba za michezo jozi moja. iv. Viatu Njoo na viatu vyeusi vyenye visigino vifupi jozi mbili na soksi nyeupe ndefu jozi mbili. Ndala (kandambili) rangi yeyote jozi moja. v. Aje na shilingi elfu kumi na tano (15,000) za sweta. Ni marufuku kuvaa sweta au jaket tofauti na hilo litakalonunuliwa hapa. vi. Aje na underskirt 2 na shimizi 3 vii. Aje na nguo za ndani za kutosha 5. VIFAA VINGINE Unatakiwa uje na : i. Bakuli, sahani, kikombe na kijiko sio vya udongo ii. Ndoo 1 ya lita kumi itanunuliwa shuleni ( sh.3,500 ) na beseni 1 (sh.2,000) litanunuliwa hapa shuleni. iii. Galoni nyeupe ya plastiki ya lita tano iliyo na mfuniko iv. Mifagio ya chelea 2 kwa usafi wa nje. v. Faili 1 vi. Bunda mbili (2) za ream za karatasi za Photocopy A-4 moja kwa kila muhula vii. Tochi ya betri 2 au taa ya solar, na saa ya mkononi (aina yoyote) kwa ajili ya kutunza muda. 6. MATANDIKO i. Godoro la mpira ft 2½ ii. Mashuka 2 ya rangi ya blue bahari iii. Chandarua VIFAA VYA DARASANI 2

3 Uje na: i. Daftari kubwa Counter Books za kutosha kadiri ya Tahasusi aliyoichagua ii. Kalamu za risasi mbili au zaidi iii. Kamusi ya Kiingereza(Dictionary). iv. Rula ya sentimeta 30 au 50 v. Kalamu za wino bluu bic zisizopungua tano vi. Mkebe wa vifaa vya hesabu (mathematical set) vii. Aje na vitabu aina vinavyoendana na Tahasusi yake. viii. Aje na Scientific Calculator ( kwa wenye Tahasusi za Sayansi tu yaani CBG NA PCB) 8. KARO YA SHULE i. KARO YA SHULE NI SHILINGI 1,500,000(Milioni moja na laki tano ) tu kwa mwaka. MALIPO YOTE YAFANYIKE KWENYE AKAUNTI ZA SHULE NA SI PENGINEPO, NA UFIKE NA STAKABADHI (BANK PAY-IN-SLIP) ORIGINAL. UNAWEZA KULIPA ADA HIYO KWA AWAMU MBILI,TATU, AU ZOTE ( yaani Tsh.750,000, 500,000 na 1,500,000). ii. AKAUNTI ZA SHULE ZIPO KATIKA BENKI ZIFUATAZO: A. BENKI YA BIASHARA (NBC). TAWI LA NYERERE-MWANZA au sehemu yoyote yenye Tawi la NBC JINA LA AKAUNTI: BUKUMBI SEKONDARI AKAUNTI NAMBA; B. BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI (MKOMBOZI COMMERCIAL BANK) TAWI LA MWANZA JINA LA AKAUNTI: BUKUMBI GIRLS SECONDARY SCHOOL NAMBA YA AKAUNTI: Mkombozi Commercial Bank ipo katika jengo lililokuwa zamani Catholic Bookshop, Barabara ya Nyerere Mkabala na Benki ya CRDB iliyoko karibu na Benki Kuu ya Tanzania. Wazazi, walezi wanaoishi Mwanza na yeyote anayeweza kuifikia Benki hiyo kwa urahisi, kuanzia sasa alipie ada (karo) ya shule kwa kutumia AKAUNTI NAMBA iliyopo hapo juu (AKAUNTI NAMBA YA MKOMBOZI COMMERCIAL BANK) iii. Uje na shilingi elfu nne (Tshs. 4,000) kwa ajili ya kitambulisho na picha iv. Uje na tahadhari (caution money) shilingi elfu tano (Tsh. 5,000) v. Uje na sh. 3,000 kwa ajili ya Tai (Tie). vi. Unashauriwa uje na fedha kwa ajili ya matumizi yako binafsi, Ukipenda unaweza kutunzia fedha hiyo kwa Matron au kwa Mhasibu wa shule. vii. Uje na sh.15,000 za Taaluma viii. Uje na sh. 35,000/= za maabara (vifaa na kemikali ) kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ix. Uje na sh. 10,000/= za matibabu. 9. MAWASILIANO Mzazi/mlezi atapata taarifa kuhusu mtoto wake kupitia UONGOZI WA SHULE NA SI VINGINEVYO. Ni marufuku mwanafunzi kuwa na simu ya mkononi hapa shuleni. 3

