Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

Size: px
Start display at page:

Download "Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe"

Transcription

1 Wewe Maisha Yako Ndoto Zako Kitabu cha Vijana Balehe

2 Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako: Kitabu cha Vijana Balehe Catherine Watson na Ellen Brazier

3 Shukurani Kitabu cha Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako ni tafsiri ya You, Your Life, Your Dreams kilichoandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na shirika la Family Care International lenye Makao Makuu Mjini New York, nchini Marekani kwa kushirikiana na shirika la Straight Talk Foundation la Uganda. Toleo la awali kabisa liliandikwa na Catharine Watson Mkurugenzi Mhariri wa Straight Talk Foundation kwa kushirikiana na Ellen Brazier ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi wa Programu ya Afrika ya Mashariki katika Shirika la Ubora wa Afya kwa Familia Duniani. Ubora wa Afya kwa Familia Duniani, Tafsiri ya kitabu hiki iliwezeshwa kwa msaada wa shirika la Tanzania German Programme to Support Health (TGPSH) kupitia Reproductive Health Component (Repro/GTZ). Kupiga chapa kitabu hiki kuliwezeshwa kwa msaada wa Richard and Rhoda Goldman Fund. Japo uratibu wa kutafsiri kitabu hiki ulifanywa na Bi Rehema L. Mwateba, aliyekuwa mratibu wa Shirika la Ubora wa Afya Kwa Familia Duniani; watu wengi walishirikishwa. Shirika la Family Care International kwa kupitia ofisi yake ya Ubora wa Afya kwa Familia Duniani Tanzania linawashukuru wafuatao kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha tafsiri hii:- Kwanza kabisa Shirika la Ubora wa Afya kwa Familia Duniani linawashukuru wafuatao kwa kufanya tafsri na kupitia maandishi na michoro ya kitabu hiki:- Taasisi za kujitolea zinaruhusiwa kutumia kitabu hiki kwa kutoa nakala au nukuu lakini hawaruhusiwi kuuza nakala hizo. Ubora wa Afya kwa Familia Duniani wangependa kuona wanatajwa kwenye nukuu au nakala hizo kama wamiliki wa kitabu hiki. Kwa kupata nakala zaidi kitabu cha Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako: Kitabu cha Vijana Balehe, tafadhali wasiliana na wafuatao: Bi. Margreth Mtafya Kilembe kwa kufanya tafsiri kutoka lugha ya Kiingereza kuwa Kiswahili. Bi. Benadicta Maganga kwa kupitia muswada kwa mara ya kwanza. Bwana Michael Kadege kwa kupitia muswada kwa mara ya pili. Bwana Abdalla Athumani Mhagama kwa kuratibu shughuli za mapitio ya wasomaji mbalimbali na kutupatia maoni ya wasomaji. Family Care International-Kenya Anwani: S.L.P Nairobi, Kenya Simu:. (254-20) Simu ya upepo: (254-20) Barua pepe: Tovuti: Family Care International 588 Broadway,Suite 503 New York,NY Simu:. (1-212) Simu ya upepo: (1-212) Barua pepe: Bwana Sunnny Kiluvia na Bwana Elikunda Matteru kwa kupitia muswada baada ya wasomaji. Kwa kuwa si rahisi kumtaja kila mtu aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika uandishi wa kitabu hiki, shirika linapenda kuwashukuru walioshiriki kuratibu shughuli za wasomaji sehemu mbalimbali nchini Tanzania:- Bi. Lucy Ikamba aliyewaratibu wasomaji wa mradi huko Mbeya Vijijini. Bi. Catherine Ndawi aliyewaratibu wasomaji, Mbeya Manispaa. Bwana Ole Sepere aliyewaratibu wasomaji, wilaya ya Pangani. Bi. Emiliana Malambugi aliyeratibu upatikanaji wa maoni ya wasomaji kutoka kwa viongozi wa madhehebu ya dini. Bwana Benard Msami aliyewaratibu wasomaji, walimu wa shule za msingi - Turiani, Morogoro Vijijini. Bwana Dickson Reginald Ituwe kwa utaalamu wake wa kupanga maandishi katika kompyuta. Bwana Juma Lugendwa kwa kuchora upya picha zilizoombwa kurudiwa na wasomaji. Bwana Stanley Matteru na Richard Ndago kwa mchango wao katika utawala. Bi. Margret Mbede na Bi. Dawa Mhagama kwa mchango wao katika uchapaji. i ii

4 Utanguzi Shukurani za pekee kwa Bi Cordula Schuemer kwa utetezi kwa vijana na kuhakikisha kuwa vijana wanapata taarifa sahihi kuhusu masuala ya jinsia na afya ya uzazi. Kwa kuwa Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu You, Your Life, Your Dreams, shirika la Ubora wa Afya kwa Familia Duniani (FCI) lingependa kuwashukuru wale wote waliohusika katika uchapishaji wa kitabu hiki kwa lugha ya kingereza.hii inatia ndani udhamini wa shirika la Ford Foundation, European Commission, William and Flora Hewlette Foundation, John D.and Catherine T. MacArthur Foundation na Blanchette Hooker Rockefeller Charitable Fund. FCI ingependa pia kuwashukuru Adolescent Reproductive Health Education Project; CEDPA; FAWE, Hesperian Foundation na United Nations haswa UNICEF kwa matumizi ya picha zao. FCI inawapa shukrani Regina C. Faul-Doyle, Timothy Kiwala, Mashet Ndhlovu, ODIA na Philip Odida kwa michoro yao. Sehemu mbalimbali za kitabu You, Your Life, Your Dreams, zilipata mchango kutoka kwa Eva Agutti, Grace Canada, Claire Mcminn, Edith Mukisa, Dr. Sarah Naikoba na Joy Oguttu. Maandishi, mifano na michoro ilichambuliwa na Dr. A. Ananie Arkutu, FRCOG, Ghana; Regina Goergen, GTZ, Tanzania; Muriithi Kinyua, Family Planning Private Sector, Kenya; Dr. Margaret Makumi,Ministry of Health, Kenya; Dr. Elizabeth Odera, Malezi Preparatory School, Kenya; Rehema Mwateba, Independent Consultant, Tanzania na Mary Waithaka, Nairobi Primary School, Kenya. Msaada katika kufanya majaribio ulitolewa na wawakilishi kutoka Ministry of Health Ghana; Family Planning Association of Kenya;Planned Parenthood Association of Ghana; Young Christian Women s Association, Ghana. Shukrani pia kwa wawakilishi kutoka Kenya Association of Professional Counsellors; Kuleana Centre for Child Rights, Tanzania; Mathare Youth Sports Association, Kenya; Media Trust for Development, Zimbabwe; Naguru Teenage Health Centre, Uganda; The New Vision, Uganda na Trendsetters Newspaper, Zambia kwa kuwanukuu vijana balehe. Kubalehe ni kipindi katika maisha ya wanadamu ambapo kijana anabadilika na kuwa mtu mzima. Kipindi hiki kina msisimko mkubwa, lakini pia ni kipindi chenye kuchanganya sana. Wakati wa kubalehe utaona mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia, pia unaweza kuwa na maswali mengi kuhusu mwili wako na uhusiano wako na wengine. Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya vijana balehe, ambao wana umri kati ya miaka 14 na 19 ili kiwasaidie kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokea wakati wa mabadiliko kutoka utoto kwenda utu uzima.kitabu hiki kinatoa taarifa sahihi kuhusu mabadiliko yanayotokea katika kipindi cha balehe, pamoja na mambo mengine, kwa mfano: jinsi ya kuwa na afya njema ya kimwili na kihisia, kuepuka magonjwa yanayosababishwa na ngono zisizotakiwa, jinsi ya kupambana na misukumo ya kufanya ngono, na jinsi ya kujiepusha na matumizi mabaya ya vileo na dawa za kulevya. Pia, kitabu kinatoa ushauri kuhusu uhusiano mwema na wazazi, marafiki, wapenzi, jinsi ya kuweka malengo ya maisha, mbinu za kufaulu shuleni na maishani na jinsi ya kukabili vikwazo. Kitabu hiki kina taarifa nyingi lakini si lazima usome kurasa zote. Unaweza kuangalia katika sehemu inayoonyesha Yaliyomo na kuona mada zinazokupendeza zaidi. Ukizimaliza, unaweza kurudi tena kwenye Yaliyomo na kuchagua tena mada inayokuvutia. Pia, unaweza kufunuafunua tu kitabu na kuangalia sehemu zenye michoro, katuni na nukuu mbalimbali toka kwa vijana. Unaweza pia kuangalia sehemu maalumu zilizo na kichwa Je, Wafahamu. Hizi zinatoa taarifa sahihi kuhusu mambo mbalimbali. Ingawa kitabu hiki kilikusudiwa zaidi kwa vijana ambao hawajaoa/kuolewa wenye umri wa miaka 14 hadi 19, zipo pia sehemu za kitabu hiki zinazowafaa vijana wenye umri uliozidi na hata walio kwenye ndoa. Kisome kitabu hiki pamoja na marafiki zako, kaka na dada zako na wazazi wako. Ongea nao na jaribu kuona wao wanazichukuliaje mada zilizomo kwenye kitabu hiki. Furahia kitabu hiki na uwe salama! FCI inawapa shukrani wafanyakazi wake wote kwa mchango wao mbalimbali katika kufanikisha uchapishaji wa kitabu Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili. Molly Anyango Mshauri rika wa Vijana Family Planning Association of Kenya iii iv

5 Kwa Wazazi, Walimu, na Watu wazima wengine Yaliyomo Watu wazima wengi hudhani kuwa vijana hawana sababu ya kuwa na wasiwasi wala matatizo. Hata hivyo, balehe ni kipindi cha kuchanganya na kufadhaisha. Maswali na dukuduku nyingi hutokea wakati huu wa mabadiliko ya mwili na hisia. Pia, vijana hujiuliza maswali yanayohusu elimu, ajira na uhusiano kwa marafiki na wazazi. Kipindi cha kubalehe kinaambatana na misukumo toka kwa marafiki. Vijana huwa na wasiwasi kuhusu maisha yao ya baadaye. Lakini kubalehe ni hatua muhimu na inayosisimua. Ni kipindi ambacho kijana hukua kimwili, kihisia na kiakili. Pia, kijana huanza kupata majukumu na kuwa na ndoto kuhusu maisha ya baadaye. Vijana balehe hujifunza kufanya uamuzi binafsi ambao huweza kubadili maisha yao ya leo, kesho na miaka mingi ijayo. Wakati wa kubalehe, kijana anahitaji taarifa sahihi ili zimsaidie kufanya uamuzi wenye nguvu na usalama. Wazazi, walimu na watu wazima wengine hupata wasiwasi kuhusu uamuzi waufanyao vijana wao unaohusu uhusiano, ngono,dawa za kulevya na vileo au kupanga maisha ya baadaye. Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa vijana wanaweza kupanga mambo yao kwa busara kama wakiwa na taarifa sahihi pamoja na mbinu mbalimbali za maisha kama vile uwezo wa kufanya uamuzi, mawasiliano, maelewano, wakisaidiwa na miongozo toka kwa watu wazima. Kitabu cha Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako kinachambua masuala mbalimbali yanayowakuta vijana balehe katika Bara la Afrika. Yaliyomo humu yameandaliwa kwa kuwashirikisha vijana wenyewe toka nchi mbalimbali. Kitabu kimebobea katika masuala ambayo vijana wenyewe waliyaona yana umuhimu: Kuingia utu uzima, kutunza afya, kukabili mifadhaiko, kuelewana na wazazi, kujenga uhusiano wa kirafiki na kimapenzi, kukabili mifadhaiko na kuvunjika moyo, afya njema ya ujinsia, kupata mimba, kutoa mimba, kukabili matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vileo, masuala ya elimu na ajira. Zipo sababu mwafaka za kutaka kuhakikisha vijana wetu wanazo taarifa sahihi kuhusu masuala haya. Vijana wanakumbana na mambo mengi yanayoongeza changamoto na uwezekano wao wa kudhurika, ikiwa majumbani, mitaani, shuleni na hata kwenye vyombo vya habari. Leo hii, kijana ana uwezekano wa kupata matatizo mengi ya kiafya kama vile magonjwa ya zinaa, VVU/UKIMWI, mimba zisizotakiwa na utoaji mimba usio salama. Kiasi cha asilimia 60 ya maambukizi mapya ya VVU katika Bara la Afrika yanatokea kwa vijana wa miaka 10 hadi 24. Hii ina maana kuwa vijana wanaambukizwa VVU kwa kasi zaidi kuliko kundi lolote lingine. Kijana aliyeko kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa VVU ni yule asiye na taarifa sahihi. Kijana wa aina hii anategemea zaidi kupata taarifa toka kwa marafiki, video au filamu na muziki wa kizazi kipya, taarifa ambazo kwa kiwango kikubwa huwa si sahihi. Kwa hiyo, kitabu hiki kimekusudia kuhakikisha vijana balehe wanapata taarifa sahihi na wanajijengea uwezo wa kukabili misukumo ya kutenda yasiyofaa, kujenga uhusiano wenye faida na la muhimu zaidi; kuwawezesha vijana wafanye uamuzi salama na wa busara. Napenda kuwasisitiza wazazi, walimu na watu wazima wengine wasome kitabu hiki na wawashirikishe vijana wao na wengineo. Aidha, nawasisitiza watu wazima waongee na vijana kuhusu taarifa zilizomo na wawashauri vijana inavyopasa. Watu wazima wawasaidie vijana kuwa salama katika kipindi cha mabadiliko kuingia utu uzima ili waweze kutimiza ndoto zao maishani. Dr. A. Ananie Arkutu SHUKURANI... ii UTANGULIZI...iv Kwa Wazazi, Walimu, na Watu wazima wengine v SURA YA 1: UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA, CHANGAMOTO KUBWA... 1 Nini maana ya ujana balehe?... 2 Ukweli kuhusu maisha...4 Maadili Stadi za maisha...6 SURA YA 2: MABADILIKO YA MWILI...9 Mfoko wa ukuaji: mwanzo wa balehe...9 Vichocheo (Homoni)...12 Via vya uzazi - Sehemu za siri...13 Nywele za mwilini na mabadiliko ya ngozi...13 Uwezo wa kufikiri SURA YA 3: WAVULANA Umbo na ukubwa wa mwili...17 Sauti yako Via vyako vya uzazi (Sehemu zako za siri) Mazoezi ya usafi...21 Kudinda kwa uume...22 Kumwaga manii kukojoa...23 Ndoto nyevu ( Kutoa manii/ Shahawa ukiwa usingizini ) SURA YA 4: WASICHANA Maumbile na ukubwa wa mwili Matiti yako Sidiria...31 Via vya uzazi ( Sehemu zako za siri )...31 Kufanya usafi wa mwili vizuri...33 Hedhi na mzunguko wa hedhi...35 Kutunza kalenda Hedhi inavyokosesha raha Ngono na hedhi Kujisikia vizuri/ Afya na usafi Utatumia nini kujihifadhi na hedhi SURA YA 5: MAMBO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI Jiweke safi, nukia vizuri Utunzaji wa meno yako Chunusi...47 Utunzaji nywele Lishe nzuri Mazoezi...51 Mapumziko mazuri...53 v

6 SURA YA 1 UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA sura ya 6: UTUNZAJ I AFYA YA AKILI NA MOYO...55 Kujiheshimu...55 Kujiamini Usiwe na wasiwasi, furahi Kukabili huzuni Kuishi vizuri na watu SURA YA 7: UELEWANO NA WAZAZI WAKO Kuthamini familia Fahamu yale wazazi wako wanayoyataka Kukidhi matarajio ya wazazi wako Mawasiliano na wazazi wako Vyanzo vingine vya kupata msaada...78 SURA YA 8: URAFIKI NA MAPENZI...81 Urafiki Jinsi ya kumtambua mtu ambaye si rafiki wa kweli Kuelewana na jinsi nyingine Kuanza uhusiano na mtu unayempenda Kujenga uhusiano wa kweli...87 Mapenzi Kupumbazika Kuachana kimapenzi SURA YA 9: UJINSIA NA NGONO Ujinsia wenye afya njema Hisia za kijinsia Punyeto Ubikira Kujamiiana Kuweka kiwango cha kujamiiana Uamuzi wa kutofanya ngono Kuzungumza na mwenzi wako kuhusu ngono SURA YA 10: KUTUNZA AFYA YAKO YA KIUJINSIA Magonjwa ya zinaa Utajuaje kama umepata maambukizi ya magonjwa ya zinaa? Kwenda kuchunguzwa magonjwa ya zinaa VVU / UKIMWI Utajuaje kama una VVU Kuishi kwa matumaini na VVU Ngono salama / Mapenzi salama Kondomu Matatizo mengine ya afya ya uzazi SURA YA 11: MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA Mimba inatokeaje? Dalili za mimba Hatari za mimba na uzazi kwa wasichana balehe Kustahimili mimba katika umri mdogo Kujitunza wakati wa ujauzito Mimba na VVU Maandalizi ya kujifungua Kujitunza na kumtunza mtoto baada ya kujifungua Kuharibika mimba Namna ya kuepuka kupata mimba Je vidonge vya kuzuia mimba ni salama? Kuzuia mimba kwa dharura Kinga mara mbili SURA YA 12: NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO Shinikizo kutoka kwa rafiki wa kiume au wa kike Shinikizo kutoka kwa watu wazima Unyanyasaji kijinsia Kudhalilisha kijinsia Ubakaji Kitu cha kufanya ubakaji ukitokea SURA YA 13: MATUMIZI MABAYA YA DAWA Aina ya dawa na vitu ambavyo vinatumika vibaya Sigara na pombe Kutawaliwa na dawa Kwa nini watu wanaanza kutumia dawa Namna ya kushughulikia shinikizo la kutumia dawa Kuacha dawa SURA YA 14: KUTIMIZA NDOTO ZAKO Kuzitambua ndoto zako Mipango ya baadaye kuhusu kazi Kuweka malengo Kufanya uamuzi mzuri (wa busara) Zingatia bila kuyumba katika malengo na ndoto zako Kufanya vizuri katika masomo shuleni Kuacha shule Kutatua vipingamizi FAHARASA MAREJELEO...193

7 SURA YA 1 Ujana Balehe: Badiliko Kubwa, Changamoto Kubwa Patric, kutoka Kenya(Umri,miaka 16) Nilichokifurahia katika ujana balehe wangu ni kuwajibika katika majukumu ya nyumbani hasa wazazi wanapokuwa hawapo. Majukumau haya nayapenda kwasababu ninadhani nimeshakua na ninaweza kujidhibiti mimi mwenyewe na wadogo zangu. Naana, kutoka Ghana. (Umri; miaka 17) Yapo mambo mengi yanayomhusu kijana balehe ambayo siyapendi. Ninakumbuka nilipokiwa na umri mdogo nilikuwa na uhuru zaidi kuliko sasa. Lakini kwa sasa zipo sheria na miongozo mingi. Watu wengi duniani wanatafsiri ujana balehe kama kipindi cha maisha kati ya miaka 10 na 19. Kama una umri wa miaka kati ya 10 na 19, basi wewe ni kijana balehe. Hongera! Wewe ni mtu muhimu sasa. Ni kweli kuwa kwa muda wote uliopita umekuwa mtu muhimu, lakini kwa sasa hivi umekuwa mtu muhimu zaidi. Unapitia mabadiliko mengi sana na unajaribu mambo mengine mapya, kutoka mwonekano mpya,kujitambua kupya kama vile kuandamana na marafiki wa jinsi tofauti,kushikana mikono na kubusiana. Wazazi wako wanaweza kukuta ujana balehe wako unautumia vibaya. 1

8 SURA YA 1 UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA Mwonekano wako mpya na kujitambua kwako kunawafanya wazazi, shangazi zako na wajomba kuwa na wasiwasi kwa sababu wasingependa upate matatizo na wala wasingependa ufanye makosa makubwa kama vile kupata mimba (au kwa kumpa mimba rafiki wa kike) wakati ungali unasoma. Zaidi ya yote wanakuwa na wasiwasi kwa sababu wanafahamu kwamba umri kati ya unaweza kuwa na athari kubwa katika ukuaji wako na aina ya maisha utakayokuwa nayo. NINI MAANA YA UJANA BALEHE? Ujana balehe ni kipindi ambacho unabadilika na kukua kimwili na kiakili kutoka utoto na kuingia utu uzima. Wakati wa ujana balehe mambo yafuatayo hutokea: Mwili wako utabadilika kwa jinsi unavyopenda uwe au wakati mwingine hata usivyopenda uwe. Utaanza kupata hisia za kutaka kujamiiana, na unaweza usijue ufanye nini baada ya kupata hisia hizo. Utaanza kufikiri bila ya kumtegemea mtu mwingine na kutaka kufanya maamuzi peke yako. Hisia zako kuhusu familia na mahusiano yako na wazazi, yanaweza kubadilika kwa uzuri au kwa ubaya. Wazazi wanaweza kukupa majukumu zaidi ambayo ni dalili nzuri kwamba wanakuamini na kukutegemea. Lakini wanaweza vilevile wakaanza kuwa wakali hata kutokuruhusu ukutane na marafiki zako. Wakati mwingine watajaribu kufanya maamuzi kuhusu masomo na mustakabali wa maisha yako ya baadaye. Wanaweza wakaonyesha kuwa na upendo mdogo kwako kuliko walivyokuwa huko nyuma na unaweza vilevile usipate mahusiano yenye upendo kama ulivyokuwa ukiwa mtoto. Marafiki zako, na hata yale wanayofikiria, vinaweza kuwa vya muhimu zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Hisia zako zinaweza kuwa na utata zaidi kuliko ulivyozoea na wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza usifahamu hasa kile unachohisi au ni kwa nini unahisi hivyo. Kwa hakika unaweza kuhisi kutaka kupendwa au kuwa karibu na mtu mwingine. Unaweza kukumbana na maamuzi mazito na zinaweza kuwepo nyakati ambapo hujui umtake nani ushauri. Ujana balehe ni kipindi maalum kwa kila mtu, kote duniani mashariki au magharibi,kaskazini au kusini.lakini pia ni kipindi chenye changamoto. Hiki ni kipindi cha mabadiliko makubwa, na mabadiliko makubwa huchukua muda. Utakutana na mambo mengi ya kuyafanyia maamuzi unapopitia ujana balehe na maamuzi mengine utakayofanya yatadumu nawe katika maisha yako yote. Yapo mambo mengi sana ambayo unaweza kuyafanya ili kupitia salama ujana balehe. Hivyo ni vema uelewe mwili wako na mabadiliko yanayotokea.ni vema ujielewe na pia uelewe kile unachokitaka katika maisha. Tumia muda kufikiria maisha yako ya baadaye na kupanga yatakuwaje. Utu uzima una majukumu makubwa hivyo basi ni lazima kujiandaa vema wakati wa ujana balehe. Wakati wa ujana usiwe mpweke na kufanya mambo peke yako. Umezungukwa na watu wanaoshughulikia matatizo muhimu kila siku. Unao ndugu wengi, kama akina shangazi, wajomba, binamu na wengi wengineo, amabao unaweza kuwaomba ushauri. Pia kwa vile wewe ni sehemu ya jamii, zipo mila na desturi nyingi ambazo mafunzo yake yanaweza kukusaidia. Mahali pengi ujana umekuwa mgumu kueleweka, na hasa siku hizi vijana wanapata matatizo ambayo wazazi wao, mabibi hata babu zao hawakuwahi kuyapitia; matatizo hayo ni: Msukumo wa kutaka kujamiiana. Madawa ya kulevya shuleni na kwenye jamii. Wazazi ambao kwa sababu ya shughuli nyingi hawana muda au wanaona aibu kuzungumza kuhusu mabadiliko yanayowatokea watoto wao. Magonjwa yaambukizwayo kwa kujamiiana ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI. Kuwa yatima kwa sababu ya UKIMWI au ajali. Vita au kuyumba kisiasa kwa nchi. Ili kuyamudu yote haya na kupitia kipindi cha ujana balehe salama unahitaji kuwa jasiri, mbunifu, mtafutaji na mwenye kujipa matumaini. Jaribu kujifunza kutoka kwa watu wanaokuzunguka ambao ni jasiri na watulivu wakati unapokutana na matatizo. Kila wakati jione kuwa utashinda matatizo yako kama walivyoweza wengine. VIJANA HUFIKIRIA KWAMBA HAKUNA JANGA LINALOWEZA KUWAPATA Ni tabia ya vijana duniani kote, katika nchi tajiri na maskini kufikiria kwamba mambo mabaya hayawezi kuwatokea. Hujiambia, Haitatokea kwangu. Wakati mwingine hujiamini sana na kuhisi wako salama mno. Je wewe uko hivi? Unadhani unaweza kujaribu kitu cha hatari na lisikupate jambo? Kwa mfano, wewe na rafiki yako wa kike (msichana) mnafahamu kuhusu dawa za kuzuia mimba. Lakini mnadhani kwamba ili mradi hamjamiiani mara kwa mara, msichana hawezi akapata mimba. Au unaweza ukawa na ufahamu mkubwa kuhusu VVU, virusi vinavyo sababisha UKIMWI. Unaweza ukafahamu kwamba maambukizi yanaweza kutokea kwa njia ya kujamiiana bila kinga, lakini unafikiri kwamba rafiki yako wa kiume hawezi kuwa na maambukizo. Unakataa kufikiri kuwa unaweza kupata maambukizo ya VVU na haiwezekani pia kwa wale watu unaowafahamu kupata ugonjwa huo. Je haya yanakuhusu? Kama ndivyo, hapa kuna mambo ambayo unahitaji kuyazingatia: Vijana wengi hujiingiza kwenye vitendo vya hatari wakidhani kuwa hawatadhurika

9 SURA YA 1 UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA Mimba inaweza ikatungwa utakapojamiiana kwa mara ya kwanza bila kinga. Kusema kweli, kila watu wawili wanapojamiiana bila kinga kuna uwezekano wa 1:12 mimba kutungwa. Maana yake ni kwamba iwapo mtajamiiana bila kinga mara moja kwa mwezi, mnaweza kukumbwa na mimba isiyotarajiwa....mimba huweza tungwa hata kamaumejamiiana mara moja.inaweza kutungwa utakapojamiiana kwa mara ya kwanza. Ili kupita kipindi cha ujana salama unahitaji angalau mambo matatu: Ukweli Kuhusu Maisha Kumbuka pia kwamba maambukizi ya VVU hutokea kwa vijana pia, na hutokea kwa vijana zaidi kuliko hata kwa wengine. Vijana wanapata maambukizo ya VVU haraka zaidi kuliko kundi lingine lolote Afrika. Maambukizi mapya kwa watu kumi,watu sita huwa ni vijana. Usiruhusu ukawa mmojawapo kati ya vijana wenye mimba zisizotakiwa au wenye maambukizi mapya ya VVU. Soma kitabu hiki kwa uangalifu ili ujue jinsi unavyoweza kufanya maamuzi mazuri, ili uwe salama na mwenye afya. Tafadhali washirikishe marafiki zako kusoma kitabu hiki ili nao pia wajifunze jinsi ya kuchagua yale yaliyo mema. Maadili Unahitaji kujua yale unayoamini ni ya kweli ili uweze kufanya maamuzi unayoweza kuishi nayo. Stadi za maisha, ili utumie ukweli unaoujua na kubakia mkweli ndani ya maadili yako. UKWELI KUHUSU MAISHA Nini maana ya hali halisi/mambo ya ukweli? Ukweli kuhusu maisha ni upi? Ukweli ni taarifa zote muhimu za mambo unayotakiwa kuyafahamu ili kuyamudu maisha ya kila siku na kufanya maamuzi mazuri. Kufahamu ukweli maana yake ni kufahamu jinsi ya kujitunza mwenyewe kimwili na kifikra kwa kula vizuri; kutunza mwili vizuri; na kutunza vizuri afya ya akili na maono yako. Kufahamu ukweli vile vile maana yake ni kufahamu jinsi mimba inavyotokea, jinsi VVU/UKIMWI na magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana yanavyosambaa na jinsi unavyoweza kuzuia usiambukizwe. Ukweli ni kufahamu ni kwa namna gani madawa ya kulevya na pombe vinaweza kuudhuru mwili na ubongo na jinsi maisha yako yanavyoweza kuharibika. Ukweli ni kufahamu njia nzuri za kumudu hali ngumu na matatizo yako, ili uweze kufanikisha ndoto zako. La muhimu zaidi, kufahamu ukweli ni kubainisha kati ya yaliyo ya ukweli na yaliyo ya uongo. Ni muhimu sana kujua mambo ya ukweli wakati unapojaribu kuchagua. Chagua lililo la muhimu na amua la kufanya. Unahitaji mambo ya ukweli ili uwe salama. Kitabu hiki kimejaa ukweli, hivyo kitakupa ukweli kuhusu: Mabadiliko yanayotokea mwilini mwako (Sura ya 2,3, na 4). Kutunza afya yako ya kimwili na kimaono (Sura ya 5 na 6). Mahusiano na watu wengine (wazazi, marafiki wa kike na marafiki wa kiume) (Sura ya 7 na 8 ). Ujinsia, ngono, na kutunza afya ya ujinsia.(sura ya 9 na 10). Mimba na madawa ya kuzuia mimba (Sura ya 11). Kulazimishwa na kujamiiana (Sura ya 12). Madawa ya kulevya na pombe.(sura ya 13). Kupanga maisha yako ya baadaye na kufikia malengo yako.(sura ya 14). MAADILI Neno maadili lina maana ya mambo unayoyaamini, unayoyathamini na tabia unazodhani ni muhimu katika maisha yako. Maadili mema ni kama yafuatayo: Kuwa mkweli. Uwazi. Uvumilivu. Ukarimu. Hisani/Wema. Kusamehe. Yaliyotajwa hapa juu ni machache tu kati ya maadili mema, waweza kuwa na mengine; kwa mfano kusoma kwa bidii, kusaidia wazazi, uaminifu kwa rafiki zako, kujitolea kwenye shughuli za jamii yako au za kidini. Maadili yanasaidia kuongoza matendo na maamuzi yako. Yanakusaidia katika kuchagua yaliyo mema kwako na kwa wengine. Kwa mfano, kijana mkarimu na mvumilivu atamsadia mwanafunzi mwenzie mlemavu au jirani yake aliyefanyiwa mabaya na watu wengine. Mtu mwaminifu atachagua kurudisha pesa za muuza duka alizomzidishia wakati akimpa chenji. Je, una maadili gani? Kipi ni kitu muhimu na chenye thamani kwako? Unaamini katika misingi gani ya maisha? Unaposoma kitabu hiki, jaribu kujiuliza kuhusu maadili yako. Kufahamu maadili yako kutakusaidia kufanya maamuzi makini ili uwe salama wakati wote wa mabadiliko ya ujana balehe. 4 5

10 SURA YA 1 UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA Ukijua unachokithamini itakusaidia kuwa mkweli kwako binafsi, hata wakati mtu mwingine anapokulazimisha kufanya kitendo unachodhani ni makosa. Maadili yako yatakusaidia kuchagua lililojema kwako; ambalo wakati mwingine, baada ya kuchagua, itabidi uishi nalo daima. STADI ZA MAISHA Jambo lingine la muhimu katika kufanya maamuzi ni kujipa muda wa kutosha. Kumbuka,unaweza kumueleza mtu kwamba ninahitaji kufikiria zaidi kuhusu jambo hili na nisubiri nitakujibu Unahitaji stadi za maisha pia ili uwe salama. Kusema kweli Stadi za maisha zinaweza kuwa stadi za kuokoa maisha, kama vile uwezo wa :- Kuelezea hisia zako. Hisia zako ni muhimu, lakini watu wengine hawawezi kujua unavyojisikia mpaka uwaeleze. Jifunze jinsi ya kuwafanya watu wengine wajue kile unachofikiri na unachokitaka kwa kusema moja kwa moja na kutumia sentensi zinazoanzia na mimi mimi ninataka mimi ningelipenda mimi ninahitaji mimi Sipendi. Fanya mazoezi ya kutumia sentensi zinazoanza na mimi mpaka utakapozoea na kujisikia huru kuzitumia. Tetea hoja yako. Una uhuru wa kufikiri na kujihisi unavyopenda. Ni vema kujifunza jinsi ya kuwasilisha mawazo yako kwa wengine bila ya kuwaudhi au kuwafanya wajisikie vibaya, usionyeshe uadui, ugomvi wala kukosoa sana. Tetea unachoamini bila kujali wanayosema watu wengine. Kila mtu ana imani na yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, mazuri na mabaya. Imani hizi zinaitwa kanuni. Wakati mwingine unaweza ukawa unajua kanuni zako lakini mambo yanaweza yasiwe wazi sana kiasi cha kukufanya utumie muda kufikiria lipi ni sahihi kwako na ni kwa nini. Iwapo unao uhakika wa usahihi wa kile unachofikiria na kwa nini unakifanya, na kwa nini hupendelei kukifanya utaweza kusimama imara na lile unaloamini. Hivyo basi msimamo wa namna hii utakupa heshima mbele za watu. Jihadhari na yanayotokana na shinikizo. Kuwa na msimamo wa pekee ndiyo stadi za Maisha. Jinsi unavyoelekea kwenye utu uzima unatakiwa kufanya maamuzi mengi peke yako. Wakati mwingine watu wengine wanaweza kukuhimiza na kukusukuma kufanya maamuzi fulani na ukushawishika kufanya hivyo. Lakini ufahamu kuwa kufanya maamuzi mazuri maana yake ni kupima chaguo zote zilizopo na kufikiria matokeo kwa kila chaguo.inaweza ikawa kazi ngumu iwapo kuna mtu anakuharakisha au anakushinikiza uamue haraka. Kitu muhimu katika kufanya maamuzi bora ni kuwa na uhakika wa kanuni zako na malengo yako ya maisha kwa ujumla. Stadi hizi za maisha zina majina yake, kama vile kuongea bila woga wala jazba Mawazo yenye ubunifu Kutatua matatizo, Kufanya maamuzi na Kujitambua. Stadi za maisha ni muhimu sana. Ukweli ni kwamba stadi za maisha ni muhimu kama ilivyo kuufahamu ukweli. Kuufahamu ukweli wa mambo peke yake hakuwezi kukulinda hadi uwe pia na stadi za maisha. Kwa mfano unaweza ukafahamu kwamba kujamiiana bila kinga kunaweza kukusababisha mimba na magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU/ UKIMWI. Vilevile unaweza ukawa umeamua kwamba hutaki kujamiiana, lakini bado ukawa huna uwezo wa kujieleza na kutetea hoja zako kwa rafiki yako wa kiume. Unahitaji Stadi za maisha ili uutumie ukweli unaoufahamu kusimama imara katika yale unayoyataka na kuyaamini, hasa pale inapotokea watu unaowajali na kuwaheshimuwanatofautiana na wewe. Je, Unazo Stadi za maisha? Unaweza ukasimama imara na kuwa na msimamo kwa yale unayoyaamini kuwa ni sahihi hata kama marafiki zako wanawaza tofauti? Unao ujasiri wa kutosha kutetea afya yako au maisha yako? Anza kuzitumia stadi zako kadri unavyoendelea kusoma kitabu hiki. Kufanya maamuzi mazuri na kusimama imara kwa unachokiamini ni stadi bora za maisha 6 7

11 SURA YA 2 Mabadiliko ya mwili Wasichana na wavulana wengi wanabalehe kati ya umri wa miaka 10 na 16. Balehe ni kipindi ambacho unabadilika kimwili, kihisia/kifikra na kiakili kutoka utoto na kuingia utu uzima. MFOKO WA UKUAJI: MWANZO WA BALEHE. Ipo tofauti ndogo sana kimaumbile kati ya wasichana na wavulana kati ya miaka 9 na 10. Japokuwa via vyao vya uzazi ni tofauti lakini vifua vyao na misuli vinafanana. Tofauti kubwa ya kimwili kati ya wasichana na wavulana huanza kujitokeza kipindi cha balehe. Kwa wastani wasichana wanaanza kuonyesha mabadiliko makubwa ya ukuaji kimwili kati ya umri wa miaka 10 au 11. Kipindi hiki cha kukua haraka kinaitwa mfoko wa ukuaji. Kwa wasichana kipindi hiki cha mfoko wa ukuaji hudumu miaka mitatu. Wakati huu wasichana wanakuwa warefu na wakubwa zaidi ukilinganisha na wavulana wa umri huo huo. Wavulana wanachelewa kidogo kufikia mfoko wa ukuaji kuliko wasichana, kwa wastani katika umri wa miaka 12 au 13. Kwa wavulana; mfoko wa ukuaji hudumu muda mrefu kuliko wasichana, ukweli ni kwamba wavulana wengine huendelea kukua mpaka wanapofikia miaka 19 au 20. Lakini kumbuka kwamba miaka hii ya ukuaji ni ya wastani tu. Vijana wengine huanza mfoko wa ukuaji mapema zaidi na wengine huchelewa. Kuanza mapema au kuchelewa hakuna athari yoyote katika namna utavyorefuka au namna utakavyokua haraka.wale wanaoanza mapema, wengine wanakua haraka wakati wengine wanakuwa taratibu. Vile vile kwa wale wanaochelewa kuanza wengine wanakua haraka na wengine taratibu. Katika kipindi hiki cha makuzi ya haraka, mara nyingi wavulana na wasichana wanajisikia hovyo. Hii ni kwa sababu sehemu mbali mbali za mwili hukua kwa wakati tofauti na kwa kiwango tofauti. Mara nyingi, viganja vya mikono na nyayo huongezeka kwanza ikifuatiwa na mikono, miguu, kiuno/nyonga na kifua. Vijana wengi wanaokua haraka hujikuta mara nyingine wakiteguka na kuanguka. Inashangaza kujiona umeongezeka sentimeta kadhaa ghafla! Mfoko wa ukuaji Mfoko wa ukuaji 8 9

12 SURA YA 2 Mabadiliko ya mwili Wavulana na wasichana wengine hukua haraka sana wakati wa balehe kiasi cha kwamba ngozi yao inashindwa kustahimili ukuaji haraka wa mifupa. Wakati mwingine inapotokea hivyo alama za misitari hutokea kwenye ngozi. Alama hizi zinaweza kupotea au zisionekane kiurahisi mtu anavyoendelea kukua, lakini zinaweza zisipotee moja kwa moja. Hata kama unajiona kukua haraka,bado balehe ni kitendo cha taratibu mno. Itachukua muda mrefu kabla hujawa mtu mzima kimwili na kifikra. Kwa wakati huu yafuatayo ni mambo ya kuzingatia. KILA MTU YUKO TOFAUTI Kila mtu hufikia balehe kwa wakati tofauti na kwa kiwango tofauti. Matiti yako yanaweza kuchelewa kukua kuliko ya rafiki zako lakini wewe unaweza ukavunja ungo mapema au unaweza kuyapata yote haya baadaye sana. Matiti yanaweza yakakua na ukavunja ungo akiwa na umri wa miaka 12 na wewe matiti yanaweza kukua na ukavunja ungo ukiwa na umri wa miaka 15. Au kama wewe ni mvulana unaweza ukawa na rafiki yako ambaye sauti yake ili badilika kuwa nzito akiwa na umri wa miaka 13. Anaweza akawa ameota mavuzi na misuli wakati wewe hujakua hata sentimeta moja! Wasichana hawa wote wana umri wa miaka 13,lakini wanakua kitofauti Kumbuka kila mtu yuko tofauti na kila yanapokutokea mabadiliko huu ndio wakati muafaka kwako. Sherifan, kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Nilianza kuona mabadiliko katika mwili wangu nikiwa na miaka 11. Matiti yalianza kuota, nywele zikaota kwapani na kwenye via vya uzazi. Nilijisikia vibaya sana kwa sababu nilipata mabadiliko haya mapema sana na nilijiona niko tofauti sana na wenzangu wa rika moja Sherry, kutoka Ghana (Umri wa miaka 19) Nilikuwa darasa la sita(6), sifahamu kama marafiki zangu walikuwa wanachelewa kukua au mimi nilikuwa nimewahi kukua, lakini nilijisikia vibaya matiti yalipoanza kukua. Niliwahi kumsikia mama akisema jinsi walivyokuwa wakitumia tapoli, kifaa kidogo cha ubao kilichotumika kusaga pilipili, kujaribu kuondoa uvimbe kwenye matiti wakati wa enzi zao. Kwa hiyo nilijaribu, kama mara tatu hivi. Lilikuwa ni jambo la kuchekesha, lakini hata hivyo haikusaidia kitu. Lakini sasa hivi waliokuwa wananitania wana matiti makubwa kuliko ya kwangu. Kumbuka kuwa mambo haya yanaisha kadri muda unavyopita. Utakapofikisha miaka 20 hakutakuwa na tofauti yoyote kwako au kwa mtu mwingine, iwapo sauti yako ilibadilika ukiwa na miaka 13 au miaka 17. Hakutakuwa na tofauti iwapo ulivunja ungo ukiwa na miaka 11 au miaka 16. Sherry, kutoka Ghana (Umri; miaka 19) Ebu tuyaache mambo yaende kama yalivyopangwa kwani hata kama hupendi huwezi kubadili kitu isipokuwa kujikubali tu. Wavulana hawa wote wana umri wa miaka 13,lakini wanakua kitofauti KILA MTU ANA MABADILIKO YAKE Kwa kutumia kigezo cha afya, haitegemei kama mwili wako unakua haraka au taratibu kuliko rika lako. Mwili wako utabadilika muda utakapofikia. Hakuna unachoweza kufanya kuhusu muda wa mabadiliko. Wasichana na wavulana wengine wenye afya nzuri huchelewa kukua kuliko wenzao wa rika moja. Wasichana na wavulana wengine wanakua mapema kuliko wenzao wa rika moja na wala hawana kasoro yoyote na wana afya nzuri pia. Lakini hata hivyo unaweza kupata matatizo kama utakuwa tofauti na wengine.kwa mfano: inaweza kuwa vigumu kwa msichana kuwa wa kwanza kuwa na matiti darasani, au mvulana kuwa wa mwisho kubadilika sauti. Hii inaweza kusababisha kutaniwa na unaweza kujisikia upo tofauti sana na kundi rika lako. Ingawa huwezi kuubadili mwili wako yapo mambo yanayokuhusu ambayo unaweza kuyabadili: 1. Unaweza kuhakikisha kuwa wewe ni mtu mzuri. Hakikisha kuwa unafanya kazi kwa bidiii katika lolote utakalokuwa unafanya (shuleni, kazini na nyumbani). Unaweza ukakuza haiba yako, ucheshi wako,pia na tabia yako. Angalia kuwa wewe ni nani na unataka uweje baadaye na wala sio vile unavyoonekana. 2. Jitahidi sana kutotilia maanani utani jaribu kupuuza na usiwaruhusu wanaokutania waone umefadhaika. Mwishowe watachoka kukutania. 3. Heshima na kukubalika na rafiki zako visije vikakushawishi kufanya mambo ambayo sio mazuri kwako. Usiruhusu marafiki zako kukulazimisha kufanya mambo ambayo unajua sio sahihi, kama vile kutania watu wengine, kutumia madawa ya kulevya au kujiingiza kwenye mambo yanayoweza kukudhuru. 4. Jielimishe mwenyewe kwa kutafuta taarifa sahihi. Hakihisha unafahamu wapi utapata taarifa unazozihitaji na majibu ya maswali yako yote wakati unapoupitia ujana 10 11

13 SURA YA 2 Mabadiliko ya mwili Pia, weka akilini haya: Watu wa umri wako mara nyingi wanajua taarifa nyingi za uongo kuliko za ukweli hasa inapokuwa ni za kuelezea balehe na kujamiiana. Marafiki zako wanaweza kukueleza mambo ambayo si ya kweli, hivyo unahitaji kufahamu wapi uende ili kupata ukweli. Kwa mfano, unaweza kuambiwa kwamba, matiti au uume utakua iwapo utajamiiana. Au unaweza kutaniwa kwamba matiti yako ni makubwa kwa sababu umekwishajamiiana. Hali kadhalika unaweza kusikia kwamba chunusi ni dalili za kwamba unatakiwa ujamiiane. Lakini hakuna lolote katika haya lenye ukweli. Yote ni uzushi/uwongo. Uzushi kama huu unaweza kuleta hatari zaidi kwa sababu unaongeza hofu. Uzushi kama huu unakufanya ufikirie kwamba unaweza kufanya mambo ili kubadilisha yale ambayo huwezi kuyadhibiti. VICHOCHEO (HOMONI) Ni kitu gani hudhibiti mabadiliko ndani ya mwili wako? Ni kitu gani hufanya ukue haraka au taratibu? Ni kitu gani hukufanya uongezeke? Mwili wako wakati wote unatengeneza homoni, ambazo ni kemikali tarishi maalumu ambayo huuambia mwili namna gani na lini ubadilike na kukua. Mfoko wa ukuaji wako husababishwa na homoni za ukuaji ambazo zinatoka kwenye ubongo kwa wingi. Pamoja na homoni za ukuaji, homoni za jinsi nazo huanza kutolewa wakati wa balehe. Kwa wasichana homoni za jinsia zinatengenezwa ndani ya ovari na kwa wavulana zainatengenezwa ndani ya korodani. Homoni za jinsi ndizo zinazosababisha tofauti katika maumbile ya mwanaume na mwanamke. Wasichana wanapoingia kipindi cha balehe nyonga zao huongezeka. Kawaida nyonga hukua haraka kuliko kifua. Nyonga ya msichana hupanuka na kujiviringa, na kiuno huonekana kidogo na chembamba. Matiti vilevile huanza kukua. Kwa wavulana, homoni za jinsia husababisha kifua kupanuka, mikono na miguu inakuwa minene yenye misuli. Matiti ya wavulana hayabadiliki sana kama ya wasichana yanavyobadilika wakati wa balehe, lakini hubadilika kidogo. Kwa wavulana wengine, matiti yao hukua kipindi cha balehe lakini kawaida hupotea kadri muda unavyokwenda. Homoni huathiri pia hisia zako. Vijana wengi hujisikia kuwa na hisia kali. Dakika moja tu anaweza kuwa na furaha na msisimko, lakini dakika inayofuata akawa na huzuni karibia kulia. Anaweza kujisikia vizuri siku moja na vibaya siku inayofuata. Mabadiliko haya katika hisia yanaitwa hisia za kuyumba. Jambo hili huwatokea vijana wengi mara kwa mara. Wakati wa ujana balehe, utengenezaji wa homoni huongezeka ghafla, kitendo ambacho huwafanya vijana wengi wawe na hisia kali za aina mbalimbali. Baadaye katika maisha utengenezaji wa homoni utapungua na utajisikia unao uwezo wa kudhibiti hisia. Weka akilini kwamba mabadiliko yote ya kimwili, kihisia na kiakili yanayotokea wakati wa balehe yanasababishwa na homoni zinazotengenezwa na mwili wako. Hakuna unaloweza kufanya kuharakisha au kuchelewesha utengenezaji wa homoni. Jaribu kukumbuka tu kwamba wewe ni wa pekee na huna kasoro yoyote. VIA VYA UZAZI SEHEMU ZA SIRI Pamoja na kuleta mabadiliko katika umbo la mvulana na msichana, homoni hufanya via vya uzazi kukua. Via vya uzazi maana yake ni zile sehemu za siri za mwili wako ambazo mara nyingi zinafunikwa na chupi/nguo za ndani. Kabla hujawa kijana balehe, sehemu za siri zilikuwa kwa ajili ya kujisaidia tu (kukojoa). Wakati wa ujana balehe hata hivyo, sehemu za siri zinakuwa kubwa. Kwa wasichana ngozi na tishu huwa laini na yenye mafuta mafuta, kwa wavulana uume huanza kurefuka na kunenepa. Korodani vilevile hukua na kuanza kutengeneza mbegu za kiume. Kipindi cha balehe via vya uzazi huanza kutengeneza majimaji pia. Wavulana huanza kutengeneza shahawa, majimaji yaliyo kama kamasi ambayo mbegu za kiume huogelea. Shahawa hutoka nje ya uume wakati mvulana anapofikia mshindo. Wasichana vilevile hutoa majimaji ya ukeni na damu ya hedhi. (soma sura ya 3 na ya 4 kwa maelezo zaidi kuhusu wavulana na wasichana) NYWELE ZA MWILINI NA MABADILIKO YA NGOZI Ngozi yako na nywele za mwilini hubadilika vilevile katika kipindi cha balehe. Kwa vijana wengi ngozi inakuwa na mafuta. Ngozi ya utotoni hupotea. Hii hupelekea chunusi kutoka, jambo ambalo ni tatizo la kawaida kwa vijana wengi (soma sura ya 5 kwa maelezo zaidi kuhusu utunzaji mzuri wa ngozi). Dalili nyingine ya balehe ni nywele kuota sehemu mpya za mwili. Wavulana na wasichana wote wanaweza kuota nywele kidogo miguuni na mikononi. Kwa kuongezea wavulana huota nywele sehemu za siri, usoni kifuani na kwapani. Wasichana vilevile huota nywele sehemu za siri na kwapani. Nywele zinazoota sehemu za siri zinaitwa mavuzi, watu wengine wana mavuzi mengi na wengine wanayo kidogo. Mavuzi husaidia kufanya eneo la via vya uzazi liwe safi, jambo ambalo ni zuri sana kwani ngozi inayozunguka via vya uzazi ni laini/nyororo sana na ni rahisi kuumia.mavuzi husaidia kuzuia jasho na vitu vingine kutoka kwenye ngozi laini ya via vya uzazi. Kipindi cha balehe huwa kina ambatana na hisia kali 12 13

14 SURA YA 2 Mabadiliko ya mwili Vijana wengine hawafurahii nywele mpya zinazoota mwilini hasa mavuzi yanapotokea kwa mara ya kwanza. Balay, kutoka Kenya (umri, miaka 16) Nilistushwa! Sikujua kama mtu anaweza kuota nywele sehemu zake za siri. Nilidhani ninaumwa, na nikamwuliza mama ambaye alinihakikishia kwamba ilikuwa ni jambo la kawaida. Diana, kutoka Zambia (Umri, miaka 17) Zilipoota, nilijisemesha mwenyewe kwamba itabidi nikubaliane na hali halisi Doglas, kutoka Zimbabwe (Umri miaka 12) Yalipoota mavuzi haikunifurahisha yalinifanya nionekane mbaya Mara nyingi, kwa mara ya kwanza utayaona mambo tofauti na wazazi wako wanavyoyaona. Unaweza kujisikia kutaka kujua imani za wazazi wako na sababu zake. Unaweza kutaka kujaribu kuishi maisha yako mwenyewe kuliko kutegemea ya kuambiwa na wengine. Unaweza kujaribu mambo mapya mwenyewe na wakati mwingine kujaribu mambo ya hatari. Mabadiliko yote haya ya akili ni dalili nzuri za kuonyesha kwamba unaingia utu uzima. Hata hivyo haina maana ya kwamba tayari umeishakuwa mtu mzima. Ingawa uwezo wako wa kiakili unaongezeka sana, bado kuna mambo mengi unakuwa hujayajua. Ukweli hutaweza kuyajua yote, kwa hiyo ni muhimu kujua wapi uende na umwone nani kwa ajili ya taarifa unayoihitaji. Kutakuwepo wakati ambapo itakuwa muhimu kutumia uzoefu na maarifa kutoka kwa waliokuzidi umri. Hivyo basi unatakiwa kuuliza maswali, usidhani unayo majibu yote. Jitahidi kujifunza mengi iwezekanavyo. Vijana wengine hutaniwa wanapokuwa wameota mavuzi au wanapokosa kuota. Bernard, kutoka Kenya (Umri, miaka 17) Marafiki zangu walinicheka ati kwa sababu mavuzi yalikuwa hayajaota. Kumbuka ya kwamba mavuzi ni kitu cha asili na yana kazi yake, kwa hiyo iwapo unayo mengi au kidogo usihofu sana. Vilevile, nywele huota kwapani kipindi cha balehe, ingawa mara nyingi ni wakati wa mwisho wa kipindi cha balehe. Wasichana wengi hawaoti nywele kwapani mpaka baada ya matiti kuanza kuota na baada ya kuvunja ungo. Kwa wavulana nywele za kwapani kwa kawaida huanza kujitokeza mwaka mmoja au zaidi baada ya mavuzi kuota. Kama mavuzi, nywele za kwapani zina kazi maalum.wakati wa balehe jasho linatoka sana na nywele husaidia kuzuia jasho lisitoke kwenye ngozi. Kwa kawaida,kwa wavulana, nywele za usoni huwa za mwisho kuota. Huanza kuota pembeni mwa midomo ya juu. Nywele zinazoota juu ya midomo ya juu (masharubu) huendelea kuota, na zingine huota sehemu ya juu ya kidevu na chini kidogo katikati ya midomo ya chini na mwisho zingine huota kwenye kidevu. Nywele hazioti kidevuni mpaka via vya uzazi vya mvulana viwe vimekomaa kabisa. Kwa wavulana wengi, nywele za usoni huanza kuota hasa wakiwa na umri kati ya miaka 14 na 18.Lakini zinaweza kuanza kuota mapema zaidi au zikachelewa. UWEZO WA KUFIKIRI Wakati mabadiliko dhahiri yanayotokea katika mwili kipindi cha balehe, akili nayo pia hubadilika bila ya kutambulika kiurahisi.katika kipindi cha ujana balehe, uwezo wa akili unaongezeka sana hasa katika kufikiri kwa makini na kutoa maoni ya kina. Matokeo ya mabadiliko haya husababisha utambulisho binafsi kuanza kujengeka.unaanza kujiona kama mtu wa kipekee. Unapenda kufikiri mwenyewe na kufanya maamuzi yako binafsi

15 Sura ya 2 MABADILIKO KATIKA MWILI WAKO Ujana, ambao kawaida huanzia umri kati ya miaka 10 na 16 ni mabadiliko ya hatua kutoka utoto kuingia utu uzima. Kila mtu anaanza kubadilika wakati wake. Wakati watu wengine hukua haraka zaidi, wengine hukua taratibu. Tunatofautiana, na hakuna unaloweza kufanya kuthibiti muda wa mabadiliko hayo. Ni yapi uyategemee unapobadilika kutoka msichana na kuwa mwanamke au kutoka mvulana na kuwa mwanaume? Mfoko wa ukuaji; viganja, nyayo, miguu, mikono, nyonga kifua vyote vitaongezeka ukubwa mwili utatengeneza homoni, kemikali maalumu ambazo hutoa ujumbe namna mwili utakavyokua na kubadilika. Via vya uzazi (au sehemu za siri) vitakuwa vikubwa na vitaanza kutengeneza majimaji (giligili). Ngozi inaweza kuwa na mafuta zaidi. Utaanza kuota mavuzi na nywele kidogo kwapani, miguuni, mikononi na kama ni mvulana, usoni pia. Utaanza kupata hisia nzito mbali mbali. Uwezo wa kufikiri utaongezeka. Bila ya kujali mabadiliko yanatokea haraka au taratibu, wakati gani yanaanza, jaribu kukumbuka kwamba mabadiliko haya ni ya kawaida na hayana kasoro yoyote. Inaweza kuchukua muda mrefu kuyazoea mabadiliko haya kwa hiyo kuwa mvumilivu na usihofu. Wavulana Katika sura ya pili umesoma baadhi ya mabadiliko kadhaa ambayo wavulana wanayapata katika kipindi cha balehe. Sura hii itakupa maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya. UMBO NA UKUBWA WA MWILI Mfoko wa ukuaji kwa wavulana wengi unaanza kati ya miaka 12 na 13. Hata hivyo wavulana wengine wanaanza ukuaji mapema zaidi na wengine wanachelewa. Wakati wa mfoko wa ukuaji, mwili wako utaanza kuwa mrefu zaidi na mkubwa. Sehemu mojawapo ya mwili wako itakayoanza kukua ni miguu. Ukweli ni kwamba, mifupa ya miguu inakua haraka zaidi kuliko sehemu zingine za mwili. Hivyo basi miguu inaweza kukua hadi mwisho kabla ya sehemu zingine kukua sana. Iwapo utajisikia kama vile unakuwa mzito ghafla, inawezekana ni kwa sababu ya miguu yako imekuwa mikubwa kuliko ilivyokuwa muda mfupi uliopita. Unatakiwa kuwa mvumilivu kwani hali hii inaweza kukuchukua muda kabla hujaizoea Mifupa mingine ya mwili nayo itakuwa zaidi kuliko mingine na kusababisha umbo la mwili kubadilika. Kwa mfano, mabega yatakua zaidi wakati nyonga inaweza kukua kidogo tu. Nyonga yako inaweza kuonekana nyembamba ukilinganisha na upana wa mabega. Inawezekana miguu na mikono ikakua zaidi kuliko uti wa mgongo, hivyo basi miguu inaweza kuwa mirefu ukilinganisha na kifua au kiwiliwili. Matokeo yake umbo lako litakuwa tofauti sana na lile la mvulana mdogo. Misuli vile vile inakuwa, hasa ile ya miguuni na mikononi. Kadri misuli inavyokua, ndivyo unavyokuwa na nguvu zaidi. Mlundikano wa misuli na mafuta utasababisha kifua kuwa kikubwa. Vile vile wavulana wengi hugundua kwamba kuna mabadiliko ya chuchu na matiti katika kipindi cha balehe. Chuchu huongezeka na kuwa kubwa kidogo. Miduara inayozinguka chuchu nayo huwa mikubwa na rangi yake kuwa nyeusi kidogo. Wavulana wengine wanajikuta matiti yao yamevimba na yanauma. Kwa wachache, uvimbe huzidi, hivyo kuwasababishia wasiwasi kuwa wataota matiti makubwa kama wanawake. Usiwe na wasiwasi, haya ni mambo ya kawaida uvimbe na ulaini unasababishwa na homoni ndani ya mwili. Uvimbe unaweza ukadumu mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu, lakini baada ya hapo hupungua kwa vile mwili unaacha kutengeneza homoni nyingi. Wakati wa mabadiliko yote haya unatakiwa kuwa mvumilivu kwani mwili wako hauna matatizo yoyote, na wewe ni wa kawaida kabisa. Hata kama hukui haraka ukilinganisha na rafiki zako wanavyokua, usiwe na wasiwasi utakua tu, muda bado. Ni wakati gani unaanza kukua na kiasi gani utakua,inategemea sifa bainifu unazorithi kutoka kwa wazazi wako. Hata ukichelewa SURA YA

16 SURA YA 3 wavulana kuanza kukua, unaweza kujikuta wewe ni mrefu kuliko wavulana wengine waliopata msukumo wa ukuaji mapema. SAUTI YAKO Sauti yako ni dalili nyingine ya uhakika kwamba unaingia kipindi cha balehe. Sauti huanza kubadilika baada ya mfoko wa ukuaji kuanza, kwa kawaida ni katika umri wa miaka 14 au 15. Sauti ya wavulana hubadilika kuwa ya chini na nzito katika kipindi cha balehe, kwa sababu ya homoni inayoitwa testosterone.aina hii ya homoni husababisha zoloto (sehemu ya mwanzo wa koromeo inayohusika na utoaji wa sauti) kuwa kubwa. Kwa jinsi nyuzi za sauti zinavyokuwa nene na ndefu ndivyo sauti inavyokuwa ya chini na nzito. Precious, mvulana kutoka Ghana (Umri, miaka 15 ) Kitu cha kwanza nilichogundua ni kukatika kwa sauti, kupanuka kifua na mabega. Nilifurahi kwa sababu niliona kwamba sasa ninakuwa kijana balehe. VIA VYAKO VYA UZAZI (SEHEMU ZAKO ZA SIRI) Uume umetengenezwa na misuli inayozunguka mrija mwembamba. Mrija huu hupitisha mkojo na shahawa. Uume una kichwa na mwili.mwili au mpini ni ile sehemu ya uume kama bomba. Kichwa ni ile sehemu ya juu ya uume. Ni sehemu ambayo ina hisia kali na inahitaji uangalifu mkubwa. Unapozaliwa kichwa cha uume kinakuwa kimefunikwa na ngozi nyembamba iliyojikunja. Ngozi hii inaitwa govi Jamii nyingi za Afrika huondoa govi kwa njia ya upasuaji. Kitendo hiki kinaitwa kutahiri. (Angalia ukurasa wa 20 kwa maelezo zaidi kuhusu kutahiri.) Ukubwa wa uume unatofautiana kati ya mwanaume na mwanaume na hauna uhusiano kabisa na ukubwa wa mwili. Mara nyingi, jinsi uume unavyokuwa mkubwa ukiwa laini ndivyo unavyoongezeka kidogo unapokuwa umedinda. Vivyo hivyo, kama ni mdogo unapokuwa laini unaweza kuongezeka zaidi unapokuwa umedinda. Panaito, kutoka Kenya. Nilipata mabadiliko ya sauti mara baada ya kupata ndoto nyevu. Vijana wengi wa kiume, hata wanaume wakubwa wanatumia muda mwingi kufikiri na kuwa na wasiwasi kuhusu uume wao. Je ni mdogo sana? Kwa nini umepinda kuelekea huku? Je, kuna tatizo lolote? Sehemu za siri za mwanaume kwa ndani Aloysious kutoka Uganda (Umri, miaka 19) Sauti yangu ilipobadilika nikiwa na umri wa miaka 15. Nilitambua kuwa nilikuwa ninakua. Nilikua haraka sana na nilifurahi. Dalili ya kwanza kuonyesha kwamba sauti yako inabadilika ni kuanza kukwaruza kwa sauti ghafla. Wavulana wengine hujisikia vibaya sauti zao zinapoanza kukwaruza, kwa vile mara nyingi haitabiliki itaanza lini. Sauti huwa ya kawaida na kubadilika katika muda mfupi. Mara inakuwa ya kawaida, dakika chache baadaye inakuwa ya juu na nyembamba. Aloysius kutoka Uganda (Umri, miaka 19) Wakati mwingine tulikuwa tunavuta uume na kulinganisha nani anao mkubwa zaidi?! Iwapo umewahi kujishangaa kama uume wako una ukubwa wa kutosha, kumbuka tu kwamba tendo la ngono halitegemei ukubwa wa uume. Kwa uhakika ni kwamba ukubwa wa uume hauna athari zozote kwa mwanamke katika kufurahia tendo la kujamiiana (ngono). Ukweli ni kwamba kufurahia ngono kwa wanawake na wanaume wengi kunategemea zaidi jinsi gani kila mmoja wapo anavyompenda mwenzie. Kilicho cha muhimu ni mahusiano na wala sio ukubwa wa uume. Kinachoning inia chini ya uume ni mapumbu. Pumbu ni kama mfuko au kifuko cha ngozi kinachoshikilia korodani au makende, ambako mbegu za kiume hutengenezwa tangu kipindi cha balehe hadi uzeeni. Ngozi ya mapumbu ina nywele kidogo na mafuta. Hudaka uchafu ambao kama haukusafishwa husababisha harufu mbaya. Katika kipindi cha utoto, mapumbu hujikunja na kuwa karibu na mwili. Lakini, kadri unapopitia balehe, mapumbu huanza kulegea na kuning inia chini, ingawa ukijisikia baridi au kuogopa au kuwa na hamu ya kujamiiana, mapumbu yako yanaweza kujikunja na kurudi karibu na mwili. Mapumbu yananing inia chini kwa sababu korodani zinahitaji kuwa katika hali yenye joto chini ya joto la mwili ili kutengeneza mbegu za kiume

17 SURA YA 3 wavulana JE UNAFAHAMU KUHUSU TOHARA? Tohara ni kitendo cha kuondoa ngozi iliyojikunja inayozunguka kichwa cha uume. Ngozi hii huitwa govi, hufunika kabisa kichwa cha uume lakini inaweza kuvutwa chini ya mpini (shafti). Kufuatana na mila na desturi za waafrika, pamoja na dini fulani fulani kama vile Waislamu na Wayahudi, watoto wanatahiriwa wakiwa na umri wa siku chache. Katika desturi nyingine za Afrika, wavulana wanatahiriwa wanapofikia balehe, utaratibu huu unachukuliwa kama utaratibu wa mpito kutoka utoto kwenda utu uzima.zipo tamaduni nyingine Afrika ambazo mila haziruhusu kutahiri kabisa. Hakuna ubaya wowote wa kutahiri au kutokutahiriwa. Kutahiriwa ni utaratibu wa kidini au kiutamaduni/kimila. Iwapo katika jamii yenu hawatahiri ni sawa sawa tu. Je, kutahiri kunaleta tofauti zozote katika hisia ya kujamiiana? Ni vigumu sana kujua jambo hili kwani kila mwanaume anayo namna yake ya kujisikia. Lililo la uhakika ni kwamba wote, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa wanaweza kufurahia ngono na wanaweza kuwafurahisha wapenzi wao. Wakati kutahiri ni utaratibu wa kidini au kimila/ kiutamaduni, watu wengine wanaamini kwamba kuna faida za kiafya iwapo mwanaume ametahiriwa kwa sababu ni rahisi kusafisha uume wake. Lakini zipo sababu zingine za kiafya zinazoweza kusababisha watu kutahiriwa. Wapo wavulana na wanaume wengine ambao govi linakuwa limeshikana sana na kichwa cha uume kiasi cha kwamba inawia vigumu kuivuta kwa chini. Hii inaweza kusababisha kuvimba kwa uume na maumivu makali. Namna pekee ya kutatua tatizo hili ni kutahiri.watu wengine wanafikiri kwamba kutahiri kunasaidia kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya ngono. Ukweli ni kwamba, hata kama umetahiriwa unaweza kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono. Unashauriwa kufanya mapenzi salama wakati wote. Mambo yote haya yana maana gani kwako? Kama utamaduni wako hauruhusu wavulana kutahiriwa, Je, ungependa utahiriwe ili iwe rahisi kuuweka uume wako msafi? Jibu ni hapana unachotakiwa ni kuwa msafi, kumbuka kusafisha kwa ungalifu chini ya govi. Kwa kawaida haya ndiyo unayotakiwa kuyafanya. Hata hivyo wavulana ambao hawawezi kuviringisha govi na wale ambao husikia maumivu uume unapodinda, wanashauriwa kumweleza mfanyakazi wa afya kwa ushauri zaidi. Sasa hivi watu wengi wanatahiriwa katika vituo vya afya. Lakini sehemu nyingine wanatahiri wataalamu wa kienyeji (mangariba) kama sehemu ya sherehe. Wakati wowote inapotokea hivyo, inatakiwa vitumike vyombo visafi, vilivyochemshwa, ili kuua vijidudu kila baada ya kumtahiri mtu mmoja. Ni hatari sana kutumia kisu kimoja kutahiria wavulana wengi kwa sababu kama mmojawapo atakuwa na maambuziki ya VVU, kisu kinaweza kueneza maambukizi kwa wavulana wengine. Iwapo utatahiriwa kimila, hakikisha utaratibu wa kisasa unatumika ili kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa mengine yanayotokana na damu. Usikubaliane kabisa na mila/desturi na utamaduni utakaosababisha maambukizi ya VVU. Taratibu hizo zinaweza kubadilishwa ukawa salama. Kwa mfano, watu wa Mbale, Uganda walichukua hatua zifuatazo ili kuhakikisha wanatahiri kiusalama: Kila aliyetaka kutahiriwa alilazimishwa kuja na kisu chake. Lazima kisu kichemshwa kabla ya kutumika. Lazima Mangariba waoshe mikono yao kwa uangalifu kabla na baada ya kumtahiri kila mtu. Je, ulikuwa unajua kwamba kuna uzushi mwingi kuhusu uume? Yafuatayo ni maelezo mbalimbali ya uzushi kuhusu uume: 1. Iwapo huufanyii mazoezi uume kwa kujamiiana, uume wako hautafanya kazi na utakuwa mdogo. Huu ni uongo! Kujamiana sio mazoezi ya uume. Uume hauhitaji mazoezi yoyote. Utafanya kazi vizuri bila hata ya kujamiiana.kutojamiiana au subira kamwe haviwezi kuudhuru uume wako. 2. Uume unaongezeka ukubwa kila unapofanya ngono mara nyingi. Sio kweli! Ukubwa wa uume wako utategemea sifa urizorithi kutoka kwa wazazi wako, na wala sio unachofanya na uume wako. 3. Uume mdogo hauwezi kumridhisha mwanamke. Sio kweli! Ukubwa wa uume unaathari ndogo sana kwa mwanamke kufurahia ngono. Hii ni kwa sababu hisia za kutaka kujamiiana kwa mwanamke zipo kwenye kinembe na eneo linalozunguka uke.uke wenyewe hauna mishipa mingi ya fahamu kwa hiyo haujisikii sana 4. Wavulana wenye uume mdogo hawawezi kutumia kondomu. Sio kweli! kondomu zimetengenezwa kwa jinsi ya kubana, hivyo kila mtu anaweza kuzitumia vema. 5. Lazima ujamiiane kila uume unapodinda. Si kweli! Kwa vyovyote vile hii sio kweli kabisa. Kwa mfano utafanya nini kama uume wako ungedinda darasani? Uume utalegea wenyewe. Kamwe huwezi kudhurika kwa kutokufanya ngono uume unapokuwa umedinda. 6. Wavulana wenye dole gumba kubwa wana uume mkubwa. Sio kweli! Watu wengi husema mambo kama haya ikiwa ni pamoja na wavulana wenye pua kubwa, miguu mikubwa, masikio n.k, lakini sio kweli. Hakuna mahusiano yoyote kati ya ukubwa wa uume na viungo vingine vyovyote vya mwili wako. Hakuna jinsi unavyoweza kufahamu ukubwa wa uume kwa kumwangalia tu. 7. Mbegu za kiume zikizidi zinasababisha mgongo kuuma, kichaa, kichwa kuuma, kuwa hanithi na kuota chunusi. Sio kweli! Hata kama korodani zinatengeneza mamilioni ya mbegu za kiume, haiwezekani mbegu hizo kujazana na kusababisha matatizo. Zaidi ya hapo mbegu za kiume haziwezi kwenda sehemu nyingine ya mwili. 8. Ndoto nyevu ni dalili ya kwamba unahitaji kujamiiana. Sio kweli! Ndoto nyevu ni njia mojawapo ya mwili kupunguza mbegu za kiume na shahawa. Sio dalili ya kwamba unahitaji kujamiiana. Mwili wako unaweza kujirekebisha wenyewe bila ya wewe kujihatarisha kwa vyovyote vile. MAZOEZI YA USAFI Ni muhimu kuosha na kusafisha uume wako kila siku, uwe umetahiri au la. Hii ni lazima iwe desturi kama unavyofanya kwa sehemu nyingine za mwili wako. Unatakiwa vile vile kuosha mapumbu, katikati ya mapumbu na mapaja na katikati ya matako. Kama hujatahiriwa, unatakiwa kurudisha nyuma govi na kusafisha eneo hilo kwa utaratibu. Unaweza kuhisi viuvimbe vidogo mwanzoni mwa kichwa cha uume viuvimbe hivyo ni matezi yanayotoa majimaji meupe yanayoitwa smegma. Smegma inasaidia govi kuteleza nyuma kiulaini. Hata hivyo, iwapo Smegma itajaa chini ya govi inaweza kusababisha harufu mbaya au maambukizi. Ni muhimu wakati wote eneo la chini ya govi liwe ni safi

18 SURA YA 3 wavulana KUMWAGA MANII KUKOJOA Unapofikia balehe unaweza kuanza kuona majimaji yenye rangi ya maziwa ambayo yananata na ni mazito, sio mepesi kama mkojo. Majimaji kama ute hutoka kupitia kwenye uume wakati mwanaume anapofikia mshindo. Kukojoa manii ni kilele cha msisimko wa kijinsia, wakati mwanaume anapokuwa amedindisha uume. Kumbuka ya kwamba sio lazima kukojoa manii kila uume unapokuwa umedinda. Kama utasubiri, uume utalegea wenyewe bila hata ya kukusababishia madhara yoyote. KUDINDA KWA UUME Iwapo hujatahiriwa rudisha nyuma govi na safisha taratibu chini yake. Kwa kawaida uume ni laini na huninginia chini. Wakati unadinda, damu nyingi huelekea kwenye uume isivyo kawaida na damu kidogo hurudi. Hii husababisha uume kuwa mkubwa na mgumu, na kusimama. Uume uliodinda kwa kawaida hujikunja kidogo kuelekea juu, na unaweza kujikunjia upande mmoja. Uume unapokuwa umedinda unaweza ukashindwa kukojoa kiurahisi kwa sababu msuli hufunga kibofu cha mkojo. Itakubidi usubiri uume ulegee ndipo ukojoe. Uume unaweza kudinda iwapo utaguswa au kushikwa shikwa, au wakati umepata mhemuko wa kutaka kujamiiana au kwa kumuona mtu anayekuvutia. Uume unaweza kudinda kwa sababu ya kuwa na wasiwasi na mfadhaiko. Ni kawaida kwa wavulana kuamka asubuhi na uume uliodinda. Ukiwa usingizini uume unaweza kudinda mara 5 mpaka 7. Hii ni kawaida kabisa na haina madhara yoyote. Kudinda kwa Uume kunawatokea wanaume wote wa umri mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wadogo na wazee. Wakati mwingine wavulana huhofu wanapodindisha mara kwa mara. Hali hii inawasumbua wakiwa darasani, ndani ya basi au hata wakati wa matembezi. Wakati mwingine zipo sababu za msingi za uume kudinda, kwa mfano, unaweza ukawa umekaa karibu na mtu anayekuvutia. Hata hivyo, kuna wakati uume unadinda bila sababu yoyote ya msingi. Nfune kutoka Zambia (Umri wa miaka 13) Kudindisha kwa uume hakuzuiliki na hutokea mara kwa mara. Wakati mwingine ni dalili ya kuonyesha una msisimko wa kutaka kujamiiana. Hali hii naichukia sana hasa ninapokuwa shuleni au hadharani. Tafadhali usiwe na wasiwasi, wewe ni wa kawaida, mwenye afya na homoni nyingi. Unaweza kufedheheka ikitokea darasani au hadharani, lakini wakati wote ni wewe peke yako unayefahamu kwamba umedindisha. Wakati mwingine wavulana wanadhani njia pekee ya kuthibiti uume kudinda ni kufanya ngono Hii sio kweli ni uzushi ikiwa ni sababu ya wavulana kufanya ngono. Uume kudinda sio dalili ya kwamba unahitaji kufanya ngono, la hasha. Majimaji kama ute yametengenezwa na vitu viwili. Karibia 10% ya majimaji ni mamilioni ya mbegu za kiume. Mbegu za kiume ni ndogo sana kiasi ambacho hatuwezi kuziona kwa macho labda kwa darubini. Ukiziona zinaonekana kuwa na kichwa cha mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Asilimia 90 ya ute huo ni majimaji yenye rangi ya maziwa yanayoitwa shahawa. Shahawa huwezesha mbegu za kiume kuogelea na pia huzipa chakula na kuziwezesha kuwa hai. Shahawa sio chakula kwa wasichana, kama watu wengine wanavyozusha. Mbegu za kiume zinatengenezwa katika Korodani/Makende (angalia kielelezo uk 19). Shahawa, ambazo ni majimaji yenye rangi nyeupe/maziwa zinatengenezwa kwenye vifuko vya shahawa. Hizi ni tezi zilizopo nyuma ya kibofu cha mkojo. Mwanaume anapofikia mshindo mbegu za kiume zinachanganyika na shahawa kutoka kifuko cha shahawa. Mchanganyiko huu huitwa manii. Manii hupitia kwenye mirija ya kupitishia mbegu na kutoka nje ya uume kupitia kwenye tundu dogo lililopo kwenye kichwa cha uume. Inaweza kuonekana kana kwamba manii nyingi hutoka wakati mwanaume anapokojoa Ukweli ni kwamba kiasi kinachotoka ni kama kijiko kidogo cha chai kilichojaa. Usije ukadharau uwezo wa hiki kijiko kidogo cha chai kilichojaa manii; kinaweza kuwa na mbegu za kiume karibia milioni mia tano!. Kila mojawapo ya mbegu hizo inaweza kumfanya msichana apate mimba. Unapofikiria mbegu za kiume zipatazo milioni mia tano, utaelewa ni kwa namna gani msichana anavyoweza kupata mimba kirahisi. Iwapo mvulana au mwanaume ana maambukizi ya VVU, kijiko cha chai kimoja kilichojaa shahawa kinaweza kuwa na mamia kwa maelfu ya virusi vinavyosababisha UKIMWI. Mbegu ya kiume Kijiko kidogo cha chai kilichoja shahawa kina mamilioni ya mbegu za kiume na kinaweza kuwa na VVU iwapo mvulana atakuwa ana maambujizi

19 SURA YA 3 wavulana Wavulana wengi wanakuwa na wasiwasi kwamba kondomu haiwezi kuhifadhi mbegu za kiume zipatazo milioni 500. Lakini mbegu za kiume ni ndogo sana na kwa hiyo kondomu inaweza kuzizuia zote ili mradi inavaliwa kwa usahihi (angalia sura ya 10 kwa maelezo zaidi kuhusu kondomu). Wavulana wengine wanakuwa na wasiwasi kwamba wakikojoa manii mara kwa mara watapunguza kiasi cha shahawa mwilini mwao. Wasiwasi wa kwamba wanaweza kuishiwa shahawa na hivyo kutokuwanazo za kutosha watakapozihitaji. Hili haliwezi kutokea hata mara moja kwani mwanaume anatengeneza mbegu za kiume na shahawa tangia kipindi cha balehe mpaka siku anayokufa. Vilevile kumbuka ya kwamba haiwezekani mbegu za kiume na shahawa zikalundikana au zikajenga shinikizo mwilini. Mwili wako ni kama mashine iliyokamilika, unazo njia za kuondoa mbegu za kiume na shahawa inayozidi, mojawapo ni ndoto nyevu. NDOTO NYEVU ( KUKOJOLEA KITANDANI) Wakati mwingine wavulana wanakojoa manii kitandani wakiwa usingizini.kitendo hiki kinaitwa ndoto nyevu wavulana wengi wanapopata ndoto nyevu huwa inakuwa ni mara yao ya kwanza shahawa kutoka mwilini mwao. Wanaweza kuamka na kukuta doa bichi kitandani au kwenye nguo. Adamu, kutoka Uganda (Umri, miaka 13) Sidhani kupata ndoto nyevu kunamaanisha ninatakiwa kujamiiana. Ni kukua tu. Ninaona aibu tu kwa vile inabidi nibadilishe mashuka kila baada ya siku moja. Wavulana wengine wanapoanza kupata ndoto nyevu wanaona ni tukio kubwa sana ambalo wanalifurahia. Panaito kutoka Kenya Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilijisikia kama nimekomaa kijinsi. Nilifurahi kuwa mmojawapo wa wale ambao tayari walishapata. Lakini ningelikuwa sijapata taarifa, ningeweza hata kwenda kumuona daktari,ninamshukuru Mungu kwamba nilijua kilichokuwa kinatokea. Adamu kutoka Uganda (Umri, miaka 13) Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilimwambia kaka yangu mkubwa ambaye alinihakikishia kwamba ilikuwa ni sehemu ya ukuaji. Wavulana wengine hawawi na furaha sana wanapoanza kupata ndoto nyevu. Hili ni jambo la kawaida vilevile. Kama hufahamu lolote kuhusu ndoto nyevu unaweza kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi. Unaweza kufikiri umekojoa kitandani au damu inakutoka au unaumwa, lakini utaona kwamba majimaji yana rangi ya maziwa/meupe, na sio kama damu au mkojo. Ndoto Nyevu kwa mara ya Kwanza Ndoto nyevu hutokea usingizini tu. Ukisinzia kidogo mchana unaweza kupata ndoto nyevu, lakini wavulana wengi hupata ndoto nyevu usiku wakiwa usingizini. Wavulana wengi wanapojikuta wamekojoa manii huwa wanakumbuka kwamba walikuwa wanaota ndoto zinazohusiana na mapenzi. Lakini unaweza kupata ndoto nyevu hata kama hujaota ndoto za mapenzi. Karibu wavulana wengi wanafedheheka wakipata ndoto nyevu. Ni sahihi kufedheheka, lakini kumbuka ya kwamba ndoto nyevu ni za kawaida wakati wa ujana balehe. Vijana balehe wengi wanapata ndoto nyevu ingawa sio wote. Mvulana hawezi kujizuia kupata ndoto nyevu; ni za asili na ni za kawaida. Ni njia ambayo mwili unatoa nafasi kwa ajili ya mbegu za kiume mpya kutoka kwenye korodani. Kupata ndoto nyevu haimaanishi uanze kujamiiana. Nfune kutoka Zambia (Umri wa miaka 13. Ninaona kama zinanichukiza Wavulana wengine wanao marafiki wasio na huruma, ambao huwatania kuhusu kupata ndoto nyevu. Ni makosa kumtania au kumcheka mtu kwa vile amepata ndoto nyevu. Ndoto nyevu ni jambo la kawaida. Bernard kutoka Kenya (Umri wa miaka 17) Nilipokuwa darasa la 8, sikutegemea kama ningeanza kukojoa manii mapema kiasi hicho. Nilimwambia rafiki yangu siri, badala ya kunieleza kwa nini yametokea, alinicheka. Nilijisikia kufedheheka. Sikutaka mtu yoyote afahamu, lakini aliwaeleza watu wengine, na wengine wakasema nilikuwa ninapiga punyeto. Nilimfuata rafiki yangu mwingine ambaye alikuwa mkubwa kwangu ambaye alinieleza kwamba ndoto nyevu ni kawaida. Unatakiwa usiwe na wasiwasi kuhusu ndoto nyevu kwa vile ni jambo la kawaida halina kasoro. Unavyoendelea kuujua mwili wako ndivyo utakavyokuwa na raha na mabadiliko unavyokuwa unayapitia. Kwa kuongezea, ukiwa na taarifa iliyokamilika utaweza kuwasaidia wavulana wadogo kuelewa kitu gani kinawatokea wanapopitia ujana balehe. Yapo maelezo na mafunzo mengi mazuri ndani ya kitabu hiki,kwa hiyo usiachie kukisoma kitabu hiki kwa undani

20 Sura ya 3 WAVULANA Katika kipindi cha balehe mvulana anategemea mabadiliko mengi kutokea. Mabadiliko haya ni ya taratibu na hutokea katika umri tofauti kwa wavulana tofauti. Yafuatayo ni mabadiliko ambayo unaweza kuyategemea: Mwili wako utakua, hasa mifupa ya mabegani, mikono, miguu na nyayo. Vilevile misuli itajengeka na utakuwa na nguvu. Sauti itabadilika halafu itakuwa nzito kadri vinyuzi sauti vinavyokuwa vinene na kurefuka. Uume wako utaongezeka na mapumbu yataanza kuninginia chini. Uume wako utadinda mara kwa mara. Unaweza kupata ndoto nyevu (kukojoa manii usingizini) usiku. Unapopitia mabadiliko haya elewa kwamba: Kila ukubwa wa uume ni sahihi. Hakuna ubaya wowote kutahiriwa na wala hakuna ubaya wowote kutokutahiriwa kwa mwanaume. Oga na kusafisha uume wako kila siku. Kila mara rudisha nyuma govi na kusafisha chini yake iwapo hujatahiriwa. Sio lazima kujamiiana eti kwa vile uume umedinda. Ndoto nyevu ni tukio la kawaida, huwapata wengi, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, sio dalili ya kwamba unatakiwa kuanza kujamiiana. Wakati wowote mabadiliko haya yanapotokea mwilini mwako ndio wakati mwafaka. Wewe ni wa kipekee na uko kawaida kabisa. Wasichana Sura ya pili ilielezea kidogo kuhusu mabadiliko ya msichana wakati wa balehe. Sura hii inatoa maelezo ya kina na naamini utayafurahia kuyasoma. MAUMBILE NA UKUBWA WA MWILI Wasichana wengi huanza kukua haraka haraka wanapokaribia umri wa miaka 10 hadi 11. Lakini wapo wasichana wanaoanza kukua wakiwa chini ya umri huu au umri mkubwa zaidi ya huu. Miguu mara nyingi huwa ndiyo sehemu ya mwili inayokua haraka. Unaweza kuwa mfupi, lakini ukajikuta miguu yako ghafla imekuwa mikubwa sana! Usijali sehemu nyingine ya mwili itakua na kulingana na hiyo miguu mikubwa. Mwili wako unakua kwa wakati wake. Mifupa mingine itaanza kukua pia kila mmoja kwa wakati wake. Mikono na miguu yako inaweza kutangulia kukua haraka wakati sehemu ya uti wa mgongo ikiwa inakua taratibu zaidi. Mabadiliko mengine unayoweza kuyahisi ni kuanza kukua nyonga. Mifupa ya nyonga inakuwa mikubwa, na laini, tishu zenye mafuta hukua kwenye nyonga, mapaja na matako. Kadri nyonga inavyozidi kupanuka, kiuno kitaonekana chembamba ukilinganisha na sehemu zingine. Mwili utakuwa wa mviringo, ukionyesha umbo la kike. MATITI YAKO Catheryn, kutoka Ghana (Umri, miaka 15) Nilikuwa na miaka 10 nilipoanza kuhisi mabadiliko ya mwili wangu. Watu waliniambia bila mabadiliko hayo nisingeliweza kuwa mwanamke kwa hiyo nilifurahi. Nilikuwa naingia katika kundi la wanawake hivyo sikuwa na budi kujihadhari. Wasichana wengine wanaanza kuota matiti wakiwa na umri kati ya miaka 8 au 9, lakini wengine yanachelewa kuota. Kuota kwa matiti kunasababishwa na homoni inayoitwa estrojeni. Estrojeni inasababisha tishu ndani ya matiti kukua ili siku moja utakapokuwa na mtoto, uweze kutengeneza na kuhifadhi maziwa. Kabla matiti yako hayajaanza kukua, pengine chuchu zako zitakuwa kubwa na kusimama kuliko zilivyokuwa awali. Mabadiliko mengine unayoweza kuyaona ni duara jeusi na kubwa la ngozi litakalozunguka chuchu zao. SURA YA

21 SURA YA 4 wasichana Unaweza vilevile kuona vinundu vidogo vidogo kuzunguka duara hilo. Hivi vinundu ni tezi ambazo ni za kawaida. Mwanamke anapokuwa na mtoto, tezi hizi zinatoa kiini kinachosaidia kulinda chuchu wakati mtoto ananyonya. Margaret kutoka Tanzania (Umri, miaka 18) Matiti yangu yalipoanza kukua, nilijisikia vizuri japo kuwa wakati mwingine kulikuwa na maumivu kidogo Kadri chuchu na duara vinavyozidi kuwa vikubwa, matiti nayo yanakuwa makubwa na kujaa. Mabadiliko haya yanavyoanza kutokea, matiti yanaanza kuuma. Unaweza kujisikia maumivu ukiyabinya au ukiyagonga. Hii ni kawaida, na hakuna haja ya kuhofu. Matiti ni sehemu ya mwili ambayo ni nyepesi kuhisi kitu. Iwapo kutatokea kiamshi cha namna tofauti, kama kuguswa au hata ubaridi, chuchu zinakuwa ngumu na husimama. Kwa wasichana wengine, matiti yao hukua taratibu na kwa wengine hukua haraka. Kwa wastani, inachukua muda wa miaka 4 matiti kukua kabisa, lakini wasichana wengine matiti yao yanakua kabisa kabla ya miaka 4, wakati wasichana wengine matiti yanaweza kuchukua hadi miaka 6 kukua kiukamilifu. Hivyo iwapo matiti yako yanachukua muda mrefu kukua tulia tu, yatakua. Debora kutoka Uganda, (Umri, miaka 15) Matiti yangu yamekua hivi karibuni, lakini ninaogopa jinsi yanavyoongezeka haraka. Sijali kuwa na matiti, ila ninatumaini hayatakuwa makubwa sana. Mara ya kwanza nilikuwa ninashangaa kwa nini yamechelewa kuota, lakini sasa ukubwa wake unanitisha. Kuna matiti ya maumbo na ukubwa mbalimbali. Ukubwa na maumbile ya matiti yanatokana na tabia vinasaba ulivyorithi toka kwa wazazi wako. Ukubwa pia unategemea tishu zenye mafuta katika matiti. Hakuna unachoweza kufanya ili matiti yako yawe unavyotaka. Hakuna kiasi chochote cha mazoezi kinachoweza kuongeza ukubwa wa matiti yako. Mazoezi yanajenga misuli lakini matiti hayana misuli. Kumbuka tu kwamba matiti yote, makubwa au madogo yana kazi kubwa moja - kunyonyesha watoto. Matiti yana maana tofauti kutoka jamii moja hadi nyingine. Katika utamaduni mwingine wanawake wanaweza kuacha matiti wazi, wakati katika tamaduni zingine wanashangaa na sio heshima hata kidogo. Katika sehemu nyingi hata hivyo kuota matiti ni tukio kubwa katika maisha ya msichana. Ni ishara ya msichana kukua. Wasichana wengi huyapenda matiti yao. Prossy,kutoka Uganda (Umri,miaka 13) Ninayapenda matiti yangu. Nilikuwa nawahusudu dada zangu walivyokuwa na matiti. Nilikuwa nachukua soksi na kuzikunja halafu naweka ndani ya gauni nionekane kama nina matiti. Barlay kutoka Kenya (Umri, miaka 16) Nilikuwa ninawahusudu wasichana wanovaa nguo zinazobana mwili. Nilifurahi nilipopata matiti, hivyo na mimi niliweza kuvaa nguo zinazobana mwili. Cathy kutoka Uganda (Umri, miaka 17) Matiti yangu yalikua nikiwa darasa la kwanza.nilijiona kama msichana mkubwa kuliko wote darasani. Ilichukuwa muda kukubaliana na mabadiliko ya mwili wangu. Lakini nilikuwa napenda nyonga yangu illivyo ya mduara. Marafiki zangu walisema nyonga yangu inashawishi na hii ilinifanya nijivunie. Sherifan kutoka Ghana (Umri, miaka 15) Nilifurahi sana kwa sababu nilianza kuonekana kama mama yangu. Nilipokuwa sina matiti nilikuwa ninavaa sidiria ya mama yangu na kuweka soksi ndani yake nionekane nina matiti kama mama yangu. Baadhi ya wasichana wanajisikia vibaya matiti yao yanapoanza kukua.pia hii ni kawaida.hii ni kwa sababu marafiki zao wa rika moja hawajaota matiti bado. Irene kutoka Uganda (Umri, miaka 16) Wakati matiti yangu yalipoanza kukua, nilikuwa ninavaa flana zinazobana sana, flana za wadogo zangu. Nilitaka kujisawazisha mwili nionekane kama sina matiti. Pia unatakiwa ujue kwamba, matiti hayakui yote pamoja sawasawa. Titi moja linaweza likawa kubwa kidogo kuliko jingine. Ukweli ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye ana matiti yanayolingana ukubwa na si rahisi kuona tofauti hizi.maumbile ya chuchu vilevile yanatofautiana sana. Wanawake wengine chuchu zao zimegeukia ndani badala ya nje, wengine chuchu zimezama ndani ya mduara n.k. Kama matiti yako ni makubwa au madogo, ni sahihi yalivyo kwako. Angela kutoka Kenya (Umri, miaka 17) Nilikuwa nina wasiwasi mno na nilikuwa ninavaa sweta wakati wote matiti yangu yalipoanza kuonekana. Nilikuwa sijisikii vizuri kwani nilikuwa ninasoma shule ya mchanganyiko na sikujua wavulana wangesema nini. Wasichana wengine wanajipinda vibaya kwa kuinamisha vifua vyao kwa sababu ya kufedheheshwa na kukua kwa matiti yao. Jambo hili linasikitisha kwa sababu kila mtu anatakiwa kuupenda mwili wake, na kutojali watu wengine wanasema nini. Vyovyote vile matiti yako yalivyo,kama ni makubwa au madogo yaliyochongoka au ya mviringo ni mazuri jinsi yalivyo

22 SURA YA 4 wasichana Rita kutoka Uganda (Umri, miaka 16) Ninayapenda matiti yangu kwa sababu yananifanya nijisikie mwanamke haswa. Wasichana wakubwa ambao hawana matiti hutaniwa na kufananishwa na wanaume Si vema watu kuwatania wasichana kuhusu matiti yao. Huu si ustaarabu. Msichana ajaribu kadri awezavyo kuwadharau na kutojali matusi yao. UNAJUA KUWA KUNA IMANI POTOFU NYINGI KUHUSU MATITI? Watu husema mambo mengi potofu kuhusu matiti, yafuatayo ni baadhi yake: 1. Wasichana wenye matiti yaliyochongoka huvutia kingono. Hii Si Kweli. Kuvutia kingono ipo kwenye akili ya anayejiona hivyo na si kwenye mwili wake. 2. Kuweka jibini kwenye chuchu au kumfanya mdudu ang ate chuchu hufanya matiti yakue haraka. Hii si Kweli pia. Homoni ndizo zinazofanya matiti yakue. Hamna kitu chochote zaidi ya hicho kitakachobadilisha matiti. 3. Wasichana wenye ngozi iliyo nyeusi kuzunguka chuchu zao wamewahi kufanya ngono. Huu ni Uongo! Kama ilivyo rangi ya ngozi yako, rangi ya mduara wa chuchu inatokana na tabia vinasaba ulivyorithi kutoka kwa wazazi wako. 4. Matiti yanaweza kuwa makubwa kama wavulana watayashikashika. Si kweli! Ukubwa wa matiti unategemea tabia vinasaba ulizorithi kutoka kwa wazazi wako. 5. Wasichana wenye matiti yaliyolala wameshawahi kufanya ngono au wameshawahi kutoa mimba. Huu pia ni Uongo! Matiti hulala/huanguka kutokana na uzito na maumbile. Kama una matiti makubwa uwezekano wa kulala au kuanguka kwa sababu ya uzito ni mkubwa zaidi. 6. Kuvaa sidiria hufanya matiti kuanguka. Uongo! Sidiria hushikilia matiti na huzuia ngozi na tishu za matiti kutanuka na kupunguza kunyumbuka. 7. Wasichana wenye matiti makubwa watakuwa na maziwa mengi kwa ajili ya watoto wao. Uongo! Uzalishwaji wa maziwa hautokani na ukubwa wa matiti; hata matiti madogo huzalisha maziwa yanayomtosheleza mtoto. NAMNA YA KUTUNZA MATITI YAKO Matiti ni sehemu nyeti, kwa hiyo kuna vitu fulani ambavyo unatakiwa uvijue kuhusu utunzaji wake. Hata siku moja using oe nywele zinazozunguka chuchu, zinaweza kusababisha madhara. Ni kawaida kuwa na vinyweleo hivyo. Kuna baadhi ya wasichana wanatokwa majimaji kwenye chuchu zao: hiki ni kitu cha kawaida. Lakini kama majimaji hayo yana damu au rangi ya kahawia unatakiwa kumwona daktari maana inaweza kuwa ni uambukizo. Kutunza matiti ni pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna anayeyashika bila ridhaa yako. Mara nyingi wavulana na wanaume hugundua kwamba matiti ya wanawake yanavutia sana, lakini hata hivyo mtu hana ruhusa kuyashika labda upende mwenyewe. Matiti ya wanawake wengi ni rahisi sana kuhisi yanapoguswa.kuguswa kunaweza kuleta ashiki ya kusisimua, na hii inaweza kusababisha utende usilotegemea au uponzeke. SIDIRIA Si lazima kuvaa sidiria kama una matiti madogo au yaliyosimama imara. Lakini kama matiti yako ni makubwa, unaweza ukajisikia vizuri kama ukivaa sidiria ambayo inasaidia matiti yasitikisike au kurukaruka unapotembea, kukimbia, kucheza dansi au kucheza michezo. Wasichana wengine waliobalehe wanafedheheka na matiti yao, hivyo kuvaa sidiria kunawafanya kutokuwa na wasiwasi na pia hupunguza kufedheheka/kujishuku. Ili kupata kipimo sahihi, wanawake wengi wanajaribisha namba mbalimbali za sidiria kuona ni ipi itamtosha vizuri. Unashauriwa kufanya hivyo. Wanawake wengine huwa wanachukuwa vipimo ili waweze kupata saizi ya sidiria. Ili uweze kupata vipimo vyako, unahitaji kujua saizi ya kifua chako pamoja na saizi ya titi.pima kifua chako, chini kidogo ya matiti, ili upate saizi ya kifua. Kisha pima sehemu iliyojaa zaidi ya matiti ili kupata ukubwa wa titi, kama viko sawa unahitaji kikombe A. Kama kipimo cha matiti ni 2.5 Sm zaidi ya kifua unahitaji saizi ya titi B. Iwapo kipimo cha matiti ni 5 Sm zaidi ya kifua basi unahitaji saizi ya titi C. VIA VYA UZAZI/SEHEMU ZAKO ZA SIRI Uke ndilo tundu pekee lililo kubwa kuliko matundu yote matatu katika eneo la via vya uzazi. Mashimo mengine ni tundu la mkojo (mbele ya uke) na mkundu (nyuma ya uke). Uke una kina cha sm 7 na upana wa sm 3 4. Ngozi yake ni laini iliyokunjamana. Uke wa mwanamke mtu mzima ni imara sana; hutanuka sana na una misuli imara. Wakati wa kuzaa mtoto uke unatanuka sana kuliko ukubwa wake wa kawaida ili kuruhusu mtoto kutoka tumboni mwa mama yake. Lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka sana. Hii ni mojawapo ya sababu ya madhara yanayompata msichana aliyezaa angali mdogo. Uke wa msichana mdogo unaweza kuchanika au kupasuka wakati wa kuzaa. Hii husababisha matatizo makubwa sana. (Soma Sura ya 11). Katika kipindi cha balehe, kuta za uke zinaanza kutoa majimaji ukeni. Maji maji hayo ni mazito na yananata kuliko mate na yana kazi yake ambayo ni kuuweka uke safi, na kutengeneza mazingira mwafaka ambapo bakteria wazuri wanaozuia maambukizo ya magonjwa wanaweza kuishi. Wanawake wengi wanaanza kuona maji maji ukeni katika nyakati tofauti katika mzunguko wa mwezi na wakati wanapopata ashiki. Hii ni kawaida. Sehemu za siri za mwanamke kwa nje 30 31

23 SURA YA 4 wasichana Upo uzushi mwingi kuhusu uke: Je? Unajua ukweli kuhusu uke? 1. Uke ni sehemu chafu kuliko sehemu zote mwilini. Si kweli! Mdomo ndio sehemu chafu kuliko zote mwilini. Ukweli ni kuwa majimaji ya ukeni na damu ya hedhi ni safi. Lakini mara baada ya kutoka mwilini, bakteria wanaweza kuzaliana kwenye majimaji na damu na kufanya yatoe harufu mbaya. 2. Uke haujazibwa mwisho, ni tundu lisilo na mwisho. Si kweli pia! Uke umezibwa na mlango wa tumbo la uzazi. Kondomu au sodo (tampon) haziwezi kusafiri hadi ndani ya kizazi. 3. Ni tabia mbaya kushika uke. Si kweli! Uke ni kama sehemu nyingine yoyote ya mwili kuishika ni kama kushika sikio. Hata hivyo uke ni sehemu nyeti ya mwili, hivyo unatakiwa kujishika wakati uko peke yako. 4. Uke ni kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Si kweli! Uke ni sehemu ya mwili wa mwanamke. Ni yake pekee yake! Usimruhusu mtu yeyote kuushika bila ridhaa yako. Eneo linalozunguka mlango wa uke linaitwa vulva. Kwa kawaida mlango wa uke umefungwa, na unalindwa na mashavu ya nje na ya ndani. Mashavu haya yana mikunjo miwili ya ngozi. Kuna tezi ndogo ndogo katika mashavu, hivyo unaweza kujihisi unatoa jasho na unatoa majimaji meupe sehemu hizo. Mbele ya tundu la mkojo, ambapo midomo ya ndani inakutana, kuna kinembe au kisimi. Kinembe ni kinundu kidogo mfano wa kunde. Kinembe hiki kimejaa neva na ni sehemu ambayo ni nyepesi kupata hisia/ashiki katika sehemu za via vya uzazi. Kinahisia kali kikiguswa. Ndani kabisa, mwisho wa uke wako kuna mlango wa mfuko wa uzazi. Mlango wa kizazi unafunga mwisho wa uke. Upo uwazi mdogo tu kwenye mlango wa kizazi, na uwazi huu unaelekea kwenye mfuko wa uzazi. Uwazi ni mdogo kiasi kwamba damu za hedhi tu zinaweza kutoka na mbegu za kiume tu zinaweza kuogelea kwenda juu. Watu wengine huhofia kwamba wakati wa kujamiiana kondomu inaweza kutoka kwenye uume na kuingia kwenye tumbo la uzazi. Hii haiwezekani kwa sababu uwazi uliopo kwenye mlango wa mfuko wa uzazi ni mdogo sana. Mlango wa mfuko wa uzazi unafunguka tu wakati wa kuzaa mtoto ili mtoto aweze kutoka kupitia ukeni na kisha nje ya mwili. Ngozi ya mlango wa mfuko wa uzazi ni laini sana, hususani kwa wasichana wadogo na wanawake wadogo. Mlango wa mfuko wa uzazi unaweza kuharibika au kuambukizwa bakteria na virusi ambavyo vinaweza kuingia mwilini wakati wa kujamiiana. Hii inaweza ikasababisha saratani ya mlango wa mfuko wa uzazi. Wasichana wanaoanza kujamiiana mapema au walio na wapenzi wengi wa kufanya nao ngono, au walio na VVU, wako kwenye hatari ya kupata saratani ya mlango wa mfuko wa uzazi kuliko wale ambao ni waangalifu katika kufanya ngono. Kutoanza kujamiiana mapema na kutumia kondomu kunaweza kukulinda usipate saratani ya mlango wa mfuko wa uzazi, (soma sura ya 10 zaidi kuhusu afya ya uzazi). KUFANYA USAFI WA MWILI VIZURI Uke na mkundu vinapaswa kuoshwa mara kwa mara na kubakia vikavu. Ni jambo zuri kuepuka kuchangia mataulo na ndugu wengine katika familia au marafiki kwani yanaweza kusababisha kuenea kwa maambukizi ya magonjwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Baada ya kuoga vaa chupi za pamba zilizo safi. Katika kipindi cha joto, epuka kuvaa chupi za nailoni kwa sababu huwa zinahifadhi unyevunyevu na joto, hali ambayo husababisha kuota bakteria. Kama huwezi kupata chupi za pamba, vaa zilizozungushiwa kitambaa cha pamba. Baada ya kukojoa au kwenda haja kubwa, unapaswa kujisafisha mwenyewe kwa kusafisha kuanzia mbele ya sehemu zako za siri mpaka kwenye mkundu. Kama ukitumia karatasi la chooni, karatasi, maji, majani au matawi ya miti kujisafisha, epuka kujisafisha kutoka nyuma kwenda mbele. Ukijisafisha kutoka nyuma kwenda mbele, kuna hatari ya kuvuta vijidudu vya maradhi kutoka kwenye mkundu kwenda kwenye uke na kwenye njia ya mkojo. Hii inaweza kukupa maambukizi ya magonjwa. Kamwe usijaribu kuosha ndani ya uke labda tu kama umeshauriwa na daktari. Kwa bahati mbaya wasichana na wanawake wengine wanaosha ndani ya uke kwa kutumia sabuni kali. Wanawake wengine wanapenda kupaka odorono au kupuliza manukato. Haya yote hayana umuhimu, na yanaweza kukuletea madhara kwa sababu sabuni, na manukato vikitumiwa ukeni vinaweza kubadilisha mfumo wa kawaida wa majimaji ndani ya uke na kusababisha ngozi ndani ya uke kuwasha. Katika nchi nyingine, kama vile, Zimbambwe na Zambia, wanawake huweka mitishamba, vipande vya nguo, na vitu vingine ndani ya uke ili kusafisha au kuufanya ubane. Kiafya, hii sio njia nzuri kwa sababu ngozi ndani ya uke ni laini mno. Unapoingiza vitu vigeni, vinaweza kusababisha majeraha madogo madogo au michumbuko na uvimbe mambo ambayo yanaweza kukufanya kuwa na maambukizi na uwezekano wa kukuweka kwenye hatari ya kupata VVU. Kwa ujumla, ni vizuri kutokuweka kitu chochote ndani ya uke wako, isipokuwa pamba za damu na dawa kama umeandikiwa na dakitari. Hakikisha tu unafuata maelekezo kwa makini. Ni vizuri kuchunguza kwa makini majimaji yanayotoka ukeni wakati wa mzunguko wa kila mwezi ili kuweza kuona dalili na mabadiliko yasiyo ya kawaida. Ukiwa makini, utagundua kwamba majimaji yanayotoka ukeni sio sawa wakati wote. Wakati mwingine yanaweza kuwa meupe wakati mwingine yanaweza kuwa meupe kidogo kama ute mweupe wa yai. Wakati wa uovishaji, majimaji ya ukeni yanaweza kuwa na utelezi zaidi na angavu. Vilevile majimaji ya ukeni yanaweza kubadilika iwapo mwanamke atashikwa ashiki. Iwapo majimaji ya ukeni yatakuwa mazito na kubadilika rangi kuwa njano, kijani au kahawia au yanasababisha muwasho sehemu za siri, unaweza kuwa umeambukizwa maradhi. Harufu mbaya ya majimaji toka ukeni, maumivu ndani ya uke na damu kutoka wakati hauko katika siku zako za hedhi ni dalili pia za maambukizi ya ugonjwa. Iwapo utapata mabadiliko yoyote kati ya haya, itabidi umwone daktari. Iwapo hushiriki ngono isiyo salama, na kama unazingatia usafi, huwezi kupata matatizo haya. Ukiutunza vizuri uke wako utajikamilisha kulingana na mazingira. Unachotakiwa kufanya ni kuosha kwa uangalifu eneo la via vya uzazi kila siku na maji safi au osha kwa sabuni ya kuogea. Tenganisha mashavu ya nje ili kusafisha uchafu unaojikusanya sehemu hizo

24 SURA YA 4 wasichana UNAJUA KUHUSU UKEKETAJI WA WANAWAKE? Katika mila nyingine, kisimi/kinembe na/au sehemu zingine za via vya uzazi vya mwanamke zinakatwa au kuondolewa kabisa. Utaratibu huu unaitwa kutahiri wanawake au ukeketaji wa wanawake. Ukeketaji huu unatofautiana katika nchi mbalimbali. Wengine hukata kuzunguka kisimi, na wengine hukata kisimi na mashavu (ya ndani na nje). Kukata kisimi na mashavu na kushona/kupunguza ukubwa wa uke kunaitwa mfyato, na huu ndiyo ukatili wa kiwango cha juu kabisa. Ni wakati gani unafanyika? Umri ambao wanawake wanakeketwa unatofautiana nchi moja hadi nyingine. Unafanyika wakati wa uchanga, utoto, ujana balehe, wakati wa kuolewa au wakati mwanamke ana mimba ya kwanza. Kwa nini unafanyika? Baadhi ya tamaduni, mila,desturi na imani zinaunga mkono wanawake kukeketwa, lakini Biblia na Korani haviungi mkono jambo hili. Katika jamii zingine wanaamini kwamba kukeketa kutalinda ubikira wa wasichana na kuwafanya wanawake wasiwe wahuni (Malaya). Pia watu wengine wanaamini kwamba kukeketa kunaongeza raha ya kujamiiana kwa waume zao, na kitendo hiki kinaaminika kuongeza uwezekano wa wanawake kuolewa na kuimarisha uwezo wa kuzaa. Unafanyikaje? Kwa kawaida wanaofanya kazi hii ni watu wazima/wazee au wakunga wa jadi wanaotumia visu maalumu, mikasi, vipande vya kioo, nyembe na vifaa vingine ambavyo si visafi kukeketea. Mara kwa mara ukeketaji unafanyikia katika mazingira machafu na mwanga hafifu. Kwa kawaida,hazitolewi dawa za kutuliza maumivu, wala za usingizi,wala dawa za kuzuia maambukizi! Madhara yake ni nini? Kukeketa wanawake kunaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya na kisaikolojia (kihisia): Kutoka damu nyingi. Kukata sehemu za via vya uzazi kunaweza kusababisha kutoka damu nyingi. Hii inaweza kusababisha kifo au upungufu mkubwa wa damu. Maambukizi ya magonjwa. Mambukizi ya magonjwa yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vifaa vichafu na pia yanaweza kutokea kwa kutumia dawa za kienyeji za kuponyesha vidonda. Maambukizi yanaweza yakaenea hadi kwenye tumbo la uzazi, mirija ya kupitishia mayai, na kwenye mayai ya uzazi na kusababisha maumivu ya mara kwa mara hata ugumba. Mambukizi ya magonjwa yanaweza kusababisha kifo. Mshituko: Mshituko kupita kiasi au kupoteza fahamu kunaweza kutokea kwa sababu ya kutoka damu nyingi na maumivu makali. Kubana mkojo: Baada ya kukeketwa wanawake wanaweza kubana mkojo kwa masaa au siku kwa sababu ya maumivu au kwa kuogopa kupitisha mkojo kwenye vidonda. Hata baada ya vidonda kupona mwanamke aliyeshonwa uke, tundu linaweza likawa dogo mno kuweza kutoa mkojo. Matatizo wakati wa siku za hedhi: Kama mlango wa uke ni mdogo sana kiasi cha kutoruhusu damu ya hedhi kutoka vizuri, damu inaweza kukusanyika ndani ya uke na tumbo la uzazi. Hii inaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa, na tumbo la uzazi kuvimba kwa sababu ya damu ya hedhi. UNAJUA KUHUSU UKEKETAJI WA WANAWAKE? (Endelea) Maumivu wakati wa kujamiiana na matatizo wakati wa kujifungua.wasichana waliokeketwa wanaweza kupata maumivu wakati wa kujamiiana pia wanaweza kupata matatizo wakati wa kuzaa iwapo njia ya uke ni ndogo kupitisha mtoto (angalia sura II). Athari za kisaikologia na kijamii: Ukeketaji kwa mwanamke unaweza kuwa na athari za muda mrefu kimaisha na kiakili. Anaweza kupoteza imani kwa jamii,wazazi au hata walezi. Anaweza pia kuathiriwa na hisia za kutokamilika, hofu, mfadhahiko na kupoteza hamu ya kujamiiana. Kwasababu ya athari kubwa za kiafya zinazotokea na kwasababu ukeketaji sio hitaji la kiafya, ndio maana watu wengi sasa huita Ukataji wa via vya uzazi vya mwanamke. (FGM = Female Genital Mutilation). Tendo hili linachukuliwa kama ni uvunjaji wa haki za wanawake na wasichana juu ya afya zao kimwili na kiakili na haki za uhuru, usalama na ukamilifu wa mwili (ujumla na ukamilifu wa miili yao). Kama wewe mwenyewe au unamfahamu msichana anayelazimishwa kukeketwa, peleka suala hili kwa utawala wa serikali wa mahali ulipo au mhudumu wa afya ili waweze kuongea na wazazi na ndugu zake juu ya athari mbaya zinazotokana na kitendo hicho. HEDHI NA MZUNGUKO WA HEDHI Wasichana wengi wanaanza kupata damu ya hedhi au kuingia mwezini kati ya umri wa miaka 10 na 16. Kuvunja ungo (mwanzo wa hedhi) ni dalili ya kwamba mabadiliko makubwa yanatokea ndani ya mwili wa mwanamke. Vilevile ni dalili ya kwamba anaweza akapata mimba akifanya ngono na mwanaume. Katika kipindi cha balehe, homoni husababisha ovari ambavyo ni viungo viwili vyenye umbile la yai kukomaa na kuanza kutoa yai kila mwezi. Kila mwanamke anazaliwa na mayai ambayo ni madogo mno kiasi kwamba hawezi kuyaona bila darubini. Mrija wa falopio Tumbo la uzazi Kadri ovari zinavyozidi kukomaa, mfuko wa uzazi pia unakua, ngozi laini inaanza kutengenezwa Uke kuzungukamfuko wa uzazi. Hivi ndivyo mfuko wa uzazi unavyofanya matayarisho ya kupokea yai lililorutubishwa.kama hakuna yai lililorutubishwa, ngozi laini inayozungukamfuko wa uzazi inakatika na kutoka kupitia mlango wa mfuko wa uzazi, kupitia kwenye uke na kutoka nje. Hii ndio damu ya hedhi au Sehemu za siri za mwanamke kwa ndani kuingia mwezini. Kwa vile ngozi laini ya mfuko wa uzazi imetengenezwakwa mishipa ya damu, inaitwa damu ya hedhi. Wasichana ambao wameanza kupata hedhi (kwenda mwezini) wanao mzunguko wa mwezi. Katika miaka michache ya mwanzo wasichana wengi mzunguko wao hauna mpangilio unaoeleweka. Ovari Seviksi 34 35

25 SURA YA 4 wasichana Hawajui ni lini wataingia mwezini tena. Inakuwa hakuna mfumo maalum, na mara nyingine wanaweza kukaa miezi kadhaa bila kupata damu ya hedhi kabisa. Hii ni kawaida, baada ya miaka michache mzunguko wa hedhi unakuwa wa kawaida. Wanawake wengine pia hawapati hedhi zao kulingana na mzunguko wa kawaida wa kila mwezi, jambo hili ni la kawaida pia. Hata kama mzunguko ni wa kawaida, muda wa mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa wanawake/wasichana. Kwa wengine mzunguko ni mfupi, siku 21 (hata chini ya hapo). Wengine mzunguko ni mrefu, siku 35. Wastani wa mzunguko ni siku 28. Tuangalie mzunguko wa hedhi wa mwanamke wa wastani ambao ni siku 28. Siku inapoanza kutoka damu, hesabu kuwa ndiyo siku ya kwanza. Katika siku 5 hadi 7 zinazofuata ukuta wa mfuko wa uzazi unajiachia na damu inatoka kupitia ukeni. Wakati huo huo mwili unakuwa umeshahisi kwamba hakutakuwa na mimba mwezi huo, na mwili utajua kwamba unahitaji tena kutayarisha yai jingine.yai jingine litaanza kuchomoka kutoka kwenye Ovari. Mara, baada ya hapo tumbo litaanza tena kutengeneza ngozi laini nyingine kuzunguka mfuko wa uzazi. Katikati ya mzunguko kama siku 14 au wiki 2 hivi tangu damu ianze kutoka ovari inaachia yai ambalo huanza kubingirika kuelekea kwenye mirija ya falopia. Hiki ni kipindi cha urutubisho.hiki kipindi ambacho uwezekano wa mwanamke kupata mimba ni mkubwa. Yai linakaa siku chache kwenye mirija ya falopia, na kama litakutana na mbegu za kiume linaweza kurutubishwa na mwanamke atapata mimba. (Angalia sura ya 11 taarifa zaidi kuhusu mimba). Kama yai halijarutubishwa linaingia ndani ya mfuko wa uzazi, kupitia mlango wa mfuko wa uzazi na uke, na kutoka nje ya mwili. Hii itakuwa inakaribia siku ya 20. Karibu wiki mbili hivi baadaye, mwili unapotambua kwamba yai halikurutubishwa, ngozi laini ya ukuta wa mfuko wa uzazi inabomoka tena kama damu ya hedhi na mzungo unajirudia tena. Hivi ndivyo mzunguko wa hedhi unavyokuwa. Wanawake walio wengi wanadhani kwamba kipindi cha uzazi nikatikati kabisa ya mzunguko, lakini hii ni kweli kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 28 tu. Kwa upande wa wanawake wenye mzunguko mfupiau mrefu, haiwezekani kuwa katikati ya mzunguko. Hii ni kwa sababu uovishaji (kutoka kwa yai) kunatokea karibu siku 14 kabla ya hedhi nyingine kuanza. Hivyo basi inamaanisha kwamba mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21 pengine anaovusha siku ya 7, ambapo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35 pengine anaovusha siku ya 21. Ukuta wa tumbo la uzazi uliotayari kupokea yai Hedhi:Kubomoka kwa ukuta wa tumbo la uzazi Mzunguko wa hedhi hautulii katika kipindi cha balehe.unaweza kuathiriwa na mfadhaiko wa mawazo, huzuni, kusafiri na mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Kwa hiyo ni vigumu sana kujua kipindi cha uzazi kitakuwa lini. Wasichana wengi wanapata mimba kwa makosa kwa sababu wanajamiiana siku ambazo wanafikiri ni salama, siku ambazo wanafikiri uwezekano wa kupata mimba ni mdogo. Wasichana na wavulana wengi wamewahi kusikia kuhusu siku salama lakini hakuna siku salama kwa wasichana balehe. Hii ni kwa sababu mzunguko wa hedhi hubadilika sana wakati wa ujana balehe. Kama mzunguko wako ni wa kawaida, unaweza ukabadilika ghafla na ukawa sio wa kawaida. Zaidi ya hapo, hakuna siku salama dhidi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono.unaweza kuambukizwa magonjwa ya ngono siku yeyote ya mwezi. Kusubiri siku salama sio njia nzuri ya kuzuia mimba au kuzuia magonjwa ya ngono. Kama ni kijana balehe uliyeanza kujamiiana usitegemee sana siku salama kama kinga. Kuna njia nzuri za kujikinga (soma sura ya 10 na 11 kwa taarifa zaidi kuhusu ngono salama na uzuiaji mimba). KUVUNJA UNGO Hakuna SIKU SALAMA kwa vijana balehe Kupata damu ya hedhi kwa mara ya kwanza ni tukio kubwa sana katika maisha ya msichana. Wasichana wengi wanakumbuka siku waliyovunja ungo. Ruvimbo, kutoka Zimbambwe (Umri, miaka 13) Nakumbuka ilikuwa mwezi Juni tarehe 10 nilipoamka na kukuta nguo zangu zina damu. Nilimwambia mama. Mama alinipa pamba na akanielekeza namna ya kuitumia. Aliniambia pia kwamba kama sina pamba ninaweza kutumia nguo za zamani. Kupata hedhi maana yake ni kwamba mwili unakua na unafanya kazi katika njia mpya. Vilevile kupata hedhi inamaana ya kwamba unaweza kupata mimba endapo utajamiiana. Lakini kupata hedhi haimaanishi mwili wako upo tayari kujamiiana au kupata mtoto, kwani uke bado ni mdogo na haujakomaa.uke hukomaa msichana anapofikia umri wa miaka 18 hadi 20. Isitoshe, nyonga na mifupa ya nyonga inaweza kuwa midogo sana kumuwezesha kuzaa kwa njia ya kawaida. Kupata hedhi ni dalili ya afya, lakini wasichana wengi wanashituka na kusikitika wanapovunja ungo mara nyingi ni kwa sababu hawakujua kilikuwa ni kitu gani na walidhani kuna kosa limefanyika

26 SURA YA 4 wasichana Diana kutoka Zambia (Umri; miaka 17) Nilishituka nilipopata hedhi kwa sababu sikujua. Lakini mama yangu akanieleza kwa nini ilinipasa kupitia hatua kama hiyo Sherifan kutoka Ghana (Umri; miaka 15) Sikujua kilikuwa ni kitu gani. Nilifadhaika na kuona aibu kwa wazazi wangu na marafiki zangu. Nilisali na kumuomba Mungu aniepushe na mambo hayo. Baadaye nilitambua kwamba ni sehemu ya maisha. Stabisile kutoka Zimbambwe (Umri; miaka 19) Sikuwa na uhakika kilichokuwa kinaendelea. Sikuwa na ufahamu wa namna ya kulikabili suala hili. Kupata hedhi kulinifanya nikose raha. Wasichana wanaojua hedhi ni kitu gani na wale ambao mama zao na dada zao wakubwa wanazungumza nao kuhusu kupata hedhi, inakuwa rahisi kwao kuikubali hali hii. Sandra, kutoka Uganda (Umri; miaka 13) Bado sijaingia mwezini, lakini hata kama nitaingia, tayari ninajua hedhi ni kitu gani na kwa vipi unaweza kukabilana na hali hiyo Demitrida, kutoka Tanzania (Umri; miaka 13) Bado sijapata hedhi, nikipata nitamwambia mwalimu mlezi wangu. Pia nitamwambia mama ili anipatie pamba au kipande cha nguo. Utajua kama umeanza kuingia mwezini utakapoona damu kidogo inatoka kwenye uke. Damu haimwagiki kama maji yanavyotoka kwenye bomba. Inadondoka taratibu. Kawaida muda utakaogundua ubichi usio wa kawaida, chupi yako itakuwa imenyonya damu yote, na nguo zako nyinginezo zitakuwa salama. Lakini wakati mwingine kunakuwa na damu nyingi au inakuja ghafla. Au inaweza kukuchukuwa muda mrefu kujionyesha, kinatokea nini. Cathy mwenye umri wa miaka 17 kutoka Uganda alichafua chupi yake hadi kwenye nguo. Cathy, kutoka Uganda (Umri; miaka 17) Ilinitokea darasani nikiwa na wanafunzi wenzangu. Nilisimama na kwenda chooni. Nikagundua kuwa nimechafua nguo. Aah, lilikuwa tukio baya sana. Nilifedheheka sana. Marafiki zangu walinisaidia lakini ilibidi nikae nyumbani wiki nzima. Kama hii itatokea, tulia. Sio kosa lako hukujua kwamba jambo hili litakutokea! Kila mtu inamchukuwa muda kuelewa namna ya kushughulikia hedhi. Unaujua Ukweli kuhusu hedhi? Kila mtu anayo maswali mengi kuhusu hedhi. Yafuatayo ni baadhi ya maswali na majibu yake: 1. Nitapoteza damu kiasi gani kila mwezi? Katika kipindi chote cha kutoka damu ya hedhi cha mwezi, kiasi cha damu itakayotoka ni kama ml za ujazo 60 hadi 70. Ukipima ml 70. za ujazo wakati wa kipindi cha Sayansi. utaona kuwa siyo damu nyingi sana. Hata hivyo huo ni wastani tu, wanawake wengine hupoteza kidogo zaidi- kiasi cha vijiko vichache tu vya chai. Wengine wanapoteza kikombe kizima kilichojaa Kama nikiweka kumbukumbu kwenye kalenda yangu naweza nikajua siku gani ni salama kwangu, Siku ambazo siwezi kapata mimba? Hapana, huwezi. Wasichana balehe huwa hedhi yao sio ya kawaida hivyo hawawezi kujua siku salama ni zipi. Isitoshe, hakuna siku salama dhidi ya maambukizi ya VVU na magonjwa ya ngono. Unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa siku yoyote na usije ukafikiri siku salama ni njia salama ya kujikinga na maambukizi. 4. Ninaweza kuingia mwezini mara mbili katika mwezi mmoja? Angalia ukurasa wa 40 Susan alipata damu ya hedhi mara mbili mwezi Aprili. 5. Naweza nikajamiiana wakati niko mwezini? Hili sio jambo zuri, hasa kama ni ngono isiyosalama (bila Kondom). Kama una VVU vitakuwa kwenye damu yako hivyo mwenzi wako anaweza kuambukizwa kwa urahisi. Vilevile wewe uko hatarini iwapo utajamiiana wakati huu na mwanaume aliye na VVU au magonjwa ya ngono. Uko hatarini kuambukizwa kuliko wakati wowote ule katika mwezi. 6. Je, ngono inatibu maumivu ya mkakamao wa tumbo wakati wa hedhi? Hapana! Ngono haiwezi kutibu maumivu ya mkakamao wa tumbo wakati wa hedhi. Huu ni uzushi tu ambao vijana wengi wanaueneza. KUTUNZA KALENDA Kwa wasichana wengi, inawachukuwa muda kuzoea hedhi. Kujisikia vibaya kuhusu hedhi ni kawaida kabisa. Jaribu kukumbuka kwamba hedhi ni dalili ya utu uzima na afya nzuri. Pia unapaswa kujua kwamba hedhi haita dumu milele. Wanawake wengi wanaacha kupata hedhi wanapokuwa mwishoni mwa miaka 40 na miaka ya 50. Umri huu unaitwa wakati wa kukoma hedhi Wasichana wengi wanaona kuna umuhimu wa kutunzakumbukumbu za tarehe aliyoingia mwezini. Hata kama hedhi haina mpangilio uliotulia kuweka kumbukumbu husaidia kutoa mwanga ni lini msichana balehe ataingia mwezini ili aweze kujiandaa.unaweza kununua kalenda ndogo na kutia alama X siku unayoanza kutoka damu. Kwa kuhesabu siku kati ya X na X utagundua mzungukowako ni wa siku ngapi na pia kama hedhi yako ina mpangilio uliotulia au la. Weka mtiririko wa siku zako za hedhi kwa kutumia kalenda 38 39

27 SURA YA 4 wasichana Susan, mwenye umri wa miaka 19, ana mzunguko wa kawaida wa siku 28. Mwezi Aprili, alianza kutoka damu tarehe 1, hivyo hedhi nyingine ilikuwa tarehe 29 ya Aprili. Mwezi Mei alipata hedhi tarehe 27. Mwezi wa sita alipata hedhi tarehe 23. Mwezi wa saba aliingia mwezini tarehe 20 Mwezi wa nane aliingia mwezini tarehe 16. Umegundua kuwa hedhi inaanza siku tofauti kila mwezi japo mzunguko wake una mpangilio uliotulia. Kumbuka, utaratibu wa kuwa na kalenda ni mzuri. Hukusaidia kufanya mandalizi ya kuingia mwezini lakini sio njia nzuri ya kujua siku salama zitakuwa lini. Kama unapenda sana kufanya ngono tafuta njia bora ya kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/ UKIMWI. HEDHI INAVYOKOSESHA RAHA Wasichana wengi matiti huvimba na kuongezeka na yanakuwa laini sana kabla ya kuingia mwezini au wakati yai limerutubishwa.hali hii haifurahishi, ila ni ya kawaida.hali hii inasababishwa na homoni zinazosababisha tishu za matiti kuwa na majimaji zaidi kuliko ilivyo kawaida. Ukivaa sidiria inayokutosha vizuri itakufanya ujisikie vizuri, na vyakula vyenye chumvi kidogo vitakusaidia kupunguza kiasi cha maji kinachohifadhiwa na mwili. Hedhi inaweza kumwathiri mwanamke katika hali yake kitabia. Kabla ya hedhi kuanza kila mwezi, wasichana wengine hujisikia kulia au kuwa na huzuni. Mara nyingine wasichana wanakuwa na hasira kwa sababu ya kuvimba matiti yao au mwili kuvimba kidogo au kuvimba sana. Hali hii mara nyingine inajulikana kama mahangaiko kabla ya hedhi na ni matatizo ya kawaida. Jaribu kuyapuuza yasikusumbue sana. Wasichana wengine hujisikia maumivu kidogo ya tumbo au mkakamao wa tumbo wakati wa siku zao za hedhi. Huu mkakamao unatokea kwa sababu misuli ya tumbo la uzazi inabana wakati ngozi laini inayozunguka tumbo la uzazi inapojiachia na ukuta. Mkakamao huo ni wa kawaida na unaweza ukavumilika. Iwapo maumivu ni makali lala chini na jaribu kuupumzisha mwili kwa kuvuta hewa nyingi na taratibu. Vilevile unaweza kuliminyaminya tumbo lako. Njia nyingine ni kuweka chupa ya maji ya moto tumboni na itakusaidia kupata nafuu. Kama njia hii haikusaidii, tafuta dawa za tumbo za kutuliza maumivu kwenye maduka ya dawa au dukani. Mazoezi pia yanaweza kusaidia japo hili halitakuwa jambo la kwanza kulifikiria. Unaweza kujisikia kama kulala chini, lakini kufanya matembezi au kukimbia huwa kunawasaidia baadhi ya wasichana kushughulikia tatizo la mkakamao wa tumbo. Ukiweza kupata kisodo aina ya tampoon unaweza hata kwenda kuogelea. Kuwa katika hedhi kisiwe kikwazo cha kufanya shughuli zako za kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya mambo unayoyafurahia. Mkakamao wakati wa hedhi na maumivu mara nyingi ndio dalili za awali za balehe na unapofikisha umri wa miaka 18 au zaidi pengine mambo haya hayatakusumbua sana. Lakini wasichana wengine hupata maumivu yasiyo ya kawaida wakati wa siku zao. Hawa mara nyingi ni wasichana wenye hedhi nzito. Wasichana wenye hedhi nzito mara nyingi wanatumia pedi nyingi usiku na mchana na bado wanaacha alama ya damu kwenye mashuka au nguo. Mara nyingine wanakosa kwenda shule kwa sababu wanatoka damu nyingi au wana maumivu makali. Hebu fikiria kukosa kwenda shule kila mwezi na madhara utakayoyapata katika masomo yako! Kuna ufumbuzi wa kushughulikia hedhi kali, hivyo usiumie bure. Iwapo kweli una maumivu makali wakati wa siku zako au unatoka sana damu kama unakosa kwenda shule kwa sababu ya siku zako muone muhudumu wa afya. Wahudumu wengine wa afya wanaweza kupendekeza vidonge vya kuzuia mimba ili kupunguza hedhi nzito yenye maumivu makali. Vidonge vinafanya hedhi isibadilike badilike ovyo ovyo na vinasaidia kupunguza kiasi cha damu inayopotea kila mwezi. Iwapo unahitaji kuonana na mganga wako mwulize kuhusu vidonge vya kuzuia mimba. Unaweza kumeza vidonge hivi hata kama bado ungali hujaanza kufanya ngono. Vidonge vina dozi ndogo ya homoni ambayo kwa asili inapatikana mwilini. Ni salama kwa vijana wanao balehe. Kama Mganga hataki kukuandikia cheti cha dawa hizo jieleze,ukipenda mwuulize ufanye nini kupunguza udhia unaoupata kila mwezi. Usikose kwenda shule kwa sababu ya tatizo linaloweza kutatuliwa. Unaweza pia kumwona mhudumu wa afya unapoanza kutoka damu katikati ya mzunguko wa hedhi au kama siku zako za hedhi zinachukua zaidi ya siku 8. NGONO NA HEDHI Hakuna ukweli kabisa kuhusu uvumi kwamba ngono inatibu maumivu ya hedhi. Ukweli ni kwamba kufanya ngono wakati wa hedhi kunaweza kukuongezea uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya ngono ukiwemo UKIMWI. Damu ya hedhi ni mazingira mazuri kwa bakteria na virusi kukua haraka. Iwapo mwanamke aliye katika hedhi amefanya ngono na mwanaume mwenye magonjwa ya ngono, kuna uwezekano mkubwa kuambukizwa kuliko wakati mwingine wowote wa mzunguko wake; vilevile kuna uwezekano wa kupata maradhi mengine hatari wakati wa hedhi. Hii ni kwa sababu mlango wa tumbo la uzazi hufunguka kuliko kawaida ili damu ya hedhi iweze kupita. Vijidudu vya magonjwa ya ngono vinaweza kusafiri hadi kwenye tumbo la uzazi na kupitia mirija ya kupitishia mayai, hivyo kusababisha maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke,na hatimaye kusababisha ugumba. Kwa mwanaume, kufanya ngono na mwanamke aliye katika hedhi ni hatari vilevile. Kama ameambukizwa VVU, damu yake itakuwa na virusi vingi vya VVU. KUJISIKIA VIZURI, AFYA NA USAFI Katika tamaduni zingine, wanawake walio katika hedhi wanachukuliwa kama wachafu. Lakini ukweli damu ya hedhi ni safi. Baada ya damu ya hedhi kutoka mwilini bakteria wanaweza wakakua ndani yake, na kusababisha inuke, ndio maana usafi ni muhimu unapokuwa katika hali hii. Wakati wa hedhi, oga angalau mara moja ili uwe msafi. Usitumie manukato kwenye via vya uzazi yanaweza kukusababishia muwasho. Vidokezi vitakavyosaidia kuzifanya siku zako ziwe nyepesi na starehe: Wakati wote kuwa tayari, zijue siku zako za hedhi ili usije ukashitukizwa. Acha kutumia chumvi nyingi, chumvi inafanya mwili wako uwe na maji mengi, hasa wakati wa siku zako.hii inaweza kukufanya kujisikia mwili mzito kuvimba tumbo kutokuwa na raha na kuwa na mfadhaiko