4 HUDUMA YA KIROHO WAKIWA HAPA SHULENI TANBIHI: Wanafunzi wote wakiwa hapa shuleni watasali katika Kanisa Katoliki ambalo lipo karibu na shule. 1. Kila kifaa kilichoagizwa ni muhimu. Hakikisha unakileta. 2. Mwanafunzi aletwe shuleni siku za kazi au Jumamosi na siyo Jumapili 3. Kutembelewa wanafunzi (visiting day) hakupo kabisa. 4. Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kuleta au kuletewa aina yoyote ya chakula 5. Mwanafunzi anayejiunga na shule hii anatakiwa:- A. KITAALUMA Kuonyesha juhudi (bidii) katika masomo.elimu anayoipata imsaidie kujikwamua na adui ujinga, maradhi na umasikini. Mwanafunzi itabidi afaulu mitihani yake yote ya mihula miwili yaani mwezi wa Juni na Desemba kwa kiwango cha 50% ili kumruhusu kuendelea na darasa lingine. B: KIMAADILI Kukua katika maadili mema akifuata maelekezo ya walimu na walezi wake, na hatimaye kuwa raia mwema atakayefaa kuishi katika jumuiya yoyote na kujenga moyo wa kuwa tayari kutumikia na siyo kutumikiwa. 6. Mwanafunzi atakayekiuka sheria za shule ataondolewa shuleni mara moja. Tunaomba mzazi/ mlezi uwe na ushirikiano na uongozi wa shule hususani maendeleo ya mwanao kitaaluma na kinidhamu 7. Mwanafunzi yeyote atakayesimamishwa masomo kwa utovu wa NIDHAMU HATARUDISHIWA FEDHA YOYOTE ILE. 8. Mwanafunzi vile vile ataongozwa na sheria/kanuni za shule zilizotungwa kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama zilivyoambatanishwa kwenye fomu hii. Nakutakia maandalizi mema na unakaribishwa sana kusoma katika Sekondari ya Wasichana Bukumbi.. Sr. Yovina F. Haule OSB Mkuu wa shule 4

5 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI NAMBA ZA SIMU: Mkuu Wa Shule: 0784524029 / 0766805826. Makamu Mkuu Wa Shule: 0714356735 / 0767356735. SHULE YA SEKONDARI

More information

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA E- mail: uchilesekondari@yahoo.com P.O. BOX 582 Mob: +255 (0) 752 476 389 SUMBAWANGA KUMB. NA. USS/JOINING/F.V/03 10 Juni 2017...... YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA SIMU NA: (027) 2642082 TANGA (OFISI) 0784 889 099 TANGA (NYUMBANI) Tovuti: www.tangaschool.sc.tz Barua pepe: tangaschool@yahoo.com JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA

More information

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018 Hills View Catholic Diocese of Tanga Magunga District Hospital Road Mob:+255-784808420, +255 718 661681, +255 714901004 www.rmet.ac.tz, email: saroce2013@gmail.com KOROGWE, TANZANIA Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018

More information

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha Kumb.Na.KSS/. Tarehe:.. Ndugu:.. SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA. 023-2402143 e-mail Kibaha Secondary@kec.or.tz www.kec.or.tz TAARIFA YA KUCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO 2018 Ninayo

More information

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS-TAMISEMI Namba za Simu Mkuu wa Shule: 0742 770 656 Makamu Mkuu wa Shule: 0767 312 266 Matron: 0766 464 076 Shule ya Sekondari Nsimbo, S.L.P.304, MPANDA. Kumb.