28 SURA YA 4 wasichana Kunywa maji mengi au juisi ya mtunda. Kula kwa wingi vyakula vyenye chuma nyingi kama samaki, maini, maharagwe, nyama na mboga za majani. Vyakula hivi vitasaidia kurudishia madini ya chuma yaliyopotea kwa sababu ya damu iliyotoka. UTATUMIA NINI KUJIHIFADHI NA HEDHI? Kihistoria, wanawake na wasichana wakati wote wamepata hedhi na wameweza kuimudu hata kama kulikuwa hakuna vifaa vya kisasa kuweza kuvinunua madukani kama sasa. Hivyo hata kama huna fedha ya kununulia pedi na tampons, unaweza kushughulikia siku zako kama kawaida. Moja ya vitu vya kawaida na rahisi sana kutumia ni vipande vya nguo chakavu. Unaweza kuvichana kwa ukubwa wa kuenea kwenye eneo la chupi yako na kuvipanga vipande vya nguo chakavu kimoja juu ya kingine. Hakikisha ni visafi vioshe vizuri na vianike ili viweze kukauka. Vianike mahali pa siri lakini penye jua ili viweze kukauka. Jua ni dawa nzuri sana ya kuua vijidudu vya maradhi. Unahitaji pia kuzibadili mara kwa mara kwa sababu inaweza kukuletea maambukizi ya magonjwa ikiachwa muda mrefu kwenye uke. Usiache sodo ndani ya uke zaidi ya masaa 8. Usiitumie usiku kwa sababu unaweza kulala zaidi ya masaa manane. Chochote utakachotumia, vitambaa vikuukuu, karatasi za chooni, pedi au sodo vibadili mara kwa mara kuepuka kuacha damu kwenye nguo au harufu mbaya. Damu ya hedhi inapokutana na hewa, inaacha harufu mbaya iliyochacha.chupi zako au nguo zikipata madoa ziloweke kwenye maji baridi, yenye chumvi kidogo, maji ya moto yanaifanya damu igande na kubakiza doa la kudumu. Hedhi ni sehemu yako. Ukijiandaa ujio wake, utaona kwamba siyo jambo kubwa la usumbufu, unaweza kujishughulisha, ukacheza na kufurahi wakati wa siku zako, na hedhi isikukoseshe kwenda shule au kazini. Karatasi za chooni pia siyo aghali, unaweza kununua mabunda matano kwa bei ya bunda moja la pedi. Itakubidi utengeneze karatasi nene na refu la kutosha. Mara nyingine karatasi za chooni zinakwaruza na zinawezakukusababishia muwasho na uvimbe kwenye ngozi yako. Pedi nazo ni nzuri, zimetengenezwa kuweza kutosha vizurikatikati ya mwili na chupi. Zina vitu vya kuifanya ijishikizevizuri kwenye chupi na kukinga tundu la uke.pedi zinakaratasi la nailoni kuzuia damu kupenya.ukitumia pedi, unatakiwa kuzitupa ndani ya choo cha shimo au kuchoma moto baada ya matumizi. Usizitupe ndani ya choo chakuvuta maji kwani zitakwama na kuziba choo. Wanawake wengine wanatumia tampon/sodo ndogo ambayo ni pamba ngumu inayoingizwa ndani ya uke wakati wa hedhi.pamba hiyo hulainika huku ikiendeleakunyonya damu inayotoka kwenye tumbo la uzazi na kuingia ndani ya uke. Kuna uzi ambao umefungwa kwenyesodo ambao unaninginia nje ya uke. Vuta uzi huu kutoa tampon. Kitu kizuri kuhusu tampon ni kwamba haisumbui, hivyo unaweza ukasahau kabisa kuwa ipo. Lakini tampon zinahitaji uangalifu zaidi. Wakati wote osha mikono yako kabla ya kuiingiza. Kama utajiandaa mwenyewe,siku zako za hedhi hazitakuwa za kutatanisha kwako

29 Sura ya Nne Wasichana Wakati wa kubalehe, msichana ategemee mabadiliko mengi ya mwili. Yafuatayo ni baadhi tu ya mabadiliko yanayoweza kutokea: Mwili utaongezeka urefu; nyonga itapanuka, mifupa ya mikono, miguu itarefuka. Msichana atapata umbo la mviringo la kike. Matiti yatakua na chuchu itaongezeka ukubwa na kuwa na rangi nyeusi. Sehemu za siri zitakomaa na kuta za uke zitaanza kutoa majimaji. Damu ya hedhi itaanza kuonekana kila mwezi. Dalili hizi hutokea kwa muda muafaka ambao ni tofauti kwa kila msichana. Wakati mabadiliko haya yanatokea, kuna vitu vichache vya kuzingatia: Kwamba matiti yana ukubwa unaotofautiana kwa kila mwanamke. Matiti yote yanavutia hivyo yalivyo na ni muhimu kwa kunyonyesha watoto. Mabadiliko Ya Msingi Katika Kutunza Mwili Sura hii inazungumzia jinsi ya kutunza afya ya mwili wako kwa ujumla. Hili linaweza kuonekana kama sio muhimu ukilinganisha na mambo mengine yaliyomo katika kitabu hiki, lakini ni muhimu kujua jinsi ya kuishi na afya njema. Kwa kweli matatizo mengi ya afya yanaweza kuepukwa kama ukila vizuri, ukifanya mazoezi, ukiwa msafi na ukijisikia vizuri. Ni wajibu wako kuangalia mambo haya kila siku, na kuonekana na kujisikia vizuri iwezekanavyo. Mwili wako ndio utakaokuwa nao katika kipindi chote cha uhai wako. Kwa hiyo unatakiwa kuutunza kweli kweli! SURA YA 5 Safisha sehemu za siri- ila sio ndani ya uke- kila siku. Vaa chupi zilizotengenezwa kwa kitambaa cha pamba. Ni muhimu kuifahamu harufu na hali ya kawaida ya majimaji ya uke ili inapotokea mabadiliko ujue kuwa ni dalili za maambukizi. Siku za hedhi kwa msichana anayebalehe hubadilika badilika hivyo hakuna siku salama za kutopata mimba wala hakuna siku salama ambazo hutaambukizwa VVU au magonjwa mengine ya ngono. Ingawa wakati wa hedhi ni kawaida kuumwa tumbo, kuvimba au kujisikia vibaya, hali hii isifanye msichana akakosa raha. Mazoezi na vyakula vyenye chumvi kidogo husaidia kupunguza maumivu. Kama maumivu yanakuwa makali na damu nyingi sana inatoka, kamuone mhudumu wa afya. JIWEKE MSAFI, NUKIA VIZURI. Kila mtu anataka kuonekana msafi, lakini kujihisi kuwa na mvuto inaonekana ni muhimu hususani katika kipindi cha ujana balehe kwa sababu ya mabadiliko makubwa yanayotokea katika mwili. Sio tu mwili unabadilika umbo wakati wa balehe, lakini vilevile unaanza kutoa harufu mpya, majimaji mapya na hofu mpya hasa kwa vijana. Hivyo kujizoesha kuwa msafi inaweza kuwa ni njia nzuri ya kujisikia raha ili kukabiliana na mabadiliko haya yote yanayotokea. Oga angalau mara moja kwa siku ili kujisikia vizuri na safi. Sandra, kutoka Uganda (Umri ; miaka 13) Siku zote oga, fua na piga pasi nguo ili uonekane nadhifu. Usafi mzuri wa mwili hususani wakati wa balehe ni muhimu kwa sababu ngozi yako inaanza kutoa majimaji zaidi kuliko ilivyokuwa wakati ukiwa mtoto, na baadhi ya haya majimaji yanaweza kusababisha harufu mbaya kama huogi. Majimaji utakayoyaona zaidi ni ya jasho. Jasho linatokana na tezi zilizopo kwenye ngozi. Tezi za jasho zinakuwa hai zaidi wakati unapofikia balehe

30 SURA YA 5 Mabadiliko Ya Msingi Katika Kutunza Mwili Kwa hiyo, vijana balehe hugundua kwamba wanatoka jasho jingi sana. Pia wanagundua kuwa jasho lao hutoa harufu na ladha yake ni tofauti kuliko jasho la maji ya kawaida analotoka mtoto ambaye amekimbia wakati wa jua. Kwapa zako zina tezi nyingi za jasho, lakini pia una tezi nyingi za jasho katika mikono yako, miguu, na hata katika via vya uzazi, hivyo utagundua kuwa unatoka jasho sana katika sehemu hizi. Harufu ya jasho lako itabadilika katika kipindi cha balehe, lakini mabadiliko haya ya harufu ya mwili ni ya kiasili na kiafya. Ni dalili ya kukua. Ingawa watu wengi wanahofia harufu ya jasho lao, hasa jasho linalotoka kwapani, kuoga mara moja au mbili kwa siku, na kuvaa nguo safi inatosha kukuweka nadhifu na safi. Kama unatoka jasho kwa wingi na linakusumbua, vaa chupi iliyotengenezwa kwa pamba na nguo zisizobana zilizotengenezwa kwa pamba.nguo za pamba zinauwezo wa kufyonza jasho kuliko nguo za mpira. Pia pamba huruhusu hewa kupita hivyo husaidia kuleta ubaridi.baadhi ya watu hununua odorono za kupaka au kupulizia marashi ili kuzuia harufu inayotoka kwapani.hivi vyote vinaweza kuwa aghali.kuoga na kuvaa nguo safi kunasaidia vema tu. Kama lilivyo jasho, majimaji mengine ni damu ya hedhi, majimaji ya ukeni, manii na utoko (vilainisho vyeupe chini govi) - kimsingi vitu hivi ni safi. Lakini punde tu majimaji haya yanapokuwa yametoka mwilini, bakteria wanaweza kuota ndani yake, na kusababisha harufu mbaya au wakati mwingine maambukizi.kwa hiyo, ni muhimu kusafisha maeneo ya via vya uzazi - eneo la uke na uume kila siku.wavulana ambao hawajatahiriwa wanahitaji kuvuta nyuma govi na kusafisha utoko (Angalia sura ya Tatu). Wasichana inawalazimu kusafisha katikati ya mashavu ya ndani na nje ya uke, lakini hawahitaji kusafisha ndani ya uke kwa sabuni kwa sababu uke hujisafisha na kujilinda wenyewe kwa kutoa uchafu. Usafi ni muhimu hususani wakati wa kipindi cha hedhi (angalia sura ya Nne). Kwa kusafishia via vya uzazi, sabuni ya kawaida ya kuogea ni nzuri kutumia. Hutakiwi kutumia sabuni zenye kemikali au zenye kuondoa harufu kwapani, kwenye via vya uzazi kwasababu zinaweza kusababishia mwasho. Kwa kuongezea, sabuni zenye nguvu za kemikali zinaweza kuuwa bakteria wazuri wanaoishi sehemu kama za uke ambao wanasaidia kulinda baadhi ya maambukizi. Baada ya kujisafisha unatakiwa kujikausha na kuvaa nguo safi. Kama una ngozi inayokauka paka mafuta ya mgando (vaselini) mafuta yeyote mengine au losheni katika viganja vyako, mikono na miguu itasaidia kulainisha ngozi.losheni inayopakwa mara baada ya kuoga inasaidia kuhifadhi unyevu unyevu katika ngozi yako. Osha mikono yako mara kwa mara. Kila mara nawa mikono yako baada ya kutoka chooni na kabla ya kula au wakati wa kuandaa chakula. Weka kucha zako safi kwa kuzikata na kuwa fupi. UTUNZAJI WA MENO YAKO Mdomoni mwako ni sehemu ambayo bacteria wanaishi pia. Kwa hiyo utunzaji wa meno ni muhimu ili kulinda afya. Bakteria wa mdomoni wanaweza kutoboa meno yako. Piga mswaki meno yako angalau mara mbili kwa siku,au baada ya mlo na kabla ya kulala. Hii inaweza kusaidia kuua bakteria ambao wanakula chakula kinachobaki mdomoni kati ya meno yako na kusababisha kuoza kwa meno au kupata ugonjwa wa fizi. Kuweka meno yako safi kunasaidia kuwa na uhakika wa kupumua hewa nzuri. Unatakiwa kusafisha kila jino - kote mbele na nyuma ya mdomo wako. Pia unatakiwa kusafisha katikati ya meno yako. Miswaki na dawa za meno ni nzuri, lakini kama huna dawa ya meno unaweza kusafisha kwa maji tu. Unaweza pia kusafisha meno yako kwa kutumia chumvi kidogo na maji, ili kulinda ufizi na maambukizi ya mdomoni. Unatakiwa kuepuka kula vyakula vyenye sukari na soda. Licha ya kwamba vinalishe kidogo, vina sababisha kuoza kwa meno. Ni muhimu kuepuka kuchangia miswaki kwa sababu inaweza kueneza maradhi. CHUNUSI Wakati wa balehe, tezi za mafuta katika mwili wako zinakuwa hai zaidi, na zinaanza kutoa vitu vyenye mafuta vinavyoitwa sebum. Unazo hizi tezi za mafuta katika mwili wako wote; zipo zaidi kwenye uso wako, shingoni, mabegani, kifuani na mgongoni. Sebum ni vitu vizuri kwa sababu vinasaidia kuufanya mwili wako uwe laini, nyororo na uonekane kijana. Japokuwa, wakati wa balehe, tezi zako za mafuta zinaweza kutoa sebum nyingi, na kuwepo sebum kwa wingi kunaweza kusababisha kuziba kwa vitundu vidogo vidogo vilivyopo katika ngozi yako. Hii inaweza kusababisha matatizo, kama chunusi. Kuwepo kwa mafuta katika ngozi yako, na kuwa na sebum za ziada zinazotolewa kipindi cha balehe, inaonyesha ni jinsi gani ambavyo unaweza kupata matatizo ya ngozi. Kuwa na chunusi ni kitu cha kawaida kwa hakika, angalau vijana 8 kati ya 10 wana chunusi wakati wa ujana balehe. Chunusi kwa kawaida zinatokea katika umri wa kati ya miaka 14 na 17, lakini hutokea vilevile kwa watu wazima, wavulana na wasichana. Baadhi ya vijana wana chunusi nyingi - tatizo linaloitwa acne. Chunusi zina kawaida ya kutokea kutegemeana na familia. Kama wazazi wako au kaka na dada zako walikuwa na chunusi, utakuwa katika nafasi ya kubwa ya kuzipata. Zinaweza kuendelea kuwa tatizo kwa baadhi ya watu hata baada ya ujana kupita. Presha za maisha zinaweza kusababisha chunusi. Vijana wengi wanajikuta wana chunusi nyingi hususani wakati wa matukio muhimu kama, mitihani, miadi au kitu chochote ambacho kitamsisimua. Baadhi ya wasichana wanakuwa na chunusi nyingi wanapokaribia kipindi cha kupata hedhi. Kuna porojo nyingi kuhusu chunusi, na watu wengine wanasema maneno ya uongo kama: chunusi ni dalili ya msichana au mvulana aliye ana hamu ya kufanya ngono. Sio kweli, ngono haitibu chunusi. Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha maumivu makali. Meno yaliyooza yanaweza kusababisha maambukizi ambayo yanaweza kudhuru sehemu nyingine za mwili wako

31 SURA YA 5 Mabadiliko Ya Msingi Katika Kutunza Mwili UTAFANYA NINI NA CHUNUSI Chunusi ni jambo la kawaida kwa vijana balehe. Kwa bahati mbaya, hakuna jinsi tunavyoweza kuzikwepa kabisa; wala hakuna matibabu ya ajabu ya kutibu chunusi. Hata hivyo, yapo mambo kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ili kushughulikia chunusi. Ni jambo muhimu sana kutunza ngozi yako, hususani kama unaishi sehemu zenye joto, vumbi na unyevu unyevu. Unaweza kutumia sabuni ya kuogea na maji ya uvuguvugu kuosha taratibu sehemu za mwili wako zenye mafuta usoni, shingoni, mabegani, mgongoni na juu ya kifua. Ukiosha sehemu hizi angalau mara moja kwa siku itasaidia kuondoa mafuta kwenye ngozi na kusababisha vinyweleo kuwa safi na wazi. Lakini usisugue sana ngozi yako au kutumia sabuni zenye nguvu na kali kwa sababu zinaweza kusumbua ngozi yako na kusababisha chunusi zaidi. Kamwe usitumie sabuni za kufulia, sabuni ya unga na dawa ya madoa, kwani zitaharibu ngozi yako. Jaribu kutoruhusu mafuta unayopaka kichwani yasifike usoni kwa sababu mafuta haya yanaweza kuzuia vinyweleo vya ngozi yako. Mwisho, kuwa mwangalifu na matumizi ya krimu za usoni na zile za kung arisha ngozi. Ingawa zimeandikwa kwamba ukizitumia ngozi yako itakuwa nyororo na nzuri, krimu zingine zinaharibu ngozi kabisa. Kwa nyongeza, dawa nyingi za kulainisha ngozi zina vitu ambavyo si vizuri kwa afya yako. Ingawa wakati mwingine unashawishika kuminya chunusi,sio vizuri. Kama utafanya hivyo, usaha unaweza kutawanya maambukizi kwenye vinyweleo vingine, na vilevile unaweza kupata makovu ya kudumu. Chunusi zinasumbua, zinaweza kusababisha maumivu na uchungu, na zinaweza kuleta usumbufu wakati mwingine. Lakini ni sehemu ya ujana balehe. Vijana wengi wanajihisi Hata kama unafikiria kwamba chunusi zako ni mbaya, watu wengine hawajaziona bado. kuwa ni wao pekee wenye kusumbuliwa na matatizo ya ngozi, lakini hii ni kwa sababu hawajui kwamba hata wenzao wa rika moja wanazo chunusi. Za kwako zinaonekana zaidi kwako kuliko watu wengine wanavyoziona chunusi zako. Unaweza kudhani kilamtu anaziangalia, na anaangalia ngozi yako mbaya tu na wala hakuangalii wewe. Lakini hii sio kweli. Watu wengine wanayo mambo mengi ya kufikiria na kwa hakika wanachoangalia ni kujua wewe ni nani na wala sio ngozi yako inaonekanaje. Kwa hiyo, usivunjike moyo na usiache chunusi chache zikunyime raha! Hautakuwa nazo milele. UTUNZAJI WA NYWELE Tunazo nywele mwili mzima, lakini zaidi kichwani, kwapani na maeneo yanayozunguka via vya uzazi. Kutunza nywele zako ni sehemu nyingine ya kutunza usafi na kutunza vizuri mwili wako. Nywele zilizopo kichwani mwako ni rahisi kuzitunza hususani kama utakuwa unazipunguza kila mara. Hata kama unakata nywele kila mara na kuzisuka, unatakiwa kuziosha ili zisiwe na vumbi na ziwe safi. Kama uko shuleni, jaribu kutochangia chanio kwa sababu unaweza kupata chawa, maambukizi ya fangasi, na minyoo. Kama utachangia vitana, hakikisha unaviosha vizuri kwa maji ya moto yenye sabuni kabla na baada ya kutumia. Watu wengine wana matatizo ya mba, hali ambayo inasababishwa na ngozi ya nywele kuwa kavu mno.mba unasababishwa na chembechembe ndogo za ngozi mfu, na watu wengine wenye mba nyingi wanatumia shampuu maalumu zenye dawa ili kuzuia mba. Ni vema kuoga mara kwa mara ili kuziweka safi nywele zilizopo kwenye mwili wako, nywele zilizopo kwenye kwapa, na nywele zilizopo kwenye maeneo ya via vya uzazi. Kama ulivyosoma sura ya 2 nywele hizi zinasaidia kuondoa jasho na uchafu kwenye mwili wako. Hata hivyo, sehemu nyingine za Afrika watu wananyoa nywele hizi kwa vile wanajisikia vizuri bila nywele hizo. Kama mila na tamaduni zako zinapinga kuwa na mavuzi yakate kwa kutumia mkasi. Usiziondoe zote kabisa kwa kutumia krimu ya kuondolea nywele au kwa kunyoa. Mafuta ya kunyolea nywele yanasumbua na kuumiza ngozi laini katika sehemu za siri. Pia kunyoa mavuzi kuna madhara yake. Kama unanyoa mavuzi, uwezekano wa kujikata ngozi ni mkubwa. Iwapo utajamiiana, mikato hii ni milango ya kupitishia VVU. Hii ni hatari. Tatizo lingine la kunyoa mavuzi ni wakati mavuzi yanaota tena. Nywele zinakuwa na incha kali kiasi cha kuweza kutoboa kondomu. Vilevile maeneo yanayozunguka via vya uzazi yaliyonyolewa yanaweza kupata maambukizi kidogo kwenye vinyweleo au sehemu ambazo mavuzi yanaota. Kunyoa mavuzi kiasi ni salama kidogo, lakini kuwa mwangalifu usiondoe nywele zote. LISHE NZURI Margareth, kutoka Tanzania (Umri; miaka 18,) Nilipokuwa darasa la sita, nilianza kuota nywele sehemu za siri. Mama yangu aliniambia kuwa, zikikua na kuwa ndefu ninatakiwa nizipunguze na kuzisafisha vizuri, la sivyo nitanuka. Lois kutoka Tanzania (Umri; miaka 13) Nimeona nywele kwenye kwapa, kwa vile sio muda mrefu nilipoziona sijazikata bado Lishe nzuri ni muhimu kwa afya njema. Kula chakula chenye virutubisho ni muhimu katika maisha yote lakini ni muhimu zaidi wakati wa utoto na wakati wa balehe kipindi ambacho mwili wako unakua na unaongezeka kwa kasi sana. Mwili wako unahitaji chakula kizuri ili ukue na upate nguvu kwa ajili ya kufanya vizuri shuleni, kucheza michezo na kufanya kazi. Wakati mwingine vijana wadogo hawali mlo wenye lishe na wanasahau kula kwa wakati maalum uliopangwa. Wanaweza kuacha mlo kamili na badala yake wakakazania kula biskuti, chips, chokoleti, vitu vitamu na soda. Hivi vyakula havina lishe, na mwili wako unahitaji zaidi ya hivi ili uwe na afya

32 SURA YA 5 Mabadiliko Ya Msingi Katika Kutunza Mwili Kila aina ya chakula ina kazi yake mwilini kwa hiyo unahitaji kula milo yenye kila aina ya chakula. Aina za msingi za vyakula ambayo mwili unahitaji ili uweze kufanya kazi vizuri ni: Vyakula vyenye wanga au vyakula vyenye kuleta nguvu : Vyakula hivi vinajumuisha ugali, fufu, mihogo, viazi vitamu, viazi mviringo, mikate, mchele, ndizi, ulezi, na mtama. Vyakula vya kulinda mwili : Vyakula vya kulinda mwili ndani yake vina vitamini na madini muhimu ambayo mwili wako unahitaji ili uweze kufanya kazi vizuri na uwe na afya. Vitamini na madini vinapatikana katika mboga za majani, (kama vile spinachi, majani ya maboga, kisamvu), nyanya, maboga na karoti. Pia matunda ya aina zote kama, papai, embe, chungwa,na nanasi nayo yana vitamini muhimu. Vyakula vya kujenga mwili : Vyakula vya kujenga mwili vina protini. Protini husaidia mwili wako uweze kukua na kujengeka vizuri, hususani wakati wa ujana balehe.pia husaidia mwili wako ujiponye na kujikarabati wenyewe ukiumia. Vyakula vya kujenga mwili vinajumuisha karanga, njegere, maharage, kunde, nyama, kuku, samaki wabichi, samaki wa kukaushwa na konokono. Mayai, maziwa, maziwa mgando na jibini yana protini vilevile. Vyanzo vingine vya protini nyama, samaki, maharage na njegere, pamoja na mbogamboga za majani ya kijani kilichokoza ni vyanzo vya madini ya chuma pia.madini ya chuma ni muhimu hususani kwa wasichana na wanawake kwasababu wanahitaji madini ya chuma ya ziada wakati wakiwa katika hedhi na wakati wakiwa wajawazito. Mafuta na vitu vitamu: Mafuta ni chanzo cha nguvu mwilini. Baadhi ya mafuta, kama vile ya karanga, ya nazi, ya mawese yanatokana na mimea wakati mengine kama vile siagi au samli yanatokana na wanyama. Mafuta yanaleta nguvu nyingi, lakini mwili unahitaji nguvu kidogo tu. Hivyo basi, ukila mafuta mengi sana unaweza ukapata matatizo ya kiafya siku za usoni.chanzo kingine cha nguvu mwilini ni sukari. Kwa ujumla vitu vitamu ni vibaya kwa meno yako. Fikiria kuhusu mlo wako na hakikisha unapata aina zote muhimu za chakula kama zilivyoonyeshwa katika ukurasa wa 51, Vyakula vya kuleta nguvu vinatakiwa kuwa ni vya msingi katika mlo wako na unatakiwa ule vyakula hivi. Vyakula vya kulinda mwili ni muhimu sana pia, kwa hiyo kula kwa wingi matunda na mboga mboga. Vyakula vya kujenga mwili ni muhimu sana, lakini huna haja ya kula mara nyingi kwa siku. Mwisho ni vyema kula kidogo vyakula vya mafuta na vyakula vitamu. NI KIASI GANI CHA NGUVU MWILI UNAHITAJI? Nguvu unayohitaji inategemea na nguvu unayotumia. Ukuaji wakati wa balehe unatumia nguvu nyingi. Kwa hakika kijana balehe anahitaji nguvu nyingi ukilinganisha na mtu mzima. Nguvu inapimwa kwa kalori. Kama ukila vyakula vyenye nguvu zaidi kuliko mwili wako unvyohitaji kwa siku, kiwango cha ziada cha karoli kitabadilishwa na kuwa mafuta na mwili wako utahifadhi mafuta hayo kwa muda. Watu wengi hudhani kuwa na mafuta mengi ni afya njema na ni jambo la kawaida, lakini inaweza kuwa ni tatizo kama ukiwa na mafuta mengi. Baadhi ya watu hususani watu ambao wanakula sana vyakula vyenye kalori nyingi (vyakula vyenye mafuta na sukari) na ambao hawafanyi mazoezi wanakuwa wanene sana. Katika baadhi ya miji ya Afrika, wapo wavulana na wasichana wengi wenye uzito mkubwa kuliko wanavyotakiwa wawe. Hii ni kwa sababu kufanya mazoezi katika miji ni vigumu. Pia vyakula vingi vya kukaangwa huuzwa mijini. Vyakula vilivyokaangwa vinaweza kuandaliwa kwa haraka na urahisi - vinaweza kuandaliwa haraka zaidi kuliko vyakula vya asili, kama vile maharagwe na michuzi. Japokuwa chakula kilichokaangwa kinaweza kuwa na ladha nzuri na kinaweza kuandaliwa haraka, sio kizuri kwa afya njema. Mlo wa chakula kilichokaangwa kinaweza kuwafanya watu wawe wanene sana na baada ya muda mrefu, kinawadhuru moyo na mishipa ya damu. Jaribu kuepuka kula chakula chenye mafuta na kilichokaangwa. Vilevile epuka chakula na vinywaji vyenye sukari. MAZOEZI Lishe bora inajumuisha mchanganyiko wa vyakula vya aina tofauti, kwa viwango tofauti Kila mtu anahitaji mazoezi: Watoto, vijana, wazee wasichana na pia wavulana. Mazoezi yanakufanya uwe mzuri ung ae, mwenye umbo zuri na macho maangavu. Yanakufanya uwe mwenye nguvu kwa sababu yanaimarisha moyo wako na mapafu; hujenga misuli na unene wa mifupa yako. Yanakufanya uwe na uwezo zaidi wa kupambana na magonjwa kwa kuongeza nguvu ya mfumowa kulinda mwili. Nfune kutoka Zambia (Umri; miaka 13) Nina afya nzuri kwa sababu nakula mlo kamili na ninafanya mazoezi kwa wingi

33 SURA YA 5 Mabadiliko Ya Msingi Katika Kutunza Mwili Mazoezi yana faida nyingine zaidi, yanaimarisha hisia zako, yanajenga kujiamini, yanakufanya ujisikie vizuri. Kama unajihisi kuwa na mfadhaiko, hali mbaya au huzuni, tembeatembea au cheza mchezo wa kurusha mpira.fanya mchezo wa kukaa na kunyanyuka. Cheza mpirawa pete. Endesha baiskeli, ruka kamba, ogelea, Cheza mpira wa wavu au mpira wa meza. Fanya kitu chochote kitachofanya moyo wako uende kasi ili kuongeza morali. Mazoezi yanaweza pia yakawa njia nzuri ya kukufanya uwe hodari katika stadi muhimu za maisha, kama kujiamini, ushirikano na kufanya kazi kwa pamoja. Watu wengi kwanza hujifunza stadi hizi wakati wakicheza michezo au wakati wanapojiunga na timu. Kufanya mazoezi mengi haimaaanishi kuwa lazima ujiunge na klabu ya michezo. Kusaidia kazi za shambani, kwenye bustani au kuzunguka nyumba yanaweza kuwa mazoezi mazuri. Shughuli za nyumbani zinaweza kujenga mahusiano mazuri na wazazi wako. Baadhi ya watu ni wakimbiaji wazuri lakini wengine sio. Baadhi ya watu wana vipaji maalum vya mpira wa miguu, kukimbia kwa kasi au kuogelea vizuri, kama vile ambavyo watu wengine ni wazuri katika hisabati au katika kujifunza lugha. Hata kama wewe si mkimbiaji, unatakiwa kufanya mazoezi kwa wingi. Kila mtu ana mwili ambao unatakiwa autumie. Kwa mfano kwa kujinyoosha, kusukuma au kujaribu mambo kadhaa. Unaweza kujikuta unapofanya mazoezi unafurahi zaidi na zaidi. Unaweza ukawa mwana riadha bila ya wewe mwenyewe kujua! Iwapo hujazoea kufanya mazoezi, inaweza kuwa vigumu unapoanza. Unaweza kujikuta unashindwa kupumua wakati wa kukimbia. Mazoezi yanaweza Kuna njia nyingi nzuri za kufanya mazoezi kukufanya ujisikie vibaya na hivyo kutoendelea nayo. Kwa hiyo, anza taratibu. Tafuta mchezo unaoupenda na jenga nguvu zako, hivyo unaweza kufanya zaidi na zaidi. Nia ni kufanya moyo wako uende kasi, kujisikia kwamba unapumua haraka kuliko kawaida, na kuwa na joto mwilini. Jaribu kufanya hivi kwa angalau dakika 20, mara 3 kwa wiki. Ruvimbo kutoka Zimbabwe (Umri;miaka 13) Naendesha baiskeli ili kujishughulisha na kwa sababu za kiafya. Vijana wanatakiwa wajishughulishe, Dunia ina mambo mengi ya kufanya. Godfrey, kutoka Zimbabwe (Umri; miaka 19) Napenda michezo, Nacheza mpira wa kikapu kuuweka mwili wangu imara na wenye afya nzuri. Maumbile mazuri hupatikana kwa kufanya mazoezi; maumbile mabaya husababisha maumivu katika kifua na mgongo. MAPUMZIKO MAZURI Endelea na mpangilio wako wa mazoezi na utaona tofauti! Pamoja na chakula kizuri na mazoezi ya kutosha, unahitaji kupumzika vya kutosha. Kupumzika kunaruhusu mwili kuhifadhi zaidi nguvu. Kupumzika kunaweza kuwa katika hali ya kupumzika kimwili au kulala usingizi Tumia muda kupumzika kila siku kwa kusoma kitabu, kufanya kitu unachofurahia, kusikiliza redio, au kwa kutafakari maisha yako. Kwa kiwango kidogo, televisheni inaweza kukufanya upumzike, lakini usitumie muda mwingi kuangalia televisheni au video. Kulala ni njia muhimu ya kupumzika. Ni wakati wa kulala tu ndio moyo wako unapunguza mapigo na misuli yako inapumzika. Hii inaruhusu mwili wako kurudisha na kujiponya na hali ya mfadhiko au majeraha. Unahitaji kulala sana kipindi cha balehe kwa sababu mwili wako unatumia nguvu nyingi. Watu wengi wanahitaji kama kiasi cha masaa 8 ya kulala usiku mmoja. Baadhi ya watu wanahitaji pungufu, na baadhi ya watu wanahitaji zaidi. Kama, unajisikia kuchoka muda wote, hakikisha unakwenda kulala mapema. Mabadiliko yote yanayotokea mwilini mwako yanachosha, kwa hiyo hakikisha unaupa mwili wako nafasi ya kupumzika! Fanya mazoezi yako kila mara na utaona maendeleo mazuri.ngozi yako itang aa. Macho yako yatang aa, utakuwa na furaha na raha. Utajiamini zaidi na kuwa na uwezo wa kuyakabili matatizo. Na kwa hakika utakuwa na nguvu na mwenye afya pia. Kwa hivyo endelea na mazoezi na usiache kufanya ati kwa sababu ni kipindi cha mitihani.wakati wa mitihani ndio unahitaji kufanya mazoezi zaidi

34 Sura ya 5 MAMBO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI Kuna vitu vichache, rahisi na vya msingi unatakiwa kuvijua kuhusu kutunza mwili wako. Utakapofikia kipindi cha balehe, utaanza kutoa jasho zaidi. Kuoga kutakufanya uwe msafi na kunukia vizuri Osha meno yako angalau mara mbili kwa siku ili kuepuka meno kuoza na pia ili utoe pumzi nzuri. Kama tezi zako za jasho, zinatoa mafuta, unaweza kuwa na chunusi. Chunusi ni sehemu ya ujana balehe na hakuna njia ya kuziekwepa. Kuuweka mwili wako safi kwa kuoga na maji na kutumia sabuni ni suluhisho lakini usisugue ngozi yako sana, na usitumie sabuni ya kufulia kwa sababu itaharibu ngozi yako Kula mlo wenye lishe ukiwa na vyakula vya kulinda na kujenga mwili. Epuka kula vitu vyenye sukari na vyakula vilivyo kaangwa Fanya mazoezi ya kutosha. Mazoezi yanaimarisha moyo wako, mapafu, na misuli, yanakuweka imara na yana amsha ari. Mabadiliko yote unayoyapitia ni muhimu sana, kwa hiyo upe mwili wako nafasi ya kupumzika kiasi cha masaa 8 kwa usiku. Kwa kujizoesha kuwa msafi, kula vizuri, kufanya mazoezi vizuri na kupumzika, utaruhusu mwili wako kufanya kazi vizuri, utajisikia vizuri, kimwili na utajisikia vizuri kiakili. Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Sura hii inahusu afya ya hisia zako. Afya ya hisia inahusisha mambo mengi, kama kujipenda, kujiamini, kustahimili wasiwasi, mfadhaiko, na huzuni na kuelewana na watu wengine. Kuwa mwenye afya nzuri ya hisia maana yake ni kujisikia vizuri wewe mwenyewe. Vile vile maana yake ni kuwa na nguvu za ndani za kuweza kustahimili raha na shida katika maisha. Madaktari hawajajua ni kwa nini mtu awe na afya nzuri kihisia na mwingine asiwe nayo. Inawezekana ni mchanganyiko wa haiba ya kuzaliwa nayo na namna ambavyo ulilelewa ukiwa mtoto mdogo. Afya nzuri kihisia inategemea pia na mtazamo wako - je upo tayari kutengeneza afya yako iwe nzuri kihisia? Kila mtu anaweza kujitahidi awe na afya nzuri ya kihisia. Hii inamaanisha kujienzi na kujiamini. Vile vile ina maana ya kujenga stadi ili kumudu wasiwasi, mfadhaiko na huzuni. Vile vile inamaanisha kujenga mahusiano na watu wengine. KUJIHESHIMU Kamusi ya Oxford inatafsiri Kujiheshimu kama mawazo mazuri kuhusu tabia ya mtu mwenyewe Iwapo unajiheshimu sana, maana yake ni kwamba unajisikia vizuri.unajua kwamba unayothamani - mtu unayestahili kupendwa. Unajiheshimu mwenyewe. Hisia za namna hii ni nzuri sana, unapojihisi kupendwa na kuheshimiwa unategemea hivyo hivyo kutoka kwa watu wengine vilevile. Unapojiheshimu sana haina maana ya kwamba wewe huwezi kujichukia au kujikasirikia mwenyewe. Kuna wakati kila mtu hukata tamaa, lakini yule mwenye kujiheshimu anakubali makosa na kusonga mbele. Kujiheshimu ni tofauti na kujidai au kuwa na majivuno mengi.watu wanaojienzi wanajipenda, lakini haina maana ya kwamba wanajifikiria wao hawana dosari yoyote, au wao ni bora kuliko wengine. SURA YA

35 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo JE UNAJUA Maana ya kuwa na Afya nzuri kihisia? Inaweza ikawa vigumu kuelezea afya nzuri ya kihisia. Lakini kawaida utaijua kwa kuona. Kwa mfano tumchukulie Rose, anaelekea kuwa na furaha wakati wote na anaonekana kuyamudu maisha ya raha na tabu. Anapopata maksi za chini anakubaliana nazo na anaongeza bidii. Akiachwa na mpenzi wake, analia lakini baadaye anaamua kwamba siyo mwisho wa dunia. Kipindi cha mitihani, huwa hafadhaiki sana. Hufanya mazoezi na kuzungumza na rafiki yake mpenzi kukabili mfadhaiko. Rose anajienzi sana. Hashindwi na hisia anapoachwa na mpenzi wake. Hujitambua kama ni mtu muhimu. Vile vile anajiamini sana. Ni kweli kwamba alifanya vibaya kwenye majaribio, lakini anajua anaweza kufanya vizuri zaidi. Hahitaji kumlaumu mwalimu. Njia anayotumia kupambana na mfadhaiko ni nzuri. Michezo na kumwambia rafiki anayemwamini matatizo yanayomsibu kunamsaidia kushughulikia wasiwasi na kisha kusonga mbele. Aidha, watu wengine wanapata shida sana kumudu raha na shida za maisha. Kwa mfano Emma, ambaye yuko katika mazingira yanayofanana na ya Rose, hufanya kila kitu tofauti. Hakubali kukosolewa badala yake humlaumu mwalimu kwa kupata alama mbaya. Akiachwa na mpenzi wake anafadhaika. Hutangaza mambo ya uongo kuhusu mvulana huyo na huanza kufanya mbwembwe na wavulana wengine. Anapokuwa na mfadhaiko anaanza kunywa pombe na kuvuta sigara. Inakuwaje Emma anapata shida sana kuyamudu matatizo haya? Jambo mojawapo ni kujienzi. Anaumia sana anapoachwa na mpenzi wake na anayamudu maumivu kwa kumsema rafiki yake vibaya. Anajaribu kujihakikishia kwamba bado anapendwa kwa kumpenda mvulana mwingine. Njia yake ya kupambana na mfadhaiko haifai kabisa, pombe na sigara vinaweza kukusahaulisha kwa muda lakini havitatui tatizo. Kujienzi ni kitu ambacho kipo ndani yako. Lakini hiyo haimaanishi huwezi kuifanyia kazi au kuhitaji kuikuza na kuijenga. Unaweza kuzingatia yafutayo ili ujenge tabia ya kujienzi: Epuka kujilinganisha na wengine mara kwa mara. Weka malengo yako, na usijihukumu mwenyewe kwa kuangalia mafanikio ya mtu mwingine. Maisha ni safari ndefu. Kuna wakati utaenda mbele na wakati mwingine utarudi nyuma. Tambua vipaji vyako na kujikubali vile ulivyo.tengeneza orodha ya mambo unayoyafanya vizuri. Je wewe ni msanii? Mwanariadha.Mwimbaji, msimuliaji wa hadithi au mnenguaji (mcheza dansi) Ni masomo gani unayofanya vizuri shuleni? Fikiria wewe ni mtu wa aina gani na kutengeneza orodha ya sifa ulizonazo. Unapenda nini kuhusu wewe mwenyewe? Wema wako? Ucheshi? Ubunifu? Umakini? Fahamu mambo yanayokuhusu ambayo ungependa kuyaboresha, lakini usijikosoe sana. Kuwa mhalisi na weka malengo ambayo yanatekelezeka na yatakayoonyesha mafanikio ili uridhike unapoyakamilisha. Jiamini, na jiambie ninaweza!. Tumia muda wako na watu wanaokujali wanaofanya ujisikie vizuri na kuongeza hadhi ya kujiheshimu. Kaa mbali na watu wanaojaribu kuharibu heshima yako, hasa kama wanafanya hivyo kwa sababu fulani. Kwa vyovyote vile kuifanyia kazi heshima yako haina maana kuwa hutaweza kupata matatizo. Kuifanyia kazi heshima yako itakusaidia matatizo kuwa mepesi. Kujiheshimu kunakulinda wewe binafsi. Wakati mtu anakutendea vibaya hisia za kujiheshimu zinapiga kelele Hee! haya ni makosa, usiruhusu mtu huyu akakutendea hivi. Hebu fikiria kana kwamba marafiki zako wamekuacha. Wamejiunga pamoja na kukuacha peke yako. Ghafla unajisikia kutetemeka na huna uhakika wa mambo yako. Ni kwa nini hawakutaki tena? Je kuna makosa umefanya? Heshima yako inaanza kufifia kama ua linavyonyauka.unaanza kujisikia vibaya. Katika mazingira ya namna hii, watu wengine hupata hofu. Wanachukua njia rahisi ya kurudisha heshima inayoshuka ili apendwe tena, hata kama itamaanisha kufanya jambo ambalo wanafikiria ni kosa. Kwa mfano, vijana wengine ambao wamekataliwa na marafiki zao wa zamani huanza kujiunga na makundi ya vijana wanaokunywa pombe, wanaovuta bangi na kujiingiza kwenye matatizo makubwa. Hivyo wanaanza nao kula madawa ya kulevya, kunywa pombe ili waweze kukubalika. Ni vizuri kutafuta kukubalika na kweli inapandisha hadhi lakini haisaidii kutatua matatizo ya kujiheshimu na wala kukubalika hakudumu. Unaweza kujisikia vizuri kwa muda lakini baada ya muda mfupi sauti ndogo ndani yako huanza kukusumbua: Watu hawa hawako makini. Sauti hii ni kwamba haujawa mkweli kwako mwenyewe, unajizuia kufanya mambo unayoyataka na unayoyaweza. Hujisikii vizuri kutokana na yale unayoyafanya kwa mkumbo... Hiyo sauti ndogo ni nafsi yako. Ni vema wakati wowote kuisikiliza. Kurekebisha kujienzi kwako ni kazi kubwa kuliko kujiunga na makundi mapya, au kupoteza mawazo kwa kutumia pombe, na madawa ya kulevya, (kwa taarifa zaidi kuhusu madawa ya kulevya na pombe soma sura ya 12). Itakusaidia zaidi kurekebisha kujienzi kwako. Unapopitia matatizo ya kujienzi, yafuatayo ni mambo machache unayoweza kuyafanya ili yakusaidie:- Jaribu kuliweka tatizo lililopo katika mtazamo sahihi. Jaribu kukumbuka kwamba dunia imejaa mambo ya raha na shida, na kwamba huu sio mwisho wa dunia. Zungumza na mtu wa karibu yako na unayemwamini kuhusu matatizo yako na hisia zako. Mtafute kijana mtoa ushauri nasaha au mtu ambaye anakujali na ambaye anaweza kukusaidia

36 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Kumbuka kuwa watu wengine wanakuthamini kutokana na vile ulivyo. Mtafute mtu ambaye atakuthamini rafiki mpya, mwalimu, dada, kaka, mzazi au ndugu mwingine. Kuwa mvumilivu. Kujiheshimu hakujengeki katika siku moja.unaweza kujisikia vizuri baada ya siku kadhaa. KUJIAMINI Unapokuwa unajenga kujienzi, unajenga kujiamini pia. Kujiamini ni jambo la msingi katika afya ya kihisia. Kama kujienzi maana yake kujisikia vizuri na ukamilifu kuhusu tabia yako na namna ulivyo, kujiamini maana yake kujisikia vizuri kuhusu uwezo wako wa kufanya mambo. Kujiamini ni jambo kubwa. Watu wanaojiamini wanajisikia huru kujaribu kufanya mambo mapya bila ya kuwa na wasiwasi mkubwa kama watashindwa. Hawaogopi kujiingiza katika mazingira mapya na kati ya watu wasio wafahamu. Hawajali hata kidogo watu wengine watawafikiriaje. Kujiamini kunavutia sana. Watu wanaojiamini mara kwa mara wanapendwa sana kwa sababu wanaonekana kufurahia maisha kwa kiwango kikubwa wanapopata changamoto mpya na uzoefu wa mambo mapya. Kujiamini kunajitosheleza. Kwa maneno mengine, kujiamini kunasabisha kujiamini zaidi. Hii maana yake ni kwamba kwa jinsi unavyojaribu kufanya mambo mapya ndivyo unavyozidi kujiamini. Hii inasababishwa na sababu mbili zifuatazo: 1. Unajifunza kwamba unaweza kufanikiwa katika mambo mengi ambayo hukuwahi kufikiria ungeweza. 2. Unajifunza kwamba hata kama unashindwa kufanya jambo fulani hakuna neno. Unapojiamini, wakati mwingine unaweza kushindwa, lakini mara nyingi utafanikiwa. Hii ni kwasababu unaposhindwa kufanya kitu, mara kwa mara ni kwa sababu unakuwa na wasiwasi au kiwewe. Unapojiamini hata hivyo unaweza kufanya mambo mapya. Kwa ujumla, wasiwasi na kutojiamini hakuleti matatizo makubwa katika kuwa makini kwa lolote unalojaribu kufanya. Lifanyie kazi suala la kujiamini, itakusaida maisha yako yote. Unaweza:- Kujifikiria kama mtu unayeweza yule ambaye unaweza kufanikisha. Kujiamini kunakuwezesha kujaribu mambo mapya bila kuhofu kushindwa Jipe changamoto. Jaribu mambo mapya na uwe muwazi katika mambo ambayo hukuyazoea. Jizoeshe kusema sifahamu jinsi ya kufanya kile lakini ningependa kujaribu JE? Unafahamu kwa nini wasichana wana matatizo zaidi ya kujiheshimu na kujiamini kuliko wavulana? Wakati mwingine wasichana wana matatizo ya kujiamini na kujienzi kidogo kuliko wavulana wa rika moja. Kwa nini iwe hivi? Je, kujienzi na kujiamini kunahusiana na jinsi ya mtu? Jibu ni Hapana kujienzi na kujiamini hakuhusiani na jinsi ya mtu. Hata hivyo heshima na imani ya mtu inaweza kuathirika sana kwa namna au jinsi anavyotendewa na watu wengine wazazi, wadogo zake, ndugu, walimu, majirani viongozi wa dini na viongozi ndani ya jamii, n.k. Kwa bahati mbaya katika utamaduni mwingine wavulana na wasichana wanatendewa tofauti kabisa; na hii inaweza kuathiri sana namna wanavyojiona na uwezo wao. Kwa mfano; katika familia zingine wavulana wanaweza kupewa nafasi zaidi katika elimu na mafunzo ya kazi; na walimu wakati mwingine wanawajali zaidi wavulana. Kwa upande mwingine wasichana wanaweza wasipate nafasi kama hiyo. Wanaweza wasiruhusiwe kucheza na wenzao au kucheza michezo kama kaka zao wanavyofanya. Zaidi ya hapo kazi ngumu wanazofanya nyumbani na shambani zinaweza zisionekane na wala zisitambulike. Matokeo yake wasichana na wanawake hujiona hawana thamani na wanaweza kuanza kuamini kwamba thamani yao ni ndogo kuliko ya wavulana na wanaume. Lakini hii sio kweli! Watu wote ni sawa. Iwapo wote watapata nafasi sawa, wasichana wanaweza kufanya vizuri shuleni, katika kazi na kitu chochote wanachotaka kufanya. Inaweza kuwa vigumu sana kama wewe ni msichana na unaishi katika mazingira ambayo mara kwa mara unajisikia huthaminiwi kama ambavyo mvulana anavyothaminiwa. Haya hapa ni mambo machache ambayo unaweza kufanya ili kuimudu hali hiyo: Wakati wote kumbuka kwamba una thamani kubwa bila kujali watu wengine wanasema nini. Wewe una akili na uwezo sawa na mvulana yeyote. Jitahidi mara dufu katika kujenga kujienzi na kujiamini kwako. Jisifu mwenyewe na ridhika unapofanya kazi vizuri. Usisubiri kusifiwa na watu wengine ambao wanaweza wasikusifu. Tumia kila nafasi uliyo nayo kujifunza stadi mpya na fanya mengi kati ya hayo. Kumbuka, kila unapofanikisha jambo utakuwa unajihakikishia mwenyewe na watu wengine kwamba unayo thamani kama ambavyo wengine walivyo nayo. Tambua changamoto unazokumbana nazo; lakini usikate tamaa. Kama unaishi katika jamii ambayo wanawake wanadharauliwa sana usitegemee hali hiyo kubadilika katika siku moja, lakini hata hivyo lisikufanye ukate tamaa. Zungumza na wazazi wako au mtu mzima yeyote anayejali. Kwa mfano; kama wazazi wanataka kukuachisha shule au wanataka uolewe jaribu kutafuta mtu wa kuzungumza naye. Eleza namna elimu ilivyo ya muhimu kwako na waombe kama wanaweza kukusaidia kumudu hali hiyo

37 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Kuwa mcheshi. Usiruhusu aibu au wanachofikiria watu wengine iwe ni sababu ya kutofanya mambo mapya. Vione vikwazo kama ni nafasi ya kujaribisha na kujifunza mambo mapya, Fikiria mwenyewe sawa, nitalishughulikia vipi tatizo hili? Ukishindwa kitu, kuwa na mtazamo sahihi. Usiwe na wasi wasi au kuchukizwa nalo. Fikiria kosa limetokea wapi na ungefanya nini cha tofauti safari nyingine. Halafu achana nacho. USIWE NA WASIWASI, FURAHI Umewahi kusikia wimbo wenye maneno ya kichwa cha habari hapo juu? Sauti yake ni rahisi na inavutia. Unadhani ni rahisi kuwa na furaha? Hata hivyo kila mtu anao wasiwasi, na vijana balehe wana wasiwasi mwingi wasiwasi kuhusu wao wenyewe namna wanavyoonekana, rafiki zao, mafanikio shuleni, maisha ya baadaye, n.k. Wasiwasi unaweza kukukosesha raha. Kwanza jiulize kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi huo. Mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi usiokuwa wa lazima. Yapo mambo mengine ambayo hayahitaji kuwa na wasiwasi nayo, kama haya yafuatayo: Mambo ambayo huna uwezo wa kuyabadili, kama vile sura yako, rangi ya ngozi yako, umbile la nywele na ukubwa wa matiti au uume. Huwezi ukabadilisha vitu hivi, kwa hiyo ni vema kuvikubali kama vilivyo. Wewe ni mzuri kama ulivyo. Isitoshe ni haiba yako ndiyo inakufanya uwavutie watu wengine. Lenga katika wewe ni nani na wala sio unavyoonekana. Mambo ya dunia ambayo huna uwezo nayo. Unaona gauni zuri dukani. Usibabaike kwa sababu huna uwezo wa kulinunua. Utahitaji mshahara wote wa mwezi mmoja kutoka kwa baba yako ili uweze kulinunua. Kwa kuongezea, hata kama ungelipata gauni hilo ungejikuta baada ya miezi michache unahitaji gauni lingine, na hata zaidi. Mambo ya dunia hayaleti furaha wala kuwa mwisho wa matatizo; kwa hiyo lenga katika mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako. Ridhika jinsi ulivyo na kile ulichonacho. Kama tu ningepata gauni lile zuri, ningekuwa na furaha zaidi Kutokuwa na rafiki wa kike au kiume. Watu wengine hupata rafiki wa kike au wa kiume kipindi cha ujana balehe. Lakini wengine hawampati mtu huyo maalumu mpaka baadaye sana katika maisha. Kwa kuongezea, mapenzi ya vijana hayadumu sana. Inaweza kuchukua muda kumpata mpenzi wa moyo. Hivyo kuwa mvumilivu usikimbilie katika mahusiano ati kwa sababu unafikiri unahitaji kuwa na rafiki wa kike au kiume wakati huo. Shinikizo kutoka kundi rika ili kufanya kitu ambacho hutaki kukifanya: Fanya mambo yale tu ambayo unafikiri ni mazuri kwako. Hata siku moja usiruhusu tamaa ya kuwafurahisha watu wengine ikufanye wewe utende yale ambayo huyataki na unafikiria ni makosa. Kuwa mpweke: Upweke ni jambo ambalo linampata mtu yeyote kwa wakati fulani katika maisha. Kutatokea muda mfupi utakapojisikia kama huna mtu yeyote wa kuzungumza naye au hakuna mtu ambaye anakuelewa vizuri. Kwa kawaida nyakati kama hizi hudumu kwa muda mfupi na kila mtu anazipitia. Lakini bila shaka zipo hali ambazo unastahili kuwa na wasiwasi nazo. Kwa mfano: Wazazi wako hawezi kukulipia karo ya shule na hujui uende wapi kuomba msaada. Hili ni tatizo kubwa ambalovijana wengi wanalipata. Zungumza na Mwalimu au mshauri katika kituo cha vijana kilichopo katika eneo lako kama wana maoni yoyote. Vilevile zungumza na viongozi wa dini au viongozi wa kijiji ili kuona kama wanamfahamu mtu yeyote ambaye anaweza kutoa msaada. Labda unaweza kubadilisha shule yenye karo nafuu au kutafuta kazi ya kufanya mwishoni mwa wiki ili kupata pesa. Wewe na rafiki yako wa kike mlifanya mapenzi yasiyo salama na sasa anafikiria huenda akawa amepata mimba. Huu ni wasiwasi mkubwa. Jambo zuri la kufanya ni kwenda kliniki kupima mimba na kupata ushauri. Nenda na rafiki yako wa kike kwa ajili ya kumpa moyo. Kama ni mja mzito, usikatae kwamba sio mimba yako. Wote mnawajibika (angalia sura ya 11 kwa taarifa zaidi kuhusu mimba). Umesikia tetesi kwamba mmojawapo wa marafiki zako wa zamani ana UKIMWI. Huna uhakika kama ni kweli, lakini je upime? Huu nao ni wasiwasi mkubwa. Ndio, nenda kwa washauri nasaha na upimaji ili uweze kutuliza akili yako au uchukue hatua zinazostahili. Nenda na mtu mmoja kwa ajili ya msaada (angalia sura ya 10 kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu VVU (UKIMWI). Mtu mzima au mwanafunzi mwenzako amekuwa anakupatia zawadi ndogo ndogo na starehe. Lakini sasa anataka mfanye ngono. Anasema anakudai pesa nyingi ambazo amekuwa anatumia kwa ajili yako. Usikubaliane na shinikizo hilo. Unaweza kuishia kupata mimba kwa makosa na kuachwa na mwanaume au mvulana. Kaa mbali naye. Kuwa jasiri na zungumza na wazazi wako, shangazi au mtu yeyote mzima kuhusu hali hii. Usijaribu kumudu jambo hili peke yako. Katika hali mbaya kama hizi wasiwasi unaweza kukusaidia. Unahitaji kufikiria sana chaguzi zote ulizonazo ili kumudu tatizo, halafu unahitaji kuzipima chaguzi na matokeo yake ili uweze kufanyia kazi yale yanayokufaa. Hata hivyo wasiwasi juu ya hali mbaya kama hizi unaweza kukuongezea mfadhaiko, yaani pale unapoanza kujisikia umeelemewa na matatizo yako na wasiwasi. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako utatoa ishara: Huwezi kuacha kufikiria tatizo. Moyo unadunda kwa nguvu. Unaweza ukajisikia unakosa hewa. Tumbo linaweza kukuuma. Unaweza kukosa usingizi au unaweza kuota ndoto mbaya (kupata jinamizi). Unaweza kuwa msahaulifu. Iwapo unazipata dalili hizi za mfadhaiko chukua hatua zifuatazo: 60 61

38 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Vuta hewa kwa nguvu. Iwapo umefadhaika sana na unajisikia kukosa hewa na kichwa chepesi, acha kufanya kile ulichokuwa unafanya na polepole vuta hewa nyingi, ukiizuia hewa ndani ya mapafu yako kwa sekunde chache kabla hujaitoa. Tafuta chanzo cha mfadhaiko Je, unaweza kuupunguza mfadhaiko? Je, umefaidhaika na kitu ambacho hustahili kuwa na wasiwasi nacho? Tengeneza orodha ya vitu vyote vinavyosababisha uwe na mfadhaiko halafu iangalie kwa makini. Je, majukumu yamezidi? Je unaweza kufanya lolote ili kupunguza orodha yako? Zungumza na watu. Hakuna haja ya kutatua matatizo peke yako. Watu wengine wamepitia wakati mgumu kama wewe na wanaweza kutambua Usijaribu kumudu wasiwasi wako peke yako. Zungumza na mtu. namna ya kushughulikia tatizo lako. Anaweza kuwa mzazi wako, shangazi au wajomba, kaka au dada, rafiki wa karibu, mwalimu, jirani, mfanyakazi wa afya, kijana mshauri nasaha, kiongozi wa dini na mzee wa kijiji. Hawa ni watu wachache ambao wanaweza kukupa ushauri. Wanaweza kupendekeza ufumbuzi ambao hujaufikiria. Fanya mazoezi. Kimbia, cheza mpira wa miguu au tembea haraka haraka, ogelea. Mazoezi ni njia nzuri sana ya kushinda mfadhaiko. Pata usingizi wa kutosha. Jaribu kwenda kulala ukiwa na hali nzuri ya akili. Epuka kuangalia televisheni (luninga) kabla ya kwenda kulala. Jaribu kupumzisha misuli yote mmoja baada ya mwingine kadri unavyolala kitandani. Kula chakula bora, Zingatia kupata kifungua kinywa, na milo yote ya siku. Tumia kusali au kutaamali. Hii ni njia nzuri ya kujituliza mwenyewe na kumudu mfadhaiko. Sala zimejaa mategemeo na hekima kuhusu namna ya kuyaendesha maisha yako ya kila siku. Fanya kile unachokifurahia Hivi ni vitu ambavyo vitakufanya uondokane na mawazo ya kuwa na wasiwasi, kama kutumia muda wako na rafiki wa karibu, kuchora, kuimba, kulima bustani, kupika, kusikiliza muziki n.k. Zifuatazo ni njia chache za kupambana na mfadhaiko ambazo unatakiwa uepukane nazo: Kutumia pombe na madawa ya kulevya kama njia ya kutuliza mawazo. Hii sio dawa. Pombe na madawa ya kulevya vinatuliza zile sehemu za ubongo ambazo zinasaidia kufikiria na kudhibiti tabia yako. Pombe na madawa ya kulevya vinaweza kukufanya utende mambo ambayo baadaye utayajutia. Kuficha hisia zako na kuyaweka matatizo yote ndani ya roho yako hakuwezi kukusaidia kuyamudu na wala kumaliza mfadhaiko wako. Mwisho wake utajisikia kama unayetaka kupasuka. Kuhamishia mfadhaiko wako kwa watu wengine. Jihadhari mfadhaiko wako usije ukakufanya kuwa na kiburi, mkali au mbaya kwa watu wengine. Hii itakufanya wewe mwenyewe ujisikie vibaya zaidi. Njia hizi za kukabiliana na mfadhaiko sio nzuri na wala hazifai. Zitazidisha ugumu wa maisha yako na zinaweza kukuongezea mambo mengine mabaya zaidi ya kukufadhaika. Mfadhaiko ni kitu unachoweza kukidhibiti, kwa hiyo usiruhusu ukutawale. KUMUDU HUZUNI Wakati mwingine matatizo yanaweza kukufanya ujisikie mnyonge na ukashindwa kupata njia ya kuyaweka maisha sawa. Hivyo kula matunda na mboga mboga, kucheza michezo na kulala usingizi wa kutosha kutakufanya ujisikie vizuri zaidi. Wakati mwingine unayo kila sababu ya kuwa na huzuni. Kwa mfano; ukifiwa na mtu wa karibu sana, utasikitika sana. Unaweza ukamkumbuka marehemu sana na kupata hisia kali ya kuhuzunika. Kama umefiwa na rafiki yako wa kiume au wa kike unaweza kujisikia mpweke sana, na unaamini kuwa hutaweza kumpata mtu mwingine kama yeye. Kupotelewa kwa namna hii ni kugumu, lakini unaweza kuyakabili matatizo. Baada ya kipindi cha huzuni, utajisikia uko tayari kuendelea na maisha. Ingawa masikitiko ya kumpoteza mtu unayempenda yatabakia palepale, mwishowe utakuwa na furaha tena. Lakini wakati mwingine watu wanakuwa na huzuni kubwa kiasi cha kutoyatamani maisha tena. Wanadhani maisha hayana maana tena na hakuna faida yoyote ya kuishi. Wanajisikia watupu na hawafai kabisa. Wanajisikia hawana raha. Wanajiona wamepoteza mwelekeo. Hisia hizi za kuwa na huzuni sana na kujiona hufai zinaitwa unyong onyevu. Kunyong onyea au kuvunjika kwa moyo kunaweza kukasababishwa na jambo linalohuzunisha kama kifo, lakini mara kwa mara watu wanaopatwa na tatizo hili wanapata shida kutambua sababu maalumu au kilichosababisha kuvunjika kwa moyo. Matokeo yake wanapata tabu kutambua kama wamevunjika moyo. Wanaweza kugundua mabadiliko mbalimbali yakiwatokea, kama vile: Kuwa na huzuni wakati wote. Kukosa nguvu. Kushindwa kufikiri vizuri. Kuumwa kichwa mara kwa mara na matatizo ya tumbo. Kushindwa kufurahia mambo ambayo mwanzo yalikuwa yanafurahisha. Mabadiliko katika ulaji, (kama vile kula pelemende) au unywaji (kunywa pombe ili kujaribu kusahau matatizo). Je, umewahi kujisikia hivi au kuona mabadiliko kama haya yakimtokea rafiki yako? Kuvunjika moyo ni jambo la hatari, iwe ni wewe mwenyewe au rafiki yako, hivyo chukueni hatua zifuatazo:- Jaribu kutambua ni kitu gani kinachofanya uwe na huzuni

39 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Zungumza na watu wengine kuhusu hisia zako Fanya mazoezi, na fanya mambo ambayo yanakufanya uwe na furaha na ujisikie vizuri. Pamoja na haya, jaribu kutoka nje ya nyumba yenu na pitisha muda na watu wengine. Jihusishe na shughuli za kanisa/msikitini au kikundi cha vijana. Kupitisha muda na watu wengine kunaweza kukusaidia kuondoa fikra za mambo ambayo yanakufanya uhuzunike sana. Kusaidia kazi watu wengine kunaweza vilevile kuwa njia nzuri ya kukufanya ujisikie vizuri. Kwa mfano; jaribu kumsaidia mtoto anayejifunza kusoma, msaidie rafiki au jirani yako kazi wanazozifanya. Inaonekana kama upuuzi, lakini utashangaa namna ambavyo kumsaidia mtu mwingine kazi kunavyoweza kukufanya ujisikie vizuri zaidi pamoja na matatizo uliyonayo. Unapojisikia hovyo, kusaidia watu wengine kazi kunaweza kukufanya ujisikie vizuri zaidi. Kama yote hayo hayakukusaidia kiasi cha kufikiria kujiua, tafadhali mtafute mtu wa kuzungumza naye mara moja. Huyu anaweza akawa ndugu yako, mwalimu au mtaalamu wa ushauri nasaha. Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengi ni washauri nasaha wazuri, na wanatoa msaada na ushauri kwa watu wakati wote. Ufumbuzi wa matatizo yako unaweza kupatikana, kwa hiyo usijaribu kuyatatua peke yako unapojisikia umenyong onyea sana. UNAJUA kwamba pombe inaongeza mfadhaiko? Watu wengi hunywa pombe nyingi wanapokuwa na matatizo wakiamini kuwa inawasaidia kusahau shida walizo nazo. Pombe hufanya ubongo uwe kama umepata ganzi na kufanya matatizo kupungua papo hapo. Kwa bahati mbaya, pombe haiwezi kutatua matatizo yako ya huzuni au kusononeka. Ukweli ni kwamba pombe inaangukia katika kundi la madawa ya kupunguza uwezo wa ubongo na sehemu zingine za mwili kufanya kazi vizuri. Pombe na dawa zingine za kupunguza wasiwasi kwa hakika zinaongezea hali ya kusononeka. Kwa kuongezea, zinamsaidia mtu akwepe kutatua matatizo yanayomfanya asononeke. Matokeo yake, pombe inaweza kuwa ngao ya kutegemewa hasa matatizo yanapotokea. Watu wengine wanatawaliwa sana na pombe kiasi cha kwamba hawawezi kuishi bila kunywa. KUISHI VIZURI NA WATU Kuishi na kuelewana na watu ni sehemu nyingine muhimu katika afya ya hisia. Mahusiano mazuri na wazazi na marafiki zako yatakufanya wewe mwenyewe ujisikie vizuri kwa ujumla na yatakusaidia kupambana na raha na shida za maisha. Kuelewana na watu wengine kunahitaji stadi muhimu kama vile:- Kujitambua: Kujitambua maana yake ni kuwa na uwezo wa kuelewa hisia zako ni zipi na kwa nini ziko hivyo. Kujitambua maana yake ni kuwa unapojisikia ovyo ovyo unaachana na kufikiria kile unachohisi iwe huzuni, hasira, kukata tamaa, wasi wasi, n.k. Na baada ya kuachana na unachohisi unaendelea na kufikiria ni kitu gani kinakufanya uwe hivyo. Kwa mfano je ni wasiwasi juu ya masomo yako? Je unashuku urafiki ambao unaonekana kufifia? Je kuna mtu amekufanya ujisikie vibaya? Kujitambua ni muhimu kwa sababu kunakusaidia uelewe tatizo na chanzo chake. Kwa kutumia taarifa hii unaweza kuanza kutatua tatizo. Kama una wasiwasi na kazi za shule, unaweza kuzungumza na wazazi au mwalimu wako na kuanza kupata msaada unaouhitaji ili ujiamini tena. Kama una wasiwasi na rafiki yako, unaweza kuchukua hatua ya kuzungumza naye na kumueleza namna urafiki wenu ulivyo wa muhimu, na kwa pamoja mnaweza kuangalia namna ya kuufanya uwe urafiki wa nguvu. Iwapo kuna mtu anakukosesha raha, unaweza kuamua kukabiliana naye ili afahamu kwamba unajisikia vibaya anapokutendea vile, au kama hiyo haisaidii, unaweza kuamua kukaa mbali na huyo mtu anayekufanya ujisikie vibaya. Kujitambua ni uwezo wa kugundua unachohisi na kinachokufanya uhisi hivyo Mwisho, kujitambua kunaweza kukusaidia kuujua udhaifu wako, - udhaifu unaotakiwa kuufanyia kazi mwenyewe. Je, unazo tabia au mwelekeo fulani ambao ungependa kuubadilisha? Kwa mfano: unaweza kugundua kwamba unapofanya vibaya mitihani yako ya shule unakuwa na tabia ya kumlaumu mtu mwingine. Mwalimu hanipendi unajisemesha mwenyewe. Au unafikiria wanafunzi wengine walikuwa wanapiga kelele kwa hiyo nilishindwa kufikiri. Ni rahisi sana kulaumu watu wengine, lakini ni tabia mbaya kwa sababu huwi mkweli na hujiwajibishi. Labda ulipokuwa mtoto ilikuwa sawa kulaumu watu wengine hasa kwa vile yapo mambo mengine ambayo watoto hawawezi kuyadhibiti. Lakini unapoingia utu uzima, unahitaji kuwajibika kwa matendo yako. Kama kuna jambo ambalo haliendi kama unavyotaka ni juu yako kujaribu kulibadilisha. Kujisikitikia na kujifanya kana kwamba wewe ni mwathirika wa matendo ya watu wengine haitatatua jambo lolote. Ushirikeli (uwezo wa kuelewa hisia za mtu mwingine): Uwezo wa kuelewa hisia za mtu mwingine ni sawa na kujitambua ijapokuwa huu ni uwezo wa kuelewa kile ambacho mtu mwingine anahisi na kwa nini anahisi hivyo. Kuwa na uwezo wa kuelewa hisia za mtu mwingine maana yake ni kuwa na uwezo wa kufikiri na kujua pale penye tatizo la mtu kama - rafiki, mzazi, ndugu, n.k. Unaweza kujua hofu zao,wasiwasi, woga na mahitaji yao, na unaweza kuelewa wanavyojihisi. Kama ambavyo kujitambua kunavyosaidia ujue mahitaji yako, ushirikeli unakuwezesha kujua hisia za mtu mwingine. Kwa mfano; kama rafiki yako ana huzuni, kufahamu tatizo lake kunaweza kukusaidia ujue namna ya kumsaidia kulitatua