More information

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shule ya Sekondari Bagamoyo Simu ya mkononi: +255 769 397 926 : +255 658

More information

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO SEHEMU A (TAARIFA ZA MWANAFUNZI) Picha ya mwanafunzi na aje na picha tatu Jina kamili (majina matatu). Tarehe ya kuzaliwa.. Uraia.. Jinsia Anuani ya mwanafunzi... Shule

More information

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI Namba za simu Shule ya sekondari Mkingaleo Mkuu wa shule -0716544244 S.L.P 1802 Makamu Mkuu wa shule -0713788225 Tarehe Matroni/Patroni-0764435107/0718495791

More information

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA TANDAHIMBA SHULE YA SEKONDARI TANDAHIMBA, S.L.P 74, 0716 / 0784 143550 12/05/2018 Kumb. Na. TSS/HS/2018/VOL. I Mwanafunzi.. S.L.P....

More information

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA SANDUKU LA POSTA 569 IRINGA TANZANIA Kumb... MZAZI/MLEZI WA...... YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA

More information

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA OFISI YA RAIS.TAMISEMI Namba za simu Mkuu wa shule 0784684613 S.L.P 23, Makamu Mkuu wa shule 0717134781 Shule Ya Sekondari Nyanduga, Tarime-Rorya, Patron: 0753379801 Email:

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU NAMBA ZA SIMU. MKUU WA SHULE: 0754 912 801 MAKAMU MKUU WA SHULE: 0765620813/0714556568 MATRON

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI. Namba za simu: SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA, S. L. P 8824, MOSHI. TAREHE... MKUU WA SHULE : 0688 460 242/ 0754 824 621 MAKAMU MKUU WA SHULE: 0787

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA Email: Galanossecondary@gmail.com SHULE YA SEKONDARI GALANOS, Website: www.galanos.sc.tz

More information

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , , KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE,0762-785899, 0765 752082, 0758 767533, EMAIL: kawawa.highschool@yahoo.com Kumb Na. 841KJ/KAWSS/2540 6 Namba ya Fomu. Tarehe.. FOMU YA USAJILI

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA. SHULE YA SEKONDARI KAHORORO, S. L. P 198, BUKOBA. Tarehe 14/5/2018 MKOA WA KAGERA

More information

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA FOMU YA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE 2018/2019 S.L.P 504, Namba za simu MPANDA Mkuu

More information

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018 JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI SHULE YA SEKONDARI WERUWERU Nambari ya simu 073-2744003/0759 659681 Email:weruweru23@gmail.com

More information

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI KAREMA Namba za simu: Mkuu wa shule: 0763414888/0784244108

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA Namba za simu: Mkuu wa shule: 0757 576 565 Makamu Mkuu wa shule: 0757 912 846 Matron: 0757 322 100 Walimu wa

More information

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI NAFASI ZA MASOMO Shule yetu, iliyoanza mwaka 1974, inazingatia taaluma na maadili kwa kufuata sera ya elimu ya Kanisa Katoliki. Ni ya mchepuo wa biashara. Inapokea wanafunzi wa kike na wa kiume, wa kutwa

More information

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI Namba za simu Shule ya Sekondary Mawelewele Mkuu wa shule: 0763401829 S.L.P 459, Makamu mkuu wa shule: 07523331155 IRINGA. Matron/Patron: Kumb.

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA

More information

Human Rights Are Universal And Yet...

Human Rights Are Universal And Yet... Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,

More information

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Desemba 2014 1 Shukurani Ripoti hii iliandikwa na Dk. Mkumbo. Ushauri wa kitaalamu ulitolewa na Elizabeth Missokia na Godfrey

More information

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery

More information

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017

More information

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya

More information

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Kwa toleo neno la waraka huu, tafadhali email:crd@hrw.org FEBRUARI 2017 ISBN: 978-1-6231-34464 Nilikua na Ndoto ya Kumaliza

More information

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh

More information

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig KITINI CHA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA SIMU YA KIGANJANI KATI YA BARAZA LA FAMASI NA WAMILIKI WA MADUKA NA WATAALAMU WA DAWA YALIYOMO UTANGULIZI... 3 SEHEMU YA KWANZA: MALIPO YA KUHUISHA VIBALI... 4 1.1

More information

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari

More information

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mpya ya Mtoto ambayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa

More information

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa mabingwa itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Mkuu Inahitaji dhabihu. Unahitaji kujisukuma hadi mwisho wako. Lakini nakupa ahadi hii,

More information

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo: HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE DODOMA TAREHE 29 AGOSTI 2008 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, leo ni takriban

More information

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Shule za umma za kata ya Fayette 1 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. Tunaamini familia ni wenzetu.