40 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Kutatua tatizo na kufikiri kwa ubunifu: Ili kupata ufumbuzi wa matatizo kunahitaji kufikiri kwa ubunifu. Kufikiri kwa ubunifu ni uwezo wa kufikiri ufumbuzi wa tatizo usio wazi. Ni uwezo wa kusumbua akili yako ili kupata fumbuzi mbalimbali bila kujiwekea mipaka ya mazoea uliyoyasikia ya utatuzi wa jambo fulani. Kwa mfano: fikiria kuwa umepata mimba ukiwa unasoma shule. Wasichana wote unaowafahamu waliopata mimba waliacha shule na hawakuweza kumaliza masomo. Kufikiria kwa ubunifu maana yake ni kutokudhani kwamba lazima uache shule eti kwasababu wasichana wengine waliacha. Labda inawezekana ukakaa shuleni ukiwa na mimba. Au unaweza kurudi shuleni baada ya kujifungua mtoto. Labda kipo kituo kwa ajili ya vijana waliozaa ambako unaweza kuendelea na masomo au mafunzo. Kufikiri kwa ubunifu kunahusisha kuzungumza na watu wengine. (walimu, vijana washauri wazazi, shangazi, wajomba marafiki) na kuchunguza chaguzi zote zilizoko mbele yako. Stadi za makubaliano. Hizi ni stadi ambazo unahitaji ili kutatua tatizo au tofauti ulizonazo na watu wengine. Kwa mfano, unaweza ukataka kutoka na rafiki yako, lakini wazazi wako wanataka ukae nyumbani. Hali kama hii inahitaji stadi nzuri za makubaliano. Inaweza ikawa vigumu kukubaliana na wakati wingine kukatishwa tamaa. Unaweza kujisikia kama upasuke, kwamba umevunjika moyo kiasi cha kusema potelea mbali na kuondoka ukiwa umekasirika na kuchoshwa. Lakini unahitaji kuwa mvumilivu na mtulivu wakati unaeleza kwa nini unajisikia hivyo, na kile unachohitaji. Vilevile unahitaji kuwa mkweli, mtu unayeelewa na kuheshimu yale ambayo watu wengine wanayahisi na kuyahitaji. Je, unajua maana ya kutatua tatizo kwa ubunifu bila woga wala jazba? Anne ana umri wa miaka 16 na ni yatima. Anaishi na shangazi yake ambaye anamtaka afanye kazi dukani kwake kila siku baada ya kutoka shule. Hili ni tatizo kubwa kwa Anne. Hapati muda wa kutosha wa kujisomea. Ameanza kufadhaika kwa vile mitihani inakaribia. Hapati usingizi vizuri usiku kwa sababu ana wasiwasi sana kuhusu masomo. Ameanza kumchukia shangazi yake. Anashangaa iwapo shangazi yake anamwona kama kitendea kazi na kwamba hampendi wala kujali maisha yake ya baadaye. Anne anajitambua. Anajua kuwa anayo tabia ya kuficha hisia zake mpaka anapolipuka kwa hasira. Tabia hii haimsaidii sana. Shangazi yake naye anakasirika na kusema ameanza kukosa heshima.safari hii anaamua kufanya mambo tofauti. Badala ya kumwambia shangazi yake kiugomvi Hunipendi anamweleza shangazi yake bila woga wala jazba Ninawasiwasi sana kuhusu mitihani yangu lakini nataka pia kukusaidia kazi za dukani. Hapa ameonyesha tabia ya kujiamini. Kwa kujieleza mwenyewe kwa njia hii, Anne amesimama imara na kuomba muda zaidi wa kujisomea. Lakini kwa wakati huo huo anaelewa shangazi yake anahitaji msaada wa dukani. Anaonyesha ushirikiano kwa shangazi yake ambaye ana majukumu mengine. Akifuata utaratibu huu, shangazi naye anaelewa pia. Kwa pamoja wanafikiri kwa ubunifu kutatua tatizo hili. Wanatengeneza ratiba inayompa Anne muda zaidi wa kujisomea jioni na pia kumsaidia shangazi yake jioni inapokuwa lazima. Inatia moyo kwa jinsi Anne alivyojisikia vizuri. Ghafla mfadhaiko unapungua na anaweza kuyafurahia maisha tena. Hata hivyo sio kila tatizo linaweza kujadiliwa na kufikia maelewano. Wakati mwingine utalenga katika matokeo ambayo yatakufanya uwe salama, hata kama mtu mwingine hatafurahia. Mathalani, rafiki yako wa kike au wa kiume amekataa kutumia kondomu pamoja na kumshawishi kwa nguvu zote. Katika hali kama hii zingatia usalama wako. Ondoka sehemu hiyo ikibidi. Msimamo: Msimamo ni stadi ya msingi katika kuelewana na watu wengine. Msimamo maana yake kutetea na kuyaenzi yale unayoyaamini wewe mwenyewe. Kuwa muwazi na mwaminifu kwako mwenyewe na watu wengine kuhusu kile unachokihitaji na kukitaka. Watu ambao hawana msimamo juu ya maisha yao huwa ni wanyenyekevu. Hata kama wanatendewa vibaya, hawajitetei. Watu ambao hawana msimamo mara kwa mara wanakosa imani ya kujienzi na kutetea mahitaji yao na kulinda hisia zao au hata miili yao ili wasiumizwe. Msimamo ni tofauti sana na kuwa mgomvi. Watu wagomvi ni watundu na hawana huruma, hawajali watu wengine wanahisi nini. Sio vizuri kuwa mgomvi kwa faida ya afya ya hisia kwa sababu, kwa undani kabisa, utajisikia vibaya kutokuwa na huruma kwa wengine. Misingi ya msimamo: Amua unachohisi au unachotaka na kiseme. Usiogope kuwa mkweli kuhusu hisia zako. Watu wanatakiwa kuziheshimu hisia hizo. Kwa mfano, labda ulijisikia vibaya na unakosa raha baada ya rafiki yako wa kiume kukugusa sehemu zako za siri. Unatakiwa kumwambia, Nilikosa raha uliponigusa sehemu zangu za siri sitaki uniguse hivyo tena. Mtu anayekupenda kweli hatataka kufanya vitendo ambavyo vinakukosesha raha. Mtazame mtu machoni: Kumwangalia mtu machoni ni kudhihirisha msimamo wako. Inamjulisha mtu mwingine kwamba hutanii kuhusu kile unachokisema na kwamba unaangalia kama wanakusikiliza au hawakusikilizi. Tamaduni nyingi haziungi mkono kumwangalia mtu machoni wakati wa mazungumzo. Wakati mwingine katika maeneo mengine huliona jambo hili ni ufedhuli (kutokuwa na ustaarabu/heshima) kijana mdogo anapomwangalia mtu mzima moja kwa moja usoni. Unaweza kufuata mila na desturi, kama kupiga magoti, kuonyesha heshima lakini kwa wakati huo huo endelea kumwangalia mtu huyo usoni kama unataka kuonyesha ujasiri/msimamo wako. Usitoe visingizio. Hisia zako ni sababu tosha. Kwa mfano, kama hujisikii kufanya mapenzi lakini rafiki yako wa kike au kiume anakulazimisha, epuka kutumia watu wengine kama kisingizio. Usiseme, mama yangu karibu atarudi nyumbani au tumbo linaniuma au ninaogopa kupata mimba au nina kazi ya kusoma kwa hiyo sio muda mzuri kwangu. Unaweza ukamchanganya rafiki yako na visingizio hivi. Anaweza kudhani unataka kwenda sehemu nyingine, au kwamba labda unataka kutumia kondomu. Anaweza asitambue kwamba unachotaka kumwambia ni siko tayari kufanya tendo hilo kwa hiyo sitaki. Kwa hiyo basi sema kile unachotaka. Usisemewe na mtu mwingine. Iwapo hutaki kufanya jambo fulani, sema mwenyewe na usiulize mtu mwingine kama ni sawa. Kwa mfano, kama mtu ana kushawishi unywe pombe au madawa ya kulevya usiseme; nisingependa, lakini kama unaona sawa? Badala yake sema Hapana, ninashukuru

41 SURA YA 6 Utunzaji Afya Ya Akili Na Moyo Sihitaji kitu chochote. Waonyeshe kwamba unajua unachotaka, hivyo hutafuti kibali chao. Usibabaishwe na hoja za watu wengine. Endelea kurudia msimamo wako juu ya yale unayoyataka na usiyoyataka. Labda rafiki yako wa kike anaendelea kukulazimisha mfanye mapenzi na ana tumia hoja hizi: Hivi hunipendi?, Unajua nilifanya mapenzi na mvulana wangu wa zamani. Simama imara na usikubali. Mwambie mimi sio mvulana wako wa zamani. Mimi ni mimi. Sitaki kufanya mapenzi na wewe. Kumbuka, unayohaki ya kubadilisha mawazo. Labda wewe na rafiki yako mlizungumza kuhusu kufanya mapenzi siku chache zilizopita, na ulimwambia mtafanya mapenzi. Lakini umefikiria kiundani na unaona ni makosa kufanya hivyo. Iwapo atasema; Lakini ulikubali mwenyewe kwamba tungefanya mapenzi. Mwambie: Nimebadilisha mawazo. Siko tayari. Kama kweli anakupenda, ataheshimu maamuzi yako mapya na atasubiri mpaka utakapokuwa tayari. Kuwa na msimamo ina maanisha kuwa na uhakika na kile unachotaka Kuwa na stadi za maisha zilizojadiliwa katika sura hii,kujitambua,ushirikeli,kutatua matatizo kwa kufikiri, kwa ubunifu,stadi za makubaliano,kuwa na msimamo ni baadhi ya nguzo za afya ya hisia nzuri.ukizifahamu stadi hizi utakuwa salama na si ajabu utafanikiwa katika vitu vingi utakavyojaribisha maishani. Sura ya Sita Utunzaji Afya ya Akili na Moyo Kuwa na afya njema ya hisia ina maana zifuatazo: Kujisikia vizuri wewe binafsi. Ni kujipenda na kujiheshimu. Pia ni kujithamini. Kujikubali kuhusu uwezo wako. Unakuwa huna wasiwasi sana kuhusu udhaifu wako na huogopi kujaribu mambo mapya. Unakuwa unajiamini. Kuweza kukabili wasiwasi na mfadhaiko. Unakuwa huna wasiwasi na mwonekano wako, huna wasiwasi kwa vile eti huwezi vitu fulani, huna wasiwasi na maneno ya marafiki zako wala huna wasiwasi kwa vile tu huna mpenzi. Kukabili huzuni. Unajitahidi huzuni na hasira zisikutawale na kukukosesha matumaini. Kutambua hisia zako na sababu za hisia hizo. Unapojisikia vibaya (iwe hasira, uchovu, kukata tamaa) acha kufikiria hisia hizo na sababu zinazosababisha ujisikie hivyo. Kuelewa hisia na sababu wanazotoa watu wengine. Unajiuliza ingekuwa wewe ungefanyaje? Unakuwa mtu unayejaribu kuelewa wasiwasi, matatizo au mahitaji ya watu wengine. Huu ni uwezo wa kutambua hisia za watu wengine. Kutatua matatizo na kufikiri kiubunifu. Unakuwa na njia nyingi za kutatua tatizo linapojitokeza. Pia unatumia njia bora zilizojificha ambazo hutatua tatizo kwa urahisi zaidi. Kumweleza mtu mwingine kuhusu hisia zako, unachokitaka na sababu zako. Unapojaribu kusuluhisha tatizo au mgongano wa mawazo unakuwa ni mtu wa kujadili bila kumvunjia heshima mwenzio. Unatafuta suluhisho lenye manufaa kwa pande zote mbili. Unakuwa ni mtu wa mapatano. Unakuwa na msimamo wako. Unasisitiza unachokitaka na unachokihitaji. Unakuwa muwazi na mkweli kuhusu hisia zako. Unakataa kushurutishwa kwa kitu usichokitaka. Hisia njema ya mtu mmoja hujengwa na waliomzunguka. Kutakuwa na muda utahitaji ushauri na msaada toka kwa wengine- toka kwa wazazi, marafiki, walimu, wajomba, shangazi, kaka, dada, viongozi wa dini au mshauri nasaha. Kitu muhimu katika kujenga hisia njema ni kuweza kuomba ushauri unapouhitaji

42 SURA YA 7 Maelewano Na Wazazi Wako Vijana wengine wamebahatika kuwa na wazazi ambao wanaweza wakaelewana na kuzungumza mambo muhimu. Lakini vijana wengi wanashindwa kuelewana na wazazi wao hasa kipindi cha balehe. Mahusiano na wazazi wao yanaanza kuwa magumu. Wanaanza kushindana na kubishana katika kila kitu na wazazi wao. Wanajisikia kama wazazi wao wamepitwa na wakati na wana mambo ya kizamani. Wanajisikia kama wazazi wao hawawaamini na hawana imani nao. Gifty, kutoka Ghana (Umri, Miaka 14) Wazazi wangu wako huru na tunashirikiana katika matatizo yangu hivyo huwa nakubaliana nao. Kila mara wananifanya nijisikie mwenye furaha na wananishauri mambo mengi. Ninataka wazazi wawe na muda mwingi kwa ajili ya watoto wao. Ni vema wazazi wazungumze na watoto wao na kuwashauri kwa sababu watoto wanawategemea sana wazazi ili ndoto zao ziwe kweli. Cathy kutoka Uganda (Umri, Miaka 17) Ukali wa mama yangu na mabadiliko katika mwili wangu vilijitokeza pamoja. Alinikataza nisijumuike na makundi, wakati mimi ndio muda niliokuwa nahitaji sana makundi ili kuweza kubadilishana mawazo. Panaito kutoka kenya (Umri, miaka 14 ) Wazazi wangu mara nyingine walinizuia kuchanganyika na vijana wenzangu. Barlay kutoka Kenya (Umri; miaka 16) Wazazi wanajaribu kutufanya tuwe wazuri lakini mara nyingine huwa wakali. Wanatuchagulia marafiki, na kitendo hicho sikipendi

43 SURA YA 7 Maelewano Na Wazazi Wako Halima kutoka Kenya (Umri; Miaka 14) Mimi na wazazi wangu mara zote hatukubaliani kuhusu mimi kutoka nyumbani bila baibui (gauni nyeusi na mtandio wanazovaa wanawake wa Kiislamu), na baada ya kumaliza mtihani hawapendi mimi nitoke kila wakati. Bila kujali upande uliofungamana nao bado kuna mambo mengi unaweza kufanya ili kudumisha na kuboresha uhusiano na wazazi wako. Wakati mwingine inaweza kuwa kazi ngumu lakini ukidhamiria na kujituma jitihada zako zinaweza kufanikiwa, maelewano yatakuwa mepesi zaidi. KUTHAMINI FAMILIA Orodhesha mambo unayoyaenzi na kuyafanya. Pengine unafikiri kuwa ucheshi ni moja ya sifa zako nzuri. Pengine unapenda unavyotabasamu. Pengine unajisikia vizuri kuhusu kipaji chako. Pengine unajisikia vizuri kuhusu kipaji chako cha useremala au wepesi katika hesabu. Baada ya hapo, jaribu kufikiria wapi hivyo vipaji vilipotoka.. Kwa mfano, Ulijifunza wapi na toka kwa nani? Unaweza kubainisha baadhi ya tabia hizi kwa wazazi wako, shangazi zako, na wajomba au ndugu zako wengine? Je, ucheshi ni wa mama yako? Tabasamu ni la baba yako? Nani alikufundisha mambo ya useremala?n.k Mara nyingine ni rahisi kuingia katika malumbano na wazazi wako na ndugu wengine katika ukoo kiasi kwamba sio rahisi kuona ni kiasi gani umerithi toka kwao. Unapata matatizo ya kuona mambo mnayofanana kwa sababu ya tofauti za mtizamo, tofauti kuhusu jambo fulani. Mara nyingine unaweza kujisikia unaaibishwa na ndugu zako. Labda wazazi wako hawana fedha za kutosha, hivyo familia yako wanaishi katika chumba kimoja hata kukufanya uone aibu kuwaleta marafiki nyumbani. Ni muhimu kuthamini familia yako na kuikubali kama ilivyo tajiri au masikini. Lenga katika kile ambacho ndugu zako wameweza kukupatia, kuliko kile ambacho hawakuweza kukupatia. Kumbuka kuwa familia yako imefanya kazi kukufanya uwe ulivyo na utakavyokuwa. Familia yako pia imekupa maadili ya kukuwezesha kuishi kama unavyoishi. Hii haina maana ya kwamba uko sawa sawa na wazazi wako. Zinaweza kuwepo tofauti nyingi kati yenu kama kulivyo kufanana kwingi. Kwa kuongezea, kipindi cha balehe ndio muda ambao vijana wengi wanataka kugundua tofauti kati yao na wazazi wao. Wanataka kujitegemea, jambo ambalo ni la kawaida na zuri. Hata hivyo, kujitegemea siyo jambo rahisi. Ukweli linaweza kuwa vigumu sana kwako na hata kwa familia yako. FAHAMU YALE WAZAZI WAKO WANAYOYATAKA Unapojaribisha muonekano na tabia mpya na njia mpya za maisha, familia yako inaweza kuona shida sana. Watashangaa nini kimekupata, wapi umepata mawazo hayo ya ajabu? Wapi kijana wao wa kiume au kike amekwenda? Huyu kijana ni nani ambaye anapenda kutumia muda wake mwingi akiwa peke yake au kuzururazurura kwenye vijiwe? Inaweza kuwa vigumu kwa wazazi kutambua kuwa unakuwa mtu mzima unayeweza kufikiri mwenyewe na ambaye unayo maoni yako. Bado wanafikiria ungali mtoto. Kuwa mtulivu wakati wazazi wanajirekebisha kwa mabadiliko yako makubwa. Grace, kutoka Kenya (Umri; Miaka 14) Hatukubaliani mara nyingine kuhusu mavazi, kwa sababu wanasema suruali na jinzi ni kwa ajili ya wanaume. Lakini ninadhani kuzivaa ni salama kwangu kuliko kuvaa gauni na sketi. Hawataki pia nisuke rasta. Wanasema ni mtindo wa watu wabaya. Lakini mimi sifikirii hivyo nachukulia kama mtindo tu. Bernard, kutoka Kenya (Umri; Miaka 17) Mara nyingine mawazo yangu yanapingana na ya wazazi wangu. Kumbuka kwamba wazazi wako walikua kipindi cha zamani tofauti na wewe. Hata hivyo, kama wazazi wako wanafuata mila, waonyeshe angalao jambo jipya zuri. Wazazi wako ni kiunganishi cha utamaduni wa zamani na wa kisasa. Huu ni utajiri kwako. Unaweza kujifunza mengi kuhusu utamaduni kutoka kwa wazazi wako na wakubwa zako. Litakuwa jambo la kuhuzunisha kama utapoteza mambo haya: Lugha ya asili au lugha ya mama. Historia ya watu wako. Vifaa vya asili vya muziki, nyimbo na hadithi Ngoma za asili na upishi. Ingekuwaje kama usingejua hata moja kuhusu utamaduni wako? Ungelikuwa nani? Ungelikuwa upande gani? Jifunze kuhusu historia yako, utamaduni, mila, muziki, ala, na kucheza ngoma Bila kuwa na fikra ya utamaduni wetu na historia yetu tutapotea. Wahenga wetu, lugha yao, utamaduni na imani ni mambo muhimu ya utambulisho wetu. Usiyadharau! Bila shaka, utamaduni wa kisasa una mambo mengi mazuri - yale yanayofanya maisha yetu yaonekane bora kama elimu, madawa ya kisasa na mawazo mapya juu ya wajibu wa wanaume na wanawake. Kwa mfano, wasichana sasa wanayo nafasi zaidi katika elimu na kazi nzuri ukilinganisha na bibi zao. Mitazamo ya zamani kama kuamini kwamba wanawake na wasichana wanalazimika kukaa nyumbani kupika na kuangalia nyumba zinabadilika. Mtazamo kuhusu kuendeleza mila za ndoa katika umri mdogo nazo zinabadilika. Kwa sasa unaishi kipindi cha kusisimua. Mambo mengi yamewekwa wazi. Unayo nafasi ya kutosha kuchagua namna unavyotaka kuishi. Unaweza ukachagua mazuri kutoka kila upande mazuri ya utamaduni wa asili na mazuri ya utamaduni wa kisasa. Unaweza kuyakumbatia unayofikiri ni mazuri, na kuyakataa yale unayofikiri ni mabaya

44 SURA YA 7 Maelewano Na Wazazi Wako Kadri unavyojaribu kufanya maamuzi yako kuhusu yapi unayotaka kuishi nayo, kati ya kiasili na ya kisasa jaribu kuwa mwangalifu kuhusu hisia na imani za wazazi na wazee wako. Zungumza nao ili kujua misimamo yao. Waeleze hisia zako na kile unachowaza. KUMUDU MATARAJIO YA WAZAZI WAKO Wazazi wengi wanatarajia mengi kutoka kwa vijana wao. Wanataka uishi maisha mazuri kuliko walivyoishi, hivyo wanataka ufanye kazi kwa bidii zaidi, ufanye vizuri shuleni, na uwe makini zaidi! Mategemeo ya wazazi wakati mwingine yanaweza kuonekana kama mzigo mzito. Mara nyingine inakuwa kana kwamba wamelenga sana katika maisha yako ya baadaye wanayofikiria uwe nayo, kiasi cha kwambahawasikilizi mawazo na matakwa yako. Huenda baba yako anataka uwe daktari, lakini huna uwezo katika masomo ya sayansi. Au pengine mama yako anategemea wewe uoe na kuishi kijijini ulikozaliwa, lakini unataka uende Chuo Kikuu ukawe mwandishi wa habari. Hali ya namna hii inaweza kuwa ngumu. Wazazi Unataka kuwa mwalimu, nasema hapana atakuwa wako mara kwa mara wanadhani wakati wote daktari. Hivyo ndivyo nataka kijana wangu wanajua kipi kizuri kwako, hata kama hawajui. Inaweza kuwa vigumu kwao kutambua kwamba wewe ni mtu unayejitegemea mwenye kipaji chako, mawazo na ndoto zako. Wanaweza kuwa wanapata shida kutambua kati ya ndoto zako na ndoto walizonazo wao. Jaribu kuwa mvumilivu na kumbuka kwamba wazazi wako wanataka maisha yako kuwa mazuri. Endelea kuzungumza na wazazi wako. Waeleze kuhusu malengo na ndoto zako, na kwa nini unataka kufuatilia ndoto hizo. Waonyesha jinsi ulivyodhamiria. MAWASILIANO NA WAZAZI WAKO Halima, kutoka Kenya (Umri; Miaka 14) Mara nyingine wazazi wangu wananipa presha kubwa. Wanategemea nifanye kila kitu vizuri na nisifanye makosa yoyote. Wananitegemea niwe sahihi, jambo ambalo halitawezekana, kwasababu sisi sote ni binadamu ambao tunaweza kufanya makosa wakati wowote!. Kukosekana kwa mawasiliano ya wazi ndicho chanzo cha malumbano kati ya vijana na wazazi wao. Cha kushangaza ni kuwa inakuwa vigumu kukaa chini na kuwa na mazungumzo yenye manufaa kwa pande mbili. Wazazi wengi hupenda sana kuwasaidia watoto waoili wapite salama katika kipindi cha balehe lakini mara nyingi hushindwa namna ya kuwasaidia. Wanaogopa kuwaaibisha au kujiaibisha wao wenyewe. Huenda hata wazazi wao pia hawakuzungumza nao juu ya balehe na mabadiliko yote anayopitia kijana. Hivyo ni vigumu sana kwao kukusaidia wakati wao wenyewe hawakupata msaada wowote. Kama ilivyo kwako, wanaweza wasiwe na uzoefu mkubwa katika eneo hili au wasiyajue majukumu yao. Kwa vipi kijana anaweza kujifunza kuongea kwa uwazi na wazazi, shangazi, wajomba, babu na bibi au jamaa yeyote katika familia? Unajenga vipi Julia, kutoka Ghana (Umri: Miaka 22) Nilipoanza kuona mabadiliko mwilini mwangu, niliona vigumu kuyazungumza kwa wazazi wangu. Lakini kadri muda ulivyoenda nilijisikia huru zaidi na niliweza kuongea nao. Niliwauliza swali lolote nililotaka kuwauliza. Waonyeshe wazazi wako kuwa unajali kuwafurahisha uhusiano wakati wanapokuamini na hasa kama mlikuwa mnabishana muda mfupi uliopita? Utaanzaje kujenga uhusiano huo? Bila shaka hakuna jibu rahisi lakini hapa kuna vidokezo unavyoweza kujaribu: Waonyeshe wazazi wako kuwa unaweza kuwafurahisha. Jitolee kuwasaidia wazazi wako katika shughuli yoyote wanayoifanya jikoni, kuzunguka nyumba au bustanini. Wakati mnafanya kazi pamoja eleza suala lako unalotaka mlijadili. Anthony, kutoka Kenya (Umri: miaka 15) Njia bora zaidi kukabiliana na wazazi ni baada ya kuwa umefanya kazi fulani ya kuwafurahisha ndipo unapoweza kwenda kuongea nao jambo unalotaka. Chagua muda mzuri wa kuongea. Uchaguzi wa muda ndio kila kitu! Chagua muda ambao wazazi wako hawajachoka sana au wakati hawana shughuli nyingi. Yaweza kuwa vizuri kusubiri hadi mwisho wa wiki wakati wanapumzika na hawafikirii sana masuala ya kazi. Anza na mada rahisi. Anza na mada ambayo sio ya kutahayarisha kwako au kwao na ambayo hamtofautiani nao sana. Katika familia nyingi wazazi na watoto wao huanza kuongea pale tu kunapokuwa na jambo zito mfano wakati watoto wanapotaka kufanya kitu wasichopenda wazazi. Hapa ni mahali pagumu kuanzia. Unaweza kuanza kujaribu kuzungumza na wazazi wako juu ya hali au tatizo la rafiki yako kwanza kabla ya kwako

45 SURA YA 7 Maelewano Na Wazazi Wako Hii inaweza kuwapa wote wewe na wazazi wako hisia za kumthamini kila mmoja wenu na inaweza kusaidia kujenga uaminifu na uelewa juu ya hali isiyokuwa ya binafsi sana. Lakini usisaliti uaminifu wa rafiki yako, pia linda siri zake. Kwa mfano unaweza kuongelea tatizo la rafiki yako kwa wazazi wako, lakini usimtaje kwa jina huyo rafiki yako aliye katika hali ngumu. Waonyeshe wazazi wako kuwa unayajali mawazo yao. Waulize wazazi wako wanafikiria nini na kwa nini wanajihisi hivyo katika hali fulani. Jaribu kuelewa mtazamo na wajibu wao. Labda unadhani wazazi wako hawataki uende disko kwa sababu ni wakali. Lakini huenda kuna kitu wanakijua kuhusu disko ambacho wewe hukijui. Huenda wamesikia kuwa wasichana hubakwa huko au watu huuza madawa ya kulevya huko. Wanaweza kuwa na sababu nzuri sana ya kuhisi hivyo na wangependa uvutiwe na sababu zao na uyajali mawazo yao. Waulize wazazi wako nini wanafikiri na kwa nini. Wanaweza wakawa na sababu nzuri kuhusu mienendo yao. Uwe na heshima. Wazazi wako, ndugu zako na wakubwa zako wanajali sana suala la heshima. Hivyo hata kama unahisi kukatishwa tamaa, jaribu kutopiga kelele na kufanya wakuone huna heshima. Pia uwe na heshima kwa maadili yao. Wakati baadhi ya maadili yanaweza kuwa sawa na ya familia yako lakini mengine yaweza kuwa tofauti. Kama unataka kuishi katika maadili tofauti na ya wazazi wako ni sawa, lakini usiwakosee wazazi wako juu ya imani zao hata kama kwako zitaonekana kupitwa na wakati au kuwa za kijadi mno kwako. Jenga kuaminika. Waonyeshe wazazi wako kuwa unawajibika na kuwa wanaweza kukuamini. Wakikuambia kuwa uwe nyumbani wakati fulani, hakikisha kuwa unakuwa nyumbani wakati huo. Uwe muwazi kwao kwa kitu unachotaka kufanya na elezea sababu zake. Usijaribu kwenda disko kwa siri wakati umewaambia wazazi wako kuwa unaenda nyumbani kwa rafiki yako. Ukijaribu kuwadanganya huenda wakagundua na utakuwa umevunja imani yao kwako. Wazazi wako wanatakiwa kuheshimu mambo yako ya faragha. Lakini usitumie vibaya faragha hiyo kwa kuishi maisha ya siri na ya hatari. Wazazi wako pia wanatakiwa waheshimu uchanguzi wako wa marafiki lakini pia unahitaji kuwaonyesha kuwa unaweza kuchagua marafiki wazuri. Usijihangaishe na watu ambao hawakujali na ambao maadili yao kimsingi yanapingana na ya familia yako. Aloysious, kutoka Uganda (Umri: Miaka 19) Unatakiwa kufanya ulichoambiwa hata kama hupendi na usiwafadhaishe wazazi kwa kufanya vitu ambavyo unajua vita waumiza moyoni. Kwa kufanya yote haya utakapoongea nao hawatakukatalia lolote utakalowaambia. Uwe muwazi kwa wazazi wako. Kumbuka kuwa unabadilika haraka sana kiasi kwamba wazazi wako wanaweza kuhisi kuwa hawakuelewi vizuri. Ni wajibu wako kuhakikisha kuwa wanakuelewa. Ongea nao kuhusu ndoto zako, matarajio yako, na mahitaji yako ili wahisi kujiamini kuwa wanakufahamu wewe na unachokitaka. Shirikiana nao katika masikitiko na mashaka yako. Waulize wangekuwa ndio wenyewe katika nafasi yako wangefanyaje. Waruhusu wazazi wako wakutane na rafiki zako ili wajue ni nani unayekwenda naye matembezini. Kwa wazazi wako, watambulishe marafiki zako ili wajue kuwa wanaweza kukuamini. Wakati wazazi wako wanapohisi kuwa wanakuelewa vizuri, watajisikia vizuri zaidi wakikuamini. Itawasaidia kuanza kukukubali kama mtu unayeelekea ukubwani na kuacha kukuchukulia kama mtoto. Itasaidia pia wakuruhusu ufanye maamuzi mengi mwenyewe. Prisca, kutoka Kenya (Umri: Miaka 14) Njia nzuri ya kukabiliana na wazazi wako ni kuwaeleza matatizo yako na kuwaomba kama wanaweza kukusaidia. Ukiwaomba hawawezi kukataa kwasababu wana mapenzi na uelewa. Unaweza kupanga siku ya kukaa nao pamoja na kubadilishana nao mawazo juu ya vitu unavyotaka kuzungumzia kwa sababu hawawezi kukataa. Waonyeshe wazazi wako kuwa unawajali. Kama unavyotaka wao wakuonyeshe kuwa wanakupenda, ni wajibu wako kuwaonyesha kuwa unawajali. Wafanyie vitu vizuri kuonyesha kuwa unawapenda na unataka kuwafurahisha. Sherifan, kutoka Ghana (Umri: Miaka 15) Unatakiwa wakati fulani uwanunulie wazazi wako zawadi. Huwa wanafurahi sana. Ni vigumu sana kuelewana vizuri na wazazi wako, na kumudu ukali wao, kuyakidhi matarajio yao makubwa, na kuyakubali maadili yao ya kiutamaduni. Itachukua muda na subira kubwa. Lakini kila dakika itakuwa na thamani kwa juhudi kidogo utakayoifanya. Itakuwa ya thamani kwa sababu kuna wakati marafiki na wenzako hawawezi kukushauri kama wazazi wako. Gifty, kutoka Ghana (Umri: Miaka 14) Unapaswa uwaheshimu wazazi wako na uweke aibu kando. Uwaeleze wazazi wako matatizo yako kwa sababu ndio watu pekee wa kuwa na majibu kwa matatizo yako. Ongea na wazazi wako mara kwa mara

46 SURA YA 7 Maelewano Na Wazazi Wako VYANZO VINGINE VYA KUPATA MSAADA. Wakati mwingine kunatokea tofauti kubwa kati ya wazazi wako na wewe mwenyewe kuhusu mitazamo mbalimbali. Umejaribu kuzungumza nao lakini hukufanikiwa. Wanakataa kukusikiliza na tatizo linazidi kuwa zito. Kwa mfano, inawezekana wazazi wakasema kuwa wanataka kukuachisha shule ili wakuoze kwa mwanaume mzee. Umejaribu kuwaelezea umuhimu wa shule kwako. Umewaeleza kuhusu ndoto yako ya kuwa mwalimu na hawajakusikiliza. Jenifer, Kutoka Ghana (Umri: Miaka 17) Unapaswa kuwasaidia nyumbani katika chochote wanachokifanya. Katika kuwasaidia mambo yote haya mapenzi kati yako na wao yatadumu muda mrefu. Sura ya 7 MAELEWANO NA WAZAZI WAKO Ujana balehe ni kipindii ambacho vijana wengi inawawia vigumu kupatana na wazazi wao. Lakini sio lazima mara kwa mara iwe hivi. Yapo mambo mengi unaweza kuyafanya kuimarisha uhusiano na wazazi wako: Thamini familia yako. Ikubali familia yako jinsi ilivyo - tajiri au masikini. Tumia muda wako kufikiria kile ambacho familia yako imekupatia, kama vile nguvu ulizonazo, kuthaminiwa na vitu vingine vinavyokuhusu wewe mwenyewe. Usiangalie tu nini hawajakupatia. Elewa imani na vitu wanavyothamini wazazi wako. Wazazi wako walikua kipindi tofauti na wewe. Hata kama unafikiria wazazi wako wanafuata mila za kizamani, tafuta yaliyo mema. Jifunze kutoka kwao kuhusu historia yenu, mila na desturi, muziki na lugha. Kuna hali nyingi ngumu kama hizi ambazo huwezi kuzimudu peke yako. Unahitaji kumtafuta mtu mzima anayeweza kukusaidia. Kama unaona ni tatizo kuongea na wazazi, jaribu kumuuliza mtu mzima mwingine kwa ushauri na msaada. Kumbuka kwamba wazazi wanakutakia mema. Kumudu matarajio ya wazazi wako inaweza kuwa vigumu, hasa ikiwa matarajio ya ndoto zao na zako yanatofautiana. Zungumza na wazazi wako kuhusu malengo yako na kwa nini unataka kuyaendeleza. Waonyeshe kuwa unayo nia na unafanya kazi kwa bidii. Evans, kutoka Kenya (Umri: Miaka 16). Kama huwezi kuzungumza na wazazi wako kutatua tatizo au mabishano, unapaswa kuzungumza na ndugu wa karibu, mtu kama shangazi yako au mjomba ambaye atakusaidia wewe na kujua lipi zuri kwako. Jaribu kuzungumza na mtu mzima mwingine ambaye ni mpole, anayejali na unayemwamini mtu anayekufahamu, kama ndugu, kaka, mtu mzima au dada, mwalimu, rafiki wa familia, baba wa rafiki yako, kiongozi wa dini au afisa jamii. Mwombe akupe ushauri na akusaidie kuzungumza na wazazi wako kuhusu jambo hilo. Hata kama huna tatizo kubwa na wazazi wako, lakini unahitaji ushauri, unaweza kujikuta kuwa ni rahisi zaidi kuzungumza na shangazi, mjomba au ndugu. Wako watu wengi wanaokujali na wako tayari kukusaidia ukiwaomba. Kuwa mwaminifu na muwazi kwa wazazi wako. Angalia wakati mwafaka wa kuzungumza na wazazi wako. Wape nafasi ya kujua utakuwa mtu mzima wa namna gani. Waonyeshe kwamba ni mwaminifu na muwajibikaji. Waonyeshe wazazi wako kwamba unajali hisia zao na unataka kuwafurahisha. Waulize wazazi wako kwa nini wanahisi wanavyo hisi. Jaribu kuelewa tatizo lao. Waonyeshe kwamba unapenda na kujali wanachofikiria. Kuwa na heshima. Hata kama hukubaliani na wazazi wako, jaribu kutokuongea kwa sauti kali au kuwaonyesha ufidhuli. Kuwa mvumilivu kwa wazazi wako. Wape muda wazoee ukweli kuwa umeanza kuwa mtu mzima mwenye maoni na ambaye anayeweza kufikiri mwenyewe. Kuwa mvumilivu kwako binafsi. Kujenga mahusiano ya karibu na ya wazi na wazazi wako inachukua muda na ni kazi ngumu. Usivunjike moyo na kukata tamaa, uhusiano mzuri hauwezi kujengwa kwa siku moja. Mara nyingine, tofauti ya maoni kati yako na wazazi wako inaweza kuwa kubwa sana. Tafuta mtu mzima anayejali na unayemwamini shangazi au mjomba, mtu mzima, rafiki wa familia, mwalimu, kiongozi wa dini au afisa ustawi na omba ushauri. Pengine wanaweza wakasaidia kutatua tatizo ulilonalo dhidi ya wazazi wako

47 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Sura hii ianahusu urafiki na mapenzi. Kila mtu anahitaji urafiki ulio mzuri na kila mtu anahitaji kujisikia anapendwa na watu wengine. URAFIKI Marafiki wanachukua nafasi kubwa katika kutufanya sisi tuonekane kama tulivyo. Wanatufanya tucheke na wanatufanya tujisikie wenye furaha. Wanatufahamisha mambo mapya na mawazo mapya, wanakuza upeo wetu. Wanashiriki ndoto zetu na kujaribu kutusaidia kutengeneza mipango ya maisha ya baadaye. Marakifi zetu pia wanaweza kujibu maswali yetu mengi hasa katika kipindi cha ujana balehe na wanatusaidia tujisikie vizuri pamoja na mabadiliko kadhaa yanayotokea. Tukiwa na matatizo, wanatutia moyo na kutusadia kutatua. Wanatusaidia kututhibitishia tulivyo. Urafiki ni muhimu wakati wa balehe na katika maisha yote Naana, kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Marafiki zangu wengi walianza kuona mabadiliko katika miili yao karibia wakati huo huo nilipoyaona mimi. Kwa hiyo sikuwa na hofu nayo. Tulijadili mabadiliko na niligundua kwamba tuna matatizo yanayofanana. Grace, kutoka Kenya (Umri wa miaka 14) Marafiki zangu ni watu wazuri. Tunaheshimiana na kupendana kama dada na kaka. Wananipenda jinsi nilivyo na kama nimekosea wananiambia wazi namna ninavyotakiwa kufanya. Wengine wanafikiri ni vibaya kuwa na marafiki wa jinsi nyingine. Mawazo yao ni mazuri na tunayajadili, tunaweza kuomba ushauri kutoka kwao

48 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Gift, kutoka Ghana (Umri wa miaka 14) Marafiki zangu wananipenda na kuniheshimu sana kwa sababu mimi ni mwaminifu na ninawashauri kuhusu nini msichana anatakiwa kufanya. Unaweza kuwa na urafiki na watu wa jinsi moja au na watu wa jinsi tofauti. Seif, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 13) Ninao marafiki wa kike watatu. Tunakaa na kuongea au kusoma pamoja. Rafiki wa kike ni kama rafiki wa kawaida tu. Evans, kutoka Kenya (Umri wa miaka 16) Mimi na rafiki yangu wa kike tunasaidiana kazi za shule na kubadilishana mawazo kuhusu maisha na namna ya kujiheshimu mbele za watu wazima. Halima, kutoka Kenya (Umri wa miaka 14) Kuwa na rafiki mvulana au msichana maana yake ni kusaidiana na kufanya maamuzi pamoja. Vile vile kuzungumza kama kuna tatizo. Wavulana na wasichana wanaweza kuwa marafiki na wanaweza kuwa na urafiki bila ya kujamiiana. Wavulana na wasichana wanaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi ambayo hayahusishi ngono. Kwa hiyo tunapotumia maneno rafiki wa kiume na rafiki wa kike haina maana ya kwamba mahusiano hayo ni ya kufanya ngono. Anthony, kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Urafiki wetu sio wa kufanya ngono au kufanya kitu chochote kitakachotufanya tujute baadaye. Urafiki wetu ni wa kusaidiana kama marafiki na sio kitu kingine. Kwame, kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Watu wanafikiri rafiki wa kike ni mtu ambaye unahusiana naye kingono tu. Rafiki wa kike ni mtu ambaye unaweza kumwomba ushauri, mtu ambaye unaweza kushirikiana naye kwenye matatizo. Urafiki mzuri na wa nguvu unapendeza sana. Unakufanya ufurahi.unachangia katika kukua kwa hisia kwa sababu unakufundisha jinsi ya kuwa karibu na mtu. Urafiki mzuri vile vile unachangia katika kujiheshimu. Ukiwa na rafiki mzuri, unajisikia vizuri. Inapendeza kuwa na mtu ambaye unaweza kumweleza siri zako. Vile vile inapendeza kuwa na mtu anayejisikia vizuri kukueleza siri zake. Unaweza kushirikiana naye mawazo bila wasiwasi wa kuchekwa. Unaweza kushirikiana naye siri na kujua kwamba hazitatoka nje. Inapendeza kufahamu kwamba rafiki yako atakupenda na kukuheshimu hata kama hukubaliani naye kuhusu jambo fulani. Kupitia urafiki wa karibu, unaweza kujifunza jinsi ya kukubali au kukataa mambo tofauti. Unajifunza pia jinsi ya kuwa na nguvu za kutosha kutetea maoni yako. Kujiamini ni muhimu kwa maisha ya baadaye na kwa mahusiano na watu wengine. Ukweli ni kwamba marafiki wanakusaidia kujenga stadi nyingi muhimu ambazo unazihitaji ili kufanikiwa maishani. Stadi hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa: Kuwasiliana vizuri na kuwa muwazi kuhusu hisia zako na mawazo yako. Kusikiliza na kujua hisia za mtu mwingine na maoni yake. Kusaidia pale mtu anapokuwa na matatizo au anajisikia hovyo. Kujadili (kwa mfano, wewe na rafiki yako hamjakubaliana kuhusu jambo fulani, utahitaji kujadiliana na kuafikiana au kufikia mwafaka). Kushirikiana, kufanya kazi pamoja na kuwajibika kwa pamoja Kukubali na kuheshimu tofauti za maoni, imani na mazoea. (Kwa mfano, wewe na rafiki yako mnaweza msiafiki kuhusu jambo fulani. Ni sawa tu. Hasa urafiki unajengeka katika kipindi cha ujana balehe kwa sababu vijana wengi wanaona aibu kuongea na wakubwa. Iwapo wazazi wako wanafikiri kutumia muda wako na marafiki ni kupoteza muda, jaribu kuwaeleza namna marafiki zako walivyo muhimu kwako na kwa nini. Unahitaji marafiki. Urafiki mzuri na wa nguvu unachukua muda na bidii kuujenga. Hautokei usiku mmoja na huwezi kupata marafiki wa kweli kila siku. JINSI YA KUMTAMBUA MTU AMBAYE SI RAFIKI WA KWELI. Inaweza ikatokea wakati mwingine mtu ambaye ulifikiri ni rafiki akageuka kuwa rafiki mbaya. Kwa mfano rafiki anapotoa siri kwa watu wengine, au anaeneza uvumi wa hovyo kuhusu wewe, huyu hafanyi vile ambavyo rafiki wa kweli anatakiwa kufanya. Rafiki wa namna hii anaweza kukuumiza, lakini hayo ndiyo maisha. Jaribu kuzungumza naye na muombe aache kufanya kitu chochote ambacho kina kukasirisha. Kama rafiki yako haachi kukufanyia vibaya, kaa mbali naye. Kupoteza rafiki inasikitisha/inahuzunisha, lakini utapata rafiki mwingine aliye bora zaidi. Ayoo, kutoka Uganda (Umri wa miaka 15) Niliwapoteza marafiki zangu wote kwa sababu hawakuheshimu maoni yangu. Sasa ninaye rafiki wa kweli mmoja tu, lakini tunaheshimiana. Marafiki wanaweza kuwa chanzo cha shinikizo Hasa shinikizo la kundi-rika ambalo ni chanzo kikubwa cha wasiwasi kwa wazazi. Shinikizo la kundi-rika mara nyingi huwafanya vijana wafanye makosa, kama kunywa pombe, au madawa ya kulevya. Shinikizo la kundi rika linaweza kuwafanya vijana wajamiiane wakati kwa kweli hawapendi kufanya hivyo. Florence, kutoka Ghana (Umri wa miaka 16) Ninapata shinikizo kutoka kwa wasichana wengine wanapojipamba na wanapotoka na kwenda kwa wavulana. Ninajishauri mwenyewe nisionyeshe tabia mbaya au kufanya mambo mabaya

49 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Katika kipindi cha ujana balehe, ni jambo la kawaida kuona vijana wakiwa katika makundi ya kirafiki, wakilazimika kufanya mambo fulani fulani katika kundi hilo au kuwa na mtazamo fulani kama unataka kujiunga au kubaki katika kundi hilo.. Jihadhari na shinikizo la kundi rika kwani lina nguvu sana kwa sababu unataka kupendwa na unataka kuwa sehemu ya kikundi; na unataka kuwafurahisha marafiki zako ndani ya kikundi na unataka kuhakikisha hubaki nyuma. Wakati wote hakikisha akili yako iko sawasawa na unakuwa mkweli. Usijihatarishe ati kwa sababu unataka kuwa na kundi la marafiki. Jambo jingine la kukumbuka: Unaweza ukatokea wakati fulani kipindi cha ujana ukajisikia kama vile huna marafiki wa karibu. Hii inaweza kukufanya ujisikie mpweke, mwenye huzuni na wasi wasi. Usihofu kuwa una tatizo lolote. Inawezekana wewe umekomaa kidogo kuliko wenzako wa umri mmoja. Labda unataka mambo tofauti na rafiki zako wa rika moja. Jinsi utakavyo kuwa unakua na kukutana na watu wapya, utatengeneza marafiki wazuri na wa nguvu. Kuwa mvumilivu. Ipo siku.! KUELEWANA NA JINSIA NYINGINE Vijana wengi wanapata shida kuelewana na mtu wa jinsi nyingine. Hawajui jinsi ya kutendeana kwa heshima na inavyofaa, na hawajui wafanye nini wanapokuwa wamezungukwa na watu wa jinsi nyingine. Vifuatavyo ni vidokezo kwa wavulana: Usimwangalie au kumpigia mlunzi msichana kwa sababu ya jinsi anavyoonekana, gauni alilovaa au namna anayotembea. Msikilize rafiki yako wa kike anachosema na elewa anaposema hapana ana maanisha Hapana na sio vinginevyo. Usijaribu kujishawishi mwenyewe kwamba anamaanisha labda au ndio wakati anaposema hapana. Usipitepite karibu na msalani wa wasichana na/au kuziba njia yao. Usiwanyanyase au kuwatisha kwa makusudi wasichana usiku au sehemu zisizo na watu. Usivumishe mambo mabaya kuhusu wasichana. Wasichana vile vile wanaweza kuwa na mtazamo mbaya kwa wavulana. Vifuatavyo ni vidokezo vya jinsi ya kuelewana na wavulana: Usiwatafute wavulana ili upate pesa au zawadi kutoka kwao. Wakati mwingine vijana wa rika lako wanaweza kukutenga kwenye kundi lao. Hii inaweza kuwa vigumu na unaweza kufikiri ufanye lolote ili ujiunge nao. Kuwa mkweli na usijihatarishe kwa ajili ya kupata heshima yao. Kubali kwamba wavulana nao wanashawishika na wanazo hisia kama zako. Usiwacheke, kuwatania au kuwafanyia mzaha. Kuwa muwazi kwa wavulana. Yaweke wazi yale unayotaka kuyafanya na yale ambayo hutaki kuyafanya. Sema yale ambayo kweli unayafikiria na usiogope kujieleza. Kuwa na uhakika, jiamini, kama hutaki kufanya jambo fulani sema HAPANA na ng ang ania hivyo hivyo. Usianzishe uzushi kuhusu wavulana. Mara nyingi wasichana na wavulana wanaishia katika mahusiano mabaya kwa sababu hawana uelewa na uzoefu wa namna ya kuishi na jinsia nyingine. Wavulana hawajui wasichana wanataka nini kutoka kwa wavulana na wasichana vile vile hawajui wavulana wanataka nini kutoka wasichana. Hapa kuna vidokezo vichache vitakavyokusaidia: Wasichana wanataka upendo, kujaliwa, uaminifu na heshima. Wasichana wanapata hofu kama wavulana hawawaheshimu. Wanapenda wavulana wanaotumia muda kuwasikiliza bila mzaha. Kuwa pamoja: Wasichana wanaona kwamba kuwa pamoja na kujumuika na wavulana kunafurahisha na kusisimua. Pia wanawapenda wavulana ambao wanaweza kuwasaidia wanapopata matatizo na ambao wanaweza kustarehe, kutaniana na kucheka nao. Uhuru: Wasichana wanataka kupewa nafasi ya kufikiri wenyewe.wanawapenda wavulana wanaotambua kwamba wasichana wana akili na wanapenda kuzitumia. Wavulana wanaojiamini: Wasichana wanawahusudu wavulana ambao wanajiamini na ambao hawawaogopi wasichana. Wavulana wasiojifanya: Wasichana wanawapenda wavulana ambao hawaigi wengine na kujifanya wana hali fulani kumbe sio. Wavulana wanataka nini? Wavulana wengi wanayataka yale yote ambayo wasichana wanayataka katika mahusiano. Wavulana wanataka upendo, kujaliwa, uaminifu na heshima. Wavulana wengi wanapenda kuwa na msichana anayejali na kusaidia mtu anayesikiliza, aliye na heshima na asiye na mzaha Kuwa pamoja: Kila mtu anapenda kujumuika. Wasichana na wavulana pia wanataka mtu ambaye wanaweza kutumia muda naye kucheka, kusimuliana hadithi na kuzungumza kuhusu maoni yao, ndoto na hata malengo. Uhuru: Wavulana wengi wanasukumwa kutenda mambo kinguvu. Wanatenda kama vile hawana hisia na hawajisikii kitu. Wanataka mtu ambaye wanaweza kushirikiana naye kimawazo na kihisia. Wasichana wanaojiamini: Tofauti na ambavyo wasichana wengi wanavyoamini, wavulana wanawapenda wasichana wanaojiamini wasichana ambao hawaogopi kujieleza wenyewe kwa uhuru. Wasichana wasiojifanya: Wavulana wanawapenda wasichana ambao ni halisi - wasichana ambao hawaigi mambo ya wengine kama kukomaa, kujisikia au kuringa. Msingi wa mahusiano mazuri ni urafiki wa nguvu sio tu jinsi mtu anavyoonekana au mvuto wa kimapenzi. Katika uhusiano mzuri, hakuna mtu anayejaribu kumdhibiti mwenzake au kumlazimisha katika kufanya mambo. Pia hakuna mtu ambaye anamnyonya mwenzake au kumtumia mwenzie kwa namna yoyote ile. Kumbuka kuwa mahusiano mazuri na ya kudumu hayaji katika muda mfupi. Inachukua muda kufahamiana kikweli kweli na kujenga urafiki wa nguvu. KUANZA MAHUSIANO NA MTU UNAYEMPENDA. Ujana balehe ni wakati ambao unaweza kuanza kujisikia una hamu au unavutiwa na watu wengine. Unaweza kumuona mtu shuleni kwako ambaye anaonekana mzuri na unafikiria ungependa muwe marafiki

50 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Lakini huna uhakiki utamuanza namna gani. Hujui kama atapendelea kuwa rafiki yako. Unachokijua ni kuwa anaweza asiwe amegundua nia yako. Prisca, kutoka Kenya (Umri: miaka 14) Njia nzuri ya kumwendea msichana au mvulana ni kumwendea kwa upole. Njia nzuri ya kuanza urafiki ni kwa kumjali rafiki yako na kusaidiana naye nyakati za matatizo. Mercy, kutoka Ghana (Umri: miaka 16) Kitu cha kwanza cha kufanya ili kuanza urafiki ni kuwa rafiki wa mtu huyo na mkishafahamiana vizuri unaweza kumuambia kilichoko kichwani au moyoni mwako kwa kuzungumza na kufungua hisia zako. Ni vigumu kumwendea mtu mpya hususani kama unampenda kimapenzi. Unaweza kuogopa kumwendea msichana au mvulana kwa sababu hutaki kukataliwa na kuumiza roho yako.kwa upande mwingine iwapo hutamfuata mtu huyo hutakuwa na mahusiano ya aina yoyote na mtu huyo kabisa. Kuna njia mbili za kujua kama mtu anakupenda na ana hamu na wewe. Unaweza kuzungumza naye wewe mwenyewe au unaweza kumwomba rafiki yako aongee naye. Iwapo utachagua kumpata rafiki wa kumwendea mtu unayempenda, kuwa mwangalifu kuchagua rafiki mzuri - mtu ambaye anaaminika sana. Usingependa kumchagua rafiki ambaye ataishia kuwaeleza watu wengine kwamba unampenda mtu fulani. Vile vile usingependa kumchagua rafiki ambaye ataongea maneno mengi na yule mtu. Kwa mfano unaweza kutaka rafiki yako ataje jina lako tu kuona kama yule mtu anakujua wewe ni nani na kama ana nia na wewe. Ujana balehe ni wakati ambao utaanza kujisikia kuvutiwa na watu wengine Kama unavutiwa na mtu, onyesha urafiki na kuwa mkweli. Tafuta nafasi ya kukutana nae. Ni sawa kabisa kumuomba rafiki yako kumuendea mtu unayempenda, lakini itafikia wakati ambao utalazimika kuongea naye wewe mwenyewe. Hii inaweza kukuwia vigumu.unaweza kuona aibu. Mikono inaweza kulowa jasho. Unapoanza kuzungumza unaweza kusahau kabisa ulichotaka kusema. Haya yote ni hisia za kawaida kwa mtu anapokuwa na hali ya wasiwasi au ya kusisimka. Jaribu kutulia na kujikumbusha kwamba wewe ni mtu unayevutia unayefurahisha na mwenye akili. Huna cha kupoteza. Kuwa mwema kwa mtu unayempenda. Anza mazungumzo naye. Tafuta anapendelea nini na nenda ukamwone. Iwapo msichana au mvulana ni mwema, chukua hatua inayofuata. Mweleze ungependa mfahamiane zaidi. Muulize kama anaweza kwenda kufanya kitu na wewe. KUJENGA MAHUSIANO YENYE NGUVU Zipo njia nyingi za kumuelewa mtu vizuri na kujenga urafiki wa karibu na mahusiano mazuri. Mnaweza kwenda kutembea naye, kwenye sherehe, kuangalia sinema au kunywa na kula pamoja. Mnaweza kucheza michezo na mnaweza kujihusisha katika shughuli za kijamii au za kidini pamoja. Mnaweza kusoma pamoja. Mnaweza kutumia muda pamoja mnapokuwa kwenye kikundi cha marafiki. Kama lengo lako ni kumuelewa mtu vizuri na kujenga mahusiano ya karibu na ya kudumu, mkifanya shughuli mbalimbali pamoja, ni vizuri zaidi kuliko kujamiiana tu. Ukweli ni kwamba kuanza kujamiiana kabla mahusiano hayajawa ya karibu na yenye nguvu kunaweza kuharibu mahusiano. Au mahusiano yenu yanaweza yakawa ya kujamiiana tu. Kumbuka ngono na upendo ni vitu viwili tofauti. Kujamiiana hakumaanishi watu wawili hawa wanapendana. Sherifan, kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Unapofanya ngono, haina maana mnapendana. Mtu anaweza akawa anakutumia, kwa sababu unapendeza na unamvutia, lakini sio kwa sababu anakupenda. Hamson, kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Ngono na kupenda havifanani. Ukilala na msichana haina maana kwamba msichana huyo anakupenda. Watu wengi wanafikiri ngono inafanya mahusiano yawe na nguvu, lakini hii sio kweli.ngono sio njia nzuri ya kuweka mahusiano, na wakati mwingine inaweza kuharibu mahusiano kabisa. Okakah, kutoka Kenya (Umri wa miaka 17) Mmoja wa marafiki zangu wa karibu aliniambia kwamba ningempoteza rafiki yangu wa kike kama nisingemridhisha kimapenzi. Kwa kweli hili lilinipa dukuduku sana kwa hiyo nilianza kujaribisha naye, hata kama hakuwa katika hali ya kutaka. Hili lilinifanya niwe na dukuduku zaidi. Nilimwuliza kwa nini alikuwa katika hali hiyo. Alinieleza kwamba kufanya mapenzi kungesababisha mimba isiyotakiwa na kama ikitokea tungepoteza hadhi yetu katika jamii. Mwishowe tuligundua kwamba wapenzi wanahitaji kuheshimiana na kuelewana, na wanahitaji kupuuza shinikizo kutoka kwa vijana wengine

51 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Marafiki wa Okakah walimwambia kwamba angempoteza rafiki yake wa kike iwapo asingefanya naye ngono, lakini ukweli ni kwamba ilikaribia kumpoteza rafiki yake wa kike kwa kumwambia wafanye ngono! Alichokuwa anaambiwa na rafiki zake haikuwa kweli. Kumbuka, watu wawili wanaweza kuwa na mahusiano ya karibu sana bila ya hata kufanya ngono. Wanaweza kubadilishana uzoefu; wanaweza kujifunza mambo mengi ya muhimu kuhusu kila mmoja wao jinsi kila mtu anavyoona maisha, jinsi watakavyofanya maamuzi pamoja, kila mmoja atakuwa mwenzi na mzazi wa namna gani na namna kila mmoja anavyoiona mipango ya maisha ya mwenzake. Yote haya ni muhimu kabla hujaanza mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote. Mnatakiwa kwanza muwe marafiki wa kweli. Ngono bila urafiki wa kweli wakati wote ni hatari kwa afya yako na kwa moyo wako. Unaweza kuumia. Kwa hiyo kwa ajili ya mahusiano yenye afya na afya ya ujinsia kuweni marafiki wa kweli kwanza. MAPENZI Ni vigumu kutafsiri mapenzi kwa sababu yanahusu hasa hisia. Mapenzi ni kitu kikubwa na kuna aina mbalimbali za mapenzi. Mapenzi kwa wazazi na marafiki, mapenzi kwa rafiki wa kiume au wa kike na mapenzi kwa jamii. Vile vile mapenzi ni hisia ngumu, na watu wanaweza kueleza maana ya mapenzi kwa njia tofauti kutegemeana na uzoefu wao na mahusiano yao ya kupenda. Mapenzi ni hisia yenye utata na watu hutoa tafsiri ya mapenzi kutegemeana na uzoefu wa mahusiano ya kimapenzi. Godfrey, kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 19) Siwezi kuyaelezea mapenzi. Ni vizuri sana kuwa katika mapenzi. Patrick, kutoka Ghana (Umri wa miaka 16) Mapenzi ni muungano wa watu wawili ukiwa na sanaa ya kuelewana na kuwa mwaminifu kwa kila mtu. Sherifan, kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Mapenzi ni kitu ambacho kipo kati ya watu wawili. Aidha mvulana au msichana. Mapenzi ni kushirikiana katika matatizo na kujaliana. Stabisile, kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 19) Kuwa na mpenzi ni mojawapo ya vitu vizuri duniani. Jennifer, kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Mapenzi ni wewe, familia yako na marafiki kushirikiana mawazo pamoja. Hivi ndivyo ninavyofahamu kuhusu mapenzi. Kuwa na mpenzi kunaweza kuwa kama uchawi. Unakutana na mtu maalumu halafu kila kitu kinabadilika. Jua linaonekana kung ara zaidi, nyasi zinakuwa za kijani zaidi na unajiona kama unatembea hewani. Kuwa na mpenzi ni tofauti na kumpata rafiki mpya. Unapokuwa na mpenzi, unaweza kujisikia joto, na hisia zilizojaa. Unaweza kujisikia kutabasamu kila wakati kwa sababu mawazo ya yule unayempenda yanakufanya uwe na furaha. Unataka kuwa na mtu huyu kila wakati. Unapata njozi za mchana za tamaa ya mambo yasiyowezekana kuhusu mtu huyo. Kuna wakati unaweza kupoteza hamu ya kula au kukosa usingizi usiku. Sherry, kutoka Ghana (Umri wa miaka 19) Ni jambo la ajabu. Huelewi kinachokupata. Huwezi kuelezea. Unajaribu kuacha kumfikiria lakini unagundua mawazo hayawezi kutoka. Unaweza ukawa unasoma kwa ajili ya mtihani lakini unaona akili yako haiendani na macho yanavyoangalia ukurasa wa kitabu. Sara, kutoka Uganda (Umri wa miaka 18) Nina miaka 18 na yupo mvulana ninayempenda sana. Anapokuwa mbali na mimi, ninashindwa kuwa makini na kitu chochote. Anapokuwepo karibu na mimi ninatetemeka na siwezi kufanya kitu chochote cha maana,hata kama akiniambia nijifanye kama hayupo. Hisia hizi zinanifanya nichanganikiwe kabisa. Angela, kutoka Kenya (Umri wa miaka 18) Inasisimumua kuwa katika mapenzi.hutaki kumuumiza.unajisikia mpya kama vile kitu kimeongezeka.wakati mwingine kujisomea inakuwa matatizo.akikuandikia barua,itasomwa kwa masaa. Penzi la kwanza ni mojawapo ya uzoefu mzito wa maisha. Kuwa na mpenzi sio sawa na uzoefu wowote ulioupata ukiwa mtoto. Ni kitu ambacho unatakiwa kukichukulia taratibu. Usikimbilie. Tunza moyo wako na wa wale unaowapenda wachukulie kwa uangalifu. Diana, kutoka Zambia (Umri wa miaka 17) Ninafikiri kuwa mapenzi yaje kikawaida kuliko inavyotokea kwa vijana ambao wanaenda kutafuta mapenzi badala ya kuacha mapenzi yawatafute. Watu wanatakiwa kuangaliana kwa njia chanya. Mapenzi yanaweza kupatikana bila kulazimisha ili usije ukajuta baadaye

52 SURA YA 8 Urafiki Na Mapenzi Kama una mapenzi ya kweli na mtu, mtaheshimiana. Hamtafanya kitu chochote kitakacho muumiza mmoja wenu. Hutamlazimisha mwenzako kufanya kitu chochote ambacho hakipendi. Utataka awe na furaha. Linganisha mapenzi yako na pointi hizi:- Mapenzi yanakufanya wewe na unayempenda kujisikia vizuri mwenyewe na kila mmoja wenu. Mapenzi ni uaminifu, kujaliana na ukweli. Mapenzi ni heshima na hadhi Mapenzi hayaruhusu mtu mmoja kumtumia mtu mwingine. Cathy, kutoka Uganda (Umri wa miaka 17) Hisia zangu haziji kwa haraka. Hii ni kwa sababu wakati wote ninataka kumjua mtu ambaye ananivutia vizuri zaidi. Ninazionyesha hisia zangu baada ya kuridhika kwamba hayupo kunitumia bali kwa mahusiano ya kweli. Mapenzi hayaweki ngono mbele kabla ya urafiki na kamwe mapenzi yasiwe sababu ya kufanya ngono isiyo salama. Mapenzi ya kweli yanahusisha hisia ya kuwajibika na kujihusisha kwa watu wengine. Ni hisia inayotafuta mambo mazuri kwa ajili ya mtu mwingine. Mapenzi hayakasirishi, yana uvumilivu wala hayana maana ya kushikanashikana. Mapenzi hayana kinyongo. Watu wengine wanadhani wivu ni dalili ya mapenzi, Si kweli; wivu ni dalili ya kutojiamini na kutoamini kuwa unajali. Unadhani lazima ni mapenzi yanakupa kiwewe! Lakini unapomfahamu mvulana au msichana huyo, hisia zinatoweka ghafla, na hujisikii kuvutiwa tena na mtu huyo. Hivyo ilikuwa kupumbazika. Kupumbazika hakuna ubaya na ni kitu cha kawaida tu. Ukweli ni kwamba vijana balehe wengi hupumbazika. Kupumbazika kunaweza kusisimua, kufurahisha na hatari isiwepo, kupumbazika hakugeuki kuwa mahusiano. Unaweza ukawa umepumbazika na mtu na usitake kuwa na mahusiano naye. Unaweza kufurahi kwa kumtamani kwa mbali. Hiyo ni sawa tu. KUACHANA KIMAPENZI Naana, kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Ninafahamu kwamba unapompenda mtu unafanya kile kilicho kizuri sana kwa ajili yake na kuwa na yale yote yanayompendeza moyo wake. Lakini sijawahi kumpenda mtu. Ninaweza kusema nimewahi kuwahusudu baadhi ya wavulana, lakini kamwe sijawahi kupenda. Sio kila mapenzi hudumu daima. Hisia za kupenda zinaweza kutoweka haraka kama zinavyokuja, lakini vile vile zinaweza kuwa za kweli na zenye nguvu. Wakati mwingine, jinsi mnavyokua watu wazima wewe na rafiki yako mnaweza mkajikuta mmeachana. Ndoto zenu zinawachukua njia tofauti. Mtajikuta yale mnayopendelea yamebadilika na mnakosa cha kuzungumza. Hamcheki tena pamoja kama mlivyozoea. Sio vizuri kwa afya yako kihisia kuwa katika mahusiano wakati hakuna mapenzi. Inahuzunisha na inaweza kuwa vigumu hususani kama mmoja wapo bado ana hisia za kupenda wakati mwingine hajisikii kabisa. Iwapo unataka kuvunja mahusiano, kuwa mkweli kuhusu sababu zinazofanya kuvunja mahusiano. Vile vile kuwa na huruma na mfikirie rafiki yako. Jaribu kutomuumiza, lakini wakati huo huo maliza mahusiano hayo usimwache aendelee kutegemea au kufikiria kwamba utabadilisha mawazo yako. Wivu si dalili ya mapenzi. Ni dalili ya kutojiamini. Hata hivyo wakati mwingine wivu ni dalili ya matatizo makubwa zaidi. Kwa mfano, wivu ni dalili ya kuwa mtu anataka kumdhibiti mtu mwingine. Mahusiano mengi ya unyanyasaji (wanaume wanapiga wake zao au wanaume wanaobaka marafiki zao wa kike) wanaanza na tabia ya wivu, ambayo hujengeka kuwa mbaya. KUPUMBAZIKA Wakati mwingine inakuwa vigumu kufahamu kama mapenzi yenu ni ya kweli. Moyo unadunda na unajisikia kukosa pumzi na kizunguzungu unapomwona mvulana au msichana fulani. Iwapo rafiki yako atakuacha, inaumiza sana. Ni vigumu kuacha kufikiria kwamba labda atabadilisha mawazo kukurudia. Inaweza kuwa vigumu kuamini kwamba hakupendi tena. Unaweza kujisikia mpweke sana na uliyekataliwa. Jipe muda wa kumudu maumivu.usikimbilie kutafuta mahusiano mapya na mtu mwingine ili ujisikie nafuu. Hata kama utakasirika na kuumia usimlaumu mtu mwingine na kamwe usieneze uvumi au hadithi mbaya kuhusu mwenzi wako wa zamani. Hizi sio njia nzuri za kuchukua kwa mtu aliye komaa. Kupoteza marafiki na kupata marafiki wapya ni sehemu ya maisha. Hatimaye utapata mpenzi wa kweli ambaye mtaishi naye, hivyo vumilia. Kwa wakati huu lenga katika kuwa mtu mwenye huruma na anayependeka. Ukijipenda, ni rahisi kupenda watu wengine na wewe mwenyewe kupendwa

53 Sura ya 8 Urafiki na mapenzi Urafiki mzuri na mahusiano mazuri yanakusaidia ujisikie vizuri. Marafiki wazuri wanakusaidia kutatua matatizo, kukuonyesha mawazo mapya na kushiriki na wewe katika ndoto za maisha yako ya baadaye. Wakati mwingine watu unaofikiria ni marafiki zako wanaweza kukushinikiza kufanya jambo ambalo hulitaki, kama vile kujamiiana au kula madawa ya kulevya. Hii tunaita shinikizo la kundi rika. Mtu yeyote anayekushinikiza ufanye jambo ambalo hutaki kulifanya sio rafiki mzuri. Usiruhusu mtu yeyote akakushinikiza ufanye jambo ambalo unajua ni makosa na ni hatari kwako. Marafiki wazuri wanaweza wakawa wa jinsi moja au jinsi nyingine. Wavulana na wasichana wanaweza kuwa marafiki bila ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Maneno rafiki wa kiume au rafiki wa kike sio lazima yamaanishe kwamba mahusiano ni ya kimapenzi. Marafiki wa jinsi tofauti wanaweza kuwa na urafiki wa karibu na kupendana sana bila ya ngono. Inaweza ikawa vigumu kuelewana na mtu wa jinsi nyingine kwa sababu wavulana na wasichana hawana uhakika nini mwingine anataka katika mahusiano. Kumbuka, watu wengi wavulana na wasichana wanataka mambo yanayofanana katika mahusiano. Wanataka heshima, uaminifu, ukweli, kuelewana na kujali. Kama unamtaka msichana au mvulana unayempenda, jaribu kuvuta subira na kuwa mkweli. Kuwa mwema. Toka, nenda ukamwone. Kama anaelekea kupenda nia yako, mwombe kama mnaweza kwenda kushiriki shughuli fulani kwa pamoja. Kujenga mahusiano mazuri kunachukua muda na uvumilivu. Ngono sio njia nzuri ya kujenga mahusiano. Ukweli ni kwamba ngono inaweza kuharibu mahusiano. Kujamiiana haina maana ya kwamba watu wawili wanapendana au urafiki wao ni wa karibu sana. Ngono bila urafiki wa kweli ni hatari kwa afya yako na moyo wako. Kumpenda mtu ni jambo nzuri sana, mapenzi yanakufanya ujisikie vizuri mwenyewe na mtu mwingine. Furahia hisia lakini usikimbilie jambo lolote. Kumbuka mapenzi yanahusu heshima na kujaliana. Mapenzi hata siku moja yasiwe sababu ya kufanya jambo ambalo litaweka afya na maisha yako ya baadaye hatarini. Mapenzi hayawezi kuwa kisingizio cha kufanya ngono isiyo salama. Mahusiano hayadumu milele. Kama ukiachwa, sio vizuri kulazimisha mahusiano. Kuwa mkweli kwa rafiki yako, lakini kuwa na huruma na umfikirie pia. Jaribu usiumize hisia zake. Kama mtu amekuacha, unaweza kuhuzunika sana na kujisikia mpweke. Lakini usikate tamaa. Siku moja utampata mtu mwingine sahihi wa kumpenda. Jipe muda wa kustahimili ulichopoteza. Usikimbilie mahusiano mapya na usieneze uzishi kuhusu mtu huyo. Ujinsia Na Ngono Kuna utata mwingi sana kuhusu neno ujinsia (sexuality) na kujamiiana. Watu wengi wanafikiri ujinsia maana yake ni kujamiiana. Wengine wanafikiri kwamba huwezi kuwa binadamu hai mwenye ujinsia na mwenye hisia za kimapenzi hadi uanze kujamiiana. Imani hizi si za kweli; kila mtu anao ujinsia tangu kuzaliwa hadi kufa. Kuwa na ujinsia kunaweza kumaanisha: Kujisikia unavutia na mwili wako umejengeka vizuri. Kujisikia mwenye hisia za kuwa karibu na mtu fulani. Kufurahia kuguswa na kukumbatiwa. Kujishika mwili wako mwenyewe. Kuvutiwa na mtu mwingine. Kufikiria hadithi za kimapenzi akilini mwako. Kuwa na mawazo au hisia za kimapenzi. Wakati wa ujana balehe ndio muda ambao unaweza kuutambua zaidi ujinsia wako - unavyojisikia, unavyofikiri, unavyojiheshimu kama mvulana au msichana, na unachokitaka kuhusu uhusiano wa karibu au pendo la mtu. Ulipokuwa mdogo pengine hukufikiria kuhusu mambo haya lakini wakati wa ujana, unaweza kuanza kufahamu maana ya kuwa mwanaume au mwanamke. Pia unaweza kuanza kuvutiwa na watu wengine na kuanza kuona hisia za kimapenzi, matamanio na ndoto. UNAJUA maana ya Ujinsia? Ujinsia ni suala lenye utata kueleweka. Ni zaidi ya kujisikia hisia za kimapenzi au kujamiiana. Ujinsia ni pamoja na: Kufahamu na kuwa na hisia kuhusiana na mwili wako na miili ya watu wengine. Uwezo wako na nia ya kuwa karibu na mtu mwingine. Uelewa wako kuhusu nini maana ya kuwa mwanamke au mwanaume. Hisia za mvutano wa kijinsia na watu wengine. Uwezo wako kimwili wa kuzaa. Ujinsia ni muhimu, unafurahisha, na ni sehemu ya asili ya kuwa mtu. Lakini wakati mwingine watu wanatumia ujinsia wao katika namna isiyofaa kwa kushawishi, kuamuru au kutania watu wengine. Hii ni pamoja na kuonyesha mapenzi kwa mzaha, upotoshaji na unyanyasaji kijinsia kama kubaka/kunajisi n.k. Usitumie ujinsia kama kifaa cha kupata kitu au kunyanyasa au kumuumiza mwingine. SURA YA

54 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono Haya ni mabadiliko ya kufurahisha, lakini yanaweza vile vile kukupoteza hasa kwa kuwa kuna miiko mingi kuhusu ujinsia na jinsia. Kwa mfano, watu wengine wanafikiri kwamba kuwa na hisia ya mapenzi ni dalili kwamba lazima wajamiiane, lakini hii si kweli kwani hisia za kimapenzi ni sehemu ya kuwa binadamu. Kila mtu anahisia za kimapenzi. Sura hii inahusu ujinsia na jinsi watu wanavyoonyesha hisia za kijinsia. Kuna mambo mengi unahitaji kuyajua ili uweze kufanya maamuzi mazuri kuhusu ujinsia na ngono/kujamiiana. UJINSIA WENYE AFYA NJEMA Kuwa mtu mwenye afya njema kijinsia inamaanisha kuwa na uwezo wa kuonyesha hisia zako katika njia ambazo hazikuhatarishii wewe au mtu mwingine. Yaani huhatarishi hisia na afya yako na wala huhatarishi hisia za watu wengine na afya zao. Kama kijana balehe, unaweza kuanza kulifanyia kazi jambo la kuwa kijana mwenye afya njema ya kijinsia. Unaweza kuhakikisha unajibidiisha kujua kadri iwezekanavyo tofauti kati ya ukweli na uongo inapokuja kwenye suala la ngono/kujamiiana. Pata muda wa kujifunza kuhusu mwili wako, hisia zako na namna ya kuwa salama na mwenye afya kijinsia. Cha muhimu zaidi, pata muda wa kufikiria chaguo lako linaloendana na vitendo vya jinsia yako. Chaguo lako mojawapo linaweza kuwa hakuna ngono au muda bado. Unaweza kusubiri kabla ya hujakimbilia kujamiiana. Unaweza kuhakikisha unaelewa matokeo ya kufanya ngono isiyo salama na namna ya kujikinga. Mara nyingine inaweza ikawa vigumu kuwa na afya njema kijinsia. Hakuna mtu atakayekufundisha kuhusu afya njema, iwe shuleni au nyumbani. Njia kuu ya kupata habari ni kupitia kwa marafiki, kaka na dada zako, video, miziki, na magazeti. Hata hivyo njia hizi zinaweza kukuchanganya na kukupoteza. Baadhi ya video nyingine na riwaya za mapenzi, ngono inakuwa kama jambo la kuvutia na halina matatizo. Ngono inakuwa kama kitu tu kinachotokea na hakuna mazungumzo kati ya watu wawili kama wanahitaji kufanya mapenzi au la, na watumie kondomu au wasitumie. Hata kama hawatumii kondomu, watu katika video na riwaya hawaonyeshi iwapo wanapata matatizo ya kupata mimba zisizohitajika au kupata magonjwa ya zinaa kama VVU/UKIMWI. Katika muziki, wanaume na wanawake wanaimba kama waliopoteza matumaini na hawajali kuhusu ngono. Wanaonekana kutojali kuhusu VVU au matatizo mengine. Wanachotaka ni mapenzi. Mawazo yangu yananiambia hapana lakini mwili unaniambia ndiyo unaendelea wimbo fulani wa rapu. Mwingine unasema: sijui umenifanya nini hadi ikanisababishia kupenda kama mwenda wazimu. Muziki ni mzuri, unagusa hisia za ndani ya moyo kabisa.video na riwaya vinaweza kukufanya uasi maisha yako ya kila siku, lakini havikusaidii ushughulikie mahusiano yako. Havikusaidii ujue kuzungumza na msichana au mvulana wako kuhusu iwapo mfanye au msifanye ngono. Na ni ukweli havikusaidii kukuwezesha uzungumze na mwenzi wako kuhusu kutumia kondomu. Hata mtu unayemfahamu anaweza akakuchanganya kuhusiana na jinsia na ujinsia. Wazazi wengi hawapendi kuzungumzia maswala ya ngono na watoto wao, hivyo inaweza kuwa vigumu kujifunza kutoka kwao. Gifty, kutoka Ghana (Umri wa miaka 14) Kwa nini wazazi wetu wanaona vigumu kutufundisha mambo ya ngono? Au ni kwa sababu wanafikiri tutajaribisha au vipi? Vijana wengi na marafiki, wanaweza kusema kuwa wameshawahi kufanya ngono hata kama hawajawahi. Unaweza kuanza kufikiria na wewe ukafanye ngono ili ulingane nao. Wenzako wanaweza pia wakazua kwamba unahitaji ngono ili upone maumivu ya hedhi au kufanya uume uwe mkubwa na wenye nguvu. Lakini mambo haya si kweli. Kujamiiana hakuwezi kukuponya maumivu ya hedhi, na wala hakuwezi kufanya uume uwe mkubwa. Kwa nyie wavulana, kaka na wajomba zenu wanaweza kuwa walichukua hatua za hatari kuhusiana na mapenzi ambazo wanazijutia hivi sasa. Cha kushangaza ni kwamba wanawashawishi muanze ngono kuhakikisha kwamba nyie ni wanaume. Kwa nyie wasichana, hakuna ambaye amewahi kukusifia huko nyuma, lakini sasa wavulana wanakuambia wewe ni mzuri, na hii inakufanya ujisikie vizuri. Je, kwa hilo tu unatakiwa uonyeshe mapenzi kwao na kuwapa matumaini? Magazeti, muziki, vitabu vya hadithi na matangazo yanatoa taarifa zinazo changanya kuhusu ngono. Inaweza ikawa vigumu kwako kuona la maana kuhusu maelezo unayopata kuhusu ngono. Hata hivyo, jambo muhimu kuhusu afya njema ya ujinsia ni kuonyesha tofauti kati ya tabia yenye mapenzi yenye afya na njia ambazo zina madhara kwako na kwa wengine. Kabla hujachukua hatua katika hisia zako za kijinsia fikiria matokeo ya hatua za matendo yako. Je wewe au yeyote yule atakuwa hatarini kupata mimba isiyotakiwa, VVU/UKIMWI au magonjwa ya ngono? Je, kutenda kutokana na hisia kutasababisha matatizo, kama vile kutoelewana? au kutoeleweka kimawasiliano katika mahusiano? Je, itasababisha mimi au mwenzi wangu kujisikia vibaya? Je, hisia za mtu yeyote zitaathirika?kuwa mwenye afya kijinsia kunamaanisha kupata muda wa kufikiri kuhusu jambo kabla ya kulifanya ili kufurahisha hisia zako za kijinsia

55 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono HISIA ZA KIJINSIA Mambo mengi utayagundua punde utakapoanza kusikia ashiki au kusisimuka kijinsia. Utayahisi mwili mzima. Kwa wanaume, dalili ya hisia ya kijinsia ni uume kusimama. Kwa wasichana, ni unyevunyevu ukeni. Hii inatokea kwa sababu damu ya ziada kutoka kwenye mishipa ya damu inaingia kwenye spongi maalum kwenye tishu ndani ya uke au uume. Kwa wavulana tishu za spongi zinavimba na kusababisha uume kuwa mrefu, mgumu, mpana na kusimama. Kwa wasichana, tishu za spongi zinavimba ndani ya kuta za uke na kusababisha utoaji wa majimaji, ambayo yanalainisha eneo la uchi na kusabisha lilowane. Unaweza kujisikia hisia za kijinsi zenye kusisimua kwa kusoma riwaya za kimapenzi au kumfikiria mvulana au msichana unayempenda. Kama ulikuwa na mvulana au msichana na mlikuwa mnashikanashikana, unaweza kusisimuka zaidi. Utafanya nini kuhusu hisia za kijinsi? Jambo la kwanza, huhitaji kufanya ngono unapopata hisia za kijinsi. Kujamiiana ni njia moja wapo ya namna watu wanavyoonyesha hisia za kimapenzi. Lakini zipo njia nyingi ambazo watu wanaweza kuonyesha hisia zao za kimapenzi - katika mazungumzo, kushikana mikono, kukumbatiana, kupakatana, kubusiana na kushikanashikana. Njia hizi za kuonyesha mapenzi zinaweza kuwa za kuridhisha na zina hatari ndogo sana ya kuambukizwa VVU (soma sura ya 10 zaidi juu ya VVU na magonjwa ya zinaa). Kupumua na mapigo ya moyo yanaweza kuongezeka. Mwili mzima unaweza ukajisikia kusisimuka na kuchangamka. Unaweza kuwa na hali hiyo ya kusisimua kwa masaa mengi. Huhitaji kwenda zaidi ya hapo. Mvulana hahitaji kumwambia msichana kuwa anahitaji kujamiiana nae eti kwa kuwa amesimamisha. Si kweli. Uume wako utaacha kusimama pindi utakapoacha kumpakata msichana. Ni muhimu kujua kwamba, si migusano yote inaleta hisia za kufanya ngono. Kama unasukumwa bila kupenda ili ufanye ngono, hutajisikia vizuri. Msisimko wa kijinsia unatokea watu wanapokuwa na furaha na wamepumzika (soma sura 12 zaidi juu ya unyanyasaji kijinsia na vitendo vya ngono visivyotakiwa). PUNYETO Punyeto ni kitendo cha mtu kushika sehemu zake za siri uume, uke, matiti au sehemu nyingine za mwili ambazo zinasisimka kijinsia. Punyeto ni mojawapo ya njia ambayo watu wanaelezea hisia zao za kijinsia. Wanaume kwa wanawake wanaweza kupunguza hisia za kutaka kujamiiana na bado wakapata starehe kwa kupiga punyeto. Kwa kweli watu wengi wanapiga punyeto kipindi fulani katika maisha yao. Wavulana wanapiga punyeto mara kwa mara kuliko wasichana. Wasichana na wavulana wengine wanaanza kupiga punyeto wakati bado watoto na wanaendelea kufanya hivyo maisha yao yote. Wengine wanaanza wanapobalehe; wengine wanaanza wakiwa watu wazima. Baadhi ya watu hawapigi punyeto, na wengine wanafikiria kuwa starehe ya ngono na kupiga punyeto ni kinyume na madhehebu yao au imani na utu wao. Katika mila nyingine, kuna uzushi mwingi ambao umekusudiwa kuwakatisha tamaa watu wasipige punyeto. Haya ni baadhi ya mambo yasiyo ya kweli kuhusu punyeto, kwamba:- Kupiga punyeto kunafanya upate kichaa. Kupiga punyeto kunafanya uote nywele kwenye kiganja cha mkono wako; kunasababisha vipele usoni au kupofuka macho. Punyeto linafanya upauke rangi ya mwili na inasabisha utumie mbegu zote za kiume. Punyeto linasababisha mtu awe dhaifu na kufanya mwanaume ashindwe kupata watoto. Punyeto linafanya uwe na majivuno na uwe mbinafsi. Hakuna ukweli kuhusu uzushi huu. Kutokana na utalaam wa kitabibu na kisayansi, punyeto linachukuliwa kama sehemu ya makuzi. Haijalishi kama utapiga punyeto au hupigi. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba punyeto ina athari mbaya kimwili ama kisaikolojia. Punyeto linaweza kuwa na matatizo iwapo tu:- Limezidi mno mtu hawezi kufanya kazi za kutwa mpaka apige punyeto. Linafanywa maeneo ya watu wote mahali ambapo watu wengine wanaweza kuona. UNAFAHAMU maana ya kilele? Kama ashiki na msisimko vitazidi kuongezeka, utakuwa unaelekea kilele. Kwa mvulana kuutambua kilele misuli yako ghafla inabana na kufanya sehemu zote za uume wako kusukuma mbegu za kiume nje ya uume. Kwa msichana misuli ya ndani na inayozunguka uke, mlango wa tumbo la uzazi na kisimi vinabana. Mara nyingine majimaji kidogo yanaweza kutoka, lakini hakojoi kama ilivyo kwa wavulana. Kilele ni kama kupiga chafya, hisia ya kukakamaa kwa misuli ikifuatiwa na kulegea. Kwa watu wengi ni muda mfupi tu kilele kinadumu kwa sekunde 10, lakini ni muda ambao unajisikia vizuri na raha na watu wengi wangependa kukionja. Kwa wasichana wengi, inawachukua muda kufikia kilele. Inahitajika kujua wapi na namna gani washikwe.na wanahitaji wawe wanafurahia na kutuliza akili. Wavulana na wasichana, wote wanaweza kufikia kilele kwa kupiga punyeto. Hivi ni vizuri.uko pekee yako, unaugundua mwili wako, na majimaji yanayotoka wakati mwili umesisimkwa hayatampa mtu yoyote mimba wala uambukizo. Unapofikia upeo wa raha ya kujamiiana kwa kushikana na kupakatana, ina ugumu kidogo. Kweli mko wawili na maji maji yanayotoka wakati wa kushikana yanaweza kuwa na VVU au magonjwa ya ngono. (soma sura ya 10 kuhusu magonjwa ya zinaa na VVU). Wataalam wa ujinsia wa binadamu wanaamini kwamba punyeto ni njia ya kawaida ya watu kufurahia na kuelezea ujinsia wao bila ya kujihatarisha katika mimba au magonjwa ya ngono, yakiwemo VVU/UKIMWI. Hakuna tatizo litakalo tokea mwilini mwako hata kama ukipiga punyeto sana. Kitu pekee kinachoweza kutokea ni viungo vya uzazi kuvimba kwa sababu ya kuvisugua mno

56 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono KUVUTIWA NA MTU WA JINSI KAMA YAKO Wakati wa kubalehe ndio wakati watu wengi wanapata kuelewa zaidi mwelekeo wao kijinsi. Mwelekeo wa kijinsi unahusu mtu ana hisia za kimapenzi na anavutiwa kimapenzi kwa nani. Watu wengi wanavutiwa kimapenzi na watu wa jinsi tofauti (kama mwanaume anavutiwa na mwanamke na mwanamke anavutiwa na mwanaume). Watu wengine wanajisikia kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsi sawa. Wanaume wengine wanavutiwa na wanaume wenzao na wanawake wengine kuvutiwa na wanawake wenzao. Huku kuvutiwa na jinsia sawa kunaitwa ubasha au usenge au ushoga. Nyakati fulani katika maisha yao, baadhi ya watu wanakuwa na hisia za kimapenzi, mawazo, ndoto na mvuto kwa mtu fulani wa jinsi moja. Marafiki wawili waliokaribu (pengine wavulana wawili au wasichana wawili) wanaweza kupendana wanapenda kuwa pamoja na wakati mwingine wanajisikia kutamaniana kimwili. Watu wengine wanaona hisia hizi zinawachanganya na kuwafadhaisha. Hisia hizi ni za kawaida, na baadhi ya watu wanazipata hisia hizi wakati fulani katika kipindi cha maisha yao. Japokuwa baadhi ya watu wanavutiwa na watu wa jinsi sawa, madhehebu mengine ya dini na mila zingine zinafikiria ubasha ni jambo baya, si la kawaida na ni tabia ambayo inaweza kurekebishwa. Watalaam wengi wanafikiria kwamba mwelekeo wa kimapenzi wa jinsi moja si jambo ambalo wanaweza kulidhibiti kama isivyowezekana kudhibiti rangi ya ngozi au nywele zilivyo. Kwa maneno mengine ubasha / usenge sio chaguo la makusudi ambalo mtu anachagua, hivyo haiwezekani kulibadilisha aidha kwa kuswali, kwa utashi au kwa kufanya ngono na mtu wa jinsia tofauti. Katika kipindi cha balehe, watu wengine wanajikuta ni mabasha/wasenge. Kujitambua kunaweza kuwa kugumu. Unaweza kujiona uko tofauti kuliko mtu yeyote anayekuzunguka, na unaweza kujisikia mpweke mno. Kama unajisikia kitu kama hiki, jaribu kuonana na mtu ili uzungumze naye, kama mshauri nasaha wa vijana, mhudumu wa afya, mwalimu unayemwamini, au jamaa yako mkubwa yeyote atakayeweza kukusaidia kujibu maswali yako na kupunguza hofu yako atakuwa amekusaidia. UBIKIRA Bikira ni mtu ambaye hajawahi kujamiiana. Kila mvulana na msichana amezaliwa bikira. Ubikira ni kinga nzuri dhidi ya VVU na magonjwa ya zinaa. Siku hizi wavulana na wasichana wengi wanaamua kubakia bikira hadi siku ya kuoa/kuolewa. Ruvimbo kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 13) Nitataka kutunza ubikira wangu. Sitafanya mapenzi na yeyote hata kwa kutumia kinga. Rafiki yangu wa kiume ni mtulivu na ndio maana ni mtu wangu. Stabile, kutoka Zimbabwe (Umri; miaka 19) Bado mimi ni bikira. Bila shaka imani yangu kubwa ya dini inanisaidia katika suala hili. Susan, umri wa miaka 18 kutoka uganda Ubikira ulifanya nionekane mwenye heshima. Wasichana wanatakiwa kutunza ubikira wao mpaka wanapoona wamepata watu wa kuwafaa. Ngono ni jambo unaloweza kuahirisha. Yakwepe mazingira yaliyo kinyume na kanuni ulizojiwekea na utaweza ukadumisha dhamira yako. Watu wengi wanachanganyikiwa na kitu kinachosababisha wasichana wapoteze ubikira. Wanafikiri ubikira wa msichana unadhihirishwa na kizinda, ambacho ni tishu nyembamba ndani ya mlango wa uke. Kizinda kina shimo dogo na hakizibi kabisa uke kwa sababu damu ya hedhi lazima itoke kila mwezi. Wasichana wengine hawana kizinda kabisa. Pengine ni kwa vile hawakuzaliwa nacho au kilinyumbuka na kuchanika kabisa wakati wa michezo. Wasichana walio na tishu ya kizinda mara nyingine wanatoka damu wanapopoteza ubikira wao. Wasichana ambao wana tishu ndogo ya kizinda au hawana tishu ya kizinda wanaweza wasivuje damu watakapojamiiana. Kwa mara ya kwanza hii inawachanganya watu. Watu wanasema: Hakuna damu, kwa hiyo hakuwa bikira. Lakini anaweza kuwa alikuwa, hajawahi kufanya ngono hapo awali hivyo alikuwa bikira. Ubikira unapotea kwa kujamiiana. Hauwezi kupotea kutokana na michezo, kwa kutumia visodo, kupiga punyeto au shughuli yoyote ile. Japo ni kweli mambo haya yanaweza kurefusha au kuchana kizinda, hii haimaanishi msichana sio bikira. Watu wanaofikiria kuwa kizinda ndio usahihi wa kuwepo bikira wanakosea. UNAJUA ukweli kuhusu ubikira? Kuna uzushi mwingi kuhusu ubikira: 1. Nimesikia kwamba msichana anaweza kupoteza ubikira kwa kucheza michezo. Je, hii ni kweli? Si kweli! Ubikira anaweza kupotea tu kwa kufanya ngono, kucheza michezo ni kuzuri kwa wasichana na haiwezi kumsababishia kupoteza ubikira. 2. Kuna mitishamba mingine inaweza kurejesha ubikira? Hapana, hakuna mitishamba inayoweza kurejesha ubikira. Ukipotea, umepotea milele. 3. Rafiki yangu anasema nikibaki bikira kwa muda mrefu, naweza kuugua magonjwa na mambo yasiyo ya kawaida? Siyo kweli! Unaweza kubakia na ubikira maisha yako yote bila matatizo yoyote mabaya. 4. Ni kweli kwamba msichana akiwa bikira kwa muda mrefu sana, kizinda chake kitakuwa kigumu na atapata matatizo ya kufanya ngono? Huu ni upuuzi! Kizinda ni kipande kidogo na chembamba cha tishu. Hakiwi kigumu kadri unavyokua na wala unaposubiri kujamiianahudhuriki kamwe. 5. Unawaweza kuwatambua bikira kwa kuwaangalia usoni? Si kweli! Huweza kumtambua bikira kwa kumwangalia kwa macho. Ni bikira peke yake anayejua hali yake. 6. Baada ya kupoteza ubikira wako, unatakiwa uendelee na ngono. Si kweli. Unaweza kuacha kufanya ngono ukipenda. 7. Nimesikia kwamba si vema kutumia kondomu ukiwa unajamiiana na msichana ambaye ni bikira kwa sababu unahitaji kutumia nguvu sana kuvunja ubikira wa msichana kiasi kwamba utachana kondomu. Je huu ni ukweli? Hapana! Mvulana na msichana ambao ni bikira wanaweza kutumia kondomu bila matatizo. Kizinda ni tishu laini sana inayochanika kwa urahisi mno

57 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono Kama walivyo wasichana, wavulana wanaweza kupoteza ubikira wao kwa kujamiiana. Watu wengine wanafikiri sio muhimu kwa wavulana kuwa bikira kama ilivyo kwa wasichana.zaidi, video nyingi unazozitazama na riwaya nyingi unazosoma zinafanya ionekane muhimu kwa wanaume kuwa na uzoefu zaidi wa ngono. Mara nyingine inaonekana kana kwamba ili uonekane mwanaume lijali lazima ufanye ngono. Lakini kufanya ngono hakukufanyi uwe mwanaume zaidi. Kwa mvulana au msichana kutunza ubikira wako ni vizuri. Ni njia nzuri sana kwa kinga ya kweli dhidi ya VVU, na magonjwa ya ngono na mimba zisizotakiwa. KUPOTEZA UBIKIRA Uwe mvulana au msichana, unapaswa wewe mwenyewe kuamua wakati gani upoteze ubikira wako. Usije kuwaruhusu watu wengine kukuamulia au kukushinikiza uupoteze. Chagua muda wako. Na chagua mtu anayefaa. Subiri hadi unakuwa na uhakika kwamba unaweza kujizuia dhidi ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/UKIMWI na mimba zisizotakiwa. Adam, kutoka Uganda (Umri wa miaka 13) Nafikiri muda mzuri wa kuanza kujamiiana ni wakati nikiwa na umri wa miaka 20. Nitamaliza masomo yangu na pengine kufanya kazi.hata kama muda huo ukifika nitatumia kondomu. Mfune, kutoka Zambia (Umri wa miaka 13) Nitasubiri hadi nioe au nipate fedha za kunisaidia kwa sababu msichana ukipata mimba nitahitaji fedha za kulelea mtoto. Mara nyingine wenzako wanaweza kukulazimisha kufanya ngono. Douglas, kutoka Zambia (Umri wa miaka 12) Vijana wengine wakubwa kwetu au waliojaliwa kuwa na miili mikubwa wanatucheka na kutuambia sisi ni bikira. Andrew, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Rafiki yangu wa kiume ananicheka na kunisihi niwe na rafiki wa kike. Wanasema utaishije bila rafiki wa kike wewe sio mwanaume. Mildred, kutoka Uganda (Umri wa miaka 17) Wakati fulani, unajisikia umeachwa na marafiki zako wakianza kuzungumzia masuala ya ngono. Unaweza tu kuingilia mazungumzo yao kutokana na ulichosoma kwenye kitabu cha hadithi au ulichoona kwenye sinema. Kama huna mwelekeo mzuri unaweza ukadanganywa. Nimechagua kubakia bikira mpaka nimpate mwanaume mzuri wa kunifaa. Lois, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 13) Nazungumza na marafiki zangu kuhusu kufanya ngono. Wapo baadhi ya wasichana na wavulana wanaosema kwamba ukikataa kufanya ngono unafanana na mtu ambaye hakusoma. Vijana balehe wengi siku hizi wanaelewa kwamba kufanya ngono ni uamuzi wao wenyewe na kwamba asiwepo mtu wa kuwalazimisha kufanya ngono. Patrick, kutoka Uganda (Umri wa miaka 17) Marafiki zangu wote wanafanya ngono na marafiki zao wa kike, na kidogo tu niwafuate kutokana na kulazimishwa na marafiki zangu. Lakini niligundua kwamba sikuwa na uhakika na nilichanganyikiwa. Isitoshe ninataka kufanya mambo yangu mwenyewe. Nitasubiri. Lois, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 13 ) Hakuna atakayenilazimisha kufanya ngono. Nitaamua mwenyewe Milensu, kutoka Zambia (Umri wa miaka 13) Sitafanya ngono kwa sababu itabidi nisubiri hadi niolewe nitakapokuwa tayari kwa matokeo ya kufanya ngono. Sitarajii rafiki zangu kunishinikiza nifanye ngono. Uamuzi ni wangu. Andrew, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Kama nitataka kufanya ngono utakuwa ni utayari wangu mwenyewe. Rafiki zangu hawatanishawishi kufanya hivyo. KUJAMIIANA Simama imara dhidi ya shinikizo la kundi rika. Usifanye mapenzi eti kwa sababu rafiki zako wanafikiri unatakiwa kufanya. Kujamiiana ni wakati mwanaume na mwanamke wana ileta miili yao karibu na mwanaume anasimamisha uume na unaingia ukeni kwa mwanamke. Kwa nini watu wanajamiiana? Kuna sababu nyingi nzuri na mbaya. Zifuatazo ni baadhi ya sababu: Upendo na mapenzi ya dhati. Kwa watu wawili walio karibu sana, kujamiiana kunaweza kuleta mapenzi ya dhati na yenye upendo. Hata hivyo watu wengine wanafanya ngono kwa sababu wanafikiri itawaletea kupendana na mapenzi ya dhati kwenye uhusiano wao. Wanafikiri kujamiiana kutathibitisha mapenzi kati yao. Hii mara nyingi haisaidii. Mapenzi ya dhati yanakuja kwa kuzungumza mambo ya uaminifu na kushirikiana katika hisia. Ngono haiwezi kuwaunganisha watu pamoja kama hawakuwa karibu kabla. Kufanya ngono hakumaanishi watu wanapendana. Kuridhisha hamu ya mapenzi na mahitaji ya kimwili. Watu wengine wanafikiri kwamba unahitaji kujamiiana ili kukidhi hisia za kufanya mapenzi kama unavyohitaji kunywa unaposikia kiu. Lakini kujamiiana hakuko hivyo. Ukweli wakati mwingine kujamiiana hakuridhishi kuliko kushikana mikono, kukumbatiana, kubusu, kama watu wawili hawana mahusiano ya karibu, kufanya ngono kunaweza kusiwaridhishe

58 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono Kujaribu kumhodhi mvulana au msichana. Watu wengi wanafanya ngono kwa sababu wanaogopa kupoteza mahusianao iwapo hawatafanya ngono. Hii ni sababu moja mbaya ya kufanya ngono. Yeyote atakayekuacha kwa sababu eti hutaki kujamiiana, hakupendi (soma sura ya 12 kwa maelezo mengi kuhusu hili). Zawadi: Watu wengine wanafanya ngono kwa ajili ya kupata zawadi, fedha au upendeleo kama kupata alama nzuri shuleni. Hili linaweza kuwa tatizo gumu, kwa mfano kama mshirika wako ndiye anayekulipia ada ya shule. Lakini hizi ni sababu zisizo sahihi za kufanya ngono. Hazitakufanya ujisikie vizuri. Usitumie mwili wako kupata chochote kutoka kwa mtu yeyote hata kingekuwa kitu gani fedha au zawadi au huduma za kipekee huwezi kuvilinganisha na mwili wako. Kujisikia umekua. Wengi wanakimbilia kufanya ngono kwa kufikiri itawafanya wajione wamekua. Lakini kufanya ngono kwa kweli hakubadilishi chochote kuhusu ukuaji wako. Ngono haitakufanya ukomae na wala haitakufanya uwe mtu mzima. Kulingana nao au kuwafurahisha wenzio. Watu wengi wanahisi kana kwamba watu wote wanaowazunguka wanafanya ngono kana kwamba wao peke yao ndio hawafanyi ngono. Hii inaweza kuwa tishio na vijana wengine wanafanya ngono kwa sababu wanafikiri vijana wengine wanafanya hivyo.ukweli ni kwamba watu wengi hawasemi ukweli kuhusu ngono, na watu wengi wanatunga tu hadithi kwa sababu wanataka kuwafurahisha watu wengine. Kupata mtoto. Kujamiiana ndiyo njia pekee ya kufanya mapenzi ambayo inaweza kukupatia mtoto. Watu wengi wanataka watoto wakati fulani katika maisha yao, lakini ni wachache wanaotaka kuwa na mtoto wakati wa ujana balehe (soma sura 11). Kujamiiana ndiyo njia ambayo watu wengi duniani wanapa VVU. Kama huko tayari kujikinga wewe na mwenzio kwa kutumia kondomu wakati wote hujawa tayari kujamiiana. KUWEKA KIWANGO CHA KUJAMIIANA. Watu wengine wanafikiri ngono ina nguvu na haiwezi kuzuiliwa na kwamba inatokea kama radi au mvua. Lakini ukweli ni kwamba kufanya ngono ni uamuzi wa makusudi. Unapofanya ngono sio kwamba ni jambo la asili lazima litokee. Ni wewe unayefanya uamuzi. Lakini pawe na maamuzi mengi kuhusu ngono. Lini? Nani? Kwa nini? Wapi? Mara ngapi? Kwa kutumia kondomu? Bila kondomu? Ngono ni uamuzi mzito. Ni uamuzi wako! Zuia sauti zote zinazosema kila mtu anafanya ngono. Jibu ni kwamba si kila mtu anafanya ngono. Na wewe sio kila mtu. Ni wewe tu. Kama unafanya uamuzi wa kufanya au kutofanya ngono, fikiria kuhusu hili: Uko tayari kuvumilia mahitaji ya ngono salama matumizi sahihi na kutumia kondomu kila mara, ushauri kuhusu VVU, kupima, na mengineyo? Vijana wengi hawako tayari kubeba wajibu wote huo; Kuwa mwaminifu kwa nafsi yako. Kama unajiona huko tayari, unaweza kusema Hapana subiri mpaka utakapokuwa mkubwa. Unahitaji vile vile kumtunza mwenzi wako, na yeye vile vile anatakiwa akutunze. Kutunzana kunachukua muda. Urafiki na kuwa karibu haujengeki kwa usiku mmoja. Kama hamjawa marafiki wa kweli unaweza kuona ngono ni kitu cha aibu. Hii ni dalili tosha kwamba huyo siyo mtu anayefaa au siyo muda sahihi kwako. Kama wewe na mwenzi wako hamko tayari kwa kujamiiiana, ishia kwenye kubusiana, kushikana mikono au kukumbatiana. Weka kikomo na kubaliana nacho usifanye kitu chochote ambacho mwenzako anakiona hakifai. Unafahamu kama mahusiano yenu ni tayari kwa kujamiiana? Jibu maswali yafuatayo kiukweli kadri uwezavyo. Weka tiki kwenye jibu ulilolichagua..1. Je, mimi na mwenzi wangu tunafahamiana vizuri Ndiyo Hapana Labda Sijui 2. Je unajisikia tumeungana pamoja na kila mmoja wetu anajiona kuwa sehemu ya mwenzi katika maisha. Ndiyo Hapana Labda Sijui 3. Je, kila mmoja amejikabidhi kwa mwenzie katika uhusiano wenu? Ndiyo Hapana Labda Sijui 4. Je, tunaaminiana? Ndiyo Hapana Labda Sijui 5. Je, tunawasiliana vizuri? Ndiyo Hapana Labda Sijui 6. Je, tunaweza tukazungumza bila wasi wasi kuhusu ngono? Ndiyo Hapana Labda Sijui 7. Je, tunafikiria kufanya ngono kwasababu kweli tunataka au kwa sababu tunashinikizwa kufanya ngono? Ndiyo Hapana Labda Sijui 8. Je, tumezungumzia kuhusu njia gani tutatumia kuzuia mimba? Ndiyo Hapana Labda Sijui 9. Je, tumezungumzia kuhusu kupima VVU kwetu wote? Ndiyo Hapana Labda Sijui 10. Je, tumezungumzia namna ya kujikinga na magonjwa ya ngono pamoja na VVU/UKIMWI? Ndiyo Hapana Labda Sijui 11. Je, tumekubaliana kutumia kondomu na njia za kuzuia mimba wakati wa kujamiiana? Ndiyo Hapana Labda Sijui 12. Je, mwenzi wangu ataheshimu haki yangu ya kusema ndiyo au hapana kila tunapofanya ngono? Ndiyo Hapana Labda Sijui 13. Je, nitaheshimu haki ya mwenzi wangu ya kusema ndio au hapana kwa kila tutakapotaka kufanya ngono? Ndiyo Hapana Labda Sijui 14. Je, ushirikiano wa mahusiano ya kimapenzi yatakuwa salama na ya raha? Ndiyo Hapana Labda Sijui Kama ulijibu hapana labda au sijui kwa swali lolote, basi labda wewe na mwenzi wako hamko tayari kujamiiana. Ni vizuri kungoja

59 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono UAMUZI WA KUTOFANYA NGONO Vijana wengi wanachagua kutofanya ngono kwa sababu nzuri sana zifuatazo: Wanaogopa kupata mimba na magonjwa ya ngono virusi vya UKIMWI na UKIMWI wenyewe na hawapendi kuhatarisha maisha yao. Bado ni wadogo mno hivyo wanajiona hawako tayari. Hawataki kuwaudhi wazazi wao. Wanaona tendo hilo ni kinyume cha maadili ya dini zao. Wako tayari kusubiri ili kushughulikia masomo yao. Wanataka kuhakikisha kuwa rafiki yake wa kiume au wa kike anampenda kikweli. Iwapo unakabiliwa na uamuzi wa kufanya ngono, kumbuka kwamba ngono inaweza kuwa na matokeo mabaya kama kuambukizwa VVU au mimba zisizotakiwa.mambo haya yanaweza kukuharibia maisha yako milele. Unahitaji kufikiri kwa makini uamuzi wako. Kumbuka kuwa: Kusubiri ndiyo njia nzuri na salama ya kubakia na afya. Unayo haki ya kusema hapana kwa ngono na kushikilia uamuzi wako. Ukiamua kusema ndio kwa ngono, lazima ujizoeze kufanya ngono salama ili kukwepa mimba, VVU, UKIMWI na magonjwa ya ngono. Bila kondomu, hakuna ngono. KUZUNGUMZA NA MWENZI WAKO KUHUSU NGONO Andrew, kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Mimi na marafiki zangu tunazungumza kuhusu ngono. Tunazungumza pia athari za ngono,kwa mfano iwapo msichana atapata mimba,tutapata matatizo makubwa, tutalazimishwa kuoa au kufukuzwa shule! Halima, kutoka Kenya (Umri wa miaka 17) Sababu nzuri sana za kuchelewa kufanya ngono ni kusubiri kupata mtu atakayefaa na kusubiri mpaka mnaoana. Maamuzi kuhusu ngono yanahusu watu wawili na yanahitaji mawasiliano mazuri na makini. Ni jambo muhimu kumweleza wenzi wako kitu unachofanya na kitu ambacho hutaki kukifanya. Watu wengi wanajisikia vibaya na aibu kuzungumza masuala ya ngono, lakini mambo haya yanakuwa rahisi baada ya muda na kuyafanyia mazoezi. Hapa kuna baadhi ya vidokezo: Fikiri ni kwa nini unataka au hutaki kufanya chochote: Jua sababu zako ni zipi ili uweze kuzieleza wazi kwa mwezi wako. Fanya mazoezi kabla: Kama huna uhakika utazungumza nini kuhusu kujamiiana na rafiki yako wa kike au kiume jaribu kuzungumza na rafiki wa karibu unayemwamini au mshauri wa vijana kwanza. Waulize jinsi ya kulizungumzia suala hilo. Pata maoni ya namna ya kushughulikia hali hii. Chagua muda mzuri na mahali muafaka: Chagua muda mzuri wa kuzungumza na rafiki yako wa kiume au wa kike, muda ambao kila mmoja wenu hana shughuli ya mambo mengine na wakati ambapo wote mnajisikia mmetulia na mmestarehe. Ni vizuri pia kuchagua sehemu nzuri. Chagua sehemu ambayo hutajali hata watu wengine wakiwasikia. Wakati huo huo chagua sehemu ambayo siyo ya kificho sana ambayo itamfanya msichana wako au mvulana wako apate wasiwasi na kupata mawazo potofu. Usingoje mpaka umepata joto la mahaba ndio uanze kuzungumzia ngono: Ni vigumu sana kuwa na mazungumzo kuhusu kujamiiana wakati mmoja au wote mnajisikia mmesisimka na katika hali ya kufanya ngono. Hakikisha mnazungumza aina gani ya mapenzi mnayataka kabla wewe na mwenzi wako kujikuta katika hali ya kuvutia kimapenzi. Kuwa mkweli kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyoona. Usiwatumie watu au sababu mbalimbali kama kisingizio. Kwa mfano kama hutaki kufanya ngono kwa sababu unataka kwanza kuolewa, usimwambie rafiki yako kwamba sitaki kufanya ngono kwa sababu naogopa kupata mimba au kwa sababu unaogopa kwamba mama atagundua. Ukimwambia rafiki yako wa kiume visingizio hivyo atafikiri kwamba unataka utumie kondomu au unataka uende kwake.ili kukwepa kutoeleweka, kuwa muwazi na eleza moja kwa moja hisia zako. Simama imara na usikubali kushinikizwa: Hata watu ambao unawaheshimu sana wanaweza kukushinikiza ufanye vitu ambavyo hutaki kuvifanya. Inaweza kuwa vigumu sana kuhimili shinikizo kwa sababu ni mtu unayempenda unataka awe na furaha. Kumbuka hata hivyo kwamba mtu anayekupenda hapaswi kufanya mambo ambayo yatakukosesha raha. Kama rafiki yako wa kiume au kike anakushinikiza pengine ni kwa sababu hawajui unajisikiaje au kwa sababu hawajali hisia zako kama ambavyo inawapasa. Simama kidete, na hakikisha wanaelewa unachokitaka

60 SURA YA 9 Ujinsia Na Ngono Zingatia hisia na silika yako: Kama moyoni mwako hujisikii kwamba kitu fulani hakikufai usikifanye. Ngoja mpaka utakapoona huna woga wowote, wasiwasi au vitu vinavyo kuhangaisha. Wakati wote jiruhusu kubadilisha mawazo. Tuseme ulimwambia rafiki yako wa kiume kwamba utafanya ngono naye, lakini ukajiona huwezi kufanya. Unayo haki ya kubadili mawazo yako. Unayo sababu nzuri ya kujisikia unavyojisikia. Hata kama umewahi kufanya ngono kabla, unaweza wakati wowote kuamua kuacha. Hakuna tatizo lolote unapoamua kuacha. Huna haja ya kutoa sababu za kutosheleza kueleza kwa nini unaacha. Wewe kumbuka tu, mtu anayo haki ya kubadili mawazo yake. Unayo haki ya kubadilisha mawazo wakati wowote. Sura ya 9 UJINSIA NA NGONO Ujana ndio muda ambao unajitambua wewe mwenyewe kama mtu ambaye unapata hisia za kijinsia. Unajitambua zaidi kuhusu ujinsia wako unajisikia, unajiheshimu kama mwanaume au mwanamke, unajua kitu gani unataka kuhusiana na mahusiano na watu wengine. Mtu kuwa na afya kiujinsia maana yake ni kuwa unaweza kuelezea ujinsia wako katika namna ambayo haikudhuru wewe au mtu mwingine. Ina maana kwamba haujihatarishi kama vile kufanya ngono isiyo salama, ambayo inaweza kusababisha mimba zisizohitajika au magonjwa ya zinaa, ukiwemo VVU/UKIMWI. Kila mtu ana hisia za kiujinsia na huhitaji kufanya ngono unapokuwa na hisia za kiujinsia. Ngono ni njia mojawapo ambayo watu wanaweza kuelezea hisia za kijinsia, kama kuzungumza, kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana n.k. Bikira ni mtu msichana au mvulana ambaye hajawahi kufanya ngono. Wasichana hawawezi kupoteza ubikira wao kwa kucheza michezo au kuvaa kisodo au shughuli nyingine yoyote. Kutunza ubikira wako na kusubiri kufanya ngono kutakuweka salama. Haitakuumiza kusubiri. Vijana wengi wanaamua kutofanya ngono, wanajiona ni wadogo mno na wanajisikia bado. Unayo haki ya kusema hapana kwa ngono. Watu wengi duniani wameambukizwa VVU kwa kupitia ngono. Kama huko tayari kujikinga wewe na mwenzi wako kwa kutumia kondomu kila mara,basi ujue huko tayari kufanya ngono. Kuzungumza kuhusu ngono na marafiki zako wa kike au kiume inaweza kuonekana kazi ngumu na ya aibu mwanzoni lakini ni vizuri kumwambia mwenzio unataka nini na kipi hutaki ili isije ikatokea kutoelewana. Chagua muda mzuri wa mazungumzo na usisubiri mpaka uwe katika joto la mahaba. Kuwa mkweli kuhusu hisia zako, na usijirahisi au kushinikizwa kufanya kitu ambacho hukihitaji. Kumbuka, hata kama umewahi kufanya ngono kabla, unaweza wakati wote ukaamua kuacha kufanya ngono. Hakuna matatizo yoyote yatakayokupata. Kama huwezi kujikinga na mimba zisizotakiwa, VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono, itakubidi uache kufanya ngono

61 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Stabisile kutoka Zimbabwe (Umri: miaka 19) Mwili wangu ni wa pekee kwangu. Ninaulinda dhidi ya magonjwa ya ngono, VVU na mimba. Mwili wako vile vile ni wa pekee. Je, unaulinda? Yapo mambo mengi unayotakiwa kuyajua kuhusu kuishi na afya nzuri na kujilinda mwenyewe dhidi ya matatizo ya afya ya uzazi. Watu wengi wanapofikiria matatizo ya afya ya uzazi, wanafikiria magonjwa ya ngono na VVU/UKIMWI tu. Haya ni matatizo ya hatari kwa hiyo ni wazo zuri kujua namna ya kujitunza na jinsi ya kuepuka majanga. MAGONJWA YA NGONO Magonjwa ya ngono ni magonjwa ambayo yanaambukizwa kwa njia ya kujamiiana au kwa kufanya ngono. Yapo magonjwa ya ngono yanayosabisha vidonda, uvimbe au malengelenge wakati yapo mengine ambayo hayaonyeshi dalili zozote. Magonjwa ya ngono yanaenea kwa kupitia mgusano wa majimaji ya watu wawili shahawa, majimaji ya ukeni na damu na kupitia mgusano na ngozi iliyoathirika. Magonjwa ya ngono yanaweza kuenezwa kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke, na kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume na hata kati ya watu wawili wa jinsi moja. Ugonjwa uenezao kwa ngono uliombaya zaidi kuliko yote ni VVU/UKIMWI. Hakuna sindano ya kinga na hakuna dawa unapokuwa umepata maambukizi. Watu wengi wanakufa ndani ya miaka 10 mpaka miaka 20 baada ya maambukizi ya VVU

62 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Magonjwa mengine ya zinaa kama kaswende, klamidia na kisonono ni hatari vilevile. Magonjwa haya yanatibika na tunaweza kuyathibiti. Lakini yanaweza kuleta athari za muda mrefu: Kusababisha ugumba yaani kushindwa kupata watoto. Kusaidia virusi vya UKIMWI kuingia mwilini kwa urahisi. Kwa ufupi, zipo njia tatu za kuepuka magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU. 1. Usifanye ngono. Ahirisha kufanya mapenzi au acha kabisa kujamiiana. 2. Unapojamiiana, hakikisha unatumia kondomu tangu mwanzo mpaka unapomaliza kitendo. 3. Nenda na mpenzi/mwenzi wako kupima VVU. Kabla ya kuanza kujamiiana. Unaweza kupima VVU zaidi ya mara moja kutegemeana ni lini ulifanya ngono isiyo salama (bila kinga) ili kuhakikisha huna VVU. (Angalia ukurasa wa 116 kwa maelezo zaidi). Hakikisha kati yenu hakuna aliye na maambukizo ya VVU kabla ya kuanza kujamiiana. Kila mmoja wenu abakie mwaminifu kwa mwenzie. Mambo haya yanaonekana kuwa rahisi. Njia za kuwa salama ni hizo tatu. Lakini, yapo mengi ya kufikiria. Iwapo ulifanya ngono na baadaye ukaamua kuacha, bado utatakiwa kupima. Unaweza kuwa na ugonjwa uenezwao kwa ngono bila ya kujitambua. Je, unajua kwa nini wasichana wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa hasa VVU/UKIMWI? Ingawa wote, wanaume na wanawake, wanaweza kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa, wanawake na wasichana wanapata maambukizo kwa urahisi zaidi kuliko wanaume/wavulana. Zipo sababu kadhaa kwa nini iwe hivyo: 1. Uume wa mwanaume unaingia ndani ya uke na shahawa zake zinaweza kuwa na maambukizo. Zikikaa ndani ya mwili wa mwanamke zinaongeza uwezekano wa kupata maambukizo ndani ya tumbo la uzazi, mirija ya falopia na ovari. 2. Kwa ujumla, wasichana wako hatarini kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa kwa sababu mlango wa mfuko wa uzazi wa msichana balehe ni laini zaidi kuliko wa mwanamke mtu mzima. Uke unaweza ukachanika wakati wa kujamiiana jambo ambalo linaweza kuongezea hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono. 3. Wasichana wengi na wanawake wanafundishwa kuwa watiifu na wanyenyekevu kwa wanaume. Hawana stadi ya kujiamini ili kuwashawishi wenzi wao kutumia kondomu kwa ajili ya kinga. Wasichana balehe wengi, walioolewa au wasioolewa, wenzi wao wana umri mkubwa kuliko wao wenyewe. Mwenzi anapokuwa na umri mkubwa kuliko msichana, inaweza kumuwia vigumu hasa msichana kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na mimba. Katika jamii nyingi inaweza kumwia vigumu mwanamke kukataa kujamiiana na mme wake au kumsisitizia watumie kondomu hata kama anafikiri mwanaume wake anaweza akawa na mwanamke mwingine. 4. Wanawake na wasichana wako kwenye hatari ya kufanya ngono bila kutaka. (kwa kulazimishwa au kubakwa), kuliko wanaume na wavulana. Katika mazingira magumu kama haya, inaweza kuwa vigumu kujikinga na maambukizi. 5. Mambo ya kimila na utamaduni kama vile kufanya ngono kavu na kuweka dawa za kienyeji, nguo na vitu vingine ndani ya uke ili kusafisha au kuubana vyote hivi vinamwongezea mwanamke hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono. Kukausha uke kabla ya kujamiiana kunaweza kuongeza uwezekano wa kuchanika na kuchubuka wakati wa kujamiiana. Kama wewe na mwenzi wako mnatumia kondomu wakati wote mnapojamiiana ni vizuri sana. Endelea!Watu wengi wanaanza kwa kutumia kondomu. Lakini baada ya muda wanaanza kufikiri. Ninamwaminimwenzi wangu, tunaweza kuacha kutumia kondomu. Hii siyo sawa! Kabla hamjaacha kutumiakondomu, wote wawili mnahitaji kupima kwa ajili ya magonjwa ya ngono pamoja na angalau, kipimokimoja cha VVU. Hata kama wewe na mwenzi wako mmepima na hamna maambukizo ya magonjwaya ngono, ni vizuri zaidi kuendelea kutumia kondomu. Je, ikitokea kwamba mmoja wenu amejamiianana mtu mwingine? Vilevile unahitaji kuzuia mimba. UTAJUAJE KAMA UMEPATA MAAMBUKIZO YA MAGONJWA YA ZINAA? Watu wengi hasa wanawake ambao wamepata maambukizo ya magonjwa ya zinaa hawaonyeshidalili zozote zile. Kwa mfano, hakuna dalili yoyote ya kuonyesha kwamba umepata maambukizo yavvu kwa mara ya kwanza. Magonjwa mengine ya ngono vilevile hayana dalili za wazi, kwa hiyo kilamtu inabidi afikirie hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa. Kama umeshafanya ngonobila kinga unaweza kuwa umejiweka katika hatari ya kupata maambukizo. Ukipata kidonda au kiupele sehemu za siri ambacho kinapotea, unahitaji kumwona mhudumu wa afya.yapo magonjwa ya zinaa mengine ambayo yana dalili zinazokuja na kupotea. Kidonda cha kaswendewakati wote kinapona na vidonda vinavyotokana na malengelenge vinapona na kujirudia. Kama umewahikupata kidonda, kiupele au lengelenge kwenye via vya uzazi, unatakiwa kumwona mhudumu wa afya.hata kama dalili za ugonjwa wa ngono zinapotea, maambukizo yanakuwepo na wala hayawezi kuponabila kupata tiba sahihi. Kwa vyovyote vile,kama umeshaanzakujamiiana au bado, ni vizuri kufahamuvia vyako vya uzazi vikoje. Ikiwa unajuavikoje ukiwa mzima, itakuwa rahisikugundua tatizo mapema. Tumia kiookujiangalia sehemu zako za siri kiurahisi.kwa mfano, kidonda cha kaswendehakiumi, kwa hiyo unaweza usigundueisipokuwa kama ukiangalia. Kwa wasichana, ni vema kufahamu mwonekano na harufu ya kawaida yamajimaji yako ya ukeni. Majimaji yaukeni ya kawaida:. Ni kama majimaji meupe ya yai. Ni maangavu au meupe. Yanatoa harufu ya kawaida au yenye afya na isiyochukiza. Hayawashi. Magonjwa ya ngono mara kwa mara husababisha majimaji ya ukeni kuwa na rangi ya njano au kijani na hutoa harufu mbaya na kali. Je, unazijua alama na dalili za magonjwa ya zinaa? Magonjwa mengine ya zinaa hayana dalili za wazi, hasa kwa wanawake, lakini mengine yanazo. Dalili za magonjwa ya zinaa kwa wanaume ni pamoja na:- Kidonda, vidonda, upele au malengelenge juu aukuzunguka uume. Uume kutoa usaha. Maumivu makali wakati wa kukojoa. Maumivu wakati wa kujamiiana. Maumivu na kuvimba mapumbu. Uvimbe usio wa kawaida au kuota vitu kwenye via vya uzazi Dalili za magonjwa ya zinaa kwa mwanamke: Kutoka kwa majimaji ukeni ambayo ni mazito; yanawasha au yana harufu na rangi isiyo ya kawaida. Maumivu sehemu za chini ya kitovu.. Maumivu wakati wa kujamiiana. Kutokwa kwa damu ukeni kusiko kwa kawaida na bila mpangilio. Kuwasha maeneo ya via vya uzazi. Uvimbe usio wa kawaida na kuota vitu kwenye via vya uzazi

63 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Magonjwa mengine ambayo hayaambukizo kwa njia ya ngono vilevile husababisha kutoka kwa majimaji yasiyo ya kawaida. (soma mwisho wa sura hii kwa taarifa zaidi). Hata bikira anaweza kupatabaadhi ya maambukizo haya. Ukiona kitu chochote cha tofauti, mwone mhudumu wa afya. Iwapomwenzi wako ameona kitu chochote cha tofauti kwenye sehemu zake za siri unatakiwa na wewe uende ukafanyiwe uchunguzi wa afya hata kama unajisikia una afya nzuri. KWENDA KUCHUNGUZWA MAGONJWA YA ZINAA. Kama umefanya ngono bila kinga, unahitaji kwenda kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa, hatakama unazo au huna dalili zozote. Kwenda kuchunguza magonjwa ya ngono kunaogopesha. Kwa bahati mbaya wahudumu wa afyawengine wanahukumu na huwa hawana huruma kwa vijana balehe. Wanafikiri hawatakiwi kufanyangono na wanawafahamisha hivyo! Siku hizi, kliniki nyingi zinatoza gharama kubwa kwa matibabu yamagonjwa ya zinaa, lakini zipo chache ambazo zinatoa huduma kwa gharama nafuu kwa vijana balehe.kwa hiyo, ulizia na ujaribu kutafuta kituo cha afya vinavyowajali vijana balehe. Hata kama wahudumusiyo wema, shikilia msimamo wako na endelea kuomba unachokitaka. Haiwezekani kwamba watakataakukuhudumia. Kuwa jasiri. Kwenye vituo vya afya vizuri utapata vilevile elimu nasaha kuhusu uamuzi muhimu kama:- Je, unataka kuendelea kufanya ngono? Je, unataka kupima VVU? Je, utazungumza vipi na mwenzi wako kuhusu kutumia kondomu? Je, unatakiwa kutumia uzazi wa mpango? Njia ipi ni sahihi kwako? Kliniki nyingi zinatoa kondomu bure, kwa hiyo anza kuzitumia kiukweli na hakikisha mwenzi wako anapata matibabu yanayostahili. Ikiwa umepata maambukizo ya magonjwa ya ngono: Mwenzi ambaye hajatibiwa atakuambukizatena. Hata kama umeachana naye badounatakiwa kumweleza aende kufanyiwauchunguzi na kutibiwa. Kama huwaambiina kama hawana dalili zozote, hawawezikujua kama wana maambukizo ya magonjwaya ngono mpaka hapo ugonjwa utakapokuwaumesababisha madhara ya kudumu kwenyevia vya uzazi. Inaweza ikawa vigumukumweleza rafiki yako wa zamani lakiniunahitaji kuwa jasiri kuongea na kumwelezamtu huyo kwamba aende kufanyiwauchunguzi. Kumwambia mwenzako inaweza kuwa vigumu lakini ni muhimu. Hakikisha unameza dawa zote ulizopewa na mhudumu wa afya. Usifanye ngono mpaka utakapoelezwa na mhudumu wa afya kwamba wewe na mwenzi wako mmepona. Jadili kuhusu afya ya kijinsia na mwenzi wako ili muweze kujikinga. Kamwe usijitibu mwenyewe magonjwa ya ngono. Unahitaji kupata dawa sahihi au dawa kutoka kwa mhudumu wa afya. Ukitumia dawa isiyo sahihi itafanya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa kuwa sugu. Kamwe usichangie dawa na rafiki yako. Kunywa dozi yote peke yako. Iwapo utakunywa sehemu tu ya dozi utawafanya wadudu wanaosababisha ugonjwa wawe sugu na vigumu kutibika. Unajua kuhusu magonjwa ya zinaa? Magonjwa yote ya zinaa yanawezesha kupata maambukizo ya VVU kiurahisi. Baadhi ya magonjwa ya zinaa ambayo yanasababishwa na vijidudu vya bakteria na yanaweza kutibika ni:- Chankroidi: Ugonjwa huu husababisha vidonda vyenye maumivu kwenye via vya uzazi na wakati mwingine kuvimba kwa tezi kwenye kinena. Tezi za limfu zinaweza kuvimba hadi kupasuka. Vidonda vinavyohusiana na chankroidi vinaongeza hatari ya kupata maambukizo ya VVU. Klamidia Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana na unaweza kukaa bila kujitokeza kwa muda halafu ukaanza kuleta matatizo. Dalili zake ni pamoja na uume au uke kutoa uchafu, maumivu wakati wa kujamiiana (kwa wanawake) na uvimbe au maumivu kwenye mapumbu. Mara nyingi, ugonjwa huu hauonyeshi dalili 70% ya wanawake na 25% ya wanaume hawaonyeshi dalili kabisa. Kama klamidia haijatibiwa, maambukizo yanaweza kuenea na kusababisha uvimbe ndani ya mfuko wa kizazi na unaweza kupata ugumba. Kwa wanaume, klamidia isipotibiwa inaweza kusabisha ugumba. Kisonono: Ugonjwa huu husababisha kutokwa usaha wa rangi ya njano/kijani na maumivu makali wakati wa kukojoa. Hata hivyo, wanaume wengine hawapati dalili zozote. Wanawake wengine wanaweza kutoa uchafu lakini wengi wao hawana dalili. Iwapo maambukizo hayajagundulika na kutibiwa, yanaweza kuenea na kusababisha ugumba/utasa. Kama kisonono hakijatibiwa husababisha pia upofu kwa watoto. Kaswende: Ugonjwa huu husababisha kidonda kidogo kisichouma. Dalili zinatokea kwenye via vya uzazi au mdomoni. Kidonda hutokea siku 9 mpaka siku 90 baada ya maambukizo. Kidonda hiki hupotea baada ya siku chache na kinaweza kisionekane tena. Maambukizo yanaweza kukaa bwete kwa muda. Baadaye kipele kisichowasha hutokea. Dalili nyingine ni pamoja na homa kiasi, uchovu, vidonda kooni, nywele kunyonyoka, kupungua uzito, kuvimba tezi, na misuli kuuma. Iwapo kaswende haikutibiwa inaweza kuleta matatizo makubwa maishani kama ugonjwa wa moyo hasa katika hatua za mwisho. Maambukizo yanaathiri ubongo pia. Wanawake wajawazito wanaweza kumwambukiza kaswende mtoto tumboni na hii inaweza kusababisha mimba kuharibika au kuzaa mtoto aliyekufa. Watoto wanaozaliwa na kaswende wanakuwa wagonjwa sana. Matibabu yanaweza kufanyika wakati wowote kaswende inapogundulika, lakini ikigundulika mapema matibabu yanachukua muda mfupi na yanafanikisha kutibu ugonjwa huo. Trikomoniasisi husababisha kutoka uchafu unaonuka, kuwasha na vijidonda kwa wanawake. Wanaume kwa kawaida hawaonyeshi dalili kabisa. Dalili zinaanza siku 3 mpaka siku 28 baada ya maambukizo. Magonjwa mengine ya zinaa yanasabishwa na virusi. Haya hayawezi kutibika kiurahisi au hayawezi kutibika kabisa. Nayo ni:- Malengelenge (herpes): Hayawezi kutibiwa na Viuavijasumu. Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana na kwa kugusana na ngozi iliyoathirika. Malengelenge husababisha vidonda vidogo kutoka kwenye via vya uzazi au kuzunguka mdomo. Vidonda vinaweza kuambatana na homa kali, maumivu ya kawaida na kuvimba tezi. Malengelenge hupasuka baada ya siku 2 hadi siku 4 na mwishowe hupona. Mtu akipata maambukizo hubakia hivyo maishani. Marudio ya mashambulizi yanategemea afya ya mtu. Watu wenye VVU wanashambuliwa mara kwa mara na malengelenge. Mtoto aliye na maambukizo ya ugonjwa wa malengelenge yuko hatarini kupata upofu, ubongo kuharibika na kifo kutokea. Kwa kuongezea, malengelenge huongeza hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema (uaviaji)