More information

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji Sera ya Faragha Katika Sera hii ya Faragha ( Sera ), sisi, Qualcomm Incorporated na makampuni yetu tanzu (kwa pamoja sisi au yetu ), tunatoa maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na

More information

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni MWONGOZO WA JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KUWEKWA KWENYE KANZIDATA YA WATANZANIA WENYE UWEZO WA KUUZA BIDHAA AU KUTOA HUDUMA (LSSP) KWENYE SHUGHULI ZA MAFUTA NA GESI ASILIA NCHINI Utangulizi 1. Mamlaka

More information

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246, P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@ twiga.com 01 June 2001 Benefits of Loan Repayment As the date of repayment nears, 15 June, groups are busy preparing crops, digging

More information

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NNE Kikao cha Thealathini na Sita Tarehe 29 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika

More information

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia : Maelekezo ya kutumia Kupatwa kamili kwa jua Jumatatu, 21 Agosti 2017 Agreement v1.4 Mar 2014 2014-2017 Eclipse2017.org, Eclipse2017.org, inc. inc. TERMS AND CONDITIONS FOR USE OF SOLAR VIEWER Please

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

Lesson 11 Weather and Seasons Hewa Majira

Lesson 11 Weather and Seasons Hewa Majira Lesson 11 Weather and Seasons Hewa Majira This lesson will introduce you to: - Vocabulary related to weather, seasons, and climate - How to ask for and give temperatures - How to understand the weather

More information

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen 1 Index latest update 26. feb. 2008 WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen Wafunaji wa nafsi ABC Mark 16:15-20 Huduma/uiinjilisti Wakristo wachache sana wameitikia mwito wa

More information

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NOVEMBA, 2016 ISBN 978-9987 - 829-02 - 9 ii YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI... 1 2.0 MABORESHO YA MFUMO WA KIBAJETI... 2

More information

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel

More information

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246 P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@twiga.com 01 October 2000 Y2K PREPARATIONS Holes and Seedlings made ready for the year 2000 programme By Gayo Mhila The process of

More information

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

SautiElimu. Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian

More information

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue? Tufundishane! Let s teach each other! This newsletter is published by The Foundation for Tomorrow and is meant to be a venue for teachers and schools to share and learn from each other s best practices.

More information

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo

More information

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Early Grade Reading Assessment for Kenya EDDATA II Early Grade Reading Assessment for Kenya Baseline Instruments: Kiswahili and English EdData II Technical and Managerial Assistance, Task Number 4 Contract Number EHC-E-01-04-00004-00 Strategic

More information

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

More information

Upande 1.0 Bajeti yako

Upande 1.0 Bajeti yako Upande 1.0 Bajeti yako Bajeti (Budget) ni muhustari wa njisi wewe (na familia yako) mnavyopata na kutumia pesa. Inaunganisha pesa zinazoingia nyumbani kwako (Kipato/ income) na zile unazotumia (matumizi/expenses).

More information

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria; HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri

More information

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03 Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03 AEG swahili Bahari ya Aegean Brosha ya maelezo hii ni kwa watu wanaofikiria kuvuka bahari ya Aegean kati ya Ugiriki na Uturuki.Kuvuka kihramu ni uhalifu katika

More information

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma

More information

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo, HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, KWENYE SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, TAREHE 08 JUNI 2008, MSIMBAZI CENTRE, DAR ES SALAAM Mhashamu

More information

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna

More information

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Taarifa ya Warsha Kuhusu Elimu-Jumuishi Iliyofanyika Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Kujifunza hakuna mwisho. Kazi ya vikundi imenipa fursa ya kujieleza bila kuhofia kuwa ningekosea.

More information

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment Background 1. On 17 th May 2011 KUWASA submitted an application for

More information

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano. HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB) WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI NA NAMNA BORA YA KUPIMA HALI YA UMASKINI AFRIKA,

More information

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa

More information

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 Kitabu hiki kimetayarishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) Equality

More information

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tatu - Tarehe 14 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu

More information

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/19 1 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, 2016 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alikalia Kiti HATI ZA KUWASILISHA

More information

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI Swahili TANGAZO LA MATARAJIO NA JUKUMU KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI Lengo letu ni kuwezesha mazingira ya jumuiya ya ushirikiano yanayowapatia wanafunzi wote kwa kila kiwango fursa ya kufikia

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA Toleo la kwanza 2012 Mwandishi: USAID DELIVER PROJECT Wachangiaji: Gary Steele, John Snow, Inc. and Judith

More information

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV) S.L.P 12183 Dar Es Salaam

More information

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia IDARA YA KUFIKIA HUDUMA ZA AFYA VERMONT Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia GreenMountainCare MIASHA YENYE AFYA BORA ZAIDI Jedwali la Yaliyomo Jedwali la Yaliyomo... 2 Karibu kwenye Programu ya

More information

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Résumé non technique Version Swahili MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA

More information

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania Benki Kuu ya Tanzania Septemba 2016 YALIYOMO 1.0 HALI YA UCHUMI WA TANZANIA... 3 1.1 UKUAJI WA UCHUMI... 3 1.2 MATAZAMIO YA UKUAJI WA UCHUMI MWAKA 2016... 4 1.3

More information

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa

More information

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu

More information

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza 1 Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA Kwa Wanaoanza For IT Services & Web Solutions Web: Email: info@dudumizi.com Phone: 0768816728 2 Matumizi bora ya Facebook kwa

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania Questionnaire for Individual Household Members/Dodoso kwa mwanakaya binafsi This questionnaire will be administered to

More information

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA:

More information

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI SIKOMBE YIZUKANJI YORADI TASNIFU YA KISWAHILI KWA MINAJILI YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (MA. KISWAHILI) KITIVO CHA SANAA

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi

More information

ORDER NO BACKGROUND

ORDER NO BACKGROUND In the matter of an Application by the DAR ES SALAAM URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (DAWASA) For a Tariff Adjustment, Submitted on January 8 th, 2008 (TR-W-08-001) ORDER NO. 08-001 1.0 BACKGROUND

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 The Human Rights Centre Uganda JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 AZIMIO LA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA KIBINADAMU SURA YA NNE YA KATIBA YA JAMHURI YA UGANDA YA 1995: MASIMULIZI YALIYOFASIRIWA KWA URAHISI NA KUFUPISHWA

More information

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Athari Zake Kwa Mifumo Ya Mbegu Inayosimamiwa Na Wakulima Na Kwa Wakulima Wadogo April 2016 CONTENTS UTANGULIZI 3 MAELEZO YA

More information

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa

More information

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump

More information

PDF created with pdffactory trial version

PDF created with pdffactory trial version المملكة العربية السعودية وزارة التعليم العالي الجامعة الا سلامية بالمدينة المنورة عمادة البحث العلمي قسم الترجمة تعريف موجز بالا سلام بل( لغة السواحلية) ١ بسم االله الرحمن الرحیم MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU

More information

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to

More information

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO KISWAHILI SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO YALIYOMO UTANGULIZI v MPANGILIO WA MASOMO YA KISWAHILI: KIDATO CHA TANO 1 FUNZO: Fasihi (Ukurasa

More information

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10. 6-15 Mei 2005. MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10. Kujenga kifuniko cha maombi juu ya mabara yote ya ulimwengu. Kufurikisha Jamii zetu kwa Maombi. Anzisha vituo vitakavyofukuta

More information

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College Theolojia 1 Ujumla Mike Taylor Semester 1 2014-2015 Munguishi Bible College MIKE TAYLOR 2014 THEOLOJIA 1 i THEOLOJIA Utangulizi! 1 1. Kumfahamu Mungu katika Injili! 3 1.1. Mawazo Makuu 3 1.2. Maana ya

More information

3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015

3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA

More information

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Saba Tarehe 13 Aprili, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Saba Tarehe 13 Aprili, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA Kikao cha Saba Tarehe 13 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge naomba

More information