64 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Unajua kuhusu magonjwa ya zinaa? (Inaendelea) Virusi vya Human Papilloma, Vinundu sehemu za siri (genital warts) Virusi hivi husababisha sugu kuota kwenye via vya uzazi. Virusi hivi vilivyofunikwa vinaweza visionekane kwa urahisi, hususani kama vitatokea kwenye njia ya uzazi ya mwanamke. Kawaida vinajitokeza wiki 3 hadi wiki 9 baada ya maambukizo. Kipindi hiki kirefu vijidudu hukaa tuli mwilini kabla ya kusababisha ugonjwa. Inamaanisha kwamba inaweza ikawa vigumu kufahamu maambukizo yalikotokea na yanaweza kuenea kwa watu wengine bila kujua. Vinundu sugu vinaweza kutibiwa na maji ya tindikali na hairuhusiwi kujamiiana mpaka vinundu vyote vimepotea. Wenzi wote wanatakiwa kuchunguzwa ili kuona kama hawana vinundu sugu. Wanawake wenye maambukizo haya wako katika hatari kubwa ya kupata kansa ya kizazi. VVU/ UKIMWI : Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. VVU vinapoingia mwilini hushambulia kinga ya mwili ambayo kwa kawaida inalinda mwili usipate maambukizo. Inaweza ikachukua miaka mingi kuona dalili za maambukizo, lakini baada ya muda mrefu mtu anashindwa kuzuia maambukizo na hata magonjwa yaliyozoeleka ambayo VVU/UKIMWI VVU (Virusi Vya UKIMWI) ni Virusi vinavyosababisha UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) UKIMWI ni ugonjwa ambao kinga ya mwili dhidi ya magonjwa inaharibiwa hatua kwa hatua. VVU vikiingia kwenye mwili wa mwanadamu vinashambulia kinga ya mwili ambayo kwa kawaida inalinda mwili usipate maambukizo. Watu wenye maambukizo ya VVU wanaitwa watu wanaoishi na VVU/ UKIMWI. Baada ya muda mrefu mtu aliyepata maambukizo anashindwa kuzuia maambukizo hata ya magonjwa yaliyozoeleka ambayo kwa vyovyote vile yasingefikia hali mbaya. Mwili unaposhindwa kujikinga na magonjwa tunasema mtu ana UKIMWI. Hakuna chanjo ya maambukizo ya VVU, na hakuna tiba mara utakapokuwa umepata maambukizo hayo. Inachukua muda mrefu mpaka dalili za VVU kuonekana. Matokeo yake ni kwamba, mtu ambaye ana maambukizo ya VVU anaweza akawa na afya nzuri kwa miaka mingi na anaweza asijue kwamba anayo maambukizo. Katika kipindi hiki anaweza kueneza VVU bila yeye kujua. Muda ambao mtu anaanza kuona dalili za virusi unategemea na uwezo wa nguvu ya kinga ya mwili na uimara wa virusi. Yapo makundi mengi ya VVU. Makundi mengine humfanya mtu augue haraka kuliko mengine. Kwa wastani inachukua miaka 5 hadi 10 kabla dalili zozote za VVU hazijajitokeza. Kwa vile virusi vinashambulia kinga ya mwili na kumfanya mtu ashambuliwe kiurahisi na magonjwa, dalili zinatofautiana sana kutegemeana na ugonjwa gani mtu anaougua. Hata hivyo dalili za kawaida ni:- Kuvimba tezi za limfu Kifua kikuu. Kupungua uzito sana na kuchoka. Kutoka jasho, hasa usiku. Homa za mara kwa mara Kuharisha kwa mfululizo. Kichefuchefu na kutapika. Kikohozi kikavu cha mfululizo. Upele mwilini na vidonda mdomoni. Hakuna dawa inayotibu VVU/UKIMWI. Lakini zipo dawa zinazowasaidia watu waishio na VVU kwa miaka mingi bila kuumwa na zinazopunguza makali ya VVU/ UKIMWI. Anti retrovirals (ARVs) ni dawa zinazopunguza kuendelea kwa virusi. ARVs zinawawezesha watu kuishi maisha ya afya nzuri. Dawa hizi haziuwi virusi moja kwa moja. Zaidi ya hapo dawa hizi ni ghali sana, ingawa zipo kampuni ambazo zimeanza kutengeneza dawa zenye gharama nafuu na zenye ubora uliosawa na dawa zilizo ghali. Hata hivyo, ni vigumu kununua dawa hizi ambazo ni nafuu katika nchi nyingi za Afrika. Matokeo yake ni kuwa watu wengi hawazipati. Dawa hizi sasa zimeanza kupatikana katika nchi nyingi za Kiafrika kwa bei nafuu. UKWELI KUHUSU VVU Zipo aina mbili za VVU zinazojulikana kama VVU 1 na VVU 2. VVU 1 inapatikana zaidi, na VVU 2 inapatikana zaidi Afrika ya Magharibi kuliko VVU 1. Vyote, VVU 1 na VVU 2 vinasababisha UKIMWI. Hata hivyo, kipindi cha kuanzia maambukizo mpaka kufikia UKIMWI ni kirefu zaidi kwa yule mwenye aina ya VVU 2 kuliko VVU 1. Sasa hivi hakuna kinga kwa aina zote za VVU wala hakuna dawa ya UKIMWI. Watu wengi wanaopata maambukizo ya VVU wanafikia UKIMWI baada ya kuishi na VVU kwa miaka 5 hadi miaka 10. Kipindi hiki cha muda ni cha wastani, inategemea na mambo kadhaa, kama:- Aina ya VVU (VVU 1 au VVU 2). Upatikanaji wa dawa na kutibu dalili zinazojitokeza sana, na pia kujiweka wazi na magonjwa mengine. Msaada wa kisaikolojia anaopewa mgonjwa. Kumbuka kwamba maambukizo ya VVU/ UKIMWI huibuka kwa njia tofauti kutegemea na maelezo binafsi. Mtu akigundulika ana virusi vya UKIMWI haimaanishi atakufa tu. Wapo watu ambao walipata maambukizo miaka 20 iliyopita na hadi leo hawajafikia hatua ya UKIMWI. Matumaini yapo! Kwa hiyo, kitu cha kwanza ni kuzuia VVU kuingia mwilini mwako. Kamwe usidhani mtu anavyoonekana ni salama kwa sababu ya vile anavyoonekana. Subiri vya kutosha kabla ya kuanza ngono kwa sababu kujamiiana ndiyo njia kuu inayoambukiza VVU. Kama unafanya ngono, tumia kondomu kila marakondomu inaweza kukukinga usipate VVU na magonjwa mengine ya ngono. Wakati wote pima VVU kabla ya kuanza uhusiano wa kijinsia na mtu mpya na hakikisha mwenzi wako naye anapima VVU. Usichangie nyembe, sindano, vifaa vya kutogea au visu vya kutahiria

65 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia VVU VINAINGIAJE MWILINI? Njia kuu inayoeneza VVU ni kujamiiana na mgusano wa moja kwa moja na majimaji ya mwilini. Katika Afrika, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa VVU wanaambukizwa kwa njia ya kujamiiana. Ni rahisi sana kwa mwanamume kumwambukiza mwanamke kuliko mwanamke kumwambukiza mwanamume. Hii ni kwa sababu ngozi na misuli ya uke, kuzunguka kinembe na kuzunguka mashavu ya nje ya uke ni laini sana. Ngozi hii inapata michubuko, vidonda na kuchanika. Michaniko na michubuko ni midogo sana kiasi kwamba huwezi kuona kwa macho, lakini ni mikubwa kutosha VVU kupita kama ngozi laini inagusana na shahawa kutoka kwa mwanaume ambaye ana maambukizo. Mwanamume anapofanya ngono na mwanamke aliye na maambukizo ya VVU yuko hatarini vilevile kupata maambukizo. Uume unakutana na majimaji ya ukeni ambayo yana VVU. Kama mwanamke ana VVU, vinasafiri kupitia kwenye mrija wa uume. Iwapo hajatahiriwa VVU vinaweza kupita kwenye ngozi hii laini hususani kama vipo vidonda, michubuko au mikato. VVU vinaweza kuenea kwa njia nyingine vilevile. Njia hizi ni pamoja na: Mama kwa mtoto wakati wa mimba, au wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha. Mgusano wa damu ya mtu ambaye ana maambukizi. Inawezekana ikawa wakati wa kuongezewa damu, kujikata na kisu cha kuchangia au wakati watu wanaotumia dawa za kulevya wanachangia sindano. Siku hizi damu inayotumika kuwaongezea wagonjwa inachunguzwa kwa makini kuhakikisha kwamba haina maambukizo.hata hivyo, sherehe nyingi za kimila kama kutahiri na kukata vitu mwilini zinaendelea kutumia njia ambazo siyo salama kama vile kuchangia kisu kimoja au wembe kwa watu wote wanaotegemewa kufanyiwa. Kamwe usichangie wembe na ndugu zako au marafiki zako na wala usichangie visu visivyochemshwa wakati wa sherehe ya kutahiri au tukio lolote la kimila. Bado haijathibitishwa kama mtu anaweza kupata VVU kupitia kwenye mate wakati wa kubusu. Hata hivyo, iwapo mtu ana mkato/kidonda mdomoni anaweza kupata maambukizo kwa kumbusu mtu ambaye anayo maambukizo ya VVU na anavyo vidonda vilevile. Kwa vile VVU vipo ndani ya shahawa na majimaji ya ukeni, kujamiiana kwa njia ya mdomoni hakuepushi hatari. Iwapo mtu ana mchubuko au kidonda mdomoni na wakati huohuo akapata shahawa au majimaji ya ukeni mdomoni, anaweza kupata VVU. VVU havienei kwa kugusana kwa kawaida kama vile kukumbatiana, kushikana mikono au kumgusa mtu mwenye maambukizo. VVU vinaishi kwa muda mfupi sana vinapokuwa nje ya mwili, kwa hiyo haviwezi kuenezwa kwa njia ya kumgusa mtu aliye na maambukizo au kuchangia vitu kama beseni, vyombo vya kulia chakula, nguo, vitabu n.k. Wengi wetu tunao wagonjwa wenye UKIMWI ndani ya familia zetu na tunatakiwa kuwatunza wanapougua. Ni muhimu unapomhudumia mgonjwa kujikinga ili usipate maambukizo. Unachotakiwa kuhofia ni majimaji ya mwilini kama vile, majimaji yanayotoka kwenye vidonda, damu ya hedhi na uharo. Jilinde mwenyewe kwa kuvaa glovu unapomsaidia kuoga au unaposafisha kitu chochote chenye damu au majimaji yoyote ya mwilini. UTAJUAJE KAMA UNA VVU? Huwezi kujua kwa kujiangalia mwili. Huwezi kutambua kama watu wengine wana VVU kwa kuwaangalia. Hata kama watu wana UKIMWI walipata maambukizo ya VVU muda mrefu na wamekuwa wagonjwa huwezi kujua kama ni UKIMWI kwa kuwaangalia labda kama wewe ni mhudumu wa afya. Hii ni kwa sababu magonjwa mengi yanayoambatana na UKIMWI yanaweza kujitokeza yenyewe kwa watu ambao hawana VVU. Kwa mfano, unaweza kuugua kifua kikuu ukiwa na VVU au usipokuwa navyo. Ipo njia moja tu ya kujua kama una VVU. Katika nchi nyingi upimaji wa VVU unaambatana na ushauri nasaha majadiliano ya undani na mtu aliyesomea, mwenye huruma na ambaye anaweza kukusaidia Mtu yeyote anaweza akawa ameambukizwa vvu ili uweze kumudu hali yako ya bila kuwa na dalili. Usitegemee muonekano wa kuwa na VVU na kujifunza jinsi mtu kuamua kuwa fulani hana vvu. ya kujihudumia. Kama hujapata maambukizo, mshauri anaweza kukuelimisha ufanye hadhari ili usipate maambukizo. Vipimo vya UKIMWI vinaaminika ni sahihi, salama na haviumi. Mhudumu wa afya anachukua damu kidogo kutoka kwenye mkono wako. Unaweza kupata majibu katika muda wa saa moja, au unaweza kuambiwa urudi baada ya wiki moja au mbili kutegemeana na kipimo Vipimo vya VVU vinafanyaje kazi? kinachotumika. Ili kujua kama ni kweli huna VVU, utaambiwa urudi kupima tena baada ya miezi 3 hadi 6 wakati kipindi cha kusubiri kimepita. KWA NINI UPIME VVU? Zipo sababu nyingi za kupima VVU. Iwapo mara kwa mara unakuwa na hofu kuhusu maambukizo ya VVU na una wasiwasi kutokana na mabadiliko ya afya yako mara kwa mara inawezekana njia pekee ya kutuliza akili ni kupima. Iwapo ulifanya ngono na mtu ambaye anaumwa na umesikia ana UKIMWI, hapo utahofu zaidi. Labda njia pekee ya kutuliza akili ni kupima na kujua kama umepata maambukizo au la. Kamwe usidhani kwamba umepata maambukizo, pima ili ujue. Mtu anapokuwa na maambukizo mwili hushituka na kutoa askari ili kupigana na maambukizo. Kipimo cha VVU kimetengenezwa kutambua kama askari wa VVU wapo au hawapo ndani ya mwili wa binadamu. Ikiwa wapo wengi, maana yake mtu huyo ana maambukizo ya VVU na kwamba mwili unajaribu kupigana na maambukizo. Kwa kawaida askari wanaopimwa na kipimo cha VVU huonekana mwezi mmoja baada ya maambukizo. Hata hivyo, mara nyingi askari wa VVU hutokea baada ya muda zaidi kama miezi 3 hadi miezi 6 baada ya maambukizo. Katika kipindi hiki kipimo cha VVU hakitaona askari. Kwa maneno mengine, miezi 3 mpaka miezi 6 baada ya maambukizo, mtu anaweza kupima na kuonekana hana maambukizo ingawa anayo maambukizo. Vile vile, mtu huyu anaweza kuambukiza watu wengine katika kipindi hiki kabla askari wa VVU hawajaonekana kwenye kipimo. Kwa hiyo,- kama mtu yuko hatarini kupata VVU na akapima na kuonekana hana VVU, bado anashauriwa kurudia baada ya miezi 6 ili kuwa na uhakika kama hana maambukizo

66 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Unafahamu kuhusu kuishi kwa matumaini na VVU? V Hamza alijua ana VVU miaka minne iliyopita. Wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 18 naye anaeleza hadithi yake: Nilitoka viupele mwilini. Hii ilinisukuma nikapime. Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu, lakini kwa msaada wa ushauri nasaha nilikubaliana na hali halisi. Niliweza kumaliza kozi yangu ya ufundi magari. Ushauri nilioupata uliniwezesha kuishi mpaka hivi sasa. Nimeweza kubadili tabia. Nimeacha kuvuta sigara na kunywa pombe. Ninaye rafiki wa kike ambaye ana VVU vilevile. Ili kuepuka kuongezea maambukizo, tunafanya ngono salama tunatumia kondomu. Vilevile ninaepuka kuwa na mfadhaiko na ninatibu magonjwa madogomadogo yanayonishambulia. Kitu kimoja cha muhimu nilichojifunza ni kuepuka kujionea huruma, na hili ndilo linalonifariji. Ninajihusisha sana katika michezo ya kuigiza ambayo inatumika kuelimisha vijana kuhusu kujizuia na VVU/UKIMWI na kuwahudumia waathirika. Ninawashauri vijana wasubiri kufanya ngono mpaka watakapokuwa wakubwa. Wale ambao wamepata maambukizo wanatakiwa kuikubali hali na kujiunga katika mapambano ili kuokoa maisha ya wale ambao hawajapata maambukizo. Hamza anaishi salama na VVU. Amekuwa jasiri na amekubaliana na hali yake. Anautunza mwili wake. Anaendelea na shughuli zake ametingwa, hapotezi muda. Ana upendo na maisha. Ana rafiki wa kike. Lakini anahakikisha hamwongezei maambukizo na wala yeye mwenyewe haongezewi maambukizo anatumia kondomu. Kuishi kwa matumaini kunaweza kukusaidia kuwa hai kwa muda mrefu. KUISHI KWA MATUMAINI NA VVU Kugundua kuwa una maambukizo ya VVU, siyo kitu rahisi kustahimili lakini unaweza kujifunza kumudu kuishi navyo. Utahitaji kupewa ushauri nasaha. Ni jambo zuri vilevile kumweleza mtu wa karibu yako ili usibebe mzigo peke yako. Kwa watu wengi ugonjwa unaendelea polepole, na wanaweza kuishi na VVU kwa muda wa miaka 10 hadi 20. Kuwa na matumaini. Wanasayansi wengi wanalifanyia kazi suala la VVU. Siku moja wataweza kufanikisha utafiti huo. Ukigundua umepata maambukizo ya VVU ni muhimu sana kuishi kwa matumaini. Kuishi kwa matumaini kunaweza kuboresha sana nafasi yako ya kuwa na afya kwa muda mrefu. Kuishi kwa matumaini na VVU maana yake ni:- Kumweleza mwenzi wako (unayeshirikiana naye ngono kuwa wewe ni mwathirika). Kuwatunza kwa upendo wale wote unaowapenda, na kushiriki ibada za dini yako. Tumia muda wako katika kumcha Mungu. Kula chakula bora kama vile mboga za majani, maharage, samaki wa kukausha kwa sababu hivi vinasaidia kuboresha kinga ya mwili. Kuishi kwa matumaini, kuikubali hali ilivyo na kutokunyanyapaliwa. Unafahamu kinachotokea unapokwenda kupima? Susan ana umri wa miaka 19, aliamua kwenda kupima na sasa anaeleza kilichotokea. Niligundua kwamba rafiki yangu wa kiume amefanya ngono na msichana mwingine. Niliachana naye. Lakini bado nilikuwa na hofu kwamba ningeweza kuwa nimepata maambukizo ya VVU. Tumekuwa tukifanya ngono isiyo salama (bila kinga). Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana. Sasa nimegundua. Nilihofu sana kuhusu VVU! Nilijua kuna njia moja tu ya kutuliza akili yangu: kwenda kupima. Siku moja nilipata ujasiri wa kwenda. Nilienda kwenye kituo cha maelezo kuhusu UKIMWI mjini Kampala. Nilipofika getini, niliogopa. Nilisimama pale kwa muda mrefu. Mwisho niliingia ndani. Niliandikishwa, nikapewa namba yangu na nikaambiwa nimsubiri mshauri. Baada ya dakika tano, alikuja na akanichukua pamoja na wengine wanne tukaenda kwenye chumba kingine. Tulipewa ushauri nasaha kama kundi. Alituuliza tulikuwa tunajua nini kuhusu VVU/UKIMWI na alijibu maswali yetu. Kilichofuata, mimi na mshauri tulikutana faragha. Aliniuliza lini nilifanya ngono kwa mara ya mwisho, nilikuwa na marafiki wa kiume wangapi na kama nilitumia kinga. Aliniambia ninaweza kutoka nje wakati wowote kama ningaliamua kutopima. Lakini nilimweleza kwamba nataka kupima. Baada ya hapo alinipeleka chumba kingine ambako alinitoa damu kidogo kutoka kwenye mkono. Alifanya haraka sana na wala haikuuma. Baada ya damu kuchukuliwa nilienda kwenye chumba cha ushauri nasaha na mshauri alizungumza na kila mtu kuhusu nini maana ya kuwa na VVU au kutokuwa na VVU. Alituuliza ni kwa jinsi gani tutamudu iwapo majibu yatakapoonyesha kuwa tumeathirika, na jinsi tutakavyojilinda tusipate maambukizi zaidi au tusiwaambukize wengine. Alituuliza namna gani tutahakikisha tunabakia watulivu iwapo majibu yatatokea kuwa hasi. Baada ya kupewa ushauri nasaha kwa kikundi, tuliitwa kwenye chumba cha faragha kupewa majibu yetu. Nilikuwa wa kwanza kuitwa. Jasho lilikuwa linanitoka na mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio. Nilitaka kukimbia nitoke, lakini niliyahitaji majibu. Majibu yako ni mazuri, huna VVU, niliambiwa na mshauri. Nilifumba macho, nikasali sala ya shukurani. -Niliapa kutofanya ngono tena bila kusisitizia matumizi ya kondomu. Mshauri aliniambia kwamba, kwa vile ni zaidi ya miezi sita tangu nilipofanya ngono kwa mara ya mwisho, ninaweza kuamini majibu haya na nisingehitaji kipimo kingine cha kuhakikisha kwamba nilikuwa sina VVU. Nilipotoka nje, nilijisikia nafuu na mwenye furaha. Na yote haya yalifanyika kwa muda wa saa moja tu

67 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Tibu magonjwa yote yanapojitokeza. Pumzika na fanya mazoezi mepesi. Jiunge na jumuia au vikundi vya kusaidia watu wanaoishi na VVU/UKIMWI. Fanya ngono salama ili usimwambukize mtu mwingine virusi au mwenyewe kujiongezea virusi vipya mwilini mwako. Kuishi chanya maana yake ni kuishi kwa kadiri ya upeo wako kila siku. Kuishi chanya ni kitu ambacho kila mtu anatakiwa kufanya hata kama hatuna maambukizo ya VVU. Vilevile ni muhimu kuwasaidia watu wengine waishi kwa matumaini na VVU. Usiwaite watu wenye VVU au UKIMWI waathirika kwa sababu siyo waathirika. Ni kama watu wengine, walio na vitu vingi vya kufanya. Wanaweza kufanya kazi na kuchangia maendeleo. Wanahitaji upendo na kusikilizwa kama watu wengine. Mara kwa mara wanahitaji msaada wa pekee kutoka kwa marafiki wa karibu. Inawapasa ndugu kuwa na mtazamo unaowajali / usiowabagua watu wenye VVU. Kamwe usiwatanie, kuwanyanyapaa au kuwasumbua katika jamii. Ulikuwa unafahamu kwamba: NGONO SALAMA / MAPENZI SALAMA UKWELI KUHUSU VVU/UKIMWI Watu milioni 42 duniani wanaishi na VVU kwa sasa. Kati ya hawa karibu robo wana umri wa miaka kati ya 15 na 24. Watoto na vijana chini ya miaka 18 wanawakilisha zaidi ya asilimia 10 ya wanaoishi na VVU*. Nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zimeathirika sana na VVU/UKIMWI, na UKIMWI ndiyo ugonjwa unaosababisha vifo vingi. Kati ya watu wote wanaoishi na VVU, milioni 29.4 ni kutoka eneo hili na kulikuwa na maambukizo mapya ya watu milioni 3.5. Kwa ujumla, VVU vinaenea kwa njia ya kujamiiana. Asilimia 90 ya maambukizo Afrika yanatokana na kujamiiana. Duniani kote, wapo watoto milioni 14 ambao ni yatima kwa sababu ya UKIMWI na kati ya hawa milioni 12.1 wanaishi Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ugonjwa huu wa mlipuko unapunguza matarajio ya muda wa kuishi katika Afrika. Mwishoni mwa miaka ya 1990, watu Afrika walitarajia kwa wastani kuishi miaka 59. Lakini kutokana na VVU/UKIMWI, matarajio ya muda wa kuishi kwa watu wa Afrika itashuka hadi miaka 45 tu kufikia mwaka Ngono salama maana yake ni kufanya mapenzi ambayo yanapunguza uwezekano wa wewe kupata magonjwa ya ngono, ikiwa ni pamoja na VVU au mimba. Ukitaka mapenzi salama kwa asilimia mia moja (100%) basi uchaguzi ulio bora zaidi ni kupiga punyeto na kuacha kabisa kujamiiana. Kama ukisoma sura ya 9 utafahamu kwamba punyeto ni salama kabisa, upo peke yako. Majimaji ya sehemu za siri ni yako mwenyewe. Huwezi kupata maambukizo kutoka kwa mtu yeyote na wala huwezi kujipa au kumpa mtu mwingine mimba. Kubusu au kumkumbatia mwenzi wako ni mapenzi salama. Mpaka sasa hivi haijathibitishwa kama VVU vinaenezwa kwa njia ya kubusu au kukumbatia. Hata hivyo, kama mmojawapo ana maambukizo ya VVU na ana vidonda mdomoni anaweza kumwambukiza mwenzake. Vilevile kuna uwezekano wa maambukizo kutokea iwapo mtagusana via vya uzazi na kupata majimaji ya ukeni au shahawa mikononi. Kama una mikato au michubuko mikononi unaweza kupata maambukizi ya VVU kama mtu mwingine ana maambukizi. Kujamiiana kati ya watu wawili ambao wote hawana maambukizo ya magonjwa ya zinaa au VVU ni mapenzi salama. Lakini, bila shaka bado patakuwa na hofu ya mimba.watu wengi hufikiria kwamba kwasababu wamekuwa na uhusiano na mtu kwa muda mrefu, wanaamini kuwa hawana VVU na magonjwa mengine ya ngono. Lakini mmoja wao akipima ndipo ukweli unadhihirika. Watu unaowaamini na kuwapenda wanaweza kukuambukiza magonjwa ya zinaa. Wanaweza wakawa hawajui kuwa wamekuambukiza. Andrew kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Ninajiamini mwenyewe; sina maambukizo ya magonjwa ya ngono kwa sababu sijawahi kujamiiana na mtu yeyote. Anthony kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Sababu nzuri kuliko zote ya kumfanya kijana acheleweshe kuanza ngono ni kwamba ana uhakika wa kutopata UKIMWI na magonjwa mengine ya ngono. Milensu kutoka Zambia (Umri wa miaka 13) Kusema HAPANA sitaki kujamiiana ni njia mojawapo ya kujikinga na hatari ya kupata magonjwa na inakufanya udhibiti maisha yako. Kondomu vilevile ikitumika vema hufanya tendo la ngono kuwa salama. Kwa kweli kondomu ni muhimu katika kukulinda wewe na mwenzi wako. Hata kama hujaanza kujamiiana, ni vema usome somo linalofuata kwani kuna siku utahitaji kuzifahamu kondomu. KONDOMU Hujachelewa kuanza kutumia kondomu. Kondomu ni mfuko laini uliotengenezwa kwa mpira ambao unavalishwa kwenye uume kabla ya kuanza kujamiiana. Mwanaume anapofikia mshindo, anakojoa shahawa ambazo hunaswa kwenye chuchu ya kondomu. Kwa vile shahawa zinakusanyika kwenye kondomu ina maana majimaji ya mwanaume hayamwingii mwanamke na wala uume haugusi majimaji ya ukeni kwa sababu uume umefunikwa na kondomu

68 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Kama ikitumika kiusahihi na kwa kukubaliana, kondomu ni kinga kamili dhidi ya magonjwa ya ngono, ikiwa ni pamoja na VVU na uzuiaji wa mimba. Kondomu zinazuia vijidudu, bakteria na virusi vilivyo ndani ya uke kukutana na uume, na huzuia mbegu za kiume, bakteria na virusi ndani ya shahawa kuingia ukeni. Ijapokuwa kondomu zinaonekana nyembamba sana, zimetengengezwa na mpira imara (lateksi) na zimejaribiwa kwa kutumia nguvu za electroniki ili kuhakikisha kwamba kiwango chake ni cha juu. Watu wengine wanasema kwamba kondomu zina matundu madogo sana ambayo yanaweza kupitisha VVU. Hii siyo kweli. VVU haviwezi kupita kwenye kondomu. Hata hivyo, kondomu inaweza kuwa na matundu kama muda wa kutumika umekwisha au imetunzwa vibaya au imewekwa visivyo. Ni muhimu sana kufuata taratibu za matumizi ya kondomu kila mara na kila wakati unapozitumia: Seif, kutoka Tanzania(Umri wa miaka 13) Ngono salama ni kutumia kondomu. Niliyasikia haya kutoka kwa watu na vilevile kwa kusoma magazeti. Sijawahi kufanya ngono. Sospita, kutoka Tanzania(Umri wa miaka 13) Nimesikia kuhusu kondomu. Nilisoma kwamba zinakukinga usipate maambukizo ya magonjwa ya ngono na VVU. Godfrey, kutoka Zimbabwe(Umri wa miaka 19) Sina uhakika kama nitafanya mapenzi na mtu yeyote bila ya kutumia kondomu. Sioni kama hilo linaweza kutokea. Chana pembezoni mwa pakiti kwa uangalifu. Usitumie meno na hakikisha kucha hazichani kondomu. Usiikunjue kondomu harakaharaka. Iweke kwanza kwenye kiganja chako na itasimama kama kofia. Valisha kondomu mara uume unapodinda vizuri na kabla haujagusa uke. Shika chuchu ya kondomu ukiwa unaiviringisha chini ya uume. Kondomu inatakiwa iende yenyewe kiurahisi. Kama haishuki kiurahisi basi jua umeigeuza ndani nje. Itupe kondomu hiyo na uchukue mpya. Usitumie kondomu iliyogeuzwa ndani nje kwa sababu inaweza ikawa na shahawa ambazo zina mbegu za kiume au vijidudu vinavyoambukiza magonjwa ya ngono Baada ya kukojoa, shika ukingo wenye bangili wa kondomu na toa uume toka kwenye uke. Hii itasaidia kuzuia kondomu isiteleze. Tupa kondomu kwenye choo cha shimo, choma au fukia ardhini. Usiache kondomu mahali ambapo watoto wataiona na wala usitupe kwenye choo cha kuvuta maji kwani itaelea. Yafuatayo ni maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia kondomu kwa usahihi ili zisipasuke na wala zisiteleze na kutoka. Angalia juu ya pakiti tarehe ya kwisha matumizi au tarehe ya kutengenezwa. Kama tarehe ya kwisha matumizi imepita, usiitumie! Kama tarehe ya kutengeneza ni zaidi ya miaka mitatu iliyopita, usiitumie! Kumbuka kuwa hata kondomu zinazotumika kuzuia mimba zisitumike zaidi ya miaka miwili baada ya tarehe ya kutengenezwa. Kamwe usitumie kondomu ambayo pakiti yake imetoboka. Zaidi ya hapo usitumie kondomu ambayo ganda lake lina rangi zilizochujuka au halina rangi kabisa au kama ganda ni gumu limekakamaa au linanata sana. Tunza kondomu sehemu ambayo kuna ubaridi kiasi, kiza na pakavu. Joto, mwanga na unyevuunyevu vinaharibu kondomu. Usitunze kondomu kwenye pochi au mfukoni. Ikiwezekana tumia kondomu zenye vilainishi au tumia vilainishi kama kondomu siyo laini. Vilainishi vinaweza kusaidia kondomu isipasuke au kuchanika wakati wa kujamiiana. Tumia vilainishi vyenye asili ya maji tu. Vilainishi vizuri ni pamoja na maji na dawa za kuulia mbegu za kiume. Majimaji ya ukeni ya asili yanaweza kuwa kilainishi. Kamwe usitumie vilainishi vyenye asili ya mafuta. Usitumie vaselini, mafuta ya maji (ya kupikia, ya watoto, ya nazi, petroli), jeli ya petroli, vipodozi vya aina zote, siagi, malai ya kokoa au majarini. Vyote hivi vinaweza kudhoofisha uimara wa kondomu. Usikunjue kondomu kabla ya kutumia. Kondomu ambayo imeshakunjuliwa ni vigumu kuivaa. Tumia kondomu mpya kila unapofanya ngono baada ya mshindo. Kamwe usitumie kondomu zaidi ya mara moja na usivae zaidi ya moja. Watu wachache wanadhurika kiafya na mipira aina ya lateksi. Hivyo kondomu hizi zinawasababishia viupele na ngozi kuwasha. Kama unalo tatizo kama hili, zipo kondomu ambazo hazitengenezwi kwa kutumia mpira wa lateksi. Tumia hizo. Zungumza na mhudumu wa afya namna ya kuzipata. Watu wengi wanaotumia kondomu wanasema zinawafanya wenza wote wawili wafurahie ngono. Wenza wote wanaweza kupumzika na kutulia zaidi wanapokuwa hawana hofu ya mimba au kupata magonjwa ya ngono. Wanaume wengine wanasema kondomu zinawasaidia wasifikie mshindo wasikojoe haraka na kuwafurahisha wenzi wao. 4. Endelea kushika chuchu ya kondomu wakati unaendelea kuiviringisha kondomu mpaka uifikishe kwenye shina kabisa. Hii nafasi ya ziada (chuchu) ni kwa ajili ya shahawa baada ya kukojoa (kufikia mshindo). Lakini pia wapo wanaume na wanawake ambao hawapendi kutumia kondomu kwa sababu wana hofu kuwa hawatafurahia ngono vizuri. Hivyo, mwanaume anaweza kumdanganya mpenzi wake kwamba hana ugonjwa hivyo kumtaka amwamini na asiwe na sababu yoyote ya kuwa na hofu

69 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Anaweza kumfanya mwanamke ajisikie vibaya kwa kumuuliza ni kwa nini hamwamini. Lakini ikumbukwe kuwa yeyote anaweza kuwa na maambukizo ya magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na VVU kutokana na uhusiano uliotangulia hata bila ya kuona dalili zozote. Kwa hiyo, ni kwa faida ya wote kutumia kondomu. Kondomu inatoa kinga kwa wale watakaohusika. Kuitumia kondomu ni alama ya kuaminiana, kuheshimiana na kujaliana. MATATIZO MENGINE YA AFYA YA UZAZI Je, unazifahamu kondomu za kike? Umewahi kusikia kuhusu kondomu za kike? Hii ni njia nyingine ya kujikinga dhidi ya VVU, magonjwa mengine ya ngono na mimba. Hiki ni kimfuko kilicholainishwa kama kondomu ya kawaida ya wanaume. Lakini, badala ya kufunika uume, inakinga uke kama kizuizi dhidi ya maambukizo. Inavyofanya kazi: Kuna pete ndogo mbili; moja ni pete ndogo ndani ya kondomu na ya pili ipo upande uliowazi ambayo hukaa nje ya mwili. Pete hizi hushikilia kondomu ya kike ikae mahali pake. Kondomu ya kike, kama kondomu ya kiume inazuia mbegu za kiume kukutana moja kwa moja na uke. Kama uume unabakia ndani ya kondomu na pete ya nje inabakia mahali pake basi kondomu itafanya kazi. Jinsi ya kutumia: Inaweza kuchukua muda ili kuweza kuivaa kondomu vizuri kama mazoezi yalivyo kwa kondomu za kiume. Lakini mwisho utazoea. Kwanza ikunje pete ya ndani iwe na alama ya nane (8). Kisha isukume ndani kiasi utachoweza mpaka utakapoona huwezi kuisukuma zaidi. Kondomu itakapokuwa imekaa sehemu yake, ongoza uume wa mwenzi wako ndani ya kondomu. Tumia kondomu ya kike moja kwa wakati mmoja. Usirudie kuitumia kondomu hiyo. Jinsi ya kuitoa: Ni rahisi sana kuitoa. Sokota pete ya juu ili shahawa zisimwagike, halafu vuta kondomu nje na itupe ndani ya choo cha shimo au choma moto au fukia ndani ya shimo. Faida yake: Kondomu ya kike ni njia pekee ya kujikinga ambayo inadhibitiwa na mwanamke mwenyewe ili imlinde dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya zinaa, VVU/ UKIMWI na mimba. Inakaa taratibu ndani ya uke na haibani uume unapoingia. Yapo matatizo ambayo yanatokea kwenye via vya uzazi lakini siyo magonjwa ya zinaa. Hata kama hujawahi kufanya ngono, yapo maambukizo ambayo unaweza kuyapata sehemu zako za siri. Unaweza ukapata maambukizo kwenye njia ya mkojo ambayo husababisha kuwashwa au maumivu unapokojoa mkojo. Ukiona uchafu wa ajabu unatoka au maumivu au damu wakati unapokojoa, unatakiwa kumwona mhudumu wa afya. Zungumza na mwenzi wako kuhusu matumizi ya Kondomu. Eleza unavyojisikia na unachotaka. KANDIDIASISI Kama sehemu zako za siri zinawasha na unatokwa na uchafu wa ajabu ukeni unaweza ukawa na kandidiasisi. Hili ni tatizo la kawaida. Ugonjwa huu vilevile unaitwa maambukizo ya hamira na unasababishwa na kuvu wanaofanana na hamira wanaoitwa kandida albicans. Ugonjwa huu unawasumbua wasichana na wanawake wengi. Wavulana wanaweza kupata kandida chini ya govi. Kandida ni kiumbe kimojawapo ambacho kwa asili kinaishi juu ya mwili. Kwa kawaida kandida hakisababishi matatizo yoyote. Kinadhibitiwa na kinga ya mwili na bakteria wengine ambao kwa kawaida wanaishi ukeni. Lakini ikiwa kinga ya mwili imeshaharibiwa na haifanyi kazi vizuri, viumbe kandida huzaliana haraka. Mara kwa mara tatizo hili hutokea kabla au baada ya damu ya hedhi kutoka na wakati wa mimba. Kandidiasisi inaweza kuenea kwa njia ya kujamiiana na mtu ambaye ana kandida wengi. Lakini inaweza kusababishwa na mambo mengine vilevile. Mfadhaiko, kama vile mitihani, kifo ndani ya familia au mabishano yanaweza kuwa kichochezi cha kandidiasisi. Wakati mwingine unaweza kupata kandidiasisi ukinywa kiuavijasumu Viuavijasumu vinaua bakteria ambao kwa kawaida wanaishi ukeni. Watu wanaoumwa kisukari na wale wenye VVU wanapata kandidiasisi mara kwa mara. Kandidiasisi si ugonjwa wa ngono kwa sababu hata bikira wanaupata. Joto linapozidi na unyevunyevu kuzunguka eneo la via vya uzazi vinaweza kusabisha kandidiasisi. Hii ina maana ya kwamba unaweza kujiletea mwenyewe kandidiasisi kwa kuvaa nguo zisizofaa. Kama, kwa mfano ukivaa nguo za nailoni, kaptura za kubana au suruali aina ya jeans zinazobana na kukaa kwa saa kadhaa huku umebananisha miguu, pengine kwenye basi, unatengeneza unyevuunyevu na joto ambalo kandida wanahitaji ili waishi. Dalili za kandidiasisi ni:- Kuwashwa kwenye via vya uzazi, wote; wasichana na wavulana. Usaha kutoka ukeni au chini ya govi unaofanana na maziwa yaliyoharibika. Kuvimba na kuwepo kwa utando telezi wa uke na midomo ya ndani au kichwa cha uume kuwa chekundu. Iwapo utapata mojawapo ya dalili hizi omba msaada kutoka kwa mhudumu wa afya mwenye ujuzi ambaye atakupatia matibatu yanayotakiwa. Matibabu yanayotakiwa kawaida ni:

70 SURA YA 10 Kutunza Afya Yako Ya Kiujinsia Dawa za kupaka zinazotibu kuvu au wakati mwingine kidonge kinachotumbukizwa ndani ya uke. Iwapo umeishaanza ngono, mwenzi wako anatakiwa kutibiwa pia ili asikuambukize tena. Vilevile, unaweza kusafisha taratibu eneo la via vya uzazi na maji yenye chumvi kidogo. Kuwa safi kwa kusafisha mara mbili kwa siku. Usifute via vya uzazi kwa sababu utasababisha vidonda ambavyo itabidi vitibiwe. Usikune uke, na nawa mikono baada ya kushika sehemu za siri. Vaa nguo safi zilizokauka na chupi za pamba. Kumbuka kuanika chupi juani. Iwapo maambukizo ya kandidiasisi yanajirudiarudia ni vema kwenda kupima VVU. Maambukizi yanayojirudiarudia ni alama ya kinga kuwa dhaifu. MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO Wanawake na wanaume wanaweza kupata maambukizo kwenye njia ya mkojo, lakini zaidi kwa wanawake kwa sababu ni rahisi bakteria kuingia kwenye njia ya mkojo. Dalili za maambukizo ni: Kutaka kukojoa mara kwa mara Kusikia maumivu makali wakati wa kukojoa Mkojo kuchanganyikana na damu. Maambukizi haya yanaweza kuepukwa kwa kujiweka safi hasa kwa kusafisha eneo la via vya uzazi kila siku na kuhakikisha unanawa baada ya kwenda haja kubwa. Wakati wote unasafisha kutoka mbele kuelekea nyuma. Ukisafisha kutoka nyuma kwenda mbele unaweza kusambaza bakteria kutoka kwenye mkundu kwenda kwenye tundu la mkojo. Hatua nyingine za kuchukua ili kuepuka maambukizo haya ni kunywa maji mengi; kukojoa mkojo mara kwa mara (usijaribu kubana mkojo kwa muda mrefu) na hasa baada ya kujamiiana, na kuvaa chupi za pamba na nguo pana zinazoweka sehemu za siri kavu. Iwapo unafikiri unayo maambukizo kwenye mrija wa kupitisha mkojo, kunywa maji mengi na nenda kamwone mhudumu wa afya kwa ajili ya matibabu. Usijamiiane mpaka dalili zote ziwe zimetoweka. KANSA / SARATANI YA SHINGO YA MLANGO WA KIZAZI Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi inaathiri mlango wa mfuko wa kizazi. Seli zinapokuwa na saratani zinaongezeka haraka kuliko seli za kawaida mwilini mwako. Seli za Saratani zinavamia na kuchukua nafasi ya tishu zilizo na afya mwilini mwako na hatimaye ugonjwa unaweza kuua. Ugonjwa huu unawapata sana wanawake wakubwa (zaidi ya miaka 40). Lakini sasa hivi unajitokeza hata kwa vijana wa umri mdogo. Saratani ya shingo ya mlango wa mfuko wa kizazi inaweza kuonekana mapema kwa kutumia utaratibu unaoitwa Pap smea. Mhudumu wa afya atatakiwa akusanye seli kwenye mlango wa mfuko wa kizazi. Kwa kutumia darubini, seli ambazo si za kawaida na ambazo zinaweza kuwa na saratani zinaangaliwa kama zipo. Ikiwa zipo seli ambazo si za kawaida zinaweza kuondolewa. Saratani ya mlango wa mfuko wa kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema. Kwa vile ni muhimu kugundua mapema saratani hiyo, madaktari wanashauri kwamba wanawake wote ambao wanajamiiana wapime kipimo cha pap smea kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano. Kama harufu mbaya au uchafu unatoka ukeni au kama damu inatoka unapojamiiana, mwone daktari kwa sababu hizi zinaweza kuwa dalili za kuwa na tatizo kwenye mlango wa mfuko wa kizazi. Unajiweka kwenye hatari ya kupata kansa ya kizazi ikiwa utaanza kufanya ngono katika umri mdogo (kabla ya miaka 20) au kama utashiriki ngono na watu zaidi ya watatu katika kipindi cha uhai wako. Kuweka sugu sehemu za siri kunaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata kansa ya kizazi. Ugonjwa wa kansa ya kizazi ni sababu ya msingi ya kukufanya uamue kusubiri hadi ufike miaka 20 ndipo ufanye ngono. Pia, ni sababu ya kukufanya uamue kuwa na mpenzi mmoja na utumie kondomu kila mara. Sura ya 10 Kujali na Kuhudumia afya yako ya kijinsia Magonjwa ya zinaa au maambukizo yatokanayo na ngono ni maambukizo ambayo yanaenea kwa njia ya kujamiiana. Yanaenea kwa njia ya majimaji ya watu wawili kama vile shahawa, majimaji ya ukeni na damu. Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika, lakini bado yanaweza kuharibu via vya uzazi na kufanya mtu asizae. Dalili za magonjwa ya ngono ni pamoja na:- Vidonda, malengelenge, uvimbe na vipele sehemu za siri. Usaha kutoka kwenye uume. Usaha wenye rangi ya ajabu na harufu mbaya kutoka ukeni. Maumivu wakati wa kujamiiana au wakati wa kukojoa. Magonjwa mengine ya ngono hayatibiki. UKIMWI ni mmojawapo wa magonjwa ya ngono ambayo hayatibiki. VVU husababisha upungufu wa kinga mwilini. Maambukizo ya VVU yanasababisha UKIMWI. (Upungufu wa Kinga Mwilini) Ugonjwa huu unasababisha kinga ya mwili (mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa) ushindwe kufanya kazi. Hakuna dawa ya kuzuia maambukizo ya VVU, na hakuna dawa ya kutibu UKIMWI. Haiwezekani kumtambua mtu mwenye maambukizo ya VVU kwa kumwangalia tu. Mtu anaweza kuwa na afya yake kwa muda mrefu kabla dalili hazijaanza kujitokeza. Mtu anaweza asifahamu kama amepata maambukizo kwa miaka kadhaa. Usije ukadhani kwamba mtu hana VVU, na usije ukadhani kwamba mtu anavyo VVU. Ni muhimu kupima. Iwapo una wasiwasi kuhusu magonjwa ya ngono, ni jambo jema kwenda kupima na kupata matibabu kama yanatakiwa. Usije ukajitibu mwenyewe na dawa na wala usichangie dawa na mtu mwingine. Iwapo utafahamu kwamba umepata maambukizo ya VVU, pata ushauri. Usijaribu kukabili tatizo hili peke yako. Kama utajitunza vizuri unaweza kuwa na afya nzuri na kuishi maisha yenye manufaa. Zipo njia zitakazokuepusha kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono pamoja na VVU:- Acha kabisa kujamiiana. Ishia kubusu na kukumbatiana tu. Iwapo umeshaanza kujamiiana tumia kondomu kila mara ili kujikinga. Hakikisha unajua jinsi ya kutumia kondomu kiusahihi. Siyo kweli kwamba matatizo yote yaliyopo kwenye via vya uzazi ni magonjwa ya ngono. Yapo maambukizo kama kandidiasisi na maambukizo ya njia ya mkojo ambayo hayasababishwi na kujamiiana. Haya husababisha pia matatizo katika sehemu za siri. Kwa ujumla, maambukizo haya yanaweza kuepukwa kwa kuimarisha usafi sehemu za siri. Iwapo unasikia maumivu au muwasho sehemu za siri mwone mhudumu wa afya

71 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Mimba inatokana na watu wawili, mwanaume na mwanamke. Wote wawili wanawajibika. Sura hii haihusu wasichana peke yao. Wavulana wanatakiwa kusoma pia. Mimba na kuzuia mimba zisizotakiwa ni wajibu wenu wote wawili msichana na mvulana. MIMBA INATOKEAJE? Mwanamume na mwanamke watakapofanya ngono isiyo na kinga, kuna uwezekano wa mwanamke kupata mimba. Mwanamume anapokojoa shahawa ndani ya uke, shahawa hizo zinaingia kwenye uke na kuogelea kwenda kwenye mlango wa mfuko wa kizazi. Zikitoka kwenye mfuko wa kizazi zitaogelea hadi kwenye mirija ya kupitisha yai na hapo zinaweza kuishi kwa muda wa siku 3 hadi 5 Kama yai litakuwa limeshaingia kwenye mirija ya kupitisha yai au litafika hapo katika kipindi cha siku 3 hadi 5, moja ya mbegu za kiume inaweza kuliingia yai na kulirutubisha. Seli mpya ijulikanayo kama Zaigoti inaundwa ikiwa ni muungano wa yai na mbegu ya kiume. Zaigoti hugawanyika sehemu mbili kutengeneza seli mbili zinazofanana. Seli mbili hizi zinagawanyika kufanya seli 4, nazo seli nne zinagawanyika mara mbili kutengeneza seli 8, na kuendelea. Mara kibonge cha seli nyingi kinatokea. Kibonge cha seli kinasafiri kutoka kwenye mirija ya kupitishia yai kwenda kujishikiza kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Kitendo cha seli kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi kinaitwa Upandikizaji. Upandikizaji unatokea wiki 3 baada ya hedhi yako ya mwisho. Huu ndio mwanzo wa mimba. Mbegu za kiume zikiogelea kwenye ukuta wa tumbo la uzazi kwenda kwenye yai Mwanzo wa mimba: yai lililoovushwa likipandikizwa kwenye ukuta wa tumbo la uzazi

72 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Kumbuka kuwa mimba inaweza kutokea kama utafanya ngono isiyo salama mara moja tu. Mimba inaweza kutokea kama mwanamume atakojoa shahawa zake karibu na uke hata kama hamkujamiiana! Shahawa zikimwagwa nje ya mlango wa uke bado zinaweza kuogelea hadi kwenye mlango wa mfuko wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi na kwenye mirija ya kupitisha yai. Utadhani hakuna uwezekano, lakini inatokea. DALILI ZA MIMBA Dalili ya wazi kuwa mimba imetungwa ni kukosa kupata hedhi. Hii ni kwa sababu ukuta wa mfuko wa kizazi hautoi damu mwanamke akiwa na mimba. Utando laini unabaki ndani ya mfuko wa kizazi na unatengeneza kiota laini kwa ajili ya mtoto kukua. Kukosekana kwa hedhi haina maana kuwa umepata mimba. Wasichana waliobalehe wanaweza kuwa na hedhi isiyo ya kawaida. Kwa miaka mingi siku za hedhi kwa baadhi ya wasichana balehe, zinaweza kuchelewa au zikakosekana mwezi mzima bila sababu yoyote. Dalili nyingine za mimba: Matiti kuwa laini Kichefuchefu (hali ya kutaka kutapika) na kuwa na mate mdomoni. Uchovu (kujisikia umechoka sana) Kutaka kukojoa mara kwa mara Kupendelea kula vitu fulani,wakati mwingine visivyo vya kawaida. Wanawake wachache huwa hawaoni dalili zozote kati ya hizo hapo juu. Kwa mfano, wanawake wengine hutoa damu kidogo sana wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya mimba zao na hivyo wanaweza kufikiri hedhi imekuwa na damu kidogo kuliko kawaida. Kama huna uhakika kuwa umepata au hujapata mimba, unaweza kufanya kipimo cha mimba. Katika sehemu nyingine, unaweza kununua kipimo cha mimba kwenye maduka ya dawa. Vilevile, unaweza kufanyiwa kipimo cha mimba kwenye kliniki. Mara nyingine kipimo kinafanywa kwa kupima mkojo na unaweza kugundua viini fulani ambavyo vinatengenezwa na mwili wakati wa mimba. Dakitari au nesi wa kituo cha afya anaweza vilevile akakufanyia uchunguzi wa mwili ili kuona kama una mimba au la. Mimba inachukuwa wiki 40 kabla ya mtoto kuzaliwa(toka mwanzo wa hedhi yako ya mwisho). Hadi utakapokosa hedhi yako - kama siku 28 baada ya siku ya mwisho ya siku zako za hedhi iliyopita - kibonge cha seli nyingi, yaani kiinitete kitakuwa kinakua katika mfuko wa kizazi kwa karibu wiki nzima. Kiinitete kinakua haraka sana. Wiki sita baada ya hedhi yako ya mwisho, ubongo na uti wa mgongo vinakuwa vimeanza kutengenezwa na moyo unaanza kupiga. Katika wiki 9 kiinitete kinaitwa fitasi. Katika wiki ya 12 fitasi inatambulika kama binadamu ila inakuwa na kichwa kikubwa. Katika wiki 20 (miezi 5) mwanamke anaweza akajisikia fitasi inachezacheza au kuzunguka ndani ya tumbo lake. Fitasi inaweza kugeuka au kusogea na inaweza pia ikashituka kukiwa na kelele zenye sauti ya juu. Ukuaji na maendeleo ya mtoto ndani ya tumbo la uzazi HATARI ZA MIMBA NA UZAZI KWA WASICHANA BALEHE Mimba ni hatari kwa kila mwanamke lakini ni hatari zaidi kwa wasichana balehe. Tatizo kubwa kwa wasichana chini ya miaka 20 ni nyonga. Mifupa inayozunguka mfereji wa kutolea mtoto haujakua vizuri. Wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo wanapata taabu katika kuzaa kwa sababu mlango wa uzazi kwenye mifupa ya nyonga ni midogo mno na mtoto hawezi kupita. Tatizo hili linaitwa uzazi wa kukwama. Kama mtoto hawezi kutoka nje inabidi mtoto atolewe kwa njia ya upasuaji. Vijijini, wanawake wengi wenye matatizo kama haya huwa hawawezi kufika hospitali kwa muda unaotakiwa. Mtoto anaweza kufia tumboni. Isitoshe mfuko wa kizazi unaweza kuchanika kwa sababu ya kipindi kirefu cha uchungu na mwanamke anaweza kufa kwa kuvuja damu nyingi. Hii ni sababu mojawapo inayowafanya wasichana balehe wengi wadogo kufa wakati wa kuzaa

73 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Uchungu wa muda mrefu unaweza kusababisha matatizo mengi. Baada ya saa nyingi za uchungu, kichwa cha mtoto kinaweza kunyoosha au kuchana uke, na kusababisha shimo kati ya uke na kibofu cha mkojo au kati ya uke na mkundu. Shimo hili linaitwa Fistula. Kwa sababu ya shimo hilo, msichana au mwanamke hawezi kuzuia mkojo au kinyesi. Mkojo au kinyesi wakati wote vitakuwa vinavuja kupitia shimo hilo na kushuka chini ya miguu. Matokeo yake msichana au mwanamke atakuwa ananuka vibaya na anaweza kuvimba miguu kutokana na mwasho wa mara kwa mara unaosababishwa na mkojo kwenye ngozi. Katika jamii zingine msichana au mwanamke wa aina hiyo hutengwa na jamii. Jibu pekee ni kumtafuta mganga mtalaamu wa upasuaji kuweza kuziba shimo. Inaweza kuwa vigumu kumpata mtalaamu wa operesheni hii, na siyo mara zote inafanikiwa. Pia kutokana na uchungu wa muda mrefu kwa wasichana wadogo kuna hatari ya kupungukiwa damu (damu dhaifu), kupata shinikizo la damu na kifafa cha mimba. Mambo haya yanaweza kusababisha uchovu, maambukizo ya magonjwa, kuumia na kifo. Wasichana wadogo pia wako hatarini kuzaa kabla ya wakati wake au kuzaa watoto wenye uzito wa chini kuliko inavyotakiwa. Kupunguza hatari ya matatizo haya unahitaji kujitunza vizuri wakati wa ujauzito mimba isije ikaharibu mwili wako na kukusababishia ulemavu wa maisha. KUSTAHIMILI MIMBA KATIKA UMRI MDOGO. Miezi tisa ya mimba ni muda wa uchovu mkubwa kwa mwili wa msichana. Kinaweza pia kuwa kipindi cha msongo na uchovu. Hata kwa wasichana walioolewa ambao wanataka kuanzisha familia, kipindi cha mimba ni kipindi ambacho matunzo maalumu yanahitajika. Kupata mtoto kwa msichana asiyeolewa kunaweza kukawa na matatizo mengi mbalimbali. Mara nyingine familia ya msichana inaweza kutoa msaada na kumsaidia katika hali ngumu aliyonayo. Kwa wasichana wengi,mimba inamaanisha mwisho wa masomo yao Watamsaidia kulea mtoto, watampeleka shule kumalizia masomo yake. Ni jambo zuri sana familia wanapotoa msaada. Lakini kwa bahati mbaya, si jambo la kawaida. Mara nyingi, mimba isiyotakiwa inasababisha msururu wa matukio. Wazazi wa msichana wanaweza ama kumwachisha shule kwa sababu ya kukasirishwa na kukatishwa tamaa, anaweza kupigwa na kufukuzwa nyumbani au anaweza kutishwa mno na vitisho vya wazazi wake akaamua kutoroka yeye mwenyewe. Maisha yake yanakuwa ni ya huzuni, maisha ya baadaye ya mtoto yatakuwa hatarini, kwa vile amezaliwa na msichana mwenye huzuni ambaye hakuwa tayari kulea. Wasichana wengi wanaokabiliwa na mimba zisizotakiwa wanajaribu kuzitoa kinyume cha sheria. Pamoja na kwamba wanajua kutoa mimba ni hatari, wanapendelea kuhatarisha maisha yao kuliko kufukuzwa shuleni au nyumbani. Kila mwaka barani Afrika, maelfu ya wasichana wanakufa au wanaharibu viungo vyao vya uzazi kwa sababu ya kutoa mimba zisizo salama. Katika nchi nyingi za Afrika kutoa mimba ni kinyume cha sheria (soma zaidi mwisho wa sura hii). Wakati mwingine mvulana aliyempa mimba msichana anaweza kupata matatizo pia. Anaweza kupigwa na baba au kaka wa msichana. Anaweza kufukuzwa shuleni au kwenye jamii. Anaweza kulazimishwa kumwoa msichana na kumtunza mtoto na hivyo hataweza kuendelea na masomo yake na malengo yake ya kazi. Pengine atalazimika kulipa faini kubwa kwa wazazi wa msichana. Ukigundua unakabiliwa na mimba isiyotakiwa, usijihukumu mwenyewe, na usijaribu kuikabili hali hiyo kimyakimya. Mtafute mtu yeyote anayeweza kukusaidia kufanya uamuzi mzuri uzungumze naye. Katika hali hiyo usifanye uamuzi wa haraka bila kutafuta maelezo na ushauri unaotakiwaau bila kufikiri kwa makini uchague lipi. Japo itaonekana ni vigumu, ni muhimu kuwataarifu wazazi wako au walezi kuhusu hiyo mimba. Utahitaji msaada wao wakati huu na baadaye, hasa kama utahitaji kuendelea na masomo. Unayo haki ya kupata elimu lakini unaweza kuhitaji msaada wa watu wengine ili urudi shuleni. Je, unajua kuwa mvulana naye anawajibu kuhusu mimba? Usijaribu kukaa kimya unapopata mimba. Unahitaji matunzo mengi na msaada. Wavulana wengi hawafikirii kuhusu uwezekano wao kuwa baba wakati wanapojamiiana. Hata hivyo, watu wawili wanahusika ili kupata mimba na kwa hiyo mvulana anao wajibu sawa na msichana. Kama umekwishaanza kujamiiana unatakiwa kuwajibika na kuwa mwangalifu. Usitegemee kalenda kwamba ni njia inayoweza kukusaidia kujikinga wewe na rafiki yako wa kike. Hakuna siku salama kwa wasichana balehe. Unaweza kumpa mimba kwa urahisi rafiki yako wa kike na mimba ya utotoni inaweza kuwa hatari na ikahatarisha maisha na afya ya rafiki yako wa kike. Inaweza kuwa vibaya pia kwa maisha yake ya baadaye, na maisha yako pia kwa kulazimishwa kuacha masomo ili umtunze mtoto. Kwa hiyo, usifanye mambo ya hatari kijinsi. Kama ukiamua, fanya ngono salama kama kukumbatiana au hakikisha kwamba wewe na rafiki yako wa kike mnatumia njia za kuzuia mimba vizuri kila mnapojamiiana. Ni afadhali kuwa mwangalifu kimwenendo, kimatendo, kifedha na vyovyote inavyowezekana kuliko kujutia baadaye. Kama utakuwa baba bila kutarajia, kubali kuwajibika kwa vitendo vyako. Jifikirie kama baba mwenye wajibu na tenda kama baba. Zungumza na rafiki yako wa kike kuhusu jinsi utakavyosaidia kumtunza mtoto. Muulize jinsi utakavyoweza kusaidia ili aweze kuilea vema mimba yenu (kama vile kumsindikiza kliniki, kumsaidia kazi n.k). Hata kama wewe na msichana hamna uhusiano wa karibu, usimkimbie, zungumza naye jinsi utakavyohusika katika maisha ya mtoto. Unatakiwa pia kuwa mwazi kwa wazazi wako kuhusu jambo hili na waeleze wakusaidie katika mazungumzo ya kushirikiana na wajibu wa kumlea mtoto na matunzo ya mama na mtoto. Zaidi ya yote usirudie kufanya kosa kama hilo tena

74 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba KUJITUNZA WAKATI WA UJAUZITO Kwa sababu mimba inaleta uchovu mkubwa katika mwili wako na ni hatari kwa afya yako ni vizuri upate matunzo yanayofaa. Anza kwenda kliniki ya wazazi mapema unapojijua umepata mimba; usingoje hadi mimba ionekane. Sababu za kuwepo kliniki ya wazazi ni kuhakikisha wewe na mtoto wako mko katika hali nzuri. Kliniki ya wazazi ni muhimu kuweza kutambua matatizo mapema na kuyatibu mapema. Jiwekee utaratibu. Fuata ratiba ya kwenda kliniki ya wazazi. Nenda mara nyingi kadiri wakunga watakavyokwambia. Tumia chandarua ili kujikinga na malaria. Pata mapumziko kwa wingi Pata madini ya ziada ya chuma yanayotolewa hospitalini au kliniki. Mwili wako unahitaji madini ya chuma kwa wingi ili uwe na nguvu na afya wakati wa ujauzito. Hakikisha unakwenda kliniki ya akina mama na unapata chanjo za lazima mapema. MIMBA NA VVU Cissy kutoka Uganda (Umri wa miaka 17) Haikuwa rahisi mara ya kwanza nilipogundua nilikuwa na mimba. Sikuwahi kufikiria ingeliweza kunitokea. Nilizungumza na rafiki yangu wa karibu akanishauri nionane na mshauri ambaye alinisihi nisitoe mimba, kitu nilichotaka kufanya. Niliwapoteza marafiki zangu, lakini niliyakubali makosa yangu, na sasa nina mtoto wa kike. Sitakubali kurudia tena kosa. Fikiria utakula nini na hakikisha unakula vyakula vya kujenga mwili kama maharage na mayai. Kula matunda Hakikisha unakwenda kliniki ya akina kwa wingi na mboga za majani. Utahitaji vilevile madini mama na unapata chanjo za muhimu kama kalsiamu. Kalsiamu inapatikana katika maziwa mapema. lakini ile yenye gharama nafuu inapatikana toka kwenye samaki wadogo wanaoliwa na miiba yake (dagaa). Ni muhimu mno kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI wakati una mimba na baadaye wakati unanyonyesha. Hii ni kwa sababu ukiambukizwa nyakati hizi, kuna uwezekano wa kumwambukiza mtoto VVU. Sisitiza matumizi ya kondomu na mwenzi wako. Wewe na mwenzi wako mnaweza kwenda kupima VVU pamoja. Kama mmoja wenu au wote mna VVU, mnatakiwa kutumia kondomu wakati wote mnapojamiiana. Iwapo wote vipimo vitaonyesha hamna VVU mnatakiwa kuwa waminifu na kuendelea kutumia njia ya uzazi wa mpango ya chaguo lenu ikiwa ni pamoja na kutumia kondomu. Ukigundua una VVU wakati wa ujauzito, mwambie daktari. Siku hizi kuna dawa ambayo unaweza kutumia ukiwa mjamzito ili kupunguza maambukizi kwa mtoto. Kwa kawaida, karibu asilimia 30 ya watoto waliozaliwa na mama walio na virusi vya UKIMWI / VVU wanakuwa wameambukizwa VVU. Lakini kwa kutumia dawa, unaweza kupunguza hatari ya maambukizo hayo. Vilevile unatakiwa kuzungumza na tabibu wako kuhusu kunyonyesha mtoto kwa sababu kuna hatari ya kumwambukiza VVU kupitia kwenye maziwa ya mama. Huduma za dawa za kupunguza makali ya VVU kwa mama wajawazito zinapatikana. Watoa huduma katika vituo vya tiba wanaweza kukueleza jinsi mpango wa huduma hizo ulivyo katika ngazi ya Wilaya. MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA Kama kijana balehe, unatakiwa kufanya maandalizi ya kujifungulia mtoto hospitalini ambako wapo wataalamu wa kutosha na vifaa vya kutosha kuweza kushughulikia matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza.usijaribu kujifungulia nyumbani au kwa wakunga wa jadi. Jitahidi kadiri iwezekanavyo kujifungulia katika kituo cha afya chenye vifaa bora, mahali ambapo wanaweza wakafanya upasuaji kuondoa mtoto kupitia tumboni kama italazimu. Mkunga au mwanamke wa makamo atakushauri vitu unavyovihitaji kwa ajili ya mtoto wako kama: nepi, nguo na blanketi. Hii itategemea sehemu unayoishi na utaratibu wa afya wa nchi hiyo. Unaweza kuhitajiwa upeleke vifaa kama pamba, glavu za plastiki, wembe mpya, sirinji mpya, sindano, sabuni na dawa za kuua wadudu. Unaweza kulazimika kuandaa usafiri wa kwenda hospitali. Jaribu kuwa na mwanamke wa makamo mwaminifu wakati wa kipindi cha uchungu, pengine mama yako mzazi, dada yako mkubwa au shangazi. Hii inaweza kukuliwaza na kukusaidia kwani uchungu unaweza kuchukua muda mrefu. Mkunga anaweza asiwe na wewe muda wote. Je, unafahamu kuwa wanawake waliokeketwa wana mahitaji maalumu wakati wa kujifungua? Tohara ya wanawake ambayo pia inajulikana kama female genital mutilation (FGM) inaweza kusababisha matatizo ya kipekee kwa wanawake wenye mimba. Tohara mbaya sana ni mfyato/ ufyataji, ambayo uke unashonwa na linaachwa tundu dogo tu kwa ajili ya mkojo na damu ya hedhi kupita. Tundu hilo lazima lifunguliwe wakati wa kuzaa mtoto ili kichwa cha mtoto kiweze kupita. Utaratibu huu, lazima ufanywe na mtaalamu wa mambo ya afya ili kuzuia matatizo zaidi. Makovu yatokanayo na tohara yanaweza vilevile kusababisha viungo vya uzazi kuchanika wakati wa kuzaa, kwa sababu ngozi haiwezi kutanuka kirahisi. Damu nyingi inaweza kuvuja. Kama mtoto hawezi kutoka, inawezekana kukawa na matatizo makubwa. Wakati mtoto amezuiwa, kuta za uke, kibofu au mkundu vinaweza kupasuka. Kutokana na hali hiyo mkojo na kinyesi vinaweza kuwa vinavuja wakati wote kupitia ukeni. Wanawake wengi wametengwa na wenzi wao kwa sababu ya harufu mbaya. Nini cha kufanya. Jiandae mapema kwa ajili ya kujifungua. Wakati wa nusu ya kipindi cha pili cha mimba, unatakiwa umwone mkunga kwenye kituo cha afya ambaye amesomea kuzalisha wanawake waliotahiriwa. Mkunga anaweza akakueleza kama kuna hatari ya kupata matatizo, au uke unatakiwa kuongezwa. Panga kuzalia katika mazingira mazuri ya afya. Kujifungulia mtoto nyumbani ni hatari mno

75 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba KUJITUNZA NA KUMTUNZA MTOTO BAADA YA KUJIFUNGUA Kama ulivyokuwa unakwenda kliniki kabla ya kujifungua, hakikisha unakwenda tena kwa uchunguzi baada ya kujifungua. Kama ulimzalia mtoto wako nyumbani hakikisha unakwenda kliniki kwa ajili ya uchunguzi ndani ya siku tatu. Kama ulimzalia mtoto wako hospitalini nenda baada ya wiki sita ili mkunga aone kama tumbo lako linarudia hali yake ya awali. Mkunga anatakiwa pia kuangalia kama huna maambukizo ya magonjwa au hutokwi na damu sana.kama ulipoteza damu nyingi wakati wa kuzaa mkunga atakupa dawa za madini ya chuma ili kusaidia kuongeza damu. Mkunga anaweza vilevile kujibu maswali mengi utakayokuwa nayo kuhusu kunyonyesha mtoto, kulala, kinga kwa mtoto, kuzuia mimba na mambo mengine. Mwanamke aliyezaa kwa mara ya kwanza mara nyingi anakuwa na maswali mengi hivyo kuongea na mkunga inaweza kukusaidia. KUHARIBIKA MIMBA Mara nyingine mimba huwa inaharibika/inatoka yenyewe tu. Tunasema mimba imetoka kwa bahati mbaya. Fitasi inakufa na inatoka kupitia ukeni. Malaria au magonjwa ya ngono huweza kusababisha kuharibika mimba. Mimba inaweza kutoka vilevile kama fitasi ina matatizo. Kama mimba itakuwa imetoka mwanamke anahitaji kumwona mhudumu wa afya ili kuhakikisha hapati maambukizo kwenye tumbo la uzazi. Mhudumu wa afya anaweza pia akatambua kilichosabisha mimba kutoka na kutoa matibabu ya magonjwa kama ya ngono. Mimba inaweza vilevile kutolewa kwa makusudi kwa kupitia taratibu za kitabibu. Mimba inaweza kutolewa na mganga aliyesomea katika mazingira ya hali ya usafi. Kutoa mimba ni utaratibu salama kitabibu kwa ujumla na ni salama kuliko kuzaa. Katika nchi nyingi za Kiafrika ni kosa la jinai kutoa mimba isipokuwa katika mazingira ya matatizo kama kubakwa au kujamiiana kwa maharimu (ndugu wa karibu) au wakati ambapo maisha ya mwanamke yako hatarini kwa ajili ya mimba au fitasi si ya kawaida na hata akizaliwa mtoto hataishi. Uthibitisho wa kitabibu unatakiwa kuwepo kuwa mhusika alibakwa kulikuwepo kujamiiana kwa maharimu au fitasi si ya kawaida. Kutoa mimba kinyume cha sheria katika nchi nyingi barani Afrika ni hatari sana. Kutoa mimba kunafanywa katika mazingira machafu na ya hatari na mara nyingi watu wengi wanaotoa mimba hawajasomea. Kwa sababu kutoa mimba hakuruhusiwi, mtoaji mimba anaweza kutoa bila utaratibu, kwa haraka na kuogopa na katika mazingira na vifaa vichafu. Mambo yote haya yanamuweka mwanamke katika hatari kubwa. Kwa hakika, katika nchi nyingi za Afrika, robo ya vifo vya wanawake wajawazito vinasababishwa na matatizo ya ama mimba kutoka au kutoa mimba. Kutoa mimba kwa kutumia njia isiyo salama kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya. Kifaa cha kutolea mimba kikiingizwa kwenye mlango wa mfuko wa kizazi kinaweza kikasababisha uharibifu kwenye kibofu cha mkojo au utumbo mdogo au mlango wa mfuko wa kizazi. Mfuko wa kizazi ulioharibika utatakiwa uondolewe. Maana yake, msichana hataweza kupata mtoto tena. Kutoa mimba kusiko salama vilevile kunaweza kusababisha kuvuja damu, maambukizo ya magonjwa na kifo. Kuingiza kifaa cha kutolea mimba kwenye mlango wa mfuko wa kizazi na kizazi kunaweza kusababisha kuvuja sana damu na msichana anaweza akavuja damu mpaka akafa. Miti shamba na vifaa vingine vinavyotumika kuanzisha uchungu mara nyingi siyo safi; vinaweza kuleta vijidudu vya maradhi katika mfuko wa kizazi. Kizazi na mirija ya kupitisha mayai ya mgonjwa vinaweza kuathirika sana kiasi cha kusababishiwa ugumba au kifo. Miti shamba, dawa au kemikali ambazo msichana anameza zinaweza kumfanya awe mgonjwa sana na anaweza akawa amejipa sumu mwenyewe. Je unajua matokeo ya utoaji mimba usio salama? Jane alipopata mimba alikuwa na miaka 15 na alikuwa Kidato cha Tatu. Alitaka sana kuendelea na shule, aliishi na shangazi yake, ambaye alimpeleka kwa mtu aliyedai ni mganga anayefanya kazi kwenye hospitali kubwa mjini Kampala. Mtu huyu aliingiza kifaa kwenye uke. Maji yakatoka. Alisikia maumivu makali sana, lakini aliambiwa asilie kwa sababu hata hivyo alitaka mwenyewe kilichomtokea. Shughuli ilichukua dakika 15. Alirudi nyumbani na alitokwa na damu wiki nzima, akidhoofu kidogokidogo kila siku. Tumbo lake liliuma na uke ukawa unatoa majimaji yenye harufu mbaya. Baadaye alipelekwa kliniki inayohudumia vijana. Kliniki waligundua amechanika sehemu kubwa ya mfuko wa kizazi. Ilibidi afanyiwe upasuaji na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki nne kutibu kidonda na maambukizo ya magonjwa. Jane bado hajui iwapo ataweza kupata watoto baadaye. Diana kutoka Uganda (Umri wa miaka 15) Kutoa mimba ni hatari sana hasa kwa kutumia miti shamba. Ni afadhali usishiriki katika ngono kabisa. Nedina kutoka Uganda (Umri wa miaka 18) Rafiki yangu wa kike akipata mimba nitamkatisha tamaa asitoe mimba kwa sababu ni hatari. Nitamsihi azae na kisha aendelee na masomo yake hapo baadaye Kutoa mimba kunaweza kuleta matokeo ya kusikitisha kijamii. Watu wengine wakijua kwamba msichana ametoa mimba, anaweza kufukuzwa shule, kutoaminika au kufedheheshwa na marafiki au na familia. Hata hivyo, wasichana wengi wanaishia kutoa mimba kwa njia isiyo salama wanapojikuta wamepata mimba. Wanasahau hatari za kutoa mimba kwa sababu ya hofu, familia zao zitakapogundua ujauzito wao. Wanakata tamaa ya kuendelea na masomo. Marafiki zao wa kiume wanaweza kuwa wamewaacha au kuwalazimisha watoe mimba

76 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba JE, VIDONGE VYA KUZUIA MIMBA NI SALAMA? Christine kutoka Uganda (Umri wa miaka 18) Nimesikia kwamba vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha saratani au pia ulemavu kwa mtoto. Utoaji mimba usio salama ni hatari sana. Unaweza kupoteza maisha yako. Kama wewe au yeyote unayefahamu anakabiliwa na mimba isiyotakiwa, tafuta msaada. Kuwa mwaminifu kwa wazazi /walezi kuhusu hali hiyo. Kama wazazi wako hawakusaidii tembelea kituo cha vijana na mwombe mshauri wa vijana ushauri kuhusu suala lako. Mwombe mshauri wa vijana akuelekeze wapi unaweza kwenda kuzungumza na mhudumu wa afya anayejali na mpole. Kama wewe au yeyote unayemjua alitoa mimba na hajisikii vizuri, nenda hospitali haraka. Kuvuja damu, homa ya baridi, homa na/au kutoka majimaji yenye harufu ni dalili kwamba kuna mahali pana matatizo makubwa. Afya yako na maisha yako yapo hatarini hivyo uchunguzi wa waganga ni muhimu sana. Hata kama sheria ni kali kiasi gani, wahudumu wa afya wana miiko ya kitalaamu ya kumsaidia yeyote atakayekuwa na matatizo. Usiache woga ukuzuie kupata matibabu na hatimaye ukapoteza uhai. Njia nzuri ya kujikinga mwenyewe dhidi ya matokeo ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama ni kukwepa kupata mimba isiyopangwa ama kuepuka ngono nzembe. NAMNA YA KUEPUKA KUPATA MIMBA Njia ya uhakika kabisa ya kutopata mimba ni kuacha kufanya ngono. Uzuiaji huu una uhakika wa asilimia 100, na ni salama kihisia na kimwili. Kama hujamiiani, hakuna jinsi unavyoweza kupata mimba au kumpa mimba msichana. Ikiwa unajamiiana, hakikisha pia kuwa wewe na mwenzi wako mnatumia kondomu kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya ngono. Unatakiwa pia kuomba msaada kutoka kliniki ya uzazi wa mpango. Unahitaji kuchukuwa hatua ili mwenzi wako asipate mtoto ambaye huwezi kumtunza kwa wakati huu. Kuna aina nyingi za dawa za kuzuia mimba ambazo ni salama kabisa kwa vijana (angalia kisanduku ukurasa wa 140). Njia yoyote utakayotumia, hakikisha unaitumia inavyotakiwa. Kwa mfano, kusahau kumeza kidonge kunaweza kusababisha upate mimba. Uvumi kama huu ni uwongo na si wa kisayansi. Tangu miaka ya 1950, mamilioni kwa mamilioni ya wanawake wametumia dawa za vidonge za kuzuia mimba. Vidonge vya kuzuia mimba vimefanyiwa uchunguzi mkubwa katika historia ya dawa. Kwa kuyafuatilia maisha ya maelfu ya wanawake kwa miaka mingi waganga sasa wanajua kwamba vidonge vya kuzuia mimba havileti saratani. Uwezekano wa wanawake wanaomeza vidonge kupata saratani ya kokwa la mayai na uwezekano wa kupata saratani kwenye ngozi laini ya kuta za tumbo la uzazi ni mdogo kuliko wanawake ambao hawajawahi kutumia vidonge hivyo. Kuna uvumi mwingine kwamba kutumia vidonge vya kuzuia mimba wakati wa ujana balehe kunaweza kuharibu kokwa la mayai na kusababisha isiwezekane kupata mimba baadaye. Huu pia ni uzushi.mwongozo wa kimataifa wa kutumia dawa za kuzuia mimba unasema vidonge ni vizuri kwa wanawake ambao bado hawajapata watoto. Ukweli ni kwamba,mara nyingine vinatumika kuwasaidia vijana balehe kuwapunguzia maumivu makali wakati wa hedhi. Huhitaji kuwa na mtoto kwanza ndipo uanze kumeza vidonge. Vidonge havitaharibu kokwa la mayai. Wasichana na wanawake wengine wanapata kichefuchefu, matiti kuwa laini na kuongezeka uzito wanapoanza kumeza vidonge. Matokeo haya huwa yanatoweka baada ya mwezi mmoja au zaidi. Karibu wanawake wadogo na wanawake wa makamo wote wanaweza kumeza vidonge. Ni wanawake wa makamo tu ambao wanaovuta sigara, walio wanene sana au wanashinikizo la damu au magonjwa fulani kwenye mfumo wao wa damu wanashauriwa wasitumie njia ya homoni kuzuia mimba (vidonge vya kuzuia mimba, sindano na vipandikizi). Unatakiwa kumwona mtoa huduma ili akupime kama huna vidokezo vya mteja wa dawa za kuzuia mimba. KUZUIA MIMBA KWA DHARURA Kuna njia moja zaidi ya kuzuia mimba ambayo hapana budi kuijua. Hii ni njia ya dharura ya kuzuia mimba. Njia ambayo unaweza kuitumia kuzuia mimba haraka baada ya kufanya ngono isiyo salama. Kwa mfano kama ulisahau kutumia kondomu au kama kondomu ilipasuka au ilitoka kwa bahati mbaya (jambo ambalo ni nadra sana kama ikitumika vizuri). Kinga ya dharura ya kuzuia mimba imeanza kupatikana sehemu nyingi siku hizi. Kama ukifanya ngono bila kinga na una wasiwasi wa kupata mimba unaweza kwenda kwa muhudumu wa afya na kumwomba kinga ya dharura ya kuzuia mimba. Ikiwa umebakwa omba kinga ya dharura ya kuzuia mimba kutoka kwenye kliniki ya mpango wa uzazi au kituo cha vijana karibu na wewe katika kipindi cha saa 72 (siku 3)

77 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Je, unajua njia zipi za kuzuia mimba ambazo ni salama kwa vijana? Njia zote hizi za kuzuia mimba ni salama kwa vijana: Kondomu: Kondomu ni mpira laini ambao huwekwa kwenye uume uliosimama kabla ya kujamiiana. Mwanaume anapotoa shahawa ( anafikia mshindo ) zinanaswa nchani mwa kondomu. Majimaji toka kwa mwanaume hayamwingii mwanamke na majimaji toka kwa mwanamke hayagusi uume wa mwanaume. Kondomu zinatoa kinga nzuri dhidi ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/ UKIMWI na huzuia mimba. Bei ya kondomu ni ndogo na zinawasaidia wanaume wengine kuchelewa kutoa shahawa mapema. Vidonge: Vidonge vina kiasi kidogo sana cha homoni. Homoni hii huzuia uovishaji kutoka kwenye makokwa ya mayai. Mwanamke aliyeingia kwenye hedhi anapomeza kidonge lakini kidonge kinafanya hedhi ya mwanamke kuwa nyepesi na maumivu kuwa mepesi. Pia matokeo ya kuzuia mimba kwa kutumia vidonge ni mazuri sana, lakini lazima umeze kila siku. Ukikosa kumeza zaidi ya siku moja unaweza kupata mimba kwa sababu rutuba inarudi pindi unapoacha kumeza vidonge. Vidonge havizuii VVU au mangojwa mengine ya zinaa. Kwa hiyo, ni vizuri iwapo unatumia kondomu, uwe na mwenzi mmoja tu na wote muwe mmepima na kuthibitisha hamna magonjwa ya ngono/vvu. Sindano: Sindano ina homoni ambazo zinazuia yai kurutubishwa. Huanza kufanya kazi katika muda wa saa 24 na hutoa kinga dhidi ya mimba kwa muda wa miezi mitatu. Kudunga sindano ni rahisi kwa sababu huhitaji kukumbuka kumeza kidonge kila siku au kufanya chochote kabla ya kujamiiana. Sindano pia inatunza siri, hakuna anayeweza kujua kwamba unatumia mtindo huu kwa kuzuia mimba. Sindano zinafanya siku zako za hedhi ziwe nyepesi na zenye maumivu kidogo ambapo zinaweza kuwasaidia vijana wanaopata maumivu au hedhi nzito. Unapoacha kudunga sindano, huwi na rutuba tena mara moja, kwa sababu homoni zinakaa mwilini kwa muda. Wanawake wengi wanakuwa na rutuba tena ndani ya mwaka mmoja wanapoacha kutumia sindano, lakini wengine wanapata mimba mapema. Sindano hazizuii magonjwa ya zinaa/vvu hivyo zinafaa tu kama unatumia kondomu au kama unaye mwenzi mmoja na wote mmepima magonjwa ya ngono/vvu. Vipandikizi: Vipandikizi ni vimrija vidogo vinavyowekwa ndani ya ngozi kwenye mkono chini kidogo ya bega. Vimirija hivyo huwa vinatoa homoni inayozuia yai kurutubishwa. Kama ilivyo kwa sindano huhitaji kukumbuka kumeza vidonge au kufanya lolote kabla ya kujamiiana. Vipandikizi vinadumu miaka mitano. Lakini vinaweza kuondolewa mapema. Ni kinga nzuri sana kuzuia mimba, lakini haizuii magonjwa ya zinaa/vvu. Kwa hiyo unatakiwa kutumia kondomu au kuhakikisha kuwa wewe na mwenzi wako hamna magonjwa ya ngono/vvu. Dawa ya kuulia mbegu za kiume (vidonge mafuta au krimu na povu): Dawa hizi zinaua mbegu za mwanaume kabla hazijaingia ndani ya mfuko wa kizazi, lakini hazimuumizi mwanaume au mwanamke. Zipo aina mbalimbali za dawa na zinaingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Dawa hizi zitumike na kondomu kwa sababu zina kinga ndogo sana dhidi ya magonjwa ya zinaa/vvu. Zaidi ya hapo, hazina kinga madhubuti kama ya vidonge au sindano katika kuzuia mimba. Tofauti na vidonge na sindano, huhitaji kuzipata kutoka kwa mhudumu wa afya; unaweza kupata moja kwa moja toka kwenye maduka ya dawa. Hii inaweza kuwa bahati kama una aibu kwenda kliniki, lakini kumbuka kutumia kondomu. Unapotumia vidonge vya dharura inakubidi umeze kiasi cha mchanganyiko wa vidonge vya kuzuia mimba baada ya saa 12 katika kipindi cha saa 72 za kufanya ngono bila kinga. Kinga ya dharura ya kuzuia mimba haifanyi kazi mimba inapokuwa imetungwa. Ndio maana ni muhimu kuipata haraka baada ya ngono isiyo na kinga. Usijaribu kunywa dawa hizi bila ushauri wa mhudumu wa afya mwenye ujuzi. KINGA MARA MBILI Je, unafahamu kuwa wanawake waliokeketwa wana mahitaji Kuchomoa/kurusha: Kuchomoa au kurusha ni wakati mwanaume anatoa uume nje ya uke kabla ya kukojoa shahawa. Njia hii sio salama kwa sababu wanaume wengi hawawezi kuutoa uume kwa wakati unaotakiwa. Mara nyingi wanaume hawajui kwamba wanakaribia kukojoa mpaka wanapokuwa wamekaribia sana. Pia, matone machache ya shahawa yanaweza kutoka kabla ya kukojoa na matone machache haya yanatosha kusababisha mimba. Kuchomoa hakuleti kinga dhidi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa. Siku salama : Wanawake wengine wanasubiri siku ambazo wanajua kwamba hawana rutuba. Utaratibu huu unafaa kwa wanawake ambao hedhi zao ni za kawaida na wenzi wao wana ushirikiano. Wasichana wa umri mdogo wengi hawana hedhi za kawaida hivyo si rahisi kujua siku salama. Kama ilivyo kwa njia ya kuchomoa, siku salama hazileti kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/vvu. Kitanzi: Kitanzi kinatumbukizwa kwenye tumbo la uzazi na mhudumu wa afya. Ni rahisi kukiingiza kwa mwanamke ambaye amewahi kuzaa, kwa hiyo haipendekezwi kwa vijana. Kitanzi kinaweza kusababisha ugonjwa wa ngono ukue na kufikia hali ya kutisha. Kwa vile vijana ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa ya zinaa, wasitumie kitanzi. Kitanzi hakitoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/vvu. Kufunga kizazi: Kukata au kufunga mirija ya kupitishia mbegu ya wanaume na wanawake ni njia ya kudumu ya kuzuia mimba. Unafanyika upasuaji ambapo mirija ya kupitishia shahawa na yai inazibwa. Njia hii inawahusu wanaume na wanawake ambao wanafikiri wamepata idadi ya watoto inayowatosha. Njia hii haifai kwa vijana kwa sababu huwezi kupata watoto baada ya upasuaji. Kufunga kizazi hakutoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/vvu. Ugonjwa wa UKIMWI umebadilisha mawazo ya watu wengi kuhusu njia za kuzuia mimba. Zamani watu walilenga katika kuangalia ni njia zipi zinaleta matokeo bora katika kuzuia mimba. Hawakujali sana kama njia ya kuzuia mimba ilitoa kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/vvu. Leo mambo ni tofauti. Kupata VVU ni maafa makubwa kuliko kupata mimba isiyotakiwa. Siku hizi watu wanazungumzia kuhusu kinga mara mbili. Kinga mara mbili ni wakati unatumia njia ambayo matokeo yake hupunguza hatari ya mambukizo ya magonjwa ya zinaa/vvu/ukimwi, na wakati huohuo, unatumia njia nyingine ambayo matokeo yake ni mazuri katika kukinga mimba zisizotakiwa. Angalia njia mbalimbali hapa chini uone jinsi zinavyotoa kinga dhidi ya mimba na magonjwa mengine ya ngono pamoja na VVU

78 SURA YA 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Sura ya 11 Mimba na uzuiaji wa mimba Wakati wote mwanaume na mwanamke wakijamiiana bila kinga, mimba inaweza kutokea. Mimba inaweza ikatokea mara ya kwanza tu mnapojamiiana bila kinga. Mimba inaweza kutungwa kama mbegu moja inakutana na yai na kulirutubisha ndani ya mwanamke. Kama yai litarutubishwa, linajishikiza kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Huu ndio mwanzo wa mimba. Hata hivyo, njia pekee nzuri ya kujikinga ni kuacha kujamiiana au kuacha zinaa. Lakini kama unavyoweza kuona hapo juu, yeyote ambaye anajamiiana, njia nzuri ya kuzuia mimba ni kutumia vipandikizi, sindano na kondomu. Stabisile kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 19) Kama mwanamume anakataa kutumia kondomu, huyo anapoteza muda. Cathy kutoka Uganda (Umri wa miaka 17) Ninapendekeza matumizi ya kondomu ili kukwepa maambukizo ya VVU/UKIMWI, magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba zisizotakiwa. Kondomu ni nzuri kwa kuzuia mimba, na zinakusaidia kukukinga wewe na mwenzi wako dhidi ya magonjwa ya zinaa/ukimwi. Unaweza kufanya ziwe kinga nzuri zaidi kwa kuchanganya vidonge na njia nyingine ya kuzuia mimba. Dalili za mimba ni pamoja na: Kukosa siku zako za hedhi Kujaa na kuuma kwa matiti Kichefuchefu Kuwa mchovu Kutaka kukojoa mara kwa mara. Mimba ni hatari hasa kwa wasichana balehe kwa sababu miili yao bado haijakomaa. Wasichana wadogo wanakabiliwa na matatizo makubwa ya afya wakati wa mimba na wakati wa kuzaa kuliko wanawake wa makamo. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu hasa kwa msichana mdogo kupata matunzo sahihi wakati wa mimba. Inashauriwa kuzalia hospitalini mahali ambapo kuna wahudumu wa afya wa kutosha na vifaa vinavyoweza kumudu matatizo yoyote ya uzazi. Wasichana balehe wengi wanapata mimba kwa makosa. Wanaamua kutoa mimba kwasababu wanataka kuendelea na shule au kwa sababu hawataki kuwaaibisha wazazi wao. Hata hivyo, katika nchi nyingi za Afrika kutoa mimba ni kinyume cha sheria na si salama hata kidogo. Kutoa mimba kusiko salama kunaweza kusababisha matatizo makubwa kiafya, kuanzia maambukizo ya magonjwa, uharibu wa via vya uzazi, kuvuja damu sana, ugumba na vifo. Njia sahihi ya kukwepa mimba ni kuacha ngono. Kuacha kabisa ni salama kwa asilimia 100. Iwapo unashiriki kujamiiana, wewe na mwenzi wako mnatakiwa wakati wote kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya ngono pamoja na VVU/UKIMWI. Njia zote za kuzuia mimba ni salama kwa vijana. Kama umesahau kutumia kinga ya mimba au kama kondomu itatoka au kupasuka, nenda haraka kwenye kliniki waombe kinga ya dharura ya kuzuia mimba. Inaweza kuzuia mimba ikiwa itatumika katika kipindi cha saa 72 cha kujamiiana bila kinga. Iwapo yeyote anasema hataki kutumia kondomu jiandae kwa jibu zuri! Na jiandae kuondoka kama atakataa kutumia kondomu. Mimba inahusu watu wawili yaani mwanamume na mwanamke. Wavulana na wanaume pia watu wazima, wote wanalo jukumu la kuzuia mimba

79 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako SURA YA 12 Wakati mwingine watu yaani wanaume kwa wanawake na wavulana kwa wasichana wanajamiiana huku kiukweli hawapendi kufanya hivyo. Wanaweza kushinikizwa na rafiki wa kiume au kike kujamiiana kama ushahidi wa mapenzi yao. Wanaweza kushinikizwa kufanya ngono ili kulipa zawadi au pesa walizopokea. Au wanaweza kulazimishwa kujamiiana na mtu ambaye ni mkubwa au ana nguvu zaidi. Ngono isiyotakiwa ni hatari. Itakuweka katika hatari ya kupata mimba na magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Vilevile, inakuweka katika hatari ya kupata magonjwa ya hisia. Unaweza kupata maumivu makali sana ya kihoro iwapo utajamiiana bila ridhaa yako. Njia nzuri ya kukwepa ngono za namna hii ni kuyakimbia mazingira mabaya yanayoweza kusababisha ukaingia katika mtego. SHINIKIZO KUTOKA KWA RAFIKI WA KIUME AU WA KIKE Wakati mwingine wavulana wanawaambia wasichana wajamiiane kama ushahidi wa mapenzi yao. Vilevile, wasichana wanawaambia wavulana vivyohivyo. Watu wengine wanafikia hatua ya kutishia kuvunja uhusiano pindi mwenzi atakapokataa kujamiiana. Inaweza kuwa vigumu iwapo mtu unayempenda na kumjali akikwambia mjamiiane. Unaweza kudhani njia pekee ya kuendeleza urafiki ni kumkubalia mfanye ngono. Unaweza kudhani ni vema kumkubalia kwa sababu unamjali na unataka afurahi. Ngono kamwe isitumike kama ushahidi wa mapenzi

80 SURA YA 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako Katika mazingira kama haya, inaweza kuwa vigumu sana kujua tofauti ya kile anachokitaka na kile wewe unachokitaka. Ni rahisi kuchanganyikiwa lipi ni sahihi kwako. Iwapo rafiki yako wa kiume au wa kike anashinikiza mjamiiane, fikiria maswali yafuatayo: Unathamini nini? Je, unaamini kwamba ni sahihi kujamiiana wakati huu katika maisha yako? Au je, huoni ni vyema usubiri mpaka baadaye, kama vile utakapoolewa au kuoa? Unajisikia vizuri kuhusu wazo la kujamiiana au wazo hilo linakufanya ukose raha? Unajisikia kama unaweza kukataa kujamiiana au hili linaenda kinyume na kile unachofikiri ni sahihi kwa msichana au mvulana kufanya? Kwa mfano, katika maeneo mengine, ni vigumu sana msichana kusema HAPANA kwa mvulana au mwanaume kwa sababu amefundishwa kwamba wakati wote anatakiwa kuwa mnyenyekevu kwa mwanaume. Katika maeneo mengine inaweza kuwa vigumu sana kwa mvulana kusema HAPANA kwa sababu amelelewa kuamini kwamba mwanaume wakati wote anatakiwa kujamiiana. Hivyo mtu anaweza kuhisi kwamba kwa kusema hapana inaweza kuleta matatizo. Unafikiri mwenzi wako ataendelea kukupenda na kukuheshimu kama ukikataa? Majibu ya maswali haya yatakueleza mengi kuhusu kama ujamiaane au usijamiiane na rafiki yako. Uwe msichana au mvulana, wote mnayo haki ya kukataa kujamiiana. Ni wewe unayetakiwa kufanya uamuzi mwenyewe kuhusu kujamiiana. Kama huamini kwamba ngono inakufaa wakati huu wa maisha yako, usifanye; bila hata kujali rafiki yako wa kiume au kike anasema nini. Kama hujisikii kufurahia wazo la ngono na hauko tayari kufanya, usifanye. Iwapo unafikiria rafiki yako wa kike au wa kiume hatakupenda ukikataa kujamiiana, ukweli ni kwamba hakupendi kama atakuchukia. Hakuna mtu ambaye anakupenda kweli atakulazimisha kufanya jambo ambalo unahisi ni baya kwako. Iwapo huna uhakika kama rafiki yako wa kike au wa kiume atakuwa na wewe ukikataa kujamiiana, labda jambo la maana la kufanya ni kusubiri na kuona. Mwambie rafiki yako kwamba unampenda lakini umeamua kwamba hauko tayari kujamiiana. Kama akisema ni sawa, basi unaweza ukatuliza moyo na kutulia. Unaweza kufurahia uhusiano wenu mzuri bila kukimbilia kufanya ngono. Hata hivyo, iwapo rafiki yako wa kike au kiume ataamua kukuacha, hii inaweza kuwa ngumu kwa sababu inakuonyesha kwamba rafiki yako alikuwa hakupendi. Unaweza kujisikia una huzuni na mpweke. Unaweza kufikiri ulifanya uamuzi usio sahihi, lakini hukufanya! Ulifanya kilichokuwa sahihi kwako. Katika kufanya uamuzi ukakuta rafiki yako wa kiume au wa kike alitaka kukutumia na wala hakuwa anakujali, bila shaka uvumbuzi huu utakuhuzunisha, lakini ni afadhali kuvumbua mapema kwani ingekuwa vibaya zaidi kama ungegundua baada ya kujamiiana. SHINIKIZO KUTOKA KWA WATU WAZIMA Wakati mwingine watu wazima ikiwa ni pamoja na waliooa au kuolewa, wanawalazimisha vijana kufanya ngono. Mara nyingi wanaume, watu wazima (wazee) wanapenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wadogo. Wakati mwingine vilevile wapo wanawake watu wazima wanaopenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wavulana wa umri mdogo. Mara kwa mara mtu mzima hutoa zawadi, pesa au huduma maalumu kwa kijana. Mtu mzima anaweza kutoa pesa kwa ajili ya karo, nguo au peremende. Iwapo mtu mzima ni kama mwalimu au dereva wa basi, anaweza kuahidi kumpa alama nzuri au kumpakia kwenye gari bure. Lakini zawadi zote hizi siyo bure. Baada ya muda mtu mzima atadai malipo kwa zawadi alizotoa. Kawaida kijana atalipa kwa njia ya ngono. Effie Kutoka Kenya ( Umri wa miaka 16) Nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa na umri wa miaka 15. Rafiki yangu alikuwa na uhusiano na mtu mzima ambaye alikuwa anampa kila alichotaka, na mama yake alifahamu kuhusu uhusiano huo na wala hakujali. Siku moja akiwa anaelekea shuleni aliona gari la mzee huyo. Aliamua kumpa lifti mpaka shuleni, lakini wakiwa njiani kuelekea shuleni yule mwanaume alipita njia nyingine na akampeleka msichana kwenye nyumba ya kulala wageni na akajamiiana naye kwa nguvu. Ingawa inaweza kufurahisha kuona mtu mzima anavutiwa na wewe na inaweza kukufanya ujisikie unapendeza na ni wa maana, uhusiano wa namna hii ni mbaya sana. Unaweza kuwa hatari kwako kwa vile: Unaweza kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa, VVU/UKIMWI na mimba. Unaweza kukatisha masomo yako. Unaweza kuwa chanzo cha hasira kwa mke wake au mume wake ambaye anaweza kukushambulia au kukudhuru. Umri unapopishana sana na kipato kinapotofautiana, vilevile uhusiano hauwi sawa. Unaweza kujisikia huna mamlaka. Unaweza kuogopa kusema hapana unapoombwa ngono kwa sababu unajua ulichukua pesa au zawadi. Unaweza vilevile kuogopa kumwambia mtu mzima kutumia kondomu. Huu ni uhusiano wa hatari sana unaweza kuharibu maisha yako ya baadaye au milele! Watu wazima wanaweza kukupatia pesa au zawadi kwa ajili ya ngono. Uhusiano huu ni hatari kwako KWA NINI UNANIPA MIMI HIZI PESA? SITAZICHUKUA! ASANTE. Kataa kupokea zawadi na pesa. Usijiingize katika deni na mtu

81 SURA YA 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako Unaweza kushawishika kuingia katika uhusiano na mtu mzima, hususani kama huna pesa za matumizi na wazazi wako hawawezi kukununulia vitu vya kukufurahisha na vilivyo vizuri. Hata hivyo, hakuna zawadi au kiasi cha pesa chenye thamani ya gharama utakayolipa. Margaret kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 17) Kitu kimoja ninachojua kuhusu wanaume ni kwamba wengi huwania kujifurahisha na mtu wa jinsi nyingine, na katika kufanya hivyo wanaweza kukuahidi hazina zote za maisha. Kwa hiyo, nimesema HAPANA kwa wanaume wengi na nitaendelea kufanya hivyo. Neema kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Alikuwepo mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anajaribu kufanya urafiki na mimi lakini nilikataa. Mwanaume huyo alikuwa anawatuma wasichana wengine kujaribu kunishawishi, lakini nilikataa. Unyanyasaji kijinsia mara nyingi unafanywa na mtu mzima anayemjua kijana na ana madaraka juu yake. Mtu mzima anaweza kuwa jirani, rafiki wa familia, mwalimu, kiongozi wa dini au kiongozi wa jamii. Mtu mzima anaweza akawa ndugu, kama vile mzazi, mzazi wa kambo, mjomba au shangazi, kaka au dada. Unyanyasaji kijinsia unaweza kuhusisha tishio, rushwa, udanganyifu, ujanja na vurugu. Mtu mzima anaweza kukutishia, au mtu mzima anaweza kukupatia zawadi ili kukufanya utoe ushirikiano. Mtu mzima anaweza pia kukudanganya au kukutegea ufanye jambo. Mtu mzima anaweza kukutishia kukudhuru wewe au familia yako iwapo utamwambia mtu yeyote kuhusu unyanyasaji kijinsia. Mtu mzima anaweza kukuchanganya akili kwa kusema uhusiano utakuwa wa siri. Kugusana kwa aina yoyote kusikokubalika ni unyanyasaji kijinsia. Iwapo mtu mzima, mwanaume au mwanamke anajaribu kukupatia zawadi au pesa na anashinikiza mjamiiane, kuwa jasiri. Sema hapana na ondoka bila kuchelewa. Waeleze wazazi au shangazi au mjomba au mwelimisha rika kilichotokea. Waombe wakusaidie uweze kuimudu hali hiyo. Usijaribu kutatua peke yako. Vijana wengine wanaingizwa katika uhusiano wa namna hii na wazazi wao. Hii ni kwa sababu wazazi ni maskini na hawawezi kulipa karo, chakula, nguo na vitu vingine. Hali kama hii ni ngumu kwa kijana yeyote. Iwapo utakuwa katika mazingira kama haya unahitaji kufikiri kiubunifu: Ni nani unaweza kumwendea kwa ajili ya msaada? Unaweza kuzungumza na ndugu wengine kama vile shangazi, mjomba, babu, bibi au kaka au dada? Huenda wakakulipia karo au wakawasaidia wazazi wako kufanikisha yote. Unaweza kuzungumza na mtu yeyote ndani ya jamii, kama vile mtu wa kanisani, msikitini au kutoka kituo cha vijana? Hawa wanaweza kufahamu namna ya kutatua tatizo lako. Je, unaweza kuzungumza na mwalimu au mkuu wa shule? Waulize namna unavyoweza kulishughulikia tatizo lako. Pengine wanaweza kukusaidia kwa kukusamehe karo au kwa kukupatia kazi ya kufanya shuleni ili uweze kulipa karo. Unyanyasaji kijinsia ni jambo baya sana na linaweza kukufanya uchanganyikiwe. Hapa kuna mambo machache ya kuyaweka maanani:- Mwili wako ni wako. Unayo haki ya kuamua nani akushike, akushike vipi na wakati gani. Mtu yeyote asiangalie au kukushika sehemu zako za siri kwa namna ambavyo utajisikia vibaya. Amini hisia zako kuhusu kuguswa na amua nini kilicho chema kwako. Usimsikilize mtu anayejaribu kukushawishi vinginevyo. Mtu akikugusa ambavyo hupendelei, sema hapana kwa nguvu na kwa sauti. Kuwa jasiri. Tafuta mtu wa kumweleza kuhusu tukio. Ongea na mzazi, shangazi au mjomba, babu, bibi, rafiki, mwalimu au mama wa rafiki yako. Pata msaada. Je, unaweza kupata pesa? Unaweza kufanya kazi, kama kuuza mboga, karanga, bisi au peremende baada ya shule ili kupata pesa? Wapo watu wengine wanaokuzunguka ambao wanaweza kukusaidia ikiwa watajua tatizo lako. Kwa hiyo omba msaada na usijaribu kulitatua peke yako. UNYANYASAJI KIJINSIA Aina yoyote ya kuguswa au kushikwashikwa kimapenzi bila ridhaa ya anayetendewa hivyo ni unyanyasaji kijinsia. Inaweza ikawa kushikwa matiti au sehemu za siri. Inaweza vilevile ikawa kujamiiana. Aina yoyote ya kukutana kimapenzi bila ya kupenda ni unyanyasaji pia. Iwapo yupo mtu anakunyanyasa kijinsia au anakushinikiza ufanye naye ngono, tafuta msaada. Ongea na wazazi au mtu mwingine anayejali

82 SURA YA 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako KUDHALILISHA KIJINSIA Unyanyasaji kijinsia hauishii katika kushikashika au kugusa mwili. Wakati mwingine matusi ya nguoni na utazamwaji wa kifuska vinaweza kumfanya mtu ajisikie vibaya. Aina yoyote ya kitu kisichovutia kijinsia unaitwa udhalilishaji kijinsia. Mifano ya udhalilishaji kijinsia ni: Kumwita msichana mchafu,anajirahisisha au mkarimu kwa sababu tu ya uvumi kwamba amekuwa na wapenzi wengi. Kupiga miluzi au kutoa maoni juu ya mwonekano wa mtu anapopita mbele yako. Utani wa kimapenzi kama vile utani kuhusu matiti au mwili wa msichana. Udhalilishaji kijinsia unaweza kutokea mahali popote shuleni, mtaani, sokoni, kanisani au nyumbani.udhalilishaji kijinsia mara nyingi unatokea kwenye mabasi wakati wa kwenda shuleni au wakati wa kurudi nyumbani. Wadhalilishaji wanaweza kuwa wageni au watu unaowafahamu, kama mwalimu, jirani, ndugu au mtu mnayefanya naye kazi au mwanafunzi. Udhalilishaji kijinsia ni jambo zito. Maneno tu yanaweza kuharibu heshima yako. Yanaweza kukufanya ujisikie kudhalilika na kukosa raha. Yanaweza vilevile kukufanya uogope. Kuogopa kwa sababu ya kudhalilishwa kijinsia ni jambo la kawaida na la asili. Hisia hizi ni silika inayokueleza uwe mwangalifu. Watu wanaotoa maneno mabaya kijinsia, kwa vyovyote vile hawajali hisia zako. Hawajali kama yanakuumiza. Maneno machafu ya kijinsia yanaweza kuwa ni onyo kwamba, jambo baya zaidi linakuja. Njia nzuri ya kumudu udhalilishaji kijinsia ni kuwaepuka watu wanaotoa maneno machafu ya kijinsia. Usionyeshe unaogopa. Kuwa mtulivu na mwenye kujiamini, na ondoka sehemu hiyo. Jaribu kuepuka hali kama hii baadaye. Kwa mfano, kama kuna mtu anakusumbua unapokwenda shuleni, jaribu kubadilisha njia au muda unaokwenda. Njia nyingine za kumudu udhalilishaji kijinsia ni pamoja na: Kutojilaumu. Kumbuka, hakuna mwenye haki ya kukunyanyasa kwa vile unavyoonekana, ulivyovaa au tabia yako ya mapenzi iliyopita. Kuongea na mtu. Usinyamaze kimya; zungumza na mzazi, shangazi, mjomba, mwelimishaji rika au mwalimu unayemwamini. Waombe wakusaidie kuishughulikia hali hiyo. UBAKAJI Ubakaji ni kitendo cha kutumia nguvu ambacho mtu analazimishwa kujamiiana.waathirika wa ubakaji mara nyingi ni wanawake, hata hivyo, wakati mwingine wavulana na wanaume wanabakwa vilevile. Ubakaji ni kitendo cha kulazimisha, utumiaji wa nguvu, kufedhehesha na ukatili. Watu wengi wanadhani kwamba wabakaji ni wageni wenye vurugu. Hata hivyo hili ni jambo ambalo sio la kawaida, kubakwa na mtu asiyejulikana ni mara chache sana. Wengi waliobakwa wanawafahamu waliowashambulia. Kawaida mshambuliaji anaweza kuwa ni rafiki wa kiume, jirani, ndugu au rafiki wa familia. Beth kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Ilikuwa tarehe 16 mwezi wa Novemba nilipomtembelea rafiki yangu. Hakuwa mpenzi wangu, alikuwa rafiki wa kawaida. Kawaida nilikuwa ninaenda huko na kukaa naye siku nzima. Lakini siku hiyo alibadilika. Alinivutia kitandani na tukaanza kupambana. Alitaka kunilazimisha tujamiiane lakini nilikataa. Baadaye alianza kusema maneno matamu na hakutaka kunisikiliza. Kisha niliruka pembeni na kumweleza kwamba sitaki nipate mimba kwa sababu mimi ningali mdogo. Nilitoka nje ya nyumba nikimuaga kwa heri. Tangu siku hiyo sijarudi tena kwenye nyumba ya mvulana huyo. Ubakaji mwingi kwa vijana ni ule wa miadi na rafiki yako na ule wa watu uliowazoea. Ubakaji wa aina hii hutokea pale rafiki wa kiume anapomlazimisha rafiki wa kike wajamiiane bila ya ridhaa yake. Pengine walikuwa wanakumbatiana na kubusiana lakini baadaye rafiki wa kiume akamlazimisha msichana wajamiiane. Ulikuwa unafahamu kwamba mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu ubakaji siyo ya kweli? Kuna uzushi kuhusu ubakaji kama ifuatavyo: Wasichana wanafurahia. Hii siyo kweli! Ubakaji unatisha na unaleta kihoro. Unaumiza kimwili na kihisia. Hakuna mtu ambaye anaweza kufurahia kubakwa. Wasichana wanaomba kubakwa wanapovaa nguo zinazochochea ashiki au wanapotembea kwa namna ya kuchochea ashiki. Siyo kweli! Hakuna mtu anayeomba kubakwa. Mwanaume hawezi kushitakiwa kwa vile msichana au mwanamke alikuwa amemchochea kwa nguo yake fupi au kwa kukaa kifuska. Siyo kweli! Wanaume wote wanao uwezo wa kudhibiti hamu ya kujamiiana. Wale wanaosema hawawezi, wanadanganya na lazima waadhibiwe. Msichana au mwanamke akisema hapana ukweli anamaanisha ndiyo. Siyo kweli! Mwanamke akisema hapana anamaanisha hapana Hamaanishi ndio au labda. Iwapo msichana au mwanamke amebakwa, yeye ndiye wa kulaumiwa kwa sababu angeweza kuzuia. Uongo! Mwathirika kamwe hawezi kulaumiwa. Mbakaji anawajibika kwa kubaka na ana makosa. Kamwe usimlaumu aliyebakwa. Ubakaji wa miadi na ule wa watu uliowazoea ni ubakaji wa kutumia nguvu, unaumiza, unakosesha raha na ni makosa. Hata kama mvulana na msichana walikuwa wanaelewana, mvulana hana haki ya kumlazimisha msichana kufanya zaidi ya kile anachotaka

83 SURA YA 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako Hata kama wameshawahi kujamiiana kabla, lakini kwa sasa msichana hataki, mvulana hana haki ya kumlazimisha. Hata kama msichana alikuwa anavaa nguo zinazochochea ashiki, mvulana hana haki ya kumlazimisha. Katika mazingira yote haya, kitendo cha mvulana kubaka ni kosa la jinai. Naana kutoka Ghana (Umri wa miaka 16) Rafiki yangu alijamiiana kwa sababu rafiki yake wa kiume alimlazimisha. Hakutaka kujamiiana lakini hakuwa jasiri kwa sababu mpaka rafiki yake anafikia kushika matiti yake hakukataa. Kwa hiyo, kijana aliendelea na kumwingilia na akashika mimba. Wakati mwingine wasichana wanaonyesha ishara zinazochanganya. Wanaweza kujionyesha kama vile wanafurahia kinachotokea, kwa hiyo mvulana anakuwa haelewi ni wakati gani anasema hataki aendelee zaidi. Hata kama msichana hatoi ishara za wazi, mvulana hana haki ya kumbaka. Kamwe kubaka si adhabu halali kwa msichana ambaye alikuwa anatoa ishara zinazochanganya. Wavulana wengine ambao wanawabaka marafiki zao wa kike wana imani potofu kwamba mwanaume atafanya kile anachotaka bila ya kujali msichana anataka nini. Wavulana wengine wana imani potofu kwamba wasichana wanaposema hapana wanamaanisha ndiyo. Hakuna lililo la kweli kati ya haya. Mwanaume wa kweli anajali na kumfikiria mtu mwingine. Husikiliza mwenzi wake anachosema na hafanyi mzaha. Wavulana wanahitaji kujifunza kuamini yale wasichana wanayoyasema. Msichana akisema hapana anamaanisha hapana. Msichana akisema acha mvulana lazima aache. Regina kutoka Uganda (Umri wa miaka 15) Nilikuwa na rafiki wa kiume. Siku moja alinialika nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana. Nilipokwenda, nilimkuta anashughulika kutengeneza chakula. Tulikula chakula pamoja na kuosha vyombo. Nilimweleza kwamba ningependa kuondoka, lakini alinisisitizia nikae kwa muda. Aliniambia kwamba kulikuwa na sinema moja nzuri sana; kwa kweli ilikuwa ni nzuri na inavutia. Lakini katikati ya sinema aliniomba nimbusu na kujaribu kunilazimisha tujamiiane. Lakini nilikataa. Nilimwambia siwezi na kumwomba aniache, ama sivyo ningepiga kelele ya kuomba msaada. Alihofu sana na akaniacha. Nilimwambia kwamba, kwasababu ya tabia yake urafiki wetu umekwisha. Kila mtu anaweza kujifunza jinsi ya kupunguza uwezekano wa kubakwa. Kama ni msichana au mvulana, kitu cha muhimu zaidi ni kuamini hisia zako. Kwa mfano, kama mtu anakufanya ukose raha au anakutishia, zingatia hisia zako na zifanyie kazi. Mwache huyo mtu au ondoka katika mazingira hayo mara moja, hata kama hakuna sababu iliyowazi ya kukufanya ukose raha. Unaweza ukawa unapata dalili zenye hila ambazo ni ishara muhimu za kukuonya. Kamwe usipuuze hisia hizi. Zisikilize hisia zako na uzifanyie kazi. Njia Nyingine za kujilinda dhidi ya ubakaji: Usikae peke yako na mtu usiyemjua na kumwamini. Ukienda kutembea fuatana na kikundi cha marafiki na kaa na kikundi hicho. Usiende au kuendelea kukaa nyumbani kwa mtu kama hakuna mtu mwingine. Usiende sehemu za upweke ambako hakuna watu wengine jirani. Iwapo katika eneo lenu watu wanabakwa sana, beba mchanganyiko wa mchanga au pilipili iliyosagwa ili uweze kumtupia machoni mtu anayekusumbua. Kama una matembezi, hakikisha (wazazi marafiki, shangazi, mjomba) wanajua unakokwenda na muda unaotegemea kurudi. Kuwa jasiri na kusema HAPANA kwa Ijue mipaka yako. Kabla hujaenda sauti na kwa nguvu kwenye miadi yako, fikiria kile unachotaka kukifanya na kile ambacho hutaki kukifanya. Usijaribu kufikiria wakati tayari upo na rafiki yako na mnakumbatiana na kubusiana. Kuwa mwazi kuhusu mipaka yako. Ikiwa hutaki kujamiiana mweleze rafiki yako bila kuficha, hasa uhusiano unapoanza ili kuhakikisha kwamba wote mna mategemeo yanayofanana. Unapotoka kwa ajili ya miadi; hakikisha unazo pesa za kwako ili uweze kurudi nyumbani kama miadi itageuka kuwa michungu. Gawana gharama na rafiki yako. Usimwache akafikiri anakudai ngono kama malipo ya pesa alizotumia kwa ajili yako. Usinywe pombe wala dawa za kulevya. Pombe na dawa za kulevya zinaweza kukufanya ushindwe kuwa mwazi kuhusu mipaka yako. Unaweza kushindwa kujimudu. Usikubali kinywaji kutoka kwa mtu usiyemjua na usiache kinywaji chako unapokwenda chooni kwa sababu mtu anaweza kuweka dawa za kulevya ndani ya kinywaji chako. Kama umetoka na rafiki yako naye akaanza kukushinikiza, kataa kwa nguvu. Usimwachie mwanya wowote wa yeye kudhani unamaanisha ndio wakati unaposema hapana. Sema kwa nguvu na kwa sauti kubwa na mwangalie moja kwa moja machoni. Usitabasamu wala usiangalie pembeni kwa aibu. Usimwonyeshe rafiki yako alama ya kuwa unataka ushawishike au kubembelezwa. Iwapo upo katika hali mbaya na kuna mtu anajaribu kukuzidi nguvu unaweza kupigana naye, bila kujali jinsia na ukubwa wa umbo. Unazo nguvu na akili ya kupigana. Tumia kila ulichonacho kujilinda. Piga ukelele mkubwa kwa mfululizo kuomba msaada

84 SURA YA 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ya ridhaa yako Vaa au weka ndani ya sanduku, nguo zilizovaliwa wakati ubakaji unatokea. Nguo hizi zitatumika kama ushahidi kuhakikisha kwamba ubakaji umetokea. Jaribu kumtafuta mhudumu wa afya ambaye ni wa jinsi yako akuchunguze mara utakapofika kituo cha afya. Iwapo wewe ni msichana mwombe mhudumu msichana akuchunguze. Mhudumu anatakiwa achunguze kama kuna mikato, michaniko au michubuko. Na anaweza kuchukua sampuli ya shahawa ukeni. Njia za kujilinda ni pamoja na: Tumia nguvu zako zote kumsukuma na kupigana Silaha nzuri uliyonayo ni vidole vyako na kucha. Mchome kwa nguvu kwa kutumia vidole ndani ya macho ya mshambuliaji. Usihofu kumuumiza. Alikuwa na nia ya kukuumiza. Tumia goti kumpiga teke la nguvu kwenye sehemu za siri. Iwapo utatumia nguvu, ataumia sana na kumsababishia maumivu mara mbili. Iwapo mtu huyo yuko juu yako na anausukumiza uso chini kwenye ardhi, tumia kisigino kumpiga teke kwenye mifupa ya chini ya mgongo, juu kidogo ya matako. Iwapo unazidiwa nguvu, tulia, jaribu kumdanganya mshambuliaji kwa kumshikashika. Halafu mchome machoni au piga mapumbu. Kimbia mara mbakaji atakapotulia kidogo kwa sababu ya maumivu. KITU CHA KUFANYA UBAKAJI UKITOKEA Wakati mwingine pamoja na jitihada zote za kujaribu kujitetea ubakaji unatokea, msichana au mvulana anaweza kuzidiwa nguvu na mshambuliaji na ukashindwa kujinasua. Hii ni hali mbaya sana, kwa hiyo ni muhimu kujua cha kufanya baada ya hapo. Ubakaji ukitokea kwako au kwa mtu unayemfahamu, haya ndiyo unatakiwa kufanya: Pata huduma ya matibabu haraka iwezekenavyo. Lazima upime vipimo kuhakikisha kwamba upo salama na kwamba majeraha yote yanatibiwa. Omba dawa za dharura za kuzuia mimba (angalia Sura ya 11 kwa taarifa zaidi kuhusu kuzuia mimba kwa dharura). Omba vilevile upime vipimo vya magonjwa ya ngono na VVU. Kipimo cha VVU utahitajika kukirudia baada ya miezi 3 hadi 6 ili kuhakikisha maambukizo hayajatokea. (angalia Sura ya 10 kwa taarifa zaidi kuhusu VVU na magonjwa mengine ya zinaa). Mwombe mhudumu wa afya aandike kila kitu anachokiona. Taarifa hii inaweza kusaidia kuhakikisha kwamba ulibakwa. Mwombe mhudumu wa afya akushauri wapi uende kutoa taarifa ya kubakwa. Iwapo mhudumu wa afya hajui, nenda kwenye kituo cha vijana au kikundi cha wanawake. Waombe ushauri namna ya kutoa taarifa kuhusu ubakaji na wapi unaweza kupata ushauri wa kisheria kama unataka kumshitaki mbakaji. Iwapo unataka kutoa taarifa kuhusu ubakaji fanya hivyo mapema iwezekanavyo. Nchi nyingi zimeweka sheria na adhabu kali kwa mtu atakayepatikana na kosa la kubaka. Ukiamua kutoa taarifa polisi au kwa viongozi wa kijiji, fanya hivyo bila kuchelewa. Unahitaji kuwa jasiri kutoa taarifa ya ubakaji kwa sababu inaumiza na kuhuzunisha kuzungumzia yaliyotokea lakini lazima utoe taarifa hiyo. Usipofanya hivyo ataondoka na kuwa huru na anaweza kumuumiza mtu mwingine. Pata nasaha. Lazima umpate mtu wa kuzungumza naye kuhusu hisia zako za hofu, huzuni, hasira na maumivu. Mtaalamu wa nasaha anaweza kukusaidia kuchambua hisia zako ili uweze kuendelea na maisha yako ya kila siku. Ni muhimu kujua kwamba katika nchi nyingi ni kosa mwanamke kutoa mimba ambayo ni matokeo ya kubakwa. Iwapo unafikiri kwamba umepata mimba, zungumza na mhudumu wa afya au waone kikundi cha akina mama ili kujua uchaguzi ulionao. Inaweza ikakuchukua muda mrefu kupona kimwili na kihisia baada ya kubakwa. Kuwa mvumilivu. Jambo la muhimu zaidi usijilaumu au kufikiria uliwajibika kwa ubakaji huo. Halikuwa kosa lako. Mwombe mzazi, shangazi, mdogo wako au rafiki wa karibu akusindikize kliniki / hospitalini au polisi ili ukapate msaada. Mtafute mtu ambaye ana nguvu, anajali na anategemewa. Mtu unayemwamini na ambaye hatasema kwa watu wengine. Usioge kabla ya kwenda kutibiwa. Ingawa wazo la kwanza la mtu ni kuoga vizuri, siyo vizuri kufanya hivyo. Watalaamu wanashauri kwamba mtu aliyebakwa asinawe hata mikono yake kwa sababu inaweza kuharibu ushahidi (uchafu, shahawa, majimaji ya mwili, nywele n.k.) ambavyo vingetumika kuhakikisha kwamba ubakaji umetokea na ni nani aliyefanya hivyo

85 Sura ya 12 Ngono ya kulazimishwa na Ngono bila ridhaa yako Ngono isiyotakiwa ni hatari; inakuweka katika uwezekano mkubwa wa kupata mimba isiyotakiwa na magonjwa ya zinaa na VVU/UKIMWI. Inaweza kuwa mbaya vilevile kwa afya ya hisia zako. Inaumiza sana na kuleta kiwewe ukijamiiana bila ya ridhaa yako. Ngono isiyotakiwa inajumuisha mambo mengi tofauti. Inaweza ikawa: Kushikwa au kuguswa kijinsia bila ya ridhaa yako. Hii ni kunyanyaswa kijinsia. Matusi ya kijinsia yasiyotakiwa ni udhalilishaji kijinsia. Kulazimishwa ngono; huu ni ubakaji. Mbakaji anaweza akawa mgeni kabisa, lakini kawaida ni watu ambao wanafahamika kwa anayebakwa kama rafiki wa kiume, rafiki, jirani au ndugu. Njia nzuri ya kujilinda ni kujifunza jinsi ya kugundua na kuepuka mazingira ambayo utakuwa hatarini kulazimishwa ngono: Epuka uhusiano na watu wazima. Uhusiano huu unakuweka katika uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya ngono na mimba kwa sababu uhusiano huu hauna usawa. Unaweza usiwe na nguvu ya kusema hapana ukiombwa ngono au kumlazimisha mtu mzima atumie kondomu. Amini hisia zako. Iwapo kuna mtu anakufanya ujisikie vibaya au uwe mwenye wasiwasi, mwache mtu huyo mara moja. Hisia zako ni ishara muhimu, usizipuuzie. Usije hata siku moja ukawa peke yako na mtu ambaye humwelewi vizuri na kumwamini. Usiende nyumbani kwa mtu kama hakuna mtu mwingine. Fuatana na kundi la marafiki na kaa nalo. Jua mipaka yako na hakikisha rafiki yako wa kiume au wa kike anaielewa mipaka hiyo. Usiwaruhusu watu wengine wakupatie zawadi au watumie pesa kwa ajili yako kwa sababu wanaweza kukuomba urudishe msaada huo kwa kufanya nao ngono. Usinywe pombe au kutumia dawa za kulevya. Kuwa jasiri, usiwachanganye watu kwamba unaposema hapana unamaanisha ndio. Usitoe ishara yoyote kwamba unataka kushawishiwa na kubembelezwa kwanza. Wakati mwingine ubakaji unatokea licha ya mtu kujitahidi kujilinda. Iwapo hili litatokea, unahitaji kupata matibabu na ushauri moja kwa moja. Mhudumu wa afya anaweza kukupatia dawa ya dharura ya kuzuia mimba. Usioge kwanza kwa sababu itakuwa vigumu kuhakikisha kwamba ulibakwa. Tunza nguo ulizokuwa umevaa wakati ubakaji unatokea. Jambo la muhimu zaidi, usijilaumu. Halikuwa kosa lako. Jipe muda wa kupona kimwili na kihisia. Matumizi mabaya ya dawa Mara nyingine watu hutumia dawa na viini kadhaa ambavyo haviponyi magonjwa. Dawa hizi zinabadili jinsi mtu anavyojisikia na anavyofikiri. Zinaweza kumfanya mtu awe mcheshi zaidi, mwerevu, mpole, jasiri na anayefurahisha kuwa naye. Dawa hizi zinaweza kumfanya mtu asiwe mwoga na asifadhaike. Lakini hisia hizi zinadumu kwa muda mfupi sana na hivyo kutumia dawa kama njia ya kujifurahisha na kufanikisha mambo yako ni hatari sana. Kutumia dawa kwa njia hii kunaitwa matumizi mabaya ya dawa. Matumizi mabaya ya dawa ni tatizo kubwa linalotukabili. Dawa zingine kama pombe na sigara ni sehemu katika maisha yetu ya kila siku kiasi kwamba hatufikirii kama ni dawa za kulevya. Lakini pombe na sigara ni dawa za kulevya na mara nyingi watu wanazitumia vibaya. Dawa zinadhuru akili yako, mwili wako, na uhusiano wako na watu wengine. Zinaweza kukufanya mgonjwa na usipate mafanikio katika maisha yako yote. Zinaweza kusababisha ufanye vibaya shuleni, upoteze marafiki na ukosane na wazazi wako. Zitakufanya utumie pesa yote utakayofanikiwa kuipata. Dawa zinaweza kufanya iwe vigumu kwako kufanikisha mpango wa kufanya ngono salama. Wakati wote unatakiwa kuwa makini kuhusu ngono. Unahitaji kuwa na uwezo wa kusema Hakuna kujamiiana, hakuna kabisa.; au ninataka busu tu na sitaki kujamiiana, au nitatumia kondomu tu. Dawa zinafanya ubongo usifanye kazi vizuri. Zinaweza kukufanya ufanye mambo ya hatari kama kufanya ngono isiyo salama. Kutokana na hiyo unaweza ukaishia kupata magonjwa ya zinaa pamoja na VVU/UKIMWI. Unaweza ukaishia kupata mimba au kumpa mimba msichana. AINA YA DAWA NA VITU AMBAVYO VINATUMIKA VIBAYA Kuna aina nyingi za dawa zinazotumiwa vibaya na watu. Zinaweza zikasababisha matatizo ya kweli. Zifuatazo ni baadhi tu ya dawa zinazojulikana na baadhi ya matatizo yanayoweza kukupata. Marijuana ambayo majina yake kadhaa ni Bangi, hashi, poti, majani, gugu, acapulco gold au fimbo ya Thai. Dawa zote hizi zinatokana na mimea. Kwa kawaida watu wanavuta majani lakini mara nyingine ipo dawa ya nguvu zaidi inayotengenezwa kutokana na mashina ya mimea. SURA YA

86 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa Bangi inaweza kumfanya mtu ajisikie ameburudika na kufurahi, au inaweza kumfanya mtu ajisikie kutetemeka sana na kuogopa. Kuvuta bangi kunaweza kusababisha macho yawe mekundu, midomo na koo kuwa mikavu na hamu ya kula kuongezeka. Unaweza kujisikia usingizi, na wasiwasi wako kutoweka katika muda ambao ulevi umekolea. Lakini ujue utashindwa kufanya uamuzi hata ule ulio mdogo! Kuvuta sana na matumizi ya muda mrefu ya bangi yana madhara kwenye mapafu na yanaweza kusababisha saratani. Uvutaji unaweza vilevile kuathiri kumbukumbu na uwezo wa kuwa makini na kuelewa mambo. Inawezekana kuwa vigumu kuendelea na masomo au kuwa na maendeleo mazuri ya kazi kwa sababu kumbukumbu na usikivu vinakuwa vimepungua. Khat, gat, miraa au mirungi ni aina ya jani linalotafunwa maeneo ya pembezoni mwa Afrika na karibu Afrika ya Mashariki yote. Hii ni dawa maarufu sana katika baadhi ya jumuia kwa sababu inafanya ujisikie kuwa macho zaidi, mwenye nguvu na mwenye kujiamini. Vilevile, inapunguza njaa. Athari mbaya za kutafuna jani hili ni pamoja na kuwa na wasiwasi, uchokozi, uhanithi (kama mwanaume hawezi kusimamisha uume) na maono ya vitu ambavyo havipo. Petroli, gundi, rangi, tina na bidhaa za viwandani zinazowekwa kwenye makopo ya kupuliza. Mara nyingine zinavutwa ili kujiweka katika hali ya ulevi. Vitu hivyo vinaweza kufanya ujisikie joto, njaa kidogo, hupunguza woga na kukufanya mwenye furaha angalau kwa muda. Baada ya kuvuta vitu hivyo, unajisikia usingizi na unajiona haupo kabisa kwenye mazingira yanayokuzunguka. Kwa kuwa vitu hivyo ni rahisi sana kununua, vinakuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa mitaani. Dawa hizi zinaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika. Unaweza kupoteza mwelekeo na ukachanganyikiwa na usiweze kudhibiti hatari zinazokuzunguka. Kwa hiyo, unaweza kugongwa na gari kwasababu utashindwa vitu rahisi kama kuvuka barabara. Kuvuta kwa muda mrefu kunaweza kusababisha ukakosa fahamu (kuzimia au kufariki), kukabwa roho (kushindwa kupumua) na kifo. Matumizi ya mara kwa mara ya vitu hivi yanaweza kukuharibu mapafu, ubongo na viungo vingine muhimu vya mwili. Dawa za kutuliza ni pamoja na valiumu na mandraksi: Dawa hizi zinaweza kukufanya ujisikie mwenye usingizi au kama umepumzika vile na uko shwari. Zinapunguza mapigo ya moyo na kupunguza kupumua.ukizidisha zinaweza kukuua kwa haraka na kiurahisi. Dawa zenye kuleta njozi, kama angel dust, LSD (pia yanaitwa tindikali, mchemraba wa sukari, dragoni na magugu yanayoua). Dawa hizi zinaweza kukufanya uhisi mambo ambayo hayapo. Dawa hizi zinasababisha kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kupoteza usingizi na kupandisha joto la mwili. Mtumiaji anaweza pia kuwa na wasiwasi, tabia ya vurugu, mfadhaiko na wazimu (ugonjwa wa akili usiotibika.) Wakati uko katika hali ya ulevi kwa sababu ya dawa na unahisi kwamba unaweza ukajiumiza. Matumizi ya muda mrefu yanaweza kuleta matatizo ya kupoteza kumbukumbu, na ukizidisha zinaweza kusababisha kutetemeka, kupoteza fahamu na hatimaye kifo. Dawa kali (narcotics) zikijumuisha dawa kama heroini (pia inaitwa junki, sukari ya kahawia na smak) na kokeini (inaitwa koki, crak na barafu). Katika Bara la Afrika dawa kali ni matatizo makubwa, na watu wengi wanazitumia. Mara nyingi zinatumika kwa kujidunga sindano inayoenda moja kwa moja kwenye mishipa ya damu. Dawa hizi ni rahisi sana kuzizoea mwilini. Ukianza kuzitumia inaweza ikakuwia vigumu kuziacha. Watu ambao wamezizoea wanaona kana kwamba hawawezi kuishi bila dawa hizo. Dawa hizi zimepigwa marufuku kabisa, na ili kuzipata shurti ufuatane na watu ambao wanavunja sheria. Dawa hizi ni ghali sana hivyo watu wengine wanaozitumia wanaanza kuiba fedha ili wapate fedha ya kutosha kuweza kuzinunua. Watu wengine wanauza miili yao ili kupata fedha ya kutosha kununua dawa hizi. Watu wengine wanaotumia dawa hizi hutumia sindano kwa kujichoma ili waweze kuzizoea mwilini. Wale wanaochangia sindano wana hatari kubwa ya kupata mambukizo ya VVU. SIGARA NA POMBE Watu wengi wanapofikiria dawa za kulevya huwa hawaorodheshi pombe na sigara. Hata hivyo, pombe na sigara mara nyingi vinatumiwa vibaya kama dawa nyingine za kulevya na zina athari zake. Tumbaku, sigara (vilevile zinaitwa, dragis, batis, na fegi) na mitemba. Nikotini ni kiambato kichochezi katika tumbaku, sigara na mitemba. Nikotini haikufanyi ujisikie uko juujuu kama ilivyo bangi au pombe na wala haiharibu uwezo wako wa kuamua. Inaweza kukufanya ujisikie mwenye nguvu nyingi na inapunguza hamu yako ya kula. Hatari moja kubwa ya nikotini ni kwamba inazoeleka sana mwilini. Umewahi kuona wavutaji wakitaka kuacha kuvuta?. Wanakuwa wanyonge, hawawezi kulala au kuunganisha mawazo, wanaudhika upesi na wanakuwa na hasira na wasiwasi. Kujisikia kwa namna hii kunaudhi kiasi kwamba watu wengi wanashindwa kuacha kuvuta na wanajaribu tena na tena kabla ya kufanikiwa kuiacha tabia hii. Siyo tu kwamba nikotini inazoeleka sana mwilini bali pia ni hatari kwa afya yako.uvutaji umeonekana kusababisha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na saratani ya koo, ulimi, mapafu, matiti na utumbo mkubwa. Uvutaji unaharibu moyo na mishipa ya damu katika mwili na inaweza kuleta hatari ya kupata shinikizo la damu, kiharusi na ugonjwa wa moyo. Pia uvutaji sigara umeonekana kusababisha uhanithi kwa wanaume. Hii ni kwa sababu uvutaji unaharibu mishipa ya damu katika uume kama unavyoharibu mishipa ya damu mingine mwilini. Pombe ni dawa ya kulevya maarufu sana Afrika na kwa kweli dunia nzima. Tofauti na dawa zingine za kulevya, pombe imehalalishwa kisheria na inapatikana kwa aina mbalimbali na kwa bei ndogo.kwa hiyo pombe ni dawa ya kulevya ambayo kuna uwezekano wa kukumbana nayo. Mara nyingi ndani ya nyumba, mmoja wa wazazi wako au wote wanaweza wakawa wanakunywa pombe. Inaweza ikawa rahisi kwako kuipata na haitaonekana kama kitu cha kutisha kwa sababu ni kitu cha kawaida katika jamii

87 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa Ni rahisi kuanza kunywa pombe na usiifikirie sana kuhusu jambo hilo. Lakini fikiria tena! Pombe ni dawa ya kulevya kama dawa nyingine za kulevya. Pombe inadumaza mfumo wa mwili. Baada ya kunywa pombe kidogo, matendo yako yanaweza yakawa ya taratibu na inaweza ikakuwia vigumu kufikiri vizuri. Ukiongeza kidogo tena, unashindwa kusema vizuri na unaweza kuwa mkali na mchokozi. Kama siyo mzoefu wa pombe au kama unakunywa sana unaweza kutapika sana au ukapoteza fahamu. Athari za muda mrefu za unywaji sana pombe ni mbaya. Nadhani unawafahamu watu katika jamii ambao ni walevi sana na ambao hawawezi kuishi bila kunywa. Unaweza ukawa umeona jinsi inavyoharibu familia, watu kupoteza kazi, na inasababisha afya kuwa mbaya, kama kuharibu ubongo na kuleta ugonjwa wa ini. Pombe ni dawa ya kulevya maarufu sana ambayo inawafanya watu wastarehe na kusahau taabu zao. Hata hivyo, kujiona umestarehe mno na kutojitambua si jambo zuri kwani kunaweza kukufanya upate matatizo. Pombe kama ilivyo kwa dawa nyingine za kubadili hali ya mtu, inaondoa uwezo wa kujizuia na mambo unayoona yatakutia aibu mbele ya wenzio. Pombe inakupa ujasiri wa kuzungumza mambo ambayo baadaye utakuja yajutia. Kwa mfano, wasichana wengi wakiwa hawajanywa hawana ujasiri wa kwenda kwa mwanaume na kumbusu kwenye mdomo lakini msichana akiwa amekunywa pombe anaweza kujisikia huru sana; anajisikia kumbusu mvulana na anafanya hivyo. Pombe inaweza pia kumfanya mvulana afanye vitu ambavyo kwa kawaida asingelifanya. Kwa mfano, mvulana anaweza akaamua kutaka kujamiiana na msichana baada ya kunywa pombe. Hata kama rafiki yake wa kike anataka au hataki, anaweza kujaribu kumlazimisha kujamiiana naye. Pombe inamfanya asiweze kumfikiria rafiki yake wa kike anavyojisikia; inamfanya pia asiweze kufikiria matokeo ya jambo analotaka kutenda. Lazarus kutoka Zambia (Umri wa miaka 15) Ninapokunywa ninasahau hatari zote zinazonizunguka. Ninasahau kila kitu kuhusu kondomu. Hivyo huwa ninafanya ngono bila kinga kwa sababu ya kishawishi cha pombe. Ninajua nina uwezekano wa kuambukizwa. Iwapo kinywaji cha kawaida kama pombe kinaweza kukuletea matatizo makubwa kama hayo, hebu fikiria kinachoweza kutokea kama ukitumia dawa kali zaidi kama kokeni. Je, unajua kwamba matumizi ya dawa za kulevya zina matatizo ya kipekee kwa wanawake na wasichana? Wakati dawa za kulevya zote zina madhara mwilini, nyingi zinawaathiri zaidi wanawake na wasichana kuliko wanaume. Kwa mfano, kuvuta sigara kunaleta madhara ya pekee kwa wanawake. Kunaweza: Kuleta matatizo ya kiafya kama mwanamke anatumia vidonge vya kuzuia mimba. Kupunguza miaka ya mwanamke ya kuzaa watoto kwa sababu tukio la hedhi kukoma litatokea mapema Kuongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya mlango wa mfuko wa kizazi na tumbo la uzazi. Kusababisha mifupa ya mwanamke kuwa dhaifu. Kusababisha iwe vigumu kwa mwanamke kupata mimba. Kuongeza hatari ya mimba kutoka kwa mwanamke mjamzito. Kufanya mwanamke azae mtoto mdogo sana au mtoto azaliwe mapema kabla ya wakati. Kumeza dawa na kunywa pombe wakati mwanamke ana mimba ni hatari kwa sababu inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya na ya mtoto kuzaliwa na kasoro, kama kuundwa vibaya kwa moyo, mifupa, kichwa na viungo muhimu vya ndani. Mtoto pia anaweza kuzaliwa na uzito mdogo, kukua taratibu na kutokuwa na uwezo wa kujifunza darasani. Matumizi mabaya ya dawa wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha uzae mtoto ambaye tayari ameathirika na dawa na hivyo kuzoeleka mwilini mwake. Kumbuka, ukiwa unatumia dawa wakati wa ujauzito, mtoto wako pia anapata kiwango kikubwa kuliko wewe. Athari kwa mtoto zitakuwa kubwa zaidi kuliko kwako. KUTAWALIWA NA DAWA Kadiri mtu anavyoanza mapema kutumia dawa, ndivyo anavyojiwekea nafasi ya kujenga matatizo makubwa yanayohusiana na dawa baadaye. Athari za dawa nyingi zinaongezeka kadiri muda unavyopita. Athari zinajijenga mwilini, kama bomu lililotegwa kwa muda maalumu likisubiri muda ufike lilipuke. Unapokunywa pombe, sheria zinazotawala tabia yako ya kawaida zinapungua. Uwezo wako wa kuamua mambo mazuri unapungua. Kwa hiyo, unapoteza uwezo wa kupima mambo. Kijana mmoja anasema haya kuhusu pombe: Pombe inaathiri uwezo wako wa kufanya uamuzi salama Kuna dalili nyingi zinazojitokeza matumizi ya dawa zinapofikia kuwa matatizo makubwa. Dalili hizo ni:- Kuongopa kuhusu kiasi cha dawa unachotumia. Hii ni pamoja na kujidanganya mwenyewe kiasi gani cha dawa au pombe unayotumia

88 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa Kuficha dawa ili watu wengine wasizione. Kuwa na matatizo ya fedha kwa sababu zote zimetumika kwa dawa. Kujiaibisha mwenyewe na wengine hadharani kwa kufanya vitendo vya aibu. Iwapo wewe au mtu yeyote unayemfahamu anaanza kuacha kufanya mambo anayoyapenda, anatumia muda kidogo kwenye kazi za shuleni, anakwepa kuwajibika, anataka sherehe na anataka kupigana baada ya kunywa au akiwa amelewa basi matumizi ya dawa yanamfanya aingie katika matatizo makubwa na anahitaji asaidiwe ili aache au unahitaji kusaidiwa ili uache. Irinne kutoka Zambia (Umri wa miaka 16) Rafiki yangu alikuwa anatumia dawa, na dawa zikamzoea mwilini. Hakuwa anaweza kukaa hata saa moja bila kuzitumia. Alizizoea hadi wakati fulani akizikosa alikuwa anapigana hovyo na ndugu zake na majirani. Moja ya matatizo makubwa ya kutumia dawa ni mwili kutawaliwa na dawa hizo. Mwili unapozoea dawa hizo inabidi uzitegemee ili uweze kufanya kazi za kila siku. Dalili za mwili kuzoea dawa ni pamoja na: Kujisikia kana kwamba dawa ni muhimu ili kukamilisha siku. Kutaka zaidi na zaidi dawa ili uweze kujisikia ipasavyo. Kuanza kuona mabadiliko mabovu ya tabia kama vile hasira, wasiwasi, vurugu za ghafla. Kupoteza fahamu (kuzimia) baada ya kuzitumia. Salome kutoka Kenya (Umri wa miaka 17) Mmoja wa marafiki zangu ambaye alizoea kutumia dawa aliugua sana. Pua yake ilikuwa inatoa damu wakati wowote. Mara nyingine alikuwa anaanguka chini. Mara mwili unapokuwa umetawaliwa na dawa, unahitaji zaidi na zaidi dawa hizo ili uweze kujisikia vizuri. Hii ni gharama na inaharibu mwili wako. Kwa dawa kali kama kokeini na heroini, mara zinapozoeleka mwilini, ukizikosa unaugua sana. Ukiacha kutumia, moja kwa moja, utapata dalili zisizopendeza, kama kutetemeka, kichefuchefu, kutapika, maumivu na shida katika kupata usingizi na kula. Hali hii inaweza ikawa mbaya kiasi kwamba utataka kurudia tena kutumia dawa hizo. Dalili hizi za kujisikia vibaya zinaitwa dalili za kujitoa. Ni hisia za mwili kutokana na dawa kuondolewa mwilini. Kwa sababu mwili wako umekuwa tegemezi kwa dawa hizi, mwili unaugua kwa kukosa dawa hizo. Julia kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Niliacha kutumia dawa rafiki yangu mpenzi aliponishauri kuhusu hatari za dawa. Mara ya kwanza nilidharau, lakini baada ya muda nilijaribu kujidhibiti mwenyewe. Niliambiwa na rafiki yangu nisizitumie kwa wiki moja, lakini nilimweleza nisingaliweza bila dawa hizo. Hata hivyo, namshukuru Mungu kwamba wiki nzima sikuzitumia na sasa najua naweza kuishi bila dawa hizo. Kuyashinda mazoea ni vigumu sana na watu tofauti wanao uzoefu tofauti. Watu wengine wana uwezo wa kuacha kutumia dawa mara moja. Watu wengine wanahitaji kuacha taratibu, kwa kupunguza kiwango cha kutumia. Hii inasaidia kuulinda mwili kutokana na mshituko wa kuacha ghafla. Kuacha kidogo kidogo kunasaidia kuruhusu mwili kuanza kujitoa kwenye dawa. Omari kutoka Tanzania (Umri wa miaka 18) Niliacha kutumia dawa baada ya kushuhudia athari zinazotokana na kujihusisha katika kutumia dawa. Baadhi ya marafiki zangu wamefariki kutokana na maambukizo ya kifua au maradhi mengine. Ilibidi niende kupata ushauri dhidi ya dawa na kwa kufanya hivyo nimeweza kuacha. Kushinda utegemezi wa dawa za kulevya kunahitaji nguvu kubwa na dhamira, ujasiri na uamuzi thabiti. Kuna wakati ambapo utajisikia kama vile huwezi. Kwa hiyo ni jambo muhimu kutafuta msaada na kuungwa mkono. Zungumza na mshauri wa vijana au mhudumu wa afya kuangalia kama kuna msaada wa vikundi au mpango unaoweza kujiunga nao. Jambo la muhimu zaidi usishirikiane na watu ambao watakurudisha nyuma. Usishirikiane na watu ambao hawatakusaidia kuacha tabia yako. KWA NINI WATU WANAANZA KUTUMIA DAWA? Njia iliyo wazi na sahihi ya kuepuka kupata matatizo ya kutawaliwa na dawa ni kutokuanza kutumia dawa kabisa. Kwa hiyo, ni vizuri kuelewa ni kwa nini watu wanaanza kutumia dawa, ili uwe mwangalifu na kuhakikisha kuwa kamwe huangukii katika mitego hiyo. Kuna sababu nyingi zinazowafanya vijana kuanza kutumia dawa kama kokeini na heroini au hizi zilizozoeleka kama pombe na sigara: Kwanza, vijana wengi wanatumia dawa kwa sababu wenzao wa rika moja wanafanya hivyo na kwa sababu wanataka kuonekana sawa katika kundi. Makundi mengine yanatumia dawa kama sehemu ya utambulisho wa kundi lao. Kama unataka kuwa sehemu ya kundi, unaweza kupata msukumo wa kutumia dawa kama wanayotumia wenzako

89 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa Wenzako wanaweza kukuomba ujaribu kutumia dawa na kudharau athari zake. Wanaweza wakakasirika au wakakutukana kama hujaribishi kuvuta. Margaret kutoka Kenya (Umri wa miaka 16) Nilikuwa na miaka 13 nilipoanza kutumia dawa. Marafiki zangu walianza kuvuta bangi. Waliniambia nivute pafu moja tu, lakini nilikataa. Wakaanza kunicheka, na kwa vile sikutaka kuambiwa kuwa ni mwoga, niliamua kuvuta pafu moja. Pili, wengi wanatumia dawa kwa sababu wanataka kukwepa matatizo katika maisha yao. Labda waligombana na wazazi wao au pengine marafiki wamewaumiza kihisia. Wanaweza kuwa wanajisikia wenye huzuni, wasiwasi au wamezidiwa na matatizo. Dawa zinaweza kuonekana kama njia rahisi ya kuepukana na matatizo. Marion kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 17) Baadhi ya marafiki zangu walianza kutumia dawa kwa sababu ya matatizo nyumbani au nje. Francis kutoka Uganda (Umri wa miaka 15) Baadhi ya marafiki zangu wamepoteza wazazi wao kutokana na UKIMWI na wanatumia dawa kusahau matatizo yao. Tatu, wengine wanatumia dawa za kulevya kwa sababu wanataka waonekane tofauti na vile walivyo. Vijana wengi hawajisikii ni wazuri vya kutosha kama walivyo. Wanataka wawe na ujasiri wa ajabu, waongee kwa sauti ya juu, waonekane wanavutia na wamekua. Dawa zinaweza kuwafanya wawe watu tofauti. Juma kutoka Kenya (Umri wa miaka 17) Ninao marafiki ambao wanatumia dawa kila wakati, kama dawa zinazoathiri akili na bangi. Wanatumia dawa hizi ili wajisikie watu wazima na bora kuliko wenzao. Lakini dawa hizi zimewasababishia wasizingatie kazi zao, ndoto, malengo na tamaa zao za baadaye. Nne, watu wengine wanafikiri dawa zitawafanya wapate ujasiri wa kufanya mambo ambayo wanaogopa kuyafanya. Kuna mazingira mengi katika maisha yanayohitaji ujasiri. Unaweza ukawa mwoga kuongea darasani au unaweza kuwa mwoga kumwendea msichana au mvulana unayempenda. Dawa zinaweza kuonekana kama njia rahisi kuushinda woga huu. Sita, vijana wengi wanatumia dawa kwa sababu ya kuchoshwa na maisha. Wanataka kuwa na furaha na hawajui kitu gani kingine kitawafurahisha. Saba, vijana wengine wanatumia dawa kwa sababu wamepoteza matumaini. Hawajisikii kama wana mpango wa maisha ya baadaye. Wanatumia dawa kwa sababu wanajiona kana kwamba hawajali kitakachowatokea. Hizi ni baadhi tu ya sababu za baadhi ya vijana kutumia dawa za kulevya. Lakini hakuna sababu hata moja inayothibitisha uhalali wa matumizi ya dawa. Kutumia dawa ni njia mbaya ya kutatua matatizo. Dawa zinafanya matatizo kuwa magumu zaidi. Ujana ni kazi ngumu, na kuna mambo mengi ungetaka kufanikisha unapokuwa kijana shuleni na nje ya shule. Unahitaji kujifunza namna ya kuvumilia matatizo, namna ya kushughulikia hisia zako, namna ya kuwa na urafiki usio na madhara, namna ya kushughulikia mabadiliko ya mwili wako. Orodha ya mambo unayopaswa kuyashinda au kuyaweza wakati wa ujana wako haina mwisho. Tatizo la dawa ni kwamba zinaweza kuingilia utaratibu wako mzima wa kupata stadi na utaalamu. Zinakusimamisha kujifunza namna ya kuvumilia mfadhaiko wa kila siku. Zinakuzuia kujifunza stadi za maisha utakazozihitaji utakapokuwa mtu mzima. Kumbuka: Huhitaji dawa ili upendwe na watu. Huhitaji dawa kuwa jasiri na shupavu. Huhitaji dawa ili kumudu huzuni au maudhi. Maryann kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Rafiki yangu Katty aliambiwa na msichana mwingine kwamba akivuta bangi anaweza kumuuliza mwalimu maswali magumu ambayo hawezi kuyajibu. Lakini mambo yalimgeukia Katty upande mwingine. Akaanza kushindwa kuyamudu masomo. Sasa hivi ni mtu aliyekata tamaa na kuacha shule. Angependa apewe nafasi tena kurudia shule lakini baba yake hataki kusikia habari hizo. Anasema kwamba alishindwa alipopewa fursa. Unaweza ukaishi bila dawa na pombe. Ndani yako unazo nguvu na nyenzo za ndani za kushughulikia hali na matatizo yoyote yale. Unahitaji kutafuta nguvu za ziada ndani yako ili kushinda tatizo hili. Kwa tatizo lolote unaloliona, msaada unaweza kupatikana. Unaweza kuzungumza na mshauri wako, mwalimu unayemwamini au mtu katika kanisa lako au msikiti wako. Zungumza na wazazi, shangazi au mjomba, kaka mkubwa au dada au rafiki unayemwamini. Msaada unapatikana ukiutafuta. Tano, vijana wengine wanaamini kuwa dawa zitawafanya wawe werevu zaidi. Wanafikiri dawa zitawasaidia wakae macho ili waweze kujisomea kwa muda mrefu na vizuri

90 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa NAMNA YA KUSHUGHULIKIA SHINIKIZO LA KUTUMIA DAWA Kumudu shinikizo kutoka kwenye kundirika linalotaka utumie dawa kama wao ni vigumu sana. Hapa kuna hadithi fupi ya kijana mmoja:- Je, maelezo haya yanakukumbusha wewe pia hali ambayo imewahi kukutokea ukiwa na wenzako? Hawa marafiki walikuwa wanahitaji sana Jeckton avute. Kwa nini walimshinikiza? Watu wengi wanataka kuungwa mkono wanapofanya jambo wanalofikiri siyo sahihi. Wanafikiri makosa yao yanakuwa madogo kama mtu mwingine anafanya nao. Marafiki zao wanapofanya jambo la kijasiri pamoja nao, hawajisikii kuogopa sana kuhusu hatari iliyopo. Kama wako katika kikundi wanajisikia kustarehe na kufurahia burudani wanazozipata kwenye dawa. Ndiyo maana watakushinikiza sana wewe. Hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kushughulikia hali hiyo: Jeckton kutoka Kenya (Umri wa miaka 15) Nilipokuwa na miaka 13, nilikuwa naelekea nyumbani nikiwa na baadhi ya marafiki zangu. Tulipita sehemu ambayo marafiki zangu mara nyingine wanaenda kukutana na baadhi ya marafiki zao. Tulipofika pale waliwakuta marafiki zao na wakapewa kifurushi cha bangi. Bila kupita muda, msichana mmoja akaanza kuvuta na akaniambia nivute pafu moja. Nilikataa, wakaanza kunicheka. Waliniita majina mabaya na wakaniambia niache kuwaaibisha. Waliniambia ilikuwa tamu sana na ingenifanya nijisikie vizuri. Kwa sababu sikutaka waelewe kwamba nilikuwa naogopa, niliamua kuvuta kidogo. Baada ya kuvuta kidogo, siwezi kusema yaliyotokea baada ya hapo maana sikumbuki tena. Nilichanganyikiwa kwa muda wa karibu siku tatu. Kumbuka kwamba huhitaji kumfanya rafiki ajisikie vizuri kwa kumuunga mkono kufanya mambo ambayo siyo mazuri kwako. Kama ni rafiki wa kweli, unaweza kumwambia rafiki yako kuwa mambo anayoyafanya ni ya hatari. Uwe mwazi kwa wenzio kwamba hutaki kutumia dawa au kitu. Waonyeshe rafiki zako kwamba unazijua akili zako zilivyo na kwamba hata wakikusihi vipi hutabadilisha mawazo yako. Ondoka kama rafiki yako anazidi kukushinikiza au anaanza kukutukana ama kukucheka. Usiendelee kujadili suala hilo zaidi. Subiri hadi atakapokuwa hatumii dawa ndiyo mwanze kuzungumza kuhusu jambo hilo. Mara nyingine tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kuliko kukataa shinikizo toka kwa marafiki. Unaweza kugundua kwamba rafiki yako analo tatizo kubwa la dawa au pombe, tatizo ambalo unaona linamharibia maisha yake. Hili nalo ni gumu kulitatua. Haya ni mambo machache unayoweza kufanya: Zungumza na rafiki yako kuhusu matumizi ya dawa wakati hajanywa au hayuko katika hali ya ulevi. Usimlaumu au kumkosoa rafiki yako. Hii itazua mabishano baina yenu. Badala yake lenga katika matatizo ya dawa na mwonyeshe rafiki yako kwamba unaogopa. Jaribu kumsaidia rafiki yako aelewe kwamba ana matatizo. Jaribu kumsaidia rafiki yako apate msaada na jaribu kumsaidia akwepe sehemu ambayo atapata shinikizo la kutumia dawa au pombe. Margaret kutoka Kenya (Umri wa miaka 16) Wengi wa marafiki zangu walikuwa wameshaharibiwa na dawa; lakini baada ya kujua hatari na ukweli kuhusu dawa niliamua kuwasaidia marafiki zangu. Wengi wamebadilika na mimi ninafurahi. Wakati mwingine watu wenye matatizo kutokana na dawa hawako tayari kukusikiliza wewe na ushauri wako. Wanaweza kuzikataa juhudi zako za kusaidia na wanaweza kukukasirikia. Mnaweza mkaishia kuwa na mabishano makali na rafiki zako, lakini angalau dhamira yako itakuwa wazi na utakuwa umejitahidi kuwasaidia. Wakati wote upo uwezekano wa urafiki kuvunjika kutokana na tabia yako ya kutokubaliana na tabia zao. Hanifa kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Nilikuwa na rafiki ambaye nilimwamini sana kwa kipindi kirefu, lakini sikujua mambo aliyokuwa anayafanya kwa kificho. Siku moja nilimkuta na watu wenye sura za ajabu, macho yake yalikuwa mekundu. Niligundua alikuwa ananuka bangi. Nilijaribu kuzungumza naye mara kwa mara lakini hakunisikiliza. Hivyo nilimtaka achague ama kuacha kutumia alichokuwa anatumia au kuacha kuzungumza na mimi. Nilifikiri angefanya uamuzi sahihi lakini nilikuwa nimekosea aliacha kuzungumza na mimi. Inaweza kuwa vigumu sana kumpoteza rafiki lakini angalau ulisimama kwenye kanuni zako, ulijaribu kumsaidia rafiki na wewe binafsi hukujihusisha na hatari ya dawa. Mara chache, baada ya muda, rafiki atabadilika. Kofi kutoka Ghana (Umri wa miaka 16) Huwa nashinikizwa na marafiki zangu kutumia dawa za kulevya ninapokuwa nao, lakini ninajizuia mwenyewe na kuwaeleza kwa ujasiri kabisa kwamba nimeridhika bila ya kutumia dawa. Hanifa kutoka Tanzania (Umri wa miaka 17) Baada ya miezi kadhaa, rafiki yangu aligundua madhara ya dawa hizo kwa maisha yake, na akaniomba tuendelee kuwa marafiki tena. Kwa sababu nilimwonea huruma nilikubali

91 SURA YA 13 Matumizi mabaya ya dawa Kama una wasiwasi kuhusu rafiki yako, jaribu kumsaidia lakini kama rafiki anakataa msaada wako urafiki hautadumu, usijilaumu. Ulifanya jambo ulilopaswa kwa kadiri ulivyoweza. KUACHA DAWA Vijana wengi wanakua katika mazingira ambayo yanazungukwa na aina mbalimbali za dawa za kulevya. Lakini siyo kila kijana katika sehemu hizi anajihusisha na dawa hizo. Wengine wanajihusisha, baadhi hawajihusishi. Wengi wanakataa dawa na shinikizo kutoka kundirika kwa sababu wanayaona matatizo yanayoletwa na dawa za kulevya. Vijana hawa wana msimamo, wanafikiri wakati wote, na wanajitegemea. Wanakaa kimya, safi na wanafanya mambo wanayoyaona mazuri kwao. Anthony kutoka Zambia (Umri wa miaka 16) Nafikiri vijana wanapaswa kujishughulisha na mambo wanayoyapenda na siyo kukaa bila shughuli kwasababu ubongo usioshughulishwa ni karakana ya kufikiri maovu. Wanatakiwa kuwakwepa marafiki wabaya na makundi mabaya. Vilevile, ni vizuri kwa afya yako kukaa mbali na dawa za kulevya. Tafuta kukubalika kwenye manufaa: Kuna njia nyingi za kujisikia umekubalika na unapendwa na watu wengine. Kuna njia nyingi zinazokubalika kuliko kutumia dawa au pombe. Jiunge na makundi ya watu waliokusudia kufanya jambo fulani, kama kuimba, michezo, maigizo, kusoma au kusafisha maeneo ya jirani. Tafuta watu watakaokupenda vile ulivyo. Tafuta nini unaweza kufanya. Tafuta watu ambao hawapotezi muda wao kubwia dawa. Jithamini: Tambua thamani yako. Itetee thamani hiyo. Kuwa na nia ya kufanikiwa katika mambo yako: Je, nini ndoto zako? Tazama maisha yako ya baadaye na ona wapi unataka kwenda. Dawa hazitakusaidia kwenda unakotaka kufika. Tumia kila chembe hai ndani ya ubongo wako: Usiruhusu chembe hai za ubongo wako zikauawa na dawa za kulevya. Soma kwa bidii na fanya vizuri katika kazi zako za shuleni. Pata msaada wa kitaalamu: Kama unapata shinikizo la kutumia dawa, nenda kazungumze na mshauri wa vijana.pata msaada kama unafikiria unalo tatizo la dawa. Jaribu kutafuta mshauri na matibabu. Hujachelewa sana kuacha kutumia dawa za kulevya hata kama umekuwa unatumia muda mrefu. Msaada unapatikana lakini unatakiwa kuchukua hatua ya kwanza kuutafuta msaada huo. Prisca kutoka Kenya (Umri wa miaka 14) Yakwepe makundi mabaya yanayotumia dawa na jihusishe na shughuli za vijana. Dawa na pombe zipo tele kila mahali na zinaweza kuwa rahisi kupatikana. Lakini kuwepo kwa dawa haimanishi kwamba ni lazima uzitumie. Unaweza kuwa mtulivu, fanya mambo yako mwenyewe na kaa mbali na dawa za kulevya. Kuwa thabiti. Jitazame kwa uaminifu kujijua wewe ni nani na jinsi unavyotaka uendeshe maisha yako. Jua kipi ni muhimu kwako, na malengo yako ya baadaye ni yapi na utayapataje malengo hayo? Fikiria wapi dawa na pombe vinaingia katika mipango yako. Je, vitakusaidia ufanikishe mipango yako ya baadaye au vitakuzuia? Vifuatavyo ni vidokezo kutoka kwa vijana kuhusu namna ya kuepukana na dawa: Jishughulishe: Jihusishe katika shughuli mbalimbali kama vile michezo au vikundi vya sanaa. Shughuli hizo zitachukua muda wa kukaa bure na zitakufanya ujisikie vizuri. Hutachoshwa na hutahitaji kutafuta dawa za kulevya kama kiburudisho. Kuwa tofauti: Usitumie dawa ili ufanane na makundi. Kuwa mwenyewe. Fanya yale yanayokupendeza. Jiheshimu: Usitumie dawa za kulevya au pombe kwa ajili ya kufurahisha watu wengine au kupata ujasiri wa kufanya kitu. Jiheshimu na watu wengine watakuheshimu. Na ukishajua watu wanakuheshimu utapata ujasiri kwa lolote unalotaka kufanya

92 Sura ya 13 Matumizi Mabaya ya Dawa Kutumia dawa bila sababu za kiafya na kupata hali ya aina fulani kunaitwa matumizi mabaya ya dawa. Kuna aina nyingi za dawa na vitu vinavyotumika vibaya kama bangi, miraa, petroli, gundi na dawa kali kama kokeini na heroini. Pombe na sigara nazo pia ni dawa na mara nyingi zinatumika vibaya. Dawa zinaweza kuwa na athari nyingi zenye kuleta madhara. Matumizi ya dawa hufanya mwili uzoee hali ambayo huwezi kufanya chochote bila ya kuzitumia. Dawa pia zinaweza kuharibu ubongo wako, moyo, mishipa ya damu, na mapafu. Matumizi ya dawa wakati wa ujauzito yanaweza kuleta matatizo makubwa kwa mtoto. Vilevile dawa zinaweza kusababisha matatizo mengine. Dawa nyingi zinaweza kukufanya usifikiri vizuri na usiwe na uamuzi mzuri. Kutokana na hilo, unaweza kuwa hatarini kupata matatizo ya muda mrefu. Unaweza kufanya ngono bila kinga na kuishia kupata mimba zisizotakiwa au kumpa msichana mimba na magonjwa ya zinaa kama VVU/UKIMWI. Zipo sababu nyingi zinazowafanya vijana watumie dawa: Kujumuika na kundirika. Kuyakimbia matatizo. Kuishinda huzuni. Kujaribu kujibadilisha walivyo ili kuonekana tofauti. Kutafuta ujasiri wa kuhimili hali ngumu au changamoto. Kujifurahisha. Kumudu hali ya kupoteza matumaini. Hakuna hata sababu moja ambayo ni nzuri ili kuhalalisha matumizi ya dawa. Dawa zitafanya matatizo yako kuwa magumu zaidi.unaweza wakati wote kuyavumilia matatizo bila kuwa na dawa ndani yako. Una utashi wa kuyashughulikia matatizo au hali yoyote ile. Dawa zinaweza zikaharibu maisha yako ya baadaye. Achana na dawa na jishughulishe. Jihusishe na michezo na mambo mengine ya jumuia. Hutahitaji kutafuta tena furaha au burudani kutokana na dawa. Kuwa tofauti. Usifanye jambo la hatari ili ulingane na wenzio. Jiamini na fanya kilicho sahihi kwako. Kama unajiheshimu watu wengine watakuheshimu pia. Kama unapata msukumo wa kutumia dawa au kama unafikiri una tatizo la dawa, pata msaada. Dawa ni kitu chenye nguvu. Usijaribu kupigana na dawa peke yako. Msaada upo wakati wote, lakini unapaswa kuchukua hatua ya kwanza ya kuomba msaada. Kutimiza ndoto zako Kila mtu anazo ndoto za maisha yake ya baadaye, ndoto za kufanya jambo kubwa na kuwa mtu muhimu na aliyefanikiwa. Ndoto hizi zinaonyesha lengo la kupata kitu fulani. Haya ni malengo yetu na matamanio yetu. Ni maono tuliyonayo kwa ajili yetu wenyewe na kwa ajili ya maisha ya baadaye. Zifuatazo ni baadhi ya ndoto chache za vijana balehe: Sherifa kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Ninataka kuwa bibi shamba na ninataka kuwa mtu maarufu. Omari kutoka Tanzania (Umri wa miaka 18) Ningependa niwe mtu ambaye watu wanakuja kwangu kwa ushauri, mtu mwenye ndoa imara na pengine kazi kama meneja ofisini. Naana kutoka Ghana (Umri wa miaka 17) Ninataka kuwa daktari, hususani kushughulikia wanawake na watoto. Patrick kutoka Kenya (Umri wa miaka 16) Ninafikiria kuwa na shamba dogo la mifugo lenye ardhi ya kutosha ili wazazi wangu wakae huko pamoja na mimi. Ningependa niwe na mke na nipate watoto watatu. Milensu kutoka Zambia (Umri wa miaka 13) Ninafikiria kuwa na nyumba yangu mjini ikiwa na sofa sebuleni. Ninataka kuwa muuguzi, niwe na kliniki yangu na niheshimiwe na jamii yangu. SURA YA

93 SURA YA 14 Kutimiza ndoto zako Ndoto yako ni nini? Ungependa uwe nani? Unajifikiriaje mwenyewe katika miaka mitano ijayo? Katika miaka15? Utakuwa nani na utakuwa unafanya nini? Sura hii inahusu kutimiza ndoto zako. Inahusu kuzifikiria ndoto zako na kutafakari ni kwa vipi unaweza kuzifikia. Inahusu kufanya uamuzi mzuri wa busara na utakaokufikisha karibu na ndoto zako. Aidha, inahusu namna ya kumudu vipingamizi vitakavyojitokeza katika maisha. Si jambo rahisi kufanikisha ndoto. Inahitaji kufanya kazi kwa bidii na kuwa na dhamira/nia. Kwa hiyo, jambo muhimu ni kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii. Fanya vitendo! Usikae chini na kusubiri mambo yakutokee. Unatakiwa kuyajenga maisha yako ya baadaye. KUZITAMBUA NDOTO ZAKO. Watu wengine wana ndoto nyingi sana na zinabadilika kila wakati. Kwa mfano mchukue Remijia wa Tanzania: Alipokuwa na miaka 6 alitaka kuwa ofisa wa polisi. Alipokuwa na miaka 8 alitaka kuwa kapteni wa meli. Alipokuwa na miaka 10 alitaka kuwa rubani wa ndege. Alipokuwa na miaka 13 alitaka kuwa mwalimu. Sasa ana miaka 19 anataka kuwa mhandisi. Kwa nini ndoto hubadilikabadilika? Je, ni vibaya kuwa na ndoto nyingi zilizo tofauti? Hapana! Ndoto ni nzuri, zinatia hamasa na zinakufanya ufanye kazi kwa bidii. Zinakufanya uangalie maisha ya baadaye na uwe na mipango thabiti. Watu wengine wanaelekea kuwa na ndoto chache. Hawajui wangependa wawe nani wakiwa wakubwa. Wanapata shida kujifikiria watakuwa vipi miaka 5 ijayo. Kama yanakugusa, usihofu. Hili ni jambo la kawaida! Haina maana kuwa huna ndoto, bali ina maana kuwa bado hujafikiria ndoto zako ni zipi. Lakini, unaweza kuanza sasa kuzitambua ndoto zako. Ndoto za watu wengi zinaathiriwa na watu wanaowazunguka. Kwa hiyo, kwanza angalia unazungukwa na nini. Fikiria kuhusu watu walio ndani ya jamii. Ni nani unaowahusudu? Ni watu gani unaowaheshimu? Mtu anaweza kuwa mwalimu ambaye anajua majibu ya maswali yote yanayoulizwa. Anaweza kuwa ni daktari ambaye alijua kilichokuwa kinakufanya uumwe miezi michache iliyopita. Anaweza akawa mchungaji wa kanisa lako. Wanaweza kuwa wazazi wako. Pata muda wa kutafakari ndoto zako za baadaye Pili, usiruhusu ndoto zako zikakwamishwa na mambo unayoyaona. Angalia hata nje ya jumuia yako. Kuna mtu ambaye umemsoma kwenye gazeti au kitabuni ambaye alifanya jambo ambalo linakushangaza? Pengine ni mwanasayansi ambaye anajifunza jinsi tembo wanavyowasiliana wao kwa wao. Pengine ni muuguzi anayewahudumia wakimbizi katikati ya uwanja wa vita. Wapo watu wengi wanaofanya mambo mengi mazuri yanayovutia na yenye manufaa na maisha yao. Watu hawa wanaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa. Wanaweza kukuanzishia ndoto kuhusu maisha yako ya baadaye. Tatu, yaruhusu mawazo yako yapae angani usijiwekee mipaka ya vitu ambavyo unaweza kufanya au ambavyo huwezi kuvifanya. Kwa mfano, usiiache ndoto kwa sababu ya mawazo yaliyopitwa na wakati, kama mawazo kuhusu kazi wanazoweza kufanya wanaume pekee au wanawake pekee. Mambo yanaenda yakibadilika. Wanawake siku hizi wanafanya kazi ambazo mama zao hawakuwahi kufikiria kuzifanya. Sasa hivi wanawake wanaweza kuwa wahandisi, marubani, madaktari, wanariadha, wanasayansi, maprofesa, wanaanga, Marais, waandishi wa habari n.k. Kama ni mvulana au msichana, unaweza kuwa mtu unayetaka kuwa, ikiwa utadhamiria na kufanya kazi kwa bidii. MIPANGO YA BAADAYE KUHUSU KAZI Vijana balehe wachache wana vipaji vya ziada katika taaluma fulani, kama hisabati, muziki au kuchora. Utafikiri kipaji kimewachagua. Wanakuwa wataalamu wazuri wa hisabati, wasanii, walimu na viongozi wa kwaya au wasanifu majengo. Watu wengine wanapendelea kitu kimoja tangu utoto wao, na mvuto huo mkubwa unarahisisha sana wakati wa kutoa uamuzi kuhusu watakuwa nani. Unaweza kumsikia mzazi akisema wakati wote tulijua kwamba John atakuwa mganga wa mifugo. Alianza kuwahudumia wanyama wadogo alipokuwa na umri wa miaka minne tu. Watu kama hawa, maisha yao yanaonekana kuwa rahisi. Inaonekana kana kwamba njia yao ya kazi imenyooka. Uamuzi wao unaonekana kuwa ni rahisi kwa sababu wanajua kabisa wanataka kufanya nini, na wanacho kipaji katika eneo hilo maalumu. Wengi hatuko hivyo. Wengi ni watu wa kawaida, wenye akili ambao tunaweza kufanya vizuri katika mambo tofauti. Uwezekano wa kuwa nani au kufanya nini ni matokeo ya mchanganyiko wa yale tunayoyapenda na tusiyoyapenda, uwezo wetu na utayari wa kufanya kazi kwa bidii na fursa tunazopata. Kufanikisha ndoto kwa watu wengi ni njia ndefu yenye kona nyingi. Wakati wote siyo moja kwa moja na hatua sahihi za kuchukua haziko wazi. Zaidi ya hapo vikwazo visivyotegemewa vinaweza kujitokeza njiani. Ni mambo ambayo yanatakiwa kushughulikiwa kwa makini sana. Jitahidi kujitokeza kwenye kazi nyingi iwezekanavyo. Bila kufanya hivyo huwezi kufahamu nafasi gani zipo duniani kwa ajili yako? Katika nchi nyingine, vijana balehe wanajitolea kufanya kazi katika mashirika mbalimbali wakati wa likizo. Wakati mwingine wanapata malipo kidogo ya kutosha usafiri kwenda na kutoka nyumbani. Lakini mara nyingi hawapati chochote. Wanajitolea tu. Usifikiri kwamba kwa vile jambo fulani siyo la shule na siyo la kazi ya kulipwa basi halina thamani. Iwapo unaweza kupata kazi ya kujitolea, pengine unaweza kupata uzoefu mzuri na wenye manufaa

94 SURA YA 14 Kutimiza ndoto zako Kwa mfano unaweza kupata fursa ya kuona jinsi utaratibu wa kazi za ofisini zinavyokuwa na utaweza kupata hisia nzuri kuhusu kazi wanazozifanya. Unaweza kujua kwamba kazi hiyo inakufaa au haikufai. Kwa vyovyote itakavyokuwa, uvumbuzi utakuwa muhimu. Kwa jinsi utakavyokuwa unaendelea utajifunza stadi mpya, utajenga mvuto mpya na utajiamini. Unapofikiria kuhusu aina ya kazi ambayo ungependa kufanya, vilevile fikiria kuhusu hatua utakazozichukua. Kwa mfano, fikiria kuhusu watu wenye sifa nzuri uliowachagua. Unafikiri walifanya nini hadi kufikia hapo walipo? Walihitaji aina gani ya elimu? Aina gani ya mafunzo kwa vitendo waliyapata? Njia bora ya kujua namna gani watu walivyofikia hapo walipo ni kuwauliza. Iwapo wapo watu ambao unawaheshimu na ambao mafanikio yao unayahusudu, waulize kama wanao muda wakuambie jinsi walivyofikia pale walipo. Kabla hamjakutana, andika orodha ya maswali ambayo ungependa kuwauliza, Kwa mfano; ni kitu gani kilisababisha kuchagua kazi wanayoifanya na ni aina gani ya elimu na mafunzo waliyapata. Wanapenda nini zaidi kuhusu kazi yao? Ni kitu gani hawakipendi?n.k. Watu wengi wanafurahi sana na kujisikia sifa wakati mtu mwingine anavutiwa na mafanikio yake na pale wanapoombwa ushauri. Kawaida watu watakuwa na shauku ya kukueleza habari zao na kukusaidia njia utakayochagua. Unahitaji ujasiri kumwendea mtu mzima ambaye humjui vizuri, lakini utashangaa wengi wao watakuwa wazuri na watakusaidia, wanaweza kukushauri jinsi ya kupanga kazi yako. KUWEKA MALENGO Ni vema kuweka malengo, mambo unayoyategemea kwa maisha ya baadaye. Vilevile, unahitaji kujiwekea malengo mahususi ambayo yanaweza kukamilishwa katika muda mfupi. Lengo ni kuwa na jambo unalotaka kulifanyia kazi. Kuna aina mbili za malengo. Malengo ya muda mfupi na mrefu. Ndoto zako ni malengo ya muda mrefu. Haya ni mambo unayoyawazia kutokea baadaye katika muda mrefu.malengo ya muda mfupi ni mambo ya muda mfupi. Ni mambo yatakayotokea kesho, juma lijalo au mwaka kesho. Malengo ya muda mfupi ya baadhi ya vijana balehe ni haya yafuatayo:- Sofia kutoka Uganda (Umri wa miaka 14) Itakapofikia mwisho wa mwaka wa kwanza wa sekondari, ninataka kushika namba za juu, nusu ya darasa. Essie kutoka Ghana (Umri wa miaka 15) Nitakapofikia umri wa miaka 16 ninataka kujua jinsi ya kutumia kompyuta. Francis kutoka Kenya (Umri wa miaka 16) Mwakani ninataka kupiga solo katika kwaya ya kanisa. Miriam kutoka Zambia (Umri wa miaka 16) Ninataka kufanya vizuri katika mitihani yangu ili niandikishwe katika shule nitakayoichagua. Patrick kutoka Zimbabwe (Umri wa miaka 18) Ninataka kujifunza jinsi ya kuzungumza mbele ya kadamnasi. Una malengo gani? Ni mambo gani ambayo ungependa kuyafanya ifikapo mwisho wa mwaka huu? Je, mwisho wa mwaka ujao? Malengo yana manufaa sana. Unapokamilisha lengo unaweza kulifuta kwenye orodha. Inakupa hisia ya mafanikio na furaha ya kukamilisha jambo. Inakufanya ujisikie vizuri. Inakuonyesha kwamba unapofikiria kitu unaweza kufanikisha. Malengo yanatakiwa yawe halisi na ambayo yanawezekana kutekelezeka- mambo ambayo unaweza kufanikisha. Wakati mwingine watu huweka malengo ambayo si halisi, kama vile kuwa tajiri sana. Watu wengi hawawi matajiri na hata wale wanaokuwa matajiri pengine walikuwa na malengo halisi kama vile kuanza biashara zao. Waliendesha biashara kwa muda mrefu kiasi cha kufanikiwa sana. Wakati mwingine watu wanaweka malengo yasiyofaa, mathalani kuhusu mambo ya kufanya mapenzi. Vijana balehe wengine wanajiambia: Likizo hii lazima nipoteze ubikira wangu. Lazima nijamiiane nikifikisha umri wa miaka 16 Nitajaribu kujamiiana na msichana mwingine zaidi ya rafiki yangu wa kike. Malengo kama haya hayana manufaa. Ukiyafanikisha pengine hutajisikia vizuri. Hebu fikiria: Hivi kweli kujamiiana ndilo lengo lako? Je, umeweka lengo hili kwa sababu tu unapata shinikizo ili usiwapoteze marafiki? Je, unafikiri marafiki zako wote wanajamiiana, hivyo wewe unabaki nyuma? Hizi siyo sababu nzuri za kujiwekea malengo. Fikiria kile ambacho wewe mwenyewe unataka kufanikiwa na weka maanani mwongozo huu wa kuweka malengo:- Hakikisha malengo yako ni mazuri na yana manufaa. Hakikisha malengo ni halisi na yanatekelezeka. Hakikisha hayakuingizi katika hatari yoyote Ukifanikisha lengo utajisikia vizuri Hakikisha ni malengo yako wewe na siyo ya mtu mwingine

95 SURA YA 14 Kutimiza ndoto zako Baada ya kuyatambua malengo yako, fikiria jinsi utakavyoyafanikisha. Weka mpango mzuri mwenyewe. Halafu jiulize maswali haya manne: Kwa nini? Ni sababu gani zinakufanya uwe na lengo hili?. Kwa nini unataka kulifanikisha? Namna gani? Hatua gani utakazozichukua kufanikisha lengo hili? Utafanya nini? Lini? Utamaliza lini kila hatua uliyoiweka katika kufanikisha lengo? Utafanikisha lengo lako lini? Nini? Utahitaji nini ili kufanikisha lengo lako? Kwa mfano: Tuchukulie labda unataka kufanya vizuri zaidi katika somo la Hisabati. Kwa nini unataka kufanya vizuri zaidi? Pengine ni kwa sababu unajua unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko ulivyowahi kufanya siku za nyuma. Unafaulu sana katika masomo mengine isipokuwa Hisabati. Una akili, na wala huhitaji kusoma sana ili ufanye vizuri masomo mengine. Hata hivyo, unaona Hisabati ni ngumu zaidi. Ni kwa namna gani utaboresha alama zako za Hisabati? Labda utaanza kufanya marudio zaidi, kwa kupata msaada wa ziada baada ya masomo na baada ya mazoezi ya maswali zaidi. Lini utachukua hatua zote hizi? Labda utaamua kutumia saa moja nzima kila siku kujifunza Hisabati baada ya kutoka shule na saa mbili siku za mwisho wa wiki. Utahitaji nini kikusaidie uboreshe alama katika Hisabati? Labda unahitaji muda zaidi. Pengine huwa unamsaidia shangazi yako shughuli za dukani kila siku jioni. Mweleze shangazi yako kuhusu lengo lako na mwombe kama anaweza kukuachia mapema ili uweze kujisomea. Pengine unahitaji maswali mengi ili ufanye mazoezi. Mwombe mwalimu wako akupe maswali ya ziada ya kufanya nyumbani. Panga mipango vizuri ili uweze kufikia malengo na ndoto zako Je, uende nyumbani baada ya masomo ukajisomee au ubaki shuleni kucheza na wenzako? Je, ukubali kujamiiana na rafiki yako wa kike au usubiri? Unatakiwa ufanye uamuzi wa busara kila siku. Mojawapo ya mambo muhimu katika kufanya uamuzi ni kuangalia mbele na kuona kitu gani kinaweza kutokea iwapo utafanya kitu fulani. Tunaita kutabiri matokeo yanayoweza kutokea. Jinsi unavyoweza kutabiri matokeo mapema ndivyo utakavyofanya uamuzi mzuri utakaoleta matokeo unayoyataka. Kwa mfano, labda unataka kuamua uende nyumbani kwa rafiki yako baada ya kutoka shuleni. Iwapo utaenda nyumbani kwao itasaidia kuimarisha urafiki wenu kwa vile msichana huyu anajulikana sana shuleni na amewaalika wasichana wengi kwao. Kwa muda mrefu umekuwa unataka kuwa rafiki na kikundi hiki kwa hiyo unafurahi sana kualikwa ili kupata wasaa wa kuwa nao Je, Unafahamu hatua muhimu za kuchukua unapofanya uamuzi? Fafanua tatizo, hali au suala ambalo unahitaji kufanyiwa uamuzi. Tambua uchaguzi wote wenye kuwezekana au njia utakazotumia. Fikiria matokeo ya kila utakalochagua. Fikiria maadili na imani yako kuhusu kinachostahili na ambacho hakistahili ni jambo gani la kufanya linaloendana na maadili yako. Fikiria jinsi uamuzi wako unavyoweza kuathiri watu wengine. Chagua jambo la kufanya ambalo kigezo chake ni ufahamu wako, maadili, thamani, malezi ya kidini na malengo yako. Tathmini uamuzi wako na jinsi unavyojisikia amua kama ulifikiria kwa uangalifu na chunguza tena ili uweze kujisikia safi na uchaguzi ulioufanya. Kwa upande mwingine, mama yako anaweza kukasirika kama ukienda bila ya kuomba ruhusa. Zaidi ya hapo unakabiliwa na mtihani wiki ijayo na ulikuwa umeahidi ungeanza kujisomea mapema. Ukienda nyumbani kwa huyu msichana, utakuwa na muda mfupi wa kujisomea kwa ajili ya mitihani, na unaweza kupata maksi chache. Ukipanga vizuri na kufanya kazi kwa bidii unaweza kutimiza malengo yako. KUFANYA UAMUZI MZURI (WA BUSARA). Kufanya uamuzi mzuri kunaweza kukusaidia kutimiza malengo yako na hatimaye kufanikisha ndoto zako. Uamuzi mzuri haimaanishi kuwa ukiwa na miaka 13 unaweza kufanya uamuzi sahihi kuhusu utakuwa nani maishani mwako. Kufikiria utakuwa nani siyo uamuzi. Hiyo ni ndoto na ni lengo la muda mrefu. Kufanya uamuzi ni tofauti. Uamuzi ni uchaguzi kati ya njia moja au nyingine zinazowezekana kutumika. Kufanya uamuzi ni kitendo cha kila siku. Utafanya mamia ya uamuzi mpaka ufikie mafanikio ya ndoto zako. Toa uamuzi wako binafsi. Usiruhusu watu wengine wafanye kwa ajili yako

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu BLOOD PRESSURE UK Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha ulemavu na vifo vya mapema kule Uingereza, kupitia kiharusi, mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.

More information

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI This booklet on menopause was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji! Yaliyomo Kuhusu kitabu hiki Kuhusu kitabu hiki.........................................................1 Unapojisikia vibaya.........................................................2 Unapoanza kuwa mzima

More information

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI This booklet on Becoming a Parent was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at. MACHAGUO

More information

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako

More information

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako Siku ya kwanza Baada tu ya mtoto kuzaliwa ni wakati wa kufurahia, lakini pia ni wa kuchosha. Kujua vitu vichache kuhusu kunyonyesha hufanya siku ya kwanza kuwa rahisi kidogo. Baada ya kujifungua Wakati

More information

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma. This booklet on HIV/AIDS was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at VIRUSI VYA

More information

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo Mazoezi ya wenye umri wa miaka 11-14 Hivi Ndivyo Nilivyo kwa wenye umri wa miaka 11-14 Kuhusu Hivi Ndivyo Nilivyo Ikiwa

More information

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre Shangazi Stella Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO Training and Research Support Centre Zimbabwe Shangazi Stella Kiongozi cha Mwezeshaji

More information

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu

More information

Human Rights Are Universal And Yet...

Human Rights Are Universal And Yet... Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted

More information

MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI: Nyongeza ya Mtalaa Kwa vijana

MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI: Nyongeza ya Mtalaa Kwa vijana MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI: Nyongeza ya Mtalaa Kwa vijana Umeigwa kwa Mtindo wa Kenya a program of the International Youth Foundation The International Youth Foundation (IYF) invests in the extraordinary

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza 1 Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA Kwa Wanaoanza For IT Services & Web Solutions Web: Email: info@dudumizi.com Phone: 0768816728 2 Matumizi bora ya Facebook kwa

More information

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango Octoba 2013 1 w 2 Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango Octoba 2013 3 4 Yaliyomo Dibaji 7 Shukurani 8 Utangulizi 10-12 Faida za Uzazi wa mpango

More information

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Early Grade Reading Assessment for Kenya EDDATA II Early Grade Reading Assessment for Kenya Baseline Instruments: Kiswahili and English EdData II Technical and Managerial Assistance, Task Number 4 Contract Number EHC-E-01-04-00004-00 Strategic

More information

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia : Maelekezo ya kutumia Kupatwa kamili kwa jua Jumatatu, 21 Agosti 2017 Agreement v1.4 Mar 2014 2014-2017 Eclipse2017.org, Eclipse2017.org, inc. inc. TERMS AND CONDITIONS FOR USE OF SOLAR VIEWER Please

More information

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Kubadilishana Tamaduni za Kijerumani na za Kitanzania Limeandaliwa na Anna Hoppenau, Johannes Hahn, Oliva Lyimo na Lisa Bendiek German-Tanzanian Partnership (DTP)

More information

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Makala ya Mshiriki wa Mafunzo Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka

More information

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST

More information

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level * 899145 4 672* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2010 Additional Materials: Answer Booklet/Paper READ

More information

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi.

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi. Uzazi wa Mpango MPANGO WA UZAZI WA W.H.O. MWONGOZO WA WATOA HUDUMA YA AFYA DUNIANI Kitabu hik nachukua nafasi ya kitabu cha Mambo ya Msingi katika Teknolojia ya Njia za Kuzuia Mimba SHIRIKA LA MISAADA

More information

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi International Labour Office Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi 1 Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2007 Kimechapwa mara ya kwanza 2007 Machapisho ya Ofisi ya Shirika la

More information

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna

More information

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI

More information

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka 0 Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Kijitabu Kielelezo; Nakala ya Bila Malipo Yaliyomo 1 Yaliyomo Utangulizi...04 Habari Fupi Kuhusu...08 Fumbo la Ulimwengu wa Ng ambo ya Pili...11

More information

Ufundishaji wa lugha nyingine

Ufundishaji wa lugha nyingine CHUO CHA ELIMU CHA KIMATAIFA OFISI YA ELIMU YA KIMATAIFA Ufundishaji wa lugha nyingine Na Elizabeth B. Bernhardt ELIMU MAZOEA KITABU NA. 20 1 Chuo cha Elimu cha Kimataifa (The International Academy of

More information

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh

More information

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery

More information

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017

More information

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig KITINI CHA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA SIMU YA KIGANJANI KATI YA BARAZA LA FAMASI NA WAMILIKI WA MADUKA NA WATAALAMU WA DAWA YALIYOMO UTANGULIZI... 3 SEHEMU YA KWANZA: MALIPO YA KUHUISHA VIBALI... 4 1.1

More information

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Shule za umma za kata ya Fayette 1 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. Tunaamini familia ni wenzetu.

More information

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI Mwongozo huu utatumika kama njia ya kuwafunza watafiti watakaohusika na utafiti unaohusu binadamu. Muongozo huu utatumika

More information

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia IDARA YA KUFIKIA HUDUMA ZA AFYA VERMONT Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia GreenMountainCare MIASHA YENYE AFYA BORA ZAIDI Jedwali la Yaliyomo Jedwali la Yaliyomo... 2 Karibu kwenye Programu ya

More information

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Imechapishwa na: The Atlas Alliance Schweigaardsgt 12 SLP 9218 Grønland 0134 Oslo, Norway Simu: +47

More information

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Desemba 2014 1 Shukurani Ripoti hii iliandikwa na Dk. Mkumbo. Ushauri wa kitaalamu ulitolewa na Elizabeth Missokia na Godfrey

More information

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246 P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@twiga.com 01 October 2000 Y2K PREPARATIONS Holes and Seedlings made ready for the year 2000 programme By Gayo Mhila The process of

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi

More information

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika (A Summary Of Arguments For And Against Individual Communion Cups) Na J D Logan Communion Cups) 1 Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi

More information

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Martha Qorro 1 1.0 Utangulizi Elimu ni suala la jamii ambalo mipango na taratibu zake zinahitaji kushirikisha wadau

More information

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way: Demane na pacha wake Author - South African Folktale Adaptation -

More information

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 Title: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Author: Stefanie Duckstein, HA Afrika/ Nahost Editor: Christine Harjes Translator: Tony Dunham Sound

More information

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ukristo leo unadhihirisha waumini karibu bilioni mbili katika maelfu ya madhehebu tofauti na tofauti na madhehebu. Kati ya hizi, zaidi ya 500 madhehebu

More information

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03 Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03 AEG swahili Bahari ya Aegean Brosha ya maelezo hii ni kwa watu wanaofikiria kuvuka bahari ya Aegean kati ya Ugiriki na Uturuki.Kuvuka kihramu ni uhalifu katika

More information

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA Toleo la kwanza 2012 Mwandishi: USAID DELIVER PROJECT Wachangiaji: Gary Steele, John Snow, Inc. and Judith

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q 88092387 SWAHILI B HIGHER LEVEL PAPER 1 SOUAHÉLI B NIVEAU SUPÉRIEUR ÉPREUVE 1 SUAHILI B NIVEL SUPERIOR PRUEBA 1 Tuesday 3 November 2009 (morning) Mardi 3 novembre 2009 (matin)

More information

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya Nordic Journal of African Studies 9(2): 49-59 (2000) Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya UTANGULIZI Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma

More information

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to

More information

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

SautiElimu. Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org ( Published on Al-Islam.org (https://www.al-islam.org) Home > Haja Ya Dini Haja Ya Dini Author(s): Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi [3] Publisher(s): Bilal Muslim Mission of Tanzania [4] Katika kijitabu

More information

Kiu Cha umtafuta Mungu

Kiu Cha umtafuta Mungu ZAIDI YA NAKALA MILLION 3 ZIMECHAPISHWA KATIKA LUGHA 59 KOTE DUNIANI K Kiu Cha umtafuta Mungu Huduma ya Daktari Richard A. Bennett ilianza katika mabaraza ya miji. Akiwa mwanafunzi chuoni, alikumbana na

More information

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu Nyenzo ya Mafunzo Vi Agroforestry Vi Agroforestry ni shirika la ushirikiano la maendeleo la Sweden, linalopambana dhidi ya umasikini na

More information

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke- Kusudi la Maisha hawatakuambia nini walihitimisha kupitia uchunguzi au hoja ya uchambuzi. Katika hali nyingi, hakika wao kukuambia nini mtu mwingine alisema... Au wao watakuambia nini kawaida kudhaniwa

More information

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mpya ya Mtoto ambayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa

More information

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili Notisi Maalum Matibabu, kama sayansi, ni somo linaloendeleza uwekezaji. Ujuzi

More information

TIST HABARI MOTO MOTO

TIST HABARI MOTO MOTO TIST HABARI MOTO MOTO Tel. +255784-537720/+255717-062960/+255782-250947, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@tist.org May 2010 Cash Payments for Trees Clean Air Action has developed a way to pay the groups

More information

United Pentecostal Church June 2017

United Pentecostal Church June 2017 Kwa Nini Tusali? Jarida la Maombi ya Wanawake Kimataifa "Chagua" Ladies Prayer International kwa Facebook United Pentecostal Church June 2017 Tuko na wafuasi Facebook katika Marekani, Hong Kong, Philippines,

More information

Upande 1.0 Bajeti yako

Upande 1.0 Bajeti yako Upande 1.0 Bajeti yako Bajeti (Budget) ni muhustari wa njisi wewe (na familia yako) mnavyopata na kutumia pesa. Inaunganisha pesa zinazoingia nyumbani kwako (Kipato/ income) na zile unazotumia (matumizi/expenses).

More information

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI/AGOSTI 2011 MUDA: 2 ½ Kiswahili Fasihi Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E) MAAGIZO Jibu maswali manne pekee Swali la kwanza ni lazima Maswali

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi 3.1 Utangulizi Miradi na jamii Lengo la sura hii ni mapitio ya mazingira pana ambayo chini ya ardhi kwa ajili ya maendeleo vijijini upatikanaji wa maji inafaa. majadiliano wakapanga meneja, au kiongozi

More information

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa, UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, MEI 2014 Na Rais Thomas S. Monson Upendo Asili ya Injili Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya maisha duniani. ninafurahia mawazo

More information

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu 134 Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu Picha tuliyonayo kuhusu Mungu ni mojawapo ya kizuizi kikubwa cha kupata uponyaji wetu. Mara nyingi huwa hatujui vizuri kwamba Mungu anatupenda kwa hivyo angependa

More information

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Gervas Zombwe 1 1. Utangulizi Katika mazingira ya kawaida kabisa ndani ya jamii yetu, Imezoeleka kusikia au kuona watu wakioanisha dhana ya elimu

More information

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa 119 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa Kukataliwa ni mojawapo ya mitindo ya Shetani ya ukandamizaji. Kukataliwa kunaweza kumzuia mwenye dhambi kumjia Mungu ili apate wokovu na kumzuia Mkristo kuufikia uwezo

More information

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini... Elimu Bora, lakini... Shukrani za dhati kwa wote waliotusaidia katika kutayarisha kijitabu hiki: Nsa Kaisi, Mshauri wa Rais, kwa mchango wake mkubwa wa mawazo Wafanyakazi wote wa HakiElimu 2003-2004 Many

More information

Mwongozo wa Mwezeshaji

Mwongozo wa Mwezeshaji JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Mwongozo wa Mwezeshaji Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka lugha

More information

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) 2016/2017 TEMBELEA ACKYSHINE.COM/SHOP KUPATA MAJARIDA MENGINE KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) Kutoka ackyshine.com/shop Melkisedeck Shine KILIMO CHA VITUNGUU (VITUNGUU MAJI) Vitunguu

More information

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR MUHTASARI WA RIPOTI YA YA MWISHO. JULY 2012 for Page i Muhtasari Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini

More information

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji Sera ya Faragha Katika Sera hii ya Faragha ( Sera ), sisi, Qualcomm Incorporated na makampuni yetu tanzu (kwa pamoja sisi au yetu ), tunatoa maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na

More information

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA Maagizo (a) Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (b) Tia sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (c) Jibu maswali

More information

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College Theolojia 1 Ujumla Mike Taylor Semester 1 2014-2015 Munguishi Bible College MIKE TAYLOR 2014 THEOLOJIA 1 i THEOLOJIA Utangulizi! 1 1. Kumfahamu Mungu katika Injili! 3 1.1. Mawazo Makuu 3 1.2. Maana ya

More information

Shabaha ya Mazungumzo haya

Shabaha ya Mazungumzo haya Karibu Katika Mazungumzo Kuhusu Mchakato wa Uhamasishaji Maendeleo ya Kanisa na Jamii CCMP/UMOJA Shabaha ya Mazungumzo haya Kuwafahamisha viongozi wa makanisa kuhusu Mchakato wa CCMP ambao umekuwa ukitumika

More information

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya Jina Nambari.. Shule... 102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI / AGOSTI. 2007 MUDA: SAA 2 ½ MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya 102/3 KISWAHILI FASIHI

More information

Kutetea Haki za Binadamu

Kutetea Haki za Binadamu Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA

More information

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump

More information

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya

More information

Palliative Care Toolkit

Palliative Care Toolkit KISWAHILI TRANSLATION INPATIENT CARE OUTPATIENT CLINIC HOME-BASED CARE DAY CARE SUPPORT HOSPITAL PALLIATIVE CARE TEAM Physical Psychological Spiritual Social Palliative Care Toolkit Improving care from

More information

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS ALLIANCE BOYS HIGH SCHOOL KISWAHILI KARATASI YA 2 SCHOOLS NET KENYA Osiligi House, Opposite KCB, Ground Floor Off Magadi

More information

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine. HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI ASKOFU MARTIN FATAELI SHAO WA DAYOSISI YA KASKAZINI YA KANISA LA

More information

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 The Human Rights Centre Uganda JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 AZIMIO LA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA KIBINADAMU SURA YA NNE YA KATIBA YA JAMHURI YA UGANDA YA 1995: MASIMULIZI YALIYOFASIRIWA KWA URAHISI NA KUFUPISHWA

More information

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Wasiojua kusoma na kuandika katika karne ya 21 hawatakuwa wale wasiojua kusoma na kuandika lakini wale ambao hawawezi kujifunza, kutojifunza na kujifunza

More information

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE FACILITY

More information

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Afya Bora, Utu na Kinga Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi 27-28 Aprili 2009, Hammamet, Tunisia Shukrani Ripoti

More information

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w MAMLAKA Tunamshukuru Bwana kwa vile alivyo na yale aliyoyatenda. Tukiweza tu kumfikiria hata tukiwa na mahitaji mbalimbali, yeye atatutimizia. Tusiwatazame watu, tusijitazame sisi wenyewe, tumtazame Mungu

More information

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza Utafiti wa mazingira ya haki za jamii za Wafanyakazi wa Ngono na LGBTI nchini Tanzania 2015 2016 Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa,

More information

K. M a r k s, F. E n g e l s

K. M a r k s, F. E n g e l s W a (any a kazi wa nchi zote, unganeni! K. M a r k s, F. E n g e l s Maelezo ya chama cha kikomunist Idara ya Maendcleo Moscow Tafsiri hii ya "Maelezo ya Chama cha Kikomunist" inatokana na maandishi

More information

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya

More information

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira Moduli ya kwanza Uhamasishaji Jamii juu ya Afya ya Mazingira Kimechapishwa kutokana na Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira Jeff Conant na Pam Fadem i COBIHESA

More information

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya

More information

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa Child Abuse & Neglect 43(2015)8 21 Orodha Yaliyomo inapatikana katika ScienceDirect Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa Nakala ya Utafiti Mbinu za kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto kuanzia chini kwenda

More information

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT 1 Ushindi Ndani ya Kristo Na W. W. Prescott Mfasiri: M. Mwamalumbili Victory in Christ - Kiswahili 2 Yaliyomo Alinipenda Mimi Aliishi kwa ajili Yangu Mimi Alikufa

More information